Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[270]

 

 

 

Jumbe za Ufunuo 14

(Toleo La 2.0 19981114-20080514)

 

Jumbe za malaika wanne wa Ufunuo  14 ni za muhimu katika kutuelekeza na kutuongoza kwenye ujio wa Masihi. Zinabeba umuhimu wenye maana re katika kutuhabarisha, kutuelekeza, na msukumo au jukumu la Kanisa katika Siku za Mwisho.

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 1998, 2008 Wade Cox )

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Jumbe za Ufunuo 14



Ufunuo 14 una jumbe nne za pamoja, ambazo zinahusiana na ujio wa Masihi na harakati za Kanisa kwa maongozi ya Mungu kupitia Yesu Kristo na watumishi na wahudumu wa mambo ya rohoni ambao Mungu amempa.

 

Ujumbe wa tano unahusu hasira ya Mungu itakayomwagika wakati atakapokuja.

 

Hehemu ya kwanza inahusisha wale 144,000 wanaotokea kwenye Mlima wa Sayuni.

 

Ufunuo 14:1-7 Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. 2 Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao; 3 na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi. 4 Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. 5 Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa. 6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.

 

Ujumbe huu una maana mbili. Unahusu wale 144,000 waliotengwa na kupewa Masihi na wale waliosimama pamoja nay eye juu ya lima Sayuni. Kwa mtazamo wa haraka unaweza kuona kana kwamba ni wote wapo pmoja na kwa mahali pamoja na kwamba tukio hili linaonyesha nyakati za mwisho huko Yerusalemu. Machakato wenyewe kwa kweli unahusu mwandamano wa matukio ya nyakati tangu kuanza kwa utimilifu wa unabii ulio kwenye Isaya 61:1-2 uliotimilika mwaka 27 BK na mwisho wa ujio wake wa pili au ujio wa Masihi.

 

Isaya 61:1-2 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;

 

Kutokana na maandiko ya tafsiri ya KJV tunaona kwamba huu umeonekana kama Mwaka wa Bwana Uliokubalika, ambao ilikuwa unamaanisha wa Yubile. Unabii huu kwa kweli ulitimilika mwaka 27 BK baada ya kujaribiwa kwake jangwani, kulikofuatia baada ya kubatizwa kwake Kristo.

Luka 4:16-21 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,
18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.

 

Kwenye andiko hili pia alizungumzia kutoka kwenye Isaya 58:6, ambalo lilikuwa ni muunganiko wa maandiko mawili. (Maandiko yote yameruka maneno kuziponya roho zalizovunjiika yanayopatikana kwenye tafsiri ya KJV; sawa na kwenye maandiko ya The Companion Bible kuhusu andiko hili)

 

Kutoka hatua hii, katika kukamilisha unabii, anaitangaza pia Yubile. Andiko hili kuhusu Mwaka wa Bwana Uliokubalika ni maelekezo ya moja kwa moja ya Yubile (sawa na Mambo ya Walawi 25:8-17). Pia kuna swali kuhusuma andiko haya kwenye Ufunuo 16:7; 18:10; 19:2).

 

Tumeona kwamba utaratibu wa Yubile unaweza kujulikana kutoka kwenye Maandiko Matakatifu, kutoka kwenye maandiko mawili ya Agano la Kale pia. Ka kwanzz kwenye Ezekieli 1:1 ambapo mwaka wa kumi na tatu umewekwa au kutajwa kama mwaka wa tano wa mambo aliyoyafana Yehoyakini. Andiko hili linachanganya kidogo tunaposhughulika na kufafanua kuhusu Adari 2 na kwa hiyo mwaka unaweza kukosewa kirahisi.

 

Mtajo wa pili unaonekana kwenye usomaji wa Torati uliofanywa na Ezra na Nehemia. Ili kulielewa andiko hili sawasawa na wakati wake muafaka, historia ya ujenzi mpya wa Hekalu inapaswa ieleweke vizuri pia na usomaji ufanyike katika mwaka sahihi. Jambo hili lote limefafanuliwa kwa kina kwenye majarida ya: Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13); Maana ya Maono ya Ezekieli (Na. 108) na  Usomaji wa Torati Uliofanywa na Ezra na Nehemia (Na. 250) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13); The Meaning of Ezekiel's Vision (No. 108); and Reading the Law with Ezra and Nehemiah (No. 250)].

 

Mchakato huu wa kipindi unafaa ukiwekwa kwenye dhana halisia kuwa ni mwaka 27 BK unaonyesha kwamba hii kweli ilikuwa ni Yubile na Kristo alikuwa anatimiza unabii wa Isaya 61.

 

Hata hivyo, ujumbe ulio kwanye Ufunuo 14:7 unaelezea jambo lililoelezwa kwenye Isaya kwamba Kristo hakunukuu na kuendelea mbele katika nyakati za mwisho. Ili kuelewa vyema maana na matendo ya andiko, tunatakiwa kuandalia kile alichokisema Kristo na maandiko ya Agano la Kale ambako ndiko alichukua mifano yake.

Luka 4:22-30 Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu? 23 Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe. 24 Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe. 25 Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; 26 wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. 27 Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu.28 Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo. 29 Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini; 30 lakini yeye alipita katikati yao, akaenda zake.

 

Walikuwa na njaa kwa kuwa kwenye mifano hii miwili alikuwa anaonysha kuwa Kristgo alikuwa anatangaza wokovu kuwa utakuwa kwa Wamataifa. Mifano yote miwili ilikuwa inalihusu Kanisa, kama tutakavyojionea. Mfano wa kwanza ulikuwa unamtaja mwanamke wa Kisidoni aliyebarikiwa na nabii Eliya. Wa pili unamtaja Naaman, mtu mwenye ukoma Mshami, aliyeponywa na nabii Elisha kwa imani yake.

2Wafalme 5:1-27 Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake Bwana alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma. 2 Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani. 3 Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake. 4 Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi. 5 Mfalme wa Shamu akasema, Haya! Basi, mimi nitampelekea mfalme wa Israeli waraka. Basi akaenda zake, akachukua mikononi mwake talanta kumi za fedha, na vipande vya dhahabu elfu sita, na mavazi kumi. 6 Akampelekea mfalme wa Israeli waraka ule, kusema, Waraka huu utakapokuwasilia, tazama, nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, ili upate kumponya ukoma wake. 7 Ikawa, mfalme wa Israeli alipousoma waraka, alirarua mavazi yake, akasema, Je! Mimi ni Mungu, niue na kuhuisha, hata mtu huyu akanipelekea mtu nimponye ukoma wake? Fahamuni, basi, nakusihini, mwone ya kuwa mtu huyu anataka kugombana nami.

 

Kulikuwa na uhaba au imani ndogo katika Israeli na mfalme aliichukulia hii kama ni chanzo cha kule chokochoko ya kuanzisha vita na Washami.

 

8 Ikawa, Elisha, yule mtu wa Mungu, aliposikia kwamba mfalme wa Israeli ameyararua mavazi yake, ndipo akatuma mtu kwa mfalme, akisema, Mbona umeyararua mavazi yako? Na aje sasa kwangu mimi, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli. 9 Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake, akasimama mlangoni pa nyumba ya Elisha. 10 Naye Elisha akampelekea mjumbe, akisema, Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi. 11 Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma. 12 Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira. 

 

Watu wengi hujidhania kuwa wao ni muhimu kuliko wengine na kwamba kuna vitu rahisi vilivyoko ndani yao. Naamani alitarajia changamoto kubwa kwa kuwa aliyatazama mambo kwa mtazamo huo. Suala la kumtakasa watu wote lilikuwa rahisi, na lilikuwa kwenye maji ya uponyaji katika Israeli katika ubatizo wa Roho wa Mungu kupitia kwa Masihi.

13 Watumishi wake wakamkaribia, wakamwambia, wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi?14 Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi. 15 Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako. 16 Lakini akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa. 17 Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana. 18 Jambo hili Bwana amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, Bwana amwachilie mtumwa wako jambo hili. 19 Akamwambia, Enenda kwa amani

 

Wengi wetu, kama watumwa wa mfumo huu wa mambo ya dunia, inatupasa kuwa kwenye mazingira ambayo kwayo tusingeweza kuwepo kwa hali zetu wenyewe tulizonazo.

 

Basi akamwondokea mbali kidogo. 20 Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta; kama Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake. 21 Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani? 22 Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili. 23 Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake.24 Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao. 25 Lakini yeye akaingia, akasimama mbele ya bwana wake. Elisha akamwambia, Watoka wapi, Gehazi? Akanena, Mtumwa wako hakuenda mahali. 26 Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi? 27 Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji

 

Gehazi aliadhibiwa kwa kuwa alijaribu kujipatia faida mbali na utaratibu halali ambavyo ulitolewa kama lulu visivyo kulipia gharama yoyote. Alipewa mikasa au maradhi ambayo ya mtu aliyeponywa kwayo. Simon Mchawi pia alijaribu kujipatia faida kutokana na udhirisho wa uweza wa Roho Mtakatifu, ambao lilipewa Kanisa, na aliondolewa-mbali. Ukuhani mpya unachukua mahala pa ule wa kwanza.

 

Hadidhi ya Naamani iliyofananishwa na wokovu wa Wamataifa Kanisani. Kitendo cha kuingia majini mara saba kinafananishwa na nguvu ya ubatizo yaliyopewa Makanisa saba na roho saba za Mungu. Inasemekana kwamba Naamani aliuchukua udongo wa mahala pale nyumbani, akimaanisha kwamba awe na sehemu ya ardhi ya Israeli na Mlima Mtakatifu wa kufanyia maombi, inafananishwa na dhana ya kwamba nchi za utawanyiko za mbali na Sayuni zifanyike kuwa sahihi kwa Mataifa walio uhamishoni mbali, kwa imani, wawe kama ni Hekalu la Mungu. Ili kulielewa andiko hili kwa usahihi na ndiyo maana andiko hili limeandikwa kwenye Ufunuo 14:1ff., tunhitaji tuende kwenye Waebrania 12:1-29.

Waebrania 12:1-29 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, 2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. 3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu. 4 Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi; 5 tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; 6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. 7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? 8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? 10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. 11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. 12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, 13 mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe. 14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. 16 Asiwepo mwasherati wala asiyemcha Mungu, kama Esau, aliyeuuza urithi wake wa mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya chakula kimoja. 17 Maana mwajua ya kuwa hata alipotaka baadaye kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi. 18 Maana hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani, 19 na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine; 20 maana hawakuweza kustahimili neno lile lililoamriwa, Hata mnyama akiugusa huo mlima atapigwa kwa mawe. 21 Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka. 22 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, 23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, 24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili. 25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni; 26 ambaye sauti yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia. 27 Lakini neno lile, Mara moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae. 28 Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho; 29 maana Mungu wetu ni moto ulao.

 

Kutoka kwenye aya ya 22, tunaona kwamba tangu wongofu hadi kwenye Kanisa la karne ya kwanza, Wamataifa walikuwa wanaletwa Mlimani na Mjin wa Mungu. Na kwa hiyo, walikuwa wanaachwa ndani ya Mji na kwenye Mlima Mtakatifu tangu kipindi cha kuongoka kwao. Mlima ni mfano wa kiroho ambao watakatifu wanasimama kwapo, kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu mbili ya kuitwa kwao kutoka umataifani. Hawa 144,000 wamejumuishwa kwenye uongozi imara. Pia hawa 144,000 wamejumuishwa kwenye baraza la wazee 72 (sawa na isemavyo Hebdomekonta[duo]ya maandik o kwenye Luka 10:1,17). Hili lilikuwa ni Baraza la wazee sabini. Baraza la Sanhedrin katika Israeli liliwekwa mbadala na Sanhedrin ya Kanisa tangu kuwekwa wakfu kwao na Kristo, na kwa uweza wa Roho Mtakatifu tangu Pentekoste. Walikuwa na mamlaka juu ya mapepo tangu kuchaguliwa na kuwekwa wakfu kwao. Tangu Pentekoste, Wana wa Skewa, japo walikuwa ni watoto wa Kuhani Mkuu, hawakuwa na uwezo wowote wa kuwakabili Malaika hawa Waovu au mapepo (Matendo 19:14 ff.).

 

Hawa wazee 72 wanawakilisha dhabihu kuu ya mwaka wa kinabii ambao ni sawa na Sabato 52, Miandamo ya Mwezi na sadaka za Sikukuu, amoja na Mganda wa Kutikiswa.

 

Mkutano au umati Mkuu unaoonekana kwenye Ufunuo 7:9. Unawakilisha sadaka za daima, lakini hakuna mtu anayeweza kuwahesabu.

 

Jumbe za Ufunuo 14 ni uwajibiko wa wale 144,000. Jumbe walizopewa hawa 144,000 zinaenda hadi kwenye kipindi cha zama saba za makanisa zilizotolewa kwene Ufunuo sura za 2 na 3. Miaka elfu mbili kwa kipindi chote cha Yubile arobaini yangu mwaka 27 BK hadi 2027 BK.

 

Malaika wa Kwanza ni Injili ya Milele ambayo itatolewa kwa kipindi hadi nyakati za mwisho. Mwishoni, utimilifu au hitimisho la Ujumbe wa Isaya 61:1-2 umetolewa (sawa na Ufunuo 14:1-7).

 

Unabii ulinenwa na Isaya ulinenwa na Masihi na uliishia kwa sehemu kwenye Isaya 61:2, kwa maandiko yote, kwa kuwa mwisho wa unabii unatokea mwishoni mwa zama au ukamilifu wa dahari.

Isaya 61:2-7 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; 3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe. 4 Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi. 5 Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu. 6 Bali ninyi mtaitwa makuhani wa Bwana; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao. 7 Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.

 

Ili kuelewa zama hizi kwa kina tunahitajika kuendelea kwenye Ujumbe wa Malaika wa Pili.

 

Sehemu ya II

 

Ujumbe wa Malaika wa Pili

Ujumbe wa Malaika wa Pili unaonyesha Ujumbe wa Malaika wa Kwanza. Ni matokeo ya kuondolewa kwa Ujumbe wa Malaika wa Kwanza ili Ujumbe wa Malaika wa Pili uweze kutolewa kwa uhakika na mafanikio. Mwishoni mwa shughuli ya kuwtia mhuri hawa 144,000, Dunia itapitia maumivu makali.

 

Habari kamili kuhusu jinsi hili litakavyotokea imechambuliwa kwa kina kwenye maandiko mengine ya Ufunuo na kwingineko.

 

Mfumo na dini yote ya Kibabeloni vitashamiri katika Siku za Mwisho kabla ya kipindi cha mwisho.

 

Ufunuo 14:8 Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.

 

Huyu ndiye Yule Kahaba Mkuu anayeyaendesha au kuyaongoza mataifa na ametajwa kwenye Ufunuo 17. Ataangamizwa na umoja au muungano wa wafalme kumi ambao watapokea mamlaka kwa saa moja na Mnyama, katika Siku za Mwisho (Ufunuo 17:12-18).

 

Saa hili la kinabii, ni kipindi kifupi sana kitakachotokea. Kinaweza kutokea kwa mtindo wa kweli wa masaa ishirini na manne tunayoyajua na sehemu ya ishirini na nne ya siku ya mwaka wa kinabii – kama majuma mawili, nk. Au kinaweza kuwa ni kipindi kitakachokuwa chini au ndani ya mwaka mmoja. Lakini, hata hivyo, ni muda mfupi ambacho nabii hizi na nguvu hizi zitajikusanya ama kutokea kwa pamoja. Nguvu ya uharibifu ya mifumo au dini hii ni kubwa. Inafanya uharibifu kama uliofanyika kwene Vita Kuu ya II ya Dunia ya miaka sita, basi itakuwaje itakapofanyika kwa kutumia zana za nyukilia kwa mwaka mmoja?

 

Ili kujua kile kinachotokea inatubidi tuende kwenye hadithi ya Gideon, Gideon alisimama katikati ya imani ya dini ya Baali na alikuwa ni mtu wa kutegemewa na kutizamwa na wengi, kama dini na mfumo huu utakavyokuwa na kuonekana katika Siku za Mwisho.

 

Waamuzi 6:32-40 32 Basi akamwita Yerubaali siku hiyo, akisema, Baali na atete naye kwa ajili ya nafsi yake, kwa sababu ameibomoa madhabahu yake. 33 Wakati huo Wamidiani na Waamaleki, na hao wana wa mashariki walikutana pamoja; wakavuka na kupanga hema zao katika bonde la Yezreeli. 34 Lakini roho ya Bwana ikaja juu yake Gideoni; naye akapiga tarumbeta; na Abiezeri walikutanika na kumfuata. 35 Kisha akatuma wajumbe waende kati ya Manase yote; wao nao walikutana pamoja ili kumfuata; kisha akatuma wajumbe waende kwa Asheri, na kwa Zabuloni, na kwa Naftali; nao wakakwea ili kumlaki. 36 Gideoni akamwambia Mungu, Ikiwa wewe utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema, 37 tazama, nitaweka ngozi ya kondoo katika kiwanja cha kupuria; na kama ukiwapo umande juu ya ngozi tu, na nchi yote ikiwa kavu, basi, hapo ndipo nitakapojua ya kuwa utawaokoa Israeli kwa mkono wangu, kama ulivyosema. 38 Ikawa hivyo; kwa maana aliondoka asubuhi na mapema, akaikamua ile ngozi, akautoa ule umande katika ile ngozi, bakuli zima la maji. 39 Gideoni akamwambia Mungu, Hasira yako isiwake juu yangu, nami nitasema mara hii tu; nakuomba, nijaribu kwa ngozi hii mara hii tu; sasa ngozi tu na iwe kavu, na uwe umande juu ya nchi yote. 40 Mungu akafanya hivyo usiku ule; maana ile ngozi tu ilikuwa kavu, napo palikuwa na umande juu ya nchi yote.

 

Gideon, au Yerubaali, alipindua madhabahu ya Baali na alipewa amri kujaribu au kuthibitisha mapenzi ya Bwana.

 

Akiwa na Wenzake, aliwakusanya pia wale waliokwua katika Asheri na Zabuloni na Naftali. Hii pia inahusiana na kufanana na Siku za Mwisho na kazi za makabila haya kwenye mchakato huu. Mbali na makabila haya walichaguliwa wale ambao walitumiwa na Mungu.

 

Waamuzi 7:1-25 Kisha Yerubaali, yaani Gideoni, na watu wote waliokuwa pamoja naye wakaondoka na mapema, wakapiga kambi yao karibu na kijito cha Harodi; na kambi ya Midiani ilikuwa upande wao wa kaskazini, karibu na mlima wa More, bondeni. 2 Bwana akamwambia Gideoni, Watu hawa walio pamoja nawe ni wengi mno hata nikawatie Wamidiani katika mikono yao, wasije Israeli wakajivuna juu yangu wakisema, Mkono wangu mwenyewe ndio ulioniokoa. 3 Basi sasa enda, tangaza habari masikioni mwa watu hawa, na kusema, Mtu awaye yote anayeogopa na kutetemeka, na arudi aondoke katika mlima wa Gileadi. Ndipo watu ishirini na mbili elfu wakarudi katika watu hao, wakabaki watu elfu kumi. 4 Bwana akamwambia Gideoni; Hata sasa watu hawa ni wengi mno; uwalete chini majini, nami nitawajaribu huko kwa ajili yako; kisha itakuwa ya kwamba yule nitakayekuambia, Huyu atakwenda pamoja nawe, ndiye atakayekwenda pamoja nawe; na mtu yule nitakayekuambia, Huyu hatakwenda pamoja nawe, basi mtu huyo hatakwenda. 5 Basi akawaleta watu chini majini. Bwana akamwambia Gideoni, Kila mtu atakayeyaramba maji kwa ulimi wake, kama vile arambavyo mbwa, huyo utamweka kando; kadhalika kila mtu apigaye magoti kunywa. 6 Na hesabu ya hao waliokunywa kwa kuramba-ramba, wakipeleka mkono kinywani, ilikuwa watu mia tatu; bali watu wengine wote walipiga magoti kunywa maji. 7 Bwana akamwambia Gideoni, Kwa watu hawa mia tatu walioyaramba maji nitawaokoa, nami nitawatia Wamidiani katika mikono yako; lakini watu hawa wote wengine na waende zao, kila mtu mahali pake. 8 Basi wale watu wakachukua vyakula vyao mikononi mwao, na tarumbeta zao; naye akawapeleka watu wote wa Israeli, kila mtu hemani kwake; bali aliwazuia wale watu mia tatu; na kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake, bondeni.

 

Kutokana na uchaguzi huu, kupunguzwa kwa idadi ya watu kulifanyika. Hii ilfanyika ili ushindi usichukuliwe kuwa umetokana na uweza bali ni kwa roho wake, asema Bwana wa Majeshi (Zekaria 4:6).

Jaribio lilikuwa ni kupambanua katika Roho Mtakatifu. Maji yalikuwa ni mfano wa Roho Mtakatifu alitenda kazi zake kupitia kwa Yesu Kristo. Namna waliyochukulia ilionyesha mpambanuo ulioonyesha kumjua Mungu Mmoja na Wapekee wa Kweli na Yesu Kristo aliyemtuma (Yohana 17:3).

 

Makundi matatu yaliundwa kutoka kwenye kundi ambayo yalikuwa yamechaguliwa kutok kwenye kundi ambalo limepunguzwa tayari, ikimaanisha sio Israeli wote wameitwa. Wale waliorepotiwa kazini ndio walioitwa. Thelathini na mbili elfu waliripoti kwenda vitani na, kwa mujibu wa Torati kutokana na maagizo ya Kumbukumbu la Torati 20, wale waliokuwa wanaogopa kwenda vitani waliruhusiwa warudi majumbani kwao. Watu elfu kumi walijiondoa na kurudi nyumbani. Waliobakia hatimaye wakapewa jaribio la kwenye maji mtoni. Ndipo hatimaye watu 300 tu walibakia.

 

Jambo la ajabu na la tofauti hapa lilikuwa ni tofauti kati ya 4 kwa 1.waliongezeka dhidi yao hadi watu 13 kwa 1, na kisha hadi kufikia watu 450 kwa 1.

 

Tofauti ya mwisho kiuwiano ilikuwa kubwa sana sawa na idadi ya makuhani wa Baali waliokuwa wanakula mezani kwa  Yezebeli, kwenye dini yao, wakati Eliya alikabiliananao peke yake (1Wafalme 18:19). Pia Eliya alikabiliana na manabii mia nne wa ashera. Miingano huu unamaana yake, hata hivyo, kwa kuwa ni Kahaba Mkuu atakayepinduliwa na kuangamizwa katika Siku za Mwisho.

 

Roho hii ya Eliya inatendakazi kwene Kanisa na mfumo au imani yake yote linaporuka na kuendelea kupambana dhidi ya mfumo au imani ya dini ya uwongo kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu mbili. Ni katika Siku za Mwisho tu ndipo litafanikiwa, na pia sio kikamilifu kwa matendo yake lenyewe.

 

9 Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Ondoka, shuka kambini; maana nimeitia katika mikono yako. 10 Lakini, ukiogopa kushuka, shuka pamoja na Pura mtumishi wako kambini; 11 nawe utasikia wanayoyasema, na baada ya haya mikono yako itatiwa nguvu; ushuke kambini. Ndipo akashuka pamoja na Pura mtumishi wake hata kufikilia mwisho wa watu wenye silaha waliokuwa kambini. 12 Nao Wamidiani na Waamaleki na, hao wana wa mashariki walikuwa wametua bondeni, mfano wa nzige kwa wingi; na ngamia zao walikuwa hawana hesabu; mfano wa mchanga wa ufuoni, kwa wingi. 13 Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, naliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika hata hema moja, ukaipiga hata ikaanguka, nao ukaipindua, hata ikalala chini. 14 Mwenzake akamjibu akasema, Habari hii haikosi kuwa upanga wa Gideoni, mwana wa Yoashi, mtu wa Israeli. Mungu amewatia Wamidiani na jeshi lote katika mkono wake.

 

Unabii huu ulitolewa na Mungu kwenye mikono ya adui na wakapunguzwa nguvu kabisa nao, ili waweze kutiwa moyo wakati adui akiwa amekata tamaa.

 

15 Ikawa, aliposikia habari ya ile ndoto, na kufasiriwa kwake, akasujudu; akarudi katika jeshi la Israeli akasema, Inukeni, kwa maana Bwana amelitia jeshi la Midiani mikononi mwenu.16 Kisha akawapanga wale watu mia tatu wawe vikosi vitatu, akatia tarumbeta katika mikono ya watu wote, na mitungi isiyo maji, na mienge ndani ya hiyo mitungi. 17 Akawaambia, Nitazameni, mkafanye kama nifanyavyo mimi; angalieni, nitakapofika mwisho wa kambi, itakuwa, nifanyavyo mimi nanyi fanyeni kadhalika. 18 Nitakapopiga tarumbeta, mimi na wote walio pamoja nami, basi ninyi nanyi zipigeni tarumbeta pande zote za kambi, mkaseme, Kwa Bwana, na kwa Gideoni. 19 Basi Gideoni, na wale watu mia waliokuwa pamoja naye, wakafika mwisho wa kambi, mwanzo wa zamu ya kati, wakati walipokuwa wamebadili wenye zamu; wakazipiga hizo tarumbeta, wakaivunja vipande vipande ile mitungi iliyokuwa mikononi mwao. 20 Vile vikosi vitatu wakapiga tarumbeta, wakaivunja mitungi, wakaishika mienge kwa mikono yao ya kushoto, na zile tarumbeta katika mikono yao ya kuume ili kuzipiga; wakapiga kelele, Upanga wa Bwana na wa Gideoni. 21 Wakasimama kila mtu mahali pake kuizunguka kambi pande zote; jeshi lote wakakimbia; nao wakapiga kelele, wakawakimbiza. 22 Wakazipiga zile tarumbeta mia tatu, naye Bwana akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia mpaka Bethshita, kuendelea Serera, hata mpaka wa Abel-Mehola, karibu na Tabathi.23 Wanaume wa Israeli walikuwa wamekusanyika kutoka Naftali, na kutoka Asheri, na kutoka Manase yote, wakawafuata Midiani.

 

Akiwa na wanaume mia tatu aliwapanga kwa uzuri na kwa makini kwenye makundi matatu, na akafanikiwa kufanya jambo la kushangaza. akisaidiwa na \mungu mwenye nguvu aliwaondoa woga mioyoni mwao na akawasababisha wafanye mauaji makuu kwa adui mmoja baada ya mwingine.

 

Kisha Waefraimu wakaitwa kama kundi kuwashughulikia na walijisikia uchungu kuachwa nje ya tukio hili. Hata hivyo, unabii mwingine ulionyesha dalili ya kwamba Dani/Efraimu pia walihusika kwenye harakati hizi za kuwaonya watu duniani katika Siku za Mwisaho (Yeremia 4:15) (sawa na jarida la Maonyo ya Siku za Mwisho (Na. 44) [The Warning of the Last Days (No. 44)].

24 Kisha Gideoni akapeleka wajumbe katika nchi yote ya vilima vilima ya Efraimu, akisema, Haya, telemkeni juu ya Midiani, na kuyashika hayo maji mbele yao, mpaka Bethbara, maana, huo mto wa Yordani. Basi watu waume wote wa Efraimu walikutana pamoja, wakayashika maji mpaka Bethbara, maana, huo mto wa Yordani. 25 Wakawashika hao wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu; wakamwua huyo Orebu pale penye jabali la Orebu, na huyo Zeebu wakamwua hapo penye shinikizo la divai la Zeebu, kisha wakawaandamia Wamidiani; vichwa vya Orebu na Zeebu wakamletea Gideoni huko ng'ambo ya pili ya Yordani.

 

Kwa hiyo, dini ya Baali katika siku za mwisho imepinduliwa na kuangushwa. Lakini ni kina nani basi hawa manabii wa Baali katika siku za mwisho? Ni rahisi kuwajua kutokana na maandiko ya bibliaical text.

 

Ni makasisi waliovaa mavazi meusi. Inawezakuwa ndiyo utambulisho wao wa kimavazi kwenye milenia.

Sefania 1:4 4 Nami nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani;

 

Ni rahisi mno kuona kwenye tafsiri ya KJV.

 

Sefania 1:4 4 Nami nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani;

 

Je, ni kina nani huyu Mkerani? Neno hili limeachwa pasi kutafsiriwa kwenye tafsiri ya KJV, na linalenga makasisi waabudu sanamu kwenye tafsiri ya RSV, kwa kuwa inamaanisha moja kwa moja mwene vazi jeusi; na tafsiri iliyo kwene KJV wote ni sehemu ya makasisi au makuhani wa dini yenye mavazi meusi, kwa hiyo, ni kwa makusudi kabisa imeacha bila ya kutafsiriwa. Bullinger ana la maana aliloandika kuhusiana na tafsiri ya The Companion Bible. Maandiko kwenye Hosea 10:3 pia yameachwa bila kutafsiriwa, kama yalivyo kwenye 2Wafalme 23:5.

 

Hosea 10:3-5 Yakini sasa watasema, Hatuna mfalme; kwa maana hatumchi Bwana; na mfalme huyu je! Aweza kututendea nini? 4 Hunena maneno yasiyo na maana; huapa kwa uongo wafanyapo maagano; basi ndipo hukumu huchipuka kama mbaruti katika matuta ya shamba. 5 Wakaao Samaria wataona hofu kwa ajili ya ndama za Beth-Aveni; kwa maana watu wa mji huo wataulilia, na makuhani wake walioufurahia, kwa sababu ya utukufu wake; kwa maana umetoweka.

 

Neno makuhani lililopo kwenye aya ya 5 kwa kweli linamaanisha Kemarim au Chemarim, linalomaanisha mwenye vazi jeusi. Neno hili mara zote limekuwa halieleweki kuwa linamaaiisha makuhani wa Baali, ndiyo peke yao waliokuwa wanavaa mavazi au majoho haya meusi.

2Wafalme 23:5 Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni.

 

Makuhani waabudu sanamu wanaoonyeshwa hapa ni sawa tu na Kemarim aliyeko kokote kule. Wanachukuliwa kama makuhani waabudu sanamu ili kuficha ukweli wa mambo. Makuhani au makasisi wanaomtumikia Mungu wa Pekee na wa Kweli, kamwe hawakuvaa na hadi sasa havai majoho meusi. Mara zote walivaa meupe.

 

Wenye majoho meusi wamekuwa wakijaribu kuumiliki Yerusalemu tangu kipindi Daudi alipoingia humo mwaka 1005 KK nab ado wangaliko kule wakijaribu kufanya hivyo.

 

Katika Siku za Mwisho, makuhani wavaa majoho meusi wa Mwanamke Kahaba wataangamizwa, na kuondolewa usoni pa Dunia kabla ya utaratibu na dini ya Masihi haijachukua mkondo wake kikamilifu, na kazi hiyo itafanywa na utawala wa Mnyama ambao alijaribu kuumiliki.

 

Ni jukumu na kazi ya Kanisa kuhubiri Ujumbe wa Malaika wa Kwanza na kuifunua dini na itikadi hii katika Siku hizi za Mwisho kwenye Ujumbe wa Malaika wa Pili (sawa na isemavyo Ufunuo sura ya 17 na 18).

 

Ujumbe wa Malaika wa Tatu

Ufunuo 14:9-20 9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, 10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. 11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake. 12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu. 13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

 

Mazingira hapa ni kwamba Mnyama ataweka mfumo utakaofanya maangamizo ya wazi kati ya Mungu na mfumo au dini yake na ule wa kishetani wa Mnyama. Sehemu kubwa ya dunia inaonekana kufuata ama kwenda kwenye mfumo au dini hii.

 

Uvumilivu wa watakatifu umetolewa nwito kuwepo, na tofauti ya alama ya watakatifu ni amri za Mungu na imani ya Yesu. Imani ya Kristo ni ile kwamba hakupenda maisha yake hadi kufa. Na ndivyo ilivyo pia kwa wateule tutapitia mateso katika nyakati hizi za mwisho. Msimamo huu wa mwisho wa dola ya Mnyama utakuwa ni tukio kuu sana la kuifunga kinywa dunia yote.

 

14 Kisha nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali. 15 Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa sauti kuu yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa. 16 Na yeye aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu wake juu ya nchi, nchi ikavunwa. 17 Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali. 18 Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana. 19 Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu. 20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili.

 

Mambo haya mawili yanaonyesha mavuno ya Mwana wa Adamu, ambayo ndiyo mavuno ya mwisho, na kisha mavuno ya shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu.

 

Kuna matukio mawili tofauti kwene jumbe mbili tofauti na viumbe. Ziko kwene maelekezo na maongozi ya Mungu, ambayo yanaonyesha matukio mawili kwenye matukio maalumu zinazochukuliwa na wajumbe au malaika wawili kwa nyakati tofauti.

 

Kwa hiyo, imani katika Siku za Mwisho imefunuliwa kupitia mchakato wa mafundo manne unaohitiisha Siri za Mungu.

 

Ujumbe wa Malaika wa Kwanza ni Injili ya Milele na kama ilivyo, haihitajiki kuibadilisha, na ina muundo na utaratibu ule ule tangu kipindi cha Kristo na Mitume. Kwa hiyo haiwezi kuwa ni imani ile ya makanisa makongwe ya kale inayotuama au kwendana na mafundisho potofu ya wanadamu au yaliyotungwa na Mabaraza ya Makanisa.

 

Ujumbe wa Malaika wa Pili unauvunjavunja mfumo na dini ya Kibabeloni. Ujumbe ule unatuama au kujengwa juu ya kazi ya mwisho ya Injili yote iliyo kwenye Ujumbe wa Malaika wa Kwanza.

 

Ujumbe wa Malaika wa Tatu unatoa maonyo juu ya mfumo au dini ya Mnyama, ambaye atamuangamiza Mwanamke Kahaba.

 

Jumbe za Malaika wa Nne na wa Tano

Ujumbe wa Malaika wa Nne una sehemu mbili, ya kwanza ikiwa ni mavuno au mshahara wa (mtu ambaye kuonekana kwake ni kama) Mwana wa Mungu).

 

Sehemu ya Pili ya Ujumbe wa Malaika wa Kwanza ni shinikizo la kikombe cha ghadhabu ya Mungu.

 

Kwa michakato hii ya jumbe tano, ndipi kipindi cha Milenia kitafunika jumla ya miaka 1,000-ya utawala wa Kristo.

 

Soma pia majarida yafuatayo:

Vita Kuu ya III ya Dunia: Sehemu ya I Dola ya Mnyama (Na. 299A) [World War III: Part I The Empire of the Beast (No. 299A)]

Vita Kuu ya III ya Dunia: Mwanamke Hakaba na Mnyama (Na. 299B) [WWIII Part II: The Whore and the Beast (No. 299B)]

Mwaka 2012 na Mpingaktisto )Na. 299D) [2012 and the Antichrist (No. 299D)]

Yubile ya Dhahabu na Milenia (Na. 300) [The Golden Jubilee and the Millennium (No. 300)]

 

q