Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[CB4]

 

 

 

Uumbaji wa Familia ya Mungu

 

(Nakala 4.020021116 – 20061104 – 20071225)

 

Hapo Mwanzo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu kulikuwako na Mmoja. Hakutokea kuwako kwa sababu alikuwako tangu mwanzo. Eloah ndilo jina lake na ni Roho. Aliamua kujiongeza Mwenyewe kwa kuumba Familia inayofanana na yeye mwenyewe. Naye alifanya kila taifa la Wanadamu kutoka katika Mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani na mipaka ya makazi yao,  kwa maana ndani yake yeye tunaishi tunakwenda na kuwa na uhai wetu maana sisi sote tu wazao wake. Somo hili linatuonyesha jinsi ya Uumbaji huo ulivyoanza hadi mwisho wake ambapo Wanadamu watakuwa ni sehemu ya Familia ya Mungu.

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Haki milki © 2002, 2005, 2006, 2007, Diane Flanagan, na Wade Cox)

 

Somo hili linaruhusiwa kunukuliwa, na kusambazwa kwa yeyote mradi tu kama litanukuliwa kikamilifu, bila kubadilishwa au kuondoa namna halisi, Jina la Mchapishaji na anuani yake na tangazo la hati milki lazima vijumlishwe. Hakuna gharama yoyote ipaswayo kuchangiwa na mtumiaji na hairuhusiwi kuuzwa nakala zake kwa msomaji. Nukuu chache zaweza kuchukukuliwa katika makala zinazo tofautiana kimtazamo na kimaoni bila kukiuka maadili ya haki milki.

 

Somo hili linapatikana pia katika Tovuti zetu popote Duniani

 

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


 

 

Uumbaji wa Familia ya Mungu




Hapo Mwanzo:

Mungu Mmoja na wa pekee wa kweli alikuwako tangu mwanzo. (Yn.17:3; 1 Yoh. 5:20). Alikuwa Mwenyewe wa pekee na wa Milele. Eloah ndilo Jina lake, katika lugha ya Kiebrania. Elaha ndilo Jina lake katika lugha ya Kikalidayo. Maana yake ni Mmoja au Moja. Anajua yote na kutenda yote. Daima hawezi kufa. Yeye peke yake ni wa Milele. (1 Tim. 6:16). Yeye ni Alpha (maana yake yeye ni mwanzo) tena ni Omega (maana yake yeye ni mwisho) (Ufu. 1:8). Anatenda kazi daima. Uumbaji umekuwako kwa sababu ya yeye. Yeye ndiye chanzo cha mambo yote yaliyokuwako na yaliyoko na yajayo. Kwa hiyo, Mungu anajiongeza yeye mwenyewe kwa kujiumba. Na Mungu alimwambia Musa, “MIMI NIKO AMBAYE NIKO” Hivi ndivyo utakavyowaambia Wana wa Israeli; “MIMI NIKO” amenituma kwenu” (Kut. 3:14). Mungu anasema hapa: “Nitakuwa kama Nitakavyokuwa “(Kutoka katika waraka wa Biblia ya (Companion).

 

Kwa ufafanuzi kuhusu Mungu Baba soma katika Somo la Mungu ni Nani? (Na. CB1).

 

Katika Uumbaji, Mungu hapo Mwanzo alimtoa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni Uweza na Nguvu za Mungu, lakini hakuwako peke yake mbali na Mungu, hadi hapo Mungu alipomtoa Roho wake katika kazi ya Uumbaji. Kwa hiyo Roho Mtakatifu alianza kutenda kazi hapo Mungu alipoanza kazi ya Uumbaji. Baada ya hapo Wana wa Mungu waliumbwa, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu katika Nguvu na Uweza wa Baba.

Ulimwengu wa Kiroho, Ulimwengu huu wa sasa na vitu vyote vilivyomo viliumbwa katika uwezo na nguvu ya Roho Mtakatifu ili mwisho wa yote Mungu, “awe yote katika wote” (Efe. 4:6). Roho Mtakatifu ndiye kiungo cha mambo yote ya Uumbaji wa yote, (Roho ndiyo kiungo cha  Uumbaji).

 

Tazama Somo la Roho Mtakatifu ni Nini? (Na. CB3).

 

Sheria za Mungu ni:

 

Sheria za Mungu zilikuwako tangu mwanzo. Ni katika Ubatizo na kupokea Roho Mtakatifu na kushika Amri za Mungu na kwa kula Karamu ya Pasaka ndipo tutakapoenenda sawasawa na Mapenzi ya Mungu.

 

Uumbaji wa Kiroho:

Uumbaji wa Kiroho (Malaika) ndiyo ulikuwa Mpango wa kwanza wa Mungu katika Uumbaji. Na ndiyo ulikuwa mwanzo na msingi wa Uumbaji wa vitu vyote (Wanadamu). Vitu vyote vya Kiroho na Kimwili hutenda kazi pamoja katika Utukufu wa Mungu. Wana wa Mungu wanaitwa Elohim. Huu ni wingi wa neno ambalo lina maana ya kwamba kuna Wana zaidi ya mwana mmoja wa Mungu. Mungu aliumba wana wengi, (Kum. 32:8; Ayubu 1:6; 2:1; 38:4-7). Na hapo ndipo Mungu akawa Baba kutokana na Uumbaji wake au kwa kuzaliwa kwa Wana hawa wa Kiroho. (Ebr. 12:9). Maandiko hayataji idadi kamili ya Wana hawa wa Kiroho. Lakini kutoka katika Ufunuo 5:11 tunajifunza hivi;

 

Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu.

 

Mungu ana Mpango. Ameweka utaratibu wa kukamilisha Mpango wake. Mpango Mkuu wa Mungu ni kuwafundisha  wana wake na kuwa  watakatifu kama Yeye alivyo Mtakatifu. Mungu ni Upendo (1 Yoh. 4:8). Upendo wa Utakatifu wa Mungu unahusika katika kila kitu, na anashirikiana na Wana  wa Kiroho pamoja na Wana wa Kimwili. Wana wa Kiroho wa Mungu hawakuelewa  mambo yote ya Mungu aliyoyatenda, Ufunuo 1:1 inasema;

 

“Ufunuo wa Yesu Kristo (kwa Yohana) aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi”; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana.

 

Wana wa Kiroho walitakiwa kuonyesha uvumilivu na subira hadi siri za Mungu zitakapofunuliwa (kwa hatua) kwa wanadamu, ili na wao vilevile waweze kuelewa Mpango wa Mungu. Biblia inatuambia ya kwamba mambo ambayo Malaika wanatamani kuyachungulia (1 Pet. 1:12).

 

Yesu Kristo ndiye alikuwa Mzaliwa wa kwanza Mwana wa Mungu:

Yesu Kristo alikuwa mmoja wa waliyoumbwa (au kuzaliwa) kati ya wana wa Kiroho wa Mungu. Yeye ni Mwanzo wa Uumbaji wa Mungu (Kama Mtawala wa kwanza katika ngazi ya Juu zaidi) (Ufu. 3:14), Mzaliwa wa kwanza wa Viumbe vyote (Kol. 1:15) Vitu vyote viliumbwa katika Kristo. (Kol. 1:16), lakini Uumbaji wote ulifanyika katika Mapenzi ya Mungu Baba.

 

Yesu Kristo ndiye alikuwa Mzaliwa wa kwanza Mwana wa Mungu:

Yesu Kristo alikuwa mmoja wa waliyoumbwa (au kuzaliwa) kati ya wana wa Kiroho wa Mungu. Yeye ni Mwanzo wa Uumbaji wa Mungu (Kama Mtawala wa kwanza katika ngazi ya Juu zaidi) (Ufu. 3:14), Mzaliwa wa kwanza wa Viumbe vyote (Kol. 1:15) Vitu vyote viliumbwa katika Kristo. (Kol. 1:16), lakini Uumbaji wote ulifanyika katika Mapenzi ya Mungu Baba.

 

Masihi alikuwa ni Mwana – Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia (Ufu. 13:8) Kristo alikuwa ni Mtiifu na Mwaminifu katika Mpango wa Baba yake, na alitimiza mapenzi yote ya Mpango wa Baba yake, katika mauti yake Yesu Kristo alitimiza Sehemu ya Mpango wa Mungu katika Ukombozi wa Mwanadamu na Jeshi lote la Mbinguni. Alitiwa mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzake wote, (Zab. 45:7; Ebr. 1:9). Jifunze zaidi kuhusu Yesu Kristo kutoka katika somo la Yesu ni nani? (Na. CB 2).

 

Hebu na tuangalie sura ya Mungu katika Maumbile ya Kiroho.

 

Kiti cha Enzi cha Mungu:

Ufunuo sura ya 4 na ya 5 inatupa mwanga wa sura ya Kiti cha Enzi cha Mungu jinsi kinavyoweza kuonekana. Sura hizi zote mbili zinamwelezea Mungu akiwa amekalia Kiti chake cha Enzi Mbinguni kikiwa kimezungukwa na Upinde wa Mvua sehemu zote. (Ufu. 4:3). Pia kuna viti 24 vinavyokizunguka, kile Kiti cha Enzi, na juu ya vile viti wameketi juu yake wazee 24, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu (Ufu. 4:4).

 

Na mbele ya kile Kiti cha Enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri, na katikati ya kile kiti cha Enzi, na pande zote za kile Kiti walikuwako wenye uhai wanne (Ufu. 4:6). Yesu Kristo ameketi katika Mkono wa kulia wa Baba (Mk. 16:19; Lk. 22:69; Matendo 7:55; Warumi 8:34). Zaburi 82:1,8 pia kuna habari kuhusu Mungu akiwa katika kusanyiko lake, na inaelezea jinsi Mungu anavyofanya hukumu yake. Kumbukumbu nyingine zinazoonyesha kuhusu kusanyiko la Baraza la Mungu zinazopatikana katika Zab. 86:8; 95:3; 96:4,5; 97:7,9; 135:5; 136:2; 138:1 Tunajifunza kuhusu Kiti cha Enzi cha Mungu katika Sehemu za kaskazini katika Isaya 14:13, na katika II Wakorintho 12:2 inatueleza ya kwamba ni katika Mbingu ya tatu.

 

Roho saba walio katika mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu:

Ufunuo 1:4 inatuambia ya kwamba kuna Roho Saba walio mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu. Na Ufunuo 4:5 inatufahamisha ya kwamba kuna taa saba za moto ziwakazo mbele ya kile Kiti cha Enzi cha Mungu, ndizo Roho saba za Mungu.

 

Zekaria 4:3 inaelezea mizeituni miwili pembeni mwa vinara saba vya dhahabu pamoja na zile nyota saba, ambazo ni Roho Mtakatifu anayebubujika katika Makanisa saba. Ufunuo 1:20 inaonyesha ya kwamba vile vinara saba ni makanisa saba na ile mizeituni miwili ni mashahidi wawili (Zek. 4:11-14)

 

Viumbe Wanne wenye Uhai:

Ezekieli 1:5-28 anatufahamisha habari zaidi kuhusu kile Kiti cha Enzi cha Mungu. Ezekieli 1:10 anaelezea habari za vile viumbe wenye uhai;

 

Kwa habari za mfano wa nyuso zao, walikuwa na uso wa mwanadamu; na hao wanne walikuwa na uso wa simba upande wa kuume, na hao wanne walikuwa na uso wa Ng’ombe upande wa kushoto, na hao wanne walikuwa na uso wa tai pia.

 

Ufunuo 4:7-8 pia inaelezea Viumbe wenye Uhai.

 

Kila mmoja wa hao viumbe wanne wenye uhai anawajibika katika sehemu moja ya robo katika sehemu yote yenye robo nne za Uumbaji wa Mungu. Mungu Baba yeye yuko katikati kabisa ya hawa viumbe wanne wenye uhai, na viumbe wanne wenye uhai ni kama ifuatavyo hapa chini.

 

Wazee 24:s

Ufunuo 4:4 inatuambia ya kwamba kuna wazee 24, ambao wamevikwa mavazi meupe na kuvikwa taji ya dhahabu katika vichwa vyao, wameketi katika viti 24 vinavyozunguka Kiti cha Enzi cha Mungu. Tumejifunza ya kwamba Wazee ishirini na wanne wanasujudu kwa kuinama mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu, kutoka katika Ufunuo 5:14 na 19:4. Wazee 24 pia wanasimamia maombi ya Watakatifu (Ufunuo 5:8) kuna wazee sita ambao wanawajibika katika kila sehemu ya robo moja ya eneo lote lenye robo nne za eneo (6x4=24)

 

Kazi ya Mduara wa Ndani na wa Nje:

Wazee 24 wanaozunguka Kiti cha Enzi cha Mungu, wanafanya Baraza (Council). Baada ya Masihi kutiwa mafuta kuliko wenzake wote na kukubalika kuwa mganda uliotikiswa na kukubalika kuwa sadaka iliyo bora zaidi, muundo wa Baraza la Kiti cha Enzi cha Mungu unakuwa kama ifuatavyo hapa chini;

 

Jumla ya idadi yote hapa ni 30, ambayo ni idadi inayofanya Baraza la ndani la Mungu aliye Juu sana Aliyetukuka. Baraza la nje linajumlisha wazee wengine 40 wanaofanya idadi ya wajumbe wote wa baraza kuwa 70. Kundi la nje lenye wazee wanne kila moja kutoka katika kundi la wale Wazee 40 wa Baraza la Nje, wanasaidiana na wale viumbe wenye uhai na kundi la Baranza la ndani la wazee 24 likiwa limegawanyika katika kundi la wazee sita sita, wanasaidia katika utawala wa sheria za Mungu. Robo kila kundi likiwa na mamlaka katika robo ya eneo lao.

 

Kuna kumbukumbu nyingi katika idadi ya namba hii ya 70 katika Maandiko. Kihistoria inaonyesha ya kwamba Musa aliwatia mafuta wazee 70 (Hes. 11:24-26). Hata katika Baraza la makuhani (Sanhadrin), ambalo ndilo lilikuwa Baraza kuu la Utawala wa Wana wa Israel lilikuwa na jumla ya idadi ya Wazee 70 wa Baraza lote. ( tazama pia Kut. 24:1,9; na Lk. 10:1,17).

 

Huu ndiyo ulikuwa asili ya Muundo wa Utawala wa Baraza la Mungu tangu awali, kutoka katika Maandiko tunaona jinsi Mungu anavyopanua Baraza lake, na tutazungumzia jambo hili kwa undani zaidi baadaye. Mungu atawaweka pia viumbe wapya kushika mamlaka ya tangu awali yaliyoachwa wazi kwa sababu ya maasi ya Jeshi la Mbinguni.

 

Uumbajii wa Mbingu na Nchi:

Baada ya Mungu (Eloah) kuumba Jeshi la Mbinguni, aliuumba dunia na vitu vyote vilivyomo.

 

Hapo mwanzo Mungu aliumba Mbingu na Nchi (Mwa. 1:1)

 

Ayubu 38:4-7 anazungumzia jinsi zilivyo Kuu Utajiri na Hekima na Maarifa ya Mungu. Inaelezea hapo Nyota za asubuhi zilivyoimba pamoja na wana wote wa Mungu. Zilipopiga kelele kwa furaha, Mungu (Eloah) alipoiumba sayari hii ya dunia.

 

Nyota ya Asubuhi, Kerubi na Seraphimu wote kazi zao na vyeo vyao ni tofauti katika kuwahudumia Wana wa Kiroho wa Mungu. Hata hivyo Malaika, (maana yake ni  mjumbe) hawakuhesabiwa kama wana wa Mungu mpaka baada ya Uumbaji wa Adamu. Mpaka wakati huo hapakuwa na haja ya kuwako kwa wajumbe. Angalia katika Somo la Jeshi la Mbinguni (Na. CB28).

 

Katika Uumbaji wa Dunia, Lusifa (maana yake Nyota yenye kug’aa) pamoja na Wana wengine wa Mungu walipewa mamlaka katika Sayari na kuamriwa kuiangalia pamoja na watu wote watakaowekwa katika sayari hiyo.

 

Dunia ni ya zamani sana. Wakati mmoja wanyama wa kale na viumbe wengine waliishi katika sayari hii. Inaonekana ya kwamba katika miaka mingi iliyopita, tufani kuu ilipiga dunia na kuuwa wanyama wengine waliokuwako katika historia.

 

Maaasi ya Lusifa:

Lusifa aliumbwa amejaa hekima na ukamilifu wa uzuri, kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikae katika Kiti cha Enzi cha Mungu. (Eze. 28:12-15). Alikuwa Mkuu na mwenye mamlaka katika mlima Mtakatifu wa Mungu, akitembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Alipewa mamlaka makuu katika Uumbaji wa ulimwengu wa Kiroho, na baadaye akapewa mamlaka katika duniani na vitu vyote vilivyomo. Alikuwa na cheo cha Nyota ya Asubuhi ya Sayari (Eze. 28:12). Lusifa alikuwa Mkamilifu katika njia zake tangu siku ile alipoumbwa, mpaka uovu ulipoonekana ndani yake (Eze. 28:15).

 

Lusifa alijaribu kouongoza Maasi dhidi ya Mungu Baba. Alisema “Nitapanda mpaka Mbinguni, nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu” (Isa. 14:13,14). Lusifa pamoja na theluthi moja ya Jeshi la Mbinguni walimwasi Mungu (Ufu.12:4). Wengine wanaamini ya kwamba nusu ya Baraza la ndani walimfuata Lusifa katika kumwasi Mungu Baba. Kwa sababu Lucifa alichagua kuasi, jina lake lilibadilika na kuitwa Shetani, ikiwa na maana ya Adui, au Mshitaki (wa ndugu zetu) (1 Pet. 5:8; Ufu. 12:10; Zek. 3:1). Adui ni mtu yule ambaye wakati wote, huhakikisha ya kwamba anatuangamiza sisi sote. Nafasi aliyoishika Shetani kama Kerubi katika kiti Enzi cha Mungu iliachwa wazi baada ya maasi yake.

 

Ezekieli 41:18-19 inaelezea jambo katika siku zijazo ambapo nafasi zilizoachwa wazi katika Baraza la ndani na la nje katika Kiti cha Enzi cha Mungu ya kuwa zitajazawa na viumbe wa dunia hii waliokuwako tangu mwanzo. Watu hawa ni wale waliokufa katika kifo cha kawaida na watafufuliwa kutoka katika ufufuo wa wafu na kubadilika na kuwa Wana wa Kiroho hapo Yesu atakaporudi mara ya pili. Wale waliomtii Mungu pamoja na sheria zake, wakati walipoishi katika umbo la kibinadamu. Hata hivyo wengine walichagua mauti kwa kutomtii na kumkana Mungu Mmoja wa kweli.

 

Hapo Shetani na Jeshi lililoanguka lilipofanya maasi, mambo yote yalibadilika na kuwa tofauti milele. Kama Lusifa, pamoja na Wana wengine wa Kiroho wa Mungu walikuwa wameumbwa Wakamilifu, lakini wote walikuwa na Uhuru wa kuchagua, kama ilivyo kwa wanadamu wote.

 

Ingawaje dunia iliumbwa kikamilifu, ilikuwa ukiwa na ilikuwa utupu (Mwa. 1:2). Inafikiriwa ya kwamba hii ilitokea baada ya maasi ya Lusifa. Lusifa na jeshi lililoanguka walitupwa chini katika dunia na kuwa tohu na bohu, ikiwa na maana ya iliyochafuka na utupu (isio faa kitu).

 

Uumbaji wa mwanzo:

Kulikuwa na aina ya viumbe waliofanana na mwanadamu walioishi hapo zamani za kale katika dunia, na walitambuliwa kuwa kama humanoids (yaani kiumbe kilichofanana na mwanadamu). Vilikuwa na mambo fulani tu yaliyofanana na mwanadamu wa sasa. Vilitembea kwa miguu miwili, lakini vilifikiriwa na kutenda tofauti na Mwanadamu wa siku hizi, ulikuwa ni uumbaji wa jeshi liloanguka. Mungu Baba hakuwa na mpango wa viumbe hawa wa kuishi diniani.

 

Kumbuka Malaika hawakujua Mpango mzima wa Mungu, na hii ilikuwa ni jaribu moja wapo la Shetani la kufarakana na Mpango wa Mungu. Mungu Mmoja wa kweli hakutakasa Uumbaji wa viumbe hivi; kwa hali hiyo hawakuwa na njia ya kupokea Roho Mtakatifu wa Mungu. Biblia inatuambia ya kwamba wao wamekufa, hawataishi, wamekwisha kufariki hawatafufuka (Isa. 26:13-14).

 

Lusifa hakuonyesha uvumilivu wala hakuwa na Imani. Badala yake alianza vita mbinguni na kumwasi Mungu pamoja na Sheria zake. Hata hivyo shetani bado ndiye mtawala wa dunia hii ya leo, na yeye pamoja na jeshi la mbinguni lililoanguka bado wana nguvu za giza za kiroho. Shetani ni mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi hata sasa katika wana wa kuasi (Efe.2:2).

 

Uumbaji wa Sayari mpya pamoja na Uumbaji wa mwanadamu mpya

Mungu anatenda kazi kwa wakati na kwa kipindi maalumu. Mungu aliruhusu karibu kipindi cha mika 6,000, ya wakati huu wa sasa kuwa chini ya utawala wa Shetani, tangu wakati wa Uumbaji wa Adamu. Tuko karibu kumaliza kipindi cha miaka hiyo 6000 katika wakati huu wa sasa. Kipindi cha shetani kitasitishwa, shetani atafugwa katika kipindi cha miaka 1,000 ya mileniamu, na kutupwa kuzimu wakati wa Utawala wa Kristo Masihi, na Nyota mpya ya Asubuhi katika Sayari mpya, karibu itang’aa. Huu utakuwa ni utawala wa kipindi cha Haki.

 

Kwa hiyo katika wakati fulani, Dunia ilikuwa tupu na machafuko, kwa sababu ya maasi ya jeshi la mbinguni. Masihi ataumba nchi mpya ili iweze kuwa nchi kamilifu kwa mwanadamu, wanyama na sayari yenyewe, na ambayo itaendelea kuwa kamilifu milele na ambapo wote wataishi katika sheria na Amri zote za Mungu.

 

Kama vile kulivyo na utawala katika Kiti cha Enzi cha Mungu, kwa hiyo kutakuwa na utawala wa kila kitu. Kila siku wakati wa Uumbaji mpya, Masihi atatengeneza mambo yote kuwa tayari katika kusaidia katika maisha mapya.

 

Kwa kuwa Mungu alijua kila kitu tangu mwanzo. Alijua ya kwamba baadhi ya jeshi la mbinguni litaasi, kwa hiyo, Mungu Mmoja wa kweli katika Upendo usio na Ukomo (usio na mwisho) na Hekima, aliumba taratibu mbili; moja ya Kiroho na moja ya Kimwili. Kila moja ya utaratibu una uwezo na uhuru wa kufanya uchaguzi, kila aina ya utaratibu una mamlaka ya aina fulani. Wana wa Kiroho wa Mungu husaidia katika kuwalinda wanadamu. Tunalazimika kumwabudu Mungu Mmoja wa kweli na kutunza familia zetu pamoja na sayari hii, na kuwasaidia watu wote ili waweze kumjua Mungu Mmoja wa kweli. Taratibu zote za Kiroho na za kimwili zimethibitishwa katika Utendaji wake.

 

Mpango wa Mungu:

Katika Hekima yake, na kwa sababu ya Upendo wake katika Uumbaji wake wote. Mungu aliandaa Mpango wa upatanisho wa mwanadamu na Jeshi lake, ili wote waweze kumrudia tena Mungu Mmoja wa kweli. Kwa sababu Mungu ni Mungu Mmoja wa kweli, anaweza kuamua ni sadaka ya namna gani itakayompendeza. Wakati wa siku za Agano la Kale, watu walimwabudu Mungu Mmoja wa kweli kwa kutoa sadaka za ndama, mbuzi na kondoo kwa kutimiza wajibu wao katika utoaji wa taratibu za utoaji wa sadaka. Hata hivyo, sadaka hizi zote zilikamilishwa kabisa na Masihi, katika mauti yake pale juu ya mti (msalabani).

 

Hatuhitaji tena kuendelea kutoa sadaka za wanyama, lakini tunalazimika kuomba na kufunga na kukusanyika pamoja na kumwabudu Mungu Mmoja wa kweli katika wakati uliowekwa. Kwa mfano, wakati huu ni wakati wa sabato ya kila wiki, miezi mipya siku kuu na kwenye karamu.

 

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanae wa pekee, ili kila mtu amwaminie asipotee, bali awe nauzima wa milele (Yn. 3:16)

 

Yesu Kristo alikuwa Sadaka Takatifu na Kamilifu na Bora zaidi. Kristo alionyesha imani yake, maana hapo mwanzo alikuwa yu namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa namna ya  Mungu (katika hali ya Kiroho) kuwa ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa akawa ana mfano wa Wanadamu. Alimtegemea Mungu wake katika mambo yake yote aliyoyatenda. Na alitenda sawa sawa na Mapenzi na uweza wa nguvu katika maisha yake yote, hata alipopata kufufuka katika wafu na kuishi milele. Tena alipoonekana ana umbo kama la mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam mauti ya msalaba na kushinda mauti na kushi milele.

 

Yeye aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao, Alipowaumba wanadamu, aliweka mipaka ya watu kwa kadri ya hesabu ya wana wa Mungu (Kumb. 32:8 RSV)

 

Maneno haya yanamaanisha ya kwamba Mungu Mmoja wa kweli aliwagawia kazi wazee 70 wana wa Mungu. Yesu Kristo Masihi alikuwa na wajibu wa kuangalia taifa la Israel. Wana wa Israeli walitakiwa kujifunza kutoka kwa Yestu Kristo na kufuata mfano wake na matendo yake ambapo Yesu hakuwa na ubinafsi katika utendaji wake wa kazi, na kujitayarisha na kujiweka tayari kuutoa uhai wao kwa ajili ya wengine. Katika mauti yake, Masihi alikomboa Jeshi la mbinguni pamoja na wanadamu na kuwaleta katika Utukufu wa Mungu Mmoja wa kweli.

 

Tunapoitikia wito wake, na kutubu na kubatizwa, tunapokea Roho Mtakatifu. Tunaweza kwenda sasa kwa ujasiri mbele  ya kiti cha Enzi cha Mungu kwa maombi (Ebr. 4:16; 10:19-20). Ni lazima tutii sheria na amri za Mungu katika maisha yetu yote. Tunapofanya kosa na kutenda dhambi, ni lazima tutubu na kuomba msamaha wa Mungu naye atatusamehe angalia somo la Roho Mtakatifu ni nani? (CB3).

 

Ufufuo wa kwanza wa Mileniamu:

Masihi atakaporudi, watakatifu waliokufa katika Kristo, watafufuliwa kwanza. Kisha wale walio hai waliosalia hata wakati wa kurudi kwa Kristo mara ya pili, watanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili kumlaki Bwana hewani, wote watabadilika (1 The. 4:16-17). Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa (yaani huu mwili wa kufa uvae mwili wa kiroho wa kutokufa). Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililo andikwa, mauti imemezwa kwa kushinda. Watakatifu watanyakuliwa katika mawingu ili kumlaki Bwana hewani, na hivyo watakuwa pamoja na Bwana Kristo milele (1 Kor. 15:51-52).

 

Kanisa ambalo ni bibi arusi wa Kristo, litatwaliwa na Yesu Kristo, Masihi, katika wakati huo, wale walio wa ufufuo wa kwanza watakuwa na miili ya Kiroho, na watatawala pamoja na Kristo yaani watamiliki juu ya nchi, pamoja na Kristo miaka 1,000 ya Mileneumu.

 

Ni nini kitakachotokea kwa shetani?:

Baada ya miaka 6,000 kuisha, aliyopewa shetani, shetani atashikwa, yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni ibilisi na shetani, atafungwa miaka elfu, atatupwa katika kuzimu atafungwa, atatiwa muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie. Katika kipindi cha mileniamu, watu wengi watajifunza kuishi katika sheria za Mungu. Wataishi maisha ya ajabu, maisha ya furaha pamoja na watoto wao. Na hiyo miaka 1,000 ya mileniamu itakapokwisha, shetani atafunguliwa atoke kifungoni mwake kwa muda mfupi tu. Inangawaje watu watakuwa wanaishi katika maisha ya furaha na amani katika wakati huo, lakini wengine watafanya maasi kwa kudangaywa na shetani. Katika wakati huo.

 

Hayo ndiyo yatakayo kuwa maasi ya mwisho. Katika wakati huo shetani na jeshi lililoanguka wataondolewa hali ya kiroho na watafanywa kuwa wanadamu (Isa. 14:15-17).

 

Watu watasema:

Wao wakuonao watakukazia macho, watakuangalia sana, wakisema, Je huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, huyu ndiye aliyetikisa falme, aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? (Isa. 14:16-17)

 

Mungu hapendi Mpango wake wowote wa uumbaji ushindwe. Kwa hiyo Jeshi lililoanguka litapata nafasi ya pili (sasa kama wanadamu) ya kutubu na kustahili kuingia katika ufalme wa Mungu. Walakini hawarudishiwa mamlaka waliyokuwanayo kabla ya maasi. Lakini bora kuwa katika ufalme wa Mungu katika ngazi yoyote kuliko kwenda kwa kama Roho Mtakatifu.

 

Ufufuo wa Pili au Hukumu Kuu katika Kiti cha Enzi cha Mungu:

Baada ya maasi ya mwisho na baada ya kumalizika kwa miaka 7,000, hukumu Kuu katika Kiti cha Enzi cha Mungu itaanza. Katika kipindi hiki nchi itakuwa na wana wa Mungu wengi. Hao wana wa Kroho watakuwa wamevikwa taji zao kama wanadamu. Ni wale waliokuwa wakiishi katika njia ya Mungu tangu mwanzo.

 

Mwanadamu yeyote ambaye hakubahatika kufufuliwa katika ufufuo wa kwanza, anaweza kupata nafasi katika ufufuo wa pili. Ufufuo wa pili ni ufufuo wa hukumu (Isa.65:20) ambapo kila mtu atatimiza umri wa miaka 100 (sikukuu 2 za ukumbusho wa miaka 50 kila moja) ili waweze kuhitimu kuwa wana wa Mungu. Miaka ya mwanadamu ilikuwa miaka 120 (Mwa: 6:3) lakini katika kipindi cha Musa ilifupishwa na kuwa miaka sabini (Zab. 90:10). Katika Ufufuo wa pili umri wa kuishi kwa mwanadamu utakuwa miaka 120, kwa misingi ya kwamba mtu atafufuliwa akiwa na umri wa utu uzima, na kisha miaka 100 ya hukumu kwa ajili ya kujirekebisha (Angalia pia katika Mhu. 8:12).

 

Kwa sababu Mungu hapendi apoteze kitu chochote, ni wazi kwamba mambo yote mabaya na mawazo yote mabaya yatakapokuwa yameondolewa katika dunia hii, watu wataona uzuri wa kuishi katika utawara wa haki. Kwa neema ya roho mtakatifu wa Mungu inadhiirisha ya kwamba wanadamu na jeshi lililoanguka wanweza kupata nafasi ya kuwa wana wa Mungu katika ufufo wa pili (tazama katika 1 Kor. 15:28)

 

Sayari itabadilika kabisa katika kipindi hicho na kuwa tofauti kabisa na wakati huu wa sasa.

 

Kukabidhi Mamlaka kwa Baba:

Wakati Utafika ambao Kristo atakabidhi Mamlaka na Ufalme kwa Mungu Baba baada ya kuharibu falme zote, mamlaka na nguvu zote zinazopingana na Mungu. Kristo lazima atawale mpaka hapo atakapoweka maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. Kwa kuwa alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, vyote vimetiishwa, ni dhaili ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.  Basi vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu  vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote (1 Kor. 15:20-28, NIV).

 

Kisha Mungu Mmoja wa kweli atarudisha Kiti chake cha Enzi katika nchi (Ufu. 21:10).

 

Maandiko hayatwambii wazi wazi jinsi mambo yatakavyo tokea au kuwa katika wakati huo au baada ya wakati huo. Lakini jambo lililodhahiri na la wazi ni kwamba Mungu Mmoja wa kweli, ambaye tunampenda, na kumwabudu na kumtii ametuandalia mahali pa ajabu pazuri ambapo Jeshi lote la Kiroho pamoja na wanadamu wale waliomtii Mungu sasa watakuwa wamehitimu na kuwa wote Wana wa Kiroho wa Mungu na wataishi pamoja katika mahali hapo pa ajabu, palipoandaliwa na Mungu kwa ajili ya Wana wake, wa Kiroho.

 

Kuna mambo mengi yanayoendana na Mpango wa Mungu, lakini thawabu  na Baraka za Mungu ni nyingi mno.

 

Hebu sasa tuangalie jinsi Mungu anavyojipanua mwenyewe.

 

Upanuzi wa Duara la Ndani na Nje Kuzunguka Kiti cha Enzi cha Mungu:

Masihi atakaporudi tunaona ya kwamba arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari (Ufu. 19:7-10). Ni dhahiri ya kwamba wale walioshinda watawekwa katika Baraza la Utawala wa Mungu sawa sawa na vipaji vyao walivyojishindia. Kwa mfano wa Musa na Eliya watashika nafasi badala ya viumbe wenye uhai wawili walioasi. Pia tunaona ya kwamba mitume 12 wanapewa majukumu katika Baraza. Mitume 12 ambao kila mmoja atawajibika katika hukumu, kila mmoja atawajibika katika hukumu ya kabila 12 za Wana wa Israel (Mathayo 19:28; ufu. 21:15-16).

 

Orodha ya Mitume kumi na wawili ni kama ifuatavyo hapa chini:

1.         Petro

2.         Andrea

3.         Yakobo

4.         Yohana

5.         Filipo

6.         Bartholomeo

7.         Tomaso

8.         Mathayo

9.         Yakobo

10.       Tadeusi

11.       Simeoni

12.       Mathiya – aliyeshika mahali pa utume wa Yuda. (Mt. 10:2-4; Mdo 1:26)

 

Tunaweza kusadiki ya kwamba waamuzi 12 watakuwa na sehemu pia katika Baraza la Utawala.

 

Waamuzi kumi na wawili ni kama ifuatavyo hapa chini:

1)         Othanieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu (Amu. 3:7-11)

 

2)         Ehudi wa Benyamini (Amu. 3:12-20)

[Hata alipokufa Ehudi wana wa Israel wakafanya yaliyo maovu tena mbele za macho ya Bwana. Bwana akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani. Kwa maana hii shamgari hakuwa mwamuzi wa Israel kama tunavyoona katika Amu. 3:31; 4:4].

 

3) Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israel wakati ule. (Amu. sura ya 4-5)

 

4) Gidioni wa Manase (Amu. Sura ya  6-8);

 

[Abimeleki mnyag’anyi wa ufalme, mwana wa Gideoni kwa suria aliyekuwako Sekemu, alijitwalia ufalme kwa hila na kuwa mfalme wa udanganyifu. Hii ndiyo maana ya neno unsurper. Mnyang’anyi wa ufalme. Yeye hakuwa katika orodha ya waamuzi kumi na wawili ya wana wa Israeli, lakini alikuwa mfalme mdanganyifu yaani mfalme wa uongo].

 

5) Tola, mwana wa Pua mtu wa Isakari (Amu. 10:1-2)

 

6) Yairi Mgiliadi (Amu. 10:3-5)

 

7) Yefutha, Mgiliadi, mwana wa mwanamke kahaba (Amu. 11:1; 12:7).

 

8. Ibizani wa Bethlehemu (Amu. 12:8-10)

 

9) Eloni, Mzabuloni (Amu. 12:11-12)

 

10) Abdoni, mwana wa Hileli, Mpirathoni wa Efraimu (Amu. 12:13-15)

 

11) Samsoni jamii ya wadani, mwana wa Manoa (Amu. 13:16).

 

12) Eli (1 Sam. Sura ya 1-4).

 

Eli na Samweli walikuwa waamuzi wa mwisho wa Wana wa Israel. Samueli alikuwa nabii na mwamuzi wa Israel aliyemtia mafuta sauli na alitumika chini yake, lakini hakuwa mmoja wa wamuuzi kumi na wawili wa Israel. Kwa sababu baada ya kifo cha Eli utaratibu wa utawala wa kifalme ulianza.

 

Taratibu za Mwenendo:

Asili ya mwenendo na utaratibu wa utawala wa makabila kumi na mbili ya Wana wa Israeli, na mpango wa makazi yao kwa kila kabila inaonekana katika kitabu cha Hesabu sura ya 2:3-31 na mabadiliko yaliyofanyika kutokana na mwenendo wa utaratibu huo unaonekana katika Ezekieli sura ya 48.

Kuanzia mashariki utaratibu ulikuwa kama ifuatavyo:

           Yuda

           Isakari

           Zabuloni

           Reubeni

           Simoni

           Gadi

           Benyamini

           Manase

           Efrahimu

           Naftali

           Asheri

           Dani

 

Tunaona katika hekalu la badaye la Ezekieli kuna mabadiliko yaliyofanyika kama ifuatavyo;

           Yusufu

           Benyamini

           Dani

           Simeoni

           Isakari

           Zabuloni

           Gadi

           Asheri

           Naftali

           Reubeni

           Yuda

           Lawi

 

Kila kabila linatengewa Mtume mmoja katika makabila matatu yaliyogawanyika katika robo nne. Lakini haya makabila 12 sio ndiyo pekee ambayo ni wazawa wa Ibrahimu.

 

Mwana wa kwanza wa Ibrahimu alizaliwa na Hajiri, mtumishi wa kike wa kimisri, aliyemtumikia sarai. (Mwa 16:1). Jina la mwana huyo aliitwa Ishmaeli. Mama yake alimwoza mwanamke wa kimisri (Mwa. 21:21). Ishmaeli anasomwa katika Mwa. 16:11,15; 21:20; 39:1 na katika waamuzi 8:24. Agano la milele ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu na lililotimizwa katika Isaka linatajwa katika Mwanzo 17:20. Wana wa Ishmaeli walibarikiwa nje ya agano la Isaka, na wana wa Israeli na Yusufu. (Mwa. 17:19-21) 

 

Maseyidi kumi na wawili wa wana wa Ishmaeli  kwa kufuata utaratibu wa kuzaliwa ni kama ifuatavyo ( Mwanzo 25:13)

 

1.         Nebayothi

2.         Kedari

3.         Abdeeli

4.         Mibsamu

5.         Mishma

6.         Duma

7.         Masa

8.         Hadadi

9.         Tema

10.       Yeturi

11.       Nafishi

12.       Kedema

 

Hawa wataunda baraza la pili la makabila 24, watakao ongezeka katika baraza la wazee 24. Kwa wakati wote tunaona ya kwamba Mungu ana viwango maalumu vya idadi ya hesabu katika kupanua utaratibu wake.

 

Baada ya kifo cha Sarai, Ibrahimu pia alizaa wana wengine kwa ketura, mwanamke aliyemwoa baada ya kifo cha Sarai. (Mwa 25:1)

 

Wana sita wa Ketura ni kama ifuatavyo:

 

1)         Zimrani

2)         Yokshani

3)         Medani

4)         Midiani

5)         Ishbaki

6)         Sua

 

Wazaliwa wote wa Ibrahim kabila 12 za wana wa Israel, kabila 12 za ishmaeli na kabila sita za Ketura – zinajumlisha Baraza la wajumbe 30.                                                    

 

 

q