Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[CB026]
Je, Dhambi Ni Nini?
(Toleo La 2.0
20030831-20061120)
Somo hili ni rejea fupi kuhusu jinsi dhambi
ilivyokuja na kuingia ulimwenguni, maana ya dhambi, na nini matokeo mabaya
yamjiaye mwanadamu kutokana kwayo, na Malaika waasi na sayari ya dhambi.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 2003, 2006 Diane Flanagan, ed. Wade Cox)
(Tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Je, Dhambi Ni Nini?
Biblia inatueleza kuhusu hii dhambi kuwa ni kitu gani. Inafafanua kuwa dhambi
ni “uasi au kuvunja sheria” (1Yohana 3:4). Dhambi ni msukumo wenye nguvu ambao
unatufanya sisi tupende kuziendea njia ambazo ni kinyume kabisa na mapenzi ya
Mungu. Kwa hiyo, badala ya kubarikiwa kwa kuyafuata mapenzi ya Mungu,
tunaadhibiwa kama tutaishi kwa kuzifuata na kuishi kwa kufuata tamaa za
Shetani, ambazo ndizo dhambi. Njia na matendo ya Shetani ni kinyume kabisa na
zile za Mungu. Mungu anazichukia dhambi (Mithali 6:16-19). atendaye dhambi
ni wa Ibilisi; (au Shetani) kwa kuwa
Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. (1Yohana 3:8).
Mkristo anakailiwa na mapambano yasiyo na mwisho kwenye maisha yake ya kila
siku katika kukabiliana na kuzishinda dhambi. Inatupasa kuwa washindi kama
tutaweza kujipatia ukamilifu wa tabia na mwenendo mtakatifu na wa haki. Shetani
anapenda na kututaka sisi kuidharau Torati au Sheria za Mungu. Kwa hiyo, kama
tutashindwa na kukata tamaa kwenye harakati zetu za kupambana na dhambi, basi Shetani
atashinda.
Je,
kuna dhambi nyingine zilizo kubwa kuliko nyingine?
Baadhi ya makanisa yanayojiita yenyewe kuwa ya Kikristo yanafundisha kwamba
kuna dhambi za mauti na zisizo za mauti. Wanasema kwamba baadhi ya dhambi ni
mbaya au kubwa zaidi ya nyingine na kwa hiyo wazitendao wanastahili kuadhibiwa
kwa adhabu kali zaidi. Wanasema kuwa dhambi za mauti ndizo zinawapelekea kwenda
jehanamu na dhambi nyingine za kawaida zinasameheka kirahisi na huenda baada ya
muda mfupi akiwa huko Pargatory mtu azitendaye dhambi hizi zisizo za mauti
anaweza kusamehewa na kwenda Mbinguni. Dhana hii inatokana na neno lililotumiwa
na mtume Paulo kuhusu ukweli kwamba kuna dhambi ambazo zinampelekea mtu kuingia
mautini. Hata hivyo, dhana au wazo ama fundisho la mtu kwenda Mbinguni na Kuzimuni
akiwa na roho isiyokufa anapokufa mauti sio fundisho la Kikristo.
Dhana na fundisho la watu kwenda ama Mbinguni au Jehanamu wanapokufa linatokana
na mafundisho ya imani za kipagani. Neno litumikalo kuelezea Kuzimuni ni Sheol,
na linamaanisha kaburini
ambako wafu huzikiwa. Hades lilikuwa ni neno la Kiyunani lililotumiwa
kwa Kiebrania, ambalo pia linamaanisha kaburi. Neno la tatu
lililotafsiriwa kama kuzimu kwenye Biblia ni Jehanamu [Gehenna],
ambayo ilikuwa ni shimo la takataka au jalala lililokuwa nje ya mji wa
Yerusalemu ambapo walipatumia kwa matumizi ya kuwachomea au kuwateketeza mbwa
na takataka nyingine. Neno linguine lililotumika kwenye Biblia ni tartaros
au tartaroo, ambalo lilikuwa ni shimo lililobakizwa kwa ajili ya malaika
wakati watakapofungwa humo. Hakuna kitu kama hicho kwenye maandiko
kijulikanacho kama kuchomwa na kuunguzwa moto milele kwenye Jehenamu.
Mtume Yohana anasema
hapa kuwa kuna dhambi zisizo za mauti.
Hii inamaanisha tu kwamba ni dhambi tunazozitenda au tunazokabiliana nazo
wakati tunaposhughulika na shughuli zetu za kila siku. Hata hivyo, kwa njia ya
toba tunawekwa huru kutokana na dhambi hizi na tunaruhusiwa kubakia kwenye
Mwili wa Kristo na kwenye Ufufuo wa Kwanza wa Wafu ulioelezwa kwenye Ufunuo 20.
Wale wanaotenda dhambi kwa makusudi watakwenda kwenye Ufufuo wa Pili wa wafu. Hata
hivyo, kila aliyezaliwa na Mungu hawezi kutenda dhambi (1Yohana 3:9).
Dhambi
ya Lusifa
Wakati Mungu alipoumba viumbe wa kiroho aliwaumba wakiwa wakamilifu. Sheria
au Torati ya Mungu pia ailikuwpo tangu mwanzoni. Lakini ni kama tunavyoweza
kufanya maamuzi mema na mabaya na ndivyo ilivyo hata kwa hawa viumbe wa kiroho
nao hufana vivyohivyo. Mungu hahitaji wanadamu au viumbe hawa wa kiroho
wanaoendelesha na kufanya mambo yao kama maroboti. Bali Mungu anawataka viumbe
hawa wote wawili, yaani wa kiroho na wa kimwili wanaopenda kutii Sheria na amri zake kutoka mioyoni mwao na sio tu
kwa sababu wanalazimishwa kufana hivyo.
Lusifa aliumbwa akiwa mkamilifu (Ezekieli 28:12-15). Alikuwa ni Kerubi
mtiwa mafuta alikuwa anakifunika Kiti cha Enzi cha Mungu. Kusifa, ambaye maana yake
ni mleta nuru, aliwa na wadhifa wa nyota
ya asubuhi wa sayari hii (Isaya 14:12). Kwa wakati huohuo, uovu ulionekana
ndani yake na alitenda dhambi na ndipo akatenda dhambi (Ezekieli 28:15-16).
Neno lililotafsiriwa kama muovu ni
SHD 5766 na lina maanisha ukengeufu, udhaifu
wa dhambi, kutoaminika, uwongo, udhalimu, na kutojali haki au dhuluma. Kwa hali hii ya kuonekana uovu ndani yake
ndipo alitenda dhambi, Mungu Baba alimtupa kutoka kwenye mlimani wa Mungu (Ezekieli
28:16). Jina la Lusifa ndipo likabadilishwa na kuitwa Shetani (Zekaria 3:1), ambalo
maana yake ni mshitaki (1Petro 5:8; Ufunuo 12:10; Zekaria 3:1). Mshitaki ni mtu
anayejaribu kutuumiza. Shetani hutuumiza sisi kwa kutushitaki mbele za Mungu.
Dhambi za Shetani zilimfanya aondolewe kutoka kwenye kazi na majukumu yake
aliyokuwanayo kama Kerubi Afunikaye Kiti cha Enzi cha Mungu. Shetni aliivunja Amri
ya Kwanza kwa kujaribu kwake kujiinua juu dhidi ya Mungu Mmoja wa Pekee na wa
Kweli. Yesu Kristo alimuelezea Ibilisi kuwa ni ‘muongo na baba wa uongo’ (Yohana
8:44).
Kazi na wajibu wa Shetani wa kuwa ni Kerubi Afunikaye kwa sasa iko wazi.
Shetani amefanywa kuwa ni mwangalizi au mfalme wa hii Dunia na alipaswa
kuhakikisha na kusaidia kuwa Sheria za Mungu zitunzwe na kuheshimiwa hapa
duniani. Shetani alipewa takriban miaka 6,000 ya kuitawala hii Dunia. Miaka 6,000
karibu inaisha na tunaweza kusema kuwa mateso yote ya duniani kwamba Shetani
hakuzifuata Sheria za Mungu au Mpango wake.
Shetani bado ni “mfalme wa nguvu za anga” (Waefeso 2:2). Hii inamaanisha
kwamba Shetani na Malaika wengine walioasi wanaweza kushawishi mia zetu na
mawazo yetu kupitia miziki, runinga, mijadala, nk. Tumeambiwa kujihadhari
katika mawazo na nia zetu (2Wakorintho 10:3-5). 2Wakorintho 4:4 inatuambia kuwa
mungu wa dunia hii amepofusha mawazo ya watu ili wasiamini.
Kimsingi, kila kitu kiliumbwa kikiwa kikamilifu lakini wakati Malaika waasi
walipojaribu kukiinukia Kiti cha Enzi cha Mungu walitupwa chini hapa Duniani (Isaya
14:13-14). Na hii ndiyo sababu Luka10:18 inasema, “Nilimuona Shetani akianguka
chini kama umeme”. Mara tu baada ya uasi wa kiroho ulioongozwa na Shetani, ambao
kwao theluthi moja ya malaika walishiriki (Ufunuo 12:4) Dunia ilikuwa tupu,
yaani tohu na bohu, au haikuwa na umbo kamili na tupu (Mwanzo 1:2).
Kwa kuwa ilikuwa imeumbwa kamilifu, Dunia iliharibiwa kwa sehemu kutokana na uasi
wa Malaika hawa waasi.
Dhambi
ya Adamu na Hawa
Kabla ya kumuumba mwanadamu hapa Duniani, dunia ilifanywa au kutengenezwa
tena na kuifanya kuwa ni mahala pazuri kukaliwa na mwanadamu pia. Soma jarida
lar Hapo Mwanzo (Na. CB5).
Mwanadamu aliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27). Wanadamu wa
kwanza waliumbwa katika hali ya ukamilifu pia. Waliishi kwa amani na
walijifunza Sheria za Mungu. Yesu Kristo, aliwa kama malaika kwenye bustani ya
Edeni, aliwafundisha Adamu na Hawa kuhusu Sheria za Mungu.
Kama tujuavyo kutoka kwenye Biblia, Shetani alimzidi akili Hawa kuhusiana na
kula tunda la mti alioakatazwa kula. Adamu na Hawa walitenda dhambi kutokana na
tama yao ya kuchukua kitu ambacho hakikuwa chao. Pia waliingia majaribuni kwa
kuiba kutoka kwenye mti ambao Mungu aliwaambia kuwa wamekatazwa. Adamu na Hawa
walilaaniwa kwa ajili ya kutomtii kwao Mungu (Mwanzo 3:14-16). Matokeo ya uasi
wao na dhambi zao, mauti yakawapata watu wote (1Wakorintho 15:22; Warumi 5:12).
Kwa habari zaidi kujifunza kuhusu kilichowatokea kina Adamu na Hawa soma jarida
la Adamu na Hawa Kwenye Bustani ya Edeni (Na.
CB6).
Matokeo
ya dhambi
Dhambo ni lile tendo la kuvunja Amri au Sheria ya Mungu (1Yohana 3:4). Tunajua
dhambi ni nini kwa kutuamanisha na Sheria za Mungu (Warumi 3:19). Kwa ajii ya
kujua zaidi kuhusu Sheria na Amri za Mungu soma jarida la Torati ya Mungu (Na. CB25). Watu wote wametenda dhambi (Warumi 5:12).
Matokeo mabaya (au mshahara) wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23). Yesu Kristo
alikuja kama mungu mdogo wa pekee aliyezaliwa katika mwii (Yohana 1:18) ili aje
kuipa fidia ya dhambi za watu wote pamoja na za Malaika walioasi. Kwa kuwa Yesu
aikuwa hapa akiwa kama mwanadamu na akaishi maisha yasiyo na dhambi, kifo chake
kililipia gharama kwa ajili yetu sisi sote. Kifo chake kilifanyika kuwa ni
dhabihu kamiifu na iliyokubaika ili kuturudisha sisi sote kwa Baba (Waebrania
7:27,28; 9:12; 10:10-19; 1Petro 3:18).
Ingawa tunajua kuwa tunaweza kumkaribia Mungu Baba yetu, bado kunaweza
kuwako na nadhara au gharama itupasayo kuilipa kwa ajili ya dhambi zetu.
Kuna mifano mingi kadhaa ya jinsi dhambi inavyoiathiri sayari yetu hii. Kwa
mfano, kwa kuwa hatuzifuati sheria na kanuni za vyakula alizoziweka Mungu, watu
wanapatilizwa kwa magonjwa sasa yatokanayo na ulaji wa nyama za wanyama najisi na
vyakula vingine vilivyo najisi pia. Viumbe najisi watokao majini (waliotajwa
kwenye Walawi 11:10) wameumbwa kwa makusudi ya kufanya kazi zao maalumu. Hata
hivyo, kwa kuwa wanaliwa na watu sasa kama chakula basi hawawezi kuzifanya kazi
zao na kusaidia sawasawa na Mpango wa Mungu kwa jinsi kama alivyowakusudia. Kwa
habari na kujifunza zaidi jambo hili, jisomee jarida la Sheria za Vyakula za Kibiblia (Na. CB19).
Mfano mwingine ni kwamba watu wengi hapa duniani hawangojei hadi kufikia
kipindi muafaka kwa kufunga ndoa kabla hawajashiriki ngono. Kwa hiyo, kuna watu
wengi sana sasa wanaoteseka na magonjwa yaliyotokana na maambukizi ya kingono
kama vile UKIMWI na mengineyo. Kwa hiyo, watoto wengi sana wanakosa kukulia
majumbani ambamo hakuna mama wala baba wa kuwahudumia na kuwapa mahitaji yao.
Kuna mifano mingi sana, lakini tatizo kuu ni kwamba ni kwa kuwa watu hawamuabudu
Mungu Mmoja, Wapekee na wa Kweli. Watu wengine wanaabudu fedha, teknolojia, au
miungu ya uwongo. Watu wengi leo wanapata mapumziko wakati wa Krismas kwa kuwa
nchi zao zinasema kuwa hii ni siku ya mapumziko. Wakati tunajua sana kuwa Krismas
inatokana na madhimisho ya wapagani wa dini na imani za kale na hatupaswi
kushiriki kwa namna yoyote ile maadhimisho haya. Soma jarida lisemalo Sababu Zinazotufanya Tusisherehekee Krismas (Na.
CB24). Kwa habari na kujifunza zaidi nasi soma jarida lisemalo Amri Kumi za Mungu (Na. CB17).
Tunatenda dhambi kila mara na tunaendelea kutenda dhambi, tunajiweka sisi
wenyewe mbali na Mungu. Lakini kila mara tunapomtii Mungu ndipo anapoyaelekeza
mawazo yetu na kuziongoza njia zetu (Mithali 16:3). Inatupasa kuomba, kujisomea
Biblia, na kujitathmini wenyewe ili kujaribu kuziona dhambi zetu. Mtume Paulo
alisema kuwa asingeweza kuijua dhambi hadi pale Torati ilipoifunua na
kumuonyesha kuwa kumbe ni kitu gani na vie ilivyokuwa (Warumi 7:7).
Dunia
iliyolaaniwa
Wakati tunapotenda dhambi kuna adhabu au matokeo mbaya yanayotupata sisi
kama mtu mmoja mmoja, na wakati mwingine yanawaambukia hata watoto na familia zetu,
taifa na hata kwa ulimwengu wote. Dunia ililaaniwa kwa sababu ya uasi wa Adamu (Mwanzo
3:17-19; Mwanzo 4:11,12).
Kama ilivyoelezwa mapema, wakati tunapozivunja sheria na kanuni ya vyakula
inaletea madhara kwa mtu binafsi, lakini pia inaleta madhara kwa ulimwengu.
Kwa kwa hatuzishiki na kuziadhimisha Sabato za mapumziko ya nchi, ardhi
inakuwa imezidi kulaaniwa zaidi. Mazao hayastawi vizuri kama yalivyopata kuwa
miaka mingi iliyopita huko nyuma. Watu wanaendelea kuugua na kuugua kutokana na
kupungukiwa na chakula bore chenye virutubisho asilia kwenye vyakula, na
ongezeko la matumizi ya makemikali na vimelea sumu kwenye mlolongo wa mchakato
wa chakula.
Kwa upande mwingine, ni kwa kuwa watu wanaendelea kuugua, sio lazima
kuamini kuwa watu hawa wanatenda dhambi. Mara nyingi sana Mungu huwaponya watu,
lakini mara nyingine anaamua kutowarejesha watu kwenye afya njema tena. Wakati
mwingine tunakuwa wazembe wa kutojiangalia vizuri nafsi zetu na kwa hiyo
tunapata magonjwa. Lakini tunaweza kurithi magonjwa pia kutoka kwa wazazi wetu.
Mtume Paulo alimudu kuwaombea na kuwaponya wengine lakini yeye mwenyewe
hakuweza kupona. Magonjwa kwenye jamii hii ni matokeo ya kuzikataa na
kuzipuuzia Sheria za Mungu kwa kipindi kirefu tangu uumbaji.
Ulimwengu
wa Shetani
Chini ya muundo au utawala wa Shetani mambo yamekuwa hayapangiliki na kila
mmoja, familia na hata taifa wanateseka. Mtu binafsi anayezitii na kuzitunza
Sheria za Mungu kikamilifu na huzipokea baraka. Sayari hii pia imeshikwa pia
imeshikwa kwenye utengamano maridhaw na inaweza kuendelea kuwasaidia watu wanayoiishi
ndani yake.
Tulifundishwa jinsi ya kuwatendea wenzetu na jinsi ya kuitendea hii sayari
yetu. Lakini dunia kwa sehemu kubwa imechagua kutozitii Sheria hizi za Mungu.
Tazama jinsi hali hii ya kutotumia vizuri kulivyotusababishia madhara,
machafuko ya mabadiliko ya tabia nchi, madhara ya maisha ya wanyama, kupotea
kwa viumbe muhimu kwenye mlolongo wa vyakula—yote haya yametokana kwa sababu ya
uvunjifu wa sheria. Hivi sasa orodha yao haina mwisho kuhusiana na mateso yale
yanayovumiliwa kwa ajili ya kutomtii Mungu.
Mambo yangekuwa tofauti kabisa kama watu wangetubu na wakaanza kumtii
Mungu. Tunapozitii Sheria za Mungu tunazipokea Baraka na kuw na amani rohoni na
kuridhika kuwa tunafanya jambo jema (Yakobo 1:25). Mtu mmoja mmoja, familia, na
dunia yote ingekuwa vyema kama wangeziamua kuzishika na kuzitii Sheria za Mungu.
Tumeambiwa kuwa tusiipende dunia au kitu chochote kilicho kwenye hii dunia.
Tukiipenda dunia, kumpenda baba hakumo ndani yetu. Duni pamoja na tama zake za
dhambi zitapita. Lakini yeye ayafanyaye mapenzi ya Mungu huishi milele (Yohana
15-17).
Mpango
wa Mungu kwa Viumbe Wake
Ingawa dunia imelaaniwa kwa ajili ya uasi wa Adamu na Hawa, Mungu aliuweka
mpango ili kuyapunguza matatizo. Wakati dhambi ilipoingia, utaratibu wa Yubile
ulianza. Utaratibu wa kuhesabu Yubile/Sabato ni utaratibu mkamilifu wa mambo
yote ya kiuchumi, mazingira, maadili na utaratibu wa kijamii kwa mwanadamu.
Unamlinda kila mtu binafsi yake na familia. Lakini mwanadamu bado anajaribu
kujitengenezea utaratibu wake mwenyewe na kuuasi utaratibu na Mfumo aliouweka
Mungu.
Yubile maana yake ni 50. Yubile inatokana na mizunguko ya miaka saba saba
ambayo ni sawa na miaka 49. Mwaka wa Yubile ni mwaka wa 50. Mambo ya Walawi
25:10 inasema, “Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika
nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila mtu
atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake”. Mungu ni mmiliki wa yote na anatutaka sisi
tuitumie hii Dunia.
Yubile inayofuatia mbele yetu itfanyika mwaka 2027/28. Masihi atakuwa
amekwisharudi hapa duniani mapema kabla ya mwaka huo ili kutayarisha mambo kwa
ajili ya Yubile hii. Tubile ile itakayoanza mwaka 2027/28 itakuwa ni Yubile ya
Yubile nay a hamsini tangu marejesho ya Ezra na Nehemia.
Tangu hapo na kuendelea, Mungu Baba yetu pamoja na Yesu Kristo wataitawala
hii dunia kutoka hapahapa Duniani. Wakati kutakapokuwa hakuna dhambi tena hapa
duniani, Mungu atakileta kiti chake cha Enzi ambacho kwa sasa kipo katika Mbingu
ya Tatu na kukilet hapa Dunini. Hakutakuwapo na jua tena wala mwezi kwa kuwa
Mungu mwenyewe ataitia nuru hii Dunia (Ufunuo 22:5). Mto wa maji ya uzima
utatiririka kutoka kwenye Kiti cha Enzi cha Mungu na cha Mwanakondoo (Ufunuo
22:1). Laana iliyoko leo duniani itaondolewa (Ufunuo 22:3).
Kwa kweli inashangaza sana hekima hii, uweza na rehema za Mungu Baba
alizonazo. Liuweka Mpango ambao unamfanya mwanadamu na Malaika walioasi kufanya
mamuzi kuchagua, lakini yaliyosababisha kutendeka dhambi na mauti. Lakini Mungu
aliweka namna hata kabla hajakiumba kitu chochote kile, ili kumrejesha
mwanadamu pamoja na Malaika walioasi warejee kwake. Kwa kipindi hiki mwanadamu
anamtii Mungu kwa kuwa wanapenda iwe hivyo. Mungu hawalazimishi watu wamtii. Ni
vigumu kufikiria muda au kipindi ambacho wandamu wote waliowahi kuumbwa watakapokuwa
wanazishika Sheria za Mungu (Ezra 7:14) na wanadamu wote watakapokuwa viumbe wa
kiroho, wakimtii na kumuabudu Mungu Mmoja, wa Pekee na wa Kweli, Eloa.
Ni juu yetu sisi sasa kufanya kazi kwa bidii tukimtii Mungu na Sheria zake
na kupunguza mateso yaliyo kwenye mfumo na wakati huu wote. Ni wajibu wetu pia kuipeleka
injili ulimwenguni kote ili watu wote waujue Mpango wa Mungu na watubu na
kubadili njia zao. Wote watapewa fursa ya kutubu na kumuishia Mungu. Kwakuwa
Mungu hapendi mtu yeyote apotee, yaonekana kuwa viumbe wote watachagua kumtii
Mungu na Sheria zake. Kwa habari zaidi na kujifunza kuhusu mchakato wa upatanisho
soma majarida ya Siku Takatifu za Mungu (Na. CB22) na Mpango wa Mungu wa Wokovu (Na. CB30).
Kuna wakati mvuri namna hii unaokuja mbele yetu, lakini kuna kazi kubwa ya
kufanya kabla ya kipindi cha Mashahidi wawili hakijawasili (Ufunuo 11:1-12) watakaofuatiwa
na kurudi kwa Masihi.
q