Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[187B]
Majukumu ya Familia
(Toleo La 2.0
20071112-20071204)
Ni kwa nini Mungu aliwaumba wanadamu wafanye kazi kama jumuia inayotenda
kazi? Maandiko Matakatofu yanafunua kwamba muundo wa familia uliwekwa kwenye ulimwengu
wa kiroho hata kabla ya kuubwa kwa mwanadamu. Maandiko yanatufunulia pia kwamba
mwajibiko ulitolewa kwa wana wa kiroho wa Mungu walioumbwa ili kulinda familia ya
mwanadamu kwa uhusiano bora na wa upendo na Baha wa uumbaji. Kwenye familia ya
mwanadamu pia, Mungu aliweka mwajibiko kuwapa baba, mama, kaka, dada na mabibi
na mababu kwa ili kuweza kuiweka sawa mambo ya kiroho na kimwili ya familia. Je,
ni majukumu gani hayo basi? Jarida hili linakwenda kujibu maswali yahoo yote.
Ni muhimu kwa uwepo na ustawi wa jamii ili kuiwezesha kuyajua mapenzi ya Mungu
kwa familia, na umuhimu wa kujua wajibu wa kila mshiriki kwenye muundo wa
familia.
Christian Churches of God
PO Box 369,
WODEN ACT 2606, AUSTRALIA
Email: secretary@ccg.org
(Hati Miliki ©
2007
Tom Schardt and Jeremy Hatchett, ed. Wade Cox)
(tr. 2013)
Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na
kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la
haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa
au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi
zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya
lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.
Jarida hili
linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org
Majukumu ya Familia
Mungu Aliyejuu
Sana Aliifanya Familia
Kabla ya kuumbwa
kwake mwandamu, familia ya Mungu ilikuwepo. Mwonekano wa muundo wa kifamilia
ulianza na kuwepo wakati Mungu Aliyejuu Sana ilifangiliwa kwa umakini mkubwa na
kuweka familia endelevu ya wana wa kiroho. Neno la Kiebrania kuelezea mwana ni ben
(SHD 1121). Limetumika zaidi ya mara 5,000 kwenye Maandiko Matakatifu, na
linatumika kwa namna mbalimbali na wanadamu pamoja na wana wa Mungu walioko
mbinguni. Agano la Kale linaelezea baraza la mbinguni kuwa ni mjumuiko wa “wana
wa Mungu” (Ayubu 1:6, 2:1).
Andiko hili la
Ayubu 1:6 kwenye Biblia ya the New Living Translation (NLT) inasomeka
hivi: “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele
za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.” Kwa kuongezea, lugha ya Zaburi 82:6-7 inafanya iwe wazi zaidi na
ijulikane kwamba hawa wana ni wakimbinguni, lakini ukweli huu umepotea kwenye
uelewa wa Ukristo wa sasa.
Mungu aliwatukuza
wana hawa kwa kupitia uweza wa Roho Mtakatifu. Ni kwa kupitia Roho Mtakatifu ndipo
Mungu huyu Mmoja na asiye na mshiriki aliunganika ma wana wake wa kiroho ili
kuiunda familia au baraza la Mungu, kama Elohim (SHD 430). Utajaji wa neno hili
“wana wa Mungu” wenye Kitabu cha Ayubu usingekuwa na maana kabisa iwapo kama
muundo wa kifamilia usingekuwepo kwenye baraza la elohim, na kama wana hawa
wasingekuwa na mwanzo wao kwa kuumbwa au kufanyizwa na Baba. Hata hivyo, wana
hawa wa roho walioumbwa wana Baba, na wana mwanzo wao kama viumbe wenye nguvu
wa Baba. Mungu Aliye Juu Sana ambaye jina lake ni Eloa (SHD 433), ndiye Baba
yao (Mithali 30:4-5). Kwenye Waebrania 12:9, anatajwa kuwa ni “Baba wa Roho
zote”.
Kwa kulielezea
kwa undani tukio hili la ajabu linalozunguka uumbaji wa wana hawa wanaoendelea
kuwepo wa kiroho wa Eloa, na
jinsi
wanavyounganika kwa kupitia Roho wake Mtakatifu, tazama majarida ya Jinsi Mungu Anavyofanyika Kuwa Familia (Na. 187) na Roho Mtakatifu (Na. 117) [How God Became a Family
(No. 187), and
The Holy Spirit (No. 117)].
Eloa aliweka
muundo wa familia kwa utaratibu mwandamano akianzia kwanza na familia yake ya
kiroho. Muundo wa familia ya mbinguni hatimaye uliowekwa kwenye muundo wa mambo
ya kawaida nay a kimwili pamoja na uwekaji wa familia ya mwanadamu. Ni muhimu
kuelewa mlolongo huu ambao kwao Eloa alipanga kuifanya familia yake yote, makundi
yote mawili, yaani wale walioumbwa kiroho na kimwili, na kuuelewa umuhimu wa
muundo wake. Aliweka kwanza familia yake ya kiroho na mpango wa wana wake ambao
kwa ujumla wawe na mtazamo chanya, upendo na uhusiano wa kufundisha kwenye
familia ya wanadamu, ambao waliumbwa kipindi cha mbele zaidi.
Waefeso 3:14-15 kwenye tafsiri ya Philips inasomeka hivi:
14
Kwa hiyo nampigia Baba
magoti, 15 ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni
na wa duniani unaitwa,
Eloa
alisababisha wanadamu kuumbwa kwa uwakilishi wa wana wake kwenye Baraza la Elohim
uweza wa kuianzisha familia ya mwanadamu “Na tumfanye mtu kwa mfano wetu” (Mwanzo
1:26) ni usemi unaoelezea uweza huu wa uumbaji uliotolewa na Eloa kwa kupitia
kwa Roho wake Mtakatifu kwa elohim kumuumba mwanadamu.
Ni kwa kupitia
kwa wana wake wa kiroho ndipo Bwana Mungu, Eloa alijifunua mwenyewe, asili yake
ya kweli na Torati yake kwa wanadamu. Wakati Mungu aliposababisha kuumbwa kwa
wanadamu, wana wake wa kiroho walipewa wajibu wa kuwa ni wajumbe na horo
watumikiao kwenye huduma yake kwa wanadamu (Waebrania 1: 14). Kwenye Matendo
7:35-38 tunaona kwamba ilikuwa ni Malaika huyu wa Bwana ndiye aliyeongea na
nabii Musa kwenye kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto na ndiye aliyewapa
Torati Israeli pale Sinai. Wana wa Eloa wanapaswa kuhudumu na kusimamia
maongozi ya Torati ya Baba yenye amri na maelekezo kwa mwanadamu.
Kwa hakika, ili
kuelewa muundo wa familia ulivyo kwenye familia ya kiroho ni jambo gumu sana
kuelewa sawa na kama ilivyo kuijua asili ya kweli ya Mungu Aliye Juu Sana
Mwenyewe, na asili ya watoto wake wa kiroho. Ingawa inapingwa na kukataliwa na dini
kongwe na za kale za Kikristo, Elohim ni jina lililo kwenye nafsi ya umoja na
siko ya Mungu mwenye nafsi ya uwingi inayojulikana kama Eloa inayowataja viumbe
wa mbinguni wenye mamlaka ya Mungu. Elohim anajumuisha wana wengi wa Eloa
wanaounda baraza la familia ya mbinguni (Ayubu 38:4-7).
Ni Eloa peke yake, Baba wa uhai na Mwanzilishi wa mpango wa familia, ndiye aliye na sifa ya kutokufa na ndiye asiye na mwanzo (1Timotheo 6:16). Ni yeye tu ndiye mwenye kujua kila kitu (Isaya 46:8-10), na haonekani kwa macho ya kibinadamu (Yohana 1:18; 1Timotheo1:17), na hakuna yeyote mwenye mwili aliyewahi kuisikia sauti yake wala kuliona umbo lake (Yohana 5:37). Tazama jarida la Mungu Tunayemuabudu (Na. 2) [The God we Worship (No. 2)].
Eloa ni Mungu wa miungu tunayemsoma habari zake kwenye Zaburi 136:2 kusema:
Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana
fadhili zake ni za milele.
Kwenye Isaya 46:9-10 tunasoma:
kumbukeni mambo ya
zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala
hapana aliye kama mimi; 10 nitangazaye mwisho
tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema,
Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Eloa ndye Mungu mwenyezi, aliye Mkuu na ni Baba wa wana wa kiroho, wakiwemo mwana wake wa kiroho aliyejulikana kwa wanadaamu kuwa ni Yesu Kristo. Masihi alimwambia Mariamu Magdalena baada ya kufufuka kwake kuwa, ufufuo aliomfanyia Mungu na Baba yake kuwa:
Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. (Yohana 20:17)
kwenye Yohana 20:17, Kristo anasema kwamba yeye ana Mungu, ambaye ndiye Baba yake. Ni suala tu linaloeleweka kuwa yeye aliye na Mungu hawezi tena yeye mwenyewe kuwa Mungu. Basi ni Baba peke yake, Eloa, ndiye aliyekamilika kwa sifa ya kuwa Mungu na ndiye ambaye peke yake hahitaji msaada wala ushauri na mamlaka nyingine ya juu yake. Yeye ndiye asili ya maisha yetu sote, yaani kwa ya aina zote mbili, yaani ya kiroho nay a kimwili. Maisha na uhai viliwekwa na huyu Mungu wa Pekee na wa Kweli, Eloa, ambaye ndiye baba wa Kristo pia, na Baba yetu sisi pia (Yohana 5:26). Amefunuliwa kwetu kupitia Kristo Mwana Wake wa pekee (Mathayo 11:25-27; Luka 10:21-22). Soma jarida la TUwepo wa Yesu Kristo Kipindi cha Kabla ya Kuzaliwa Kwake Kimwili (Na. 243) [The Pre-Existence of Jesus Christ (No. 243)].
Eloa ndiye Mungu wa Pekee na wa Kweli, ambaye ndiye pekee anayestahili kuabudiwa (Kutoka 20:3; 34:14; Mathayo 4:10; Yohana 4:21-24; 1Wakorintho 14:25; Ufunuo 4:8-11; 5:13-14; Ufunuo 22:8-9). Roho wa Eloah aliwezesha wana kuwa na uwezo wa kuwa miungu wadogo kwa kuzitenda kazi zake (Zaburi 82:1-6; 1Wakorintho 8:5).
Imani-dhana ya Waamini Utatu kuhusu asili
ya Mungu inatafsiri vibaya asili hii ya Baba na inazusha imani ya uwongo ya
kumuweka Elohim kwenye mtazamo wa kuwepo kwa hypostases watatu au
muunganiko wa watu watatu na kwamba wanastahili kufanyika na kuonekana kuwa
wanaumilele sawa na wana hadhi sawa na mamlaka kwenye muundo huu wa kiutatu. Ni
sawa na imani na mafundisho mapotofu ya Wabinitariani na Waditheisti wanayoendelea
kufundisha na kuamini siku hizi kuhusu asili ya Mungu kwa kudai kwamba kuwa
viumbe wawili wenye hadhi sawa ya kimungu katika Elohim mmoja. Imani na mafundisho haya ni ya makosa kwa
kuwa yanatafsiri vibaya familia ya kiroho ya Mungu. Wanakataa na kupinga ukweli
na uhalisia wa Mungu wa Pekee wa Kweli (Zaburi 82:1-8; Isaya 46:8-10) ikiweka
familia, kuanzia kwanza kwenye chimbuko la watoto wake wengi wa kiroho, kama
tunavyoona kwenye Ayubu 1:6, 2:1 na 38:4-7.
Dhana potofu
kuhusu asili ya Mungu pia inamzuia mtu asiujue mpango wa Eloa wa kujumuisha
uumbaji wa mwandamu kwenye familia ya Elohim. Ni hatima ya mwanadamu kwa
mapenzi ya Eloa kuwa afanyike kuwa mmoja wapo kwenye familia ijayo ya viumbe hai
wasiokufa. Wanadamu walioumbwa watapewa fursa ya kupewa uwezo wa kutokufa na
kuwa pamoja na Elohim wakiwa na Yesu Kristo (Zaburi 82:6; Yohana 6:51-58;
10:34; 1Wakorintho 15:22-27). Soma
jarida la Watakatifu Kama Elohim (Na. 1) [The Elect as Elohim (No. 1)] kwa mjadala wa kina kuhusu dhana hii ya mwanadamu
kufanyika kuwa mshiriki mmojawapo kwenye familia ya Mungu.
Majukumu
kwenye familia ya kiroho
Wana wa
Eloa wanapaswa kuwa na mikakati ya kusimamia na kufundisha Sheria au Torati ya
Amri na maagizo kwa mwanadamu. Tangu kipindi cha uumbaji wa Adamu na Hawa kwenye
Bustani ya Edeni, na kwa maongozi na maelekezo ya Eloa, watoto wake walipewa
majukumu ya kuwafundisha hawa ‘wazazi wetu wa kwanza’.
Maana ya neno miti ile iliyokuwepo Bustanini inatumika
kama neno linalomaanisha viumbe wa kiroho. Jambo hili limechanganuliwa kwa kina
kwenye jarida la Fundisho Kuhusu Dhambi ya Asili Sehemu ya
1, Bustani ya Edeni (Na. 246) [The Doctrine of Original Sin Part I The Garden
of Eden (No. 246)].
Kwenye Matendo
7:35-38 tunaona kwamba alikuwa ni Malaika wa Bwana ndiye aliyesema na Musa
kwenye kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto, na ndiye aliyetoa Sheria za
Torati kwa Israeli pale Sinai. Huyu Mwana wa Mungu alihitimisha au kukamilisha
kanuni na majukumu muhimu za kuwatumikia watu kwa maongozi na kumuwakilisha
Baba yake. Ni muhimu pia kumjua huyu Mwana huyu kuwa ni nani hasa na namna
alivyotumikia akiwa kama Mjumbe wa Mungu, anayetokea mara nyingi sana kwenye
Agano la Kale (soma jarida la Malaika wa YHWH (Na. 24) [The Angel of YHVH (No. 24)].
Waebrania 2:2 Kwa
hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. 2 Kwa maana, ikiwa
lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata
ujira wa haki,
Kinyume kabisa na
mafundisho ya Kristo, wahubiri na watumishi wa uwongo wanadai kwamba Sheria ama
Torati ya Mungu haina umuhimu na maana tena na haina umuhimu kuishika kwa siku
zetu hizi. Lakini tunaona jinsi Kristo alivyomjibu yule kijana alipomuuliza
swali kuhusiana na jambo hili kwenye Mathayo 19.
Mathayo 19:16-19 inasema:
Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema,
ili nipate uzima wa milele? 17 Akamwambia Kwani
kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika
uzima, zishike amri. 18 Akamwambia, Zipi? Yesu
akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, 19
Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi
yako.
Kristo mwenyewe
alisema kwamba hakuja kuitangua Torati ya Baba yake (Mathayo 5:17-19).
Waliojumuishwa
kwenye mjumuiko huu wa wana wa kiroho ni yule malaika aliyeasi ambaye hatimaye
alikuja kujulikana kwa jina la bilisi au Shetani
na Mshitaki wetu. Huyu mwana muasi alitenda mambo na kuwaza kinyume kabisa na
Mpago wa Baba yake. Kwa ubatili wake huu wa mawazo, alichukua fursa ya kuwa
mshitaki na mharibifu dhidi ya Mipango ya Baba yake kwenye familia ya kiroho na
kuwa na ushawishi chanya katika kuitumikia na kuiongoza familia ya mwanadamu kwenye
uhusiano wa haki na wakiutakatifu na Baba yao (soma Isaya 14:12-15; Ezekieli
28:14-19). Badala ya kuwa ni chombo cha haki na utakatifu cha kuilisha na
kuiendeleza familia yenye kudumu siku zote hadi ifikie kwenye kiwango
kinachohitajika kwenye urithi wa vipawa au cha Baba cha kuurithi uzima wa
milele kwenye muundo wa kiroho, Shetani amekuwa ni chombo cha kuleta mauti na
kuwa ni baba wa uwongo (Yohana 8:44).
Shetani aliwekeza
nguvu zake kwenye mkakati wa kuiangamiza na kuiharibu familia ya mwanadamu baada
ya jaribio lake lililoshindwa la kuuharibu na kuuangamiza muundo wa familia ya
kiroho. Alijaribu kukiinua kiti chake cha enzi juu zaidi ya nyota nyingine zote
(wana wengine) wa Baba yake (Isaya 14:14). Anaendelea kuwadanganya wanadamu hata
leo kwa kueneza mafundisho ya uwongo yanayoonekana kufanana na muundo wa
familia ya kiroho na kuwazuia wanadamu wasiijue asili ya Baba yao na asili
halisi ya Yesu Kristo na nafasi yake.
Alikuwepo
Bustanini na kuwadanganya wazazi wetu wa kwanza, Adamu na Hawa, ili wafanye
dhambi kwa kumuasi Mungu (Mwanzo 3:1-24). Soma jarida la Amri ya Kwanza: Dhambi ya Shetani (Na. 153) ;The
First Commandment: The Sin of Satan (No.153)].
Pia tazama
majarida ya: Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya 2, Kizazi cha Adamu (Na. 248) na Msalaba: Chanzo Chake na Maana Yake (Na. 39) [Doctrine
of Original Sin Part 2 The Generations of Adam (No. 248), and The Cross: Its Origin and Significance
(No. 39)] kwa kuwafanya wajadili kuhusu ulivyokuwa na maana
ya ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya kwenye Bustani ya Edeni mshitaki huyu
ametumia mbinu ile ile kufanikiwa kushawishi mawazo na nia za kidini za
wanadamu kuendelea kufikiri hivyo hadi leo.
Wakati Eloa
alipowatawanya watu na kuwaweka kwenye mipaka mbalimbali na kuwapa urithi,
aliwapa kila mmoja wa watoto wake wa kiume uwezo wa kuongoza na kuyaelekeza
mataifa Sheria au Kanuni zake, na jinsi ya kumuabudu yeye ambaye ndiye Mungu wa
Pekee na wa Kweli, na ambaye ndiye Baba yao. Mwana wake ambaye hatimaye alikuja
kuzaliwa kimwili hapa duniani na ambaye alikuwa na uweza wa kipekee wa kimungu
maishani mwake, yaani Yesu KRisto, alitumwa kwao Israeli. Kwenye Kumbukumbu la
Torati 32:8-9 tunasoma hivi:
Yeye Aliye Juu
alipowapa mataifa urithi wao, Alipowabagua wanadamu, Aliweka mipaka ya watu Kwa
kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli. 9 Maana, sehemu
ya Bwana ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake.
Ni huyu mwana wa
kiroho, Yesu Kristo, aliyewekwa wakfu tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu (1Petro
1:18-20) ili kuachana kabisa na wadhiwa wake wa kiroho wa kuwa na kufanyika
kuwa mwanadamu aliyezaliwa hadi kuweza kuishi maisha yasiyo na dhambi katika mwili
na hatimaye kutolewa sadaka. Alipewa wajibu mzito na wakuogofya ili kuyatoa
sadaka maisha yake ili kuwapatanisha wanadamu, wote wawili, yaani wana wa
kiroho Mbinguni waliotenda dhambi na idadi nzima ya wanadamu watenda dhambi.
Kwa kuyafuata
Maandiko Matakatifu tunajua kwamba wana wa kiroho walioanguka dhambini wa Eloa
wana fursa ya kutubu kutokana na dhambi zao na kuikubali dhabihu iliyotolewa
kupitia kwa Kristo kwa niaba yao kwa kusamehewa kwa dhambi zao.
Wakolosai
1:19-20 kwenye Biblia inayoitwa Complete Jewish Bible (CJB) kuwa:
Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; 20 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
Kristo alikwenda kuzimuni na kuwahubiria Malaika walioanguka dhambini na kuwekwa kifungoni huko Tartaros.
1Petro 3:18-19 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;
Na kwamba ndiko alihubiri kwenye kiwango cha kueleweka na umuhimu wa kila mmoja kupitia kwenye wokovu. Kwa hiyo mapepo wanaweza kuokolewa kama walivyokuwa (na kama walivyo) walengwa kwenye huduma ya Yesu Kristo. Ili kuelewa kwa kina zaidi kuhusiana na hilo, soma jarida la Hukumu ya Mapepo (Na. 80) [The Judgment of the Demons (No. 80)].
Ni kutokana na imani ya Kristo kwa Baba yake na utii wake kwake jambo lililomfanya ainuliwe juu kwa wenzake, amavyo ni juu ya wote ambao ni wana wengine wa kiroho wa Eloa. Zaburi 45:7 na Waebrania 1:9 vinamtaja Kristo kuwa ameinuliwa juu baada ya kufufuka kwake na Baba yake. Maandiko haya Matakatifu yanasema kuwa “Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio..”
Ukristo wa itikadi za kikale—yakiwemo na makanisa ya Mungu ya leo—wameshindwa kushikilia maana yaliyolengwa kwenye maandiko haya Matakatifu. Kitendo chao cha kuyaeneza dhana ya uwongo ya kwamba Kristo anasifa sawa ya umilele na Baba yake ni madai na mafundisho ya kipuuzi nay a uwongo yaliyochukuliwa kutoka kwenye fikra za kidunia za falsafa ya imani ya Kihellemism na Kinostiki iliyokubalika na kuaminiwa na ulimwengu mchanganyiko wa Wayunani wenye asili ya Kirumi mapema kabla ya kuja na kuzaliwa kwa Kristo kimeili hapa duniani. Kwa makosa kabisa alitangazwa kwenye imani yao kuwa yuko sawa na Baba yake kwenye muundo wa kiimani wa Waamini miungu Miwili au wa Binitariani kuhusiana na Uungu kwenye Baraza la kidini la Nicea lililoketi mwaka 325 BK. Baraza hili liligushi maamuzi ya Baraza la Chalcedon ya mwaka 451 BK ambayo yaliwaingiza Kristo na Roho Mtakatifu wa Eloa kwenye muundo wa Kiuungu. Na sasa Shetani anajaribu na kuendeleza mkakati kwenye jaribio lake na imani ya Kanisa lake lenye mchanganyiko wa Kiyunani na Kirumi ili kuharibu uelewa wote maarifa ya asili ya Baba yake na kusudi la kufanyizwa kwa familia ya Mungu.
Wana wa kiroho wa Mungu walioanguka dhambini wanajua ya kwamba huyu ni Mungu wa Pekee wa Kweli, ambaye ndiye Baba yao, na wanatetemeka mbele yake. Ndiyo kitu kinachowasubiria kwa ajili ya uasi wao na uvunjifu au uasi wa kanuni na mwenendho wao ambavyo kwayo inawafanya watetemeke. Yakobo 2:19 inasema: Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
Kristo haoni aibu kuitwa kuwa ni ndugu zake wa kike na wakiume wale wote wanaoitwa sasa na kuingizwa kwenye Mwili wa Kristo, kwa mujibu wa makusudi ya Baba yetu wa mbinguni. Waebrania 2:10-17 inasema:
Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake
na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu,
kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso. 11
Maana yeye atakasaye na hao
wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu
zake; 12 akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu
zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa. 13 Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena,
Tazama,mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu. 14 Basi,
kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki
yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani,
Ibilisi, 15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao
yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 16 Maana
ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. 17 Hivyo ilimpasa
kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye
rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu
wake.
Majukumu ya
Wazazi
Kutoka
mwanzo wakati Eloa alipowaumba hawa wana wa kiroho, alipanga kwa umahiri sana
kueneza kwenye mamlaka ya familia ya mwanadamu kupitia kwa mume wan a mke
Baraka zote za kuzaana na kuongezeka katika maisha ya mwanadamu na kulisha na
kuwalea watoto. Baraka ya inayofuatana na kuwa na familia inafanya na kusababisha
mwajibiko mkubwa na haipaswi kuchukuliwa kijujuu. Wazazi wanapaswa kuwafundisha
watoto wao kuwa wawe na uhusiano wa karibu na Mungu wa Pekee na wa Kweli, Eloa
na wazijue na kuzitii Sheria na amri zake.
Agizo la msingi
kuhusu majukumu haya ya wazazi limetolewa kwenye Kumbukumbu la Torati 6:4-9 ikisema:
Sikiza, Ee Israeli;
Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 5 Nawe
mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa
nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa
katika moyo wako; 7 nawe uwafundishe
watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo
njiani, na ulalapo, na uondokapo. 8 Yafunge yawe dalili
juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. 9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya
malango yako.
Wazazi wachamungu
wanapewa thawabu kuu kwa ajili ya mtoto mwenye busara (Mwanzo 27:46; Mithali
10:1). Msisitizo mkubwa umewekwa kwenye majukumu ya wazazi kuwaelekeza watoto
wao kuzishika na kuheshimu Sheria za Mungu (Kutoka 13:14; 20:10; Kumbukumbu la
Torati 11:19; Yoshua 4:6). Kwa upande wao, watoto wanawajibu na kupaswa kuwatii
wazazi wao. Kwenye uhusiano huu ni muhimu sana kujua kwamba kijineno kisemacho kutii kinapoandikwa mahali pengine
popote kwenye Agano la Kale kinachukulia kuwa ni kitu muhimu kwa mtu au au kile
ambacho ni tabia za lazima.
Eloa hakuumba
mtoto wake yeyote na kisha awaangamize. Bali anaumba kutokana na tabia na asili yake, ambayo ni upendo, na
anawalisha watoto wake kwa kusukumwa na upendo. Inawapasa wazazi pia kufuata mfano
wake. Na ndiyo maana kitendo cha kutoa mimba ni kibaya na kinachukuliwa kuwa ni
uuaji, isipokuwa pale tu inapoonekana kuwa mama atakuwa hatarini kama
haitatolewa. Sheria ua Torati yake Eloa inaendeleza na kufafanua asili yake na
yeye haui yeyote kati ya watoto wake. Uytoaji mimba unaofanywa kwa lengo la
kuzuia tu kuzaa mtoto kunaharibu lengo safi la kijamii na dhamira njema kwenye
jamii zetu.
Ni muhimu kwa
wazazi kuyaelewa maana neno “kuabudu” na matumizi yake yalivyo kwenye Maandiko
Matakatifu ili yaweze kuchukuliwa katika kuwafundisha watoto Yule anayestahili
wao wamuombe dua zao na kumuabudu. Kuomba dua ni namna mojawapo ya kuabudu,
jambo linalostahili kumfanyia Baba peke yake. Mathayo 6:6 tunasoma:
Bali wewe usalipo,
ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali
mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Shetani alimpeleka
Kristo jangwani ili amjaribu kwa kuahidi kumpa falme zote za hapa duniani iwapo
tu kama Kriisto angeinama tu chini ili kumsujudia. Shetani alikuwa anajaribu
kumtia majaribuni Kristo ili atende dhambi—na angetenda dhambi kama
asingesimama imara. Kristo alimkemea Shetani. Mathayo 4:10 inasema:
Ndipo Yesu
alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu
wako, umwabudu yeye peke yake.
Krisssto kamwe
hakuelekeza dua zake ama kumuabudu au kujitukuza mwenyewe. Kamwe hakudai kuwa
yeye ni Mungu. Bali kitu alichokifanya tu ni kwamba alijiita kuwa yeye ni Mwana
wa Mungu.
Yohana 10:36 inasema:
je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia,
Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?
Neno la Kiyunani
linaloelezea kuabudu ni proskuneo (SGD 4352) linalotokana na neno pros,
ambalo ni kuelekea, na kuneo, hadi kwenye busu. Neno Proskuneo linanekana mara kwa mara likimaanisha “kuabudu”
na lina maana tofauti. Linamaanisha kufanya kusujudu.
Kuonyesha kumheshimu mtu. Linatumika kama tendo la kuonyesha utii au
heshima kuu.
Kuabudu kunaweza pia kuelezewa kwa vebu mbalimbali za lugha ya Kiyunani. Nazo ni kama:
Tangazo la: (1) Tendo la kumuabudu Mungu halijaelezwa popote kwenye Maandiko Matakatifu. Kitecho cha kuzitilia maanani vebu za hapo juu kunaonyesha kwamba halikuhusiana na kusifu, kwa kiasi kikubwa linaweza kuchukuliwa kuwa ni utambuzi wa moja kwa moja kuhusu Mungu, kwenye asili yake, tabia zake, njia au namna zake na matakwa yake, iwe ni kwa kuonyesha kwa nje ya moyo kwa kumsifu na shukurani au kwa matendo yaliyofanywa kwa kutambua hivyo. (2) kwenye Matendo 17:25 therapeuo, "kutumikia, kumtumikia" (kwa hiyo RV), inasema "anaabudiwa."
(maelezo yaliyoko hapo juu yanatokana na kamusi maarufu ya Vine's Expository Dictionary of Biblical Words.)
Majukumu
kwenye Ndoa
Mungu aliweka muundo wa kifamilia kwa wanadamu na kumpa kipaumbele cha kwanza mwanaume na mwanamke wakiwa ni mmume na mke tangu wale wa kwanza (Mwanzo 2:24). Kwa kujibu wa amri ya Mungu, mwanaume anapaswa kuwaacha baba yake na mama yake na kuambatana na mke wake na kuwa mwili mmoja. Kwenye kitabu cha Mwanzo 2:25, usemi wa “Mwanaume na mke wake” ni mwongozo dhahiri wa uhusiano wa mwanadamu uliokusudiwa kuwa na mwanamke. Mwongozo huu wa Mungu unapingana na ushauri wa kwanza wa Mtume Paulo kuhusu mwanaume unaoonekana kwenye 1Wakorintho 7:6, kama inavyosema, “sio kwa amri,” bali zaidi sana ni kwamba ni wazo la kwanza tu la Pauulo khusisna na suala hili. Soma pia kwenye jarida la Ndoa (Na. 289) [Marriage (No. 289)].
Kutoka kwenye Mwanzo 1:26-28, tunaon pale ambapo elohim alimfanya mtu kwa sura na mfano wake. Tangu kuumbwa kwa mwanadamu haikuwa tu kwa sisi kufanana na Mungu kwenye mwonekano wa kimwili na viumbe wa mbinguni au elohim bali pia ilipangwa kuwa sisi tuwe kama miungu midogo au elohim kwa mchakato wa hatua moja hadi nyingine, kwa kupewa kwanza wajibu na elohim wa kuwalisha na kuwaelekeza wale walioumbwa kwa sura na mfano wake kwenye uhusiano wa kifamilia. Tunayajua hayo kutokana na maneno ya Kristo mwenyewe alisema, “Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? 35 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);” (Yohana 10:34-35), akinukuu kutoka kwenye Zaburi 82:6 inakosema: Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
Kwa hiyo, sisi tunaungana na ndugu zetu wa kiroho walio elohim, kuwa ni wana wa Mungu Aliye Juu Sana. Tukiwa ni viumbe wanadamu tuliofanyika kupitia Kristo. Kristo pia anajulikana kuwa ni kaka yetu, kwa hiyo ulikuwa ni uweza wa Baba yake ambaye ni Baba yetu pia, Mungu wake ambaye ni Mungu wetu pia (Yohana 20:17), hicho ilikuwa ndicho chanzo cha kuumbwa kwa mwanadamu.
Warumi 8:29 inasema: Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.
Sisi tunajulikana pia kama ndugu wa malaika wote waliobakia kwenye ulimwengu wa roho wa baba yetu wa Mbinguni.
Ufunuo 12:10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
Amri ya Mungu kwa mwanaume kwenye Mwanzo 1:28 ilikuwa ni kuzaa na kuongezeka kuijaza Nchi kwa njia ya kuzaa kunakotokana na mpangilio wa kifamilia ulioonyeshwa kwenye Mwanzo 2:24 mpangilio wa kuwa mume na mke. Je, ni kwa nini Mungu alimpa mwanaume amri hii? Mwanaume alitakiwa kujifunza kutokana na yaliyopo kwenye nchi anayoikaa duniani ambayo alitwaliwa kutoka kwayo, chini ya Sheria za Mungu, somo la kiroho kuhusu Ufalme au familia ya Mungu. Mfano wake ukiwa ni hizi Siku Takatifu ambazo ni siku za hapahapa duniani na nyakati zake ambazo hutufundisha masomo makubwa sana yanayoonyesha na kuashiria hatua ya Mpango wa Mungu katika kuwaleta watoto wa kimwili wa Mungu kwenye familia ya kiroho ya Ufalme wake. Kwa kuwa Mungu alianzisha utaratibu mkamilifu wa kijamii wa mume na mke, unaashiria taswira ya uhusiano uliopo kati ya Kristo na Kanisa ulioonyeshwa kwenye waraka kwa Waefeso ambako inasema hivi.
Waefeso 5:22-33 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana
wetu. 23 Kwa maana mume ni
kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa
mwili. 24 Lakini kama vile
Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila
jambo. 25 Enyi waume,
wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili
yake; 26 ili makusudi
alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate
kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo;
bali liwe takatifu lisilo na mawaa. 28 Vivyo hivyo
imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe
hujipenda mwenyewe. 29 Maana hakuna mtu
anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye
anavyolitendea Kanisa. 30 Kwa kuwa tu viungo
vya mwili wake. 31 Kwa sababu hiyo mtu
atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa
mwili mmoja. 32 Siri hiyo ni kubwa;
ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. 33 Lakini
kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi
mumewe.
Soma majarida ya Torati na Amri ya
Saba (Na. 260), Mithali 31 (Na. 114) na Wimbo Ulio Bora (Na. 145) [Law and the Seventh
Commandment (No 260); Proverbs 31 (No. 114) and Song of Songs (No. 145)].
Kutokana na
Maandiko haya Matakatifu tunaweza kujionea wazi kwamba Yesu Kristo aliwajibika kwenye
uongozi wa Kanisa, ambalo ni sehemu ya Mungu, familia ya Baba yetu. Wajibu wa
wanaume ni kuiongoza familia wakifuata mfano wa Kristo. Kristo anatajwa pia
kuwa ni Adamu wa mwisho (1Wakorintho 15:45,47). Hii inamaana kwamba Adamu wa
kwanza alikuwa na majukumu hayahaya, ila alishindwa kuyatimiliza.
1Wakorintho 15:45-47
Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa
mwisho ni roho yenye kuhuisha. 46 Lakini hautangulii
ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. 47 Mtu
wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. Thus it
is written,
Ni kwa kuwa Adamu
alishindwa kuongoza sawa na maelekezo aliyopewa kwa hiyo ilimpasa Kristo aje na
kuyatimiliza majukumu hayo. Kitendo
hicho kinaelezwa kuwa ni siri kubwa na Mtume Paulo.
Waefeso 5:29-32 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake
po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. 30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. 31 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake
na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. 32 Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena
habari ya Kristo na Kanisa.
Adamu wa kwanza
alipaswa kumchunga mke wake kwa namna sawa na vile Kristo alivyolitunza Kanisa
lake la kweli la Mungu. Adamu wa kwanza alishindwa, bali Adamu wa pili
amefanikiwa, sawa na tunavyojionea kwenye Mathayo 16:18.
Mathayo 16: 18 ….
nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Kristo ni mfano
wetu wa uongozi tunapoelewa kile ambacho wanaume wanachokitarajia kukifanya
kwenye mahusiano yao mema na familia zao.
Katika Efeso
5:23, tunaona kwamba mwanaume ni “kichwa cha mkewe”, ambavyo inamaanisha kwamba
ana mamlaka yote mawili pamoja na jukumu kwa familia yake yote, akianzia kwa
mke wake. Ni kwa bahati sana, kuna wanaumme wengi wanaoonyesha mamlaka yao lakini
pasipo kuonyesha maana yoyote ya uwajibikaji. Watu hawa wachache wamefanyika
kuwa sababu ya wanawake wengi kudai haki ya uhuru na kutotii miwajibiko yao na
kuuasi utaratibu wa muwajibiko wa kifamilia. Matokeo yake ya mwisho ni kwamba
familia inapata mateso kwa njia moja au nyingine, pamoja na jamii nzima yote
kwa ujumla. Ongezeko la kiwango cha matukio ya kuachana na kupeana talaka kunaonysha
mporomoko wa maadili kimataifa. Uamuzi wa kuachana ni machukizo na unamadhara
makubwa kwa watoto wetu na kunawasababishia kuteseka yakiwa ni matokeo
yatakayoishia kukumbukwa maishani mote.
Kutokana na 1Wakorintho
11:3 tunaona kwamba Mungu, Baba yetu alimpa mamlaka Kristo, na Kristo amewapa
mamlaka haya wanaume, na kwa hiyo wanaume wanawajibika kuwapangia kazi na mambo
yakufanya yaliyo wajibu wao wanawake ili kukamilisha malengo ya namna zote na
matarajio yanayohitajika kwenye familia (sawa na isemavyo 1Petro 3:7).
1Wakorintho 11:3 Lakini
nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke
ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. [yaani Baba].
1Petro 3:7 Kadhalika
ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo
kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu
kusizuiliwe.
Inawapasa wanaume
wagawe majukumu kama anavyofanya Mungu na Kristo wake. Haitakiwi mwanaume
azembee kwenye wajukumu yote. Adamu alizembea kuwajibika kwenye Bustani ya
Edeni. Hawa akaachwa akabiliane kujadilina na nguvu ambayo alikosa uwezo wa
kuishinda. Matokeo yake “milango ya mauti” iliimshinda mwanamke na kwa wanadamu
wote kwa ujumla (Mwanzo 3:1).
Wanaume wanapaswa
kuwaongoza wake zao na kuwafundisha watoto wao. Kwenye jukumu hili wanaume
wanatakiwa kuwafundisha watoto wao kwa namna ya mfano na kuitunza Kalenda ya
Mungu kiusahihi na kuwaelezea maana na umuhimu wa kutunza Sabato, Miandamo ya
Mwezi, Sikukuu zote na Siku nyingine Takatifu zilizoamriwa na Mungu.
Hebu na tuangalie
sasa uanzaji wa ndoa kama ulivyotiliwa mkazo na Yesu Kristo (Mathayo 19:1-12).
Mathayo 19:1-12 Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo, akatoka
Galilaya akafika mipaka ya Uyahudi, ng'ambo ya Yordani. 2 Makutano
mengi wakamfuata, akawaponya huko. 3 Basi Mafarisayo
wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa
kila sababu? 4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya
kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye,
ataambatana na mkewe; na hao wawili
watakuwa mwili mmoja? 6 Hata wamekuwa si wawili tena,
bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. 7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya
talaka, na kumwacha? 8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya
ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo
haikuwa hivi. 9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu
atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine,
azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. 10 Wanafunzi
wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. 11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno
hili, ila wale waliojaliwa. 12 Maana wako matowashi
waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi
waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa
matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na
alipokee.
Kwenye aya ya 5, Kristo
anasema kwamba wanaume na wanawake wanatakiwa waishi maisha yenye uhusiano wa
mke na mume mmoja tu “na wawili hawa watakuwa mwili mmoja”, sio watatu au zaidi
ya hawa wawili, na ni kwenye mambo ya ndoa tu, “ataungana na mke wake”. Kristo
anafafanua pia kwamba mwanaume na mke wasiendelee tena kufanya mambo yao kiufichouficho
na ubinafsi na wanapaswa sasa kuishi kwa mtindo wa watu wenye hisia mbili, kama
inavyosema kwa wazi aya ya 6 kwamba: “nao sio wawili tena bali ni mwili mmoja”.
Na kwa kuwa ni kifo tu ndicho kitakachomtenganisha mtu kutoka kwenye kifungo
hiki cha kimwili, na ndiyo maana ndiyo maana umewekwa utaratibu huu wa mke na
mume mmoja na Kristo.
Kwa ajili hii,
Mungu ameamuru kwamba kila aina yoyote ya muunganiko wa kingono nje ya ndoa hii
iliyohalali ni dhambi na uasi na ni kinyume kabisa na maisha wanayopaswa kuishi
kwenye familia ya Mungu. Iwapo kama mtu atakiuka na kuiasi Sheria hii ya Mungu
na kuamua kuuandama kukahaba au uzinifu, matokeo yake yako wazi kwa kila mtu,
ambapo kwamba ataumbuliwa kwa kukumbwa na magonjwa na kuendelea kuyaandama
maisha yasiyo ya uaminifu tena kwenye ndoa kiasi cha kufikia kufanya matendo ya
kuzalisha watoto wa kuuza kwenye masoko ya magendo, na matukio mengine ya
kusikitisha ya utoaji mimba na kuua vichnga. Moja wapo ya mapatilizo an madhara
ya kuendekeza ngono za uzinifu nje ya ndoa na moja ya sababu za maadili kupua
kwenye jamii na uharibifu mkubwa imeelezewa
vizuri kwenye makala ya Familia kwenye
Biblia ya the International Standard Bible Encyclopedia (ISBE) kwenye
kifungu kinachoiongelea amri ya 7 ikisema.
“Wakati iliwa ni
kweli kwamba kwenye sheria za uhusiano wa kingono katika Israeli kwa mtu anayetenda
dhambi hii nje ya mahusiano yaliyopo ya kifamilia alitendewa vikali ili awe
mfano kwa wote, na tena tunapokumbuka ni mapema kiasi gani maishani ndoa
ilifanyia katika siku hizo za kale, na pia uchumba kwenye umri wa utoto
ulivyochukuliwa kuwa ni kitu kitakatifu sawa tu na kama ilivyokuwa ndoa, tunaona
kwa sasa juhudi za kuifuta amri ilikuwa iko kwenye kiwango cha juu cha
kimataifa ingawa ni kitu kilichosaidia kwa kiasi kikubwa kuzilinda familia.
Familia ni taasisi iliyoanza aiku nyingi sana nay a kwanza na inayomfanya
mwanadamu kuwa-na uwezo mkubwa na kutakasika sana. Ni kwa taasisi hii ndipo
amri hii inasimama kuisimamia. Inawazuia watu wasiivunje na kumfanya mtu
aondolewe na kutengwa mbali na uharibifu na upweke. Hebu fikiria jinsi watoto
wote wanavyozaliwa, na unataswira kiwango kidogo alichonacho cha unyama ambacho
mambo yote yanayohusu majukumu ya kijamii ya kibaba yakiondoka, na ikiwa hata
yale ya umama yakipungua kwa kufanya malezi na uangalizi wa kawaida tu katika
kipindi kifupi tu kijacho ns kumuacha akiwa ni kichanga kisicho na msaada tena.
Hebu na ujiulize sasa kwamba ile dhana ya kuwa ndoa itakuwa ni kitu cha watu
wote na kwamba watoto wanaozaliwa kwenye ndoa wanapaswa kushikamana nayo kwa
umakini mkubwa nawe sasa una mbingu mpya na nchi mpya kwenye kupapatikia ngono ya
wanadamu wasiojali.”
Kwa mujibu wa utaratibu
wa mafunzo wa Mungu wa mambo ya kawaida ya kimwili yanayowakilisha mambo ya
kiroho, maongozi ya kifamilia waliyopewa wanadamu yanakuwa ni mafundisho pia
yanayoelekea uhusiano wa kiroho ulio kati ya Malaika walio na umoja na Baba na
hadi kwake.
Mungu amempa
mwanadamu wajibu wa kuzaana na kuongezeka: Mungu
akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na
kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe
chenye uhai kiendacho juu ya nchi (Mwanzo 1:28). Kwa hiyo, kwa ajili hii, mwanaume ana wajibu mkubwa wa
kuieneza na kuikuza familia ya Mungu kwa kujifunza uhusiano wa kibaba ba
kiumama katika kuwalisha watoto, kuwafundiisha Sheria za Mungu na kuwaongoza
wafuate njia hiyohiyo ya kuwafanya watoto wao kuwa wazazi na mababu wazuri kutoka
kizazi kimoja hadi kingine wakiwa kwenye malezi ya ndoa ya baba ba mama mmoja.
Hebu na tuone sasa
uhusiano wa kila mmoja wao kama Mungu alivyokusudia kwenye uumaji wake wa vitu.
Jukumu la Baba
Jukumu la baba
kwenye familia ni kuwa kama mwakilishi wa Mwenyezi Mungu na Baba. Wajibu wake
ni kuwa mleta mahitaji na huduma zote kwa mahitaji yote ya kifamilia, kuweka
mahusiano mema na kusimamia masuala yote ya kiroho.
Sio jambo dogo
kama baba atakataa kutoa mahitaji kumhudumia mke wake na watoto, kama
tunavyoona kutoka kwenye makemeo ya Mtume Paulo kuhusu wale wasiojali kuhudumia
familia zao kwa kuwapatia mahitaji yao.
1Timotheo 5:8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio
wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko
mtu asiyeamini.
Hii inaonekana pia kwenye madhihaka ya Sulemani
anapomdhihaki mwanaume mvivu akimhamasisha awe mchapakazi kwenye Mithali 6:6-11.
Wakati majukumu ya mleta mkate yanapotolewa kwa baba hapo
Mungu alupomwambia Adamu kuwa atapata mkate kwa jasho uso wake (Mwanzo 3:19), anawajibika
pia na hawezi kukataa ama kupuuzia utoaji wa huduma za kiroho kwa familia yake.
Kabla ya kuwekwa kwa huduma za kikuhani katika Israeli, baba
alikuwa na jukumu la kutoa dhabihu za wanyama kwa ajili ya familia yake, kama
tunavyouona mfano wa Ibrahimu kwenye Mwanzo 12:8 na kwenye Ayubu 1:5. Akiwa kama mkufunzi-mwenza pamoja na mama
wa watoto, baba amepewa jukumu kubwa wa kuiongoza familia kwa kuifundisha
Sheria na maelekezo au kanuni za Mungu (Kutoka 12:26-27; Kumbukumbu la Torati
6:6-7; Mithali 22:6; Waefeso 6:4).
Kumbukumbu la Torati 6:6-7 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika
moyo wako; 7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na
kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na
uondokapo.
Waefeso 6:4 Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na
maonyo ya Bwana.
Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye
hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Kiongozi wa
kiroho, ambaye bi baba, ana wajibu kama mlinzi wa kiroho wa kuwaelimisha dhidi
ya matendo maovu na tabia za dunia zinazofanyika na kuonekana kuwa za kawaida
na kuchukua kipaumbele kwa watoto wetu na marafiki zao, wanapokuwa wanatenda
mambo yaliyo kinyume na maelekezo ya Torati ya Mungu.
Warumi 16:19 Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu,
lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo
mabaya.
Ikiwa tutakuwa
hatuna hatia kwenye mambo mabaya na kuwafundisha watoto wetu hivyohivyo ndipo
itatupasa kuwakataza wasijihudhurishe kwenye kila aina ya mambo ya burudani
kwenye vituo vya runinga, michezo ya kuigiza au picha za video na kuangalia
wavuti za Intanet zilizo kinyume na Sheria za Mungu. Ni rahisi kutumia vyombo
vya habari na mawasiliano vya kisasa na maonyesho ya burudani na kuvifanya
mbadala wa wazazi, lakini hata kama jumbe zake zikiwa murua, kila moja ya hizi
zinapoingia bado zitafanya mchosho kwenye tabia za mtoto. Soma jarida la Mitindo ya Ibilisi (Na. 42) [The Devil's Designs
(No. 43)].
Kwenye jukumu
hili la kuwa kiongozi wa kiroho pia kunakuja na wajibu wa kuwaadibisha watoto.
Tunajifunza kutoka kwenye Zaburi na Mithali kwamba watoto hawana asili ya
kurithi mambo mema, na kwamba kwa asili wana tabia tafaruku za kupenda kufuata
tabia na matendo maovu kama ilivyo tabia iliyoko kwenye kila mwanadamu. Daudi
alikiri kufanya dhambi hii asilia ya kibinadamu ambayo ilianza kutoka kipindi
cha kuzaliwa kwake.
Zaburi 51:5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya
uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
Aya nyingi zilizo
kwenye kitabu cha Mithali zinalitaja hitaji na umuhimu wa kumuonya na kumkanya
mtoto aziache njia zake mbaya za dhambi.
Mithali 22:15 Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia
mbali.
Mithali 23:13-14 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana
ukimpiga kwa fimbo hatakufa.14 Utampiga kwa fimbo, Na
kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.
Kwa kuwakanya
watoto wetu kwa kutumia fimbo ya kuwakanyia tunayotakiwa kuwapiga kwa upendo
basi sio tu kwamba tutakuwa tunayaepusha maisha yao au uhai wao usiingie
kaburini kabla ya umri wao, bali pia tunakilinda kizazi chetu au hata na wajuu
zetu pia.
1Samweli 3:13 Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili
ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia.
Kila mtoto anatakiwa afundishwe kwamba anatarajiwa na wao
na pale ambapo mipaka hii inawekwa, ni sawa kama baba yetu wa mbinguni
anavyotufanyia sisi kwa kutupa Sheria zake. Mara tu baada yam toto
kutahadharishwa juu ya viwango hivi ndipo ahdabu inatakiwa itolewe, kwa ajili
ya kukiuka na nilazima ajulishwe kwanza na aliue kosa lake, vinginevyo mtoto
atakuwa na tabia ya kutoiogopa haki na kuwaheshimu walio na mamlaka. Kumkanya
mara kwa mara kutamfanya ajue kuwa Baba yetu aliye Mbinguni anamaanisha kile
anachokisema, na kwamba hafanyi hukumu isiyo ya haki na kumuonea mtu. Kwa
mujibu wa Maandiko Matakatifu ni kwamba, ili kuruhusiwa na kushika njia yenye
upinzani mdogo pale maonyo yanapotakiwa kufanyika, ni chanzo cha kuchukizwa kwa
watoto wetu.
Mithali 13:24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi
mapema.
Ni wazi kabisa
kwamba baba anawajibika kuwazuia watoto wasitende dhambi na tabia za namna hiyo
kwa kuwaadhibu.
Kwa mfano
tunaojifunza kwenye kitabu cha Waamuzi ambao tunaona kilichotokea mababa
wachamungu waliposhindwa kuwafanya watoto wao wamche Mungu.
Waamuzi 2:10-22 inasema: Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa
waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua
Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
11 Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za
macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali. 12 Wakamwacha
Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata
miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote,
wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha Bwana, akaghadhibika.13 Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi. 14 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia
katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya
adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao. 15 Kila walikokwenda mkono wa Bwana ulikuwa juu yao
kuwatenda mabaya, kama Bwana alivyosema, na kama Bwana alivyowaapia; nao
wakafadhaika sana. 16 Kisha Bwana
akawainua waamuzi, waliowaokoa na mikono ya watu hao waliowateka nyara. 17 Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya
uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka
upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana bali
wao hawakufanya hivyo. 18 Na wakati Bwana
alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na
mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili
ya kuugua kwao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua. 19 Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi
nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili
kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za
ukaidi. 20 Basi hasira ya Bwana ikawaka juu ya
Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili wamelihalifu agano langu
nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu; 21 mimi
nami tokea sasa sitalifukuza taifa mojawapo la hayo aliyoyaacha Yoshua
alipokufa; 22 ili kwa njia ya hayo nipate kuwajaribu
Israeli, kwamba wataishika njia ya Bwana kwenda katika njia hiyo, au sivyo.
Katika tawala za
dunia yetu leo, Ukomunisti, Usoshalisti na hata na Udemokratiki/Urepacliki
vimeipa Nchi wajibu wa kuwaelimisha watoto walio kwenye mataifa yao, na
wameenda hatua zaidi kwa kutumia sheria ili kudhoofisha wajibu huu wa baba
kwenye familia kwa kumuondoea mamlaka yake kwa watoto wakiwa kwenye umri mdogo.
Kitendo hiki kimeondoa jambo la msingi na muhimu kwenye jamii na kuliweka mbali
sana na familia na kuwaweza karibu na mtu mwingine. Machapisho yetu, vyombo vya
habari na hata shule zetu vimekazana sana kuwekeza dhana hii potofu ya kila mtu
kuwa bora na hahitaji wa kumuonya, na huku serikali zetu zikisaidia mkakati huu
kwa kupitisha sheria zinazolenga kulidhoofisha wajibu huu muhimu wa baba na
mama kwenye familia. Matokeo yake, hesima na utiifu wa watoto kwa wazazi wao
umepungua, huku kukiacha ubaradhuli mkubwa wa kimatakaba ya watu kwenye taifa,
licha ya kihoro kikubwa kilichofanyika kutokana na mtenganisho mpangilio
maalumu wa majukumu ya kifamilia na utaratibu aliouweka Mungu kwa viumbe wake.
Kwa uasi huu
ulioongezeka dhidi ya uadibishaji majumbani, ongezeko la uzembe na ukengeufu
vinajitokeza, ambavyo ni matokeo ya kuonbgezeka kwa kiwango cha upungufu wa
utajiri au mali zilizotunzwa kwa ajili ya watoto kwa kazi za mikono ya baba zao
na babu zao. Ni kizazi kidogo tu kilichopo na mamlaka ya mababa zilizopotea, na
jamii inaanza kupungua nguvu zake kwa kwenda chini.
Maandiko ya Charles
de Ribbe kwenye kitabu chake cha Le Play’s studies kwenye sehemu aliyoiandika
kuhusiana na mwili wa binadamu anaweka msisitizo linganifu wa kizazi hiki cha
familia iliyopungukiwa na mamlaka kamili na serikali zetu zinazounga mkono hali
hii akisema.
“Kama tukirudisha
mamlaka kwa baba, basi tutairudisha upya huduma ya Mungu kwa utaratibu wa muda
nfupi…. Kadiri muda unapopita zaidi, ndipo tunapojua kwamba ni muhimu kurudisha
mamlaka kwenye familia. Haiwezekani kuiweka serikali bora kwa kutumia kanuni zenye
makosa zilizofanywa na wanadamu. Kwenye nchi iliyo na huzuni ambayo tunajikuta
sisi wenyewe, wokovu unaweza tu kuja kutoka kwenye mamlaka ile iliyomahiri na
iliyoungana, ambayo inaheshimu sheria asilia, na kubakia tiifu kwa watumishi
wake saidizi. Ni mamlaka ya kifamilia tu ndiyo inaweza kuhitimiliza hilo ambalo
ni kipaumbele na bora zaidi kulazimisha kila mamlaka ya watu iliyoko.”
Maandiko
Matakatifu yanaweka wazi kwamba mipakai ya mamlaka imewekwa na Mungu na ni ya
muhimu katika kuimarisha familia na nchi.
Warumi 13:1-7 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa
Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo
amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao
watajipatia hukumu. 3 Kwa maana watawalao
hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya.
Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; 4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako
kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga
bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili
ya ghadhabu. 5 Kwa hiyo ni lazima
kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri. 6 Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa
kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo. 7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi;
mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.
Onyo kutoka kwa
Mungu linakuja kwa kupitia nabii wake Malaki kuhusu kizazi hiki cha wanadamu.
“Angalieni,
nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na
kuogofya. 6 Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee
watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia
kwa laana.” (Malaki 4:5-6)
Ni wazi kabisa
kutokana na aya hii kwamba mababa na watoto wao katika siku za mwisho
watashindana na kuchukiana na watapoteza mwelekeo wa uhusiano wao ambao
uliwekwa na Mungu kwa kuzishika Sheria zake, na kwamba nabii Eliya alitabiriwa
kuwa atakuja na ataileta kweli hii ya muundo wa kifamilia na kuurudisha tena
Maisha ya baba ni
mfano wa kile watoto wanachotakiwa kufanya na kwamba mabinti wanatakiwa kuomba
kuwapata wa kuwaoa. Mwanamume ni nguzo ya mamlaka kwa familia na ni mfano wa
kweli wa Mwenyezi Mungu, ambaye ni Baba wa wote wenye mwili. Baba kwa mamlaka
aliyopewa na Mungu, ni muhusika wa usalama wa maisha ya watoto wake na ni
mhusika muhimu kwenye unusurishaji wa maisha, ni kama Mungu Baba
anavyotushughulikia wakati wote. Sambamba na hilo, watoto wanakuwa wametakaswa
kutokana na busara yake na kwa mafundisho ya Torati (2Nyakati 13:18; Yohana
17:19; 1Wakorintho 7:14). Yeye ni mfano
wa Mungu Baba wa wote na anatakiwa aenende kwa mfano wa sifa hii akiwa ni
mwakilishi, kama mhusika na ustawi wa maisha na mhusika kuhakikisha ustawi wa
maisha hayo kwa kuwalea kwenye kumjua na kumpenda Mungu na baba wa Milele. Watoto hawa wataonekana kuwa ni taswira
njema kwa muumba na baba yao kwa maisha ya mfano waanayoyaona kwa baba zao. Soma jarida la Ukristo na Malezi ya Watoto (Na. 186)
[Christianity and Childrearing (No. 186)].
Jukumu la Mama
Jukumu la mama ni
yeye ndiye anayenyonyesha na ndiye mtu ambaye uhai wa mtu unaanzia. Baba na
mama ndiyo wanaowezesha kupatikana kwa watoto, ni mfano wa kama Baba na Mwana
wake walivyoumba mtu hapo mwanzo. Mungu akasema, “Na tumfanye mtu kwa mfano wetu,
kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama,
na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa
mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” (kutokana na Mwanzo 1:26-27). Kila mtoto
aliyezaliwa ameumbwa kwa mfano na sura ya baba na mama yake wa kimwili
Kwenye Yohana 1:3-4
inaongelea kuhusu wana wa Eloa, ambaye ni neno la Mungu, “Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye
hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 4 Ndani
yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.” (LITV). Kama Baba Mungu alivyompa uhai mwanadamu
kupitia Neno, ndiposa pia kwamba baba ni mtoa uzima anayepitia mwili wake kwa
watoto kupitia kwa mama. Kisha mama anachukua jukumu kubwa la kumpa uhai mtoto
kwa kumbeba kwenye mimba tumboni kwa kipindi chake cha kuwa kiumbe cha tumboni,
na kuendelea kuaribu mkubwa kwa hiki kiumbe kichanga ambacho kwacho anatakiwa
akitunze hadi kipate uzima. Na mara anapozaliwa tu, ndipo anakuwa na jukumu la
kuhakikisha anamtunza kwanza na anafanya hivyo kwa kumnyonyesha mtoto na
kumlisha na kumchangamsha akihakikisha kuwa mtoto anakua akiwa na hali njema
ambaye hatimaye anaweza kumrithi au kuchukua mahala pa baba yake au mama yake
kwenye kazi hii ya majukumu ya kiuongozi ya uzaaji na ufundishaji kama
ilivyofanyika kwenye familia yao.
1Timotheo 5:14 Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani;
ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu.
Mithali 29:15 Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana
aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.
Kutokana na fungu
hiki la maandiko la kitabu cha Mithali tunaona kwamba ni wajibu wa mama
kuelimisha watoto washike Sheria za Mungu kama sehemu ya malezi ya mtoto.
Akikosa kufanya hivyo atajiletea aibu hatimaye.
Kwenye miaka ya
mwanzoni ya maisha ya watoto, baba humsaidia mama kwenye majukumu ya utunzaji
na kumlea mtoto sambamba na kuwa mshauri na kuwa chanzo cha kuitia familia.
Kadiri watoto wanapoendelea kukua na kuendeleza jukumu hili la kielimu ndivyo
itakavyokuwa pia kwamba watoto watakuwa wakivutiwa sana na baba yao zao na dada
zao na mama zao. Kila maendeleo yam toto yatashamirishwa na umoja kati ya baba
na mama. Kuna mengi ya kufaidika kwenye uimara na ulinzi wa maisha ya watoto
kwa kushuhudia upendo wan je na kushuhudia matendo ya mume anavyomfanyia
mkewake na akifanya hivyohivyo kwa kumletea zawadi na kumuonyesha upendo kila
siku kunaweza kuwafanya wengine wajione kuwa ni wa muhimu na waaina yake na
wanapendwa.
Sambamba na hali hii ya kushirikishana majukumu ya kuwalea watoto, mama/mke pia anawajibu wa kuyatunza na kusimamia mambo ya nyumbani kwenye familia yake, ambayo ni pamoja na kuweka vitu kwenye mpangilio wa kupendeza na kuandaa chakula chenye virutubisho na afya njema na kwa mujibu wa maagizo ya Torati na Sheria za Mungu. Anamsaidia pia mume wake kwenye masuala ya utoaji zaka, kuzitii Sheria na Torati ya Munguna maandalizi yenye kuhakikisha kuwa wanazitunza Sabato za Mungu vizuri na kwa utakatifu wake. Soma jarida la Jukumu la Wanawake wa Kikristo (Na. 62) [Role of the Christian Woman (No 62)].
Jukumu la Watoto
Majukumu
yam toto wa kiume na wa kike ndiyo yanayowafanya hatimaye na wao wafanyike kuwa
baba na mama, na hatimaye wawe babu na bibi. Ni mchakato unaowapelekea wawe
wanafunzi kwanza na hatimaye kuwa waalimu. Kwa namna hiyohiyo wanadamu
wanafundishwa na Mungu ingawaje watoto hawa wa kiroho au elohim haya wafanyike
kuwa wasaidizi wazuri, yaani elohim. Hii inaweza kuwa ni taswira kwa jukumu la
wengine, yaani anaweza kuwa ni kaka yake mkubwa au dada yao mwenye mamlaka
yanayoendelea kutoka kwa wazazi wao ya kuwasaidia kuwaelimisha wadogo zao
kwenye familia yao. Wakati mamlaka haya yaliyotolewa kwa kaka au dada mkubwa
yanapotumiwa vibaya kwa kuchukuliwa kijuujuu bila kutilia maanani au hata
yanapodhalilishwa, yanaenda sambamba na kitendo cha kuwaadhibu wana wa kiroho
wa Mungu wanapoasi. Kiongozi mkubwa wao anapokuwa mzembe kwa kupuuzia na
kutotilia maanani mamlaka yachukue mkondo wake kwa kiwango cha kumaanisha
kabisa, inaweza kufananishwa na jukumu alililolifanya kaka yetu mkubwa Yesu Kristo.
Baba yetu wa Milele anapenda utii (1Samweli 15:22). “Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za
kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni
bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu”. Na anapendu kuwa waonyeshwe utii mababa na wamama kutoka kwa watoto wao
moja kwa moja ameagiza hili kutoka kwenye Amri ya Tano (Kutoka 20:12 na
Kumbukumbu la Torati. 5:16, sawa na Waefeso 6:2-3).
Kutoka 20:12 Waheshimu
baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na
Bwana, Mungu wako.
Kumbukumbu la Torati
5:16 Waheshimu baba yako na mama yako; kama
Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate
kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
Kwa ajili ya
asili ya kimaumbile iliyopo kwenye upendo unaoendelea kwa mtiririko ukitokea
kwa Baba kwenda kwa watoto wake, umuhimu wa Amri hii ni mkubwa sana kuliko kazi
ya wazazi kwa watoto wao.
Baba ametajwa
kwanza hapa kwenye mifano hii miwili, ila mama ametajwa kwenye Mambo ya Walawi 19:3:
Kila mtu na amche
mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi Bwana, Mungu
wenu.
Kwenye aya zote
tatu, baba na mama wanachukuliwa na kuonekana kuwa wako sawa. Baraka za mama ziko
wazi, na yeyote anayemtii na kumheshimu baba anazipokea sawa na kwa kumfanyia
mama. Yuko sawa na anapokea stahili sawa za kuheshimiwa kulikoamriwa kwenye
amri ya Mungu.
Agano Jipya pia
linasisitiza kuwatii wazazi kufanywe na watoto wao.
Waefeso 6:1 Enyi
watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
Wakolosai 3:20 Ninyi
watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza
katika Bwana.
Soma pia jarida
la Torati na Amri ya Tano (Na. 258) [Law and
the Fifth Commandment (No. 258)].
Amri hii ya Mungu
ya kuwaasa watoto wawatii wazazi wao kwa ahadi ya kuongezewa siku zao hapa
duniani, Mungu anatuagiza hata sisi pia. Mapatilizo ya kumuasi Mungu kwa
kuidhihali Amri hii nay a kutowatii wazazi wetu ni maisha yetu kufupishwa hapa duniani.
Kumuonyesha mzazi kutomtii, kwa Mungu ni dhambi na kosa bay asana.
Kutoka 21:15 Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.
Utii na heshima
iliyoagizwa wafanyiwe wazazi, ndyo hiyohiyo pia iliyoamriwa kufanyiwa mababu na
mabibi wakubwa.
Mambo ya Walawi
19:32 Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu
wako, Mimi ndimi Bwana
Wakati kijana
anapokoacha kutii na kujionyesha kwenye jamii kuwa anamajivuno au kuzidharau
sheria kutowaheshimu wala kuwatii wanaostahili kupewa heshima na wazee ndipo
jamii isiyojali na isiyo na utaratibu inajikita hapa duniani.
Isaya 3:5 Nao watu
wataonewa, kila mtu na mwenziwe, na kila mtu na jirani yake; mtoto atajivuna
mbele ya mzee, na mtu mnyonge mbele ya mtu mwenye heshima.
Jukumu la Bibi
na Babu
Mababu na mabibi
wana majukumu ya kuiwezesa familia iendelee vizuri na kuiefanya iendelee na
bidii ya kuziheshime Amri na Sheria za Mungu sawa na mazingira waliyolelewa
kwayo na kufundisha. Wanawajibika kuifanya familia ijikite na kuendelea
kuzipenda Sheria za Mungu ili kuifanya isisobwe wala kuyumbishwa na mawimbi
mengine ya kimafundisho ya uwongo ya kidini kwa pande hii hadi ile nyingine na
desturi au mapokeo ya wana wa dunia hii.
Mababu na mabibi hawa
wana wajibika kuhakikisha kwamba watoto wao wanaendele kudumu kwenye njia
nyembamba na kuwaongoza watoto wao kwenye maongozi ambayo vizazi vyao
vilivyopita walilelewa kwayo.
Kwenye kizazi cha
hivi karibuni aha jamii za kimagharibi za Kimarekani na ongezeko la famila kubwa
za watu wanaoishi pamoja na kutembeleana, watoto wameanza kujitenga na wazazi
wao mara tu baada ya kufikia umri wao wa ujana. Wakati jamii inapochukua hatamu
za familia zao, watoto wetu watapelekwa mbali mashuleni kwa ajili ya kupata
elimu ya juu, ambako wataanza mchakato endelevu wa kuwatenganisha na maisha ya
kifamilia ambayo ndiyo ilikuwa kiini cha na msingi wa kumfundishia Sheria za
Mungu. Utaratibu huu unaoanza na kuchukua hatamu hatimaye unaendelea hadi
kwenye kipindi cha ajira ya mtu, na hata kama ajira itakuwa ni ya kwenye jamii
ile ile. Mwajiriwa anakuwa ndiye wa kulaumiwa au kuondolewa wakati matatizo yanapotokea
kwenye kazi yake ya wakati huo. Na ndipo anatafuta maeneo mengine ya kupata
ajira mpya au kujiajiri mwenyewe, na hapo ndipo anaweza kuichukua au anasiweze
kuichua familia yake na kwenda nayo pamoja naye. Wakati mwingine mtenganiko huu
wa familia na baba unachukua kipindi cha miezi kadhaa, kisha unachukua miaka, hatimaye
inafikia hata utelekezaji na hatimaye unaishia kwenye kuacbana na kupeana
talaka ambayo inaigawa katikati hata familia ya watoto wengi yenyewe.
Kwa kukosekana
familia za wengi kuishi pamoja kwenye jamii zetu ambayo ndiyo umti wa mgongo
kwenye ukoo, kabila, na hata taifa, ndyipo tunaposhuka chini kwenye maadili ya
kupendana na kuzua chuki na hali ya kuwa watu tuio na heshima na adabu, jambo
ambalo limeonywa sana kwenye Isaya 3:5. Kweye familia zinazokaa pamoja kwa
kundi watu wake mali na raslimali zote stahiki huwa chini ya mamlaka ya mababu na
wanaacha wafe wakiwa mbali na watoto na wajukuu zao ambao walikuwa
wakiwategemea. Na kwa kuwa walikuwa wanakosa upendo na taabu zilizosababishwa
na kizazi chao, na kuamua kuondoka na kwenda mbali siku za mwisho huku waakiwaacha
watoto waliowazaa kwenye nyumba za ndugu zao wa zamani. Kwenye mifano kadhaa
mingine kutokana na udhaifu wa akili na kimawazo na hali mbaya ya kiafya, masuala
mengine ya kiuangalizi kama vile vifaa vya kulishia vinatakiwa wasaidiwe, bali
dhana kuhusu wazee walioko kwenye jamii zetu kuonekana kama wasio na umuhimu na
kero kwenye familia za kimakundi inaendelea kukua zaidi na zaidi na kuonekana
kuwa ni kitu marufu. Madhara yanayotokana na kupuuzia kuishika Amri ya Tano
yanazidi kujitokeza na kuonekana kila mahali na siku za kuishi watu hapa duniani
zinazidi kupungua katika kila aina ya jamii za watu ambazo zinaendelea
kuipuuzia na kuivunja Sheria hii ya Mungu.
Urudishaji
mtazamo wa kuwaheshimu wazee walio kwenye familia zetu kwa kuwajali na
kuwahudumia wazazi wetu wakiwa kwenye miaka yao ya mwisho ya kuishi kwao hapa
duniani kutafanyika kwa kuruhusu utamadunishaji ulio kwenye Sheria na Amri za
Mungu uendelezwe kutoka kizazi kimoja hadi kingine, na kuweka msisisitizo zaidi
kwa watoto wawatii na kuwaheshimu walio kwenye mamlaka kuanzia viongozi na
wakubwa wao na kwa Mungu.
Hitimisho
Majukumu haya ya
kila mmoja kwenye utaratibu wa familia aliouweka Mungu yana maana tu na mashiko
kwa watoto wake wa kiroho na kimwili waliochaguliwa kwa mujibu wa Torati yake. Wakati
mwanadamu kwa ujumla wake anapoishi kinyume na maelekezo ya Baba yetu wa
mbinguni, fikra hii huonekana kuwa ni jambo lisilowezekana kabisa kuifikia. Msingi
wake unapaswa kwanza ujengwe imara kwenye maoongozi ya Torati au Sheria za Mungu,
pamoja na mwanaume aungane na mkewe na kuwa mwil mmoja na hatimaye iendelee
kwenye mtandao wa vizazi viwili ya familia hii iliyobarikiwa na utaratibu unaweza
kuanzishwa, kukubalika kwamba kila mwana familia anaitilia maanani na kuitia moyoni
mwake amri inayoagiza kuungana kwenye ndoa kwa wale wanaizishika Amri za Baba wa
Mbinguni (2Wakorintho 6:14-18).
2Wakorintho 6:14-18 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi
isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana
shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu
gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye
asiyeamini? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la
Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu
alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa
Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. [Mambo ya Walawi 26:12; Ezekieli 37:27] 17 Kwa hiyo,
Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami
nitawakaribisha. [Isaya 52:11] 18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu
wa kiume na wa kike, [2 Samweli 7:8, 14; Isaya 43:6].
Wakati kipengele chochote mojawapo ya hizi kikiondolewa
hali ya kutojiamini na masikitiko hutokea na hatimaye familia huishi maisha
yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu wakiwa kama watoto waliomuasi Mungu kwa
sasa. Kristo alitabiri kutatokea mateso yatakayotokana na wanafamilia na
marafiki ambao wanaishi kinyume na mapenzi ya Mungu.
Luka 21:16-17 Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki
zenu, nao watawafisha baadhi yenu. 17 Nanyi mtachukiwa
na watu wote kwa ajili ya jina langu.
Tunatakiwa kufanya kile kilicho ndani ya uwezo wetu ili kuendeleza
utaratibu wa kifamilia ambao Mungu ameuweka ili kumfanya mwanadamu aweze
kuzaliana na hatimaye kumheshimu Mungu. Hata hivyo, kaka yetu mkubwa Kristo anasema
kwamba utimilifu wa uhusiano wa familia kwa kila mmoja kwa mwingine huonda hali
ya udanganyifu miongoni mwa walio kwenye familia ya watoto watiifu wa Mungu.
Kwa kuwa hawa ni wana na mabinti wa Bwana, na Mungu Mwenyezi na ndugu wa kiume
na wa kike wa mzaliwa wa kwanza Kristo.
Mathayo 12:46-50 Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake
walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye. 47 Mtu
mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka
kusema nawe. 48 Akajibu, akamwambia yule aliyempasha
habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? 49 Akawanyoshea
mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! 50 Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu
aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.
Amina
q