Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[091]
Ibrahimu na
Sodoma
(Toleo La 2.0
19950212-20000201)
Jarida hili linaelezea matendo
yaliyosababisha kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora. Mwenendo wa Ibrahimu pia
umetathminiwa kwa kina, na harakati zake za kuiombea msamaha Sodoma na Gomora. Fundisho kwa
dunia ya leo liko wazi kutokana na maelezo haya. Mwenendo na harakati za
Lutu na familia yake pia vina maana na fundisho kwetu
Christian Churches of God
PO Box 369,
WODEN ACT 2606, AUSTRALIA
Email: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1995, 2000 Wade Cox)
(tr. 2013)
Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na
kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la
haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa
au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi
zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha
husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.
Jarida hili
linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org
Ibrahimu na Sodoma
Jarida hili
linaelezea kile kilichosababisha au kupelekea kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora.
Habari hii inafaa itangulie kusomwa wakati wa maandalizi ya maadhimisho ya
Pasaka. Kipindi kilichotangulia tukio la gharika kuu kilishuhudia dunia ikiwa
na lugha na usemi mmoja na ikiwa chini ya kuhani mmoja, aliyekuwa anahudumu
huko Salemu chini ya Melkizedeki. Cheo na huduma ya Melkizedeki vimekuwa ni
mambo yaliyobakiwa kwenye utata usioeleweka vizuri, kwa kuwa habari zake na
historia yake havieleweki vizuri.
Mwanzo 11:1-32 Nchi
yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. 2 Ikawa
watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya
Shinari; wakakaa huko. 3 Wakaambiana, Haya, na tufanye
matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala
ya chokaa. 4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na
mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate
kutawanyika usoni pa nchi yote. 5 Bwana akashuka ili
auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6 Bwana
akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo
wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili
wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana
akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo
ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya
waende usoni pa nchi yote.
Hapa tunasona
mtawanyiko wa watu uliotokea kwa sababu ya jambo la kiimani au kidini
lililotokea au kuanzishwa huko Babeli chini ya dini iliyoanzishwa na Nimrodi huko
na Akadi, Ereki na Kalne. Kutoka hapo aliijenga miji ya Ninawi,
Rehoboth na Kalah (Mwanzo 10:10-11). Kuhani wa
Mungu kwa vyovyote vile alikuwa Shemu
akiwa ni mwana wa Nuhu. Nuhu aliishhi miaka mia tatu na hamsini baada ya
gharika kuu (Mwanzo 9:28), na alikufa alikwa na umri wa miaka mia tisa na
hamsini (Mwanzo 9:29).
10
Hivi ndivyo vizazi vya
Shemu; Shemu alikuwa mtu wa miaka mia akamzaa Arfaksadi miaka miwili baada ya
gharika. 11 Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi
miaka mia tano, akazaa wana, waume na wake. 12 Arfaksadi
akaishi miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela. 13 Arfaksadi
akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na
wake. 14 Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi.
15 Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na
mitatu, akazaa wana, waume na wake. 16 Eberi akaishi
miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. 17 Eberi
akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, waume
na wake. 18 Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa
Reu. 19 Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia
mbili na kenda, akazaa wana, waume na wake. 20 Reu
akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. 21 Reu
akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, waume na
wake. 22 Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa
Nahori. 23 Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka
mia mbili, akazaa wana, waume na wake. 24 Nahori
akaishi miaka ishirini na kenda, akamzaa Tera. 25 Nahori
akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia na kumi na kenda, akazaa wana, waume na
wake. 26 Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na
Nahori, na Harani. 27 Na hivi ndivyo vizazi vya Tera.
Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu. 28 Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi
aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo. 29 Abramu
na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la
mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa
Iska. 30 Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto. 31 Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani,
mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika
Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko. 32 Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera
akafa katika Harani.
Kuna dondoo za
maana sana zinazojitokeza kutoka kwenye andiko lililoko kwenye sura hii ya Mwanzo
11. La kwanza linahusiana na umri wa Shemu na meingine mengi. Kutoka kwenye
andiko hili tunaweza kuzipata siku baada ya gharika kuu za kuzaliwa kwao na vifo
vyao.
Shemu aliishi
baada ya gharika kuu miaka 502 na maisha yake yana dalili za kuwa alikuwa
kiongozi au mtawala wa mataifa. Tunaweza kujitengenezea chati kuelezea mambo
haya kama ifuatavyo hapa chini.
Mababa |
Umri
wa Kuzaliwa mwana |
Kuzaliwa |
Kufa baada ya miaka ya gharika kuu |
Shemu |
100 |
|
Gharika kuu + 502 |
Arfaksadi |
35 |
Gharika + 2 |
Gharika + 440 |
Shalaki |
30 |
Gharika + 37 |
Gharika + 470 |
Eberi |
34 |
Gharika + 67 |
Gharika + 531 |
Pelegi |
30 |
Gharika + 101 |
Gharika. + 340 |
Reu |
32 |
Gharika + 131 |
Gharika + 370 |
Serugi |
30 |
Gharika + 163 |
Gharika. + 393 |
Nahori |
29 |
Gharika + 193 |
Gharika + 341 |
Tera |
70 |
Gharika + 222 |
Gharika + 427 |
Harani Nahori Abramu |
|
Gharika + ? Gharika + ? Gharika
+ 292 |
Kabla ya Gharika + 422 |
Mtawanyiko wa mataifa ulitokea wakati Abramu alipokuwa na umri wa miaka 48, wakati wa kifo cha Pelegi miaka 340 baada ya gharika kuu (Seder Olam Rabbah, Sura ya 1).
Abramu (Abraham) aliondoka
Harani baada ya kifo cha Tera mnamo mwaka + 427 baada ya Gharika. Alikuwa na
umri wa miaka sabini na tano (Mwanzo 12:4). Tunauhakika kwamba mababa walikuwa
hai kipindi cha kufa kwake Tera na alipoitamalaki nchi ya Kanaani Abramu, walikuwepo
kina Shemu, Arfaksadi, Shalaki na
Eberi. Shemu alikuwa ni mkubwa. Kwenye Mwanzo 9:26, Yehova anatajwa kuwa ni
Mungu wa Shemu na Yafeth aliiyekuwa
anaishi hemani mwake. Shemu hapa anabarikiwa, ingawaje Yafeti ni mkubwa kuliko yeye (Mwanzo 10:22). Shemu kwa hiyo
anakuwa ni kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana katika kipindi hiki cha Ibrahimu. Mgawanyo
wa wengine haujulikani, ila Shemu alikuwa
na Arfaksadi na Elamu na Ashuru,
ambao walijigawa na kujiunga pamoja kuwa Waashuru. Ufalme wa kale wa Elamu ulipounganika
na wengine, uliunda chanzo cha Dola ya Babeli (tazama jarida la Kuanguka kwa Misri (Na. 36) [The Fall of Egypt
(No. 36)].
Mtawanyiko wa
makabila unaashiria kwamba mgawanyiko wa mataifa kwenye miji na kwenye maeneno vinadhibiti
uwezekano wa kazi ya kikuhani kwa Mungu Aliye Juu Sana huko Salemu, kuwa ni
Shemu au Arfaksad, aljyepewa kile kinachojulikana kama
makazi ya wana wengine. Arfaksadi
alikufa miaka + 440 baada ya Gharika kuu, jambo linaloonyesha kuwa ni kipindi
ambacho mababa walikuwa wangali hai bado na alikuwa mkubwa, na ndiye aliyetajwa
kuwa ni Melkizedeki au Mfalme Wangu Mwema na Mtakatifu, ingawa kina Shalaki au Eberi bado wanawezekana (sawa
na ilivyo kwenye jarida la Melikizedeki (Na. 128) [Melchisedek (No. 128)]. Shemu aliitwa kuwa ni baba wa wana wote wa Eberi (Mwanzo 10:21). Kwa hiyo
inawezekana kwamba jina Waebrania linauhusiano mpana zaidi ya Waisraeli hadi
kwa watu wengine wanaohusiana. Hili ni somo la haki yenyewe.
Mwanzo 12:1-20 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika
nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi
nitakayokuonyesha; 2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na
kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3 nami nitawabariki wakubarikio, naye
akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. 4 Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru;
Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano
alipotoka Harani. 5 Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu
mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu
waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia
katika nchi ya Kanaani. 6 Abramu akapita katikati ya nchi mpaka
mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile
walikaa katika nchi hiyo. 7 Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako
nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea. 8 Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio
upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande
wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea Bwana madhabahu huko,
akaliitia jina la Bwana. 9 Naye Abramu akasafiri, akazidi kwenda pande
za kusini. 10 Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu
akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi. 11 Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia
Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso; 12 basi itakuwa, Wamisri watakapokuona
watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai. 13 Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri
kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako. 14 Basi ikawa Abramu alipofika Misri, Wamisri
wakamwona huyo mwanamke ya kwamba yeye ni mzuri sana. 15 Wakuu wa Farao wakamwona, nao wakamsifu
kwa Farao; basi yule mwanamke akachukuliwa nyumbani mwa Farao. 16 Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye
alikuwa na kondoo na ng'ombe, na punda waume, na watumwa, na wajakazi, na punda
wake, na ngamia. 17 Lakini Bwana akampiga Farao na nyumba yake
mapigo makuu, kwa ajili ya Sarai, mkewe Abramu. 18 Ndipo Farao akamwita Abramu, akasema,
N'nini hili ulilonitendea? Mbona hukuniambia ya kuwa huyo ni mkeo? 19 Mbona ulisema, Huyo ni umbu langu, hata nikamtwaa
kuwa mke wangu? Basi sasa, huyo mke wako umchukue, uende zako. 20 Farao akawaagiza watu kwa ajili yake, wakampeleka
njiani, na mkewe, na kila alichokuwa nacho.
Uondokaji wao kwenda kernye nchi ya Misri uliharakishwa kwa ajili ya ukosefu
wa imani. Abramu hakuwa na imani
ambayo kwayo Mungu angeweza kuitimiliza ahadi yake ya kumpa nchi ambayo angempea
chakula kwayo. Pia hakuwa na imani ya kutosha ambayo Mungu angemlinda kwayo, kwa
hiyo akakimbilia kwa Wamisri. Hii ni hali hakisi tuliyokuwa nayo pia hata sisi
tulipokuwa tunaishi bila imani siku za kabla ya kuongoka kwetu. Abramu akaenda Misri na zaidi sana
akamkana mke wake huko na kumruhusu awe suria wa Farao pamoja na watu wa
nyumbani mwake. Mungu akamuadhibu farao kwa ajili ya uwongo wake na kwa
vimitisho kwa suala ya Abramu. Hali ya kutozijua sheria na amri za
Mungu haikumsaidia kuwa ni kisingizio ingawaje hadi kipindi hiki torati ilikuwa
haijatolewa bado kwa Musa. Tukio hili lilitangilia kwanza na likapelekea
kutolewa kwa torati kwa Musa kwenye kipindi kilichofuatia cha takriban miaka
mia nne, lakini bado mtu huyu alihukumiwa kwa kuzivunja amri hizi. Kwa hiyo,
nafasi ya Maandiko Matakatifu ni kwamba hayakufanyi usihukumiwe au kushitakiwa
kwa udhuru kwamba torati ilikuwa haijatolewa bado kwa Musa. Amri kumi za Mungu ziliandikwa
kwenye vibao vya mawe kwakuwa Waisraeli walikuwa ndiyo kwanza wanatoka utumwani
na walikuwa hawajui lolote kuhusu sheria. Watu hawa kwenye kipindi cha ukuhani
mkuu wa Shemu hawakuwa wajinga wa kutojua chochote. Sheria za Mungu zilikuwepo
hata siku za Nuhu na za Gharika Kuu, na kwingineko kote tangu Babeli hadi Misri
na Farao aloojua vema sana na kujua kwamba Shemu alikuwa ni mrithi halali wa
Mungu. Kwa hiyo, ndoa na sheria za Mungu zilijulikana tangu kipindi cha gharia
kuu miongoni mwa mataifa. Torati kama ilitolewa kwa Musa na ndiyo ilikuwa ni
sheria kuu iliyoenea kote kwa jinsi inavyoeleweka kwa ujumla.
Mtume Paulo, kwenye maandiko yake ya Agano Jipya imetafsiriwa kwa ufinyu
sana, alipokuwa anawaandikia Wakolosai na Wagalatia kuhusu suala hili la kwamba
sheria hizi ziliandikwa kwenye ,mawe. Torati iliandikwa kwenye vibao vya mawe
na mfano anaoutoa Paulo kulinganisha hauweki umuhimu wa uwepo wa uwepo wa ukuhani
na sheria kabla ya Musa. Nuhu alielewa shera na gharika kuu iliwaadhibu mataifa
kwa kuwa walikuwa waovu na ilifutilia mbali mfumo wote wa viumbe na wanadamu—na
kundi la watu ambao hawana sehemu kwenye ufufuo wa kwanza wa watu. Sheiia
zilikuwepo na torati ilikuwa inafahamika.
Mwanzo 13:1-18 Abramu akapanda kutoka Misri, yeye,
na mkewe, na kila alichokuwa nacho, na Lutu pamoja naye, mpaka kusini. 2 Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha,
na kwa dhahabu. 3 Akaendelea kusafiri kutoka kusini
mpaka Betheli, mahali pale palipokuwapo hema yake kwanza kati ya Betheli na Ai;
4 napo ndipo palipokuwa na madhabahu aliyofanya hapo
kwanza; naye Abramu akaliitia jina la Bwana hapo.
Kwa hiyo, Abramu alitubu.
Akafukuzwa aondoke Misri kwa kuwa alimdanganya Farao na akaenda zake na akitembea
kwa miguu hadi mahali alipokuwa ameijenga ,adhabahu yake, mahali ambapo Mungu
alimtokea na akatubu.
5 Na Lutu aliyesafiri pamoja na
Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng'ombe na kondoo, na hema. 6 Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao
zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja. 7 Kukawako
ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku
zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi. 8 Abramu
akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala
kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu. 9 Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami,
nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume; ukienda upande
wa kuume, nitakwenda upande wa kushoto. 10 Lutu
akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina
maji, kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya Bwana,
kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari. 11 Basi
Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa
mashariki; wakatengana wao kwa wao. 12 Abramu akakaa
katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa katika miji ya lile Bonde; akajongeza
hema yake mpaka Sodoma. 13 Lakini watu wa Sodoma
walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya Bwana. 14 Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu,
Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa
kusini na wa mashariki na wa magharibi; 15 maana nchi
hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele. 16 Na
uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; hata mtu akiweza kuyahesabu
mavumbi ya nchi, uzao wako nao utahesabika. 17 Ondoka,
ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa
wewe nchi hiyo. 18 Basi Abramu akajongeza hema yake,
akaja akakaa kwenye mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea
Bwana madhabahu huko.
Mungu alimbariki
Abramu na pia Lutu alipokuwa pamoja na Abramu kama mwanae. Uamuzi alipewa Lutu
kuamua ni nchi gani aliyokuwa anaipenda aende. Lutu akaichagua nchi nzuri ingawaje
ilikuwa inakaliwa na watu waovu.
Mwanzo 14:1-24 Ikawa
siku za Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, na Kedorlaoma
mfalme wa Elamu na Tidali mfalme wa Goimu, 2 walifanya
vita na Bera mfalme wa Sodoma na Birsha mfalme wa Gomora, na Shinabu mfalme wa
Adma, na Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari. 3 Hawa wote wakakutana panapo bonde la
Sidimu, kwenye Bahari ya Chumvi. 4 Miaka kumi na
miwili walimtumikia Kedorlaoma, hata mwaka wa kumi na tatu wakaasi. 5 Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme
waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi
katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,
Wanefili walitajwa kwenye kitabu cha Isaya. Jambo hili limefafanuliwa kwa kina kwenye majarida ya Wanefili (Na. 154) na Kuanguka kwa Misri (Na. 36) [The Nephilim (No. 154) and The Fall of Egypt (No. 36)]. Imani au dini ya Ashitoreti na imqani hzo zote zilizoandikwa kwenya aya za 5 na 6 pia zinahusu na mambo ya imani za kidini ambazo zilishamiri na kuhusiana na huko Yeriko (tazama jarida la Kuanguka kwa Yeriko (Na. 142 [The Fall of Jericho (No. 142)].
6 na Wahori katika mlima wao Seiri, mpaka Elparani iliyo karibu na
jangwa. 7 Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio
Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari. 8 Mfalme wa Sodoma, na mfalme wa Gomora, na mfalme wa Adma,
na mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari, wakatoka wakapanga vita
panapo bonde la Sidimu; 9 wapigane na Kedorlaoma
mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu, na Amrafeli mfalme wa Shinari, na
Arioko mfalme wa Elasari, wafalme wanne juu ya wale watano. 10
Na bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami. Nao wafalme wa
Sodoma na Gomora wakakimbia, wakaanguka huko, nao waliosalia wakakimbia
milimani. 11 Wakachukua mali zote za Sodoma na Gomora
na vyakula vyao vyote, wakaenda zao. 12 Wakamtwaa
Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda
zao.
Kwa hiyo watu hawa waliyaasi mamlaka na hukumu yao ilikuwa ni ujio wa Lutu, ambaye alikuwa ni mgeni kwao na ambaye alikwenda utumwani pamoja nao. Basi uji kwamba kama utakuwa unalitumikia taifa potofu lenye kutenda dhambi, Bwana atalipeleka utumwani, basin a usishangae kuona wewe unakwenda utumwani pamoja nao wale unaowatumikia au unaoshirikiana nao.
13 Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania;
naye amekaa panapo mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu
ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu. 14 Abramu
aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake,
waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata
mpaka Dani. 15 Akajipanga apigane nao usiku, yeye na
watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa
Dameski. 16 Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na
Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu.
Hadithi hii
inaendana na ile ya Gideon. Idadi yake ni sawa na matukio yanafanana sana (tzama
jarida la Jeshi
la Gideoni na Siku za Mwisho (Na. 22) [Gideon’s Force and the Last Days (No. 22)].
17
Abramu aliporudi
kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa
Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme. 18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai,
naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. 19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu
Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe
Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu
la kumi la vitu vyote. 21 Mfalme wa Sodoma akamwambia
Abramu, Nipe mimi hao watu, na hizo mali uchukue wewe. 22 Abramu
akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye juu
sana, Muumba mbingu na nchi, 23 ya kuwa sitatwaa uzi
wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako, usije ukasema,
Nimemtajirisha Abramu; 24 isipokuwa hivyo walivyokula
vijana, na sehemu za watu waliokwenda nami, yaani, Aneri, na Eshkoli, na Mamre;
na watwae wao sehemu zao.
Mawazo mengine
kadhaa yanainuka juu ya hili. Tuna mfano wa Melkizedeki hapa ambapo andiko
linatoa wazo kubwa zaidi. Ibrahimu akatoka nje na ilikuwa ni lazima kwake kuwaokoa
watu waovu na kumuokoa mfalme muovu ili weze kumuokoa Lutu na familia yake. Pia
Abramu akatoa zaka yake kwa Melkizedeki. Sheria ile ilikuwa haijatolewa bado.
Haikuwa hata imewekwa kwenye orodha ya Amri Kumi za Sinai. Hata amri ya kutoa
zaka ilikuwa haijatolewa bado kwa kipindi cha miaka mia nne, bali tunaona kuwa
Ibrahimu hapa anatoza zaka yake kwa imani, kwa kuwa baada ya kurudi kwake
kutoka Misri, Ibrahimu alikuwa ameongoka. Alipaswa kwanza aondoke kutoka Misri,
ndipo aiimarishe imani pamoja na Isaka, ambaye naye alikwenda Misri na kisha kuondolewa
kutoka huko. Ibrahimu alizirithi ahadi. Ili kuzifanya ahadi zake zitimilike
kwake na aanzishe laini ya ukoo ambao utaurithi ukuhani wa Mungu Aliye Juu
Sana, naye pia airithi kutoka kwenye huduma ya Melkizedeki aliyekuwa akihudumu
huko Salemu na aliyekuwepo kipindi cha Ibrahimu, ambacho ni miaka takriban mia
nne baada ya gharika kuu.
Kwa hiyo kuna
ukuhani unaoendelea wa Mungu hapa duniani na ambao unamjumuisha Ibrahimu.
Hakuna kipindi chochote ambacho kimewahi kutokea kwamba kusiweko na sheria hapa
duniani, au ambacho hakikuwa na kuhani. Kutoka Adamu hadi kipindi cha Ibrahimu ni
miaka elfu mbili ya kwanza ambayo kwayo Mungu hakuwahi kuacha au kuwaacha watu
ambao amewaweka kwenye sayari hii kabisa. Baada ya kufa kwake Shemu huduma ya
ukuhani walipewa wana wa Isaka waliotokana na Ibrahimu. Hakukuwa na pengo. Kulikuwa
na kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana na asiye na uzao kama ulivyokuwa ukuhani wa
kina Haruni ambao ulikuja kuwekwa baadae. Ukuhani huu ulikuwa kwa kutokana na
wana wa Nuhu, na Ibrahimu alistahili kuuchukua ukuhani huu. Unaweza kujisomea
mabadilishano kupitia kwa Ibrahimu na Melkizedeki ili kupata maana yake zaidi (soma
jarida la Utoaji wa Zaka (Na. 161) [Tithing (No. 161)].
Watu wa Sodoma walikuwa
ndio waliotajirishwa na Abramu na watumwa wake wakawa ni ndugu na Lutu waliokaa
kati yao. Kuna maadili muhimu kwenye hadithi hii. Watu wa Sodoma na Gomora
walipewa rehema na utajiri kwa sababu watu wa Abramu walikuwa kati yao.
Mwanzo 15:1-21 Baada
ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope,
Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana. 2 Abramu
akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na
atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? 3 Abramu
akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi
wangu. 4 Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyu
hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. 5 Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu
nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 6 Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki. 7 Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru
wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi. 8 Akasema,
Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi? 9 Akamwambia,
Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa
miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa. 10 Akampatia hao
wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila
ndege hakuwapasua. 11 Hata tai walipotua juu ya mizoga
Abramu akawafukuza. 12 Na jua lilipokuwa likichwa
usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia. 13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako
utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa
muda wa miaka mia nne. 14 Hata na taifa lile,
watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi. 15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa
katika uzee mwema. 16 Na kizazi cha nne kitarudi hapa,
maana haujatimia uovu wa Waamori bado. 17 Ikawa, jua
lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita
kati ya vile vipande vya nyama. 18 Siku ile Bwana
akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa
Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati, 19 Mkeni, na
Mkenizi, na Mkadmoni, 20 na Mhiti, na Mperizi, na
Mrefai, 21 na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na
Myebusi.
Hapa ahadi inatolewa
kwa Abramu ya watoto na uzao mwingi. Hata hivyo, tukio ka kwenda utumwani Misri
linatabiriwa pia. Ndege wapenda nyama wanaishambulia dhabihu na wanajaribu
kuibeba na kuondoka nayo. Kushambuliwa kwa watu wa Ibrahimu ilikuwa ni kiwango
cha hukumu ya mataifa. Huu ndiyo msingi wa mfano wa kondoo na mbuzi kwenye
Agano Jipya. Ni baada ya utumwa huu ndipo wateule watakapotoka na mali nyingi.
Utumwa huu kama
ulivyo tu wenyewe ni mfano wa utumwa wa mataifa chini ya mateso ya Shetani,
ambayo kwayo Masihi atawakomboa katika siku za mwisho.
Waamori walikuwa hawajaondolewa
bado kwa kuwa uovu wao ulikuwa haujatimia bado. Kwa maneno mengine wangeweza
kutubu lakini ulikuwa sio muda muafaka wa kuwashughulikia kwa wakati ule. Kwa
hiyo ndpo Israeli walipaswa waende utumwani nchini Misri ili kuwaimarisha na
kisha warudi na kuurithi utajiri wote wa Waamori. Na wakati huo huo wawaondoe
Warefaimu (Rephaim) na uzao mwingine
wote wa majitu.
Kuna mlolongo
mzima wote wa matendo hapa. Israeli wasingeweza kuimarika hapa iwapo kama
wangeendelea kubakia wakiishi kwenye nchi ya Kanaani. Wangekuwa wanene sana na
wachovu, na kwa hiyo walipaswa waende utumwani kwanza. Huko ndiko wangeweza kuongezeka
idadi yao.
Miaka kumi baada
ya kurudi Kanaani, Abramu akapewa Hajiri na akamzaa Ishmaeli (Mwanzo 16:1-7), na akakimbia kwa kuwa Sara alimchukia na
kumtesa.
Malaika wa Yahova
(Yehova) anayeitwa kuwa ni Mungu Aonaye
akamwendea Hajiri na amamsihi arudi kwa Sara. Akamahidi kuwa atamuongeza yeye
na mwanae Ishmaeli aliyezaliwa wakati Abramu alipokuwa mwenye umri wa miaka
themanini na sita (Mwanzo 16:16). Hii ilikuwa ni miaka 430 baada ya gharika kuu.
Shemu, Arfaksadi, Shalaki na
Eberi walikuwa wako hai bado.
Akiwa na umri wa
miaka tisini na tisa, Abramu alipewa jina lake la Ibrahimu na Bwana akafanya
agano naye na Ibrahimu (Mwanzo 17:1-23). Hii ilikuwa ni miaka 443 baada ya
gharika kuu na Arfaksadi akafa
miaka mitatu baadae.
Mwanzo 17:1-27 Abramu alipokuwa mtu wa miaka
tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi,
uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. 2 Nami nitafanya
agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana. 3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema, 4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa
mataifa mengi, 5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu,
lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.
6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami
nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7 Agano
langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na
vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako
baada yako. 8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada
yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami
nitakuwa Mungu wao. 9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe
ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. 10 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na
wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. 11 Mtatahiriwa nyama ya
magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi. 12 Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume
katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni
asiyekuwa wa uzao wako. 13 Mzaliwa nyumbani mwako, na
mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika
mwili wenu, kuwa agano la milele. 14 Na mwanamume
mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake;
amelivunja agano langu. 15 Mungu akamwambia Ibrahimu,
Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara. 16 Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam,
nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu
watatoka kwake. 17 Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi
akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia, kwake atazaliwa mtoto?
Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa? 18 Ibrahimu
akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako. 19
Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe
utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la
milele kwa ajili ya uzao wake baada yake. 20 Na kwa
habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza
sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu. 21 Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara
atakuzalia majira kama haya mwaka ujao. 22 Mungu
akaacha kusema naye, akapanda kutoka kwa Ibrahimu. 23 Ibrahimu
akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote
walionunuliwa kwa fedha yake, wanaume wote wa watu wa nyumba ya Ibrahimu,
akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, kama Mungu alivyomwambia. 24 Naye Ibrahimu alikuwa mwenye umri wa miaka tisini na
kenda alipotahiriwa nyama ya govi lake. 25 Na Ishmaeli
mwanawe alikuwa mtu wa miaka kumi na mitatu, alipotahiriwa nyama ya govi lake. 26 Siku ile ile akatahiriwa Ibrahimu na Ishmaeli mwanawe. 27 Na watu wote wa nyumba yake, wazaliwa nyumbani, na
wanunuliwa kwa fedha katika mkono wa mgeni, wakatahiriwa pamoja naye.
Tunaelewa sasa maana
yake. Ilikuwa ni ishara ya utakaso wa mioyo kwa Roho Mtakatifu. Yenyewe ilikuwa
ni mfano, agano ambalo lilielekeza mwelekeo wa agano jipya ambalo lilikuwa ni
Yesu Kristo. Na ambalo halikuwa na halieleweki. Ni ashirio la kimwili lenye
maana ya kiroho.
Hapa agano
lilikuwa limeweka hasa kwa akupitia Sara pia. Kwa hiyo inamaanisha kuwa uzao
huu haukuwa ni wa Ibrahimu tu bali ulihusika na Sara pia. Na hapa jina la mtoto
linatolewa na Mungu mwenyewe akamuita jina lake Isaka na wale makabila kumi na
mawili walitajwa kuwa ni watawala. Utawala na ufalme umeenea kwa Wamataifa kwa
kupitia makabila haya. Wafalme nyumba kumi na mbili waliendelea kutokana na
waamuzi au mitume kumi na mbili kama baraza la watu ishirini na nne lakini Wamataifa
wanapaswa kushiriki kwenye makabila hayo kwa kupitia Agano Jipya. Tohara hii ilipaswa kuwa ni ya mioyo na
agano la tohara liliashiria kuanzishwa kwa agano halisi.
Wajumbe watatu
kutoka kwa Mungu walimjia Ibrahimu na wakambariki kabla hawajaenda kuwashughulikia
watu wa Sodoma na Gomora. Waliitwa Yehova na sio Adonai (tazama tafsiri ya
Companion Bible hasa kwenye aya za 2-3, na appendix 32: uingizaji wa jina la
Adonai badala ya Yehova kwenye Mwanzo 18:3, 27, 30, 32; 19:18, 20:4 ulifanyika
kwenye tafsiri ya Massorah ss 107-15 (Kwa mujibu wa chapisho liitwalo Ginsberg’s
edition)).
Walibadili jina
la Yahova isomeke Adonai kwakuwa hawakuupenda ukweli wa kuonekana kuwa walikuwa
ni malaika walioitwa kuwa ni Yahova. Hawa walikuwa ni Elohim watatu na hakuna
mwanadamu aliyewahi kumuona Mungu, kwa hiyo kulikuwa na Yahova watatu wengine
zaidi ya Mungu Baba. Na hii ndiyo maana waliyabadili maandiko ya Kiebrania.
Tafsiri ya The Companion Bible inaeleza kwa kina jambo hili. Kuna upotoshaji
mara 134 uliofanywa kuhusu jina hili la Yehova (Yahova) na kuitwa Adonai yaliyoorodheshwa
kwenye Appendix 32. Pia kuna mahali panapoonyesha kuwa Elohim alichukuliwa sawa
na Yehova (Yahova).
Mwanzo 18:1-21 Bwana akamtokea
Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake
mchana wakati wa hari. 2 Akainua macho yake
akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga
mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, 3 akasema,
Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi
mtumwa wako. 4 Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu,
mkapumzike chini ya mti huu. 5 Nami nitaleta chakula
kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu.
Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. 6 Basi
Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga
safi, uukande, ufanye mikate. 7 Ibrahimu akapiga mbio
kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi,
naye akahimiza kuiandaa. 8 Akatwaa siagi na
maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao
chini ya mti, nao wakala. 9 Wakamwambia, Yu wapi
Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani. 10 Akamwambia, Hakika
nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa
kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake. 11 Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao
mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. 12 Kwa
hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na
bwana wangu mzee? 13 Bwana akamwambia
Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee? 14 Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa
muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa
kiume. 15 Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana
aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka. 16 Kisha
watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja
nao awasindikize. 17 Bwana akanena, Je!
Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, 18 akiwa Ibrahimu
atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? 19 Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na
nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili
kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake. 20 Bwana
akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao
zimeongezeka sana, 21 basi, nitashuka sasa
nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.
Ahadi ilikuwa
haijatolewa bado kwa Ibrahimu bali kilikuwa ni kipindi hiki ambacho Mungu
aliamua ashughulike na mataifa ya Kanaani ambao walikuwa ni waovu sana wote.
Kwa jambo hili Ibrahimu
aliwaombea wenye haki walio kwenye mataifa haya na pia aliwaombea ndugu zake. Hii
ni ishara ya tabia za wateule. Tunatakiwa kuwaombea watu wote walio kwenye
taifa tunaloishi. Inaweza kuwa kwamba kilichomsukuma Ibrahimu kufanya hivyo ni
kwa kuwa ndugu yake Lutu na familia yake walikuwa huko, kwa hiyo alikuwa
anaguswa na kile kilichokuwa kinaenda kutokea kwa watu hawa ambao pia ni ndugu
zake.
Mwanzo 18:22-33 22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini
Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. 23 Ibrahimu
akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? 24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji,
utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? 25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na
mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
26 Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini
mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao. 27 Ibrahimu
akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu
tu. 28 Huenda wakapunguka watano katika wale
hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema,
Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. 29 Akazidi
tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya
kwa ajili ya hao arobaini. 30 Akasema, Bwana asiwe
na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema,
Sitafanya, nikiona humo thelathini. 31 Akasema, Tazama,
nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema,
Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. 32 Akasema,
Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi?
Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. 33 Basi
Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi
mahali pake.
Hapa Yehova
alikuwa ni Malaika wa Yahova (Yehova), Elohim wa Israeli tunayemjua kuwa alikuwepo
toka zama ya kabla ya kuzaliwa kwake kimwili ambaye ni Kristo. Mungu (Aliye Juu
Sana na malaika zake Elohim) alikusudia kwenda kuwaangamiza watu bali asingeweza
kufanya hivyo hata kama angekuta watu kumi tu wenye haki wamebakia humo. Ndipo
tunajifunza kuwa wajibu wa wateule katika kuyaokoa mataifa ni mkubwa.
Mwanzo 19:1-14 Basi,
wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa
Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. 2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani
mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema
mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. 3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake.
Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala. 4 Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma,
wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote. 5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja
kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua. 6 Lutu
akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake. 7 Akasema,
Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi. 8 Tazama,
ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu
mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa
wamekuja chini ya dari yangu. 9 Wakasema Ondoka hapa!
Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe,
anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana
huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango. 10 Lakini
wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga
mlango. 11 Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni
kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango. 12 Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa
zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe
katika mahali hapa; 13 maana tutapaharibu sisi mahali
hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka
tupaharibu. 14 Lutu akatoka akasema na wakweze,
waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu
Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze. 15 Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema,
Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya
mji huu. 16 Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika
mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana
alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. 17 Ikawa
walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala
usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. 18 Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu! 19
Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema
zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani
nisipatwe na yale mabaya, nikafa. 20 Basi mji huu u
karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi
yangu itaishi. 21 Akamwambia, Tazama, nimekukubali
hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena. 22
Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo
humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari. 23 Jua
lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. 24 Ndipo
Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni
kwa Bwana. 25 Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na
wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile. 26 Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya
chumvi. 27 Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali
aliposimama mbele za Bwana, 28 naye akatazama upande
wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa
nchi ukapanda, kama moshi wa tanuru. 29 Ikawa Mungu
alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika
maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu. 30 Lutu
akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa
sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake
wawili. 31 Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni
mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia
yote. 32 Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo,
tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao. 33 Wakamnywesha
baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana
habari alipolala wala alipoondoka. 34 Ikawa siku ya
pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe
mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye. 35 Wakamnywesha
tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana
habari alipolala wala alipoondoka. 36 Basi hao binti
wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. 37 Yule
mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata
leo. 38 Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina
lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.
Kitendo cha Lutu wa kuwatoa binti zake kwa wanaume kilikuwa na maana kwamba walikuwa wameposwa ama kuchumbiwa na watu wawili wanaotajwa hapa kuwa ni wakweze kwa kuwa kitendo cha kuchumbiwa tu hakikumaanisha wala kuhalalisha ndoa. Kwa hiyo, hukumu ingewaangukia wao wenyewe kama wangewachukua na kuwafanya wake zao kwa kuwa mabinti hawa walikuwa ni mabikira safi katika kipindi chote cha kuchumbiwa kwao. Walilijua hili na ndiyo maana walimkasirikia sana Lutu kwa kuwa walimuona kuwa anawahukumu kwa tendo hilo. Maana ya kiroho huenda inaweza kuhusika na Kanisa wakati mataifa yanahukumiwa kwa matendo yao sawa na wateule. Makanisa mawili ya siku za mwisho yanaharibiwa sana na ukwngeufu wa siku za mwisho. Kanisa la Wasadi limekufa na Walaodikia limetapikwa. Makanisa haya yote mawili yameondolewa kwenye rehema. Ni masalia yao tu ndio wanaoendelea kujikongoja. Hapa tunana kwamba hawa wawili wanajikongoja kwa kupitia watoto wao (Moabu na Amoni) kwa baba yao asilia. Pia kuna uwezekano mwingine kwa wanawake hawa wawili. Wanaweza kuhusika kwenye imani ya maagano na jinsi mataifa yanavyowachukulia. Kwa kibinadamu hawawezi kuingia kwenye mlango ulio salama kwa kuwa wamepigwa na upofu kwa kuwa hawaifikilii toba. Maana ya hawa watu wa Sodoma kupigwa na upofu ni kwamba walikuwa hawataki kutubu kabisa, kwa hiyo ilikuwa ni budi waingie hukumuni. Wasingeweza kuokoka. Wangefanya uharibifu kwa kuingia kwao ndani na ndiyomaana walipigwa upofu na milango lifungwa. Walipewa firsa ya kuokoka bali hawakuchukua hatua stahiki kwa kuwa hawakutubu. Wokovu wa hawa watu hawa ulitolewa kwa wana wao wawili.
Hapa wakweze Lutu walidhania kuwa hakuwa anaongea neno la maana wakati kwamba mahali penyewe palikuwa kwenye hatihati ya kuhusuriwa. Na hivi ndivyo itakavyokuwa kwenye siku za mwisho.
Mwanzo 19:15-22 And when the morning arose, then the angels hastened Lot, saying, Arise, take thy wife, and thy two daughters, which are here; lest thou be consumed in the iniquity of the city. 16 And while he lingered, the men laid hold upon his hand, and upon the hand of his wife, and upon the hand of his two daughters; the LORD being merciful unto him: and they brought him forth, and set him without the city. 17 And it came to pass, when they had brought them forth abroad, that he said, Escape for thy life; look not behind thee, neither stay thou in all the plain; escape to the mountain, lest thou be consumed. 18 And Lot said unto them, Oh, not so, my Lord: 19 Behold now, thy servant hath found grace in thy sight, and thou hast magnified thy mercy, which thou hast shewed unto me in saving my life; and I cannot escape to the mountain, lest some evil take me, and I die: 20 Behold now, this city is near to flee unto, and it is a little one: Oh, let me escape thither, (is it not a little one?) and my soul shall live. 21 And he said unto him, See, I have accepted thee concerning this thing also, that I will not overthrow this city, for the which thou hast spoken. 22 Haste thee, escape thither; for I cannot do any thing till thou be come thither. Therefore the name of the city was called Zoar. (KJV)
Kamusi ya Tsoar (SHD 6820) inatoa maana yake kuwa ni kidogo. Limechukuliwa kutoka kwenye
kamusi ya SHD 6819 Tsa’ar ambayo maana yake ni kuwa ndogo au kwa lugha
fumbo ni yenye kupuuzwa au chenye kushushwa hadhi. Mji wenyewe haukuwa na matatizo au mapatilizo na
ulishushwa chini. Kwa hiyo ulibakizwa kwa kuwa ulifanya huduma njema ya
kuyaokoa maisha ya Lutu kwa kutoa ilinzi wa namna fulani wakati mji mkubwa na
mataifa yakiangamia. Hii ni dhana ya mahali pa kukimbilia pa salama ambapo
unaweza kukimbilia kutoka sehemu moja hadi nyingine na kupewa pumziko, wakati
uharibifu utakapokuwa ukitokea karibu yako. Kuna imani dhana inayoamini kuwa
Mungu ataweka mkono wake juu yako na kukuhudumia mahitaji yako yote hapo, ili
kwamba kama itakuwa ni mbali sana kwa wewe kwenda basi utapewa maskani (sawa na
inavyosema kwenye jarida la Mahali pa Usalama (Na. 194) [The Place of Safety (No. 194)].
Mwanzo 19:23-38 The sun was risen upon the earth when Lot entered into Zoar. 24 Then the LORD rained upon Sodom and upon Gomorrah brimstone and fire from the LORD out of heaven; 25 And he overthrew those cities, and all the plain, and all the inhabitants of the cities, and that which grew upon the ground. 26 But his wife looked back from behind him, and she became a pillar of salt. 27 And Abraham gat up early in the morning to the place where he stood before the LORD: 28 And he looked toward Sodom and Gomorrah, and toward all the land of the plain, and beheld, and, lo, the smoke of the country went up as the smoke of a furnace.
Tatizo la mke wa Lutu lilikuwa ni kwamba hakuwa ametubu kikamilifu na uhusiano wake na dhambi za dunia. Aliangamia kwa ajili ya nia iliyokuwa moyoni mwake. Kuanganizwa kwa Sodoma na Gomora ni mfano wa kitu halisi kinachokwenda kutokea hapa duniani siku za mwisho.
Tumejionea jinsi mataifa yanavyoangamia kwa matendo yao wenyewe katika siku hizi za mwisho. Uharibifu wa mazingira upo kila mahali kwa wazi kabisa kama tunavyojionea wenyewe. Sio tu kuwa ni Urusi ndiyo iliyosababiusha matatizo. Nchi ya Marekani ndiyo mchafuaji mkuu wa mazingira kwa vile lilivyokuwa ni taifa lenye viwanda vikubwa. Nchini Urusi tumetangaziwa kuhusu nyambizi ya nyukilia iliyozama. Uharibifu wake wa mazingira umegharimu kiasi cha mwagiko wa lita 400 za maji yenye mionzi inayotokana na uzalishaji wa mionzi ya nyukilia inayotiririkia kwenye kwenye muundo wa mito ya huku Urusi. Urusi ni muuzaji mzuri wa silaha za nyukilia. Nchi ya Iraq imejikinga kwa kiasi cha takriban 85% ya kiwango au uwezo wake wa zamani. Maangamizi yake yako dhahiri na hayaepukiki. Wale Malaika wane wanaendeleza mikakati ya maangamizo sasa kwa kasi ya ajabu (tazama jarida la Janga la Ukame Ulimwenguni na Unabii wa Biblia (Na. 218) [Global Warming and Bible Prophecy (No. 218)].
29 Ikawa
Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu
katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu. 30 Lutu
akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa
sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake
wawili. 31 Yule
mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi
atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. 32 Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo,
tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao. 33 Wakamnywesha
baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana
habari alipolala wala alipoondoka. 34 Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia
mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu,
ukaingie ukalale naye. 35 Wakamnywesha tena baba yao mvinyo
usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala
alipoondoka. 36 Basi
hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. 37 Yule
mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata
leo. 38 Na
yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa
Waamoni hata leo. 29 Ikawa
Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu
katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu. 30 Lutu
akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa
sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake
wawili. 31 Yule
mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi
atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. 32 Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo,
tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao. 33 Wakamnywesha
baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana
habari alipolala wala alipoondoka. 34 Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia
mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu,
ukaingie ukalale naye. 35 Wakamnywesha tena baba yao mvinyo
usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala
alipoondoka. 36 Basi
hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. 37 Yule
mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata
leo. 38 Na
yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa
Waamoni hata leo.
Binsi wa Lutu walijua kwamba dunia
ingeanbamizwa tena kwa moto katika siku za mwisho. Pia waliijua habari ya
gharika kuu kwakuwa Shemu alikuwa yungali hai bado katika siku zao. Ibrahimu
alikufa miaka 519 baada ya gharika kuu akiwa na umri wa miaka mia moja na
sabini na tano alitofautiana na Shemu kwa tofauti ya miaka kumi na saba tu. Eberi alikuwa bado hai na alitofautiana na
Ibrahimu kwa miaka kumi na nne tu. Wana wa Eberi walikuwa ni wengi kwa kweli na
walistahili kabisa kuitwa watu.
Waamoni na
Wamoabi walijiunga na Israeli na hatimaye wakafanyika kuwa maadui wa Israeli.
Walikuwa na hatima yao kama tutakavyojionea huko mbele. Watu hawa walifanya
kile walichoweza kufanya kwa kuwa walijua kuwa unabii ungetimia kwa yaliyosemwa
kuhusu siku za mwisho na walidhania kuwa walikuwa kwenye siku hizi za mwisho.
q