Makanisa ya kikristo ya
Mungu
[257]
Amri Kuu ya
Pili
(Chapisho La 3.0
19981008-19990526-20070228-20120804)
Amri hii Kuu ya Pili inafanana na ile ya
Email: secretary@ccg.org
(Hakimiliki ©
1998, 1999, 2007, 2012 Wade Cox)
(tr. 2012)
Masomo
yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na
kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu
Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote
kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org
Amri Kuu ya
Pili
[jarida
hili linatakiwa lisomwe kabla ya kulifafanua ile ya Tano na ambayo ni Amri
nyingine zinazofuatia.]
Mungu
alimpa Musa utaratibu wa Torati kwenye maandiko yaliyo
kwenye Kutoka 20. Amri Kumi ziligawanyika katika amri kuu mbili kama tulivyoona kwenye tathimini ya Amri Kuu Kwanza (soma
jarida la Amri
Kuu ya
Kutoka 20:1-17 Mungu
akanena maneno haya yote akasema, 2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri,
katika nyumba ya utumwa.
[I] 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
[II] 4
Usijifanyie sanamu ya
kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu
mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana,
Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata
kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 nami
nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
[III] 7 Usilitaje
bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu
alitajaye jina
[IV] 8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa..
[V] 12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
[VI] 13 Usiue.
[VII] 14 Usizini.
[VIII] 15 Usiibe.
[IX] 16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
[X] 17Usiitamani nyumba ya jirani yako,
usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala
mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho
jirani yako.
Mgawanyo wa sheria za Torati kwa sehemu mbili za Amri Kuu ulifanywa baadae na Kumbukumbu la Torati. Muundo wake umeonyeshwa kwa wazi sana, kwa kuzifanya zile amri nne za kwanza zihusike na kuonyesha kwetu upendo wetu kwa Mungu, na zile sita za mwisho zihusike na upendo wetu kwa wengine au majirani zetu. Kwa hiyo sheria hizi zilifungamanishwa kwa utaratibu ulio muhimu na dhahiri.
Wajibu wetu ni kwa Mungu na pia kwa wanadamu wenzetu. Wajibu wet uni kuwa tunaofaa na wenye mapokeo mema kwa Mungu wetu aliye Hai. Yeye ni Mungu wa waliohai na sio wa wafu.
Mathayo 22:29-40 inasema: Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa
hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. 30 Kwa
maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni. 31 Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno
lililonenwa na Mungu, akisema, 32 Mimi ni Mungu wa
Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali
wa walio hai. 33 Na makutano waliposikia, walishangaa kwa
mafunzo yake. 34 Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba
amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja. 35 Mmoja
wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu; 36 Mwalimu,
katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, Mpende
Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako
zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya
kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii,
Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40 Katika amri hizi
mbili hutegemea torati yote na manabii.
Sehemu ya kwanza ya torati
inashughulika na upendo wetu kwa Mungu. Inatakiwa
tufanye hivyo kwa mioyo yetu yote na kwa akili zetu
zote na kwa roho zetu zote. Sehemu ya pili ni kumpenda
jirani yetu,
1Yohana 4:20-21 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni
mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu
ambaye hakumwona. 21 Na amri hii tumepewa
na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
Muundo wa
Amri Kuu ya
Amri Kuu ya Pili imetokana na amri sita zilizo kwenye zile Amri Kumi. Ni katika tendo letu la kuziua kiroho kwa hii Amri Kuu ya Pili ambapo tunaonyesha uwezekano kwa sisi kuingia hukumuni kwa kiwango kikubwa cha mambo ya Sheia au Torati.
Muundo wa hii
ya Pili unatokana na mlolongo huo huo wa kufikiri mambo ya msingi yanayotokana
na Amri Kuu ya
[V] 12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
Amri ya Pili ina ahadi inayohusiana na mpango wa maisha ya kimilele ya elohim. Ilipaswa kuwa hivyo tangu mwanzo.
[VI] 13
Usiue.
Tendo la
kuua linatokana na dhambi na hamu ya kujionea
uharibifu wa kuharibu viumbe vingine. Mawazo haya yanatoka kwa
adui na nshitaki wetu ibilisi. Si mpango wa Mungu
kumfanya kiumbe yeyote aangamie, kwa kuwa wataokolewa wote kwa wakati wake
muafaka, hata Malaika zake. Kwa kuwa upendo wa Mungu
ni mkamilifu na hana upendeleo (soma jarida la Kondoo Aliyepotea na Mwana
Mpotevu (Na. 199) {Lost Sheep and the Prodigal Son (No. 199)].
[VII] 14 Usizini.
Tendo la kulinda maadili ya familia na
uaminifu wa umoja ni ashirio au mwonekano asilia wa tabia ya uadilifu na
uaminifu ya Mungu. Ndoa ni mfano ashirio wa uhusiano
kati ya Kristo na Kanisa. Hatuwezi kuivunja moja bila ya
kuiathiri nyingine. Uhusiano wowote ambao unaingilia maadili ya familia,
kupunguza wajibu na mamlaka ya mume nay a mwanamke, ni
uzinifu na yanaathiri na kuhatarisha kwa kuendeleza fikra potofu za kiuzinzi
kwa mwanamke. Mwanaume ni kuhani kwenye nyumba yake
hasa akiwa
Ukubwa wa
dini hizi au itikadi ya maisha ya useja kwa makasisi vinaonekana kuwa haviwezi
kuwafanya kuokoka mbali na matendo haya.
[VIII] 15 Usiibe.
Mambo ya mtu binafsi yake yanaonyesha kwenye muundo wa Torati,
[IX] 16 Usimshuhudie jirani yako uongo.
Mfumo mzima wote wa mambo ya haki
unatuama kwenye kweli. Mfumo wote wa mpango wa wokovu unaweza
kuwa salama tu iwapo
[X] 17Usiitamani nyumba ya jirani yako,
usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala
mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho
jirani yako.
Mambo ya kiroho yanayoihusu Totati yameorodheshwa kwenye mambo haya yaliyoandikwa kwenye Amri Kumi, ambayo kwamba namna zote za kujaribu kuzivunja ni matokeo ya mawazo ya kibinadamu na ni kuivunja Torati hii yote. Ni kwa kuyazuia majaribu tu yatokanayo na mawazo kunaweza kutufanya tujifunza kikweli kumpenda mwenzako na kupendana sisi sote kwa roho na kweli.
1Wakorintho 13:1-13 inasema: Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo,
nimekuwa
Ukamilifu wa Sheria au Torati ni upendo na kuhudumiana. Torati yenyewe imewekwa kwa nia ya kumlinda mtu na mambo yaliyo kwenye taratibu za kidunia au za kimwili, wakti Roho Mtakatifu ameletwa ili kuhudumia yale yaliyo kwenye mlolongo wa kiroho. Roho Mtakatifu ni wa muhimu ili tuweze kuifuata vema na kikamilifu Sheria ya Kamilifu ya Uhuru.
Sheria Kamilifu ya Mungu ya Uhuru
imewekwa ili kutuwezesha sisi tuwe kwenye mahusiano
kamilifu nay eye na kwa kila mmoja wetu. Kwa hiyo, amri ile ya sita na nyingine zote zinazofuatia zinaelekea kwenye mwisho huu,
na kwamba sisi tupendane sote na tumpende jirani yetu
q