Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[CB20b]
Jinsi ya Kuipangilia
Kalenda ya Mungu
(Toleo La 1.0
20061106-20061106)
Jarida hili linaelezea kanuni na taratibu za kuhesabu zilizotumika kuziweka
au kuzipangilia siku na tarehe za Kalenda Takatifu ya Mungu.
Christian Churches of God
PO Box 369,
WODEN ACT 2606, AUSTRALIA
Email: secretary@ccg.org
(Sheria ya Hatimiliki © 2007 Jacques Guérard, ed. Wade Cox)
(tr. 2015)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu
bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja
na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa
mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha
lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni katika
tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Jinsi ya Kuipangilia Kalenda ya Mungu
Kwenye jarida
hili tutaonyesha kanuni ya msingi, taratibu na jinsi ya kuhesabu kukovyotumiwa
ili kupata msingi wa kuamua jinsi ya kuipangilia Kalenda Takatifu ya Mungu na
jinsi ya kuupata mwezi wa Kwanza wa Mwaka Mpya kwa mujibu wa vipindi vya mpito
vya vipindi vya kutoonekana mwezi vya Mwezi Mpya vya taasisi ya elimu ya mambo
ya anga na nyota. Mizunguko hii ya mwezi imeainishwa vyema na dondoo zote za
kimahesabu zinaweza kupatikana kwenye vyanzo rasmi vya kisayansi kama vile
taasisi ya NASA na nyinginezo. Maana na tafsiri ya maneno yaliyotumika kwenye
kuamua mpangilio wa kalenda yametolewa mwishoni mwa jarida ili kuyaona na
kuyasoma kiurahisi.
Kalenda ya Mungu
inakwendana na Uumbaji wake – kwa kuweka mianga midogo na mikubwa. Haitegemei
waka kutuama kwenye kitu kingine chochote kilichotengenezwa na mwanadamu, kama
vile kwenye kalenda ya Kigregoriani au kalenda ya Kiyahudi ya Hilleli. Kalenda
ya kweli ya Mungu inashabihiana na mwandamo na mzunguko wa mwezi, kwa hiyo
inaendana na mizunguko ya mwezi, ambavyo ni, mzunguko wa mwezi mwandamo. Ili
kujifunza kwa kina kuhusu Kalenda hii ya Mungu, tafadhali soma majarida ya Kalenda ya Mungu (Na. CB20) na Siku Takatifu za Mungu (Na. CB22).
Kwanza kabisa,
tutaona majedwali fulani kadhaa na dondoo za vipindi vya mpito vya muunganiko
kati ya miezi na siku za kulingana masaa usiku na mchana za majira ya baridi
yaliyopo kutokana na utambuzi wa mamlaka maalumu ya kisayansi. Pili, tutatathimini
kanuni za msingi ili kupangilia siku za Miandamo ya Mwezi Mpya za kuzishika
baada ya kuzipata siku hizo kutoka kwenye taasisi ya Saa za Ulimwengu mzima
zijulikanazo kama Universal Time (au Greenwich Mean Time) na kuziweka kwenye
saa za kimahalia za Yerusalemu. Tatu, tutaziona dondoo za ikwinoks ya majira ya
baridi ili kupangilia tarehe au siku ya kuutangaza Mwaka Mpya au mwanzo wa
mwezi wa Kwanza majira ya baridi.
Kutangazwa kwa
tarehe au siku ya Mwezi Mpya kwenye maeneo yote mahalia na makanisa yaliyoko
ulimwenguni kote kunategemea na siku ya Mwezi Mpya na Siku Takatifu wakati
kunapozama juna na kuanza giza kwetu sisi mahali popote tunapoishi.
Isaya 2:3 Na
mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana,
nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda
katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika
Yerusalemu. (sawa pia na Mika 4:2).
1. VIPINDI VYA MUUNGANIKO WA
MIEZI, MIAKA YA 2001-2100 BK
Tuna chanzo cha kuzipata siku za miunganiko ya mwezi mmoja hadi mwingine
kwenye tovuti ifuatayi na taasisi ya NASA ifuatayo: http://aa.usno.navy.mil/data/docs/MoonPhase.html
Tarehe zote zimeandikwa kwa kufuata kalenda ya Kigregorian na masaa
yameandikwa kwa kufuata majira ya Saa za Ulimwengu zijulikanazo kama Universal
Time (yaani mstari wa Greenwich). Dondoo hizi zimetumika katika kuipangilia
siku ya kwanza ya mwezi mpya kwenye Kalenda ya Mungu.
2. IKWINOKS
ZA MAJIRA YA BARIDI ZA MIAKA YA
1992-2020 BK
Ikwinoks ni wakati ambao jua linapita au kukatiza Dunia kwenye mstari wa
Ikweta, ambapo inafanya usiku na mchana Ulimwenguni kote kuwa sawasawa masaa au
urefu wake. Tukio hili hutokea kwenye tarehe za March 20 au 21 na pia tarehe 22
Septemba. Ikwinoks inatusaidia kupangilia kuanza kwa mwaka. Kama saa 9:00 alasiri.
Dhabihu ya siku ya 14 Abibu haifanyiki au kutolewa hadi baada ya ikwinoks ya
majira ya baridi, tunafanya nyongeza au kuongeza mwezi wa 13.
Chanzo cha dondoo za ikwinoks za majira ya baridi zinapatikana kutoka
kwenye tovuti ifuatayo ya taasisi ya Jeshi la Marekani ifuatayo: http://aa.usno.navy.mil/data/docs/EarthSeasons
Kufuatia kanuni hiyohiyo kwa ajili ya Miandamo ya Mwezi Mpya kama ilivyo
hapo juu 20 March, kwa mujibu wa ainisho la Mungu.
3. DONDOO YA MAJIYA AU MASAA YA
EENT HUKO YERUSALEMU
Neno la Mwisho wa Majira ya Jua
Kuchwa Jioni, au End Evening Nautical Twilight (EENT)
ni neno la kisayansi la kipindi halisi ambacho giza linaanza upande fulani
maalumu. Muda huu ni wakati siku mpya inaanza na siku iliyopita inaisha kwa
mujibu wa uumbaji wa Mungu. Soma jarida la Kuanza Kwa Mwezi na Siku (Na. 203). Jedwali la nyakati au
masaa ya EENT huko Yerusalemu laweza kupangiliwa kwenye Kompyuta kwa kipindi cha
mwaka mmoja – au siku 365 – moja kwa moja kutoka kwenye tovuti ya Interneti ya http://aa.usno.navy.mil/data/docs/RS_OneYear.php kwa kutumia
dondoo zifuatazo: mstari ulalo au longitude Mashariki nyuzi 35’ 19, mstari
ulalo au latitude Kaskazini nyuzi 32’ 34, na masaa 2 mashariki mwa Greenwich.
4. KUAMUA
MPANGILIO WA TAREHE AU SIKU ZA MWEZI MPYA
A. Pata siku ya mpito ya muunganiko kwenye dondoo za
Mwezi Mpya.
Utumiaji wa dondoo kupata siku za miunganiko ya miezi, tunaweza kuamua
kupangilia siku za Mwezi Mpya za kushika huko Yerusalemu. Kwa mfano, tutaamua
kupangilia siku ya Mwezi Mpya kuwa ni Mwezi wa Kwanza wa Kalenda Takatifu ya
Mungu katika mwaka 2008, au mwaka wa 31 wa Yubilee ya 120. Tunaukuta Mwezi Mpya
saa 11 jioni siku ya 14 ya ushirika wa meza ya Bwana tarehe 7 March 2008. http://aa.usno.navy.mil/data/docs/MoonPhase.php
B. Amua kupangilia Mwezi Mpya kwa masaa mahalia ya
Yerusalemu.
Yatupasa kulinganisha saa ya kuanza kwa muunganiko wa Mwezi Mpya kulikoonyeshwa
kwenye jedwali kutokana na Masaa ya Kimataifa ya Universal Time (UT) na masaa
mahalia ya Yerusalemu kwa kuongeza tu masaa 2 na kufikia saa 1 jioni, siku ya14
(saa 1:14 jioni) kwa masaa mahalia ya mwanzo wa Mwezi Mpya huko Yerusalemu.
Wakati yanapoongezwa masaa 2 kwa kukatiza kwenye usiku wa manane (saa 6:00
usiku), yatupasa kusogeza siku vizuri, ambavyo ni, kwa kuifanya iwe siku
inayofuata ya kalenda ya Georgian. Hii kwa hiyo ni kuusogeza mbele muda wa
dondoo la jedwali.
Kwenye tarehe 7 March 2008, tunakuta kuwa saa 12:34 jioni (saa 12:34 jioni)
kwenye jedwali la masaa yaliyowekwa kwenye Kompyuta ya EENT likitumia masaa 2 mashariki
mwa mstari wa Greenwich.
http://aa.usno.navy.mil/cgi-bin/aa_rstablew.pl
Wakati mwingine tunapaswa kurekebisha tarehe ya siku ya kuadhimisha
wakati siku asilia ya Mungu inapoanzia wakati wa giza wakati mwanadamu anapofanya
mwanzo usiku wa manane. Kwa hiyo kunakuwa na tofauti ya masaa 6 kati ya maana
mbili yanayoendana na kipindi cha kati ya masaa ya EENT huko Yerusalemu na
usiku wa manane. Hata hivyo, majira ya baridi siku inaweza kuishia mapema sana
kama saa 11:00 jioni (saa 11:00 jioni) na majira ya joto inaweza kuishia muda mrefu
wa saa 4:00 usiku (saa 4:00 usiku) kwenye maeneo mengine ya dunia. jambo la msingi
na muhimu kukumbuka hapa ni kwamba siku ya Mungu huanza na kuishia jua
linapozama na giza kuanza. Kwa lengo la kufafanua dhana ya “tangu kuzama jua na
kuingia giza hadi usiku wa manane” tutauita muda huu kuwa ni kipindi cha masaa 6,
tukijua kwamba muda linapoanza kuingia “giza” hutofautiana kwa mwaka mzima.
Kwa hiyo twaweza kusema siku ya Mungu huanza na kuishia kwenye wastani wa
masaa 6 kabla ya tafsiri aliyoifanya mwanadamu hivi karibuni. Wakati Mwezi Mpya
unapojitokeza kwenye kipindi hiki cha masaa 6, yatupasa kupeleka mbele siku
iliyoonyeshwa kwenye jedwali na kuihamishia kwenye siku inayofuatia ili
kuishika siku sawasawa na maana aliyoiagiza Mungu.
Kwenye mfano wetu, siku inabadilishwa hadi siku inayofuatia kwenye
jedwali la siku kwa kuwa muda wa kuanza Mwezi Mpya wa tarehe 7 March ulikuwa ni
baada ya masaa ya EENT ya siku ile.
Kwa hiyo, kwa kuwa mwanzo wa Mwezi Mpya wa tarehe 7 March 2008 ilikuwa saa 1:14
jioni (1:14 jioni), ambayo ni baada ya saa za EENT (12:34jioni, au saa 12:34 jioni),
mwanzo wa Mwezi Mpya uliadhimishwa tarehe 8 March.
5. JINSI YA KUAMUA MWANZO WA MWAKA MPYA (ABIBU 1)
Maamuzi ya ni
mwezi gani wa Kwanza na siku ya Kwanza ya mwaka, yatupasa kuupata kwanza Mwezi
wa Kwanza ulio karibu sana na ikwinoks ya majira ya baridi. Siku ya 14 ya mwezi
wa Abibu unaweza kuwa ndio huohuo wenye siku ya ikwinoks, lakini haiwezi
kuadhimishwa KABLA ya ikwinoks ya majira ya baridi. Hii ni kwa ajili ya kutoa
sadaka mbili za Pasaka zinazotokea kwenye mwaka huohuo wa kalenda. Hata hivyo,
inapasa iwe katia siku ya 14 inayotokea kabla ya siku ya ikwinoks, mwezi wa
kumi na tatu unapasa uongezwe ili kuzuia kutokea kwa hilo. Kimsingi, pia ina
maana kwamba siku ya 15 ya mwezi wa Abibu ni budi kila mara itokee baada ya
siku za ikwinoks.
A. Pata majira ya ikwinoks ya majira ya baridi.
Kwenye majedwali kwa ajili ya mwaka 2008 iliyowekwa kwenye tovuti ya: http://aa.usno.navy.mil/data/docs/EarthSeasons.html siku ya ikwinoks
ya majira ya baridi au ya joto kwenye Ncha ya Kaskazini mwa dunia ni March 20, saa
11:48 asubuhi kwa saa za UT. Ikwinoks ya majira ya joto inatokea karibia kwenye
siku hiyohiyo kila mwaka. Tunaongeza siku 2 ili kuifanya iendane na muda
mahalia wa masaa ya Yerusalemu saa 1:48 asubuhi. Kwa kufuata kanuni hiyohiyo
kwa mionekano ya Mwezi Mpya hapo juu, tunaamua kuipanga siku ya ikwinoks kuwa
ni tarehe 20 March sawasawa na malengo ya Mungu.
B. Pata mwanzo wa Miezi Mipya ya kabla na baada ya
ikwinoks ya majira ya baridi.
Kutokana na
majedwali ya kwenye tovuti ya http://aa.usno.navy.mil/data/docs/MoonPhase.html, tunakuta siku ya kuanza Mwezi Mpya
kukitokea hata kabla ya siku ya ikwinoks, March 20, na mwanzo wa Mwezi Mpya
ukifanyika mara tu baada March 20. Siku ya Mwezi Mpya iliyo karibu sana na
ikwinoks ndiyo hufanyika kuwa ni mwezi mpya wa Mwaka wa Kwanza, ambayo ndiyo
Siku ya Kwanza iitwayo siku ya 1 Abibu. Katika mwaka 2008, tulikuwa na
mwonekano wa Mwezi Mpya tarehe 7 March, saa 11:14 jioni saa za UT (saa 1:14 saa
za Yerusalemu) na kuonekana kwa Mwezi Mpya kulikuwa Aprili 6 saa 9:55 alfajiri (11:55
majira ya Yerusalemu). Tunakuta kwamba Mwezi Mpya ulikuwa siku ya March 7 ukiwa
ni mwezi wa karibu zaidi na ikwinoks ya majira ya baridi ya March 20. Kwa kuwa
Mwezi Mpya ulianza saa 1:14, baada ya saa za EENT (12:34) huko Yerusalemu na
kabla ya usiku wa manane, tunaisogeza siku hadi siku inayofuatia. Kwa hiyo, March
8 ikafanyika kuwa ni Siku ya Kwanza ya Mwaka, yaani, mwanzo wa Mwaka Mpya, siku
ya 1 Abibu.
Hili ni hitimisho la utaratibu wa kuamua jinsi ya kuipangilia Kalenda ya
Mungu. Siku zote za mwanzo wa Kalenda ya Miezi Mipya na Mwaka Mpya inaweza
kupatikana kwenye jarida la Kalenda ya Mwezi Mpya na Siku Takatifu (Na. C3).
Na tuombe basi ili Baba na Mwumbaji wetu, Eloah afundishe watu wote
kuhusu Kalenda yake ili kwamba wote wamuabudu yeye kama inavyotakiwa na kwa
siku sahihi.
Soma pia kwenye jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156).
***************
Maana ya Maneno yaliyotumika:
Utusitusi wa
Mawio na Machweo ya Jua [Astronomical twilight]: kunatokea wakati wa jioni mara tu jua linapokuwa
limefikia kiwango cha zaidi ya nyuzi 18° chini ya upeo wa macho na huzama
wakati jua linapofikia kwenye nyuzi 18° za upeo wa macho majira ya asubuhi.
Kipindi cha Muunganiko Kati ya Mwezi wa Zamani na
Mwezi Mpya [Conjunction]: mkutaniko au muunganiko wa muundo
wa mbinguni kwenye mstari huohuo wa wima au uliosimama wima, yaani, hali ya
mihimili miwili au zaidi ya mbingu wakati mistari ya wima ni ile ile – inaonekana
kuwa kwenye mstari wa kila mmoja wapo.
Utusitusi wa
Nchi [Civil twilight]: unaanza
majira ya asubuhi wakati kitovu cha jua kinapokuwa chini ya nyuzi 6° chini ya
upeo wa macho, na kuishia kwenye mawio ya jua. Utusitusi wa nchi wa jioni unaanzia
jua linapokuchwa na huishia wakati kitovu cha jua kikiwa zaidi ya nyuzi 6° chini
ya upeo wa macho.
Utusitusi wa Ukomo wa Zamu ya Jioni ya Mabaharia [EENT]: Utusitusi wa Ukomo wa Zamu ya Jioni ya
Mabaharia ni muda halisi ambao giza linaanza kwenye maeneo fulani maalumu.
Ikwinoks [Equinox]: ikwinoks ni kipindi ambacho jua linavuka kwa kupita kwenye mhimili wa Dunia
wa ikweta, kikifanya usiku na mchana karibu Ulimwenguni kote kuwa na urefu
sawa. Hali hii inatokea mara mbili kwa mwaka: mmoja hutokea majira ya baridi na
hii hutokea kwenye tarehe za 20/21 March na nyingine hutokea majira ya joto
mnamo tarehe 22 Septemba.
Kuongeza Mwezo wa Ziada
[Intercalation]: ku-intercalate maana
yake ni kuingiza mwezi wa ziada ili kuufanya mwaka wa kalenda ulingane na
kalenda ya mfumo wa mwaka wa mzunguko wa jua.
Mstari wa
Mlalo [Latitude]: umbali
uliowekwa wa mastari wa wima wa kaskazini au kusini kutoka kwenye mstari wa
ikweta unaoonesha uso wa Dunia, unaopimwa kwenye nyuzi za umbali.
Mstari wa Wima
[Longitude]: umbali
uliowekwa wa mastari wa wima wa mashariki mwa uso wa Dunia, uliopimwa kwenye nyuzi
au digrii kutoka kwenye ukanda fulani wa mstari unaozitenganisha kanda (mstari
wa kutoka Kaskazini hadi Ncha ya Kusini mwa Dunia). kwa kawaida, mstari huu
unaotenganisha kutoka ukanda wa Greenwich, Uingereza inatumika.
Mchanganyiko wa Mwezi na Jua [Lunisolar]: inahusiana au inatokana na uhusiano wa
mseto wa mwezi na jua (mfano, mzungko wenye
mseto wa mwezi na jua).
Kalenda ya
Mchanganyiko wa Mwezi na Jua [Lunisolar calendar]: ni kalenda ambayo tarehe au siku zake zinaashiria
vyote viwili, yaani mwonekano wa mwezi na nyakati za jua. Kwa kawaida kuna
nyongeza ya lazima ambayo kwamba mwaka una idadi yote ya miezi lakini, na kwa
namna yoyote, kila mwaka una miezi 12 bali kila mwaka wa pili au wa tatu una
miezi 13. Mara saba kwenye kipindi cha miaka 19 tuna mwaka wenye miezi 13.
Kukomaa na
Kupanda kwa Mwezi/ Kuweka nyakati [Moonrise/set times]: nyakati hizi zinategemea na mwelekeo wa
mwezi – yaani mwezi mpya wenye giza kamili, mwezi kamili na robo ya kwanza na
ya pili. Mwezi unainuka na kuchwa kila siku ni kama lifanyavyo jua. Kwa habari
zaidi kuhusu mwelekeo huu wa mwezi, soma tovuti ifuatayo: http://www.calculatorcat.com/moon_phases/moon_phases.phtml
Utusitusi wa Kubadilishana Zamu ya Jioni ya Mabaharia [Nautical twilight]: inamaaniha kuwa ni wakati kiini cha jua
kiko zaidi ya 6° chini ya upeo wa macho lakini chini kuliko nyuzi 12°. Kipindi hiki
asubuhi mara nyingi kinaitwa kuwa “nuru ya kwanza” kabla ya mapambazuko, na kwa
jioni kinajulikana kuwa cha “kuingia usiku” baada ya magharibi. Kipindi hiki
cha Utusitusi Jioni ya Muda wa Kubadilishna Zamu Mabaharia unafanana na ule wa EENT.
Mwezi Mpya [New Moon]: Mwezi Mpya wa wataalamu
wa elimu ya nyota na anga, wakati mwingine unajulikana kama mwezi wa giza, hutoke kimwelekeo na
kipindi cha mpito cha kutooekana mwezi kwenye uficho kwa tukio la kupatwa kwa
mwezi na Jua kwenye mstari wa wima, wakati Mwezi unapoacha kuonekana kutoka
Duniani.
Majira ya Jua
[Solar time]: hupimwa au
huamuliwa kwa mwenendo wa Dunia kwa kuhusiana na jua.
Mawio ya Jua [Sunrise]:
muonekano
wa kwanza wa jua wakati wa asubuhi.
Machweo ya Jua
[Sunset]: kuzama chini
kwa jua – mwonekano wa mwisho wa jua jioni.
Masaa ya
Ulimwengu [Universal Time]: mfumo wa masaa unaopimwa kwa kutegemea mfumo Kuanza kwa Masaa Kutokanako
na Majira ya mstari wa Greenwich, lakini yanahesabiwa tangu saa 0, ambayo ni
sawasawa na usiku wa manane ya mfumo wa Masaa ya mstari wa Greenwich.
q