Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[092]

 

 

 

Roho

(Toleo La 3.0 19950225-20010127-20071215)

 

Fundisho kuhusu Roho ni dhana iliyoanzishwa kutokana kosa la uasi inayosema kwamba mwanadamu hawezi kufa tu moja kwa moja. Kwa ujumla, mfumo ya imani ya walimwengu ulimwenguni kote hudai na kuamini kuwa roho huishi milele. Mtazamo wa kimafundisho wa Kibiblia kuhusu roho umegeuzwa na mporomoko wa kiroho wa Kanisa la kwanza, kama tunavyojionea kwenye mafundisho yaliyo kwenye jarida hili.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki ©  1995, 2000, 2001, 2007 Wade Cox)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

Roho


Mafundisho ya kibiblia kuhusu Roho yako wazi na ni mafundisho rahisi, ambayo yamegeuzwa mporomoko wa kiroho uliojitokeza kwenye Kanisa la kwanza. Mafundisho ya imani ya kidini kwa ujumla yamekuwa ni moja ya kile kinachodaiwa na kuaminiwa kuwa roho ni kitu kinachodumu milele. Haya siyo mafundisho ya kweli ya kibiblia. Mwendelezo wa kile kinachaitwa mtazamo wa Kikristo na uhusiano wake na mtazamo wa kibiblia ndiyo mambo yanayotazamwa na kufafanuliwa hapa.

 

Roho na Biblia

Kama ilivyoelezewa na Cox, kwenye jarida lake la Uumbaji: Kutoka Kwenye Teolojia ya Kianthropomorfiki hadi Kwenye Anthropolojia ya Kiteomorfiki (Na. B5) [Creation: From Anthropomorphic Theology to Theomorphic Anthropology (No. B5)], dhana hii ya kuamini kuwa roho inaendelea kuishi ikiwa kama kitu kinachoendelea kuishi baada ya kifo imekuwa ni kisa cha mara kwa mara kinachotokana na imani za Waaminism za Kibabeloni, na ambazo zinatokana kwenye chimbuko la mafundisho ya kiteolojia ya Wakaldayo. Na dhana yenyewe inatuama kwenye itikadi ya kuamini miungu mingi na iliyoanzishwa na waabudu miungu mingi. Biblia inaeleza wazi kabisa kwamba wafu wanabakia hivyo hivyo hadi kipindi cha ufufuo wa wafu, uwe ule wa Kwanza ama ule Ufufuo wa Pili. Hakuna mtu aliyewahi kufufuka kutoka kwa wafu zaidi ya Kristo; wateule wengine wote wanabakia kuwa bado wamelala tu mautini (1Wathesalonike 4:13-18). Ila wafu walioko mautini watafufuliwa kutoka kwa wafu:

1Wakorintho 15:16-18  Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. 17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. 18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. 

 

Kwa kweli, Kristo alifufuka kutoka kwa wafu akiwa ni malimbuko ya waliolala mautini (1Wakorintho 15:20). Daudi alikufa na akazikwa na kaburi lake tunalo hadi siku hii ya leo (Matendo 2:29).

Yohana 3:13 Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.

 

Umuhimu wa ufufuko wetu au wa miili unatokana na fundisho hili. Kitendo cha kukana ufufuo wa wafu au wa miili ambayo imekuwa ni kitu cha kimtindo tu kwenye imani ya Watrinitariani, sio jambo sahihi, inawa hali hiyo inatokana na kuelewa kimakosa maana na matukio yanayo ambatana na maadhimisho ya dhabihu ya Pasaka na sadaka yake. Ni muhimu kushughulika na ufufuo kwa undani wake hapa ili kufikia kiwango cha kuuelewa uhusiano wake na Kristo na wanadamu na Mungu, na maana ambayo kwayo Biblia inasema kwamba mwanadamu ataurithi uzima wa mileie.

 

Fundisho kuhusu Roho linaonekana kufanyiwa propaganda kwa lengo la kuliwekeza mioyoni na akilini mwa wanadamu waamini kuwa mtu anaendelea kuishi baada ya kufa kwake jambo ambalo ni uwongo kabisa, na ukweli ukiwa ni kwamba wanamngojea Mungu tu ndiye atakayeweza kuwafufua na ndipo watakapoendelea kuishi. Maelezo ya kibiblia kuhusu ushawishi au dhana hii ya ujuzi huu wa kuwasiliana na wafu au ibada hizi za kuwasiliana na kuwauliza mashauri wafu inaeleza kwamba ni udanganyifu uliozoeleka kiasi cha kuonekana kuwa ni kitu cha kawaida, na kazi ya udanganyifu inayofanywa na Malaika walioasi au mashetani. Na ilikuwa ni kutokana na imani hii ndiyo ilimpelekea mfalme Sauli aende kumuona mwanamke mchawi wa Aendori. Mwanamke huyu mchawi aliaminikiwa kuwa alikuwa na roho ya utambuzi iliyojulikana kama "&! Öwb au obe, kwenye kipindi chake cha kupagawa kwake na mashetani au yanapompagawisha na kuwavuta walengwa kwa njia ya kijichupa au gudulia, jambo lililokuwa linatumiwa na watu wenye kutumia mbinu za kupeleka sauti ya mwangwi au na waomba mizimu wanaotumia mbinu hizi ili kudanganya watu wakijifanya kama ni mizimu inaongea au roho za utambuzi kwa udanganyifu. Fikra potofu za kudhani kwamba roho za wafu zinaweza kuitwa kutoka kuzimuni ziliko inachukuliwa kuaminika zaidi na wengi wanadiriki kuifananisha kimakosa na andiko linaloonyesha kama Samweli aliitwa akaja kutoka kwa wafu. Na pia madai yanayoendelea kutolewa kuwa mtu yule alikuwa ni pepo kuwa ndiye Yule mwanamke aliyemuona; hata hivyo mwanamke Yule alistushwa na kile alichokiona:

1Samweli 28:13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi.


 Neno alilolitumia kuelezea miungu hapa ni elohim, lenye maana ya kiumbe mmoja (au viumbe) na aliyesema na Sauli alikuwa ni elohim aliyemuondolea Sauli ufalme wake na kumtangazia hukumu yake. Kitendo cha kuwasiliana na roho hizi za utambuzi bi ushirikina kwa kuwa kinaivunja Amri ya Kwanza ya Mwenyezi Mungu na ni kitecho cha uasi kwa Mungu (1Samweli 15:23).

 

Akitaja kwa hofu aliyokuwa nayo, alihitimisha kuwa haukuwa uweza au nguvu aliyoijua au aliyokuwa anashindana nayo. Hakuna pepo wala shetani angaliyeweza kumuondoa Sauli kutoka kwenye ufalme wake, na wasingeweza kuchukua madaraka. Madai ya kwamba mtu huyu alikuwa ni malaika waovu au pepo yanaweza kutuama tu kwenye mtazamo wa kwa pale ambapo kiumbe hiki kinafanya kazi yake kinyume na mapenzi ya Mungu, basi kiumbe hicho mara moja kitakuwa kwenye mamlaka ya malaika au elohim waovu. Mfano huu unaonekana kuwa kinyume na maneno aliyoyasema Paulo, ambaye alilijua swali hili kwa mtazamo wa kimafundisho. Elohim mwenye mamlaka hii kwa mara moja lazima awe ni miongoni mwa Malaika waliowatiifu kwa Mungu. Makosa ya kiuelewa kwa jambo hili huenda yanatokana na makosa ya kitafsiri yaliyoko kwenye tafsiri ya Biblia za NKJV, na NIV, na kadhalika kwa kuwa waliozitafsiri hawakujua maana ya neno elohim na walikuwa kwenye imani na mafundisho yanayosema kuwa  Roho inaendelea kuishi baada ya mtu kufa. Mtu huyu kwa namna yeyote ile ni elohim, anawezakuwa ni wa mrengo wa Malaika watiifu au ule wa Malaika waovu na waasi, na kwamwe haikuwa ni roho ya nabii Samweli.

 

Kwenye sababu zilizoainishwa kwenye jarida la Uumbaji (Na. B5) na za hapo juu. Fundisho linalodai kuwa roho haifi na inadumu milele ni la uwongo na linatokana na mafundisho potofu ya teolojia ya Kikaldayo. Ukombozi na kuchaguliwa kwa namna ya kushirikishana Roho ni dhana iliyo kwenye mchakato wa muundo wa kiroho wa kiumbe. Ni kwa nini basi Mungu aunde muundo wa kulinda uhai wenye utata sana kuliko unavyohitajika, ukihusisha na muundo ulio na utata zaidi wa uharibifu? Utata unahitajika kwenye mlolongo wa kiumbe ukihusisha vyote viwili yaani mwanadamu na roho, na uharibifu mkubwa zaidi na mbaya wa mtu wa ulimwengu wa kiroho. Kutokana na maandiko mengine ya biblia, yalielezea kwa kina ukweli wa kwamba, kwenye ufufuo wa wafu roho itaitafanyizwa na kuwa ni mwanadamu wa kimwili ili washughulikiwe pamoja na Shetani ambaye atafanyika kuwa mwanadamu na hakuna namna nyingine bali alikuwa mwenye dhambi. Mwanadamu wa kiroho atafanywa kuwa wa kimwili na atakufa iwapo kama waliasi kwa kutenda dhambi. Waasi watendadhambi wote watakufa na watatupwa kwenye ziwa la moto na kuungua huko kama makapi, sawa na itakavyowapata watu wengine wote waliokataa kutubu. Watakomeshwa kabisa na hawataishi. Fundisho la Roho kuendelea kuishi ni kitu kinachokusudia kuendelea kuwafanya watu waamini kuwa kuna mchakato endelevu wa mzunguko wa maisha usiojali mapenzi mema ya Mungu, neema ya Mungu na uweza wake. Inaonekana kana kwamba inamwambia Mungu kwamba “Mimi naenda kuishi, iwe umependa au hupendi na hakuna utakalonifanya kunizuia mimi kuendelea kuishi.”

 

Mabishano haya yote yamepata upenyo wake kwenye teolojia ya uhuru wa Kimashariki ya uingiliaji. Ilipata mpenyo wake kwenye teolojia ya Dini kuu na uingiaji nchini na watembeleaji. Watu waliiamini imani hii ingawa ilikuwa ni ya uwongo na udanganyifu. Waliiamini kwakuwa walikuwa ni watu waliokuwa na hamu kubwa ya kidini. Fundisho la kibiblia kutoka kwenye Mhubiri 12:7 ni kwamba roho inamrudia Mungu aliyewapa, lakini hii haina maana kuwa ni viumbe vinavyoishi, lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. (Mhubiri 9:5). Hata hivyo, fundisho lililoko linaendelea kubaki hivyo kwenye aya zote za biblia ambayo ni kwamba kuna ufufuo wa miili wa wafu (Ayubu 19:26; Ezekieli 37:1).

 

Kitabu cha Ufunuo kinaonyesha aina mbili za ufufuo wa wafu. Wa kwanza utatokea kipindi cha kurudi kwake Masihi mwanzoni mwa Millennia. Umeelezewa kwenye Ufunuo 20:4 na unahusiana hasa na kufufuliwa kwa wateule, ambao watafanya kazi ya kumsaidia Kristo kwenye utawala wake wa Milenia. Usaidizi huu utakuwa unaandaa tendo la pili la kuweka kiwango ambacho kwacho mapepo watahukumiwa nacho kwenye Kiti Kikubwa Cheupe cha Hukumu, ambayo imeelezwa kwenye Ufunuo 20:5.

 

Ukweli ulioko kuhusu jinsi sisi tutakavyohusika kwenye utawala wa miaka elfu moja ni jambo linaloeleweka sana. Shetani asingeweza kuhukumiwa hadi pale Jesu Kristo alipokuja hapa na kuja kufanya kazi na kuyatoa uhai wake kwa ajili ya watu aliowaokoa. Alipaswa kujaribiwa jangwani. Wakati Kristo alipojaribiwa na kutakiwa amtende dhambi Mungu na amuabudu Shetani, alikataa. Kwa hiyo, Shetani alihukumiwa kwa mujibu wa kile alichokifanya Kristo. Kwa namna hiyo hiyo, ndvyo mapepo wengine waliobakia watahukumiwa kwa jinsi tunavyotenda na kuishi sisi. Mwishoni mwa Milenia, watu wote waliowahi kuweko ulimwenguni kote watafufuliwa na kushughulikiwa kweny kipindi kwenye kipindi chote kitakachowekwa cha hukumu na cha kuadibishwa, ambacho kinaonekana kuwa huenda kitakuwa ni cha urefu wa miaka mia moja, kwa mujibu wa Isaya 65:20. Fundisho hili la roho kuishi milele halina nafasi wala mashiko kwenye mfundisho na imani ya kibiblia. Fundisgo lililopo la Biblia linasema kwamba Mungu anafanya kazi na wanadamu na kuwahukumu kama ilivyoaelezewa kwa kina kwenye jarida la Tatizo la Uovu.

 

Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

 

Dhana na mafundisho ya zama Baada ya Utawanyiko kuhusu Kristo na Ufufuo wa wafu

Pia uangalifu ulikuwepo kwenye kazi ya uandishi ya Uumbaji na mafundisho ya kiteolojia kuhusu nafasi ya usaidizi ya Kristo ya wanazuoni Watetea dini wa kwanza aliokuwako baada ya zama za utawanyiko wa Wayahudi huko Yerusalemu mwaka 70 BK. Ilikuwa ni kipindi hiki ndipo Kanisa lilianza kuingiliwa au kushambuliwa na fundisho hili na kuwapinga moja kwa moja wale waliokuwa wanafundisha elimu hii inayotokana na wakufundi wa elimu ya dini zas ulimwengu kwa kutumia vigezo vyenye mashiko. Pia umakini uliwekwa kwa mwandishi Anders Nygren kwenye kitabu chake cha Upendo wa Agape na wa Eros [Agape and Eros (kilichotafsiriwa na Philip S. Watson, Harper Torchbooks, New York, 1969)], ambacho kwacho mfia dini maarufu aitwaye  Justin Martyr alionyesha tofauti kubwa iliyokuwepo kati ya Mungu na mwonekano wa neno, Logos akisema yafuatayo:

Logos liko njiani kuwa la kimungu lakini sio neno lenye mkazo sana... Ni Baba tu ndiye peke yake hajazaliwa na hakosei wala hawezi kutenda dhambi na ni ndiye Mungu. Yeye ndiye Muumbaji na ni Baba wa vitu vyote (Dial. lvi. 1.).

Hajaja kwetu, emebakia kila mara juu mbinguni na hajajitokeza kamwe kwa mtu yeyote na hajashirikiana wala hana ushirikiano na mtu yeyote. (Dial. v. 4.) 

Kimahusiano nay eye, Kristo ndiye aliye wa cheo cha chini yake, ambaye ni *,bJ,D@H 2,`H [deuteros theos], 'Mungu mwingine mbali na yeye aliyeviumba vitu vyote.' (Dial. lvi. 1.)

 

Nygren anasema kwamba:

Patano hili la usaidizi kwenye elimu ya teolojia kuhusu Ktisto ya Watetea dini bila shaka ilichukuliwa kutoka kwenye mawazo na imani ya Wayunani kuhusu Mungu (ukurasa wa 280).

 

Kama ilivyosemwa kwenye Uumbaji, Nygren amekosea kuhusu jambo hili, kama itakavyokwenda kuonwa kwenye tathmini ya mafundisho ya Agano la Kale na Jipya lilivyoonyeshwa hapo juu. Mfia dini Justin Martyr yoko karibu kidogo kuliko yeye; hata hivyo, tofauti na matendo ya uumbaji vinahusiana Logos, na sehemu yake haieleweki na hawa wanaomhukumu Nygren kina Loofs kuwa sahihi anapowataja hawa Watetea dini kuwa:

Fundisho lao kuhusu neno au Logos sio fundisho ‘kuu’ la teolojia inayomhusu Kristo zaidi ya kuwa ya kawaida tu, bali zaidi sana kuwa ni ya kima cha chini sana zaidi ya tathmini halisi ya Kikristo juu ya Kristo. Sio Mungu aliyejidhihirisha kwa Kristo, bali ni Logos yaani (depotenzierte) au uvuvio wa Mungu, Mungu ambaye ni Mungu aliyejishusha kutoka kwa yeye Mungu aliye juu. (Loofs: Leitfaden zum Studium der Dogmengeschichte, 4 Aufl. 1906, p. 129, ibid.)

 

Lakini hawa wote, kina Nygren na Loofs wamekosea kwenye tathmini yao kuhusu kile kilichokuwa sahihi na halisi kwenye Ukristo. Walikuwa wanajaribu kuyatafsiri upya mafundisho ya Nikea kuhusu Kristo, maarufu kama ya ki Ante-Nicene, ambayo yanafuata kwa ukaribu sana mafundisho ya kibiblia kwenye mtzamo wa kisasa, na ambayo hayahusini kabisa na maandiko matakatifu.

 

Malaika wa Ukombozi alikuwa ni mmoja kati ya washiriki wa  Maraza la Elohim, wakiwa chini ya Elohim mwenyewe, ambaye Eloa (Baba Mungu na Muumbaji). Malaika huyu wa Ukombozi alifanyika kuwa ni Nyota ya Alfajiri akichukua mahala pa Shetani, aliyekuwa hapo zamani kuwa ni Nyota ya Asubuhi. Kwa kupitia matendo yake ya unyenyekevu Kristo alimhukumu Shetani, na ndiye pekeyake kati ya Jeshi la Malaika atayehukumiwa na Biblia (Yohana 16:11). Nukuu kwenye 1Henoko inasema kwamba takriban Mashetani 20 wamekwisha tiwa hatiani (tazama sura ya 3). Hata hivyo, Biblia inaonyesha kuwa ni moja tu, na kwa kweli umuhimu wa mafuatano yenye mashiko ya hukumu ndiyo yangeelekea hili kufanyika kisahihi. 

 

Katika kushughulika na fikara ya Nyota wa Alfajiri huyu mpya na Yule wa kale na kipindi cha mpito au cha ukombozi, inaweza kuwa ni jambo linalochanganya kumuacha mmoja wa hawa malaika waovu na mwenye nguvu kuliko wote (Kerubi Mwenye Kufunika Mbawa) kwenye amri, na kumuweka elohim mwingine duniani aliondolewa kwenye ukuhani na kumchagua na kumfunza kwa kipindi cha ghafla mahala alipokuwa huyu malaika muasi, na mataifa haya yote yaliyo chini ya uangalizi kupitia kwenye uasi. Hata hivyo mchakato wa ukombozi na wa kimafundisho vimepunguzwa kwa namna hii. Umuhimu wa kutendeka hukumu ya haki na isiyo na upendeleo kwa kutoa mfano imeonyeshwa pia. Ni kwa sababu hii ndipo Kristo, kwa ulazima angeweza kutenda dhambi, na ndipo Mungu angeonekana kuwa anao upendeleo kwenye hukumu na kwamba ni kweli kabisa kwa vile Shetani alivyojaribu kumkosea kiumbe ambaye alikuwa ni kama sawa tu na roboti.

 

Hakuna kiasi chochote cha fikra ambacho kingelazimisha wazo la kuishusha kiwango na kuiharibu sayari (ambayo inatokea kila siku siku hizi) mara tu baada ya mchakato umekwisha wekwa tayari kwenye mwenendo. Hakuna dalili za majadiliano na malaika muasi iliyoweza kuonyesha maangamizi yasiyo na maana kama matokeo ya itikadi na imani yao ya kuamini na kuabudu miungu mingi au wepo wa nje ya mapenzi, asili na upendo wa agape wa Mungu. Ni sawa na imani ya mwanadamu inafikia kwenye kiwango cha kutorudi zaidi ya yale wasiyoweza kufikiwa kwayo au kuitwa kwenye toba katika zama hii na kwa hiyo wamekusudiwa kuangamizwa ili waweze kukombolewa katika mazingira mema kwenye Ufufuo wa Pili wa wafu. Na hii ndiyo maana ufufuo huu wa wafu unapaswa utendeke katika mwili.

 

Fumbo lililo kwenye Mpango wa Wokovu na ufufuo ni kitu kingine ninachogonga uelewa wa wwatu wengi kuhusu mwendelezo mzuri kama ilivyo kuwa ni utata kuelewa juu ya Malaika walioasi wakiwa kwenye mwili wa kigoroti. Shetani na Malaika walioasi wanajifanya kuwa kama Malaika wa Nuru (2Wakorintho 11:14), na hakuna tofauti ya kibiblia, hakuna kumbukumbu ya tofauti ya mwonekano wao na uwezo wa kujizuia. Wanadhaniwa kuwa na uwezo wa kuchukua maumbo ya kibinadamu au maumbo mengine mengi na wanaweza kujitokeza kwenye ndoto na kwenye maono. Vita na matokeo yake vinaonekana kuweko mawazoni na ni tabia ya mwanadamu, na ili kulinda matumizi mabaya au upotevu wanarudiwa tena katika mwili kwenye ufufuo wa wafu. Hawana maisha yasiyoweza kufa (tazama jarida la Uumbaji). Nygren aliijua hatua hii kwa usahih sana pale aliposema: 

Kanisa la kale linatofautiana kwa kiasi kikubwa sana na Uhellenism kwenye imani yake kwenye Ufufuo wa wafu. Mapokeo ya Wakristo yanaamini juu ya ‘Ufufuo wa Miili,’ imani ambayo Watetea dini waliyapinga na kuyashabikia mafundisho ya Kihellenisti yanayoamini ‘Roho kuendelea kuishi bila kufa.’ Tabasiri yake ilikuwa macho na kimakusudio, na kwa bila sababu kama hivi ilikuwa ni upinzani wao dhidi ya roho ya Ehellenisti uliohisiwa na kanisa la kwanza. Mafundisho ya Kihellekini na Kiplatoniki ua kuwa roho haifi ilionekana na Watetea dini kuwa sio fundisho la kimungu na ni la kufuru, ambalo zaidi ya yote linatakiwa kushambuliwa na kukomeshwa kabisa.

(kitabu cha Justin, Dial. lxxx. 3-4) kauli mbiu yao kwa jambo hili ingelazimu kuwa ni neno la Tatian: 'Hakuna Kutokufa, O Kiyunani, ni roho iliyo ndani yake yenyewe, bali ni kufa. Ndipo haiwezekani kabisa kutokufa.' (Tatian, Oratio ad Graecos, xiii. 1). Tofauti kati ya Ukristo na usio Ukristo kwa jambo hili ni kubwa sana ya imani ile ya ‘Ufufuo wa miili' ingekuwa ni alama yake. Mtu anayeamini juu ya ‘Roho kutokufa’ anaonyesha kwahiyo kuwa yeye sio Mkristo. Ni kama alivysema Justin kuwa: 'Iwapo kama wewe umeanguka kwa wale wanaoitwa Wakristo... na wanaosema kwamba hakuna ufufuo wa wafu, lakini kwamba roho zao, wanapokufa, zinachukuliwa na kwenda mbinguni, wasichukuliwe kama ni Wakristo (Dial. lxxx. 4) (ibid., pp. 280-281).

 

Mabwana hawa wawili hapo juu wanaweweka kwa wazi sana hatua muhimu na ya kuvutia kati ya Mkristo na falsafa ya uwongo ya Kikristo. Kama ilivyosemwa kwenye jarida la Uumbaji:

… tofauti za msingi za kifalsafa kati ya Ukristo wa Uwongo na mafundisho ya ‘Roho kuto Kufa’, na ile ya Wakristo wa kale na mafundisho yake ya ;Ufufuo wa Miili’, ni kwamba fundisho hili la Roho ni la majigambo la kimwili binafsi na hili la Ufufuo wa Miili ni lina mashiko ya Kiteolojia. Kwa hiyo ni lazima kwamba kutakuwa na mgongano kati ya lengo lililosemwa la mfumo na tafsiri yake ya maelezo ya kibiblia ambayi hayaungi mkono na maridhiano na ni juu ya utaratibu unaodaiwa kuwa ni msingi wake (ukurasa 62).

 

Hapo mwanzoni kabisa ilisemwa kwamba ni masomo ya kina ya kibiblia ndiyo kwayo yangeweza kufunua falsafa na pia mgongano endelevu. Mlinganisho huu ungeweza kufanya tathmini yenye mgongano. Kwa kuendelea kutoka kwenye Uumbaji, tunagundua kwamba fundisho hili la Roho kuendelea kuishi linakutikana kwenye mafundisho ya Plato maarufu kama Plato's Timaeus, ambako kila roho inasemekana kuwa imeunganika na nyota yake moja inayoishi na ambayo imekuwa ni chanzo cha kuwepo kwake humu Duniani na ambayo inarudi wakati wa kufa (41dff.). David Ulansey analielezea wazo hili kwenye kitabu chake cha The Origins of the Mithraic Mysteries (Oxford, 1989, pp. 86-87), ambako anasema yafuatayo:

'Tunalikuta wazo lililoendelezwa kikamilifu kwenye mafundisho yanayojulikana kama Empedotimus ya mwanafunzi wa Plato aitwaye Heraclides Ponticus, ambayo kwayo Nia ya Maziwa inaonekana kuwa ndiye njia ambayo roho inapitia kwenye chini kwenye uhai mpya. (Kwenye kitabu cha Heraclides Ponticus, tunawaona Burkert, Lore na Science, ukurasa wa. 366; na Gottschalk, Heraclides wa Pontus, ukurasa wa 98)

Wazo hili la roho kutokufa lilifanyika kuwa lenye kutetewa sana kipindi hiki cha Wah ellenistiki hadi kipindi cha kuhukumiwa kwa Franz Cumont, na Warumi kilipokuja kuwa ni taswira maarufu ya maisha baada ya kufa.

Kwa mujibu wa Cumont, anasema 'ingawaje kumbukumbu na mwonekano wa kuishi kwa imani ya kwanza ni kwenye maisha ya wafu makaburini na na kushukia taratibu kwenye shimo kuzimuni ingeweza kuaminiwa, bali fundisho lingaliloweza kuaminiwa tangia hapo na kuendelea lilikuwa ni la kidini la roho kuendelea kuishi’ (kitabu cha Franz Cumont, cha Chimbuko la Dini Mbalimbali kwenye Upagani wa Kirumi wa huko New York: Dover, 1956, ukurasa wa 39). Ni sawa tu kama kwenye mkazo wa maandiko ya Gnostiki tunaona kwamba safari ya roho ingawaje mambo ya mbinguni yameruhusu au kuachilia na kuonyesha kuwa ni hatari na kwamba nguvu za kuzimuni zinahitaji kuzimwa kwenye kila hatua' (tazama mfano kitabu cha Liturujia ya Mithras Liturgy, cha huko Meyer, maarufu kama Dini za Kisiri za Kale, kurasa za 211-21).

Mvutiwo wetu kwa jambo hili ni kwamba dhana hii ya roho kuendelea kuishi imeelezwa na kutajwa na mababa wa kanisa la kwanza aitwaye Origen (akimnukuu mwandishi wa riwaya za kipagani Celsus) ambayo yalikuwa ni mafundisho ya dini ya kipagani ya Mithra. Kwa mujibu wa Celsus, kwenye Dini hii ya Kisiri ya Mithra, kuna ishara ya vitu viwili mbinguni, ishara moja wapo ni ya nyota zilizowekwa sawia na nyingine ni ile iliyoonekana kwenye sayari nay a kiwango cha roho inayoonekana kule. Ishara ni kwamba kuna ngazi na malango saba na juu yake kuna malango mengine manane. (Origen, Contra Celsum, ukurasa 334 (6.22)). Kwa kuongezea hapo, mtazamo wa Uplato Mamboleo unaonyesha kuwa imani ya Umithraism ni fundisho lenye utata kusema kuwa rohi unadmmu pasipo kufa ikienda na kutoka kuzimuni na kuifanya iweze kumuingia kiumbe mwingine anayezaliwa.

 

Jinsi ilivyosemwa huko nyuma:

… hii inachukua mahala pa udanganyifu aliofanyiwa Adamu kwenye kitabu cha Mwanzo akiambiwa kuwa ‘Hakika hutakufa’ imani inayotokana na Dini za kipagani za Kisiri za Wababelonia na jinsi walivyozifanya upya tena kutoka kwenye dini za Waariyani wa Kihindu nay a Wayunani nay a watu wa Mashariki.

Ni mfumo unaotokana na falsafa ya kujiona au kujifikiria wenyewe ambayo inazidisha imani juu ya miungu mingi na ambayo inaongeza kwa kiasi kikubwa tofauti ya tabaka kutoka kwenye mfumo wa kitabaka wakihusisha imani ya Mungu. Mpangilio huu wa kitabaka unasababisha madhara makubwa kwenye mfumo mzima. Mwambatano wake unazidi na kwa kweli mtengano na mtafaruku. Kimantiki, mchakato huu unangukia kwenye Majivuno ya Kisaikolojia na Uherodi, ambavvyo vinaendana kws pamoja kwa kweli.

Mfumo wowote unaotuama kwenye mtazamo wa ubinafsi na kwenyendo na unaofuatilia kiwango cha kadiri cha kila mtu hatimaye utashindwa na uwekezaji wa kadiri. Dhana hii ya miungu mingi unaweza kuwa ni chanzo cha aina ya mtazamo wa kimungu unaoweza kuonekana kukirudiwa mara kwa mara kwa kuwa uanzishajiwa mafundisho uko kwenye kiwango kikubwa. Mafundisho haya kimsingi yalipinga ukweli wa Mungu kuwa kiini na mwaamini Mungu yeyote analazimika kuwapinga. Kwa usemi rahisi ni kwamba huwezi kuamini katika imani ya roho kusihi milele na halafu ukawa ni Muamini Mungu mzuri (imenukuliwa kwenye jarida la Uumbaji (Na.B5), ukurasa 63).

 

Dhana hii ilihusika na kwenye umri na hukumu iliyoongelewa na kufafanuliwa kwenye jarida la Matatizo ya Uovu. Kipengele kilichonukuliwa hapa kinaonyesha asili ya mafundisho yaliyoko hadi kwenye zama ya Watetea dini wa kwanza.

 

Madhara ya fundisho hili la Roho kutokufa yalikuwa makubwa sana hasa kwenye kipindi cha karne ya tano, ambapo Augustine alisema kwamba miili ya kiroho sio roho, bali ni miili tu ambayo:

… sio kwa ajili ya kupungukiwa na virutubisho vya asilia, bsli ni kwa bahati ya kiwango na ubora wake  [utakuwa] unaishi mbinguni wenyewe (Mji wa Mungu, xiii.23).

 

Augustine aliandika kwenye ukurasa wa (xxii.29) kuwa:

Ndipo Mungu [baada ya ufufuo wa wafu] ataonekana na yale macho kwenye uhalisia wa milki yao (kwenye mazingira haya ya kufanyika kwao upya) ya kitu chenye kiwango kinachofahamika, uweza wa kupambanua mambo yaliyo sio ya asili ya visivyo na uhai. Tena, ni vigumu kama sio haiwezekani kabisa, kuliunga mkono wazo hili kwa ushahidi wowote wa kifungu cha Maandiko Matakatifu.

 

Mtu anaweza kuuliza kuwa ni kwa namna gani mchakato huu wa mabadiliko wa uelewa wenye msingi wa muundo wa mambo ya maisha baada ya kifo unavyweza kutokea. Umuhimu wa uelewa pia ulikuwa na maana kuu sana kwenye uelewa wa mambo yenye matukio muhimu ya Agano Jipya. ght well ask how this process of change in mfuatano wa matukio unaitwa kuwa Matukio ya Kristo au kerygma na wanateolojia. Mtazamo kuhusu roho na uhusiano wake na Uungu unaathiri uelewa wa dhana ya kuzaliwa upya kwa Yesu Kristo. Kuelewa kikamilifu kwa mfumo wa mwili, ni jambo la muhimu la kwanza ili kufanyiza mafundisana kiusahihi kuhusu kuja dunianai na kuzaliwa ho ya kibiblia kwa jambo hili.

 

Kuja duniani na kuzaliwa kwa Yesu, jinsi neno au  Logosalifanyika Mwanadamu

 Kutokana na Yohana 4:24, tunaona kwamba Mungu ni Roho. Tafsiri ya Yohana 4:24 inasema kuwa Mungu ni Roho kwenye Biblia zote, yaani NKJV, NIV, NASB, NEB, JB, TEV, RSV, Moffatt, Zwingli. Andiko hili limetafsiriwa Mungu ni roho kwenye biblia za KJV, RV, Noli, J.F.B. kitabu cha Fafanuzi cha Commentary, Vincent's Word Studies in the New Testament. Biblia ya Amplified Bible inalitafsiri andiko hili kuwa Mungu ni roho (inaonyesha ni Kiumbe aliye wa Kiroho). Nukuu ya Origen kwenye Yohana 4:24 imetafsiri kuwa Mungu ni roho na kwenye baraza la Nikea lijulikanalo kama Ante-Nicene Fathers kwa Kumpinga Celsus, Bk. 2, Sura ya 71 (ANF, Vol. 4, uk. 460); Bk. 6, Sura 70 (ANF, Vol. 4, uk. 605); De Principis Bk. 1, Sura 1 (ANF, Vol. 4, uk. 242). Tafsiri ya ANF inalitafsiri andiko hili pia kama alivyolitafsiri Tatian Akifanya rejea kwenye lugha ya Kiyunani (ANF, Vol. 2, uk. 66) na pia kwa Tertullian kwenye kitabu chake cha Kumpinga Praxeas, Sura 7 (ANF, Vol. 3, uk. 602); na Dhidi ya Hermogenes Sura 32 (ANF, Vol. 3, uk. 495). Kwa hiyo Tertullian alielewa lugha ya Kiyunani kwa namna hii pia. Kulinganisha na uandishi wa Kiyunani kuhusu “Mungu” mwingine kwenye maandiko haya yanafanya kwa mfano, 1Yohana 4:8, 1Yohana 4:16, 1Yohana 1:5. Nia ya kumfanya Mungu kuwa ni Roha pekee inatokana na muundo wa imani ya Waplatoniki kukiwemo na fikara ya Wademiurge, na Wastoiki fikara ya Kidunia ya Wafilo inayochanganika na ya Kiyahudi ya Shekina na ya Memra iliyotokana na wazo lake la Logos. Imani ya Kibiblia ina idadi ya matamko ya msingi yanayobeba dodoso au dalili ya utofauti. Kwa mfano, Kristo alikuwa na wanamna yake peke yake ambaye alikuwa kwenye mikono ya Mungu alipokuwa anakufa.

 

Luka. 23:46  mikononi mwako naiweka roho yangu.

 

Roho hii ni tofauti na Roho Mtakatifu, ambaye ni Roho wa Kweli na anayetokana na Baba (Yohana 5:26), lakini inaonekana kuwa na uhusiano wa kimshikamano naye na kwa kweli inategemeana nayo. Muundo wa mchakato huu unaonekana kutokana na kufuata kikamilifu na mlolongo uliowekwa kwa wanadamu na ulioonyeshwa hapo juu– ambao kwamba kila mwenye mwili atakufa. Kristo alikufa pia (Yohana 3:16; Warumi 5:8; 2Wakorintho 5:14-15; 1Petro 2:24). Kristo alikubali kuutoa uhai wake kama ilivyoeleza hapo juu.  

Yohana 15:13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

 

Uhai wa Kristo ulitolewa kama sadaka ya kuondoa makosa ya wengi (Mathayo 20:28; Marko 10:45). 1Petro 3:18 inasema kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi na kondoo (tazama Yohana 10:11). Paulo anasema kwamba Kristo alikufa na kufufuka na kwamba ufufuko na kupaa mbinguni kwa Kristo ni mambo muhimu ya msingi kwa Imani yetu, kama ulivyo ufufuo wa wote wenye mwili.

 

1Wakorintho 15:12-14 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? 13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; 14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.

 

Ufufuo wa wafu Wote

Mashiko yaliyo kwenye usemi huu wa Mtume Paulo ni kwamba namna ya kifo na ufufuko wa Kristo ni sawa tu na ilivyo na itakavyokuwa kwa wateule, aliowafia (1Yohana 3:16). Ufufuo wa wafu, umeandikwa kwenye Ufunuo 20:4 nk, kisha inafuatiwa na watu wote kwa ujumla wao. Kristo alikuwa na uzima ndani yake ambao aliruzukiwa na Baba (Yohana 5:26). alisemekana kuwa ni Adamu wa mwisho. Mtume Paulo anajibu maswali yaliyoko kuhusu ufufuo wa wafu akisema: 

1Wakorintho 15:35-49 Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani? 36 Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa; 37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo; 38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake. 39 Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki 40 Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. 41 Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota. 42 Kadhalika na kiyama ya watu. hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; 43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; 44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko. 45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. 46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. 47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. 48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. 49 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni. 

Paulo anasema kwamba mwili na damu haviwezi kuurithi Ufalme wa Mungu, wala uharibifu kuurithi kutokuharibika (aya ya 50). Hali halisi inajulikana kuitangulia kutoka kwenye hali ya mwili hadi kwenye kuzaliwa upya kunakofanyika kwa njia ya ubatizo baada ya kutubu, akiwa anajua na kutubu akiwa mtu mzima anapoitwa na Mungu. Kwa hiyo basi, ubatizo unaweza tu kufanyika baada ya toba na mtumzima. Wakati maandiko yaliyo kwenye Marko 16 tangia aya za 9-20 zinakubaliana kwa ujumla kuwa ama imeandikwa kama nyongeza kutoka kwenye maandiko asilia au marekebisho ya aya (na ambayo inaonekana ingeweza kuondolewa kwenye kipindi cha zamani), andiko lililo kwenye aya ya 16 inaonyesha kuwa dhana ya kufanya toba kwa njia ya imani ilikuwa ni ya muhimu ili kuupata wokovu Asiyeamini atahukumiwa inaonyesha kuwa toba na imani vilikuwa ni vitu muhimu ili kustahili kubatizwa. Na ndiyo maana watoto wameondolewa haki hiyo kwa kuwa hawawezi kufikia kwenye kiwango cha kujua mabaya na kuweza kufanya toba. Kwa hiyo, ubatizo wa watoto wadogo ni kitendo kilicho kinyume kabisa na hali yenye maana inayohitajika kufanyiwa ubatizo na ilikuja julikana kwenye zama za karne chache tu zilizopita.

Kuzaliwa Tena Kwa Njia ya Ubatizo

Maisha ya kiroho ya mwanadamu na muungo au imani juu ya kuzaliwa mara ya pili na kuijua gennao vimeelezwa vizuri sana kwenye jarida la Uuumbaji. Itikadi hii  ya kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya ubatizo katika toba kumpokea Roho Mtakatifu ni muhimu ili mtu aweze kuuingia Ufalme wa Mungu (Yohana 3:3-5). Kutokana na Warumi 8:23, tunda la kwanza la Roho linatolewa na mtu hulipokea kwenye ubatizo, lakini tendo la kufanywa Wana linatokea kwa tendo la ukombozi wa mwili. Tendo la kuzaliwa mara ya pili linafanyika wakati wa ubatizo kwa ishara ya kifo na kufufuliwa ambayo uzamishaji wa mwili wote hufanyika. Kitendo hiki cha kumzamisha mtu mwili wote majini kiliaminika kuwa ni tendo endelevu na cha lazima sio tu kwa Kanisa bali pia ni ishara ya ubatizo wa Yohana aliyoitumia alipokuwa anawabatiza watu kwenye Mto Yordani. Kristo alienda kwa kupitia mchakato huu na Roho Mtakatifu alimshukia kutoka kwa Baba kwa umbo la njiwa (Mathayo 3:16; Marko 1:10; Luka 3:22; Yohana 1:32). Kila Injili inathibitisha mchakato huu. Kwa kweli, ukweli unajitokeza na kuonekana ili kwamba mchakato wenyewe umethibitika kuwa ni muhimu katika Kristo ukiwa ni mfano wa kwanza au tunda la kwanza. Kuna watu wengine wanaoonekana kwenye Agano la Kale ambao walimpokea Roho Mtakatifu pasipo kufuata utaratibu wa kawaida unaojulikana na kuzoeleka wa kuwekewa mikono uliozoeleka. na mtu. Daudi aliomba kwamba Roho Mtakatifu asiondolewe kutoka kwake (Zaburi 51:11). Daudi alitiwa mafuta na Samweli Hata hivyo, wengine hawakutiwa mafuta kwa wazi au kikamilifu.

 

Biblia yenyewe inatuambia kwamba ufufuo wa wafu na uelewa wa muundo wa kiroho vilikuwa kwenye mabishano ndani ya vikundi vya kidini au madhehebu ya Kiyahudi. Masadukayo walifundisha kwamba hakutakuwepo na ufufuo wa wafu, wala hakuna malaika, wala hakuna roho (Matendo 23:8). Mafarisayo walikubali na kuamini mambo haya yote mawili (Matendo 23:8), na Kristo aliwakubali mafarisayo na kusema kuwa ni wao ndio walioketi kwenye kiti cha Musa na kwamba wanastahili kuheshimiwa na watu kuwatii (Mathayo 23:2).

 

Inaonekana kuwa Mafarisayo walikumbwa na mtindo wa kupenda mali na utajiri jambo ambalo linapaswa kuepukwa suala hili la kujilimbikizia mali na utajiri. Mtume Paulo aliendeleza mtazamo usioendana na waumini kujikita kwenye mahangaiko ya kutafuta mali Kristo atakapokuja. Ni jambo lililo dhahiri kwa kila msomaji wa Biblia kwamba kipindi cha takriban miaka elfu mbili kimeshuhudia wateule wengi wakifa. Mchakato huu, kwa ajili ya dhana na fundisho la kumpokea Roho Mtakatifu kwenye ubatizo, jambo hili la kufa lilijulikana kama kulala mautini au usingizini. Mtu wa kale alikufa kwenye ubatizo, na mtu mmoja mwingine aliyezaliwa upya au aliyezaliwa kwa roho. Mtume Paulo anasema:

1Wakorintho 15:51-53 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.

 

Mchakato unaoongelewa hapa ni Ufufuo wa wafu wa Kwanza ulioelezwa kwenye Ufunuo 20:4. Ufufuo wa Pili ni ule utakaofanyika baada ya miaka elfu wa hii dunia kuwa chini ya utawala wa Kristo. Huu ni ufufuo wa jumla wa wote waliokufa huko nyuma ambao unatajwa kwenye Ufunuo 20:11-15. Kwenye 1Wathesalonike 4:15, Paulo anasema kwamba hatuta ‘zuia’ au kuwatangulia waliolala. Kristo atakuja na wafu waliokufa katika Kristo – wale waliobatizwa na kisha wakafa – watafufuliwa kwanza na kisha watakuwa pamoja na wale walio hai, watabadilishwa na kuwa wakiroho kabisa. Jinsi mchakato huu utakavyokuwa imefafanuliwa kwenye jarida la Tatizo la Uovu. Hawa watakaobadilishwa na kuwa kwenye hali ya kiroho ndipo watakutanika pamoja na Kristo huko Yerusalemu ambako kutoka hapo ulimwengu wote utatawaliwa kutoka hapo katika utawala wa Kristo kwa kipindi cha millennia au miaka elfu. Zekaria 14 inaelezea mambo yatakvyokuwa kipindi hiki. Mchakato wa kuanzishwa kwake umeainishwa kwenye Zekaria 14:1-15. Ulazima wa kwenda kuadhimisha huko Yerusalemu na kuishika Sikukuu ya Vibanda ili mvua inyeshe kwa majira yake sahihi umetajwa. Kwa hiyo, kutokana na Maandiko haya Matakatifu, kuwepo kwa makundi mawili ya watu yatakayojitokeza hapa duniani kipindi hiki cha miaka elfu baada ya kurudi kwa Kristo. Hawa ni wateule wa kiroho watakaokuwa chini ya Kristo, na ni watu waliosalia kutokana na Vita vya Siku za Mwisho ambao watapewa ulinzi kwa kuiweka vizuri tena sayari hii. Wateule watakuwa ndyo walinzi wa mambo yatakavyokuwa na watu watakaobakia (Isaya 30:21).

 

Kama kundi, Wasabato wa Kiadventista wana mkakati wa makusudi kabisa wa kutoweza au kupuuzia kuamini juu ya utawala huu wa milania As a group, Seventh-Day Adventists have a serious inability to comprehend the millennial structure (tazama sehemu ya Nyongeza). Kwa mujibu wa maandiko ya Ellen G. White, wanatafsiri na kukifanya kuwa ni cha kiroho tu kipindi hiki cha Milenia na kwa hiyo hawawezi kuhesabu kukamilifu kwa manabii. Waamini unyakuo wengine wana tatizo kama hilihili pia.

 

Mchakato ambao Biblia unautumia katika kuwashughulikia wale watakaobaki Kristo ajapo ni kwamba ni kubadilishwa miili. Wafu watafufuliwa na kubalidishwa miili yao pamoja na wale watakaobakia hai bado. Ni sawa na hilo, wale watakaokuwa mwishoni mwa kipindi hiki cha utawala wa milenia wa Kristo na ambao hawakuasi, na wale walio kwenye Ufufuo wa Pili waliofufuliwa watapelekwa hukumuni kwa kipindi kinachooneka kuwa kuenda kitakuwa cha miaka mia moja (kutoka kwenye Isaya 65:20). Mwishoni mwa miaka hii mia moja, waongofu waliookoka watabadilishwa miili yao. Watenda dhambi wasiotubu wataruhusiwa kufa na watatupwa kwenye Jehenamu ya moto; au kwa maneno mengine, miili yao itaunguzwa. Sababu inayofanya kuwa ni muhimu kuuelezea mchakato huu hapa ni kwamba mchakato na mlolongo wa uvunaji matunda ni muhimu katika kuelewa uji wa Kristo wa kuzaliwa kwake. Kufa na kufufuka kwake Kristo.

 

Krristo alikuwa ni limbuko la wote wenye mwili. Alikuwa ni mfano wa kile kitakachotokea kwa wateule, na kisha kwa wanadamu kwa ujumla. Kristo ndiye pekee aliyezaliwa na Mungu na Mwana wa Mungu (monogenes theos na uion; Yohana 1:18; 3:16; 1Yohana 4:9; pia tazama Luka 7:12, 8:42, 9:38; Waebrania 11:17 kwa kulinganisha au kuainisha). Alikuwa ni mzaliwa wa pekee (prototokos) wa viumbe wote (Wakolosai 1:15), kwa hiyo, mwanzo wa uumbaji wa Mungu (Ufunuo 3:14, sio kama ilivyoandikwa kwenye tafsiri ya NIV; tazama hapo juu). Fundisho la kibiblia ni kwamba Kristo alikuwa ni Mwana wa Mungu na alikuwa ni tofauti na Mungu, ambaye ametajwa kuwa ni Mungu Baba. Wakati Kristo alipokufa alidumu na kuendelea kuwa na mwili uliokufa kwa siku tatu, bali hakuruhusiwa auone uharibifu au kuoza (Zaburi 16:10). Hata hivyo, roho yake ilimrudia Mungu wake, ambaye ni Baba. Na Baba akamfufua kutoka kwa wafu kwa mamlaka yake au amri yake, ambayo alimpa Kristo kabla ya kufa kwake (Yohana 10:18), na ambavyo ndivyo alivyoamua hata kabla ya kuwekwa kwa msingi wa dunia (Ufunuo 13:8). Umuhimu wa sadaka hii na kwa hiyo pia wa ufufuo wake vimekusudiwa kwa kuutoa uhai wake au kwa kuweka msingi (kataboles) wa dunia (kosmou).

 

Dhana na Fikra Potofu ya Kisasa

Kinachojulikana na kisicho na shaka ni kwamba Kristo alikuwa ni mtumishi mtiifu. Kutokana ilivyo hapo juu, kifo na kufufuka kwake vilikuwa ni lazima kwenye Imani yetu. Mchakato wote huu unafanya taswira ya kile kinachojulikana kuwapata wateule, na hatimaye kwa watu wote kwa ujumla. Ukristo ulioko leo umetuama kwenye idadi ya mambo na mafundisho ya uwongo, yaliyoelezwa hapo chini. Kwa ufupi, unajaribu kudai mambo yafuatayo:

 

1: Mungu na Masihi (na Roho Mtakatifu) ni wamoja wanaotokana na kila mmoja wao kuwa na nafsi yake na wanauweza sawa na haiba sawa na mawazo na ni vigumu sana kuelezea Utu na muungano wao. Pia kwamba huyu elohim anagawanyika kwenye nafsi mbili na Roho, wakiacha kutilia maanani tofauti iliyopo kati ya Eloa na Baraza lake. Kutokana na uchambuzi uliofanyika hapo juu, huu ni uwongo.

 

2: Kwamba mwonekano wake na kazi za kipindi cha kabla ya kuzaliwa kwake katika mwili Kristo hakuwa malaika wa YHVH.

 

3: Kwamba Kristo alikuwa ni Mwana pekee wa Mungu kalba ya uumbaji wa dunia (tazama Ayubu 1:6; 2:1; 38:7). Madai haya ni ya uwongo. Ni lazima kuwe kuna mchakato mahsusi wa kuja kwake duniani kwa kuzaliwa kimwili uliofanywa kwa ajili ya Kristo akiwa tofauti nae, na ni tofauti kutoka na Mungu. Ukristo wa leo haulielezi jambo hili.

 

Kristo na Shetani walikuwa sio Nyota mbili za Asubuhi peke yao (tazama Ayubu 38:7; Isaya 14:12; Ufunuo 2:28; 22:16). Madai na uhakika wa kuwepo Nyota wengi ws Asubuhi na Baraza la Elohim yanaonyesha uenezaji na uimarishaji wa mamlaka kwenye mifumo mingi. Kila mmoja wa watu hawa anauhusiano na utambulisho na Baba ambao hauwezi kubaguliwa na ule uhusiano wa Kristo. Ukweli wa kuwa Kristo ni mshiriki kwa watu hawa unamaanisha kuwa hawezi kuwa Mungu wao. Kwa hiyo, uhusiano wake na Baba ni way eye kuwa mdogo. Kwa hiyo, ujio wake na kuzaliwa katika mwili hapa duniani hauwezi kukamilika kwa namna ya madai yao ya kumfanya kuwa ni mshiriki sawa kwenye cheo cha Uungu. Kwa hiyo, andiko linadai kwa kusema hivi:

 

4: Kwamba Kristo ni Mungu kwa namna hii hii kwamba Mungu kama Mungu ni ya uwongo.

 

Yeye ni mdogo kwa Mungu na ni mtumishi tu (Waebrania 1:9), aliyetumwa na Bwana wa Majeshi (Zekaria 2:10-11). Kwa hiyo hawezi kuchukuliwa au kuwekwa uzani sawa wa kuabudiwa na Mungu au kufanyiwa dua, kinyume kabisa na Kutoka 34:14, Mathayo 4:10 nk.

 

Upuuzi mwingine unaofuatia ulioendelezwa kutoka kwenye madai ya kuwepo kwa Kristo na kumfanya kuwa tofauti, na zaidi sana kuliko kwenye hali ya kuzaliwa kwake hapa duniani ni kwamba angeweza kujiomba yeye mwenyewe kama Mungu. Fikra ya namna hiyo inakataa kabisa tofauti iliyopo kati ya Baba na Mwana na ukamilifu wa mpango mkamilifu wa ufufuo. Haya ni mafundisho ya Mpingakristo (1Yohana 2:22; 4:3; 2Yohana 7). Mabishano haya yameendelea hadi kwenye fikra ya kudhania kwamba kwamba Kristo na Mungu walikuwa na matakwa mamoja na kwamba Kristo hakuwa na mapenzi tofauti ambayo kwayo alimshirikisha Mungu kwa utii aliokuwa nao. Hili limekanushwa kwenye sura ya 2. Wazi hili ndipo liliendelezwa kwa kusema kuwa:

 

5: Asili ya kimbinguni inakubali kwamba hakuna faida wala hasara kwa Kristo (fikra hii ni tofauti kutoka ilivyo hapo juu).

 

Dhana iliyoko kwenye jambo hili ni kwamba:

6: Kwamba Roho Mtakatifu ametolewa kwa kipimo (kinyume na ilivyoandikwa kwenye Yohana 3:34, RSV; Warumi 12:6); na kwamba

 

7: Kristo asingeweza kutenda dhambi (kutoka kwenye sababu au madai ya uwongo kuhusu uasilia wa kimbinguni inatokubali kuwa hakuna faida wala hakuna hasara zaidi tu ya uweza wa Mungu wa kuelewa kila kitu, ambaye alijua tangu mwanzo kuwa Kristo asingeweza kutenda dhambi); tazama hapo juu.

 

Maendeleo ya mabishano haya yanaendelea kwenye madai haya:

8: Kwamba Kristo alikuwa na cheo sawa na Mungu kwa namna ambayo kwamba alikuwa sawa na mwenye umilele sawa na Mungu, madai yaliyo kinyume kabisa na andiko la Wafilipi 2:6 na 1Timotheo 6:16, yanayoonyesha kwamba Mungu huishi milele bila kufa. Umilele wa Kristo au uzima wa aioonion (1Yohana 1:2), na kwamba Viumbe wote wametokana na yeye ambaye ni Mungu wa Kweli (Yohana 5:20).

 

Wote wawili, yaani Kristo na malaika wateule wana asili moja tu (Waebrania 2:11, RSV) wakiwa na sifa ya kuishi na kutokufa kutokana na utiifu uliotakiwa kwa Baba (Yohana 5:19-30), alioyetuumba sisi sote (Malaki 2:10-15). Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.


(Yohana 5:26), na sisi ni warithi pamoja naye, tuliochaguliwa kuwa na uzima ndani yetu kwa mamlaka ya Mungu. Inakuwa lazima kwa Wakrito wa leo kufanya madai ya uwongo kuwa:

 

9: Kwamba malaika wateule sio Wana wa Mungu kwa namna iliyoko ya sawa na Kristo alivyo kuwa ni Mwana wa Mungu na kwamba sio warithi pamoja naye, kinyume na inavyosema Warumi 8:17; Wagalatia 3:29; Tito 3:7; Waebrania 1:14; 6:17; 11:9; Yakobo 2:5; 1Petro 3:7.

 

Katika kuiunga mkono jambo hili, matumizi yake yamekuwa ya kimakosa:

10: Kwamba Mungu Mtukufu mwenyewe alishuka hapa chini katika mwili na kuishi pamoja na wanadamu (wakiyachukulia maandiko yasiyo rasmi na yasiyoandikwa na mwandishi asilia yaliyo kwenye 1Timotheo 3:16 kwenye fasiri ya Codex A, iliyofanyizwa kwenye fasiri ya KJV na iliyoingizwa na kutiliwa mkazo kwenye mhutasari wa biblia ya NIV) kinyume na Yohana 1:18 (na Yohana 1:14 ambapo ilikuwa ni logos, au memra, aliyefanyika kuwa mwili) na maandiko mengine kadhaa yanayomuweka mbali Kristo na Mungu wa Pekee wa Kweli (Eloa au Theon, ambaye ni Mungu Baba), Mungu wa Yesu Kristo (Yohana 17:3, 20:17; 1Wakorintho 8:6; 2Wakorintho 1:3), anayesimama kwenye Jina Lake (Mika 5:5).

 

Maelezo yaliyokosewa yaliyoko hapo juu ya Ukristo mambo leo yanaathiri uelewa kuhusu dhana ya kuja kwa mwokozi na kuzaliwa kimwili hapa duniani. Hii inatokana ukweli kwamba fikra ya jinsi Mungu alivyo mmoja inaeleweka vibaya na wamini Utatu. Shema (Kumbukumbu la Torati 6:4) imetathminiwa baadae. Huyu aliyetajwa kwenye Kumbukumbu la Torati 6:5 anajulikana kama Mungu Aliye Juu Sana, Mungu aliyemtia mafuta Kristo kama Elohi wa Israeli, kwenye Zaburi 45:6-7. Umoja wa Mungu ni muhimu sana kwa imani juu ya Mungu mmoja au Umonotheism, na ni sharti endelevu iliyo kwenye umoja ulio chini ya mapenzi mhimilifu kwa makubaliano na mwingiliano wa kiroho kupitia Roho na Uweza wa Mungu (1Wakorintho 2:4-14) ambayo kupitia Kristo, ni kuelekea kwa Mungu (2Wakorintho 3:3-4). Imani ya Utatu hukataa umoja muhimu kwenye imani juu ya Mungu mmoja au Umonotheism na kwa kweli ni waamini miungu mingi. Inadaiwa kuwa ilitokea kwa sababu watawala hawakuelewa, kuwa havijavuviwa na roho (1Korintho 2:8,14). Kristo aliweza kujifanya kuwa Mungu, na alimudu kufikia kima cha utimilifu wa Kiuungu kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

 

Fundisho la Kanisa la Kwanza 

Namna ya hili tendo la kuja duniani na kuzaliwa katika mwili imebakia kuwa ni fumbo kubwa. Hata hivyo, hakuna shaka kwamba hatushughuliki na sehemu tu ya matendo kwa Kiumbe ambaye kwa namna fulani ameacha asili yake Mbinguni kana kwamba angekuwa na sayari mbili tofauti za kuishi kwa muda. Dhana na fikra kama hii haina mashiko ya kibiblia kabisa. Tukiwa tumewekwa kwenye misingi na imani ya kibiblia kwenye kipindi cha Kristo, tunaweza kujionea jinsi fundisho hili lilikuwepo kindi cha karne ya kwanza nay a pili. Kutokana na maandiko tuliyonayo ya Justin Martyr na Irenaeus, tunajua kwamba uelewa umeongezeka kwenye Kanisa la kwanza. Justin Martyr anasema kuwa Mungu alifundisha kitu hichohicho kwa manabii kama Musa nah ii ilikuja jitokeza hapo juu (tazama kitabu cha Dial. na Trypho, Sura ya XXVII, ANF, Vol. I, ukurasa 207). Justin alifundisha kwamba Mungu alianzisha, kama huko mwanzoni, nguvu ya namna fulani, kutokana yeye mwenyewe ambayo inaitwa Roho Mtakatifu” sasa Utukufu wa Bwana, sasa ni Mwana, na tena ni Hekima, tena Malaika, kisha Mungu (theos), na kisha Bwana na Logos. Justin anamuonyesha yeye kuwa kama Kapteni wa Jeshi la Bwana aliyemtokea Yoshua (ibid., LXI). Eneo hili lilichukuliwa ili kuonyesha kilichoandikwa kwenye mithali 8:21. Ambapo Hekima ilitajwa kuwa ni Masihi, aliyefanywa na Mungu. Mapenzi ya Mungu hatimaye yatimilizwa na Masihi. Justin (ibid., LXII) anaendelea kusema kwamba, kwenye uumbaji Mungu alifunikwa na viumbe wengi waliokuwa tofauti nay eye mwenyewe. Na kwa hiyo Musa aliaminika kutangaza kwamba uumbaji ulihusika na yapata viumbe wawili ambao wasifa wao ulikuwa ni tofauti na wasiofanana. Waditheists wanajaribu kutenganisha watu hawa na kuwa wawili, na waamini Utatu wanaigawa hii kwenye viumbe vitatu vilivyo tufauti hypostases. Ikitolewa na Watrinitarian wenyewe, mabishano kati ya Wabinitariani na Watrinitariani huenda yakawa hayana maana. Hawa elohimu kwa kweli walikuwa ni wengi, kutoka kwenye maandiko mengine yaliyotajwa hapo juu, hususan Zaburi 45:6-7, walioitwa kuwa ni washika wa Kristo.

 

Irenaeus (mwaka 125-203 BK) aliandika juu ya swala hili la wasifa enezi wa elohim (au theoi kwa Kiyunani) kwa wanadamu. Irenaeus ni wa muhimu kwa kuwa alikuwa mwanafunzi wa Polycarp, mwanafunzi wa Yohana (tazama kitabu cha Butler, cha Maisha ya Watakatifu (Lives of the Saints), Burns & Oates, U.K., 1991, ukurasa 56). Kwa hiyo tunaweza kuwa wasafi kwa namna fulani tukisema kwamba uelewa wa Irenaeus (aliyeuawa kwa ajili ya kughushi) aliweka wastani wa Kanisa la kwanza. Kwa kweli aliwasaidia Waquartodecimans na kuwatete kuhusiana na utata uliojitokeza kuhusu maadhimisho ya Pasaka (Butler, ibid., ukurasa 197), ingawaje alitengwa mbali ya Asia Ndogo, akapelekwa huko Lyon. Kwenye kitabu chake kiitwacho Dhidi ya Uzushi (Against Heresies) alifundisha ukweli kwamba wateule au malaika wangeishi kama elohim. Irenaeus alishikilia kuamini kwamba malaika na muumbaji wa ulimwengu walikuwa sio viumbe wasiomjua Mungu mwenyezi wakionekana kuwa walikuwa ni viumbe wake pia na waliumbwa na yeye (Bk. II, Ch. VI, ANF, ukurasa 365). Irenaeus hakumtaja muumbaji wa ulimwengu, ambaye alikuwa ni Masihi, kama Mungu aliye Juu Sana au Mwenyezi (Sura ya VI, ibid.). kutokana na kazi hii ineonekana kwamba fikra za Wayunani kuhusu Demiurge na Pleroma yameshambulia mawazo yao ambayo yaliitwa Aeons, na yalikusudia kuvutia fikra za kibiblia ambayo wanamifano wa Kiyunani, kwayo yanaharibu maana yake. Wagnoistiki walilazimika kwa chinichini kuwa sehemu ya dini ya Siri. Mwendelezo wa mwisho wa kwenye imani ya Utatu umeelezewa baadae.

 

Irenaeus (na Justin) walifundisha kwamba ufufuo wa wafu ulikuwa ni wa kimwili, na kwamba Mungu atailinda miili isioze na idumu bila kufa (jarida la ANF, Vol. I, uk. 403). Mungu anaaminika kuwa ni Muumbaji (ibid., uk. 404), ikimpingwa Kristo aliyeumba ulimwengu kwa mamlaka ya Mungu (uk. 405). Irenaeus anafundisha kwamba Roho Mtakatifu alihusika na wote wawili, yaani Baba na Mwana (kutoka Zaburi 45:6-7) akiwa Elohim au Theoi; Baba anamtuma Mwana Irenaeus alifundisha kwamba Zaburi 82:1 ilikuwa inawataja Baba, Mwana na malaika (ambao ndio walengwa wa Kanisa) pale aliposema: 

Mungu alisimama katikati ya Kutaniko la miungu (theoi), akiwahukumu miungu (Adv. Her., Bk. III, sra ya VI, ANF, Vol. I, uk. 419).

 

Anaonekana kutokuwa na uelewa mkamilifu eneo la udugu wa wateule, ambao ulienea kwa Malaika wote wakiwa ni wapendwa kwenye Ufalme. Yohana alionyeshwa Ufunuo akiwa kisiwani Patmo alipofungwa akiwa amekwisha mfundisha tayari Polycarp. Ufunuo 12:10 inasema kuwa malaika ni ndugu zao wateule. Ufunuo 4 na 5 inaonysha kuwa wateule wamejumuishwa na Baraza la Wazee ili kuwa wafalme na makuhani kati ya Malaika. Kristo alisema kwamba wateule watafanana na malaika (isaggelos: kutokana na neno isos na aggelos, ambayo yana nadharia ya kuwa sehemu yao wakiwa sawa).

 

Irenaeus aliamini kuwa Kanisa lilikuwa ni sinagogi ya Mungu, ambalo Mwana alikutanika kwa ajili yake mwenyewe. Mungu wa miungu Zaburi 50:1 inaonekana kumtaja Mungu. Bwana wetu na Masihi alikuwa ni theos au Mungu atakayekuja kwa ujio wa wazi na hatakuja kwa uficho wala hatanyamaza (Zaburi 50:3), na aliyeonekana wazi kwa wale wasiomtafuta (Isaya 65:1). Jina miungu lililo kwenye Zaburi 50:1 linawahusu wateule ambao Kristo anaaminika kuwa aliwasema kuwa: “Ninyi miungi nanyi ni wana wa Aliye Juu (Yohana 10:34-35 sawa na Zaburi 82:6). Kwa hiyo ni makosa makubwa kwa Kanisa kusema kuwa kwa kipindi chake cha millennia ambayo Kristo amekuwa akilitumia andiko ambalo limekuwa likiwataja mahakimu wote wa Yerusalemu, wakati mwanafunzi wa Polycarp waliamini kuwa alikuwa anawataja wateule kama elohim. Wale waliomwamini Kristo waliaminika na Iranaeus kuwa walikuwa ni Wana wa Mungu walio warithi pamoja na Kristo, na ndio elohim. Iranaeus anaamini pia kwamba Kristo alikuwa Mwana wa Mungu aliye Mimi Niko Ambaye Niko (YHVH) (kutokana na Kutoka 3:14). Kwa hiyo, uchukuaji wa jina hili ulikuwa kwa ajili ya kupewa au kuruzukiwa. Irenaeus alimnukuu Isaya hivi:

 

Isaya 43:10 Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo

 

Soncino analieleza jambo hili kama hivi:

Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu (EI) awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo

 

Nukuu kutoka kwa Irenaeus na Soncino zinatofautiana, ambazo kwa kuzidi au kwa upungufu Irenaeus, anaonyesha kuwa ‘MIMI’ inamaanisha kumtaja Mungu, ambaye ni Baba. Akitajwa kama mtumishi kwenye Soncino inaonekana na Irenaeus kumtaja Masihi.

 

Soncino inajaribu kufananisha jina Mtumishi Wangu na mashahidi wa kale wa Israeli, ingawaje hakuna mamlaka ya kirabi yanayotajwa. Kinachuonekana kuwa ni hakika ni kwamba andiko hili lilionekana kama linaashiria kwamba ni Mungu pekee, na sio Masiri, ndiye alikuwepo huko nyuma kabla ya yote. Baba, Masihi wanatofautiana na Mungu. Irenaeus anaonysha kwamba uelewa wake katika Isaya 44:9 na Yeremia 10:11 kuhusu suala la vinyago au sanamu ilikuwa ni kwamba vinyago hivi vilikuwa ni sanamu za mashetani (Adv. Her., Bk. III, Ch. VI, ANF, p. 419). Mashetani hawa waliondolewa kutoka kwa theoi au elohim. Akifananisha na Yeremia 10:11, Irenaeus ananukuu hivi: 

Miungu ambao hawajaumba mbingu na nchi, na waangamie kwenye dunia iliyo chini ya mbingu. Kwa kuwa kutokana na ukweli wa yeye kuwa mshiriki aliyeunganishwa na maangamivu yao anawaonyesha kuwa hakuna miungu (elohim au theoi) yeyote.

 

Kwa hiyo sanamu zenyewe zilonyeshwa kueleweka kuwa sio sanamu za kawaida, bali zaidi sana ni zilikuwa na miili ya mashetani ambazo (tazama pia kitabu cha Bk. III, Ch. XII:6, ibid., uk. 432). Hiki ndicho kilikuwa kipimo kilichoeleweka kipindi cha ulimwengu wa kale. Kwa hiyo kitendo cha kuwaondoa mapepo hawa kusafisha na hatimaye kuhukumiwa kuliwaondoa kwenye kundi la elohim.

 

Irenaeus anaonyesha kwa maelezo Kutoka 7:1 kwamba Musa alikuwa kwa kweli amefanywa kuwa elohim kwa Farao, lakini hakuweza kutajwa kikamilifu kuwa ni Bwana au Mungu na manabii. Zaidi tu ni kwamba Musa anatajwa na Roho kama Musa, mtu na mtumishi wa Mungu mwaminifu (Waebrania 3:5; Hesabu 12:7), ambavyo ndivyo pia alivyotajwa Masihi kwenye maandiko. Kwa hiyo, kila elohim ni mtumishi mwaminifu wa Eloa, Elyon.

 

Irenaeus (uk. 421) anasema kwamba Kristo alikiri kuwa ‘ya kaisari apewe Kaisari’ na ‘ya Mungu apewe Mungu;, kwenye Mathayo 6:24, katika kumtumikia Mungu na sio mungu mammon. Kwa hiyo, Kristo alijiweka kando kutokana na kudai kuwa yeye ni Mungu (tazama ukurasa 422). Aliinukuu Wafilipi 2:8, Irenaeus anaonyesha kuwa uhusiano kati ya Kristo na Mungu na Mwamuzi ulitokana na Mungu wa Wote kwa kuwa alikuwa mtii hadi kufa (Sura ya XII:8, uk. 433). Irenaeus anainukuu Septuagint (LXX) kwenye Isaya 9:6 akisema kwamba Masihi alikuwa ni Emmanueli mjumbe [au Malaika] wa Shauri Kuu la Baba (Sura ya XVI:3, ibid., uk. 441). Kwa hiyo alionyesha kwamba Malaika wa Shauri Kuu wa Agano la Kale (LXX) alikuwa anajulikana kuwa ni Kristo. Irenaeus anakataa wazo la kwamba mateso ya Yesu yanaweza kumtenganisha na Masihi kwa madai kwamba Kristo alitajwa kuwa ni mwenye huruma na kuteseka. Kwa maneno mengine, anakataa jaribio kwa kudai kwamba mwili wa kimbinguni wa Masihi ungeweza kutofautishwa na Yesu mwanadamu hapa Duniani. Hili lilifanyika kuwa ni fundisho la dini ya Wagnostiki likiibadilisha Injili ya Marko na kuzipuuzia na nyingine.

 

Pia Irenaeus anaonyesha misingi wa makosa ya dini hizi potofu. Waebioni wanadaiwa kuwa waliitumia Injili ya Mathayo peke yake. Kwa hiyo walifanya hitimisho zenye makosa kuhusiana na nafasi ya Kristo. Waathanathias au Watrinitariani walilitumia jina Waebioni baadae kama kujaribu kufanyiza mafundisho udogo kicheo au wanaoamini hivyo wakitumia kila namna ya ushawishi kwenye kila msitari na namna yeyote ya kizushi za hawa Waebioni kwa kila namna iliyotumika kwenye mabishano ya mtaguso wa nikea ambao uliitwa kwa jina la Waarian. Madai haya ni ya uwongo kutoka kwenye mahojiano yaliyofanywa na waandishi wa Kanisa la kwanza na ambao walikuwepo siku za kabla ya mtaguso wa Nikea, na kugundua walikuwa wasabonist.

 

Irenaeus alikuwa anasisitiza kwamba kulikuwa na Mungu mmoja tu au Baba, aitwaye Mungu Baba. Masihi alikuwa ni Mwana wake. Anasema pia kuwa Marcion aliiongeza Injili ya Luka ili kuwekeza mafundisho yake. Wavalentinia waliitumia Injili ya Yohana kuzikanganya nyingine na pia kwa kuzijumuisha injili za uwongo. Ukweli ni kwamba basi, kama sasa, Maandiko matakatifu yanapaswa kutumika pamoja, kwa bidii na sio kwa kuyachagua. Irenaeus anaonyesha uelewa mkubwa wa asili iliyoko kwenye Injili hizi nne na maana zake kwa kuhusianisha na Makerubi (ibid., Bk. III, Ch. XI:8, kurasa 428-429). Irenaeus alikataa dhana ya kuwa Yesu aliweza kuteseka na kufa na kufufuka tena, na kwamba yeye aliyewahi kuruka na kwenda mbinguni alikuwa ni mwingine. Irenaeus aliamini kwamba “Kristo ambaye Mungu alimuahidi kumtuma, alimtuma katika Yesu, waliyemsulibisha na Mungu akamfufua (ibid., Ch. XII:2,4,5; kurasa  430, 431).

 

Hakuna mchanganyo kati ya Mungu na Kristo kwenye mawazo ya huyua mwana teolojia na anasema hapa wazi kabisa, kwamba Mitume hawakumbadili Mungu, bali Kristo alitumwa na Mungu. Irenaeus anasema:

Wapenzi, msiiamini kila roho, Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. (sura ya. XVI:8 akiinukuu Yohana 1 Yohana 4:1,2. Kumbuka: Tafsiri ya Vulgate na Origen zinakubaliana na Irenaeus, Tertullian inaonekana kukubaliana na maandiko yote mawili). Socrates anasema (VII:32, uk. 381) kwamba kifungu kiliharibiwa na wale waliotaka kutofautisha ubinadamu wa Kristo kutoka kwenye ule wa kimbinguni. Polycarp (Ep., c, vii) anaonekana kukubaliana na Irenaeus na ndivyo alivyofanya Ignatius pia (Ep. Smyr., c,v) (tazama ANF, ibid., uk. 443, iliyonukuliwa pia na Burton, kwenye kitabu chake cha Shuhuda za Ante-Nicene hazi Umbinguni wa Kristo (Ante-Nicene Testimonies to the Divinity of Christ)].

 

Kwa hiyo, kila fundisho linalotafuta kumtenganisha Kristo kwa kumuunganisha kwenye eneo linguine na wote wawili, yaani mamlaka ya kidunia na kimbinguni lilichukuliwa na Kanisa la kwanza kuwa ni Fundisho la Mpingakristo. Tendo la kuyabadili au kuyageuza maandiko linaonekana kuwa na lenye asili ya Kimashariki. Maandiko ya Biblia bado hayajasahihishwa hadi leo.

 

Irenaeus anasema kwamba Roho wa Mungu alimshukia Kristo kwa umbo la njiwa ili aweze kutimiliza yaliyoatabiriwa kwenye Isaya 11:2 kusema: Na roho ya Bwana atakaa juu yake, na pia Isaya 61:1: Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; Kwa hiyo sio yeye aliyekuwa anaongea bali ni Roho wa Baba yenu ndiye anayeongea ndani yenu  (Mathayo 10:20) (Sura ya XVII:1, ibid., uk. 444). Kwa hiyo, Roho Mtakatifu alijulikana kuwa ni wa Mungu na sio alitoka kwa Kristo, bali zaidi sana ni kwa kupitia Kristo kama ilivyoelezwa hapo juu. Hii ilikuwa ni kwamba:

… Mwana wa Mungu, alifanyika kuwa Mwana wa Adamu akifanyika kuwa kwenye udugu na mkutaniko naye ili aishi kwenye ulimwengu wa wanadamu, ili aishi na wanadamu na kuwa kati yao alizifanya kazi za Mungu, akiyatumikia mapenzi ya Baba kwao, na kuwarejesha kutoka kwenye tabia na miendendo yao ya zamani hadi kwenye upya wa Kristo (ibid.).

 

Irenaeus alifundisha kwamba wateule wangewekwa kwenye maisha yasiyo na kifo ili wapokee hali ya kufanywa wana kama Wana (Sura XIX:1). Roho aliwaunganisha wateule kwa Mungu, akiyaleta makabila mbalimbali kweny umoja na kuwatoa kwa Baba malimbo ya mataifa yote (ibid., XIX:2). Kristo alikuwa ni chombo cha matendo yake, lakini hakuwa ni mlengwa kwenye ibada au kuabudiwa na wala sio msanifu mkuu wa mambo yake. Hata hivyo, alikuwa ni Mshauri wa Ajabu na Mungu mwenye Nguvu aliyeandikwa kwenye Isaya 9:6, na Hakimu kwenye Danieli 7:13 (ibid.). Hata hivyo, Kristo alimtambua na kumheshimu Baba kuwa ndiye Mungu wake, kama alivyofanya Daudi, (tukiinukuu Zaburi 22:1) ambapo Daudi alisema:

Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha?

 

Kristo tena alisema haya alipokuwa mtini, kama ilivyonukuliwa kwenye Mathayo 27:46 na Marko 15:34. Maandiko haya yote mawili yanamtaja Eloa, Mungu Mkuu na ni Mungu na Baba wa Kristo. Maneno yaliyotumiwa na Kristo ni ya Kiaramu, wakati aliposikika akisema:

 

Eloi, Eloi, la'ma sabaki-th'a'ni.

 

Hii ni tafsiri ya kimaandiko ya lugha ya Kiingereza iliyotokana na fasiri ya kiimandishi ya Kiyunani yenye chanzo asilia cha lugha ya Kiaramu inayosema 'eli, 'eli lamah 'azabthani. Neno linalomtaja Mungu hapo ni la Kiaramu la El hapo kama Mungu anayeelezea mapenzi yake kwa Mwanae. Mungu hakumsahau wala kumuacha Kristo kama inavyosema Zaburi  22:24 kuwa: 

Maana hakulidharau teso la mteswa, Wala hakuchukizwa nalo; Wala hakumficha uso wake, Bali alipomlilia

 

Kwa hiyo unaona hapa kuwa Mungu na Kristo walikuwa watu tofauti hapa. Kristo hakuwa anaongea tu hapa kimasihi kama sauti ya Mungu, ni kama ulivyokuweko ulazima wa kutofautiana uliopo kwenye Maandiko Matakatifu yanayohitaji utendaji wa kimbinguni kwenye usaidizi na ambao hauwezr kutangiliwa. Hakuna mwingine bali Kristo na wateule waliitwa na Mungu (elohim) kwa kuwazidisha. Irenaeus anasema yafuatayo: 

Hakuna mwingine aliyeitwa Mungu kwenye Maandiko Matakatifu isipokuwa Baba wa wote, na Mwana ba wale waliopewa uwana (Adv. Her., Bk. IV, Pref. 4, ANF, p. 463): [na pia]

[Sura ya ] 1. Kwa kuwa hii ni hakika na imara (sic), kwamba hakuna Mungu mwingine au Bwana aliyetangazwa na Roho, isipokuwa yeye ambaye ndiye Mungu, atawalaye juu ya yote, pamoja na Neno wake, na wale wanaompokea Roho wa kufanywa wana [tazama iii. 6,1], kwamba ni wale wanaomwamini Mungu mmoja na wa pekee, na Yesu Kristo Mwana wa Mungu, na ni kama walivyofanya kwao wenyewe wakisema kuwa hakuna aliye kama Mungu, au jina [hakuna jingine] aliye kama Bwana, na ni kitu gani kilicho muhimu zaidi, [kwa kuwa ni kweli (sic)] kwamba Bwana wetu [alitenda sawa na], aliyetuamuru sisi kuwa kutomkiri mwingine yeyote ila Baba, isipokuwa yeye tu aliyeko mbinguni, ambaye ni Mungu mmoja na Baba mmoja;...(ibid., uk. 463).

 

Kwa hiyo ni upuuzi kudai kujaribu kudhani kuwa kuelewa kuwa ni wateule ndio watakaokuwa elohim haikueleweka kama fundisho asilia la karne mbili za kwanza za Kanisa, ikichukuliwa kwamba Irenaeus alikuwa ni kiunganisho cha karibu sana tuliyenaye na mafundisho yake, na yuko wazi sana anasema na kuamini. Zaidi sana, inaonekana pasipo na shaka kwamba imani ile ni mpango muhimu wa Maandiko Matakatifu, na sio tu kuwa ni wa Maandiko Matakatifu kikamilifu – ambao tafsiri ya kibiblia ilikuwa ni Agano la Kale (Danieli 10:21; Mathayo 21:42; 22:29; 26:54; Marko 12:10,24; 14:49; 15:28; Luka 4:21; 24:27,32,45; Yohana 2:22; 5:39; 7:38; nk.) lakini pia kwenye Injili na kwenye maandiko ya Agano Jipya. Kwenye ukurasa huuhuu kunaelezea kuhusu wateule wa elohim, waliotajwa kwenye Yohana 10:35, Kristo anaonyesha fikara yah ii kwamba Maandiko Matakatifu hayawezi kutanguka. Kutokana na hapo juu, mafundisho ya Kanisa la kwanza yanaonekana wazi kuwa ni ya mfumo wa mkubwa na mdogo, yakihusisha pia fundisho la uzima wa milele unaotegemea kwa Roho Mtakatifu anayewezesha kazi ya ufufuo wa wateule wakiwa kama theoi au elohim kwenye Ufufuo wa Kwanza wa wafu wakati Masihi atakaporudi.

 

Fundisho kuhusu Roho kwa hiyo liliwaingia wateule sana baadae sambamba na dini ya Siri nay a Mungu wa Utatu. Kanisa asilia la kwanza lilishikilia kuamini juu ya ufufuo wa wafu na kikikataa mafundisho ya Roho kuendelea kuishi na kuyachukulia kuwa ni ya kipagani. Mabishano juu ya kukubaliana na Kanisa la Kikristo lenye mafundisho ya Kihelleniki na kuwaona kuwa wako sahihi zaidi ya ilivyokuwa imani ya mwanzoni ya Kiyahudi, sawa na wale walioyageukia mafundisho na imani ya Ebionite, au kuondolewa wakichukuliwa kuwa wamebobea kwenye Ukristo wa itikadi ya Kiyudea ambayo kwa kweli ilitoa mwanya kwenye Ukristo wa itikadi kali nay a wastani uliokuwa chini ya uangalizi wa Wamataifa kama ilivyoelekezwa na Mtume Paulo, jambo ambalo ni uwongo. Mabishano haya yalileta kile kilichosemwa na Paulo kwenye nyaraka zake mbili zote wa Wakolosai na wa Wagalatia. Mabishano kama hayahaya yametumika kuingiza makosa ya fundisho la Roho kutokufa (tazama jarida la Mafundisho ya Kisocrati ya Roho (Na. B6) [The Socratic Doctrine of the Soul (No. B6))].

 

Fundisho hili la Roho ni dhana ya uasi unaorithiwa unayosema kwamba hakika mwanadamu hatakufa  (Mwanzo 3:4). Ni jaribio la kuchukua nadharia ya hukumu kwa ajili ya dhambi isiwepo kwa wanadamu. Dhana ya kwamba mwanadamu atakuwa kama elohim katika kuelewa peke yake iliingizwa na Shetani kwa mujibu wa Mwanzo 3:5. Uwezo wa kuwa kama elohim kwa ujumla unategemea na ufufuo wa wafu, kupitia kwenye neema iokoayo Yoshua au Yesu Kristo akiwa Masihi. Kitendo cha kupinga kuwepo kwa kipindi cha utawala wa Milenia ni sehemu ya udanganyifu na kujaribu kudai urithi usiojulikana kanuni yake wa uzima wa milele. Uzima wa milele unaweza kupatikana tu kwa kumjua Mungu wa Pekee na wa Kweli na mwana waike Yesu Kristo. Hakuna kitu kama hicho ya ‘roho isiyokufa’. Ni uwongo unaotokana na imani za Kibabelonia, na ambayo imeenea ulimwenguni kote. Watu wanaamini uwongo kwa kuwa hawamwamini wala kumtii Mungu. Pasipo na Roho Mtakatifu, mawazo yao yanamchukia Mungu (Warumi 8:7), na hayawezi kumtii Mungu au kumudu kuwa kwenye asili yake. Wateule wamechukua asili ya Mungu wakiwa kama warithi pamoja na Yesu Kristo (2Petro 1:4). Ni Mungu tu ndiye asiyeweza kufa (1Timotheo 6:16). Anakaa kwenye nuru inayofikiwa na hakuna mwanadamu aliyewahi kumuona wala anayeweza kumuona. Ni kwa njia ya Roho tu ndipo tunavyoweza kumaribia Mungu na hiyo inategemea na utii wetu na dhabihu ya Yesu Kristo, ambaye ndiye muombezi wetu na Mungu Mmoja na wa Kweli (Yohana 17:3; 1Yohana 5:20; Wagalatia 3:19-20; 1Timotheo 2:5; Waebrania 8:6; 9:15; 12:24).

 

Tunapaswa kutarajia ufufuo wa wafu ili tuweze kuwa wanadamu katika ulimwengu wa roho tukiwa kama wana wa Mungu, wakati tutakapomuona Mungu na kumkaribia kwa dhahiri na kwa matendo. Kwa hiyo sasa tunakikaribia Kiti cha Enzi cha neema kwa njia ya roho.

 

Nyongeza

Kushindwa kwa Waadventista Wasabato ( Wa-SDA) kuelewa na kuendana kama unavyosema unabii wa Isaya na Zekaria unatokana na wao kujikita kwenye maandiko mapotofu ya Ellen G. White, ambayo yamechukulia kipindi cha millennia kuwa ni cha kiroho na kuyatafsiri mambo yote kwa mtazamo huu wa kiroho na kudhania kwamba Shetani atakuwa hapa duniani peke yake. Huu ni uwongo wa dhahiri kabisa umesababishwa na ukosefu wa kuelewa wa waandishi wao ambao wameyaelezea maneno ya manabii Isaya na Zekaria yanayoonyesha kuwa Kristo atakuja kuzianzisha tena ulimwenguni kote ibada za Sabato, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu Zilizoamriwa zinazokutikana kwenye mambo ya Walawi 23 (sawa na Isaya 66:23; Zekaria 14:16-19). Kama mfano wa kushindwa huku kuelewa marejesho yatakayokuweko kipindi cha milenia yanaonekana kwenye kitabu cha Robert D. Brinsmead, aliyeandika mengi kuhusu suala la Usabato na Torati (tazama makala yake ya Kuutathmini Upya Usabato, (Sabbatarianism Re-examined, la Juni 1981). Brinsmead anashambulia mafundisho kadhaa na imani ya Wa-SDA na anajaribu kukana fundisho linaloelezea mtawanyiko wa Waingereza, ila ameweka sawa mtazamo wake kuhusu unabii unaolingana na elimu ya mambo na mwenendo wa mambo ya ulimwengu, na kusema kuwa Maandiko Matakatifu yalikuwa yanaeleza mambo kiroho na siyo kimwili, wakati ambapo kwa mfano, nabii Isaya alimuainisha kuwa alikuwa anataja matukio yatakayotokea kimwili kabisa.

 

Wa-SDA wanaonekana hawajachukua kwenye na kupeleka kwenye mabaraza yao wazo lolote lile linalohusika na ukweli kuhusu kipindi hiki cha millennia, na ya kuwa kitafanyika kiukweli na sio kiroho na utawala wake na Kristo utakuwa hapa duniani kwa miaka elfu. Badala yake, Ellen G. White na Wa-SDA walizua fundisho la kunyakuliwa kwenda mbinguni, ambapo kwenye Ufufuo wa Kwanza wa wafu watenda dhambi wote watauawa na kwamba wenye haki wote watanyakuliwa na kupelekwa Mbinguni na kwamba Shetani ataachwa peke yake hapa Duniani kwa kipindi cha miaka elfu moja, akingojea hadi ile hukumu ya mwisho. Na hii ndiyo wanavyoamini, ambavyo ni kinyume kabisa na maelekezo chambuzi ya Maanago ya Kale na Jipya. Hivi wanavyoamini hakuna msingi wala mashiko ya Kibiblia lakini wao wanaamini tu hivyo.

 

Maranyingi sana, tunapowapata watu wakishughulikia mambo haya wanakuwa hawausomi unabii wa Agano la Kale kama tunavyousoma sisi. Wanasema na kudhani kuwa hakuna ukweli kwenye unabii wowote wa Agano la Kale, unaoelezea marejesho ya kweli ya Israeli hapa duniani. Wanasoma wakiwa na mifano ya kiroho, kwa hiyo kwa watu hawa unabii hauwezi kuwaeleza au kuwaonyesha kile unachokikusudia au kinachousema. Maranyingim tunaokuwa kwenye andiko la 66:23 linalosema kuwa Sabato na Miandamo ya Mwezi vitarejeshwa na kuadhimishwa, wanasema kuwa huenda kuna mkazo wa kiroho umaonishwa na kukaziwa hapa. Ila haviendi kurejeshwa Sabato zenyewe na kwa hiyo ndipo hata Brinsmead anaweza kuziondoa Sabato zilizowekwa msingi wake kwenye andiko hili, ambalo linasema wazi sana kwamba Kristo atakuja kuzirejesha upya. Ni upingaji na msimamo chuki tu kichwani na ambao ni suala linaloleta maswali mengi sana kujiuliza juu yake. Ni msimamo ambao hauna nafasi kwenye akili za mtu imara. Hakuna ukweli kwao wanaoujua au kuushikilia kutokana na unabii wa biblia kwa namna yoyote ile kuhusu marejesho yanayokwenda kufanywa siku zijazo za mwisho. Wanalisikia neno la kweli na la uzima ila wana udanganyifu unaowafanya waendelee kupotoka na kutoliamini jambo hili. Bali wamekuwa wakiuamini uwongo tu na kuupenda.

 

Imani ya Brinsmead kuhusu andiko la Isaya 40:3-4 hadi Yohana Mbatizaji peke yake (tazama Sura ya 7) inaonyesha kuwa haelewi ukweli Ujio ws Masihi kwa hatua mbili, na Mfalme Masihi ni mtu halisi atakayekuja kutawala Siku za Mwisho. Tafsiri ya The Companion Bible inaionyesha Isaya 40:3 ikionysha kwamba andiko hili halijatimilika bado. Tafsiri ya kiroho ya Wa-SDA kuhusu kipindi cha millennia inawasuta wao wenyewe na waandishi wao. Kwa kweli tafsiri hii ya uwongo inakwenda kuiangamiza imani hata ya Brinsmead mwenyewe. Brinsmead anashikilia kuamini kwamba, “mara tu baada ya imani ya kweli ya kikatoliki inavyopasa kuingia kila mahali, ndivyo inavyopaswa pia kupenya kila wakati. Hakuna wakati ulio mtakatifu kwa wenyewe tu kama ulivyo tena zaidi ya kila mahali ni patakatifu au kila kitu ni najisi. Kwa hakika sheria zilizokuwa zinahusiana na mahali na nyakati zilikuwa ni za kipindi kifupi tu zilizowekwa kwenye huduma au kanuni za kidini hadi kipindi cha matengenezo (Sura ya10, uk. 37).

 

Kwa hiyo, tunaona kule anakokwenda hadi kipindi hiki. Anauchukulia kimakosa ukweli wenye msingi wa kisayansi kuhusu sheria ya vyakula ukweli kuhusu utofautishaji kati ya mambo matakatifu na yaliyo najisi, akidhania kwamba Kristo amebatilisha tofauti zote kati ya yaliyo ya kidunia. Basi hakuna maana ya kusema tokeni ndani yake na muwe watakatifu; kwa kuwa ninyi ni watakatifu wa watakatifu na kwamba Hekalu la Mungu li ndani yetu. Nasi tu Hekalu la Mungu. Na kwamba utofauti huu hauna maana, licha ya ukweli kwamba ni fundisho la kibiblia.

 

Malumbano haya yanasababishwa na uwepo wa uweza wa Kristo wa kubadilisha nyakati na Sheria kwa mintaarafu sawa na Mungu, na ni Utrintari uliorithiwa. Zaidi sana, ukengeufu umetabiriwa kutokea kwenye Danieli 7:25, na ni machukizo kwa Mungu Aliye Juu Sana. Malumbano yote, mawili yote kutoka kwenye imani ya Kiadventista na kutoka kwenye imani ya Utatu, inatuama kwenye fundisho la Roho kutokufa.

 

Marejesho mapya yatakayofanywa na Kristo yanaonyesha kwamba kuna aina mbili ya viumbe. Wale wa daraja la kwanza, wanaoitwa wateule, watakaofufuka kwenye Ufufuo wa Kwanza na ambao watafanyika kuwa viumbe katika roho wakati Kristo akija. Kundi la pili ni lile ni la wale watakaokuwepo kwenye Ufufuo wa Pili utakaotokea baada ya kipindi cha utawala wa millennia, na linawajumuisha watu walioishi kipindi cha Milenia na wale waliokufa ambao hawakuwa na sehemu kwenye mafundisho ya wale walio na sehemu kwenye Ufufuo wa Kwanza (Ufunuo 20:1-6). Tazama jarida la Ufufuo wa Wafu (Na. 143) [The Resurrection of the Dead (No. 143)].

 

Shetani atafunguliwa baada ya miaka elfu na anakwenda kuwadanganya mataifa, walio pande nne za Dunia (Ufunuo 20:8-9). Imani ya Kiadventa haioni masshiko yoyote kwenye maandiko haya kwa ajili ya maandiko mapotofu ya Ellen G. White. Hawezi kuuelewa ufufuo wa miili wa dunia nzima, na teolojia yake inapingana na asili ya uwepo wa Mungu.

q