Makanisa ya kikristo ya Mungu

[258]

 

 

 

Torati na Amri ya Tano

(Toleo La 2.0 19981008-19990526-20120522)

 

Imeandikwa: Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. Amri hii ya Tano ni amri ya kwanza yenye ahadi na ambayo inaweka msingi mkubwa kwenye jamii zetu. Ni chanzo cha kwanza kwa muundo wa baraka wa amri zote unaopelekea kuipa mashiko na kujulikana kuwa ni Amri Kuu Kuliko Zote. Kama tukimpenda jirani yetu kama tunavyojipenda wenyewe.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hatimiliki © 1998, 1999, 2012  Wade Cox)

(tr. 2012)

 

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

 


Torati na Amri ya Tano

 


Amri hii ya Tano imeandikwa kwenye Kutoka 20 na Kumbukumbu la Torati 5.

Kutoka 20:12 Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

 

Kumbukumbu la Torati 5:16 Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

 

Amri hii ya Tano ni amri pekee nay a kwanza yenye ahadi. Ni amri ya kwanza au ni kiini cha amri zote na hufungamanisha na ile Amri Kuu na ya Pili inayotuamuru kumpenda jirani kama tunavyojioenda sisi.

Mathayo 19:18-19 Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, 19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Kama hilivyo amri nyingine zote, amri hii imesisitizwa pia kwenye Agano Jipya.

Waefeso 6:1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.

 

Wakolosai 3:20: Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.

 

Familia kama kiini cha jamii

Uumbaji ulitegemezwa kwenye mfumo wa kifamilia kwenye Bustani ya Edeni (soma jarida la Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya 1, Bustani ya Edeni (Na. 246) [The Doctrine of Original Sin Part I The Garden of Eden (No. 246)] na Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemu ya 2, Kizazi cha Adamu (Na. 248) [The Doctrine of Original Sin Part 2 The Generations of Adam (No. 248)]. Familia hutengeneza tofali lililo kiini cha jengo la kwenye jamii zetu. Familia ya kibinadamu ilianzishwa na Mungu, na ilikusudiwa iongezeke na kuendeleza hali ya kufanyika kuwa mfano wa Mungu, na kufanyika kuwa ni hekalu la Mungu (sawa na Mwanzo 1:27-30; Mwanzo 2:7,18).

 

Baba ni nguzo ya nyumba kama alivyo mama pia. Anawajibu ulio sawa na wajibu mkubwa kwa utendaji wa milele wa familia, kama tunavyoona kwenye Mithali 31:10-31. babaanawajibu pia kwa utendaji kazi na mwenendo mzima wa familia kama inavyohusiana na jamii. Kusugi la lile linalosemwa kwenye Mithali 31 ni kuonysha utendaji kazi ulio laini na mpangilio wa familia na jamii, na kama inavyohusiana kwenye utaratibu wa kiroho wa Kanisa. Na kama mama alivyo kwa baba na ndivyo pia Kanisa linapotakiwa kuwa kwa Karisto na ndivyo wote kwa Mungu (soma jarida la Mithali 31 (Na. 114) [Proverbs 31 (No. 114)].

 

Familia pia ina wajibu mpana kwa mujibu wa sheria, ambayo haitakiwi kudharauliwa au kuchukuliwa ki juu juu tu na ki wepesi. Kwa ajili hii alama ya mtumwa ni kitu kilicho kwenye jamii, inaonyeshwa kwa alama ya mwewe anayeruka hewani (Kutoka 21:6). Kwa jinsi hiyohiyo, kiongozi wa nyumba hubeba wajibu mkubwa kwa mujibu wa sheria (Kutoka 22:8). Kwa ajili hii, tunaendelea kuwa ni watoto wa Mungu aliye Juu na wana wa Mungu. Haijaandikwa kuwa “Je, sikusema kuwa ninyi ni miungu?” …wana wa Aliye Juu ninyi nyote” na Maandiko hayawezi kutanguka (sawa na Zaburi 82:1-6; Yohana 10:35).

Zaburi 82:1-6: Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu. 2 Hata lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya? 3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara; 4 Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu. 5 Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika. 6 Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.

 

Utaratibu na mfumo mzima wote ni kwa familia ya wana wa Mungu, ya aina zote mbili yaani kiroho na kimwili.

 

Viumbe wote humtegemea mwanadamu kama ilivyo familia, kwenye mpango wa Mungu (Mwanzo 1:28). Na ndivyo ulivyo utaratibu wa familia, na kama ilivyo kwenye familia ya Mungu.

1Petro 3:1-7: Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. 6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote. 7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

 

Kuwaasi wazazi kuna ahadi yake pia.

Mithali 30:17: Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila.

 

Familia hufanyika kuwa kiini cha kwanza kaeika jamii. Jamii kama utaratibu imeonyeshwa kwenye familia, kwa njia ya neema na inaonekana kuwa Mungu alitupeleka tukiwa na sura na tabia zake, kwa mwana wake tumjuaye ambaye ni Yesu Kristo.

Tito 2:1-15: 1 Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima; 2 ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi. 3 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; 4 ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; 5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe. 6 Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi; 7 katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, 8 na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu. 9 Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu, 10 wasiwe waibaji; bali wauonyeshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu katika mambo yote. 11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; 14 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema. 15 Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.

 

Kwa ajili hii wazazi wanatakiwa kujiangalia na kuwapa watoto wao na kuwaandalia hatima yao ya mbele yao na sio kuyarudia yale yaliyokwisha pita nyuma.

2Wakorintho 12:14: Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto.

 

Kwa jinsi hii, kuna mzaliwa wa kwanza mmoja tu mwenye stahili ya kurithi kwenye familia, jambo ambalo halitegemei na idadi ya wake waliopo kuwa ni wangapi (Kumbukumbu la Torati 21:15-17).

Kumbukumbu la Torati 21:15-17: Akiwa mtu yuna wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa; 16 ndipo itakapokuwa ya kwamba siku atakayowarithisha wanawe alivyo navyo, asimweke mwana wa ampendaye kuwa mzaliwa wa kwanza mbele ya mwana wa asiyempenda, naye ndiye mzaliwa wa kwanza huyu; 17 lakini amkubali mzaliwa wa kwanza mwana wa yule asiyempenda, kwa kumpa mafungu mawili katika vyote alivyo navyo; kwa maana ndiye mwanzo wa nguvu zake; haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.  

 

Watoto wanawajibu pia kwa wazazi wao ambao kama wakikosea adhabu yao ni kifo (Kumbukumbu la Torati 21:18-21). Adhabu hii ya kifo huhusika kwa wazazi, na kisha kwenye hali ambayo inawahusu wazee, na inaendelea kwa hali mtambuka hadi kuwafikia watu wengine.

Kumbukumbu la Torati 21:18-23: Mtu akiwa na mwana mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikizi, 19 ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake; 20 wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni mwasherati, tena ni mlevi. 21 Waume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa. 22 Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti; 23 mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku iyo hiyo; kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije ukatia unajisi katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi wako.

 

Tunaona sasa kwamba msingi wa jamii ni familia na familia ni tofali la jengo la taifa. Nidhamu ya jamii inategemea na familia ikiwa kama chanzo msingi zha kwanza, na haki ya kuadhibu na kuchukua uhai inategemeana na jinsi familia ilivyo. Wazazi wetu walitupa maisha kwa jinsi ya ndoa na uzazi, kwa hiyo tendo la kushiriki au ushiriki kwenye uzazi hutokana na uweza wa Mungu Mwenyezi.

 

Amri inayotutaka kuwa watakatifu

Kwa kuwa familia inafanya kazi kwa njia za kawaida, wajibu wa kazi ya Mungu ni wa kiroho. Tuna Baba yetu mmoja tu.

Malaki 2:10: Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu?

 

Mungu ametuumba sisi na kwa mapenzi yake tunaishi na tumeumbwa.

Ufunuo 5:8-10: Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. 9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, 10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

 

Kumbuka jinsi maandiko yanavyosema kuwa “watatawala hapa duniani.”

 

Yeye anayetakasa na yule anayetakaswa wana wana chanzo kimoja.

Waebrania 2:11: Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;

 

Hatupaswi kumuita mtu yeyote baba, kwa kuwa baba yetu ni Mungu peke yake na aliyeko mbinguni, naye ndiye Mungu wetu na Baba yetu naye ndiye Baba Mungu na Baba wa Yesu Kristo aliyemtuma.

Mathayo 23:9: Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.

 

Yeye ndiye pekee anayepaswa kuwa mlengwa kwenye kujitoa kwetu na kwenye maombi yetu.

Mathayo 6:1-15 inasema: Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. 3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; 4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. 9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, 10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupe leo riziki yetu. 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. 13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.] 14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

 

Uhusiano na Baba Mungu ni jambo muhimu na la kwanza, lakini ni kwa Amri ile Kuu nay a Kwanza tunagundua umuhimu wa Amri Kuu nay a Kwanza, inayoelezea upendo wa Mungu. Kwa hiyo unaweza kuwa mtakatifu na kila unachokifanya kitakuwa kitakatifu, kutoka kile unachokula na unachokifanya au kukizalisha.

Kutoka 22:31: Nanyi mtakuwa watu watakatifu kwangu mimi; kwa hiyo msiile nyama yo yote iliyoraruliwa huko kondeni na mnyama wa mwitu; mtawatupia mbwa nyama hiyo.

 

Mambo ya Walawi 11:44 Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi.

 

Mtu binafsi ni mtakatifu na hapaswi kunajisika, kwa kuwa ilikuwa ni Mungu ndiye aliyetuokoa na kutufanya kuwa watakatifu.

Mambo ya Walawi 11:45 Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.  

 

Mambo ya Walawi 20:26: Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu

 

Kusudi la kuumbwa kwa mwanadamu

 

Familia takatifu

Kama Israeli ilivyotakatifu, na ndivyo familia ilivyo ni takatifu. Taifa ni la Mungu, na ufalme umewekwa kwa Kristo aliye wa uzao wa Daudi, ufalme utakaodumu milele. Sisi ni watu wa nyumbani mwa familia moja, na familia ile inatawaliwa na waamuzi walio kwenye nyumba ya Daudi, ambayo ni ya Masihi nay a ukuhani wa Melkizedeki. Kwa kuwa mfalme wangu ni mtakatifu (Melkzedeki) au Bwana wangu ni mtakatifu (Adonizedeki) ni cheo cha kumtukuza mfalme wa milele wa Yerusalemu (sawa na zinavyosema Mwanzo 14:18; Zaburi 110:4; Yoshua 10:1; na pia G. Vermes, kitabu chake cha kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza cha The Dead Sea Scrolls in English [(Gombo la Kiingereza lililopatikana kwenye Bahari Mfu) linalomwelezea Melchizedek na maana yake)].

2Samweli 7:10-16: Tena nitawaagizia mahali watu wangu Israeli, nami nitawapanda, wapate kukaa mahali pao wenyewe, wasiondolewe tena; wala wana wa uovu hawatawatesa tena, kama hapo kwanza; 11 naam, kama vilivyokuwa tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi, wawe juu ya watu wangu Israeli; nami nitakustarehesha mbele ya adui zako wote. Tena Bwana anakuambia ya kwamba Bwana atakujengea nyumba. 12 Nawe siku zako zitakapotimia, ukalala na baba zako, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufalme wake. 13 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara milele. 14 Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu;
15 lakini fadhili zangu hazitamwondoka, kama vile nilivyomwondolea Sauli, niliyemwondoa mbele yako. 16 Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara milele.

 

Kwa hiyo Masihi amepewa cheo cha ubaba kwa wana wa wanadamu walio wana wa Mungu.

Isaya 9:6-7  Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. 7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.

 

Ataitwa mwana wa Mungu.

Luka 1:32-35: 31 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. 34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? 35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

 

Kwa yeye, haki imewekwa kwa familia ya wanadamu (Isaya 11:4, 5) kama sehemu ya uzao wa Ibrahimu (Wagalatia 3:6, 9). Yeye ndoye aliyechaguliwa kuwa mrithi wa vitu vyote na aliyetumwa aongee na wanadamu (Waebrania 1:1,2) na inathibitisha kudumu kwa kiapo (Waebrania 6:17). Ikiwa ni kwa imani ndivyo tulivyoonywa na Mungu kupitia kwa Nuhu wa kizazi cha Kwanza, kwa kuitumikia nyumba ya Mungu, na kwa Mwana kwenye kizazi cha Pili cha Adamu, na kwa imani tunayafuata mashauri yake (Waebrania 11:7). Kama sisi tu mali ya Kristo kwa njia ya imani, basi sisi tu wa uzao wa Ibrahimu na warithi kwa mujibu wa ahadi (Wagalatia 3:16, 29), tukiwa pia ni wana wa Adamu na ni wana wa Munbu (Luka 3:38).

 

Kwa Adamu wa kwanza tuchukua taswira ya kidunia, na kwa Adamu wa pili tunachukua taswira ya kimbinguni.

1Wakorintho 15:45-49: Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. 46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. 47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. 48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. 49 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.

(sawa na Mathayo 28:18,19; Ezekieli 21:27)

 

Familia yake ni familia yetu kwa kuwa tunayafanya mapenzi ya Mungu (Yohana 19:25-27). Kwa hiyo, familia ina viwango viwili ambavyo ni vya familia ya kidunia na vya kimbinguni.

Mathayo 12:46-50: Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye.
47 Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. 48 Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? 49 Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! 50 Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.

 

Kwa hiyo, sisi sio wana wa mwanamke mtumwa bali ni wana wa uzao wa kweli na kwa hiyo sisi ni warithi (Wanzo 21:10; 25:1-6). Tofauti hii ni ya mstari wa wana walio kwenye imani, katika urithi wa Mungu, uolioainishwa kwenye sheria, ikiwa ni utofautidhaji na yule asiye mwaminifu.

Mambo ya Walawi 25:45-46: Tena katika wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu. 46 Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumwa wenu katika hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana wa Israeli, wenyewe kwa wenyewe.

 

Kwa hiyo uanzishaji wa taifa lionekanalo huanzia kwenye masuala ya kiroho, na utofautishaji wake umefanywa ili kuonyesha kuwa ni kwa njia ya wokovu peke yake na kuingia kwa taifa ndipo watu wote watakuwa kwenye milki ya uzima wa milele.

 

Ili tuweze kuonekana kuwa tunaliweza hilo kwenye pikindi cha mafunzo kimewekwa na Masihi na ukuhani wake mpya (kama inavyosema Ufunuo 20:1-9). Katika siku ile tutakuwa kama miunngu (elohim) kama Malaika wa Yahova vichani mwetu Zekaria 12:8). Na uzao wake utakuwa wa milele (Zaburi 89:4).

Zekaria 12:8: Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao

 

Kufuatiwa na ufufuo wa pili na kipindi cha kuwafundisha viumbe wote (Isaya 65:20), ndipo sisi sote kwa kila mmoja na viume wote tutakwenda mbele kuelekea kwenye hatima yetu. Na ndipo Mungu hatimaye atafanyika kuwa wote ndani ya yote na katika yote, nasi tutakuwa ni mahala pa makao ya Mungu, tukiwa kama Hekalu la Mungu milele.

Waefeso 4:6: Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.

 

Haya ni matukio ya mwisho ya vile Mungu anavyokwenda kuwa (Kutoka 3:14).

 

Utakaso na usafishaji

Kwenye mchakato huu tunapaswa kutakaswa na kuwa safi. Kuns smri ya muhimu inayoelezea jambi hili, ambayo inahusisha usafi wa watu na sayari na mazingira.

 

Amri inayohusu vyakula inapatikana kwenye Mambo ya Walawi 11:1-47 na Kumbukumbu la Torati 14:1-21 (soma jarida la Sheria ya Vyakula (Na. 15) [The Food Laws (No. 15)].

 

Taifa na watu walitakaswa na kutenga mbali ili kwamba Mungu awatembelee. Hata hivyo, kwa taifa la kimwili linaloonekana, aliweka viapo na kuongea nao kwa kupitia malaika wa Yahova. Kanmuni hizi zimeorodheshwa kwenye kitabu cha Kutoka 19:10-25,

Andiko kamili ambalo tunaweza kulisoma katika mwaka wa saba. Sheria hizi zinaelezea jinsi Mungu anavyoweza kufanya kazi kupitia taifa na kupitia Kanisa. Sheria hii hapo mwanzoni walipewa watu sabini na hatimaye kwa taifa. Watu walitakaswa kwanza na mchakato wa utakaso unafanywa na Kanisa na taifa kwa mwelekeo wa kila mwaka ulianzia Siku ya Kwanza ya Mwaka Mtakatifu. Na inaendelea hadi siku ya Saba ya mwezi wa Kwanza, ambako utakaso kwa ajili ya dhambi zilizofanywa pasipo kujua au kwa kupotoshwa hutubiwa na watu hujitakasa nazo (soma jarida la Utakaso wa Hekalu la Mungu (Na. 241) [The Sanctification of the Temple of God (No. 241)] na Sikukuu za Mungu na zinavyohusiana na Uumbaji (Na. 227) [God’s Feasts as they relate to the Creation (No. 227)]. Tofauti hii ilifanywa ili kulionyesha taifa kuwa kulikuwa na mchakato wa kutofautisha ambao kwao wangemeendea Mungu. Mahisi amefanya mchakato huo mahala pa Kanisa kwa njia ya ubatizo wa Roho Mtakatifu.

 

Kwa hiyo, utakaso ni sehemu ya mchakato unaomfanya mtu kuwa mtakatifu na mwenye kukubalika katika kumuishia Mungu aliye hai.

Mambo ya Walawi 20:7: Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

 

Kuweka ka mamlaka

Mungu ameweka malmaka yake hapa dunia kwa kupitia viongozi wake aliowawachagua na kuwaweka. Mungu aliongea na watu kwa kupitia watumishi wake waliosimama kati yake na wanadamu ambao walikuwa ni manabii (Amosi 3:7). Tendo hili lilifanyika kwa mwelekeo endelevu wa mamlaka yaliyotoka kwa manabii wa Mungu na kuwaendela viongozi wa mataifa.

Kutoka 4:11-23 inasema: Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana? 12 Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena. 13 Akasema, Ee Bwana, nakuomba, tuma kwa mkono wake huyo utakayemtuma. 14 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Musa, akasema, Je! Hayuko Haruni, ndugu yako, Mlawi? Najua ya kuwa yeye aweza kusema vizuri. Pamoja na hayo, tazama, anakuja kukulaki; naye atakapokuona, atafurahi moyoni mwake. 15 Nawe utasema naye, na kuyatia maneno kinywani mwake; nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na pamoja na kinywa chake, na kuwafundisheni mtakayofanya. 16 Naye atakuwa msemaji wako kwa watu, hata yeye atakuwa mfano wa kinywa kwako, nawe utakuwa mfano wa Mungu kwake. 17 Nawe utatwaa fimbo hii mkononi mwako, na kwa hiyo utazifanya zile ishara. 18 Basi Musa akaenda na kurejea kwa Yethro mkwewe, na kumwambia, Nipe ruhusa niende, nakusihi, niwarudie hao ndugu zangu walioko Misri, nipate kuwaona kwamba wako hai hata sasa. Yethro akamwambia Musa, Haya, nenda kwa amani. 19 Bwana akamwambia Musa huko Midiani, Haya, nenda, karudi Misri; kwa kuwa wale watu wote waliokutaka uhai wako wamekwisha kufa. 20 Basi Musa akamchukua mkewe na wanawe, na kuwapandisha juu ya punda, naye akarudi mpaka nchi ya Misri; na Musa akaichukua ile fimbo ya Mungu mkononi mwake. 21 Bwana akamwambia Musa, Hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; lakini nitaufanya mgumu moyo wake, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao. 22 Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu; 23 nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako.

 

Mungu ndiye aliyekuwa anawachagua na kuwaweka viongozi katika Israeli.

Hesabu 27:12-23 inasema: Bwana akamwambia Musa, Panda wewe juu ya mlima huu wa Abarimu, uitazame nchi niliyowapa wana wa Israeli. 13 Na ukiisha kuiona, wewe nawe utakusanyika pamoja na baba zako, kama Haruni ndugu yako alivyokusanyika; 14 kwa sababu mliasi juu ya neno langu katika jangwa la Sini wakati wa mateto ya mkutano, wala hamkunistahi, hapo majini, mbele ya macho yao. (Maji hayo ndiyo maji ya Meriba ya Kadeshi katika jangwa la Sini.) 15 Musa akanena na Bwana akisema, 16 Bwana, Mungu wa roho za wenye mwili wote, na aweke mtu juu ya mkutano, 17 atakayetoka mbele yao, na kuingia mbele yao; atakayewaongoza watokapo, na kuwaleta ndani; ili mkutano wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji. 18 Bwana akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu mwenye roho ndani yake, ukamwekee mkono wako; 19 kisha ukamweke mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wote; ukampe mausia mbele ya macho yao. 20 Nawe utaweka juu yake sehemu ya heshima yako, ili mkutano wote wa wana wa Israeli wapate kutii. 21 Naye atasimama mbele ya Eleazari kuhani, naye atamwulizia kwa hukumu ya ile Urimu mbele za Bwana; kwa neno lake watatoka, na kwa neno lake wataingia; yeye na wana wa Israeli wote pamoja naye, mkutano wote pia. 22 Musa akafanya kama Bwana alivyomwamuru; akamtwaa Yoshua, akamweka mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wote; 23 kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama Bwana alivyosema kwa mkono wa Musa.  

 

Kwa hiyo, uchaguzi uliofanywa na makuhani wakitumia Urimu na Thumimu, ulisimama kuwa kama ni ushauri thibitisho tu wa Bwana katika kumthibisha Kiongozi wateule wa Israeli. Kiongozi huyu akiwa kama mfalme alithitishwa kwa mujibu wa desturi na taratibu za mataifa. Kristo na sio mwanadamu ni mfalme, ingawa Mungu amefanya kazi zake zote kwa mujibu wa sheria au torati.

Kumbukumbu la Torati 17:14-20 inasema: Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, itaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kando-kando yangu; 15 usiache kumweka yule atakayechaguliwa na Bwana, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako. 16 Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa Bwana amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile. 17 Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno. 18 Tena na iwe, zamani aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika chuo, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi; 19 na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya; 20 moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kuume wala wa kushoto; ili apate kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya Israeli.

 

Ni mtu yule tu aliye wa kabila la Israeli ndiye atawatawala Israeli. Mfalme anafungiwa kwenye maongozi ya torati au sheria za Mungu na kwenye maelekezo yote yaliyoagizwa kwenye torati.

 

Agano la kufanya tohara liliwahusu Israeli na manabii walilijua hili kuwa ni kama mfano wa maumivu yaliyotokana na maisha yao venant.

Kutoka 4:25-28: Ndipo Sipora akashika jiwe gumu na kuikata govi ya zunga la mwanawe, na kuibwaga miguuni pake akasema. Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi. 26 Basi akamwacha. Ndipo huyo mkewe akanena, U bwana arusi wa damu wewe, kwa ajili ya kutahiri. 27 Bwana akamwambia Haruni, Nenda jangwani uonane na Musa. Naye akaenda, akamkuta katika mlima wa Mungu, akambusu. 28 Musa akamwambia Haruni hayo maneno yote ya Bwana ambayo alimtuma aende nayo, na ishara hizo zote alizomwagiza.

 

Agano la tohara lililenga kwenye agano la mioyo yao kwa Roho Mtakatifu, na kwa hiyo tohara haikuwa kitu muhimu kwa watu wa mataifa wanapokuwa wanaongoka. Musa alikuwa ni mtu mwenye ulimi usio tohara (Kutoka 6:30) lakini aliponywa na kufanyika kuwa elohim kwa Farao (Kutoka 7:1; pia soma jarida la Torati na Amri ya Kwanza (Na. 253) [Law and the First Commandment (No 253)] na Torati na Amri ya Pili (Na. 254) [Law and the Second Commandment (No. 254)].

 

Tendo hili la kuwatahiri watoto wa familia zao alilopewa Ibrahimu na likaanzisha tena na kuedelezwa na Musa na Yoshua (soma Yoshua 5:8; Yohana 7:22) zinazoelezea kuhusu kutahiriwa kwa njia ya Roho Mtakatifu na wajibu wa wateule (soma Matendo 7:8; 10:45-11:2). Wamataifa waliambiwa haikuwa lazima kwao kutahiriwa wanapoingia kwenye mkutano wa Israeli kwa Roho Mtakatifu. Kwa kuwa kwa amri kuu twaweza kusema kwamba sio kila alyetahiriwa alikuwa Muisraeli na sio kila asiyetahiriwa alitengwa mbali na agano hili la Ubaba na Mungu wa Israeli.

Kutoka 12:49: Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini.

 

Wakati ule Musa alipowakusanya wazee wa Israeli na Musa na Haruni akasema nao (Kutoka 4:29-31).

Kutoka 4:29-31: Musa na Haruni wakaenda, wakawakusanya wazee wote wa watu wa Israeli. 30 Haruni akawaambia maneno yote Bwana aliyonena na Musa akazifanya zile ishara mbele ya watu. 31 Watu wakaamini, na waliposikia ya kuwa Bwana amewajilia wana wa Israeli, na ya kuwa ameyaona mateso yao, wakainama vichwa vyao wakasujudu.  

 

Mamlaka ya taifa ndiyo njia ambayo Mungu alishughulika nayo pia katika kuieneza na kuweka utaratibu wa familia.

Hesabu 12:1-16 inasema: Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. 2 Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao. 3 Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. 4 Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. 5 Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. 6 Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto. 7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; 8 Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? 9 Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake. 10 Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma. 11 Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi. 12 Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake. 13 Musa akamlilia Bwana, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana. 14 Bwana akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena. 15 Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena. 16 Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga kambi katika nyika ya Parani.

 

Jukumu la kuweka na kuyatendea kazi mzmlaka ni la Mungu. Ndiyo maana inanenwa kamba uasi ni sawa na dhambi ya uchawi, kwa kuwa tendo hili la kuasi linaanzisha nia ya moyo wa mtu ya kupingana na mapenzi ya Mungu na ni matokeo ya mtu kuwa mwabudu miungu wengi (soma 1Samweli 15:23).

 

Kazi ya mamlaka

Hata watiwa mafuta wa Mungu waliwajibika kuzitunza sheria hizi zilizo kwenye amri ya tano na jinnsi zinavyohusiana na familia na ndoa. Wazazi wa Musa pia waliwajibika kuzitunza hivyo hivyo. Kwa hiyo, busara kubwa itokea kwa kuhani na nabii mwingine. Kwenye kitabu cha Kutoka 18 tunaona kwamba Musa alikuwa amewamini mke wake na wanawe na mkwa wake mzee Yethro aliyekuwa kuhani wa Midiani, akairudisha familia ya Musa na kuwapa ushauri wa jinsi ya kuwahukumu Israeli na utaratibu wake wa kuwapatia watu haki zao na jinsi ya utawala.

Kutoka 18:1-27 inasema: Basi Yethro, kuhani wa Midiani, mkwewe Musa, alisikia habari ya mambo hayo yote Mungu aliyokuwa amemtendea Musa, na Waisraeli watu wake, jinsi Bwana alivyowaleta Israeli watoke Misri. 2 Ndipo Yethro mkwewe Musa akamtwaa Sipora, mke wa Musa, baada ya yeye kumrudisha, 3 pamoja na wanawe wawili; katika hao, jina la mmoja ni Gershomu, maana alisema, Mimi nimekuwa mgeni katika nchi ya ugenini; 4 na jina la wa pili ni Eliezeri, kwa kuwa alisema, Yeye Mungu wa baba yangu alikuwa msaada wangu, akaniokoa na upanga wa Farao. 5 Basi Yethro, mkwewe Musa, pamoja na mke wa Musa na wanawe wawili wakamwendea Musa huko nyikani, hapo alipokuwa amepanga, kwenye mlima wa Mungu; 6 naye akamwambia Musa, Mimi Yethro mkweo nimekuja kwako, na mkeo, na wanawe wawili pamoja naye. 7 Basi Musa akatoka nje ili amlaki mkwewe, akasujudia na kumbusu; nao wakaulizana habari; kisha wakaingia hemani. 8 Musa akamwambia mkwewe mambo hayo yote Bwana aliyomtenda Farao na Wamisri kwa ajili ya Israeli, na mambo mazito yote yaliyowapata njiani, na jinsi Bwana alivyowaokoa. 9 Yethro alifurahi kwa ajili ya wema wote Bwana aliowatendea Israeli, kwa alivyo waokoa mikononi mwa Wamisri. 10 Kisha Yethro akasema, Na ahimidiwe Bwana aliyewaokoa na mikono ya Wamisri, na mkono wa Farao; aliyewaokoa watu hao watoke mikononi mwa Wamisri. 11 Sasa najua ya kuwa Bwana ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa unyeti. 12 Yethro mkwewe Musa akamletea Mungu sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; na Haruni akaja, na wazee wote wa Israeli, wale chakula pamoja na mkwewe Musa mbele za Mungu. 13 Asubuhi yake Musa akaketi ili awapishie hukumu watu; na hao watu wakasimama kumzunguka Musa tangu asubuhi hata jioni. 14 Mkwewe Musa alipoyaona yote aliyowafanyia watu, akasema, Ni jambo gani hili uwatendealo hao watu? Kwani wewe kuketi hapo peke yako, na watu wote kusimama kwako tangu asubuhi hata jioni? 15 Musa akamwambia mkwewe, Ni kwa sababu watu hunijilia mimi wapate kumwuliza Mungu; 16 wakiwa na neno, hunijilia; nami naamua kati ya mtu na mwenziwe, nami nawajuvisha amri za Mungu, na sheria zake. 17 Mkwewe Musa akamwambia, Jambo hili ufanyalo si jema. 18 Huna budi utadhoofika wewe, na hawa watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako. 19 Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao; 20 nawe utawafundisha zile amri na sheria, nawe utawaonyesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo inawapasa kuifanya. 21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi; 22 nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe. 23 Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani. 24 Basi Musa akasikiza neno la mkwewe, akayafanya yote aliyokuwa amemwambia. 25 Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi. 26 Nao wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno dogo wakaliamua wenyewe. 27 Kisha Musa akaagana na mkwewe; naye akaenda zake, mpaka nchi yake mwenyewe.

 

Musa alikuwa anawajibika kumtumikia Mungu akiwa kama mwombezi wao, na watu waliokuwa hawana tuhuma za wizi na ubadhirifu walichaguliwa kuwa maakida wa makumi, wa hamsini, wa mamia na wa maelfu, na watu hawa walifanyika kuwa ni maakida wa Israeli. Mambo yaliyokuwa makuu tu kwao ndiyo walimpelekea Musa aliyekuwa na wale waliokuwa kwenye malmaka makuu.

 

Kutokana na utaratibu huu, tunaona kuwa familia zinapangwa kwa kufuata makundi ya kumikumi, na kumi wa hamsini, na kisha kwa mamia, na halafu kwa maefu na kutoka hapo kwa wakuu wa maelfu na hatimaye kwa wakuu wa makabila. Makundi yaha yalikuwa ni ya watu 28,000. Kutoka kwenye makabila haya ambako kisha tunapata watu sabini walio wajumbe wa Elohim mwenye HAki. Kwa hiyo kwa muundo huu wa familia ndio uliunda tifa, ambayo hatimaye ilifanyika kuwa ni familia ya mataifa, yote yakiwa kwenye utaratibu na kwenye mamlaka yanayoilinda na kwendana.na mapenzi ya Mungu na Torati yake.  

 

Chini ya mamlaka yake tunafanya mambo kwa jina lake nasi kwa hiyo tunaitii amri ya tatu, ambayo inafuatia zile amri za kwana na ya pili. Tukiwa kama wana wa Mungu Mmoja na Wapekee ndipo tunafanyika kuwa ni mtu mmoja na wa kweli, ambao wanafanyika kuwa waliokusudiwa tangu mwanzo kuwa ni miungu wadogo yaani elohim, ambao kutoka kwao Eloa anakuwa ni yote katika yote na ndani ya yote. Kwa hiyo, sisi tunafanyika kuwa ni Hekalu la Mungu.

1Wakorintho 3:16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?  

 

Tumeita wote ili kufanyika kuwa wana na Mungu aliye Hai (Hosea 1:10). Eloa amejiongeza mwenyewe na kuwa Elohim kama kiumbe mwenye uwezo wa kujiongeza.

 

Kumbukumbu la Torati 6:13: Mche Bwana, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.  

Jina la Mungu ni kitu chenye mamlaka ya mapana yake kati ya watu wake, kwa jinsi ya kiroho na kimwili. Kwa hiyo neno elohim linawahusu Malaika wa mbinguni na waamuzi na watawala wa taifa la kidunia la Israeli (Kutoka 22:18).

Kumbukumbu la Torati 16:18-20 Weka waamuzi na maakida katika malango yako yote akupayo Bwana, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki. 19 Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki. 20 Yaliyo haki kabisa ndiyo utakayoyafuata, ili upate kuishi na kuirithi nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

 

Kutakuwa na haki kwenye hukumu zetu zote tunazozifanya kwa hukumu ya haki.

 

Malaika wa Mungu wote wanaitwa Hayoha wanapokuwa wakifanya kazi zake alizowatuma (ndivyo ilivyoandikwa kwenye Mwanzo 18:3, 27; neno hili linafanywa kwa kuwaongeza viumbe kwenye uwingi kwenye maandiko yote ya Mwanzo 19 kwa mfano). Yahova ilitumika pia kwa malaika wengine wawili waliokuja na viumbe wengine watatu walioitwa Yahova. Alibakia na Ibrahimu alipokwenda kwa Lutu huko Sodoma, ambako alitajwa pia kuwa ni Yahova (soma jarida la Malaika wa YHVH (Na. 24) [Angel of YHVH (No. 24)]. Tangu kipindi cha Sethi ambaye ni mtoto wa Adamu, ndipo watu walianza kuliitia jina la Yahova (Mwanzo 4:26).

 

Tunaona kwamba kutoka amri hii ya tatu, ndipo tunaendelea hadi kwenye amri ya nne iliyo kama kiwango cha juu cha utakatifu kwa wakati sawa na kwa mamlaka au utawala.

Mambo ya Walawi 19:1-3: Bwana akanena na Musa, akamwambia, 2 Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu. 3 Kila mtu na amche mama yake, na baba yake, nanyi mtazitunza Sabato zangu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.  

Kutoka kwenye Amri Kuu ya Kwanza tunaiona ile ya tano ambayo inaungana na amri hizi nne za kwana na kuendelea kimtiririko kutoka kwazo.

 

Mamlaka ya kuupa uweza wa kutendea kazi au kuchukulia hatua yamewekwa kwa mtu mmoja na sio kwa wawili. Hii inamaanisha ni kwa Mungu na kwa Wateule, ambao wote wanafanya chini ya mapenzi yake yeye Mungu, aliye wa Pekee na wa Kweli (Yohana 17:3). Kwa hiyo, Kristo hawezi kufanya neno lolote kwa aonavyo yeye (Yohana 5:30). Kuelelewa jambo hilo ni muhimu sana kwa utaratibu wa imani ya Wateule, kwa namna zote mbili, yaani kiroho na kimwili, na imeonyeshwa mfano wake kwenye muundo wa mahusiano ya kifamilia pia.

 

Kunapokuwa na mgongano, ndipo kiapo au nadhiri ya mke haiwezi kuifunga familia. Na ndivyo ilivyo, kuwa ni kweli hata mapenzi ya Mungu hushinda zaidi ya yale ya Wateule wake. Tunaona kuwa sheria hii imeandikwa kwenye kitabu cha Hesabu 30:1-16, inayoagiza kusomwa kwa Torati kila ufikapo mwaka wa Saba au mwaka wa Sabato. Mume wa mwanamke au baba yake ikiwa hana mume, anaruhusiwa kuitangua nadhiri alichoiweka mwanamke. Na kama atabakia kimya siku ambazo alimsikia akikiwekea nadhiri hiyo, ndipo kitabalia kama kilivyo na atakuwa amejifunga. Bali iwapo kama atakitangua ndipo kitakuwa hakina nguvu na kitakuwa kimetanguliwa kabisa. Bali ni nadhiri ile tu ambayo mwanamke mjane atakachokiweka baada ya kufa mume wake ndicho kitabakia kimesimama hivyo tu.

 

Kwa hiyo, mwnamke yu chini ya mume wake. Kwa kuwa amechukuliwa kutoka kwenye familia moja na kukabidhiwa kwenye familia nyingine ambayo ni ya mume wake. Ni mfano ulio sawa tu na Kanisa ambalo limechukuliwa kutoka kwenye kabila la mzazi na kuwekwa au kupelekwa kwenye kabila la mume, kwenye familia inyomtii Mungu wa Pekee na wa Kweli. Na kama kichwa cha kila mwanamke ni mwanaume, ndivyo ilivyo kuwa kwamba kicwa cha Kanisa ni Kristo aliye chini ya mamlaka ya Baba.

 

Kichwa cha kila mwanamke ni mwanaume (kwenye familia) na kichwa cha kila mwanaume ni Masihi, na kichwa cha Kristo mtiwa mafuta ni Munbu.

1Wakorintho 11:3: Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu

 

Familia ya kimwili inaendelea na kuenea tu hadi kifo, bali ile ya kiroho huendelea hadi umilele, ambako hatutaoa wala kuolewa, bali tutakuwa kama malaika (Luka 20:34-35) kama elohim (Zekaria 12:8). Kama alivyo Masihi, malaika ni ndugu zetu (soma Zaburi 22:22; Ufunuo 3:5; Mathayo 10:32; 6:11; 12:10).

 

Familia kama kabila la Israel

Familia zinafanywa na makabila na kwa vikundi vilivyo ndani ya makabila. Hii inaonekana kwenye Hesabu 2.

Hesabu 2:1-33 inasema: Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2 Wana wa Israeli watapanga kila mtu penye beramu yake mwenyewe, na alama za nyumba za baba zao; kuikabili hema ya kukutania ndiko watakakopanga kwa kuizunguka pande zote. 3 Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea maawio ya jua, ndio wale wa beramu ya marago ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu. 4 Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa sabini na nne elfu na mia sita. 5 Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Isakari; na mkuu wa wana wa Isakari atakuwa Nethaneli mwana wa Suari; 6 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na nne elfu na mia nne; 7 na kabila ya Zabuloni; na mkuu wa wana wa Zabuloni atakuwa Eliabu mwana wa Heloni; 8 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na saba elfu na mia nne. 9 Hao wote waliohesabiwa katika marago ya Yuda walikuwa mia na themanini na sita elfu na mia nne, kwa majeshi yao. Hao ndio watakaosafiri mbele. 10 Upande wa kusini kutakuwa na beramu ya marago ya Reubeni kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Reubeni atakuwa Elisuri mwana wa Shedeuri. 11 Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa arobaini na sita elfu na mia tano. 12 Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Simeoni; na mkuu wa wana wa Simeoni atakuwa Shelumieli mwana wa Suri-shadai; 13 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na kenda elfu na mia tatu; 14 na kabila ya Gadi; na mkuu wa wana wa Gadi atakuwa Eliasafu mwana wa Deueli; 15 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa arobaini na tano elfu na mia sita na hamsini. 16 Wote waliohesabiwa katika marago ya Reubeni walikuwa mia na hamsini na moja elfu na mia nne na hamsini, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaosafiri mahali pa pili. 17 Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na marago ya Walawi katikati ya marago yote; kama wapangavyo marago, watasafiri vivyo, kila mtu mahali pake, penye beramu zao. 18 Upande wa magharibi kutakuwa na beramu ya marago ya Efraimu kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Efraimu atakuwa Elishama mwana wa Amihudi. 19 Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini elfu na mia tano. 20 Na karibu naye itakuwa kabila ya Manase; na mkuu wa wana wa Manase atakuwa Gamalieli mwana wa Pedasuri; 21 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa thelathini na mbili elfu na mia mbili; 22 tena kabila ya Benyamini; na mkuu wa wana wa Benyamini atakuwa Abidani mwana wa Gideoni; 23 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa thelathini na tano elfu na mia nne. 24 Wote waliohesabiwa katika marago ya Efraimu walikuwa mia na nane elfu na mia moja, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaosafiri katika mahali pa tatu. 25 Upande wa kaskazini kutakuwa na beramu ya marago ya Dani kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Dani atakuwa Ahiezeri mwana wa Amishadai. 26 Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa sitini na mbili elfu na mia saba. 27 Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Asheri; na mkuu wa wana wa Asheri atakuwa Pagieli mwana wa Okrani; 28 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa arobaini na moja elfu na mia tano; 29 kisha kabila ya Naftali; na mkuu wa wana wa Naftali atakuwa Ahira mwana wa Enani; 30 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na tatu elfu na mia nne. 31 Wote waliohesabiwa katika marago ya Dani walikuwa mia na hamsini na saba elfu na mia sita. Hao ndio watakaosafiri mwisho kwa kuandama beramu zao. 32 Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli kwa nyumba za baba zao; wote waliohesabiwa katika marago kwa majeshi yao, walikuwa mia sita na tatu elfu na mia tano na hamsini. 33 Lakini Walawi hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli; kama Bwana alivyomwagiza Musa.

 

Makabila haya kumi yapo kwenye makundi kumi manne ya makabila matatu. Makundi haya yana maana zake pia kwa muunganiko wake.

 

Biblia inayaelezea jinsi makabila haya yalivyokuwa yanahesaabiwa na kupangiliwa. Milki ya kila kabila ilitolewa kulingana na ukubwa.wa kabila ulivyo, na kwa idadi ya majina ya wanaume waliokuweko na waliofikia umri wa kwenda vitani, ambao ni kuanzia umri wa miaka ishirini na kwenda mbele.

Hesabu 26:1-62 inasema: Ikawa baada ya hilo pigo, Bwana akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia,
2 Fanya jumla ya mkutano wote wa wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani. 3 Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia, 4 Fanyeni jumla ya watu, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama Bwana alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri. 5 Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu; 6 na wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; na wa Karmi, jamaa ya Wakarmi. 7 Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tatu elfu na mia saba na thelathini. 8 Na wana wa Palu; Eliabu. 9 Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na Bwana; 10 nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara. 11 Pamoja na hayo, hao wana wa Kora hawakufa. 12 Na wana wa Simeoni kwa jamaa zao; wa Yemueli, jamaa ya Wayemueli; wa Yamini, jamaa ya Wayamini; na Yakini, jamaa ya Wayakini; 13 wa Sohari, jamaa ya Wasohari; wa Shauli, jamaa ya Washauli. 14 Hizi ndizo jamaa za Wasimeoni, watu ishirini na mbili elfu na mia mbili. 15 Na wana wa Gadi kwa jamaa zao; wa Sifoni, jamaa ya Wasifoni; wa Hagi, jamaa ya Wahagi; wa Shuni, jamaa ya Washuni; 16 wa Ezboni, jamaa ya Waezboni; wa Eri, jamaa ya Waeri; 17 wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli. 18 Hizi ndizo jamaa za wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, arobaini elfu na mia tano. 19 Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani. 20 Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera. 21 Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli. 22 Hizi ndizo jamaa za Yuda kama waliohesabiwa kwao, sabini na sita elfu na mia tano. 23 Na wana wa Isakari kwa jamaa zao; wa Tola, jamaa ya Watola; wa Puva, jamaa ya Wapuva; 24 wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni. 25 Hizi ndizo jamaa za Isakari kama waliohesabiwa kwao, sitini na nne elfu na mia tatu. 26 Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli. 27 Hizi ndizo jamaa za Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, sitini elfu na mia tano. 28 Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu. 29 Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi. 30 Hawa ndio wana wa Gileadi; wa Abiezeri, jamaa ya Waabiezeri; wa Heleki, jamaa ya Waheleki; 31 na wa Asrieli, jamaa ya Waasrieli; na wa Shekemu, jamaa ya Washekemu; 32 na wa Shemida, jamaa ya Washemida; na wa Heferi, jamaa ya Waheferi. 33 Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na wana waume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa. 34 Hizi ndizo jamaa za Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni hamsini na mbili elfu na mia saba. 35 Na wana wa Efraimu kwa jamaa zao; wa Shuthela, jamaa ya Washuthela; wa Beredi, jamaa ya Waberedi; wa Tahathi, jamaa ya Watahathi. 36 Na wana wa Shuthela ni hawa; wa Erani, jamaa ya Waerani. 37 Hizi ndizo jamaa za wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, thelathini na mbili elfu na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao. 38 Na wana wa Benyamini kwa jamaa zao; wa Bela, jamaa ya Wabela; na wa Ashbeli, jamaa ya Waashbeli; wa Ahiramu, jamaa ya Waahiramu; 39 wa Shufamu, jamaa ya Washufamu; wa Hufamu, jamaa ya Wahufamu. 40 Na wana wa Bela walikuwa Ardi na Naamani; wa Ardi, jamaa ya Waardi; wa Naamani, jamaa ya Wanaamani. 41 Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia sita. 42 Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao. 43 Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa sitini na nne elfu na mia nne. 44 Na wana wa Asheri kwa jamaa zao; wa Imna, jamaa ya Waimna; wa Ishvi jamaa ya Waishvi; wa Beria, jamaa ya Waberia. 45 Wa wana wa Beria; wa Heberi, jamaa ya Waheberi; wa Malkieli, jamaa ya Wamalkieli. 46 Na jina la binti wa Asheri aliitwa Sera. 47 Hizi ndizo jamaa za wana wa Asheri kama waliohesabiwa kwao, hamsini na tatu elfu na mia nne. 48 Na wana wa Naftali kwa jamaa zake; wa Yaseeli, jamaa ya Wayaseeli; na wa Guni, jamaa ya Waguni; 49 wa Yeseri, jamaa ya Wayeseri, wa Shilemu jamaa ya Washilemu. 50 Hizi ndizo jamaa za Naftali kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia nne. 51 Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, mia sita na moja elfu, na mia saba na thelathini (601,730). 52 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 53 Watu hawa watagawanyiwa nchi hiyo iwe urithi wao, vile vile kama hesabu ya majina yao ilivyo. 54 Hao waliozidi hesabu yao utawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka hesabu yao, utawapa urithi kama upungufu wao; kila mtu kama watu wake walivyohesabiwa, ndivyo atakavyopewa urithi wake. 55 Lakini nchi itagawanywa kwa kura; kwa majina ya kabila za baba zao, ndivyo watakavyopata urithi. 56 Kama kura itakavyokuwa, ndivyo urithi wao utakavyogawanywa kati yao, hao wengi na hao wachache. 57 Na hao waliohesabiwa katika Walawi kwa jamaa zao ni hawa; wa Gershoni, jamaa ya Wagershoni; na wa Kohathi, jamaa ya Wakohathi; na wa Merari, jamaa ya Wamerari. 58 Hizi ndizo jamaa za Lawi; jamaa ya Walibni, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya Wamala, na jamaa ya Wamushi jamaa ya Wakora. Na Kohathi alimzaa Amramu. 59 Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu umbu lao. 60 Tena kwake Haruni walizaliwa hawa, Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. 61 Tena Nadabu na Abihu wakafa, hapo waliposongeza moto wa kigeni mbele za Bwana. 62 Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa ishirini na tatu elfu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli.   

 

Ardhi iligawanywa kwa kura au kwa vipimo, jambo ambalo ni adimu sana kufanyika leo. Kwa hiyo, yubile ilihusika na ugawaji upya wa ardhi hiyo kwa kuipigia kura tena.

 

Kwa watu hawa waliohesabiwa huko Sinai, hawakuwa ni wale wanaume walioachwa wakati wanahesabiwa kwenye uwanda wa Moabu, hesabu ambayo iliwacha Kalebu wana wa Yefume na Yoshua mwana wa Nuni, kwa sababu zake Bwana na kuwa wengine wote wafe wangekufa hakika jangwani.

Hesabu 26:63-65: Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko. 64 Lakini katika watu hao hapakuwa na mtu hata mmoja wa wale waliohesabiwa na Musa na Haruni kuhani; waliowahesabu wana wa Israeli katika bara ya Sinai. 65 Kwa kuwa Bwana alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.   

 

Hii ilikususia kwa wote ambao hawakupenda kuingia kwenye Nchi ya Hahadi kwa njia ya ubatizo wa Roho Mtakatifu, kwa kipindi chote cha Yubile arobaini za kanisa kuwa jangwani, kwa kipindi tangu kifo cha Masihi hadi kipindi cha kuja Kwake mara ya pili. Wale ambao hawajatubu na kukubali kubatizwa hawakuingia kwenye nchi ya Israeli na kurithi milki ya Mungu, bali waliangamia jangwani. Na ingawaje wao ni miongoni mwa makabila haya, watu hawa hawataingia kwenye familia ya Mungu hadi kwenye Ufufuo wa Pili.

 

Kuitii sheria

Taifa limefanywa kwa utaratibu wa familia.

Hesabu 2:34 Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote Bwana aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyopanga penye beramu zao, na ndivyo walivyosafiri, kila mtu kwa jamaa zao, kwa nyumba za baba zao.

 

Upatanisho kwa njia ya sadaka ya damu ulifanyika kufuatana na nyuma ya kila familia.

Kutoka 12:3:  Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;

 

Familia na taifa yanalinwa kupitia na utii wao kwenye sheria hizi za Mungu. Hakuna taifa lililoruhusiwa kuwa liabudu sanamu, na taifa la Israeli ndilo limebahatika kuwa msingi wa sheria hii. Kwa ajili hii, familia za wote wawili, yaani mwanadamu na ya mnyama wanalindwa (Kutoka 23:24-26).

Kutoka 23:26 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza

 

Adhabu waliyoahidiwa itawapata kwa kuabudu sanamu  ilikuwa ni kwenda utumwani na kuangamizwa na kufutwa kizazi chao na taifa lao (soma Amosi 5:25-27; pia jarida la Torati na Amri ya Pili (Na. 254) [Law and the Second Commandment (No. 254)].

 

Torati ilifundishwa kwenye familia na watoto waliiheshimiwa na kuitii tangu wakiwa kwenye umri mdogo wa utoto wao.

Kumbukubu la Torati 32:46: akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii.

 

Maisha ya kila mmoja wao kwenye familia na taifa yalirefushwa kwa kutilia kwao maanani jambo hili.

Kumbukumbu la Torati 32:47: Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.  

 

Hii ndiyo kiini msingi cha torati yote na manabii. Torati haipaswi itafsiriwe kwa kufuata mapokeo ya watu (Marko 7:10-13), bali ni kwa mujibu wan eno la Mungu lililonenwa na watumishi wake manabii.

 

Kikomo cha mamlaka ya mwanadamu

Mamlaka na uweza wote ukiwemo ule aliopewa Masihi, vilitoka nab ado vinatoka kwa Mungu, ikiwa ni hekima na uelewa wake (sawa na Mathayo 21:23; Zaburi 62:11).

Danieli 2:20-22  Danielii akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. 21 Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa; 22 yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake.

 

Mungu Mwenyezi humpa mamlaka na uweza mtu yeyote anayempenda na kama apendavyo yeye mwenyewe (Danieli 4:25). Hii anaweza kupewa hata Mataifa, Mpagani, au hata miongoni mwa wale Malaika waliosi, au anaweza kuwatunukia Wana wa Mungu (Kumbukumbu la Torati 32:8). Kwa hiyo, tunatakiwa watu wote kuitii mamlaka iliyopo (Warumi 13:1-5).

 

Mungu anapaswa kuheshimiwa na kumtii kwa kila anachokiamuru na hata pale ambapo mapenzi ya wanadamu nayayazidi yale ya Mungu, bado Mungu anapaswa kuheshimiwa na kumtii tu.

Matendo 5:29: Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu

 

Tendo la kumtii Mungu kama Baba yetu ni utiifu kwenye amri na sheria zake (Kumbukumbu la Torati 28:58-59).

 

Wakati mamlaka ya Mungu inapotolewa na kupewa wanadamu na wakati mfalme anapopewa mamlaka ya kututawala, ndipo mamlaka hii haitakiwi apewe (sawa na Kumbukumbu la Torati 17:14-20 lisemavyo hapo juu). Hakuna mtu aliyetakiwa apewe utawala mpaka awe anaendana na sifa zilizoandikwa kwenye totati ya Mungu. Watoto wake ni lazima pia waendane na kutii amri zilizoandikwa kwenye torati hii.

 

Maoni na mashauri ya familia yanatakiwa kutafutwa (Mithali 23:22, 25). Familia pia inawajibu wa kutoa masahihisho ya kwanza kikamilifu. Nidhamu na kuuadhisha pia ni wajibu mmojawapo wa familia na sio busara au vema kujiondoa na matendo na kuonyesha ukarimu au kuadhibu kwa kutumia fimbo kwa kumuonya mtoto (Mithali 13:24; 19:18; 23:13-16; 22:15). Kila asikiaye maonyo hupata maarifa na hekima (Mithali 15:32, 33).

Mithali 15:32-33: Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu. 33 Kumcha Bwana ni maonyo ya hekima; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

 

Waebrania 12:11: Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.

 

Marekebisho yoyote yatakayofanywa kwa vijana yatatapa ijara au malipo yake siku za mbele kwa mwenendo huo uliorekebishwa. Hali ya kutomrekebisha motto au kijana itasababisha athari ya jamii yote kuharibika. Tatizo kuu kwenye jamii yetu inayoonekana ukosefu wa maelekezo au mafundisho ya kibiblia na kutoadibishwa kwenye miaka ya mwanzoni, na mambo ambayo vijana wanakutana nayo kwenye masomo yao.

Mithali 22:6: Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee

 

Elimu ya kijana haiwezi kupewa kwa wengine kwa mafanikio. Ni wajibu wa wazazi kuwaelimisha na kuwaadibisha watoto wao. Inapotokea kuwa wajibu huu unapoondolewa au kutotiliwa maanani au kudharauliwa, ndipo jamii inapoanza kuwa isiyoaminika nay a watenda maovu.

Mithali 29:15: Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.  

 

Na hii ndiyo maana talaka ni jambo la hatari sana, kwa kuwa inasambaratisha familia na inaondoa hali ya vijana mumwamini na kumpenda Mungu au kuyapenda mambo yote yaliyo kwenye utaratibu na maagizo ya Mungu.

 

Hali hii ya kurekebishwa au kuadibishwa inatakiwa ienee kwa watu wa ngazi zote na umri wote kwenye jamii yetu.

Mithali 1:7: Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.  

 

Maadili ya watu hutoka kwenye familia na familia inatuama kwenye sheria. Na hii ndiyo sababu moja wapo inayoweka umuhimu wa kusomwa Torati katika mwaka wa saba ambao pia ni wa Sabato.

Kumbukumbu la Torati 4:7-9 Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo? 8 Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo. 9 Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;

 

Sambamba yake, amri hii inapaswa isomwe kwa kurudiwa rudiwa kwenye familia na kwa wote wanaoishi kwenye nyumba zetu (soma Mithali 4:10).

Kumbukumbu la Torari 6:6-7: Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; 7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

 

Mkakati huu wa kusoma na kufundisha torati unapaswa kufanywa katika kila miaka saba, na unatakiwa ufanywe kwa taifa zima (Kumgukumgu la Torati 31:10-13). Tendo hili la kusoma linafanywa ili kujitathmini matendo yetu yote.

 

Kuyalinda mazingira pia ni jambo muhimu na limeagizwa na torati, pasi kujali kwa familia kuwa ni ya wafugaji au la, au ni kwa muda waliodumu wakizitii sheria na amri hizi za Mungu (Kumbukumbu la Torati 22:6-7). Hii inalenga kote kuwili bila kujali kama wanyama hawa ni waporini au wa kufugwa majumbani.

Mambo ya Walawi 22:28 Tena kama ni ng'ombe, au kama ni kondoo, msimchinje huyo na mwanawe wote wawili kwa siku moja.

 

Hii inaenda mbali hadi kukataza tendo la kumtoa ndama kwa nguvu anaponyonya maziwa ya mama yake. Hii ni kuonyesha kwa wazi sana kuwa tendo la kupika lilikuwa limekatazwa, kwa kuwa linapingana kabisa na dhana inayohusu familia, pia inaonekana kuwa na uhusiano fulani na mafundisho ya dini ya kipagani ya urutubisho na dini ya mafumbo ya urisi.

Kutoka 23:19 Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

 

Utaratibu mzima wa torati unatakiwa ushikwe ili kumfanya kila mtu binafsi na familia waweze kuvumilia (Kumbukumbu la Torati 4:20).

Kumbukumbu la Torati 5:29: Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa kunicha, na kushika amri zangu zote sikuzote, wapate kufanikiwa wao na watoto wao milele!  

 

Amri ya jinsi ya kuenenda kama taifa mbele za Mungu inahusu pia hadi kwenye masuala ya ardhi ambayo Bwana atakupa wewe.

Kumbukumbu la Torati 7:12-26 inasema: 12 Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako; 13 naye atakupenda na kukubarikia na kukuongeza tena ataubarikia uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, maongeo ya ng'ombe zako, na wadogo wa kondoo zako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa. 14 Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo. 15 Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao. 16 Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa Bwana, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani litakuwa ni mtego kwako jambo hilo. 17 Nawe kama ukisema moyoni mwako, Mataifa haya ni mengi kunipita mimi; nitawatoaje katika milki yao? 18 Usiwaogope; kumbuka sana Bwana, Mungu wako, alivyomfanya Farao na Misri yote; 19 uyakumbuke hayo majaribu makuu yaliyoyaona macho yako, na hizo ishara, na maajabu, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoka, aliokutolea nje Bwana, Mungu wako; ndivyo atakavyowafanya Bwana, Mungu wako, mataifa yote unaowaogopa. 20 Tena Bwana, Mungu wako, atampeleka mavu kati yao, hata hao watakaosalia, hao wajifichao, waangamie mbele zako. 21 Usiingiwe na kicho kwa sababu yao; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu katikati yako, Mungu mkuu, mwenye utisho. 22 Naye Bwana, Mungu wako, atayatupia nje mataifa yale mbele yako kidogo kidogo; haikupasi kuwaangamiza kwa mara moja, wasije wakaongezeka kwako wanyama wa mwitu. 23 Ila Bwana, Mungu wako, atawatoa mbele yako, atawatia mashaka, mashaka makuu, hata waishe kuangamizwa. 24 Na wafalme wao atakutilia mkononi mwako, nawe utalipoteza jina lao litoke chini ya mbingu; hapana mtu atakayeweza kusimama mbele yako, hata utakapokwisha kuwaangamiza. 25 Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako; 26 na machukizo usitie ndani ya nyumba yako, usije wewe kuwa kitu cha haramu mfano wake; ukichukie kabisa, na kukikataa kabisa; kwa kuwa ni kitu kilichoharimishwa.

 

Amri hizi walipewa Israeli, kwa kuwa waliokuwa wenyeji asilia wan chi ya Kanaani walikuwa wamelaaniwa kwa ajili ya kuabudu kwao sanamu.

 

Utaratibu huu wote wa familia, taifa na sheria ulimlenga Masihi, familia ikiwa ni wanaoitunza tu kwa kielelezo.

Yohana 10:7-16 inasema: Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. 8 Wote walionitangulia ni wevi na wanyang'anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. 9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. 11 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. 12 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. 13 Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. 14 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; 15 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.

 

Kwa hiyo, utaratibu wote mzima wa familia na sheria vinakuwa kielelezo cha taifa moja lililo kama Israeli chini ya Mungu likiwa na Masihi akiwaongoza.

 

Kuiasi sheria au torati

Tendo la kuziasi sheria au totati kwa familia ni jambo linalopelekea hukumu na hukumu yake ni kifo (Kumbukumbu la Torati 21:18-23) kama tulivyojionea hapo juu. Kwa hiyo, hukumu ya kifo ilikuwa ndiyo wanayostahili wazazi kwa mahala pa pili (Kumbukumbu la Torati 17:6-7). Hakuna mtu anayeweza kuhukumiwa kifo bila kutiwa mikononi mwa mashahidi wawili.

Kumbukumbu la Torati 17:6-7: Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili, au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja. 7 Mikono ya wale mashahidi na iwe juu yake kwanza kwa kumwua, kisha mikono ya watu wote. Uondoe vivyo uovu katikati yako.  

 

Familia ilikuwa inapimwa kwa kufuatana na sheria au torati. Machukizo ya kufanya ukahaba, usagaji na ufiraji yamekatazwa kufanyika kwenye familia, na kuendelea kuyafanya kumekatazwa kabisa kwa walio kwenye Nyumba ya Mungu. Hakuna kahaba wala afanyaye ushoga (na mapato yao hayaruhusiwi kumtolea Mungu) na hawataweza kuingia Hekaluni na kwenye Hekalu la Mungu

Kumbukumbu la Torati 23:17-18: Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili.

 

Familia yote inawajibika kuisimamia sheria na hukumu ya kifo.

Kumbukumbu la Torati 13:6-10: Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako; 7 katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia; 8 usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche; 9 mwue kweli; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote. 10 Nawe mtupie mawe hata afe; kwa kuwa alitaka kukupotoa na Bwana, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa,

 

Masihi alituonyesha mtazamo sahihi wa torati wakati torati ilipokuwa imepotoshwa na kuvunjwa na mapokeo ya Mafarisayo na shule za marabi. Hii ilitokea kwa tendo lake la uponyaji walivyokshutumu kuwa alikuwa anaihalifu au kuivunja torati.

Marko 7:6-13 inasema: Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami; 7 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, 8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. 9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. 10 Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe. 11 Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; 12 wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; 13 huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.

 

Kwa ajili hii iliwapelekea Yuda na Walawi kuondolewa mbali ma kwenda utumwani kwa karne kadhaa, nako bado waliendelea na shingo ngumu wasilisikie neno la Mungu aliye Hai, bali wakajifanyia amri zao wenyewe zilizoyafuata mapokeo ya wanadamu (Kumbukumbu la Torati 28:58-68).

 

Mamlaka kwenye familia

Mamlaka ya kwenye familia hupangiliwa na baba, ikiwa kama nyumba ya Mungu. Kwa sababu hii tumeona kwamba kiapo anachoweka mwanaume kwa Mungu kinabakia hivyo kikimfunga, na kiapo cha mwanamke hubakia kwenye maamuzi ya mwanaume. Baba na hata baadae kwenye ndoa, mume anaweza kutangua kiapo alichokiweka binti yake au mkewe iwapo kama ataona kinaendana kinyume mamlaka aliyonayo na wajibu wake. Hii ni moja ya sababu ya Adamu kutwishwa lawama kwa dhambi aliyoifanya Hawa pia. Kristo anawajibika kutuwakilisha sisi kwa Mungu bila kunyanzi wala mawaa. Hii inatokana na shera ya utoaji dhabihu.

Mambo ya Walawi 22:19-20: ili mpate kukubaliwa, mtaleta mume mkamilifu, katika ng'ombe, au katika kondoo, au katika mbuzi. 20 Lakini mnyama ye yote aliye na kilema msimtoe; kwa kuwa hatakubaliwa kwa ajili yenu.  

 

Sisi tu malimbuko ya Mavuno ya Mungu. Na kama Kristo alivyokuwa hana waa, ndivyo hata sisi tunatakiwa tusiwe na mawaa kwa kuwa ni wake wa Bwana arusi, tliosafishwa na kufanywa weupe kwa damu ya Mwana kondoo (sawa na Danieli 11:35; Ufunuo 3:18; 6:11; 7:13-14; 15:6-7; 19:7-10).

 

Wawakilishi hawa wote wamewekwa kwenye familia na wazazi kwa mfano wa kwanza. Kwa jinsi hii Mungu anawajibika kuwapatia watoto wake kwa sheria zake mwenyewe. Kwa hiyo, Wateule wote anapewa kwa uweza wake wa kuwa anajua kila jambo na uwezo wake wa kila jambo na kwa mapenzi yake na upendo wake mkamilifu. Kiumbe yule ambaye hajuia mambo yote yajayo hawezi kuwa Mungu. Kwa hiyo, Mungu akiwa ni kiumbe anayeyajua mambo yote, amewapa watoto wake upendo wake kamili unaotokana na sheria na Amri Kuu mbili Hesabu 30:1-16 na jarida la Kondoo Aliyepotea na Mwana Mpotevu (Na. 199) [Lost Sheep and the Prodigal Son (No. 199)].

 

Mamlaka ya familia yanaanzia kwenye kichwa. Kwa hiyo nadiri cha mwanamke kinaweza kutanguliwa na yeye aliye kichwa cha nyumba, kukionekana kuna mgongano fulani wa maslahi ya familia. Kukaa kimya kutachukuliwa kuwa ni ishara ya kukubaliana na uamuzi huo au utata (kama inavyosema Hesabu 30:1-16 hapo juu).

 

Kumuapia Mungu Kanisani ni jambo linalotufunga na hukumu yake ni kifo iwapo kama itafanywa kwa Roho Mtakatifu, kama ilivyowatokea kina Anania na mke wake Safira ambao wote wawili walikuwa wanajaribu kuvunja sehemu ya nadhiri yao (Matendo 5:1-10).

 

Wajibu kwa familia

Wazazi wanawajibika kuitunza familia. Yeye asiyewatunza watu wa nyubani mwake mwenyeweni mbaya kuliko asiye amini. Wajibu huu amepewa baba kwa upande wa kwanza, na mama ni kwa sehemu ya pili, mjukuu ni kwa tatu na hatimaye ni kwa familia yote mzima kama ni ya watu wengi au Kanisa.

1Timotheo 5:1-16 inasema:  Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu; 2 wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote. 3 Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli. 4 Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu. 5 Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku. 6 Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.
7 Mambo hayo pia uyaagize, ili wasiwe na lawama.
8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini. 9 Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja;
10 naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema. 11 Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa; 12 nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza.
13 Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa. 14 Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu. 15 Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani. 16 Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.

Neno mjukuu (kwenye aya ya 4) ambalo kwa Kiyunani ni ekgonos, ambalo limetafsiriwa wapwaze kwenye farisi ya KJV. Ijulikane kwamba ayah ii ilitafsiriwa kutoka kwenye tafsiri ya Kiingereza ilikuwa ni kawaida kutumia neno wapwaze walipokuwa wanamaanisha wajukuu (sawa na kitabu cha Shakespeare cha Othello).

 

Familia ni mtoaji, lakini Kanisa familia kamilifu na kiini cha imani. Ni wajibu wa wanawake vijana kuolewa na kuzaa watoto kama wakibarikiwa kufanya hivyo.

 

Haki ya kuishi kwenye familia

Wajibu wa kulinda maisha kwenye familia wamepewa wazazi na mara nyingi wajibu huu umehakikishwa na Munbu, kama tunavyoona kwenye kitabu cha Kutoka  2:1-10.

Kutoka 2:1-10 inasema: Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaondoka akaoa binti mmoja wa Lawi. 2 Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu. 3 Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto. 4 Umbu lake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata. 5 Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kisafina katika majani, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta. 6 Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania. 7 Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu? 8 Binti Farao akamwambia, Haya! Enenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto. 9 Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonyesha. 10 Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa, akasema, Ni kwa sababu nalimtoa majini.

Mungu wa dunia hii anausongo sana kutafuta uhai wa wateule. Alitafuta kumwangamiza Musa na wana wa Israeli. Kwa jinsi hiyo hiyo alitaka kumwangamiza Masihi (Mathayo 2:1-23), nab ado anaendelea kutafuta jinsi ya kuliangamiza taifa na Kanisa, ambalo ni Israeli (Ufunuo 12:13-18).

 

Ni wajibu wa familia kulinda uhai wa taifa. Mungu atatuletea wokovu: Masihi atakuja kuwaokoa wale wote wanaomngojea kwa hamu kubwa. Hadi kipindi kile, Kanisa litakuwa linapitia kwenye maajaribu yatakayolifanya kupitia kwenye tanuu la moto wa mateso. Na kila mtoto atakayeyatishia maisha ya wazazi wake kwa kuhangaikia uhai wake au wa wa mttoto huyo kama inavyoonekana kwenye aya za hapo juu. Jambo hili limeelezewa pia kwenye jarida la Torati na Amri ya Sita (Na. 259) [Law and the Sixth Commandment (No. 259)].

 

Maingiliano ya kijamii

Kila mtu anawajibika kwa nwenendo wake na jinsi ya kuishi kimahusiano kwenye familia yake, awe mwanamke au mwanaume na mfano wa kwanza ukiwa ni mahusiano ya ndani (Kutoka 21:15), na ni kote kuwili, yaani kwenye familia na kwenye jamii ikiwa ni mfano wa pili.

Kutoka 21:17: Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.

 

Mambo ya Walawi 20:9: Kwa maana kila mtu amlaaniye baba yake au mama yake hakika atauawa, amemlaani baba yake na mama yake; damu yake itakuwa juu yake

 

Maelekezo haya yametolewa kwa marudio kwa mara tatu ili kusisitiza umuhimu wake.

Kumbukumbu la Torati 27:16: Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.

 

Umri unapaswa kuheshimiwa.

Mambo ya Walwi 19:32: Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi Bwana.

 

Kuwalinda waheni

Wana wa Yakobo walikuwa nafsi sabini. Kipindi cha Musa, wazee hawa waliwakilisha wana wa Yakobo na serikali ya Israeli. Tunamuona pia Masihi kuwa alikuwa na wanafunzi sabini, na mapepo waliwatii wakiwa kama wazee wa Kanisa ambalo ni Israeli wa kiroho na matokeo ya mwisho ya serikali ya Mungu (Kutoka 1:1-22). Ni kwa sababu hii ndipo wana wa Mungu wanateswa na Mungu wa dunia hii na mfumo wake. Ulinzi wao unafanywa na Mungu, kama tunavyoona jinsi walivyofanya wale wakunga wa Misri ambao walitata thawabu. Zawadi hii ya ulinzi imetolewa pia kwenye mfano wa kondoo na mbuzi (Mathayo 25:31-46).

 

Ulinzi wa familia kwa mambo yanayohusu hisia za kimaeneno

Familia ni kiini cha kundi la kabila ambalo ni utaratibu wa familia enezi. Kwa hiyo, kabila ndilo linalounda taifa makabila yanalindwa kwenye ardhi zao kwa mujibu wa tirati ya Mungu. Ilinzi huu wa makabila umeandikwa kwenye kitabu cha Hesabu 27:1-11 kwenye hadithi inayowahusu mabinti wa Selofehadi. Selofehadi alifia jangwani kwa dhambi zake alizozitenda mwenyewe na hakuwa wa wana wa kiume. Urithi wake ulilindwa na kupewa binti zake ambao walikuwa na urithi uliokuwa ni haki yao, bali walipewa sharti la kutoolewa na wanaume wa nje ya kabila lao. Hii inafanya taswira ya wongofu na urithi wa wateule. Urithi wao ulipaswa ubakie kwenye familia yao na kupewa kizazi kijacho nah ii ndiyo amri ya sheria ya hukumu katika Israeli.

 

Kwa hiyo, wale walio na urithi wataoa ndani ya kabila la baba yake, na ndipo kabila na familia italindwa ndani yake (soma Hesabu 36:1-12). Kwa jinsi hii, familia inayotoka Familia ya Kifalme italindwa na ardhi yote itakayotunzwa kipindi cha Yubile (soma Ezekieli 46:16-18). Hakuna kitakachochukuliwa kwa dhuluma, na mchakato wake ni endelevu.

 

Kuwalinda wajane na yatima

Mungu ndiye Mlinzi wa wale wote wasio na ulinzi na malipo yanafuata toka kwa Mungu.

 

Yohana 19:26: Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao.  

Kwa hiyo Kanisa ndilo lenye wajibu wa kwanza wa familia. Mariamu alikuwa na watoto wa kiume wane na idadi kadhaa ya watoto wa kike wakti Kristo alipomwambia Yohana maneno yafuatayo.

Yohana 19:27: Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.  

Nduguyake Kristo alikuja na kujiunga na Kanisa na akafanya mambo makuu akiwa ni mzee wa Kanisa, bali hii haikuathiri msimamo uliowekwa hapa.

 

Zaburi 68:5-6: Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu. 6 Mungu huwakalisha wapweke nyumbani; Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa; Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu.  

Mungu atashughulika na mahitaji ya wajane na yatima (soma Isaya 10:2; Yeremia 49:11). Kwa mujibu wa nabii Ezekieli, Mungu anakemea sana uhaitia unajisi Israeli. Kwa jinsi hii, taifa linalaumiwa kwa kuwa moto uliwashwa na baba zao na mama zao na wakafanya uzinzi na kujinajisi kiroho (soma Ezekieli 22:1-16). Mungu aliwatawanya Israeli kama matokeo ya kufanya kwao hivyo (soma Kumbukumbu la Torati 4:27; 28:25,64).

Kutoka 22:21-24: Usimwonee mgeni, wala kumtendea jeuri; kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. 22 Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima. 23 Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao, 24 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima

 

Kuwalinda wageni na walioajiriwa kwenye familia ya Mungu

Kuna sheria inayohusu jinsi ya kuwalinda ili wasidhulumiwe watumishi walioajiriwa, kuwaachilia huru watumwa na kusamehe madeni na kuwalinda wageni.

Mambo ya Walawi 25:14-17: Tena kama ukimwuzia jirani yako cho chote, au kununua cho chote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe; 15 kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe. 16 Kama hesabu ya miaka ilivyo ni nyingi ndivyo utakavyoongeza bei yake, na kama hesabu ya miaka ilivyo ni chache ndivyo utakavyopunguza bei yake; kwani yeye akuuzia mavuno kama hesabu yake ilivyo. 17 Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu

 

Kutoka 23:9 Usimwonee mgeni; maana, ninyi mwajua moyo wa mgeni ulivyo, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri

 

Tuna Baba mmoja tu, Mungu Maoja aliyetuumba sisi sote (Malaki 2:10). Mungu kama Baba yetu anawaokoa wana wa Israeli na kuwarrejeza tena kwake (soma Isaya 49:15-26). Hata maadui zetu wanapaswa kulindwa kutoka kwenye manyanyaso na uovu wao (Kutoka 23:5).

 

 Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.”

Kumbukumbu la Torati 10:18-19 Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. 19 Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.

 

Mambo ya Walawi 19:33-34: Na mgeni akikaa pamoja nawe katika nchi yako, usimdhulumu. 34 Mgeni akaaye pamoja nawe atakuwa kama mzalia kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.  

 

Mataifa wanaoabudu sanamu wawakuruhusiwa kuachiliwa nyumba zao na iliamriwa watokomezwe kabisa kutoka kwa wana wa Israeli na wana wa Mungu aliye Hai. (Kumbukumbu la Torati 7:1-26). Sio kwa kuwa Israeli walikuwa ni wazuri sana, bali kwa sababu ya uasi na matendo maovu ya mataifa haya ndio maana waliangamia mbele ya Israeli (soma Kumbukumbu la Torati 9:1-29).

 

Mgogoro huu mkubwa na wa dhahiri kwa kile torati inachotaka unaelekewa kama matengenezo ya familia na mahusiano ya kijamii kwenye jamii, yaliyopelekea uhusiano wao kwa Mungu. Ibada ya sanamu inapaswa kupigwa vit kutoka kwenye jamii zetu.

 

Sheria kuhsu familia na uthibi wa kijamii kupitia mahakama  

Sheria kuhusu familia ni ya mpango kazi muhimu wa kisheria kama haki yake yenyewe ilivyo. Inaanzia kutoka maandiko haya na maandiko mengine yaliyo kwenye jarida la Torati na Amri ya Saba (Na. 260) [Law and the Seventh Commandment (No. 260)] utoaji huo wa hati ya talaka unaruhusiwa, ingawaje Mungu anachukia kuachana.

 

Zinaa ipo kwenye kundi la mambo yanayotoa ruhusa kwa wanandoa kuachana na ni tendo linalouhusisha mwili ukishiriki na ni sawa na ibada ya sanamu. Nabii Malaki alitumwa Yuda kwa kuwa katika kpindi hiki taifa lilikuwa limeanza kufanya ibada ya kigeni ndani ya Israeli na walikuwa wamewaoa binti za Mungu mgeni, jambo lililowapelekea wao kwenda utumwani. Kwa hiyo, mtazamo wa kila mmoja wetu ni wajibu wa wazazi. Mamlaka makubwa waliyonayo wazazi na Mungu anayelihukumu taifa na likiwa kama familia ya kitaifa (Malaki 2:10-17).

 

Watu waliruhusiwa kuachana kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao na hali yao ya kutotahiriwa mioyo yao na kuongoka, na hali ya upotofu wa hisia na fikra zao, lakini haipaswi iwe hivyo kwa wateule.

 

Maranyingi kuna viwango aina mbili za ndoa kwenye jamii zetu. Ya kwanza ni ile iliyoko kati ya wasio batizwa au kati ya mteule na mwanandoa asiyebatizwa bado. Na ya pili ni ile ya kati ya watu wawili wa imani moja. Mwanzoni kabisa ilionekana kwamba mapenzi ya Mungu yalikuwa kwamba kila mwanaume awe na mke mmoja tu (Mwanzo 2:24), lakini mtazamo huu ulionekana kuachwa mbali na mababa zetu waliofanya agano na Mungu. Utaratibu wa kuoa umewekewa mfano wake kwenye uhusiano wa mtu mmoja na taifa na Mungu, na kwa hiyo uaminifu ni kitu muhimu cha kuangalia sana kwenye mahusiano ya ndoa.

 

Kwa mujibu wa Torati na tafsiri inayohusinisha na Kristo, kuna mambo kadhaa yanayohitaji kuyatolea maelezo na ufafanuzi kuhusu amri ya saba. Kikomo cha idadi ya wake kwa mwanaume mmoja nawake unaweza kuwa ni mambo yanaendana na jinsi sheria na tatatibu za kila taifa ilivyo. Korani (Qur’an) inafuata mengi yaliyokuwa kwenye mapokeo ya marabi, ambayo yanaweka idadi ya wake wane (baadhi ya marabi walivuka hadi kuchukua wake watano) kwa mtu wa kawaida, na kumi na nane kwa mfalme.

 

Agano Jipya linaweka kikomo cha mke mmoja tu kwa mzee wa Kanisa, na kwamba mtu haruhusiwi kuwa mzee wa kanisa kama ana wake zaidi ya mmoja (1Timotheo 3:2; Tito 1:6). Inampasa Mzee awe ameoa, na ndoa ikiwa kama wajibu wa kwa kila mwanaume kwa mujibu wa agizo alilopewa Adamu. Kwa hoyo, mwanaume anaweza kutalikiwa na kuoa mke tena kabla hajawa mshirika wa Kanisa, bali wengi wao huwa hawaachi mara ile wanapojiunga na Kanisa, isipokuwa kwa makundi fulani muhimu tu. Kuna mengi aliyofundisha Masihi na yamefafanuliwa vema kwenye jarida Torati na Amri ya Saba (Na. 260) [Law and the Seventh Commandment (No. 260]).

 

Uhusiano kwa familia huishia kwenye ndoa, na kwa hiyo ridhiaa ya wazazi inahitajika kwa mujibu wa torati ya Mungu.

Kutoka 22:16-17: Mtu akimshawishi mwanamwali, aliyeposwa na mume, na kulala naye, lazima atatoa mahari kwa ajili yake ili awe mkewe. 17 Ikiwa baba yake huyo mwanamwali akataa kabisa kumpa, atalipa fedha kama hesabu ya mahari ya mwanamwali ilivyo.  

Kwa mujibu wa Torati, ridhaa ya wazazi ni ya muhimu kwa binti yao hata kama akiwa ameisha fikia umri mkubwa.

 

Viapo vya ndoa ni vikali sana kiasi cha kuwataka wanandoa kukubali kuwa ni kifo tu ndicho kitawatenganisha (Mathayo 22:29-30; Marko 12:24-25). Mambo yenye utata kwenye ndoa na yanayoweza kusababisha kuachana yameelezwa kwenye jarida la totati na amri ya saba. Familia ni jingo la matofali la taifa na pia ni Mpango wa Mungu. Mashambulio ya kuanzisha kwa ndoa ni shutuma dhidi ya familia iliyo kwenye Mpango wa Mungu. Hakuna mtu anayeweza kuwa Kanisani na akazipuuzia sheria ya ndoa na wajibu wa familia. Ustawi wote wa maisha ya ndoa huliunganisha na huendelea hadi kwenye taifa. Na vivyo hivyo ni kwamba udhibiti wa uhai ni wa familia kwanza kisha unalihusisha taifa.

 

Amri ya tano inamlenga Masihi, anayefanya kazi kama Baba wa Milele kwa mamlaka aliyopewa na Baba wa milele, ambaye ni Mungu Mwenyezi. Ni yeye peke yake ndiye asiyeweza kufa na wala hana mwisho, na hakuna mtu aliyewahi kumuona na wala anayeweza kumuona (1Timotheo 6:16; wala aliyewahi kuisikia sauti yake wakati wowote ule (Yohana 5:37)). Kila baba anasimama mahala pa Masihi na mke wake anasimama mahala pa Kanisa. Wote wana wajibika kwa Mungu kwa mambo yote. Kichwa cha kila mwanaume ni Kristo na kichwa cha Kristo ni Mungu (1Wakorintho 11:3; Waefeso 5:23).

 

Kiti chako cha enzi, Mungu, Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako. (Zaburi 45:6-7; Waebrania 1:8-9).

 

Kwake tunatarajia kutoka kwake kichwa hiki cha milele wa familia na mfalme wa amani. Biblia inatuambia kuwa kuna mababa wengi (Waefeso 3:14), na wote wako chini ya Mungu Mmoja na Wapekee wa Kweli (Yohana 17:3).

 

Sisi ni daraja la Kristo na chini ya manuni zake tutaielimisha na kuifundisha dunia, kama familia, vipindi vyote viwili, yaani kwa utaratibu wa milenia na kwenye ufufuo wa Pili (soma Ufunuo 20:1-15).

 

Ni kwa kulielewa hilo tu ndipo tunalazimika kuwa wa familia iliyo ya Mungu, na Mungu akifanya kazi ndani yetu tukiwa kama viumbe wenye mfumo enezi ambao tumeitwa na kufanya kazi kama Mungu, na tunayoyajua malengo ya Amri Kuu nay a Pili inayosema: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe” Tumekusudiwa kuwa watu wake Mungu sisi sote ni wana wa yeye Aliye Juu—na Maandiko Matakatifu hayawezi kntanguka (Yohana 10:34-35).

 

q