Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[CB22]
Siku Takatifu Za Mungu
(Toleo 3.0 20020512-20061223-20081217)
Watu wengi duniani wanashika siku takatifu za dini na kusherekea siku ta taifa. Hii karatasi itafunua mpango wa Mungu.
Christian Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Copyright ă 2002, 2006 Diane Flanagan and Wade Cox)
(Tr. 2009)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Siku Takatifu Za Mungu
Watu wengi kote ulimwenguni huwa na likizo na siku za kusherekea, tofauti ni siku za Mungu katika Bibilia. Siku zile watu wanasherekea ni kama siku za taifa, siku hizi mambo muhimu huwa imetendeka kwa nchi, watu wengine husherekea siku kulingana na imani ya dini zao, lakini twahitaji kuangalia Bibilia tuone siku zile twahitaji kusherekea.
Wakristo wa kweli, wanamwabudu Mungu mmoja wa kweli (Kumb 6:4; Jn. 17:3, 1 Tim 6:16; Jn. 5:20) na kushika amri na sheria zake (Ufunuo 12:17, 14:12, 22:14). Mungu alifunua mpango wake wa wokovu kwenye sikuu. Tukitii Mungu na tukimheshimu na tufuate sheria, tutaweza kumfurahisha Mungu naye atatulinda.
Amri ya nne yasema hivi, kumbuka siku ya sabato na uitakase (Kut. 20:8-11; Kumb 5:12-15). Sabato ni ishara katiya Mungu na mtu, Inatukumbusha ya kwamba Mungu ni yeye aliyeumba (Kut 31:15-17). Sabato ni siku ya furaha kwa sababu tunakutana na wale wenye imani moja na sisi. Hii ni siku ya saba ya wiki jumamosi, sio siku ya kwanza ya wiki, Jumapili kama wengi wanavyoamini, Bibilia yasema ya kwamba tufanye kazi siku sita (Kut. 10:9,11) na siku ya saba ni sabato (Jumamosi) lazima tutakase siku hii na tuungane pamoja na wengine kusoma kumtii Mungu zaidi, tunapotii sabato kwa hakika tutaweza kushika na kutakasa sikukuu zingine. Hatutaweza kufanya kazi wakati wa sikukuu ya mwaka au mwandamo wa mwezi au kununua siku hizi. Kwa kuwa sote ni sawa kama sabato (Yeh. 17:21-22) Amos 8:5, Neh 10:28-31, 13:15-19) zaidi juu ya sabato, angalia karatasi Siku ya Sabato (No. CB21).
Kwa kuwa kila wiki tuna siku muhimu na Mungu, sabato hivyo ndivyo hata kwa mwezi tuna siku muhimu ille tunatumia kumwabudu na kusoma mengi juu ya Mungu, hiyo siku ni mwandamo wa mwezi. Kuna 12 miandamo kwa mwaka, hata ingawa mara saba kwa miaka 19 tuna miandamo 13 ile tunahesabu kuweka kalenda na siku zake. Mungu wetu ni Mungu wa sheria na mipango na kila kitu kinakuwa kikamilifu, ili tuweza kushika siku takatifu za Mungu tunahitaji kuwa na kalenda angolia karatasi Kalenda Takatifu ya Mungu (No. CB20).
Mwandamo wa mwezi ni siku ya kwanza ya kila mwezi, na sabato ya bwana na hatufanyi kazi siku hii (Amos 8:5). Mwandamo wa mwezi unaweza kuwa siku yoyote ile kila mwezi, lakini lazima tuangalie kalenda tujue siku yenyewe ili tujitayarishe mapema. Makanisa ya Kikristo ya Mungu iko na kalenda, inaonyesha siku hizi za kila mwezi kwa mwaka mzima.
Siku za kale watu walienda kuongea na manabii siku za muandamo wa mwezi (1 Sam 20:5,18; 1Wafalme 4:23). Kanisa la zamani lilishika muandamo wa mwezi na sabato kwa karne nyingi (Kol. 2:16). Muandamo wa mwezi ni wa kila wakati na utaangaliwa tena Yesu atakapokuja tena kutawala (Isa. 66:23; Eze. 45:17; 46:1,3,6). Watu wakikataa kushika hii siku, basi kwao hakutanyesha.
Katika historia, wakati mwingine watu was Mungu waliacha kushika kalenda ya Mungu vizuri hata wengine wakaabudu miungu mingine, lakini Mungu wa kweli anasimamisha nabii wake ili kurudisha watu kwa sheria za Mungu. Na watu wanaposoma na kujua sheria wanaona makosa yao, kwa hivyo uguguo ni kusoma na kujua sheria za Mungu. Hii inafuatana na kushika sabato mwendamo wa mwezi, sikukuu na siku takatifu wakifuatilia kalenda ya Mungu sawa sawa.
Kuna siku mbili maalum za mwandamo wa mwezi katika mwaka mrefu, ya kwanza ni mwezi wa Abib (Mwezi wa tatu/nne) mwanzo wa mwaka mpya katika kalenda ya Mungu. Hii ni tarehe tofauti kila mwaka. Wakati mwingine ni mwezi wa tatu mara ingine ni mwezi wa nne. Kwa hivyo tunaona tarehe moja Januari, siku wengi wanasherekea haina maana katika kalenda ya Mungu.
Kutoka kwa Bibilia tunaona ya kwamba mambo muhimu yalitendeka siku ya kwanza, siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi maji yalikauka juu ya nchi wakati wa Nuhu (Mwa 8:13). Naye Musa alisimamisha hema ya kukutanua siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza (Kut. 40:2). Ezra alianza kusimamisha hekalu ya pili siku ya kwanza ya mwezi (Ezr. 7:9).
Siku zingine takatifu ni siku ya tarumbete. Ni siku ya saba ya mwezi katika mwaka na siku ya sikuku. Hiyo siku imeelezwa katika karatasi hii.
Siku takatifu za mwaka
Habari ya siku takatifu za mwaka iko (Law 23:1-44; Hes. 28 na 29; Kum 16:1-16). Siku takatifu zafunua mpango wa Mungu wa wokovu kwetu kila mwaka, angalia karatasi; Mpango wa Wokovu (No. CB30). Siku takatifu zimegawanywa kwa vikundi vitatu vya mafuno. Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watokee mbele za Mungu na kutoa thabiu (Kut 23:14-17; 34:23,24 na Kum. 16:16). Mara tatu kwenda mahali jina la Mungu liko. Kwa hivyo viongozi wa kanisa wachague mahali wataweka siku kuu ya Bwana, hatuwezi kushika sikukuu nyumbani kwetu (Kum. 16:2,15,16).
Kwa hivyo, kuna mabadiliko kwa hii wakati wa mwaka wa Tatu wakufuata utaratibu. Wakati huu pesa tunasokusanya tunapatia viongozi wa kanisa ama kupatia kanisa. Hii pesa hutumiwa kuhudumia maskini (Kum 14:28-29).
Siku ya kwanza ya mafuno ni pasaka, hapa tunakumbuka kifo cha masihi msalabani, ya pili ni penteoste, haya mafuno ya kanisa na wale wamechaguliwa ya mwisho ni sikukuu ya vibanda. Hii ni sikukuu inayosimamia wanadamu wote na viumbe vilioonguka, na kugeuka kuabudu sanamu na kutii Mungu mmoja wa ukweli, kwa hivyo wanapatanishwa na Mungu.
Siku takatifu ni
v Pasaka na sikukuu ya mkate usiotiwa chachu (15th Abib, first month)
v Sikukuu ya kupiga baragumu (21st Abib)
v Siku ya pendekosti (esabu siku 50 kutoka usiwi)
v Siku ya tarumbete (1st Tishri, 7th month)
v Siku ya upatanisho (10th Tishri)
v Sikukuu ya vipande (15th Tishri)
v Siku ya mwisho ya Bwana (22nd Tishri)
Hizi siku lazima tusiweke kama sabato, ni ishara kati ya Mungu na watu wake (Kut. 31: 13,17; Eze 20:12,20).
Pasaka
Maelezo ya pasaka inonyesha uokovu wa wa wana wa Israeli. Lakini hiki inaonyesha uwokovu wa Ulimwengu nzima. Mungu alituonyesha kwamba kwa kutoa Wana wa israeli misri, Alitutoa kwa dhambi ata toa ulimwingu nzima kutoka kwa dhambi. hizo zote inachukua siku 21ya kusafishwa ambayo ina anza siku ya kwanza ya mwesi (Abib). Hii iniitwa “kusafiswa wa hekalu”. Kama tume batizwa sisi ni hiyo hekalu.
Wabatizwa wa kanisa ana ukumu siku ya saba wa mwezi kwa wale ambayo hawa jui nji ya Mungu (Ezek. 45:17-20). Siku ya kumi ya mwezi wa kwanza mwanakondoo alikuwa anachaguliwa na kuwekwa kando kwa pasaka ya mwana-kondoo (Kut. 12:3). Waisraeli walikuwa wamehimizwa kuwa kondoo lazima awe hana ila, mume wa mwaka mmoja (Kut. 12:5).
Kupitia malaika wa Yehova, Musa aliwaambia wana wa Israeli vile watakavyoiweka pasaka. Nao waisraeli waliambiwa kuwa kama familia zao ni za watu wachache wa kuweza kumaliza kondoo mzima, basi wangeligawanya na familia zingine jirani (Kut. 12:4). Nayo siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule (Abib) kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watawachinja tena wamehimizwa kutuaa badhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomia (Kut. 12:7). Watu wote wangekaa katika zile nyumba watakayemla mwana-kondoo kwa pasaka (Kut. 12:7-13).
Na ile damu iliyoko kwenye kizingiti cha juu mlangoni ilikuwa ishara kuwa nyumba na watu walio dani “watapitiwa juu yao”, wakati wana wa Misri walipopata pigo la vifo usiku huo (Kut. 12:13) walikuwa wameambiwa kuwa watakula mwana-kondoo usiku huo, ikiwa imeokwa motoni yote na kula pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga na mboga zenye uchungu (Kut. 12:8,9). Hakuna chochote cha mwana-kondoo kingebakia mpaka asubuhi; bali kitu kilichosalia hata asubuhi kilichomwa kwa moto (Kut. 12:10).
Na usiku wa manane wa siku ya kumi na tano Bwana aliwapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri. Hakuna nyumba ambayo haikuwa na mauti kwa mzwaliwa kwanza kwa mwanadamu hata kwa mzwaliwa kwanza kwa mwanadamu hata kwa wanyama (Kut. 12:29). Kuanzia hapo Farao aliwaruhusu wana wa Israeli kuondoka Misri na kuabudu Mungu wao kama walivyoelekezwa. Tumeambiwa tuweke usiku huo kama ukumbusho milele (Kut. 12:24). Angalia karatasi Musa na Kutoka (No. CB16).
Mambo yaliyotokea kwa wakati uliopita ni mfano au usaidizi wa kuelezea mambo yatakayotokea wakati ujao. Mwana-kondoo aliyetolewa na kuchinjwa usiku wa pasaka ilikuwa kielelezo cha vile Yesu Kristo angekuja na kuwa mwana-kondoo wa sadaka (Yn. 1:29-30, 1Pet. 1:19). Yeye ndiye sadaka ya kweli (Ebr. 7:27, 9:12; 10:10-14; 1Pet 3:18) na kutupatia kusikizana na Mungu Baba. Hii ilikuwa mara yake Kristo ya kwanza kutembelea nchi kama mtu na alikuja kutimiza jukumu la makuhani.
Katika maisha yake, Yesu Kristo aliweka chakula. Kwa siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza (Mt. 26:20-25; Mk. 14:12-26; Jn. 13:26). Huu ulikuwa ulaji wa usiku baada kula pasaka ya kweli, wakati mwana-kondoo alitolewa na kuchinjwa. Kwenye usiku wa mwisho wa Kristo duniani alitoa ishara zake jipya kwa wahiriki wa kanisa waliobatizwa (Mt. 26:26-30, Mt. 14:22-26; Lk. 22:15-20; Jn. 6:53-58). Hii inahusu kuoga miguu (Jn. 13:1-5) kula na kunywa kwa mwili na damu ya Kristo.Hii inaitwa meza ya Bwana. Ni jambo linalohusu watu wazima waliobatizwa pekee. Meza ya Bwana infanywa upya kwa kila mwaka kwa ubatizo wa agano letu na Mungu. NI moja ya mikate miwili ya kanisa.
Kwa hivyo ni mara moja tu kwa mwaka tunapaswa kula mkate na kunywa divai ya meza ya Bwana. Sio jambo tunaloweza kufanya kila wiki au kila siku, kama vile makanisa mengi yanavuoamini wakati wa kushirikiana kula chakula takatifu.
Hivi sasa katikati ya siku ya kumi na nne ya Abib watu wanatayarisha chakula kwa usiku wa kutazama. Wakati wa saa tisa (3 p.m.) za siku ya 14 za Abib tunakuwa na ushirika wa ukumbusho wa sadaka ya Kristo na kifo. Wakati pasaka ya kwanza kondoo alichinjwa kwa 30 CE Kristo alikufa msalabani. Wachanche wa marafiki wa karibu wa Yesu waliomba mwili wake ili wamzike kwenye kaburi karibu na pale alipokuwa wakati wa kufa (Mt. 27:57-60). Walimzika wakati wa jioni (angalia karatasi Yesu ni nani? (No. CB2)).
Kwa giza la siku ya 15 ya mwezi wa kwanza wa usiku wa kutazama. Huu ni usiku ambao mharibifu alipitia nchi ya Misri (Kut. 12:12, 29-30). Ni jambo la maana sana kuungana na watu wanaoamini kama sisi na wanakula chakula na mwana-kondoo, mboga zenye uchungu na mkate usiotiwa chachu. Ni usiku wa maombi na kusoma; ni usiku wa maana sana kwa sababu watoto wanauliza, “Hii sherehe inamaanisha nini?”(Kut 12:26). Halafu hapa watu wanaeleza maana ya usiku na ishara zake kwa wote kusikia na kusoma kumheshimu Mungu (Kum. 4:10; 10:12,20, 14:23, 17:19, 31:12,13).
Nayo siku ya 15 ya Abib ni siku ya mkate usiotiwa chachu. Mungu anatwambia tuondoe chachu yote isiwe katika nyumba zetu kabla ya kwenda kwa pasaka (Kut. 12.15). Kwa hivyo tunatakikana kuondoa vitu vyote kama vile unga wa ngano, chachu na mikate kwenye kabati na mahali tunapoweka vitu vya kula na kupika tunahitaji kusafisha. Hii ni kazi ya kuonekana na hatuhitaji mno kuiweka maanani na kusahau maana halisi ya pasaka na siku za mkate usiotiwa chachu.
Tumeambiwa tule mkate usiotiwa chachu kwa siku saba (Kut.12:17-20). Kwa hivyo hatukuli mikate, keki kwa sababu zinakuwa na chachu. Chachu ni kitu ambacho kinafanya vitu kuongezeka. Chachu ikiwekwa kwa kitu kingine inafanya pande kuwa nzima mara moja. Kristo alikufa siku ya Jumatano masaa ya alfajiri kwa 300 CE. Alikuwa kwenye kaburi siku 3 na usiku 3 kama vile ishara ya Yona inavyotuambia. Angalia karatasi Yesu ni nani? (No. CB2). Kristo alifufuka kutoka kwenye wafu katika sabato za wiki. Alipaa mbinguni, au alienda mbinguni wakati wa saa tatu siku ya Jumapili asubuhi. Yesu Kristo alikuwa amekubaliwa kama sadaka ya kweli. Kila mwaka wakati wa sherehe ya mkate usiotiwa chachu tunaweka mganda wakati wa saa tatu za mchana siku ya Jumapili, kwa ukumbusho wa tokeo hili (Law 23:10-14).
Mganda sio siku takatifu, kwa hivyo baada ya saa tatu za mchana za kushiriki kurudi kwenye kazi ya kulipwa. Tunapaswa kuendelea na kuungana na waumini wale wengine kwa siku zilizobakia za sherehe ya mkate usiotiwa chachu. Kutoka kwa mganda tunaanza kuhesabu siku hamsini mpaka wakati wa pentekoste (Law 23:15,16). Kwenye kalenda tunaweza kuhesabu siku hamsini mpaka wakati wa pentekoste.
Kuna kazi kwa kila siku saba za sherehe ya mkate usiotiwa chachu. Siku ya saba ya Abib ya sherehe pia ni siku takatifu. Hii ni siku ya ishirini na moja ya Abib na inafanwa kama sabato (Kut. 12:15-18, Law 23:8, Kum. 16:8).
Kama mtu angeliweza kuchukua pasaka kwa sababu ya motto, safari au kwa mambo mengine yanayoweza kutokea, yeye angeweza kuchukua pasaka ya pili, inayotokea baada ya mwezi mmoja wa pasaka ya kwanza (Hes. 9:6-13).
Kwa wakati wakuweka pasaka tunaona kuwa makanisa mengi inaweka siku ya kufufuka kwa Yesu. Tutanena mengi kuhusu hii siku kwa karatasi ingine ambako tutasoma kuwa ni sherehe ya wakosa dini kwa miungu ishta. Pasaka iligeuzwa kuwa (Easter) siku ya kufufuka kwa Yesu wakati wa karne ya pili wakati kulikuwa na kutoelewana kwa kanisa kwa tarehe ya meza ya Bwana. Hii ilikuja kuwa kinyume cha quartodeciman.
Pentekoste yafunua mavuno ya pili na kusimamia wateule wa Mungu. Hawa ni wale wanaomwamini Mungu sasa na wale waliokufa wakiwa wamwemwamini, hawa walitii sheria na kutii mapenzi ya Mungu. Pentekoste ni siku ya hamsini, tukihesabu kutoka siku ya kuleta mganda wa sadaka ya kutikiswa nah ii ni siku ya Jumapili. Pentekoste yatufundisha vile Mungu anatupatia Yubile moja kwa muda wa miaka hamsini maishani mwetu na hili twaweshezwa kuelewa mpango wa Mungu, tena yatendeka kwa sabato saba kamilifu (Law 23:15, Kum 16:9).
Mwaka wa 30CE ni siku mitume walikusanyika pamoja kama vile Kristo alivyowaahidi kufanya; na walijazwa roho mtakatifu na wakaanza kunena kwa lugha (Mdo. 2:14). Kila mtu alinena kwa lugha yake mwenyewe, na watu elfu tatu walibatizwa (mdo 2:41)
Leo, tunaenda mahali penye jina la Mungu na kushika pentekoste (Kum. 16:6; Mt. 26:17-19). Na mara tatu kwa mwaka tunaagizwa kutoa sadaka za wiki twahitaji kuziangalia na kushika sabatu za Bwana (Hes. 28:26). Kwa hivyo tuna sabato mbili na tunahitaji kujitayarisha Ijumaa mapema, kazi ya kunua yahitajika kufanyika mapema Ijumaa, kama vile tunavyofanya siku ya kuleta mganda wa sadaka, huanza saa tatu na hafa pentekoste huanza saa tatu pia.
Mwandamo wa mwezi wa kwanza wa mwezi wa saba ni siku ya baragumu. Yashikwa kama sabato, na tunaungana pamoja na wanaoamini kama sisi (Law 23:24,25; Hes 29:1). Siku hii inafunua baragumu ya saba itakayolia wakati wa kurejea kwa masihi hapa duniani kuchukua mahala pa shetani. Yesu atarejea kama mfalme na kuleta mpango wa Mungu wa kutii sheria na mpangilio wake. (Rev 20:1-3)
Kwa wakati Fulani, baada ya kurejea kwa Yesu hapa duniani. Malaika wa Mungu atamfunga shetani hadi kuzimu (Ufu 2 19:7-10). Wakati huu kuna wale waliolala wakiwa wamekubali masihi na walio hai, waliosalalia watanyakuliwa pamoja ili waungane n masihi (1Kor 15:6,18, 1Thes 4:13-16, 2Pet 3:4). Watu hawa watageuza miili na kupewa ya kiroho. (1Cor. 15:51-52), hili jambo litatendeka kama kifo, lakini itatendeka maramoja, wateule wataenda kuwa na masihi huko Yerusalemu, ili wamsaidie Yesu kutawala nchi (Ufu 20:4-6) huu ni ufufuo wa kwanza na Bibilia yasema ya kwamba ni ufufo ulio bora (Ebr. 11:35).
Siku ya kumi, mwezi wa saba, tunashika siku ya upatanisho (Law 23:27,28; He 29:7). Inafunua kufungwa kwa shetani (Ufu. 20:1-3). Hapa watu wazima waliobatizwa ni waumini wa kanisa, wanafunga kuanzia 9th jioni hadi 10th usiku wa mwezi wa saba (Law 23:27-32). Anayekataa kujitesa siku hiyo atakataliwa na Mungu (Law 23:29).
Shetani atakapofungwa, Yesu na wateule watakuwa na wakati wa kutayarisha nchi ili waanze miaka elfu, watu watapangwa na kabila zao, hekali la Bwana litawekwa huko Jerusalemu, na watoto na watu wazima wasiokuwa na mwili war oho wanahitajika kutayarishwa kuwa makuhani na wafalme.
Siku ya kumi na tano mwezi wa saba (Tishri) tunaweza kusherekea sikukuu ya viwanda, ni sabato ya Bwana na tunaungana pamoja na wateule wa Mungu (Law 34-35, Hes. 29:12), Ni mara ya tatu tunayoambiwa tuwe pale penye jina la MUngu na tutoe sadaka, hii uanza mbele ya mchana wa 15th (Kum 16:16-17). Siku ya upatanisho yafunua siku ile Yesu ataleta mpango wa Mungu wa kutii sheria hapa duniani.
Kwa miaka elfu dunia haitakuwa na utawala wa shetani, watu watapokea baraka wakitii sheria za Mungu na laana kwa wale wasiotii sheria (Ufu. 20:7). Mwisho wa miaka elfu, shetani ataachiliwa tena (Ufu. 20:8) Shetani atawadanganya watu kumuasi Mungu tena na kukataa Yesu, sheria za Mungu na utawa la wa Yesu. Masihi na wateule wataukomesha wasi wa shetani na watu wake kwa mara ya mwisho; Maovu yote, kama vile wizi, kuua, kudanganya na mengine yatatupwa katika ziwa la moto, itaishi kama akumbusho kwa kila mtu (Ufu. 20:10). Itakumbusha watu ya kwamba maovu yote yameharibiwa.
Watu wengine wanafikiri ya kwamba watu watachomwa milele, lakini hii si kweli, Mungu wetu ni wa huruma na hatarushu watu kuteseka milele kwa kuwa Mungu aliumba viumbe vyote, ako na uwezo wa kusimaliza pia, kama vile tu Yesu Kristo alikuwa kiumbe cha kiroho na akawa mwanadamu. Satan na malaika walioanguka watafanywa viumbe wa kimwili (Isa 14:16, Eze. 28:16-19) kama vile kuna watu waliokufa bila kumjua Mungu na njia zake, hivyo ndivyo shetani na maleika watapata nafasi, ya kuwa viumbe wa kiroho, lakini hawatapata mamlaka kama walivyokuwa hapo awali.
Siku kuu ya mwisho inawekwa kama sabato (Law 23:36, Hes. 29:35) inafunua ufufuo wa pili. Itakuwa baada ya miaka elfu ikiisha (Ufu. 20:5, ni ufufuo wa kufundisha na luonya (Jn. 5:19). Wale wafu wote watafufuka na kuwa na miaka ishirini wale walikufa kama watoto au watu wazima watafufuka na miaka ishirini. Watakuwa na yubile mbili au miaka 100 yakusoma njia za Mungu (Isa. 65:20). Mungu hapendi yeyote yule angamie (1 Pet 3:9; 1 Tim 2:4; Tit 2:11) Ama afe kifo cha pili. Hakukuwa na ufufuo baada ya kifo cha pili, kwa kuwa Mungu aliumba vitu vyote, wanadamu wote kutoka kwa Adamu na hawa na malaika walioanguka watapa mamlaka katika ufalme wa Mungu.
Kutakuwa na nchi mpya na mbingu mpya na hakutakuwa na bahari (Ufu 21:1). Yerusalemu mpya itashuka kutoka mbinguni kuja duniani (Ufu 20:10). Hakutakuwa na mwezi au jua kwa kuwa utukufu wa Mungu na mwanakondoo atakuwa mwangaza wa mji. Hekalu lina milango kumi na miwili na watu wote wa dunia wataingilia mlango mmoja wa kabila kumi na mbili na mitume kumi na wawili, Mungu atakuwa yote kwa wote (1Kor. 15:28; Efe 4:6). Watu na malaika watafanya kazi pamoja na malaika katika mpango wa Mungu.
Watu wengi wanaamini sikuu na siku takatifu zimepita, ama zinaitwa siku takatifu za wayahudi, lakini walipewa yuda na Israeli, watu wengine wanaamini kuwa mpango wa Mungu ulikwisha Yesu aliposulubishwa msalabani. Lakini kifo chake kilikuwa mwanzo wa kurudisha mwanadamu kwa Mungu, tangu Adamu na Hawa watende dhambi kwa kifo chake Yesu Kristo ni wa kwanza katika ufufuo kuingia kwa Mungu.
Kila sikukuu yasimamia mpago wa Mungu unapoendelea, kwa hivyo lazima tuishike, Mungu alipea Kristo sikukuu na Kristo akapeana kwetu. Yesu na mitume walishika sabato mwandamo wa mwezi, na sikukuu (Kol. 2:16) kanisa kimeshika sabato mwandomo wa mwezi sikukuu zaidi ya miaka elfu mbli katika maika elfu ua Yesu walimwengu watashika sabato mwandame wa mwezi na sikukuu (Isa 66:23, Zec 14:16-19).
Sikukuu ni wakati wafuraha, tunaweza kuangalia wakati Yesu atarundisha ufalme kwa Baba yake, kila mtu atashika sikukuu na siku takatifu kama vile Baba atakavyoamuru!
q