Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[056]
Jinsi ya Kuadhimisha Sikukuu [056]
(Jarida 2. 1 19940917-20000209)
Jarida hili linahusika na kufundisha kuhusu mwanzo wa uadhimishaji wa sikukuu zote zilizoandikwa katika kitabu cha Mambo ya Walawi 23 ambayo inatoa mwendekezo wa jinsi ya kuielewa amri ya nne ya Mungu.
Christian Churches of God
E-mail:
secretary@ccg.org
(Copyright © 1994,
[Ikahaririwa 1997], 2000 Wade Cox)
(Tr. 2005)
Masomo
haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami
yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa
mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi
zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha
lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
This paper is available from the World
Wide Web page:
http://www.logon.org
and http://www.ccg.org
Jinsi ya Kuadhimisha Sikukuu [056]
Sura yote ya Mambo ya Walawi 23
inashughulika na kuelezea kuhusu sikukuu zilizoamriwa na Mungu. Ni jambo la
kufaa kuipima sura ile. Sikukuu zinazo fuatana moja baada ya nyingine kwa
mujibu wa maandiko matakatifu na zote zina muingiliano wa kimahusiano. Mamlaka
kwa ajili ya hizi sikukuu yameelekezwa kwenye maandiko matakatifu.
Kwanza, tutaangalia kuhusu amri ya nne ya Mungu. Huwezi au huruhusiwi
kuitunza amri moja kati ya amri hizi kumi za Mungu na ukaivunja au kuiacha
nyingine. Sabato inahusiana na sikukuu hizi. Zinasimama kutokana, au kwa pamoja
na Sabato. Ni sikukuu za Mungu, na sio sikukuu za mwanadamu (tazama jarida la: Sheria
na Amri ya Kumi ya Mungu [256].
Mambo ya Walawi 23:1-3, inasema: Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena wa wana wa Israeli, na kuwaambia, Sikukuu za BWANA, ambazo mtazipigia mbiu kuwa ni makusanyiko matakatifu; hizi ni sikukuu zangu. 3 Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yoyote; ni Sabato kwa BWANA katika makao yenu yote.
Sabato ni sikukuu. Si jambo sahihi kuifanta
siku hii kuwa ni ya kufunga saumu au kuifanya kuwa ni siku ya maombolezo. Hata
hivyo, ni kweli kuwa inatokea wakati mwingine tukikosa kuwa na uchaguzi wa
kutokea mambo haya-kama maombi ya kiroho-na maandalizi lazima yafanyike kwa
ajili ya Sabato. Tumeamriwa kukutanika. Huwezi au huruhusiwi kuiadhimisha ukiwa
nyumbani (tazama jarida la Sabato [031]. Ndivyo inavyotakiwa kufanywa
kwa sikukuu nyingine zote. Zote zimeamriwa watu kukusanyika mahali pale ambapo
Bwana, Mungu amepachagua.
Mambo ya Walawi 23:4 inasema: 4Sikukuu za BWANA ni hizi, ni makusanyiko matakatifu; ambazo mtazipigia mbiu kwa nyakati zote.
Ni jukumu la Israeli kutangaza na kupiga
mbiu kwa ajili ya sikukuu hizi kwa watu na kuagiza makutaniko yao. Si suala la
kuuliza kuwa kama utaachwa malangoni kwako.
Mambo ya Walawi 23:5-8, inasema: 5 Mwezi wa kwanza; siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni, ni
pasaka ya BWANA. 6 Na siku ya kumi na tano ya mwezi ya mwezi ule
ule ni sikukuu kwa BWANA ya mikate isiyotiwa chachu; mtaila mikate isiyochachwa
muda wa siku saba. 7 Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu
msifanye kazi yoyote ya utumishi. 8 Lakini mtasongeza
sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyiko
takatifu; msifanye kazi yoyote ya utumishi.
Inaendana na Sikukuu ya mikate isiyotiwa
Chachu. Hairuhusiwi kufanya kazi ya namna yoyote kabisa. Ni kutaniko takatifu.
Kuna wajibu wa kutoa sadaka kwa njia ya moto kwa Bwana kwa muda wa siku saba na
siku ya saba yake ni yakuitisha kutaniko takatifu. Ukijumlisha sadaka zote
(zitolewazo kwa moto), wanahesabu na kuwakilisha kwa wakati mmoja mkamilifu wa
mzunguko wa 19. ni lazima uzitunze zote ili kumalizia mzunguko. Kuna mzunguko
mwingine wa idadi kamili ya dhabihu kwenye sikukuu hizo, ambazo zina maan
nyingine zinazohusiana na serikali ya Mungu, lakini tutaziona hizo mahali
pengine.
Mambo ya Walawi 23:9-14, inasema: 9 Kisha BWANA akanena na Musa na kumwambia. 10 Nena wa wana wa Israeli, na ukawaambie, Hapo mtakapo kuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; 11 naye atautikisa mganda mbele za BWANA ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa. 12 Na siku hiyo mtakapoutikisa mganda, mtasongeza mwana kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. 13 Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba zilizochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini. 14 Nanyi msile mikate wala bisi wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote.
Sheria au amri za serikali za kidunia
hazitakiwi zifanikiwe kuzikomesha. Sababu ya kwendana navyo kuanzia Pasaka na
kuendelea, ni kukuonyesha kuwa kuna msingi wa sadaka na mavuno, kama vile
zinavyoelekeza zote kwenye mavuno. Zinaanza na Yesu Kristo, kisha zinaendelea
hadi kwa wateule, kisha zinawakilisha mavuno makuu ya jumla kuvunwa katika siku
za mwisho. Mmavuno yote haya huanza kutoka wakati wa malimbuko, na halafu
zinajengeka na kukua hadi kufikia ukubwa mkuu. Kila moja ni ya muhimu ili
kuweza kuiendeleza inayofuatia. Kwa hiyo, kuna utaratibu mzima wa maendelezo
(tazama jarida la: Pasaka [098]; Ushirika wa Meza ya Bwana [103]; Usiku wa
Kuuangalia Sana [101]; Maana ya Kuohwa Miguu [099]; Maana ya Mkate na Divai
[100]; Sadaka ya Mganda wa kutikiswa [106b]; Kifo cha Mwana kondoo [242].
Mambo ya Walawi 23:15-21 inasema hivi: 15 Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mlioyouleta mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba, 16 hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea BWANA sadaka ya unga mpya. 17 Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA. 18 Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtasongeza wana kondoo saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza, na ng’ombe mume mmoja, na kondoo waume wawili; watakuwa sadaka ya kuteketezwa aka zao kwa BWANA, pamoja na sadaka yao ya unga, na sadza kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza iliyosogezwa kwa BWANA kwa njia ya moto. 19 Nanyi mtamsongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wana kondoo wawili waume wa mwaka wa kwanza kuwa dhabihu ya sadaka za amani. 20 Kisha kuhani atawatikisa pamoja na hiyo mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA, pamojana wale kondoo wawili; watakuwa watakatifu kwa BWANA , wawe wa huyo kuhani. 21 Nanyi mtapiga mbiu siku iyo hiyo; kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; msifanye kazi yoyote ya utumishi; ni amri ya milele katika makao yenu yote, katika vizazi vyenu.
Hii huokwa na chachu. Kwa hiyo tumesafiri
kuanzia kusikotiwa na chachu hadi kwenye kutiwa na chachu; tumehesabu siku 50
na sasa tumeenda kwenye Pentekoste na tunatoa sadaka ya chachu. Chachu ile ni
Roho Mtakatifu atendaye kazi kwa wateule. Pentekoste inawakilisha kuitwa kwetu
tutoke. Haya ndio mavuno yetu. Tunaelekea mbele tukipitia kwenye maelfu ya
miaka kufikilia utimilifu wa siku za mwisho. Hii ndio sikukuu yetu. Hii ndio
inayotuwakilisha sisi. Pasaka inamwakilisha Kristo, Pentekoste hutuwakilisha
sisi na sikukuu inayofuatia inawakilisha utaratibu mwingine wa ukuu. Inawakilisha
mamlaka yetu, utawala na mavuno ya wokovu wa watu na wa sayari (tazama jarida
la Roho Mtakatifu [117].
Mambo ya Walawi 23:22 inasema: Nanyi hapo mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, msivune kabisa kabisa pembe la shamba lako, wala msiyakusanye masazo ya mavuno yako; utayaacha kwa ajili ya huyo masikini, na mgeni, mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Kuna mambo yaliyoachwa kwa ajili ya watu
wengine. Tuna wajibu endelevu wa kuwasaidia watukufikia pale, na kuwapa nguvu
na ustahimilifu. Kuna maana ya kiroho na pia ya kimwili nyuma yake. Unatakiwa
kuwapa wote yote mawili. Unatakiwa kuwaongoza na kuwasaidia maskini ili waweze
kuhudhuria kwenye sikukuu ili wakue katika imani kiroho.
Mambo ya Walawi 23:23-25 inasema: 23 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 24 Nena
wa wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, kutakuwa
na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa kuzipiga baragumu, ni kusanyiko
takatifu. 25 Msifanye kazi yoyote ya utumishi; nanyi
mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto
Hii ni Sikukuu ya Baragumu. Hayakutajwa
aina yoyote ya mavuno pale. Haina kitu cha kufanyia hapa. Kristo atakuja akiwa
kama Masihi ili atuokoe na kuanzisha utawala wake hapa kwenye sayari hii ya
dunia. Sisi tuna sehemu katika mpango huu. Hakuna mavuno wakati wa Baragumu.
Mavuno huwa watati na kuanzia Pentekoste (tazama jarida la: Baragumu [136].
Sisi sote, wakati wa Pentekoste,
tulichaguliwa na kutolewa nje ya mifumo ya kidunia. Kama kungekuwa na mavuno
wakati wa Baragumu, basi mavuno hayo yasingelifanya kazi yoyote hadi Masihi
alipokuja. Lakini mavuno yalikuja na roho Mtakatifu, na sio kwa wakati wa
kumngojea Masihi aje na kuwa kama mfalme wa Israeli. Hii ndio maana sisi hatuna
aina yoyote ya mavuno au sadaka yoyote inayotolewa wakati wa sikuu ya Baragunu
na haipaswi kabisa kutolewa. Pia ndivyo inavyokuwa kwa siku ya Upatanisho.
Mambo ya Walawi 23:26-32 inasema Kisha BWANA akanena na Musa na kumwambia, 27 Lakini siku ya kumi ya mwezi wa huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtasongeza sadaka kwa BWANA kwa njia ya moto. 28 Nanyi msifanye kazi yoyote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ni kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za BWANA, Mungu wenu. 29 Kwa kuwa mtu awayeyote asiyejitesa mwenyewe siku iyo hiyo, atakatiliwa mbali na watu wake. 30 Na mtu ye yote afanyaye kazi ya namna yo yote siku hiyo, mtu huyo nitamwangamiza atoke katika watu wake. 31 Msifanye kazi ya namna yoyote; ni amri ya milele katika vizazi vyenu, katika makao yenu yote. 32 Itakuwa kwenu Sabato ya kusitarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zen; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.
Ni kuanzia kwenye hizi zijulikanazo kama
Sabato ambazo huanzia tangia jioni hadi jioni, kwa kuwa siku ya Upatanisho ni
mlango wa kufungulia Sabato kama inavyo elezewa katika jarida la Upatanisho
[138]. kitu pekee kinachotakiwa kwendanacho kwenye siku ya Upatanisho
ilikuwa ni kodi ya hesabu ambayo iligawanywa wakati wakati Hekalu lilipoondolewa.
Mamlaka ya hekalu yaliondolewa kwa baraka za baraza la wazee sabini. Kipindi
cha miaka arobaini kilikuwa cha kuwapa Yuda nafasi ya kutubu. Ilikuwa kabla
hawajatubu ndipo Hekalu likawa limeondolewa.
Hii kodi ya hekalu haikuwa sadaka kabisa.
Isingeweza kufanyika kama sadaka kwa maana ya mtu mmoja angeweza kutoa atoavyo
au zaidi ya mwingine, kwa kuwa kulikuwa na kiwango maalumu ambacho haikutakiwa
kukikiukwa kilichotakiwa kutolewa na kila mtu. Kupitia utoaji huu, basi
kuliwezesha kuwa kila mtu aliweza kuhesabiwa na alitakiwa kulipa kwa mujibu wa
taratibu za kuhesabu watu zilivyokuwa zinahitajika. Malipo yalishafanywa na
Kristo. Kristo ataanzisha tena Hekalu na utaratibu wake katika Yerusalemum,
wakati atakaporudi tena. Huenda pia Kristo akaanzisha tena mambo muhimu
yahusuyo maongozi. Inaonekana kwamba uanzilishi uko pale kwa ajili ya dhabihu
ili kusaidia katika utaratibu wa kimaongozi katika Hekalu. Mtu anaweza
kufikiria kuwa ingeweza kuwekwa, na Kristo ataanzisha hiki. Sisi tu Hekalu la
Mungu, sio Hekalu lililojengwa kwa mikono na kuwekwa malahi pamoja, sio
lililoko Yerusalemu. Hili ndilo, sasa, halina kodi kamilifu, na kwa kweli,
linaendana na utoshelevu kamili wa dhabihu ya Masihi. sio sadaka itolewayo kwa
kufuata mazingira fulani. Hairuhusiwi kuchangiza sadaka yoyote hadi siku ya
Upatanisho-“Hakuna mtu anayeruhusiwa kutoa zaidi ya mwingine”. Inasema waziwazi
kabisa huwezi kubadilisha kiasi hiki. Kinatakiwa kiwe katika utaratibu au
mtazamo wa kodi tu.
Kwa hiyo ndiposa tunaijenga Sikukuu ya
Vibanda au ya vijumba vya nyasi-kwa kipindi cha mwisho.
Mambo ya Walawi 23:33-44 inasema pendeza; 33 Kisha BWANA akanena na Musa na kumwambia, 34 Nena wa wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda ya siku saba kwa BWANA. 35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yoyote ya utumishi. 36 Mtamsongezea BWANA sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea BWANA sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. 37 Sikukuu za BWANA ni hizi, ambazo mtazipigia mbiu ya kuwa ni makusanyiko matakatifu, ili mumsongezee BWANA sadaka kwa moto, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na dhabihu, na sadaka ya kinywaji, kila sadaka kwa siku zake, 38 zaidi ya hizo Sabato za BWANA, na zaidi ya matoleo yenu, na zaidi ya hizo nadhiri zenu zote, na zaidi ya sadaka zenu za hiari, ambazo mwampa BWANA. 39 Lakini siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, hapo mtakapokuwa mmekwisha kuyachuma mavuno ya nchi, mtaweka sikukuu ya BWANA muda wa siku saba; siku ya kwanza kutakuwa na kustarehe kabisa, na siku ya nane kutakuwa na kustarehe kabisa. 40 Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, muda wasiku saba. 41 Nanyi mtaishika kuwa sikukuu kwa BWANA muda wa siku saba katika mwaka, ni amri ya milele katika vizazi vyenu; mtaishika katika mwezi wa saba. 42 Mtakaa katika vibanda muda wa siku saba; wazalia wote wa Israeli watakaa katika vibanda, 43 ili vizazi vyenu kujua ya kuwa niliwaketisha wana wa Israeli katika vibanda hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri; mimi ndimi BWANA Mungu wenu. 44 Naye Musa akawaambia wana wa Israeli hizo sikukuu za BWANA
(tazama majarida ya Kusanyiko [139];
Ufufuo wa Wafu [143]; na Mji wa Mungu [180].
Hatuwezi kuziondoa aukuacha hata mojawapo
wa sikukuu hizi. Zote hizi ziko kwenye sehemu ya sheria, kama endelezo la
Sabato za kila wiki. Dhabihu zinazotolewa kwa ajili yake zinatokana na mfumo wa
zaka, uliowekwa ili kulinda yale matoleo. Kuna kodi maalumu kwa ajili ya sadaka
za Sabato. Ni kodi nyingine kwa ajili ya zaka. Tutashughulika nayo baadae. Kwa
ufahamu wetu, jambo hili halijaelekezwa kwenye karne hii (tazama jarida la Utoaji
wa Zaka [161].
Tumepata ukweli kuhusu tulivyopitia hatua
hizi. Kuna mfano wa jumla wa kutoa zaka pale kama kusanyiko lililo amriwa; la
kuwa ni Sikukuu. Mungu amesema kuwa tunatakiwa tuende; na tukaishi kwanye
vujumba vya nyasi. Hakuna uchaguzi. Kila mtu binafsi yake anao wajibu
kuhudhuria Sabato na sikukuu hizi. Umuhimu huu unatokana na sababu yenye ukweli
kwamba kila mtu binafsi yake ni sehemu muhimu katika kama Hekalu la Mungu
katika mtazamo wa ushiriki wa Roho Mtakatifu na kwa yeye asiyeshiriki
kuhudhuria sikukuu katika kutaniko alilotakiwa, anaonyesha kutotilia maanani au
kutopenezwa na wazo au agizo hili la udhimishaji. Kila mmoja binafsi yake
amepewa Roho Mtakatifu kwa njia ya ubatizo ambaye kwayo amemwezesha kuwa ni
sehemu katika Hekalu la Mungu. Kristo alifanyika kuwa ni mfano kwetu sisi sote.
Bado Kristo bila kukosa kabisa aliadhimisha
sheria na sikukuu alizozianzisha akiwa kama Malaika wa Agano pale Sinai.
Sikukuu hizi na jinsi alivyoziadhimisha zimeandikwa katika Injili za Mathayo
26:17-20; Luka 2:41-42 na tena Luka 22:15. tunaona kuwa wazazi wa Kristo
walikwenda Yerusalemu kuadhimisha sikukuu ya Pasaka. Tunaona pia kuwa Kristo
alikuwepo, kule Hekaluni, kwa mara mbili zote zote, yaani akiwa wakati wake wa
kijana na kama mtu mzima (Yoh. 2:13-23; 5:1; 7:10; 10:22).
Kristo alizishika sheria ambazo
alizisimika.
Maranyingi sana watu wanahofia sana kuhusu
ni kwa namna gani watakwenda kuadhimisha sikukuu za Mungu. Wanajiuliza maswali
mengi kama vile: “Mimi nimepata kazi”, “nina nyumba”, “nina familia”-vitu
vyote hivi. Vitu hivi tulivyobarikiwa navyo vidiingilie ibada yetu kwa Mungu.
Mungu ametupa idadi kubwa ya ahadi, zikiwemo zile za kulinda mali na raslimali
zetu. Kristo alisema angewazizingira hao wanaowaogopa. Unaweza ama kupigwa ama
na Mungu au kwa yale yanayofanywa na wanadamu. Lakini hutapigwa vita na yote
kwa pamoja. Kama utapigwagwa na Mungu, basi utazitii amri zake.
Zaburi 33:18 inasema Tazama, jicho la
BWANA li kwao wamchao, Wazingojeao fadhili zake. Kwa hiyo, Mungu ametoa
ahadi ya kuwa atawaangalia wale wote wanaomcha na kumtegemea yeye. Zaburi
34:7-9 inasema: Malaika wa BWANA hufanya kituo; Akiwazunguka wamchao na
kuwaokoa. Malaika huyu wa Mungu ni Yesu Kristo.
Sasa, ahadi hii ipo katika Zaburi inayosema
kuwa atafanya makao nasi na kutuokoa.
Zaburi 34:8, inasema: Onjeni mwone ya kuwa
BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.
Kuna ahadi ambazo Bwana amezifanya.
Atamtuma mjumbe au malaika wa Bwana, mjumbe wa Agano lake kwako na
atakuakikishia kuwa upungukiwi na kitu chochote. Wala hutapoteza raslimali zako
au vitu ulivyopewa mbaraka zake na yeye. Sababu kwa nini umepewa sikukuu hizi
ni kwamba kwazo ni ishara ya wateule-kama njia ambayo kwayo utaratibu wake
unaweza kuonekana na kufahamika. Ni ishara kama bendera tuliyopewa.
Zaburi 60:4
inasema:4Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli [Sela]. Kwa usahihi zaidi ingeweza kusomeka kama kuinua
juu kwa sababu ya kweli. Unaweza kuiona kweli ya Bwana kwenye bendera
aliyotupa sisi. Hii imefanyika kwa kwa kupitia njia kuu ya sikukuu hizi.
Tunazijua sikukuu kuu tatu ambazo ni Pasaka, Pentekoste na Sikukuu ya vibanda.
Wanaume wote walitakiwa kuhudhuria. Hii
ilikuwa ina maana sawa au mfano wa watu wote waliokuwa wanaweza na kutakiwa
kwenda kufanya kazi za kijeshi na jamaa zao. Masharti yaliwekwa wazi na
kuandikwa katika kitabu cha Kutoka 23:17; 34:23; Kumbukumbu la Torati 16:16;
Zaburi 42:4; 122:4; Ezekieli 36:38; Luka 2:41; Yohana 4:45.
Wageni waliruhusiwa kujihudhurisha kwenye
sikukuu kwa mujibu wa Yohana 12:20; na Matendo 2:1-11. Hii inamaanisha kwamba
maana ya haya yote imetolewa kwetu, ili tujue kuwa sikukuu sio ishara
iliyotengwa au isiyoambatana kwa wateule. Tunaruhusiwa kuwa na watu ambao sio
miongoni mwa washirika wa kanisa mbali na wale waumini waliobatizwa ambao sio
miongoni mwa washiriki kama mwili wa Yesu Kristo. Wanaruhusiwa kuhudhuria. Ina
maana kuwa, kama tunamtii na kumcha Mungu, tunayo ile bendera tuliyopewa ambayo
imesimikwa na Bwana. Bendera hii tumepewa ili tuweze kuelewa na ili kwamba wengine
waweze kutuelewa sisi ni kina nani.
Sikukuu pia ilihudhuriwa na wanawake
(1Sam.1:3,9; Lk. 2:41-42). Ilikuwa ni ya muhimu kwa Israeli wote na wala
haikuwa ya kundi fulani tu maalumu la watu hivyo ni ya wote-waume kwa wake na
kwa wageni waishio katika malangoni mwao. Kwa maana nyingine hii iliendelea
hadi kufikia kwa wateule wakiwa kama Israeli wa kiroho.
Kanisa la Agano Jipya liliadhimisha sikukuu
kama inavyoonekana kwa mujibu wa matedo ya mtume Paulo (Mdo. 18:21; 19:21;
20:6,16; 24:11,17). Hakuna mashaka wala maswali kuamini kuwa kanisa la Agano
Jipya chini ya maongozi ya mitume kuwa waliadhimisha sikukuu hizi. Sikukuu hizi
ni za lazima na zinatufungamanisha. Adhabu kwa kushindwa kuzitunza Sikukuu hizi
inaonekana katika kitabu cha nabii Zekaria 14:16-19. Hili jambo muhimu sana
lapaswa likumbukwe.
Zekaria 14:16-17 inasema: 16 Hata itakuwa ya kwamba kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Yerusalemu, watakwea mwaka baada ya mwaka ili kumuabudu Mfalme, BWANA wa majeshi, na kuishika sikukuu ya Vibanda. 17 Tena itakuwa ya kwamba mtu awayeyote wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, BWANA wa majeshi, mvua haitanyesha kwao
Hapa tunaongelea kuhusu waliosalia. Watu
hawa watakwenda kutembea kinyume chake Yerusalemu na wote wataangamizwa. Na
kila atakaye salia atakwea mwaka baada ya mwaka kumwabudu Bwana wa Majeshi na
kuishika Sikukuu ya Vibanda. Huyu ndiye mfalme tunayemuongelea habari
zake-yaani Bwana wa Majeshi. Na kama jamaa yeyote hapa duniani wakiacha kwenda
kumwabudu Mfalme, basi mvua haitanyesha kwao.
Zekaria 14:18-19 inasema: 18 Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao;
itakuwako tauni, ambyo BWANA atawapiga mataifa wasiokwea ili kushika sikukuu ya
Vibanda. 19 Hii ndiyo adhabu ya Misri, na adhabu ya
mataifa yote wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda.
Ni kweli kwamba sio mataifa yote ya dunia
yataweza kufika huko Yerusalemu, bali ni wajukumbe au wawakilishi ndio watakao
panda kwenda huko. Pia ni jambo linaloonekana dhahiri kwamba Sikukuu ya Vibanda
kwa wakati huo.itaadhimishwa duniani kote. Adhabu kuwapata wale wasio tuma
wajumbe wao kukwea kwenda kujihudhurisha itakuwa njaa kali itawakumba!
Watakumbwa na ukame mkuu hadi pale watakapo itunza sikukuu hii kama ilivyoamriwa.
Hii ina maana ya kiroho. Kama hujihudhurishi kwenye sikukuu, hutaweza kujalizwa
na uweza wa Roho Mtakatifu-na pia huwezi kamwe kukua kiroho: wala kamwe
hutaweza kupokea chakula na urojorojo wake. Hii ndiyo maana ni muhimu sana
kujihudhurisha pale na kula chakula cha kiroho na nyama, kisha ukue katika
upendo kila mmoja na mwingine. Iwapo kama Kristo atakwenda kuanzisha hizi tena
katika mtazamo wa kimsingi hapa duniani kwa kusisitiza uendelezaji wake wakti
wa utawala wa Milenia, na hivyo itakuwa ni muhimu kwetu kuaidhimisha kwa msingi
ule ule kama kanisa la kwanza walivyo adhimisha-na kwa kweli, hii ndio wajibu
wetu kuwa tuzishike Sabato-zote kati yake.
Ahadi muhimu na za msingi zinapatikana
katika kitabu cha Kutoka 34:16-24 ambzo ni za muhimu sana.
Kutoka 34:21-24 inasema hivi: 21 Utafanya kazi siku sita, lakini katika siku ya saba utapumzika,
wakati wa kulima mashamba, na wakati wa kuvuna pia, utapumzika. 22 Nawe utaitunza sikukuu ya majuma, nayo ni ya malimbuko ya mavuno ya
ngano, na sikukuu ya kukusanya vitu mwisho wa mwaka. 23 Mara
tatu kila mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele za Bwana MUNGU, Mungu
wa Israeli. 24 Kwa kuwa mimi nitazitupa nje taifa za watu
mbele yako na kuipanua mipaka yako; wala hapana mtu yeyote atakayeitamani nchi
yako; hapo utakapokwea kwenda kuhudhuria mbele za BWANA Mungu mara tatu kila
mwaka.
Ahadi tumepewa kama isemavyo kuwa: wala hapana
mtu yeyote atakayeitamani nchi yako; Huu ni ulinzi wa mamlaka ya kimbinguni unaotokana kwa
wewe kutunza sikukuu. Hili ni neno la Mungu. watu husumbukia mashaka ya wezi.
Wakati mmoja tunaoukumbuka kututokea kupatwa na matatizo ni ule tulipochukua
kipindi cha siku ya ziada baada ya wakati wa sikukuu katika mwaka mmoja na
tukakuta vitu vyetu vimeondolewa miongoni mwa mali zetu. Huu ndio wakati wetu
pekee tunaoukumbuka kukumbwa na matatizo binafsi, na tukio hili lilitokea kwa
ajili ya faida yetu kwa kweli. Lilitokea na kutupata kama kwa nia ya
kushinikiza akilini mwetu tukumbuke jinsi kanuni ya ulinzi ilivyo.
Ufungamanisho huu ulitokea kwa wakati wake
muafaka wa sikukuu. Unapaswa kuujua muda kuafaka. Kalenda na uamuzi wa majira
ya kudhuria sikukuu kufanywa na mteule mwenyewe. Kufanya hili kwa kufuata
mkumbo wa Wayahudi ni kukosea (tazama jarida la: Kalenda ya Mungu [156].
Mfano hai ulikuwa ni sikukuu ya mwaka 1990. sikukuu iliadhimishwa kwa kuanzia
na siku ikiwa imechelewa na kuishia siku ikiwa imechelewa (kulingana na
maadhimisho ya mwandamo wa mwezi), kwa sababu kalenda ya Wayahudi ilikuwa na
makosa. Hivyo ikafanya kuwa maadhimisho ya sikukuu ijulikanayo kama Siku
Iliyokuuya Mwisho yakafanyika katika siku ambayo ilikuwa kwa hakika sio
yenyewe.
Mshirika mmoja akauliza swali akasema: Je,
kwani Mungu ataiheshimu Kalenda ya Wayahudi hata kama itakuwa imekosea kwa
mujibu wa kalenda ya mwandamo wa mwezi kama sisi tujuavyo? Akaambiwa utapata
jibu lako kesho. Tutafanya maombi usiku huu ili kwamba Mungu atufunulie kama
anaweza kuikubali sikukuu ikiandandaliwa au kufanyika katika siku iliyokosewa
au la. Siku iliyofuatia, ambayo ilikuwa ni adhimisho la Siku ya Mwisho
Iliyokuu huko Canberra, tukaenda na kukaa chini kwenye ibada. Ibada ilishindwa
kuendelea kwa sababu ya mambo makuu mawili yaliyoonekana kushindwa
yaliyolazimisha mlango kufunguliwa na ibada isimamishwe. Kulitangazwa
mivunjiko, ajali na matatizo mengine katika siku ile ya mwisho. Mtu aliyekuwa
na nguvu za kushuhudia mambo yake makuu na alichanganikiwa na hakuweza kuelewa,
au alisahau. Lakini matatizo ya kweli yalikuwa pale.ili tuweze kuelewa.
Nikasema: sasa umepata jibu lako. Naye akasena: hakika ni balaa!
Tulipata jibu letu. Jibu lilikuwa ni
kwamba, Mungu kamwe habatiki siku inayoadhimishwa kimakosa, na kwamba kalenda
ya Wayahudi ina makosa na iko kinyume na mapenzi ya Mungu.utaratibu ule
uliashiria pia kwa msimamo wa jinsi vile unavyo itunza sikukuu. Miaka kadhaa
iliyopita tulikuwa kwenye sikukuu na kijana mmoja akaibiwa akiwa kwenye
sikukuu. Akaniandikia ki waraka nami nikamrudishia. Nilisema, unapaswa ujiulize
wewe mwenyewe kwa nini umeruhusu wewe mwenyewe uibiwe. Sababu ilikuwa ni kwamba
alikuwa anarudi nyumbani na kufanya kazi kwa wasi wasi kuwa asije akapoteza
kazi yake. Hakuwa na imani kwa ahadi zisizo na masharti ambazo Mungu ametoa, ya
kwamba wala hakutakuwa na mtu atakayetamani mali zake. Wengi wetu tumelazimika
kuachilia ajira zetu ili tuweze tu kumheshimu Mungu. Lakini Mungu mara zote
aliturudishia. Ili litimie neno lake kuwa hutapungukiwa na kitu, kama tu
utazishika sheria za Mungu. Sikmsikia tena neno kwa mtu yule, lakini alitakiwa
ajihoji dhamiri iliyokuwa nafsini mwake iliyomsukuma kuishika sikukuu.
Inatakiwa umwogope mno Mungu kuliko unavyo waogopa wanadamu. Ukiona unawaogopa
na kuwatii zaidi wanadamu basi ujue kuwa huna imani kwa Mungu.
Hii ndiyo jumla ya hesabu zote. Ukweli ki
kwamba tunayekabiliana naye ni adui na mshitaki wetu anaye haribu kila kitu
chetu kabla ya wakati wa sikukuu, kama mjuavyo sana wengi wenu. Kila mmoja wetu
anakumbana na nyundo kabla ya sikukuu hadi wakati baada ya Siku ya Upatanisho
unapovunya vifungo vya madhaifu na walioonewa na kuteswa wakaachwa huru. Ikiwa
kama huja adhimisha Siku ya Upatanisho vizuri kama inavyotakiwa, ujue kuwa bado
hujavunya kungwa za madhaifu na utateseka zaidi. Inakubidi umweke Mungu mbele
kwanza kiliko kitu kingine chochote. Watu wanaweza kuhitaji kutikiwa maanani au
kuonekana kwa sababu mbali mbali kadhaa. Mara nyingi jamaa au wana familia
wanadai kuwa ndugu yao akaenao ili kuwafanya kuwa wasiweze kuhudhuria kambi la
sikukuu. Wenyi wa watu jinsi hii huwa hawaji kile wanachokifanya. Sio kosa lao.
Sio kwamba kama walioamka asubuhi na kusema: Naenda kumchokoza mtu huyu kwa
makusudi kabisa. Yule adui au mshitaki wetu huwachungulia akiwasagia meno
ya chuki. Watafanya chochote. Tumeona mamo haya yakitokea wakati wanafunzi
wanapokuwa wamegongwa na hotuba za Chuo Kikuu kuhusu ukweli huu. Mwanangu mimi
mwenye wa kike alikuwa amesalimiwa kusema Hulazimiki kufanya kile ambacho
baba yako hufanya. Akajibu Mimi siendi kuadhimisha sikukuu kwa sababu
baba yangu anafanya-bali naiadhimisha kwa sababu Mungu ameniambia.
Watakasirika na kuja juu na kujaribu
kukusukumilia mbali. Wengine wataichukulia hii kuwa kama mazoezi ya kukuumiza.
Unatakiwa uwe na imani kuu kwa Mungu. Unatakiwa kuichukulia sikukuu kama ni
kusanyiko la lazima, na unatakiwa uwepo pale. Ukweli ni kwamba kuwepo kwetu
pale ili kumtii Mungu kunamtibua na kumchukiza sana Shetani-ni kama inavyotokea
tukiwa tunaadhimisha katika siku zilizo sahihi. Shetani amefanya kila kitu
kiwezekane kuwatoa watu mbali na kumtii Mungu. Ameshinikiza kalenda ijulikanayo
kama kalenda ya Hillel II ya mwaka wa 358BK na kuichapisha kalenda hiyo ili
kwamba kwayo watu wasiweze kuishika sikukuu kwa siku zilizo muafaka, iwapo kama
utafuata kalenda ya Kiyahudi hutaweza kuzishika sikukuu vyema, kwa kuwa siku
zake huishia nje ya siku zenyewe kwa kadiri walivyotia mapokeo yao mbele ya
neno la Mungu. Hii ndiyo maana Hillel inasema: Hii itadumu hadi kurudi kwake
Masihi. Masihi hataweza kuitakabali ile. Bali ataitupilia mbali na kalenda
ya Kiyahudi na kuitia muhuri, kwa kuwa hawana mamlaka nayo juu yake.
Wanachojaribu kukifanya ni kukuzuia wewe
kutokana na kuzishika sheria za Mungu kwa uaminifu na kukuchanganya au
kuingilia imani yako kwa kufuata mapokeo ya wanadamu. Utaratibu huu umeenea
mbali hadi kufikia kweye kanuni za taratibu za sheria za kidunia, ambazo
zimewekwa kwa nia ya kusimama kinyume chetu. tuna uhuru mkubwa sana kwa majira
haya zaidikuliko wakati mwingine wowote katika historia ya kanisa, ingawa ni
mzigo kwetu. Kutakuwepo wakati itakapokuwa si huru na wakati huo utakuwa ni
wakati nyeti sana. Inatubidi tufanye zaidi ya vile tulivyonavyo na kufanya kwa
kadiri tuwezavyo na kuwa tangazo la kwa kadiri vile tunavyojua. Tunatakiwa
tufaidiane usaidizi wa kila mmoja kwa mwingine katika upendo na wema.
Tunatakiwa tupeane kila mmoja na mwingine zawadi au karama za kiroho, ili
kwamba tuweze kuendelea kama familia, na kujua maana ya kujitoa sadaka kwa
ajili ya kutumikiana.
Utaratibu huu wote mzima haufungamanishwi
kwa mzunguko wa Yerusalemu. Wala haufungamani na sehemu yoyote maalumu, lakini
pale ambapo Mungu amepachagua aweke mkono wake, kadiri sisi tulivyokuwa hatupo
katika Yerusalemu, na kwa sababu tusingeweza sisi sote kuwemo Yerusalemu, hata
kama tulipenda iwe hivyo. Wakati majira yakiwasili, watu wengi watapanda kwenda
Yerusalemu. Mataifa yote yatakwea, na hutaweza sasa kutosheleza kuwemo mataifa
yote mle Yerusalemu, hivyo basi itabidi kuwemo na muelekeo maalumu. Hili ndilo
hali halisi. Sio ni kwa ajili ya uwepo wa Hekalu na hema ya maskani.
Kutoka 33:7-11 inasema: 7 Basi desturi ya Musa, ilikuwa kutwaa ile hema, na kuikitanje ya marago mbali na hayo marago, akaikita, hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa BWANA, alitoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya marago. 8 Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema, watu wote waliondoka wakasimama, kila mtu mlangoni pa hema yake. Akamtazama Musa, hata alipokwisha kuingia hemani. 9 Ikawa Musa alipoingia humo hemani, ile nguzo ya wingu ikashuka, ikasimama mlangoni pa ile hema, naye BWANA akasema na Musa. 10 Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango wa hema; watu wote wakaondoka wakasujudu, kila mtu mlangoni pa hema yake. 11 Naye BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumishi wake Yoshua mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.
Kuazungumzia kuhusu hema ya kukutania hapa.
Hii iliitangulia Maskani. Hii ni nje ya kambi kwa sababu unajua ya kuwa Maskani
ilikuwa ni mahala pa katikati pa kambi. Uwepo wa Mungu ulikuwa kwenye lile
hema.
Wakati Musa alipokwenda kwenye hema ya
kukutania, watu wote waliinuka na kusimama kwenye milango ya hema zao na
walimtazama Musa hadi alipoingia ndani. Wingu la moto lilikaa katika mlango wa
hema. Kisha wote walipomoka kuabudu. Kisha Bwana aliongea na Musa kama vile mtu
anavyoongea na rafiki yake. Yoshua mwana wa Nuni hakwenda hema ya kukutania.
Sikukuu sio mwelekeo wa mahali pa maalumu
pa kufanyia, lakini ni mahali pake ambapo Mungu ameweka mkono wake kupitia
makuhani wake. Kwa kupitia nguzo ya moto, Yesu Kristi ataanzilisha ataanzisha
Roho wake kwenye maeneo na kulibariki eneo kilo wakati sisi tukiwa ko huko.
Mungu Hukaa katika maskani ndani ya watu
kwa Roho wake Mtakatifu (Yoh.14:3, 15:-18, 23). Mungu amefanya maskani yake na
sisi sasa katika misingi endelevu. Lakini haina maana kuwa tusiadhimishe
sikukuu kwa mahali palipo maalumu, mahali ambapo Mungu ameweka mkoko wake kwa
ajili ya kutaniko takatifu. Hilo pia haliwezi kuondoa ukweli kwamba tunavyo
vitu maalumu vya kufanya. Ukweli kuhusu kuwa sisi ni Hekalu kama ilivyoelezewa
katika 2Wakoritho 6:16 hauna maana kuwa basi hatuhitajiki kushika sheria au
Sabato. Zote zinafungamanishwa kwa pamoja. Watu husema Kama hatutakwenda
kwenda kushika Sikukuu ya Vibanda, halafu tukawa hatuendi na kuishika Sabato
kama kutanio takatifu! Lakini
ukifanya. Kristo alisema ataanzisha tena mambo hayo yote atakapokuja na kama
hutaweza kwenda kuzitunza utapatwa na njaa. Hii haina maana kuwa unaweza kukaa
tu nyumbani na ukasamehewa kutokana siku hizi zote. Tunaenda kwenye sikukuu ili
kushirikishana kila mtu na mwenzake na kusikia neno la Mungu. Kuna wajibu kwetu
sisi sote kufanya kilicho katika uwezo wetu. Kuhusu ukweli kwamba majarida haya
ya kujisomea yanawaendea watu ulimwenguni kote sasa ni ishara kuwa neno la
Mungu haitarudi nyuma bure na anategemea kuona vitu kutoka kwetu.
Haitoshi tu kusema Ooh, tunaye Roho
Mtakatifu na hatutakiwi kufanya jambo lolote. Kwanza mwite Yesu. Huu ni
aina ile ile ya maneno yaliyoenda hadi kwenye Mtaguso wa Baraza la Kalkedoni;
lililopelekea kuondoa amri ya kuitunza Sabato katika Mtaguso wa Baraza la
Laodikia mnamo mwaka 366BK; ulio pelekea ubovu katika Mtaguso wa Baraza la
Elvia mnamo mwaka 300BK. Mambo haya yote yalifanyika mapema kabla. Tunao wajibu
kuhakikisha kuwa tunafanya kwa sehemu yetu bila kujalisha kuwa tu wachache kwa
kiasi gani, maadamu bado kungali mchana kwa kufanya kazi. Muda unakuja ambao
hakuna mtu atakayeweza kufanya chochote. Hii ndio maana tunajiweka katika hali
tuliyonayo. Hii ndio maana maktaba ya mafundisho yetu yame pelekwa na
kusambazwa kila mahali na kila maeneo mbalimbali ya kona za dunia. Kila mmoja
wetu anatakiwa kufanya zaidi ya vile tunavyofanya kwa kadiri ilivyo kwamba kuna
nuru ya kutosha ya kufanya kazi.
Kuna masharti yatakiwayo katika maandalizi
kutuwezesha kufika kule. Sio tu kule kuwa na imani na maamuzi ya kuacha kazi
yako na kumfuata. Bali unataliwa kujua kuwa sisi sote tuna wajibu wa kutumika,
kifedha sawa sawa na kimwili. Ndio maana, tunatakiwa kujiandaa kupanda kwenda
kujihudhurisha kwenye sikukuu hizi. Kumbukumbu la Torati 12:17-19 inasema kuwa
kuna utaratibu kufuatwa katika kutumia fungu la zaka ya pili. Unahitajika
kutunza kwa kuweka mbali fungu lako la zaka ya pili kwa ajili ya kukuwezesha
uhudhurie kwenye sikukuu.
Kumbukumbu la Torati 12:17-19 inasema: 17 Usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya nafaka yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zozote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako; 18 lakini hivyo utakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, wewe, na mwanao mume na mke, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako, katika yote aliyoyatia mkononi mwako. 19 Jilinde nafsi yako usimwache Mlawi siku zote uishizo katika nchi yako.
Hii ni kama kiini cha aya zinazotuelezea
kuwa huwezi kukaa nyumbani na kufanya mambo haya. Unatakiwa uwemo kwenye kambi
ya sikukuu ili uweze kutumia zaka hii na kutoa kila aina ya sadaka. Kuna sadaka
za aina tatu tu zitolewazo kila mwaka. Haziwezi kutolewa ndani ya malango ya
mji wako (pamoja na mwaka usio wa kawaida wa tatu wa mzunguko wa Sabato, ambao
ni mwaka wa zaka ya tatu). Sadaka ya sikukuu inatakiwa itolewe nje ya malango yako.
Tumefungiwa kwenye ulimwengu huu na Mungu ametukomboa kutoka katika Misri.
Ametutoa na kutupeleka katika hema ya kukutania na nguzo ya moto na wingu. Kuna
maana yenye mfano wa kiroho ndani yake. Roho wa Bwana yuko pale ili atukumbushe
sisi kuwa bado tuko Misri na kwenye Jangwa la dhambi kukingojea kuja au kurudi
kwa Bwana wetu.
Utaratibu iliopp katika sayari hii sio ule
wa Yesu Kristo. Mashindano yote ya kanisa zima ni kuwa wanao Ufalme wa Mungu na
huu ni uwongo. Kama wangekuwa na Ufalme wa Mungu, na kuwa kwenye shirika la
Bwana wetu, wangefanya kile ambacho Bwana wetu anasema, lakini hawafanyi hivyo.
Kwahiyo unatakiwa unde zako mbili nao. Yeyote anayesema kuwa Wewe nipe tu
sadaka yako na wewe mwenyewe unaweza kubakia umekaa tu nyumbani ukiwa umetoa na
hakuna tatizo achukuliwe kuwa huyo hajasoma isemavyo Biblia.
Kumbukumbu la Torati 16:16 inasema hivi: Mara tatu kwa mwaka na watokee wanaume wako wote mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua; katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na katika sikukuu ya majuma, na katika sikukuu ya vibanda; wala usitokee mbele za BWANA mikono mitupu.
Kwa mujibu wa vile isemavyo hapa inaonyesha
kuwa kunatakiwa kuwe na matoleo ya sadaka mara tatu kwa mwaka. Zaka zinatakiwa
ziliwe nje ya malango ya nyumba yako. Kwa mantiki hiyo, hii itajumlisha
Pentekoste (Kum. 12:10-21). [Kwa ajili ya umbali tu na kwa vitu visivyoweza
kufikika huko mbali ndivyo peke yake viliruhusiwa viliwe ndani ya malango tena
ni kwa yule tu anayebaki nyumbani na mwenye sababu za msingi (Kum. 12:21)
tazama jarida la Kumbukumbu la Torati 12:17-28 [284]. Hii ni sababu
nyingine utakayoona kwa nini hakutakiwi kuwa na sadaka nyingine kwenye sikukuu
ya Baragumu na pia sadaka hazitolewi katika ibada ya siku ya Upatanisho. Hii ni
kwa sababu wanafanya tendo la kukumbuka jinsi walivyokuwa wangali bado utumwani
Misri, wakati Mungu, ili alipompeleka Masihi atupatanishe. Hayo sio matendo
yetu. Pia wao wanapata msukumo pamoja na familia zao-kimtazamo wa kitaifa. Kwa
mujibu wa mfumo huu ulivyo, tumeitwa tutoke chini ya awamu tatu za mavuno na
sadaka zitolewazo kwa awamu tatu za mazao ni wajibu wetu. Tunatakiwa kijiandaa,
na kamwe hatutakiwi kujihudhurisha mbele zake mikono mitupu.
Kumbukumbu la Torati 12:19 inasema: jilinde nafsi yako usimwace Mlawi siku zote uishizo katika nchi yako.
Walawi hawakuwa na urithi wowote na ndivyo
inavyokwenda kutokea wakati wa utawala wa Milenia. Sheria hiyo iko pale ili
kwamba wale watu wapate kutunzwa waweze kula. Walikatiliwa mbali na Israeli kwa
sababu Israeli walifanyika waabudu sanamu. Si kwamba Israeli waliamka tu
asubuhi moja na kuamua kuwa waabudu sanamu, la hasha. Bali Walawi ndio
waliwaruhusu na kuwafanya wawe waabudu sanamu, kwa kupitia mafundisho ya uongo
na mtindo wao wa kuongelea mambo kiulaini ulaini, na matokeo ya mwisho ilikuwa
waliondolewa mbali kwa sababu walifikia mahali pa kuwa hawana la kufanya!
Hatuwezi kuongelea au kufundisha mambo kiulaini ulaini na kuhifadhi amani yetu
wakati ambapo ibada za sanamu zinawakumba watu wa Mungu na tukitarajia kufanya
kazi kwenye mwisho wake. Hiyo ndiyo sheria au kanuni. Tukishindwa basi
tutahukumiwa, na tukikimbia kama alivyofanya Yohana Marko basi tutashughulikiwa
vinginevyo tutatakiwa kutubu na kujinyenyekeza kwa kurejea maisha yetu kwa
Mungu. Hatiwezi kujificha mbele za uso wa Mungu. Utaratibu wote mzima ni
mwajibiko wa matayarisho. Kila mmoja ana wajibu wa kuandaa, basi na uwe hapa,
na uwe umejipanga vizuri zaidi kwa namna hiyohiyo uliyopewa. Kama bado hujapewa
mbinu, basi omba nawe utapewa. Maneno ya Mungu hayataangukia chini bure. Basi
na tujue kuwa tunao wajibu. Kama wewe upo kwenye shirika la kidini
lililokengeuka, unalazimika kujiandaa kwa ajili ya kuupata ukweli wa neno.
Alama ya wateule ni kweli ya neno. Hutakiwi uwe tofauti na ukweli wa neno.
Iwapo kama huna kiasi cha kutosha cha nguvu za Roho Mtakatifu ili kukuwezesha
kuingia kwenye Ufalme wa Mungu.
Wakati wa sikukuu, tunda la Roho Mtakatifu
upendo. Na hii ndiyo alama ya mwenendo wa mteule. Tunda hili linatarajiwa
kuonekana kwa dhahiri wakati huu wa sikukuu yaani upendo ambao ni alama yetu
kuu, tunda letu, na linatakiwa lionekane kwa dhahiri kwa wote ambao wajue kuwa
ndivyo tulivyo. Hatutakiwi kusimuliwa, kuulizwa au kuombwa kuwanao au
kuuonyesha. Tunatakiwa kuhumiana kwa wazi kabisa kila mmoja na mwingine na
kuonyesha tunda la Roho Mtakatifu. Wengi wetu, kwa vipindi vingi sana,
wamefanya hivyo na unaweza kumwelezea ni nani ambaye Roho Mtakatifu anafanya
kazi ndani yake kwa sababu kuna kitu ambacho wanakifanya. Watu wanaohudhuria
kambi za sikukuu hizi kwa mara yao ya kwanza, inapasa wakiri na kusema kuwa
watu hawa kweli wanapendana na wanatakiwa wapatwe na mshangao waonapo jinsi
tunavyo hudumiana kila mtu na mwenzake kwa upendo. Haijalishi kuwa tuko wangapi
au ni kwa kiasi gani tunavuma, vile tunavyofanya mambo yetu kwa pamoja
inaonyesha jisi tulivyo na naongelea kwa mtazamo wa roho ya upendo kama ni
sehemu katika mfumo wa maisha katika kipindi cha utawala wa milenia. Kwa hiyo
wakati Masihi atakapousimamisha mfumo wa milenia, alama au ishara kuu itakuwa
ni haki na utauwa (1Kor. 13). Zitafuatana na tunda la haki na utauwa, chini ya
utaratibu utakaotawala mfumo wa Yubile.
Ulimwengu utashuhudia upendo ukitawala kila mahali na ulimwengu mzima utakuwa na amani ya kweli. Kwa hiyo, sikukuu huashiria jinsi vile tulivyo, jinsi tunavyofikiri na jinsi tunavyotenda.
q