Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[CB19]

 

 

 

Sheria za Kibiblia za Ulaji wa Vyakula

(Toleo La  2.0 20020410-20061224)

 

Biblia imejumuisha kanuni na sheria ili kutufundisha aina ya vyakula vinavyoruhusiwa kuliwa. Pia inatuelekeza jinsi wanyama wanavyotakiwa kuuliwa na aina au makundi gani ya mnyama wasiyoruhusiwa kuliwa. Vyakula hivi vimeitwa kuwa ni vyakula safi na najisi.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 2002, 2006 Carrie Farris and Wade Cox)

 (Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Sheria za Kibiblia za Ulaji wa Vyakula


 


Mungu anatutaka tujue tunavyopaswa na tusivyopaswa kuvila.

 

Mungu anatuonyesha kwenye Mambo ya Walawi 11 na Kumbukumbu la Torati 14 mambo tunatopaswa kula na tusiyopaswa kuyala. Ametupa mwongozo wa kanuni ya vyakula bora kiafya nay a mtindo wa kimaisha. Mungu ana sababu nzuri sana kwa kutupa sisi Sheria hizi. Vyakula anavyotuambia kuwa tunaruhusiwa kuvila ni vyema sana kwetu na vinatusaidia tukue tukiwa na nguvu. Vyakula anavyotuambia tusivile vinatufanya kushambuliwe na magonjwa.

 

Sheria ya Mungu kuhusu wanyama

 

Wanyama Safi

Mambo ya Walawi 11:1-3 Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2 Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi. 3 Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala.

 

Kumbukumbu la Torati 14:3-6 Usile kitu cho chote kichukizacho. 4 Wanyama mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, 5 kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima; 6 na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla.

 

Hii inamaanisha kwamba tunawezakula mnyama yeyote ambaye amepasuka au kuwa wazi kwato zake na anayecheua. Baadhi ya wanyama hawa tunaoweza kuwala ni ng’ombe, paa, na nyati, pamoja na kondoo na mbuzi.

 

Kutoka kwenye Mambo ya Walawi 7:22-24 tunaambiwa kuwa tusile mafuta ya yeyote kati ya wanyama hawa, au kumla mnyama aliyekufa mwenyewe tu kibudu au aliyeuawa kwa kuraruliwa na mnyama mwingine. Wakati tukikatazwa kula mafuta, tunaweza kuyatumia kutengenezea vitu vingine, kama vile sabuni na mishumaa, haikatazwi kuyatumia hivyo.

Mambo ya Walawi 7:22-24  Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 23 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Msile mafuta yo yote, ya ng'ombe, wala ya kondoo, wala ya mbuzi. 24 Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa ajili ya matumizi mengine; lakini msiyale kabisa.

 

Tumekatazwa pia kula damu ya wanyama hawa wote.

 

Mwanzo 9:4  Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.

 

Mambo ya Walawi 3:17 Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.

 

Kumbukumbu la Torati 15:23 Pamoja na haya usile damu yake; uimwage nchi kama maji.

 

Wanyama Najisi

Ni kama vile Mungu alivyotuambia wanyama tunaoweza kuwala, ndipo ametuambia pia wanyama ambao hatupaswi kuwala.

Mambo ya Walawi 11:4-8 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 6 Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. 8 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.

 

Kumbukumbu la Torati 14:7-8  Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu; 8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.

 

Hapa Mungu anatueleza kuwa tusiwale wanyama kama vile nguruwe, sungura, ngamia na farasi. Kunasababu nzuri sana na za muhimu za kutukataza kuwala wanyama hawa. Madaktari wamegundua kwamba kitendo cha kuwala wanyama hawa kinapelekea matokeo mabaya sana na madhara kwenye moyo, ini na maeneo mengine kwenye miili yetu.

 

Nguruwe au nyama ya nguruwe zinauwezo mkubwa wa kueneza magonjwa kwa mwanadamu kuliko mnyama mwingine yeyote. Wakati neno “nyama ya nguruwe” linapotumika, linahusisha kutaja aina zote za vitu vinavyotokana na paja la mnyama huyu—nguruwe, bakoni na soseji zinazotengenezwa kwa au kwa kuchanganywa na nyama ya nguruwe pia. Madaktari sasa wanajua kwamba kuna uhusiano kati ya ulaji wa nyama ya nguruwe na mlipuko wa ugonjwa wa ini. Hata watoto wanaweza kukumbwa na ugonjwa huu. 

 

Haijalishi kuwa ni mazuri kiasi gani mazingira yanayotumiwa kuwafudia hawa nguruwe, bado hatari ya madhara ya ugonjwa wa cirrhosis ya ini unaotokana na ulaji wa nyama ya nguruwe hauwezi kuepukika au kwisha. Pia hali ni mbaya zaidi kwa wale wanaofanya mambo yote mawili, yaani watu wanaokunywa pombe au aina yoyote ya kileo na huku wanakula nyama hii ya nguruwe, wanaonekana kuwa kwenye hatari kubwa sana ya kuwa na muathiriko na kupatwa na ugonjwa wa ini. Ni nyama hii ya nguruwe yenyewe ndiyo sababu kuu na ni mzalishaji mkubwa wa vijidudu vinavyosababisha ugonjwa huu vinavyoitwa kitaalamu cirrhosis.

 

Ili kupata habari zaidi na maelezo ya kina na taarifa zake kuhusu jambo hili muhimu kuhusu ulaji wa nyama ya nguruwe yamefafanuliwa kwa kina kwenye jarida la Sheria ya Vyakula (Na. 15).

 

Sheria za Mungu kuhusu samaki

 

Samaki walio safi

Mambo ya Walawi 11:9 Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao.

 

Kumbukumbu la Torati 14:9 Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula;

 

Mungu anatutaka tujue kwamba samaki yeyote aliye majini hapa duniani aliye na magamba na mapezi yu safi na anatufaa kumla. Kuna samaki wengi walio na magamba na mapezi, akiwemo samoni, sangara, changu, dagaa, na wengine wengi. 

 

Samaki najisi

Mungu pia anataka tujue ni samaki gani wasiosafi ambao hatupaswi kuwala.

 

Mambo ya Walawi 11:10-12  Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu, 11 watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu. 12 Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu.  

 

Kumbukumbu la Torati 14:10 na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu.

 

Hii inajumuisha samaki wengi na wa aina mbalimbali na samaki wenye gamba jumba, wakiwemo papa, papaupanga, katfish, nyangumi, pomboo, dagaakamba, kaa, kambakoche, chaza mdogo, chaza mkubwa, na wengine wengi.

 

Tena Mungu ana sababu nzuri sana kwa kuweka sheria hii ya kukataza ulaji wa aina hii ya samaki. Madaktari wanajua sasa kwamba aina hii ya samaki na hawa wenye gamba-jumba wana kiwango kikubwa sana cha chuma kizito na kiuasilia wanauwezekano mubwa sana wa kuwa na sumu ndani yao. Wanaweza kuwa na madhara makubwa sana kwa mwanadamu. Hatahivyo, samaki hawa najisi pia wana umuhimu mkubwa wa kufanyika kuwa walaji wazuri wa mizoga na ya samaki wengine na wa vitu vingine vichafu ambavyo sisi tunakula. Kwa kuwala samaki hawa waliokatazwa tunasaidia kuharibu mazingira. Samaki hawa najisi wanafanya kazi ya kusaidia kusafisha mazingira kwa kula mizoga ya samaki. Samaki wengine wasio na magamba wanasaidia kusafisha sehemu ya chini ya mito na maziwa.

 

Sheria ya Mungu kuhusu ndege warukao

 

Ndege walio majisi

Mambo ya Walawi 11:13-19  Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu; 14 na mwewe, na kozi kwa aina zake, 15 na kila kunguru kwa aina zake; 16 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; 17 na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa; 18 na mumbi, na mwari, na mderi; 19 na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo.

 

Hii inaonyesha kuwa ni ndege wengi ambao hawafai kwa kuliwa, lakini kwa kweli ni kwamba tunaweza kuwala kiasi kikubwa cha mchanganyiko wa ndege au wa aina mbalimbali.

 

Mungu pia ana sababu yake nzuri kwa kutukataza tusile aina hizi za ndege. Moja ya sababu zake za wazi sana ni kwamba, wengi wao, kama sio wote, wa ndege hawa ni walamizoga. Hii inamaana kwamba wanakula vitu vingi na vya aina mbalimbali wakiwemo wanyama waliokwishakufa tayari, au mizoga. Hii inawafanya wasifae kwa matumizi hasa ya kuliwa na wanadamu kwakuwa wanakuwa na virusi vingi vya magonjwa wanavyotembeanavyo vilivyotokana na baadhi ya wanavyovila. Pia wana kimeng’enya au sumu maalumu kwenye miili yao inayowasaidia kuyeyusha nyama za mizoga hii ya wanyama na aina nyingine ya viumbe naajisi, na kimeng’enya au sumu hii inamadhara makubwa sana kwa wanadamu.

 

Ndege Walio Safi

Ndege hawa walio safi ni wa jamii ya kuku, bata mzinga, njiwa na huwa – wale wote walio ni mazalia. Bata, bata bukini na bata maji mwenye shingo ndefu pia ni miongoni mwa ndege walio safi.

 

Wengi wengine wote wa ndege ni najisi. Sayansi inatafuta kwa kina zaidi kuhusu habari ya uwezekano wa kubeba virusi vya magonjwa kunakofanywa na hawa ndege najisi. Yaonekana kwamba magonjwa haya yanapita kutoka kwao hadi kwa ndege safi na wasionajisi, kwa walio kwenye kundi la bata, kwenye maeneo kama vile huko Hong Kong, wakati walipofungwa pamoja kwa kuchanganywa na nguruwe kutoka kwenye mwingiliano na ndege wasio safi na vikapitia kwenye mnyororo wa vyakula.

 

Mlipuko wa homa ya mafua kutoka bara Asia umeonekana kutokana na chanzo hiki. Sote tunajua kuhusu mlipuko wa mafua makali ambayo ni ya kawaida kutokea kila majira ya baridi na unaowafanya watu kuugua sana. Ndege waliosafi kwa ujumla wako huru kutoka kwenye matatizo haya, lakini kutokana na mazingira fulani hawa nao wanaweza kuadhirika. Kanuni za jumla za kiafya kuhusu maambukizi zinakutikana kwenye Mambo ya Walawi 11 na zinapaswa kufanyiwa kazi inapokuwa lazima.

 

Sheria za Mungu kuhusu wadudu

Mambo ya Walawi 11:20-23  Tena vyote vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, hivi ni machukizo kwenu. 21 Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi; 22 katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake. 23 Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu.

 

Inaweza kuonekana kuwa si kitu cha kawaida kwetu na kwa mtu yeyote kula wadudu aina ya kunguni, lakini kuna wengine sehemu fulani za dunia huwala nzige na huwafanya kuwa ni chakula chao cha kila siku. Iwapo kama utakuwa na njaa sana kupindukia, unaweza kuwala wadudu hawa pia. Mungu anasema kuwa ni vyema sana kuwala hawa nzige, senene na panzi.

 

Sheria ya Mungu kuhusu wanyama wenye nyayo na kucha na wasio na kwato

Mambo ya Walawi 11:27 Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni.

 

Tusile paka au mbwa au aina nyingine yoyote ya wanyama wenye miguu minne na wenye nyayo na kucha ambao hawana kwato.

 

Sheria ya Mungu kuhusu wanyama wagugunaji na vitambaavyo

 

Mambo ya Walawi 11:29-31 Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zake, 30 na guruguru na kenge, na mjusi na goromoe, na lumbwi. 31 Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; awaye yote atakayewagusa, wakiisha kufa, atakuwa ni najisi hata jioni.

 

Mambo ya Walawi 11:41-42 Na kila kitu kitambaacho juu ya nchi ni machukizo; hakitaliwa. 42 Kila aendaye kwa tumbo lake, na kila aendaye kwa miguu minne, na kila aendaye kwa miguu mingi, maana, ni vyote vyenye kutambaa vitambaavyo juu ya nchi, hamtavila, kwa kuwa ni machukizo.

 

Hapa Mungu anatutaka tujue kwamba hatupaswi kula vitu jamii ya nyoka, jamii ya kenge au mjusi, panya, panya-buku, jamii ya mchwa au kumbukumbi, minyoo, na aina nyingi nyinginezo amazo ni nguchiro, vinavyotambaa, na jamii ya kunguni. Wengi wetu hatupendi kuvila vitu hivi hata hivyo kabisa.

 

Watu wa ulimwengu huu huenda kinyume na sheria hizi za Mungu zihusuzo vyakula

 

Watu wengi sana ulimwenguni hula vyakula na vitu alivyovikataza Mungu na alivyotuambia tusile. Baadhi ya vitu wanavyokula sana na kuonekana vya kawaida kwao ni nyama ya nguruwe na samakigamba au wa magome. Kuna wale ambao wanakula vitu vyote hivi ambavyo Mungu amevikataza kwa kutuambia tusivile.

 

Wengine hata husema kuwa haijalishi kwa Mungu kuhusu tunavyokula wala yeye hajali tena kabisa, lakini hii siyo kweli.

 

Yesu alisema kuwa Torati haitapita kamwe hadi yote yatimilike (Mathayo 5:17-18). Kwa hiyo, hadi mambo yote kwenye Biblia yatakapotimia tunapaswa kuzishika Sheria za Mungu, na kuzishika sheria za vyakula ni sehemu ya Torati ya Mungu.

 

Mathayo 5:17-18 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.

 

Watu wengine husema kuwa andiko la Matendo 10 limeyafanya mambo yote kuwa sawa na limeturuhusu kula vyakula najisi. Hatahivyo, andiko la sura ile lilitumika ili kumuonyesha Petro kwamba Mungu amaufanya wokovu kuwa wazi kwa Wamataifa ambao hadi kipindi kile walichukuliwa kama watu najisi. Andiko lile halihusiani kabisa na dhana hii ya vyakula safi na najisi au kuhusiana na ulaji wa nyama.

 

Inasema pia kwene Warumi 2:13-15 kwamba Mungu ameziandika Sheria zake mioyoni mwetu na kwamba siyo watu wanaoisikia Sheria lakini ni kwa Yule aitendaye Sheria ndiye atakayehesabia haki.

Warumi 2:13-15 Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki. 14 Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. 15 Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;

 

Mungu anatupenda na anataka tuzijue Sheria zake mioyoni mwetu kama ilivyo kwenye Biblia yake. Ametupa mwongozo wa kile tunachotakiwa kula. Pia ametufanya tujue kuhusu vitu tusivyotakiwa kuvila. Ili tuishi tukiwa na afya njema na tukimpendeza, ni lazima na tunapaswa kuzitii Sheria zake. Kama wanadamu walifanya sehemu yao katika kulinda na kuyatunza mazingirta yao kuwa safi, ndipo sayari na Dunia hii kuwa ni mahala pazuri sana na watu wangekuwa wenye afya njema sana kuliko.

 

Kwa maelezo zaidi kujisomea kuhusu sheria hizi za vyakula na mambo mengine yanayohusiana nayo, rejea kwenye jarida la Sheria za Vyakula (Na. 15).

q