Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[CB30]
Mpango
wa Mungu wa Wokovu
(Toleo La 2.0 20020701-20061216)
Mara nyingi
watoto wanauliza maswali mengi sana kuhusu Mungu na jinsi anavyotuwazia au
Mpango wake Kwetu sisi. Jarida hili linajibu maswali haya na kuelezea sababu
inayotufanya sisi tuhitaji Mpango wa Mungu wa Wokovu, na mpango huo ni nini na
jinsi tunavyotakiwa kuwa ili tuweze kustahili kuwa nao.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki ©
2002, 2006 Carrie Farris and Wade Cox)
(tr. 2014)
Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na
kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la
haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa
au ku
Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya::
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Mpango wa Mungu wa Wokovu
Kwa nini tunahitaji Mpango
wa Mungu wa Wokovu?
Wakati Mungu alipomuumba mwanadamu kwanza, alimuumba kwa sura na mfano wake
na kwa kunafafa na yeye.
Mwanzo 1:27 Mungu
akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba
Adamu na Hawa walikuwa ni wanadamu wa kwanza aliowaumba Mungu. Walikuwa ni
sehemu ya familia yake. Waliishi kwenye Bustani ya Edeni na hawakuwa na dhambi
yoyote aliyomfanyia Mungu, ambayo maana yake ni kwamba hawakuivunja amri yoyote
katika Torati ya Mungu. Hivi ndivyo ilivyokuwa hadi ale Hawa alipojaribiwa kula
matunda ya mti ambao Mungu aliwaambia wasile.
Mwanzo 2:16-17 Bwana
Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya
usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Wakati Hawa alipolichukua lile tunda lililokatazwa, alitanda dhambi.
Aliivunja Amri ya Mungu. Pia alimmegea kipande Adamu naye akala lile tuna naye
akatenda dhambi (Mwanzo 3:1-6).
Kwa kuwa Adamu na Hawa walimuasi Mungu kwa kuvunja Sheria yake, walifukuzwa
watoke bustanini na Mungu akawalaani na kuiweka laana juu yao.
Mwanzo 3:16-19 Akamwambia
mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa
watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. 17
Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda
ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako;
kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma
na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; 19 kwa
jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo
ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Laana hii haikuwa kwa ajili ya Adamu na Hawa peke yao. Bali ilikuwa ni kwa
wanadamu wote watakao wafuata wao kutenda matendo haya ya uasi, hadi kwetu sisi
leo pia. Laana inatuambia sisis
kwamba tutapatwa na maumivu na mateso sisi sote na kwamba hatimaye tutakufa
sote na miili yetu itayarudia mavumbi. Kutokana na dhambi hii ya kwanza, ndipo
mauti ikaja; na pia iliwafanya watoto wa Adamu kuwa wana wa wanadamu na sio
tena kuwa wana wa Mungu kama ilivyokuwa imekusudiwa hapo kabla.
Warumi 5:12 Kwa
hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti;
na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
Kama hatukuwa na Mpango wa Mungu wa Wokovu, basi tungekufa na kusingekuwa
na kingine zaidi. Tungerudi
tu kwenye mavumbi ya Nchi na hivyo ndivyo ingalivyokuwa tu. Lakini Mungu
hapendi mtu yeyote apotee milele.
2Petro 3:9 Bwana
hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali
huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
Ili tuweze kuishi, au tusife milele, Mungu aliweka Mpango wa Wokovu kwa ajili
yetu, ili kutufanya tuwe kwa mara nyingine sehemu ya familia yake.
Je, Huu Mpango wa Mungu wa
Wokovu Ni kitu gani?
Baada ya Adamu, Mungu alifanya agano na watu wake. Mwanzoni kabisa,
alilifanya na Mababa wa imani, na ndio peke yao waliokuwa wanazishika Amri zake.
Dunia ilijaa maovu kiasi ilistahili kuangamia kwa gharika. Nuhu na familia yake
waliokoka na kuanzisha ulimwengu mpya usio na maovu yaliyokuweko huko nyuma.
Kupia Ibrahimu Mungu aliandaa kundi la mataifa na kuwachagua Israeli kuwa taifa
lake teule, ambalo kupitia kwalo aliweza kufuua Mpango wake. Aliwapa Torati
iwaongoze na walimtolea sadaka za dhambi ili wasamehewe. Pia aliwapa Siku zake
Takatifu. Hizi Siku Takatifu zimetolewa ili kutuonyesha jinsi Mpango wa Mungu
ulivyo. Katika siku hizi, watu wa Mungu
walimtolea Mungu sadaka za aina mbalimbali za kuteketezwa. Tunaweza kujisomea
kwa kina zaidi kuhusu siku hizi Takatifu kwenye jarida la Siku Takatifu za Mungu (Na. CB22) [God’s Holy Days (No. CB22)].
Mungu alijua kuwa agano hili lisingeweza kufanya kazi pasipo msaada wa Roho
Mtakatifu kuwepo ndani ya mwanadamu, kwa kuwa alijua kwamba mwanadamu angeendelea
kutenda dhambi. Ingawa mtenda
dhambi alikatiliwa mbali na Mungu wa Pekee na wa Kweli. Kwa hiyo Mungu alitabiri
kwamba mfumo mpya wa Agano lake ungeanzishwa na agano kuwekwa kama maagano mengi
madogomadogo au ahadi na makubaliano vikiwemo ndani yake (Soma jarida la Maagano ya Mungu (Na. 152) [The Covenants of God
(No. 152)]. Utaratibu huu mpya wa agano uloiwekwa
katika Kristo, ulileta tumaini na wokovu.
Yeremia 31:31-34 Angalia,
siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na
nyumba ya Yuda. 32 Si kwa mfano wa agano lile
nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa
katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume
kwao, asema Bwana. 33 Bali agano hili ndilo
nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia
sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu
wao, nao watakuwa watu wangu. 34 Wala hawatamfundisha
kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana
watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni
mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka
tena.
Ilitabiriwa pia kwenye Biblia kwamba Mungu atamtuma Masihi wake, ambaye ni
Mtiwa Mafuta wake, kuja kuwaokoa watu wake.
Yeremia 23:5-6 Tazama
siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye
atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika
nchi. 6 Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli
atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.
Aya hizi zilikuwa zinatabiri ujio wa Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, na ujio
wa Roho Mtakatifu, ambaye Mungu alikuwa anakwenda kuwapa watu wote waliomuamini
Mwanae wa Pekee.
Yesu alikuja kuwafundisha watu kuhusu utaratibu huu mpya wa agano na Mungu.
Hakuja kuitangua Torati
ambayo Mungu alikuwa ameiweka na kuwapa watu wake. Bali alikuja kuwafundisha
watu na kuwasisitiza kuishika Torati na kuwafikisha kwenye toba watubie dhambi
zao walizomtenda Mungu.
Mathayo 5:17-18 17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au
manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa
maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala
nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.
Toba maana yake ni kujisikia vibaya na kujutia mambo mabaya tuliyoyatenda
na kuondoka kwenye kutenda mabaya na kutenda mema, au kumrudia Mungu na
kuyafanya mapenzi yake.
Yesu alifundisha pia kwamba inatupasa kubatizwa, ambayo maana yake ni
kwamba baada ya kutubu kwetu na maisha yetu kumrudia Mungu, tunatakiwa
kuzamishwa majini kwa dakika kadhaa, kitendo kinachomaanisha ishara ya
kuyafisha matendo yetu ya zamani na kufufuka na maisha mapya na Mungu.
Mathayo 28:19-20 Basi,
enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba,
na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha
kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku
zote, hata ukamilifu wa dahari.
Tunaweza kubatizwa tu tunapokuwa na umri wa mtu mzima. Bali wakati huohuo,
iwapo kama tuna wazazi waaminio tunakuwa tumetakaswa kupitia wao (1Wakorintho
7:14). Hii inamaana kwamba Mungu hutuangalia kwa upendo mkubwa tunapokuwa chini
ya ulinzi wa wazazi wetu. Inaamikika kuwa wazazi waaminio huwafundisha watoto wao
Torati ya Mungu, na kwa watoto hawa watakuwa wanaendelea kuzishika Sheria au
Torati hii hadi watakavyokuwa watu wazima au wazee. Kwenye Kanisa la Mungu watoto
huwa hawabatizwi. Hii inamaanisha kwamba tunatakiwa kwanza tuzijue dhambi zetu
na kujutia matendo yote mabaya tuliyoyatenda, kabla hatujaenda kwenye kisima au
mto wa maji au pahali popote enye maji mengi ili kubatizwa na tukahuishwa na
kuwa hai (kutakaswa).
Yesu pia alikuja ili awe Mwokozi wetu. Hii inamaana kwamba alikuja ili
atufie ili atuoshe au kutusafisha dhambi zetu. Wakati Kristo alipokufa
alifanyika kuwa Mwanakondoo wetu wa Pasaka. Hakufanya dhambi yoyote kamwe, bali
alilipa gharama ya wenye dhambi, ambayo ni mauti. Alifanya iwezekane kwa sisi
kumwendea Mungu sisi wenyewe bila kuwaendea makuhani au kasisi. Yeye pia
alikuwa ni dhabihu ya mwisho, ambayo maana yake ni kwamba hatuhitaji tena
kumtolea Mungu dhabihu nyingine yoyote ya wanama.
Kwa hiyo Kristo alifufuka kutoka kwa wafu akiwa ni
malimbuko ya mavuno ya Mungu. Hii inamaanisha kwamba yeye ni wa kwanza miongoni
mwa wengi wataofufuliwa toka kwa wafu na kuishi tena kwenye Mbingu Mpya na Nchi
Mpya.
1Wakorintho 15:20 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao
waliolala.
Ufunuo 21:1 Kisha
nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza
zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Pia Kristo alifanya iwezekane karama za Roho Mtakatifu wazipate wana wa
Mungu. Roho Mtakatifu ni uweza au nguvu za Mungu, inayotuwezesha kupata asili
ya Mungu mwenyewe na ni kipawa anayoitoa bure kwa yeyote anayeiomba. Tunaweza
kujisomea zaidi kuhusu Roho Mtakatifu kwenye jarida la Roho Mtakatifu Ninini? (Na. CB3) [What is the Holy Spirit? (No. CB3)].
Kristo, kwa kupitia Roho Mtakatifu, ndpo tunavyoweza kuyaelewa Maandiko
Matakatifu au Biblia na ndvyo Mungu anavyotuonyesha yalle anayotaka tuyafanye.
Mungu anatuonyesha kwamba ameliweka Agano lake Jipya ambalo aliliongelea kwenye
Yeremia 11. Warumi 2:14-15 ikimaanisha kwamba kwa sasa Roho Mtakatifu anaongoza
mawazo na matendo ya watu wa Mungu.
Warumi 2:14-15 Kwa
maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya
torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. 15 Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao,
dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au
kuwatetea;
Yesu pia alisema kuhusu kurudi kwake Duniani, na kwamba atawakusanya
wateule wa Mungu kutoka kokote waliko Duniani. Wateule ni watu wanaoyafanya
mapenzi ya Mungu na maagizo yake. Yesu pia anasema kwamba hakuna ajuae kipindi
au siku ya kuja kwake ila Baba yake peke yake.
Marko 13:26-27 Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. 27 Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu.
Marko 13:32 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
Wakati Kristo atakapokuja atatawala kama Mfalme wetu kwa kipindi cha miaka elfu.
Wateule watasaidia utawala wake wakiwa kama makuhani. Watu hawa watakuwepo
kwenye kile kinachoitwa kuwa ni Ufufuo wa Kwanza wa wafu—kwa maneno mengine ni
kwamba watakuwa ni wafu wa wa kwanza kufufuliwa na kuwa hai tena kai ya wafu
waliolala mauti.
Ufunuo 20:4-6 Kisha
nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona
roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno
la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea
ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai,
wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. 5 Hao wafu
waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. 6 Huo
ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika
ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani
wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
Watu wengine wote waliosalia ambao waliishi bali hawakuyatenda yale
aliyoyapenda Mungu wayafanye, watafufuliwa tena baada ya miaka elfu ya utawala
wa Kristo akiwa ni Mfalme. Huu unaitwa Ufufuo wa Pili wa wafu. Watu kwenye Ufufuo
wa Pili wa wafundishwa kuishi sawa na maongozi ya Torati ya Mungu na wataweza
kuwa na fursa ya kuwa ni sehemu ya familia ya Mungu. Hii inaitwa hukumu. Kama
hawatamrudia Mungu, hakika watakufa kwa mara ya nwisho na hawataweza kuwa hai
tena.
Tunawezaje kuwa sahihi
kwenye Mpango wa Mungu?
Mungu anatupenda, na sisi sote. Hapendi hata mmoja wetu apotee kama
tulivyokwisha jionea tayari. Bali pia anatupenda kiasi cha kutosha kwa kutupa
Mwanae wa pekee ili awe ni sadaka yetu ya dhambi, ili sisi tuwe sehemu ya familia
yake tena. Ila sio watu wengi wanaoelewa jambo hili sasa.
Yohana 3:16 Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
1Yohana 3:1-2 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.
Siku moja sisi sote tutabadilika na kuwa viumbe wa kiroho. Hakutakuwa na
mwanaume wala mwanamke, bali ni kama malaika au viumbe wenye miili ya kiroho. Sote tutafanyika kuwa ni Wana wa Mungu na
tutafana kazi pamoja na Kristo. Kristo alitufia ili kwamba tutakapoamka kutoka
malaloni mwetu (kifo) tuishi pamoja naye (1Wathesalonike 5:10). Hebu fikiria na
kutarajia kwamba siku moja tutamuona Kristo na kuwa pamoja naye pamoja na
viumbe wengine wenye miili ya kiroho.
Namna pekee ya kufanyika kuwa familia ya Mungu ni kumuamini yeye na Mwanae
wa Pekee, Yesu Kristo. Tunapaswa pia kuitii Torati yake, kutubu dhambi zetu, na
kubatizwa tunapofikia umri wa utu uzima. Hili ni jambo ambalo tunapaswa wote
tuliangalie kwa kina.
Kumbuka kuwa jambo ambalo Mungu anatutaka tukifanye ni kumpenda na kumtii
yeye. Kadiri tunavyofanya
hivyo ndipo tutakuwa ni sehemu ya familia yake milele.
Kumbukumbu la Torati
7:9 Basi jueni ya kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye Mungu;
Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika
amri zake, hata vizazi elfu;
q