Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[279]

 

 

 

 

Waraka wa Yakobo

(Toleo La 1.0 20060501-20060501)

Matatizo mengi yanayotokea kwenye Makanisa ya Mungu yanaweza kukomesha kwa kufuata kanuni zilizowekwa na kuelekezwa kwenye Waraka wa Yakobo ulioandikiwa makanisa yaliyokuwa kwenye hali ya mtawanyiko mahala pengi.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 2006 Wade Cox)

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Waraka wa Yakobo


 


Waraka huu uliandikwa ukiyalenga makabila kumi na mawili yaliyokuwa kwene hali ya utawanyiko, kwa wale waliokuwa Uhamishoni, ambao wengi wao walikuuwa huko Uyunani (kama ilivyo pia kwenye Yohana 7:35). Idadi ya makabila imekamilika, bila shaka ni waliogawanyika Yuda na Galilaya, na kama ilivyokuuwa. Inaonekana kuwa ndivyo utakavyokuwa mkakati wa kuliunganisha tena taifa chini ya Yesu Kristo.

 

Yakobo 1:1-27

Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu. 2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4 Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.

 

Kila majaribu au mateso (yanayojulikana kama majaribu) ambayo yako mbele yetu yanakusudia kutuimarisha na kutukamilisha. Tunajifunza kutokana na makosa yote tuyafanyayo na kwa kila jaribu na misukosuko tunayoipitia. Huu ni mchakato wa kujaribiwa (dokimion). Kwenye mchakato ule tunajifunza uvumilivu au subira ya watakatifu.

 

5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. 6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. 7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. 8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote. 9 Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa; 10 bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka

 

Mungu anaiimarisha imani kwa kupitia hekima kwa wale wanaoihitaji. Imani Kanisani inaanza, lakini kwa wale walio wa daraja la chini na walio matajiri. Mungu hana upendeleo kwa mtu yeyote. Kusudi la busara au hekima ya imani ni kutufanya sote tufikiri vizuri. Kuwa na mawazo mawili au njia mbili mawazoni mwetu ni kuonyesha kukerwa na kuvutia mchakato au mwendelezo dhaifu au kutokuwa na afya njema. Hivi ndivyo ilivyo dhana au maana ya mtu wa kuwa na njia mbili au kutangatanga na asiye imara kiimani. Tumeitwa ili kujitoa kikamilifu, na busara, na kuchukuliana na uimara.

11 Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.

 

Utajiri wa kidunia au wa duniani hapa ni kitu cha kupita tu na sio vitu vya kuhangaikia sana au kutafutwa kwa nguvu zote zaidi ya imani. Maelezo yaliyo kwenye Injili zote yako wazi sana kwamba ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia kwenye ufalme wa Mungu. Mitego iliyopo ni kwamba wanaikinza imani na kuwadhanganya wale wanaoitangaza.

 

Majaribu yanatupata kutokana na tama za miili yetu na udhaifu na kujaribiwa na dunia inayotuzunguka. Jukumu letu ni kuyavumilia majaribu ili hatimaye tupokee taji ya uzima. Majaribu hayaji kutoka kwa Mungu, lakini uwezo wa kuyavumilia unatoka kupitia Roho wa Mungu.

 

12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. 13 Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. 14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. 15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. 16 Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. 17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.

 

Mungu anatupa sisi vitu vilivyo na ulazima kwa ustawi wa maisha yetu na wokovu wetu. Usiwaangalie wanadamu kama kigezo chako bali mwangalie Mungu. Ni kwa kupitia mapenzi ya Mungu sisi tuliumbwa, ili tuwe malimbuko ya jamii yote ya Wanadamu kwa Mungu.

 

18 Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake. 19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;

 

Kila mmoja wetu anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia mambo lakini sio wepesi kunena, tunapaswa kuwa tulio rahisi kuchukulika na kulisubiri Kanisa na kuwapa heshima stahiki wazee wanaotuongoza katika imani. Wagundue wale wanaoleta au kusababisha migawanyiko na mambo ya kughadhibisha katika imani kwa kuwa huo sio utkatifu wala sio haki na uchaji wa Mungu.

 

20 kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu. 21 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.

 

Watumishi wa Siri za Mungu wamepewa hekima ili waweze kutuandaa vizuri na kutuongoza au kutuelekeza kwenye imani. Je, Mungu anaweza kuandaa imani na kuiacha kwa walinzi wa imani wasio na busara? Hapana, Hafanyi hivyo, na maishani mwetu Kanisani tunapaswa kuonyesha uvumilivu, heshima na upendo ili kwamba tusiweze kutumiwa na adui wetu. Basi na tusiwe tunasema tu habari ya imani na neno la Mungu. Basi na tufanye sasa!

 

22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. 23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.

 

Mwenendo wetu na uwe sawasawa na Sheria kamilifu ya Uhuru. Miriamu alikuwa amenia makuu na aliadhibiwa kwa kuwa hivyo. Aliadhibiwa kwa kuwa na ukoma na akapelekwa nje ya Marago yao na kutengwa kwa muda wa siku saba, sawasawa na maelekezo yaliyo kwenye Torati ya Mungu, ambayo ni Sheria kamilifu ya Uhuru. Usiende mbele zaidi ya wajibu wako na mamlaka yako ambayo tumepewa na kuminiwa nayo. Na tuuzizuie ndimi zetu kuyanena, kwa kuwa kila yanayotutoka mioyoni mwetu ndiyo yanayotutia unajisi.

 

25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake. 26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.  

 

Kama hatutazizuia ndimi zetu ndipo dini yetu haitakuwa na maana yoyote. Shetani ni mshitaki wa ndugu zetu. Ni kazi ya malaika hawa walioasi kutushitaki sisi. Kazi yetu ni kusaidiana na kupendana. Yakobo anatuambia kuhusu tunachotakiwa kufanya kwa usahihi.

 

27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

 

Katika sura ya 2 Yakobo anaendelea kwa kuielezea umuhimu wa imani na matendo.

 

Yakobo 2:1-17           

Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu.

 

Kuhusu tabia ya kuwapendelea watu inaeelezewa kwenye mwendelezo wa sura ya 2 na ni muhimu kuielezea au kuikemea kwa kuwa kupendelea watu ni dhambi. Tutakuwa wote tunaivunja amri na Sheria kwa kutenda dhambi hii. Kanisa linaweza kuathirika vibaya na hata kumeguka kwa ajili ya tabia hii ya kuwapendelea watuwenye fedha au uwezo.

 

2 Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; 3 nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, 4 je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?  

 

Mungu ametuchagua sisi tulio dhaifu na wanyonge, ili awaaibishe wenye nguvu. Yatupasa tuwe matajiri wa imani kama waridhi wa ufalme wa Mungu na tuonyeshe kuwa tunaheshimiana bila kujali hali ya mtu. Na tusiruhusu kuingia kwenye mtego wa mambo ya mali na utajiri.

 

4 je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? 5 Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? 6 Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! Matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu? 7 Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa?  

 

Tusipunjane na kufanyiana mabaya katika hukumu. Tunapohudumiana inatupaswa tuhukumiane kwa haki na sio kwa kuoneana wala kwa kushitakiana kwa uwongo. Shahidi wa uwongo hatabakia salama pasipo kuhukumiwa.

 

 8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema. 9 Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji.

 

Kitendo cha kumpendelea mtu ni dhambi. Uvunjaji wa sheria ni mojawapo ya uovu na uvunjifu wa sheria zote.

 

10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. 11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.

 

Inatupasa kunena na kutenda kama sheria zinavyotutaka kufanya kwa kuwa tutahkumiwa kwa Torati ya Mungu.

 

12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.  

 

Kwenye hukumu zote tunapaswa kuonyesha rehema na tunapaswa kuwajali na kuwainua ndugu wengine kwa kuwarekebisha na kwa mafundisho yote.

 

13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.

 

Kwenye matendo yote tunapaswa kuonyesha imani yetu na kwa kazi zetu. Kazi hizo zote zinajumuisha huduma za ndugu wapendwa kwa namna zote.

 

14 Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa? 15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, 16 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?  

 

Haya “mambo”yaliyotajwa hapa sio ya kimwili tu peke yake; bali ni ya kiroho pia. Watu wanahitaji kufanikiwa, kimwili na kiroho na ni wajibu wa Kanisa kuendeleza na kutiamoyo zaidi kuliko kukatisha tamaa au kulaumu kusiko na maana wala lazima.

 

14 Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?  

 

Matendo yanathibitisha au kuonyesha imani. Tunahitajika kuhitimisha sheria kimwili na kiroho na kuhudumiana kwa imani.

 

17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. 18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.  

 

Haitoshi kumuamini tu Mungu Mmoja na Wapekee na wa Kweli. Mapepo yanaujua ukweli huo na kwa kutetemeka.

 

19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.  

 

Chanzo kikubwa cha mambo hapa ni pale Yakobo anaposema kwamba imani bila matendo imekufa.

 

20 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?  

 

Sura ya Imani kwenye Waebrania 11 imewekwa kwenye mwonekano hapa ambapo imani ya Ibrahimu ulioneshwa kwa matendo, kama ilivyokuwa imani ya kila mtu ambayo ilionekana kuwa waliishi kwa imani.

 

21 Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? 22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale. 23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. 24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake. 25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? 26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

 

Kwa hiyo mwili pasipo na Roho Mtakatifu umekufa. Na ndivyo ilivyo pia kuwa imani bila matendo imekufa. Kama tutamhuzunisha Roho na kumzima tunakuwa tumekufa.

 

Ulimi

Kwenye sura ya 3, Yakobo anaendelea dhana nyingine kuhusu ulimi. Ulimi ni kiungo kikubwa na cha muhimu sana ambacho Shetani anakitumia sana pia Kanisani. Tumejionea na kushuhudia maasi Kanisani yanayotokana na masengenyo au uzushi na ndimi zinazoshuhudia mambo ya uwongo. Watu wengi wamekuwa wakiangamia kwa masengenyo na mambo ya kuzuliana mabaya. Kumekuwa na mambo yasiyofaa yaliyoanzishwa na ya kukwaza kwenye Sikukuu moja hadi nyingine kwa aina ile ile ya masengenyo mabaya. Namna hii haiwezi kuvumilika ya yanapaswa kupelekwa kwenye uongozi. Wakati Mungu anapoamua kushughulikia jambo hili, watu wanaondolewa kutoka Kanisani, wakati mwingine kwa idadi kumbwa ya wale walioliathiri.

 

Tumejionea masengenyo yakitokea Kanisani ambayo yanaonekana kutokuwa na mwisho na yasiyo kemewa. Ushahidi wa uwongo umeendelea kuwashutumu viongozi au hali ya kutokuwa na mtangamano wa kiakili unaotokana na hali ya kuwapendelea watu, mashitaka au shutuma zinazotokana na hukumu mbaya ya nabaraza ya Makanisa na matmizi mabaya ya fedha miongoni mwa watu wanaofanyakazi kwa kujitolea wakiwatumikia ndugu wapendwa wenzao wengine.

 

Ushahidi wa uwongo unaweza kuendelea na kuwa masengenyo yenye kuharibu watu nyuma yake yakilenga kuanzisha aina fulani ya mwndelezo wa shutuma ambayo hatima yake yanakuwa ni uasi. Yanafanikiwa tu wakati yanaporuhusiwa kufanikiwa kupitia udhaifu wa kiroho wa baraza la Kanisa. Sio vizuri sana kuona au kuliachia Kanisa likiharibiwa na matumizi haya mabaya ya ulimi. Mungu anachukua hatua ya kulisafisha Kanisa kwa kutumia matokeo mabaya ya dhambi hiyohiyo yenyewe kwa udhaifu wa kiroho ili kuwaondoa. Wakati mwingine wale walio wapya kwenye imani wanadanganyika pia.

 

Yakobo anatuambia sisi kuwanyenyekea viongozi wetu kwakuwa kutonyenyekea ni tatizo kwenye Kanisa lililoharibiwa na masenhenyo. Kwenye aya ya 1 anatuambia tusinie makuu kwa kuwa kunapelekea hukumuni na lawamani.

 

Hatimaye Yakobo anaonyesha kile ambacho ulimi unachoweza kukisababisha au madhara yake yalivyo kutokana na amri na maelekezo ya Kanisa la Mungu.

 

Yakobo 3:1-18 inasema:

Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi. 2 Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu. 3 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote. 4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha. 5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana. 6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum. 7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu. 8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti. 9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo. 11 Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu? 12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.

 

Ujuzi Kanisani unaonekana kwa jinsi mtu anavyonena kwa upole na busara.

 

13 N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzu. na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. 15 Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. 16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.

 

Chuki na mabishano ni uwanja ambao Shetani anautumia ili kufikia malengo ya kujiinua na majivuno na chuki. Kanisa limejionea tunda la matendo ya watu wenye kunaia makuu na wanawake waongo wanapofanya kazi pamoja ili kuliharibu kanisa. Watu wengi wameharibiwa na hali hii. Inaonekana kuwa ili kufanikisha malengo haya, hakuna mashitaka au shutuma za pamoja yaliyo makubwa kuliko mengine. tumejionea pia hali hii ya kuwapendelea watu ikishindwa kushughulikia mambo. Tunahukumiwa dhamiri zetu na dhambi hizi zote. Tumejionea makanisa yakinunuliwa kwa fedha na yakiandaliwa kumharibu au kumuangamiza mtu yeyote na kitu chochote na kuvunja sheria yoyote.

 

17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. 18 Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

 

Tunda la haki limepandwa kwa amani yao inayoweka amani kwa kuwa wao wamefanyiwa kwa upole na kwa urahisi sana. Kunai makuu na tama ni kitu kinacholeta au kusababisha vita na kuushinda uovu na chuki. Wivu na kutamani kitu alichonacho mwingine, wakati kwamba chuki ni hukusudia kuharibu mambo yote mawili na mtu anayekuwanayo.

 

Mungu atatupa kile tunachomuomba kama tutafanya sawasawa na mapenzi yake na tukimuomba kwa haki. Mambo mengi tunayomuomba kila mara yanakuwa sio sahihi kwa mambo tusiyoyahitaji.

 

Yakobo 4:1-16

Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? 2 Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! 3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.

 

Sote tuna tatizo na dhambi. Sisi sote tumeondolewa kwenye tamaa ya mali nay a kimwili.

 

4 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. 5 Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? 6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. 7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

 

Huenda hii ni changamoto kubwa sana tuliyonayo sisi sote. Hebu na tujitoe na kujinenyekesha kwa Mungu na tumshinde adui.

 

8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. 9 Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. 10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza. 11 Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.

 

Kanisa linashughulika na utendaji wa hukumu na sheria. Kanisa linaweka kwenye jumuia yake utaratibu wa kuhukumu mambo. Hebu na tuone kwenye Mathayo 18.

 

Mathayo 18:10-35 inasema:

Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. 11 [Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.] 12 Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? 13 Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko wale tisa na tisini wasiopotea. 14 Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.

 

Mojawapo kati ya matatizo tunayokutana nayo kwenye mabo haya ya kiroho ambayo yanasababisha chuki na shutuma au lawama miongoni mwa wapendwa. Mafundisho poofu nay a uwongo huja Kanisani na watu wenye tabia hii ya kunai makuu. Wanasababisha watu kuanguka na kuiacha imani au kukengeuka. Kwa mfano, wakati Mungu alipoigawanya Israeli na Yuda na mgawanyiko ule ulikuwa na ruhusa ya Mungu, Aliyachukua makabila ya kaskazini na kuyatenda na Yuda na ufalme wao wakiongozwa na Yeroboam. Yeroboamu akaenda huko Shekemu, lakini kwa kipindi cha majuma tu walianza ksimamisha sanamu za ndama wa dhahabu huko Betheli na Dani. Kwa hiyo, dini ya uwongo na potofu ilianzishwa kwa kipindi kifupi sana. Ili kuzuia wazo la kuinganisha tena Kanisa, Yeroboamu akaiweka kalenda kutoka moyoni mwake na ambayo inafanana na ile ya Mwandamo wa Mwezi Mpya iliyoanzia baada ya kipindi cha ikwinoks, na ambayo iliwekwa ikianzia tahere 25 Machi. Kalenda hii inajulikana hata leo kama Kalenda ya Wasamaria.

 

Kuna watu kwene Kanisa la Mungu wanaopenda kuitambulisha na kuuingiza kalenda ya Wasamaria na wanaotaka kuwapotosha watu kwa mafundisho ya uwongo. Ni kwa jinsi hiyohiyo, watu wanaotaka kuingiza mafundisho ya mwezi mchanga wanatafuta jinsi ya kuligawa Kanisa la Mungu.

 

Wanauadhimisha wakati mwingine hata hapa nchini Australia, wakati mwezi mkamilifu uliwa kwenye siku ya 15 wakati ukiwa haujawa mwezi mkamilifu sana bado. Jambo hili halimaanishi kwamba siku ile haijawa ni ya mwezi mkamilifu. Wakati mwezi mkamilifu ukiwa kwenye hatua iliyochelewa ya mwendelezo wake, haufikii kwenye wastani wake hasa hadi unapokuwa kwenye mzunguko wa upande mwingine wa dunia.

 

Watu wanatumia jambo hilo ili kujaribu kuieneza kalenda ya Hilleli na wakitafuta kusababisha migawanyiko na kuligawanya Kanisa. Mambo haya yote yanafanyika kwa lengo la kuligawanya Kanisa na kuliharibu kwa kupitia mafundisho ya uwongo na imethibitika kufanikiwa miongoni mwa watu wasioelimika.

 

Kwenye aya ya 15, inaendelea kusema yafuatayo:

15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. 16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.

 

Utaratibu huo umekuwa umewekwa Kanisani kwa kiwango cha kuheshimika na ni mara chache sana umekuwa ukipingwa au kukataliwa.

 

17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.  

 

Tumeona watu wakidiriki kuyashutumu mabaraza ya Kanisa kwa kuwapendelea watu, kwa kutotoa hukumu au kuizungusha hukumu kwa jinsi isiyo ya haki au kuwa ni ‘wajumbe ndiyo’. Malalamiko haya yamekuwa yakitolewa kwa wazi na hadharani au pengine kwa uficho, na machoni pa Kanisa lenyewe lililotoa hukumu hiyo. Wakati Kanisa linapojikanganya kwenye hukumu, wale wasioathirika wanapenda kwenda kwenye sheria, wakikata rufaa kwenye vyombo vya sheria dhidi ya hukumu iliotoewa Kanisani inapokuwa inawafaa wao. Kwetu sisi watu hawa tunawachukulia kama wapagani au wamataifa waso na Mungu mioyoni na maishani mwao.

 

18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. 19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.

 

Hii ni ahadi ya Mungu, kwa kupitia Kristo, kwa Kanisa na kwamba sisi tutawahukumu malaika. Ni kwa kiasi gani basi tunaweza kuhukumu mambo ya watu walio Kanisani.

 

21 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? 22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

 

Msamaha unahitajika kwa kiasi endelevu, kwetu sisi wote. Hata hivyo, kunapaswa kuwepo na toba. Tunasamehe kutoka mioyoni mwetu na tunapata kutokana na kazi tuliyoifanywa kwa mikono yetu. Tukiwasamehe wengine, na ndipo Mungu hutusamehe sisi pia. Lakini ili mtu aweze kuaminiwa, kunabidi lionekane kwanza tunda la toba ndani yake. Kusamehe ni jambo linalotulazimu kuwanalo, yaani kumsamehe mtu aliyetuksea.

 

23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. 24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi. 25 Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. 26 Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. 27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. 28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata,akamshika koo,akisema Nilipe uwiwacho. 29 Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. 30 Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. 31 Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. 32 Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; 33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? 34 Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. 35 Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

Hatuwezi kumsamehe mtu na huku tukishikilia aina fulani ya malipo au fidia itolewe nao, au huku tukinung’unika au kuyashikilia mambo tunayoyatenda. Na wala tusipende kuwalaumu vikali ndugu zetu. Hakuna mtu anateweza kukizuia kile kilicho katika Roho. Hakuna mtu anayeweza kuishi sawa sawa na vile ilivyo kwenye Kanisa. Italila Kanisa kama inavyofanya saratani.

 

Wazo la kujinyenyekesha sisi wenyewe kwa Mungu ni moja ya amani na wanadamu kwenye mapenzi ya Mungu. Inatupasa kumpinga Shetani naye atatukimbia. Tunapaswa kumkaribia Mungu naye atatukaribia. Na tuisafishe mikono yetu, sisi ni wenye dhambi wakubwa; na tuitakase mioyo yetu, na tusiwe watu wa kutangatanga au wenye nia mbili. Tumeambiwa tujitese, na tuomboeze na kuhuzunika; na kicheko chetu kigeuke kuwa maombolezo ay huzuni na furaha yetu kuwa huzuni, na tujinyenyekeshe machoni pa Bwana,  naye atatuinua juu au kututukuza. Wala tusidanganyane wala kusemana vibaya, wapendwa. Yeye amneneaye mwenzake vibaya na kumhukumu ndugu yake, basi anainene vibaya sheria, na anaihukumu sheria; bali kama tutaihukumu sheria, ndipo mioyo yetu hitakuwa watendaji wa sheria, bali ni wenye kuhukumu tu.

 

Hakuna aliyemchagua mtu mwingine kuwa ni hakimu wake, isipokuwa ni mahakama ya Kanisa. Na hukumu hii na itendeke kwa haki na utakatifu na watu wenye roho na walioitendea kazi imani kwa miaka mingi. Tusitafute wala  tusipende kulaumiana au kueneza lawana na kuchafuana au kutafuta kumshushia hadhi mtu yeyote miongoni mwetu kama ilivyowahi kutokea. Na usijaribu kuwa hakimu hadi utakapochaguliwa kuwa hakimu wa Kanisa.

 

Na pia tusijaribu kutafuta faida au kufaidika kwa kumshuhudia ushuhuda mbaya au wa uwongo mtu mwingine wakati kukiwa hakuna mashitaka. Hakuna aliye wa muhimu kiasi cha kuwa mhukumu au hakimu isipokuwa kwenye mahakama ya Kanisa.

 

Yakobo 4:12 inaendelea kwa kusema:

12 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine? 13 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; 14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. 15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi. 16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya. 17 Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

 

Kwa maneno mengine ni kusema, kama tutakuwa tunajua mambo, basi tunapaswa kuyafanya, na kama hatutayafanya, itakuwa dhambi. Tumetenda yale ambayo Bwana alitutaka tuyafanye tangu mwanzo. Tunajua kwamba Bwana analitaka Kanisa kwa kipindi kingine cha zaidi ya miaka saba mingine ijayo. Tutaihitiwisha il kazi. Mungu na atatusaidia, na haitakuwa ni kitu cha kukanganya.

 

Yakobo 5:1-20

Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. 2 Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3 Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. 4 Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. 5 Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. 6 Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi. 7 Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. 8 Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. 9 Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. 10 Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.11 Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma. 12 Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu. 13 Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi. 14 Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. 15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.

 

Sio kazi ya kulilalamikia Kanisa tu linapoitendea kazi dhambi inapojitokeza miongoni mwetu na kuyatoa majukumu ya kuyafuta. Mungu hutusamehe dhambi zetu tunapobatizwa na kwene maadhimisho ya Pasaka. Maombi ya mwenye imani htmuokoa sisi na yanatuunganisha pamoja na hulisaidia Kanisa. Sisi sio wengi hapa duniani. Kila adhimisho la Sikukuu, mara tatu kwa mwaka, ni hija ambako tunakutana kila mmoja wetu kwa watu wale wale hadi pale Mungu amchague na kumuongeza mtu kwenye ushirika hu. Ni kazi na wajibu wetu kuutunza mwili huu, na kama kuna mtu aliyepotea kwa ajili ya sisi kumkwaza ni makosa yetu. Tusijione kuwa ni wenyewe tu na kutoutilia maanani ukweli kwamba kuna watu wamefanyiwa hila hadi waondoke kwenye imani. Mungu hutuongeza na ni yeye ndiyr anayewachukua kutoka kwetu.

 

Hatari iliyoko ni kwamba, tunajiona vizuri tu wakati Mungu anapowaondoa watu kutoka kwetu. Hata hivyo, baadhi ya watu wanaondolewa kutoka kwetu kimakosa wananyonywa na wale wanaotgaka kutuangamiza. Wala tusiwalaumu. Bali na tumlaumu mshitaki wa ndugu zetu anayetushambulia.

 

16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

 

Sisi miongoni mwetu ambao hatuna uwezo wa kusaidia kimwili tunaweza kuomba kwa bidii kwa kuwa maombi yananguvu na yanathiri karibu kazi zetu kama sio zote.

 

17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. 18 Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake. 19 Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; 20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.

 

Hii haimaanishi kuwa kila mtu amepangiwa kukosoa au kurekebisha au kusahihisha mawazo yasiyo sahihi na mwenendo wa wapendwa. Kila kitu tunachokifanya kinapaswa kitendeke kwa kuzingatia upendo na wema, na sio kwa shutuma na sio kwa kupenda kujitafutia lawama au mashitaka dhidi ya ndugu zetu.

 

Ni bahati mbaya sana kwamba ni Yakobo peke yhake tu ndiye aliandika waraka mmoja tu kwa kuwa uelewa wake ulikuwa ni kmubwa sana kuliko wa Paulo. Uwezo wake ulikuwa ni mkubwa sana kwa kuwa pia alikuwa ni mtume kiongozi na ndugu yake Kristo. Kwenye uelewa wake wa sheria na sheria kamilidu ya uhuru anatupa muongozo kwamba tunapaswa kuzishika na kuzitenda sheria na tuendende kwazo. Tunapaswa kuchukuliana na ushirika ambao Yakobo anauelezea kwa kuwa ulikuwa unaenenda kinyume na waraka huu wa Yakobo na alipoona kwamba Kanisa lilikuwa linakaribia kwenye uangamifu au uharibifu.

 

Kitendo cha kuwapendlea watu hupelekea kuwepo kwa mgawanyiko na mafarakano. Tabia hii ya kuwapendelea watu au upendeleo imebaka kuwa ni dhambi moja kubwa kabisa kubakia kwenye Makanisa ya Mungu.

 

q