Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[040]
Heri
(Toleo La 3.0 19940702-19991127-20070202)
Jarida hili
linatafakari neno Heri na maana yake. Kila moja ya Heri hizi imefafanuliwa kwa
utaratibu muafaka. Utimilifu wa Injili inayosisitiza afya na uzima yn utajiri
au mafanikio kumetathiminiwa pia. Nafasi ya Nafasi ya katika utendaji wa mambo
ya kimaongozi imejadiliwa pia.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1994, 1996, 1999, 2007 Wade Cox)
(Tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Heri
Heri zilizotajwa
na kutolewa ni za maana sana. Mahubiri haya aliyoyafanya Kristo na kuandika
kwenye Mathayo 5 yananguvu na matokeo makubwa sana.
Heri hizi ni
mibaraka kwa Kanisa lake, na kwa watu wake. Zimechukuliwa kama mfano wa
kuufuata au kigezo cha maisha na matendo ya wateule. Hata hivyo, zinaelezewa na
Wakristo wa makanisa kongwe ya kale kwa namna dhaifu na potofu; kanuni zake
zikilinganishwa na Injili ya udhaifu au yenye mapunguvu. Kusudi la kuandika
jarida hili ni kufafanua jinsi tunavyoweza kujifunza kutokana na Heri hizi kwa
namna bora, njema na imara.
Inasema kwenye Mathayo
5:1-12:
Mathayo 5:1-12 Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; 2 akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, 3 Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. 4 Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. 5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. 6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. 7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. 8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. 9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. 10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. 11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. 12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Kristo analiambia
Kanisa hapa, kitu kilicho cha hakika au cha kwanza kukifuata au kukifanya
wanafunzi wake. Kisha anaendelea kuelezea kuhusu chumvi.
Mathayo 5:13-16 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. 14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. 15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. 16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Kristo haishii
hapa tu. Wakristo wengi wamesikia mambo haya huko nyuma, lakini wameshindwa
kuyachambua kwa ujumla na kuweka kwenye mifuko midogo. Hawaichambui. Kristo
anaongelea kwa mfuatano wa mambo kwa ujumbe halisi. Anaendelea kwa kusema hivi:
Mathayo 5:17-20 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. 19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. 20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Hawa ni watu
kwenye Kanisa la Mungu, na wamekuwepo kwa kipindi cha karne kadhaa, na ni ambao
wamefundishwa umuhimu wa kuzishika Sheria au Torati kwa namna mbalimbali. Wamefundishwa
na kufundisha kwamba hatuna sababu ya kuzishika au pengine idadi nyingine ya
mambo ya Kitorati. Kwa kweli kuna mambo mengine yahusuyo Amri na Torati ambazo
hatuendelei kuzishika leo kwa sababu ya desturi za jamii inayotuzunguka tunayoishi
nayo. Hata hivyo, hii sio ni kwa sababu amri na Sheria hizo zimetanguka la
hasha, bali ni jamii tunayoishi nayo ndiyo imezikataa na kuziondolea mbali na
kuzifanya zisitumike. Tena, katika siku fulani kadhaa zilizopita, baadhi ya
Makanisa ya Mungu yametumia utetezi wa kwamba, kwa kuwa hatuzishiki tena hata
mojawapo ya maagizo haya ya Torati, basi hatuhitaji kushika agizo linguine lolote
la amri hizi leo. Kwa mfano, imeenezwa ushawishi kuwa hizi Siku Takatifu
hazihitajiki kuadhimishwa kwa kuwa eneo au nafasi ya Torati hii inapotakiwa kuadhimishwa
haliadhimishi tena.
Udadisi huu
umefanywa kwa msingi kwamba jamii inakataza biashara ya kuuza mabinti (Kutoka
21:7) na maisha ya ndoa za wake wengi (Kutoka 21:10). Swali la kujiuliza ni
kwamba Siku Takatifu (Kutoka 23:10-19) hazihitajiki kuadhimishwa. Mchakato huu
huu wenye mashiko unaedelea hadi kwenye Sabato na Amri za Mungu (Kutoka
20:1-17; 23:1-13). Kama tulivyojadili kwenye maeneo yaliyopita, Torati
haijatganguka bado kukiwepo na ndoa za matala, uuzaji wa mabinti au kuhusu
uvaaji wa riboni za bluu kwenye nguo zetu (Hesabu 15:37-38; soma jarida la Amri ya Kwanza: Dhambi ya Shetani (Na. 153) [The
First Commandment: the Sin of Satan (No. 153)]. Torati bado upo kwenye ukamilifu wake na
hakuna hata yodi moja au kinukta kidogo kitakachopita. Sheria za kutoa sadaka
za wanyama hazitumiki leo kwa kuwa sisi ni Hekalu. Wakati atakapokuja Masihi
ataaiamsha tena imani na kuizisha tena. Lakini sio jukumu letu. Masihi alikuwa ni
dhabihu ya ondoleo la dhambi na sadaka yake inatosha kututakasa na ambayo imetolewa
mara moja tu kwa wote. Hii ndiyo Sheria pekee ambayo imehitimishwa katika
ukamilifu wake. Sheria zingine hazitumiki kwa kuwa jamii haiuzi tena mabinti
zao. Sheria za Australia na karibuni nchi zzote za magharibi haziruhusu ndoa za
mitala lakini Sheria zipo pale kwa ajili ya wanajamii wazitende, na ndoa za
mitala hazijakatazwa kwenye Biblia. Zaidi tu ni kwamba zimeruhusiwa.
Mfano huu
umetumiwa sio kwa nia ya kutia moyo ndoa hizi ila ni kwa nia ya kuonyesha jinsi
sheria inapofanya kazi na kudumu kwenye ubunifu au tunzi mbalimbali za jamii ya
wanadamu. Kutakuja kipindi ambacho jamii zatu haitakuwa imara na Mungu
atashughulika na sisi moja kwa moja na kuziharibu njia. Ataruhusu
tushughulikiwe na mataifa, kwa baraka na laana zilizoandikwa kwenye Kumbukumbu
la Torati 28 (soma jarida la Baraka na Laana (Na. 75) [The Blessings and the Curses (No. 75)].
Wakati watu wetu
wanapokufa kabisa kati ya mamilioni (Isaya 3:25) na wanawake wanapotembea wakifanya
uzinifu na watoto haramu waliozaliwa nje ya ndoa kwenye mataifa yetu, watazishika
pindo za nguo zao na huku wakiwaambia wakisema: "Mtuondolee aibu yetu"
(Isaya 4:1). Haya ni Maandiko Matakatifu, na Maandiko Matakatifu hayawezi
kutanguka (Yohana 10:35).
Mambo haya yote
yanafanyika ili kutimiliza makusudi maalumu ya Masihi na kuzifanya jamii za
wanadamu ziende sawasawa na mapenzi ya Mungu. Na hii ndiyo sababu iliyopelekea
tupewe Torati.
Tutazitathmini
hizi Heri na kwenda moja kwa moja kwenye lengo lililoko nyuma yake na kuuona
uweza inayokuwanayo.
Heri ya kwanza inasema: Heri
walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Huu ni mkanganyo
wa wazi. Sisi tu maskini wa roho kwa hiyo tunakwenda kuurithi Ufalme wa Mbinguni.
Wakati kwamba kila tulichofundishwa kinasema kuwa tunapaswa kuwa matajiri wa roho.
Inatupasa tufanye kazi na kujishughulisha ili kutimiliza na kuishi katika roho
na kukua katika roho. Je, mambo haya yanawezekanaje? Je, inamaana kuwa tu kwamba
kuwa maskini war oho kunamaanisha
kuwa ni umaskini kwa maana ya udhaifu au uduni katika roho? Hapana, haimaanishi
hivyo. Kuwa maskini wa roho kunamaanisha kwamba ni sisi kujitoa kikamilifu na
kwa hiyari yetu kuwa sadaka kwa kadiri tuwezavyo kwa jirani zetu, ndugu zetu—na
hapo tunakuwa maskini kwa hiyari kwa
kujinyenyekeza na kuachilia mambo yetu yenye faida kwa watu tunaowatumikia.
Inamaana kwamba utajiri, kama ulivyo tu peke yake, sio kigezo cha mtu kuonekana
kuwa ni mteule. Mtazamo huu unapingana moja kwa moja na injili zinazohubiriwa
siku hizi zinazosisitiza utajiri na mafanikio kuwa ni kigezo cha imani.
Katika miaka ya
hivi karibuni, mambo mengi sana ya namna tofauti yamekuwa yakifundishwa na
Kanisa la Mungu kuwa kuna injili inayosisitiza utajiri, mali na mafanikio –
ikiwa ni falsafa ya kwamba magonjwa
yanatokana na dhambi na kwamba mafanikio
ni matokeo ya utakatifu. Imani au fundisho la kwamba magonjwa yanatokana na
dhambi yanatokana na imani ya Kishamanism; na ni mafundisho potofu nay a
kizushi. Ni mafundisho ya mapepo na tunakutana na mafundisho hayo kwenye
makabila ya watu waliorudi nyuma wa jamii ya Kiasia wanaoishi chini ya imani ya
kishetani ya kimapepo. Magonjwa yanayoila hii dunia yametokana na athari
zilizotokea takriban miaka 6,000 ya uasi dhidi ya Sheria au Torati ya Mungu.
Baadhi yao, kama
sio wote, miongoni mwa watu wetu kwa kiasi fulani wanaathari za kijenetiki kwa
sababu ya maasi haya. Baadhi ya watu wanalazimika kwa njia ya ajira hadi kuwa
kwenye mazingira yanaayowafanya waugue na wanahitaji kusaidiwa na kuonewa huruma.
Watu wetu makanisani mwetu siku za huko nyuma walikuwa madaktari. Waliieneza
Injili kwenye bara lote la Ulaya walitembelea majumbani, wakiwaponywa watu na
kuwasaidia kwa namna mbalimbali. Magonjwa na maradhi hayakuchukuliwa kuwa ni
matokeo ya dhambi na wazee wetu hawa wa imani waliohudumu huko nyuma. Bali waliwapenda
watu walijaribu kuwaokoa. Waliwaponya, kuwalisha, kuwavalisha nguo na waliyahatarisha
maisha yao ili kuwaokoa kwa kuwahubiria neno la Mungu. Walikubali kutoa mali
zao, kujitoa sadaka na kujikana, na walisafiri ulimwenguni kote wakitembea kwa
miguu, na walijinyenyekesha na kuyatoa maisha yao na maisha yao mazuri
wakayatoa kwa faida ya wengine ulimwenguni. Walijaribu kuwaleta watu wote kwa
Kristo, wakifanya hivyo kutokana na upendo waliokuwanao kwa watu wote na
kujitoa kikamilifu na huku wakizidi kupendana kama ndugu.
Watu wetu
waliyatoa maisha na nafsi zao kikamilifu kwa ajili yaw engine kwa kipindi cha
karne kadhaa. Mwenye makanisa mengi ya karne ya kwanza walikuwa na ushirikiano
mwema. Mitume waliweka utaratibu ambaokwamba walitoa fedha zao zote kwenye
mfuko wa ushirika wao ambao ni kanisa na waliishi pamoja.
Hii haikutokana
na jambo lingine lolote. Kama tutajaribu kufanya hivyo kwenye karne hii basi
watu wengi wangeondoka na kuachana kabisa hata kabla hatujaanza. Tumesikia
ikisemwa, wapende ndugu zako wapendwa
wote, lakini kuna wengine unapaswa kuwapenda kwa mbali. Mtazamo kama huo unonyesha
kuna matatizo makubwa sana ya kiroho, sio kwa hawa wanaosema hivyo tu, bali na
wale waliosababisha kutokea mawazo haya. Watu wengine hawajui matokeo
yanayoletwa na miendendo yao.
Kwa hiyo, tunaona
hapa kwamba fundisho la kuwa maskini wa roho halimaanishi kuwa duni au kuwa na kiwango cha chini kiroho. Bali
inamaanisha mtu kuwa maskini kwa kuweka maslahi yaw engine mbele, na kazi za
Yesu Kristo kuiweka juu zaidi ya maslahi yetu binafsi.
Heri ya pili inasema:
Heri
wenye huzuni; Maana hao watafarijika.
Ni wapi basi
tunapotapa wazo la kujlia kwa kuomboleza? Kwani kulia huku kwa kuomboleza ni
nini? Je, kulia kwa kuomboleza kunawezaje kuwa baraka? Kulia na kuomboleza
kunatokana na kupotelewa na kitu; au sivyo? Kwenye Ezekieli 9:4 tunapata wazo
la maana yake. Kristo kwa kweli anaendeleza tu dhana hii ya kile alichokuwa
anakisema Ezekieli. Tunaanza kutoka aya ya 1. Kichwa chake cha somo ni Mauaji ya Kuwachinja Waabudu Sanamu.
Ezekieli 9:1-11 Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni
mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na
kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake. 2 Na
tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande
wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja
kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni.
Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba. 3
Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa
kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule
aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. 4 Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya
Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia
kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. 5
Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma
yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; 6 Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na
watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama;
tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele
ya nyumba. 7 Akawaambia, itieni nyumba
unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, enendeni. Wakaenenda,
wakapiga-piga katika mji. 8 Tena ikawa,
walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema,
Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu
yako juu ya Yerusalemu? 9 Ndipo akaniambia,
Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao
mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, Bwana ameiacha nchi hii, naye Bwana
haoni. 10 Nami, jicho langu halitaachilia,
wala sitaona huruma; lakini nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao. 11 Na tazama, mtu yule aliyevaa bafta, mwenye
kidau cha wino kiunoni, akaleta habari, akisema, Nimefanya kama ulivyoniamuru.
Mchakato huu unaanzia
kutoka kwa walio na vyeo vya juu sana vya wateule hawahawa na unaendelea kwa
kushuka chini hadi kwa watu wetu. Tumepigwa mhuri ili tulie na kuombolea kadri
tuwezavyo na kupiga kite kwa huzuni, tukilia na kutubu na kushinda. Wale ambao hawatalia na kuomboleza na
kutubu watauawa: wanaume, wanawake na watoto. Huu sio ujumbe kwa wenye dhambi
na waovu. Taifa la Australia, kwa mfano, litatiishwa na kunyenyekeshwa kwa
upanga. Mji wa Sydney utatubia maadhimisho yake ya kikuu yake ya kipagani ya
Mardi Gras. Mambo haya ni machukizo machoni pa Mungu na wataondolewa mbali
nazo; na siyo mbaya kusema kwamba neno la Mungu linasimama. Watu hawa wanayaita
mambo mema kuwa ni mabaya nay ale mabaya huyaita mema. Ni machukizo machoni pa
Mungu na yanachoma mianzi ya pua yeke. Mungu atawaacha waangamizwe.
Kazi na wajibu
wetu ni kuwaonya watu na kuzumbea kuahirisha kufanya hivyo kunamaanisha kuwa
watoto watakufa. Na hii nd iyo maana tunabarikiwa kama tutalia na kuombolea na
kuhuzunika na kunyongeka. Lakini tunapaswa kufanya hivyo kwa matendo, na sio
kwa kujionyesha. Tunapaswa kuwa kimbelembele kwa kile tunachokifanya, na
tusitende. Sio ni suala la kuonyesha kuhuzunika kwetu tu. Inatupasa tuondoke na
kutoka hapo na kwenda kuwaambia. Inatupasa kutoa wito wa kutubu kwenye taifa
hili – libadili mioyo ya mababa, au vinginevyo nchi hii itakufa. Huu sio
mkosolewo wa kurithi tulionao lakini ni kuyapigia mstari tu matatizo muhimu. Uwezo
wetu wa kuishi kama taifa na idadi ya watu wetu kwenye Milenia unategemea kwa
kile tunachokifanya sasa. Hata idadi ya Wamataifa inategemea ni kwa kiasi gani
tunafanya vizuri kazi yetu. Tuna zana chache na kuna watu wengi sana wamebalia
na makosa ya zamani, kwa kuzembea na kujihesabia haki mwenyewe.
Heri ya tatu
inasema: Heri wenye upole; Maana hao
watairithi nchi.
Inakanganya
kusema tunapaswa kulipa changamoto wazo hili na ulimwengu, lakini je, tunapaswa
kuwa wapole? Je, kuwa mpole
maana yake ni nini? Je, upole ni dhambi au uhdaifu? Hapana! Upole sio ugoigoi
au udhaifu.
Musa alikuwa mpole
kuliko watu wote, lakini hakuna, kwa kuonyesha fikra yoyote, aliweza kusema kuwa
alikuwa dhaifu. Kwa jinsi hiyohiyo, nguvu haitokani na wala haielezeki kwa namna
ya, madai ya kimapokeo au nguvu za kutumia silaha, au matumizi ya wadhifa au
cheo, au kwa kutumia mamlaka. Nguvu hazimaanishi kuwa na nafasi ya kiwadhifa na
kutumbua au kutoa nje matumbo ya mtu aliye chini yetu. Nguvu inasababisha vifo
vya watu wetu. 1Wakorintho 13 ni sura ya upendo, kama tujuavyo wote. Kusaidia,
kwa maana ya upendo, unaofanyika bila masharti hujulikana kama ni upendo wa
agape ambao ni wa Mungu. Ni suala la kimapendo ambalo limenenwa kinywani mwa
Kristo alipokuwa mtini akisulibiwa wakati aliposema: “Baba wasamehe maana
hawajui watendalo”. Upendo huu ni upendo wa aina aliyousema
Stefano midomoni mwake walipokuwa wanampiga kwa mawe hadi kufa. Alionyeshwa
maono ya Ufalme yakimjia kupitia upendo huu. Jambo hili limeelezwa kwa kina kwenye
swali lililo kwenye Heri mbili za mwisho.
Kutoka kwenye 1Wakorintho
13 tunaweza kupata wazo la kile alichokuwa anakisema Kristo kwa namna ya kusema
juu ya upole huu na kuirithi Nchi. Ni aina ya upole unaotokana na kujifanya
kuwa mdogo na chini ya wapendwa ndugu zetu.
Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
Kunapaswa kuwa na
mwonekano wa wazi ya majukumu yetu. Ni maneno matupu, ni kwa kupayukapayuka tu,
ndiyo ya kuongelea kuhusu imani yetu na kutofanya lolote. 1Wakorintho 13 inaongelea
uweza wa kinabii, ili kuelewa siri na uelewa. Inaelezea kuhusu imani inayoweza
kuondoa milima. Hata hivyo, kama tukikosa upendo ambao unaendana na imani yetu
umekosa malengo, kwa kuwa nguvu zote za Roho Mtakatifu zimetolewa kwa watu hao
wanaoweza kuelezea kwa upole – kwa kupendana kila mtu na mwenzake. Hatujapewa
Roho kwa umbo lolote lile au nguvu hadi tujue jinsi ya kuielekeza kwa kila
mmoja kwa upendo.
Tutapewa karama
za kutosha zitusaidie. Kiwango cha chini cha upendo tunachokionyesha, ndipo
kumzima Roho Mtakatifu itakapokuwa. Kama hatutashinda udhaifu huo, tutakapompoteza
Roho Mtakatifu.
Tumewaona
watu watu wakijaribiwa kwenye uelewa wao juu ya Uungu. Wale wasiopatana na
jaribio hili kama wanavyostahili na kufanya maamuzi mabaya, hupoteza kile walichokuwa
wakikijuua tayari.
Hatua ya kwanza
ni Amri Kuu ya Kwanza (imeelezewa kwenye amri nne za kwanza) ambayo ni: mpende
Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote na kwa roho yako yote.
Upole ni aina ya mwenendo unaotuama kila kitu kwenye usaidizi wa Amri ya Kwanza.
Watu wa Mungu
wameachana na ndoa zao, ndugu zao, mambo yao ya usitawi, mali zao, na kila kitu
kwenye Kanisa. Kila mmoja wetu ameitwa ili atoe sadaka kitu fulani. Kila mmoja
wetu ameitwa na ameitwa kutumikiana ili tuweze kuendeleza na kukuza upendo na
nguvu katika Roho Mtakatifu. Tutairithin nchi kwa kuwa Bwana wetu Yesu Kristo,
atapewa, na amepewa uweza ule na ufalme na mamlaka akiwa kama Nyota ya Asubuhi.
Nasi tutapewa uweza huu pia, kama kiti chake cha enzi (Ufunuo 2:26-28;
3:12,21). Tutafanya hivyo kwa ajili ya asili yake au nafasi ya kujinyenyekesha
na kuachilia faida na nafsi zetu, na kutumikiana.
Ni lazima
tuendeleze mambo haya kwa
kiwango cha juu sana tuwezavyo. Wakati mwingine inatokana na shughuli za
kutafuta mahitaji ya wengine. Ni namna ya kuonyesha upendo wetu ili kutegemea
kupata mahitaji ya wengine. Tuna familia kubwa na tunapaswa kuyaona mahitaji ya
kila mmoja wetu hata kabla mtu hajayaeleza. Kwa kufanya hivyo kutaondoa hali ya
kupoa kwa upendo kama dunia inavyoona na kufanya kuwa ni tunda la wajibu
unaoendelea. Ni kipimo cha kuonyesha upendo, kuonyesha kuwa tun ajali. Kuona na
kutarajia kitu fulani ni zawadi isiyoelezeka, kwa kuwa tunawaondoa ndugu zetu umuhimu
wa kuweza kuuliza. Hakuna mmoja wetu anayestahili kuuliza kitu chochote.
Kinachofuatia kutokana
suala la upole, tunaendelea kwenye suala la mapigano. Bwana wetu ana uweza wa
kuamua kutuokoa au kutotuokoa. Anauwezo wa kuamua kutupeleka utumwani au
kutotupeleka utumwani. Ni kwa namna hiyohiyo, anaweza kuwatendea wale wote
wanaotegemea nguvu zao na wasimtumikie Mungu kwa mioyo yao yote na nia zao zote
na kwa roho zao zote, hatimaye watashindwa. Watakwenda ama kwenye utumwa wa
kihalisi wa Israeli, au kwenye ule utumwa wa Ufufuo wa Pili.
Ufufuo wa Pili ni
shule ya uadibisho ambayo kwamba watu wote hujifunza kumpenda Mungu kwayo na
wataona matokeo ya kile wanachokifanya. Bwana wetu alishalipa gharama ili
kutuweka huru sisi kutokana na hayo na kutupa sisi fursa ya kuongoza. Tunaongoza
kwa kupitia upole na uvumilivu wetu dhidi ya majaribu.
Kwenye Ufunuo 6,
tunaona jinsi dhana hii inavyoendelea. Mihuri hii imeelezewa kwa kina kwenye majarida
ya Mihuri Saba (Na. 140) na Baragumu
Saba (Na. 141) [T he Seven Seals (No.
140) and The Seven Trumpets (No. 141)]. Hapa tunaona suala la kushindwa kuwa mpole. Kile
kinachotokea kwenye mchakato wa kugongwa muhuri ni kwamba mihuri hii inatokana
moja kwa moja na hizi Heri. Mihuri hii ni matokeo ya wazi ya kushindwa kuishika
Amri Kuu nay a Kwanza, na Amri Kuu ya Pili ambayo ni kumpend jirani yako kama
unavyojipenda wewe mwenyewe. Kwa pamoja, hizi zimefungamanishwa kwenye Amri
Kumi za Mungu (sawa na yanavyosisitiza majarida ya Torati ya Mungu (N. L1) na Mlolongo wa Majarida
ya Torati au Sheria (Na.252-Na. 263) [T he Law of God (L1) and the Law series (No. 252-No. 263)].
Mhuri wa kwanza
unaendelea kutoka kwenye dini ya uwongo – kutoka kwenye mfumo unaochukua
mbadala wa kiserikali ulio juu ya misingi na utaratibu wa kibiblia na Torati ya
Bwana na Mungu wetu.
Mihuri hii
imefunguliwa ki makamio kutokana na uvunjifu wa Sheria za Mungu na kuzikataa
kwao Heri zilizotolewa.
Kama
zilivyovunjwa, mhuri wa kwanza umefunguliwa kwenye dini ya uwongo kwa kuwa
haina upole. Hakuna nia wala haja ya kujinyenyekeza na kuachilia matakwa na
faida za kibinafsi na kuwasaidia watu wote. Kwa kuwa dini ya uwongo
iliyosimamishwa pale haina nia moja ya kumtumikia Mungu Mmoja Wapekee na wa
Kweli na maamrisho ya Torati yake. Mafarakano yanayosababishwa na mifumo ya
vyeo vya uongozi ya kidini ya vikundi vya kidola hulazimisha hali ya kukosa
usawa ambao unaendeleza tena hali ya kushindwa kufikia vigezo vilivyo kwenye
Heri mioyoni mwetu. Kupenda kunageuka kuwa tamaa mbaya ya ngono, ambayo
inapelekea migongano. Hatimaye
kunatokea Vita. Kutoka vita huja magonjwa, vifo na njaa. Hii ni mihuri minne ya kwanza na ni ya mwisho. Kama
moja iliondoka na nyingine huondoka pia.
Kinachofuatia
hatimaye, ni kwamba wanavunja mhuri wa tano wa mateso ya kidini, kwa kuwa kama
tukiwa na dini ya uwongo, tunakuwa na pande mbili za imani na tunakuwa namungu
wa uwongo. Tunapokuwa na dini ya uwongo tunakuwa na muwako wa tamaa mbaya za
madaraka. Tukikosa upole, tutateseka.
Mhuri wa tano ni
matokeo ya mateso yanayoinuka, yanayofuatia hali ya ukosefu wa upole, na
unatokana na hamu ya maumivu na kuwadhuru wale wasiokubaliana nasi.
Mhuri wa sita ni
ishara za mbinguni. Zitaonyesha
kuwa Kriso atashughulika na mambo na kuingilia mara moja kwa utaratibu endelevu.
Kwa ishara,
Kristo anaonyesha kuwa ataukomesha mfumo uliopo hapa duniani kwa kutumia mabavu
haya haya na tama na mamlaka ya watu wale ambao watapingana na kupigana.
Katika kipindi
kile wote wataletwa kwenye Bonde la Kukata Maneno na kuangamizwa kwa nguvu za silaha
zao wenyewe. Kristo hatawaua, kwa maana kwamba atafanya hayo kwa maamrisho ya
moja kwa moja ya Mungu ili kuwaangamiza tu na hatimaye kuwaua watu hawa.
Wanaruhusiwa kuendelea na dhambi zao, ambazo zinatokana na kushindwa kwao
kuzishika kanuni za Heri. Watauana, mwanaume, mwanamke na mtoto, kwa mamilioni,
ambayo karibu yataangamiza sayari hii yote.
Dunia
inahamasisha itikazi za ukabila. Watu wanaoongea Kiingereza pia wanahamasisha
kwa namna hii. Mawazo ya watu wetu yameharibiwa kimpangilio wa kihila kwa
kutumia maonyesho ya sinema za Hollywood na vyombo vya habari, kwa kuonyeshwa
matukio ya machafuko sambamba na matukio mengine yasiyojenga fikra zetu.
Ulaya
imejitangazia vita kupigana wenye kwa wenyewe takriban mara mbili katika karne
ya 20 kwa kitendo cha kiwendawazimu mkubwa. Baadae
ikafuatiwa na kipindi cha Vita Baridi cha miaka 50 kilichotokea kama matokeo ya
Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Kwa sasa inakaribia kulipuka tena kutokana na
ubabarianism au ushenzi na udhulumaji. Imekuwa na itikadi ya kibaguzi tena.
Watu wa jamii ya kiaborigini wanashambuliwa. Kile kinachoonekana kama usafishaji wa
kimaadili na ubabariani wa kikabila uliofanywa kwa vita vya Balkani ni dalili
tosha inayoashiria Vita Kuu ya Tatu ya Dunia, kama Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe
huko Uhispania ilivyokuwa kiashirio cha Vita Kuu ta Pili ya Dunia. Kushindikana
kwa uwezo wa kisiasa wa kukabiliana au kumthibiti Mnyama kumesababisha kuwepo
kwa mlolongo wa matukio yanayoleta mhemko. Watu hawa wanapelekeshwa na roho ya
kupenda mali na utajiri na misisimko, kupitia tama zao mbaya, kupenda kwao vyeo
na umaarufu, na majigambo, mambo ambayo yatawaangamiza wenyewe na sayari yote
hii.
Wapole watairithi
Nchi kwa kuwa hakutakuwepo na mtu atakayesalia akiwa hai. Kristo ataingilia
kati uwendawazimu huu na kukifupisha kipindi hiki kwa ajili ya wateule kwa
Mpango wa Mungu (Mathayo 24:22).
Wakati wa kila
awamu ya kufanyiwa kazi kwa mihuri hii saba, dunia ingeweza kutubu. Kwenye
mhuri wa saba kuna baragumu saba, halafu vitasa saba, na vitasa hivi saba
vinaiwakilisha ghadhabu ya Mungu. Na katika kila kimoja inasema: na wala hawakutubu (Ufunuo 16:9). Wakati
wa kipindi hiki hakuna mtu atakayeruhusiwa kuingia Hekaluni mwa Mungu hadi kutokee
mapigo saba ya tauni na hitimike (Ufunuo 15:8). Kwahiyo, pasipo tona hakuna
wongofu au wale wasiotubu hakuna atakayeongoka.
Kwene kila moja
ya mapigo hayo, Mungu ataruhusu kuwepo na mahali pa salama pa kukimbilia. Ni
sawa tu na kama tunavyokuwa na mtu aliyeangukia kwenye kitanzi, na kisha
tukasema: “Je, umeumia?” naye akasema “Hapana!” kwa kweli, mwanadamu umejiweka
kwnye kitanzi na kinamyonga taratibutaratibu hadi kufa, jeraha la kujitesa kwa
makusudi. Mungu anasema kwa ukali sana kwamba “usijipige risasi ya mguunimwako
wewe mwenyewe, itakuumiza”, kwa kuwa hatujipigi risasi miguuni mwetu kwa mapigo
endelevu.
Heri ya nne
inasema: Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
Hamu ya namna hii
ni ya kuwa na njaa na kiu ya kumjua Mungu. Zaburi 119 inaonyesha wazo lililo kwenye
Torati, na haki na utauwa unaotokana na Sheria za Mungu. Wateule wamejazwa Roho
Mtakatifu lakini kumekuwa na bidii kwenye hali yao ya njaa na kiu chao. Hawali
chakula cha kimwili; bali wanakula chakula cha kiroho.
Majarida yenye
vichwa vya maneno Roho Mtakatifu (Na. 117) na Tunda la Roho Mtakatifu (Na. 146) [The Holy
Spirit (No. 117) and Fruit of the Holy Spirit (No. 146)]
inapasa yaonekane kuhusiana
na Heri hizi na kujazwa na Roho. Ni
Roho Mtakatifu na matunda yake yote yaliyoelezewa kwenye 1Wsakorintho 13, na
kwenye maandiko menhineyo yote yanayomlenga Paulo, inaonyesha kuwa ni kujazwa
na Roho tu ndiko kunakochukua mkondo wake.
Heri
hizi0zinafungua mlango, na kunafuatia nyingine nyuma yake kwa kiwango tuwezacho
ili tuonekane kuwa ni chumvi ya Dunia na kuwa ni nuru zaa Hekalu. Tunaweza
kufanyika kuwa nuru kwa Wamatgaifa.
Hata hivyo, sio
watu wengi miongoni mwetu. Chumni hutiwa tu kwenye chakula au ni sehemu ndogo
kwenyekiungo au kiambato. Wazo hilohilo linakutwa kwenye habari za Gideoni naa
wale 300. Sisi tu wachache; tumeitwa mmoja
kutumika mjini, na wawili wa kutoka kwenye familia (Yeremia 3:14).
Yeremia 3:14 Rudini, enyi watoto wenye
kuasi, asema Bwana; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji
mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni;
Na hii ndiyo sababu
kuna watu wachache sana wanaoielewa kazi kwa kipindi hiki cha mwisho. Mungu
anamwaga Roho wake kwa wanadamu kwanza kabisa kupitia kwa wateule wake (Matendo
2:1-33) na hii inaendelea kwenye Siku hizi za Mwisho (Yoeli 2:28-32; Matendo
2:17-21).
Eliya alidhani kuwa
alikuwa ni mtu wa mwisho aliyebakia. Kwa uchungu alikuwa aksema kwamba: “hakuna
mwingine aliyebakia. Lakini ee, Mungu wangu, niko peke yangu hapa; Mimi ni wa
muhimu”. Alikuwa na upweke na
hali ya upweke na kushuhudia ubatili kwa ajili ya majukumu ya kazi au huduma
yake. Paulo alimuua Stefano, lakini yeye alisema, wakati inapotokea hali ya chini ya – kutokulaumika (Wafilipi 3:6). Aliandika
kwamba baada ya kuongoka kwake na baada ya kuuawa kwake Stefano! Kulikuwa na
mtu mmoja mnyofu, Yesu Kristo na sisi sote ni wenye dhambi. Kristo, hata hivyo,
alisema hakuna aliye mwema ila ni Mungu peke yake (Mathayo 19:16-17). Wote
wamepungukiwa na utukufu wa Mungu, Paulo alihitimisha. Dhambi ni dhambi na
inaendelea kkutoka kwenye dhambi na uovu wa mawazo na moyoni. Wateule wengine
waliomtangulia Masihi, kaka vile wazazi wa Yohana Mbatizaji, walikuwa watachaji
wa Mungu na wasiolaumiwa kutokana na desturi za wakati ule (Luka 1:6). Yatupasa
sote kuwa ni watu tusioshitakiwa neno baada ya kuongoka kwetu (1Wakorintho 1:8;
Wafilipi 2:15; 1Wathesalonike 5:23; 1Timotheo 3:2,10; 5:7; Tito 1:6,7; 2Petro
3:14).
Paulo, hata hivyo,
alikujakuelewa baadae kwamba alikuwa ni mwenye dhambi mkubwa (Warumi 7:1-25).
Baadhi yetu
tunatenda dhambi mioyoni mwetu. Dhambi nyingine ni za kweli na na za kukusudia. Lakini tumapimwa kutoka mioyoni
mwetu na sio kwa yale tunayoyafanya tu peke yake. Hili ni wazo la kusikitisha
na la kutisha. Moyo unatoa fursa kubwa wa kutenda dhambi. Mara nyingi
tunashangazwa na kwango yanachowaza mawazo yetu. Vyombo vya habari vya leo
zinatoa fursa ya kuwaza na kutenda dhambi ya mawazo ambayo yaliendelea kutoka
siku za zamani huko nyuma.
Swali hili hatimaye
linaendelea hadi kwenye suala la rehema. Sio jambo la bahati mbaya kuwa neema
inafuatia baada ya kuwa na njaa na kiu ya haki kwenye utaratibu huu wa hizi Heri.
Yatupasa kuwa wapole ili tupate au tustahili kupata, kile tunachotakiwa kukijua
na kwamba tunamhitaji Roho Mtakatifu, neema ya Mungu na sadaka ikomboayo ya
Kristo. Tunahitaji kujazwa Roho ili tuweze kuzinyenyekeza nafsi zetu. Ubatili
wetu na kujiamini kwetu vinakuwa vimeshushwa na kumtegemea Kristo. Baadhi yetu
kwa hakika tunahitaji kunyenyekeshwa kimwili ili tuweze kuingia kwenye Ufalme
wa Mungu. Baadhi yetu tumeandikiwa kujeruhiwa na kupata hasara ili kuweka mawazo
yetu mahala ambapo tunaweza kushughulikiwa na Mungu mwenyewe. Kila jambo
linafanyika kwa nia nzuri kwa wale wanaompenda na kumtumikia Mungu, na kwa wale
walioitwa kwa makusudi yake (Warumi 8:28).
Heri ya tano ni: Heri wenye rehema; Maana hao watapata
rehema
Zekaria 7:8-10 Kisha neno la Bwana likamjia Zekaria,
kusema, 9 Bwana wa majeshi amesema hivi, ya kwamba, Fanyeni
hukumu za kweli, kila mtu na amwonee ndugu yake rehema na huruma; 10 tena msimdhulumu mjane, wala yatima, wala mgeni,
wala maskini; wala mtu awaye yote miongoni mwenu asiwaze mabaya juu ya ndugu
yake moyoni mwake.
Limekuwa ni
fundisho linalofundishwa na makanisa ya Kiutatu au Utrinitariani kwamba yatuna haja ya kuishika imani
pamojja na watu wasiokuwa wa dhehebu letu. Walifundisha kwamba tuna namna
iliyotofauti ya kuwashughulikia watu kama tutakuwa wa imani moja. Kwa masuala
ya uaminifu na ya wajane na yatima na masikini kwa mujibu wa Torati, jambo
ambalo sio sahihi wala sio kweli. Mungu hanaupendeleo wala haangalii sura ya
mtu (Matendo 10:34).
Watu shirika,
Wamataifa, wanatuamini kwa kuwa hatuna upendeleo wala hatumuonei huyu na kumchukia
Yule, kwa mujibu wa amri za Torati. Hukumu ya Torati itatoka na kuendelea mbele
ikikatiza ulimwengu huu pasi kujali madaraja ya watu, rangi ya ngozi aliyonayo
mtu, au daraja la maisha aliyonayo mtu kwenye jamii.
Zekaria 7:11-13 Lakini hao walikataa kusikiliza, wakageuza
bega lao, wakaziba masikio yao ili wasisikie. 12 Naam, walifanya
mioyo yao kuwa kama jiwe gumu, wasije wakaisikia sheria na maneno ya Bwana wa
majeshi, aliyoyapeleka kwa roho yake kwa mkono wa manabii wa kwanza; kwa sababu
hiyo ghadhabu kuu ikatoka kwa Bwana wa majeshi. 13 Ikawa
kwa sababu alilia, wao wasitake kusikiliza; basi, wao nao watalia, wala mimi
sitasikiliza, asema Bwana wa majeshi.
Kunakwenda kuwa
na muda ambapo Bwana wa Majeshi hatakuwa anasikia. Hatakwenda kuyasikiliza
mataifa yatakapomlilia na itashughulikiwa kisawasawa na kwa haki wakati ambapo yatayageykia
mataifa mengine yatakayopewa mioyo ya jiwe ili yatushughulikie.
Zekaria 7:14 Lakini
nitawatawanya kwa upepo wa kisulisuli, katikati ya mataifa yote wasiowajua.
Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa ukiwa nchi baada yao, hata hapakuwa na mtu
aliyepita kati yake, wala aliyerudi; maana waliifanya nchi iliyopendeza sana
kuwa ukiwa.
Maangamizo na
vita vitafuatia kutokana na kushindwa kulishika kwa bidii neno la Mungu.
Zekaria 8:1-6 Neno la Bwana wa majeshi likanijia, kusema, 2 Bwana wa majeshi asema hivi, Mimi nina wivu kwa ajili ya Sayuni, wivu mkuu, nami nina wivu kwa ajili yake kwa ghadhabu kuu. 3 Bwana asema hivi, Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji wa kweli; na Mlima wa Bwana wa majeshi utaitwa, Mlima mtakatifu. 4 Bwana wa majeshi asema hivi, Wazee wanaume na wazee wanawake watakaa tena katika njia za Yerusalemu, kila mtu ana mkongojo wake mkononi, kwa kuwa ni mzee sana. 5 Na hizo njia za mji zitajaa wavulana, na wasichana, wakicheza katika njia zake. 6 Bwana wa majeshi asema hivi, Ingawa hili ni neno lililo gumu mbele ya macho ya mabaki ya watu hawa katika siku hizo, je! Liwe neno gumu mbele ya macho yangu? Asema Bwana wa majeshi.
Inaonekana kuwa
kwa mwanadamu haiwezekani, lakini sio kuwa haiwezekani hivyo pia kwa Mungu.
Mungu anaweza kumuinulia watoto Ibrahimu kutoka kwenye mawe yaliyoko nyikani,
na atafanya hivyo. Tupo kwenye kujengwa tayari kwa kuanzisha kipindi na utawala
wa Milenia. Haya yote yanahusiana na Masihi na kuuanzisha Ufalme wa Mungu.
Ndipo suala la haki na rehema linafuatia kwenye uwezo wetu wa kushughulikia na
kusaidiana kila mmoja wetu na mwingine kwa njia ya haki.
Heri ya sita ni: Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona
Mungu.
Kwa kuvionyesha
vigezo na viwango hivi katika Roho Mtakatifu kama watu tuliokwisha kubatizwa
katika Roho Mtakatifu na kama watoto tuliozaliwa wa Mungu, ndipo tutaupokeo
mhuri wa Mungu. Kwa kupokea kwetu mhuri huu wa Mungu tutaweza kuzipokea nguvu za
Roho na tutamuona Mungu. Paulo aliandika kwamba hakuna, wala kwa umbo la
kimwili, aliyewahi kumuona Mungu na hatakuwepo mtu wa namna hiyo kamwe (1Timotheo
6:16). Na hii ndiyo dhana mojawapo ya kuwa Paulo na Yohana waliifanyia kazi;
kusema kwamba hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu, kwa kuwa Mungu ni uweza wa
kiroho. Tunapaswa kuwe kwanza kwenye umbo hili la kiroho ili tuweze kumuona
Mungu, na hakuna mtu anayeweza kuwa wa namna hiyo. Ni umbo ambalo litawezekana
tu kuwanalo baada ya ufufuko wa wafu.
Heri ya saba inasema hivi: Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana
wa Mungu.
Kupatanisha ni
mojawapo ya kuonyesha uwepo wa Roro Mtakatifu. Kuleta amani ndiyo njia atakayoitumia
Yesu Kristo katika kuitawala hii dunia. Utawala wake utaiunganisha dunia yote
na kunai mamoja kwa maongozi ya Mungu. Imani hii ya kuamini kuwa Mungu ni Mmoja
iitwayo Umonotheism haimaanaishi kuwa Mungu ni mmoja lakini ana vichwa vitatu,
hapana. Bali Umonotheism ni itikadi inayoamini kuwa Mungu ni Mmoja, kwa kuwa
kila mtu, yaani Yesu Kristo na wengine wote akiwemo Roho Mtakatifu,
wamejishusha na kwa Mungu na kujidunisha. Wanayashiriki mapenzi ya Mungu, umbo
na uwezo wa kupenda na kupenda. Tumeitwa kwenye mfumo wa kushiriki na kuyatenda
mapenzi yake na maagizo yake na upendo wake. Yesu Kristo mwenyewe alisema:
"Chakula
changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, [nikaimalize kazi
yake]" (Yohana 4:34). Hili
linapaswa kuwa jambo muhimu kwetu. Na ndiyo maana imani hii ya Kimonotheism
ilivyo na inavyofundisha na kuamini. Sisi sote tuna Roho mmoja aliyetoka kwa
Mungu na ndiye anayemuwezesha na kumfanya Yesu Kristo kuwa wamoja na Mungu.
Ndiye anayetufanya hata sisi kuwa ni sehemu ya Mwili wa Yesu Kristo ambaye
ndiye kiongozi na kichwa wetu, kutufanya sisi sote tuwe ni sehemu ya Mungu
ambaye ni yote katiks yote na ndani ya
yote (Waefeso 4:6). Yeye siyo wa Utatu, wala hana nafsi nyingine zaidi
yake. Imani ya Utatu in atuzuia kwa kupingamiza sisi tusimuone Mungu na tusiwe
wamoja na Mungu, kwa namna ileile moja kama alivyo Yesu Kristo kuwa ni mmoja na
mshiriki wa karibu kwa Mungu. Imani ya Kibinitarianism inaendeleza makosa
hayohayo ya Watrinitarian ya hapo juu.
Ili kufanyika
kuwa watoto wa Mungu tunapaswa kuwa wapatanishi na tuonyeshe tunda la Roho
Mtakatifu. Je, tunawezaje basi kuwa wapatanishi? Ni kwa kuyaona na kuyajali
mahitaji na kuguswa nayo na kuwajibika. Kujinyenyekesha na kujishusha na
kuwainua ndugu zetu. Tunaweza kusema kuwa, “Siwezi kufanya kitu kwa ajili ya
ndugu yangu. Sipendi kufanya kitu
chochote nje ya mapenzi ya Baba yangu. Sipendi kufanya mambo zaidi kwenye Mwili
huu ambalo ni kanisa la Bwana wangu na kwa mapenzi ya Baba yangu. Kama Baba
ameamua kutoingilia kati, nami basi nitakufa kwenye mchakato huo, na basi hayo
ndiyo mapenzi ya baba yangu, lakini nitaishi na kuwa imara zaidi ya huko nyuma
na kinyume na watu walivyotarajia”.
Tunapatanisha
lakini sio kwa kuwa kunatishwa na mtu yeyote hapa duniani. Roho Mtakatifu ni
roho wa uweza na wa akili timamu – na siyo roho wa woga na ulegevu. Ni kwamba
baadhi yet utu wadhaifu kimwili na hatuwezi kupigana na kundi kubwa na kubeba
vitu vizito bali vidogo. Sisi sote tu dhaifu kimwili kwa namna fulani na nguvu
zetu zinatokana na uweza wa Mungu. Ukweli wa kwamba Kristo ametuweka kwenye
nafasi ambayo hatuwezi kuyashusha na kuyatiisha mataifa (kuangamizwa kabisa kwa
sayari hii) ni muhimu kwa kuwa kuna ndugu na wapendwa wengi ambao walihukumu
kimakosa na kwa upendeleo. Iwapo kama wangekuwa wanafanya maonyesho kungekuwa
na viumbe wengi wa aina isiyojamiiana na kungekuwa pia na maiti nyingi za watu.
Baadhi ya makanisa yangechoma moto kila kitabu kilichopo hapa duniani kama
alikuwa wanafanya maonyesho haya kwa kipindi cha miaka ishirini iliyopita; na
wengine wangependa bado kufanya hivyo. Wanawake wengi wangeuawa kwa kuchomwa
moto kwa ajili ya ulozi na kungekuwa na kiwango kidogo cha tabaka karibuni. Ni
kama tujuavyo sisi sote, miji mingi yenye matendo maovu nay a kikatili imewekwa
wakfu kwa jina la Mungu.
Kwenye Heri ya nane, Kristo alisema: Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana
ufalme wa mbinguni ni wao.
Mauji ya ushuhuda
ya Stefano kwenye kitabu cha Matendo ni ya muhimu sana. Stefano analiambia
Baraza la kidini kwenye Matendo 7. Mara tu baada ya kumaliza kusema hayo,
walikasirika sana na kusaga meno yao. Wakasema, Amesemaje? Kwenye Matendo 7:51 aliwaambia,
akisema:
Enyi wenye shingo
gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio
Walijua kuhusu
tohara ya mioyo maana yake. Nabii Isaya aliwaambia wote hawa kuhusu jambo hili na
walijua, hayakuwa mafundisho mapya. Kristo alikuwa amekwishaonekana kwa
kutambulishwa na manabii. Lakini hawakumsikiliza. Hiki ndicho alichokuwa
anakisema Stefano naye hawakupenda kuambiwa hivyo.
Katika Mathayo
23:31,37 na Luka 11:50, Kristo alimaanisha kabisa kuwauliza Mafarisayo kwa
kusema: "Ni yupi kati ya manabii ambaye mababa zenu hawakumtesa?" Haisemi hapa kwamba, "Nathani mliwafanyia
hivyo karibia wote". Bali aliwauliza
wamwambie ni yupi miongoni mwao ambaye hawakummtesa? Manabii wote pamoja na kila
aliyenena kwa Jina la Mungu waliteswa na bado wanaendelea kuteswa hata leo.
Waliwaua wale waliowatabiria juu ya ujio wa mwenye haki ambaye Stefano aliwaambia
kuwa wamemtaliti na kumuua. Aliwaambia akisema: "ninyi mlioipokea torati
kwa agizo la malaika msiishike" (Matendo 7:53). Ulikuwa
ni utambulisho wa Mafarisayo wa Kiyahudi. Walikuwa na Torati ila hawakuishika
wala kuiweka mioyoni mwao.
Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo,
wakamsagia meno. Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake,
akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono
wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu
amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba
masikio yao, wakamrukia kwa nia moja, wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe.
Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli.
Wakati wakiwa wanampiga mawe, Stefano
aliomba akisema:
Bwana Yesu, pokea roho yangu. 60
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii.
Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake.
Sauli alikkuwepo
akishuhudia wanapomuua. Nguo zake ziliwekwa miguuni mwake kwa kuwa yeye alikuwa
ni Farisayo aliyepewa wajibu wa kushuhudia au kusimamia mauji haya. Iliamriwa
kuwa mtu asiuawe kwa ushadi wa kuonwa na mtu mmoja tu au wakili mmoja peke
yake, ni lazima kuwe na ushihidi wa wengi. Wakati wa zama za Kushitakiwa watu
kwa kupinga mafundisho ya dini, mamlaka ya kiutawala iliweka kigezo kutoka kwa
Wawakilishi au Mahaliafa wa Papa. Lakini Sauli alimuua Stefano kwa kumrushia
jiwe la kwanza na ilikuwa mhalifu ni kazi yake na wajibu wake kumrushia jiwe la
kwanza. Kmsingi, shahidi ndiye alikuwa ntu wa kwanza kumrushia jiwe ili auawe.
Bila kufanya hivyo, wauaji wa Stefano wasingekuwa na udhuru wa kujitetea. Paulo
angekuwa ametubu kikamilifu kwa ajili ya jambo lile, badala ya kusema tu maneno
ya kutokuwa na hatia. Hakuwa safi na kwamba hakuwa na hatia kwa kuwa alikuwa
ameivunja Amri ya Mungu iyosema: Usiuwe.
Alimuua mtu asiye na hatia.
Hatimaye, kwenye Heri ya tisa, tunasoma: Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi
na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu..
Kristo aliweka
wazi hilo. Alifundisha kuwa mateso yatatokea na kumpata kila mtele. Watu
waliowatesa wateule ni wale walio kwenye mamlaka au tuseme ni wale walio kwenye
madaraka yanayojiita Makanisa au Makutaniko ya Mungu. Hii ndiyo imani ya
Kiyahudi lakini mateso makubwa yalikuja kutokea kwenye kile kinachoitwa leo
kama Ukristo mkongwe wa siku nyingi. Yanaendelea kwenye kwenye imani za Kiprotestant
na hata kwene Makanisa haya ya Mungu. Hawa ni wale wanaosema kuwa ni Wakristo,
na kumbe sio. Wale walionje ya Makanisa haya makongwe ya kale na huku wakidai
kuwa nayo ni Makanisa ya Mungu yanayowatesa wateule kwakuwa hawamjui Bwana wetu.
Isaya 66:5 anasema:
Lisikilizeni neno la
Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi,
waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe Bwana, tupate kuiona
furaha yenu; lakini watatahayarika.
Kwa kweli, wateule
wamekataliwa na Sinagogi ya wale wanaodhani kuwa kwa kufanya hivyo wanampendeza
Kristo. Wanafikia hata kiwango cha kujaribu kuwaua wateule. Ni nani aliyemuua
nabii Isaya kwa kile kinachodaiwa kuwa alichanwa vipande viwili kwa msumeno? Ilikuwa
ni makuhani. Ni nani alimpiga mawe hadi kumuua nabii Yeremia? Mapokeo
yanatuambia kuwa ni manabii wa Anathothi. Ni watu hawahawa wanaojiita kuwa ni
nguzo za nuru ndiyo wanaorudia kututesa sisi kwa kuwa hawamjui Bwana wetu.
Wanadhani kuwa wao ni watakatifu lakini hawana Roho Mtakatifu. Haishiki Torati
kwakuwa mawao ya kimwili waliyonayo ni adui wa Mungu (Warumi 8:7). Sio tu suala
la kwamba watu hawa ni maadui wa Mungu. Bila ya Roho Mtakatigu na kuwa karibu
na Mungu hatuwezi kuzishika Sheria na Amri za Mungu kwa kuwa zinashabihiana na
asili alisia ya Mungu. Mungu anachokisema na kukazia ni kwama: “Nimeweka
utaratibu. Nimewaumba watu ninyi na hamkuwepo hpo kabla ya mimi kuwapa Roho
wangu”.
Mlingano wake
unafanana sana na mfano wa kuwa na meli bandarini ikiwa na jenereta yake ikiwaka.
Taa zake pia zote zinawaka, lakini imesimama tu pasipo kwenda mahala popote na
ni mota ndogo ya usaidizi ikiwa inaunguruma. Mota kuu ikiwa hata haijawashwa.
Watu hawa hawawezi kujisaidia walichonacho. Hawajaweza hata kujifunga mikanda
yao. Wanaendelea kuwasha ile ndogo ya kusaidia na huu ni mfano unaofanana na
ulio sawa nayo. Ipo karibu nusu ya uwezo wake; hawana nguvu. Taa ziko
zimewashwa, lakini hakuna kinachoendelea. Ni wakati tunapoanza kuwasha injini
kwa Roho Mtakatifu na ndipo tunapoweza kufanya kazi. Na ndipo tunapoweza
kuondoka bandarini na kuendelea na safari tukienda mahala kokote katika mapenzi
ya Baba yetu.
Kusema
maneno yote maovu kinyume chetu kwa kutushitaki kwa uwongo kwa sababu ya imani
yetu kwa Kristo sio kitu kigeni. Iliyoko hapo juu ni mifano ya aina ya mashutumu
uliyoyapitia kwa kipindi cha zaidi ya karne kadhaa. Kwakuwa hatukuwa na uwezo
wa kuandika vitabu, basi hatujuweza kuwa na toleo la vitu vyetu kwa watu walionje
ya imani. Walichoma moto maandiko na vitabu vyetu, wakiita maandishi maovu nay
a waovu na kusema kuwa yale tunayoyafanya ni hatari na machukizo makubwa kama
vile kumuabudu Mungu Mmoja wa Kweli, kufunga saumu, kuzishika Sabato, na kuvaa
mavazi yasiyoonyesha kujitukuza. Walituua kwa kututundika mitini na kwa
kutuchoma moto, kwa sababu ya mambo haya. Ulikuwa ni mtindo wao kuvaa kama
ndege tausi. Ukristo huu wa zamakale ulitutesa na kutuchukia kwa ajili ya mambo
haya yote. Walikuwa na kiwango kidogo sana cha mambo ya kutushitaki au kutulaumu
kwenye Imani yetu (soma jarida la Wajibu wa Amri ya Nne jibu wa
Amri ya Nne Kwenye Makanisa ya Mungu yanayshika Sabato (Na. 170) [The Role of the Fourth Commandment in the
Historical Sabbath-keeping Churches of
God (No. 170)] na jarida linguine la
Migawanyo ya Jumla ya Makanisa
yanayozishika Sabato (Na. 122) [General Distribution of the Sabbath-keeping
Churches (No. 122)].
Watu wetu
wengi wameitwa watoke dhambini. Mara nyingi dunia huwalaumu watenda dhambi. Hata hivyo, wanapoongoka na
wanapokubalika na kusamehewa kwa kupitia Makanisa ya Wapendwa. Kukubalika huku
kusiko na masharti kwa wenye dhambi kwenye neema iokoayoya ubatizo wa Yesu
Kristo ni mhuri na alama ya Kanisa la Mungu na wateule wake.
Kristo alisema,
“Furahini, na
kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo
walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu”.
Basi na
tuchukuliane na mateso ya dunia kwenye nuru ya matumaini iliyoko ndani yetu. Basi
na tukazane kwa bidii yote ili kuifanya kazi ya Mungu.
Inatupasa kuwa
chumvi ya Dunia na nuru ya Ulimwengu. Yesu Kristo ni nuru ya ulimwengu na kwa
kupitia sisi anaieneza injili. Mungu amechagua kututumia sisi zaidi kuliko kazi
nyingine yoyote. Ametuita ili kutupa uweza ilituwe wenye nguvu. Ametuita
tuingie, sisi wadhaifu na msingi. Baadhi yet uni wadhaifu, wengine ni imara na
wengine wako kotekote kuwili. Lakini ametuita sisi sote tuingie, na sio
kutuacha tukiwa kwenye hali ile, bali kutufikisha mahali pa kupata nguvu kwa
kupitia Roho Mtakatifu.
Kipimo cha nguvu
ile ni hizi Heri na kwa jinsi tunavyoweza kuachilia mambo yenye faida kwetu
binafsi kwa ajili ya Mungu na wapendwa wetu waliomo Kanisani. Wale miongoni mwetu
wanaishi peke yao wapo kwenye familia zetu; na wale waio na watoto miongoni
mwetu, ni wazazi na wale kati yetu walio peke yao basi hawapo pekeyao tena.
Bali sisi sote ni familia kubwa, yenye nguvu, katika Roho mmoja. Kristo
anatuambia kwenye hizi Heri jinsi ya kufuka pale na jinsi ya kuitensa kazi zake.
Tumetwa sio kwa udhaifu au kufanywa wadhaifu, bali kupewa nguvu au uweza.
q