Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[278]

 

 

 

 

Dhabihu  Sadaka

(Toleo La 1.1 19990623-19990717)

 

Dhana au wazo la utoaji wa dhabihu na sadaka halijaeleweka kwa usahihi sana makanisani. Ni kwa miaka mingi sana makanisa ya Mungu yamekuwa haiishiki Idi ya Penyekoste kiusahihi na kwa kweli hayajafikia kiasi cha kuelewa vyema ya yale yanayotakiwa kufanyika kwenye Sikukuu na dhabihu zake. Mtu anapaswa aishi kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu. Jarida hili linaangalia juu ya dhana ya ni nini hasa dhabihu na ni nini hasa maana ya hizi Sikukuu.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki ©  1999 Wade Cox)

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Dhabihu za Sadaka


 


Jarida hili linakwenda kufafanua kwa kina kuhusu dhana na utoaji wa sadaka.

 

Kutoka 23:14ff.

Kutoka 23:14-20 Mara tatu kila mwaka utaniwekea sikukuu. 15 Utaiweka sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu; utakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba kama nilivyokuagiza, kwa wakati uliowekwa, mwezi wa Abibu (kwa maana ndio mwezi uliotoka Misri); wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu;

 

Sasa hilo linamaana sana na liko wazi. Hakuna hata mtu mmoja, atakayekuja mbele za Bwana mikono mitupu

 

16 tena, sikukuu ya mavuno, hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani. 17 Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU. 18 Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi. 19 Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

 

Dhana iliyo kwenye aya za 14 na 15 linahusiana na agizo lisemalo kuja mbele zangu. Neno-dhana lililo kwene tafsiri ya Companion Bible ni kwamba hii ni neno lililoandikwa kwa Kiebrania cha kisasa, lakini hili na vifungu kumi vingine zilikuwepo tayari kwenye tafsiri ya Sopherim na ni kwa kuonyesha tu. Maandiko ya zamakale yanasomeka (ya yanapasa yasomeke) “kuuona uso wangu”. Dhana yote nzima kukuhusu Uso wa Mungu ilitumika kama mfano au Synecdoche kwa mujibu wa Bullinger kwenye Biblia ya the Companion, lakini ukweli wa mambo ulikuwa ni kwamba huu Uso wa Mungu alikuwa ni Malaika wa Yahova. Kwenye aya ya 20 inaendelea mbele kwa musema:

 

20 Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.

Uso wa Mungu alikuwa ni Kiumbe wa Uwepo wake; ambaye ni Yahova aliyewatokea Isrfaeli na kuwaendesha Israeli kwa kuwafundisha Torati. Dhana nzima iliyo kwenye andiko hili ni kwamba haturuhusiwi kwenda huko na kuwa mbele za Uso wa Bwana na hata mahala pengine kwenye sikukuu hizi mikono mitupu.

 

Idi ya Majuma (au Pentekoste) ni ya pili kati ya hizo tatu zinazotolewa sadaka. Tunawajibu wa kukutanika pamoja ili kuiadhimisha Pentekoste na hatupaswi kwenda tukiwa mikono mitupu.

 

Kwenye Matendo 2:1 tunaona kwamba kunaulazima wa kukutanika kama Kanisa kwenye sikukuu ya Pentekoste.

Matendo 2:1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

 

Ni Sikukuu ambayo tunalazimika kwa moyo mmoja na mahali pamoja. Kwa hiyo, sio suala tu la kuisika nyumbani. Tumeamriwa na Mungu kujihudhurisha kwenye Sikukuu ya Pentekoste kwenye mahali alipopachagua, kwa namna hiyohiyo na kwenye Sikukuu mbili nyingine ziadhimishwe pia, zinazojulikana kama Pasaka na Idi ya Vibanda, na tusijitokeze mikono mitupu (Kumbukumbu la Torati 16:16).

 

Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwepo wote mahali pamoja. Kwa maneno mengine, yawezekana kuwa walikutanika pamoja tangu siku ya Sabato na huenda walikusanyika pamoja kwa ajili ya Sikukuu ya Pentekoste. Huenda hii ni dhana ya kuhusu Sabato ya pili baada ya Pentekoste baada ya (the Sabbatton deuteropro) iliyo kwenye Luka 6:1.

 

Tangu maadhimisho ya kwanza ya Kanisa ya Pentekoste, Roho Mtakatifu aliwashukia wale waliokuwepo kwa nguvu nyingi. Waliweza kunena kwa lugha nyingine na kunena maneno ya kinabii na kutumia au kutumiwa na Roho Mtakatifu. Ilipasa isemwe kwamba ni kuadhimisha visivyo sahihi sikukuu hii ya Pentekoste kunazuia uwezo wa Kanisa kutumiwa na Roho Mtakatifu aweze kuzuia na kukingwa kutoka kwenye hali ya uasi na tama za mwili.

 

Kutokana na maelezo na maagizo ya Kumbukumbu la Torati 16 tunaona kutoka kwenye aya ya 1 amri inaanza kutoka mwezi wa kwanza na inasema:

Kumbukumbu la Torati 16:1 Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka Bwana, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku Bwana; Mungu wako.

Haya ni marudio ya kile kinachosemwa kwenye Kutoka 23.

Kumbukumbu la Torati 16:2-6 Nawe umchinjie pasaka Bwana, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua Bwana apakalishe jina lake. 3 Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoka nchi ya Misri, siku zote za maisha yako

Ni dhahiri sana na wazi sana kwamba ilipoandikwa hakukuwa na mahali maalumu ambapo palichaguliwa na Bwana ili aliweke jina lake. Hakuwa ameliweka jina lake huko Yerusalemu kikamilifu. Wakati Torati ilipoandikwa, iliandikwa kwa ajili ya nyakati zote, kwa kuwa Yerusalemu haikuwa inakwenda kuwa ni mahali ambapo Bwana amelikalisha jina lake kikamilifu na kwa wakati wote. Tangu mwaka 70 BK, Yerusalemu imekuwa ikiangamia na Kanisa na Hekalu vimekuwa jangwani. Ni wazi sana kuwa agizo tulilopewa la kuamrishwa la kulifanya jina la Bwana kuwa ndicho lengo kwenye maadhimisho ya Idi hizi tatu: Pasaka na Siku za Mikate Isiyo na Chachu, Pentekoste na Idi ya Vibanda na Mkutano wa Makini. Kanisa lipewa wajibu wa kuliweka jina la Mungu mahali pake stahiki na tumeamriwa kuhudhuria kwa kuwepo huko.

 

Inaendelea:

4 Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale cho chote usiku kucha hata asubuhi. 5 Usimchinje pasaka ndani ya malango yako yote akupayo Bwana, Mungu wako;

 

Ni wazi kabisa kwamba inatupasa kuwa nje ya nyumba zetu tunapoziadhimisha Idi za Paasaka na tutaona pia kuwa tumeamriwa pia kuadhimisha Pentekoste na Idi ya Vibanda. Huu sio wakati wa kukitofaautishaganisha kitu kwa mtu binafsi, wala kitu chakulitofauisha au kulinganisha Kanisa. Kanisa na viongozi wake wanatakiwa kupachagua mahali pa kuliweka jina la Bwana mahali maalumu. Pasaka imeelezzewa kwa wazi kuwa haipaswi kuadhimishwa au kuliwa ndani ya marago au nyumba zetu. Maelezo haya yanapelekea hadi kwenye Sikukuu nyingine kama tutakavyoona.

6 ila mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, ndipo mtakapomchinja pasaka jioni, katika machweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka Misri. 7 Nawe umwoke na kumla mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; kisha asubuhi yake ugeuke uende hemani mwako.

Kwa hiyo tunawea kurejea hemani mwetu au kwenye makazi yetu katika Siku Takatifu ya kwanza, lakini hatupaswi kuwa majumbani mwetu au maskani mwetu wakati wa maadhimisho ya Pasaka.

Inaendela:

8 Siku sita utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na uwe mkutano mtukufu kwa Bwana, Mungu wako, usifanye kazi yo yote. 9 Jihesabie majuma saba; tangu wakati uanzao kutia mundu katika mmea utaanza kuhesabu majuma saba.

 

Mwanzoni mwa mavuno ya shayiri wakati wa mwanzoni mwa miganda au masuke ya kijani kibichi ya shayiri yanakusanywa ili yaweze kuchomwa. Hayavunwi ili yatwangwe au kusagwa; kwa kuwa yako ya kijani bado. Tendo hili hufanyika siku ya Jumapili kwenye juma la maadhimisho ya Mikate Isiyo na Chachu. Wanaendelea kuhesabu kuanzia wakati huu.

 

Kishe tnajihesabia majuma saba. Hii ni muhimu na tutakwenda kuiona sababu au maana ya kuhesabu majuma haya saba baadae.

10 Nawe sikukuu ya majuma umfanyie Bwana, Mungu wako, kwa kutoa sadaka ya hiari ya mkono wako, utakayotoa kwa kadiri akubarikiavyo Bwana, Mungu wako;

Kwa hiyo hatutakiwi kuja mble za Bwana mikono mitupu na tunapaswa kwenda mahali ambapo Bwana amelikalisha jina lake. Agio hili ni kwa watu wote. Viongozi wa kanisa wanaowajibu wa kupaandaa mahali ambapo watu watajihudhurisha kwa maadhimisho haya na hakuna mtu anayeruhusiwa kwenda au kujihudhurisha hapo akiwa mikono mitupu. Kuna utoaji wa sadaka; sadaka ya hiyari mikononi mwetu

... Kila mtu na atoe kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya Bwana, Mungu wako, alivyokupa.

 

Katika kuziangalia Baraka za Bwana, sadaka hii inapaswa iwe inatolewa kwa hiyari, na isiwe ikitolewa huku mtu akimnung’unikia Mungu kama hatukufanikiwa tungependa kuwa kama tulivyokuwa miaka ya nyuma

11 nawe utafurahi mbele ya Bwana, Mungu wako, wewe na mwana wako na binti yako, na mtumwa wako na mjakazi wako, na Mlawi aliye ndani ya malango yako, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio katikati yako, katika mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake.

Ni wazi kabisa hapa kwamba agizo la wanaume wote waende mbele a Bwana ni amri ya lazima, lakini pia wanasindikizwa na wake zao na binti zao. Wanawake kwa mazingir fulani wanazuiwa kusafiri kwenda maeneo fulani, au vinginevyo wahudumiwe kwa uangalizi kama wa watoto; kwa hiyo Torati haijatubebesha mzigo wowote sisi ambao tusioweza kuubeba. Sheria iko wazi sana kuhusu wanawake. Mungu amewaambia wanaume waende peke yao iwapo kama wake zao hawataweza kuhudhuria. Inaenda kinyume na watumishi walio kwenye familia za Walawi na wageni na mayatima na wajane walio katikati yetu, mahali ambapo Bwana Mungu wetu amepachagua ili alikalishe jina lake hapo.

 

Kwa hiyo, ni dhahiri sana kuwa kuna agizo na umuhimu linalotutaka kupachagua mahali pa kujihudhurisha na mwingine yeyote anayehusika kwenye jamii na nyumba na watu wote wanaojiri kwenye huduma za familia zetu. Walawi wanategemea matoleo yetu pia. Kwa hiyo, dhana yote nima lililo kwenye kanisa likionekana kama ni idara ya kikuhani na watu wote wanaohusiana na kanisa. Sio sehemu inayowapasa Walawi na wala zaka hii sio sehemu ya Walawi. Ibrahimu alitoa zaka yake kwa Melkizedeki kwenye zama ambayo hata Lawi alikuwa haja zaliwa, na ukuhani wet uni wa mfano wa Melkizedeki ,bna sio wa Lawi. Lawi alikuwa ni kuhani wa mpito, ambaye alifanyika kuwa ni sehemu ya shirika au ukuhani mkubwa na mpana linaloitwa Ukuhani wa mfano wa Melkizedeki, ambao kwa huo, Ibwahimu baba yetu alitoa aka yake kwa huo, wakati sisi tulipokuwa viunoni mwake. Ukuhani wet uni pamoja na Melkiedeki, na utoaji wa aka haujakoma au kutanguliwa; na sio tangu siku za Nuhu.

 

Kwa hiyo tunakwenda kwenye Sikukuu ya Vibanda, jambo ambalo sio linaloongelewa hapa.

 

Kwenye Mambo ya Walawi sura ya 23 tutaona utaratibu na amri fulani sasa kutoka kwenye maadhimisho ya Mganda wa kutikiswa. Tunaelezea utaratibu wa kuhesabu hadi Pentekoste, ambacho ni kipindi maalumu cha kuhesabu kuanzia saa tatu kamili asubuhi ya Jumapili. Hii ni kwa mujibu wa ilivyokuwa inafanyika katika kipindi cha Hekalu chini ya Masadukayo. Marabi wa Kiyahudi (waliotokana na Mafarisayo) walianza kuadhimisha kimakosa tangu walipoondoka Israeli, wakati walipokwenda uhamishoni. Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa mara zote ilitolewa siku ya Kwanza ya Juma katika kipindi cha Hekalu; na kila mara ilikuwa ni saa tatu asubuhi na ndipo ilichukuliwa rasmi kuwa ni wakati wa kuhesabu hadi kufikia hesabu ya hamsini yangu muda huu wa saa tatu za asubuhi na ni tangu Jumapili hadi Jumapili. Hivi ndivyo’ilivyokuwa ikifanyika katika kipindi cha kamba ya kubomolewa Hekalu cha takriban miaka 1,500. Hivi ndivyo Wasamaria na Masadukayo walivyokuwa wakifanya. Haikukoma hadi kwa warithi wa Mafarisayo walipoanza kuichezea kalenda na kibadilisha kwenye takriban karne ya pili BK.

 

Mambo ya Walawi 23:9-12 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 10 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; 11 naye atautikisa mganda mbele za Bwana ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa.  

 

Siku inayofuatia baada ya Sabato ilikuwa ni siku ya kwanza ya juma, ambayo siku hizi tunaiita Jumapili.

12 Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. 13 Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini. 14 Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote..

 

Katazo hili la kula bisi bado linaendelea kwenye Mganda wa Kutikiswa. Haturuhusiwi kula bisi ya mavuno mapya hadi ifikapo siku ya Mganda wa Kutikiswa. Tunakula bisi za mavuno ya miaka iliyopita hadi kufikia mavuno ya malimbuko ya Mganda wa Kutikiswa. Tutaona kwamba walipokuwa Israeli wanaiteka na kuikalia nchi ya ahadi chini ya Yoshua.

15 Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mliyouleta mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba; 16 hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka ya unga mpya.

Kwa hiyo kuna siku hamsini zenye Sabato saba kamili ndani yake. Sabato au Sabatoni hizi saba kamili. Kuna siku sita za kazi inaopelekea kwenye siku ya saba ya juma, ambayo ni siku ya mapumziko ya Sabato. Sabato saba kamili inatufikisha kwenye Sabatoa ya saba na halafu siku inayofuatia (kesho yake au siku inayofuatia baada ya Sabato) ni siku ya kwanza ya Juma, ambayo tunaiita Jumapili. Marazote Pentekoste inaangukia siku ya Jumapili ikiandhimisha na kanisa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 2000, isipokuwa kwa kosa moja tu dogo kwenye karne yak mi na moja.

17 Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa Bwana.

 

Sasa hii inapendeza kwamba mikate hii miwili, ndiyo mikate miwili pekee kati ya utaratibu wote wa sadaka ambayo ndiyo imeagizzwa itengenewe kwa kuitia chachu na kuwa mikate yenye chachu ndani yake, ikiashiria Roho Mtakatifu waliyempokea siku ya Pentekoste takriban mwaka 30 BK, baada ya kusulibiwa kwa Kristo, wakati Roho Mtakatifu alipoingia kwenye jingo lile kwa lugha na moto na kwapa uweza ndugu wapendwa na kuwaongoa.

18 Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtasongeza wana-kondoo saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza, na ng'ombe mume mmoja, na kondoo waume wawili; watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, pamoja na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. 19 Nanyi mtasongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wana-kondoo wawili waume wa mwaka wa kwanza kuwa dhabihu ya sadaka za amani. 20 Kisha kuhani atawatikisa pamoja na hiyo mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana, pamoja na wale wana-kondoo wawili; watakuwa watakatifu kwa Bwana, wawe wa huyo kuhani. 21 Nanyi mtapiga mbiu siku iyo hiyo; kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; msifanye kazi yo yote ya utumishi; ni amri ya milele katika makao yenu yote, katika vizazi vyenu. 22 Nanyi hapo mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala msiyakusanye masazo ya mavuno yako; utayaacha kwa ajili ya huyo maskini, na mgeni; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Jambo hili linaendelea kupitia kwenye sadaka ya Mganda wa Kutikiswa hapa ukiwa kwa Makuhani wale walioitwa na kuchaguliwa na baada ya ule wenye mfano wa Melkizedeki, siku ya Pentekoste na hadi kwenye Idi ya Vibanda. Kwa hiyo, katika miaka hii 2,000, Kanisa lina Makuhani na Wafalme, waliochaguuliwa na kutengwa mbali, kuteuliwa na kulindwa na kutikiswa tangu saa 3:00 asubuhi sadaka ya kutikiswa ya Pentekoste. Kwa hiyo, tuna sadaka ya Mganda wa Kutikiswa inayotolewa siku ya Jumapili wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyo na Chachu na sadaka hii nyingine ya Kutikiswa hutolewa siku ya Pentekoste. Sadaka ya Pentekoste ni kubwa zaidi ya ile ya Mganda wa Kutikiswa.

 

Kwa hiyo, ni wazi sana kwamba tunashughulika na mwendelezo wa dhana hii ya Mganda wa Kutikiswa. Haya yote, yanamaanayake katika kulielewa kanisa na nafasi yetu. Tunatakiwa kukutanika pamoja na kusafiri na kuwa wamoja ili kuiadhimisha sadaka hii na Sikukuu hii ya Pentekoste kwa roho njema kama ilivyokuwa inaadhimishwa. Inapaswa kuwa mahali ambapo Bwana Mungu wetu atapachagua na sio kwenye makazi na majumbani mwetu. Sikukuu yote ya Pentekoste iliadhimishwa kwa siku moja, lakini tuna Sabato pia.

 

Sabato na siku Pentekoste zinafanya kuwa sikukuu mbili kwa pamoja, na inatupasa kufunga safari na kuhudhuria kama sikukuu mbili zilizo pamoja. Andiko halisemi kuwa mara mbili kila mwaka na Pentekoste iwapo kama tutakuwa karibu na mahali hapa palipochaguliwa. Bali inasema kuwa ya mwisho ni Idi ya Vibanda. Maandiko hayasemi Idi ya Vibanda au labda Pasaka na Pentekoste kama tunadhani kuwa hiyo ni sahihi sana. Bali andiko linasema ishike Idi ya Pasaka na Mikate Isiyotiwa Chachu kwa muda wa siku saba na haturuhusiwi kuila Pasaka tukiwa majumbani mwetu. Watu wengi wakati mwingine hudhani kuwa hii ni tafsiri inayojitegemea. Lugha hii ni lugha iliyowazi. Kwa kuwa baadhi ya Makanisa ya Mungu hayaishiki Idi za Pasaka na Pentekoste vizuri kwenye mashirika yao ya mwanzoni na sasa wanakabiliana na ukweli wa kuishika kisahihi, na haifanyi kuwa na tafsiri ya kipekee. Inamaana kwamba walikosea kabisa huko nyuma, na kwamba walikuwa hawamtii Mungu bali walikuwa wanamausi. Sio suala la tafsiri ya kipekee nay a jinsi mtu anavyojionea au ni maamuzi yetu. Hatuna la kusema kuhusu hili. Tunazishika sheria na amri za Mungu na kwenda kwenye Sikukuu au vinginevyo tutakuwa tunajiondoa wenyewe mbali na Ufalme wa Mungu. Kuna chaguo moja tu; Kumtii Mungu au kutomtii Mungu. Na iwapo kama Bwana ni Mungu ndipo basin a umuabudu yeye, sawa sawa na anavyoamuru.

 

Tutaona kwenye Mhubiri 12.

Mhubiri 12:12-14 Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili. 13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. 14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.

 

Kwa hiyo hakuna shaka kabisa hapa kuwa hizi ni amri za Mungu nah ii ndiyo kazi yote nzima ya mwanadamu na anachotakiwa ni kuzitenda amri hizi. Tunachotakiwa kuamia ni iwapo kama tutamtii Mungu au kama hatutamtii. Kanisa linapaswa kuzitenda kazi lilizopewa kwa kuzishika amri za Mungu, na kwa kufanya kwetu hivyo ndipo tunaweza kufanya maamuzi na kuyafanya mambo ambayo tumeamriwa. Iwapo kama tukiamua kuwa shindano limekuwa gumu sana na tunakata tama kwalo, hayo ni maamuzi yetu. Inatupasa kushindana kana kwamba ttashinda na inatupasa kuendelea kushindania bila kukona. Inatupasa kupia hatua na kusonga mbele ili tuweze kuvumilia hadi mwisho. Watu wengi wanakimbia kwa hatua ndogo na bila kufika mbali. Watu wengi hudhani kuwa ni dhana ya kiakili au zoezi linayohitaji kutumia akili nyingi. Wanaisoma Biblia na wanadhania kwamba kwa kuisoma kwao tu inatisha na hawahitaji kufanya chochote zaidi, au wanakuwa wapata malengo tofauti, au kuna mtu mwingine anayewaambia visivyo au vinginevyo.

 

Mungu ameiweka kalenda na ametupa sisi sheria ili tujue kile anchokifanya. Tumewekwa kwenye mahala ma maana sana. Tumepewa fursa ya kuwa na sehemu kwenye ufufuo wa kwanza wa wafu na fursa ya kuuingia Ufalme wa Mungu juu ya mamilioni kwa mamilioni ya watu. Litakuwa ni jambo la kijinga kuitupa na kuipoteza fursa hii kwa kufanya mambo yenye kuleta madhara makubwa, kwa kuwa tulikuwa ni wazembe na wavivu sana wa kwenda kwenye Sikukuu, kanakwamba iliamriwa kuwa tusiende, au kwamba hatukupenda kwenda, au ni kama hatujawahi kufanya hivyo huko nyuma. Mtu yeyote anayezidharau amri za Mungu, atahesabiwa kuwa ni mdogo kwenye Ufalme wa Mungu. Watu wanaofanya hivyo, wao wenyewe hawatakuwa na sehemu kwenye ufufuo wa kwanza wa wafu. Na kwene ufufuo wa pili wa wafu, watu walioitupilia mbali fursa hii watakabiliana na fursa ya kusema tu kuwa ‘lakini nilimfuata’. Lakini walimfuata kwenye ufufuo wa pili wa wafu lakini watakuwa wamechelewa sana walipambiwa ukweli ule kwenye ufufuo wa pili. Fusra yet uni sasa na tutakuwa ni wajinga sana tukiipoteza

 

Yatupasa kufikiri yale tunayoyafanya. Kanisa lina wajibu wa kutusaidia na sote tunawajibu wa kukutana na hatutakiwi tukutanike tukiwa mikono mitupu tunapojihudhurisha kwenye kila moja ya sikukuu hizi. Sikukuu zote zinapaswa kuzingatiwa na kuadhimishwa.

 

Kama tukijitoa na kumkabidhi Mungu njia zetu, atathibitisha mawazo yetu. Sio kwa njia nyingine yoyote iliyopo. Basi na tuzishike sikukuu hizi kikamilifu naye atatupa ueklewa zaidi.

 

q