Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[019]

 

 

 

Umri wa Kubatizwa kwa Kristo

na

Urefu wa Kipindi cha Huduma Yake

 (Toleo La 3.0 19920101-20050314-20071213)

 

Mwaka wa aliozaliwa Kristo umesababisha malumbano ya kuujua au kuuamua kwa miaka mingi sasa. Inaonekana kuna mpango wa makusudi wa kuuficha. Huenda imefanywa hivyo ili isikadirike na kupata kipindi mjaarabu cha mwaka wenyewe halisi ili kuzuia kuchanganywa na maadhimisho ya imani za kipagani zikihusianishwa na kuzaliwa kwake. Hata hivyo, kuna idadi kadhaa ya mambo ya kweli na muhimu yanayoendana sambamba na kuzaliwa kwake na kipindi cha kubatizwa kwake.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 1992, 2000, 2005, 2007 Wade Cox)

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Umri wa Kubatizwa kwa Kristo na Urefu wa Kipindi

cha Huduma Yake


 


Imeelezwa na kusisitizwa sana na baadhi ya watu wa kanisa kwamba kifungu kilicho kwenye Luka 3:23 kinaashiria kwamba Kristo alibatizwa akiwa na miaka thelathini kamili. Kifungu hiki kimetafsiriwa kwenye tafsiri ya Mfalme Yakobo au King James Version kama:

“Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini”

 

Tafsiri ya Moffatt inatafsiri kifungu hiki kama:

“Wakati huo Yesu alikuwa anaumri wa takriban miaka thelathini.”

 

Maneno yaliyotumika ambayo imetafsiriwa kwayo ni maneno mawili ya Kiyunani. Moja kati ya yale neno hili limetokana nalo la alianza linatokana na neno •DP`:,<@H (kutoka archomai). Hii inamaanisha katikati ya au kuanza kwenye wakati muafaka. Neno asilia ambalo ni chimbuko lake ni archo, kuwa kwenye daraja au cheo cha kisiasa kwanza au mamlaka, kwa maana ya kutawala kama sehemu ya eneo dogo lake.

 

Neno la pili ni ¦Jä< JD4V6@<J" (ètõn triákonta) au miaka thelathini, muongo wa thelathini. Kwa hiyo, maana sahihi ni kwamba Kristo alitangulia miaka thelathini yake, au kwa maneno mengine, Kristo alikuwa kwenye zama yake ya ujana wa miaka thelathini, kama tungalivyoweza kusema.

 

Maenezo haya yana mabadiliko mnyumbuisho mengine yasiyoendana nayo, na kwa ajili ya hali yao ya kutochukuliana kwao na ugumu wao hujikuta walifanya mkanganyiko kwenye Maandiko Matakatifu mahala pasipotakiwa kuwa.

 

Mfano wa mkanganyiko usio na umuhimu unaonekana kwenye uwekaji kikomo huu wa miaka thelathini na sharti la kwamba alizaliwa kipindi cha utawala wa Herode Mkuu, yaani kabla ya Pasaka ya mwaka 4 KK, na kuzaliwa kipindi cha hesabu ya watu ya kodi ya ulirnwengu wote iliyoamriwa na Augustus, na aliuawa wakati Quirinius akiwa Liwali wa Syria (Luka 2:3). Sasa basi, Sulpicius Quirinius aliliteua au kulichaguliwa Baraza la Roma mwaka 12 KK, lakini hakumteua kuwa Liwali wa Syria hadi mwaka 6 BK, na kufa huko Roma mwaka 21 BK.

 

Maneno halisi yaliyotafsiriwa kuwa Liwali wa Shamu au Syria yanamaana ya wakati Quirinius “alipokuwa na amri ya kifalme”: Schürer anasema kwamba hii ilikuwa ni kitu kimoja kama ofisi ya Liwali (kwa mujibu wa kitabu cha History of the Jewish People in the Age of Jesus Christ, [Historia ya Wayahudi Kipindi cha Yesu Kristo] vol. 1, p. 424).

 

Ushahidi wa hivi karibuni unaodaiwa na wataalamu wa mambo ya kale unatajwa kuwa kwamba kulikuwa na hesabu ya watu iliyoamriwa na Quirinius mwaka wa 12 KK, mwaka aliofanywa kuwa ni Mwaklishi na kupewa majukumu haya ya kushughukilia mambo ya upande Mshariki. Kwa kweli aliongoza kikosi cha jeshi dhidi ya waasi wa pande za milimani (Wahomodenses au Wahomonadenses) huko Alecia na kwa kufanikiwa kwake alipokea ushuru wa kodi huko Rome. Wahomonadenses walikuwa ni wafungwa au mateka wa Wacilician wanyang’anyi walioishi upande mpaka wa kusini mwa Galatia na waliitwa jina hilo na Strabo. Quirinius alitumia miaka 14 kuwatiisha watu hawa kati ya mwaka 12 KK na 2 BK. Kwa aajili ya utaalamu au ufundi huu alitakiwa amsindikize Kaisari Gaius kuelekea mashariki akiwa kama mkufunzi waake mwaka 2 BK.

 

Kwa kweli, Quirinius alihitimisha mkakati wake wa kuhesabu watu mwaka 6/7 BK yeye mwenyewe, lakini haiwezekani kabisa kuidhania kuwa hii ilikuwa ni hesabu ya watu iliyofanyika wakati wa kuzaliwa kwa Kristo., p. 423).

 

Ofisi ya Liwali wa Syria ilishikiliwa tangu mwaka 10/9 KK hadi yapata mwaka 7/6 KK na Sentius Saturninus, na tangu mwaka 7/6 KK hadi 4 KK na Quinctilius Varus. Na ndiye aliyekomesha waasi baadae huko Palestina ambayo yalienea na kushika kasi baada ya kifo cha Herode. L. Calpurnius Piso anadhaniwa na wengi kuwa alikuwa ni Mwakilishi wake tangu mwaka 4-1 KK baada ya Kaisari Gaius kufanyika kuwa Jumbe Imperium, huenda pamoja na Liwali wa kawaida huko Syria.

 

Schürer anadhani na kukadiria kuwa anayedhaniwa kuwa huenda mtangulizi wa Sentius Saturninus alikuwa ni Titius, na anahitimisha pia kutokana na maagizo ya Utozaji kodi ya Herode Mkuu, Phillip na Agrippa (na Agrippa II) kwamba “Kodi za Warumi zisiwe zinakusanywa huko Palestine wakati wa utawala wa Herode na matokeo yake hakuna hesabu ya watu iliyofanyika huko Roma kabisa” (ibid., p.430).

 

Pia Schürer anakataa utengenezaji wowote wa muundo wa kigrama unaohalalisha wazo la kwamba hesabu hii ya watu ilikuwa ni ya kwanza ilifanyika kabla (au mapema zaidi yake) kipindi ambacho Quirinius alikuwa Liwali wa Syria (ibid., p. 42l). zaidi sana, mtindo na utaratibu wa kiuandishi wa Luka unaweka kando uwezekano wa kile kinachodaiwa kuwa ni matumizi ya kigrama.

 

Schürer anadhania kuwa huenda Quirinius alikuwa ni Liwali wa Galatia-Pamphylia wakati wa vita na Wahomonadenses (tangu Strabo XII 6,5 (567) 9 Tat. Ann. III, 48); anasema katika mwaka wa 4-3 KK (ibid., p. 259). Hatahivyo, hakuna sababu ya kutojumuisha vipindi vya mwanzo vya tangu mwaka wa 12 KK. Kwa kweli, inawezekana sana kwamba tangu mwaka 12 KK au 8 KK, Quirinius alikuwaainafanyia kazi komandi yote ya kijeshi ya kaskazini mwa Syria, au kwa muda tu kwenye komandi hii ya Syria baada ya Sentius Saturninus. Kwa mujibu wa T.P. Wiseman, hesabu kamili ya wakazi wa nchi ya mwisho ilifanyika kabla ya Quirinius kwa kuwa Liwali wa Syria mwaka 6 BK alikuwa katika mwaka 8 KK, wwakati ambapo Quirinius alikuwa Kamanda wa Jeshi na Liwali kama alivyokuwa katika Galatia-Pamphylia, kama waasi walikuwa upande wa kusini wa maeneo ya Galatia.

 

Mnamo mwaka 4 BK Augustus aliamuru ifanyike hesabu ya watu kwa sehemu fulani, na mwaka 6 BK uhesabuji huu uliendelea na kuyajumuisha majimbo kwa asilimia tano ya kodi ya urithi (Vicesima hereditatis).

 

Ugumu ulioonekana dhahiri kutokana na malumbano ya kuhusu hesabu ya watu iliyofanyika mwaka 6 iliyotajwa ni wakati alipokuwa Liwali wa Syria. Ilikuwa ni kama miaka 10 hivi baada ya kufa kwa Herode, na kwa hiyo haiwezekani.

 

Luka anasema kwamba hii ilikuwa ni ile hesabu ya watu ambayo “iliwajumuisha watu wa ulimwengu wote”. Baada ya kuondolewa kwa Archelaus, Palestina iliongezwa katika Syria kwa sababu za kimaongozi na kodi, kwa mujibu wa Josephus (A. J. XVIII, 1, 1, 2).

 

Hesabu ya watu iliyofanyika mwaka 12 KK au mwaka 8 KK kwa amri ya Augustus ni jambo kubwa sana kuliongelea zaidi ya hesabu ya watu ya Wapalestina, na dhahiri kabisa tu kwamba Josephus anajaribu kuiwekea kikomo hesabu hii katika mwaka 6 BK wakati Quirinius alipokuwa Liwali wa Syria.

 

Matendo 5:37 inaonyesha siku za kutoza kodi sambamba na kuinuka au kuibuka kwa Yuda wa Galilaya. Kuibuka huku kwa Yuda wa Galilaya kulitokea baada ya kuibuka kwa Theudas na wafuasi wake wapatao 400 (aya ya 26).

 

Kuibuka kwa Yuda wa Galilaya kunakadiriwa Schürer kuwa ilikuwa ni mwaka 6 BK. Wanahistoria wanamuonyesha Gamalieli kuwa ni kama uanzilishi wa Ukristo ilisaidiwa na Gamalieli, na kumtaja Theudas wa kwenye Matendo kuwa ni kama Theuda nabii wa uwongo wakati wa mamlaka ya Hakimu wa kwanza aliyepelekwa huko Palestina na Claudius, yaani Cuspius Fadus katika miaka ya 44- 46? BK.

 

Schürer anaondoa uwezekano wa wanaoamini kuhusu Theuda mapema kabla ya mwaka 6 BK (ibid., Vol. 1, pp. 456-457, note 6), na kumbuka kuhusu mamlaka ya Matendo kidogo. Ni dhahiri sana kuwa anatilia maanani utozwaji kodi ulioelezewa kwenye Matendo kuwa ni kama utozaji huu au hesabu hii ya watu wa Quirinius kwenye dhana hii akiwa kama Liwali wa Syria mwaka 6 BK. Haijalishi kabisa kuamini au kusema kuwa wana wa Yuda Mgalilaya, Yakobo na Simoni waliamriwa kusulibiwa na Tiberius Julius Alexander (?46-48 BK), mrithi wa Fadus.

 

Ni jambo lisilowezekana kabisa kwamba utozaji kodi unaotajwa na kitabu cha Matendo wa mwaka 6 BK, lakini utozaji kodi ule sio uleule utozaji uliotajwa kwenye Luka kuwa ulifanyika alipozaliwa Yesu.

 

Mtangamano kamili unajitokeza, hata hivyo, iwapo kama tarehe ya uhesabuji wa watu wote ulioamriwa na Augustus na haukufanyika upande wa mashariki kwa kuzuiwa na Quirinius ni ule wa mwaka 12 KK au hata mwaka 8 KK. Kwa hiyo, Kristo anafikisha umri wa miaka kati ya 39 au 35 wakati alipobatizwa, yaani ni hadi kwenye thelathini hizi. Kwa hiyo kuna miaka kati ya tisa au minne kati ya kuzaliwa kwake na kufa kwa Herode. Hii inaruhusu haja ya kufanyia udadisi, kuhusu uendaji wake huko Misri, mikanganyiko na matatizo ya familia ya Herode, yanavyoleta kuzozania urithi na makazi ya zama za nyuma kujitokeza na kufanyika maamuzi ya kuwaua wenye hekima na wana waliotokana na nyumba ya kifalme wote wa Yudea kwenye miaka ya 5/4 KK, na kunafanya kusiwe na ugumu wa kuwianisha mirejesho yote mitatu ya kibiblia. La kulijua sana ni kwamba familia ya Herode na urithi wa makazi yake tena na uwongo na usaliti wa kizazi chake, vilianza mnamo mwaka 12 KK, kuanzia kila wanahistoria wanachokijua kuwa ni kama awamu ya tatu nay a mwisho na ni awamu ya mwisho ya utawala wake.

 

Maandiko ya Tertullian yanatupiliambali baadhi ya mambo muhimu, ingawaje anajichanganya mwenyewe.

 

Kweny tukio hili la kiusaliti akiandika Kitabu kiitwacho Dhidi ya Marcion [Against Marcion], Tertullian anasema kuwa ushahidi wa kihistoria ulikuwa kwamba Kristo alizaliwa wakati hesabu ya watu ikiwa imefanyiwa huko Yudea na Sentius Saturninus (Adv. Marc., IV, 19, 10, ANF III, p. 378). Luka (sura ya 2) inasema wakala waliyeisimamia huko Yudea alikuwa (Sulpicius) Quirinius. Tertullian anamuelezea Saturninus tena kwenye kitabu au makala ya De Pallio akisema 1. Usemi huu wa Tertullian umepimwa na Sancelemente na wengine ambao wanaosema kwamba Saturninus alikuwa liwali wa Yuda katika kipindi cha kuzaliwa kwa Kristo, na wakaiweka tarehe hii kuwa ni mwaka 747 A.U.C. Tertullian akishikilia hivyo na kuandika kwenye kitabu chake cha Adversus Judaeus VIII, anadai kabisa kwa kuupa mwaka 751 A.U.C kuwa ni kama mwaka aliozaliwa Kristo.

 

Anachosema ni kwamba Kristo aizaliwa katika mwaka wa arobaini na moja wa Mfalme Augustus alipokuwa anatawala kwa 'xx na viii' miaka (28) baada ya kufa kwa Cleopatra (51-30 KK). Augustus anadhaniwa na Tertullian kwenye kitabu chake kuwa aliendelea kuishi baada ya kuzaliwa kwa Kristo kwa miaka kumi na mitano zaidi, maarufu kwa tarakimu ya 'xv' (15). (Aliheabu kiusahihi miaka hii na kuwa ni kama miaka 437 na miezi 6 baada ya Dario.)

 

Kaisari aliuawa mwezi Machi mwaka 44 KK na Octavian alirejeroa Roma ili amrithi au ahukue kiti chake mwaka 42 KK. Kwa hiyo, miaka 56 tangu mwaka 43/2 KK unatupeleka hadi kwenye mwaka 14 BK, mwaka wa kufa kwake.

 

Augustus anasemekana kuwa alitawala miaka 44, na alikufa mwaka 14 BK. Hata hivyo, ni baada ya kupinduliwa kwa kina Mark Anthony na Cleoptara. Tertullian anasema kuwa alitawala kwa miaka 56. Kwa hiyo, kwa ajili hiyo Kristo alizaliwa mwaka wa 41 wa kutawala kwake, na miaka 28 baada ya kufariki kwa Cleopatra, yaani ni mwaka wa 2/1 KK, miaka miwili baada ya kufariki kwa Herode – ambayo haiwezekani kibiblia. Hesabu hii kwenye kitabu hiki cha Adversus Marcionem inafanya kuzaliwa kwa Kristo kuwe ni mwaka 6/5 KK. Kwa hiyo, ingeweza kuwa ni mwishoni kabisa mwa uliwali wa Saturninus, hata kama tunakadiria kwa kuzingatia kipindi cha upana wa siku zinazoonewa mashaka hadi mwezi Septemba wa mwaka 7/6 KK. Kwa hiyo Qurinius, ambaye alikuwa mpakani mwa Syria na Galatia wakati ule vitani waliyokuwa wanapigana na wanyang’anyi wa Kicilician Wahomonadenses, wanaweza kuwa wametumwa na Saturninus huko Yudea kwa ajili ya hesabu hii ya watu ya mwaka wa 6 KK, na Kristo alizaliwa mwaka uliofuatia wa 5 KK, kwa hesabu za Tertullian na Luka kwenye maandiko mengine ya kale.

 

Sentius Saturninus alikuwa ni liwali wa Syria tangu mwaka 744-748 (sawa na kitabu cha ANF, ibid., fn. 3) au mwaka wa 10/9 hadi 7/6 KK. Aug. W. Zumpt anaenda mbali zaidi kuthibitisha kuwa Publius Sulpicius Quirinius hakika ndiye alikuwa liwali wa Syria wakati wa kuzaliwa kwa Kristo. Mawazo hayo hapo juu yanaweza kuwa ya kweli kabisa.

 

Josephus anamuita Volumnius pamoja na Saturninus (Jumbe katika mwaka 19 KK) (Jos. Ant., XVI, 9, 1, p. 280). Hata hivyo, kwenye kitabu kijulikanacho kama Vita Vya Wayahudi [Wars of the Jews] (I, 27, 1) anamuita Volumnius tou stratopedarchen na kwenye kurasa za I, 27, 2 anamuita epitropos. Kwa hiyo Schürer anaamini (vol. 1, p. 257) Volumnius alikuwa  ni afisa msaidizi wa kikosi cha wapanda farasi Saturninus na hakimu wa jimbo. Saturninus amatajwa pia na Josephus kwenye kitabu chake cha Antiquities XVI, 10, 8, (344); II, 3 (368); XVII, 1, 1 (6); 2, 1, (24); 3, 2, (57). Kutumiwa kwa Qurinius na Saturninus kulionekana kabisa kuwa ni kwa namna moja tu ya mkaguzi wa shughuli ya kuhesabu watu ya Yudea ya wakati ule. Schürer hafichi au kufunika hali hii, ya kile kinachoonekana ni ufafanuzi wa wazi. Rekodi zinawaonyesha wote wawili, kama tunavyoona pia kwa Volumnius na Saturninus hapo juu.

 

Kifo cha Herode linafanya kazi muhimu katika kuweka tarehe ya mwisho inayoonekana kuwezekana kuwa kuwaliwa kwa Kristo kulifanyika, kama tunavyojua kutoka kwenye Injili ya Mathayo 2:12 kwamba kuja kwa Mamajusi au wataalamu wa elimu ya Nyota na vitu vilivyo juu winguni kuliishia kwa mataalamu hawa kurudi kwenye nchi yao wakipitia njia nyingine, ili kwamba wajiepushe wasirudi kwa Herode. Yusufu alionywa ndotoni na Malaika wa Bwana waondoke na waende Misri, kama tunavyosoma kwenye Mathayo 2:13-16:

Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.

 
Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;


Akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwanangu.


Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi.

 

Kwa hiyo, kipindi cha kutembelewa na Mamajusi na kinachotarajiwa kuzaliwa kwa Kristo vilikuwa ni hadi miaka miwili kabla ya kuuawa kwa watoto huko Bethlehemu. Jambo hili linaweza kuonyeshwa na Josephus kwenye hesabu zake za kipindi walichouawa watu muhimu katika Yuda na Herode kipindi cha nyuma kabla ya kufa kwake.

 

Kwa hakika, hesabu hizi zinakuja miezi mingi kabla ya kufariki Herode – na huenda ni kipindi cha miaka miwili – ambapo huenda Kristo alizaliwa ndani ya kipindi cha miaka miwili cha tukio lililoripotiwa kufanywa hiko Bethlehemu, kipindi ambacho Herode hajafariki.

 

Kuhitimisha ukimbiliaji wao na kwenda Misri, kipindi husika hakikuweza kupugua chini ya mwaka mmoja. Wanahistoria wanakielezea kipindi hiki cha kufariki kwa Herode kuwa ni kipindi cha kati ya siku ya 1 hadi ya 14 Nisani (sawa na tarehe 28 Machi hadi 10 Aprili) ya mwaka wa 4 KK kwa sababu zifuatazo:

1. Warithi wawili wa kiti cha Herode walikuwa ni Archelaus na Antipas.

 

Archelaus, kwa mujibu wa Dio IV 27.6, alikuwa amefukuzwa na Augustus mwaka wa 6 BK katika mwaka wa kumi wa utawala wake (pia A. of J. XVII, 13, 2(342) wa Vita 1(5)) alisahihisha maelezo ya mwanzoni ya B.J.: II, 7, 3, aliyesema kuwa mwaka wa tisa. (Hii ilikuwa ni wakato wa ujumbe wa Aemilius Lepidus na L. Arvuntius.) Na kwa hiyo alianza utawala wake katika mwaka wa 4 KK.

 

Antipas alikuwa amefukuzwa na Caligula wakati wa majira ya baridi ya mwaka 39 BK. Kwa kuwa kuna utata wa kimahesabu tangu mwaka wa 43 wa utawala wake, utawala wake ulianza mwaka wa 4 KK.

 

2. Kutokana na hesabu za Josephus za kuhesabu kipindi hiki, kama alivyoshauri Mishnah, kutoka mwezi Nisan hadi Nisan ya miaka ya kutawala kwake na kuigawanya miaka, kuwa sehemu inayotangulia mwezi wa Nisan omehesabiwa kama miaka kamili; kwa hiyo Schürer anakiweka kifo cha Herode kuwa kilitokea katikati ya siku ya 1 na 14 Nisan, mwaka 4 KK.

 

Kipindi kifupi sana kabla ya kufariki kwa Herode kulikuwa na tukio la kupatwa kwa mwezi; tukio hili la kupatwa kwa mwezi limeelezewa kwa kina na Josephus (kwenye A. of J., XVII, sura ya 4). Kulikuwa ma matukio mawili ya kupatwa kwa mwezi yaliyotokea kipindi hiki: moja lilitokea mwaka 5 KK na jingine katika mwaka 4 KK. Kupatwa kwa mwezi kulikotokea mwaka 4 KK ilikuwa ni tarehe 13 Machi, na hii ni kulingana na rekodi za Josephus. Josephus anaweka kumbukumbu kwamba nafasi ya Kuhani Mkuu, Matthias, ilichukuliwa na Yusufu, mwana wa Ellemus, awe Kuhani Mkuu (kutokana na hali ya yeye mwenyewe kunajisika kutokana na ndoto mbaya alizoota usiku uliopita). Hii ilikuwa ni siku ya funga ya saumu ya Wayahudi. Funga ya saumu ya Esta iliangukia tarehe 13 Machi, mwaka 4 KK, na matukio haya pamoja nay ale ya kupatwa kwa mwezi. Hakuna kumbukumbu inayoonyesha kama kulikuwepo kupatwa kwa mwezi mwaka wa 3 KK au wa 2 KK, na inaonekana tu katika mwaka wa 5  KK tarehe 15 Septemba na mwaka w 1 KK tarehe 9 Januari ambapo kulikuwa na tukio hili la kupatwa kwa mwezi pia na kabla ya Pasaka ya mwaka 4 KK. Tafsiri ya Marcus ya Josephus ina mengi yaliyoandikwa kuhusu sehemu hii kuliko ile ya Whiston na inasaidia sana. Schürer, kwa kiasi chake, amelielezea jambo hili kwa kina kwenye kitabu chake kiitwacho Historia [History] (Vol. 1, pp. 326-328).

 

Kwa kipindi cha miaka miwili cha kutembelea kwa Mamajusi kwenye Mathayo 2 kinahesabiwa, kwa hiyo Kristo asingeweza kuzaliwa katika kipindi kingine chochote zaidi ya kile cha baada ya Pasaka ya mwaka 6 KK. Wakati Yusufu aliporejea kutoka Misri alimkuta Archelaus anatawala huko Yudea, kwa hiyo kurudi kwake kutoka Misri kungefanyika katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Archelaus, yaani mwaka 4 KK.

 

Kutoka kwenye Luka tunajua kuwa Mariamu, kimakosa sana anaitwa Maria, alipandisha kwenda Yerusalemu baada ya kutakasika kwake kwa mujibu wa desturi na maagizo ya Torati akafuatana na Yusufu ili akamtoe mtoto kwa Bwana, na kwenda kutoa dhabihu iliyohitajika kwa mujibu wa desturi ya utoaji wa dhabihu (Luka 2:22-24). Tukio hili lilitangulia lile la wao kukimbilia Misri. Luka haelezei tukio hili la kukimbilia Misri; zaidi tu anaelezea kuwa walirejea Nazareth. Kipindi cha kutakaswa kwa ajili yam toto wa kiume ni siku 40 (+1) siku ya (8 ni ya kumtahiri na kisha siku thelathini na tatu) (Mambo ya Walawi 12:1-4; sawa na jarida la Utakaso na Tohara (Na. 251) [Purification and Circumcision (No. 251)].

 

Kwa hiyo. Kristo asingeweza kuwa amezaliewa baadae zaidi kuliko Februari 4 KK hata kama Yusufu alikuwa amekwitoka kimbilia Misri baada ya kufa kwake Herode. Hii ni wazi kabisa kuwa haikufanya, kama ilivyokuwa kwamba hakukuwa na matarajio ya kifo chake wakati walipoondoka, na Yusufu aliishi Misri hadi ale Maalaika wa Bwana alipomtokea Yusufu wakati alipokufa Herode. Ni wazi kaisa kwamba Kristo asingeweza kuzaliwa katika mwaka ujulikanao kama ni wa 4 KK, na tangu siku au tarehe ya kutoza kodi na kipindi ch miaka miwili kati ya ujio wa Mamajusi na mauaji ya watoto wachanga yaliyofanyika huko Bethlehemu ni kipindi kinachoonyesha kuwa ni cha miaka miwili. Kipindi hiki, pamoja na kile cha kukimbilia Misri mapema kabla ya kifo cha Herode, inaonyesha kuwa haiwezekani kuwa Kristo alikuwa amekwisha zaliwa tayari baada ya Pasaka ya mwaka 6 KK. Miaka ya kuhesabu watu kwa hiyo, ni jambo jingine kubwa kulijua.

 

Kwa sababu ya kifo cha Herode wakati wa Pasaka ya mwaka 4 KK, Kristo angekuwa na umri usiopungua miaka 31, na kwa kutazama baadhi ya taarifa za kbiblia inaonekana kuwa kana kwamba alikuwa na umri wa miaka 35 au 39. Kwa yeye kuwa na umri wa chini ya miaka 31 ni lazima awe alizaliwa mwaka 6 BK, na tafsiri inamaanisha muongo wa tatu, yaani katikati ya miaka ya 20 (yaani mwaka 22), lakini hii haiwezekani kama inavyoikanganya Injili na sharti la kuwa na umri wa miaka 25 ili aruhusiwe kuhudumu Hekaluni na kuwa na umri wa miaka thelathini ili aruhusiwe kufundisha.

 

Tarehe ya mwanzoni kabisa kudhaniwa ni mwaka 8 KK pamoja na tukio la kuhesabu watu wote lililofanyika kabla ya kufariki kwake Herode, na kumfanya Kristo awe na umri wa miaka 35 mwanzoni mwa mwaka wa 27/8 BK.

 

Haiwezekani hata hivyo, kwamba Quirinius aliweza kuamrisha hesabu ya watu wote mwaka 12 KK ili kuzitamalaki Galatia, Kapadokia na Syria kwenye vita dhidi ya majambazi, kama uporaji ulivyoripotiwa pia kuwa ulifanyika mapema kuanzia Trachonitis wakati Augustus alipourudisha kwa Herode mwaka 24/23 KK. Anaweza kabisa kuwa aliitumikia kamandi yote ya kijeshi ya eneo adi pale M. Titius alipofanyika kuwa Liwali wa Syria.

 

Angeweza pia kufanya hivyo akiwa kama kamanda au jemadari wa kijeshi chini ya Liwali Saturninus na mbele ya Varus mwaka 8/7 au 7/6 KK, kama sehemu ya hesabu ya jumla ya watu iliyoamriwa na  Augustus.

 

Wanahistoria kia Gerlach, Quandt na Hahn wanafafanua madaia ya Zumpt pamoja na mtazamo wa kuwa Qurinius alitumwa huko Syria pamoja na Quinctilius Varus (6-4 KK) akiwa kama liwali wa akiba na wa nyongeza, na afanye shughuli za kuhesabu watu vilevile (pia soma kitabu cha Schürer vol. 1, p 424). Kwa hiyo, kwa mtazamo huu tunaweza kuona kuwa aliwasili mnamo mwaka 6 KK wakati Varus alipowekwa madarakani badala ya Saturninus.

 

Sanclemente aliwakilisha mtazamo kama huo kwa kuweka kuwa Qurinius ametumwa huko Syria akiwa kama liwali kahsusi aliyeandaliwa na mamalaka ya juu zaidi ya yale ya liwali wa Kisyria wa wakati ule, aliyejulikana kwa jina la Saturninus.

 

Schürer Kwenye kitabu hichohicho (ibid.) anadhania kwamba maneno ya Luka, kwamba yeye alikuwa na kamandi bora zaidi ya kijeshi, inamaanisha mapema sana kabla yake: wakati alipokuwa liwali wa Syria. Hata hivyo, anaweza kabisa kuwa alikuwa na kamando bore zaidi ya majeshi huko Asia Ndogo kwa ajili ya vita dhidi ya Mauaji ya Kimbari ya Kuwaangamiza Wsayahudi maaufu kama mauaji ya Homonadenses, na alikuwa na kamandi ya Kijeshi kwa ajili ya Galatia na Syria. Maelezo yote yanafanya hesabu zote ziwe kwenye uwiano na mtangamano. Mtazamo wa Wanahistoria wote ni kwamba alikuwa na kamandi hii mwaka wa 6 KK mwanzoni mwa ukomo wa utawala wa Warus. Kwa hiyo imepingwa wazo la kwamba mchakato wa kuhesabu watu uliamrishwa ufanyike kwenye nusu ya mwisho ya mwaka 6 KK iliendelea vema kwenye mwaka 5 KK.

 

Mwaka 23 KK Augustus alimpeleka M. Agrippa, rafiki yake mkubwa na mshauri wake aende huko Syria, na mnamo mwaka 21 KK akampeleka mjukuu wake. Wadhifa wake ulikuwa ni Makamu wa Kaisari atawalaye maeneo yaliyombali na Bahari ya Ionian (Josephus, A. of J., XV, 10,2) na alipewa nguvu kubwa za kiutawala zaidi ya anayoshahili kupewa Liwali au Jumbe wa kawaida. Hatahivyo hakuweza kwenda kwenye kisiwa cha Lesbos kilichoko huko Mytilene tangu mwaka 23-21 KK. Alirejea Roma ambako alikuwa na shughuli nyingi upnde wa Magharibi kwa kipindi cha miaka mine. Mnamo mwaka 16 KK alirejea hadi Mashariki ambako alibakia hadi mwaka 13 KK, na alitumika shughuli zake ya kiutawala kwa kupitia Manaibu wake. Kwa hakika ntu huyu aliendesha majukumu yake ya kiutawala huko Mashariki, na hasa huko Syria, hajulikani, lakini alipewa kamandi ya kijeshi ya Quirinius na akapandishwa cheo hadi kuwa Jumbe mwaka 12 KK, inaonekana kabisa kuwa aliweza kuwa alisimamia mikkati yote ya kamandi ya kijeshi hadi M. Titius alipochukua tena uthibiti katika Syria, na tunajua kuwa alifanya hivyo hadi mwaka 10 KK, kama anavyosema Josephus kwenye maandiko yake, akimtaja yeye kuwa kama Liwali wakati wa mzozo wa Herode alipogombana na wanaw. Mabishano na migongano hii na ile iliyofuata baadae ya kugombea urithi yaliyoibuka kwenye familia ya Herode yanaweza kuwa yaliishia katika kpindi cha kuzaliwa kwa Kristo, au hata wakati aliokuwa anatarajiwa kuzaliwa, kwa mujibu wa unabii, kama kkulivyokuwa na ushahidi mwingi kwenye dini na madhehebu mengi katika jamii zetu ya matarajio ya Masihi wa Haruni.

 

Kuzaliwa kwa Kristo, mapema sana kabla ya mwaka 12 KK, bado ni jambo linaloonekana kuhitaji kusahihishwa kabisa kwenye kila kinachojulikana kama rekodi iliyochukuliwa kwa mujibu wa Injili, na uwezekano mkubwa wa harakati za mwaka 8 KK haziwezi kuzimwa.

 

Hakuna hesabu ya watu ya dunia nzima inayokumbukwa kuwa ilifanyika mwaka 6 KK au 5 KK. Taarifa za Luka zinaweka wazi sana jambo hili na zinajitosheleza. uhesabuji huu wa watu unawezekana kuwa ulifanyika vizuri kwa mujibu wa matakwa ya Augustus, hususani kwa ajili ya muono wake kwa matatizo yalilojitokeza huko Galatia-Pamphylia, Syria na Yudea. Jaribio lolote linalokusudia kufanya madai ya kimapokeo ya kidini kuwa Kristo alibatizwa akiwa na umri wa miaka 30 yanaanzisha mabishano yasiyo na ulazima wowote na kutofautisha yanayosemwa kwenye Injili hizi zote na yanayosemwa hata na Biblia yote kwa ujumla.

 

Ili kuweka wakati ambao Kristo alibatizwa na kutoka hapo lini alianza huduma yake, na maana ya wakati wa kuanza huduma yake yalikuwa nini, inatupasa tuanze kwanza na kuitafakari huduma ya Yohana Mbatizaji.

 

Tunajua kutoka kwenye Luka 3:1 kwamba Yohana “alianza kuhubiri katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio,”, jambo ambalo lisingeweza kuanza mapema kabla ya mwezi Octoba ya mwaka 27 BK kama kalenda ya kidunia inayotumika sasa ingekuwa ilitumika upande wa Mashariki. Tiberius alianza kutawala tarehe 17 Septemba, 14 BK, na mnamo mwaka 27 BK unafika kwa hile tu mwezi wa Septemba ikihesabiwa kama mwezi wa kwanza na mwaka wa pili ukaanzia mwezi Octoba, 14 BK. Kwa hiyo hii inaanzisha mwaka wa 15 mwezi Octoba, 27 BK. Wito wa Yohana kuwahubiria watu habari ya toba huenda ulianza tangia Siku ya Upatanisho ya mwaka ule, na kuendelea hadi Pasaka ya mwaka 28 BK wakati alipotiwa mbaroni na kufungwa gerezani. Tunajua kwamba Kristo alibatizwa wakati fulani baada ya mwezi Octoba, 27 BK, na kabla ya Pasaka ya mwaka 28 BK.

 

Ubatizo wa Kristo ulitanguliwa na mwanzo rasmi wa huduma yake na idadi ya matukio yalitokea baada ya kubatizwa kwake, mapema kabla ya kuanza kwa huduma yake wakati wa kufungwa kwake gerezani Yohana Mbatizaji.

 

Kutoka kwenye Luka 3:21, tunajua kwamba Kristo hakuwa miongoni mwa wale aliowabatiza kwanza Yohana, lakini ni kwamba alibatizwa baada ya watu wengi wakiwa wamekwisha kubatizwa; kwa hiyo, kubatizwa kwake kunawezekuwa kulifanyika baada ya Octoba, 27 BK – yawezekana mwaka wa 28 BK.

 

Mwandamano wa nyakati tangu kubatizwa kwake pamoja na siku ya kubatizwa kwake, kisha funga yake ya saumu ya siku 40 usiku na mchana. Alirudi kwa Yohana Mbatizaji na kuwafundisha na kuwaandaa wanafunzi wake kwa takriban siku 3 (Yohana 1:35-45). Siku ya tatu kulikuwa na arusi huko Kana ambako alifanya muujiza wa kuyageuza maji kuwa divai (Yohana 2:1). Kisha akaenda Kapernaum ambako “hakukaa siku nyingi” (Yohana 2:12). Kisha Pasaka ilikuwa imekaribia.

 

Kwahiyo, kipindi kilichojiri kati ya kubatizwa kwa Kristo na Pasaka ya mwaka 28 BK kilichukua jumla ya siku 44, pamoja na ‘siku chache kadhaa’ (aay ya 6). Kipindi hiki kisingeweza kuwa kilizidi siku hamsini. Kikpewa pea ya kipindi tangu Pasaka hadi Pentekoste, siku 50 mwishoni mwa kuhudumu kwake, kipindi kilichotangulia hapo huenda ni cha siku 50 pia. Ni hakika kisingeweza kuwa zaidi ya hapo, na kingekuwa cha chini ya hapo. Kwa hiyo, kubatizwa kwake kungefanyika mwaka 28 BK mwezi wa Februari. Kwa hiyo, alipobatizwa alikuwa na wastgani wa umri wa miaka 31 kamili na henda zaidi kidogo.

 

Tunajua kutoka Mathayo sura ya 4 kwamba Kristo hakuanza kuhubiri hadi baada ya Yohana Mbatizaji kufungwa gerezani, wakati alipohamia Kapernaumu (aya za 12-13). Aya ya 17 inasema wazi kabisa: “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”. Mfululizo wa matukio kuanzia aya za 18-22 yanaonyesha kwamba kia Petro, Andrea, Yakobo na Yohana waliitwa baada ya Yohana Mbatizaji kufungwa gerezani, lakini huu ni mpangilio unaoshabihiana wa mtiririko wa habari ili kusaidia mlolongo wa mambo tangu aya ya 23. Mchakato huu upo kwenye Marko 1:14-20, na aya ya 21 inafuatia kuelezea kuingia kwake mjini Kapernaumu.

 

Tunajua kutoka Yohana 2 kwamba Yesu alitenda muujiza wa kuyabadili maji na kuwa divai kabla hajaanza huduma yake (soma Yohana 2:4). “Wakati wake (au saa) ulikuwa haujafika”; na alikuwa na wanafunzi wake pamoja naye, nah ii ilikuwa ni kabla ya kutembelea Kapernaumu.

 

Kutoka Yohana 1:35 tunjua kwamba Andrea, ndugu yake Petro, alikuwa ni mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji na akaja kumfuata Kristo. Alimpeleka Petro kwa Kristo akimwambia kuwa amemuona Masihi (Yohana 1:41), aliyemuita jina la Petro (Kefa). Mathayo 4:18-22 na Marko 1:14-20 kwa hiyo zinafupisha urefu wa hadithi wa kuitwa kwa wanafunzi wa kwanza. Inaonekana kuwa imechukuliwa kutoka Injili ya Yohana ambapo waliitwa na kuatiza mapema kabla ya wakati, na kwamba huu ndiyo ujumbe uliotangulia kuzinduliwa kwa kazi yenyewe.

 

Yohana 2:22 inaonyesha kwamba baada ya arusi ya Kana ya Galilaya, Yesu na wanafunzi wake walikwnda huko Yudea, ambako alishinda huko kwa kipindi fulani na wao wakibatiza, ingwa yeye mwenyewe hakubatiza (Yohana 4:2). Yohana Mbatizaji alikuwa akibatiza pia huko Ainoni karibu na Salimu, na hi ilikuwa ni karibu na Pasaka ya mwaka 28 BK (Yohana 2:13).

 

Tafsiri ya Moffatt inaiweka sehemu hii kwenye mchakato wa kubadili ufuasi Yohana 3:22-30 katikati ya Yohana 2:12 na 13, kana kwamba Yohana alikuwa hajatiwa bado gerezani kwenye eneo hili; lakini kana kwamba Yesu ameishaanza tayari kutenda miujiza wakati wa Pasaka na anachukua hii ili kuonyesha kwamba Yohana alikuwa amekwisha fungwa gerezani. Kwa kweli, Kristo asingeweza kuanza kuhubiri mapema kabla ya Pasaka ya mwaka  28 BK au vinginevyo basi Injili zitakuwa zinapingana, na Neno la Mungu litakuwa limejikanganya.

 

Maandiko kutoka tafsiri ya “The Authorised” kwenye Injili ya Yohana, kama imechukuliwa kwa mlolongo wa matukio, inaashiria kwamba aliingia Hekaluni katika Pasaka ya mwaka 28 BK aktenda miujiza, na kisha akaenda nje ya nchi ya Yudea ambako wanafunzi wake walikuwa wakibatiza wakati ambapo Yohana Mbatizaji alikuwa akibatiza huko Ainoni. Maandiko ya tafsiri hii ya “The Authorised” kwa hiyo yanaonyesha kwamba kipindi halisi alichohubiri Kristo kilikuwa chini ya miaka miwili, kikifuatia baada ya Pasaka ya mwaka 28 BK.

 

Kristo alihubiri hadi Pasaka ya mwaka 30 BK, wakati alipokamatwa na kusulibiwa. Aliuawa majira ya alasiri, siku ya 14 Nisan/Abibu, ambayo ilikuwa ni siku ya Jumatano, tarehe 5 Aprili, 30 BK. Siku inayodhaniwa ya tarehe 25 Aprili mwaka 31 BK imechelewa sana kwa karne nyingi (soma jarida la Nyakati za Kusulibiwa na Kufufuka (Na. 159) [Timing of the Crucifixion and the Resurrection (No. 159)].

 

Hii ilitimiliza unabii wa Ishara ya Yona, kwa kuwa Yona hakuanza kuhubiri hadi alipoingia Ninawi kwa mwendo wa siku moja ya siku yake ya kwanza. Yona alihubiri Ninawi kwa mafanikio akitumia kpindi cha chini ya siku tatu kamili, na Ninawi ilipewa siku arobaini za kutubu na walitubu. Yuda walipewa kipindi cha chini (lakini sema) ya miaka mitatu cha huduma ya Yohana Mbatizaji (sawa na mwendo wa siku moja kuingia Ninawi) na miaka miwili mingine ya huduma ya Kristo kwa hesabu ya siku kwa mwaka (sawa na siku mbili). Kwa utaratibu huohuo, Yuda walipewa miaka 40 ya kutubu. Lakini hawakutubu na waliangamizwa tangu Siku ya Upatanisho ya mwaka wa 70 BK hadi siku ya 1 Abibu, 70 BK, kuhimisha maana ya ishara ya Yona kwa awamu yake ya pili (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)].

 

Madai ya kwamba huduma ya Kristo ilikuwa ni ya miaka mitatu na nusu yamechelewa nay a uwongo na kwa hakika sio ya kiroho. Yanapotosha ukweli wa ishara ya kweli na maana ya huduma ya Kristo na yanaondoa uelewa wa kweli. Madai haya yanatokana na tafsiri potofu ya Maandiko Matakatifu yanayohusiana na ujenzi wa Hekalu na juma la sabini la miaka. Kwa kweli, mafundisho haya mapotofu na yasiyojali ukweli yameyafanya maandiko ya Danieli 9:25 yajaribu kufuata tafsiri ya Authorised Version ili kukanganya maana halisi kuhusu kipindi hiki, kuanzia tarehe ya uwongo nay a bandia ya utawala wa Cyrus Macrocheir, aliyeitwa Artashasta au Artaxerxes I na Wayunani.

 

Ishara ya Yona ni alama pekee iliyopewa huduma ya Kristo. Sio tu kuwa alidumu kwa siku tatu usiku na mchana kaburini na kisha akafufuka, bali zaidi sana tu ni kwamba inaendana na kuzingirwa na mpangilio wote wa ujenzi wa Hekalu na wa juma la sabini la miaka. Inamaana ya zaidi yanayotokea kwenye maono ya nabii Ezekieli kwenye sura ya 1 na kuonekana kwa wale Makerubi wane. Kipindi cha Yubile kilipisha kipindi cha Mangojeo ya Masihi wa Haruni na Masihi wa Israeli, tukio ambalo ni mwendelezo wa Ishara ya Yona.

 

q