Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[CB25]

 

 

 

 

Torati ya Mungu

(Toleo La  2.5 20030828-20061114-20121114)

 

Hii ni hitimisho fupi ya Torati ya Mungu na jinsi inavyohusika au kutenda kazi kwenye maisha yetu. Baadhi ya taarifa zimechukuliwa kutoka kwenye jarida la Amri Kuu ya Kwanza (Na. 252) iliyochapishwa na kanisa la CCG.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

(Hati Miliki ©  2003, 2006 Diane Flanagan, ed. Wade Cox)

(Tr. 2014)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Totari ya Mungu  


 


Torati au Sheria ya Mungu inatokana na asili yake hii. Sheria hii imewekwa kwa manufaa yetu na kwa manufaa ya sayari hii yote ya dunia. Familia zetu, miji yetu, mataifa yetu na hata kwa faida ya ulimwengu wote mzima kwa zaidi pale tunapoishika Torati au sheria za Mungu (Zaburi 55:19). Tunaitii Torati ya Mungu kwa kuwa tunapenda kufanya hivyo. Tunafanana na asili kamilifu ya Mungu (2Petro 1:4). Kama Mungu na Torati yake hawatenganishi, ni sahihi sana kwamba inafuatia kama sisi tunapozishika Sheria za Mungu na kwamba ndipo hata sisi tunazidi kufanana tena na tena kuwa sawa na Mungu (1Yohana 3:2). Torati hii ni ya Eloa (Ezra 7:14). Ni kama Mungu alivyo wa milele na habadiliki, na ndivyo ilivyo pia kwamba Torati yake ni ya milele na milele, na pia haibadiliki.

 

Ni kama alivyo Mungu wa Pekee na wa Kweli kuwa ni pendo (1Yohana 4:8) ndivyo pia ilivyo Torati nayo ni upendo (Warumi 13:10). Jambo linguine la kufurahisha sana ni kwamba, kama vile Mungu alivyo ni mtakatifu na mwenye haki, ndivyo ilivyo pia kwamba Torati yake ni takatifu na inajali haki (Zaburi 119:172). Torati ni takatifu, na njema (Warumi 7:12) na kweli (119:142). Hii inaonekana kumaanisha kwamba Mungu amoja na Torati yake wanaendelea wote kuishi.

 

Sheria au Torati ni kamilifu (Zaburi 19:7) na ni sheria kamilifu na yenye uhuru (Yakobo. 1:25, 2:12). Sheria kamilifu ya Mungu nay a uhuru imekusudiwa kutufanya sisi tuwe kwenye uhusiano mkamilifu pamoja naye na wengine. Hatahivyo, Roho Mtakatifu ni wa muhimu ili tuweze kuifuata sheria hii kamilifu ya uhuru kikamilifu. Hii itakuwa sahihi kwa kadiri tunavyoendele kuikulia imani na kuishika Torati ya Mungu.

 

Amri za Mungu

Totari imefanywa kwa migawanyiko miwili ya Amri Kuu Mbili. Hii inafanya misingi ya Torati yote na Ushuhuda wa manabii, pamoja na ule wa Yeu Kristo, kama ilivyoandikwa kwenye Biblia. Amri Kuu ya Kwanza imeandikwa kuwa: “Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. na Amri Kuu ya Pili inafanana nayo ikisema: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.”

 

Kwa kweli ujumbe wote kutoka kwenye Biblia hadi kwenye historia yote zimekuwa zikihusika na kumfanya mwanadamu ampende na kumtii Mungu na kumpenda jirani. Amri hizi Kuu Mbili ndizo zilizogawanywa hadi kuzifanya kuwa Amri Kumi. Hizi ni msingi muhimu wa torati yote, lakini torati haijakomea tu kwenye hizi Amri Kumi peke yake. Bali inapasa iwe kwenye mioyo yote na akili na rohoni. Amri sita za mwisho zinahusika na umuhimu wa kumpenda binadamu mwenzetu. Yatupasa kuwapenda majirani zetu kama nafsi zetu, kwakuwa kama hatutawapenda majirani zetu tunaowaona, tutawezaje kumpenda Mungu tusiye muona (1Yohana 4:20-21).

 

Kazi yetu ni kuwa tayari na kutubu kikweli kwa Mungu Aishiye. Yeye ni Mungu wa waliohai na sio wa wafu (Mathayo 22:32).

 

Kristo alikuwa ni elohim au mwanadamu katika ulimwengu wa kiroho aliyewafundisha kina Adamu na Hawa Torati ya Mungu. Dhambi iliingia duniani kwa kupitia Adamu (Warumi 5:12-14). Kwa hiyo, Torati ya Mungu ilikuwa pia iikishikwa kweenye Bustani ya Edeni. Ia alikuwa ni huyuhuyu Krtisto akiwa kama Malaika pale Sinai, aliyempa tena Musa ile Torati (Kutoka 20:1,22; Kumbukumbu la Torati 4:12,13; 5:22). Iliandikwa na Yahova (Kutoka 31:18; 32:16) kwenye mawe (Kutoka 24:12; 31:18) na akapewa Musa (Kutoka 31:18). Musa alizoweka hizi mbao kwenye Sanduku la Agano (Kumbukumbu la Torati 10:5).

 

Torati hii inahusika na mambo ya kimwili. Hii ni kanuni ya wema na ubaya. Yatupasa tuishike torati hii yote (Yakobo 2:10). Tunahukumiwa na Torati (Yakobo. 2:12).  Kuishika torati kunatufanya kuwe mbali na woga, kujisikia hukumu au kujisikia vibaya. Sheria hizi sio ngumu sana kwetu kuzishika (Kumbukumbu la Torati 30:10-11).

 

Kuvunja Sheria ni Dhambi

Kutokana na Torati ndipo tunaweza kujua dhambo ni nini au ipi (Warumi 3:7, 20). Dhambi ni uvunjifu wa sheria (1Yohana 3:4). Hatupaswi kuvunja sehemu yoyote ya sheria hizi (Mathayo 5:19). “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.” (Yakobo 2:10). Kwa mfano, kama tutafanya kila kitu vizuri na tusiishike na kuiheshimu siku ya Sabato na kuitakatifusha ndipo tunakuwa tumevunja sheria.

 

Ili kujifunza zaidi kuhusu dhambi jisomee jarida la Dhamb ni Nini? (Na. CB26).

 

Nia au mapenzi ya mwili ni uadui au yapo kinyume na Mungu. Hayapendi kuzitii Sheria za Mungu (Warumi 8:7). Mungu alijua hilo lingekuwa ni sababu kwa hiyo aliiuweka mpango kamilifu ili kumridisha kiumbe wake kwake mwenyewe.

 

Kitendo cha kuikataa Torati ya Mungu ndicho kimesababisha kuwepo na huzuni nyingi na mateso mengi ulimwenguni leo. Mwanadamu anapenda kufana mambo yake mwenyewe na yanayopendeza machoni pake mwenyewe. Kuna njia ionekanayo njema machoni pa mtu lakini mwisho wake ni mauti (Mithali 16:25). Kuitii Torati ya Mungu kutarejeshwa tena na Masihi, au vinginevyo, mataifa watakufa kwa njaa. Kuiasi Torati ya Mungu ni kitendo kinachoadhibika kwa namna zote mbili, yaani kwa mtu mmoja mmoja na kwa kikundi ia. Mungu anayatendea mataifa kama anavyozitendea familia.

 

Dhana inayohusiana na neema

Ni kwa kupitia Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, ndipo kazi za Ibilisi zinaharibiwa (1Yohana 3:8). Ni Kristo ndiye anayetusafisha dhambi zetu zote (1Yohana 1:7).  Ingawa mshahara wa dhambi ni mauti, karama ya Mungu ni uzima wa milele kwa kupitia Yesu Kristo (Warumi 6:23). Kwa kuwa Mungu alimkomboa au kumrejesha mwanadamu kwake pamoja na waasi wote kutoka mautini, neema imeonekana (Warumi 5:12-21). Neema ni zawadi ya bure kutoka kwa Mungu. Inatubidi tuishi na tuenende kwa Roho (Warumi 8:4-6). Sheria inabidi ishikwe kwa kiwango cha kiroho sasa. Sheria haijaondolewa na neema iwapo kama tutaishika sheria katika Roho Mtakatifu.

 

Hatujaokolwa kwa kuzishika sheria bali tumeokolewa kwa neema. Bila Roho Mtakatifu hatuwezi kuzishika sheria kikamilifu. Tunazishika Sheria kwa sababu tunataka kumpenda na kumtii Mungu. Mara zote yamekuwa ni makusudi ya Mungu kwamba tuishike sheria, lakini mfalme wa dunia hii amewafundisha watu kinyume na ameibadili Sheria za Mungu na Kalunda yake ili wasizishike kikamilifu. Akaiweka Kalenda iliyo kinyume na na kalenda ya Mungu na kuufuata utaratibu mwingine wa ibada ni kukufuru, na uvunjaji wa sheria. Ni kumuabudu mungu mwingine.

 

Torati ni ya kiroho

Sheria ni ya kiroho (Warumi 7:14). Kristo aliitukuza au aliiweka sheria kwenye kiwango cha juu sana cha kiroho (Isaya 42:21).

 

Kwa kweli Kristo alizisisitiza, au alikiinua kiwango na sasa tunapasa kuishika torati kwa maana ya kiroho na kuongezea njia za kimwili. Musa na manabii wengine wote, hadi kipindi cha Masihi walizishika, na hatimaye sheria ziliandikwa kwenye mioyo ya wateule. Wale waliobatizwa wanahukumiwa katika roho kuhusu hizi sheria (Yakobo 2:12; Warumi 2:27; 2Wakorintho 3:6).

 

Sheria za Kiibada na za Sadaka

Sheria za ibada zilinenwa na Yahova (au Kristo), zikaandikwa na Musa (Kutoka 24:3,4,Kumbukumbu la Torati 31:9) na zikatolewa kama nyongeza kwenye Amri Kumi (Kutoka 24:12). Iliandikwa kitabuni na Musa akawapa Walawi ambao waliambiwa waiweke kwenye Sanduku la Agano (Kumbukumbu la Torati 31:25-26). Inajiri mambo ya kiibada na utakatifu. Inaelekeza utoaji wa sadaka kwa ajili ya dhambi (soma Mambo ya Walawi sura za 1-2). Sadaka ya Kristo ilizikomesha sadaka hizi au ilikomesha umuhimu wa kuendelea na mfumo huu wa sadaka (Waefeso 2:15, Wakolosai 2:14). Sheria hii haukusababisha kitu chochote kuwa kikamilifu (Waebrania 7:19).

 

Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi waliambiwa umuhimu wa kuendeleza utaratibu wa kumtolea Mungu dhabihu. Kwa hiyo, utaratibu wa kuto dhabihu ulikuwepo hata kipindi cha Adamu na Hawa hadi mwaka 30 BK, ambao ulikuwa ni mwaka ambao Masihi aliuawa na kufanyika kuwa sadaka ile kamilifu na iliyokubalika. Mungu aliwapa Yuda miaka 40 ya kutubu na kubadilika lakini hawakubadilika. Hekalu la Yerusalemu lilikuwa bado linaendelea kufanya ibada hizi za kutoa dhabihu za wanyama, lakini mnamo mwaka 71 BK Vespasian alifunga sehemu ya mwisho iliyobakia ya hekalu huko Leontopolis, iliyoko huko Misri.

 

Kristo aliyahitimisha mambo yote yahusuyo na mambo ya sadaka; kwa hiyo utaratibu wa kutoa sadaka hautumiki tena leo. Utoaji huu wa sadaka utakuja kurejeshwa tena huko Yerusalemu, lakini itakuwa ni sadaka ya asubuhi tu ndiyo itatolewa (Ezekieli 46:13). Sadaka za alasiri ambayo tunaambiwa kwenye Hesabu 28:3-4 zimebadilishwa kwenye Ezekieli 46.  Thamani na kiwango cha wanyama, nafaka na pia mafuta pia zimebadilika (Ezekieli 46:1-15). Baadhi ya sehemu za utaratibu wa utoaji wa sadaka hatuwezi kuzielewa kikamilifu hadi wakati Yesu Kristo atakapokuja tena hapa duniani na kuanzisha utaratibu na mambo mengine wakati wa kipindi cha utawala wa Milenia.

 

Ni kitu gani basi kilichogongomelewa mtini (kwenye mti)?

Imani ya Makanisa kongwe ya siku hizi hufundisha kimakosa sana kwamba Torati ya Mungu ndiyo iliyogongomelewa msalabani (mtini) kwa kifo cha Kristo. Wameitafsiri kimakosa Wakolosai 2:14-15. Andiko hili linaelezea kuhusu “hati ya masitaka yetu” liyo chini ya Torati. Hiki ndicho kilichogongomelezewa pale mtini, na sio Torati yenyewe ya Mungu. Mara tu baada ya Kristo kutolewa sadaka aliziweka dhambi zetu mbali sana kama vile mashariki ilivyo mbali na mashariki, kwa kuwa alilipa adhabu ya mauti kwa ajili yetu. Ingawaje Kristo alilipa gharama kwa dhambi za wote wenye mwili, bali bado tu tunahitaji kuishika sheria. “Hati hii ya mashitaka” inaitwa cheirographon.

 

Mapokeo ya wanadamu

Tunaambiwa kuishika Torati ya Mungu na siyo mapokeo ya wanadamu. Tumeona wote mapokeo haya au imani hizi za wanadamu. Tunaweza pia kuyasoma maneno ya Yesu Kristo kuhusu jambo hili (Mathayo 15:2-6; Marko 7:3-13). Tunaambiwa kuwa kama watanena kinyume na torati na ushuhuda wa Kristo hakuna nuru kwao (Isaya 8:20). Sheria zilizotungwa kienyeji na Mafarisayo zilifanyika kuwa mzigo kwa watu wa Yuda. Hii siri ya uasi ilikuwa inatenda kazi Kanisani hata wakati wa kina Paulo na Yohana (2Wathesalonike 2:7-10; 1Yohana 2:3-5).

 

Tumeamriwa pia kuvundisha tofauti iliyopo kati ya yaliyo matakatifu na yasiyo matakatifu au yaliyo ya sikuzote na yasiyo ya sikuzote (Mambo ya Walawi 10:10; Ezekieli 44:23)    

 

Ufunuo 22:18-19 inatuambia kuwa hatuwezi kuzibadilisha Sheria za Mungu au kuyabadilisha Maandiko Matakatifu. Kama tukijaribu kuzibadilisha sheria zilizo kwenye Kitabu cha Mungu (Biblia), basi Mungu atatuondolea sehemu yetu kwenye mti wa uzima (Ufunuo 22:14). Wengine watajaribu kubadilisha au kuondoa kile ambacho Maandiko Matakatifu yanasema, na wanapojaribu kuiondoa Torati ya Mungu: lakini hii ni uwongo na haiwezekani. Na tusimsikilize mtu yeyote, mwanaume au mwanamke anayetuambia kuwa sheria za Kristo zimetanguka.

 

Kristo alisema hata yodi moja ndogo (ambayo ni sehemu ndogo sana ya torati) haitaweza kutanguka au kubadilika hadi mbingu na nchi zitakapoondoka (Luka 16:17). Tunajua sote kwamba mbingu na nchi bado zipo hata leo. Kwa hiyo, tunajua kwamba ndipo Torati yote ya Mungu inaendelea kusimama.

 

Mungu ameziweka Sabato na Miandamo ya Mwezi na Sikukuu. Imani au dini ya uwongo na bandia ya kuabudu siku ya Jumapili na kuadhimisha siku za Krismas na Easter ni mifumo na imani za Mungu Utatu na za Kipagani. Hizi haziruhusiwi wala hazikubaliki na Mungu. Ukristo wa siku hizi unaosema kuwa Torati au sheria za Mungu zimetanguka hawaelewi tofauti iliyopo kati ya torati na manabii na ujumbe wa Kristo na wa Mitume.

 

Tumeamriwa kusoma Torati katika mwaka wa Saba wa mzunguko kuanzia kwenye Siku ya Ukumbusho wa Kuzipiga Baragumu na kuishia siku ya mwisho ya Sikukuu ya Vibanda. Torati inasomwa pia kwenye miaka ya Yubil. Hii imeamriwa ili kuwafanya watu wasisahau au kupotoka au kupoteza mwelekeo kutokana na maagizo na amri za Torati. Shirika hili liitwalo makanisa ya Kikristo ya Mungu yaani [Christian Churches of God] husoma Torati na imefanya hivyo katika miaka ya 1998 na 2005 na 2012, mwaka mwingine unaofuatia  wa “Usomaji wa Torati” ni 2019, na tena 2026 na kisha kwenye miaka mingine ya Sabato itakayofuatia Yubile ijayo. Yubile ya mwisho ilikuwa ni mwaka wa 1977 na inayofuatia itakuwa ni katika mwaka mtakatifu wa 2027/28.

 

Kupatanishwa na Baba

Mungu anajua kila kitu (Isaya 46:10; Zaburi 147:5; Mathayo 24:36). Alijua kuwa viumbe wa kiroho watakavyotenda na jinsi mwanadamu atakavyotenda lakini hii haimaanishi kwamba Mungu anathibiti kila mienendo yetu. Bali inaonyesha tu jinsi alivyo na hekima yake ilivyo ya kushangaza na jinsi uweza wake wa kuelewa kila kitu ulivyo. Tangu Mungu alivyojua kuwa Shetani na Malaika wenzake waasi kuwa hatimaye wataasi, au kutenda dhambi na mwanadamu angetenda dhambi pia hatimaye, aliweka mpango mbadala uwepo hata katika kipindi cha kabla ya kuanza kwa mchakato wa uumbaji.

 

Mpango huu ulihitaji kuwepo na damu ya dhabihu ili kumrejeza mwenyedhambi kwa Mungu Baba. Kristo alikuja akiwa kama sadaka bora, kamilifu na inayokubalika (Waebrania7:27-28; 9:12; 10:10-19; 1Petro 3:18). Alikubaliwa na Mungu Baba kama Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa (Mambo ya Walawi 23:9-14; Yohana 20:17; soma bango kitita kwenye biblia ya The Companion Bible) kuhusu siku ya ikwanza ya juma ya mwaka 30 BK, mwaka ambao Kristo alisulibiwa.

 

Kristo sasa ndiye Kuhani wetu Mkuu (Mathayo 20:11-18: Zaburi 110:4). Alilipa deni au garama ya wale wote waliotenda dhambi kwa kuwa alijitoa sadaka mwenyewe na aliishi maisha yasiyo na dhambi (Waebrania 4:15: 1Yohana 2:2). Alikuwa mtii hadi kufa (Wafilipi 2:8). Kristo ndiye aliyeleta wokovu kwa wanadamu kwa kuwa kwake mtiifu kwa Baba yake. Soma jarida la Yesu ni Nani? (Na. CB2).

 

Ni jinsi gani watu wote wangeweza kumjongea Mungu Baba. Tunapofikisha umri wa utu uzima ndipo tunaweza kubatizwa na kumpokea Roho Mtakatifu. Soma jarida la Roho Mtakatifu ni Nini? (Na. CB3). Kabla ya kufanyika ubatizo inatupasa kumfundisha mlengwa na sisi sote umuhimu wa kufanya toba kuzitubia dhambi zetu. Mara tu tunapotubu na kubadilisha njia zetu, ndipo Mungu hutusamehe kabisa na dhambi zetu. Hata kama hatujabatizwa, inatupasa kumuomba Mungu atusamehe dhambi zetu. Inatupasa pia kuwaambia wale tunaowaumiza kuwa samahani au kuwataka radhi; ila tunahitaji kujitahidi kutorudia makosa hayohayo tena.

 

Baraka za Kuishika Torati ya Mungu

Wakati Kristo alipokuwa mwanadamu katika mwili alizishika Sheria zote za Torati (Mathayo 5:18-19). Mwili wa Kristo ambao ni Kanisa, linazishika Sheria za Mungu (Warumi 2:13, Zaburi 119:1-3). Mkristo anayeishika Torati amebarikiwa (Yakobo 1:25). Mtu aliyeongoka au mwongofu anahitajika aishike Torati (Zaburi 119:1 nk.).

 

Ili sisi tuwe na sehemu kwenye Ufufuo wa Kwanza wa wafu inatupasa kuzishika amri au Torati ya Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12). Ufunuo 22:14 inasema, “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.” Andiko hili la aya ya 14 kwenye Biblia the Companion Bible linsema kuzifua nguo zaon ni kuzishika amri na sheria za Mungu. Kwa habari zaidi kuhusu Amri za Mungu soma jarida la Amri Kumi za Mungu (Na. CB17).

 

Kama tutazishika amri za Mungu, ndipo Mungu atakaa katikati yetu (Yohana 14:15, 15:10). Kama tunataka kuingia kwenye uzima wa milele, inatupasa kuzishika amri za Mungu (Mathayo 19:17). Kwa kuishika Torati ya Mungu, ndipo hata sisi tunafanana na Mungu, tukifanana na yeye (2Petro 1:4).

 

Mungu kamwe habadiliki na wala hapiti au kupitwa na wakati (Malaki 3:6; Yakobo 1:17). Hebu na tujaribu na kujitahidi sasa kuzishika Sheria na amri zake kikamilifu sana kwa kla siku na siku zote ili tuwe kama Mungu zaidi na zaidi (Waefeso 4:23-25). Hebu na tufurahie na kuburudika tunapoishika Torati yake Eloa (Zaburi 119:1 nk.) na tuwe mfano kwa wanadamu wengine tukitilia maanani jinsi utaratibu wa Mungu kuhusu sheria uiivyo na unavyoanya kazi.

 

q