Makanisa ya Kikristo ya Mungu

 

[191]

 

 

 

Yeroboam na Kalenda ya Hilleli

(Toleo la 3.0 19970118-19990612-20070907)

 

Jarida hili linamuelezea Mfalme Yeroboam, mfalme wa kwanza wa makabila kumi ya Israeli, na jinsi alivyouchukua ufalme kutoka kwa mtoto wa Sulemani kwa sababu ya kitendo cha kuabudu na kuzitumikia sanamu kilichofanywa na babayake yaani mfalme Sulemani. Pia linaelezea dhambi alizofanya Yeroboam kwa masuala ya Sikukuu na ibada za sanamu. Linaelezea pia kuhusu vuguvugu la wa Quartodeciman na halafu maadhimisho ya Easter kwa Kanisa la zamani na jinsi ya kuamua kuanza kwa mwezi wa Nisani kulivyofanywa na kanuni za kale. Hii imepatikana kinyume na matendo ya mwanzoni ya Yuda ambayo kwayo yamepelekea kuanzisha kwa kile kinachoitwa leo kuwa ni Kalenda ya Hilleli.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

(Hati Miliki © 1997, 1999, 2007 Wade Cox)

(tr. 2013)

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

 


Yeroboam na Kalenda ya Hilleli


Kuna wafalme wawili wa Israeli wenye jina hili la Yeroboam. Wa kwanza ni Yeroboam mwana wa Nebati na Zerua, kutoka kwenye mji wa Zereda huko Efraim (kwa mujibu wa Encyc. Judaica, Vol. 9, ukurasa 1371.). wa pili ni Yeroboam mwana wa Yehoashi au Yoashi. Mtu tunayemzungumzia na kuelezea habari zake ni Yeroboam mwana wa Nebati. Alikuwa ni Muefraimu, ambao walikuwa ni tofauti na Waefraimu wa Bethelehemu. Jina lake lina maana ya Yeye anayepigana vita ya watu au watu watashindana (SHD 3379; kutoka 7378, ruwbkushikamana na 5971, ’niko au watu). Yerubaali (Baali atashindana) pia ni ishara au inamaanisha sawa na jina la Gideon (SHD 3378). Yeroboam au Yeroboamu (halina herufi J kwenye Kiebrania) alimkimbia Sulemani na akaenda Misri hali alipokufa mfalme Sulemani.

1Wafalme 11:26-27  Na Yeroboamu wa Nebati, Mwefraimu wa Sereda, mtumwa wake Sulemani; ambaye jina lake mamaye aliitwa Serua, mwanamke aliyefiwa na mumewe; yeye naye akainua mkono wake juu ya mfalme. 27 Na hii ndiyo sababu ya yeye kumwinulia mfalme mkono. Sulemani aliijenga Milo, akapafunga palipobomoka pa mji wa baba yake Daudi.

 

Neno Millo limechukuliwa kwenye Kiebrania likimaanisha kutia au kujaza, na linatokana na neno la Kiashuru mulu, ambalo maana yake ni trrasse au terrace. Shekemu pia alikuwa na nyumba huko Millo (Waamuzi 9:6). Nji wa Millo unatajwa ukijumuishwa na mzingiro wa boma uliofanywa na Daudi baada ya kuuteka mji wa Yerusalemu (2Samweli 5:9; 1Wakorintho 11:8). Ujenzi wake hapo kwanza uliamriwa na Sulemani (1Wafalme 9:15,24; 11:27). Inatajwa kuwa ni nyumba ya Millo kwenye Waamuzi 9:6 na pia inatajwa kwenye kifo cha Yoashi (2Wafalme 12:20 – Henda na 12:21). Mji huu yaonyesha kuwa ulikuwa upande wa magharibi ya mji wa

Daudi ukiunganisha maeneo kati ya Yebu na Moria. Hezekia aliuimarisha (kama inavyosema 2Nyakati 32:54).

 

Inaonekana kuwa kuzungushia ukuta au ngome kwenye miteremko iliyojitokeza inaweza kuwa ndiyo maana yake pia. Kunawezekana kuwa kulikuwepo na utaratibu wa kikanuni kama alivyochukua Yeroboam na kuwa ni sababu ya mashambulizi linaweza kuwa na uhusiano na mungu wa ngome au wa vita na kulifanya liashirie ibada ya sanamu. Maana yake haieleweki vizuri. Maelezo yake yanamfanya mtu afikirie ujenzi wa mahekalu kwenye viwanja vya kuta zilizozungushiwa kuta za boma ya mji wa Uru.

 

Kutoka Agada, tunaona kwamba Yeroboam anamkemea Sulemani kwa kufunga milango iliyowekwa kwenye kuta za Yerusalemu zilizojengwa na Daudi, ili kwamba Israeli wote waweze kutembelea mjini Yerusalemu na kuhudhuria Sikukuu. Inaonekana kwamba Sulemani aliifunga milango hii ili kuwapendeza binti za Farao (Sanh. 101b). Hali hii ilikuwa ni kongwa kubwa sana ambayo aliitumia Yeroboam kuruzukiwa kwa ajili ya juhudi zake za kupigania haki ya uhuru wa kuabudu wa watu, lakini alipopata ufalme slijaribiwa kuzuia kufanyika kwa matu wasiende tion is quite ironic in that Jeroboam wasembezi haya haya akiwazuilia watu wasiende Yerusalemu. Jambo ambalo alilipigania sana watu kuwa na uhuru wa kuabudu (pia tazama kitabu cha TJ. Av. Zar. 1:1, 39a; Sanh. 101b; cf. Encyc. Judaica, ibid.).

 

Tunaendelea kwenye 1Wafalme 11.

1Wafalme 11:28-43 inasema: Na huyo Yeroboamu alikuwa mtu hodari, shujaa; Sulemani akaona ya kuwa kijana huyo ni mtu mwenye bidii, akamweka juu ya kazi yote ya nyumba ya Yusufu. 29 Ikawa zamani zile Yeroboamu alipokuwa akitoka katika Yerusalemu, nabii Ahiya, Mshiloni, alikutana naye njiani; naye Ahiya amevaa vazi jipya, na hao wawili walikuwa peke yao mashambani. 30 Ahiya akalishika lile vazi jipya alilokuwa amelivaa, akalirarua vipande kumi na viwili. 31 Akamwambia Yeroboamu, Twaa wewe vipande kumi, maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nitaurarua ufalme, na kuuondoa katika mkono wa Sulemani, nami nitakupa wewe kabila kumi, 32 (lakini yeye atakuwa na kabila moja kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi, na kwa ajili ya Yerusalemu mji ule iliouchagua katika miji yote ya kabila za Israeli); 33 kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake. 34 Walakini sitauondoa ufalme wote katika mkono wake; lakini nitamfanya awe mkuu siku zote za maisha yake, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi niliyemchagua kwa maana alizishika amri zangu na sheria zangu, 35 lakini nitauondoa ufalme katika mkono wa mwanawe, nami nitakupa wewe kabila kumi. 36 Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko. 37 Nami nitakutwaa wewe, nawe utatawala kama roho yako inavyotamani, nawe utakuwa mfalme juu ya Israeli. 38 Tena itakuwa, ukiyasikia yote nitakayokuamuru, na kuenda katika njia zangu, na kutenda yaliyo mema machoni pangu, ili kuzishika amri zangu na hukumu zangu kama Daudi mtumishi wangu alivyotenda, basi, nitakuwa pamoja nawe, nitakujengea nyumba iliyo imara, kama nilivyomjengea Daudi, nami nitakupa wewe Israeli. 39 Tena nitawatesa wazao wa Daudi kwa sababu hii, lakini si daima. 40 Basi Sulemani akataka kumwua Yeroboamu, lakini Yeroboamu akaondoka, akakimbilia Misri, kwa Shishaki, mfalme wa Misri, akakaa katika Misri hata wakati wa kufa kwake Sulemani. 41 Nayo yaliyosalia ya Sulemani, mambo yake na yote aliyoyafanya, na hekima yake, je! Hayo siyo yaliyoandikwa kitabuni mwa mambo yake Sulemani? 42 Na siku alizotawala Sulemani katika Yerusalemu juu ya Israeli wote zilikuwa miaka arobaini. 43 Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa katika mji wa Daudi baba yake; na Rehoboamu mwanawe akatawala mahali pake.

 

Tunaona hapa kwamba Yeroboam alitoroka kwakuwa Sulemani alikuwa anatafuta kumuua. Huenda hii ndiyo hatimaye ilisababisha maasi. Kitabu cha Wafalme hakiliweki wazi sana jambo hili, lakini tafsiri ya  Septuagint inasema kwamba Yeroboam alifanikiwa kuanzisha kikosi cha askari wa magari wapatao 300 na alikuwa na ngome yake kwenye mji wa Zereda (au Serera). Maasi yalishindwa na Yeroboam akalazimika kukimbilia Misri (pia tazama kitabu cha Encyc. Judaica, ibid.). Tafsiri ya Biblia ijulikanayo kama LXX pia kinanukuu kwamba Shishaki alimtoa shemeji yake kwa Yeroboam ili awe mkewe, na Abiya alikuja kwenye muungano huu.

 

Yeroboam alikuwa mtiwa mafuta wa Bwana. Sulemani alifikia kuwa ni mwabudu sanamu na uzao wake uliadhibiwa. Kwenye andiko hili, inaonekana kuwa ni kama Shishaki wa Misri alikuwa ni shemeji yake Sulemani. Huenda yeye ni mrithi asiyefaa. Na sasa tunaendelea kuangalia namna ambayo kwamba Mungu aliuathiri nguvu na ukubwa wake ufalme huu wa mwana wa Sulemani, yaani Rehoboam.

1Wafalme 12:1-15  Rehoboamu akaenda Shekemu; maana Israeli wote walikuwa wamekwenda Shekemu, ili kumfanya mfalme. 2 Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati alipopata habari (maana alikuwa akaliko Misri, huko alikokimbilia awe mbali na mfalme Sulemani; Yeroboamu akakaa huko Misri, 3 wakapeleka watu kwenda kumwita); basi Yeroboamu na jamii yote ya Israeli wakaenda, wakamwambia Rehoboamu, wakasema, 4 Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa utupunguzie utumwa mzito tuliotumikishwa na baba yako, na lile kongwa zito alilotutwika, nasi tutakutumikia. 5 Akawaambia, Enendeni zenu hata siku ya tatu, kisha mnirudie tena. Watu wakaenda zao. 6 Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee waliokuwa wakisimama mbele ya Sulemani, baba yake, alipokuwa hai, akasema, Mwanipa shauri gani ili niwajibu watu hawa? 7 Wakamwambia wakasema, Ukikubali kuwa mtumishi wa watu hawa leo, na kuwatumikia, na kuwajibu, na kuwapa maneno mazuri, basi watakuwa watumishi wako daima. 8 Lakini akaliacha shauri lile la wazee, walilompa, akataka shauri kwa wale vijana waliokua pamoja naye, na kusimama mbele yake. 9 Akawaambia, Mwanipa shauri gani ili tuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakinena Utufanyie jepesi kongwa lile alilotutwika baba yako? 10 Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliokuambia, wakisema, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, bali wewe utufanyie jepesi, uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. 11 Basi kama vile baba yangu alivyowatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge. 12 Basi, Yeroboamu na watu wote wakamfikia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu. 13 Mfalme akawajibu watu wale kwa ukali, akaliacha shauri lile wazee walilompa; 14 akawajibu kama vile walivyomshauri vijana, akasema, Baba yangu alilifanya zito kongwa lenu, bali mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge. 15 Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa Bwana, ili alitimize neno lake, Bwana alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa kinywa cha Ahiya Mshilon 

Yeroboam aliwekwa mahala pake na Mungu ili aweze kuligawanya kwa mrithi wakuu – lakini hili halikueleweka hadi kipindi cha baadae sana. Upuuzi wa kiushauri wa vijana uliongezeka sana. Kazi na uzungushaji ngome vilikuwa vimekwisha fanywa na Daudi na Sulemani. Angeweza kupunguza uzito wa kongwa na akawa mfalme, lakini Mungu hakupenda iwe hivyo. Masharti ya ufalme wa Sulemani yalikuwa ni awe mtiifu kwa Mungu na kwa Sheria na Torati yake. Jambo hili lilipelekea maana kubwa kama tutakavyojionea baadae.

 

1Wafalme 12:16-20  Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao. 17 Lakini kwa habari za wana wa Israeli waliokaa katika miji ya Yuda, Rehoboamu aliwatawala wao. 18 Ndipo mfalme Rehoboamu akampeleka Adoramu, aliyekuwa juu ya shokoa, nao Israeli wote wakampiga kwa mawe hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda katika gari, ili akimbilie Yerusalemu. 19 Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi hata leo. 20 Ikawa, Israeli wote waliposikia ya kwamba Yeroboamu amerudi, wakapeleka watu wakamwita aje mkutanoni, wakamfanya mfalme juu ya Israeli wote; wala hapakuwa na mtu aliyeshikamana na nyumba ya Daudi, ila kabila ya Yuda peke yake.

 

Mungu alitenda jambo litokee na Mpango wake ulifanikiwa. Watu wenyewe hawakugundua kile kilichokuwa kinatokea. Yeroboam ndiye alikuwa mrithi aliyestahili na ndiye angaliyeweza kuyaunganisha makabila chini ya Efraimu, ila Mungu alijua kuwa angeshindwa. Hata hivyo, alimfanya kuwa mfalme.

 

1Wafalme 12:21-24 Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda, pamoja na kabila ya Benyamini, watu wateule mia na themanini elfu, waliokuwa watu wa vita, ili wapigane na nyumba ya Israeli, waurudishe ufalme tena kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani. 22 Lakini likaja neno la Mungu kwa Shemaya mtu wa Mungu, kusema, 23 Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, na jamaa yote ya Yuda na Benyamini, na watu waliosalia, ukisema, 24 Bwana asema hivi, Msiende, wala msipigane na ndugu zenu wana wa Israeli; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakalisikiliza neno la Bwana, wakarudi, wakaenda zao, sawasawa na neno la Bwana.

 

Mungu pia alizuia umwagaji damu usio wa lazima kwa kuwarudisha myumbani Yuda na Benyamin kwa upande mwingine, na makabila mengine kumi kwa upande mwingine.

 

Ingawa Yeroboam alifanywa kuwa mfalme na Mungu na akatumika kuchukua mahala pa nyumba hii iliyogeukia na kuabudu sanamu chini ya Sulemani, bado hakuwa na imani ya kutosha kwa Mungu kuwa angeweza kumlinda na kumfanya awe huko.

 

1Wafalme 12:25-33 Ndipo Yeroboamu akajenga Shekemu katika milima ya Efraimu, akakaa huko. Akatoka huko akajenga Penueli. 26 Yeroboamu akasema moyoni mwake, Basi ufalme utairudia nyumba ya Daudi.27 Kama watu hawa wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, ndipo mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu, mfalme wa Yuda; nao wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda. 28 Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. 29 Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili akamweka katika Dani. 30 Jambo hili likawa dhambi, maana watu walikwenda kuabudu mbele ya kila mmoja, hata huko Dani. 31 Tena akafanya nyumba za mahali pa juu, akafanya na watu wo wote, watu wasio wa wana wa Lawi, kuwa makuhani. 32 Yeroboamu akaamuru kushika sikukuu katika mwezi wa nane, siku ya kumi na tano ya mwezi, mfano wa sikukuu iliyokuwa katika Yuda, akapanda juu ili kuiendea madhabahu. Akafanya vivyo katika Betheli akiwatolea dhabihu wale ng'ombe aliowafanya; akawaweka katika Betheli wale makuhani wa mahali pa juu alipokuwa amepafanya. 33 Akatoa dhabihu juu ya ile madhabahu aliyoifanya katika Betheli, siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, mwezi aliouwaza moyoni mwake mwenyewe; akawaamuru wana wa Israeli waishike sikukuu hiyo, akapanda kuiendea madhabahu, ili kufukiza uvumba.

Aliujenga Shekemu na kisha akauzungushia boma mji wa Penueli uliokuwa mashariki mwa ukingo wa Yordani (1Wafalme 12:25), na hatimaye alionekana pia kuwa alikwenda Tirza (1Wafalme 14:17; sawa na. 1Wafalme 15:21).

 

Yeroboam aliamua kuanzisha mfumo wa kidini ambao kwa kweli ulikuwa ni wa ibada za sanamu. Alianzisha imani ambayo ilikuwa karibu sawa na ile iliyokuweko Hekaluni ya ibada asilia ya Yerusalemu ikiwa na Sikukuu zided to reintroduce a religious system that was inlezile lakini kiini na kituo cha kufanyia ibada ilikuwa na msingi wake kwenye sanamu ya ndama wa dhahabu, ambaye anakiweko ambacho pembeni yake amesimama Mungu (Encyc. Judaica, ibid.). dini hii waliijua Israeli tangu siku walizokuwa jangwani. Kutokana na kile tunachokijua sasa kuwa ni utaratibu wa ibada za watu wa Uru, ndama alikuwa ndiye alama ya ibada za watu wa Uru – inayoonekana kwenye majumba ya kujiliwaza yaliyo nje ya mji wa Alaka Huyuki (tazama kitabu ccch Wataalamu wa Uchimbuzi (Archaeological Diggings), Vol. 3, Na. 6, Dec 96/Jan 97, ukurasa. 41). Waajemi wameifanyiza upya sanamu hii ili kufanya yule ng’ombe dume aliyekuwa anamuwakilisha Ahriman, ambaye ni mungu wa giza. Mtazamo huu wa kiulimwengu wa mapigano kwenye sayari za juu bilashaka ni alama ya dume la ng’ombe aliyechinjwa ni alama ashirio ya dini na ibada za mungu Mithras, iliyochukuliwa kutoka kwa wa Zoroastrian na kufuatiwa na elimu-dunia (sawa na ilivyoandikwa kwenye jarida la Mdama wa Dhahabu (Na. 222) [The Golden Calf (No. 222)].

 

Mji wa Dani kwa upande wa kaskazini na Betheli kwa upande wa kusini ilikuwa ni mahali patakatifu pa imani po ofu ya dini hii kabla ya kipindi cha kuanzishwa kwa utawala wa wafalme (Encyc. Judaica, ibid.).

 

Inaonekana kuwa Yeroboam alitengwa na baraza la kidini la Sanhedrin kwa kuwa matendo yake yote aliyoyafanya ikiwemo na kupaweka tena mahali pa juu katika Dani na Betheli, kulituama kwnyre mtazamo wa kuchukulina na uvumilivu wa kidini uliopelekea kutumia kuabudu ndama jambo ambalo ni kinyume na amri ya Torati (TJ. Av. Zar. na Sanh, loc. cit., cf. Encyc. Judaica, ibid.). hii ni hali sawa na jinsi tulivyo leo. Hata hivyo, makabila haya hawakudanganjika na dini hii isipokuwa kabila la Dani, ambalo liliabudu sanamu iliyochongwa na Mika katika zama hizi za makabila (Hesabu 2:10). Inaonekana kuwa Walawi walijitahidi kupinga na kuzuia ibada hizi za sanamu na ndipo Yeroboam akaanzisha mfumo mpya mwingine wa Makuhani ambao uliwaweka kando Walawi (TJ. Av. Zar., loc. cit.). walawi waliandika habari kwamba Yeroboam aliweka walinzi ili kuzuia—maumivu ya kifo—ya wanaokwenda kuzitunza sikukuu mjini Yerusalemu (Tosef., Ta’an. 4:7; Sanh. 102a). Watu na hata mtoto wa mfalme, walizihalifu amri hizie (MK 28b, cf. Encyc. Judaica, loc. cit.).

 

Katika mwaka wa hamsini wa utawala wa Yeroboam, Shishaki, mfalme wa Misri, aliamua kuishambulia Israeli. Mikakati yake iliyoandikwa kwenye Biblia ilisababisha kile kiliccchotokea huko Yuda (1Wafalme 14:25-28; 2Nyakati 12:2-12). Hebu na turudi kwenye yale michoro ya ukutani mwa hekalu la Karnaki huko Misri ili kuona ni miji gani iliyokuwa imetekwa na Shishaki, na tutaona kwamba inaonekana kuwa Israeli walitaabika sana. Kwa hiyo, mlingano na muonekano huu sio tu kwamba unafanana tu kwenye Biblia bali pia unafika mbali kutupa taarifa za huko. Shishaki alishambulia jimbo la kusini la Ufalme wa Israeli kupitia huko Gezeri na Gibeon, kupenyeza bonde la Sukoth na kisha kugeukia upande wa Beth-Shean na bonde la Yezreeli, hatimaye akarudi Misri kwa njia ya uwanda wa pwani. Uweza wa nguvu za kijeshi za Misri ulikoma kwa utekwaji rahisi na usiotarajiwa. Wataalamu wa uchimbuzi wa mambo ya kale wamegundua kwamba Gezeri, Beth-Shean, Taanaki na Megido ziliangamizwa kipindi cha kampeni hii. Kwa hiyo mafanikio ya Abiya kuyashinda majimbo ya Israeli yanatakiwa kuonekana kwenye wepesi wa udhaifu iliyoikumba kampeni ya Wamisri, lakini pia ni kwa shinikizo juu ya hili kutoka kwa Aram-Damascus wa kaskazini mashariki na Wafilisti wa kusini magharibi. Hii inaweza pia kuwa iliungwa mkono na mapigano na majimbo ya Trans-Jordan ambayo yalikuja kuwa huru zaidi (Encyc. Judaica, op. cit., ukurasa 1373).

 

Pia Yeroboam aliamua kubadilisha maadhimisho ya Sikukuu ya Vibanda kutoka nyakati zake asilia za Mwezi wa Saba na kuisogeza hadi mwezi wa Nane alifanya hivyo kwa kusudi la kufanya ibada ionekane kuwa ni sawa na ni ile ile, lakini ikiwa isiyo sawa na ile iliyo kwenye taratibu asilia za Hekaluni. Jambo hili lina fundisho lenye madhara makubwa kwa Kanisa la siku hizi ambayo Mungu anaonyesha kwa matendo yake hapa kwamba hawezi kuuvumilia wala kusamehe na kuachia uendelee utaratibu wa ibada wenye mjumuisho na ushirika wa namna za ibada za sanamu, au unabadili utaratibu uliowekwa wa maadhimisho ya Sikukuu kwa kuiweka kwenye majira mengine mbali na mwezi uliowekwa na ambao ameuweka mwenyewe kwa mujibu wa ishara za mbinguni. Kalenda ya Mungu haitegemei na hesabu na mipangilio na muafaka wa kibinadamu. Imewekwa na inadumu kwa nyakati zote na uumbaji unaonyesha mpangilio wa mabadiliko ya nyakati na majira. Mwandamo wa Mwezi Mpya unaunganisha mipangilio kati ya jua, mwezi mwandamo na Dunia, na unaweza kupimwa kiuhakika hadi kwenye kipindi kingine cha karne kadhaa zijazo. Tukio hili la kipindi cha kutoonekana mwezi, pamoja na lile la mwezi mkamilifu na robo ya kwanza nay a mwisho, vimepandiliwa kwa mujibu wa maji kujaa na kupwa.

 

Tunaweza kufanya mabatiyo tusiyoweza kuyajua kupata hakika jinsi mfumo huu wa dini mpya ulivyokusudia kubadili hadi kwenye namna mpya iliyoanzishwa tangu kale na ambayo inaendelea kudumu hadi leo, na hii ndiyo chanzo cha kuanzishwa kwa kalenda ya watu wa Samaria. Ilianza siku za kale zaidi kuliko ile inayojulikana kama kalenda ya Hilleli na inarudi nyuma zaidi hadi kipindi cha zama za Hekalu kabla ya Kristo.

 

Imani au Dini ya Wasamaria

Kwenye jarida la Malumbano ya Wa-Quartodeciman (Na. 277) [The Quartodeciman Disputes (No. 277)], tuligundua uwiano wenye kufanana wa Wasamaria na ule wa Masadukayo katika kuamua namna ya kuiweka kalenda ya Hekalu na kupanga majira ya kuadhimisha Pasaka wakati wa kipindi cha Hekalu na siku za Kanisa la kwanza tunarudia hapa baadhi ya maandiko hayo. 

 

Kuandama kwa Mwezi Mpya kulikuwa ndiyo jambo la muhimu sana katika kuamua kuanza kwa miezi, na Mwandamo wa Mwezi wa Kwanza wa Abibu au wa Nisani, (na sio wa mezi wa Saba wa Ethanimu au wa Tishri), ndiko kilikuwa kigezo cha kutangazwa kwa mwezi wa kwanza wa mwaka mpya, kama ilivyofanywa na kujulikana na Wayahudi kutoka karne ya tatu ya zama hizi. Mfumo wa Rosh HaShanah, ulio kwenye utaratibu wa leo wa kuamua kutangazwa kwa mwaka mpya, hauwezi kuchukuliwa kuwa ni wa kibiblia au ulichukuliwa kwenye maadhimisho ya zama za Hekalu, wala kuchukuliwa kuwa ni maadhimisho sahihi ya Wakristo—Wayahudi.

 

Kitabu maarufu kiitwacho Filo wa Alexandria, yaani Philo of Alexandria [kilichotafsiriwa na F. H. Colson, (Harvard University Press, Loeb Classical Library, Cambridge, MA, 1937), The Special Laws, II, XI, 41] kinatuambia kwamba: “[Sikukuu] ya tatu kwenye mwandamo wa mwezi mpya uliofuatia kipindi cha mwezi kutoonekana na jua”. Na kwenye chapisho la II, XXVI, 140: “Huu ni Mwandamo wa Mwezi, au mwanzo wa mwezi mwandamo, unaojulikana kuwa ni kipindi kilicho katikati ya kipindi cha kutoonekana mwezi na kinachofuatia, urefu ambao umehesabiwa kikamilifu pasi kukosewa na wanazuoni wa elimu ya anga nyota”. Yapaswa ijulikane pia Kitabu maarufu kilichochapishwa cha Hendrickson Publishers toleo la (1993) la tafsiri ya C. D. Jonge ya mwaka 1854 haina taaarifa sawa kama iliyoko kwenye tafsiri ya Colson na jinsi inavyotuambia. Dalili zilizoko ni kwamba vipindi vya kutoonekana mwezi viliamuliwa ili kuamua ama kuashiria mwanzo wa mwezi.

 

Wasamaria na Masadukayo makundi yote mawili yaliaweka kalenda kwa kuanzia kipindi cha mwezi kutoonekana, maadhimisho ya Mwandamo wa Mwezi yalitangazwa na kufanyika kwa kutegemea majira haya ya kutoonekana kwa mwezi kwa namna yoyote ile kwenye kipindi cha Hekalu, isipokuwa kwa Essene tu aliyekuwa na kalenda isiyobadilika ambayo kwamba siku ya 14 Abibu iliangukia siku ya Jumanne ya kila mwaka kwenye mzunguko wa kamilifu wa kalenda. Wasamaria bado wanatangaza siku ya kwanza kwa kufuata kipindi cha kutoonekana mwezi hadi leo (sawa na ilivyoandikwa kwenye jarida la Kalenda ya Mundu (Na. 156) [God’s Calendar (No. 156)].

 

Wasamaria walianzisha makosa kwenye kalenda yao walipoanzisha utaratibu wa kutangaza mwanzo wa Mwezi wa Kwanza kwa kusema kwamba Mwandamo wa Mwezi kila mara ni lazima uwe kwenye majira ambayo saa za usiku na za mchana ni sawa au baadae kidogo, ambayo walitangaza kuwa kinaangukia kila mwaka tarehe 25 Machi. Uhesabuji wa miaka ya (1988-2163 BK), kama ulivyoonyeshwa na Kasisi Eleazar ben Tsedeka, umejumuishwa kwenye kitabu cha maombi kuhusu Pasaka na Mazzot, Knws tplwt hg hpsh whg hmswt (Holon, 1964, pp. 332-336; sawa na Reinhard Pummer Samaritan Rituals and Customs, kurasa 681-682, fn. 201 in Alan D. Crown Ed. The Samaritans, 1989, J. C. B. Mohr (Paul Siebeck) Tübingen). Ukweli huu unaonyesha pia kuwa tunatazamia chanzo asilia cha kale, ambacho msingi wake ni kwenye kalenda inayotumika wakati siku hii ya usiku na mchana masaa kuwa sawa iliangukia tarehe  25 Machi. Tarehe hii ilitangulia siku nyingi kabla ya kipindi cha Kristo na ilikubalika kwa kuweka uwiano wa kalenda ya kaisari Yulio au Julius Caesar (sawa na. David Ewing Duncan, The Calendar, 4th Estate London, 1998, uk. 81).

 

Hii inaonekana kuwa huenda ni chanzo cha kuwapo makosa haya. Kitendo cha watu wa kale kuamua siku ya mwezi kutoonekana ya tarehe 25 Machi kinaonekana kuwa kilichukuliwa kutoka kwenye mapokeo ya kipindi cha kwanza cha Hekalu la Kwanza na la Pili na inaonyesha kwamba huenda sisi tunaangalia suala zima la Kalenda ya Yeroboam. Kitendo chake cha kuamuru Sikukuu iadhimishwe mwezi wa Nane—kililaaniwa na Biblia—na kingeweza kufanikiwa kutokea kwa tendo la kufanya Mwandamo wa Mwezi ufanyike kwenye kipindi cha masaa ya jua kuwa sawa usiku na mchana au baadae kidogo. Hii inaonyesha kuwa haikuweza kubadilishwa kwa suala la Wasamaria tangia kuanguka kwa taifa la Israeli. Na kwa sababu hii waliangukia kwenye laana na wamebakia kuwa ni masalia pekee ya Israeli ambao hawajabarikiwa na ahadi ya uzaliwa wa kwanza ya Yusufu. Kazi ya kuhesabu ya Wasamaria ilifanywa kwa siri, huenda ni kwa kulifanyia uangalifu jambo hili. Hata hivyo, wao pamoja na Mafarisayo kila mara waliamua mambo ya kalenda kwa kutegemeza na siku ambayo mwezi hauonekani, ambavyo ndivyo ilivvofanyika kipindi chote cha zama za Hekalu.

 

Kalenda ya Wasamaria kwa hiyo iliondoka kwenye msingi sahihi wa uelewa wa Mwandamo wa Mwezi na Msingi wake, bali ulichukuliwa kwenye baraza lenye makosa ya uwekaji kwa usahihi na kuweka siku ya mwanzo wa mwaka kimakosa. Kwenye miaka hiyohiyo wakati wa Mwandamo wa Mwezi wa Mwezi wa Kwanza ulioangukia kabla ya siku hii ya masaa kuwa sawa usiku na mchana, waliamua kutangaza kuanza kwa mwaka mpya kwenye Mwezi wa Pili na kufanya Sikukuu iadhimishwe mwezi wa Nane badala ya Mwezi wa Saba wa kweli na sahihi kwa mujibu wa mwaka unaofuata mwezi mwandamo. Huenda hii ilikuwa ni chanzo cha makosa yaliyofanywa kwenye imani na mtazamo wa Yeroboam. Na kwa kweli, ili kugundua kakosa kunabidi kukubali kuwa Wasamaria ni masalio ya mfumo huu wa zamani wa Israeli na sio wote waliojichanganya na hatimaye kuzuka kwa makabila ya Cutheans na Wamedi, ikiwa kama ni propaganda ya Wayahudi ambayo inaumiza sana kuiongelea. Ukweli ni kwamba, wanachanganyika na nasaba zote mbili.

 

Utaratibu huu wa ibada uliofanywa na kupangwa na wanadamu, siku hizi imeshika hatamu, kwa kuwa utaratibu wa kuabudu wa Wayahudi ulioanzishwa na kalenda ya Hilleli umefuata kikamilifu sana kile alichokifanya Yeroboam. Kwa mfano, mnamo mwaka 1997 – ulikuwa ni wa kuadhimisha kikamilifu mtindo na muono wa kibinadamu uliojulikana kama wa maahirisho ya--kalenda ya Hilleli yaliyotangulia kwenye mwezi wa kweli wa Pili na sio katika mwzui wa Kwanza na, kwa hiyo Sikukuu ikaadhimishwa mwezi mmoja kwa wote. Chini ya utaratibu wa Hilleli, Sikukuu ya Vibanda ya mwaka 1997 ilifanyika mwezi wa Nane na sio mwezi wa Saba. Makosa haya yalitokana na utaratibu huu unaojulikana kama wa ahirisho na ambao hauna mashiko wala maagizo yoyote kwenye Biblia. Utaratibu wote wa uwekaji wa utaratibu wa Kalenda umetolewa kwenye majarida ya GKalenda ya Mungu (Na. 156) na pia Tishri na Uhusiano Wake na Siku ya Masaa ya Usiku na Mchana Kuwa Sawasawa (Na. 175) [God’s Calendar (No. 156) and also Tishri in Relation to the Equinox (No. 175)].

 

Kanuni za siku za kale ziko rahisi na wazi sana. Mwansamo wa Mwezi wa Nisani unachukuliwa kuwa ni ule unaoandama majira yaliyo karibu na siku ya masaa ya usiku na mchana kuwa sawa. Siku Takatifu ya kwanza ya Mikate Isiyotiwa Chachu (siku ya 15 Nisani) inapaswa kila mara iwe baada ya siku ya masaa kulingana usiku na mchana. Siku ya 14 Nisani inaweza kuangukia siku hii ya masaa kulingana usiku na mchana, lakini – siku ya 15 Nisani haiwezi. Hii inahesabiwa wakati jua linapokuwa kwenye umbo la Aries (tazama kitabu cha Schürer, History of the Jewish People in the Age of Jesus Christ, Calendar Appendix III, (Historia ya Wayahudi Kipindi cha Yesu Kristo, Kaleanda na Nyongeza III), na pia majarida tuliyoyataja hapo juu). Kwa hiyo, Idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu haiwezi kufanyika siku hii ya usiku na mchana kuwa sawa au kabla yake na haiwezi kufanyika zaidi ya tarehe 20-21 Aprili. Hakuna maadhimisho ya Pasaka yanayoruhusiwa kufanyika baada ya tarehe 20-21 Aprili (kama ilivyoainishwa pia kwenye jarida la Mwezi na Mwaka Mpya (Na. 213) [The Moon and the New Year (No. 213)].

 

Hii inajulikana na inaadhimishwa na matawi yote ya Kanisa tangu kipindi cha Kristo. Tangia karne ya pili na cha malumbano ya Waquartodeciman (tazama jarida la Pasaka (Na. 98) [The Passover (No. 98)], kanisa huko Roma lilianza kuadhimisha sikukuu ya Easter, lakini bado alikuwa wanaendelea kuzishika sheria za zama kale kwa kuichukulia Nisani kuwa ni mwezi wa maadhimisho ya Easter kwa kuwa ilikuwa inaangukia pia kwenye mwezi huu wa Nisani.

 

Kanisa huko Roma, hata hivyo lilifanya mabadiliko ya sheria. Siku ya Ijumaa ilifanywa kuwa iwe ni siku ya kusulibiwa na sio siku ya 14 Nisani (aambayo ni Jumatano ambayo Krsto alisulibiwa kwayo; tazama jarida la Kipindi cha Kusulibiwa na Kufufuka (Na. 159) [Timing of the Crucifixion and the Resurrection (No. 159)]. Kalenda iliyojulikana mapema zaidi ya kanisa la kale la mrengo wa Jumapili katika kujitahidi kwake kuifanya iwepo ni ile ambayo ilimilikiwa na Willibrord, aliyekuwa mtume wa Kkiingereza aliyehudumu hko Frisians (Askofu aliyewekwa wakfu mwaka 695 BK, aliyetajwa kwenye maandiko). Kalenda ile inaweka siku ya kusulibiwa kwa Kristo kuwa ni tarehe 25 Machi na Yakobo ndugu yake kuwa alisulibiwa pia tarehe hiyohiyo (akifuatiwa na Tertullian). 25 Machi ilikuwa ni siku iliyokubalika kwa kare kadhaa, ila ilikataliwa na Kanisa Katoliki la Roma kwa kuwa inaharibu na kupinga juhudi za kuiaminisha dhana na fundisho la kusulibiwa siku ya Ijumaa. Tehere 25 Machi ilikuwa ni Jumapili katika mwaka wa 31 BK na huenda ilitokana na kazi ya kuhesabu kwenda nyuma hadi mwaka 31 BK ukiwa kama mwaka uliofikiriwa kuwa ndio alisulibiwa kwawo. Tarehe 25 Machi, 31 BK ilikuwa siku ya 14 Nisan kwa mujibu wa Mwandamo wa mwezi na ikiwa ni siku ya kweli ya mwezi kutoonekana ya utaratibu wa kale wa kalenda ya Hilleli. Kwa jinsi ilivyo, inaonekana kama utaratibu wa kuahirisha haukulazimishwa. Makosa aliyyafanya Tertullian huenda yalisababishwa na maandiko ya Josephus ambayo yalimyanya kuamini kuwa ni mwaka 31 BK badala ya mwaka 30 BK. Mnamo mwaka 30 BK, tarehe 14 Nisan iliangukia siku ya Jumatano, na tena iliangukia kwenye siku halisi ya mpito cha Kuandama Mwezi pasipo ahirisho. Huenda Tertullian alifanya makosa ya kimahesabu kwa mwaka wa kumi na tano wa Tiberius (kama ilivyoelezwa kwenye jarida la Kipindi cha Kusulibiwa na Kufufuka (Na. 159) [Timing of the Crucifixion and the Resurrection (No. 159)] (pia tazama kwenye kitabu cha Cath. Encyc., Vol. III, art. ‘Calendaar’, p. 163 kwa tarehe, ingawaje elimu ya wafiadni maarufu kama Syriac Martyriology inasema kuwa kina Yohana na Yakobo waliuawa tarehe 27 Desemba, kwenye kitabu hicho cha hapo juu., ukurasa 162).

 

Tarehe za Tertullian zinaonyesha mambo mawili. La kwanza ni kwamba hakukubali kuwa kusulibiwa kulifanyika siku ya Ijumaa kwenye miaka hii inayoonewa mashaka (14 Nisan iliangkia tarehe 25 Machi tu mwaka 31 BK). Hata hivyo, tarehe 25 Machi 31 BK ilikuwa siku ya Jumapili. Kwa hiyo kuhesabu kwa namna hiyo hakuwezi kwendana na jinsi Injili inavyosema (tazama jarida la Kipindi cha Kusuibiwa na Kufufuka tulilolitaja hapo). Pili, ni kam Tertullian alivyoandika siku nyingi kabla ya 358 BK, tunajua kuwa uahirishaji haukutiliwa maanani mapema kabla ya kalenda ya Hilleli ilipofanyiwa hesabu kutoka hitimisho. Tarehe ya 25 Machi pia ina maana yake kwenye ibada za mungu Attis, na kuingizwa kwenye Ukristo kupitia dini za fumbo (sawa na ilivyoandikwa kwenye jarida la         Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235) The Origins of Christmas and Easter (No. 235)].

 

Kansa lililoluwa huko Roma lilibadilisha kutoka kuifanya Pasaka iwe Sikukuu ya Kwanza ya Mikate Isiyotiwa Chachu kuwa inaichukua mahali pa siku ya mchana na usiku kuwa sawa na kwenye kipindi ambacho Easter ilikuwa ni Jumapili ya Kwanza iliyoifuatia Mwezi Mwandamo wa Pasaka (ambayo ni kipindi cha Mwezi Kamili, siku ya 15 Nisan). Mwandamo wa Mwezi uliganyika kabla ya siku kulingana masaa usiku na mchana, bali Mwezi Mkamilifu haukuangukia kipindi cha kabla ya siku hii ya masaa kulingana. Kwa hiyo, siku ya 14 Nisan inawezekana iliangukia siku ya masaa kulingana, ila siku ya 15 Nisan iliangukia siku ya masaa kulingana.

 

Katika karne ya pili Kanisa liliingia kwenye malumbano kuhusu kubadili maadhimisho ya Pasaka kutoka siku za 14-15 Nisan hadi Easter, ikaamuliwa kama tunavyoona hapo juu. Hili lilikuwa ndilo hasa jambo lililosababisha utata kwa wa Quartodeciman. Utata huu uliendelea na kuenea kati ya askofu Anicetus wa Roma (aliyemfuatia Pius mwaka 157 BK) na Polycarp, mwanafunzi wa Yohana na askofu wa Smirna. Alikuja Roma (yapata mwaka 160-162) kwenye uzee wake kushirikiana pamoja na Anicetus kuhusu kuanzusha kwa mafundisho mapotofu ya Easter. Kanisa la Mashariki kila mara lilipenda kuendelea na Pasaka tangu siku ya 14 Nisan haijalishi ni siku gani ya juma iliangukia. Huko Roma kulianza kujulikana siku ya Ijumaa na Jumapili. ambayo ilikuwa ni maadhimisho Easter ya kipagani au Ishtar (kama iliyoandika kwenye Cath. Encyc., art. ‘Anicetus’, Vol. I, p. 514). Polycarp hakufanikiwa kumshawishi Anicetus akiwa anakata tama na wazo lake la kipagani na kurudi, bali uhusiano kati yao uliliimarishwa na kulindwa (ibid.). hali hii iliendelea hadi takriban mwaka 190 BK. Eusebius anaandika kwenye kitabu chake (Eccl. Hist., V, xxiii) kwamba wakati au kipindi cha utawala wa Papa Victor kwamba:

Swali kuhusu kitu kidogo muhimu liliibuka kipindi kile. Dayosisi ya Asia yote, kama kutoka kwenye mapokeo yao ya kale, ilishikilia kwamba siku ya kumi na nne ya mwezi, kwenye ile siku ambayo Wayahudi waliamriwa kumtoa sadaka mwanakondoo, ndiyo inayofaa kilamara iadhimishe kuwa ni sikukuu ya kutoa uhai au Pasaka [epi tes tou sõterion Pascha eotes], sambamba na hilo ikaamuriwa mkwacba ndiyo iwe siku ambayo kwamba kipindi cha mafungo walichojiwekea kihitimishwe siku hii, yaani siku yoyote ya juma inaweza kufanyika tendo hili (Cath. Encyc., Vol. V, art. ‘Easter’, p. 228).

 

Makanisa kayika Asia yalihitimisha mafungo siku ya 14 Nisan kwa kushiriki Ushirika Mtakatibu wa Meza ya Bwana ili kwamba Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu ifuatie baada ya Siku hii ya Ushirika wa Meza ya Bwana. Maanalio ya mlo yalifanywa na mlo wa Kutoka 12 uliandaliwa mahsusi kwa ajili ya siku ya 15 Nisan. Dini ya Warumi hata hivyo ilianzisha utaratibu wa kuhitimisha mfungo siku ya Jumapili (tazama kitabu hikihiki cha Eusebius, ibid.; sawa na ilivyosndikwa kwenye Cath. Encyc., ibid.) kinachohusisha imani hii na imani ya kumuabudu mungu mke Easter au Astarte/Ishtar.

 

Tendo hili la kubadilisha na kuiadhimisha Easter badala ya Pasaka lililofanywa huko Rumi linaonekana kuwa lilifanyika kipindi cha Sixtus, askofu wa Roma takriban mwaka 120 BK (tazama waraka wa Irenaeus unavyosema kuhusu jambo hili; sawa na Cath. Encyc., ibid.). Irenaeus anasema kwamba Polycarp alikuja kutoka Roma akiwa na swali hili mnamo takriban mwaka 150.

 

Ni kwa jinsi hii ndipo Irenaeus aliwakataa na kuwapinga wa Quartodeciman na itikadi yao ila hathubutu kabisa kumshutumu au kumlaumu Victor (takriban mwaka 189-199) kwa kuwatenga wafuasi wa Asiatics na kwa kutoifuatia tabia ya kuvumiliana ya waliomtangulia. Ukweli unaoonyeshwa hapa uko dhahiri kabisa. Irenaeus hakupenda kutengwa na kwa hiyo anadaiwa kuwa aliikubali Easter ichukue mahala pa Pasaka kwa kuwa Roma ilisimama kati yake na pande za Mashariki. Ni kama ilivyo kwa watu wengi Kanisani leo, yeye alikubali kukabiliana na mateso ya nje bali hakuweza kukabiliana na ukengeufu uliokuwa ndani yake.

 

Baada ya juhudi za Victor za kuwakomesha wa Quartodecimans kuwakomesha na kuwaondolea mbali. Kwa mujibu wa kitabu cha Origen (cha Philosphumena, VIII, xviii) inaonekana kuwa aliwachukulia ni watu dhaifu kwa utendaji kazi walio na umahiri usiona na maana (sawa na Cath. Encyc., op. cit.).

 

Hakuna mwandishi kwenye siku za kabla ya Justin Martyr (takriban mwaka 140) aliyewahi kuitaja Jumapili kuwa ni siku inayofaa kufanyiwa maadhimisho haya ya Pasaka kwa Kanisa (Cath. Encyc., ibid., p. 159). Tendo la kutenga kipindi cha ,mafungo ya Pasaka ya maandalizi pia hakikuwa ni cha siku arobaini tu kama kilivyo kwenye siku za leo. Ulikuwa ni utaratibu wa kiimani wa maandalizi yaliyopelekea kwenye maadhimisho ya Pasaka (kwa mujibu wa Cath. Encyc., ibid.). Utaratibu wa kikanuni wa Mitume  na Maendelezo nya Mitume viliifanya Pasaka au Easter kuwa ni maadhimisho makubwa na maarufu miongoni mwa Sikukuu zote. Kwa mujibu wa Tertullian, matukio ya mateso na ufufuko wa Bwana vilichukuliwa kwa uzito sawa na neno Pascha (au Pasaka) viliwekwa kwenye siku zote mbili au kwenye kipindi kilichokuwa kati ya ufufuko na siku ya Jumapili (ambayo ilikuwa ni siku ya Mganda wa Kutikiswa na ambacho ndicho kwacho, hesabue ya kuelekea siku ya Pentekoste inaanza kwayo) (ibid., p. 159).

 

Utaratbu wa kuhesabu na kuigiza imani ya sikukuu ya Easter na maadhimisho yake kwa watu ulifanywa kwa mujibu wa Baraza la Mtaguso wa Nicaea, lakini hakuna kumbukumbu kwenye utaratibu wa Kikanuni wa maamuzi haya (kwa mujibu wa kitabu cha Cath. Encyc., ibid., p. 160; cf. Turner, Monumenta Nicaeana 152; cf. Vol. V, art. ‘Easter’, p. 228). Rekodi imechukuliwa kutoka kwenye madai ya nyongeza yaliyofanywa kwenye kitabu cha Eusebius kiitwacho Life of Constantine (III, xviii, et. seq.). Constantine alitafuta kutoka kwenye dokumenti hii kufanya hali ya uwiano usiokuwepo na kuiweka mbali itikadi ambayo Wayahudi wanasema kwamba:

Na kwanza na kabla ya yote kabisa inaonekana kuwa ni kitu kisicho sahihi kusherehekea sikukuu hii muhimu sana na takatifu na kwamba tulipaswa kufuata wanavyofanya Wayahudi, bali bila woga kabisa tumeinajisi mikono yao kwa dhambi kuu...kwa kuwa tumepokea kutoka kwa Mwokozi wetu namna nyjngine...

 

Watu wengi (kutoka Roma katika Italia na Misri na Afrika) walikumbwa na wimbi hili la kuikubali sikukuu hii ya Easter, lakini makanisa katika Syria na Mesopotamia, pamoja na kituo chao kikuu katika Antiokia, walikuwa hawajaachana na mafundisho na itikadi ya wa Quartodeciman. Kanuni hii ilirenukuliwa na kuandikwa kwenye nyaraka zinazohusu mabishano haya kwamba kwenye maadhimisho ya kale ya Wayahudi, siku ya 14 Nisan inapaswa kuwa siku kabla ya ile ya masaa kulingana usiku na mchana. Na kwa hiyo, siku ya 14 Nisan inaweza kuangukia siku ya masaa usiku na mchana kulingana na siku ya 15 Nisan inapaswa kila mara iangukie siku hii ya masaa ya usiku na mchana kulingana. Jambo linguine tunalopaswa kulijua ni kwamba Constantine, kwenye waraka unaohusu mabishano yanayopinga uadhimishaji wa Easter na wa Quartodeciman yaliyoelezwa hapo juu, anasema kwa masikitiko makubwa sana kwamba Wayahudi “wakatimwingine waliadhimisha Paschas mbili kwa mwaka mmoja, akimaanisha kwamba Paschas mbili ambazo wakati mwingine ziliangukia kati ya kipindi kimoja cha masaa ya usiki na mchana kulingana hadi cha pili chake" (kwa mujibu wa kitabu cha Cath. Encyc., Vol. V, op. cit.).

 

Maadhimisho haya yanaonekana kwamba itikadi ya marabi ilikuwa imetanguliwa na kitendo cha kuongeza mwezi mmoja na kuwa na mwaka mrefu. Sababu pekee kwa kufanyika kwake hivyo ilikuwa ni kuwezesha mapokeo yake yashikwe na kuepuka marejeo ya Sabato zinazohesabiwa nyuma kwa nyuma. Kalenda hii ya Hilleli haikuwepo huko nyuma hadi mwaka 358 BK, au 344 ilipoanzishwa huko Babeloni. Na hivyo basi tuaweza kuhitimisha kwa kusema kwmba utaratibu huu wa kuhesabu wa kalenmda hii ya Hilleli haikuwa ikitumika wala kujulikana kama ilivyoanza tu mwaka 325 BK. Wasamaria kila mara walianza mwaka tangia kuonekana kwa Mwezi Mwandamo wa baada ya tarehe 25 Machi.

 

Auamuzi uliofanywa na baraza ulikuwa ni kwamba "Easter na iadhimishwe katika Jumapili ya kwanza baada ya kipindi cha kwanza cha mwezi mkamilifu kinachofuatia siku ya masaa ya usiku na mchana kulingana" (Vol. III, op. cit.). utaratibu huu unafanya maadhimisho ya Easter yaangukie kipindi cha mapema sana cha tarehe 22 Machi na cha mapema zaidi ya tarehe 25 Aprili (ikimaanisha kuwa ni tehere ya mapema sana iwezekanavyo ya Jumapili na ndiyo ifanyike Sikukuu hii ambayo itaangukia kwenye kipindi cha siku saba za baada ya Pasaka). Hii ni kitu kingine tofauti na Pasaka na taratibu zake tena kuna mabadiliko na mpishano  ulio tofauti kati yake kuhusiana na tarehe iliyowekwa na ile ya zamani asilia. Utaratibu wa Helleli kwa hakika, unaweka mifumo miwili hii mbali kwa kipindi cha takriban zaidi ya mwezi mmoja (kama ilivyotokea mwaka 1997). Maamuzi ya Baraza ka kuweka Kanuni la Nicaea yalifanywa huko mjini Constantinople (mwaka 381) lakini nyaraka za Constantine zanaonyesha dhahiri kuwa ziliandikwa kabla ya mkutano huu uliounda Kanuni I ya Mtaguso wa Antioki a wa mwaka 341 ikionyesha kwamba maaskofu wa Syria kangia kipindi hiki walikubaliana na mafundisho na itikadi ya Warumi, ambayo kwa kweli yalitokana na maamuzi yaliyopitishwa huko Alexandria. Kanuni na sheria zilijulikana kuwa ni kama ifuatavyo:

1.      Easter ni lazima iadhimishwe na watu wote ulimwenguni kote na ni siku hiyohiyo ya Jumapili;

2.      Jumapili hii ni lazima iwe ile inayofuatia siku ya kumi na nne ya mwezi inaoadhimishwa Paschal;

3.      Mwezi ndio uwe kigezo cha upangaji wa maaadhimisho ya paschal [au Pasaka] ambavyo ni siku ya kumi na tano inayofuatia siku ya masaa ya mchana na usiku kulingana majira ya baridi [kutokana na sheria za kale ni siku ya 14 Nisan iliangukia kwenye siku ya masaa ya usiku na mchana kulingana majira ya baridi na sio kabla yake; nah ii ndiyo maana ya usemi huu kwamba inayofuatia baada ya siku ya usiku na mchana kulingana masaa ya majira ya baidi];

4.      Ni kwamba matoleo mengine yanapaswa yafanyike – huenda na makanisa ya Alexandria ambayo yamebobea sana kwenye elimu ya kuhesabu nyota na mambo ya angani – ili kuweza kuweka majira kamilifu na tarehe ya kuadhimisha Easter na kuwasiliana na ulimwengu mwingine uliobakia (tazama jarida liitwalo Leo to the Emperor Marcian in Migne, P. L., LIV, 1055).

 

Kwa hiyo uwekaji wa siku ya kuadhimisha Easter unaofanywa na waumini wa mrengo wa Jumapili ulitokana na imani na itikadi za kale ya uhesabuji wa mwezi wa Nisan, na uliutangulia utaratibu wa kalenda ya Hilleli. Ufafanuzi kuhusu jinsi walivyoamua na kuweka unaonyesha kwamba utaratibu wa Hilleli haukuwa unatumika hata kwa namna ya kiusaidizi, zaidi ya kuwa tu ya ile ya uahirisho na mara nyingine hata kwenye kiwango cha kupuuzia nyongeza ya mwezi mmoja, jambo ambalo kwa kweli lilikuwa ni sahihi.

 

Kwa hakika, Kanisa lilikuwa likiiadhimisha Paska kiusahihi hadi kufikia kipindi cha Polycarp na cha mabishano ya wa Quartodeciman kipindi ambacho karibu Kanisa liparaganyike mapande mawili. Nusu ya waumini wa Kanisa waliitunza vyema hadi kufikia takriban mwaka 190 BK.

 

Wakiweka msingi wao kutoka kwenye mtaguso huu wa Nicaea, makanisa ya mrengo wa Jumapili yanashikilia msimamo wao kuwa sikukuu ya Easter ya mwaka 1997 iliyofanyika kwenye siku mbili za mwisho za Mikate Isiyotiwa Chachu na sio siku ya kwanza kama walivyofanya tangu mwanzoni. Hata hivyo, wanaendelea bado kuhesabu kwenye mwezi wa Nisan kwa mujibu wa kanuni hizohizo walizozitumia siku za kale. Walikuwa wanafanya hivyo kwa kipindi cha takriban miaka 200 kabla ya kuanzishwa kwa kalenda ya Hilleli iliyoanzishwa mwaka 358 BK kwa kuwa ilichukuliwa kuwa ni iliyotokana na markebisho ya siku za karibuni zaidi na kukiuka sheria zinazosimamia uataratibu wa kupanga siku ya maadhimisho ya Sikukuu.

 

Hakuna kanisa lilote, liwe la Kiutatu ama lenye kuamini Mungu mmoja lililochuua utaratibu uliofuatia wa Wayahudi au wa Hilleli. Haikufanyika hivyo hadi ilipofika takriban karne ya ishirini ndipo utaratibu huu wakimakosa wa kupanga kalenda ulichukuliwa na Kanisa, na ni kwenye tawi peke yake. Hakuna wakati wowote ambao Kanisa lilifuata utaratibu wa Wasamaria wa kupangilia mwaka kutoka tarehe 25 Machi. Hata hivyo, tutajionea hilo kwenye jarida la Mwezi na Mwaka Mpya (Na. 213) [The Moon and the New Year (No. 213)] ambao hatimaye ulikuja kuwa ni Mwaka Mpya kwenye mataifa yaliyo kwenye nchi zinazojulikana kama za Anglo-Saxons na kwenye nchi ningine nyingi hatimaye. 

 

Utaratibu Mpotofu Kuhusu Mwezi wa Nane

Tutakwenda kujionea sasa ni kwanini Mungu alimshughulikia Yeroboamu kwa kitendo chake cha kuweka utaratibu mbaya wa maadhimisho ya mwezi wa Nane.

 

1Wafalme 13:1-3 Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba. 2 Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako. 3 Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika.

 

Mungu anatoa mafundisho kadhaa hapa kwenye andiko hili. Anasema kwamba anamtia mafuta mtu mwingine, na anatabiri marejesho mapya yatakayofanywa na Yosia. Kwa hiyo kwa kupitia unabii anamtaja Yule atakayekuwa mtiwa mafuta wake anayetuatia na kuwa atakuwa nani. Hii ilitokea wakati mfalme alipokuwa yungali madarakani bado.

 

Yeroboam alidhania kuwa angeweza kumuua nabii huyu wa Mungu. Hakujua kuwa ni Mungu peke yake ndiye anayeshughulika na manabii zake, na wanaweza kuuawa tu pale anapoamua na kuona kuwa wamekwisha timiliza mapenzi yake na ndipo vifo vyao vinaweza kuwa ni mfano au ushuhuda dhidi ya imani ile ambayo kwayo wametumwa kuionya.

 

1Wafalme 13:4-10  Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia maneno ya yule mtu wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli, alinyosha mkono wake pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake aliounyosha ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena. 5 Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la Bwana. 6 Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu, Umsihi sasa Bwana, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba Bwana mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza. 7 Mfalme akamwambia mtu wa Mungu, Karibu nyumbani kwangu ujiburudishe, nami nitakupa thawabu. 8 Mtu wa Mungu akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa; 9 maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la Bwana, kusema, Usile chakula cho chote wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia. 10 Basi akaenda zake kwa njia nyingine, wala hakurudi kwa njia ile aliyoijia Betheli.

 

Somo linalomhusu huyu nabii ni la muhimu. Mungu anawatumia watumishi wake  manabii wawaelekeze na inawapasa kuyatii. Tukio hili zima limefanywa kuwa kama somo kwetu katika utii wetu kwa Mungu. Mkosaji anaweza kurejeshwa upya tu kwa kupitia kwa msemaji aliyepewa ujumbe na Bwana. Ayubu alikuwa mfano wa jambo hili, na Yeroboam aliujua ukweli huo ksms tunsvyomuona akiomba aponywe.

 

1Wafalme 13:11-32 inasema:  Basi nabii mmoja mzee alikuwa akikaa katika Betheli; na wanawe wakamwendea wakamwambia kila neno alilolitenda yule mtu wa Mungu siku ile katika Betheli; na maneno aliyomwambia mfalme, hayo nayo walimwambia baba yao. 12 Baba yao akawaambia, Amekwenda zake kwa njia ipi? Kwa maana wanawe walikuwa wameiona njia ile aliyoiendea yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda. 13 Akawaambia wanawe, Nitandikieni punda. Wakamtandikia punda, naye akampanda. 14 Akamfuata mtu wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni, akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda? Akamwambia, Mimi ndiye. 15 Akamwambia, Karibu kwangu nyumbani, ule chakula.16 Naye akamwambia, Siwezi kurudi pamoja nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala sinywi maji pamoja nawe hapa; 17 kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana, Usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia. 18 Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo. 19 Basi mtu yule akarudi pamoja naye, akala chakula, akanywa maji nyumbani mwake. 20 Hata ikawa, walipokuwa wameketi mezani, neno la Bwana likamjia nabii yule aliyemrudisha; 21 akamlilia yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda, akinena, Bwana asema hivi, Kwa sababu umeiasi kauli ya Bwana, wala hukuishika amri ile aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, 22 bali umerudi, ukala chakula ukanywa maji, hapo alipokuambia, Usile chakula, wala usinywe maji; maiti yako haitaliingia kaburi la baba zako. 23 Basi ikawa, alipokwisha kula chakula na kunywa maji, yule nabii aliyemrudisha akamtandikia punda. 24 Na alipokuwa amekwenda zake, simba alimkuta njiani, akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti. 25 Na tazama, watu wakapita, wakauona mzoga umetupwa njiani, na yule simba akisimama karibu na mzoga, wakaenda, wakatoa habari katika mji ule alimokaa yule nabii mzee. 26 Na yule nabii aliyemrudisha njiani alipopata habari, akasema; Ndiye yule mtu wa Mungu, aliyeiasi kauli ya Bwana; kwa hiyo Bwana amempambanisha na simba, simba akamrarua, akamwua, sawasawa na neno la Bwana alilomwambia. 27 Akawaambia wanawe, akasema, Nitandikieni punda. Wakamtandikia. 28 Akaenda, akamwona yule maiti ametupwa njiani, na punda na simba wamesimama karibu na maiti; yule simba alikuwa hakumla maiti, wala hakumrarua punda. 29 Nabii yule akamtwaa maiti wa yule mtu wa Mungu, akamweka juu ya punda wake, akamrudisha; yule nabii mzee akaenda mjini mwake, kukaa matanga, na kumzika. 30 Akamweka maiti katika kaburi lake mwenyewe; wakamlilia, wakisema, Aa! Ndugu yangu! 31 Hata ikawa, alipokwisha kumzika, akawaambia wanawe, akasema, Nikifa mimi, nizikeni katika kaburi hili alimozikwa yule mtu wa Mungu; iwekeni mifupa yangu kando ya mifupa yake. 32 Kwa maana neno hilo alilolia juu ya madhabahu katika Betheli, kwa neno la Bwana, na juu ya nyumba zote za mahali pa juu zilizo katika miji ya Samaria, hakika litatimizwa.

 

Nabii alijaribiwa ili kumfanya awe mtiifu. Nabii mwingine akaje kumdanganya. Aliruhusiwa afanye hivyo ili iwe mfano wa mashahidi wa uwongo. Nabii wa kwanza alikuwa ni mfano wan eno la Bwana na akashuhudia nguvu za matendo yake. Ila hatimaye alipokabiliana na nabii mwingine aliyenena maneno kinyume na maelekezo aliyopewa na Mungu, alimuamini mtu mwingine na sio neno la Mungu alilolijua kuwa ni la kweli. Alilipa gharama ya kosa hili kwa uhai wake. Ili kuonyesha kuwa ametilimiza unabii, kakuzikwa kwenye makaburi ya baba zake, bali manabii walimzika kwenye kaburi lake mwenyewe, ambalo hatimaye angeweza kuzikiwa na Yule aliyesababisha kifo chake.  Jambo hili linafanyika hata kwenye siku zetu hizi na kwenye mazingira yetu pia. Tumeona maelekezo ya neno la Mungu. Tumejionea jinsi tulivyoitwa na uweza wa Mungu, lakini bado tunafuata maelekezo ya wanadamu na sio neno la Mungu. Hili limekuwa ni tatizo kwa muda mrefu sasa kwenye nchi hii, na Mungu anatenda kazi akishughulika na Kanisa. Waumini walio kwenye Kanisa la Mungu wajiepushe kuwa kama alivyokuwa Yeroboam, vinginevyo, au kila mmoja wao, awe mkubwa au mdogo, watapoteza na kukosa kuwa na sehemu katika Ufalme wa Mungu.

 

1Wafalme 13:33-34  Baada ya hayo Yeroboamu hakuiacha njia yake mbovu, lakini akafanya tena makuhani wa mahali pa juu, wa watu wo wote. 34 Kila aliyetaka akamfanya wakfu, ili wawepo makuhani wa mahali pa juu. Jambo hilo likawa dhambi kwa nyumba ya Yeroboamu, hata kuiharibu, na kuifuta usoni pa nchi.

Ni kama Yeroboam alivyowaweka utumishini waalimu wa uwongo waliofundisha na kuzua mafundisho ya uwongo na kushamirisha ibada za sanamu, ndivyo ilivyotokea pia kwa Kanisa lilijichanganya kwa kuyapa nafasi mafundisho ya uwongo, kwa kuliona neno la Mungu halina nguvu na kufundisha mawazo ya wanadamu. Watu wanaofundisha kwa lengo la kujipatia ajira ndio hasa waliofuata mafundisho haya ya uwongo. Mijada ya uwongo imeshamiri sana ikilenga kuhalalisha mafundisho ya uwongo. Moja ya mifano kuhusu wajumbe au watumishi wa Mungu (tazama jarida la Watumishi wa Mungu (Na. 184) [The Oracles of God (No. 184)]. Mijadala imeenea kwa kusema kuwa Wayahudi wana manabii wa Mungu na kwamba wanahusika na mambo yote ya Kalenda. Kama hilo ni kweli, ni kwa nini watu hawahawa wanalikubalia Agano Jipya lililokataliwa na imani ya Kiyahudi? Ne, ni kwa nini wanaiadhimisha Pentekoste siku ya Jumapili wakati Wayahudi wanaitunza siku ya 6 Siwani?

 

Waalimu hawahawa wenye mafundisho ya uwongo wanasema kile kilicho muafaka na sio kile kilicho sahihi.

 

Yeroboam bado hajatubu kwa uovu wake huu.

1Wafalme 14:1-5 Siku zile akaugua Abiya, mwana wa Yeroboamu. 2 Yeroboamu akamwambia mkewe, Ondoka, tafadhali, ujibadilishe, wasikujue kuwa mkewe Yeroboamu; ukaende Shilo; tazama, yuko huko Ahiya nabii, aliyeninena mimi ya kwamba nitakuwa mfalme juu ya watu hawa. 3 Twaa mkononi mikate kumi, na kaki, na mtungi wa asali, ukamwendee; naye atakuambia kijana atakuwaje. 4 Akafanya hivi mkewe Yeroboamu, akaondoka, akaenda Shilo, akaja nyumbani kwa Ahiya. Basi Ahiya hakuweza kuona; kwa kuwa macho yake yamepofuka kwa sababu ya uzee wake. 5 Bwana akamwambia Ahiya, Angalia, mkewe Yeroboamu anakuja akuulize mambo ya mwanawe; kwa maana hawezi; hivi na hivi umwambie; kwani itakuwa akiingia atajifanya kuwa mwanamke mwingine.

 

Watu hao hawakumuogopa Mungu. Nguvu za Mungu na uhusiano wa Mungu na watumishi wake manabii haikueleweka. Yeroboam alitaka kuwaomba msaada na ushauri manabii, bali hakuamini kamwe kuwa walikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Mungu. Ni makuhani waliowekwa wakfu tu peke yao ndio walichukuliwa kuwa na umuhimu wa muda mrefu wa kudumu. Na hii ndiyo sababu manabii walikuwa wanauawa. Walichagua kumtii Mungu na sio wanadamu.

 

1Wafalme 14:5-16  Bwana akamwambia Ahiya, Angalia, mkewe Yeroboamu anakuja akuulize mambo ya mwanawe; kwa maana hawezi; hivi na hivi umwambie; kwani itakuwa akiingia atajifanya kuwa mwanamke mwingine. 6 Ikawa, Ahiya alipoisikia sauti ya miguu yake, akiingia mlangoni, alisema, Karibu, mkewe Yeroboamu; mbona wajifanya kuwa mwingine maana nimetumwa kwako wewe, mwenye maneno mazito. 7 Nenda, umwambie Yeroboamu, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa kuwa nilikutukuza miongoni mwa watu, nikakufanya uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli, 8 nikaurarulia mbali ufalme utoke nyumba yake Daudi, na kukupa wewe; walakini wewe hukuwa kama mtumishi wangu Daudi, aliyezishika amri zangu, na kunifuata kwa moyo wake wote, asifanye lo lote ila yaliyo mema machoni pangu; 9 lakini umekosa kuliko wote waliokutangulia, umekwenda kujifanyia miungu mingine, na sanamu zilizoyeyuka, unikasirishe, na kunitupa nyuma yako; 10 tazama, kwa hiyo mimi nitaleta mabaya juu ya nyumba yake Yeroboamu, nami nitamkatia Yeroboamu kila mwanamume, aliyefungwa na aliyeachwa katika Israeli, nami kuondoa nitawaondoa waliobaki wa nyumba yake Yeroboamu, kama mtu aondoavyo mavi, hata itakapokwisha pia. 11 Yeye afaye wa Yeroboamu mjini mbwa watamla; afaye mashambani ndege wa angani watamla; kwa kuwa Bwana amelinena hilo. 12 Basi ondoka, urudi nyumbani kwako; na miguu yako itakapoingia mjini huyo kijana atakufa. 13 Na Israeli wote watamlilia, na kumzika, kwa maana ndiye peke yake wa Yeroboamu atakayeingia kaburini; kwa sababu limeonekana ndani yake jambo lililo jema kwa Bwana, Mungu wa Israeli, nyumbani mwa Yeroboamu. 14 Tena Bwana atajiinulia mfalme wa Israeli atakayeiharibu nyumba ya Yeroboamu siku ile; na nini tena hata sasa? 15 Kwa kuwa Bwana atawapiga Israeli kama manyasi yatikiswavyo majini; naye atawang'oa Israeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, naye atawatawanya ng'ambo ya Mto; kwa sababu wamejifanyia maashera yao, wakimkasirisha Bwana. 16 Naye atawatoa Israeli kwa ajili ya makosa ya Yeroboamu, aliyoyakosa, ambayo kwa hayo amewakosesha Israeli. 

 

Dhambi za viongozi wa watu ziliwafikia watu wao. Dhambi za Yeroboam zilikuwa ni kubwa sana. Ya kwanza ilikuwa ni ile ya kubadili maadhimisho ya Sikukuu hadi mwezi wa Nane. Alihukumiwa kwa ajili ya jambo hili. Hata hivyo, hakukata tamaa kuiabudu miungu yake ya uwongo na kwa sababu hiyo na kwa Maashera, Israeli walifukuzwa na kupelekwa mbali utumwani, nyumba ya Yeroboam ilihukumiwa na kulikuwa na vita na Yuda siku zote za uhai wake, kwa wote wawili, yaani na rehoboam na Abiya (1Wafalme 15:6-7).

 

1Wafalme 14:17-20 Basi mkewe Yeroboamu akaondoka, akaenda zake, akafika Tirza; naye alipofika kizingitini kwa nyumba, huyo kijana akafa. 18 Israeli wote wakamzika, wakamlilia; sawasawa na neno la Bwana, alilolinena kwa mkono wa mtumishi wake Ahiya nabii. 19 Na mambo yake Yeroboamu yaliyosalia, ya kupigana na ya kutawala, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli. 20 Na siku alizotawala Yeroboamu zilikuwa miaka ishirini na miwili; akalala na babaze, naye Nadabu mwanawe akatawala mahali pake.

Yeroboam aliwasababisha Israeli wafukuzwe na kwenda mbali utumwani kwa ajili ya uongozi wake mbovu na dini yake ya uwongo. Yuda nao hawakuwa na afadhali yoyote, na mabaki au masalio ya Wasamaria walikuwa ni wachache na kundi dogo na wakiwa wamebakia kwa ajili ya kutimiliza usemi na ni mchanganyo wa moja kwa moja kuhusu haki ya uzaliwa wa kwanza ya Efraimu, ambaye kwaye wanadai kuwa ni wazao wake. Efraimu ni donge aminifu. Uzao wake utafanyika kuwa mataifa mengi (Mwanzo 48:19; 49:26). Masihi atarudi hivi karibuni na Wasamaria na Wayahudi watafanywa wayajue makosa yao kwenye kipindi hiki cha muhimu sana ambacho ulimwengu wote utamuabudu Mungu Mmoja ma Wapekee na wa Kweli.

Israeli wanarithi ahadi waliyopewa licha yakustahili na kujitoa kwao. Mungu atayafungua macho yao na watayaona makosa yao zitakapofika Siku Hizo.

q