Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[027]

 

 

 

 

Ruthu


(Toleo la 2.0 19940515-200000802)

 


Kitabu cha Ruth kinaashughulika na sehemu maalumu za sheria za urithi pia ni hadithi ya sehemu moja wepo ya jammaa ya Kristo na ni mfano wa uhusiano kati ya Kristo na Kanisa.   Si vivi hivi tu hadithi ya msichana kutafuta hupa na himaya ya mwanaume.

 

 

 

 

 Christian Churches of God

POBox 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Barua Pepe: secretary@ccg.org

 

 

(Hati Miliki © 1994, 2000 Makanisa ya Kikristo ya Mungu. Edited by Wade Cox)

(tr. 2012)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakaotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Ruthu



Biblia tunayo leo haidokezi utaratibu asili wa vitabu vya maandiko ya kiebrania.  Maandiko ya kiebrania, au Agano La Kale, viligawanywa katika mikusanyo haina tatu ya vitabu vijulikanavyo kama Sheria, Manabii na Zaburi.  Wakati Yesu alifufuka na tokea wakati wa wanafunzi wake wakati walikuwa wakila chakula, aliwafungua fahamu zao kwa kumtambua akitumia sheria, manabii na zaburi. 

Luke 24:44-45 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. 25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! (Biblia Takatifu BT)

 

Katika mpangilio huu wa asili, kitabu cha Ruth kilikuwa sehemu ya kusanyiko la vitabu vya “Zaburi” vinatajua hivyo sababu kitabu cha Zaburi kilikuwa cha kwanza katika kusanyko hili).  Zaidi sana Kitabu cha Rutu kilikuwa nambari ya tano katika “vitabu vya zaburi” pamoja na vitabu vingine vine kilikuwa sehemu ya kundi ndogo la vitabu vinavyoitwa. Hati za sikukuu za Villiitwa hivyo sababu vilisomwa katika sherehe za sikukuu tofauti za mwaka. Zaidi sana, katika sikukuu vitabu hivi ndivyo vilivyokuwa vinasomwa na hata husomwa leo navyo ndio ndio hizi:

 

Kitabu                         Sikukuu

Wimbo uliobora                  Passaka

Ruthu                                     Sikukuu ya majuma (Kama Pentecost)

Maombolezo                        kifungo katika tarehe ya Ab

Muhubiri                               Sikukuu ya vipanda

Esta                                        Sikukuu ya Purim

 

Kusudi wazi la kitabu cha Ruth ni kusaidia kuelezea asili ya Nyumba ya Daudi na hivyo ni kiini hasa cha sehemu ya jamaa ya Masihi.  Walakini kuna mengi zaidi katika kitabu hiki kuliko mambo haya. Kupitia mifano ndani yake kuna maelekezo na mwongozo kwa wakristo, tukijiandaa sote pamoja na binafsi  Kuwa bibi-arusi wa Kristokatika wakati wa kurejea kwake.  Pia kinatuonyesha majukumu ya uongofu wa watu wa mataifa.

 

Kwa Mtazamo wa juu juu

Walakini, kabla hatujaingia katika masomo ya kiroho ya hiki kitabu, tutarejea nyuma kwa haraka tukitazama, maelekeo ya hadithi yake na kupata mtazamo wa juu juu katika asili yake. Kitabu cha Rutu ni moja kati ya vita viwili tu katika Biblia vilivyotajua kwa jina la kike.  Kingine ni kitabu cha Esteri. La kupendeza katika kitabu cha Rutu ni pale mwanamkle wamataifa kufanyandoa na mwanamume Muebrania, hambapo katika kitabu cha Esteri mwanamke myahudi kufanya ndoa namwanamume wamataifa. Katika kitabu Ruth hatimaye aliolewa na Boaz amabaye ni waukoo waSalmon, aliyemuoa Rahab kahaba, ambaye alitubu wakati Israeliilichukuwa umiliki wa chi ya ahadi. Rahabu alikuwa mwanamke mwingine wamataifa, na wote Rahabu na Ruth wametajwa zaidi sana katika maelezo ya idadi ya kitabu cha Matayo, juu ya ukoo wa Kristo (taz. Ukoo wa Masihi (No. 119)).  Hadithi za hao wanawake pia uonyesha kuwa ujumbe wamungu haukuwa tu kwa Israeli bali pia utaenezwa katika mataifa mengine yote.

 

Kitabu hiki kilizinduliwa wakati wa waamuzi kukiwa na njaa Yuda. Mtu mmoja kwa jina Elimeleki (maanake Mungu wangu ni Mfalme) na mke wake kwa jina Naomi (maanakemwenye kupendeza), na wanao wa kiume wawili, Mahlon (ugonchwa), na chilion (kutoboa) alitoka Bethlehem kwenda nchi ya Moab.  Kukimbia njaa.  Elimeleki alikufa na wanaye wakajitwalia wanawake kutoka kwa wmoabu waliowazingira, amabao ni Orpah(paa) na Ruth(urafiki).  Wamoabu ni wazaliwa wa Lot, kupitia wasichana wake, baada ya ya kuanguka kwa Sodom na miji ya maeneo tambarare.  Hivi wamoabu katika dhana hiyo walihusiana na Israeli, Ijapokuwa si katika ibada yao, au katika utamaduni wao. Kulingana na sheria (Kumbu.7:1-7), Waisraeli hawangeoa wanawake wa kanani, bali wanawake wa moabu walikubalika.  (Walakini, mwanaume wa Moabu hakuruhusiwa kuingia katika mkusanyiko wa bwana (Kumb. 23:30 hata hadi kwenye kizazi cha kumi.

 

Miaka kumi baada ya kifo che Elimeleki, vile vile wanawe wawili Mahloni na chilion walikufa. Pengine, (katika kupewa majina  kuna tetesi kuwa kulikuwa na mwelekeo wakuzaa magonchwa katika familia hii na hivyo labda sababu nyingine mungu aliwajilia wafe  badala ya kukuza kizazi cha Daudi kupitia Elimeleki.  Neno kutoboa pia laweza kuashiria shauku ambayo haijaidhiniswa, au mfano wa maana ya kimaandishi huenda ni matokeo ya namna ya majina wana walipewa. Kuna uwezekano pia kuwa walijaribiwa na sanamu za nchi geni.  Inaonekana hata hivyo kuwa Naomi alizikilia sana urithi wake, utamaduni na itikadhi na pia kumfundisha Yule mjane mkwe wake.

 

Naomi alipata kufahamu kuwa njaa imekatika Yuda na hakuna haja kukaa Moabu, aliamua kurejea nyumbani.  Wale wajane wakwe wake waliamua kumfuata.  Lakini ni mmoja tu, Ruthu, mwishoni alimfuata.

 

Bila mwanamume wa kuwaliza, wote wawili Naomi na Ruthu walikuwa fukara na hivyo Ruthu alitoka nch hili kuokota masalio katika mashamba wakati wa msimu wa mavuno. Kulingana na sheria wakati wa msimu wa mavuno chakula katika pembe za shamba hasikuguswa na nafaka yoyote iIlioanguka wakati wa mavuno iliwachua kwa niaba ya maskini kukusanya. Lawi 19:9 kadhalika, mashamba haya kuchua bila masalio wala misabibu zilizoanguka na hizi hazikukusanywa, pia vilichelezwa kwa ajili ya maskini (Lawi 19:10).  Kwa kujaliwa, Ruthu alienda kuokota mazao katika mashamba ya Boaz. Naye Boaz alikuwa mtajiri sana na alikuwa jamaa ya mume wa Naomi aliokufa.  Alimuhaidi ulinzi na faraja.  Naomi alipoona kuwa Mungu alijihusisha katika hili, alimshauri Ruthu kumkaribia Boaz wakati mavuno yalikwisha na kumwonyesha shauku lake la kuolewa naye.  Ruth alifanya hivyo lakini ndugu mwingine wa Jamaa ya Elimeleki alikuwa amejitaja mwanzo kwamba atamrithi Ruth.  Boaz alimkomboa kutoka kwa huyu mrithi na akamuoa.  Kitabu kimetamatishwa Boaz na Ruth wakiwa wamejaliwa mtoto wa kiume na Naomi akishangilia kwa ajili ya mkukuu wake, ambapo ndipo Daudi na mwishowe Yoshua masihi walizaliwa.

 

Ruth na kujishugulisha kwa wakristo:

Sifa moja ya maana sana kati ya tabia yake Ruthu alikuwa ni mwepesi wa kuajilia kila kitu katika maisha yake.  Aliacha vyote vilivyokuwa bora kwake.  Mfano inchi yake (kwao), jamaa yake marafiki wake utamaduni wake, ibada yake kwa ufupi, shirikisho lake lote na kumfuata Naomi hadi Israeli na kushimama naye na watu wake, na kufanya ibada kwa mungu wake.

 

Ruthu 1:1-18. Ikawa zamani za Waamuzi walipoamua, kulikuwa na njaa katika nchi. Akaondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili. 2 Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki, na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili Maloni na Kilioni, Waefrathi wa Bethlehemu ya Yuda. Wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko. 3 Akafa Elimeleki, mumewe Naomi; na yule mwanamke akasalia na wanawe wawili. 4 Nao wakaoa wake katika wanawake wa Moabu; na jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili Ruthuu. Wakakaa huko yapata miaka kumi. 5 Wakafa na Maloni na Kilioni wote wawili; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia. (Biblia Takatifu BT)

 

Kuambatana na mwandamizi wa Biblia katika nukuu yake kwenye fungu la 6, kuna jambo la kuvutia ambalo ni Naomi aliporejea Bethlehemukatika mwaka wa 1326 kutangulia ukumbuzo wa sikukuu ya pili katika 1325/24 BCE. Sikukuuu ilianza tokea wakati wa kupatanishwa kwa mwka wa Sabato na ikaendelea hadi kupatanishwa kwa mwaka wa ukumbusho wa sikuu katika mwaka wa 1324. Mwaka 1326 ulikuwa mwaka wa mavuno mara tatu. Kiangazi kilikuwa kimetamakatika katika Yunda na watu wake wangeweza kuvuna mazao yao na kujiandaa kwa pumziko la mwaka wa sababu ya mashamba. Mungu utenda kulingana na takuimu yake mwenyewe na maagizo yake Eliaz (taz. Masomo haya Takuimu ya Kalenda ya Mungu [156]; Sheria na Amri ya Nne [256]; Usomaji wa Sheria Kama Ulivyofanywa na Ezra na Nehemia [250] na  Orodha ndogo ya wakati (Nam. 272)).

 

6 Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana huko katika nchi ya Moabu amesikia ya kwamba Bwana amewajilia watu wake na kuwapa chakula. 7 Basi akatoka pale alipokuwapo, na wakweze wawili pamoja naye; wakashika njia ili kurudi mpaka nchi ya Yuda. 8 Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; Bwana na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia. 9 Bwana na awajalie kuona raha kila mmoja nyumbani kwa mumewe. Kisha akawabusu; nao wakapaza sauti zao wakalia. 10 Wakamwambia, La, sivyo; lakini tutarudi pamoja nawe kwa watu wako. 11 Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, mrejee; kwani kufuatana na mimi? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu, hata wawe waume zenu? 12 Enyi wanangu, mrejee; nendeni zenu; kwa kuwa mimi ni mzee, siwezi kupata mume tena. Kama ningesema, Natumaini; kama ningepata mume hata usiku huu, na kuzaa watoto wa kiume; 13 je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa Bwana umetoka juu yangu. 14 Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthuu akaambatana naye. 15 Naye akasema, Tazama, shemeji yako amerejea kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urejee wewe umfuate shemeji yako. 16 Naye Ruthuu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; 17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami. 18 Basi alipomwona kuwa amekaza nia yake kufuatana naye, aliacha kusema naye.

 

Daraja la ahadi ya Ruthu ilikuwa tofauti kabisa kulinganisha hile ya Olpah. Wakati Naomi alitamka nia yake ya kuaja Moabu nakurudi katika nchi yake, wote Orphah na Ruthu walianza safari pamoja naye.  Lakini wakati Naomi aliteta, Orpah aliikufa moyo na kuaja ndiposa akarudi kwa watu wake, wakati ambapo Ruthu alimkumbatia Naomi. 

 

Ruthu 1:19-22 Hivyo hao wakaendelea wote wawili hata walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote ulitaharuki kwa habari zao. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi? 20 Akawaambia, Msiniite Naomi niiteniMara, kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana. 21 Mimi nalitoka hali nimejaa, naye Bwana amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa Bwana ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa? 22 Basi Naomi akarudi; pamoja na Ruthuu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri. (Biblia Takatifu BT)

 

Wakati wa mavuno ya shayiri ambao ulikuwa wakati wa passaka.  Kukata shayiri mara ya kwanza ilikuwa zadaka ya kutikisha mganda, amabayo ilitekelezwa wakati wa sikukuu ya kwanza ya juma kufuata sabato ya kila juma katikati ya sherehe ya sikukuu. Kunayo mafundisho mengi muhimu katka hili kwa wakristo.  Naomi aliishi kama mgeni katika nchi geni, kama muwakilishi wa Mungu wa kweli kwa jinsi ya maisha yake.  Katika hili alikuwa kama kanisa la Mungu.  Wote Orpah na Ruth walifanyika kuwa watu wa jamaa yake. Wote kwa pamoja waliweza kupata msiba wa kuogofya.  Sasa ulifika wakati Naomi alijiishi kurudi kwao, na kuendelea na maisha. Mkwe wake mmoja akaahidi kumfuata Naomi na akashawishika kujitoa katika “agano’ hii.  Walakini, mkwe mwingine alikuwa hakika katika agano lake na kwa dhati alikuwa mwepesi kulipa gharama ya hile ahadi, iliyokusudia kufikisha hatima kabisa maisha yake ya awali.

 

Haina ya ahadi ambayo Ruth alidhirisha ndio haina ya ahadi sisi kama wakristo tunapaswa kutwaa.  Kwetu, toba na ubatiso vinaonyesha kakataa kabisa ubinafsi na kujiweka katika ahadi kweli ya kutuelekeza katika upeo mpya na maisha mapya katika Bwana. 

 

Warumi 6:1-5 Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu; 2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu; 3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili, 4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwanawetu; 5 ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake; (Biblia Takatifu BT)

 

Wakolosai 3:3-4 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. (Biblia Takatifu BT)

 

Walakini, Olpah alidhihirisha haina ya sikitiko la kidunia, hali ya majuto ambayo hayakumwelekeza kwenye ahadi kweli na ya bandiliko. Alitazama nyuma kwenye yale mambo angeyacha na mwisho akurudi kwayo. Kwa bahati mbaya kuna wakristo wengine walio na tabia hii, wanaojidai kutunza agano (“hakika tutaenda nawe”) na wanatulia kwa muda tu, lakini wakati chekecheo linawajia wanarudi nyuma kwenye lile waliloitwa kuhebuka nalo.

 

2 Wakorintho 7:10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti. (Biblia Takatifu BT)

 

Luka 9:62 Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu. (Biblia Takatifu BT)

 

Kwa upande mwingine Ruthu ni mfano dhahili wa ahadi halisi na anashiria wale wakristo ambao ni wepesi kuajilia kila kitu, ikiwemo maisha yao ili kumfuata Kristo ikilazimu.

 

Watu wa mahali pale walimkumbuka Naomi amabaye kwa kawaida alimwomboleza mumewe na watoto wake. Aliwadokezea machungu yake aliokuwa nayo kwa kuwapoteza wapendwa wake wakati alisema aitwe mara (SHD 4755 uchungu). Hata hivyo, kwaku yapata hayo alikuwa pia amepitia majribu makubwa na hakupoteza imani, kwa hivyo akarudi kwa watu wa nchi yake na kwa watu wake mwenyewe, labda wakati wa passaka na mikate iliotiwa chachu.

Sote tutakabiliana na kuwapoteza wapendwa wetu na majaribu megine katika mwendo wa maisha yetu na hii ni sehemu ya maendeleo yetu ya Kiroho hivi kwamba tusipoteze imani.

 

Ruth na kuokota mazazo

Wakati Naomi na Ruthu walipowasili Bethlehemu, Ruthu alichukua jukumu na kutoka kwenda kuokota masalio katika mashamba na hivyo kujitafutia riziki yeye mwenyewe na mama mkwewe.

 

Ruth 2:1-3 Basi huyo Naomi alikuwa na ndugu ya mumewe, mtu mkuu mwenye mali, wa jamaa yake Elimeleki, na jina lake aliitwa Boazi. 2 Naye Ruthuu Mmoabi akamwambia Naomi, Sasa niende kondeni, niokote masazo ya masuke nyuma yake yule ambaye nitaona kibali machoni pake. Akamwambia, Haya, mwanangu, nenda. 3 Basi akaenda, akaja akaokota masazo kondeni nyuma ya wavunaji; na bahati yake ikamtukia kwamba akaifika sehemu ya shamba iliyokuwa mali yake huyo Boazi, ambaye alikuwa wa jamaa yake Elimeleki.

 

Ruthu alienda mashambani kuokota masalio na “ikatokea” kwamba alienda  kuokota masalio katika shamba la Boaz aliyekuwa mumewake baadaye. Hii huwa ni kazi ya kustahili.Neno kuokota katika kiebrania ina maana ya –chukua/ kusanya, okota. Ambaye ilimaanisha kukusanya masalio na kumimina sehemu ya nafaka, wakati mmea ulipokuwa unavunwa.  Sasa mwokotaji akupanda mmea, mwokotaji hakubalia mmea au hakutunza mmea ulivyokuua. Hizi kazi zote zilikuwa za mwenye shamba.Mwenye kuokota alikuwa mtu tu ambaye aliruhusiwa kushiriki katika fadhili za juhudi za mwingine. Katika hali mingi hii hudokeza uhusiano wa wakristo  kwa mume wao ambaye ni Kristo wakati ujao. Ni Mungu aliyetwalika. Fumbo la mpanzi liko katika kitabu cha Matayo 13.

 

Matayo 13:3-9, 18:23 Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. 4 Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; 5 nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; 6 na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka. 7 Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga; 8 nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini. 9 Mwenye masikio na asikie……………….

18 Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi………

23 Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini. (Biblia Takatifu BT)

 

Mfano hunapendeza sababu kama “mbengu” ya injili imetabakaa kotekote baadhi yake ilianguka  katika udongo mzuri pahali ambapo umea na kunawili na kuzaa matunda. Kristo alisema kuwa udongo mzuri ni wale wanalizika neno na kulifahamu kwa kulisikia.

 

Luka 8:15 Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia. (Biblia Takatifu BT) 

 

Ni jambo la kawaida kwamba ulimwengu wote haujaufahamu au kutenda kulingana na matakwa ya injili ya ufalme wa Mungu. Mbegu lazima ianguke katika udongo mzuri. Injili lazima ipokelewe, baadaye kumea na kuendelea kuzaa matunda katikati ya watu ambao wanalifahamu neno. Kuna mambo mengi yanayousika hapa. Kwanza, kunayo kutawanyisha mbengu na kulisikia neno, pili kunakulifahamu, mwisho, kulishika kwa moyo mzuri na wa uadilifu. Jambo la mwisho ni kitu ambacho tunaweza kuthibiti. Walakini, mambo mawili ambayo yanadhihili kwamba Mungu au Kristo wanatekeleza wajibu wao chini ya uelekevu wake, na ni lazima atafanya hivyo kwetu.

 

Kristo ndiye anandaa “mchanga” wa maisha yetu ili kutufanya kuweza kupokea makusudio ya neno la Mungu, au “mbegu”.Mbona “mchanga” mwingine mwingine ni mzuri? Ni kwa sababu Kristo anatenda katika maisha, mara sote uonyesha ,miaka mingi mapema, ili kubuni kanuni zile ambazo zitztufanya kuwa tayari kupokea “mbegu”wakati unapowadia ili kutawanyisha katika maisha yetu.

 

Katika Bibilia tunapata taarifa nyingi za watu ambao walialikwa katika kutiisha njia na ambao maisha yao yalitayarishwa kwa ajili ya mbegu. Kwakati ilipokelewa.  Mfano, kuna kualikwa kwa Muethiopia Towashi:

 

Matendo 8:26-39  Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa. 27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, 28 akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. 29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. 30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? 31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. 32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. 33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi. 34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? 35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. 36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? 37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.] 38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. 39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi. (Biblia Takatifu BT)

 

Muethiopia bila shaka alikuwa ameogozwa na kuandaliwa kwa hili naye Kristo, hivyo wakati wa mwaliko wa Mungu ulipofika alikuwa amejiandaa, mwepesi na wa kupokea mbegu ya lnchili.

 

Muethiopia na wengine kama yeye waliandaliwa na kubatizwa .Philipo aliondolewa kimiujiza inaonyesha kwamba Roho Mtakatifu ungetembea pamoja na Methiopia. Kanisa la Ethiopia liliazishwa kama kanisa jipya la kujitegemea kutokana na kitendo hiki Makanisa ya Uhabeshi yalikuwa hadi miundo yenye nguvu kiroho. Mahali Fulani ambapo ukufikia karne ya nne wakati ambapo wakristo katika Asia ndogo walikuwa wanatezuka. Wahabeshi walimtuma Asakofu Mueses kuingia ndani ya Asia kuanzisha na kuuda makanisa katika yaliokueko Uchina (cf. Migawanyo Mikuu ya Makanisa Yanayoishika—Sabato [122]).

 

Si kwamba Mungu kwanza anaadaa mchanga kabla ya kutawanya mbegu katika mwelekeo wetu, Bali pia utuongoza katika njia, utujaza ujuzi na nafasi ili kwamba mbegu zikawez kumea na kunawili vizuri na kuzaa matunda. Paul aliandika 1Wakoritho 3:6-7.

 

Kila mmoja wetu anayo sehemu yake ya kutekeleza katika ukuaji wa Ukristo na kushinda vile Paulo anaelezea katika mafungu yanayofuata. Kwa yote, vyema ni Mungu anayefanya kazi kupitia kwake kristo naye utunza ujuzi ule ambao uelekeza katika ukuaji wetu.

 

Mungu hawezi “kuchezea” maisha yetu, lakini kuna shaka kiasi kwamba anaelekeza na kutia moyo yeyote kati ya haya matukio katika maisha yetu hili kufahamika zaidi ndani yetu. Hivyo tu kama Ruth, mwenye kuokota. Kristo anatenda kazi katika maisha yetu na yupo na haki kupokea ufanishi wa juhudi zake.

 

Boaz ni mfano wa Kristo

Wakati Ruth alianza kazi ya kuokota katika mashamba ya Boaz, alimtabua na kumhoji ili kuelewa kuwa yeye alikuwa nani. Baadaye Alielewa kuwa alikuwa mkwewe Naomi,  alifanya mpango maalum kwa ajili yake, kwa kuakisha kuwa Ruth alipata hifadhi na wafanyikazi wake kunufaika.

 

Ruth 2:4-14 Na tazama, Boazi akaja kutoka Bethlehemu kawaamkia wavunaji, akasema, Bwana akae nanyi. Nao wakamwitikia, Bwana na akubariki. 5 Kisha Boazi akamwuliza mtumishi aliyewasimamia wavunaji, Na huyu je! Ni msichana wa nani? 6 Yule msimamizi aliyewasimamia wavunaji akajibu, akasema, Ni yule msichana Mmoabi aliyerudi pamoja na Naomi, kutoka nchi ya Moabu; 7 naye akasema, Tafadhali niruhusu kuokota masazo, na kukusanya nyuma ya wavunaji kati ya miganda; basi akaja, naye ameshinda tangu asubuhi hata sasa, isipokuwa alikaa nyumbani kitambo kidogo. 8 Basi Boazi akamwambia Ruthuu, Mwanangu, sikiliza; wewe usiende kuokota masazo katika shamba lingine, wala usiondoke hapa, lakini ukae papa hapa karibu na wasichana wangu. 9 Macho yako na yaelekee konde walivunalo, ufuatane nao; je! Sikuwaagiza vijana wasikuguse? Tena, ukiona kiu, uende kwenye vyombo, nawe uyanywe waliyoyateka hao vijana. 10 Ndipo aliposujudia, akainama mpaka nchi, akamwambia, Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanifahamu, mimi niliye mgeni? 11 Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo. 12 Bwana akujazi kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake. 13 Ndipo aliposema, Bwana wangu, na nipate kibali machoni pako; kwa sababu wewe umeniburudisha moyo, na kumwambia mema mjakazi wako, ingawa mimi si kama mmojawapo wa wajakazi wako. 14 Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza. (Biblia Takatifu BT)

 

Kuokota masalio ilikuwa kazi ngumu na bila hakika ya kufanikiwa kama wavunaji wageakikisha  kutopakisha chochote katika kazi zao. Pia kwa wanawake wajanga kulikuwa na uwezekano wa kujeruhiwa wakifanya kazi ya kuokota katika mashamba. Katika hali ya Ruth yeye alikuwa mgeni hivyo angeweza kukejeliwa sana. Walakini, Boaz alimhakikishia ulinzi. Na pia aliwaelekeza wavunaji wake kuacha nyuma nafaka zaidi makusudi hili juhudi za Ruth ziweze kufanikiwa na aweze kufarijika.

 

Ruth 2:15-17 Naye alipoinuka tena ili aende kuokota masazo, huyo Boazi aliwaagiza vijana wake akisema, Mwacheni aokote hata kati ya miganda, wala msimkemee. 16 Tena mtoleeni kidogo katika matita na kukiacha, na akiokote, wala msimkataze. 17 Basi Ruthuu akaokota masazo kondeni hata jioni; kisha akazipura zile nafaka alizoziokota, zikawa yapata efa moja ya shayiri. (Biblia Takatifu BT)

 

Alimkaripia Ruthu, Boaz alionyesha upendo na himaya na sikitiko la jinsi Kristo anatutendea. Wakati mwingi tunakata tamaa na kuvunjika moyo katika juhudi zetu za kupanda na kuokota kile ambacho Kristo anatuandalia. Labda tunaaza kumshutumu Mungu. Mpango wake utatimia kweli? Je unijali mimi kama nafsi? Mbona maisha ni magumu?

 

Kristo na Mungu wanafahamu mawazo haya na wanaelewa masikitikoyet na mahitaji yetu. Kristo anayo hamu ya kutuandalia makao na ameeneza amani yake katika maisha yetu:

 

Luka 13:34 Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka. (Biblia Takatifu BT)

 

1Petro 5:6-7 Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; 7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. (Biblia Takatifu BT)

 

Mungu na mwanawe ambaye nimwokozi wetu hawatatuondokea.

 

Waebrania 13:5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.

 

Jinsi Boaz alimtuza Bibi arusi wake wa hatimaye, Ruthu, ndivyo Kristo atakavyotulinda sisi kwa juhudi na huruma.

 

Ruthu 2:18-2318 Akajitwika, akaenda zake mjini. Akamwonyesha mkwewe zile alizoziokota; akavitoa vile vyakula alivyovisaza alipokwisha kushiba, akampa. 19 Basi mkwewe akamwuliza, Je! Umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Na abarikiwe yeye aliyekufahamu. Naye akamwarifu mkwewe ni nani ambaye alifanya kazi kwake, akasema, Yule mtu niliyefanya kazi kwake leo jina lake aitwa Boazi. 20 Naye Naomi akamwambia mkwewe, Na abarikiwe huyo na Bwana, ambaye hakuuacha wema wake, wala kwa hao walio hai wala kwao waliokufa. Kisha Naomi akamwambia, Mtu huyu ni wa mbari yetu, mmojawapo wa jamaa yetu aliye karibu. 21 Naye Ruthuu Mmoabi akasema, Naam, akaniambia, Ukae papa hapa karibu na vijana wangu, hata watakapomaliza mavuno yangu yote. 22 Kisha Naomi akamwambia Ruthuu mkwewe, Mwanangu, ni vizuri wewe ufuatane na wasichana wake, wala watu wasikukute katika konde linginelo lote. 23 Hivyo yeye akafuatana na wasichana wake Boazi na kuokota, hata mwisho wa mavuno ya shayiri na mavuno ya ngano pia; naye alikuwa akikaa kwa mkwewe.(Biblia Takatifu BT)

 

Hii ndiyo kiini cha uaminifu wetu kwa  Kristo katika majukumu ambayo amegawanya. Paulo alisema kuna usimamizi mbalimbali na mashirika mbalimbali bali Bwana ni mmoja. Tunapaswa kudumu katika imani ya Kristo katika wakati wote huu wa mavuno yake hadi mwisho wa dunia.

 

Haturuhusiwi kurudi nyuma kwenda katika mashamba za mabwana wengine ambao wametulemea (Lile jeshi lililoanguka). Tunastahili kudumu katika  kanisa la Mungu.

Ya kwamba, tunapaswa kudumu katika ubako wetu kwa ajili ya Kristo kipindi chote cha mavuno yake. Tokea mavuno ya shyiri ya roho mtakatifu (Pentekosti).

 

Tokea mavuno za shajiri hadi yale ya ngano ni sawa na tangia Kristo kupitia mavuno yake ya Kanisa katika ufufuo wa kwanza lakini hatuwezi koma hadi pale mavuno yote yamekwisha. Kivingine tunapaswa kutenda kazi hadi kurudi halisi kwake Masihi. Haturuhusiwi kukoma.

 

Ruthu alitafuta uposi kwa ujasiri

Jambo la kuvutia katika maisha ya Ruth ni lile kwamba alikuwa mwanamke mwenye ujasiri na mwenye kusadiki. Katika enzi zile kulikuwa na siku za ndoa zilizoratibiwa na pia siku ambazo mwanaume aliruhusiwa kuchagua mwanamwali wa kumposa. Kwa undani zaidi, tafakari hali ambayo Ruth alikuwemo. Alikuwa ni mtu wa mataifa najisi, na katika misemo ya kiutamaduni hakuwa  mmoja wa watumishi wa Boaz.

 

Ruth 2:13 Ndipo aliposema, Bwana wangu, na nipate kibali machoni pako; kwa sababu wewe umeniburudisha moyo, na kumwambia mema mjakazi wako, ingawa mimi si kama mmojawapo wa wajakazi wako. (Biblia Takatifu BT)

 

Bado alikuwa mjasiri na shupavu kwa kumuliza yule Boaz, mtu tajiri, mtu aliyeheshimika na mmiliki wa mashamba ampose. Bila shaka aliamini maamuzi ya Naomi. Naomi alifahamu kwamba mkono wa Mungu ulikuwa juu ya jambo hili. Kulikuwa pia na swali halali hapa kwamba ujasiri wake haukutokana na tama yake mwenyewe.

 

Ruthu 3:1-18 Kisha Naomi akamwambia mkwewe, Je! Mwanangu, si vizuri nikutafutie raha, ili upate mema? 2 Basi na huyu Boazi, je! Siye wa mbari yetu, ambaye ulikuwapo pamoja na wasichana wake? Tazama, usiku wa leo atakuwa akipepeta shayiri pale ugani. 3 Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; walakini usijionyeshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa. 4 Nayo itakuwa wakati atakapolala, utapaangalia mahali alalapo, nawe uingie, uifunue miguu yake ujilaze hapo; na yeye atakuambia utakalofanya. 5 Akamwambia, Hayo yote unenayo mimi nitayafanya. 6 Basi akashuka mpaka ugani; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza. 7 Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala penye mwisho wa chungu ya nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo. 8 Na ikawa usiku wa manane yule mtu akasituka, akajigeuza; na kumbe! Yupo mwanamke amelala miguuni pake. 9 Akasema, Ama! Ni nani wewe? Akamjibu, Ni mimi, Ruthuu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu. 10 Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na Bwana; umezidi kuonyesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, kama ni maskini kama ni matajiri. 11 Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana mji wote pia wa watu wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema. 12 Tena ndiyo kweli ya kuwa mimi ni wa jamaa yako aliye karibu; lakini kuna mtu wa jamaa aliye karibu kuliko mimi. 13 Wewe ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo jamaa; Bwana aishivyo. Ulale wewe hata asubuhi. 14 Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake hata asubuhi; akaondoka mapema asijaweza mtu kumtambua mwenziwe; maana Boazi amesema, Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika penye uga. 15 Tena alisema, Lete hapa shela yako uliyoivaa, uishike; naye akaishika; naye akampimia vipimo sita vya shayiri akamtwika; kisha huyo mwanamke akaenda zake mjini. 16 Basi alipofika kwa mkwewe, huyo akamwuliza, Je! Mwanangu, imekuwaje? Akamwambia yote yule mtu aliyomfanyia. 17 Akasema, Na vipimo hivi sita vya shayiri amenipa; maana akaniambia, Usiende kwa mkweo mikono mitupu. 18 Naye mkwewe akasema, Basi, mwanangu, tulia; hata utakapojua jinsi litakavyotukia jambo hili; kwa sababu mtu huyu hataridhika, asipolimaliza jambo hilo leo. (Biblia Takatifu BT)

 

Matakwa ya Ruthu yalikuwa Boaz angelala naye nakuonana kimwili. Mfano katika yote haya kujifunika blanketi wa Boaz miguuni pake na pia katika maneno wakati Boaz kufanya hivyo inamaana kwamba alimuliza Boazi kutekeleza majukumu kama mrithi wa jamaa yao chini ya sheria za kilevirate. Alidai haki zake kwa kutiwa mimba hili kumzaa mototo kuwa mzao wa mume wake aliyekufa na hivyo wote wawili yeye na mama mkewe wangechukua urithi wao katika kabila la Yuda na katika mlango wa Ephratah Bethlehemu. Na hii ilikuwa haki yake. Onan alikufa kwa kukataa urithi kama huu nakukataa kanuni kama hizo (cf. Makoza ya Onani (Nam. 162) na Kizazi cha Masihi (Nam. 119)). Boaz alimtambua Ruth kuwa mwanmke wa thamani (mke mwandilifu. kjv).

 

Boaz aliitikia haki za madai ya sheria ya kilevirati ambazo pia ni haki zake Ruthu ,lakini zaidi sana Boaz alitafuta pete ya heshima na akakubali ombi la kumposa na alitafuta kulipia mwenyewe, kwa kumlipa mrithi wa karibu wa Elimeleki, aliyetangulisha  takwa la kumposa Ruth.

 

Kwa jinsi hii nasi pia tutafute kwa ujasiri mkono wa Bwana kaita ndoa yake. Kristo asubiri kutuposa (kunena kiroho) katika sheria na muundo uliowekwa kwa ajili yake na Mungu.Ruth ni ishara ya kanisa ,kwa pamoja ataanda biarusi wa Kristo na Kristo ameasisiwa kuwa kama mfalme na mwana wa Mungu katika uweza wa ufufuo wake kutoka mauti.(Warumi 1:4).Atarudi katika dunia hii hili kufufua kwenye utukufu na kuingia katika ukoo wa upendo pamoja nasi inavyoashiriwa katika ndoa ya kibinadamu.

 

Waefeso 5:25-32 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. 28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. 29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. 30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. 31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. 32 Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. (Biblia Takatifu BT)

 

Kwa hivyo nasi tunapaswa kutumainia lile tukio la furaha lililo mbele yetu kwa bidii na kufadhaika.

 

Ufunuo 22:17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure. (Biblia Takatifu BT)

 

Ufunuo 22:20 Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu. (Biblia Takatifu BT)

 

Jambo la shauku tutatafakari ni kwamba, katika ndoa yetu na Kristo, itakuwa ndoa ya viumbe waliosawa, wa Elohimu kwa Elohimu. Kristo hataposa viumbe wasiomfanana katika utukufu.Tutakuwa katika upeo mmoja na ule wake ,tukiwa katika roho iliyotukuzwa ya vijana na wasichana wa Baba yetu na ambaye ndiye Mungu na Baba wa Kristo, na washirika wa urithi pamoja naye. Yeye ni kichwa chetu vile mume alivyo kichwa cha mke wake, bali wote ni sawa katika upeo na utu.

 

Waebrania 2:11 Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;(Biblia Takatifu BT)

 

Romans 8:16-17 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. (Biblia Takatifu BT)

 

Romans 8:28-29 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. 29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.(Biblia Takatifu BT)

 

1Yohana 3:1-3 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba,  kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. 3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. (Biblia Takatifu BT)

 

Hii uhusu pia jeshi pale awali.

 

Boaz kumkomboa Ruthu

Ingawa Boaz na Ruthu walitamani kuoana, Boaz hakuwa na hamu kumuoa Ruth kwa sababu ya jinsi sheria za ndoa zilivyotenda kazi chini ya sheria ikiwa mtu alikufa bila kumuacha mrithi, huyu mjane na akimposa katika ndoa na kujaliwa mtoto wa kiume wa kwanza ndiye alihesabiwa kurithi jina la ndugu aliyekufa. Leo hii katika mfumo wetu wa pendo na ndoa hili limeonekana kupote. Bali wakati ule lilifaulisha mambo mawili. Jambo la kwanza, iliakikishiwa kwamba jina la mtu aliyepotea katika Israeli na pili, ilikuwa njia ya kuwaliza wajane kwa kuwastawisha. Kiunabii, Mungu alianzisha sheria hii hili kulinda urithi wa makabila ya Isreali na usalama wa kijamii wa familia. Kutumika katika Ruth na kwingine inaashiria masomo muhimu ya kiroho ya kitabu hiki cha Ruth na walio katika ukoo wa Masihi yawezatenda ilivyotendeka. kwa hii  tunafahamu nia ya ukombozi wa watu wa mataifa katika Ukuhani uliorejeshwa wa Melikizedeki (au Melezedeki: Taz. Melkizedeki (Nam.128)).

 

Kumbukumbu la torati 25:5-9 Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe. 6 Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli. 7 Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu. 8 Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu, 9 ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi. (Biblia Takatifu BT)

 

Mwana wa Elimeleki alikufa bila kuaja mrithi. Hapakuwa na mtu wa kuendeleza jina la Elimeleki ama urithi wake (hivyo Elimeleki hakuwa  na wana wengine) waundugu wa Elimeleki, wao wakiwa jamaa wa karibu na  katika uzao wao, walikuwa na wajibu wa kutekeleza jukumu la kumtoa mrithi chini ya sheria za Livirate, jukumu hili likamwangukia ndugu na mrithi wa jamaa yake katika kabila lao. Hili upatikana pia katika asili ya amri nyingine katika Lawi 25:25.Amri hii nyingine unena:

Lawi 25:25 Kwamba nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye. (Biblia Takatifu BT)

 

Naumi alikuwa mzee sana hivi kwamba angeweza kupata watoto (Ruthu 1:12) na hivyo hangeweza kumtwalia Elimeleki mototo wa kurithi jina lake. Mali ya mlango wake na urithi havingeuswa milele,bali tu kwenye mavuno wakati wa mfumo wa ukumbusho wa sikukuu.

 

Naumi na Ruth bila shaka walilazimika kutokana na umaskini na kukosa waume na vifaa vya mavuno, wakuhusa sehemu ya urithi ulikuwa wa Elimeleki. Lilifanyika hIli kulinda mali ya mavuno kama urithi katika  makabila na familia, kulikuwa na sharti kuwa mtu wa ukoo wa Naumi kuchukua Ruth katika  ndoa  hata kama alikuwa Mmoabu hili limefahamika kutoka kwa funzo la Onan na Yuda. Mungu alimwangamiza Onan sababu alikataa kutekeleza jukumu lake na Tamar mkwewe (anayerejelewa hapa) alilazimika kufanya uzinzi na baba mkwe Yuda hili kuifadhi urithi wake mwenyewe na ule wa mume wake. Kumbuka, Ruth alikuwa mtu wa mataifa na hivyo “najisi”katika macho ya watu wengi wa Israeli. Boaz kwa hiari alitaka kumposa Ruth na katika hilo kumzalia Elimeleki mototo kijana hili kuendeleza jina la Elimeleki, lakini kulikuwa na ndugu mwingine aliyekuwa wakaribu kwa Elimeleki kuliko Boaz na ambaye alikuwa “amedai” mapema kumrithi Ruth.

 

Hii ni bora zaidi katika ujamaa wetu baina ya kristo na jeshi. Tazama katika hili kwa namna ya kiroho na kumtazama kristo na jeshi ambao wamekabithiwa wajibu wa kushughulikia wanadamu .Tumetolewa nchi ya watu wa mataifa wao si wamiliki wa Kristo wao ni wa jeshi.

 

Boaz, akiwa anaedelewa haya, ilihitajika huyu ndugu mwingine kutangulia haki zake na kanuni zilizo kwa na kununua au kukomboa mali na huku pia kutangulia kumposa Ruthu.

 

Ruthu 4:1-12 Basi Boazi akakwea kwenda mpaka langoni, akaketi pale; na tazama, yule mtu wa jamaa aliyekuwa karibu, ambaye Boazi amemnena, akapita. Naye akamwita, Haya! Wewe, karibu, uketi hapa. Naye akaja akaketi.
2 Kisha akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, Ninyi nanyi, ketini hapa. Wakaketi. 3 Kisha akamwambia yule jamaa, Huyu Naomi, aliyerudi hapa kutoka nchi ya Moabu, anauza sehemu ya ardhi aliyokuwa nayo ndugu yetu, Elimeleki; 4 nami ilikuwa nia yangu nikujulishe wewe, na kukuambia, Uinunue mbele ya hawa waliopo na mbele ya wazee wa watu wangu. Kama wewe utaikomboa, haya, uikomboe; lakini kama hutaikomboa, uniambie ili nijue mimi; kwa kuwa hakuna mtu wa kuikomboa ila wewe, na baada yako ni mimi. Naye akasema, Nitaikomboa mimi. 5 Ndipo Boazi aliposema, Siku ile utakapolinunua shamba mkononi mwa Naomi, unamnunua Ruthuu pia, huyu Mmoabi, mkewe marehemu, ili makusudi umwinulie marehemu jina katika urithi wake. 6 Basi yule jamaa aliyekuwa wa karibu akasema, Mimi sitaweza kulikomboa kwa nafsi yangu, nisije nikauharibu urithi wangu mwenyewe; basi haki yangu ya kulikomboa ujichukulie wewe, maana mimi sitaweza kulikomboa. 7 Basi hii ilikuwa desturi zamani za kale katikaIsraeli, kwa habari ya kukomboa na kubadiliana, ili kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo walivyohakikisha neno katika Israeli.
8 Basi yule jamaa akamwambia Boazi, Wewe ujinunulie mwenyewe. Akavua kiatu chake. 9 Naye Boazi akawaambia wale wazee na watu wote, Leo hivi ninyi ni mashahidi ya kwamba mimi nimenunua yote yaliyokuwa ya Elimeleki, na yote yaliyokuwa ya Kilioni na Maloni, mkononi mwa Naomi. 10 Tena, huyu Ruthuu Mmoabi, mkewe Maloni, nimemnunua awe mke wangu, makusudi nipate kumwinulia marehemu jina katika urithi wake, jina lake marehemu lisikatike miongoni mwa ndugu zake, wala langoni pa mji wake; leo hivi ninyi ni mashahidi. 11 Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. Bwana na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu. 12 Nyumba yako na ifanane na nyumba yake Peresi, ambaye kwamba Tamari alimzalia Yuda, kwa wazao atakaokupa Bwana katika mwanamke huyu. (Biblia Takatifu BT)

 

Kitendo cha kumtoa mwingine kiatu au kubazi ilikuwa kutia alama mukataba, ulikuwa utamaduni wa enzi zile, asili yake uonekana kuwa mwenye aliyekuwa na haki ya kukanyanga ardhi lilikuwa ya mmiliki wa shamba. Hapo sasa kupokezana kubazi uliwakilisha kuhamisha mali/shamba:

 

Zaburi 60:8 Moabu ni bakuli langu la kunawia. Nitamtupia Edomu kiatu changu, Na kumpigia Filisti kelele za vita. (Biblia Takatifu BT)

 

Katika jambo hili Mungu anasema kwamba atahamisha shamba la Edomu kwake mwenyewe. Inavyoonekana desturi hii ilienea katika mataifa ya zamani ya India na Ujerumani na hata katika karne iliyopita ilitumika katika nchi za mashariki.

 

Walakini, upeo wa kiroro wa haya yote ni kwamba Boaz kwa hiari alimkomboa Ruth, na kwa kweli lazima angemkoboa kabla ya kumposa. Hivyo ndivyo ilivyo pia na kristo. Mchakato wa ukombozi wetu, kurejeshwa kwetu kwa Mungu kupitia kwake kristo, kulianza na kifo cha kristo katika siku ya Pasaka

 

1Petero 1:18-19 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. (Biblia Takatifu BT)

 

Bali kuhusu sisi ungali unaendelea na  utaendelea hadi ufufuo wa kwanza wakati miili yetu itabadilishwa kutoka  umbo la mnyama kwenda kuwa umbo la kiroho na kule kuchaguliwa na kufanywa wana katika familia ya Mungu utakamilishwa.

 

Warumi 8:23 Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu. (Biblia Takatifu BT)

 

Waefeso 1:14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake. (Biblia Takatifu BT)

 

Waefeso 4:30 Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi. (Biblia Takatifu BT)

 

Boazi ni kipeo cha Kristo ambaye alikiri haki ya kurithi kabla. Katika Kumbu kumbu 32:8 tunasoma kwamba Mungu aligawa mataifa kuambatana na hesabu ya wana wa Mungu. Kila taifa lilikabidhiwa wana wa Mungu. Walikuwa na haki katika mataifa haya kwa kuyaongoza na katika maedeleo. Jeshi hili la mbiguni lazima lingetangulia urithi wao kwa Kristo. Kristo angetekeleza ukombozi na jeshi walikabidhiwa jukumu kwa ajili ya hawa wanadamu tokea wakati wa uumbaji kuendelea hadi wakati uduma ya Yesu Kristo. Walipewa miaka 4000 kufanya majukumu yao waliongezewa miaka 2000 zaidi baada ya Masihi kuwepo hapa hili kutekeleza majukumu yao.

 

Kinachofanyika ni kwamba Masihi analitoa kanisa kwenye mataifa ya inche ya Israeli na kuwakomboa kutoka kwa urithi wa jeshi lililoanguka mwanzoni chini ya shetani aliyekuwa kama nyota ya asubuhi. Deni ililipwa na kristo na anakabiliana na upeo huo. Mungu anatoa mgawo wa watu toka mataifa yasiyo ya Israeli kuwaelekeza kwake Kristo hili kuendeleza kanisa. Hiki ndicho kinaendelea hapa katika Boaz na ukombozi.

 

Mfano wa Naomi

Moja kati ya vipeo vya kupendeza vya kitabu cha Ruth ni upendo mkubwa ambao Naomi mamamkwe alikuwa nayo kwake. Ni kwa ajili ya mfano wa Naumi ambapo Ruth alikuwa mwepesi kuwachwa nyuma vitu vyote alikuwa anapenda jamaa yake, watu wake, nchi yake, ibada yake.

 

Wakiwa nyumbani Yuda ni Naomi ambaye aliona mkono wa Mungu kwa jinsi Ruth alikutana na Boaz wakati alieda kuokota mazazo. Kwa kweli, isipokuwa Naomi, Ruth asingefahamu Boazi na angebaki mtu wa mataifa kushiriki ibada za miungu ya uongo pale Moabu. Naomi ndiye aliyemshawishi Ruth kutafuta ujumba kwa Boazi.

 

Katika mambo haya, Naomi alikuwa kama Kanisa akiwakilisha ushirika wa mwili, vile inavyoleta wengine katika kuonana na Kristo na Mungu. Kanisa ndilo lina tushawishi na kutuongoza sisi binafsi kutafuta ndoa kwa bwana arusi wetu anayekuja. Hili limebaki kwetu kama wakristo, tunapoedelea na maisha yetu, kuonyesha kiwango kipi mfano wetu wakipekee unaotuorodesha tunapotangamana na watu wengine. Hatujui ni nani Mungu atamwalika kuingia katika muugano katika zamani hizi, natunaelewa kwa hakika kuwa wote waume kwa wake na watoto siku moja watapata mwaliko kuingia Kanisani katika ufufuo wa pili. Hivyo yatupasa sasa kila moja wetu kuweka mfano mzuri awezavyo kwa wengine, sababu vizuri sana uenda ikawa kwamba mfano wetu ndio Mungu atatumia kulenga ule wa ambao unaongoza “Ruth” mwingine kuelekea kwa Kristo.

 

Ruth 4:13-22 Basi Boazi akamtwaa Ruthuu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na Bwana akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume. 14 Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe Bwana, asiyekuacha leo hali huna wa jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli. 15 Naye atakurejezea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto saba, ndiye aliyemzaa. 16 Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake. 17 Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi. 18 Hivi ndivyo vizazi vya Peresi; Peresi alimzaa Hesroni; 19 na Hesroni akamzaa Ramu; na Ramu akamzaa Aminadabu; 20 na Aminadabu akamzaa Nashoni; na Nashoni akamzaa Salmoni; 21 na Salmoni akamzaa Boazi; na Boazi akamzaa Obedi; 22 na Obedi akamzaa Yese; na Yese akamzaa Daudi. (Biblia Takatifu BT)

 

Kitabu cha Ruth ni kitabu kidogo, bali kina umuhimu. Katika ukweli wake ni hadithi nzuri na yenye mguzo sana, pia ni ujumbe wa ushauri na wenye kutia moyo kwa wakiristo wakijiandaa kwa ajili ya ndoa kati yao na mfalme wao na Bwana anayekuja upesi,Yoshua ambaye ni Masihi. Tunayo heri ya ajabu mbele yetu.

 

Hebu na tukase mioyo yetu kwa hilo kusudi lililo mbele yetu na hebu ile ahadi ya Ruth rahisi lakini hodari itutie moyo ili tusukume mbele milele siku baada ya siku.

 

Ruth 1:16-17    Naye Ruthuu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; 17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami. (Biblia Takatifu BT)

 

q