Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[146]
Tunda la Roho
(Jarida 2. 0 19951104-20000902) Kanda
Katika kuendeleza jarida lenye kichwa cha somo: Roho Mtakatifu tunaendelea kuendeleza fundisho la nafasi ya Roho Mtakatifu na uhusiano wake kwenye Uungu. Kutokana na uelewa wa tungaliyoweza kuielewa kiusahihi zaidi, kutokana na maelezo ya kibiblia, nia yake na kisha matokeo yake ya mwisho kwa wateule.
Christian Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Copyright © 1995, 1998, 1999 Wade Cox)
(Tr. 2005)
Masomo haya yanaruhusiwa
kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila
kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati
miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au
kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa
toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila
kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti
yetu ya:
http://www.logon.org
au http://www.ccg.org
Tunda la Roho [146]
Katika kuendeleza jarida lenye kichwa cha somo: Roho Mtakatifu [117] tunaendelea kuendeleza fundisho la nafasi ya Roho Mtakatifu na uhusiano wake kwenye Uungu. Kutokana na uelewa wa tungaliyoweza kuielewa kiusahihi zaidi, kutokana na maelezo ya kibiblia, nia yake na kisha matokeo yake ya mwisho kwa wateule.
Ili kuweza kumjua Roho Mtakatifu kwanza tunabidi tumjue Mungu na Kristo na uhusiano uliopo. Kijarida hiki kirahisisha, kwa sehemu, kwa yaliyofundishwa kwenye jarida lisemalo Roho Mtakatifu [117]. Majarida yameandikwa yakihoji kuhusu Mungu hasa ni nani na pia yakitaka kuelezea kuhusu Kristo kuwa pia ni nani na majarida haya yanakuwa yakisomwa. Kwa kifupi, Mungu Baba ni:-
Yesu mwana wa Mungu ni:
Roho Mtakatifu ni:
Maandiko haya matakatifu yanahitajika kusomwa kwa uandalifu sana. Kama hatutaweza kumjua huyu Mungu tunayemwabudu, hatuzaiweza kuyajua mapenzi yake. Bila ya kuelewa mapenzi ya Mungu, haiwezekani kumpendeza na hatutaweza keeingia Ufalme wa Mungu katika ufufuo wa kwanza. Roho Mtakatifu ni msaidizi anayetuwezesha kuielewa Biblia, na kwenye Biblia Mungu hufunua maelekezo yake na mpango wake kwetu.
Mungu ni Roho na wakati wote yu hai na anaendelea kuishi. Ni Mungu pekeyake huishi milele bila kufa (1Tim. 6:16). Kristo amesema katika Ufunuo 3:14 kwamba yeye ni mwanzo wa Uumbaji wa Mungu. Kristo ndiye mhusika wa kwanza katika uumbaji wa Mungu kutoka kwenye vizazi na hatimaye uumbaji wote umeanzia kutoka kwake na kwa njia yake. Wazo kuhusiana na muda lilianzia na uhusiano kati ya viumbe wawili, kwa hiyo Kristo ni mwanzo wa elohim wote. Kizazi cha elohim ulianzisha mwanzo wa nyakati. Yesu Kristo hakuwa Mwana pekee wa Mungu kuwepo kabla ya kuwekwa kwa misingi ya dunia, bali walikuweko wengine wengi (Ayu. 1:6; 2:1; 38:7). Shetani alikuwa ni miongoni mwa hao wana wa Mungu. Pamoja na wana wengine wa Mungu, Shetani alikuwa na uwezo wa kuingia kwenye kiti cha enzi cha Mungu kwa wakati wowote. Biblia inasema wazi wazi kabisa kuwa Shetani alikuwepo wakati wa mateso au majaribu ya Ayubu kule kwenye chumba cha kiti cha enzi cha Mungu.
Vile vile hakuwa Kristo tu kutajwa kama Nyota ya Asubuhi; bali walikuweko wengi wengine. Hawa wote walikuwa ni wana wa Mungu, kwa kupitia Roho Mtakatifu (Lk. 11:9-13). Roho Mtakatifu ni nguvu au uweza ambao kwaye Mungu hufanya kazi zake. Wakati Kristo aliposema kuwa alikuwa ndani ya Mungu na Mungu alikuwa ndani yake (Yoh. 17:21-23), ilikuwa ni kwa kupitia Roho Mtakatifu tu ndipi jambo hili linawezekana. Kwa jinsi hiyohiyo, wakati tunapompokea Roho Mtakatifu wakati wa tunapobatizwa, Mungu hufanya makao ndani yetu na Kristo vile vilae hushuka na kufanya makao ndani yetu, na hivyo Mungu huwa ni yote katika yote na ndani ya yote (Efe. 4:4-6).
Ni jambo la muhimu sana kuwa tunapaswa kujua kuwa kuna Mungu mmoja tu wa Pekee na wa Kweli naye ni Baba wa wote.
Hatua
za kufuata katika Kumpokea Roho Mtakatifu
Kwanza kabisa hata kabla hatujabatizwa, Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yetu akituleta kwa Mungu kupitia Kristo (Ebr. 7:25). Kwa njia ya toba na ubatizo tunapomkea Roho Mtakatifu na aningia ndani yetu, na kwa kuwekewa mikono juu yetu na mojawapo wa watumishi wa Mungu. Tendo la kuwekewa mikono juu yetu kama lilivyo enyewe tu halitoi mamlaka yoyote. Hatua hii inaleta maana tu ya ashirio rasmi kwa Kanisa kuridhia haja ya kila mtu katika kumpokea Roho Mtakatifu. Mzee wa Kanisa kama alivyo mwenyewe tu hana uweza kutoka ndani yake wa kupa mtu nguvu hizi. Bali yeye huomba tu kile ambacho Roho Mtakatifu anachokifanya. hatimaye Roho humjia na kumtia nguvu kila mtu binafsi yake. Hili ni mwanzo wa kweli wa mafunzo yetu. La muhimu tupaswalo kulijua ni kwamba tunastahili sote kumpokea kwa njia ya Ubatizo na kumpokea Roho Mtakatifu ili kuanzia kujifunza. Tumepewa silaha ya kuanzia ambaye kwayo tunaweza kufanyika kuwa askri wa Mungu. Kwa maneno mengine ni kuwa tunakuwa tumekabithiwa bunduki, au mfumo ambao kwa huo tunaweza kufanya kazi. Watu wengi wapo chini ya uelewa uliotokana na mapokeo yaliyokuwemo hasa hasa kwenye karne ya ishirini, ya kwamba wakiwa wamebatizwa tu na kuingia Kanisani, ndipo hapo wokovu wao ni wa uhakika. Wanadhani kuwa hawahitajiki kufanya kitu kingine chochote. Kwa kweli hali hii ilipelekea kwa baadhi yao wakate tamaa kusoma na kulinganisha mambo yote. Huu sio ukweli wa mambo tu kama tujuavyo sasa. Tunaupata Ufalme wa Mungu kupitia Roho Mtakatifu kwa neema na sio kwa kazi zozote zinazostahili kufanya kama malipizi. Hata hivyo, hatuwezi kuuingia Ufalme wa Mungu pasipo kufanya bidii au kufanya kazi kwa njia ya utii. Hii ni tofauti kuu na ya muhimu sana ambayo mara nyingi limeshindikana kueleweka na wengi. Kwa hatua hii, tanalazimika kusoma na kujipatia kila tunachoweza kupata. Kristo alisema kuwa chakula chake yaani nyama na kinywaji chake ni ilikuwa ni kuyafanya mapenzi ya Mungu na kukamilisha kazi yake (Yoh. 4:34); sasa ni zaidi sana kwetu kuwa hivyo. Pia Kristo alisema kwamba tutaishi kwa kila neno litokalo kwenye kinywa cha Mungu (Mt. 4:4). Kwa hiyo, Biblia ni kitabu chetu cha kuwanacho karibu, ni neno la unabii lililo hai, ambalo laweza kueleweka tu kupitia Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu hutuongoza na kutukia kwenye kweli yote (Yoh. 14:17; 16:13; 1Yoh. 4:6; 5:6), na katika kusema kweli kwenye mambo yote hivyo tutakua zaidi kama Kristo, aliye mfano wetu na kiongozi wa mambo yote. Roho Mtakatifu ni Roho wa Mungu (Rum. 8:14) na ni Roho wa imani (2Kor. 4:13) anayechunguza mambo yote na anajua mambo yote (1Kor. 2:10-11; 12:3) na ni msaidizi mwenye kutuwezesha sisi ili tufikie kwenye kima cha kuwa wana wa Mungu (yaani elohim). Kwa kupitia Yesu Kristo, mwombezi wetu, amemruhusuo Kristo kutusaidia, kutufundisha na kutufariji na kutuwezesha tuweze kuzifanyia kazi nguvu za Mungu, kutukirimia vipawa na karama za Roho Mtakatifu (Gal. 5:22-23). Tumeletwa pamoja, kila mmoja wetu akiwa na vipaji maalumu na tabia, ili tuweze kufanya kazi zake, ambazo sisi hatuwezi kuzifanya kikamilifu wakati tukiwa peke yetu (1Kor. 12:7-31). Tumebatizwa katika mwili wa Kristo (Kristo mwenyewe akiwa ni kichwa) na sio kwenye dhehebu au dini kubwa. Kristo ndie kichwa; sisi tu mwili. Roho Mtakatifu ni damu ambayo inaufanya mwili na kichwa kuwa hai na kufanya kazi zake kama kitu kimoja. Kama Israeli walivyofuata nguzo ya moto na wingu (yaani Malaika wa Yahova au Yehova) jangwani, ili kwamba sisi lazima tumfuate Kristo popote anapotuongoza. Yeye ni elohim kwenye vichwa vyetu (Zek. 12:8). Kama kanisa tuliloko leo halifundishi mafundisho yanayoendana na mahibiri au mafundisho ya sheria na manabii, Kristo hatakuwepo hapo na tuna wajibu wa kumtafuta na kumfuata yeye tu. Tumeitwa tutoke duniani ili tuishi maisha ya utumishi na kujitoa. Walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache (Mt. 20:16; 22:14). Wateule (wale wazishikao amri zote za Mungu) walichaguliwa, kama Kristo alivyokuwa chaguo la Mungu (Lk. 23:35).
Wateule wamechaguliwa na Kristo (Yoh. 6:70; 15:16,19) kwa maelekezo ya Mungu (1Pet. 2:4). Kwa hiyo Mungu ametutoa kwa Kristo, na hatimaye sisi tumejaliwa kuzijua siri za Ufalme wa Mungu (Mk. 4:11).
Roho Mtakatifu huwezesha mapenzi ya Mungu yajulikane, na hufanyika kuwa msaidizi wetu tunapoongea na Mungu kwa njia ya maombi kupitia Kristo. Hufunua uelewa wetu kwenye Neno la Mungu na kwa njia ya imani kuturuhusu tufanyike elohim kama Kristo alivyo, vichwani mwetu (Zek. 12:8).
Roho Mtakatifu sio kuwa yeye ni kitu tu kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu wanaoubeza Ukriso. Tukisema na kuamini kuwa yeye ni nafsi ya tatu katika Uungu, basi tonaondoa ule uwezo wake wa kufanya kazi ndani yetu. Sisi wakati mwingine tunamtenganisha na Mungu na tunajiweka wenyewe kwenye majikumu madogo ya Yesu Kristo kwa namna ambayo tunatofautiana kutoka na kamwe hatuwezi kufikia kwenye kima cha mwana wa Mungu, jambo ambalo sio sahihi. Roho Mtakatifu ni nguvu na ishara inayotia nguvu ya Mungu. Mungu ametukirimia sisi Roho Mtakatifu ili tushiriki kuwa na tabia zake za asili (2Pet. 1:3-4).
Mtume Petro anasema hivi:
2Petro 1:3-4, inasema: Kwa kuwa uweza wake wa uungu umenikirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani ilikwamba kwa hiyo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu ulioko duniani kwa sababi ya tamaa.
kwa yiyo, Mungu alituita kwa ajili ya utukufu wake mwenyewe na ubora na kutufanya tuwe warithi wa Roho wake ili tuweze kumjua yeye Mungu. Kwa hiyo Roho hutuwezesha sisi kutenda kazi za Mungu. Kwa hiyo kunatakiwa tuzae matunda ya Roho Mtakatifu. Matunda haya ni yale yanayo ambatana na toba yetu (Lk. 3:8). Haya ndio matunda yale, au tunda, la haki (Flp. 1:11). Kama anavyosema mtume Paulo, mwanamichezo hapati tuzo hadi pale anaposhindana kwa kufuata sheria za mchezo ule. Kumewekwa sheria au taratibu kwa ajili ya kumpendeza Roho Mtakatifu. Hatuwezi kupewa au kupokea tuzo kwa njia nyingine nje ya kuzifuata sheria hizi.
2Timotheo 1:6-14 inasema: Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uchochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. 7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. 8 Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mtumwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu za Mungu, 9 ambaye alituokoa akatuita wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele,
La msingi ni kwamba Mungu katuita sisi tuingie kwenye Ufalme wa Mungu kwa makusudio yake mwenyewe na sio kwa sababu ya kitu cho chote tulichonacho. Tumeitwa ili kufanya kazi. Mungu ndiye aliyetuweka sisi humo kazini. Jinsi tunavyofikia mwisho wa mapatano yetu na njia yetu ya kupata ufufuo wa kwanza, ni kazi ifanyikayo wakati ule tu tunapoitwa na kukirimiwa Roho Mtakatifu. Lakini ni jambo la muhimu pia kuzaa matunda ya haki katika Roho Mtakatifu kwa kuzishika amri za Mungu na ushuhuda wa imani ya Yesu Kristo. Hiyo ndiyo sifa yetu stahili. Neema ya Mungu alipewa Yesu Kristo. Kwa kweli, hakumiliki neema hii ya Mungu toka moyoni mwake kwa haki yake mwenyewe.
10 na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;
Ni Mungu peke yake ndiye asiyeweza kufa lakini alikuwa Kristo ndiye aliyeshinda mauti kwa matendo yake na kurudishwa kwenye kutokuharibika yaani kuto kufa kwenye nuru. Tunaweza kushiriki hali ya kutokufa kwa sababu ya Kristo. Kristo alistahili na kisha alipewa hali ya kutokufa na hivyo kila mara iliendelea mbele hadi kwetu.
11ambayo kwa ajili ya hiyo naliwekwa niwe mhubiri na mtume na mwalimu.
12Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, sitahayari; kwa maana namjua
yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka
amana kwake hata siku ile.
Kwa maneno mengine ni kusema kuwa Roho Mtakatifu hulinda siri za Mungu mpaka Siku ya Bwana. Kile kilichoaminiwa kwa mtume Paulo ni kwamba asingeweza kufa. Itaadhimishwa na Roho Mtakatifu na ilifungiwa kwenye Biblia. Hakuna mtu atakayeweza kuiharibu Biblia. Ni agizo la Mungu. Tuna neno lenye uvuvio la Mungu.
13 Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo ulio katika Kristo Yesu. 14 Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.
Kwa hiyo, tunda la kwanza la Roho Mtakatifu ni mlinzi wa kweli ya Mungu. Hili ni dhumuni la kwanza na lengo lengo. Roho mtakatifu ni wa uweza na upendo na kiasi. Kwa hiyo matunda yanayodhihirishwa kwenye kifungu hiki yametolewa kuelekea kwenye lengo la kwanza la wateule ambalo ni ulinzi wa kweli ya Mungu kama kitu cha kwanza haki. Tunda lingine ni Rehema ambalo tutaliona huko mbele (Yak. 3:17). Wateule wanamuabudu Baba katika Roho na Kweli (Yoh. 4:23-24). Kweli ni kama nanga katika kumuabudu Mungu. Hatuwezi kumuabudu Mungu vizuri hadi pale tumuabudupo katika Roho Mtakatifu na kweli. Roho Mtakatifu ndiye anayetuwezesha katika kuilinda kweli. Tunda lililo kiini ni uwezo wetu kwanza katika kumuabudu Mungu wa Pekee wa Kweli. Uwezo wa Roho Mtakatifu kuonyesha matunda haya umewekwa kwenye nafasi ya kumuabudu Mungu Baba. Kwa hiyo, kuilinda kweli ni kulinda uwezo wetu wa kufanya kazi na kuabudu. Ushuhuda wa Roho Mtakatifu na wa manabii na hivyo wateule ni kweli (Yoh. 5:33). Ni kweli ya Mungu tu ndio itatuweka huru (Yoh. 8:32). Shetani alianguka chini kwa kuwa hakukaa kwenye kweli (Yoh. 8:44).
Yohana 8:31-47 inasema: Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. 33 Wakamjibu, sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru? 34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35 Wala mtumwa hakai nyumbani siku zote; mwana hukaa siku zote. 36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. 37 Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Ibrahimu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu. 38 Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo. 39 Wakamjibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu. 40 Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyosikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo. 41 Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu. 42 Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma. 43 Mbona hamyafahamu hayo nisemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu. 44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo. 45 Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki. 46 Ni nani mioyoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki? 47 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.
Dunia huzuia kweli ya Mungu. Walimwua Kristo na walitafuta kuwaua wanafunzi wake na wafuasi wake. Hii ndivyo kwa sababu mawazo ya mwanadamu ni uadui na Mungu (Ru. 8:7).
Warumi 8:1-8 inasema: Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. 2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu umeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. 3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; 4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. 5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. 6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. 7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
Sheria imedhoofishwa na mwili. Sheria inaweza tu kushikwa vizuri kwa kupitia Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, Roho Mtakatifu hadhoofishi sheria lakini huziimarisha. Sheria hutunwa kaika Roho na kweli. Kuweka mawazo ya mtu katika Roho ni uzima na amani. Kwa hiyo, mawazo yaliyowekezwa kwenye vitu vya kimwili ni uadui na Mungu na sheria zake. Mawazo wa mtu wa kimwili ambaye haja ongoka anatambulikana kwa madai kuwa sheria za Mungu hazina ulazima wa kuzishka. Dini za uwongo za dunia hii hutafuta kuzishushia hadhi nia na uweza wa sheria.
Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu (Rum. 1:18).
Mtume Paulo anaelezea kuwa watu hawa hawakuzilinda kweli na walikosea kuhusiana na Uungu. Tabia za Mungu za asili zilikuwa ni msingi wa kosa katika Kanisa la Roma na hapa ndipo fundisho hili lilichukua pahala pake. Nipo walipoiongolea mbali Sabato na kuchukua utaratibu au mfumo wa kimamboleo. Ilikuwa ni kwa msukumo wa mfumo wa Kirumi wa Kiyunani ambao ulimulinua Kristo hadi kumfikisha kwenye kilele cha kuwa sawa na Mungu na walikuwa ni wao walioanzisha hatua hii ya ibada ya sanamu.
Kinachokatazwa katika Warumi sura hii ya 1 ni yale yatokanayo na dini ya uongo, yanayotafuta kuupiga vita Uungu na kubadilisha ukweli wa Mungu. Kwa sababu hii wamepewa tamaa ya mwili (Ru. 1:25-27). Mafundisho haya ya uongo yalikuwa yanaendelea kuenea kwa njia ya kuambukiza katika Rumi.
Tunajua kuwa Baba ni wa kweli na anatutia nguvu kupitia Roho wa Kweli (Yoh. 14:17; 15:26; 16:13). Kristo alishuhudia kweli na wale walio wana wa ukweli huisikia sauti yake (Yoh. 18:37).
Kama mtu si wa upande wa kweli husema uongo na uongo hauruhusiwi katika Ufalme wa Mungu (Ufu. 21:8). Watu wote wamesema uongo (Zab. 116:11). Kwa hiyo tunaalikwa kwenye toba kosa hili. Kwa hiyo ni jambo lenye maana sana kwamba tuishikw kweli na kuendeleza siri za Mungu, huku tukisukumwa na kweli. Kweli ya Mungu sio ni dhana tu. Matendo yetu yanatakiwa yaendane na kweli ya Mungu. Iwapo kama hatutasukumwa na kile tunachojifunza kwenye Bibla, basi sisi sio wana wa kweli.
Sisi sote tumefanya dhambi lakini toba inatakiwa ili kumpendeza Roho Mtakatifu. Ili kumjua Mungu tunatakiwa kuzishika amri za Mungu au vinginevyo tutakuwa waongo na kweli haimo ndani yetu.
1Yohana 2:4-5 inasema: Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. 5 Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake.
kwa hiyo, kushika amri ni muhimu katika kuishika kweli na ndili lengo la Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu anahitaji matendo kutokana na kuijua huku kwa kweli. Kwa hiyo, katika kusoma neno la Mungu na sio kusukumwa kwenye matendo katika ni kiashirio cha mazoea ya mvuto wa ushabiki wa kidini. Mshabiki wa kidini ni mtu anayelisikia neno la Mungu lakini haguswi nalo, zaidi sana atalichukulia kama ni somo tu la kujipatia ujuzi. Kristo anafanya kazi kwenye sayari nyingine mahali pengine. Sisi sote tunao wajibu ili kujua kile Roho wa kweli na kazi kwa ile kweli.
Tunatakiwa kukutana na kufanya kazi pamoja ili kuchangia kazi ya Mungu. Kazi ile itajulikana na kweli. Inabidi kila mmoja wetu ajiulize swali la msingi kwamba: Je, Kristo kama angekuwepo leo, angekubaliana na mimi kwa matendo ninayoyafanya, na ya kuwa nafanya kwa kiasi cha kutosha ili kufikia lengo la kueneza injili ya Ufalme wa Mungu? Iwapo kama hatujitoi kusaidia kazi ile ambayo tumeijua kama tuko karibu sana na kweli inayopatikana, basi tupo kwenye hatari kubwa sana ya kuwa mashabiki wa kiroho na hatutaweza kuingia kwenye Ufalme wa Mungu.
Tunda la pili la Roho Mtakatifu ni Upendo
Wazo lote zima kuhusu uvunjaji wa sheria na malipizi ya dhambi vimefanywa kuwa ni kivuli kutoka katika Agano la Kale. Pasipo malipizi hakuwezekani kumpokea Roho Mtakatifu. Malipizi haya yalikuwa yaje kutoka kwenye Jeshi la malaika kama tunavyoona kutoka kwenye Ayubu 33:19-30.
Ayubu 33:19-30 inasema: Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake; 20 Hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri. 21 Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane; Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje. 22 Naam, nafasi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi. 23 Kwamba akiwapo malaika pamoja naye. Mkalimani, mmoja katika elfu. Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo, 24 Ndipo amwoneapo rehema, na kusema, Mwokoe asishuke shimoni; Mimi nimeuona ukombozi. 25 Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto; Huzirudia siku za ujana wake; 26 Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia; Hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejezea mtu haki yake. 27 Yeye huimba mbele ya watu, na kusema, Mimi nimwfanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea, Wala sikulipizwa jambo hilo; 28 Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga. 29 Tazama, hayo yote ni ya Mungu anayeyafanya, mara mbili, naam, hata mara tatu kwa mtu. 30 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.
Mwombezi wa wanadamu ni malaika, mmoja miongoni mwa maelfu. Hii inaashiria ni mmoja kati ya walio kwenye uongozi wa juu. Mwombezi aliyekuwa amepewa aliyetoa maisha yake na nguvu zake ni Kristo. Tendo la kupunguzwa kwenye cheo na malipizo kumeonekana hapa katika kitabu Ayubu. Hii ni kwa sababu tendo kuu la pili la upendo na liliashiiria kuwa ni tunda la Roho Mtakatifu katika kukomesha Mpango wa Mungu. Tendo kuu la kwanza la upendo lilikuwa ni uumbaji wa elohim au bene elohim, yaani wana wa Mungu, kwa Mungu akijiongeza mwenyewe. Mmoja kati yao ilimbidi afe ili kuwakomboa wanadamu na kulipatanisha Jeshi kwa Mungu.
Ukombozi wa wanadamu unaendelea na hapa tunaona kuwa hauna kikomo kwa wakati wowote. Tunaona kwamba ukombozi ni mara mbili au mara tatu. Ni kusema kwamba Mungu anachukuliana na udhaifu wa wanadamu kupitia ukombozi wa Jeshi la wateule. Mwombezi alikuwa Masihi aliyetenda kwa upendo wa Mungu upendo kwa wapendwa.
Swali lote zima la upendo limesimama kwenye upendo wa Mungu kama amri kuu ya kwanza. Kwa hiyo, amri nne za kwanza kati ya zote kumi, ni ufunguo wa muhimu katika kuujua upendo wa mwanadamu. Kwa hiyo, kweli ni ya muhimu sio tu katika kuujua ukweli, bali pia katika kufikia katika kumjua Mungu mwenyewe na hivyo kuweza kumpendeza Roho Mtakatifu. Haitoshi kule kumkiri tu kuwa Yesu ni Bwana. Maandiko yanasema kuwa kama tusipoyafanya mapenzi ya Baba yetu aliye mbinguni hatutaingia kwenye Ufalme wa Mungu (Mt. 7:21). Kama tukiyatenda mapenzi ya Baba, tutaishi milele (1Yoh. 2:17). Hawa ni watakatifu. Hawa ni wale wanao zishika amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu Masihi (Ufu. 12:17). Wale 144,000 ambao uongo haukuonekana vinywani mwao (Ufu. 14:5). Hawa pamoja na wateule wanaunda kundi la watakatifu wanaozishika amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu (Ufu. 14:12). Waliozifua nguo zao au kanzu kwa biblia za tafsiri nyingine husema (wanaoshika amri za Mungu, Biblia ya RSV) wana haki (mamlaka) kuuendea Mti wa Uzima na kuingia kwenye Mji wa Mungu. Huko nje kuna miongoni mwa wengine wengi, wapendao uongo na kuufanya (Ufu. 22:14-15).
Mji wa Mungu ni fundisho la kiroho. Maelekezo ya jinsi mji
ulivyo ni mfano matunda na matendo ya Roho Mtakatifu katikati ya Jeshi la
wateule. Vyombo vya dhahabu na vya chuma huwakilisha tabia ya Roho Mtakatifu.
Vile vya lulu ni wale wenye kupokea tuzo kubwa chini ya uangalizi wa waamuzi
thenashara wa Israeli. Hivyo basi, hekima ya Roho Mtakatifu huchukuliana na
kufurahi pamoja na kweli, ambayo ni ya muhimu katika kuuingia Mji wa Mungu
(angalia Ufu. 21:10 hadi 22:5 na jarida la Mji wa Mungu [180].
Upendo
kama tunda la Roho Mtakatifu
Matokeo ya upendo kupitia Roho Mtakatifu ni mengi kwa matokeo ambayo yana mtambulisha.
1Wakorintho 13:1-13 inasema: Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
Tunaona hapa kuwa ukiri wa imani tu hautoshi. Haitoshi kumwita Kristo kuwa ni Bwana. Inatakiwa kuambatane ne matendo. Ni kwa njia ya matendo yetu ndipo tunaonyesha imani yetu (Yak. 2:18). Imani bila matendo imekufa (yak. 2:26). Kwa njia ya matendo ndipo imani inafanyika kuwa kamilifu (yak. 2:20-22). Matendo yanaweza kuikamilisha imani iliyotegemezwa kwenye upendo.
2Tena ijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha masikini, tena nikijitoa mwili wangu niungue kwa moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
Tunaona hapa kuwa imani ni kuzijua siri zote na inaweza kuhamisha milima, hauna maana.
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu, hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli, 7 huvumilia yote; huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote
Uvumilivu na wema unaoonyesha mfano wa Roho Mtakatifu hauambatani na tabia ya majivuno au kutokuwa na adabu kwa wengine. Mungu hufanya kazi pamoja nasi kupitia Roho Mtakatifu. Watu humwona Mungu alivyo kwa kupitia yale tunayoyafanya, kisha ndipo hupata wazo la yale Mungu anayotaka wayafanye na kuwa. Kwa hiyo, dunia yote huhukumiwa kwa matendo ya Roho Mtakatifu na kimsingi ni kwa upendo wa Mungu. Upendo katika mtazamo wa Roho Mtakatifu unatakiwa uwe ni chanzo cha upendo wa Mungu anavyoweza kujionyesha mwenyewe. Upendo hausisitizi kwa namna yake wenyewe. Wala hauchochei hasira au uchungu wa moyoni. Ili kuonyesha tabia hizi za uvumilivu na wema huhitaji udhati wa kujaliana kila mtu na mwenzake.
Kinyume chake, tabia hizi zilizo kinyume yaani za majivuno, kukosa adabu, hasira na uchungu hayaonyeshi kuwa kuna kujaliana. Wazo la kufurahia haki ni chanzo cha nderemo za ushindi zinazoonekana wakari rafiki anapofanya vizuri kwa kitu fulani. Hivyo wateule wanaweza kuonyesha furaha ya dhati wakati mtu mwingine anapofanikiwa. Wakati mtu Fulani anaporudi kutoka kwenye upotevuni kuna furaha kuu mbinguni; viivyo hivyo zaidi sana kwetu sisi. Kwa ajili hii, sisi tunachukua vitu vyote, tukitumainia vitu vyote na kuamini kila kitu. Tunavumilia mambo yote kwa utukufu mkuu wa Mungu kwa kuwa tumejitoa na kuwekwa wakfu na Mungu na jirani zetu kwa upendo. Kama hatutawapenda jirani zetu ambao tunawaona, tutawezaje kumpenda Mungu ambaye hatuja muona. Kudhihirisha tendo moja ni muhimu na uhalisi wa kitu jambo lingine. Kwa upendo tumikianeni na mpende jirani yako kama kama nafsi yako (Gal. 5:13-14). Pia muipende kweli na muokolewe (2The. 2:10).
8 Upendo haupungui neno wakati wowote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwemo lugha yakiwepo maarifa yatabatilika. 9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabi kwa sehemu; 10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika. 11 Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo kitoto. 12 Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana. 13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Tabia zetu zisizokuma za upendo wetu kwa Mungu ni sawa kabisa na kipawa cha uzima wa milele. Kwa kuwa bila ya endelezo la moja hakuwezekani kuwepo na endelezo la ile ya nyingine. hali ya kukoma kwa unabii imejumuishwa na muungano mkamilifu na maarifa, kunakotokana na ushiriki wa Roho Mtakatifu. Kutokana na dhana hii tunashiriki maarifa ya Mbinguni. Kwa hiyo ni kusema kuwa maarifa makamilifu watashirikishwa kikamilifu watele na Mungu. Kisha kutoka hapo unabii utakoma. Ushirika mkamilifu ni ule utokanao na tabia za asili za kimbinguni hufanya ndimi zinene maneno yasiyo ya kawaida kueleweka. Tutapewa lugha mpya kabisa. Kunena kwa lugha kutapita zake kwa sababu tutapewa lugha moja itakayotumika kuwasiliana na itakuwa yenye kiwango cha usawa wa kiroho. Lugha zote zitapita zake lakini upendo wa Mungu utawekwa mfano wa vile tutakavyokuwa baada ya jumbe hizi za kinabii, maarifa na ndimi zitakapo kuwa zimekwishapita zake. Maarifa kamili yataondoa dhana ya kutojua na kwa hiyo maarifa kama usemi, ambao pia unaashiria kutokuwepo kwake, vita koma. Tutajua kama tujulikanavyo (1Kor. 13:12). Maarifa na ujuzi wetu si kamili na ni machanga. Kwenye ufufuo wa kwanza tutamuona Mungu uso kwa uso katika maana ya kiroho. Ulimwengu wa kiroho utafunuliwa na nguvu zake zote. Hii inaweza kuonekana tu na kushirikishwa kwenye upendo. Pasipo upendo, kila mtu anapelekea kwenye ufufuo wa pili kwenda kujifunza tena na kujiunza upya ili aweze kushiriki.
Kwa hiyo, ujuzi mkamilifu unatokana na upendo wa Mungu. Kwa kupitia Roho Mtakatifu tunaweza kuendeleza upendo wa kweli na mkamilifu ambao unahitajika na muhimu kwetu. Upendo unadhihirika kwa imani kwenye shari. Hivyo basi mabo haya yaani imani, tumaini na upendo ni vitu vinavyoenda pamoja vya Roho Mtakatifu lakini upendo ni mkuu kuliko hivi vingine vyote.
Wagalatia 5:22-23 inasema: Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi, juu ya mambo kama hayo, hakuna sheria.
Kutoka kwenye Upendo kunafuatia mambo mengine katika mafuatano ya Roho Mtakatifu:
Furaha imechukuliwa kutoka kwenye toleo la sura ya Mpango wa Mungu, uliofikia uzoefu wa kila mtu, ama kwa mahusiano na Mungu, au kwa kupitia kufikiwa kwa malengo na kila mtu katika mahusiano yake na Mungu. Ni kwa kupitia upendo tu ndipo upendo wa kweli unaweza kuona. Furaha ile tu hali ya kujitosheleza hutawala hisia kimwili.
Amani hutokana na uhusiano madhubuti au mkamilifu unaotokana na upendo wa Mungu na tumaini na imani inayomtegemea yeye yaani Mungu. Kutokana na upendo wa Mungu tunajionea upendo kwa jirani ambayo ni Amri Kuu ya pili.
Wana amani nyingi sana wampendao Bwana. Mungu ni Mungu wa amani (Rum. 16:20; Flp. 4:9). Mungu ametuita katika amani (1Kor. 7:15). Alimchubua Shetani; sisi hatuhitaji kufanya hivyo. Kuwa imara au timamu kiroho ni uzima na amani (Rum. 8:6). Amani hutoka kwa Mungu Baba yetu (Rum. 1:7; 1Kor. 1:3; Kol. 1:2; 1The. 1:1; 2The. 1:2; Tit. 1:4; Flm. 3). Hivyo basi wale wote wasiomtii Mungu hawawezi kupata amani. Amani inaendana na utii kwa Mungu. Hakuna amani kwa wabaya, asema Mungu wangu (Isaya 57:21). Hii ndio maana amani isiyotegemea neno la Mungu hushindwa. Wanatangaza amani, na maafa yatawashukia bila kutazamia kabisa. Kifungu cha maandiko matakatifu katika Isaya 57:19-21, kinahusiana na swali lote lihusulo Baraka na laana za Kumbukumbu la Torati 28 (tazama jarida la baraka na laana [075].
Isaya 57:19-21 inasema: Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA, nami nitamponya. 20 Bali wabaya watafanana na bahari iliyochafuka, maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka. 21 Hapana amani kwa wabaya, asema Mungu wangu.
Pia tuliitwa kwenye ndoa yanye amani. Wakti wenzi wetu wa ndoa wanapokubali kuishi na sisi tunatakiwa kujitahidi kuilinda au kuleta amani majumbani mwetu. Mara nyingi hii huwa ni jambo gumu sana kufanywa lakini hakuna jaribu ambalo tutashindwa kulibeba au kutokana na kile ambacho Mungu hataweza kutufungua kwacho.
Uvumilivu ni wa muhimu katika kuzaa tunda la Roho Mtakatifu. Kristo alilielezea tatizo hili kwenye mfano wa Mpanzi.
Luka 8:15-18 inasema: na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia. 16 Hakuna mtu ambaye akiisha washa taa huifunika kwa chombo, na kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kiango, ili waingiapo wapate kuona nuru yake. 17 Kwa maana hakuna neno lililositirika; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kutokea wazi. 18 Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang’anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.
Usemi huu unamaana ya kuwa tunafanya kazi na kusoma na Roho Mtakatifu tunapata zaidi na zaidi. Kama hatutafanya kazi, kusoma na kumchochea Roho Mtakatifu tutazidi kupokea kidogo na kidogo. Kisha ataondoka zake kutoka kwetu na tutabaki tumekaukiwa. Kwa hiyo, tunatakiwa tuombe, kujisomea na kufunga saumu na kufanya kazi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu ili tuweze kumpendeza Roho Mtakatifu na kukulia kila tunachokifanya.
Kulisikia neno chanzo chake ni kulishika neno la Mungu. Kwa hiyo, neno ni amri ya Mungu na ushuhuda wa Kristo. Kutokana na kulifahamu neno na maambatano yake, tunda la Roho Mtakatifu hudhihirika. Kwa hiyo, tendo yanayotokana na kusikia na kulishika neno la Mungu humtangaza Roho. Tendo lolote lile liwe vyovyote kati ya pande mbili yaani zuri au baya kudhihirika kupitia Roho Mtakatifu. Wale wote wasio enenda sawa sawa na neno la Mungu wana ule uelewa mdogo na finyu ambao huchukua kuondolewa kwa muda.
Kupitia hali ya uvumilivu, tunachukua mioyo au utu wetu (Lk. 21:19). Tunajifunza uvumilivu kutoka kwenye dhiki, au kutokana mateso tunapata ustahimilifu. Hatua hii inaendelezwa kwa njia ya kuhesabiwa haki kwa njia ya imani kupitia Kristo na upendo wa Mungu ambalo umemiminwa kwenye mioyo yetu kupitia Roho Mtakatifu.
Warumi 5:1-5 inasema: Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, 2 ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; wa kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. 3 Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi, 4 na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthibiti wa moyo ni tumaini, 5 na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.
Kwa hiyo, hapa tuna kitu uvumilivu au ustahimilivu kuendelea kutoka kwenye mateso na hatimaye kujitoa kwenye uzoefu, ambao unaitwa tabia. Kutoka kwenye uzoefu au tabia tunakutana na tumaini. Hatulionei haya tumaini letu kwa kuwa Roho Mtakatifu, ambnaye alitolewa kwetu kwa upendo wa Mungu.
Neno lililotumiwa katika Wagalatia 5:22-23 yanatafsirika kama utu wema katika Biblia ya Kiingereza tafsiri ya mfalme Yakobo kifupi KJV na imeandikwa wema katika Biblia nyingine ya RSV ni neno la Kiyunani kwa mujibu wa kamusi ya SGD 5544 likisema chrestotes ambalo limechukuliwa kutoka SHD 5543 likisema chrestos maana yake kutumika au matumizi, ambalo ni ubora wa kimaadili kwenye tabia au mwenendo kwa hiyo, utu wema, (u)zuri, wema. Nia hapa ni kwamba, unyenyekevu na utu wema au upole wa tabia, ambyo kwa kweli yaweza kutumika kwa kazi ya Mungu. Ina uzuri wa asili wa ndani wa tabia.
Wazo au maana hapa ya neno wema ni rahisi. Limechukuliwa na kuhamishwa kutoka kwenye neno la Kiyunani SGD 19 likisomeka kama agathosune maana yake ni wema au ubora.
Hili neno hutokana na SGD 4102 likisomeka pistis lililo chukuliwa na kuhamishwa kutoka SGD 3982 kufuatilia kwa nyuma, mfano, mwandamo, Ufalme maana yake ni kuvutiwa na ukweli wa kidini au ukweli wa Mungu au mwalimu wa dini.
Lina maana yake maalumu ya kutegeme kwa Kristo kwa wokovu. Kidhana humaanisha mara nyingi kwa taaluma. Kwa kupanua ina maana tegemezi kwenye mfumo wa kidini wa kweli yenyewe. Kwa hiyo, inabeba maana ya uhakikisho, imani, kuamini, kisha imani na uaminifu.
Kwa hiyo, tunda la Roho ni imani na kweli ya kibiblia na neno la Mungu. Kushikilia imani mara tu baada ya kuachiliwa inatafutwa kwa bidii na mguso. Kuonea mashaka juu ya uvuvio wa vifungu vya maandiko ni ashirio la tatizo la Roho Mtakatifu kwa mtu binafsi.
Upole au Utulivu
SGD 4236 imechukuliwa na kuhamishiwa kutoka kwenye SGD 4235 ikisema upole. Kwa kudokezea inamaana ya mwanadamu na hivyo ukimya.
Kiasi au Hali ya Kujitawala
Neno hili katika SGD 1466 husomeka egkrateia [hutamkwa engkratiah] limechukuliwa na kuhamishwa kutoka katika SGD 1468 likisomeka egkrates [matamshi yake ni engkratace] lenye maana ya kuwa imara kwa ajili ya kitu au umiliki, kwa hiyo, kuwa na kiasi au kujitawala katika hamu na hivyo kuwa na hadhari. Maana yake limechukuliwa kama kiasi kama kuridhika au kujizuia, ambako kunahusika na kujizuia kwenye masuala ya tamaa ya ngono (tazama kamusi ya Oxford University Dictionary).
Tumejionea nduzo tatu ambazo ni upendo, imani na tumaini, lakini upendo ndio uliokmuu. Kisha kutoka kwenye upendo tunaendeleza tunda jingine. Yote haya yanategemeana au kufungamanishwa pamoja na kweli. Kweli ndiye muhuri mkuu wa Roho Mtakatifu. Kutoka kwenye kweli tunaingia kwenye mambo haya ambayo ni furaha, amani, uvumilivu au ukimya, utu wema, uaminifu au imani, upole au utulivu, kisha kiasi au kujitawala.
Kwa hiyo mambo haya yanafuatana moja baada ya jingine ili kuongezea kwenye hesabu ya maeneo, ambayo hudhihirisha utendaji kazi wa nguvu za Mungu ndani ya kila mtu. Kila mteule hutaabika na majaribu na dhiki katika kuendeleza tabia za Kiungu. Ushindaji wa mabo haya huonyesha maendeleo ya Roho Mtakatifu kwa mtu binafsi.
Tunaweza kujichunguza na kujihukumu sisi wenyewe na wengine kwa kulinganisha na tunda la Roho Mtakatifu. Tunapimwa na kuhukumiwa na jamii inayotuzunguka kwa kutulinganisha na tunda la Roho Mtakatifu – yale tunayoyafanya, yale yanayotoka vinywani mwetu na kwa jinsi tunavyofanyiana sisi wenyewe kwa wenyewe. Tunda la Roho Mtakatifu ni nguvu ya kweli ya imani yetu na ni kiini cha upendo kinategemea na kweli. Kama hatuna upendo basi si kitu sisi na hatuna lolote. Hili ni tunda kuu, lakini kweli ndio lengo muhimu na Mungu wetu ni Mungu wa kweli. Vitu hivi vyote vimefunga manishwa kwa pamoja katika upendo, lakini kwa hakika kabisa tunda la Roho Mtakatifu ni la muhimu sana kabisa kwa ajili ya kuonyesha kazi ya upendo.
Majarida mengine yatakayoweza kukusaidia kukujenga ni haya:
Wateule kama miungu midogo - elohim [001].
Mungu Tunayemuabudu [002].
Malaika wa YHVH [024).
Roho Mtakatifu [117].
Siri za Mungu [131].
Baraka na Laana [075].
q