Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[247]
Uimbaji wa Tenzi Kwenye Ibada za Kikristo
(Toleo
La 1.0 19980424-19980424)
Kazi ni kufafanua
Muhtasari wa kitabu kijulikanacho kama Joseph Stennett’s Hymns for the
Lord’s Supper [Tenzi za Kuziimba Kwenye Ushirika wa Meza ya Bwana]. Kitabu
hiki kinaelezea historia ya matumizi ya Nyimbo zinazotumiwa na Makanisa ya
Mungu ya Sabato yanayotumia lugha ya Kiingereza na chimbuko au msingi wa
kibiblia wa iumbaji wa nyimbo za tenzi sio tu kwenye mlo wa Ushirika wa Meza ya
Bwana peke yake lakini ni kwa matumizi yake kwa ujumla. Kinaonyesha upenyo au
mwanya uliojificha au iliyofichika kwenye utaratibu wetu wa zamani au wa
mwanzoni ya ibada za watuza Sabato na teolojia kwa mafundisho ya uwongo.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1998 Dr Thomas McElwain)
(Tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Utangulizi wa Nyimbo za Tenzi za Joseph Stennett Kwa
Ajili ya Mlo wa Ushirika wa Meza ya Bwana
Huenda mtu muhimu
na anayekumbukwa na kupendwa na wengi kwenye uendelexaji wa tathnia ya utunzi
na uimbaji tenzi katika kipindi cha karne ya kumi na saba huko Uingereza
alikuwa ni Mchungaji au Rev. Joseph Stennett (1663-1713). Alihudumu kwene
Kanisa la Mungu la Kibaptist la Kisabato lililokuwa likikutanika kwenye Ukumbi
wa Pinner, ushirika uliojulikana kama Pinnar’s Hall Seventh Day Baptist Church
ambako alihudumu kama Mchungaji kwa kipindi cha miaka 23 ya mai0ha yake.
Alipoanza huduma yake na kuanza kuhubiri madhabahuni mwaka 1690, moja ya kitu
cha kwanza alichokifanya ilikuwa ni kuanzisha mchakao wa uimbaji kwene kutaniko
lake kwa kutumia tenzi za kuziimba. Mara ya kwanza, mchakato huu uliishia tu
kwenye ibada na tukio la ubatizo na ushirika wa Meza ya Bwana, lakini Stenett
mwenyewe alitunga nyimbo za kuimba siku za Sabato pamoja na siku nyingine
nyingi.
Hakuna ushahidi
unaonyesha kwamba kuna tenzi ziwazozote mbali ya hizi za Stennet zilizowahi
kutumika kuimbwa kwenye Kanisa lolote miongoni mwa makanisa yanayozishika
Sabato ya huko London kwenye kipindi cha karne ya kumi na saba. Kwa kutilia
maanani kipindi hiki, mtu anawezakuhitimisha kwa kusema kwamba hakukwepo na
uimbaji wowote uliokuwa ukifanyika kwenye makusanyiko ya Kibaptist kwa ujumla
wake ambayo yalijulikana na kuwa maarufu zaidi ya kusanyiko hili la huko Mill
Yard. Pinner’s Hall, Hususan kwene kusantiko la Kibaptist, na inawezekana sana
kwa walipokuwa wakikusanyika waliimba Zaburi tangu kuanzishwa kwake.
Uhalali wa
kuepuka uimbaji wa kikundi ulikuwa ni kwamba uimbaji ni kitendo
kinachoidhihirisha imani, na ni makosa na unafiki kuweka uimbaji kimakundi ya
watu wengi ambayo yanaweza kujumuisha watu ambao hawajaikiri imani kutoka
mioyoni mwao kikamilifu. Marufuku na upingaji huu wa kuunda makundi ya uimbaji
yalipata umaarufu sana na mashiko kwenye zama za miaka ya 1690 ambayo Stennett
anaielezea kwenye utangulizi wa maelezo ya kitabu chake cha Nyimbo, na
anaelezea kwa kirefu kwa kumuomba mtu mwingine aandike kitabu cha kutetea
kitendo hicho. Nakala za maandishi haya ya pande mbili zimenukuliwa na
kuandikwa kwenye somo hili. Nukuu kutoka kwenye Maandiko Matakatifu yaliyotajwa
kwenye futinoti za kitabu asilia zimetolewa kwenye mabano. Maandiko ya Biblia
ya mwanzoni yametolewa kwa mtindo wa kawaida, wakati ufafanuzi wake umeandikwa
mwa maandishi ya ulalo. Nimefana
mandiko ya ulalo sehemu zote, na
kutoa ufafanuzi wangu kwa maandiko ya uandishi wa kawaida.
Utetezi
usiojlikana kuuhusu uimbaji huu wa tenzi kwa vikundi ambao unaonekana kwenye
mwanzo wa vitabu vya Stennett huenda ni moja ya watetezi wenye mashiko na nguvu
kubwa na walioelezea kifasaha na kwa uangalifu mkubwa kuwahi kukutikana katika
historia ya jambo hili. Mtu anaweza kumdhania kuwa huenda ni Stennett mwenyewe
tu ndiye aliyeandika lakini ni kwa vifungu vinavyowasifu mwandishi wa tenzi.
Ingekuwa sio vizuri na kutotenda haki kudai kuwa Stennett alijisifia mwenyewe
mno hata kwenye kujibadilisha. Zaidi sana, ni kwamba tasnifu au makala inaishia
kwa utenzi usio na mashiko sana kuelezea kuwa haiwezekani kuwa imeandikwa na
shairi lenye kiwango cha utunzi na uandishi wa Stennett.
Vitabu
vilivyoandikwa na marehemu Mchungaji na Mwanafunzi wake Mr. Joseph Stennett.
Toleo la IV. London: Lililochap[ishwa Mwaka M.DCC.XXXII, kurasa 56-71 kinasema.
…Kupenda ukweli,
na huruma ya kusaidia vinatilia maanani wakristo walewale walio waadilifu na
wakini, na ambao mawazo yao yako timamu kuhusu hofu au haya ya ufuataji wa
sheria na kanuni za uimbaji kwenye ibada za Mungu, ili waviruke au kuviondoa
vyote hivi ili vibakie vile tu vilivyokubalika na kuwa sehemu muhimu katika
ibada ya kutukuza, ikinipata msukumo wa kupenda vile inavyostahili sana rafiki
mwene akili nyingi au mwerevu na mbunifu ili kuambisha kwenye kitabu hiki cha
tenzi, majadiliano yaleyale kwenye somo hilo, pamoja na akiba au msaada
aliokuwanao kabla hajanikaribisha mimi, katika kunielezea mimi sababu
zilizopelekea kufana ubaguzi dhidi ya uimbaji wa zaburi, nk, ambavyo yeye
mwenye alikuwa akifanya hivyo hapo zamani, akawa ameondolewa.
Hi ni wazi sana
kwamba kulikuwa na jambo jema kwa kupinga uimbaji huu wa vikundi. Kulipaswa
kuwepo na upinzani kama huo hata kwenye kutaniko la kusanyiko lililojulikana
kama Kanisa la Pinner’s Hall, au vinginevyo isingekuwa ni lazima kuandika
maneno haya ya kuuhalalisha. Upinzani ulikuja hasa kutoka kwenye Halmashaui Kuu
ya Kanisa la Baptist, ambao kwa wakati mwingi watu wa imani Quakers
wanavyofanya kwenye liturjia yao.
Urafiki huu, na
tumaini nililojitahidi kumfanya ashawishike (kwa Baraka za Mungu) lingeweza
kuwa na madhara yale yale kama yawapatavyo watu wengine walio kwenye mazingira
yanayofanana, yakimfanya asiweze kukataa ombi langu; ingawaje hakunipa uhuru wa
kulitaja jina lake… Joseph Stennett (ukurasa wa 56)
Kifungu: Kwa
mkono mwingine.
Kwa maombi ya
mchungaji na mwandishi, aliyeambisha mjadala huu kwa ufupi kwenye
tenziziufuatazo, kwenye uthibitisho wa matendo ya uimbaji wa nyimbo za sifa kwa
Mungu, kuwa kama sehemu ya ibada ya kikristo. Na mimi nimefungamanisha zaidi
sana, kwa kuwa nimefanya kazi kubwa sana chini ya kuibagua elimu kwa mlingano
sawasawa, na ambao bado unashawishi kile amacho kwa sasa kinathamini kazi
yangu, kwa mamlaka ya juu, pamoja na ile ya Kristo na mitume wake.
Kigezo cha
ubaguzi wa kielimu unaonyesha jinsi ulivyotetea kwa nguvu ilikuwa ni upinzani
kwenye uimbaji wa kimakundi. Huu ulikuwa ni kabla ya Uamsho wa Wamethodist na
utamaduni au desturi ya nyimbo za wa Wesleys, kutosema lolote kuhusu Isaac
Watts, ambaye hakuonekana kwenye mwonekano ulio numa ya Joseph Stennett
aliyeanzisha uimbaji wa kivikundi wa tenzi au vitabu vya nyimbo kwenye
kusanyiko la Pinner’s Hall.
Sitaona shaka kwa
kuwapokea hao wakristo ambao wanamtazamo tofauti. Sitaweza tu kuifayia haki, na
kutosema haki, ya kitu kama hicho (ukurasa 58) ambaye atasoma muktasari huu,
ili kudhania kuwa inawezekana kwao kukosea na kuwa sawa sawa na kupenda
kuipokea kweli, ambayo itawezesha kukithi haja ya swali litakaloweza kujitokeza.
Mwandishi amakusudia kutumia ukweli kama kigezo na
inahitaji kwa msomaji kuweka kando ubaguzi na kuwa tayari kukubali kuwa
inawezekana kuwa wazo hili limekosewa. Ni changamoto la namna gani basi!
Mtu anayesoma
agano jipya kwa mkazo na mtazamo wowote, anatakiwa ajue kwa kutaja mara kwa
mara wa kuimba zaburi, na tenzi, na nyimbo za kiroho.
Wainjilisti
(Mathayo 26. 30. Na Marko 14. 26. Na wakati walipokuwa wakiimba tenzi au
nyimbo, &c.) Mathayo na Marko wote wawili wanatuarifu kuwa, Mwokozi wetu
mbarikiwa, pamoja na wanafunzi wake, waliimba nyimbo walipokuwa wanahitimisha
mlo wa Ushirika wa Meza ya Bwana, kisha alianzisha sheria endelevu kanisani.
Halleli Mkuu wa
Zaburi 111-118 bado anatumiwa miongoni mwa Wayahudi kwa sikukuu kadhaa za kila
mwaka. Ikionyesha kuwa kitabu cha tano cha Zaburi, Zaburi 107-150, inaonyesha
ushahidi wa kuwa vilikusanywa kwa utaratibu uliopo vikiwa ni nyimbo ya sikukuu
za kila mwaka, kuna uwezekano mkubwa sana kuwa Yesu na wanafunzi wake “waliimba
nyimbo” kutokana na ukusanyaji wakati wa mlo wa Pasaka. Mwandishi anaashiria
kwamba mlo wa Meza ya Bwana ndipo ulianzishwa kuwa ni amri ya milele na
endelevu kwenyr Kanisa pamoja na uimbaji wa vikundi kama sehemu ya amri
zilizoanzishwa. Udhaifu wa mwandishi unaonekana kuwepo kwa namna au kiasi
fulani. Kama tutakiri kwamba sheria pamoja na ile ya uimbaji wa vikundi au
mkusanyiko kwa msingi wa andiko hili, tunapaswa pia kukubali kuwa sheria
zikiwemo zile za vitabu vilivyopo vinavyoashiria, kuwa zote au sehemu ya vitabu
vya Helleli Mkuu kwenye kitabu cha Zaburi. Hakuna kitu kwenye maandiko haya ili
kuashiria kitu kingine zaidi.
Mtakatifu Luka kwenye historia ya kitabu cha Matendo ya
Mitume anatuambia, kwamba Paulo na Sila walipokuwa gerezani, na wakiwa
wamepigwa mijeledi kwa ajili ya hudua yao, saa za usikuwa manane waliomba na
kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwasikia. (Matendo 16.
25).
Mtume Paulo
anawakemea Wakorintho kwa majivuno yao wa bure kwa ajili ya karama
walizoruzukiwa, hususan zile za kunena kwa lugha mpya, (IWakorintho 14. 15. Nitaomba
kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa
akili pia. (akiwaambia kwamba walipaswa kuimba kwa uelewa, ambavyo waliwa huku
hawaelewi lugha wanayoitumia kuimba, na ingawaje (ukurasa wa 59) ikieleweka na
wageni waliohudhuria, au mtu aliyeelekezwa kinachojiri.
Mwandishi
anafanya madhanio hapa ambayo hayawezi kukubalika na baadhi ya Wabaptist wa
leo. Tunadhani kuwa karama hii ya kunena kwa lugha ni uweza wa kusema ukweli na
lugha mpya inayoeleweka, na siyo usemi wa kutatarika tu kwa lugha isiyoendana.
Anadhania kwamba tatizo analolielezea Paulo ni matumizi ya lugha kama hizo
mbele ya wasikilizaji wanaojua lugha nyingine tofauti, kwa lengo la “majivuno
ya bure au yasiyo na maana”. Mwandishi anaonyesha kutoka hili kwamba uimbaji
kwenye mkusanyiko unapaswa uwe kwa lugha inayotumika na kueleweka na watu.
Mchakato huo kwa hiyo unaendelea zaidi ya vile ilivyoelezewa kwenye andiko.
IWakorintho 14 kwa kweli inatoa tafsiri ya andiko lililotokan kwenye lugha mpya.
Uandishi au maandiko ya Paulo hayaashirii kwamba Kiebrania kisitumike
kiliturjia, kama ilivyofanyika kwenye masugagogi na makanisani, pamoja na
usomaji sambamba wa Targum au fafanuzi za maandiko kwa lugha ya kawaida.
Maandiko ya Paulo yanasema tu kwamba sehemu ya isiyoendana au kukubalika ya
liturjia inapaswa kutafsiriwa.
Mtume huyohuyo anawasifu wote wawili
(Waefeso. 5. 19, 20. mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo
za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru
Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; (Waefeso, na Wakolosai 3. 16,17). Neno la Kristo na
likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa
zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni
mwenu. Na kila
mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu,
mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.) Wakolosai inasema
kuimba zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni.
Mwandishi hataji
mambo ambayo zaburi, tenzi, na nyimbo za kiroho zinachomaanishwa na Paulo.
Haiwezekani kudhania kwamba hakuna kikomo chochote kwa kile kingalichoweza
kujumuishwa au kutojumuishwa kwenye mkusanyiko wa kundi. Kinachodhaniwa kuwa
huenda Paulo anakielezea kwene maandiko yake haya yanokana na Zaburi ya
Kibiblia, ambazo zimeandikwa kwenye tafsiri ya Septuagint inayojumuisha maelezo
matatu ya Kiyunani anayoyatumia Paulo hapa, ambayo ni “zaburi, tenzi, na nyimbo
za kiroho”. Makundi haya ya nyimbo ndiyo zile Zaburi za Biblia. Mwandishi
hatambui kwenye waraka wake wowote kwenye somo au fundisho la kwamba nyimbo
anazozielezea Paulo zawezakuwa zilikuwepo wakati huo wa Paulo, na maneno yake
yayawezi kukanushika kupunguza nguvu kwenye nyimbo zilizoandikwa kipindi cha
baadae.
Mtume (Yakobo 5. 13 anasema. Mtu
wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe
zaburi.) Yakoboanawasihi pia Wakristo walioko uhamishoni wa makabila kumi na
mbili anaowaandikia, kuonyesha furaha yao kwenye mazingira yoyote kwa kuimba
zaburi za kumsifu Mungu.
Yakobo pia
anaamuru uimbaji wa Zaburi za Biblia.
Sasa zile
zinazohitajika zikusanywe kutoka kwenye mifano hii yote, maelekezo, na taratibu
za matendo haya, bali uimbaji ule humtukuza na kumsifu Mungu ni sehemu ya ibada
za mbinguni kwenye kanisa la kikristo? Na kwa kweli mtu yeyote angefanya
hitimisho hili kutokana na usomaji wa vifungu hivi, na ambaye hajawahi kusikia
mkanganyo wowote kuihusu. Kwa kweli inawezekana kuweka pingamizi dhidi ya kitu
chochote. Ukosoaji wa Kigrama unawezakuwa ulifanyika, na msikumo wa kiujenzi
unaweza kuwekwa kwenye maneno ya wazi na dhahiri sana; lakini kama (ukurasa wa
60), zingeruhusiwa kanuni zilezile katika kutafsiri Maandiko Matakatifu kwa
ujumla, kama ilivyotumiwa kuwa ni kiini au chanzo cha nguvu za maandiko
niliyoyataja; nimetaja wenye uwazi wake na unaweza kuonekana kuwa kitu chenye
kukitilia mashaka, na ale mafundisho yaliyowazi sana na yenye mashiko
kupinduliwa. Hata hivyo, kwa kuwa kuna watu wanaobakia wakiwa hawaguswi bado
kwenye shughuli hii, nitajitahidi, pasipo kuwataja wao moja kwa moja, kuviruka
vikwazo vyao vyote, na kuuthibitisha ukweli, kwa kuonyesha,
Mwandishi
anaelezea suala la uimbaji au kutoimba wakati wa ibada. Hatilii maanani hatua
hii kwamba kuwe au kusiwepo na uimbaji kwenye mtutaniko. Kwa suala lililotajwa
au linalohusika, mijadala hii inaonekana kuwepo. Maandiko ya Biblia anayoyataja
yanaashiria wazi au hata yanautaja uimbaji wa kivikundi.
1. Uimbaji huu
unatajwa kwenye maandiko mbalimbali yaliyotajwa kiusahihi.
2. Kwamba ulikuwa
unafanyika kama sehemu ya ibada takatifu.
3. Kwamba ulikuwa
unafanyika kwa Sauti za pamoja.
1. Kwamba uimbaji
uliotajwa na kurudiwarudiwa kwenye maandiko kadhaa wa kadha, yanapaswa
yajulikane kiusahihi na sio kwa namna ya kifumbo. Kwa hili, hakuwezi kuwa na
kipingamizi kilichowekwa ila ni kwa baadhi ya ukosoaji uliopandikizwa wa chanzo
chake; kwa kila anayeelewa lugha ya Kiingereza, anajua kwamba uimbaji ni tendo
la kuelezea au maneno kwa kutumia sauti iliyopangiliwa, kwa kufuata kanuni za
kimuziki; na kama usemaji halisia ni kuelezea maneno kwa mujibu wa kanuni za
kigrama, zote mbili zikiwa zimefanywa kwa muigizo na matendo, pasipo uzoefu au
ujuzi na (ukurasa wa 61) dhana ya ama; kwa usawa asilia , kwa kanuni zote
mbili, yaani zenyekupunguzika na zile za bandia. Uimbaji kwa Kiingereza
umechukuliwa kwa namna nyingine; hakuna kwa msomaji wa Kiingereza cha kawaida
anayeweza kuoneashaka kuwa hii haiwezi kuwa ndiyo maana yake.
Ni kama ilivyo
kwenye neno lake asilia lililotufanya kutokana na (Mathayo 26. 30 ‘Umnhsantej. Marko 14. 30 ‘Umnhsantej. Matendo 16. 25. Umnoun.) neno wainjilisti (evangelists)
linatokana na vebu, ambayo maana yake ya kwanza ni kuimba utenzi au wimbo wa
kusifu.
Wakati mwingine
kwa kweli imechukuliwa kabisa kuwa ni kusifu, pasipo kuhitaji maana. Lakini hii
ni kanuni fulani ya utafsiri wa maandiko yote; kuchukua maneno kutoka kwenye
maana yake ya kwanza na yaliyosahihi zaidi, isipokuwa kama kuna maana iliyo
njema zaidi iliyotakiwa au kukusudiwa basi ni kwa nini mtazamo na maana hiyo
usikubalike mahali panapohitaji kuwekwa sawa. Sasa kwenye mifano inayotiliwa
maanani kwa sababu kama hii inaweza kuibuliwa, na kwa hiyo inapaswa kuchukuliwa
kama ilivyo kwenye tafsiri, wanaimba tenzi au wimbo wa kusifu.
Kwenye waraka wa (I Wakorintho 14. 15. Yalw tw pneumati, yalw de kai tw
noi.) Wakorintho na ule wa (Yakobo 5. 13. Euqumei tij; yalletw.) Mtakatibu Yakobo neno lililotumika tangu mwanzo linamaanisha
uimbaji halisi. Na wakati mwingine pia linatumika kwenye iumbaji au upigaji wa
vyombo vya muziki; lakini wakati (ukurasa wa 62) unaonyesha kuwa ni sauti, haichukuliwi
kwa namna nyingine yoyote zaidi ya ile uimbaji uliokusudiwa. Kwenye waraka wa
(Wakolosai 3. 16. Adontej.) Wakolosai tunalikuta neno linguine ambalo linamaanisha pia
uimbaji mzuri, lakini wakati mwingine linatumika kuelezea uandishi wa shairi au
nakala aya; ambayo ni maana ya neno ambalo ninaamini kuwa hakuna atakayeshindana
nalo kwa mahala hapa, na mkabala napo ambalo hakuna maana nyingine yoyote inayoweza
kutiwa kwenye neon hili ila ni lile tu la uimbaji mzuri.
Kwenye waraka wa (Waefeso 5. 19. Adontej kai yallontej.) Waefeso, maneno yote mawili yaliishia kwa kutaja kilichofanyika.
Ili kwamba ni kama Mtakatifu Paulo alivyokuwa hakutunga kabisa kuelezea uimbaji
sahihi, haikuwezekana kwake kwa maneno kujielezea mwenyewe kwa uzuri zaidi na
kuishia akiamua tu.
Yote hii, nadhani inatuama kwene
uthibitisho kamili, ambao tafsiri yetu ipo kwene jambo hili kila mahali
likiwemo, na ule uimbaji mzuri ulioelezewa kwenye mifano yote iliyotolewa. Ni
kama kwenye midundo fulani mahsusi ambayo maneno yanapaswa,kuelezewa, imeachwa
mno kwa makusudi kama mdundo au mpangilio wa utunzi au mwelekeo tofautina
kuweka lafundhi ya sauti katika kusema. Heshima ndiyo kikomo pekee; na kama
mdundo wa sauti unavyopaswa kuwa tukutu na la kipuuzi, kwa hiyo haiwezekani
kuwa ni mdundo wenye mpangilio wa kumuziki uwe mwepesi na (ukurasa wa63) kutoka
hewani; kwa namna zote mbili zipasavyo kuwa kwenye ibada takatifu iwe bora na
kamilifu, ili iwe ndiyo mwelekeo wetu wa kujitoa na kujieleza kwa Mungu.
Mjadala wa mwandishi unaonekana kuendelea kuwepo kwamba imbaji mzuri ndiyo unaokusudiwa kwenye maandiko anayoyataja. Anaendelea mbele kwa kudokeza Maandiko Matakatifu hata hivyo, kwenye huu mbahatisho. Anasema kwamba midundo yenyewe imeachwa kuwa ni uhuru wa kuichagua kwenye maana hiyohiyo ya kunena. Hakuna dodoso kama hiyo kwenye maandiko. kinyume chake, mitume kwa wazi sana wamefanya rejea zao kwenye Zaburi zilizo kwenye Biblia na huenda inatokana na maandiko mengine ya kwenye Biblia. Kinachoashiria kwa hiyo ni kwamba zilikuwa zikiimbwa kwa tyuni za kimapokeo zilizojulikama wakati ule wa mitume. Hakuna ruhusa iliyotolewa kutumia uimbaji wao. Mwongozo wa mwisho wa mwandishi unaonyesha wazi sana kuwa ni za wakati huu wa mwanzoni, ambao ulisababisha ruhusa ya matumizi ya matendo yasiyoendana na Maandiko Matakatifu kutumika kujiingiza kwenye huduma na masuala ya ibada ili ziwe.kwa hiyo, kadri ya maudhuhi ya Biblia pekee ilikuwa inatumika, basi hakuna cha kujiuliza kuhusu masuala ya unadhifu, utukutu, upuuzi, nk. Mara tu baada ya “unadhifu” unapofanyika kuwa ni kikomo pekee, kanisa linakuwa wazi kwa utoshelevu wa kila mara kwa jinsi muziki na maneno vinapoendana sambamba. Hii ni hali iliyopo sasa kwenye Ukristo. Ushawishi wa mwisho wa mtunzi na mwandishi unpaswa uonekane kufedheheshwa kwa kila mwanadamu wa siku hizi. Anadai kwamba muziki wote unaofanywa kwenye ibada uwe “iliyochujwa na inayofurahisha”, na kamwe “usiwashe tu na kutolewa hewani”. Kuna kila mfanano unaoonyesha kuwa hata muziki wa “kuwashwa na kutolewa hewani” wa wakati wetu huu ungekuwa ni najisi au uchafu kwenye Ukristo wa siku hizi.
2. Kwamba uimbaji huu uliotajwa kwenye
maandiko kadha wa kadha na kurudiwarudiwa ulifanyika na kuchukuliwa kamani
sehemu ya ibada takatifu.
Tenzi au nyimbo zilizoimbwa kwenye ushiriki
wa ekaristi zilizoimbwa na Bwana wetu na mitume wake, zilikubalika hata na wale
wanaokataa kwamba zilikuwa zinaimbwa zikifanywa kama ni tendo la kusifu na
kumshukuru Mungu. Kwa kuwa inakubalika kwa pande zote kwamba kuimba tenzi ni
kusifu, iwe kwa njia ya wimbo au kwa kutafakari tu; na kuwa na uhakika kuwa
Mungu alikuwa ndiye mlengwa na kwamba ndiye aliyekuwa wanamkusudia kumuomba.
Kwenye mfano wa
Paulo na Sila maneno yameeleza kuwa walimuimbia na kumsifu Mungu.
Kwa Waefeso ndipo
mtume anawaambia hivi: mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni,
huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba
sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo Na kwa
Wakolosai anasema, ni karibu na maneno yaleyale: Neno la Kristo na likae kwa
wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na
nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na
kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, (ukurasa wa 64) fanyeni yote katika jina
la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye. Kwa zote mbili zilizoandikwa
tunaweza kuona matendo, kushukuru au kusifu; mlengwa akiwa ni Mungu kwa kupitia
kwa mwombezi, na uimbaji unaotoka ndani moyoni.
Mtume Yakobo
anasema: Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka?
Na aimbe zaburi. (Yakobo 5. 13.) ambayo inahitaji maombi ya bidii kama haya ya
kuelezea mahitaji yetu na masikitiko yetu kwa Mungu, na ndivyo ilivyo, kuwa
uimbaji ni njia sahihi ya kuelezea furaha na shukurani zetu. Na kwa kweli
muziki na shairi zote ni njia sahihi za kuelezea na kuonyesha hisia au hamasa.
Zinaweka uzito na kufikisha kwenye lengo kusudiwa la upendo na furaha
vinapofanyika kwa upole na usraarabu, zinasaidia na kurahisisha kuhamasisha
masikitiko na huzuni. Kwa hiyo tunakuta mwimba zaburi mfalme akiimba moja
wakati tenzi kadhaa kwa taratibu za kusifu na wimbo usizo wa ya toba na ya kimaombolezo,
na tena kwa maombi ya muwako na dua kwa Baraka zinazohitajika. Ili kwamba
hakuna kitu kinachotakiwa kuelezewa kwa Mungu kisiweze kutojaa kuimbwa mbele
zake.
Anachosema
Mtakatifu Paulo kuhusu jambo hili kwa Wakorintho ni; Nitaomba kwa roho, tena
nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia. (I
Wakorintho 14. 15.)inaonekana wazi kunenwa kuhusu ibada ya hadhara kanisani
inayojumuisha na maombi; ambapo alitaabika kwa mdhaliliko huo huo na uimbaji,
kutoka kwenye ubatili (ukurasa wa 65) ns matokeo makubwa ya namna hiyohiyo
kanisani, kwaa walioipokea karama ya kunena kwa lugha na kujivuna kwa kunena
lugha hizo mbele za watu wasioijua kugha hiyo isiyojulikana; wakati kwamba
walitakiwa wote wawili waombe na waziimbe sifa za Mungu kwa lugha hizo, ili
wote waliohudhuria waelewe, na wajiunge kwenye tendo lile la ibada kwa kujitoa
kwa hofu na kumaanisha na huku wakijua.
Na tena, Paulo
haongelei kunyume na utumiaji wa liturjia au taratibu za ibada za Kiebrania,
bali anaongelea kinyume na hali ya kutoelewa kwa kile kinachonenwa. Sura inatoa
tafsiri kuwa ilikuwa inafanyika sehemu zote mbili, yaani kanisani na kwenye
sinagogi kutumia Targum sambamba na maandiko yaliyo kwenye lugha inayoeleweka
na iliyozoeleka. Mwandishi anaenda mbali sana kwene hitimisho yake.
Sasa kutokana na
kile kilichosemwa chini ya kichwa hiki cha habari inaonyesha kwamba kwenye
sehemu zote zilizorudiwa rudiwa, uimbaji ulioelezewa kuwa ulifanywa kwa Mungu
akiwa kama mlengwa wa haraka wa kila kilicho cha lazima kuendeleza tendo lolote
la kidini, au ni sehemu ya ibada takatifu.
Mwandishi
anadhania kwamba yale yote yanayohitajika kuanzisha na kuchukua hatua zozoye ni
sehemu ya ibada takatifu ni ile inayohitajika kumfanyia Mungu akiwa kama
mlengwa wa kwanza na stahiki. Kwa hili anakubaliana na Wabaptist wa leo.
Mtazamo huu ni dhana tu, hata hivyo. Ni jambo linalokubalika sana kudai msingi
wa Kimaandiko kwa kila kitu kinachopelekwa kwenye kutaniko la ibada.
3. Na sasa
naonyesha kuwa uimbaji wa nyimbo za kumsifu Mungu ulifanyika kwa sauti za
pamoja za watu kadhaa kwa pamoja. Inasemekana kuwa Bwana wetu na wanafunzi
wake, kwa mujibu wa injili zote mbili za Mathayo na Marko kwamba waliimba wimbo
(kwa idadi ya umoja) wakti Kristo alipokuwa anaubariki mkate na kushukuru,
wakati alipokitwaa kikombe, wote wanaelezea (kwa idadi ya umoja) kama
ilivyofanywa kwa Kristo kuendelea kwake kuimba, na wengine wote walijiunga naye
kwa kimoyonimoyoni tu. Na kwamba waliungana na Kristo kwenye tendo lile.
Natumaini hakuna mtu anayeona shaka; ingawaje ilisemekana kuwa alishukuru na
kuubarikiia kwa majina ya wao wote, na kwa niaba yao na pia kwa ajili yake
mwenyewe. (ukurasa wa 66) alitangaza kuungana kwake kwenye dua ya pamoja na
kutoa shukrani zao kwa Mungu. Lakini hapa kifungu hiki kimebadilishwa, na
muinjilisti anatuambia kwamba waliimba wimbo kana kwamba ni kwa sauti ya
pamoja, na pia kwamba walikuwa na moyo na roho moja. Jambo hili ni kama ilivyo
kwenye maana iliyowazi na isiyo na utata ya maelezo, na kwa hiyo hakuwezi kuwa
na maana nyingine iliyokusudiwa kwa utofauti wa vifungu hivi.
Rejea za
mwandishi vinabaki kuwa na mashiko, kama andiko linavyoeleza maombi haya
kufanywa na kiashirio cha mtu mmoja “yeye” na uimbaji ikionyeshwa kufanywa
wengi kwa kiashiria cha “wao”.
Mtkatifu Luka
anatuambia kwamba wafungwa waliwasikia Paulo na Sila wakiimba wote wawili na
wakiwa wameungana kwa pamoja na kwa moyo mmoja kumuomba Mungu. Naamini kuwa
hakuna mtu aliyedhania kuwa walitamka maombi kwa pamoja. Ni wazi sana kwamba ni
nyimbo za kusifu ndizo walizokuwa wameungana kuziimba kwa pamoja, na kwamba ni
sauti zao tu ndizo zilipalizwa juu kiasi cha kuwafanya wafungwa wenzao
wawasikie.
Mwandishi
anafanya hitimisho lisilo na mashiko sana kuhusu maombi. Kuna uwezekano mkubwa
sana kwamba Paulo na Sila waliomba kwa pamoja, jambo linaloashiria kwamba
huenda waliomba kwa kutumia maneno yatokanayo kwenye Maandiko Matakatifu ambayo
wote wawili waliyajua na kuyatumia. Rejea za mwandishi zimeweka msingi wake
uzoefu wake aliokuwanao kutoka kwa Wabaptisti wa maombi ya kujitoa au hiyari,
na ambayo inawezekana sana kuwa bado yapo, lakini ni jambo ambalo halijasemwa
au kudokezwa kwenye maandiko. rejea yake kuu ambayo ni ya uimbaji wa pamoja,
kwa upande mwingine, inaonekana kuwepo bado.
Kuna kifungu
kingine katika historia ya Matendo ambacho, nadhani kama kitaangaliwa kiurahisi
au kikipuuzwa kwenye malengo haya. Kwenye sura ya 4 aya ya 24 inasema kuwa wali
(yaani mitume ambao wakati huu walikuwa huko Yerusalemu, na waumini ambao
walikuwa wamejumuika nao, wakikutanika pamoja) walimpazia Mungu sauti zao kwa
amoja, wakisema, nk. Kutoka kwenye kifungu hiki inaonekana kwamba ibada hii kwa
hiyo ilifanyika ili kutoa shukurani (ingawa ilihitimishwa na dua) na kwamba
kwenye mazingira yaleyale na ghafla, yliyotokana na kufunguliwa kwa Petro na
Yohana kutoka kwenye mahabusu ya baraza la Sanhedrini; kulikotokea baada ya
kuhojiwa na wakaachiliwa (ukurasa wa 67) bila ya kuadhibiwa, nah ii ilitimiliza
unabii wa Daudi wa Zaburi 2:1. Sasa suala linakuwa ni kule kushukuru na na
shukurani na kwamba zilifanywa kwa sauti ya pamoja na kwa moyo mmoja. Sioni
sababu ya kuonea shaka lakini ni kwamba ilifanyika kama tenzi au nyimbo
takatifu; kama isingedhaniwa kwamba walitamka maneno ya kinabii tupu kwa sauti
za pamoja; ambapo ni jambo ninaloamini hakuna mtu aliyeweza kushindana nao.
Hakuna mahali popote tulipowahi kusoma maombi yakinenwa kwa sauti ya pamoja,
lakini ni nyimbo za sifa ndizo zinaweza kuimbwa kwa sauti ya pamoja
nimekwishapewa mifano. Na kitendo hiki hapa cha kutoa sifaa kwa pamoja na
kufanywa kwa sauti ya pamoja, ingawaje haisemi kuwa waliimba, lakini bado ni
zaidi ya kubahatisha kudhania kuwa waliimba; kwa kuwa, ingawa misemo yote
(ambayo neno linaitumia) sio kuimba, huku ikiwa na uhakika uimbaji wote ni
kusema au kitendo cha kutamka maneno.
Dhana ya
mwandishi haieleweki vizuri, lakini inaonekana kuwa na mashiko.
Mifano hii,
nadhani inatosha kuthibitisha kuwa uimbaji wa sauti za pamoja ulikuwa
unafanyika kwenye makanisa ya wakristo.
Licha ya udhaifu
uliojionyesha katika kuelezea hoja zake kutokana na kupuuzia au kuachana na
mambo ambayo hakuyakusudia kuyaelezea, lengo lake kubwa ambalo Maandiko
Matakatifu bilashaka yanashindania kuwa uimbaji wa kivikundi au wa pamoja
ulikuwa unafanyika kwenye kanisa la mitume, kama ni kitu kinachoendelea
kufanywa.
Idadi ya kile
kinachosemwa, ni kwamba kutoka kwenye maandiko chepushi ya Maandiko Matakatifu,
yaliyokusanywa kutoka kwenye agano jipya, inaonekana kwamba nyimbo za kumsifu
Munguzilikuwa zikiimbwa kwa sauti za pamoja kwenye kanisa la kikristo, ikiwa ni
sehemu ya ibada takatifu; na kwamba jambo hili limeruhusiwa kwenye matukio
kadha wa kadha, ikiunganishwa na kukubalika na makanisa mengi kadhaa ambayo
mitume (ukurasa 68) waliyaandikia nyaraka zao. Kutokana na yote haya, kiasilia
inafuatia kwamba, sasa ni wajibu wa wakristo kuimba nyimbo za kumsifu Mungu,
kwa namna zote mbili, yaani wawapo kwenye makusanyiko ya hadhara na wawapo
kwenye ibada zao za kibinafsi za sirini, na wafanye hivyo.
Kutokana na hoja
iliyoonekana ya kwamba uimbaji wa pamoja ndiyo ulikuwa unafanywa na mitume na
ndiyo waliouanzisha, mwandishi anahitimisha kwa kusema kwamba uimbaji wa pamoja
kwenye makusanyiko ndiyo unaotakiwa kufanywa hata sasa. Hitimisho lake
linaonekana kuwa na mashiko.
Kwa kusema kwake
hivyo kutoka kwenye Maandiko Matakatifu, nitaongeza ushuhuda mmoja mgeni, ili
kuthibitisha kuwa kilikuwa ni kitendo endelevu cha wakristo wa zama kale,
kwenye makusanyiko yao ya kidini, waliimba kwa sauti za pamoja, tenzi au nyimbo
za kumsifu Kristo na Mungu. Na hiyo ni ya Pliny kijana; ambaye alikuwa ni
liwali wa Ponto na Bithinia ya Asia Ndogo, pamoja na mji wa Byzantium;akiwa sio
afisa mwenye cheo au daraja la kawaida,
bali akiwa ni mtu wa daraja na cheo cha Luteni na aliyekuwa wa karibu kwa
mfalme na mwenye mamlaka ya juu yasiyo ya kawaida. Mtu huyu mkubwa kwa kipindi
kirefu alikuwa mtiifu kwa amri zilizotolewa na Bwana wake, akitimiza wajibu
wake kwa kuwahukumu na kuwatendea vibaya sana wakisto; lakini akakuta kwamba
kama ataendelea kuwaadhibu kutokana na yale waliyoyaona kuwa ya muhimu wao wenyewe
wakristo, basi angeweza kuliangamiza jimbo lake lote kwa uamuzi aliouona kuwa
hauepukiki na ni lazima akuandikie waraka mfalme mwenyewe amuelezee jambo hili
na hali halisi ilivyo, na kbwamba baada ya kupewa jukumu na mchakato huu wa
kuwaangamiza wakristo, na ukaidi wao wanapoishikili na kudumu hadi kifo, na kwa
idadi kubwa ya wale waliyoikumbatia hirizi au uchawi huu (ukurasa wa 69) mpya,
kama anavyoiita; anahusisha kile kilicho kwenye tathmini aliyoikuta kuwa ni
hesabu ya matendo ya kikristo. (Affirmabant autem hanc fuisse suminam vel culpæ
fuæ, vel erroris; quod essent soliti stato die ante lucem convenire, carmenque
Christo, quasi Deo, dicere secum invicem, seque sacramento, non in scelus
alimquod obstringere, sed ne furta, ne latrocinia, ne adulteria committerent,
ne fidem fallerent, ne depositum appellari abnegarent: quibus peractis morem
sibi discedendi fuisse, rursusque coeundi ad capiendum cibum promiscuum tamen
& innoxium. Plin. Ep. Lib. 10. Ep. 97.) "Waliithibitisha, anasema,
kwamba idadi yote ya machukzo au makosa yaliyojiri humo; kwamba hawakuwa kwenye
siku iliyopangiwa wakutane pamoja kabla ya kuchomoza jua, na kuimba kwa pamoja
nyimbo za tenzi kwa Kristo na kwa Mungu, na kujiweka wakfu kwa kushiriki
sakramenti, wakijiweka wakfu kuwa wasifanye wala kushiriki matendo yoyote ya
dhambi, lakini wajiepushe na uibaji, ukabaji, uasherati, na kuishika imani, na
kufanya marejesho kila nadhiri waliyoaminiwa nayo; na baada ya waliishia hapo,
na kukutanika tena kwa mlo wa kawaida, na ambayo ilikuwa haina chochote kisicho
cha kawaida au mhalifu au mtenda jinai.” Waraka huu aliandikiwa Trajan na kisha
mfalme yapata miaka sabini na moja baada ya kufariki kwa Mwokozi wetu, yapata
mwaka 104 BK. Na katika kipindi cha miaka sabini ya utawala wa Trajan. Kwa mamlaka
hii isiyoonewa mashaka tunaona ni kwa kiasi gani wakristo wa nyakati zile
walivyojitoa kimatenzo; pamoja na makusanyiko yao ya kidini (ukurasa 70)
waliimba nyimbo au tenzi kwa Yesu Kristo na kwa Mungu.
Kama ushahidi
kwamba Wakristo katika mwaka 104 BK waliimba uimbaji wa pamoja na kimakundi,
Pliny bilashaka alikuwepo, ikidhaniwa kuwa ni waraka wenye hamasa kubwa wa
Pliny. Cha kushangaza, hii ndiyo nia na lengo la mwandishi. Hata hivyo,
anaendelea kwenye uingiliaji kwamba haanzishi wala kujadili kwamba Wakristo
walimuimbia tenzi Yesu na Mungu. Kwanza kabisa, inaonekana kwamba Pliny alikuwa
anaweza rejea za kiteolojia za namna ile. Tunaweza kumuamini kwa jambo hili la
uimbaji wa kimakundi au wa pamoja kama huu, lakini sio kwa mtazamo wa
kiteolojia wa uimbaji wa tenzi. Tena mwandishi hafanyi ukosoaji wowote wa
kihistoria hata hivyo.
La pili, mnamo
mwaka 104 BK, fundisho la Utatu lilikuwa halijafafanuliwa bado. Mwandishi
anaendelea mbele zaidi ya maneno ya Pliny kwa kuonyesha dalili kwamba Wakristo
waliotajwa walimuimbia nyimbo za tenzi Yesu kama Mungu, akiwa ni kama mlengwa
kwenye Utatu. Ingawa tenzi za Stennet ziliendana vilivyo na vifungu vya Biblia,
kuna rejea mbili au tatu za uwepo wa Kristo huko nyuma kabla ya kuzaliwa kwake.
(Wimbo namba 29, mstari wa 5, ukurasa 121), na takriban rejea moja inayomtaja
Kristo “kama Mwama pekee na wa milele wa Mungu" (Wimbo namba 36, ubeti wa
7, ukurasa 131). Ingawa dhana hii ya uwepo wa Yesu kabla ya kuzaliwa kwake
duniani kwa ujumla haiashirii maana ya Utatu, kwenye jambo hili, bali unatuama
kwenye maelezo ya “Mwana wa milele wa
Mungu”, kama ifanyavyo. wa Yesu kabla ya kuzaliwa kwake duniani kwa ujumla
haiashirii maana ya Utatu, kwenye jambo hili, bali unatuama kwenye maelezo ya “Mwana wa milele wa Mungu”, kama ifanyavyo. Maelezo
yaliyofuatia ni ya fomula ya mwanahistoria wa Kikalvini katika juhudi zao
zakuupinga uyunitatiani wa Servetus. Stennett na atetezi mkubwa wa imani ya
Utatu ya mrengo wa Kikalvini. Kwa kumtegemea Pliny kuutetea Utatu ni kitu
kisicho na maana ua kilichopitwa na wakati.
Mwandishi
anafanya rejea za Biblia ili kuanzisha uimbaji wa tenzi za kivikundi. Lengo
lake la kuutambulisha uimbaji wa tenzi hatimaye ulikuja kuwa dhahiri. Utaratibu wa ibada au liturjia ya
Kimaandiko haitoshi kuuadia fundisho la Utatu. Anaacha suala zima la uimbaji
kuwa wa wazi, ikiwa kama utakuwa wa “heshima”, akiashiria kuwa Biblia
haikubaliani na chochote kile. Baada ya kuthibitisha kwamba uimbaji wa wote na
wamakundi ulikuwepo haya kwene kanisa la kwanza, anaruka hadi kwenye hitimisho
la kwamba tenzi na nyimbo za Watrinitariani sio tu kuwa ziliruhusiwa peke yake,
bali zina mashiko kutoka kwenye Maandiko Matakatifu. Mjadala huu haukujadiliwa
hata hivyo, zaidi ya kuonekana au kudhihirishwa tu. Hadaa hii ya wazi hii
ilipaswa iwe na uadilifu kwa kweli na kutoadilika pia.
Tatu, hakuna
msaada wa Kibiblia kwa mikusanyiko ya zama za kabla ya uamsho. Na inawezekana
pi asana hata mapema ya kabla ya mwaka wa 104 BK ambayo Pliny alipokuwa
anaabudu siku za Jumapili asubuhi. Na inakuwa ndiyo sababu, Wakristo
wanaoelezewa wanaweza kuwa ni mfano kabisa wa washika Sabato, kwa kuwa
wanajiunga kwenye matendo yasiyo na utangulizi wa maagizo ya Biblia.
Kuhusu tunzi
zifuatazo nasema tu kwamba masomo yamechaguliwa vyema, na cha kushangaza
yamechukuliwa kwenye tukio, vizuri na kwa kusisimua kunakotokana na mtangamano
wa karamu kuu ya upendo, ambayo ni mlo wa ushirika wa meza ya Bwana,
ulioanzisha ili kukumbuka kutolewa kwa dhabihu kamilifu, ambayo kwayo pekeyake,
tulikombolewa kutoka kwenye maangamizo ya milele, na kuchaguliwa kuwa na sehemu
kwenye baraka za milele. Shairi linasisimua na tulivu, maelezo yake yako wazi
nay a haki, na kila stahiki kuwa na kiini stahiki; na ndiyo maana nimeruhusu
kufanywa kwenye matumizi ya wazi nay a wote na siri au kibinafsi kwa wakristo
wanaojitoa, ambao vifua vyao vinamuwako wa moto wa mbinguni, na ambao mioyo yao
imehamishwa na hisia endelevu na iliyopo ya upendo wa mtakatifu.
Sifa za mwandishi
kuzisifia tenzi za Stennett si jambo la kulionea mashaka kwenye tendo la
maelezo ya kweli na stahili za mashairi. Tenzi au nyimbo nyingine za Stennett
zimebakia kuwa ni kigezo cha karne kadhaa sasa. Mwandishi anaonyesha kujitoa,
uungwana, muwako wa moto wa kimungu, na hisia ya kudumu ya upendo mtakatifu.
Kumbuka kwamba vigezo vyote hivi zinatakiwa kwa haraka. Zingekuwa safi zote
kama kungeongezewa kigezo kingine kimoja zaidi, kigezo cha Kibiblia. Lakini
Stenett amekuwa muangalifu sana. Kuna nukuu za Biblia karibu kwenye kila mstari
wa tenzi zake. Kutaja mfundisho yasiyo ya kibiblia, kama vile Utatu, ni chache
sana na ni vigumu kuzikuta. Matokeo yake ni ya kiundani sana, kupenyeza au
kuingiza polepole mafundisho ya uwongo kwenye maandiko yaliyojiwekahuru kwa sehemu
kubwa kutoka kwayo. Nyimbo hizi za zamani zi hatua ya kwanza kwenye maendeleo
ya kihistoria yaliyoelezewa na nabii Amosi kuwa ni nyimbo za hekaluni
zilizogeuzwa kuwa maombolezo (Amosi 8:3). Iligharimu karne tatu na nusu
kukamilisha, lakini mwishowake, madhabahu ya miwe iliyojipenyeza na kuenea
karibu kwenye ulimwengu wote wa Wakristo ni utimilifu wa mwisho wa maneno ya
nabii Amosi.
q