“Siku ya Sabato ni Takatifu kwa Bwana kwa mujibu wa Amri ya Nne ya Mungu
(Kutoka 20:8-11). Amri hii imewekwa ili kuwafanya watu
wote wapumzike (Kumbukumbu la Torati 5:14). Siku hii inajulikana kama
siku ya Jumamosi kwa mujibu wa mpangilio wake wa kimahesabu uliotokana kwa
mujibu wa chanzo chake cha tangu uumbaji. Inajulikana na
mataifa yote kama ni siku ya Sabato na kwamba
inaangukia siku ya Jumamosi ya kalenda iliyoko sasa ya juma. Siku hii ya saba iko kwenye mzunguzo endelevu na haiwezi kuwekwa kwenye
siku nyingine yoyote” (Cox, W.E., “A” kwenye jarida lake la Sabato
(Na. 31) [The Sabbath (No. 31)], lililochapishwa
na CCG. 1994-2008, ukurasa wa 2).
Siku ya Sabato
Utaratibu wa jinsi ya kuitunza Sabato hii ya juma umeainishwa kwenye kitabu
cha Kutoka 20 na Kumbukumbu la Torati 5.
Kutoka 20:8-11 inasema:
Ikumbuke
siku ya Sabato uitakase. 9
Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato
ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako,
wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa
kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa
siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo,
akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
Kumbukumbu la Torati
5:12-15 inasema:
Ishike siku ya Sabato
uitakase, kama BWAA,
Mungu wako, alivyokuamuru. 13 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 14
lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi
yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi
wako, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni
aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vilevile
kama wewe. 15 Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri,
na ya kuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko na mkono
wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wako,
alikuamuru uishike Sabato.
Katika
Kamusi ya Kiebrania iitwayo Strong
Hebrew’s Dictionary (SHD 7676), neno sabbat
linamaana ya kupumzika yaani kutoka kwenye shughuli ngumu za mahangaiko,
(kusababuisha kuacha, kujiachia, kujifanyiza) kusimama au kuachana na shereheko: (kufanya
kuwa) mapumziko, kupumzika, kutoshughulika, kuachana au kuachilia.
Kutoka
23:12 inasema: "Siku sita
utafanya kazi yako, na siku ya saba utapumzika; ili
kwamba ng'ombe wako na punda wako wapate kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako
na mgeni wapate kuburudika”.
“Maadhimisho
ya Sabato yanaendana na kicho kwa Bwana na kupaheshimu
Patakatifu pake (mambo ya Walawi 19:30), jambo ambalo sisi tunalifanya. Kwa
hiyo, siku hii ya Sabato iliwekwa kwa ajili ya
wanadamu ili kuitakatifusha Maskani yake Bwana na kuifanya iwe mahali maalumu
na muafaka pa kuweka makazi yake Mungu. Sambamba na hilo, Sabato inaendana na
tendo la kuwaheshimu mama na baba (Mambo ya Walawi 19:3)” (Cox, “A”,
kitabu hichohicho, ukurasa wa 4).
Siku ya saba huanzia mwishoni mwa siku ya sita ya juma, ambayo ni
Ijumaa kama tulivyozoea kuiita, wakati giza
linapoanza (EETN) (Mwanzo 1:5; Zaburi 104:20; Mambo ya Walawi 23:32. Matendo
27:27-33). Sabato hii ya siku ya saba inabakia kwa wanaoiadhimisha na kuitunza
ambao pia ni watu wanaolirejesha u[ya agano (Waebrania
4:9; Wakolosai 2:16-17).
Waebrania 4:9-11 inasema: Basi, imesalia raha ya Sabato [SGD4520] kwa watu wa Mungu. 10 Kwa maana yeye aliyeingia katika raha
yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake.
11 Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije
akaanguka kwa ,fano huohuo wa kuasi.
“Tendo hili la kuitunza Sabato linaendana na ukusanyikaji pamoja na kufanya ibada, kama
ilivyofundishwa na Mtume Paulo (Waebrania 10:23-25). Tendo la kukusanyika siku
ta Sabato limeamriwa na Mungu kwenye kitabu cha Mambo
ya Walawi:
Mambo ya Walawi 23:1-3 inasema: Kisha BWANA
akanena na Musa, na kumwambia, 2 Nena na wana wa
Israeli, na kuwaambia, Sikukuu za BWANA,
ambazo mtazipigia mbiu kuwa ni makusanyiko matakatifu; hizi ni sikukuu zangu.
3 Mtafanya kazi siku sita; lakini siku
ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko
takatifu, msifanye kazi ya namna yoyote; ni Sabato kwa BWANA katika makao
yenu yote.
Neno la Kiebrania litumikalo kuelezea mapunziko ni migra, ambalo maana yake ni kuitisha
makutano na kukutanika (pamoja), na kwa mujibu wa Kitabu cha fasiri cha Young’s
Analytical Concordance, neno Migra ndilo lililotumika kwenye Mambo ya
Walawi 23:4-44 kuyaelezea makutaniko yote matakatifu yaliyoamriwa na Mungu kuwa
ni Sabato zake kuu na takatifu. Ili kuwasaidia watu wake wazitunze Sabato zake na kuzitakatifuza, Mungu aliwapa siku ya sita kuwa ni siku
ya maandalio (kama inavyosema Kutoka 16:1-21).”
Maandalio ya Sabato
“Tumeamriwa kufanya maandalio au kuiandaa
Sabato ifikapo siku ya sita ya juma (kama
inavyosema Luka 23:54). Kwa kufanya maandalio maalumu na
halisi tunaweza sote kuwa na mapumziko muafaka ya Sabato kwa kadri alivyotuamuru
Mungu, na kuitunza Sabato hii kwa hali yake takatifu. Wakati baba yetu amri ya
kuitenga siku ya kufanya maandalio na amri ya kuitunza
Sabato, alikuwa anatutengenezea njia ya kumfuata yeye na kuyashika mapenzi yake
(sawa na ilivyo kwenye Mwanzo 2:2-3). Kama
tutazitii amri zake na kuacha kuyafanya yanayotupendeza
wenyewe na yenye ‘kutufaidisha’ sisi wenyewe siku ya Sabato, ndipo tutaweza
kumjua Mungu wa Kweli na Kristo wake, jambo linalotupelekea kuupata uzima wa
milele (Yohana 17:3). Pia soma jarida la Uzima wa Milele (Na. 133) [Eternal Life (No. 133)].
Tunapoitumia siku hii ya maandalio kwa
kuitafakari na kuichukulia Sabato kuwa ni siku ya kuwa karibu na Mungu na
kujitenga na dunia na mambo yake yote na kuweka kando mambo yetu mengine yote,
na kuwa mbali na mambo yetu mengine yote ya kidunia na kutojihusisha nayo na
kuyafanya wakati Sabato itakapoanza. Na tunapokutanika pamoja katika siku hii
ya Sabato na kujifunza kujifunza Neno takatifu la Mungu kama alivyofanya
Mariamu, tunakuwa tumeamua ‘kuchagua uamuzi mzuri’” (Kwa mujibu wa Cox, W.E.,
“B” jarida lake la Ijumaa: Maandalio ya Sabato (Na. 285) [The Juma’ah: Preparing for the
Sabbath (No. 285)], na kitabu chake cha CCG, 1999-2008, ukurasa
wa 2,9).
Hakuna Kufanyakazi Siku ya Sabato
“Hatupaswi kuwa
wavivu na kutofanyakazi. Chochote tunachoweza kukifanya kwa mikono
yetu, na tukifanye kwa bidii na nguvu zetu zote (Mhubiri 9:10). Kwa kuwa kile tunachokipanda ndicho tunachokivuna (Wagalatia 6:7).
Pia tunatakiwa kuwatumikia na kuwasaidia ndugu zetu
wapendwa wengine wote, hususan walio wageni miongoni mwetu (3Yohana 5-7).
Hakutakiwi
kufanywa kazi yoyote siku ya Sabato kwa mtu yeyote
binafsi yake wala kwa kikundi chochote kwenye jamii kilichopo kwenye milki ya
Israeli. Bali Amri na Sheria ilitakiwa itunzwe ama
kuadhimishwa na Israeli wote—kwa mgeni na kwa Muisraeli wote amri ilikuwa ni
moja tu. Nehemia anatupa mfano kwa dhana hii ya
jinsi sheria au amri inavyopaswa kutunza na kuadhimishwa siku ya Sabato gives
us examples as to the manner in which.
Nehemia 10:28-31 inasema: Na watu waliosalia,
makuhani, walawi, mabawabu, waimbaji, Wamethini, na hao wote waliojitenga
katika watu wa nchi kwa torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao,
kila mwenye maarifa na akili; 29 wakaambatana na ndugu zao, wakuu zao nao
wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea torati ya Mungu,
iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda,
amri zote za BWANA, Bwana wetu, na hukumu zake na sheria zake; 30 wala
tusiwaoze watu wan chi binti zetu, wala kuwatwalia wana wetu binti zao; 31 tena
watu wan chi wakitembeza biashara, au
chakula chochote, siku ya Sabato, tusinunue kwao siku ya Sabato, au siku
takatifu; tena kwamba tuuache mwaka wa saba, na madai ya kila deni
Hairuhusiwi kubeba mzigo wowote siku
hii ya Sabato, wala haukuruhusiwa kuingizwa kwenye mji wa
Yerusalemu (Yeremia 17:21). Kwa hiyo tunapaswa kufurahia siku hii ya Sabato na kuleta furaha kwenye Nyumba ya Bwana, Mungu wetu. Kwa hiyo,
hata kufanya kazi kwenye mali za mtu kumekatazwa
pia siku hii ya Sabato. Inatakiwa iwe hivyo ili
kuipisha na kuitakativusha Sabato na ndiyo inayotakiwa itukuzwe peke yake.
Kuishika Sabato ni
sharti la muhimu kwa mwanadamu ili aweze kuurithi ufalme wa Mungu wa Israeli. Hakuna mzigo ulioletwa ama kuingizwa ndani ya malango ya mji.
Wafalme na Wana wa ufalme wote wataketi kwenye kiti cha
enzi cha Daudi. Na kama
maonyo haya hayatatiliwa maanani ndipo mji utaangamizwa kwa moto (Yeremia
17:27). Kwa hiyo, Sabato ni ishara na chanzo cha kubezwa
na kuteswa kwa wale walio wa Nyumbani mwake Mungu. Mfale na
kuhani wawaka hasira kwa kutiwaunajisi Sabato (Maombolezo 2:6).
Maombolezo
2:6 inasema: Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu, Kana kwamba
ni ya bustani tu; Ameziharibu sikukuu zake; Bwana amezisahauzisha katika Sayuni
Sikukuu za makini na sabato; Naye amewadharau mfalme na kuhani Katika uchungu
wa hasira yake.
Kwa hiyo, sabato inajulikana kuwa
inawakilisha mfumo wa kipekee kwa watu wa Mungu.
Inaendelea kuwa ya muhimu kwao wote na hakuwezi kuwa
na kufanyika mauzo au biashara siku hii ya Sabato au kwenye Siku Takatifu
yoyote iliyoamriwa, kwa mtu yeyote mongoni mwao au hata kumruhusu Mmataifa (asiye
miongoni mwa aweaminio).
Yeyote anayeitia unajisi Sabato sharti
lililowekwa ni kuuawa (Kutoka 31:14; Hesabu 15:32-36).
Hukumu hii inamaanisha au kuashiria ufalme wa milele
walioahidiwa ama kupewa wateule. Wanakatiliwa mbali na
watu wao, ambayo kutouingia uzima wa milele. Hii ni ishara
kati ya Mungu na wana wa Israeli milele
(Kutoka 31:17). Neno
milele maana yake ni
Olam (SHD 5769) na linamaanisha tendo la wakati wote, lisilokoma, la milele, lenye kudumu hivyo (milele), lisolo
na mwisho, nk.
Kazi ya Makuhani Siku ya Sabato
Ni jambo la kawaida sana kwamba makuhani
wakiwa Hekaluni wanaweza kuihalifu Sabato (na ni kawaida) na hawahesabiwi kuwa
na hatia (Mathayo 12:5; sawa na Hesabu 28:9-10; pia tazama Nehemia 13:7; Ezekieli
24:21; Yohana 7:22-23). Kwa hiyo, kazi zozote tunazozifanya sisi wateule zinazohusiana
na kumfanyia Mungu ibada siku hii ya sabato haina
makosa wala haihesabiwi hatia. Na kwa kweli, kulikuwa
na dhabihu nyingi sana
zilizokuwa zikiletwa Hekaluni siku ya Sabato kuliko siku nyingine yoyote ile ya
juma.
Sadaka ya kuteketezwa motoni ililetwa na kutolewa na kuhani kwa niaba ya wana wote wa Israeli siku
ya Sabato, kuwa sadaka ya milele kwao (Mambo ya Walawi 24:8). Sadaka hii
iliamriwa kutolewa na wateule kwamba waitoe na
kuiombea na kutoa shukjurani wao kwa Bwana kila siku ya Sabato. Kwa hiyo tumeamriwa kutoa sadaka zetu tunapokusanyika. Kinachoelezewa
inazidi kwenye ayah ii ya mambo ya Walawi 24:1-4 ni
kwamba inampasa kuhani ahakikishe kuwa taa zote ziwe zijazwa mafuta safi ya kila siku
yaliyofanywa kwa kukamua mzeituni. Kwa hiyo inatukumbusha leo
kuwa maandalizi ya wateule ni wajibu wa kila siku, na taa za wanawali ni lazima
zitengenezwe na ni kazi ya kila siku, yaani Sabato hadi sabato nyingine.
Wanatakiwa na ni wajibu wao kabisa kuzitunza na
kuziadhimisha Sabato hizi za Mungu (Ezekieli 44:24).
Nehemia aliamuru kuwa hata wageni wazitunze pia Sabato. Huyu ni mfano wetu kwa jinsi tunavyopaswa
kuitunza Amri hii inavyopaswa kufuatwa na kuishika. Nehemia 13:22 inaonyesha
kuwa ni wajibu wa Bwana—kuhani mpya wa
wateule—kujitakasa wenyewe na kulinda malango ili kuhakikisha Sabato
zinaadhimishwa katika utakatifu wake.
Kadiri tunwezavyo, tujitahidi kuwa
tunaacha kufanya kazi, au kusimamisha shughuli zetu zote siku ya Sabato, na tusinunue wala kuuza, na tunapaswa kufanya hivyo, na
tunapaswa kupingana na kushinda aina yoyote ya upinzani. Hatupaswi
kununua pia kwenye Siku Takatifu. Tusiende kwenye mikahawa siku za
Sabato na Siku Takatifu za Bwana.
Nehemia 13:15 Siku hizo naliona katika Yuda watu wengine waliokanyaga
mashinikizo ya mvinyo siku ya sabato, na wengine waliochukua miganda, na
kuwapakia punda zao; tena na mvinyo, na zabibu, na tini, na namna zote za
mizigo, waliyoileta Yerusalemu, siku ya sabato; nami nikashuhudia juu yao siku ile waliyouza
vyakula.
Nehemia 13:19 Ikawa malango ya Yerusalemu
yalipoanza kuwa na giza kabla ya sabato, naliamuru milango
ifungwe, nikaamuru isifunguliwe hata sabato iishe; na baadhi ya watumishi wangu
nikawaweka juu ya malango, ili usiingizwe mzigo wo wote siku ya sabato.
Nehemia 10:31 tena watu wa
nchi wakitembeza biashara, au chakula cho chote, siku ya sabato, tusinunue kwao
siku ya sabato, au siku takatifu; tena kwamba tuuache mwaka wa saba, na madai
ya kila deni.
Kuwasha moto siku ya Sabato
Amri isemayo, “Hamtawasha moto katika nyumba zenu kwa siku ya Sabato” inamaanisha tendo la
kuwasha kwa mnajiri wa kikazi au kuwasha kwa nje na sio kuwasha majumbani na
kwa matumizi ya nyumbani (Kutoka 35:1-3).
Hata Hekaluni kulikuwa na dhabihu za daima. Watu walikuwa wanawasha moto muda wote. Na kama tukirudi nyuma na kuangalia aya za kwanza
asilia, na kuona jinsi Sheria hii ilivyotolewa, amri hii ilikuwa inahusika na
dhana ya kufanikisha na kufanikisha. Hakuna kazi ya ujenzi au
ubomoaji uliofanyika au kuruhusiwa kufanywa Siku ya Sabato” (Cox, “A”,
op. cit., kurasa za 2, 3, 4, 5).
Aya
zilizo kwenye Kutoka 35:4-35 zinafafanua kazi kubwa inayoonyeshwa kwamba kwazo
moto isiwashwe siku za Sabato.
“Hii pia haiathiri uwashaji
wa moto kwa lengo la kupasha maji moto au kupasha moto
kwa aina yoyote, ambao ni muhimu kwa ajili ya uzima wa watu kunakutumika sehemu
nyingi za Dunia zenye hali ya hewa baridi. Inavyotokea hivyo, basi siku ya maandalio
itumike kwa kazi ya kukusanya kuni au kununua mafuta
na kwa ajili ya kupikia, lakini siku ya Sabato kumekatazwa kabisa. Ni kwa sababu hii ndiyo maana Kristo alikula masuke mashambani
siku ya Sabato (Mathayo 12:2). Hukumu kwa asiyeenda
kujihudhurisha na kumwabudu Mungu siku ya Sabato ni kifo. Kwa hiyo, kazi yoyote
ya namna hii kuifanya Siku ya Sabato ni tendo la
kuivunja Sheria na kuiwekwa kwenye Ufufuo wa Pili na kupelekea kwenye mauti ya
pili” (sawa na Hesabu 15:32-36)” (Cox, “B”, op. cit., ukurasa wa 6).
“Ndipo hapa kwamba lile tendo la Bwana la kuchuma masuke siku ya
Sabato lililaumiwa. Hata hivyo, Bwana alionyesha
kwa matendo kwamba yeye alikuwa ndiye Bwana wa Sabato
na sio kwamba alikuwa anakusudia kuonyesha kuwa Sabato haina umuhimu kuitunza kama ilivyoelekezwa hapo mwanzoni. Ni jambo muhimu kuwa na tabia ya kuandaa chakula cha kutosha ili kukila siku ya
Sabato kama inavyoelekezwa kwenye ayah ii na pia kwenye Aheria na Amri za Agano
Jipya (Mathayo 12:1-12).
Kuwatunza
wagonjwa siku ya Sabato
Kristo alitoa pia amri
inayohusu kuwaponya wagonjwa. Amri hii inapaswa ifanywe siku ya Sabato. Kwa
hiyo, vi jambo jema sana kuwaponya na kuwalisha au kuwahudumia
wagonjwa siku ya Sabato.
Yohana 7:23 Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya
sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona
mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?
Marko 3:1-5 Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza; 2 wakamvizia ili kuona kama
atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki. 3 Akamwambia
yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati. 4 Akawauliza,
Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au
kuiua? Wakanyamaza. 5 Akawakazia macho
pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao,
akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima
tena.
(sawa
na Luka 6:8-10; 13:14-16; 14:3; Mathayo 12:10-13).
Kama inavyoruhusiwa kufanya tohara siku ya
Sabato, ndivyo pia inaruhusiwa kufanya tohara ya mioyo yetu kwa
njia ya kutoa na kwa uweza wa Roho. Hebu na
tuhukumiane kwa hukumu ya haki kwa kutathmini mema tuyafanyayo siku hii ya
Sabato (Yohana 7:21-24).
Ng’ombe anapotumbukia shimoni
Fundisho la ng’ombe au punda
kutumbukia shimoni ni
jambo la dharura na nadra kutokea. Haitoshi kufanya jambo lililopangwa
mapema hapo kabla nyuma yake. Luka 14:5 inaonyesha kwamba ni muhimu kushughulika mabo ya dharura siku ya Sabato. Na kwa kweli, hii inahusu na dhana au hali ya kuwaponya watu siku
ya Sabato. Tendo la kuwahudumia vizuri wagonjwa siku ya Sabato ni tatizo kubwa sana.
Kwenye Kumbukumbu la Torati 5:14, kunaonekana kabisa
kwamba Amri na Sheria hii imewekwa wazi kwa wote,
yaani wanadamu na wanyama.
Moyo na nia safi kuhusu Sabato
Moyo safi unatakiwa siku
ya Sanato. Haipaswi mtu kuyaangalia maslahi na mambo
yake na kushughulikanayo, kwa kuwa kwa kujiepusha na hayo kutamfanya awe na
hali ya uaminifu, kujitolea na kujitoa na kuwasaidia wengine (Amosi 8:5).
Sabato inapaswa itunzwe kwa usafi wa moyo (Isaya 1:13). Haitakiwi
itiwe unajisi (Isaya 56:2, 4-7).
Isaya 56:2 Heri afanyaye haya, na mwanadamu
ayashikaye sana;
azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote.
Siku ya Sabato ni ya furaha, na sio ya maombolezo (Isaya 58:13-14). Sabato ni ya kuifurahia
na kuifanya ifurahiwe na wote walio kwenye nyumba ya Mungu (Zaburi 118:24).
Isaya 56:4-7 inasema: Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika
sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na
kulishika sana
agano langu; 5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya
kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti;
nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. 6 Na
wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa
watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;
7 Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na
kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao
zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya
sala kwa mataifa yote.
Kristo alikuwa ni
mkuu kuliko Hekalu, kama sisi tulivyo wakuu
kuliko Hekalu lililojengwas la kimwili. Sisi ni Hekalu na Hekalu lilijengwa kwa
ajili yetu (Marko 2:27), ili tuweze kuzitunza Sabato kama maandalio ya nyumba
ili kutufanya sisi tuwe haiba ya Mungu” (Cox, “A”, op. cit., kurasa za
2,3,4,5).
Sabato
kama ishara-alama ya Kanisa
“Sabato imeorodheshwa kuwa ni alama muhimu
ya watu wa Mungu. Ni ishara kati yetu sisi na Mungu
atutakasaye. Kwa mujibu wa (SHD 226), neno ishara linaitwa owth au oth na linamaana
ya ishara, alama, kielekezi, ushahidi,
nk. Mungu hutumia ishara au alama fulani ili
kuwatofautisha na kuwambulisha watu wake kwa uhusiano wake maalumu naye.
Kutoka 31:12-17 inasema: Bwana akasema na Musa, na
kumwambia, 13 Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na
kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na
ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana
niwatakasaye ninyi. 14 Basi mtaishika hiyo
Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake
atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo
itakatiliwa mbali na watu wake. 15 Kazi itafanywa siku
sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa Bwana;
kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato, hakika yake atauawa. 16 Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato,
kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. 17 Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani
kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na
kupumzika.
“Utazishika Sabato zangu” (nyingi). “Sabato zinaelekea hadi kwenye kilele chote cha ibada zinazofanywa
kwenye Siku Takatifu zilizoorodheshwa na kutajwa kuwa
ni Sabato za Mungu. Hukumu ya kifo ni ya kiroho.
Sabato haiwezi kutenganishwa na ishara ya
Kanisa. Pia ni ishara ya wana wa agano ambao hawajaitwa
bado na kujiunga na Kanisa. Iwapo kama ilikuwa ni ishara ya wateule, basi imani ya
Kiyahudi ingekuwa na sehemu katika Ufufuo wa Kwanza,
jambo ambalo halipo hivyo.
Hali ya kuiweka Imani pamoja lilikuwa ni fundisho muhimu la Mungu. Sabato, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu zilizoamriwa na Mungu yalikuwa ni mambo
yasiyoweza kutofautishwa katika kumwabudu Mungu. Hii pia ilikuwa inaenda
sambamba au kupewa mshiko na kutambua umuhimu wa
sheria ya vyakula kwa hali ya undani na umuhimu wake kwa ujumla (soma jarida la
Sheria Kuhusu Vyakula (Na. 15) [The Food Laws (No. 15)]. Kwa hiyo, Sabato
nay ale yanayofuatananayo yote yalikuwa ni ishara ya
ibada ya kweli iliyolenga kumwabudu Mungu wa Pekee na wa Kweli (Yohana 17:3). Mungu
huyu ambaye pia huitwa Eloah, alikuwa ni yeye yule
aliyeabudiwa na watu wa Yuda na ndiye aliyefunuliwa kwenye Agano Jipya. Pia
angalia na kulisoma jarida la Mungu Tunayemwabudu (Na. 2) [The God We Worship (No. 2)].
Msingi wa kibiblia
kuhusu mafundisho asilia umetuama kwenye Amri Iliyokuu na ya Kwanza (kama
ilivyoelezewa kwenye jarida la Amri Iliyokuu nay a Kwanza
(Na. 252) [The First Great Commandment (No.
252)].
Kwa jinsi hii tunaona kwamba amri hii ya nne ndiyo
amri pekee yenye sara au mtazamo mkuu na wenye muundo mkuu na muhimu. Sabato na Siku Takatifu ni sehemu ya muundo wa amri hii ya nne na
inamuingiliano na amri nyingine zote.
Kutokana na neno linalotoka kwa Yesu Kristo
mwenyewe, Baba Mungu anakuwa ndani yake na lengo la kwanza muhimu na hukamilisha
lengo la Imani (Mathayo 22:37-38; Marko 12:30; Ufunuo 1:8). Ufunop wa kumjua Mungu Mmoja wa Pekee na wa Kweli ni muhimu katika
kuupata uzima wa milele (Yohana 17:3; 1Yohana 5:20). Kwa hiyo, Amri hii ya nne haiishii kwake yenyewe tu bali ni ashirio la kwanza la
mteule na ukweli wa utii wao kwa Mungu.
Amri hii ya nne pia
inaendelea mbele hadi kuufanya mfumo wote wa ibada za kibiblia za Miandamo ya
Mwezi, Sikukuu zilizoamriwa na Siku Takatifu na pia kwenye utoaji wa zaka. Soma
jarida la Utoaji
wa Zaka (Na. 161) [Tithing (No. 161)] ambayo
inahusiana na mfumo wa malimbuko na Agano la Mavuno (saoma pia jarida la Agano la
Mungu (Na. 152) [The Covenant of God (No. 152)].
Sabato ni ishara ya
Kanisa la kweli la Mungu. Sio ni dalili. Ishara ya kwanza ni Imani
juu ya Uungu, ambao unatokana na fundisho la kibiblia la Imani ya kuwa Mungu ni
Mmoja ya muundo na mwonekano wa Kiunitari.
Ishara nyingine za Wateule
Ishara inayoonekana kwa nje ya wateule ni
utunzaji wa Sabato, na ushiriki wa Meza ya Bwana au Mlo wa Pasaka, vikifuatiwa
na adhimisho la Mwandamo wa Mwezi na maadhimisho ya Siku zote Takatifu
zilizoamriwa. Ubatizo ni ishara ya pili kumpokea Roho
Mtakatifu ni mhuri au ishara ya ndani. “Ishara muhimu na
ya kwanza ya agano kwa watu ilikuwa ni tohara (Mwanzo 17:10-14). Hii
ilitimilizwa kwa amri au utaratibu wa ubatizo (soma jarida la Toba na
Ubatizo (Na. 52) [Repentance and Baptism (No. 52)]” (Cox, W.E., “C” na Wajibu wa Amri ya Nne katika Historia ya Makanisa ya
Mungu ya Watunza—Sabato (Na. 170) [The Role of the
Fourth Commandment in the Historical Sabbath-keeping Churches of God (No. 170)], CCG, 1996-2000, ukurasa wa 2,3,18).
“Kama
ilivyokuwa tangu siku za Kristo, ubatizo wetu ndio ukiri na agano letu la
kudumu kwenye agano hili. Ubatizo huu ni ishara kwa mataifa, ambao unafanya mambo kwa namna ile
ile kama ilivyokuwa ishara ya zamani ya tohara
iliyofanywa na Israeli. Alama hii ashirio ilichukuliwa kutokana na desturi ya kufanya tohara ya kimwili na kufanywa kuwa ni
tohara ya kiroho ya mioyoni. Kanisa liliwekwa kwenye kiwango cha mwajibiko wa utii
kwa Amri za Mungu, ambapo linafanya hivyo kwa kufanya tohara ya mioyo (Kumgukumgu
la Torati 30:6; Yeremia 4:4)” (Cox, W.E., “D” kwenye jarida la Agano la
Mungu (Na. 152) [The Covenant of God (No. 152)],
CCG, 1996-1999, pp. 2,13).
Kumbukumbu la Torati 30:6 BWANA, Mungu wako,
atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili
umpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate
kuwa hai. (sawa pia na Kumbukumbu la Torati 10:15-16)
“Ubatizo wa Roho
Mtaakatifu ni siahara ya kwanza pia ya wateule kupitia kwa Yesu Kristo katika
Mwili mmoja (Mathayo 28:19; Matendo 1:5; 11:16; Warumi 6:3; 1Wakorintho 12:13; Waebrania
9:11-28).” Ishara nyingine ni adhimisho la Pasaka na
Mikate Isiyotiwa chachu, kama tunavyojionea
kwenye kitabu cha Kutoka 13:9-16.
Kutoka 13:9-16 inasema:
Nayo itakuwa ishara
kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya
macho yako, ili kwamba sheria ya Bwana ipate kuwa kinywani mwako; kwani Bwana
alikutoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo. 10 Kwa
hiyo utaitunza amri hii kwa wakati wake mwaka baada ya mwaka. 11 Itakuwa hapo Bwana atakapokuleta katika nchi ya
Wakanaani, kama alivyokuapia wewe na baba zako, na kukupa, 12
ndipo utamwekea Bwana kila afunguaye tumbo, na kila mzaliwa wa kwanza
uliye naye, azaliwaye na mnyama; hao waume watakuwa ni wa Bwana. 13 Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa
mwana-kondoo; na kwamba hutaki kumkomboa, utamvunja shingo; na kila mzaliwa wa
kwanza wa binadamu katika wanao utamkomboa. 14 Kisha
itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza keshoni, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia,
Bwana alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake; 15 basi ilikuwa hapo Farao alipojifanya kuwa mgumu ili asitupe
ruhusa kuondoka, Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote waliokuwa katika nchi
ya Misri, wa binadamu na wa mnyama; kwa ajili ya hayo namtolea Bwana wote
wafunguao tumbo, wakiwa waume; lakini wazaliwa wa kwanza wote wa wana wangu
nawakomboa. 16 Jambo hilo litakuwa ni ishara mkononi
mwako, na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa Bwana alitutoa Misri kwa uwezo
wa mkono wake.
“Mwendelezo huu wa
amri ya nne unakusudia kuweka mkazo wa sheria na amri za Mungu kwenye matendo
yetu (mikononi) na kwenye fikra zetu (kwenye vipaji vya nyuso, kati ya macho).
Ni ishara ya amri ya Bwana (Kumbukumbu la Torati 6:8) na
jinsi alivyowaokoa Israeli (Kumbukumbu la Torati 6:10).
Ishara hizi za maadhimisho ya Sabato na Pasaka ni mhuri uliogongwa mkononi na kwenye paji la uso
kwa Wateule wa Bwana Mungu. Pamoja na Roho Mtakatifu
wanaweka msingi wa mhuri wa wana wa Mungu uliotajwa kwenye Ufunuo 7:3. kwa hiyo, ishara ya wateule inatuama kwenye amri ya kwanza. Kristo alisema, “Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke
yake (au kumtumikia)”
(Mathayo 4:10; Luka 4:8). Kumtumikia ni lile
tendo la kumfanyia ibada kwa mujibu wa isemavyo biblia.
Adhimisho la siku ya Upatanisho ni ishara nyingine ya agano la watu. Tendo la kushindwa
kuitunza siku hii ya Upatanisho limewekewa hukumu ya kumtenga mtu huyo mbali na watu wake, au kwa maneno mengine ni kwamba mtu huyu
atengwe mbali na mwili au bodi ya wana wa maagano wa Israeli ambao ni Kanisa la
Mungu leo (Mambo ya Walawi 23:29) (Cox, “C”, kitabu hicho hicho,
ukurasa wa 3).
“Ili
kufanya ukumbusho wa maagano yetu ya kuzishika amri za
Mungu, Biblia inatuamuru pia kuwa tuvae utepe wa rangi ya bluu kwenye kingo au
mwishoni mwa mavazi yetu (sawa
na isemavyo Hesabu 15:37-41).
Kwa kuwa sheria hii haihusiani na kipindi chochote cha muda wowote, au mahali haisemi mahali
au shughuli zinazohusiana nayo, inabakia kuwa ni uamuzi wa mtu binafsi kuendelea
kufanya hivyo ama la. Na zaidi sana ni kwamba hakuna adhabu
iliyotajwa kufanyiwa mtu asiyefanya hivyo. Bali
ikiwa ni ukumbusho wa kila mtu binafsi yake, agizo
hili linaeleza tu jinsi haja ya kumkumbuka, kumpenda na kutimiliza amri za
Mungu kwa kuzishika” (McElwain, T., et.al., “E” jarida
la Utepe
wa Bluu (Na. 273) [Blue Ribbons (No. 273)],
iliyoandikwa na CCG, 1998, ukurasa wa 1,
4).
Jinsi ya kuitendea kazi Sheria hii
Kwa kuhitimisha ni kwamba, “Sabato hii ya
siku ya saba ya juma inatakiwa itunzwe na kuadhimishwa (kama
isemavyo Kutoka 20:8-11; Kumbukumbu la Torati 5:12-15) ikiwa ni amri ya daima ya
Bwana Mungu wetu ambayo ni mojawapo ya Amri Kumi za Mungu. Amri hii haipaswi
kuitia unajisi na mtu yeyote milele. Sabato ni takatifu. Na kila anayeitia unajisi Sabato adhabu yake ni kifo na kukatiliwa mbaliau kutengwa na watu wake (Kutoka 31:14-15).
Ni agano la milele kati ya Mungu na wana wa Israeli na ni ishara ya milele kati yao na Mungu, ili wamjue
kuwa yeye ndiye muumbaji (Kutoka 31:15-16). Wakristo wote ni
Israeli wa kiroho na Wamataifa wote wanapaswa kuja kwenye taifa hili la
Israeli. Kwa hiyo, Sabato ni ishara kati ya Mungu na
wanadamu au watu wake wote na ni kwa wakati wote milele. Adhabu au hukumu
iliyoagizwa kufanyiwa mtu anayeitia unajisi Sabato ni kuuawa
iliwa ni pamoja na yule anayemkufuru Roho Mtakatifu na kuwa hana sehemu kwenye
ufufuo wa kwanza bali ule wa pili wa hukumu (soma Ufunuo 20:5). Sabato ni siku ya furaha na inapaswa iheshimiwe kama
ni Siku Takatifu ya Bwana. Sio siku ya kuyafanya mambo yako mwenyewe au ya
kutimilizia haja zako bali ni ya kuitisha makutaniko
matakatifu (Isaya 58:13-14). Hakuna kazi inayotakiwa ifanywe
wala mzigo unaoruhusiwa kubebwa siku hii ya Sabato (Yeremia 17:21-22).” Wala haturuhusiwi kununua (Nehemia 10:31)
wala kuuza (Nehemia 13:15) siku hii ya Sabato (soma jarida la Tangazo la Imani
ya Imani ya Kikristo (Na. A1) [Statement of Beliefs of
the Christian Faith (No. A1
)], ya CCG, toleo la 4., mwaka
1997, ukurasa wa 22).
“Amri ya Sabato haitengani na amri ya kwanza na amri nyinginezo. Taifa la Israeli
liliadhibiwa kwa ajili ya kushindwa kwao kuyatunza
maagizo na amri za Mungu” (Zekaria 14:16-19). Hata hivyo, Sabato zinakataliwa na wanadamu kwa ajili ya imani yao iliyoshamiri mioyoni mwao ya kuabudu
sanamu” (Cox, “C”, op. cit., ukurasa wa 18).
Miandamo ya
Mwezi
“Siku ya Mwandamo wa
Mwezi ni mojawapo ya Sikukuu zilizoamriwa na Bwana Mungu. Imeorodhesha kwenye kitabu
cha Hesabu 10:10.
Hesabu 10:10 inasema: Tena
katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu
zilizo amriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya
sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo
zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu, mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Aya hii inatuambia kwamba pia
baragumu zilikuwa zinapigwa siku zote za Kuandama kwa
Mwezi, kwenye Siku Takatifu na siku ya Sabato wakati kulivyokuwa kunatolewa sadaka
za kuteketezwa na za amani (Soma pia jarida la Baragumu ya Pembe za Kondoo na ya Fedha (Na. 47) [The
Shofar and the Silver Trumpets (No. 47)]. Dhabihu hii ilitimilizwa katika Kristo. Sikukuu na Sabato hizi zinabakia kama
zilivyo, hazikukoma au kubatilishwa.
Siku hii ya Mwandamo wa Mwezi iliadhimishwa sawa na Shabbatown au Sabato Takatifu. Dhabihu zilikuwa zinatolewa kuwa ni ukumbusho kama
tulivyojionea hapo juu” (sawa na kwenye Hesabu 28:11-15).
Jinsi hiyohiyo ya kuadhimisha
hutumika kwenye Miandamo ya Mwezi kama
inavyofanywa pia kwenye Sikukuu nyingine zote na Sabato.
1Mambo ya Nyakati 23:31
na kumtolea BWANA
sadaka zote za kuteketezwa, katika siku za Sabato, na mwezi mpya na sikukuu
zilizoagizwa, kwa hesabu, kadiri ya agizo lake, daima mbele za BWANA
Kwa hiyo tunaona kwamba Miandamo ya
Mwezi ndiyo inayopelekea au kuamua ni majira gani
yatakuwa Sabato na Sikukuu. Sawa kama zilivyo Sikukuu
na Sabato, umuhimu wa kutoa dhabihu siku ya Miandamo ya Mwezi vilitimilizwa kwa
kuja kwake Masihi, lakini maadhimisho ya Miandamo ya Mwezi yenyewe hayakukomeshwa
ama kuondolewa.
2Mambo ya Nyakati 31:3 Tena akaweka
sehemu ya mfalme ya mali
zake kwa sadaka ya kuteketezwa, yaani, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na
jioni, na sadaka za kuteketezwa za Sabato na mwezi mpya na sikukuu, kama ilivyoandikwa katika torati ya BWANA.
Tunaona pia kwamba maadhimisho na ibada hizi za Miandamo ya Mwezi zilirejeshwa tena na Ezra
(soma Ezra 3:5). Kwa hiyo, marejesho makuu yalihusisha maadhimisho na ibada hizi za Miandamo ya Mwezi.
Ezra 3:5 Na baadae sadaka ya kuteketezwa ya
daima, na za mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za BWANA, zilizoamriwa na kuwekwa
wakfu, na za kila mtu aliye mtolea BWANA sadaka kwa hiari yake.
Maadhimisho haya yasieleweke vibaya
au kutafsiriwa kuwa ni ibada za kuabudu mwezi, jambo
ambalo limekatazwa kabisa.
Kumbukumbu la Torati 4:19 Tena usije
ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la
mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana,
Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.
Kumbukumbu la Torati 17:3 Naye amekwenda kutumikia miungu mingine na
kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote,
nisivyoagiza mimi;
Tendo la kuziadhimisha Sabato na Miandamo ya Mwezi pamoja na Sikukuu zilizoamriwa kumefanya
Mpango wa Mungu na mwenendo mzima wa mzunguko wa dunia au uumbaji wake. Kalenda ya jua haina uwezo huo. Kalenda inayofuata miandamo
ya mwezi ni alama ya watu watakatifu. Alipokuwa
anaitafakari Kutoka 12:2, Mekilta alisema kwamba “mataifa” yanajulikana kwa jua, bali Israeli wanajulikana kwa mwezi.
“Mwandamo wa
Mwezi ndiyo mwanzo wa siku ya kwanza ya mwezi mpya (Hesabu 10:10; 28:11). Hakuna
mfumo wowote unaotegemea kwenye mzunguko wa mwezi
uliopo leo. Kalenda ya Hilleli imekoma na kutoweka
kabisa kwa ajili hii.
Siku ya Mwandamo wa
Mwezi ilijulikana kama siku kuafaka kwa kutoa maono na unabii, huenda kama inavyoonekana kwenye 2Wafalme 4:23 lakini hasa
kwenye Ezekieli 26:1; 29:17; 31:1; 32:1 (na kwenye Isaya 47:13; Hagai 1:1). Hii
inaipinga kabisa dhana waliyokuwanayo wanajimu na wachawi
wa Babeli na taratibu zao, kama tunavyoona
kwenye Isaya 47:13.
Sabato na
Miandamo ya Mwezi zote ziliadhimishwa kwa kufanya mapumziko kwa kuacha kufanya
kazi, kama tunavyoona kwenye Amosi 8:5. Ilikuwa
ni siku ya furaha. Vicheko
vivyokusudiwa kusikika Siku Takatifu, Mwezi Mpya na
Sabato viliondolewa kama tunavyoona kwenye Hosea 2:11.
Hosea 2:11 Tena
nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na
siku zake za mwandamo wa mwezi, na Sabato zake na makutaniko yake yote yaliyo
amriwa.
Hii ni kwa sababu ya kutokuwa waaminifu kwao na ibada ya sanamu.
Mungu huwaangamiza watu wake kwa sababu hawakuzishika
sheria zake. Hatimaye ni kwamba aliuharibu utajiri wa
taifa.
Hosea 2:12
inasema:
12 Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, Hii ndio ujira wangu
niliopewa na wapenzi wangu; nami nitaifanya kuwa misitu, na wanyama porini
wataila
“Tunaona kutoka kwenye aya fulani kadhaa kwamba Mwandamo wa Mwezi wa mwezi fulani
unaadhimishwa kwa namna yake maalumu (1Samweli 20:5; Ezekieli 45:18-20).
Ezekieli 45:18-20 Bwana MUNGU
asema hivi; Mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, utatwaa ng'ombe mchanga
mume mkamilifu; nawe utapatakasa mahali patakatifu. 19 Na
kuhani atatwaa baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi, na kuitia juu ya miimo ya
milango ya nyumba, na juu ya pembe nne za daraja ya madhabahu, na juu ya miimo
ya lango la ua wa ndani. 20 Nawe utafanya vivyo
hivyo katika mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi kwa ajili ya kila mtu
akosaye, na kwa ajili ya mtu aliye mjinga, ndivyo mtakavyoifanyia nyumba
upatanisho.
Tendo la kuisafisha maskani
linalotangulia kufanyika siku ya Mwandamo wa Mwezi wa
mwezi wa Kwanza (Nisan) mwanzoni mwa Mwaka Mtakatifu (soma jarida la Utakaso wa Hekalu la Mungu (Na. 241) [Sanctification of the Temple of God (No. 241)]. Utakaso huu wa uwa wa ndani ambao ulikuwa ni inawaonyesha watakatifu kwa
mwonekano wa gurudumu la ndani la maono ya nabii Ezekieli. Utakaso kwa ajili ya dhambi zilizofanywa bila kukusudia ama za
kupotoshwa ulifanywa kikamilifu tangu Siku ya Saba ya Mwezi wa Kwanza ambao pia huitwa wa Nisan. Makuhani walipaswa
kujiandaa na taifa pia.
Siku ya
kwanza ya Mwandamo wa Mwezi wa Saba (Tishri) ulikuwa
wa muhimu sana
pia (pia soma jarida la Baragumu
(Na. 136) [Trumpets (No. 136)].
Mambo ya Walawi 23:24
Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi wa saba, siku ya
kwanza ya mwezi, kutakuwa na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa kuzipiga
baragumu, ni kusanyiko takatifu.
Nehemia 8:2 Naye Ezra, kuhani,
akaileta torati mbele ya kusanyiko, la wanaume na wanawake, na wote walioweza
kusikia na kufahamu, siku ya kwanza na mwezi wa saba.
Siku ya Mwandamo wa Mwezi wa Saba
ambao ni mwanzo wa marejesho ya amri ya Usomaji wa Torati unaofanyika katika kila mwaka wa saba wa mzunguko wa
Yubile wa kila siku za Sikukuu ya
Vibanda (soma Kumbukumbu la Torati 31:10-12 na pia soma jarida la Jinsi Walivyosoma Torati Ezra na Nehemia
(Na. 250) [Reading the Law with Ezra and Nehemiah (No. 250)].
Nehemia 8:18 Tena siku baada ya siku, tangu
siku ya kwanza hata siku ya mwisho, akasoma katika kitabu cha torati ya Mungu. Wakafanya sikukuu muda wa siku saba; na siku ya nane
palikuwa na kusanyiko la makini, kama ilivyoagizwa.
Alama ashirio
hapa ni kwamba mwaka wa saba au wa Sabato unaonysha mzunguko wa milenia wa
miaka elfu, unaoanzia na kurudi kwa Masihi, ambaye atafanya utawala wa Sheria
atakazoziamuru kutoka Yerusalemu. Na Sheria hizi zitaenea ulimwenguni kote na zikiyafanya mataifa yajinyenyejeshe kwake. Usomaji wa Torati kwenye Sikukuu ya Baragumu kulikofanywa na Nehemia
ilikuwa ni kitendo kinachoashiria marejeo ya Masihi yatakayoambatana na mlio wa
Baragumu (sawa na ilivyoandikwa kenye jarida la Mlolongo wa Ratiba ya Nyakati (Na 272) [Outline Timetable of the Age (No. 272)].
Kutoka kwenye
kipindi cha zama jangwa cha utawanyiko, hatimaye Mungu
atashughulika na Israeli na kuirejesha upya. Ikumbukwe kwamba wateule wake
Kristo ni sehemu ya hawa Israeli na watachukuliwa kama taifa (Hosea 2:14-23).
Miandamo ya
Mwezi iliadhimishwa na Kanisa la Wakristo wa kwanza
waliokuwa na Mitume na hata walipokuwa kwenye zama ya utawanyiko na jinsi
walivyokuwa wanaadhimisha sio jambo tunalopaswa kulitolea hukumu. Walikuwa wanaendela
bado kuadhimisha ibada hizi huko Ulaya kwenye karne na kumi na saba (soma
jarida la Mgawanyo
wa Jumla wa Makanisa Yanayoshika Sabato (Na. 122) [General Distribution of the Sabbath-keeping Churches (No.
122)];
na kitabu cha Wasabato wa Transylvania (The Sabbatarians In Transylvania) kilichoandikwa na
Samuel Kohn (1894), ambacho nakala yake ya tafsiri ya Kiingereza imechapishwa
na idara ya machapisho ya CCG,
mwaka 1998).
Wakolosai 2:16-17
Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au
vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa
mwezi, au sabato; 17
mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni
wa Kristo.
Miandamo ya Mwezi ni muhimu kwa ustawi wa wanadamu. Kalenda hii imepuuzwa na mahala pake kuchukuliwa na ile inayoitwa ni kalenda ya wanadamu au ya walimwengu
iliyopewa siku za kipagani zinazoendana na kuwatukuza wanadamu. Nchini
Marekani, kalenda hii ya wanadamu imepambwa kwa
kuwekewa siku muhimu za mapumziko kwenye siku za kipagani. Jambo
hili halipaswi kupuuzwa au kufumbiwa macho.
Siku hizi za
Sabato na Miandamo ya Mwezi ziliadhimishwa kwa uzito
sawa kwa masuala ya kibiashara na shughuli zote. Shughuli za kibiashara au za
kununua na kuuza zilikatazwa siku hizo nz hata leo
zisifanyike katika siku zote, yaani za Mwandamo wa Mwezi na za Sabato.
Amosi 8:4-6 inasema: Lisikieni hili, ninyi mnaopenda kuwameza wahitaji, na kuwakomesha maskini wa nchi, 5 mkisema,
Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na sabato nayo, tupate kuandika
ngano? Mkiipunguza efa na kuiongeza shekeli, mkidanganya watu kwa mizani ya
udanganyifu; 6 tupate kuwanunua maskini kwa fedha, na
wahitaji kwa jozi ya viatu; na kuziuza takataka za ngano.
Katazo hili ni tatizo kubwa kwa Waisraeli wa leo. Hatahivyo na kwa kweli, hakuna uwezekano wowote wala mahala
panapoonyesha kuwa Sabato na Miandamo ya Mwezi zinaweza kuonyesha tofauti ya
maadhimisho yake, zaid kama ilivyo kwenye Sikukuu ambazo zimeorodheshwa mbali
na Amri Kumi, na ambazo zinachukuliwa kama Shabbatown
– ambazo ni lazima ziadhimishwe zote.
Nabii Amosi anaendela
kuelezea na kuwaonya Israeli kwa kukosa kwao kuzitunza
Sabato na Miandamo ya Mwezi kikamilifu.
Amosi 8:8-12 inasema:
Kwa ajili ya hayo, je! Haitatetemeka nchi, na
kuomboleza kila mtu akaaye ndani yake? Naam, itainuka yote pia kama huo Mto;
nayo itataabika na kupwa tena kama Mto wa Misri. 9 Tena
itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri,
nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana. 10 Nami
nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami
nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upaa katika kila kichwa; nami
nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho
wake kama siku ya uchungu. 11 Angalia, siku
zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa
chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana. 12 Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka
upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na
huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione.
Adhabu ya
moja kwa moja kwa wanaoyaasi maneno ya Mungu ni kile tulichokipokea.
Njaa ya kukosa kulisikia neno la Mungu hutokea kama adhabu kwa wanaomuasi Mungu. Tendo la
kuzitia unajisi Sabato na Miandamo ya Mwezi kwa
kufanya matembezi na kufanya biashara kwa makusudi ya kuzivunja Amri ni sababu
za kwanza. Nyumba ya Yakobo walikumbwa na machukizo
haya ingawaje walihifadhiwa salama na hawakuangamizwa, kama
nafaka zinavyopeperushwa kwenye chombo cha kupepetea (Amosi 9:8-15).
(Cox, W.E., “F” jarida la Miandamo ya
Mwezi (Na.125) [The New Moons (No. 125)], CCG,
1995-2007, kurasa za 5-10).
Maana ya Miandamo ya Mwezi Kwenye
Mpango za Mungu
“Mwanzo 1:14
inaonyesha kuwa Mungu aliweka mwanga katika mbingu ili
kufanya tofauti kati ya mchana na usiku na kama
ishara ya majira. Mwezi Mpya hutupa utaratibu na muda
wa Sikukuu na hasahasa hutanguliwa na Sabato, ambayo husimamia tando la
kukamilisha siku saba, wakati Miezi huanzia kutoka siku ya nne. Nuru hutenga
nuru na giza
(Mwa.1:18). Mwezi huashiria nuru ya nuru ya ulimwengu katika giza ambalo
huitawala. Jua lilitumia kufananisha na Kristo (Malaki
4:2).
Malaki 4:2-5 Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina
langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka
nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini.
3 Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu;
katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi. 4
Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili
ya Israeli wote, naam amri na hukumu.. 5 Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku
ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya.
Mwezi unamaana pia kwa
kuwa uko kwenye mwonekano. Mwandamo wa Mwezi ni alama
ashirio ya kuanza kwa shughuli ngingine kwenye kila mzunguko. Kuna miezi kumi na miwili katika kila mwaka (mbali na ule mwaka mkubwa) (1Wafalme
4:7; 1Nyakati 27:1-15). Miezi hii inachukuliwa kwa
ujumla kuwa na urefu wa siku 30 kila mmoja (Mwanzo 7:11; 8:3-4; Hesabu 20:29; Kumbukumbu
la Torati 21:13; 34:8; Esta 4:11; Danilei 6:7-13). Pia tazama
jarida la Kalenda
ya Mungu (Na. 156) [God’s
Calendar (No. 156)].
Mwandamo wa
Mwezi ni “mwanzo wa mwezi mwandamo, ujulikanao kama kipindi kilicho kati kati
ya kipindi giza
ambacho mwezi hauonekani hadi kingine kinachofuatia, urefu ambao kwa kweli
hauhesabiwi kwenye shule zinazoshughulika na elimu ya mambo anga au nyota.” (Judaeus Philo, kwenye kitabu chake cha Kanuni Mahususi, II, XXVI, 140 (The Special Laws, II, XXVI, 140, F.H.) cha Colson, kwenye
Machapisho ya Chuo Kikuu cha Harvard, huko Cambridge
mwaka 1737 (Harvard University Press, Cambridge
MA, 1937).
Kwa kuongezea nukuu hii kunamaandiko
mengine yanayohusu Miandamo ya Mwezi na jinsi ya kuanza
kwake ambayo inaitaja siku halisi hasa ma Kuandama kwa Mwezi.
Tunaposhughulikia suala la maadhimisho
ya Sikukuu kwa mujibu wa amri za Mungu, tunaona pia
kwamba Philo ana la kusema akilinganisha na Shria
Muhimu zinazoihusu amri ya nne na jinsi inavyoshabihiana kwa jisi ifuatayo:
{**Lichwa cha somo cha kitabu cha Yonge,
kinachoandika kwa alama, Kingamo la Amri Muhimu aina
yake, ambazo Zilielezewa kwa Maandako chapisho Matatu ya Mdahalo, Ilioitwa ni
ya Tatu, ya Nne na ya Tano Kuhusu Viapo na Makumbushio yake Yanayoyahusu;
Kuhusu Sabato Takatifu, Kuhusu Heshima Inayotakiwa Wapewe Wazazi).
....
Tafsiri ya Yonge
inahusisha ufanyiaji kazi kwenye hatua hii. Kwa Nambari Saba. Mgawanyo wake unaofuatia unaanzia na kuishia na numerali za kirumi I (= X kwenye Loeb). Loeb nyingine zinazofuatia zimewekewa nambari.
X. (39) Amri inayofuatia ni ile inayohusu siku saba takatifu, ambazo zimewekewa
nambari kinyumbulisho ya kuwa ni sikukuu za muhimu sana. Kwa mfano, kuna kuachiliwa kwa wanaume ambao kwa asili walikuwa huru, lakini ambao walidhania
baadhi ya nyakati muhimu zisizoonekana, ambazo wamekuwa ni watumwa na ambao
uwekwaji huru huu unakuwa kila kipindi cha miaka saba. Na tena kuna madeni ya
kibinadamu unaowahusu wadeni, kama wanavyowasamehe wadeni
ndugu zao, ambao wanawasamehe madeni yao
kila mwaka wa saba. Pia kuna mapumziko yanayotolewa kwa
ardhi yenye rutuba, bila kujali kama ipo
kwenye maeneo ya milimani au kwenye utambarare au mabondeni, mapumziko ambayo
yanakuwa kila baada ya mwaka wa saba. Zaidi ya yote, kuna amri nyinginezo
ambazo zilianzishwa kwa kuuadhimisha mwaka wa hamsini.
Na kwa mambo yote haya huleta mnyumbulisho (pasipo
kuangalia maana yoyote ya kimafumbo) inatosha kuwaongoza wale wote walioachwa
kwenye ujuzi kamilifu, na kuwafanya hqata wale walio na mashaka au wagumu
kwenye mitazamo yao
wakubaliane zaidi na kupendezwa. (40) Sasa tumeishasema tayari kwa upana wa
kiasi fulani kuhusu umuhimu wa namba saba, tukielezea ni nini asili yake kuelekea
kwenye namba kumi, na pia jinsi uhusiano wake ulivyo kwa muongo mmoja wenyewe, na
pia kwa namba nne, ambayo ni msingi wa muongo mmoja. Na sasa, inapokuwa imehusishwa
kwenye mwito wa kawaida kutoka kwenye kiini chake, ni mchakato wa wito wa
kawaida kuona kuwa namba ya kawaida ishirini na nane; ambayo inazidishwa kwa hali
sawa na mlingano wa kawaida ulio sawa na maeneo yote, ambayo inafanya kikomo
chake kuwa ni kote kuwili yaani mzingo na mlingano pembe. Pia nilionyesha jinsi
zilivyo idadi ya nambari za mambo ya uzuri ambayzo zinaweza kuzidi kutoka
kwenye mabo yanayoizidia, na ambayo hatujawa na muda
wa kuyaangalia kwa sasa. Bali tunapaswa kuyahoji na
kuyachunguza kila kimoja wapo miongoni mwa mambo haya muhimu yaliyoko mbele
yetu kama yako pamoja, ikianzia na kile cha
kwanza. Jambo la kwanza linalotakiwa kutiliwa maanani ni
lile la maadhimisho ya Sikukuu. [Tafsiri ya Yonge inahusisha
ufanyiaji kazi kwenye hatua hii. Kuonyesha Kwamba Sikukuu Zipo Kumi Idadi yake. “Mgawanyo”
huu unaanzia na numerali ya kirumi I (= XI kwenye
Loeb); ikionyesha kila moja ya sikukuu hizi kumi peke yake na kuendelea kupitia
kwenye nambari za Loeb 214. aya nyingine zinazofuatia numerali
za Loeb)
XI. (41) Sasa kuna idadi ya sikukuu
kumi, kama sheria
zinavyoziandika na kuziorodhesha.
Ya kwanza ni
ile ambayo huenda mtu anaweza kushangazwa kuisikia ikiitwa sikukuu. Sikukuu hii
ni ya kila siku.
Sikukuu nyingine ya pili ni ile ya siku ya saba, ambayo Waebrania kwa lugha yao huuita Sabato.
Ya tatu ni
ile inayokuwa kipindi cha baada ya kipindi cha kutoonekana mwezi au cha
muunganisho wa mwezi ambayo inatokea siku ya kuandama kwa mwezi wa kila mwezi.
Ya nne ni ile
ijulikanayo kama Pasaka ambayo pia inaitwa
Pasaka.
Ya tano ni
ile ya malimbuko ya mazao ambayo kwayo hutikiswa mganda mtakatifu (Kumbuka kuwa
Mganda wa Kutikiswa ni moja ya Sikukuu kumi zilizokuwa na mashiko makubwa zama
hizi za Hekalu).
Ya sita ni ile
ya Mikate Isiyotiwa Chachu, inayoadhimishwa baada maadhimisho ya sikukuu
yamekwisha tayari.
Ya saba ni
ile inayoadhimishwa siku ya saba ya majuma saba.
Ya nane ni
sikukuu inayoaadhimishwa sambamba na mwandamo wa mwezi, ambayo ni sikukuu ya
baragumu.
Ya tisa ni ile
inayoadhimishwa kwa kufunga saumu.
Ya kumi ni sikukuu
ya vibanda, ambayo ni ya mwisho miongoni mwa sikukuu zote za mwaka,
inashoishilia kwa kukamilisha idadi ya kumi. Tunatakiwa sasa kuanza na sikukuu ya kwanza.
[Kumbuka kuwa, hapa Philo anajumuisha
na Siku ya Mkutano wa Makini na Sikukuu ya Vibanda na
kuzifanya ziwe kumi badala ya kumi na moja.]
Tunagundua hapa kwamba katika
kutambulishwa kuhusu Sikukuu hii ya tatu inayojulikana kama ya Mwandamo wa Mwezi,
Philo anatumia neno ambalo halijawahi kuonekana anaposema baada ya kipindi cha kutoonekana mwezi au cha muunganiko cha mpito na
wengine wameitaja kama kipindi kinachofuata
kwa maana ya “kwa mujibu wa” au “kama alivyokusudiwa na” kipindi cha mpito.
Hata hivyo, anastahili kwa jinsi hii kwa kusema inayotokea siku ya Mwandamo wa Mwezi wa
kila mwezi. Kwa hiyo andiko hili liko wazi sana kwamba Mwandamo
wa Mwezi ni suku ambayo kipindi hiki cha mpito hutokea. Kwa mafafanuzi Philo kwa hiyo anaendelea kuelezea kwamba mwezi unahesabiwa tangu
kipindi kimoja cha kutoonekana mwezi hadi kingine kama kinavyoamriwa na
wanazuoni wa shule za utafiti wa mambo ya anga na nyota, kama
ilivyoandikwa hapo juu.
Tafsiri ya Yonge inapungukiwa na sehemu
ya 140 na maandiko 142-144 (ambayo yametolewa hapo chini) na anaelezea kipindi na
teolojia iliyo nyuma ya Mwandamo wa Mwezi na sababu inayopelekea kuendelea kwa
mujibu wa kipindi hiki cha kutoonekana mwezi, na siku ya Kundama kwa Mwezi kuwa
ni ile siku ya giza.
SIKUKUU YA TATU
XXVI. (140) Kufuattana na kanuni tuliyoichukua, tunaendelea kuiongelea sikukuu ya
tatu, ambayo ni ya mwandamo wa mwezi. Kwanza kabisa na kabla ya mambo yote, kwa
kuwa ni mwanzo wa mwezi, na ni mwanzo wa idadi au majira, ya mwelekeo wa
kuufikia mwezi wa Pili, kwa kuwa katika kipindi hiki kunakuwa hakuna mwangaza
wowote angani kote. (141) Tatu, kwa kuwa kwenye kipindi hiki uweza wa mwili wote
wenye nguvu na wa muhimu hupulinguzia sehemu yake ya msaada ulio muhimu kwa mwili
uliodhaifu na usio wa muhimu sana, kwa kuwa kipindi cha kuandama mwezi ndicho
jua linaanza kuuangazia mwezi kwa nuru ambayo inaangaza kwa mwonekano wa nje,
na kisha kuufanya uonekane mzuri kwa mng’ao wake kwa wanaoutazama. Na hii, ni
kama inavyoonekana kuwa ni fundisho la dhahiri la wema na unyenyekevu kwa
mwanadamu, kuwafundisha kuwa hawapaswi kufanya jitihada ya kuwashirikisha mema
yao mazuri kwa wengine, bali ni kuwaiga viumbe wa mbinguni, jambo linaloweza
kusababisha wivu na kuitesa Roho. {17}{sehemu ya
142-144 zilirukwa kwenye tafsiri ya Yonge kwa kuwa chapisho ambalo ndiyo Yonge
aliitegemea alipokuwa anatafsiriwa, Mangey, alikosa matirio yake. Mistari hii
imetafsiriwa upya kwa toleo hili.} (142) Sababu ya nne
ni kwamba vitu vyote vilivyo mawinguni, mwezi unazunguka kwa kupitia kwenye
ukanda wa sayari unaopitia sayari zote kuu, yaani ukanda wa zodiaki kwa kipindi
cha chini ya jinsi ilivyopangiwa; na unakamilisha mzunguko wake kwa mzingo wa
kile mwezi. Kwa ajili hii sheria imeheishimu mzingo, kipindi ambacho mwezi
umekamilisha kutoka kwenye chanzo chake ambapo ndipo ilianzia mzunguko wake,
kwa kuiita siku ile kuwa ni sikukuu ili kwamba iweze kutufundisha tena somo
jema ili kwenye mambo yanayohusu maisha tuweze kufikia kikomo cha uwiano mwanzo
wake. Hii itatokea iwapo kama tutashika hatamu kwenye
msukumo wetu wa kwanza wenye nguvu ya maana na haiwaruhusu kukataa hatamu na
kukimbia tukiwa huru kama wanyama pasipo mtu
yeyote wa kuwaongoza wanyama.
http://www.earlyjewishwritings.com/text/philo/book28.html
Kwa
hiyo sio makosa. Mwandamo wa Mwezi huwa ni
kipindi kile cha mpito cha giza la kutoonekana
mwezi kama inavyoaminika na wanazuoni wa shule
za elimu ya mambo anga na nyota huko Yerusalemu. Tendo la kuahirisha Mwandamo wa Mwezi lililofanywa na imani ya Kiyahudi kunamaanisha
kuahirisha sikukuu zote na kuzifanya kuwa hazina maana. Huko ni
sawa na kutia Mungu kidole puani kwa kutumia Sheria na Amri zake. Kwa hiyo,
Mwezi unapokuwa Unaandama ndipo mfumo na utaratibu wa
sikukuu unapoanzia.
Mpango mzima wa
Wokovu unaonekana kwenye kila Mwandamo Mpya wa Mwezi kupitia utaratibu wa hesabu
ya Sikukuu na mwonekano wake kwenye mzunguko wa mavuno halisi ya uvunaji mazao”
(Cox, W.E., “G” jarida lake la Mwandamo wa Miezi Katika Israeli (Na.132) [The New Moons of Israel (No. 132)], CCG,
1995-2008, ukusara wa 3,5,6,7).
“Mkutano mzima – viongozi na watu – wanaamriwa
kufanya ibada kwa siku zote mbili, yaani kwenye Sabato na Miandamo ya Mwezi (soma
pia Ezekieli 46:6,9-10).
Ezekieli 46:1-3 inasema: Bwana MUNGU asema hivi; Lango la ua wa ndani,
lielekealo upande wa mashariki litafungwa siku sita za kazi; lakini siku ya
sabato litafunguliwa, na siku ya mwezi mpya litafunguliwa. 2 Naye
mkuu ataingia kwa njia ya ukumbi wa lango lile, upande wa nje, naye atasimama
karibu na mwimo wa lango, nao makuhani wataitengeneza sadaka yake ya
kuteketezwa, na sadaka zake za amani, naye ataabudu penye kizingiti cha lango;
kisha atatoka; lakini lango lile halitafungwa hata wakati wa jioni. 3 Watu wa nchi nao wataabudu mbele ya mlango wa lile lango
mbele za Bwana, siku za sabato, na siku za mwezi mpya.
Utoaji dhabihu siku ya Mwandamo wa Mwezi
kwa kweli jambo kuu na muhimu zaidi kuliko lile la siku ya Sabato (Ezekieli
46:4,6). Hakuna tofauti iliyofanywa kati ya Mwandamo wa Mwezi na Sabato ya juma, bali siku zote mbili ni takatifu
na haziruhusiwi kufanya biashara siku hizo.
Amosi 8:5 mkisema, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na sabato nayo, tupate kuandika ngano? Mkiipunguza efa na
kuiongeza shekeli, mkidanganya watu kwa mizani ya udanganyifu;
(Cox, W.E.,
“H” jarida la Mavuno ya Mungu, Dhabihu ya Mwandamo wa Mwezi, na Wale
144,000 (Na. 120) [The Harvests of God, the New Moon Sacrifices, and the 144,000
(No. 120)], CCG, 1995-2007, ukurasa 13).
“Mwandamo wa
Mwezi ni tukio muhimu katika mfumo wa mambo anga na ambalo linatabirika
kamilifu pasipo makosa. Linapaswa lichukuliwe mwanzo wake kutoka kipindi
linapotokea huko mjini Yerusalemu ili kufanya umoja wa
ibada za kidini ulimwenguni kote, ili kuweko na ongezeko la kimawasiliano. Hii
inafanyika kwa kufuata jinsi yanavyosema Maandiko Matakatifu ambayo yanauita
mji wa Yerusalemu kuwa ni Kiti cha enzi cha Mungu (Yeremia 3:17), ni kitovu cha
sheria na ni kituo ambacho kwacho zitatoka kwenye kipindi cha utawala wa Masihi
(Isaya 2:3), na kwa maji ya Roho Mtakatifu (Zekaria 8:22; 14:8-21). Mungu
ameliweka jina lake pale milele (2Nyakati 33:4)” (Cox, W.E.,”I”
jarida la Kalenda
ya Mungu (Na. 156) [God’s Calendar (No. 156)], CCG,
1996-2008, ukurasa 13)
“Siku Takatifu
za kila mwaka zinapatikana katika Walawi 23:1-44, Hesabu 28:16-29, 35 na katika
Kumbukumbu la torati 16:1-16. Siku hizi Takatifu za kila mwaka ni taswira ya
Mpango wa Wokovu wa Bwana . ni
za muhimu na lazima na zinaweka umuhimu wake fulani wa kiishara kati ya Mungu
na watu wake. Siku hizi Takatifu zinaadhimishwa na
kuchukuliwa sawa na Sabato.
Siku hizi
Takatifu ni:
Pasaka na Idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu (Law. 23:7; Hes.28:18, 25);
Pentekoste
(Law.23:21; Hes.28:26);
Baragumu
(Law.23:23; Hes.29:1);
Upatanisho
(Law.23:26; Hes.29:7)
Vibanda
(Law.23:35; Hes.29:12);
Siku ya
Mkutano wa Makini (Law.23:36;
Hes.29:35).”
Jarida la (Msingi wa Imani wa Imani ya Kikristo (Na. A1) [Statement of Beliefs of the Christian Faith (No. A1)], CCG, toleo la 4
ed., 1997, ukurasa wa 24.)
Sikukuu tatu zilizoamriwa
kuadhimishwa kila mwaka ni Pasaka na Mikate isiyotiwa
Chachu, Pentekoste au Idi ya Majuma, na Sikukuu ya Vibanda
Kumbukumbu la Torati 16:16 "Mara tatu kwa mwaka na watokee wanawaume wako wote mbele za Bwana,
Mungu wako, mahali atakapochagua; katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na
katika sikukuu ya majuma, na katika sikukuu ya vibanda; wala wasitokee mbele za
Bwana mikono mitupu.”
Kutoka 23:14 " Mara tatu kila mwaka utaniwekea sikukuu.
Pasaka
Sikukuu ya Pasaka ni
ishara ya wanadamu wakikombolewa kutoka kwenye utumwa wa dhambi na adhimishola
Idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu inawakilisha ishara ya kuondoa dhambi na kutoshiriki
tena miongoni mwetu na ni ishara waliyoifanywa Israeli na hizi ni Siku mbili
Takatifu zilizo tofauti. Pasaka huishia siku ya kumi na
nne jioni, na si ku ya mwisho ya Mikaye Isiyo na Chachu ni siku ya ishirini na
moja ya mwezi wa Kwanza (Abibu).
Kumbukumbu la
Torati 16:1-2 Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka Bwana, Mungu wako, kwa kuwa
ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku Bwana; Mungu wako. 2 Nawe umchinjie pasaka Bwana, Mungu wako, katika kundi la
kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua Bwana apakalishe jina lake.
Masaa 36 ya kwanza ya maadhimisho ya
Pasaka pamoja na Ushirika wa Meza ya Bwana na mlo wa
siku ya 15 havitakiwi kufanyika majumbani au ndani ya malango yetu. Matukio
haya hufanywa kwa kutanguliwa na siku ya maandalizi ambayo
ni siku ya 14 ya mwezi huo huo wa Nisan.
Kumbukumbu la Torati 16:5-7 Usimchinje
pasaka ndani ya malango yako yote akupayo
Bwana, Mungu wako; 6 ila
mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, ndipo
mtakapomchinja pasaka jioni, katika machweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka Misri. 7 Nawe
umwoke na kumla mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; kisha asubuhi yake
ugeuke uende hemani mwako.
“Mahala panapolazimu kushuriki ili kuitii na kudhimisha amri hizi na utaratibu ambao Kristo
mwenyewe alionyesha mfano kwa kuanzisha na kushiriki Meza ya Bwana na Mlo wa
Pasaka. Kama hatutaishiriki ibada na maadhimisho haya, basi tunakuwa hatuna ushirika na Yesu Kristo
(Yohana 13:8).
Yohana 6:53-56 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa
milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa
maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani
yangu, nami hukaa ndani yake.
Adhimisho la kwanza la Ushirika wa Meza ya Bwana ni kufanyika kwa utaratibu wa kuoshana
miguu, ambalo linafuatiwa na tendo la kushiriki kuumega mkate na kunywa divai.
“Ishara hiyohiyo iliyoifanywa kwa dhaihu ya aliyojitoa
Kristo imeonekana kwa mifano hii miwili ya kula mkate na kunywa divai” (Cox,
W.E., “J” jarida la Ushirika wa Meza ya Bwana (Na. 103) [The Lord’s Supper (No. 103)], CCG,
1995-2008, ukurasa wa 4-5).
Mkate wenye chachu hautakiwi kabisa
kutumika kwenye ibada ya maadhimisho haya ya Meza ya Bwana (sawa na ilivyoandikwa kwenye Kutoka 23:18).
Kutoka 34:25 " Usisongeze damu ya sadaka yangu pamoja na mkate uliotiwa
chachu; wala hiyo sadaka ya sikukuu ya pasaka haitasazwa hata asubuhi.”.
Pia sona
jarida la Maana
ya Kuoshana Miguu (Na. 99) na Maana ya Mkate na Divai (Na. 100) [Significance of the Footwashing (No. 99) and Significance of the Bread and Wine (No. 100)].
Maelekezo ya jinsi ya Kuadhimisha
Pasaka
Maelekezo
yaleyale yahusuyo Pasaka yanapatikana kwenye kitabu cha Kutoka 12.
Kutoka 12:1-51 inasema: Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, 2
Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi
kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. 3 Semeni na
mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa
mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba
moja; 4 na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani
yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya
hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu
yenu kwa yule mwana-kondoo. 5 Mwana-kondoo
wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika
mbuzi. 6 Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko
lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. 7 Nao watatwaa
baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu,
katika zile nyumba watakazomla. 8 Watakula nyama
yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena
pamoja na mboga zenye uchungu. 9 Msiile mbichi,
wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu
yake, na nyama zake za ndani. 10 Wala msisaze
kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi
mtakichoma kwa moto. 11 Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa
viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni
pasaka ya Bwana. 12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami
nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa
mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. 13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami
nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu,
nitakapoipiga nchi ya Misri. 14 Na siku hii
itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana; mtaifanya iwe
sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele 15 Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza
mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote
atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba,
nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli. 16 Siku ya kwanza
kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko
takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo
kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu. 17 Nanyi mtaitunza
ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi
nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo
katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele. 18 Mwezi wa kwanza,
siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata
siku ya mwezi ishirini na moja jioni. 19 Muda wa siku
saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote
atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa
Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika
nchi. 20 Msile kitu chochote kilichochachwa; mtakula mikate
isiyochachwa katika makao yenu yote. 21 Hapo ndipo Musa
akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama
jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka. 22 Nanyi twaeni tawi
la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha
juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye
yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. 23 Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo
damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya
mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. 24 Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele. 25 Itakuwa hapo mtakapoifikilia hiyo nchi, Bwana atakayowapa, kama
alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu. 26 Kisha itakuwa,
hapo watoto wenu watakapowauliza, N'nini maana yake utumishi huu kwenu? 27 Ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya Bwana, kwa kuwa alipita juu ya
nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa
nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia. 28 Basi wana wa
Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama Bwana alivyowaamuru Musa
na Haruni, ndivyo walivyofanya. 29 Hata ikawa,
usiku wa manane Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri,
tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata
mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa
kwanza wote wa wanyama. 30 Farao akaondoka
usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu
katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu. 31 Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu
wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, kamtumikieni Bwana kama mlivyosema. 32 Twaeni kondoo zenu na ng'ombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu,
mkanibariki mimi pia. 33 Wamisri nao wakawahimiza watu,
kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote. 34 Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo
vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani. 35 Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri
vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi. 36 Bwana akawajalia
kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri
nyara. 37 Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi,
walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu,
bila kuhesabu watoto. 38 Na kundi kubwa la watu
waliochangamana mno wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng'ombe, wanyama wengi
sana. 39 Nao wakaoka mikate isiyochachwa ya ule unga waliouchukua
walipotoka Misri, maana, haukutiwa chachu, kwa sababu walitolewa watoke Misri,
wasiweze kukawia, nao walikuwa hawajajifanyia tayari chakula. 40 Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana, muda waliokaa ndani ya Misri,
ulikuwa ni miaka mia nne na thelathini. 41 Ilikuwa mwisho
wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi
yote ya Bwana yalitoka nchi ya Misri. 42 Ni usiku wa
kuangaliwa sana mbele za Bwana kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu
ndio usiku wa Bwana, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote
katika vizazi vyao. 43 Bwana akawaambia Musa na Haruni, Amri ya pasaka ni hii;
mtu mgeni asimle; 44 lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa fedha,
ukiisha kumtahiri, ndipo hapo atamla pasaka. 45 Akaaye kwenu
hali ya ugeni, na mtumishi aliyeajiriwa, wasimle pasaka. 46 Na aliwe ndani ya nyumba moja; usiichukue nje ya nyumba nyama yake yo
yote; wala msivunje mfupa wake uwao wote. 47 Na wafanye jambo
hili mkutano wa Israeli wote. 48 Na mgeni
atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia Bwana pasaka, waume wake wote na
watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka; naye atakuwa mfano mmoja na
mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu ye yote asiyetahiriwa asimle. 49 Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa mgeni akaaye kati
yenu ugenini. 50 Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli wote; kama Bwana
alivyowaagiza Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya. 51 Ilikuwa siku ile
ile moja, Bwana akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao.
The First Passover Instituted
Sikukuu hii
inatakiwa iadhimishwe kwa kutokula mikate isiyotiwa chachu kipindi chote hiki (Kutoka
12:8, 15-20; 12:3,6; 23:15; Mambo ya Walawi 23:6; Hesabu 9:11; 28:17; Kumbukumbu
la Torati 16:3, 4; Marko 14:12; Luka 22:7; Matendo 12:3; 1Wakorintho 5:8). Adhabu
kwa mtu anayedharau na kuitia unajisi Sikukuu hii ni
kukatiliwa mbali na watu wake au kutengwa kutoka kwenye mkutano wa wateule (Hesabu
9:13), isipokuwa kama kuna unajisi au safari
iliyoainishwa hapo juu. Kuna amri moja tu kwa wote,
yaani kwa mgeni na kwa mpita njia (Hesabu 9:14).
Kumbukumbu la
Torati 16:3-4 inasema: Usimle
pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula
naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi
ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoka nchi ya Misri, siku
zote za maisha yako. 4 Wala isionekane kwako chachu
muda wa siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo
siku ya kwanza jioni, kisilale cho chote usiku kucha hata asubuhi.
Wale ambao
hawajajiandaa kushiriki kuila Pasaka au wale wanaosafiri wanatakwa kuila Pasaka
kwenye mwezi unaofuatia (Hesabu 9:6-12; 2Nyakati 30:2-4).
Hesabu 9:1-23 inasema: Kisha Bwana akanena na Musa
katika bara ya Sinai, mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya kutoka kwao
katika nchi ya Misri, akamwambia, 2 Tena, wana wa Israeli
na washike sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa. 3 Siku
ya kumi na nne ya mwezi huu, wakati wa jioni, mtaishika kwa wakati wake
ulioagizwa; kwa amri zake zote, na kama hukumu zake zote zilivyo, ndivyo
mtakavyoishika. 4 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli
kwamba waishike sikukuu hiyo ya Pasaka; 5 Nao
wakaishika Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati
wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote Bwana aliyomwagiza
Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli. 6 Basi
walikuwako watu waume kadha wa kadha waliokuwa na unajisi kwa ajili ya maiti wa
mtu, hata wasiweze kuishika Pasaka siku hiyo; nao wakaenda mbele ya Musa na
Haruni, siku hiyo hao watu wakamwambia, 7 Sisi
tu hali ya unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu; nasi tumezuiwa kwa nini hata
tusipate kumtolea Bwana matoleo kwa wakati wake ulioagizwa, kati ya wana wa
Israeli? 8 Musa akawaambia, Ngojeni hapo; hata nipate
sikiza Bwana atakaloagiza juu yenu. 9 Bwana akanena na
Musa, akamwambia, 10 Nena na wana wa
Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, ye yote atakayekuwa na
unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote,
ataishika Pasaka kwa Bwana; 11 mwezi wa pili, siku
ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate
isiyotiwa chachu na mboga za uchungu; 12 wasisaze
kitu chake cho chote hata asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria
yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika. 13 Lakini
mtu aliye safi, wala hakuwa katika safari, naye amekosa kuishika Pasaka, mtu
huyo atakatiliwa mbali na watu wake; kwa sababu hakumtolea Bwana matoleo kwa
wakati wake ulioamriwa, mtu huyo atachukua dhambi yake. 14 Na
kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa Bwana;
kama hiyo sheria ya Pasaka ilivyo, na kama amri yake ilivyo, ndivyo
atakavyofanya; mtakuwa na sheria moja, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo
aliyezaliwa katika nchi. 15 Na siku hiyo maskani
iliposimamishwa, lile wingu likaifunika maskani, yaani, hema ya kukutania;
wakati wa jioni likawa juu ya maskani, mfano wa moto, hata asubuhi. 16 Ndivyo ilivyokuwa sikuzote; lile wingu liliifunika kwa
mfano wa moto usiku. 17 Na kila
lilipoinuliwa lile wingu juu ya ile Hema ndipo wana wa Israeli waliposafiri; na
mahali lilipokaa lile wingu, ndipo wana wa Israeli walipopiga kambi yao. 18 Kwa amri ya Bwana Wana wa Israeli walisafiri, na kwa
amri ya Bwana walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa
katika kambi yao. 19 Na lile wingu
lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, ndipo wana wa Israeli walipolinda
malinzi ya Bwana, wala hawakusafiri. 20 Na pengine lile
wingu lilikaa juu ya maskani siku chache; ndipo kwa amri ya Bwana walikaa
katika kambi yao, tena kwa amri ya Bwana walisafiri. 21 Na
pengine lile wingu lilikaa tangu jioni hata asubuhi; na lile wingu
lilipoinuliwa asubuhi walisafiri, au kama likikaa usiku na mchana pia,
lilipoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri. 22 Ikiwa
lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka,
wana wa Israeli walikaa katika kambi yao, wasisafiri; 23 bali
lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya Bwana walipiga kambi yao, na kwa amri ya
Bwana walisafiri; wakayalinda malinzi ya Bwana, kwa mkono wa Musa.
Tumeamriwa kuhakikisha
tunaziadhimisha sikukuu hizi sawa sawa na ilivyoagizwa
na kwa kipindi kizima cha siku saba kamili. Kwenye Kutoka 12:16 hapo juu
tumeona kwamba inasema kwamba siku ya kwanza na ile ya
saba tunatakiwa kuitisha kutaniko takatifu na kazi isifanywe siku hizo zote, bali
twaweza kuzifanya zile ambazo kwazo twaweza kuwezeshwa kula tu.
Kumbukumbu la
Torati 16:8 Siku sita
utakula mikate isiyotiwa chachu; na siku ya saba na
uwe mkutano mtukufu kwa Bwana, Mungu wako, usifanye kazi yo yote.
Sadaka hii ya Mganda wa Kutikiswa inatolewa katika
siku ya kwanza ya juma, maarufu kama Jumapili
(majira ya saa 9 kamili asubuhi) wakati au ndani ya kipindi cha Idi ya Mikate
isiyotiwa Chachu. Sadaka hii inaashiria tendo la Kristo kuingia kwenye chumba
cha Kiti cha Enzi cha Mungu ili akubaliwe baada ya
ufufuko wake kutoka kwa wafu kama ilivyoonyeshwa
kwenye kitabu cha Danieli 7:13-14 na Yohana 20:17. Kristo
alifanyika kuwa ni sadaka ya kutikiswa, ambayo ni malimbuko wa mavuno yote (Kutoka 29:24-27;
pia tazama Mambo ya Walawi 7:30, 34; 8:27, 29; 9:21; 10:14, 15; 14:12, 24;
23:11-20; Hesabu 5:25; 6:20; 18:11, 18)” (Cox, W.E., “K” jarida la Pasaka (Na. 98) [The Passover (No. 98)], CCG, 1995-2008,
ukurasa 2,3,8,9).
“Adhimisho la
Mganda wa Kutikiswa ni amri ya lazima linaloendana na
adhimisho la Sikukuu ya Pasaka na inahusiana na zote mbili za kipindi cha
Pentekoste na ulaji wa mavuno mapya” (Mambo ya Walawi 23:9-14) (Cox, W.E., “L” jarida la (Mganda wa Kutikiswa (Na. 106b) [The Wave Sheaf Offering (No. 106b)], CCG, 1995-2008, ukurasa 2).
Idi ya Majuma au Pentekoste (Kutoka
23:16; 34:22) hufanyika siku ya hamsini tangia siku ya kutolwa kwa Mganda wa Kutikiswa ambayo huwa katika siku ya kwanza ya
juma, au Jumapili ilifuatiwa na Sabato saba kamili. Idi hii ya Majuma ni ishara mavuno ya wateule, ambayo inafananishwa na mavuno
ya ngano. Soma jarida la Jinsi ya Kuhesabu Kufikia Pentekoste (Na. 173) [The Omer Count to Pentecost (No. 173)].
Idi hii ya Ukumbusho wa Kuzipiga baragumu huadhimishwa siku ya Kwanza ya mwezi wa
Saba (Tishri) ni siku ya mapumziko na kufanya
mkutano mtakatifu (Mambo ya Walawi 23:24). Siku hii Takatifu kwa
kawaida inaonekana kuwa ni ashirio la baragumu ijayo itakayopigwa na Malaika
Mkuu Mikaeli na kwenye Maknisa ya Mungu inawakilisha kurudi kwa Masihi. Pia
soma jarida la Baragumu (Na. 136)
[Trumpets (No. 136)].
Siku ya Upatanisho ni
ya kuitisha kusanyiko takatifu na kwenye siku hii tunazitesa nafsi zetu (Mambo ya Walawi 23:27). Inaangukia katika siku
ya 10 ya mwezi wa Saba
na inamaana ya upatanisho wa Israeli na Mungu hapa Duniani kipindi cha kuja
kwake Masihi. Soma pia jarida la Upatanisho (Na. 138) [Atonement (No. 138)].
Kumbukumbu la Torati 16:13-15 Fanya sikukuu ya vibanda siku saba, utakapokwisha
kuyakusanya yatokayo katika sakafu yako ya nafaka, na katika kinu chako cha
divai; 14 nawe utafurahi katika sikukuu yako, wewe,
na mwanao, na binti yako, na mtumwa wako, na mjakazi wako, na Mlawi, na mgeni,
na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako. 15 Siku saba mfanyie sikukuu Bwana, Mungu wako, mahali
atakapochagua Bwana; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, atakubarikia katika maongeo
yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa.
Sikukuu ya Vibanda au Sikukuu ya
Kukusanyika (Kutoka 23:16; Kumbukumbula Torati 29:12-40) ni kiashirio cha zama ya utawala wa milenia ambapo Masihi
atakuwa ni mtawala. Sikukuu hii huwa inaanza tangu siku ya kumi na Tano ya wezi wa Saba
ambayo pia ni Siku Takatifu. Inafuatiwa na Sikukuu
nyiungine inayokwenda kipindi kimoja katika siku ya 22 inayoitwa ni Siku ya
Mkunato wa Makini ambayo ni Sikukuu muhimu sana kuiadhimisha pia. (Mambo ya Walawi
23:34; Kumbukumbu la Torati 16:13-15; 31:12-13). Sikukuu hii ya Mkutano wa Makini huashiria ufufuo wa pili na wa mwisho
utakaofanyika baada ya kipindi cha miaka efu moja kinachojulikana pia kama Molenia na cha ujio wa Mji Mtakatifu wa Mungu. Soma
jarida la Maadhimisho ya Sikukuu
(Na. 56) [Keeping
the Feasts (No. 56)].
“Kuna
taratibu zinazotuongoza katika kufanya maandalizi ya jinzi ya kuadhimisha
Sikukuu hizi. Haitosho tu kwa sisi kufanya
maamuzi ya kuacha kufanya kazi zetu na kwenda kushika sikukuu hizi, bali
tunapaswa kujua kwamba sisi sote tunapaswa kujiandaa kifedha na kimwili pia. Hii
inamaanisha kwamba tunatakiwa tufanye maandalizi kwanza na
ndipo tuende kuziadhimisha Sikukuu hizi. Kumbukumbu la Torati 12:17-19 inasema
kuna utaratibu na kanuni za kutumia zaka ya pili.
Tunatakiwa kuitenga kando zaka ya pili ili tuitumie
tunapokwenda kwenye Sikukuu hizi.
Kumbukumbu la Torati 12:17-19 Usile ndani ya
malango yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala
wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng'ombe wala ya kondoo, wala nadhiri
zako uwekazo zo zote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya
mkono wako; 18 lakini hivyo mtakula mbele za Bwana,
Mungu wako, mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, wewe, na mwanao mume na
mke, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe
furahi mbele za Bwana, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako. 19 Jilinde nafsi yako usimwache Mlawi siku zote uishizo
katika nchi yako.”
(Cox, W.E,
“M” Keeping the Feasts (No. 56), CCG,
1994-2007, ukurasa wa 8).
Zaka hii ya pili inatakiwa itumike kwenye kipindi hiki
tunachojihudhurisha kwenye Sikukuu hizi kwenye maeneo yetu wakati umbali
unapokuwa mkubwa kufikia kwenye mahali palipochaguliwa kufanyika Idi hizi.
Kumbukumbu la Torati 12:21 Na mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, apaweke jina
lake, pakiwa mbali nawe mno, ndipo utakapochinja katika kundi lako la ng'ombe na kondoo alilokupa Bwana kama
nilivyokuagiza, nawe utakula ndani ya malango yako, kwa kufuata yote
inayotamani roho yako.
Kama tunavyowea kujinea, utaratibu wa kujiwekea akiba ya zaka hii umefungamanishwa na
maadhimisho haya ya Sikukuu.
Kumbukumbu la
Torati 14:22-29 inasema: "Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi
katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. 23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali
atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na
mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili
upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima. 24 Na
njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno
atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia
Bwana, Mungu wako; 25 ndipo uzibadili ziwe
fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali
atakapochagua Bwana, Mungu wako; 26 na zile fedha
zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai,
au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za
Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; 27 na
Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi
pamoja nawe. 28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa
fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;
29 na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na
mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako,
na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi
yote ya mkono wako uifanyayo.
Sikukuu hizi zinafanya kazi ndani ya
mfumo wa Yubile. Soma pia jarida la Sikukuu za Mungu na Jinsi Zinavyohusiana na Uumbaji
(Na. 227) [God's
Feasts as they relate to the Creation (No. 227)].
Jinsi Sikukuu hizi zinavyohusika kuwa
ni sehemu ya Mpango wa Wokovu wetu
Kusudi la Mpango wa
Mungu limefunuliwa na utaratibu na mpangilio wa hizi Sikukuu, kwa namna
zilivyopangiliwa zikiwa ni amri mhumu kuagizwa na Biblia. Sikukuu hizi
ziliamriwa na Yahova (Yehova) na akapewa maagizo yake
nabii Musa. Sikukuu hizi ziliamriwa kuwa zitangazwe kwa kupigiwa mbiu kuwa ni
siku takatifu na ambazo wanatakiwa kufanya ,akutaniko
matakatifu kwa Bwana. Ikumbukwe pia kwamba Sikukuu hizi ni
za Bwana na aliziita mwenyewe kuwa hizi
ni Sikukuu Zangu (Law. 23:2). Zimeitwa
na kujulikana kuwa ni Sikukuu za Bwana kwenye Mambo ya Walawi 23 na 2Nyakati 2:4. Neno sikukuu zenu lilitumika pia kwenye
kitabu cha Hesabu 15:3 na 29:39. Neno sikukuu zao limetumika kwenye kitabu cha
Isaya 1:14 na 5:12 kwa matumizi yaliyo kinyume na ukweli halisi ulivyoandikwa
kwenye nakala hasilia za kale. Sikukuu hizi hazina uhusiano wowote na mambo ya kidunia wala hazihusiani na mifumo yoyote ya
watu wa dunia hii. Na haziwezi kubadiilika kwa sababu
yoyote ile au kuondolewa hadi utakapokuja Mpango wale kamili wa Wokovu, ambao
kwazo huwakilisha, kipindi ambacho mpango wake huu utakapokuwa umeondolewa au
kufikia tamati yake.
Mambo ya
Walawi 23:2-44 inasema: "Nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Sikukuu za Bwana, ambazo
mtazipigia mbiu kuwa ni makusanyiko matakatifu; hizi ni sikukuu zangu. 3 Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya
kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote; ni Sabato
kwa Bwana katika makao yenu yote. 4 Sikukuu za Bwana ni
hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo mtayapigia mbiu kwa nyakati zake. 5 Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa
jioni, ni pasaka ya Bwana. 6 Na siku ya kumi na
tano ya mwezi ule ule ni sikukuu kwa Bwana ya mkate usiotiwa chachu; mtaila
mikate isiyochachwa muda wa siku saba. 7 Siku
ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu msifanye kazi yo yote ya utumishi. 8 Lakini mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto siku
saba; siku ya saba ni kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. 9 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 10 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa
mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo
mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; 11 naye
atautikisa mganda mbele za Bwana ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya
pili baada ya Sabato kuhani atautikisa. 12 Na
siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume mkamilifu wa
mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. 13 Na
sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba
uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto kuwa
harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini.
14 Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata
siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni
amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote. 15 Nanyi
mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mliyouleta
mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba; 16 hata
siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea
Bwana sadaka ya unga mpya. 17 Mtatoa katika makao
yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa;
itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa Bwana. 18 Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtasongeza wana-kondoo
saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza, na ng'ombe mume mmoja, na kondoo
waume wawili; watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, pamoja na sadaka yao ya
unga, na sadaka zao za kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza iliyosongezwa
kwa Bwana kwa njia ya moto. 19 Nanyi mtasongeza
mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wana-kondoo wawili waume wa mwaka wa
kwanza kuwa dhabihu ya sadaka za amani. 20 Kisha
kuhani atawatikisa pamoja na hiyo mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya kutikiswa
mbele za Bwana, pamoja na wale wana-kondoo wawili; watakuwa watakatifu kwa
Bwana, wawe wa huyo kuhani. 21 Nanyi mtapiga mbiu
siku iyo hiyo; kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; msifanye kazi yo yote ya
utumishi; ni amri ya milele katika makao yenu yote, katika vizazi vyenu. 22 Nanyi hapo mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune
kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala msiyakusanye masazo ya mavuno yako;
utayaacha kwa ajili ya huyo maskini, na mgeni; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 23 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 24 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi wa saba, siku
ya kwanza ya mwezi, kutakuwa na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa
kuzipiga baragumu, ni kusanyiko takatifu. 25 Msifanye
kazi yo yote ya utumishi; nanyi mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto. 26 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 27 Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya
upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi
mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto. 28 Nanyi
msifanye kazi yo yote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ili kufanya
upatanisho kwa ajili yenu mbele za Bwana, Mungu wenu. 29 Kwa
kuwa mtu awaye yote asiyejitesa mwenyewe siku iyo hiyo, atakatiliwa mbali na
watu wake. 30 Na mtu ye yote afanyaye kazi ya namna yo
yote siku hiyo, mtu huyo nitamwangamiza atoke katika watu wake. 31 Msifanye kazi ya namna yo yote; ni amri ya milele katika
vizazi vyenu, katika makao yenu yote. 32 Itakuwa
kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya
mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu. 33 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 34 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano
ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana. 35 Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye
kazi yo yote ya utumishi. 36 Mtamsongezea Bwana
sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu;
nanyi mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi
yo yote ya utumishi. 37 Sikukuu za Bwana ni
hizi, ambazo mtazipigia mbiu ya kuwa ni makusanyiko matakatifu, ili mmsongezee
Bwana sadaka kwa moto, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na dhabihu, na
sadaka za kinywaji, kila sadaka kwa siku yake; 38 zaidi
ya hizo Sabato za Bwana, na zaidi ya matoleo yenu, na zaidi ya hizo nadhiri
zenu zote, na zaidi ya sadaka zenu za hiari, ambazo mwampa Bwana. 39 Lakini siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, hapo
mtakapokuwa mmekwisha kuyachuma mavuno ya nchi, mtaweka sikukuu ya Bwana muda
wa siku saba; siku ya kwanza kutakuwa na kustarehe kabisa, na siku ya nane
kutakuwa na kustarehe kabisa. 40 Nanyi siku ya kwanza
mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti
minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za Bwana, Mungu wenu,
muda wa siku saba. 41 Nanyi mtaishika kuwa
sikukuu kwa Bwana muda wa siku saba katika mwaka; ni amri ya milele katika
vizazi vyenu; mtaishika katika mwezi wa saba. 42 Mtakaa
katika vibanda muda wa siku saba; wazalia wote wa Israeli watakaa katika
vibanda; 43 ili vizazi vyenu vipate kujua ya kuwa
niliwaketisha wana wa Israeli katika vibanda, hapo nilipowaleta kutoka nchi ya
Misri; mimi ndimi Bwana Mungu wenu. 44 Naye Musa akawaambia
wana wa Israeli hizo sikukuu za Bwana.
Kristo aliziadhimisha zote, yaani
Sabato ya juma, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu zote
hizi. Kanisa la Mitume pia waliadhimisha Sabato, Miandamo ya Mwezi na Sikukuu zote hizi (Makolosai 2:16) na ndivyo lilivyofanya
kanisa kwa kipindi chote cha zaidi ya miaka elfu mbili. Katika kipindi cha
Milenia mataifa yote pia wataziadhimisha Sabato zote hizi, yaani za juma, na Miandamo ya Mwezi na Sikukuu zote (Isaya 66:23; Zekaria
14:16-19).
Mchakato mzima wa
kuzielezea na kuwafanya wateule wajulikane miongoni mwa vikundi vyote
vinavyojiita Wakristo unatimilika kwa kutegemea kama
wanaziadhimisha au kuzijua Siku hizi Takatifu zinapokuwa zinatikea hadi
kutakapofika Ufufuo Mkuu au wa Pili ambao ni wa watu wote. Siku hizi takatifu
hazitaweza kukoma hadi siku ile ya Mkutano Mkuu wa
makini utakapokamilisha sehemu ya mpango wake. Kila Sikukuu inawakilisha
utaratibu huu endelevu wa Mpango wa Mungu na kwa tafsiri
nyingine huitwa mfumo wa mavuno ambao bado unadumu na kwa sasa umefunuliwa
kwetu.
1Petro 2:5 Ninyi nanyi, kama
mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu
za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
Ukristo Mamboleo wa
sasa hauuna habari na wala hauzijui na kuziadhimisha Sikukuu hizi hali
inayowafanya washindwe kuelewa lolote lililo kwenye Mpango huu wa kibiblia.
Makanisa haya ya kisasa hayatilii maanani maelekezo au amri hizi ambazo Biblia
(ambayo ni msingi wa dini ya Ukristo wa Kiyahudi) inaonyesha kuwa ziliwekwa
tangu mwanzo wa uumbaji kama ulivyoelezwa kwenye kitabu cha Mwanzo na hatimaye
zinatolewa na kuamriwa na Mungu kupitia nabii Musa na watumishi wake wengine
waliofuatia. Sheria hizi zinaelezea kwa kina jinsi ya
kuiishia Imani na kuelezea umuhimu wa Sikukuu zake.
Sikukuu hizi zimeamriwa na Mungu kwa
kupitia Kristo na Kristo ameziendeleza na kuaiwekea utaratibu kwa kuweka
maelekezo yake kwa wateule na hatimaye kwa watu wa mataifa yote kwa utaratibu
mwelekeo wa Milenia. Kristo ni yeye yule, jana leo,
kesho na hata milele (Waebrania 13:8). Mungu hana kigeugeu
(Malaki 3:6; Yakobo 1:17). Kwa hiyo, hakuna mabadiliko na kwa hiyo, siku wanazozishikilia kuwa ni takatifu kwa
wanadamu zilizotolewa na kuelekezwa kwenye Sheria na amri hazibadiliki.
Siku hizi Takatifu na
Sabato zimesusiwa na kupotezewa naama na umuhimu yake kwa makusudi kabisa. Hiyo
ndiyo ahadi ambayo Mungu mwenyewe ameiweka kwa kupitia
manabii wake watakatifu. Mungu alisema hivyo kupitia nabii Amosi kwa kulilinganisha taifa la Israeli kwenye Siku za Mwisho
sawa na kapu la matunda ya wakati wa hari (Amosi 8:1). Trndo la kushindwa
kumtii Mungu ni chanzo kikubwa. Adhabu inayotokana na hali hii ya kumuasi Mungu ni kwamba maadhimisho haya ya
Sabato na Sikukuu kubadilika kuwa ni maombolezo. Hii inafuatia na kukumbwa na njaa ya kukosa kulisikia neno la Yahova
(Yehova) (Amosi 8:11-14). Ni kwa ajili ya kushindwa kuelewa
asili ya Mungu Mmoja wa Pekee na wa Kweli (Yohana 17:3; 1Yohana 5:20) watu
wanaadhibiwa (Hosea 8:5-9).
Wateule wanahukumiwa
kutokana na jinsi wanavyomjua Mungu Mmoja, wa
Pekee na wa Kweli, jambo ambalo kanuni ya aheria inavyotaka na kuwa ikamilike
ndani ya mioyo ya watu kwa jinsi ya kila mtu peke yake na binafsi yake.
Jambo kuu hapa
siyo Sabato au Sikukuu au Sheria au Amri, bali ukweli wa kwamba Mungu, baba
yetu ni Mmoja na wa Pekee na wa Kweli (Yohana 17:3; 1Yohana 5:20) na kwamba, ni
yeye tu peke yake hawezi kufa (1Timotheo 6:16). Mtu anaweza kuitunza Sabato nab
ado anaweza kuwa ni mtu mwenye imani potofu. Iwapo kama hatuta shikilia kwa bidii ukweli huu tutaondolewa mbali
kutoka kwa wateule na tukatolewa kwenye upotevu mkuu na tukaamini uwongo (2Wathesalonike
2:11).
(Cox, W.E., “N” The Holy Days of God (No. 97), CCG,
1995-2007, kurasa za 2,5,6,7,8,11).
“Moja wapo ya maandalizi ya Sikukuu
hizi zote ni tendo la kutafakari na kushukuru kwa
baraka zote ambazo Mungu, baba yetu ametubarikia amabazo hatimaye zinafanyika kuwa
ni sadaka tunazomtolea kama kumrushia yeye mwenyewe aliyetukirimia. Hatuwezi kujionyesha
tu tukijihudhurisha kwenye Sikukuu kwa kufanya maamuzi
ya wakti ule tu kwa kulinganisha na kile tulichonacho mifukoni mwetu kwa wakati
ule, au kwa kuandika hawala ya kuchukulia fedha benki na tukifikiri kuwa
tumetimiza wajibu wetu kama Wakristo.
2Wakorintho 9:7 Kila mtu na atende kama
alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu
humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
Tunapaswa kutilia maanani kile ambacho
Mungu alichotufantia kwa kutoa sadaka inayoendana na
ukweli wa baraka zake alizoturuzukia.
Kumbukumbu la Torati 16:17 Kila mtu na
atoe kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya
Bwana, Mungu wako, alivyokupa.
Mara tatu kila mwaka Mungu ametuamuru
tukutanike mahali alipolikalisha jina lake, na na
kamwe tusiende mbele zake Bwana mikono mitupu.
Kumbukumbu la Torati
16:16 "Mara tatu kwa
mwaka na watokee wanawaume wako wote mbele za Bwana, Mungu wako, mahali
atakapochagua; katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na katika sikukuu ya
majuma, na katika sikukuu ya vibanda; wala wasitokee mbele za Bwana mikono
mitupu.
Neno hili la “mahali alipopachagua”
limebadilishwa kwa mara nyingi na linategemea kwa
mahali kwenye mataifa ambayo Mungu ametupa kuyamiliki. Sikukuu hizi
zinaadhimishwa na kusherehekewa kwenye mataifa tuliyopewa na haitegemei kuwa ni
mjini Yerusalemu” (Cox, W.E., “O” jarida la Sadaka au Dhabihu (Na. 275) [Offering (No. 275)], CCG, 2006, ukurasa
wa 2,3).
“Maelekezo kuhusu
jinsi ya kupachagua mahali hapa yanapatikana kwenye kitabu cha Kutoka 23:17-19.
Kutoka 23:17-19 Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana
MUNGU. 18 Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja
na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata
asubuhi. 19 Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako
utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya Bwana, Mungu wako. Usimtokose
mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
“Mafuta” ni
dhabihu mojawapo itolewayo kwenye Sikukuu. Haina maana kuwa ni mafuta yale
yaliyokatazwa kwenye Sheria ndiyo yaliwe hapa (kama
ilivyoandikwa kwenye Mambo ya Walawi 3:17). Neno hilohilo ndilo linaloonekana kwenye
kitabu cha Mwanzo 45:18 na Nehemia 8:10.
Mambo ya Walawi 3:17 Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu
vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.
“Kwa mujibu wa
Amri na Sheria zake, sadaka zinaweza kutolewa mara tatu kila mwaka—na siyo kila Siku Takatifu. Pia utoaji na makusanyo yanatakiwa yafanyike katika kila siku ya kwanza
ya Sikukuu hizi jioni yake ya kwanza ya kila Sikukuu, na isibakizwe hata
asubuhi yake. Kuna maana nzuri kufanya hivyo, yaani ni
kwamba ili kuwafanya masikini na Walawi wale na maandalio yalifanywa kabla ya
Sikukuu. Masihiataurudisha utaraibu huu kwenye kipindi cha utawala wa Milenia, lakini hii ni mojawapo ya sheria na amri za
Mungu zinazotakiwa kufanywa hata leo” (soma pia jarida la Makutaniko (Na. 139) [Ingathering
(No. 139)].
Sikukuu ya
Ukumbusho wa Kuzipiga Baragumu haikuandikwa kwenye Kumbukumbu
la Torati 16. Sambamba na hilo kumekatazwa kabisa kutoa aina yoyote ya
sadaka tunapojihudhurisha kuiadhimisha Siku ya Upatanisho. Kwa hiyo, kutajwa tu
kuwa ni mara tatu
kwa mwaka na ndivyo ilivyagizwa na inamaana hiyohiyo tu. Mahusiano yake
yanalenga kuelezea mavuno makuu matatu ya Mungu ambayo ni: Masihi akiwa kama ni
sadaka ya Mganda wa Kutikiswa, Wateule wakiwa kama ni wahusika wa ufufuo wa
Kwanza (sawa na mavuno ya ngano ya wakati wa Pentekoste), na mavuno makuu ya
mwisho wa dunia yaliyo kwenye taswira ya Sikukuu ya Vibanda.
Tendo la kufanya machangizo na kutoa sadaka za kila juma kufanywa Kanisani ni kinyume na
amri na sheria za Mungu. Changizo analolitaja mtume Paulo kuwa lifanyike siku ya kwanza ya juma, au Jumapili,
halikuwa ni agizo au ashirip la kuwekwa kwa sheria nyingine ya kuabudu siku ya
Jumapili na wala hakumaanisha kuanzishwa kwa utaratibu mpya wa kutoa sadaka kwa
kila juma (1Wakorintho 16:2-4)” (Cox, W.E. “P” jarida la Zaka (Na. Tithing (No. 161), CCG, 1996-2007, kurasa
za 12,13).
“Sadaka iliyotakiwa iligeuzwa kutoka
umuhumu wake hadi kufanyika kuwa sadaka ya kiroho ya kila siku zilizo kwenye
mfumo wa Siku Takatifu, tangia Sabato, Miandamo ya
Mwezi na Sikukuu. Dhabihu zitolewazo kwa mujibu wa
amri na Sheria ziliamriwa kwa kufanyika makusanyo au changizo maalumu yaliyoratibiwa
kwa mujibu wa mamlaka ya kitaifa. Matoleo au changizo la Mfalme limeelezwa kwenye
jarida la Zaka (Na. 161) [Tithing (No. 161)].
Ezekieli
45:14-17 na sehemu ya mafuta iliyoamriwa,
katika bathi ya mafuta, itakuwa sehemu ya kumi ya bathi katika kori moja,
ambayo ni bathi kumi, yaani homeri; maana bathi kumi ni homeri moja; 15 na mwana-kondoo mmoja wa kundi katika mia mbili, katika
malisho ya Israeli yenye maji; kwa sadaka ya unga, na kwa sadaka ya
kuteketezwa, na kwa sadaka za amani, ili kuwafanyia upatanisho, asema Bwana
MUNGU. 16 Watu wote wa nchi watatoa toleo hili kwa
ajili ya mkuu katika Israeli. 17 Tena itakuwa kazi ya
mkuu kutoa hizo sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na sadaka za vinywaji,
katika sikukuu, na katika mwezi mpya, na katika sabato, katika sikukuu zote za
nyumba ya Israeli zilizoamriwa; atatengeneza sadaka ya dhambi, na sadaka ya
unga, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani, ili kufanya upatanisho kwa
ajili ya nyumba ya Israeli.
Sadaka hii
zilikuwa ni zaka ya zaka ya mafuta na nusu sadaka ya
zaka ya dhabihu ya nyama. Mfalme aliifanya iwepo na
kutolewa katika Sabato, Miandamo ya Mwezi, Siku Takatifu na dhabihu. Kwa hiyo, sio sahihi kudai kwamba zaka iliondolewa na mahala pake
kuchukuliwa na sadaka kwa kuwa kwa sababu zilitolewa na hali mtengano” (Cox,
“F”, op. cit., p. 5).
Hesabu 31:50-54 inasema: Nasi tumeleta matoleo ya Bwana,
aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali,
na timbi, na pete za muhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho
nafsi zetu mbele ya Bwana. 51 Musa na Eleazari
kuhani wakapokea kwao hiyo dhahabu, maana, vile vyombo vyote vilivyofanyizwa. 52 Na dhahabu yote ya sadaka ya kuinuliwa waliyosongeza kwa
Bwana, ya maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, ilikuwa shekeli kumi na
sita elfu na mia saba na hamsini. 53 (Kwa kuwa hao watu
wa vita walikuwa wametwaa nyara, kila mtu nafsi yake.) 54 Basi
Musa na Eleazari kuhani wakapokea hiyo dhahabu mikononi mwa hao maakida wa elfu
elfu na wa mia mia, na kuileta ndani ya hema ya kukutania, ili iwe ukumbusho
kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za Bwana.
Hesabu 3:44-51inasema: Kisha Bwana akanena na Musa, na
kumwambia, 45 Uwatwae Walawi badala ya wazaliwa wa
kwanza katika wana wa Israeli, na wanyama wa Walawi badala ya wanyama wao; na
hao Walawi watakuwa wangu mimi; mimi ndimi Bwana. 46 Tena
kwa kuwakomboa hao watu mia mbili na sabini na watatu, wa hao wazaliwa wa
kwanza wa Israeli, ambao wamezidi ile hesabu ya Walawi, 47 utatwaa
shekeli tano kwa kichwa cha kila mtu kwa hiyo shekeli ya mahali patakatifu
(shekeli ni gera ishirini); 48 na hizo fedha ambazo
waliosalia wamekombolewa kwazo utampa Haruni na wanawe. 49 Basi
Musa akawatoza fedha za ukombozi, hao waliozidi hesabu ya wale waliokombolewa
na Walawi; 50 akatwaa hizo fedha kwa wazaliwa wa kwanza
wa wana wa Israeli; shekeli elfu moja na mia tatu na sitini na tano kwa shekeli
ya mahali patakatifu; 51 kisha hizo fedha za
ukombozi Musa akampa Haruni na wanawe, kama neno la Bwana, kama Bwana
alivyomwagiza Musa.
Zaka hii ya zaka zote alipewa Kuhani
Mkuu ili kumfanya aendelee kulihudumia Hekalu na adumu
kwenye huduma na maongozi yake (2Wafalme 12:1-19; 22:5-6; Ezra 6:8).
1. Mwaka wa saba wa maachilio ambao watu wanaachiliwa kutoka kwenye shughuli
za utumwa na shokoa (Kutoka 21:2-6, Kumbukumbu la Torati 15:12-18),
2. Kusameheana
madeni (Kumbukumbu la Torati 15:1-6),
na
3. Ni Sabato au mapumziko ya Ardhi (Kutoka 23:10-11; Mambo ya Walawi
25:1-7, 19-24).
Kwenye mwaka huu wa
Sabato au mwaka wa Saba, tunauadhimisha kwa
kuisoma Torati ya Mungu kila siku hasa kwenye maadhimisho ya Sikukuu ya Vibanda
(Kumbukumbu la Totati 31:10-13; Nehemia 7:73; 8:1-18).
Kumbukumbu la Torati 30:10 ukiwa
utaifuata sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa kuyashika
maagizo yake, na amri zake zilizoandikwa katika chuo hiki cha torati;
ukimwelekea Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote.
“Neno linalotakiwa kutumika kukitaja kitabu hiki cha Sheria za Mungu ni Torah au Gombo la Torati. Bullinger anafanya mlingano kama huohuo na pia
anakielezea kama kilivyoandikwa kwenye 2Wafalme 22:8 na 23:25, na anaiweka hoja
yake kutoka kwenye Kutoka 17:14 hadi anapoichukulia kwenye 2Wafalme 22:8-13 kwa
kulinganisha na 23:25 ambapo inaonyesha kwamba Kitabu chote kizima cha Torati
kilipaswa kiheshimiwe na kwa kuwa sio taifa tu lingaliloadhibiwa (sawa na aya
ya 14).
Tunaona kutoka kwenye Nehemia 8:18 kuwa Torati ilisomwa kila siku na
kwamba haipaswi isomwe tu katika siku ya mwisho ya Mkutano wa Makini, au kwa
siku nyingine yoyote peke yake. Sikukuu iliadhimishwa kila siku na kwa mujibu
wa ilivyoagizwa na Torati, na siku ya Nane kulikuwa na kusanyiko takatifu
iliyojulikana kama ni Siku Kubwa ya Mkutano wa Makini (sawa na Mambo ya Walawi
23:36; Hesabu 29:35) iliyofanywa kwa sadaka zake maalumu (sawa na ilivyoandikwa
na Soncino).
Tendo hili la kusomwa kwa Torati linaondoa uwezekano na hatari ya kujipenyeza
imani za kimapokeo na pia husaidia kulinda na kurejesha maadhimisho ya Yubile
na Sabato za Mapumziko ya Ardhi. Pia inaonyesha utii wetu kwenye mapenzi ya Mungu
na huwatia nguvu watu wetu na kuwapa maono ya Mpango
wa Wokovu” (Cox, W.E., “Q” jarida la Jinsi
Usomaji wa Torati ulivyofanywa na Ezra na Nehemia (Na. 250) [Reading the Law with Ezra and Nehemiah (No. 250)], CCG,
1998-2007, ukurasa 11).
“Mwaka huu wa
Sabato huendana na ardhi kupumzishwa kutoilima wala kuichimbwa kwa matumizi ya
kibiashara au mavuno. Maelekezo ya mari hii
yameandikwa kwenye kitabu cha Mambo ya Walawi 25:1-7 ambayo yanakataza upandaji
wowote wa mazao ya aina yoyote mashambani au kuvuna zabibu au vichala vya
mizabibu (Kutoka 23:10). Maongeo ya mashambani na
zabibu za vichala zilivyokaa wazi pia havitakiwi kukusanywa kwenye mwaka huu wa
saba wa mzunguko wa miaka hii mitakatifu. Bali zinaweza kutumiwa kama chakula na wamiliki wenyewe, watu wa nyumbani wake na
watu masikini au wageni wapitao au waliokuja kwenye nchi yao. Kwa hiyo, nchi inatakiwa iwe huru na
isifanyiwe kazi yoyote ingawaje itamea mazao ya namna fulani ambayo yatamea
yenyewe tu pasipo kupandwa wala kulimiwa na mtu” (Cox, “P”, op.cit., ukurasa
wa 13).
Nchi au ardhi yote ni
ya Mungu na haitakiwi kuuzwa kwa kipindi cha kudumu. Sisi ni
wa milki yake Mungu.
Mambo ya Walawi 25:23 Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wasafiri wangu
Hatupaswi kudai umiliki wa mito,
kwa kuwa ni Mungu aliyeifanya hiyo na ni milki.
Ezekieli 29:9 Nayo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa; nao
watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; kwa sababu amesema, Mto huu ni wangu, nami
nimeufanya.
Wakati ardhi inaponajisika Mungu
huihukumu nchi nzima na wakazi wake kutapikwa kwa
kufukuziliwa mbali watoke mbali na nchi hiyo.
Mambo ya Walawi 18:25-30 … na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza
uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa. 26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala
msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati
yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya
machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa
najisi;) 28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi
pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia
mbele yenu. 29 Kwani mtu awaye yote atakayefanya
machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu
wao. 30 Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili
kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia
kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana,
Mungu wenu.
Tendo la
kuzivunja amri ma sheria za Mungu zilizoandikwa kwenye Torati yake Mungu
husababisha hukumu. Adhabu na matukio
yatakayofuatia kama hatutasikiliza na kuishika Torati hii,
vimeandikwa kwenye Mambo ya Walawi 26:14-33.
Mambo ya Walawi 26:14-15 " Lakini msiponisikiza,
wala hamtaki kuyafanya maagizo hayo yote; 15 nanyi
mkizikataa amri zangu, na roho yenu ikichukia hukumu zangu, hata ikawa hamtaki
kuyafanya maagizo yangu yote, bali mwalivunja agano langu;
Mambo ya Walawi 26:43 Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa
pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu, naam, ni kwa
sababu wamezikataa hukumu zangu, na roho zao zimezichukia amri zangu.
Tunapokuwa tukipanda aina yoyote ile
ya miti ya matunda, matunda yamekatazwa kuliwa yanapokuwa yanatoa mazao yake ya
kwanza yatokayo kwenye mwaka wa kwanza.
Mambo ya Walawi 19:23-25 Nanyi hapo mtakapoingia nchi ile, mkiwa mmepanda miti ya
namna zote kwa ajili ya chakula, ndipo mtayahesabu
matunda yake kama ni kutotahiriwa; muda wa miaka mitatu miti hiyo itakuwa kwenu
kama kutotahiriwa; matunda yake hayataliwa. 24 Lakini mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa ni
matakatifu, kwa ajili ya kumpa Bwana shukrani. 25 Na
katika mwaka wa tano mtakula katika matunda yake, ili ipate kuwapa maongeo
yake; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Vilevile kama
tunavyojionea kwenye kwenye mwaka wa nne matunda yote yanachukuliwa kuwa ni
matakatifu ya yanatakiwa yapelekwe kwa makuhani yakiwa kama
sadaka kwa Bwana.
Hesabu 5:9-10 Tena kila sadaka ya kuinuliwa, ya vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, watakavyosongeza kwa kuhani, itakuwa ni yake. 10 Tena vitu vilivyowekwa wakfu na mtu awaye yote, vitakuwa
ni vya kuhani; kitu cho chote mtu atakachompa kuhani, kitakuwa chake.
“Tendo la kuiadhimisha Sabato hii ya
Mapumziko ya ardhi ni la muhimu, ingawa linashutumiwa
na kuonekana kuwa linaenda kinyume na maendeleo ya uchumi au ustawi endelevy wa
taifa. Hukumu kwa kutoitunza sheria hii ya Sabato na
mapumziko ya ardhi na kutoutunza mwaka wa Yubile ni nchi au taifa zima kwenda
utumwani (Mambo ya Walawi 26:33-35).
Mambo ya Walawi 26:34-35 Hapo ndipo nchi itakapozifurahia Sabato zake, wakati
itakapokuwa hali ya ukiwa, nanyi mtakapokuwa katika nchi ya adui zenu; ndipo
nchi itakapopumzika, na kuzifurahia Sabato zake. 35 Wakati wote itakapokuwa na ukiwa, itapumzika; ni hayo
mapumziko ambayo haikuwa nayo katika Sabato zenu, hapo mlipokaa katika nchi
hiyo
Yuda walikwenda utumwani kwa kuwa roho ya kuzipenda amri za Mungu iliondoka kwao na
wakanajisika. Yaani ni kusema kwamba, walizitia unajisi Sabato za nchi na utaratibu
wa Yubile ulipotea kiasi cha kwamba Wayahudi walikuwa wanauza ardhi yao kwa mtindo
wa kujodisha ufikapo mwaka wa Saba, na kumpa mtu asiye Myahudi alilime na hata
kwa mtu wa tatu zaidi alilime na hatimaye wakarudi na kuyadai mashamba yao mwaka
unaofuatia, na hali kadhalika walifanya hivyohivyo kwa shughuli nyingine za
kibiashara ambazo walifanya kwa kukodisha au kuweka poni kipindi chote cha
Sikukuu kikifika, na kadhalika wa kadhalika. Hii ilionyesha
kuwa walikuwa wanamdhihaki Mungu.
2Nyakati 36:20-21 Na wale waliookoka na upanga
akawachukua mpaka Babeli; wakamtumikia yeye na wanawe hata kulipoingia milki ya
Uajemi; 21 ili kulitimiza neno la Bwana kwa kinywa
cha Yeremia, hata nchi itakapofurahia sabato zake; kwa maana siku zote ilipokaa
ukiwa ilishika sabato, kutimiza miaka sabini.
Kwenye kitabu cha 2Nyakati 36:20-21, tunaona
kwamba lengo la unabii uliotolewa na nabii Yeremia (Yeremia 29:10), ilikuwa ni
kwamba Yuda walichukuliwa na kupelekwa utumwani na Yerusalemu na nchi ya Yuda
vikabakia ukiwa kwa kipindi cha miaka 70, ili kuifanya nchi na arhi yake
vipumzike na kuzifurahia Sabato zake—kwa kuwa Yuda waliacha kuzitunza Sabato na
hawakuzishika sheria zake kikamilifu kwenye kipindi kama hicho hicho cha majuma
ya miaka 70 iliyokuweko huko nyuma yao, kama vila; tangu kujengwa kwa Hekalu la
Sulemani, ambayo ilikuwa ni kipindi cha historia yenye kutukuka ya Israeli
iliyofanywa maana yake na Makerubi aliyoonyeshwa nabii Ezekieli kwa njia ya
maono. Inapaswa ijulikane pia kwamba taifa lililotumiwa kuiadhibu na kuihusuru Yuda hatimaye lilianguka na Yuda ikarejea na
kufanywa upya” (Cox, W.E., “R” kwenye jarida lake la Maana ya Maono ya Ezekieli (Na. 108) [The Meaning of Ezekiel’s Vision (No. 108)], CCG, 1995-2008,
ukurasa wa 3, 4).
Milki
mbalimbali za maeneo au nchi waliyopewa makabila ya Israeli zinaonekana kwenye
kitabu cha Yoshua sura zile za 14 hadi 19.
Yoshua 18:1-10 inasema: Kisha mkutano mzima wa wana wa
Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania kuko;
nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao. 2 Zilisalia
katika wana wa Israeli kabila saba ambazo hazijagawanyiwa bado urithi wao. 3 Yoshua akawauliza wana wa Israeli, akasema, Je! Hata lini
mtakuwa walegevu katika kuingia kwenu na kuimiliki hiyo nchi, ambayo yeye
Bwana, Mungu wa baba zenu, amewapa? 4 Haya, jichagulieni
watu watatu kwa ajili ya kila kabila; nami nitawatuma, nao watainuka waende
kati ya hiyo nchi, na kuiandika kama urithi wao ulivyo; kisha watanijilia mimi.
5 Watu hao wataigawanya nchi iwe mafungu saba; Yuda atakaa
katika mpaka wake huko upande wa kusini, na nyumba ya Yusufu watakaa katika
mpaka wao upande wa kaskazini. 6 Nanyi mtaiandika nchi
iwe mafungu saba, kisha hayo maandiko yake mtaniletea mimi hapa; nami nitawapigia
kura hapa mbele ya Bwana, Mungu wetu. 7 Kwa
maana Walawi hawana fungu kati yenu; Kwa kuwa huo ukuhani wa Bwana ndio urithi
wao; tena Gadi, na Reubeni, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wamekwisha pata
urithi wao ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki, ambao walipewa na
Musa, mtumishi wa Bwana. 8 Basi watu hao
wakainuka wakaenda; kisha Yoshua aliwaagiza wale waliokwenda kuiandika nchi,
akawaambia, Endeni, mkapite katikati ya nchi, na kuiandika habari zake, kisha
mnijie tena hapa, nami nitawapigia kura kwa ajili yenu hapo mbele za Bwana huko
Shilo. 9 Basi watu hao wakaenda, wakapita katikati
ya nchi, wakaandika habari zake katika chuo, na kuigawanya kwa miji yake, hata
iwe mafungu saba, kisha wakamrejea Yoshua maragoni huko Shilo. 10 Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za
Bwana katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi
sawasawa na mafungu yao.
Yoshua 19:51 Hizi ndizo
nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa
Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya kabila za wana wa Israeli,
walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya Bwana,
hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya
hiyo nchi.
Miji ya makimbilio imeelezewa kwenye
sura yote ya 48 ambako kunajumuisha pia wajibu wanaotakiwa kuufanya katika
kugawiwa milki ya ardhi kwa makabila haya.
Yoshua 20:2-9 inasema: "Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Haya, toeni hiyo miji ya
makimbilio, ambayo niliwaambia habari zake kwa mkono wa Musa; 3 ili kwamba mwenye kuua mtu, aliyemwua mtu awaye yote
pasipo kukusudia, na pasipo kujua, apate kukimbilia kuko; nayo itakuwa ni
mahali pa kukimbilia kwenu, kumkimbia huyo ajilipizaye kisasi cha damu. 4 Naye ataikimbilia miji hiyo mmojawapo, naye atasimama
hapo penye maingilio ya lango la huo mji, kisha atanena neno lake masikioni mwa
wazee wa mji; nao watamtia kwao ndani ya mji, na kumpa mahali, ili apate kukaa
kati yao. 5 Na kama huyo mwenye kujilipiza kisasi cha
damu akimwandamia, ndipo hawatamtoa huyo mwuaji kumtia mkononi mwake huyo; kwa
sababu alimpiga mwenziwe naye hakujua, wala hakumchukia tangu hapo. 6 Naye atakaa katika mji huo, hata hapo atakaposimama mbele
ya mkutano kuhukumiwa, hata kifo chake kuhani mkuu mwenye kuwapo siku hizo;
ndipo yule mwuaji atarudi, na kuuendea mji wake mwenyewe, na nyumba yake
mwenyewe, hata mji huo alioutoka hapo alipokimbia. 7 Nao
wakaweka Kedeshi katika Galilaya katika nchi ya vilima ya Naftali, na Shekemu
katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-arba (ndio Hebroni) katika nchi ya
vilima ya Yuda. 8 Tena ng'ambo ya pili ya Yordani pande za
Yeriko upande wa kuelekea mashariki wakaweka Bezeri ulioko nyikani, katika nchi
tambarare ya kabila ya Reubeni, na Ramothi katika Gileadi katika kabila ya
Gadi, na Golani katika Bashani katika kabila ya Manase. 9 Miji
hiyo ndiyo miji iliyoamriwa kwa ajili ya wana wa Israeli wote, na kwa ajili ya
mgeni akaaye kati yao ugenini, ili kwamba mtu awaye yote atakayemwua mtu pasipo
kukusudia apate kimbilia huko, asife kwa mkono wa mwenye kujilipiza kisasi cha
damu, hata hapo atakapokuwa amekwisha simama mbele ya mkutano.
“Miji iliyochaguliwa ilikuwa ni ile ambayo pia walipewa Walawi, ambako kwa kawaida sheria
za Mungu zilitakiwa zijulikane sana
na kuheshimiwa au kuogopwa” (sawa na tunavyoona kwenye Yoshua 20, hasa ukisoma
Biblia inayoitwa The NIV Study Bible, ukurasa wa 318).
Aina ya Sabato
“Mwaka wa Sabato unaruhusu kila mtu
awe huru kutokana na kazi zote shokoa na za kitumwa zilizoandikwa kwenye amri hii
ya nne kufanywa kwenye siku zote za wiki kwa mwaka wote, isipokuwa tu siku za
Sikukuu, Miandamo ya Mwezi na Sabato na zile wanazozifanya siku za kawaida na
walizotakiwa kuzifanya kila siku na zinazofanywa kwenye jamii zao. Watu
wanaweza kuutumia mwaka wa Sabato kwa kujisomea masomo
waliyoyachagua kujifunza, na hasa yale yanayoihusu Biblia na ambayo yanaweza
kuwasaidia kuwapa maarifa ya kupata faida ya kiuchumi. Katika mwaka wa kawaida, mtu anapoamua kuutumia mwaka mzima wote kwa
mapumziko na kuacha kufanya kazi yoyote, basi ajua kwamba anaivunja amri hii ya
nne.
Umuhimu wa
kujiepusha kutokana na kufanya biashara ya kuiuza ardhi na mazao yanayopatikana
kila mwaka unapifika mwaka huu unamtaka kila mmoja aache kufanya shughuli za
aina yoyote zinazomfanya mtu aweze kutoa zaka ambayo alikuwa anapata kwa kazi
zake za kawaida. Ni ukweli usiopingika kwamba sio watu wote ni
wakulima na sio wote wanategemea kuendesha maisha yao kutokana na mazao au maongeo ya ardhi. Kwenye
jamii zetu za leo watu wengi wanafanya shughuli za
kawaida na ni wachache sana
miongoni mwao wanaoweza kupata fursa ya kupewa likizo na kulipwa kwa ajili ya
Sabato. Hata hivyo, hii hafanyi kutoa fursa au udhuru kwa
watu kutoishika sheria hii au haki yake mbayo kila mtu ameamriwa kuitunza kwa
mujibu wa Amri na sheria hii. Ni suala la kuamua tu kwa
mtu kuamua ama kufanya kazi na kuingiza mapato yake kwa kufanya kazi zaidi ya
kushughulikia shughuli na biashara ya mazao.
Mungu ameahidi kwamba tutapata mazao
mrngi sana
kwenye miaka inautangulia miaka hii ya Sabato na Yubile. Hii ilikuwa ni kuwahakikishia kuwepo kwa akiba kubwa ya zaka na mazao
yaliyotolewa zaka ingekuwepo ili kutuwezesha tuweze kuitunza miaka hii ya
Sabato na Yubile.
“Kwa uhuru huu mkubwa waliokuwanao
watu kwenye mwaka huu wa Sabato, utaratibu na mfumo wa
utoaji zaka uliwekwa huru kwa mtu kutoa ulimwachia mtu mwenyewe aamue kama anakitu kimpasacho kukitoa zaka ama la.
“Ni juu ya kila mmoja kuamua kile
anachoweza kukiweka wakfu na kukitenga mbali kama zaka
yake ya pili kwa mapato aliyoyapata katika miaka sita iliyotangulia nyuma yake
na kama bado kimesalia hadi kwenye mwaka huu wa Saba
ambao pia ni wa Sabato. Katika miaka hii mitakatifu ya Sabato, fedha zote zinazotolewa
Kanisani zinahesabiwa kama sadaka tu ya kawaida”
(Cox, “P”, op. cit., ukurasa wa 13,14).
“Mungu ameweka amri maalumu inayohusiana
na madeni na wadeni wetu na jinsi ya kusameheana
ufikapo Mwaka huu wa Sabato, sheria inayo julikana kama
ni ya “mwaka wa maachilio”
Imeandikwa kwamba:
Kumbukumbu la Torati 15:1-17 Kila miaka saba, mwisho wake,
fanya maachilio. 2 Na jinsi ya maachilio ni hii, kila
mkopeshaji na akiache alichomkopesha mwenziwe, wala asimlipize mwenziwe wala
nduguye; kwa kuwa imepigwa mbiu ya maachilio ya Bwana.
Tunatakiwa sote kusamehe madeni kwa wadeni wetu wote kwenye mwaka huu wa Sabato, hasa kama tutaombwa tuwasamehe.
3 Waweza kumtoza mgeni; lakini kila
uwiacho kwa nduguyo mkono wako utamwachilia. 4 Lakini hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa Bwana atakubarikia
kweli katika nchi akupayo Bwana,
Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;)
Hata hivyo, tutaendelea kuwadai madeni
yetu wale ambao hawapo kwenye imani moja nasi na ambao
sio wapendwa wenzetu.
5 kwamba utaisikiza tu kwa bidii sauti
ya Bwana, Mungu wako, uyatunze maagizo haya yote nikuagizayo leo, kuyafanya. 6 Kwani Bwana, Mungu wako,
atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini
hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao.
Torati ya Mungu inatukataza tusiende
kuwakopa mataifa wasio ndugu zetu wa imani moja. Hii
itakuwa hivyo hasa kwa ajili ya baraka alizotuahidia
kuwa atatupa kwa wingi, na kwa hiyo kamwe tusiwaendee na kuwakopa. Hata hivyo, tumeamriwa pia tusitoze riba wala faida yoyote
tunapokopesha. Mungu amesema kwenye Zaburi 15:5, kwa
hiyo ni kila mtu binafsi yake atasimama kwenye kutaniko la Bwana. Inasema: “Yeye
ambaye hautii mkono wake katika kutafuta faida kwa
riba, na wala hachukui zawadi dhidi ya asiye na hatia. Yeye
afanyaye hivyo hataondolewa kamwe.”
7 Kama akiwapo mtu
maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika
nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala
usimfumbie mkono wako nduguyo maskini; 8 lakini
mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika
ahitajiayo. 9 Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni
mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; jicho lako likawa
ovu juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi
kwako.
Iwapo kama
tutawaona watu wakiwa kwenye uhitaji tumeamriwa kuwakopesha. “Ikiwa kama mwaka wa Sabato umekaribia tumeonywa kwamba tusiifanye
migumu mioyo yetu kwa kutowakopesha ndugu zetu walio kwenye imani moja nasi.
10 Mpe kwa kweli, wala moyo wako
usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia Bwana, Mungu wako, kwa neno hili
katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako. 11 Kwa maana maskini hawatakoma katika
nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako
nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako. 12 Ikiwa nduguyo, mume wa Kiebrania, au
mwanamke wa Kiebrania, akiuzwa kwako, naye amekutumikia miaka sita; basi mwaka
wa saba mwache huru aondoke kwako.
Watu wa mataifa na Wayahudi wote
wanamiliki na kufanya shughuli za kibenki na wanaenda kinyume na sheria au amri
hii ya Mungu na kuitumia vibaya na kinyume amri hii inayohusu jinsi ya
kuwafanyia wajirani na Waebrania (aya ya1-11) na hii ni kinyume na utumwa (aya
ya 12). Mmonaki au mtawa wa Kiingereza alianzisha
mfumo huu kwa nia ya kuweka ili kusaidia vita. Lakini utaratibu huu inaenda
kinyume kabisa na sheria za Mungu na utakomeshwa
hatimaye kipindi cha Yubile atakayoianzisha Masihi katika kipindi cha utawala
wake (Cox, “P”, op. cit., ukurasa wa 14).
13 Nawe utakapomwacha huru aondoke
kwako, usimwache aende zake mikono mitupu; 14 umwangalie kwa wema katika kundi lako, na sakafu yako ya
nafaka, na kinu chako cha divai; mpe kama alivyokubarikia Bwana, Mungu wako. 15 Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa
katika nchi ya Misri, akakukomboa Bwana, Mungu wako; kwa hiyo mimi nakuamuru
neno hili hivi leo. 16 Hata
itakuwa, akikuambia, Siondoki kwako; kwa sababu akupenda wewe na nyumba yako,
kwa kuwa yu hali njema kwako; 17 ndipo
utwae uma, uupenyeze katika sikio lake uingie katika ubao wa mlango, naye
atakuwa mtumishi wako milele. Na kijakazi chako naye mfanye vivyo.
“kwa hiyo, tunaweza
kuwakopesha watu lakini sio kuwawekea riba. Ni vibaya sana kuwasababishia
watu wafilisike na kuwatoza riba watu binafsi au hata mataifa au kufanya aina
zozote za kujipatia faida kubwa kutoka kwao. Kwa hiyo tendo la kuyafutia madeni
mataifa yanayoendelea ni jema na la muhimu kwa kila
mtu au taifa linalodai wanaiamini Biblia.
Kila taifa linawajibika kujitawla na kujihudumia lenyewe kwa mujibu wa sheria za Mungu na
yanapaswa kujimudu kifedha yenyewe. Iwapo kama
yatashindwa kujimudu yenyewe, ndipo wanapojikuta yakiishi kaisha yasiyopaswa
kuwa hivyo kwao au maisha ya kitumwa.
Pia kuna masharti waliyopewa ndugu
zetu kutoka mataifa yote ambayo ni agizo la kujisaidia
wenyewe na sio kudumu wakiwoomba fedha ndugu zao wengine walio mahala pengine
kwa kufanya hivyo kila mara na pasipo kukoma. Hatutaweza kuwafanya watumwa watu
wetu kwa kuwatoza riba kwa ajili ya kuwapa wenzetu kwa
mtindo wa kuwafanya wenzetu kuwa watumwa. Kila mmoja wetu atahukumiwa kwa jinsi anavyowafanyia wenzake wengine, kwa namna zote
mbili yaani kama taifa na kama mtu binafsi.
Jinsi ulimwengu ulivyo kwa siku hizi kwa mfumo wake shirikishi ambao ni kama hauko sawa. Utaanguka na
kukoma kwa uzito wake wenyewe na mfumo wake mbaya uluojiwekea. Mungu ataruhusu
uanguke na ataurejesha upya. Ataurudisha upya kwa kuweka amri na sheria zake katika kipindi cha mwisho wa
mateso na misukosuko.
Pasipo kutoza riba na
kwa mujibu wa Torati ya Mungu tunaweza kupata utajiri na kuishi maisha ya kheri
kabisa. Tunapoishi kinyume na utaratibu ndipo
tunajifanyia maovu na dhambi. Sheria ya Mungu na
taratibu zake hufanya kazi kwa namna inayoonekana kama
ya kiamri na sio ya haki huria.”
http://www.ccg.org/_domain/ccg.org/Sabbath/2005/S_07_09_05.htm
Kutokana na Maandiko Matakatifu hapo chini tunaona kwamba kitendo cha
kukopesha fedha kwa nia ya kutoza riba kumekatazwa kwenye maandiko haya ya
Agano la Kale. Riba hii isichukuliwe kwa namna yoyote
ile ya utoaji wa fedha, kimsaada au mali ya mtu. “Riba ni kiasi cha fedha kinacholipwa pamoja na fedha iliyokopeshwa
(ni
kikanuni), au hutolewa kama kiasi kilichozidi
kutokana na deni lililotolewa” (kwa mujibu wa Kamusi maarufu ya Macquarie
ABC Dictionary).
Kutoka 22:25 "Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio
pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida.
Mambo ya
Walawi
35:36-37 Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe. 37 Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako
kwa kujitakia faida. .
Kumbukumbu la
Torati 23:19 "Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu cho
chote kikopeshwacho kwa riba;
Riba au faida
ya ziada huitwa tokos (kwa mujibu wa SGD 5110) na
imetumika mara mbili kwenye maandiko ya Agano la Kale, kitabu cha Mathayo 25:27
na Luka 19:23, kwenye mfano wa talanta.
Mathayo 25:27
basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo angu na faida
yake.
Ieleweke kuwa, Kristo hakuwa anabariki tendo hili la kudai faida ya ziada
au riba kwenye Maandiko haya Matakatifu. Maana aliyoikusudia Kristo kwa kutoa mfano huu ilikuwa ni kusisitizia juu ya Ufalme wa
Mungu na hakumaanisha masuala ya fedha.
Tendo la
kukopesha fedha ili upate kitu cha nyongeza ni riba
pia na wizi na Mungu amekataza matendo haya na ametangaza hukumu kwa wanaofanya
hivyo. Katika kipindi cha utawa;a wa Masihi, kila mtu anayekopesha fedha kwa
kufanya mambo haya ya riba atatiwa hukumuni na atafanywa alipe tena kama
atakavyoamriwa atakapohukumiwa kwa hukumu itakayochukuliwa kama wizi na utapeli
kulingana na Sheria. Pia soma jarida la Torati na Amri ya Nane (Na. 261) [Law and the Eighth Commandment (No. 261)].
Wakati Adamu na
Hawa walipotenda dhambi, sio tu kuwa walitolewa tu kutoka Bustani ya Edeni,
bali Mungu pia aliilaani ardhi ambayo waliishi ndani yake na kula kutokana
kwayo (Wanzo 3:17-18). Hata hivyo, ili kumlinda mwanadamu
na sayari hadi atakapokuja na kuirejeza upya Masihi yote kwa Mungu mwishoni mwa
miaka 7000, mfumo wa Yubile unaendelea kufanya kazi kwa faida ya sayari hii yote
tunapokuwa tunazifuata na kuzitii Amri za Mungu.
“Mfumo wote wa
Kalenda unatuama kwenye Yubile. Yubile moja ni mzunguko wa kipindi cha miaka
hamsini, am,bacho kinaonekana kwenye ujenzi wa Hekalu na
Kanisa lililo kwenye utaratibu wa Biblia. Inafanywa kwa
mizunguko sana
ambayo kila mmoja una miaka saba. Yubile huashiria mwelekeo wa
maisha ya mwanadamu na ukuaji wake wa miaka hamsini.
Mwaka wa
Yubile huesabiwa kutoka Siku ya Upatanisho ya mwaka wa Arobaini na tisa au
Yubile, wakati ardhi yote inarejeshwa kwa makabila ya wamiliki wake asilia. Thamani
yote ya ardhi huamuliwa kwa mtindo huu wa ulingano (Mambo
ya Walawi 25:15). Mwaka huu huadhimishwa na Yubile hupigiwa mbiu kwenye Siku ya
Upatanisho ya mwaka wa Arobaini na tisa (Mambo ya Walawi 25:8-9), na kisha
kuadhimishwa mtakatifu kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi kwenye Siku ya
Upatanisho ya mwaka wa Hamsini (Mambo ya Walawi 25:9-13), ili kwamba ardhi
ianze kulimwa tena na kupandwa kwa mavuno ya majira ya baridi ya mwezi wa Abibu
wa mwaka wa Kwanza wa Yubile inayofuatia. Mwaka huu (wa
50) ni wa nane kwa kufuata utaratibu wa mzunguko wa miaka ya kawaida (Mambo ya
Walawi 25:22) (Cox, W.E., “P”, op. cit., kurasa za 27, 28).
Kwa mujibu wa
kitabu cha fasiri cha (SHD 6944, kodesh) neno takatifu lina maana moja na linapaswa tendo la kula kile ambacho
kimekatazwa au kitu haramu kutoka kwenye maongeo ya mavuno ya tatu ya mwaka
uliopita wa Sabato na maongeo yaliyohifadhiwa ya mavuno.
“Mtazamo huohuo wa
kujitoa na kujiandaa kwa ajili ya kuutunza utaratibu wa Sabato umeenea hadi
kwenye kipindi chote kizima cha Yubile na kinaendelea hadi hata kwenye mavuno
makuu ya mwaka unaotangulia kabla ya Sabato ya saba ya Yubile. Katika mwaka ule, Mungu kuwabarikia watu wake mavuno maradufu
yatakayoweza kutosheleza kwa kipindi cha Miaka Miwili mitakatifu inayofuatia
mbele yake.”
Kwa maneno mengine, mavuno makuu mara
tatu yanavunwa katika mwaka wa Arobaini na nane wa
Yubile katika mwaka wa sita wa mzunguko wa mwisho ili kwamba miaka mingine
miwili ya Sabato na Yubile iweze kutumika pasipo kupungukiwa au kuwa ba uhitaji.
“Mchakato huu hutokea kwenye kila
mwaka wa saba wa mzunguko huu kwenye mwaka wa sita na
ndipo mavuno maradufu hutokea, lakini kwenye mwaka wa kabla ya maadhimisho ya
Yubile tunajionea mavuno makuu mara tatu kulingana na kawaida yake kama ilivyoahidiwa. Kwenye mwaka wa
Yubile, ambao hapa unaitwa na kujulikana kama
mwaka wa nane katika mzunguko, inaruhusiwa kupanda mbegu mashambani baada tu ya
kupita Siku ya Upatanisho tangu Pasaka ya mwaka wa tisa.
Mungu kuachilia baraka
za kimwili kwa Israeli wanapozitii amri zake. Ndivyo anavyowabarikia pia
Israeli wote wa kiroho wanaotembea kwenye njia zake kwa maarifa makuu na
kuelewa na kwa uweza wake katika Roho Mtakatofu” (Cox, “B”, op. cit., ukurasa wa
6).
Kila mmoja wetu ni
mali
ya Mungu (soma Mambo ya Walawi 11:2, 11,
21).
Kutoka 19:5 ' Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu
kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,
Walawi hawakupewa
ardhi ya kuimiliki katika Israeli. Ila
kulikuwa na miji na maeneo ya malisho ya wanyama iliyotengwa rasmi kwa kutumiwa
na Walawi, pamoja na zaka zote na baadhi ya sadaka au dhabihu zilizotolewa
walipewa wao.
Kumbukumbu la Torati 18:1-8 inasema:
"Makuhani Walawi, kabila yote ya Lawi, wasiwe na fungu wala urithi pamoja na Israeli; watakula sadaka za
Bwana zifanywazo kwa moto, na urithi wake. 2 Wala
wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.
3 Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao
sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na
tumbo. 4 Malimbuko ya nafaka zako, na divai yako,
na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, umpe. 5 Kwani
Bwana, Mungu wako, amemchagua katika kabila zako zote, asimame atumike kwa jina
la Bwana, yeye na wanawe milele. 6 Na akija Mlawi
atokaye katika malango yako mojawapo, katika Israeli yote alipokuwa akikaa,
akaja kwa mapenzi yote ya nafsi yake mahali atakapochagua Bwana; 7 na atumike kwa jina la Bwana, Mungu wake, kama wafanyavyo
ndugu zake wote, Walawi wasimamao huko mbele za Bwana. 8 Wawe
na fungu sawasawa la kula, pamoja na haya yaliyomfikilia kwa kuuzwa urithi wa
baba zake.
Binti za Selofehadi, aliyekufa bila
kuacha mtoto wa kiume, walifikiriwa kupewa milki yao na jina la baba yao
kwenye ukoo wake.
Hesabu 27:1-11 inasema: Wakati huo wakakaribia hao binti za Selofehadi, mwana wa
Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, wa jamaa za Manase
mwana wa Yusufu; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya; Mala, na Noa, na
Hogla, na Milka, na Tirsa. 2 Nao wakasimama mbele
ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya wakuu, na mkutano wote,
mlangoni pa hema ya kukutania, wakasema, 3 Babaetu
alikufa nyikani, naye hakuwamo katika mkutano wa hao waliojikutanisha kinyume
cha Bwana katika mkutano wa Kora; lakini akafa katika dhambi zake mwenyewe;
naye alikuwa hana wana wa kiume. 4 Kwa nini basi jina la
babaetu kufutwa katika jamaa zake kwa sababu alikuwa hana mwana wa kiume? Tupe
sisi urithi pamoja na ndugu zake babaetu. 5 Basi
Musa akaleta neno lao mbele ya Bwana 6 Bwana akanena na
Musa, na kumwambia, 7 Hao binti za
Selofehadi wananena lililo haki; kweli utawapa milki ya urithi pamoja na ndugu
za baba yao; nawe utawapa urithi wa baba yao. 8 Kisha
utanena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Mtu akifa, naye hana mwana wa kiume,
ndipo utampa binti yake urithi wake. 9 Tena ikiwa hana binti,
mtawapa nduguze urithi wake. 10 Na ikiwa hana ndugu,
mtawapa ndugu za babaye huo urithi wake. 11 Tena
ikiwa babaye hana ndugu, utampa huyo aliye karibu naye katika jamaa zake huo
urithi wake, naye atakuwa nao; na neno hili litakuwa ni amri ya hukumu kwa wana
wa Israeli, kama Bwana alivyomwagiza Musa.
Kama tuonavyo hapo juu, kutokana na jinsi Musa alivyomuuliza Bwana hukusu milki ya nchi
ulipaswa kubakia kwenye ukoo wa baba yake hadi kuwafikia mabinti zake. Waume
zao waliokuja baadae waliwachukua majina ya kike ya jamaa yao. Milki yao hii inategemea kwenye
mlolongo wa uzao wa jamii yao.
Mungu amemchukulia Israeli kama mtoto wazaliwa wake wa
kwanza (Kutoka 4:22). Kwa hiyo, wazaliwa wote wa
kwanza katika Israeli ni wake.
Kutoka 13:2 "Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila
afunguaye tumbo katika wana wa Israeli, wa binadamu na wa mnyama; ni wangu huyo"
Wazaliwa wa
kwanza walibidi kukombolewa. Wazaliwa wa kwanza wa
wanyama wa kufugwa pia walikombolewa kwa dhabihu ya mwana kondoo. Wanadamu
walitakaswa kwa Bwana kwa uhai wao wenyewe, na sio kwa
kuuawa (soma mfano wake kwenye kitabu cha Kutoka 13:13, hasa kwenye tafsiri ya The
NIV Study Bible, ukurasa wa 105).
Kutoka 13:13-22 Kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa
mwana-kondoo; na kwamba hutaki kumkomboa, utamvunja shingo; na kila mzaliwa wa
kwanza wa binadamu katika wanao utamkomboa. 14 Kisha
itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza keshoni, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia,
Bwana alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake; 15 basi ilikuwa hapo Farao alipojifanya kuwa mgumu ili
asitupe ruhusa kuondoka, Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote waliokuwa
katika nchi ya Misri, wa binadamu na wa mnyama; kwa ajili ya hayo namtolea
Bwana wote wafunguao tumbo, wakiwa waume; lakini wazaliwa wa kwanza wote wa
wana wangu nawakomboa. 16 Jambo hilo litakuwa ni
ishara mkononi mwako, na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa Bwana alitutoa
Misri kwa uwezo wa mkono wake. 17 Ilikuwa hapo Farao
alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi
ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije
wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri; 18 lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara
kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali
wamevaa silaha. 19 Musa akaichukua ile mifupa ya
Yusufu pamoja naye; maana, alikuwa amewaapisha sana wana wa Israeli, akisema,
Mungu hana budi atawajilia ninyi; nanyi mtaichukua mfupa yangu kutoka hapa
pamoja nanyi. 20 Nao wakasafiri kutoka Sukothi,
wakapiga kambi Ethamu, kwenye mpaka wa ile jangwa. 21 Bwana
naye akawatangulia mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo, ili awaongoze njia; na
usiku, ndani ya moto mfano wa nguzo, ili kuwapa nuru; wapate kusafiri mchana na
usiku; 22 ile nguzo ya wingu haikuondoka mchana, wala
ile nguzo ya moto haikuondoka usiku, mbele ya hao watu.
Mwana mzaliwa wa
kwanza wa kiume au mkubwa kuliko wote alipewa urithi mara dufu ya mali
zote zinazorithishwa.
Kumbukumbu la Torati 21:17 lakini amkubali mzaliwa wa kwanza
mwana wa yule asiyempenda, kwa kumpa mafungu mawili katika vyote alivyo navyo;
kwa maana ndiye mwanzo wa nguvu zake; haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.
Nabii Ezekieli anaonyesha urithi
milki wa ardhi. Urithi wa
familia umelindwa kwa utaratibu huu wa Yubile na hakuna atakayeweza
kunyang’anywa au kudhulumiwa mali
zake.
Ezekieli 46:16-18 "Bwana MUNGU asema hivi; Mkuu akimpa mwanawe awaye yote
zawadi, ni urithi wake, itakuwa mali ya wanawe; ni milki yao kwa kurithiwa. 17 Bali
akimpa mmoja wa watumishi wake baadhi ya urithi wake, itakuwa mali yake mpaka
mwaka wa kuacha huru; ndipo itakapomrudia mkuu; lakini urithi wake, huo utakuwa
wa wanawe. 18 Tena mkuu hatawaondolea watu urithi wao,
hata kuwatoa kwa nguvu katika milki yao; atawapa wanawe urithi katika mali yake
mwenyewe, watu wangu wasije wakatawanyika, kila mtu mbali na milki yake”
Tunakumbushwa kuwa kuna adhabu kubwa
imewekwa kwa kuivunja na kupuuzia kuiadhimisha Yubile.
Yeremia 34:17 Basi Bwana asema hivi, Hamkunisikiliza kumtangazia uhuru
kila mtu ndugu yake, na kila mtu jirani yake; tazama, mimi nawatangazieni
uhuru, asema Bwana, yaani, wa upanga, na njaa, na tauni; nami nitawatoa ninyi
mtupwe huko na huko katika falme zote za dunia.
Kama tunavyojionea hapo juu utaratibu wa umiliki unaotuama kwenye Yubile unalinda vizazi vyetu
kwenye safu ya uzao wetu. Hata hivyo, kaswali mapya yanajitokeza kutoka kwenye
hesabu ya binti za (walioitwa ili wamiliki ardhi ya baba yao, kama tunavyoona
kwenye kitabu cha Hesabu 27:1-11), kama ni kitu gani kingepaswa kutokea kwenye ardhi ya jamii yao kama wangeolewa na watu wa makabila
mengine.
Hesabu 36:1-4 Kisha wale wakuu wa nyumba za mababa ya jamaa ya wana wa
Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, katika jamaa za wana wa Yusufu, wakakaribia,
na kunena mbele ya Musa, na mbele ya wakuu walio juu ya nyumba za mababa ya
wana wa Israeli; 2 wakasema, Bwana alimwagiza bwana wangu
awape wana wa Israeli nchi kwa kupiga kura iwe urithi wao; tena bwana wangu
aliagizwa na Bwana awape binti za Selofehadi ndugu yetu huo urithi wa baba yao.
3 Wakiolewa na watu wa wana wa hizo kabila nyingine za wana
wa Israeli, ndipo urithi wao utatwaliwa na kuondolewa katika urithi wa baba
zetu, na hiyo kabila watakayotiwa ndani yake itaongezewa urithi wao; basi
urithi huo utaondolewa katika kura ya urithi wetu. 4 Tena
itakapokuwapo hiyo yubile ya wana wa Israeli, ndipo urithi wa hiyo kabila
ambayo wamekuwa ndani yake utaongezewa huo urithi wao; hivyo urithi wao
utaondolewa katika urithi wa kabila ya baba zetu."
Uamuzi ulikuwa ni
kwamba kila binti aliyepata irithi kutoka kwenye kabila la baba yake alipaswa
kuolewa na mtu kutoka kwenye kabila lake
hilohilo ili kwamba
familia na kabila viweze kulindwa.
Hesabu 36:5-9 Basi Musa akawaagiza wana wa
Israeli kama neno la Bwana lilivyokuwa,
akasema, Kabila ya wana wa Yusufu imenena yaliyo haki. 6 Bwana
ameagiza neno hili katika habari ya binti za Selofehadi, akasema, Na waolewe na
waume wawapendao; lakini na waolewe katika jamaa ya kabila ya baba zao. 7 Hivyo hapana urithi wo wote wa wana wa Israeli utakaotoka
kabila hii kwenda kabila hii; kwa kuwa wana wa Israeli watashikamana kila mtu
na urithi wa kabila ya baba zake. 8 Na kila binti
atakayemiliki urithi katika kabila yo yote katika wana wa Israeli, ataolewa
katika jamaa moja ya kabila ya baba yake, ili wana wa Israeli wapate kumiliki
kila mtu urithi wa baba zake. 9 Hivyo hapatakuwa na
urithi uwao wote utakaotoka kabila hii kwenda kabila hii; kwa kuwa kabila za
wana wa Israeli zitashikamana kila mmoja na urithi wake mwenyewe.'"
Binti hawa wa
Selofeadi walikubali na kutii kama Bwana
alivyowaamuru, na milki zao aikabakia kwenye jamaa ya baba zao.
Hesabu 36:10-12 Basi hao binti za Selofehadi
wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Musa; 11 kwa
kuwa Mala, na Tirsa, na Hogla, na Milka, na Noa, binti za Selofehadi waliolewa
na waume, wana wa ndugu za baba yao. 12 Waliolewa katika
jamaa za wana wa Manase, mwana wa Yusufu, na urithi wao ukakaa katika kabila ya
jamaa ya baba yao.
Mungu aliahidi kwamba mtu fulani kwenye ukoo wa jamaa zao wa Rekabu hadi wa Yonahabu ndio
watasimama kila mara mbele zake.
Yeremia 35:16-18 Basi, kwa kuwa wana wa Yonadabu, mwana wa Rekabu,
wameitimiza amri ya baba yao aliyowaamuru, lakini watu hawa hawakunisikiliza
mimi; 17 kwa sababu hiyo, asema Bwana, Mungu wa
majeshi, Mungu wa Israeli; Tazama nitaleta juu ya Yuda, na juu ya wenyeji wote
wa Yerusalemu, mabaya yote niliyoyatamka juu yao; kwa sababu nimesema nao,
wasinisikilize; nimewaita, wala hawakuniitikia. 18 Naye
Yeremia akawaambia watu wa nyumba ya Warekabi, Bwana wa majeshi, Mungu wa
Israeli, asema hivi, Kwa sababu mmeitii amri ya Yonadabu, baba yenu, na
kuyashika maagizo yake yote, na kutenda sawasawa na yote aliyowaamuru; basi,
kwa sababu hiyo, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Yonadabu,
mwana wa Rekabu, hatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu hata milele"
Ukoo wa
familia hii utabakia kwa kuwa walifuata amri ya baba yao. Watoto wetu watapokea faida ya muda
mrefu kutokana na jinsi tunavyozitii amri za Baba yetu
wa Mbinguni, na hakuna hata moja ya amri zake zitakazoweza kukomeshwa au
kutanguliwa.
Mathayo 5:18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi
zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote
yatimie.
Mpango wote mzima haujakamilika bado na amri hii itabakia imekamilika. Sadaka au dhabihu
iliyokubalika ya Masihi haikutangua torati bali imefungua
awamu nyingine ya Mpango huu na kuwaruhusu Mataifa wasio Wayahudi kupata fursa
ya kuingia kwenye mpango wa Roho mtakatifu wa kufanywa wana na kufanywa kuuwa
ni Israeli wa kiroho.
Wana wa Rekabu
waliotii amri za baba yao
walifanywa kuwa mfano wa watu wa Yuda waliomuasi Mungu.
Yeremia 35:12-15 Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia, kusema, 13 Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Enenda
ukawaambie wana wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, Je! Hamtaki kupokea
mafundisho, myasikilize maneno yangu? Asema Bwana. 14 Maneno
ya Yonadabu, mwana wa Rekabu, aliyowaamuru wanawe, kwamba wasinywe divai,
yametimizwa, na hata leo hawanywi; maana waitii hiyo amri ya baba yao; lakini
mimi nimesema nanyi, nikiamka mapema na kunena, bali ninyi hamkunisikiliza
mimi. 15 Pia naliwapeleka watumishi wangu wote,
manabii, kwenu ninyi, nikiamka mapema na kuwapeleka, nikisema, Rudini sasa,
kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiwafuate
miungu mingine, ili kuwatumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi
na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza.
Jinsi ya Kuthaminisha Mali
Iwapo kama
mtu ataiweka wakfu nyumba yake kwa Bwana, thamani yoyote ambayo kuhani ataiweka
ndiyo itakayodumu na kubakia hivyo. Na inwapo kama mtu atapenda kuikomboa ndipo mtu huyo
atalazimika kuongeza sehemu ya tano (20%) kutoka kwenye thamani iliyowekwa na
nyuma hiyo itabakia tena kuwa yake (Mambo ya Walawi 27:14-15).
Mambo ya Walawi 27:14-15 "Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa Bwana ndipo kuhani
ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama
kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa. 15 Tena
mtu huyo aliyeweka nyumba yake iwe wakfu kama akitaka kuikomboa, ndipo
atakapoongeza sehemu ya tano ya hiyo fedha ya hesabu yako, nayo itakuwa mali
yake
Nyumba zilizojengwa kwenye miji yenye
maboma huwa ni milki ya kudumu ya mnunuzi na wazao
wake. Hazirudishwi kwa mwenyewe unapofika mwaka wa
Yubile. Lakini nyumba zinazojengwa vijiji visivyozungushiwa na
boma yanahusika na sheria inavyosema kuhusu mwaka wa Yubile. (mfano ni inavyoelekezwa kwenye Mambo ya
Walawi 25:29-31 hapa chini).
Mambo ya Walawi 25:9-55 inasema:
Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya
kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho
mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. 10 Na
mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote
kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila mtu atairudia
milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake. 11 Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande
mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za
mizabibu isiyopelewa. 12 Kwa kuwa ni yubile;
utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani. 13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake. 14 Tena kama ukimwuzia jirani yako cho chote, au kununua
cho chote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe; 15 kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo
utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo
atakavyokuuzia wewe. 16 Kama hesabu ya miaka
ilivyo ni nyingi ndivyo utakavyoongeza bei yake, na kama hesabu ya miaka ilivyo
ni chache ndivyo utakavyopunguza bei yake; kwani yeye akuuzia mavuno kama
hesabu yake ilivyo. 17 Wala msidanganyane;
lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 18 Kwa sababu hii zitendeni amri zangu, mkazishike hukumu
zangu, na kuzifanya; nanyi mtakaa katika hiyo nchi salama. 19 Nayo
nchi itazaa matunda yake, nanyi mtakula na kushiba, na kuketi humo salama. 20 Na kama mkisema, Je! Mwaka wa saba tutakula nini?
Angalieni hatutapanda mbegu, wala kukusanya maongeo yetu; 21 ndipo
nitawaamria baraka yangu iwe juu yenu mwaka wa sita, nayo utazaa matunda hesabu
ya miaka mitatu. 22 Na mwaka wa nane mtapanda mbegu, na
kuyala yale matunda, akiba hiyo ya zamani, hata mwaka wa kenda, hata matunda
yake yatakapoletwa ndani, mtakula hiyo akiba ya zamani. 23 Nayo
nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni
na wasafiri wangu. 24 Nanyi mtatoa
ukombozi kwa ajili ya nchi, katika nchi yote ya milki yenu. 25 Kwamba
nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye
karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye. 26 Na
kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo
ya kutosha kuikomboa; 27 ndipo na aihesabu
hiyo miaka ya kuuzwa kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua;
naye atairejea milki yake. 28 Lakini asipoweza
kujipatia mwenyewe, ndipo hiyo iliyouzwa itakaa mkononi mwake huyo aliyeinunua,
hata mwaka wa yubile; na katika yubile itatoka, naye atairejea milki yake. 29 Tena kwamba mtu anauza nyumba ya kukaa, iliyo ndani ya
mji wenye kuta, ndipo ana ruhusa kuikomboa katika mwaka mmoja mzima baada ya
kuiuza; atakuwa na amri ya kuikomboa muda wa mwaka mzima. 30 Na
kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani
ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi
vyake; nayo haitatoka katika yubile. 31 Lakini nyumba za
vijiji, ambavyo havikuzingirwa na kuta, zitahesabiwa pamoja na mashamba ya
nchi; nazo zina ruhusa ya kukombolewa, nazo zitatoka katika yubile. 32 Pamoja na hayo, miji ya Walawi, nyumba za miji ya milki
yao, Walawi wana ruhusa ya kuzikomboa majira yo yote. 33 Tena
kama mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa, ndipo nyumba iliyouzwa, na mji wa milki
yake, itatoka katika yubile; maana, hizo nyumba za miji ya Walawi ni milki yao
kati ya wana wa Israeli. 34 Lakini konde la
malisho ya miji yao lisiuzwe kwa kuwa ni milki yao ya daima. 35 Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake
umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri. 36 Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili
ndugu yako akae nawe. 37 Usimpe fedha yako
upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida. 38 Mimi
ndimi Bwana, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya
Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu. 39 Tena kwamba nduguyo
amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimtumikishe mfano wa mtumwa; 40 kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au
mfano wa msafiri; naye atatumika kwako hata mwaka wa yubile; 41 ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe
pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba
zake. 42 Kwa kuwa hao ni watumishi wangu,
niliowaleta watoke nchi ya Misri; wasiuzwe mfano wa watumwa. 43 Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako. 44 Tena katika habari za watumwa wako na wajakazi wako,
utakaokuwa nao; mataifa walio kando-kando yenu, katika hao mtanunua watumwa na
wajakazi. 45 Tena katika wana wa wageni wakaao kati
yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika
nchi yenu; wao watakuwa milki yenu. 46 Nanyi mtawafanya
kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa
watumwa wenu katika hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana
wa Israeli, wenyewe kwa wenyewe. 47 Tena kama mgeni au
mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza
kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni; 48 baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni
mwa ndugu zake ana ruhusa kumkomboa; 49 au mjomba wake, au
mwana wa mjomba wake, ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu awaye yote aliye karibu
naye wa jamaa yake, ana ruhusa ya kumkomboa; au kwamba yeye mwenyewe amepata
mali, ana ruhusa ya kujikomboa mwenyewe. 50 Naye
atafanya hesabu na huyo aliyemnunua, tangu mwaka huo aliojiuza hata mwaka wa
yubile; na ile bei ya kuuzwa kwake itakuwa kama hesabu ya hiyo miaka ilivyo;
atakuwa pamoja naye kama majira ya mtumishi aliyeajiriwa yalivyo. 51 Kwamba ikali imesalia miaka mingi, kama hesabu yake
ilivyo ndivyo atakavyolipa bei ya ukombozi wake, katika hiyo fedha ambayo
alinunuliwa kwayo. 52 Tena kwamba imesalia
miaka michache tu hata mwaka wa yubile, ndipo atafanya hesabu naye, kama hesabu
ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi wake. 53 Kama mtumishi aliyeajiriwa mwaka hata mwaka, ndivyo
atakavyokuwa pamoja naye; asitawale juu yake kwa nguvu mbele ya macho yako. 54 Tena kwamba hakukombolewa kwa njia hizi mojawapo, ndipo
atatoka katika mwaka wa yubile, yeye, na watoto wake pamoja naye. 55 Kwa kuwa wana wa Israeli ni watumishi; ni watumishi
wangu niliowaleta watoke katika nchi ya Misri; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Kuna sehemu mbili zenye maandiko
yanayoielezea Yubile na ambayo yanaweza kuchukuliwa
sawa na yale waliyoyaeleza kina Ezra na Nehemia tunapowaona nukuu za jinsi
walivyoisoma Torati. Nukuu moja inatoka kwenye Agano la Kale na
lingine ni utimilifu wa unabii ulitolewa kwenye Agano la Kale kwenye Agano
Jipya unaomlenga Masihi.
Nukuu ya
maandiko ya Agano la Kale iko kwenye Ezekieli 1:1-3.
Ezekieli 1:1-3 inasema: Ikawa katika mwaka wa thelathini,
mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa pamoja na watu waliohamishwa,
karibu na mto Kebari, mbingu zilifunuka, nikaona maono ya Mungu. 2 Siku ya tano ya mwezi, nao ulikuwa ni mwaka wa tano wa
kuhamishwa kwake mfalme Yehoyakini, 3 neno la Bwana
lilimjia Ezekielii, kuhani, mwana wa Buzi, kwa dhahiri, katika nchi ya Wakaldayo,
karibu na mto Kebari; na mkono wa Bwana ulikuwa hapo juu yake.
Kwa hiyo basi, tunapolingakisha na
majenzi na marejesho mapya yaliyoonekana nyakati za nabii Ezekieli ya Yubile
yalikuwa ni yale yaliyoangukia mwaka wa 574/3 na pia yale ya mwaka 524/3, na tena
mwaka 74/3 na 24/3 kwenye karne za nyakati za Kabla ya Kuzaliwa Kristo (BCE), na
27/28 na 77/78 kwenya kipindi cha nyakti hizi. Mtazamo huu unapata mashiko kwa kusaidiwa na ukweli mwingine mkuu wa unabii unaomhusisha
Masihi.
Baada ya kutangulia miaka kumi na tano ya kufawala kwake Mfalme Tiberio, ambao haukuwa
mapema sana na
mwaka wa kidunia na tarehe ya Oktoba, 27 BK, Yohana Mbatizaji alianza kuhubiri
na kuwabatiza watu ubatizowa toba (Luka 3:1-22). Ndipo Roho Mtakatifu alimwita
Yesu kutoka Nazareti ili akabatizwe na Yohana kipindi fulani na kitambo baada
ya Yohana kuanza huduma yake, au kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa tangu
mwezi Oktoba ya mwaka wa 27 BK. Mara tu baada ya Kristo kubatizwa ndipo
aliongozwa na Roho kwenda nyikani ambako alijaribiwa na Ibilisi kwa siku
arobaini (Luka 4:1-2). Baada ya kurudi kwake maana na
ilieleweka kidogo maana ya unabii kuhusu yeye kuwa unakamilika.
Luka 4:13-21 inasema: Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda
zake kwa muda. 14 Yesu
akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi
zote za kandokando. 15 Naye alikuwa
akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote. 16 Akaenda
Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama
ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17 Akapewa
chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta
kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa
kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu
wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 Akaanza
kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.
Kisha, Masihi alirudi Galilaya kutoka
kwenye majaribu yake, na kufika mjini Nazareti akiwa
ametimiliza unabii alioutoa Mungu kupitia kwa nabii Isaya. Andiko hili
linapatikana kwenye Isaya 61:1-2 na linapatikana tena
kwenye Isaya 58:6.
Isaya 61:1-2 "Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa
sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma
ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao
waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza
mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote
waliao;”
Kwa hiyo, tendo alilolifanya la ‘Kusoma
maandiko kutoka gombo la nabii Isaya’ alililolifanya lilifanyika katika mwaka
wa Yubile, ambalo lilienda sambamba na kipindi alichotabiri nabii Ezekieli, na fasiri ,aarufu ya Biblia inayoitwa Naves Topical Bible inayaelezea maandiko haya kuwa yamehusiana
kabisa na tukio la Yubile (sawa na alivoandika kwenye kitabu chake cha Yubile, ukurasa wa 755). Huu pia ulikuwa Mwaka wa Maachilio wa watu kusamehewa na
kuwa huru (sawa na Ezekieli 46:17). Kwa hiyo, ndio Kristo alipoitangaza Yubile
ya mwaka 27 BK, mapema kabla haujaja mwaka mpya na
siku ya 1 Nisan. Andiko hili kuhusu Masihi linabakia kuwa ni
ushahidi usiopingika wa pili kutoka kwenye Ezekieli, na linathibitisha
ufafanuzi wake wa majira yaliyoandikwa kwenye gombo la Nehemia linaloelezea
yanayojiri kwenye mfumo na taratibu za Sabato na Yubile” (Cox, “R”, op. cit., ukurasa wa 3).
“Yubile hutokea kwenye miaka ya 24 na 74 KK na 27 na 77 BK ya kila karne. Yubile iliyofuatia
ambayo ni Yubile ya arobaini tangu kuanza kwa huduma ya Masihi na Yubile ya
arobaini na nane tangu kujengwa upya kwa Hekalu na majeresho mapya ya usomaji wa
Torati yaliyofanywa na kina Ezra na Nehemia, yatafanyika mnamo Mwaka Mtakatifu
wa 2027/8. Mwaka 2028 utakuwa ni mwanzo wa kipindi cha Yubile ya Yubile na cha
Milenia mpya ya utawala wa Masihi na ambao utakuwa pia ni mwaka wa kwanza wa
miaka mingine hamsihi, yaani 1/50” (Cox,
“I”, op. cit., ukurasa wa 28).
Yubile ya Dhahabu
“Tangu Siku ya Upatanisho ya mwaka wa 2027 dunia itakuwa imeishaingia kwenye kipindi chake cha
milki ya Milenia ya nchi yote. Tendo hili litatanguliwa na
maadhimisho ya Yubile ya Dhahabu, au huitwa pia Yubile ya Yubile.
Ifikapo siku ya Kumi ya mwezi wa Saba ya mwaka wa 49 ya Yubile ya 120, au Jumapili ya
tarehe 20 Septemba 2026, kuanzia jua linapozama na kupisha giza ya siku iliyotangulia, ndipo mwaka wa
Yubile utaanza. Kwa kipindi cha mwaka huu, mataifa yatapangwa upya na kuwekwa sawa na milki zao stahiki. Kwenye Siku ya
Upatanisho ya mwaka wa Hamsini wa Yubile ya 120, mbiu
ya Yubile itapigwa, na ifikapo siku ya 23 ya mwaka wa Saba,
inayofuatia mara tu baada ya Siku Kuu ya Mkutano wa Makini mwishoni mwa Sikukuu
ya Vibanda, ndipo marejesho ya ardhi kwa wamiliki wake asili yatafanyika. Watu
wote watarejeshewa ardhi au mashamba yao.
Ndipo wataanza kulima na kupanda kwa mavuno ya kwanza kuvunwa kipindi hiki cha
Milenia kwenye Pasaka ya mwaka 2028. Mavuno makuu yatakayovunwa kwenye
Ukanda-dunia wa pande za Kusini (Southern Hemisphere) itakuwa
imefanyizwa upya na kufuata majira yake na mavuno yake. Ukanda-dunia wa Pande za Kaskazini (Northern Hemisphere) utakuwa umeharibiwa
vibaya sana kwa
ajili ya vita vilivyopiganwa. Itabidi Dunia ifanywe upya
tangu mwaka 2028 hadi 2077. Kipindi hiki kitashuhudiwa
kikipitwa na mabadiliko makubwa yatakayobadili mitazamo yote na mwenendo wa
ongezeko la watu duniani” (Cox. W.E., “S” jarida la Yubile ya Dhahabu na
Milenia (Na. 300) [The Golden Jubilee and the Millennium (No. 300)], CCG, 2006, kurasa
za 4-5).
Utendaji sahihi wa
mwaka huu wa mfumo huu wa kibiblia wa aina zote mbili, yaani wa kutoa zaka na
sheria unategemea na kwendana na Yubile. Mfumo huu unaoenda pamoja na usomaji kiusahihi na makini wa Torati. Kwa hiyo, tuna
agizo endelevu na lisilokoma la kuiheshimu na
kuyashika maagizo ya Torati, amri ambayo haitakoma wala kutanguka, wala
kubadilika (Mathayo 5:18; Luka 16:17). Torati hii ya Mungu inatangulia kutoka
kwenye asili na hali asilia ya Mungu na itadumu kuwa hivyo
milele, kama Mungu alivyo na sifa ya tabia ya
kutobadilika.
1Yohna 5:3
Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike
amri zake; wala amri zake si nzito.
Pia soma jarida la Uhusiano kati ya Dhana ya Wokovu kwa Neema na Torati (Na. 82) [The Relationship between Salvation by Grace and the Law (No.
82)].
Kuba baraka
na laana zinazoweza kuwapata Israeli wote kwa jinsi watakavyoamua kati ya
kuzitunza ama kuacha kuzitunza amri hizi za Mungu. Imeandikwa hivyo kwenye
Kumbukumbu la Torati 28:1-68, tendo la kuzishika amri hizi ni
jambo lililowazi sana
kwamba linaonyesha jinsi mtu anastahili kusaidiwa au kukataliwa na Mungu. Hata
hivyo, kuziasi amri za Mungu hupekelea adhabu kwa wote
wawili, yaani kwa mtu binafsi na kwa taifa na kwa wote.
Laana
itamuandama mtu anayeasi maagizo yaliyoandikwa kwenye Torati hii ya Mungu. Mungu
huyafanyia mataifa ka hali sawa na jinsi
anavyozifanyia familia. Mataifa yahoo pia huadhibiwa, yakifanika kuwa ni Wenyeji wanaowatumikisha au kuwafanyia watu kwa namna
isiyo sawa. Amri hizi zote na sheria zake zinapaswa
kuheshimiwa. Adhabu ya kutofanya hivyo ni jambo
endelevu lisilo na mwisho kwa wale wote wanaoziasi, jambo linaloonekana kwenye
maongeo ya ardhi. Taifa lnafanyiwa sawa kama
wanavyofanyiwa watu. Watu watakumbwa na baa la njaa. Mambo
yanavyokuwa hapa duniani yanauhusiano mkubwa na sheria
na amri za Mungu.
Baraka na
laana ni ishara na dalili za jinsi Israeli walivyo na zitabakia kuwa hivyo milele. Tunavyosema Israeli tunawajumuisha
pia wale watu wa kiroho; kwa hiyo baraka na laana zitabakia
zikiwa hivyo milele kwa wale wanaoliitia jina la Yesu Kristo na kuingia
hukumuni. Kwa hiyo, kuna ahadi waliyopewa Israeli kwenye mambo yao yote somo hili hutolewa ili kutufanya
tujionee hatari yote itokanayo na kukosa kwetu na tunavyoshindwa kuwafanyia
vizuri watu wetu . soma jarida la Baraka na Laana (Na. 75) [The
Blessings and the Curses (No. 75)].
“Sabato zitakuwa zinaadhimishwa na
wote wenye mwili wakati watakapokuwa wanajihudhurisha kwenye ibada mbele za
Bwana, kwa Mwandamo mmoja wa mwezi hadi mwingine na toka Sabato moja hadi ile nyingine
(Isaya 66:23)” (Cox, “A”, op. cit., ukurasa wa
5).
Isaya 66:18-23 inasema: "Nami nayajua
matendo yao na mawazo yao; wakati unakuja
nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu
wangu. 19 Nami nitaweka ishara kati yao, nami
nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao
upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari
yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa. 20 Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa
sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya
nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema
Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika
chombo safi. 21 Na baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani
na Walawi, asema Bwana. 22 Kama vile mbingu
mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo
uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 23 Na itakuwa, mwezi
mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu
mbele zangu, asema Bwana.
“Marejesho haya mapya ya Sabato na Miandamo ya Mwezi yataendana na marejesho mapya ya
maadhimisho ya Sikukuu hizi zilizoamriwa na Mungu.
Zekaria 14:16-19 Hata itakuwa, ya kwamba kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Yerusalemu, atakwea
mwaka baada ya mwaka ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, na kuishika
sikukuu ya Vibanda. 17 Tena itakuwa, ya kwamba mtu awaye yote wa jamaa zote
zilizomo duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa
majeshi, mvua haitanyesha kwao. 18 Na kama jamaa ya
Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako tauni, ambayo
Bwana atawapiga mataifa, wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda. 19 Hii ndiyo adhabu ya Misri, na adhabu ya mataifa yote, wasiokwea ili
kushika sikukuu ya Vibanda.
“Kwa hiyo, kutakuwa na marejesho mapya yaliyo kamili hadi pale maadhimisho ya
Miandamo ya Mwezi yatakayofanywa panoja na maadhimisho ya Sikukuu. Kwenye
jumuia hii ya kisasa, jambo hili huonekana kuwa ni
gumu sana. Na
ndiyo maana Masihi ataushusha chini utaratibu wote huu wa
kidunia wakati atakapokuja. Mataifa yatafanywa upya kwa sheria za Torati
zitakazoamriwa kutoka mjini Yerusalemu” (Cox, “F”, op. cit., ukurasa wa
9). .
************
Bibliography/Tulikotohoa:
Christian Churches of God, Statement of Beliefs of the Christian Faith (No. A1), CCG, 1994-1997
Cox, W.E., “A”, The Sabbath (No. 31), CCG, 1994-2008
Cox, W.E., “B”, The Juna’ah: Preparing for the Sabbath (No. 285),
CCG, 1999-2008
Cox, W.E., “C”, The Role of the Fourth Commandment in the Historical
Sabbath-keeping Churches of God (No. 170), CCG,
1996-2000
Cox, W.E., “D”, The Covenant of God (No. 152), CCG,
1996-1999
McElwain, T., et.al.,
“E”, Blue Ribbons (No. 273), CCG, 1998
Cox, W.E., “F”, The New Moons (No. 125), CCG. 1995-2007
Cox, W.E., “G”, The New Moons of Israel (No. 132), CCG,
1995-2008
Cox, W.E., “H”, The Harvests of God, the New Moon Sacrifices, and the 144,000
(No. 120), CCG, 1995-2007
Cox, W.E., “I”, God’s Calendar (No. 156), CCG,
1996-2008
Cox, W.E., “J”, The Lord’s Supper (No. 103), CCG,
1995-2008
Cox, W.E., “K”, The Passover (No. 98), CCG, 1995-2008
Cox, W.E., “L”, The Wave Sheaf Offering (No. 106b)
Cox, W.E, “M”, Keeping the Feasts (No. 56), CCG, 1994-2007
Cox, W.E., “N”, The Holy Days of God (No. 97), CCG,
1995-2007
Cox, W.E., “O”, Offering (No. 275), CCG, 2006
Cox, W.E., “P”, Tithing (No. 161), CCG, 1996-2007
Cox, W.E., “Q”, Reading the Law with Ezra and Nehemiah (No. 250)
Cox, W.E., “R”, The Meaning of Ezekiel’s Vision (No. 108)
Cox, W.E.,”S”, The Golden Jubilee and the Millennium (No. 300), CCG,
1996-2008
Cox, S., The Shofar and the Silver Trumpets (No. 47), CCG, 2003
Cox, W.E., Atonement (No. 138), CCG,
1994-2007
Cox, W.E., Eternal Life (No. 133), CCG, 1995,
2000
Cox, W.E., General Distribution of the Sabbath-keeping Churches (No.
122), CCG,
1995-1999
Cox, W.E., God's
Feasts as they relate to the Creation (No. 227), CCG, 1998, 2007 (based on a paper by A. Williams, 1997)
Cox, W.E., Ingathering
(No. 139), CCG, 1994-1999,
2007
Cox, W.E., Law and the Eighth Commandment (No. 261),
CCG, 1998, 1999
Cox, W.E., Outline Timetable of the Age (No. 272), CCG, 1998,
2002, 2006
Cox, W.E., Reading the Law with Ezra and Nehemiah (No. 250), CCG, 1998,
2007
Cox, W.E.,
Repentance and Baptism (No. 52), CCG, 1994,
1998, 2007
Cox, W.E., Sanctification of the Temple of God (No. 241), CCG, 1998,
2000, 2007
Cox, W.E., Significance of the Bread and Wine (No. 100),
CCG, 1995-2007
Cox, W.E., The Blessings and the Curses (No. 75), CCG, 1994-2007
Cox, W.E., The First Great Commandment (No. 252), CCG, 1998, 1999
Cox, W.E., The God We Worship (No. 2), CCG, 1994,1998
Cox, W.E., The Food Laws (No. 15),
CCG, 1994-2008
Cox, W.E., The Omer Count to Pentecost (No. 173),
CCG, 1996-2009
Cox, W.E., The Relationship between Salvation by Grace and the Law (No.
82), CCG, 1994-2007
Cox, W.E., Trumpets (No. 136), CCG, 1994-2007
Johnson, B., Significance of the Footwashing (No. 99),
CCG, 1995, (ed. Cox. W.E., 1999, 2007)
Kohn, Dr. S., Die Sabbatharier in
Siebenburgen, Budapest,
1894, tr. McElwain, T., & Rook, B., Intro. Cox, W.E., CCG Publishing, 1998
Sabbath Message: http://www.ccg.org/_domain/ccg.org/Sabbath/2005/S_07_09_05.htm
Early Jewish
Writings: http://www.earlyjewishwritings.com/text/philo/book28.html
Judaeus Philo, The Special Laws, II, XXVI, 140, F.H. Colson, Harvard University Press, Cambridge MA,
1937
The NIV Study
Bible, Zondervan Bible Publishers, MI, USA, 1985