Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[CB31]
Mafunzo
Kuhusu Maombi Sehemu ya A
Mwongozo
wa Mwalimu
(Toleo 2.0 20021230-20070123)
Mafunzo mwongoza haya yalitokana na karatasi la tufunze jinsi ya kuomba (Nambari 111) na yafaa kushirikiana na mafunzo ya maombi sehemu ya pili karatasi lakazi (Nambari CB32)
Christian Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Copyright ã 2002, 2007 Leslie
and Russell Hilburn, ed. Wade Cox)
(Tr. 2009)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Mafunzo
Kuhusu Maombi Sehemu ya A
Mwongozo
wa Mwalimu (CB31)
Huwa ni vigumu kwetu kuelewa umuhimu wa maombi / sababu ya kuomba. Twajua kwa omba Mungu ni mjua yote, kwa hiyo ni kwanini twafaa kuzugumza naye kuhusu vitu / mambo ambayo tayari anayajua? Na ni kwanini tutahitaji kumuomba vitu wakati Bibilia yatuambia kuwa tayari ajua mahitaji yetu?
Kinaya kunajitokeza kwenye ukweli kuomba ni haswaa wakati ule wa maombi ndio majibu yanakuwa wazi. Tunapokuwa watu wa kuomba kila wakati na ushahifi wa maombi yetu ukawa na ushahidi wa maombi yetu akawa wazii, ndipo tutaweza kuanza kuelewa kuwa maombi ni chombo muhimu cha lazima ambacho twawasiliana na kutoa utukufu kwa Baba yetu mwenye upendo ambaye ni Mungu.
Leo tutauliza maswali sita rahisi kuhusu maombi.
Tazama: Unapolipatia kila jibu la maswali haya. Peana muda kwa watoto kutoa majibu yao. Wahimize watoto kuchukua nafasi katika kila swali kama muda unavyoruhusu. Jaribu kuyaandika majibu yao kama yaonekana kuna andiko Fulani ya kudhibitisha fikra zao. Hii yaweza kuangaliwa baadaye mchana, na watoto kuonyeshwa maandiko / andiko katika mafunzo yao ijayo.
Swali
la 1: Ni kwanini sisi uomba?
Muulize mtoto mmoja asome Zaburi 94:11 “yenye mfanzaye mwanadamu hekima. Bwana ajua fikra za mwandamu, ya kuwa ni pumzi.”
Katika kifungu hiki Bibilia yatuambia kuwa Mungu ajua mawazo ya mwanadamu. Kwa hiyo ikiwa ajua mawazo yetu ni kwanini tuombe?
A.
Kumtukuza Mungu
Isoma Isaya 43:7 kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwuomba naam mimi nimemfanya” (KJV). Katika andiko hili Bibilia yatufunza kuwa sababu ya Mungu kutuumba ni kwa utukufu wake. Njia moja tunayoweza kumtukuza Mungu ni kupitia maombi.
Twafaa kuomba kwa ajili ya kumtukuza Mungu na kujenga uhusiano naye kwa kupitia kwa mwanawe Yesu Kristo.
B.
Fuata maajizo ya Kristo
Twamtazamia Yesu Kristo kama mwalimu wetu na twataka kufuata mfano wake. Mtoto mmoja asome Mathayo 6:7. Nanyi mkiwa katika kusali msipayuke payuke kama watu wa mtaifa. Maana wao hudhani yakuwa watasikiwa kwa sababu ya maeno yao kuwa mengi (NKJV). Sikiza kwa makini kwa neno la pili Kristo alisema unapoomba hakusema ukiomba.
Yesu pia atufunza kuwa tunapoomba tuombe kwa jina lake. Mtoto mmoja asome Yohana 14:13-14. “Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu nitalifanya, nitalifanya ili baba apate kutukuzwa katika mwana; mkiliomba lolote kwa jina langu nitalifanya.
Swali la 2: Sisi huomba kwa nani?
(Acha muda watoto wajibu.)
Muulize mtoto mmoja asome Mathayo 4:10 “Yesu akamwmambia, nenda zake shetani” kwa maana imeandikwa msujudie Bwana Mungu wako umwabudu yeye peke yake.”
Yesu Kristo atuambia kuwa twafaa kumwabudu Mungu baba pekee. Aliashiria kutoka agano la kale Kumbukumbu la Torati 6:13 mche, Bwana Mungu wako; ndiye utakayemtumikia na kuapa kwa jina lake; muulize mtoto mmoja asome andiko pia.
Maandiko mengine yasusoma ambao yaashiria Mungu kawa chombo chetu cha maombi ni kama:
· Wakorintho 8:5-6: kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake, yuko kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo.
· Yohana 17:3 na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo aliyemtuma.
Swali la tatu: Je twajiandaa vipi kwa maombi?
(Acha muda watoto wajibu)
A.
Uliza kwa imani
Muulize mtoto mmoja asome Mariko 11:24 kwa sababu hiyo nawaambia, yeyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba myajapokea, nayo yatukuwa yenu.
Waacha watoto wasome “Lakini mtu wa kwenu akupingukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu wala hakemel, naye atapewa. Ila aombe kwa imani, pasipo shaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana” (James 1:5-7).
Katika maandiko haya mawili, Bibilia yatupa agizo la wazi kuwa lazima tuombe kwa imani.
Pia mtu asome Wahibrania 11:6. Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Hivyo basi twaona kwa kukusanya maandiko haya yote pamoja kwa maombi yetu kuwa ya manufaa kwetu ni lazima tuwe na imani na lazima tuamini mambo matatu yafuatayo.
· Kuna Mungu mbinguni
· Mungu asikiza maombi yetu
· Mungu ajibu maombi yetu
Lazima tukumbuke pia ya kwamba saa zingine majibu ya Mungu kwa maombi yetu sio kama tulivyotarajia au wakati wake ni tofauti na wetu. Saa zingine Mungu hutufanya tungojee ili tujifunze.
Subira na kuepuka dhambi au tujifunze mambo tofauti tofauti. Au pengine ana jambo jingine akilini mwake kwetu.
Ni lazima tujue / tukumbuke kuwa Mungu atatenda wakati ufaao kwa ajili ya kitu alichoona, na kulingana na Warumi 8:28. Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao. Katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake maombi sio kumlazimisha Mungu kutenda jinsi tunavyomuomba bali ni kwenda kwa Mungu kwa imani kamilifu kuwa tunachohitaji atatupa.
B. Omba na moyo wa toba.
Bibilia pia yatufunza kuwa maombi yaweza kuingilia maombi yetu. Soma Isaya 59:1-2 tazama mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoka wala sikio lake si zito, hata lisiweze kuisikia 2Lakini maovu yenu yamewafikiria ninyi na Mungu wenu na dhambi zenu zimeuficha uso wake usiuone, hata hataki kusikia.
Ikiwa twajua sote hutenda dhambi basi tutaelewa kuwa andiko hili yatuonyesha kuwa twahitaji kuongea na Mungu kuhusu dhambi zetu, kutubu na kumuomba Mungu atusaidie kutubu. Hatutenganisha na Mungu kila wakati.
Mtoto mmoja asome Methali 28:9 yeye aliyeuzaye sikio lake asiisikie sheria. Hata sala yake ni chukizo. “Hii yatuonyesha jinsi sheria za Mungu zilivyo muhimu na jinsi tunavyohitajika kujaribu kuvifuata mara kwa mara bila kusita.
Pamoja na haya kuna maagizo katika kitabu cha Marko 11:25 muulize mtoto mmoja asome andiko hili. Nanyi kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. “Ikiwa twataka Mungu atusamehe dhambi zetu (na tumetambua tunamhitaji afanye hivyo) ni lazima tuwasamehe wale watu walioukosea sisi pia.
C.
Omba kwa moyo wa upole
Lazima tuwe wapole kila / kabla tunapoomba soma Luka 18:10-14 “watu wawili walipopanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuri, “Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyanganyi wadhalimu, wasinzi, wala kama huyu mtosha ushuru. 12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. 13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakudhubutu hata kuinua macho yake mbinguni bali alijipiga – piga kifua akisema. Ee Mungu uniwie radhi mimi mwenye dhambi 14 Nawaambia huyu alishuka kwenda nyumbani kwake ameshesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa na ajidhilaye atakwezwa.
D.
Omba kwa moyo wa shukrani
Mtoto mmoja asome Wafilipi 4:6 “msijusumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu
Swali la nne: Sisi huombea wapi?
(Acha muda watoto wajibu)
Mtoto mmoja asome Mathayo 6:5-6:
Tena msalipa, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin nawaambia, wamekwisha pata thawabu yao 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Hii yatuonyesha tunapswa kuomba kwa siri.
Je tunapoomba kwa pamoja na familia zetu au kwenye makanisa? Je Bibilia yatupa mfano soma Matendo ya Mitume 12:11-12. Hata petro alipopata fahamu akasema, sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempelekea malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi. Na alipokuwa akidikiri haya akafika nyumba kwa mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wzkiomba.”
Hapa kikundi cha watu walikuwa wakiomba pamoja. Lakini kama mfano uliopeanwa na Kristo, walikuwa wakiomba pamoja katika nyumba ya siri.
Swali la tano: Sisi uomba masaa / wakati gani?
(Acha
muda watoto wajibu)
A.
Omba bila kukoma
Mtoto mmoja asome Wathesalonike 5:17-18 “17 Shukurni kwa kila jambo; 18 Shukuru kwa kila jambo, maana hayo hayo ni mapenzi ya Mungu kwetu katika Kristo Yesu utafsiri mengine husema omba bila kukoma. Hii haimaanishi kuwa twafaa kuomba kila wakati, bali twafaa kuomba kwa roho ufaao, tayari kwa maombi kila wakati.
B.
Mfano wa Danieli
Mfano mwingine katika Bibilia yatoka kitabu cha Danieli. Mtoto mmoja asome Danieli 6:10. “Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Mfano wa Danieli ni mfano mwema kwetu. Tunapoomba tukiamka asubuhi, saa zingine mchana, na usiku kabla ya kwenda kulala tunafursa ua kumuuingiza / mhusisha Mungu katika siku yetu nzima wakati wa asubuhi tukiomba tunamuonyesha Mungu kuwa tunatambua kuwa twamhitaji kila siku na pia twaweza kumuomba atulinde siku nzima. Unapoomba mchana twakumbuka kuwa Mungu ana umuhimu kwetu kuliko kazi zetu za kila siku. Kwa kutengeze wakati kwa ajili ya Mungu twajikumbusha kuwa Mungu ndiye nambari moja. Mwisho tunapochukua muda kuomba kabla ya kulala, twaweza kumshukuru Mungu kwa kila siku
Swali sita: Jinsi uomba kwa ajili gani / kuhusu nini?
(Wape watoto nafasi wajibu)
Ingawa hapana jibu sahihi au usio sahihi kwa swali hili, Bibilia yatupa mwelekezo kwa mambo ambayo twaweza kujumisha katika maombi yetu, na mambo tunayofaa kufikitia kuhusu tunapoomba.
A.
Jinsi / mfano wa maombi
Mtoto mmoja asome Mathayo 6:9-13 basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe ufalme wako uje 11Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni utupe leo riziki yetu 12 utusamehe makosa yetu kama sisi tuwasamehevyo walio tukosea 13 Na usitutie majaribuni lakini utuokoe na yule mwovu.
Watoto wengine ambao wamehudhuria makanisani mengine ombi hili laweza kuwa wanalojua. Pengine wamevishika akilini na wamevirudia katika vikundi vikubwa. Walakini lazima tutazame aliyosema Yesu Kristo. Alisema “ombeni hivi”. Hakusema myasema maneno haya ya ombi hili mara kwa mara kwa marudio isiyo na maana. Mfano wa ombi hili ndilo lafaa kuwa jinsi tunaomba.
Ombi hili lahusisha vitu vifuatavyo.
Anza kwa kumuabudu Mungu, kumtukuza na kuangalia vungu wake.
Maombi yetu lazima yawe kwa upole na mapenzi ya Mungu. Twafaa kumjulisha Mungu katika mipango yetu kuanzia mwanzo na wala kuanza kuomba kuhusu jambo wakati wa mwisho. Hili yatusaidia kutukumbusha kuwa twataka kufuatia mapenzi ya Mungu na wala si mapenzi yetu.
Kuombea mahitaji yetu ya kimwili na kiroho. Acha tutazame anayotufunza Luka. Mtu asome Luka 11:13. “Basi ikiwa ninyi mlio waovu. Mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema. “Je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho mtakatifu hao wamwombao!” Lazima tumwomba Mungu roho wake mtakatifu afanye kazi pamoja nasi. Twajua kuwa ni kupitia toba, ubatizo na kuwekelwa mkono tu ndio twapokea Roho mtakatifu wa Mungu. Ingawaje hufanyakazi nasi kabla ya ubatizo, ukitupelekea kwa Mungu na kwenye njisi ya maisha yake.
Tuombe kwaajili ya msamaha kwa ajili ya dhambi zetu / ktotekeleza wajibu wetu. Tunapoomba msamaha wa dhambi zetu yamaanisha twazitambua dhambi zetu dhidi ya mwenyezi Mungu.
Lakini msamaha huja kwa malipo / sadaka. Lazima tuwasamehe wenzetu ili tusamehewe. Mtoto mmoja asome Mathayo 6:14-15. “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nini. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Omba kwa ajili ya ulinzi wa Mungu kumbuka kuwa Mungu ndiye mlinzi wetu pekee.
B.
Mifano mingine ya mambo tunafaa kuomba
kuyahudu.
Omba kwa ajili ya mahitaji yaw engine mtoto mmoja asome Waefeso 6:18-19
18 Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote. 19 Pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya injili. Hapa Paulo atupa maagizo kuwamboe mitume wote ambao wametajwa katika kitabu cha Ufunuo 14:12 “Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu.
Tuwaombe viongozi wetu. Mtoto mmoja asome Timotheo 2:1-2. “Basi kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote 1 Kwa ajili ya wafalme wa “wote wenye mamlaka tuishi maisha ya utulivu na amani katika utawala wote na ustahivu
Tuwaombe adui zetu. Mtoto mmoja asome Luka 6:28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi waombeeni wale ambao wawaonea ninyi
C.
Yote yakisinfikana
Ikiwa hatujui cha kuombea, tunapewa msaada kupitia kwa roho mtakatifu mtoto mmoja asome Warumi 8:26-27 Kadhalika Roho Mtakatifu hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea watakatifu kama apendavyo “Mungu” Roho wa Mungu atatuongoza kuombea mambo kulingana na matakwa ya Mungu.
Tukizingatia majibu ya maswali haya ya sita, ambayo ni kwanini, nani jinsi gani, wapi, wakati gani / masaa gani, tutanza safari yetu kwa maisha mema, yaliyojaa maombi. Lazima ukumbuke kuwa sababu ya maombi lazima iwe kwaajili ya kumtukuza Mungu na kujenga uhusiano naye. Maombi ni zaidi ya kurudia –rudia maneno. Ni kujenga uhusiano wa kimwili kati ya Mungu na utu kupitia kwa Yesu Kristo.
q