Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[025]
Alama ya Mnyama
(Toleo La 2.0 20010525-20060703)
Fundisho kuhusu Alama ya Mnyama limekuwa ni mojawapo ya nyama inayoendelea
na tarajio la sehemu ya ile wanaodaiwa kuwa ni imani ya Kikristo. Hata hivyo,
dhana na fundisho hili limekuwa likikosewa kuleweka kwakr kwa kiasi kikubwa sana
kulinganisha na unabii wote wa Biblia. Umakini katika usomaji wa Maandiko
Matakatifu na kuiruhuru Biblia ijitafsiri yenyewe kutampelekea mtu kuelewa kuwa
ni jambo tofauti sana na mafundisho makongwe na yakizamani ya makanisa ya zama
kale. Ingawaje kuelewa kuhusu huyu Mnyama ni nani na ishara ya alama yake ni
ipi ni muhimu sana na inasaidia katika kumpeleka mtu kwenye uelewa mzuri na
kamilifu wa nabii nyingine nyingi na mchakato mzima wote ulio kwenye Mpango wa
Mungu.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki ©
2001, 2006 Scott Rambo, ed. Wade Cox)
(Tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Alama ya Mnyama
Kwa kipindi chote cha takriban miaka 1900 au zaidi watu wamekuwa
wakitangatanga kutaka kujua kuhusu ni nini hasa maana ya alama ya Mnyama. Je,
ni nini hasa maana ya alama hii ambayo watu wanaiogopa sana kuipokea, alama hii
ambayo wakati wake watu hawataweza kuuza wala kununua? Je, ni kiolezo cha
compyuta ndicho kitakachochokewa kitaalamu kwenye nyuso za watu au mikononi?
Je, ni kitu kitakachokuja kwa mwonekano kama wa tatuu au chanjo? Je, ni nini
hasa alama hii ya Mnyama?
Onyo kuhusu alama hii ya Mnyama limetolewa na kuandikwa kwenye nabii nyingi
kadhaa za kitabu cha Ufunuo.
Ufunuo 13:16-17 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; 17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
Ufunuo 14:9-11 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, 10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. 11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.
Kwa hiyo, ni je, alama hii inamaana gani au inataja nini? Je, jana la
mnyama huyu ni lipi, na tarakumu hii y jina lake ni kitu gani basi? Ili kuelewa
maswali haya inatupasa kutafakari maana ya neno na dhana nzima ya hii alama na
ya mnyama kama zilivyoelezewa kwenye Biblia. Haitakuwa vizuri kubahatisha au kinadharia
kuhusu maana ya maneno haya. Mtume Petro alisema, “Mkijua neno hili kwanza, ya
kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu
fulani tu.” (2Petro 1:20). Hii ni pointi ya msingi ya kwa nini suala hili la
alama ya mnyama limeshindwa kueleweka kabisa na kupotoshwa. Badala ya kuyaacha
Maandiko Matakatifu yajitafsiri yenyewe, watu wanapenda kuitafsiri Biblia kwa
kufuata mujibu wa imani zao zinavyopenda na kuelekeza. Kwa sababu hii ndipo
ulimwengu umejionea manabii wengi wa uwongo wakitokea mmoja baada ya mwingine
wakitoa ama kufundisha nabii za uwongo kuhusiana na maana ya alama hii ya
mnyama. Namna pekee ya kuelewa kinachomaanishwa kwenye neno hili “alama ya
mnyama” ni kwa kuyasoma Maandiko Matakatifu kama nabii Isaya alivyosema hebu na
tuiruhusu Biblia ijitafsiri yenyewe.
Isaya 28:9-13 Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini? 10 Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo. 11 La, bali kwa midomo ya watu wageni, na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa; 12 ambao aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yeye aliyechoka; huku ndiko kuburudika; lakini hawakutaka kusikia. 13 Kwa sababu hiyo neno la Bwana kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo; ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, na kunaswa, na kuchukuliwa.
Kwa kuangalia kwa karibu na kwa kuweka kituo hadi kituo, mstari hadi
mstari, tunaweza kujipatia uelewa mzuri wa somo hili. Kwa kufanya hivyo, tutaona
kwamba matumizi ya biblia ya neno alama linatumika
tu pale inapokusudia kwa kumaanisha au kwa mtazamo wa kutiwa alama kwenye
vipaji vya nyuso au mkononi. Tutajionea pia kwamba matumizi ya biblia ya neno mnyama ni sawa na kama linavyotumika kwenye
unabii.
Tunahitaji kuona maana ya kimaandiko ya Maandiko Matakatifu mengine tofauti
tofauti ili kuelewa kikamilifu maana hii ya alama
ya mnyama. Mawazo haya yamefungamana na mifano ya vitu na mifano au
mionekano ya kiroho kwa pale inapotaka kuchambuliwa ili kuweza kuelewa
kikamilifu migawanyo ya nabii hizi. Haiwezekani kuelewa kinachoendelea na alama hii ya mnyama kwa kutumia tafsiri ya moja kwa moja ya kimwili ya
Biblia. Haya ni mawazo yanayohusiana na ambayo yamefunuliwa tu pale mtu anapochimba
kwa kupitia kina-ardhi cha moja kwa moja ya kimwili na kwenye kina ya kiroho.
Mji wa Yerusalemu Mpya una milango ya lulu (Ufunuo 21:21). Maana inayohukuliwa
na milango hii ya lulu ni kama ifuatavyo. Milango ya mji ni njia ya kuingilia
mjini. Lulu tunayoijua imetengenezwa kwa
kupitia magamba/ ya chaza ambayo imechukuliwa kutoka kwenye kipande cha changarawe
na hatimaye ilifanyika mchakato wa mahali pa tabaka la lulumizi karibu na jiwe
la changarawe hadi lulu hafifu na isiyo na dhamani iundike. Na ndivyo pia siri
za Mungu zinaeleweka kama habari ya ukweli uliodhahiri ambao umewekewa tabaka
na maana za kiroho makusudio yake. Ili kuelewa maana hizi za kiroho ni kuiona
milngo ya mji wa Mungu (pia jisomee jarida la Mji wa Mungu (Na. 180) [The City of God (No. 180)]. Na hii ndiyo sababu pia Kristo alisema
tusitupe lulu mbele za nguruwe, wasije wakazikanyaga kwa miguu yao na wakaturudi
na kuturarua.
Mathayo 7:6 Msiwape
mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije
wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Kristo alikuwa anasema kuwa tusiyafunuo mambo yaliyo kwenye fumbo za Mungu
kwa nguruwe waliopo, kama tutakavyoonyesha baadae, hawa ni wale Malaika walokengeuka
pamoja na wafuasi wao, wasijewakaitumia elimu ile tena na kuwapotosha wateul
wote. Na hii ndiyo sababu siri za Mungu zimefunuliwa kwa sehemu na kwa utaratibu
na zote ni kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kwa kweli malaika wenyewe wanatamani
kuziona siri hizi.
1Petro 1:12 Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao
wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa
yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu
aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.
Nyingi ya siri
hizi zimetiwa mhuri na kufungwa hadi ufike watati wenyewe muafaka uliokusudiwa
wa mwisho, ambao ndiyo huu tulionao sasa (soma jarida la Mchakato wa Ratiba ya Kipindi-Zama (Na. 272) [Outline
Timetable of the Age (No. 272)].
Alama
Neno la Kiyunani lililotumika kwenye Ufunuo ambalo kwenye lugh ya
Kiingereza limetumika kuadikwa “Mark”
yaani Alama, ni neno charagma {khar'-ag-mah} kutoka kwenye
Kamusi ya Kiyunani ijulikanayo kama Strong’s Greek Dictionary #5480 maana yake
ni:
1) stemp au mhuri, au alama iliyochapwa
1a) ya stempu au mhuri uliogongwa kwenye kipaji
cha uso au kwenye mkono wa kuume uliwa ni alama au ishara ya wafuasi wa
Mpingakristo
1b) mhuri au alama iliyochapwa kwa farasi
2) vitu vilivyochongwa, na kuwa sanamu, kazi ya
kuchongwa
2a) sanamu ya kuabudiwa
Neno la Kiebrania linalofanana na neno hili Alama kwenye Agano la Kale ni neno 'owth' {oth}, kwa mujibu
wa Kamusi ya Kiebrania ya Strong’s
Hebrew Dictionary #0226 ikimaanisha:
1) ishara, dalili au kiashirio
1a) ni mhuri au alama inayotofautisha
1b) bango au bendera
1c) ukumbusho
1d) ishara ya kimiujiza
1e) ishara
1f) onyo
2) kete, tepe, kiwango, miujiza, uthibitisho
Neno hili limetafsiriwa kama ishara kwenye fafanuzi au maana nyingi, lakini pia linamaanisha alama inayotofautisha. Kuna ishara au
alama iliyotolewa na Mungu kwa wale wanaozishika Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa
Chachu na Torati.
Kutoka 13:6-10 6 Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku
saba, nayo siku ya saba itakuwa ni sikukuu ya Bwana. 7 Mikate
isiyochachwa italiwa katika hizo siku saba; mkate uliotiwa chachu usionekane
kwako, wala chachu isionekane kwako, ndani ya mipaka yako yote. 8 Nawe utamwambia mwanao siku hiyo, ukisema, Ni kwa sababu
ya hayo Bwana aliyonifanyia hapo nilipotoka Misri. 9 Nayo
itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako,
ili kwamba sheria ya Bwana ipate kuwa kinywani mwako; kwani Bwana alikutoa
utoke Misri kwa mkono wenye uwezo. 10 Kwa hiyo
utaitunza amri hii kwa wakati wake mwaka baada ya mwaka.
Kumbukumbu la Torati
6:1-9 Na hii ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru Bwana, Mungu wenu,
mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki; 2 upate kumcha Bwana, Mungu wako, kushika amri zake zote,
na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za
maisha yako; tena siku zako ziongezwe. 3 Sikiza
basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka
sana, kama Bwana, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa
na asali. 4 Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu,
Bwana ndiye mmoja. 5 Nawe mpende Bwana,
Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo
wako; 7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na
kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na
uondokapo. 8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako,
nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. 9 Tena
yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.
Ni kama mnyama wa Ufunuo alivyo na alama
inayotiwa kwenye vipaji vya nyuso na mikononi mwa wale wanaomuabudu, na ndivyo
hivyohivyo pia Mungu anayo alama au mhuri inayotiwa kwenye vipaji ya nyuso na
mikono ya wale wanaomuabudu. Suala hili limetathminiwa kwa kina kwenye jarida
la Jukumu la Amri ya Nne Kwenye Historia ya
Makanisa ya Mungu Yanayozishika Sabato (Na. 170) [The Role of the Fourth
Commandment in the Historical Sabbath-keeping Churches of God (No. 170)]. Mhuri au alama hii inwekwa upande paji
la uso kwa kuwa hapo ndipo mawazo ya mtu yanatungwa. Mhuri au alama hii pia
inapigwa kwenye mkono kwa kuwa hapo ndipo mawazo ya moyo wa mtu hutekelezewa na
kutedewa kazi. Ni kwa kuzifuata hizi Amri za Mungu, kwa namna zote mbili, yaani
kwa moyo na kwa matendo, ndipo mtu anapokea alama hii ya Mungu. Ni kama
ilivyoandikwa kwenye Kutoka 13:6-10, amri hizi zinajumuisha pamoja ushikaji wa taratibu
zilizowekwa na Mungu za imani na ibada, kwa mfano, kuziadhimisha Sikukuu kama
vile Idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu na nyinginezo.
Ishara na alama hii ya Mungu siyo ya kimwili,
ya kawaida; ila ni ishara na alama za kiroho. Hakuna hata mmoja kati ya manabii
wala Yesu Kristo mwenewe aliyeyekuwa na alama ya kimwili kwenye vipaji vya nyuso
zao wala mikononi mwao zilizowaonyesha kuwa wao ni watu wa Mungu. Zaidi tu ni kwamba
walikuwa na alama za kiroho, ikiwa kama msaidizi wake wa kimwili katika
matumizi ya chapa ya ng’ombe, inayoonesha umiliki na raslimali unaohakikishwa kwa
alama, na utii na madai halali ya umiliki kwa yule aliye na alama au ishara yake.
Tunaona mahali pngine kwenye kitabu cha
Kutoka inaposema kwamba Sabato ni alama au ishara nyingine pia.
Kutoka 31:12-17 Bwana akasema na Musa, na kumwambia, 13 Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia,
Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika
vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye
ninyi. 14
Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu
atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika
siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake. 15 Kazi
itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa,
takatifu kwa Bwana; kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato,
hakika yake atauawa. 16 Kwa ajili ya hayo
wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi
vyao vyote, ni agano la milele. 17 Ni ishara kati ya
mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na
nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.
Sabato, ikiwa
kama ni moja ya siku zilizoamriwa na Mungu kuwa watu kuziadhimishe, ni ishara
pia kati Mungu na watu wake (soma jarida la Sabato (Na. 31) [The Sabbath (No. 31)]. Kumbuka pia kwamba hii ni ishara ya
milele. Haitakoma hata na kuja kwake Masihi. Haijabadilishwa kamwe kuwa siku ya
Jumapili na Mungu wala na Yesu Kristo. Jumapili wakati wote ilikuwa nab ado
inaendelea kuwa siku ya ibada ya wale waliomuasi Mwenyezi Mungu na walioziasi
Amri na Sheria zake. Ni bahati mbaya sana, kuwa wengi wa wale wanaojiita kuwa
Wakristo wa siku hizi, wanaichukulia Jumapili kuwa ni Siku ya Bwana. Yesu Kristo
mwenyewe alisema kuwa yeye ni Bwana wa Sabato, na sio Bwana wa Jumapili wala wa
siku nyingineyo yote (soma jarida la Siku ya Bwana na Siku za Mwisho (Na. 192) [The Day
of the Lord and the Last Days (No. 192)]
Mathayo 12:8 Kwa
maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
Na hata utunzaji
huu na kuabudu siku za Sabato umepuuzwa pia na wanaoiadhimisha ibada za Juma'a
au Ijumaa, badala yake, yaani umma wa
Waislamu ambao wanahatia kubwa kwa kuamua kwao kufanya hivyo. Mtume wao
aitwaye Muhammadi, kamwe hakukusudia waumini wake waihalifu Sabato na badala
yake wameifanya ile siku ya maandalio kuwa siku takatifu kwa kuzingatia haki
yao wenyewe (soma jarida la Ijuma’a Kwa Maandalio ya Sabato (Na. 285) [The Juma'ah: Preparing for the
Sabbath (No. 285)].
Sabato ni adhimisho
la siku ya saba ya juma la uumbaji, siku ambayo Mungu alistarehe na kupumzika katika
kazi zake zote. Ni siku
ambayo inaashiria pia tukio kuu la mapumziko ya kipindi cha miaka 1,000 ya
millennia. Sabato oilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, na sio mwanadamu sio
kinyume chake, yaani mwanadamu kwa ajili ya Sabato, na sio siku nyingine (Marko
2:27).
Alama na mhuri wa Mungu kwa hiyo imetolewa kwa wale wanaozishika amri za
Mungu na kwa wale wanaomuabudu yeye sawasawa na jinsi alivyoamuru na sio kwa jinsi
wanvyoona sawa kumuabudu yeye. Wale
waliotiwa mhuri wa Mungu wanamuabudu kwa kuzishika amri zake na kwa kuzishika
Sikukuu zilizoamriwa na sio kwa kuyaiga matendo ya mipagani na kuyaita matendo
hayo kuwa ni ya Kikristo. Tunajua kwamba Mungu hapendi watu wamuabudu kwa jinsi
namna hiyo, yaani kwa jinsi wanavyoona vyema wenyewe.
Kumbukumbu la Torati
12:29-32 Bwana, Mungu wako,
atakapoyakatilia mbali hayo mataifa mbele yako, huko uingiako kuyamiliki, nawe
ukawatwaa, na kuketi katika nchi yao; 30 ujiangalie,
usije ukanaswa ukawafuata, wakiisha kuangamizwa mbele yako; wala usije ukauliza
habari za miungu yao, ukisema, Mataifa haya waitumikiaje miungu yao? Nami
nifanye vivyo. 31 Usimtende kama haya Bwana, Mungu wako;
kwani kila yaliyo machukizo kwa Bwana, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu
yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya
moto. 32 Neno niwaagizalo lo lote liangalieni
kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze.
Tunapaswa
kufanya na kuadhimisha kile Mungu anachotuagiza. Hii haiwezi kufanyika kwa
kudai tu kwamba maagano yote mawili, yaani Agano la Kale na Jipya yamegeuzwa
kwa kiasi kwamba hatujui kile ambacho maandiko asilia yanavyosema, kama
unavyofanya Uislamu. Gombo la Chuo lililogunduliwa kwenye Bahari ya Chumvi
linathibitisha kuwa tuna maandiko yaliyoandikwa kwenye wakati wenyewe muafaka
sasa kama yalivyokuwapo hata kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammadi. Kuran (Kora)
haiwezi kueleweka pasipo kuitumia sambamba Biblia. Ni kwakuielewa Torati tu na
ushuhuda wa manabii wa nyakati zote mbili, Agano la Kale na Jipya, ndipo Kurani
inaweza kueleweka vizuri. Na hii ndiyo maana Mtume mwenyewe aliagiza usomaji wa
Maandiko Matakatifu.
Maana iliyoko kwenye Kumbukumbu la Torati 12 inapaswa iwe ya wazi sana vya
kutosha kwa watu wote kuona. Inafanyika kwa Wakristo (Israeli wa kiroho), kiasi
chochote kidogo knachofanyika kwenye taifa la kimwili la Israeli. Kama Waislamu
wa kweli, kwa kile kilichofundishwa na mtume na Makhalifa Wanne waliokuwa mkono
wake wa Kuume na Viongozi, mwanzo wake ulikuwa ni tawi la Ukristo, na hii
inatendeka sawasawa na wale wanaodai kuwa wana imani ya Kiislamu. Mungu habadiliki.
Ni yeye yule, jana, leo na hata milele. Matendo mengine ya kipagani ambayo
alichukizwa nayo hata kabla ya kuja kwa Masihi, pia alikuwa amechukizwa baada
ya kufa kwake Msihi. Wakiwa kama Israeli wa kimwili hawakupaswa kunaswa na mitego
wa matendo haya ya kipagani, na ndivyo tunavyopaswa kuwa sisi kama Israeli wa
kiroho, yaani, kama Kanisa tusiingie mtegoni kukumbatia imani na matendo haya
ya kipagani.
Kwa kuzibadilisha amri na Sikukuu zalizoamriwa na Mungu, imani zote hizi
mbili, yaani Ukristo mkongwe wa kale na Uislamu wamejikana wenyewe mhuri
halisia wa Mungu. Hakuna mahali kwenye Biblia inaposema kwamba Mungu amemtia
alama kwa yeyote anayemuabudu kwa namna wanazoabudu mataifa ya kipagani. Kwa
makosa/default na bahati mbaya sana, wale wanaoitwa Wakristo na Waislamu wamejinyima
wenyewe mhuri huu wa Mungu. Hawazishiki Sabato, wala Idi za Mikate Isiyotiwa
Chachu, au sheria za Mungu, zote ambazo Maandiko Matakatifu yanasema ni ishara
ya mhuri wa Mungu. Badala yake, tuna Ukristo wa zama kale unaodai kwamba sheria
na amri za Mungu zimegongolomewa mtini wengine huita msalabani wakati zilikuwa
ni chierographon —yaani nakala
ya uhuru ambazo kwazo tunawiwa na Mungu kwa dhambi zetu – zizilopigiliwa
mtini. Kwa bahati mbaya, wanadai kuwa sheria zinapaswa kushikwa na kisha
wanaendelea kusema kwamba siku ya kwanza ya juma ndiyo Sabato ya sasa ikichukua
mahali a Sabato ya kweli ya siku ya saba ya juma. Wanakataa kusikiliza kwa
uwazi na maneno yenyewe ya Masihi pale aliposema kuwa hakuja kuitangua torati.
Mathayo 5:17-19 Msidhani
ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali
kutimiliza. 18 Kwa maana,
amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja
ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. 19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri
moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa
katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo
ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
Anisa Katoliki la Roma linadai kwamba lina mamlaka
ya kuzibadilisha Sheria. Hata hivyo, Masihi anasema kuwa wale wanaofanya hivyo,
na kuwafundisha wengine kufana hivyo, watakuwa duni kwene Ufalme wa Mungu.
Katika siku za mwisho dunia haitaruhusiwa kupata madhara hadi idadi kamili
ya watumishi wake Mungu watiwe mhuri wake.
Ufunuo 7:2-3 Nikaona
malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye
hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi
na bahari, 3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari,
wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya
vipaji vya nyuso zao.
Watumishi hawa wa Munguj katika siku za mwisho wanatiwa mhuri kwenye vipaji
vya yuso zao kwa kuwa wanasheria za
Mungu mioyoni mwao, na, kwa kipindi kirefu wamekuwa wanazishika amri hizi kwa
matendo. Hawa ndio wale waliotabiriwa na nabii Yeremia.
Yeremia 31:33 Bali
agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema
Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami
nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Kutaniko la Mungu
katika siku za mwisho ni wale waliorudia agano. Hawa ni wale ambao Mungu
ameziweka sheria zake ndani yao. Hii ndiyo kusudi ya mfano wa Sanduku la Agano.
Sanduku liie, ambalo Mungu alimpa Musa na kazi ya watu ilikuwa ni kuwaelekezea
wateule. Ni kama alivyosema Mtume Paulo kuwa wateule ni Hekalu la Mungu.
2Wakorintho
6:16 Tena pana mapatano gani
kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai;
kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea,
nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Sanduku hili
lilisimamishwa ndani ya hekalu. Sanduku hili lilikuwa ni ishara mioyo ya
wateule (soma jarida la Sanduku la Agano (Na. 196) [The Ark of the Covenant (No. 196)]. Ni ndani ya mioyo ya wateule ndimo Mungu
aweka Sheria zake, ni sawa tu kama zile mbao zilizoandikwa Toarti zilivyotiwa
ndani ya sanduku la agano. Torati ya Mungu inaanzia na zile amri kuu mbili za
Mungu. Amri hizi kuu mbili zilisisitizwa na Kristo.
Marko 12:28-31 Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? 29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; 30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. 31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
Yesu alisema kuwa sheria zote na yote yale yaliyosemwa na manabii yanatuama
kwenye amri hizi mbili kuu. Utaratibu wote wa ibada umefungamanishwa na amri
hizi kuu mbili. Zimevunjwavunjwa kwenye vipande na kuwa Amri Kumi, ambazo
zimeandikwa kwenye vibao ambazo ziingizwa kwenye Sanduku la Agano. Kila moja ya
Amri hizi Kumi zilikuwa zimeelekezwa zaidi na Musa na manabii. Kumuabudu Mungu
kwa kuzisika Sabato, Sikukuu zalizoamriwa na Siku Takatifu, kumeungamanishwa moja
kwa moja na Amri Kuu ya Kwanza. Kwa hiyo, ni kama Yesu alivyosema, ili kuupata
uzima wa milele, ni lazima mtu azishike amri.
Mathayo19:17 Akamwambia
Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia
katika uzima, zishike amri.
Wale waliotiwa mhuri
na Malaika wa Mungu na kuwa na mhuri wa Mungu ndio wale watakaokuwa wanazishika
Sabato, Miandamo wa Mwe zi Mpya, na Sikukuu alizoziamuru Mungu, pamoja na amri
nyingine zote zilizobakia (sokma jarida la Torati ya Mungu (Na. L1) [The Law of God (No. L1)].
Kinyume chake, alama ya mnyama ni alama ya wale ambao hawamuabudu Mungu
kama alivyoamuru, bali wanamuabudu mungu wa uwongo sawasawa na imani na mifumo
ya uwongo ya ibada. Lakini ni huyu mnyama ndiye watu wengi karibu ulimwenguni
kote humuabudu? Ili kuuelewa mfumo wa mnyama katika siku za mwisho yatupasa
turudi nyuma kwenye kitabu cha Mwanzo.
Wanyama wa Kondeni
Tunajua sote historia ya Adamu na Hawa kwenye Bustani ya Edeni (soma jarida
la Fundisho la Chanzo cha Dhambi Sehemu ya 1 Bustani ya Edeni
(Na. 246) [The Doctrine of Original Sin Part I The
Garden of Eden (No. 246)].
Kuna mambo mengi sana yanayoendelea kuhusu habari hii zaidi ya zile zilizodhahiri
zijulikanazo. Mtu asipochimba kwa kina kiroho ya habari hii, kijuujuu inaonekana
kuwa ni kama hadithi au simulizi tu inayosimuliwa ili mashiko kidogo nje ya
mwanadamu halisi na kinachotufanya tutofautiane na viumbe wengine duniani. Kwenye
Mwanzo 3:1 nyoka aaliyemdanganya Hawa anatajwa kuwa “mwerevu kuliko kuliko hayawani
wengine wote, aqliyewaumba Bwana Mungu”.
Mwanzo 3:1 Basi
nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.
Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti
yote ya bustani?
Huyu sio nyoka halisi wa kimwili anayenena hapa, lakini ni kiumbe ambaye
alikuwa ni Kerubi aliyemuasi Mungu. Neno la kiebrania litumikalo kumtaja nyoka
ni nachash {naw-khawsh'}, limechukuliwa
kwenye neno ambalo shina lake ni nachash
{naw-khash'} ambalo maana yake ni mwenye nuru
na limeitwa serpent kwa Kiingereza,
yaani nyoka kwa Kiswahili.
Huyu mwenye
kutoa nuru ni Kerubi Mwenye Mabawa Yafunikayo; Malaika wa Nuru au Mleta Nuru au
Lusifeli aliyeandikwa kwenye Isaya 14 na kwenye Ezekieli 28:13-17.
Ni kwa namna hiyohiyo
imetumiwa kwa nyoka wenye sumu kali walioandikwa kwenye Hesabu 21:6,9. Wametakwa
kama nachashim maserafi. Nyoka wakali
waliitwa hivyo kwa sababu ya muwako wa hisia kutoka kwenye majeruhi waliyoumwa,
lakini inawezekana kuwa huenda pia walielekezwa na malaika wakati Waisraeli
walipowanenea Musa na Mungu maneno mabaya wakiwanung’unikia kwa kuwaleta kangwani.
Neno sarafi maana yake ni kuwaka. Serafi aliyeandikwa kwenye Isaya
6:2 waliitwa mwenye kuwaka. Kwa hiyo,
malaika hawa walikuwa wakali au mwenye haiba ya ukali na wa shaba ing’aayo.
Nyoka wa zamani (2Wakorintho 11:3) anajigeuza kama
malaika wa nuru (2Wakorintho 11:14). Kwa hiyo nyoka anatumika kama mfano wa
Shetani aliyeongea na mwanamke na kumdanganya yeye Hawa.
Nyuka huhu au
kerubi mwenye mbawa zifunikazo alisemekana kuwa alikuwa mwerevu (maana yake
nyingine ni mlaghai au mjanja) kuliko hayawani wote wa kondeni.
Kuna kitu kuhusu usemi huu kinachoonekana cha tofauti kidogo. Tunajua kwamba
nyoka ni kiwakilisho cha Shetani, Kerubi mpakwa mafuta na mwenye mabawa
yafunikayo. Tunaambiwa kwenye Ezekieli kuhusu hekima yake.
Ezekieli 28:12-15 Mwanadamu,
umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe
wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri. 13
Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa
kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu,
na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya
matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako
zilitengenezwa tayari. 14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye
kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa
Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. 15 Ulikuwa
mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana
ndani yako.
Huyu mfalme wa Tiro aliyetajwa hapa ni jina lingine la fumbo la Shetani. Ilikuwa
ni yeye aliyekuwa pale Bustanini Edeni, ambaye alikuwa mkamilifu tangu siku ya
kuumbwa kwake hadi uovu ulipoonekana ndani yake. Kerubi huyu mwenye mbawa zifunikazo
alizingirwa na idadi ya wengi, na hekima nyingi. Kutokana na hili kulionekana
maneno yasiyo na maana na yakipumbavu kulinganisha hekima yake na ile ya
hayawani wa kondeni, kama usemi huu wa wamyama
wa kondeni inapaswa ichukuliwe moja kwa moja kuwa ni wanyama. Ufafanuzi wa
hapa ni kwamba wanyama hawa wengine wa kondeni wanahusiana na viumbe wengine wa
kiroho walioasi pamoja na Shetani. Tutaona baadae jinsi wanama hawa wa kondeni
wanavyohusiana na wanyama wa kwenye viabu vya Ufunuo na Danieli. Aina hii ya
mifano inaonekana pia inapotajwa miti ya bustanini (soma jarida la Lusifa: Mpeleka Nuru na Nyota ya Asubuhi (Na. 223)
[Lucifer: Light Bearer and Morning Star (No. 223)]. Kutoka kwenye Ezekieli 31 tunaona kwamba
Farao na Waashuru wanafananishwa na miti.
Ezekieli 31:2-18 Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri, na jamii ya watu wake, Je!
Umefanana na nani katika ukuu wako? 3 Tazama, Mwashuri
alikuwa mwerezi katika Lebanoni, wenye matawi mazuri, na kifuniko chenye uvuli,
na kimo kirefu; na kilele chake kilikuwa kati ya matawi mapana. 4 Maji yalimlisha, vilindi vilimsitawisha; mito yake ilipita
pande zote za miche yake; naye akapeleka mifereji yake kwa miti yote ya
kondeni. 5 Basi kimo chake kilitukuzwa kuliko miti
yote ya kondeni, na vitanzu vyake viliongezeka; matawi yake yakawa marefu, kwa
sababu ya maji mengi, alipoyachipuza. 6 Ndege wote wa
angani walifanya vioto vyao katika vitanzu vyake, na chini ya matawi yake
wanyama wote wa kondeni walizaa watoto wao, na chini ya uvuli wake mataifa
makuu yote walikaa. 7 Basi hivyo alikuwa mzuri katika
ukuu wake, katika urefu wa matawi yake; maana mizizi yake ilikuwa karibu na
maji mengi. 8 Mierezi ya bustani ya Mungu haikuweza
kumficha; misunobari haikuwa kama vitanzu vyake, na miamori haikuwa kama matawi
yake, wala bustanini mwa Mungu hamkuwa na mti wo wote uliofanana naye kwa
uzuri. 9 Nalimfanya kuwa mzuri kwa wingi wa matawi
yake; hata miti yote ya Adeni, iliyokuwa ndani ya bustani ya Mungu, ilimwonea
wivu. 10 Basi Bwana MUNGU asema hivi; kwa kuwa
umetukuzwa kimo chako, naye ameweka kilele chake kati ya mawingu, na moyo wake
umeinuka kwa urefu wake; 11 mimi nitamtia katika
mikono yake aliye mkuu kati ya mataifa; naye atamtenda mambo; nimemfukuza kwa
sababu ya uovu wake. 12 Na wageni, watu wa mataifa
watishao, wamemkatilia mbali na kumwacha; juu ya milima na katika mabonde yote
matawi yake yameanguka, na vitanzu vyake vimevunjika karibu na mifereji yote ya
nchi; na watu wote wa dunia wameshuka, wakitoka katika uvuli wake na kumwacha. 13 Juu ya magofu yake ndege wote wa angani watakaa, na
wanyama wote wa jangwani watakuwa juu ya matawi yake; 14 kusudi
mti wo wote, ulio karibu na maji, usijitukuze kwa sababu ya kimo chake, wala
usitie kilele chake kati ya mawingu, wala mashujaa wake wasisimame katika kimo
chao kirefu, naam, wote wanywao maji; maana wote wametolewa wafe, waende pande
za chini za nchi, kati ya wanadamu, pamoja nao washukao shimoni. 15 Bwana MUNGU asema hivi, Katika siku ile alipotelemka
mpaka kuzimu naliamuru matanga, nalikifunika kilindi kwa ajili yake, nikiizuia
mito yake, nayo maji makuu yalizuiwa; naliamuru Lebanoni kumwombolezea, na miti
yote ya kondeni ilizimia kwa ajili yake. 16 Niliwatetemesha
mataifa kwa mshindo wa kuanguka kwake, hapo nilipomtupa chini mpaka kuzimu,
pamoja nao washukao shimoni; na miti yote ya Adeni, miti iliyo miteule na iliyo
mizuri ya Lebanoni, yote inywayo maji, ilifarijika pande za chini za nchi. 17 Hao nao walitelemka kuzimuni pamoja naye kwa watu
waliouawa kwa upanga; naam, wale waliokuwa mkono wake, waliokaa chini ya uvuli
wake kati ya mataifa. 18 Umefanana na nani, hivi
katika utukufu na ukuu, kati ya miti ya Adeni? Lakini utashushwa pamoja na miti
ya Adeni, hata pande za chini za nchi; utalala kati ya hao wasiotahiriwa;
pamoja na hao waliouawa kwa upanga. Huyu ndiye Farao, na jamii yote ya watu
wake, asema Bwana MUNGU.
Miti hii na wanyama wa kondeni ina maana ya kiroho, iliyoelezewa kwa kina
kwenye jarida la Kuanguka Kwa Misri (Na. 36) [The Fall of
Egypt (No. 36)]. Aina hii ya mifano inaonekana kwa kupitia Biblia
na inafunuliwa kwa watumishi wa Mungu katika siku hizi za mwisho (Danieli
12:9-10). Mawazo haya sio rahisi kuelewa na hayajafunuliwa hadi mtu apite
kipengele kimoja hadi kingine, mstari hadi mstari. Mtu anaweza pia kuona
muunganiko hapa kati wanyama wa kondeni na Malaika waovu wsalioanguka kwa
matendo ya Masihi.
Mathayo 8:28-32 Naye
alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana
naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. 29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe,
Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? 30
Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha. 31 Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende,
tukaingie katika lile kundi la nguruwe. 32 Akawaambia,
Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka
kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini.
Marko 5:1-13 Wakafika
ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. 2 Na
alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini,
mwenye pepo mchafu; 3 makao yake yalikuwa pale makaburini;
wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; 4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na
minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna
mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Na sikuzote,
usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na
kujikata-kata kwa mawe. 6 Na alipomwona Yesu kwa
mbali, alipiga mbio, akamsujudia; 7 akapiga kelele kwa
sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha
kwa Mungu usinitese. 8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo
mchafu, mtoke mtu huyu. 9 Akamwuliza, Jina lako nani?
Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. 10 Akamsihi
sana asiwapeleke nje ya nchi ile. 11 Na hapo milimani
palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. 12 Pepo
wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. 13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia
katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia
baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.
Mara nyingi Yesu Kristo ametajwa kama pepo aliyetupwa nje ya watu. Je, ni
wapi alipelekwa wapi? Waliamriwa wakawaingie nguruwe, wanyama wa kondeni, ambao
hatimaye waliingia na kutumbukia majini na wakafa. Maji yale ambayo ni wanyama
asilia walikoenda kufananishwa na maji ya roho, ambao watachukuliana na
kuwaangamiza Malaika walioasi, sawa na kama maji ya Bahari ya Shamu yalivyowlifunika
na kuliangamiza jeshi la Wamisri. Yesu Kristo kwa kweli alikuwa anatoa unabii
ya kile ambacho hatimaye kingetokea na kuwapata Malaika hawa walioasi. Kwa
kuwakomesha mapepo (wanyama wa kondeni wa kiroho) kwa kuwaamuru waingie kwa
nguruwe (wanyama asilia wa kondeni) Masihi alikuwa anaonyesha kuwa maangamizo
yangewafuatia Shetani na mapepo zake. Kwa hiyo, ni uweza wa Masihi alioruzukiwa
na Mungu, kuwakomesha Malaika hawa waasi kwa kuwaamuru waende na kuwaingia
wanyama na kuwaua majini, sawa na kama mtu wa kale anapokufa kwenye maji ya
ubatizo na kupewa upya wa uzima. Malaika waasi watapewa pia fursa ya ubatizo kubatizwa
na kuufikia uzima mpya. Waasi wataangamizwa na kukomeshwa kabisa na wale
wanaohusika watashushwa chini hadi shimoni, na watakuwa ni viumbe wanaoonekana,
na kwa kuyubu kwao na kubatizwa kwenye maji ya Roho Mtakatifu watarudishwa
kwenye upya wa uzima kupitia kwa Masihi kwa nguvu za Roho Mtakatifu.hii ndiyo
kile kinachojulikana hapa kuwa ni kukemea mapepo. Dhana hi inaonekana pia kwenye
kitabu cha Waamuzi wakati Samsoni alipochukua asali kutoka kwenye mzoga wa simba
ambaye alimuua hapo kwanza.
Waamuzi 14:5-11 5 Ndipo Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia
Timna, wakafika mashamba ya mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba
akamngurumia. 6 Roho ya Bwana ikamjilia kwa nguvu,
naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu cho chote
mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya. 7 Basi akatelemka na kuzungumza na huyo mwanamke; naye
akampendeza Samsoni sana. 8 Kisha baadaye akarudi ili
kumtwaa, naye akageuka kando kuuangalia mzoga wa huyo simba; na tazama, nyuki
wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na asali. 9 Akatwaa
asali mikononi mwake akaenda mbele, huku akila alipokuwa akienenda,
akawafikilia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa
ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba. 10 Basi
babaye akamtelemkia huyo mwanamke; Samsoni naye akafanya karamu huko; kwa kuwa
vijana ndivyo walivyokuwa wakifanya. 11 Basi ikawa
hapo walipomwona, wakamletea wenziwe thelathini, wawe pamoja naye.
Marafiki au washirika thelathini ni mfano wa baraza
la ndani la Malaika. Kitendo cha kurina asali kutoka kwenye mzoga wa simba
kunamaanisha hali ya kusafisha na kukila kitu ambacho ni najisi na kisichoweza kujisafisha
chenyewe.
Hapa tuna mifano miwili na yote inamuashiria Masihi
akishughulika na kitu safi (soma marida la Samsoni na Waamuzi (Na. 73) [Samson and the Judges (No. 73)].
Na turudi nyuma kwenye dhana ya kuhusu mnyama. Neno mnyam lililotumika kwenye Mwanzo 3:1 ni la Kiebrania ambal ni chay {khah'-ee} kwa mujibu wa kamusi ya
Strong’s Hebrew Dictionary #2416. Neno hili linatumika kama ifuatavyo kwenye
tafsiri ya King James Version: ishi 197, ihai 144, mnyama
76, kuwa hai 31, kiumbe 15, kukimbia 7, kitu chene uhai
6, tepetepe 6, misc
19.
Kwa hiyo, inamaana, zaidi ya kile tunachokitaja kuwa ni mnyama. Nyoka (au nachash)
alilaaniwa zaidi kuliko hayawani wote wa kondeni. Hayawani wa kondeni
walilaaniwa pia, lakini nyoka ilibidi alaaniwe zaidi kuliko hayawani wengine
wote waliokuwepo.
Mwanzo 3:14 14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo,
umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni;
kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
Nano kulaaniwa ni la Kiebrania la
'arar {aw-rar'} kwa mujibu wa kamusi ya Strong’s Hebrew Dictionary #0776
lenye maana ya:
1) Kulaani
1a) (Qal)
1a1) kulaani
1a2) na alaaniwe (kijineno kinachotumika kama laana)
1b) (Niphal) kulaaniwa, laaniwa
1c) (Piel) kulaani, kuwa chini ya laana, kutamka laana kwa ajili ya kitu au mtu
1d) (Hophal) kulaanika, kulaaniwa
Inatum ka kwa
namna ya kama Mungu kuwalaani wale ambao wanamrudia na kufuata njia zake.
Zaburi 119:21 Umewakemea
wenye kiburi, Wamelaaniwa waendao mbali na maagizo yako.
Yeremia 11:3 ukawaambie,
Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Na alaaniwe mtu asiyeyasikia maneno ya
maagano haya,
Malaki 2:2 Kama hamtaki kusikia, na kama hamtaki
kuitia moyoni, ili kulitukuza jina langu, asema Bwana wa majeshi, basi
nitawapelekeeni laana, nami nitazilaani baraka zenu; naam, nimekwisha
kuzilaani, kwa sababu hamyatii haya moyoni.
Hebu na turudi kwenye andiko la Mwanzo 1:26, tunaona kwamba mwanadamu
aliumbwa kwa mfano wa Mungu (ambaye ni Elohim), na alipata mamlaka ya kutawala
kila kitambaacho.
Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu
kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa
angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu
ya nchi.
Hakukuwa na watu wawili kwenye aya hii. Kwanza kabisa, ilikuwa ni kwa namna
ya kimwili ukweli kuhusu uumbwaji wa mwanadamu na kwamba alikuwa na uwezo wa
kutiisha na kuwatawala hayawani wote walioko duniani. Maana haya yanatambulika
sana. Pili, aya hii ilikuwa ni unabii pia wenye maana ya kiroho na utendaji, ambao
ni kwamba mtu huyu hatimaye atakuwa na mamlaka wa kuwatawala Malaika walioasi –
wanyama wa kiroho wa kondeni. Wakati idadi kamili ya wateule wanakombolewa
kutoka duniani na wakifanyika kuwa wafalme na makuhani kwenye ufalme wa Mungu,
ndipo hatimaye watatawala hapa duniani pamoja na Kristo.
Ufunuo 20:4-6 Kisha
nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona
roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno
la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea
ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai,
wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. 5 Hao wafu
waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. 6 Huo
ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika
ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani
wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
Ni katika kipindi hiki ambapo unabii wa 1Wakorintho utatimilika pia, na
Malaika walioasi watahukumiwa na watakatifu (soma jarida la Hukumu ya Mapepo (Na. 20) [The Judgment of the
Demons (No. 80)].
1Wakorintho 6:2-3 Au hamjui ya kwamba watakatifu
watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili
kukata hukumu zilizo ndogo? 3 Hamjui
ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
Ili kuwa waangalizi au walinzi wa sayari yetu hii na Yesu Kristo na
kuanzisha sheria za haki za Mungu, mwenendo wa wateule utatumiwa kama kigezo
cha kuwahukumu Malaika walioasi. Hatimaye watakapokuwa wanahukumiwa na kukutwa
wakitaka, watashughulikiwa na Mungu. Hii itafanyika kwenye Ufufuo wa Pilo wa
wafu. Inawezekana kabisa kuwa hii ingechukua mkondo wake mapema sana iwapo kama
Adamu na Hawa wasingeasi na kumfuata Shetani. Hata hivyo, tunajua kwamba uasi
wao ulijulikana tangu mwanzoni na Mungu na kwamba yeye alishakuwa na mpango
tayari ambao hatimaye ungefanikisha kuhitimisha mapenzi yake, pamoja na yale
yaliyotajwa kwenye Mwanzo 1:26.
Wakati wa Ufufuo
wa Pili wa wafu, Malaika hawa waasi watashushwa chini hadi kuzimu shimoni (Ezekieli
31). Watalazimika kwa shuruti kuwa na miili ya kibinadamu kwa namna sawa tu na
kama Masihi alivyojigeuza, na kuuacha mwili wa kimbinguni na kuwepo kwake kule,
na kuchukua umbo na hali ya utumwa na mtumishi na kuwa mwanadamu (Wafilipi
2:6-8). Ukweli ni kwamba, Yesu Kristo aliamua kufanya hivyo kwa hiyari yake kwa
kumtii Mungu, wakati kwamba Malaika walioasi watashurutishwa kubadilika kwa
nguvu za Mungu. Ni katika kipindi hiki ambapo ndipo watajionea mshahara wa
dhambi zao za uasi. Katika kipindi hiki watapewa fursa ya kutubu na kusamehewa
kwa rehema kubwa na kwa upendo wa Mungu (soma jarida la Kondoo Aliyepotea na Mwana Mpotevu (Na. 199) [Lost
Sheep and the Prodigal Son (No. 199)].
Mapenzi haya kwa hakika yanapaswa kufundishwa tena jinsi ya kyafuata na
kufundisha sheria za Mungu, sawasawa na zilivyofundishwa na kukaziwa umuhimu
wake na \Yesu Kristo na wateule wake. Kwa hiyo jambo la pili kuhusu unabii ulio
kwenye Mwanzo 1:26 litatimilika miaka elfu saba tangu kipindi cha Adamu. Ndipo
maangamizo ya Malaika walioasi yalikuwa yanawekewa mfano ama ashirio na matenzo
au kazi za Masihi aliokuwa anayafukuza mapepo na kuyaamuru yawaingie nguruwe,
na kwa Samsoni alipokula asali iliyotoka kwenye mzoga wa simba. Pia tunajionea
tena matukio ya kimwili kama yalivyoandikwa kwenye Biblia yakitupa njia ya
utimilifu wake wa kiroho.
Mnyama
Neno hili la
mnyama limeandikwa tena kwenye kitabu cha nabii Danieli sura ya 7. Hapa tunaona
kuna wanyama wanne ambao wote wanatokea baharini.
Danieli 7:2-7 Danielii
akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo
pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. 3
Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.
4 Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa
ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika
nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa
kibinadamu. 5 Na tazama, mnyama mwingine, wa pili,
kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo
kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama
tele. 6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine,
kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege;
mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka. 7 Baadaye
nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye
nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana;
alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na
umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
Wanyama hawa wanne
tena hawatajwi kwa maana ya viumbe wa kimwili, bali ni viumbe wanaotajwa kwa
mfano tu hapa. Tunaambiwa kwenye Danieli 7:17 kwamba wanyama hawa ni wafalme
wanne ambao wataiuka na kuwepo duniani. Wanyama wanne hawa habari zo zinafanana
na sehemu nne za madini tofauti tofauti za sanamu aliyoiona ndotoni mfalme
Nebukadneza kwenye Danieli sura ya 2.
Danieli 2:31-45 Wewe,
Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa
sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa
lenye kutisha. 32 Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa
ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na
viuno vyake ni vya shaba; 33 miguu yake ni ya chuma;
na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo. 34 Nawe
ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga
sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande. 35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile
fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya
viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane
mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa,
likaijaza dunia yote. 36 Hii ndiyo ile ndoto, nasi
tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme. 37 Wewe, Ee
mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na
nguvu, na utukufu; 38 na kila mahali wakaapo wanadamu,
wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye
amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.39 Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo
kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote. 40 Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa
maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi
vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta. 41 Na
kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa
mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani
yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika
na udongo wa matope. 42 Na kama vidole vya zile nyayo
vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una
nguvu, na nusu yake umevunjika. 43 Na kama vile
ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya
nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma
kisivyoshikamana na udongo. 44 Na katika siku za
wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele,
wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande
vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. 45 Na
kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya
kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na
ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa
baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.
Maeneo haya ya
sanamu hii, yanajumuisha madini mbalimbali yanayopungua thamani yake kadiri
yanavyoshuka kutoka kichwani kwenda chini hadi kwenye vidole, yakimaanisha falme
nne ambazo zimetawala hapa duniani, kuanzia kwa yeye mwenyewe Nebkadreza wa
Babeli aliwa ndiye kile kichwa na kushuka hadi chini kwenye ufalme wa vidole
kumi, ambao utaangamizwa mwishoni mwa zama hizi. Ufalme huu wa mwisho
utaangushwa na kuangamizwa kwa jiwe lishukalo toka mbinguni ambalo halikuchongwa
kwa mikono ya mwanadamu. Jiwe hili si mwingine ila ni Masihi. Yeye ndiye jiwe
kuu la pembeni la Hekalu.
Matendo 4:10-12 jueni
ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa
Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina
hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. 11 Yeye
ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu
la pembeni. 12 Wala hakuna wokovu katika mwingine
awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu
litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Kwa hiyo tuna
mnyama wa Ufunuo mwenye vichwa saba na pmbe kumi, na tuna ufalme wa mwisho wa
sanamu ya Danieli sura ya pili yenye vidole kumi. Hivi ni vitu viwili
vinavyowakilisha wazo moja. Kwa hiyo ni kwamba katika siku za mwisho kabla ya
kurudi kwake Masihi na kuja kutawala hapa duniani, kutakuwa na ufalme unaotajwa
kama mnyama, na ambao utakuwa na mungano ama utajumuisha wafalme kumi ambao
watayatoa mamlaka yao kwa huyu mnyama mmoja ili kumpa nguvu na uweza, na
watafanyan hivyo kwa saa moja au wakati mmoja (Ufunuo 17:13). Watawala hawa
kumi wanafanana au wanamaana moja na wana kumi wa Hamani walioangikwa kwenye
mti uliochongwa ambao habari zao zipo kwenye Kitabu cha Esta (soma jarida la Ufafanuzi wa Kitabu cha Esta (Na. 63) [Commentary on Esther (No. 63)]. Waliangikwa wote kwa pamoja kwa kuwa kwa
pamoja wanafanya muungano huu wa vidole kumi vya Danieli sura ya 2, na pembe
kumi za Ufunuo 13 za katika siku za mwisho.
Ufunuo 13:1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe
kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa
vyake majina ya makufuru.
Watafanya vita na Mwanakondoo, lakini Mwanakondoo atawashinde.
Ufunuo 17:14: Hawa
watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni
Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa,
na wateule, na waaminifu.
Wanyama hawa kwa hiyo wanaonekana kuwa kama falme za dunia hii, ambazo
zilikuja kuwa na nguvu juu ya watu wote wa duniani hapa. Sehemu muhimu au jambo
la msingi linaloonekana kuendena nayo inapatikana kwenye Kumbukumbu la Torati
32:8.
Kumbukumbu la Torati
32:8-9 Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao, Alipowabagua
wanadamu, Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli. 9 Maana, sehemu ya Bwana ni watu wake, Yakobo ni kura ya
urithi wake.
Hapa tunaambiwa
kwamba wakati wana wa Adamu walipotawanyika na kupewa urithi wao (hapa ni
kwenye mnara wa Babeli) mipaka yao iliwekwa sawasawa na idadi ya wana wa Mungu.
Hii inaonekana kwenye
tafsiri za RSV, the Septuagint na the Dead Sea Scrolls. Hii ilijulikana vizuri sana
kwamba kulikuwa na mataifa sabini pale, na kila moja likiwa chini ya himaya ya
kiumbe fulani wa kiroho, mwangalizi, mmoja wa wana wa Mungu. Mojawapo ya mataifa haya lilikuwa ni la
Israeli ambalo lilichaguliwa na Yahova. Tunajua kuwa kiumbe huyu ni Mwana wa
Mungu aliyefanyika kuwa mwanadamu na aliyekufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu,
ni yeye ambaye kwa lugha ya Kiingereza anaitwa Jesus Christ, yaani Yesu Kristo (soma jarida la Malaika ya YHVH (Na. 24) [The Angel of YHVH (No. 24)].
Viumbe wa kiroho walio na mamlaka juu ya mataifa walikuwa ni hayawani wa wa
kondeni waliotajwa kwenye kitabu cha Mwanzo. Kwa mujibu wa nabii Danieli
kulikuwako wanyama wanne waliotabiriwa watainuka na kufanya dola au falme
kubwa. Wa mwisho kati ya wanyama hawa wanne atakuwa na atakuwa na vichwa saba
na pembe kumi. Vichwa hivi saba vinasemekana kuwa ni milima saba ambayo yule
mwanamke (kahaba aliyeandikwa kwenye Ufunuo aliyelewa kwa damu ya watakatifu)
anaketi, lakini hawa ni wafalme saba pia. Hii milima saba ni zote mbili zipo
kwenye muonekano wa kimwili wa milima ya duniani, lakini pia kwa lugha ya
kimafumbo ni kama falme saba au urejesho wa ufalme huohuo kulingana na urefu wa
vipindi vya nyakati. Pembe kumi zinawakilisha ia wafalme kumi, ambao watampa
nguvu zao na mamlaka yao yote huyu mnyama.
Kitu cha muhimu
kukumbuka hapa ni sanamu ya Danieli 2. Pale tunaona sanamu moja yenye madini ya
namna mbalimbali. Ilikuwa ni moja kumbwa na iliyounganika kikamilifu kwa kila
upande ukiwa umeungana na sehemu iliyotangulia kama kuirithi nyuma yake. Kwa
hiyo, hizi falme nne hazikuwa ni falme zimetengana kabisa, zikiwa hazina la
kusaidiana wala kutegemeana kila mmoja na mwenzake, bali zilikuwa
zimeunganishwa zote na kuwa sehemu moja ya mfumo mzima wote. Mfumo huu mmoja
ulianzia kwa Wababeloniani, na ukaendelea hadi kwa Wamedi na Waajemi, hadi kwa
Wayunani wa Makedonia, na hatimaye utaishia kwa mnyama wa mwisho, ambaye ni
Dolan a mfumo wa Kirumi (soma jarida la Dini za Siri Sura ya 1 Kuenea Kwa Imani za Siri za Wababeloniani (Na.B7 1) [Mysticism Chapter 1 Spreading the
Babylonian Mysteries (No. B7_1)].wakati wa Dola hizi, mfumo wa uwongo na potofu wa
ibada ulianufaika. Ni kama ilivyoandikwa ma kusemwa kwenye Danieli 7:25, mnyama
huyu ataazimu kubadili majira ya sheria. Hivi ndivyo ilivyotokea chini ya mfumo
wa mnyama wa Kirumi na mwanamke kahaba uliombeba akiuendesha.
Marira au nyakati zilizozibadilishwa ni zile zinazoihusu kalenda. Kalenda
inayotumika na iliyomaarufu leo ulimwenguni kote imechukuliwa kama ni kitu cha
kawaida tu na kama ni sahihi, lakini ni ishara ya kuibuka au kubuniwa kwa mfumo
huu wa Kirumi. Ikaondoa na kuyabadili maelekezo ya Biblia ya siku kuanza jioni
wakati wa kuzama jua, bali hii ikawaelekeza watu kuwa siku inaanza usiku wa
manane. Ibadadilisha maelekezo ya Biblia ya kwamba mwaka mpya uanze tangia
Mwandamo wa Mwezi Mpya ulinaofuatiwa na ikwinoks ya majira ya baridi ili kwamba
Pasaka iadhimishwe katika kipindi hiki, lakini mwaka wa hawa unaanzia katikati
ya majira ya baridi ya maeneo yaliyo kwenye ncha za kaskazini. Kalenda hii ikabadilisha
utaratibu wa Kibiblia wa mianzo ya miezi ijulikane kwa kigezo cha Kuandama kwa
Mwezi Mpya kama neno la Mungu linavyosema, lakini miezi ya hawa ikawa inaanza
siku yoyote tu pasipo kuzingatia utaratibu huo wa Maandiko Makatatifu, na
badala yake miezi yao ikaanzia tu kwa kutegemea na uholela wa idadi ya siku
iliyowekwa kwenye mwezi wa kalenda ya Kirumi.
Mnyama huhu anasemekana kuwa na mke ambaye ni kahaba aliyempanda juu yake
akimuendesha. Neno kahaba limetumika
kwenye Agano la Kale kwa kuwataja wateule wa Mungu, yaani Israeli. Ndipo, kama
vile Israeli wa kimwili walivyofanya ukahaba na Wamisri na Wababeloni, na
ndivyo ilivyo pia kwa Israeli wa Kiroho wanavyofanya ukahaba. Huyu mwanamke
kahaba mwenyewe ana jina lililoandikwa kwenye paja la uso wake linalosomeka: BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA
NA MACHUKIZO YA NCHI. (Ufunuo
17:1-5). Ni rahisi sana kuona sababu ya hili kuwa ndilo la kahaba huyu.
Amechapwa mhuri wa Wababelonia kwenye paji la uso wake. Mafundisho yake yanatokana
na imani za kale za kifumbo za dini za kale za Wababeloni. Imani na mafundisho
mapotofu na ya uwongo Nebukadreza wa Babeli yalitiririka yakishuka kutoka
kwenye kichwa cha dhahabu yakashuka chini yakipitia kwenye madini mengine yote
yaliyooneshwa kuwa ni dola zilizofuatia kwenye Danieli sura ya 2.
Wakati
alipoyaingiza na kuyachanganya mafundisho haya ya imani fumbo za Kibabeioni kwenye
dini yake mpya inayojiita kuwa ni Ukristo, ndipo kahaba huyu mkuu aliazimu
kuibadili Sabato kutoka siku ya saba ya juma iliyoamriwa iadhimishwe kwenye
maandiko, akaweka ibada nyingine zilizoadhimishwa siku ya kwanza ya juma. Jambo
hili liliwafanya hata wale wanaodai kuwa wanamuabudu Mungu wa Pekee na wa Kweli
wapoteze kigezo cha kuwafanya wastahili kutiwa mhuri wa Mungu. Kahaba huyu
anayeendesha akiwa amempanda mnyama hakuishia hapa. Alidiriki pia kuzibadilisha
sheria ambazo pia ni torati ya Mungu. Aliziunganisha pamoja amri ya Pili ya
Mungu na ile ya Kwanza, akazifanya kuwa ni moja, na kisha akaigawanya ile ya
Kumi na kuifanya ziwe mbili, ili kuzifanya zionekane zimetimia zote kumi. Alifanya
haya yote ili kumruhusu kutamani sanamu wa wapagani na avinyago vya dhahabu na
fedha ambazo alijipamba kwazo yeye mwenyewe, sawa na kama Mtume Yohana
alivyoonyesha kahaba huyu kwenye maono ya Ufunuo 17:4. Alimkufuru Mungu kwa
kuyapotosha mataifa yote aliyoyashinda kwenye vita. Aliyaingiza maovu na
mapotovu yote kwenye kile alichokiita Ukristo na akaendelea kuwadanganya wale
wote ambao walikuwa hawajaitwa wala kuchaguliwa na Mungu. Kwa kuwalaghai kwake
kuwapa thamani ya Ukristo au jina hilo na huku akiwapotosha kwa kuwafanya
waendelee na taratibu na imani za mataifa walizozitumia kuabudu na kuitumikia
miungu yao, aliupotosha kabisa ulimwengu wa Kikristo. Ikawa watu hawa
wanaojiita kuwa Wakristo hawaziadhimishi tena Sikukuu zilizoamriwa na Mungu na
kuzichukulia kuwa ni siku takatifu, na badala yake wakaziadhimisha sikukuu na
siku za miungu wa kipagani (soma majarida ya Malumbano ya Wakwuartodeciman (Na. 277) na Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235) [The Quartodeciman Disputes (No.
277) and The Origins of Christmas and Easter (No. 235)]. Matokeo mabaya ya hili yalikuwa ni kutoujua
tena mpango wa Mungu wa wokovu kwa wanadamu, ambao unajulikana tu kwa kuzijua
na kuziadhimisha Sikukuu zake alizotuamuru kutitunza.
Shetia za Mungu
za ulaji wa vyakula zilipaswa kushikwa na ualaji wa vyakula najisi ulibidi
uepukwe (soma jarida la Sheria za Vyakula (Na. 15) [The Food Laws (No. 15)]. Huenda ulaji wa vyakula safi na najisi
zina mashiko ya kiroho ambayo yanauhusiano na kuonyesha utii wetu kwa Mungu nwa
kwenye Amri na Sheria zake. Ni kama Hawa alivyomfuata Shetani kwa kumsikiliza
na kumuasi Mungu na akala tunda kutoka kwenye mti uliokatazwa, na vivyo hivyo
ndivyo ilivyo kwa walio kwenye ibada na imani hii wanamfuata Shetani katika
kumuasi Mungu na kula vyakula najisi. Vyakula najisi vinamaana sawa tu na ibada
najisi. Tunajionea tena mlingano wa wanyama wa kondeni sambamba na vyakula najisi. Ni kama walivyo wanyama
wavkundeni waliopo walivyo safi kuwala na baadhi yao sio safi. Wale walio safi
kama Masihi alivyosafi kwa chakula cha kroho. Yeye ni mkate wa kiroho wa uzima.
Na hii ndiyo sababu sheria za vyakula ziliwekwa kama kama zilivyokuwa. Na kwa
mara nyingine tena, zikaonyeshwa dhahiri kwa kiroho.
Mambo haya yote
yakuchukiza aliyafanya kahaba huyu kwa nguvu na utukufu, asijue kwama matendo ya
kipagani na aina ya ibada ambazo aliziingiza kutoka kwenye imani za mataifa ya
kipagani na kuzifanya kuwa kama zake mwenyewe, yalikuwa yanafanyika kwa ushawishi
wa miungu hii ya kipagani, Malaika walioasi, amao walikuwa na mamlaka hay ohayo
juu ya mataif haya ya kipagani. Badala ya kushika ukamilifu na utakatifu na
kuifuata njia nyembamba na iliyopindapinda na kuzishika amri za Mungu, pasipo
kuchepuka na kwenda upande wa kuume wala wa kushoto, akajichukulia njia yake
mwenyewe.Alifanya ukahaba na wafalme wa dunia, na mamlaka za kiroho za mahali
pa juu. Na kama hiyo haikufosha aliwaua na kuwaondolea mbali watakatifu wa
kweli wake yeye Mungu, aliye juu kama ilivyotabiriwa kwenye Danieli 7:25. Alipewa
mamlaka kwa wakati ,Snakati mbili na nusu wakati. Hii hi miaka 1260 ya kudumu
kwake iliyojulikana hapo zamani kama Dola Takatifu ya Kirumi iliyoanzia mwaka 590
BK hadi mwaka 1850 BK. Wakati wa kipindi hiki alilewa kwa damu za watakatifu na
mashahidi wa Yesu Kristo (Ufunuo 17:7) (sawa
na majarida ya Migawanyo Mikuu ya Makanisa ya Mungu Yanayozishika
Sabato (Na. 122) na Vita vya Waunitarian na Watrinitarian
(Na. 268) [General Distribution of the Sabbath-keeping Churches (No. 122) and The Unitarian/Trinitarian Wars (No. 268)]. Isitoshe, aliwafanya wote wakaao duniani
walew au aliwalewesha kwa mvinyo wa uasherati wake (Ufunuo 17:2). Mvinyo huu ni
mafundisho yake, misingi ya imani yake, na mfumo wake wa ibada na kuabudu,
ambazo zote zilichukuliwa kutoka kwenye mitindo ya ibada za miungu ya kipagani.
Hatimaye, kahaba huyu alichanganikiwa kwa kuona kuwa wengi wa aliowalevya
mvinto wa uasherati wake hawakuendelea kumfuata. Walitafuta njia za kujiondoa
kutoka kwake na kujitenga naye. Kwa hiyo, haya makanisa yote ya Kiprotestant ni
mabinti wa huyu kahaba aliyetajwa kwenye Ufunuo 17:5. Badala ya kuachana nao
mafundisho yake mapotofu ya kizushi na kurudi kwenye njia iliyopindapinda na
nyembamba (imani ya kweli iliyofundishwa na Yesu Kristo) hatimaye wakajiunga na
kuendelea kuendeshwa na yeye na wakijifanya kuwa wamejitanga na kuachana na
matendo yake, na huku wakiendelea kuyashika karibu mafundisho yake yote na
wakiwa na kiu cha kunywa damu ya watakatifu kama afanyavyo yeye. Walianza
kumuabudu Mungu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu (Mathayo
15:9).
Kwa hiyo, mnyama wa mwisho wa Danieli na Ufunuo kwa kipidi cha miaka 1260 likuwa
akiendeshwa akiwa amepandwa juu na huyu kahaba. Alibadili sheria na nyakati au
majira kiasi cha kwamba dunia yote ilidanganyika. Mfumo wa mwisho utakuwa ni
tofauti sana kutoka kwenye mfumo wa ufalme wa Mungu na kwamba utakuwa wa
tofauti na vigumu saba kwa watu wa Mungu kutoka nje ya yeye na kumuacha kama
walivyoamriwa kufanya hivyo (Ufunuo 18:4). Ili kutoka nje na kuachana naye
inambidi mtu kufuata mfumo ambao umepingwa sana hapa duniani na mfumo au imani
ya mnyama. Inampasa mtu kuzishika siku za maadhimisho ya Sikukuu zilizoamriwa
na Mungu, na siyo sikukuu za kipagani zilizowekwa kwa heshima ya miungu wa
kipagani. Kwa hiyo, ni uamuzi wa mtu, aidha kutiwa mhuri wa Mungu kwa kuzishika
na kuziadhimisha amri zake na Siku zake Takatifu, au kupigwa chapa ya mnyama
kwa kuzifuata amri zake na sikukuu za kipagani. Mwishoni kulikuwa na kipindi
cha mateso wakati wa Mhuri wa Tano wa Ufunuo. Hii ilikuwa ni Mauji Makubwa ya
Kuangamiza Wayahudi na waamini Sabato huko Ulaya yaliyopewa jina la Holocaust yaliyofanyika katika karne ya 20 na
yataendelea hata kwenye karne hii ya 21 na hatmaye tutashuhudia kuuawa au kuangamizwa
kwa yule mwanamke kahaba ambaye ataangamizwa na yule mnyama mwenyewe (soma
jarida la Ujumbe wa Ufunuo 14 (Na. 270) [The
Messages of Revelation 14 (No. 270)].
Kipindi hiki itakuwa vigumu kumudu kununua au kuuza bila kuwa na alama ya
mnyama. Na kwa watu wengi, ni vigumu sana kutofanya kazi au kufunga biashara
siku za Sabato, Miandamo ya Mwezi, katika Siku Takatifu za Mungu, na kubakia na
ajira yenye manufaa makubwa. Hata hivyo, wakati umewadia na unakuja upesi ambao
ni kama inavyosema Ufunuo 13:17, kwamba hakuna mtu atakayeweza kununua au kuuza
asipokuwa na alama hii ya mnyama. Ambavyo kwamba, mtu asipokuwa tayari
kufanyakazi siku za Sabato, Miandamo ya Mwezi na Siku Takatifu zilizoamriwa na
Mungu, mtu hataweza kubakia na ajira yake au na shughuli ama biashara yake. Kwa
mambo haya yote muhimu yanayoendana na maisha ya kisasa, kama vile kodi ya
serikali, pango ya nyumba, huduma za bima, nk, itakuwa ni vigumu kubakia bado umetiwa
mhuri wa Mungu na huku ukiendana sambamba kufanikisha mambo yako kwenye mfumo
huu utakaowekwa na huyu mnyama.
Je, alama hii ya mnyama itakuwa ni kitu kinachoonekana wazi kama vile kimelea
cha compyuta itakayoingzwa miilini mwa watu. Huenda inweza kuja kwa njia hiyo, lakini
hii itakuwa ni alama inayoonekana wazi tu. Alama yenyewe hasa ni ya kiroho
ambayo watu wanagongwa na kuwanayo hata sasa na wanakuwanayo asipo hata wenyewe
kujijua! Kwa hiyo, wakati watu wengi wanapoogopa na kujiwekea tahadhari wakidhania
kuwa huenda kutakuwa na siku moja watalazimika kupokea alama hii ya mnyaka kwa
namna iliyo wazi na kama kitu kinayoonekana wazi wakitiwa kwenye vipaji vya
nyuso zao au mikononi mwao, watakuwa wameikwisha tiwa alama hii kiroho kwenye
vipaji vya nyuso zao na mikononi mwao. Hivi ndivyo Ufunuo 12:9 inavyosema: “Yule joka
akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani,
audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa
pamoja naye.” Joka huyu mkubwa
kwa kweli anaudanganya ulimwengu wote, hata na wale wanaojiwekea tahadhari
kubwa kutopenda kuipokea alama hii ya mnyama.
Tarakimu ya Mnyama
Chanzo kingine kilichopelekea kutolewa kwa nabii za uwongo kwa miaka mingi kinahusu
tarakimu ya mnyama. Tunaambiwa kwene Ufunuo 13:18 kwamba Yeye aliye na akili, na
aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake
ni mia sita, sitini na sita (666). Inaeleweka vyema na,imeandikwa vizuri kwamba tarakimu hii ya 666 inahusiana na imani za
kidini na mifumo ya Kibabeli. Alama ya mungu Isis ni
SSS ambayo ina tarakimu inayofanana na hii ya 666’ alama hii imekuwa ikitumiwa
kama ishara au alama ya dini za waabudu jua tangu zama za Wababeloni hadi sasa.
Makuhani wa zamani wa Kibabeloni waliigawana mbingu kwa vilimia/thelathini na
sita. Inajulikana kwamba hesabu ya tarakimu ya kwanza ya thelathini na sita ni
666. Makuhani wa kipagani walikuwa na namna ya kuiwakilisha au kuitumia migawanyo
ya tarakimu thelathini na sita kwa kuzipangilia kila moja ya fungu la idadi ya
thelathini kwenye meza yenye mistari sita kwa mafundu sita, ambazo walizitunda
kwenye tasbihi au kamba maalumu ambazo walizivaa shingoni mwao. Kila mstari na
kila fungu pamoja na kila mzingo ziliongezwa haki kufikia 111. Idadi ya mistari
yote na mafungu yote kwa hiyo ilikuwa ni 666. Kwa hiyo, tunaona kwamba makuhani
hawa wa zamani wa kipagani sio tu kuwa walikuwa wanaijua tarakimu hii bali pia
waliitumia kama sehemu ya elimu yao wa mambo ya nyota na kama chombo cha
kufanyia ubashiri na ulozi. Elimu ya nyota na anga pamoja na ubashiri au ulozi
ni sehemu ya imani na mifumo ya Wababeloni.
Ufunuo 13:8 inasema kwamba tarakimu hii ya 666 sio
tu kuwa ni ya mnyama, bali hii pia ni hesabu au tarakimu ya kibinadamu. Maelezo
ya jinsi ya kuliewa jambo hili yametolewa na nabii Isaya.
Isaya 14:4-17 utatunga
mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na kusema, Jinsi alivyokoma mwenye kuonea;
Jinsi ulivyokoma mji ule wenye jeuri! 5 Bwana
amelivunja gongo la wabaya, Fimbo ya enzi yao wenye kutawala. 6 Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu, Kwa mapigo
yasiyokoma; Aliyewatawala mataifa kwa hasira, Ameadhibiwa asizuie mtu. 7 Dunia yote inastarehe na kutulia; Hata huanzilisha kuimba.
8 Naam, misunobari inakufurahia, Na mierezi ya
Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti
aliyetujia. 9 Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili
yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio
wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao
vya enzi. 10 Hao wote watajibu na kukuambia, Je! Wewe
nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi! 11
Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza
wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. 12 Jinsi
ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi
ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe
ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu
kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za
mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya
mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. 15 Lakini
utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo. 16 Wao
wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye
aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme; 17 Aliyeufanya
ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?
Aya
elekezi ili kuelewa jambo hili ni ile ya kumi na sita inayosema: " Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme". Kwa kweli, Shetani atatazamwa kama ni mtu
aliyeifanya dunia itetemeke. Yeye alikuwa ni Kerubi kwenye mabawa yafunikayo
anayeonekana kwenye dini za kipagani kwa umbo la mtu mwenye vichwa vinne (soma
jarida la Serikali ya Mungu (Na. 174) [The Government of God (No. 174)]. Kushushwa huku kwa Shetani kutafanyika
mwishoni mwa kipindi cha Milenia kwenye Ufufuo wa Pili wa wafu (aya ya 9).
Ilikuwa ni Shetani aliyekuwa kiongozi au Malaika
Mkuu anayeonekana akionyeshwa kwa umbo la mtu asiye na kichwa au aliyeondolewa
kichwa chake kwenye dini hizi potofu aliyeanguka kutoka kwenye neema na kutoka
mbinguni. Yeye ndiye yule mtu ambaye
tarakimu yake ni 666. Tarakimu hii imekuwa ikitumika na kuwekwa au kujumuishwa kwenye
falme zote za ulimwenguni ikiwa imeanzia huko Babeli.
Wakati kukiwa hakuna shaka kuwa tarakimu hii 666
kuwa inahusika na harakati za dini za siri za kishetani, kuna tarakimu nyingine
iliyoandikwa kwenye moja ya maandiko yaliyopendwa sana ya maandiko ya zamani ambayo
ilitumika kama mbadala wa hii namba 666. Kama alivyosema Del Washburn kwenye
kitabu chake Theomatics II ukurasa wa 500, “kwenye kitabu
kilichochapishwa mjini London mwaka 1932, na kupewa kichwa cha jina Kitabu Cha Ufunuo, Chanzo cha Chimbuko la
Ukristo [The Book of Revelation, A Key to Christian Origins], maelezo haya
ya chini kwa kitabu ya ufafanuzi yanayoonesha kuendelea kwa maasi yanaonekana
yakisema hivi.
Tarakimu ya 616 imetolewa
kwenye moja ya maandiko mawili mazuri sana. C (Codex Ephraemi Rescriptus, Paris), na toleo la
Kilatini la Tyconius (DCXVI. ed. Souter kwenye Jarida la Theo., SE la Aprili, 1913), na kwenye toleo la
zamani la Kimarekani la (ed. Conybeare, 1907). Irenaeus alilijua hili [ masomo
ya mwaka 616], lakini hakuchukuliana nayo wala kuiiga (Haer. v, 30,3); Jerome aliiiga
na kuichukua (De Monogramm, ed. Dom G. Morin ya Rev. Benedictine, 1903) huenda
ni ya kihalisia. Tarakimu hii ya 666 imewekwa mbadala wa tarakimu ya 616 na huenda
kwa kuilinganisha na tarakimu nyingine ya 888, namba ya Yesu (Deissmann), au
kwakuwa ina umbo la mzingo, tarakimu ya 36 za kwanza (1+2+3+4+5+6...+36=666).”
Huenda kunawezakuwa na umuhimu hapa kuangalia kichwa cha maneno cha
Kitheomatikia. Theomatikia imefafanuliwa na Washburn kuwa ni tarakimu au hesabu
za Mungu. Ni sawasawa tu na Gematria, lakini haishabihiani na hii. Theomatics ni
elimu ya jinsi wazo linavyoendana au kushabihiana kwenye Biblia, iwe kwenye
Kiebrania au Kiyunani, linapotokea kwenye uandishi kwa namna ambayo thamani ya
herufi ya maneno yaliyo kwenye dhana maalumu yanaongezeka hadi kwenye nambari fulani
au kwa kuizidiaha namba ile. Kwa mfano, kuna idadi kadhaa ya majina ya Shetani
kwenye lugha zote mbili, Kiebrania na Kiyunani ambayo yote yanahitimika kwenye
tarakimu ya 276. Muonekano huu halingani kila mara, bali unashikamana na tarakimu
iliyoko ndani ya kiwango cha nyongeza au kupunguza au kutoa mbili. Kwene kitabu
hiki, Washburn aliweza kuonysha kwa ushawishi mkubwa sana (na kwa mujibu wa
kanuni zilizoanzishwa za kisayansi za kusawazjsha) kwamba miunganiko hii ya neno
na kifungu hulinganishwa hapo kwa mtindo au mwonekano, na isingeweza kufanywa
kwa kutokea tu bahati njema.
Sasa basi, kama tukiichukua tarakimu ya 616 kuwa ni namba ya mnyama, basi tutaona
uwepo wa vifungu vingi na maneno kutoka kwenye maagano yote mawili, yaani la
Kale na Jipya ambavyo vitakuwa na thamani ya kitheomatiki iliyosawa na namba
616 au namba 616 nyingi. Hapa kuna baadhi ya vifungu vinavyoonyesha thamani ya
kitheomatiki ya namba 616:
Mwanzo 1:25 aliumba hayawani wa duniani baada ya aina zake; Mwanzo 1:26 aliumba
kila kiumbe kitambacho juu ya nchi; Mwanzo 1:28 akatawale kila kiumbe kilicho
hai na kitambaacho; Mwanzo 2:19 kutoka katika nchi kila hayawani; Mwanzo 3:1 wanyama
wa kondeni ambao; 2Wakorintho 11:3 inasema isijekuwa kwa namna fulani kama
nyoka alivyodanganya; 2Wakorintho 11:3 akashawishika au kudanganyika; 1Timotheo
2:14 kudanganyika; Ufunuo 17:1 kabaha mkuu aketiye juu yake; 1Wakorintho 6:16 kahaba;
Ufunuo 17:5 Babeli ya siri na machukizo ya nchi; Mathayo 10:15 kila Sodoma na Gomora; Ufunuo 18:4 kushiritiki
dhambi zake; Ufunuo 17:17 kila moja ya
zifuatazo mnyama, kahaba, uovu (udhaifu au uchafuko); Mwanzo 3:14 ulimlaani
mnyama; Ezekieli 28:14 kerubi mpakwa mafuta; Mambo ya Walawi 11:41 kila kiumbe
atambaaye; Marko 1:23 unajisi; Warumi 1:23 wanyama na watambaao; Mathayo 6:32 giza;
Yohana 3:6 wenye mwili; Danieli 7:17 wanyama wakubwa; Luka 16:8 kwa wana wa
kizazi hiki; Waesfeso 5:6 kwa wana watiio; Mathayo 13:38 magugu ni wana.
Kuna linaloshangaza kwa namna yoyote ile kusikia kwama mpakwa mafuta huhu
ambaye pia ni Kerubi mwenye mabaya yafunikayo, joka, anashirikiana na mnyama,
pamoja na giza, na kahaba, na uwongo, na Babeli ya Siri, pamoja na Sodoma na
Gomora na nyingine, na wengine, na wengine? Kutoka kwenye mirejesho yote hii
tunaweza kuona dalili za kiroho. Tunajua kuwa Shetani ni mfalme wa nguvu za
anga. Tunajua pia kwamba ameudanganya ulimwengu wote. Tunajua pia kwamba
matukio yaliyotokea kwenye Agano la Kale ni mafundisho kwetu na tuyapambanue au
tuyachuje. Ni kwa kuyajua mambo haya tu mdipo tunaweza kuona jinsi ulimwengu
mzima wote ulivyodangwanywa. Matukio halisi ambayo sio ya kiroho ya Agano la
Kale yalifanyika ili kuwapa jinsi ya kutimilika kwake kiroho kwenye Agano
Jipya. Mfano mmojawapo kuhusu hili ni Pasaka. Damu halisia iliyokuwa inamwagika
ya Mwanakondoo wa Pasaka ambayo iliwalinda Israeli kutoka kwa Malaika wa kifo
ilikuwa ni mfano tu uliokuwa unaashiria damu ya Masihi ambayo itawaokoa wateule
kutokana na mauti ya pili. Tunajonea hayo pia tunapofananisha matukio ya kimwili
ya kitabu cha Mwanzo na utilifu wake kwenye Ufunuo. Nyoka aliyemdanganya Hawa
kwenye Mwanzo ni mnyama yuleyule anayemdanganya huyu mwanamke kahaba na
ulimwengu wote kama tunavyoona kwenye kitabu cha Ufunuo. Ni kama alivyodanganyika
Hawa hadi akala tunda la mti uliokatazwa kwa ulaghai wake na hekima yake potofu
na kwa ujanja wake, na ndivyo anavyomdanganya huyu kahaba kwa kupitia mbinu
hizihizi kama zilivyoelezewa na na falme za mnyama. Ni kwa dini za kimafumbo na
kisirisiri za Wababeloni, kama zilivyoingizwa na kushirikishwa kwenye falme zote
za ulimwenguni za huyu mnyama, na ndivyo pia Kanisa lilivyorubuniwa ili limfuate
nyoka. Ni kama mwanamke Hawa alivyoumbwa kutokana na Adamu, mwanadamu wa kwanza,
na akadanganywa na nyoka, na ndivyo ilivyo kwa mwanamke huyu ambaye ni Kanisa
alivyochukuliwa na taifa ambalo lilikuwa ni mzaliwa wa kwanza wa Mungu, taifa
la Israeli, na likadanganywa ya nyoka huyuhuyu. Ni kama vile Hawa alivyokula tunda
kutoka kwenye mti uliokatazwa kinyume na mapenzi ya Mungu waliyoelekezwa, na
ndivyo alivyofanya pia huyu kahaba, anakula chakula cha kiroho kilichokatazwa ambacho
ni vyakula na wanyama waliokatazwa, na na kushiriki matendo yaliyokatazwa na
kuiabudu miungu ya uwongo, vitendo ambavyo vinapingana moja kwa moja na mapenzi
ya Mungu. Ni kama Hawa alivyomsababishia Adamu kutenda dhambi, na ndivyo alivyofanya
kahaba huyu, anamsababishia mwanadamu kutenda dhambi kwa kuzifuata njia za kahaba
huyu. Na ni kama masalio walivyoondolewa nje ya uzao wa Hawa na kutengwa mbali
wakiwa kama wateule wake Mungu, na ndivyo ilivyo kwamba kuna masalio waliotolewa
watoke nje mfumo wa imani na dini ya huyu mnyama ambao unaongozwa na huyu
kahaba, na wametengwa na kuwekwa mbali wakiwa kama ni watu wateule wake Mungu.
Huyu joka amejaribu kwa jitihada kubwa kuwadanganya
na kuwapotosha wanadamu tangu mwanzo na kuwaondoleambali wale alioshindwa
kuwadanganya. Amejaribu kwa namna zake zote alizoweza kuwaangamiza wanadamu na
kuwaweka mbali kutoka kwenye makusudi na lengo alilowawekea Mungu wao. Kwa ni
jambo kubwa somo hilo kuliendeleza kwenye jarida hili, lakini na tutoe mifano
michache ya majaribio yaliyofanywa ya mapenzi na nia za Shetani inayotosha kuonyesha
jinsi alivyojaribu kubadilisha unabii wa kuangamia kwake uliotolewa kwenye
Mwanzo 1:26, na Mwanzo 3:6.
Kumdanganya Hawa lilikuwa ni jaribio lake la kwanza.
Na huenda hakuonambali asijue kwamba Mungu tayari alishaandaa mpango wa kuwakomboa
wanadamu kutoka kwenye mshahara wa dhambi zao, au huenda alidhania kuwa angefanikiwa
kuutokomeza mpango huo. Jaribio la pili ni lile la Abeli (ambaye sadaka yake
ilikuwaliwa na Mungu) aliyeuawa na ndugu yake Kaini ambaye sadaka yake
haikukubaliwa. Hadithi hii pekeyake inamlinganisho kati ya wana wawili wa Mungu,
Yesu Kristo (au Yahova Elohim) na Shetani.
Kwa kuwa ilikuwa ni sadaka ya Yesu Kristo kama Mwanakondoo wa Mungu ambayo
ndiyo inakubalika na Mungu. Shetani hakuandaliwa kuyatoa maisha yake kwa kutoa
sadaka. Kwa hiyo, ni kama vile Kaini alivyomuua ndugu yake Abeli, ndivyo
Shetani alivyomuua Kristo. Katika kipindi cha Nuhu wengi waliotokana na uzao wa
kinasaba ya wanadamu walijiingiza na kujichanganya na Wana wa Mungu wakichanganya
damu na binti za wana wa wanadamu (Mwanzo 6:4) kwa kiasi kwamba ni Nuhu peke
yake ndiye alikuwa ndiye mkamilifu kwenye kizazi hiki chote, na hii inamaanisha
katika mchanganyo wa kinasaba. Na hii ndiyo sababu iliyompelekea Mungu kuingamiza
dunia yote kwa gharika ya mvua ili kwamba Nuhu tu na familia yake waendelee
kuijaza Dunia wakiwa na mbegu isiyochanganyika. Katika kipindi cha Kanisa,
baada ya kujaribu baada ya kujaribu tena na tena kwa kipindi cha takriban miaka
4,000 kuwaangamiza wateule wake Mungu, ndipo sasa anawafuatia masalia ya yule
mwanamke wa Ufunuo 12:6. Anamtumia mwanamke kahaba wa imani kongwe ya Kikristo
ili kuwafuatilia kwa mfululizo na kuwakomesha pasipo huruma au kwa ukatili
mkubwa mawasali wale wachache waliobakia ambao ni Ekklesia au Kanisa la kweli, ambao wangali bado wakizishika amri za
Mungu na Ushuhuda wa Kristo.
Kwa hiyo, hebu na turudi nyuma hadi kwenye wazo
letu la tarakimu ya 666 ambayo Shetani mwenyewe aleigonga kwenye falme zake
mwenyewe, na namba 616, ambayo kama ikichukuliwa kitheomatiki inaonekana kumuonyesha
moja kwa moja Shetani na udanganyifu wake kwa wanadamu. Huenda tarakimu zote
mbili zinauhusiano na mnyama, moja ni ile ambayo Shetani mwenyewe anapenda
itumike na nyingine ni inayotuama kwenye tarakimu za kitheomatiki za Maandiko
Matakatifu na ambayo inamlenga moja kwa moja Shetani akwa kama mnyama wa kiroho
anayeziongoza falme za huyu mnyama wa duniani. Cha kufurahisha zaidi kutokana
na tarakimu hizi za gematria ni kwamba, namba 666 inapungua hadi tisa na namba 616 hadi
nne (soma jarida la Maana ya Namba au Tarakimu (Na. 7) [Symbolism of Numbers (No. 7)]. Namba
Nne inawakilisha kazi ya uumbaji na inahusu uumbaji wa dunia na vitu vilivyoumbwa
ndani yake. Namba Sita inaaminika kuwa ni namba ya Kibinadamu. Mwanadamu
aliumbwa siku ya sita. Matumizi ya tarakimu hii na uwingi au uzidishaji wake
wote umehusiana na uumbaji na ni matokeo ya kazi ya mwanadamu na mfumo wa
uumbaji. Namba Tisa ni namba ya ukamilifu au hitimisho la mchakato wa hukumu.
Ni 3x3 na huu ni ukamilifu wa muundo wa
harakati. Tarakimu hii inakutikana kwenye mambo yote yahusuyo hukumu. Namba tatu inamaanisha ukamilisho kwa maana ya
mistari mitatu ya alama. Siku ya Tatu ilikamilisha mambo ya msingi wa uumbaji. Kwa
hiyo, inonekana kwamba, kwa kujumuisha namba 666 na mfumo wake wa dini yake ya
uwongo, Hsetani anajaribu kumtoa mwanadamu (6) na kwa kukamilisha mfumo wake wa
dini ya uwongo (3) akiwapeleka wanadamu wote hukumuni (9) kwa kiasi kwamba watashindwa
hukumu ile na wasiweze kumuweka mbadala wake na wale waliomuasi. Hata hivyo,
tunajua kwamba Yesu Kristo hatashindwa, na ndipo kwa kutumia tarakimu hii 616
kumuelezea au kumuonysha Shetani na kazi zake mbovu. Mungu anasema kwamba
Shetani atashindwa na hatimaye atakuwa ni sehemu ya viumbe wenye kuonekana
dhahiri (4).
Tunapoiweka Kumbukumbu la Torati 32:8 pamoja na
Ufunuo na Danieli, tunaweza kuona wanyama waliotabiriwa ni falme za ulimwengu
huu zinazoongozwa na viumbe lio kwenye ulimwengu wa kiroho. Kuna mnyama mmoja
kwa wastani, Shetani, aliye na uthibiti wote kamili wa falme hizi zote. Na hata
angeutoa ufalme wake wote kwa Masihi iwapo tu kama angemuabudu. Na hii ndiyo
sababu mtume Paulo alifanya rejea kwa kiasi kwamba tunapigana vita vya kiroho
dhidi ya majeshi yaliyo kwenye ulimwengu wa roho. Majeshi haya yaliyo kwenye
ulimwengu wa roho yana uwezo wa kutawala mawazo na nia ya mwanadamu. Ni aina
hii ya uthibiti ndio unawezesha Malaika hawa waasi kuanzisha au kuweka mfumo wa
uwongo wa kidini na ibada kwa wanadamu. Malaika hawa waasi (hayawani wa
kondeni) wanajaribu kwa makusudi kabisa kuukomesha au kuuharibu mpango wa Mungu
ambao ulikuwa ni, kama ulivyoonekana kwenye Mwanzo 1:28, wa kumpa mwandamu
mamlaka ya kuwatawala samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kwa kila
kiumbe kilichohai kitambaacho juu ya nchi. Mamlaka haya ni pamoja na kuwatawala
Makaila hawa wasioasi. Kwa kufanya hayo yasitokee, wamejaribu kwa kipindi cha
takriban miaka 6,000 sasa kumfanya mwanadamu atengane na kuwa mbali na Mungu. Wameuinua
ufalme mmoja baada ya mwingine hapa duniani, ambazo zilitumika kuwafundisha
wanadamu uwongo na kuwapotosha.
Wakati huu, Yesu Kristo (Yahova Elohim) amekuwa
akifanya kazi ili kuweka idadi kamili ya wateule hasi mahali ambapo watakuwa
tayari kuchukua maongozi ya sayari hii na kuanzisha ufalme utakaoongozwa na
Yesu Kristo mwenyewe. Kazi yake yote imefanywa kwa maelekezo Mungu Mmoja wa
Pekee na wa Kweli. Ufalme huu utaanzishwa na kuongozwa kwa mujibu wa sheria au
Torati ya Mungu iliyotolewa na Malaika wa Agano, ambaye anadhaniwa na baadhi ya
watu kuwa alikuwa ni Yesu Kristo (soma majarida ya Malaika wa YHVH (Na.
24) na Uwepo wa Yesu Kristo
Kabla ya Kuzaliwa Kwake Rasmi (Na. 243) [The Angel of YHVH (No. 24) and The Pre-Existence of
Jesus Christ (No. 243)]. Atayatawala mataifa kwa fimbo ya chuma.
Atakapokuja atawakusanya wateule, wale walitiwa alama au mhuri wa Mungu, na
atafanya vita na mnyama na wale waliopigwa mhuri wake. Ataazianzisha sheria
zote za Mungu ambazo yeye mwenewe alimkabidhi nabii Musa, ni torati ileile ambayo
huyu kahaba na binti zake wanadai kuwa zimeondolewa na hazifai kuzishika tena
na ambazo hata Waislamu wanazipuuzia kutozishika.
Wsasa tungeweza kujua vya kutosha kuhusu habari
za alama ya mnyama na tujiuze sisi wenyewe swali hili: “Je, mimi namuabudu
mnyama, au ninamuabudu Mungu Mmoja aliye Wapekee na wa Kweli?” Basi, na Tokeni kati yake anyi watu wangu!!
q