Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[CB82]
Kipindi cha Utakaso cha
Siku 21
(Toleo La 2.0
20060527-20090302)
Yesu Kristo alilitakasa Hekalu hili la Yerusalemu mapema kabla ya Pasaka
likiwa ni onyo na ishara kwetu kwamba na sisi tunatakiwa kulitakasa Hekalu ili
tustahili kuula mkate na kuinywa divai ya Ushirika wa Meza ya Bwana.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki ©
2006, 2009
Christian Churches of God, ed. Wade Cox)
(Tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Kipindi cha Utakaso cha Siku 21
Kalenda ya Mungu imeorodhesha
siku za kumfanyia Mungu ibada za kila mwaka zikiwemo Sikukuu zake, nazo
zimeandikwa kwa uwazi kwenye Mambo ya Walawi 23 na Kumbukumbu la Torati 16. Siku
ya kwanza ya Mwaka Mpya inaweka mwanzo wa mchakato wa kalenda nzima kwa kipindi
cha mwaka mmoja. Siku hii ya kwanza ni ya muhimu kwa kuwa ni siku ya Mwandamo
wa Mwezi Mpya, lakini pia ni mwanzo wa kipindi cha kila mwaka cha kujitakasa.
Kipindi hiki cha utakaso cha kila mwaka kinadumu kwa kipindi cha siku ishirini
na moja na kinaishia katika siku ya mwisho wa idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu.
Siku ishirini na moja
katika mwezi wa kwanza zinaashiria kipindi cha siku ishini na moja cha mwezi wa
Saba ambayo inanzia na Mwandamo wa Mwezi Mpya ambayo pia ni siku ya Ukumbusho
wa Kuzipiga Baragumu na inaishia siku ya mwisho ya Sikukuu ya Vibanda.
Tutaliongelea jambo hili kwa kina zaidi kwenye jarida la Ondoleo la Dhabi na Upatanisho (Na. CB 40) [Atonement and Reconciliation
(No. CB140)].
Kila mwaka, wakati wa mlo
wa Meza ya Bwana, waumini watuwazima na waliobatizwa wanalirudia agano lao
waliloliweka kwa njia ya ubatizo la kumuweka Mungu kwenye kipaumbele cha kwanza
na kufuata njia yake ya uzima iliyoelekezwa kwenye Torati. Ni kipindi ambacho tunajiangalia
matendo na mwenendo wetu uliyopita na wa sasa na kujaribu ama kujitahidi kuweka
dhambi mbali na fikra za mawazo yetu na matendo yetu. Hatahivyo, Mungu
hatarajii mchakato huu uchukue siku moja tu. Na wala hatarajii kuwa mchakato
huu ukiwa unamlenga mtu mmoja tu. Bali mchakato huu wa utakaso unaanzia siku ya
kuanza kwa Mwaka Mpya na kuishia siku ya mwisho ya maadhimisho ya Mikate
Isiyotiwa Chachu. Ni jumla ya siku Ishirini na moja, au kipindi cha majuma matatu
na inahusisha kwa kiasi kingi zaidi kuliko kuwa ni ya utakaso wa mtu mmoja
mmoja.
Je, huu utakaso au kutakaswa
maana yeke ni nini? Kutakasa maana yake ni qadash (SHD 6942) na hagiazo
(SGD 37). Maana yake tafsirika inajumuisha kuweka wakfu, takasa, tayarisha,
rasmisha, tukuza, kuwa kakatifu, takaswa, tengwa mbali. Kwa maneno mengine,
inamaanisha kutengwa mbali au kutengwa na matendo maovu, au kufanya mtakatifu.
Inamaana pia kuwekwa wakfu na rasmi,
au kuwa safi kwa maana ya kiroho.
Utakaso ni matokeo ya
uwepo wa Mungu kwenye kitu fulani au kwa mtu fulani. Mungu aliitakasa Maskani
kwa uwepo wake (Kutoka 29:43); watoto wanatakaswa na Mungu kwa ajili ya mzazi
anayeamini (1Wakorintho 7:14). Tunachotakiwa kufanya kwenye mchakato huu wa
utakaso ni kujiandaa sisi enyewe kwa uwepo wa Mungu kwa kuondoa ama kuachana na
dhambi. Sehemu ya Mungu ni kukaa ndani yetu kwa Roho wake Mtakatifu
anayetufanya sisi kuwa ni Hekalu la Mungu.
1Wakorintho 3:16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
Hatuwezi kufanyika kuwa hekalu hadi tutakapojiandaa kikamilifu na, kama kwa namna fulani tukionekana kuwa hatufai kwa kuwa hekalu, tunatakiwa kuondolewa na kukataliwa hekaluni na kisha turudishe tena hadi mahala petu maridhawa au panapotustahili (1Wafalme 6:7).
Mungu aliitakasa
siku hii ya saba na kuitakatifuza.
Mwanzo 2:3 Mungu
akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu
alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya
Mungu alilitakasa
taifa la Israeli.
Kutoka 31:12-13 Bwana akasema na Musa, na kumwambia, 13 Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.
Usiku
uliotangulia kabla ya kusulibiwa kwa Yesu alimuomba Mungu, Baba yake. Kwenye
maombi yake alimuomba Mungu awatakase kwa kweli yake wale wote waliomjua Mungu
na kumuamini Yesu Kristo.
Yohana 17:14-19 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. 16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. 18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. 19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
Tumetakaswa na Mungu kupitia imani iliyo katika Yesu Kristo.
Matendo 26:15-18 Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambaye wewe unaniudhi. 16 Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako; 17 nikikuokoa na watu wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao; 18 uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.
Uwepo wa Mungu,
kupitia Roho Mtakatifu ni kitu kinacholitakasa hekalu na kulitakatifuza. Hii
inaendana na yote mawili, yaani hekalu la kimwili na la kiroho ambalo ndiye
sisi.
Kipindi cha
Utakaso cha kila Mwaka
Mchakato wa
utakaso unaanzia mwanzoni mwa Mwandamo wa Mwezi Mpya wa mwaka mpya. Mwanzo wa
Mwaka Mpya ulikuwa na maana au umihimu kwa namna nyingi. Ardhi ilifanywa upya
katika kipindi cha Nuhu katika Siku hii ya Kwanza ya Mwezi wa Kwanza.
Mwanzo 8:13 Ikawa
mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji
yalikauka juu ya nchi. Nuhu
akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi
Nabii Musa
aliambiwa aisimamishe Maskani katika siku hii ya kwanza ya mwezi wa kwanza.
Kutoka 40:1-2 Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza utaisimamisha hiyo maskani ya hema ya kukutania.
Matengenezo
yaliyofanywa na mfalme Hezekia yalianza siku hii ya kwanza ya mwezi wa kwanza
ya Mwaka Mpya.
2Nyakati 29:12-17 Ndipo
wakaondoka Walawi, Mahathi mwana wa Amasai, na Yoeli mwana wa Azaria, wa wana
wa Wakohathi; na wa wana wa Merari, Kishi mwana wa Abdi, na Azaria mwana wa
Yehaleleli; na wa Wagershoni, Yoa mwana wa Zima na Edeni mwana wa Yoa; 13 na wa wana wa Elisafani, Shimri na Yeueli; na wa wana wa
Asafu, Zekaria na Matania; 14 na wa wana wa Hemani,
Yehueli na Shimei; na wa wana wa Yeduthuni, Shemaya na Uzieli. 15 Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa, wakaingia, kama
alivyoamuru mfalme kwa maneno ya Bwana, ili waisafishe nyumba ya Bwana. 16 Nao makuhani wakaingia nyumbani mwa Bwana, katika mahali
pa ndani, ili waisafishe, wakatoa uchafu wote waliouona hekaluni mwa Bwana,
wakautupa nje uani mwa nyumba ya Bwana. Walawi wakautwaa, ili wauchukue nje
mpaka kijito cha Kidroni. 17 Basi wakaanza kutakasa
siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, hata siku ya nane ya mwezi wakafika katika
ukumbi wa Bwana; wakaitakasa nyumba ya Bwana katika muda wa siku nane;
wakamaliza siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza.
Tunapewa pia mfano wa Jesu Kristo alipolisafisha Hekalu la Yerusalemu mapema kabla ya kusulibiwa kwake. Tunajua kutokana na hesabu ya kipindi cha ujio wake mjini Yerusalemu siku ya 8 ya mwezi wa kwanza ambako Yesu alilisafisha Hekalu ndani ya kipindi hiku cha siku Ishirini na moja ya Utakaso wa Hekalu. (Soma jarida la Hesabu ya Kipindi cha Kusulibiwa na Kufufuka (Na. 159) [Timing of the Crucifixion and the Resurrection (No. 159)].
Tunajua kwamba leo Mungu anamchukulia kila mteule kama sehemu ya hekalu la kiroho (1Wakorintho 3:16-17; 6:19). Hata kama tuko hatujabatizwa bado, bado tunahitaji kuchukua hatua ya kutakaswa ili tuweze kujifunza kumcha Mungu na kuzishika amri zake na kupita njia zake ili tupewe uwezo wa kuelewa.
Mwili wa Yesu Kristo, kama Hekalu lililokamilika la Mungu, ilimlazimu atakaswe kwanza mapema kabla hajaila Pasaka. Kama ilivyotathminiwa hapo kabla, uwepo wa Mungu ndiyo unaolitakasa hekalu na kulitakatifuza. Hata hivyo, kuna mifano mingi ya kibiblia ambapo Mungu anamtumia mwanadamu afanye kazi ya kuvitakasa vitu vitakatifu.
Mungu, kwa kupitia Malaika wa Uwepo wake, alimwambia Musa awatakase Israeli.
Kutoka 19:10-11 Bwana akamwambia Musa, Enenda kwa watu hawa,
ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao, 11 wawe tayari kwa siku ya tatu;
maana siku ya tatu Bwana atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa
wote.
Alimwambia Musa pia amtie mafuta Haruni na kumtakaa.
Kutoka 40:12-13 Kisha utamleta Haruni na
wanawe hapo mlangoni pa hema ya kukutania, nawe utawaosha kwa maji. 13 Kisha utamvika Haruni mavazi matakatifu; nawe utamtia
mafuta, na kumweka awe mtakatifu, ili apate kunitumikia katika kazi ya ukuhani.
Hezekia aliingilia
kati na kuwatakasa Israeli.
2Nyakati 30:17-20 Kwa
maana kulikuwa na wengi katika kusanyiko ambao hawajajitakasa; kwa hiyo Walawi
wakamchinjia pasaka, kila mtu asiyekuwa safi, ili kuwatakasa kwa Bwana. 18 Kwani wingi wa watu, naam, wengi wa Efraimu, na wa
Manase, na wa Isakari, na wa Zabuloni, hawakujisafisha, lakini wakala pasaka,
ila si kama ilivyoandikwa. Naye Hezekia alikuwa amewaombea, akisema, Bwana
mwema na amsamehe kila mtu, 19 aukazaye moyo wake
kumtafuta Mungu, Bwana, Mungu wa babaze, hata ikiwa si kwa utakaso wa
patakatifu. 20 Bwana akamsikia Hezekia, akawaponya
watu.
Sisi pia tunajitakasa wenyewe
pale tunapozifuata Sheria na Torati ya Mungu na kuzitii.
Walawi 11:44-45 Kwa
kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa
kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha
aina yo yote, kiendacho juu ya nchi. 45 Kwa kuwa mimi
ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi
mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu.
Makabila na
mataifa yanatakaswa kwa matendo yetu, kama sisi tulivyotakaswa na Kristo na
matendo yake (Waebrania 10:10).
Ayubu alifanya
sehemu yake kuitakasa familia yake pale alipotoa sadaka ya kuwaombea kwa ajili
ya dhambi walizozitenda pasipo kujua ama kwa kupotoshwa.
Ayubu 1:4-5 Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika
nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao
watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao. 5 Basi
ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao
akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa
kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa
wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya
Ayubu sikuzote
Tunapowatakasa
wengine au sisi wenyewe, basi tunauandaa uwepo wa Mungu.
Kipindi cha
Siku Sabasaba Tatu:
Siku hizi 21 za
kila mwaka kinaweza kinaweza kugwanywa kwa vipindi vitatu vya siku siku
sabasaba.
Awamu ya
Kwanza – Siku Saba za Kwanza
Awamu ya kwanza
inaanzia na Mwandamo wa Kwanza wa Mwezi Mpya na kinaishia katika siku ya 7 ya mwezi
wa kwanza ambayo ni siku ya kufunga saumu. Kipindi hiki cha kwanza ni cha pale tunapoanza
kulisafisha hekalu (ambalo ni sisi wenyewe), lakini tunaombea mataifa ya dunia
yajue umuhimu wa kutakaswa. Hapo zamani, mchakato huu wa kulitakasa taifa
ulifanywa na wana wa Lawi (makuhani), na kisha kwa mwonekano wa kimwili
walikuwa ni wana wa Sadoki. Huduma hii sasa inafanywa na Kanisa na ukuhani ulio
wa mfano wa Melkizedeki. Kwenye kitabu cha Yoeli, Biblia inatuonyesha kwamba
kitendo cha kufunga saumu ni njia ya kuwatakasika na kuwapatanisha Israeli na
Mungu.
Yoeli 1:14 Takaseni saumu, iteni
kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa
Bwana, Mungu wenu, Na kumlilia Bwana,
Katika Siku hii
ya Saba ya Mwezi wa Kwanza, tunaenda mbele za Baba yetu na kwenda kuomba
msamaha kwa ajili ya bdhambi tulizozitenda kwa kupotoshwa ama kutokujua
kulikosababishwa na mambo tusiyoyajua vema yaliyoko kwenye jamii zetu na
kuwaombea ambao wengine wanamjua Mungu lakini hawataki kutubu na kutakasika
(Ezekli 45:18-20; Waebrania 5:1-2).
Ezekieli 45:18-20 Bwana MUNGU asema hivi; Mwezi wa kwanza,
siku ya kwanza ya mwezi, utatwaa ng'ombe mchanga mume mkamilifu; nawe
utapatakasa mahali patakatifu. 19 Na
kuhani atatwaa baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi, na kuitia juu ya miimo ya
milango ya nyumba, na juu ya pembe nne za daraja ya madhabahu, na juu ya miimo
ya lango la ua wa ndani. 20 Nawe
utafanya vivyo hivyo katika mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi kwa ajili ya
kila mtu akosaye, na kwa ajili ya mtu aliye mjinga, ndivyo mtakavyoifanyia
nyumba upatanisho.
Waebrania 5:1-2 Maana
kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu
katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi; 2 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye
kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu;
Utakaso Kanisa ni
mchakato unaopelekea watu kutakasika na Mungu kwa njia ya maombi na kufunga
saumu na kulisoma neno lake. Maandiko Matakatifu yanatuambia kufungua vifungo
vya uovu, kutua mizigo mizito, na kuwaacha huru wanaoonewa, na kuvunja kila
nira, ili watu wetu waweze kupatanishwa na Mungu wetu (sawasawa na Isaya
58:6-12).
Tnaweza kufunga
saumu na kuomba kwa niaba ya wale ambao hawayabatizwa na kwa niaba ya wasiomjua
Mungu na mapenzi yake. Tunaweza pia kufunga na kuomba kwa ajili ya wale
wasioweza kujitakasa wenyewe. (Kwa kujifunza hilo zaidi, tazama jarida la Utakaso kwa Ajili ya Dhambi Zilizofanywa Pasikujua
na kwa kupotoshwa (Na. 291) [Sanctification of the Simple and Erroneous (No.
291)]. Tunayatoa maisha yetu kwa jinsi ya mfano
kwa ajili ya ndugu zetu wakike kwa wakiume kwa kufunga na kuomba ili kuwaleta
watu wote kwenye uelewa halisi wa Mungu ili afanyike kuwa ni yote katika yote
na ndani ya yote.
Wakati Musa
aliposimama mbele za Israeli na kuinua mikono yake juu, tunaona kwamba
alihitaji [ia usaidizi. Ndipo Haruni na Huri walisimama na kuishikilia mikono
yake kuelekea juu na ndipo ilisaidia kusababisha ushindi na wokovu kwa Israeli
lakini ni kwa kupitia kitendo chao kile cha kuishikilia mikono iangalie juu (Kutoka
17:8-13). (Soma jarida la Musa na Waisraeli Wakielekea Sinai (Na. CB40) [Moses
and the Israelites Move on to Sinai (No. CB40) ili kujisomea kwa kina zaidi habari hii)]. Ndivyo tulivyo hata sisi,
tumepewa Kristo atusaidie kuwaokoa Israeli na kuwaleta kwenye haki na utauwa.
Mungu anawatumia wanadamu ili kuhimisha kazi yake kama fundisho litufikishalo
kwenye ukuaji na maendeleo.
Baadhi ya mambo kati ya mengi tunatotakiwa kuyaombea
wakati tunapofunga ni haya yafuatayo: wengi wapewe karama au kipawa cha kuitwa
na Mungu na nguvu za Roho Mtakatifu zimwagike juu yao; tupewe fursa njema ya
kuwafundisha vyema watu kwenye Njia na Mapenzi ya Mungu na kwamba watu warejee
kwenye Imani ya kweli; tuwezeshwe kurekebisha kikwazo cha uelewa na kurejesha
njia ya utakatifu; kazi ya karejesho au matengenezo isikumbwe na mkanganyo kwa
kushindanisha au kuifananisha na kazi ya manabii wa uwongo na mafundisho yao; kuwahamasisha
waumini au waaminio na viongozi wa Makanisa yote ya Mungu ili wahamasike na
waendelee kuwa na moyo mkuu; ili kuwe na amani na uhuru kwa watu wote; na kwamba
wote walindwe na hila za Yule Muovu (sawa na Luka. 11:1-4). (Imechukuliwa
kutoka kwenye jarida la Kalenda ya Pasaka (Na. A P2009) [Passover Calendar
2000 (A_P2009)].
Tunakumbushwa kwambat: "Kuomba kwake mwenye
haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii." (Yakobo 5:16; 2Nyakati 30:18-20).
Kipindi cha Pili cha Siku Saba (siku ya 8 hadi ya 14)
Tangu Siku ya Nane hadi ya kumi na Nne ya Mwezi wa Kwanza
tunapaswa kuendelea na wajibu wetu binafsi yetu kwa Mungu. Ni kipindi cha
kutafakari na kipindi cha kujikumbusha kuhusu vipaumbele vyetu vinatakiwa kuwa
ni vipi na inahitimishwa na mlo wa ushirika wa Meza ya Bwana unaofanyika Siku
ya Kumi na Nne. Inatupaswa kumuweka Mungu wetu mbele kwanza, familia yetu ya
pili na kazi zetu, masomo yetu au shughuli zetu nyingine zote ziwe kwenye
kipaumbele cha tatu. Tunatakiwa kutafakari na kujitazama huko nyuma tulifanya
nini na tuliwezaje kushindwa ama kushinda mwaka uliopita, na tutafanyaje
tofauti na tuliposhindwa kwa mwaka huu unaofuatia. Kwa mfano, tunaweza
kutafakari juu ya tabia zetu katika bidii ya maombi, utoaji au usomaji wetu wa
maandiko matakatifu na jinsi ngani tutajitahidi kufanya vizuri zaidi mwaka huu
ulioanza kuanzia hapa.
Kipindi hiiki cha mgawanyo wa siku saba za pili
kinajumuisha siku ya 10 ya mwezi. Hii ni ile siku ambayo Mungu aliwaamuru Israeli
wamchukue Yule mwanakondoo wa Pasaka na wawe naye karibu. Alitakiwa awe ni
mwanakondoo mume na mkamilifu na wa mwaka mmoja (Kutoka 12:3-5). Mwanakondoo huyu
wa Pasaka alikuwa anamwakilisha kimwili Yesu Kristo aliyekuja baadae na kuwa ni
mwanakondoo wetu wa Pasaka.
1Petro 1:18-21 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa
vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu
usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 19
bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila,
asiye na waa, yaani, ya Kristo. 20
Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya
dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; 21 ambao kwa yeye mmekuwa wenye
kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na
tumaini lenu liwe kwa Mungu.
Siku ya Kumi ya
Mwezi wa Kwanza ni wakati mzuri kwetu kutafakari juu ya uhusiano wetu Yesu
Kristo ulivyo. Yeye ni Kuhani wetu Mkuu (Waebrania 4:14), ndugu au kaka yetu (Warumi
8:16-17) na ni mfalme wetu tunayemngoja kurudi kwake hivi karibuni (Yeremia
23:5).
Inatupasa
tukumbuke kwamba tumetakaswa kwa damu ya Yesu Kristo. Ni kupitia dhabihu yake ndipo
tumepewa fursa ya kuupata uzima wa milele.
Siki ya mwisho
kipindi cha siku saba za pili ni Siku ya Kumi na Nne ya Mwezi wa Kwanza.
Mwanzoni mwa Siku hii ya Kumi na Nne ya mwezi ni siku ya kuadhimisha ushirika
wa Meza ya Bwana. Hii ni ibada ambayo waumini watuwazima na waliobatizwa
wanatafakari wito wao, ubatizo na wajibu wao kwa Mungu wa Pekee na wa Kweli.
Kwenye ibada hii ndiko waumini watu wazima na waliobatizwa wa Kanisa wanafanya
tendo linalofanyika mara moja tu kwa mwaka la kuoshana miguu (Yohana 13:1-5) na
kuula nkate na divai (vinavyoashiria au kuwakilisha mwili na damu ya Kristo). Ibada
hii inahudhuriwa na washirika waliobatizwa peke yao kwa kuwa ni wasaa wa
kulitafakari na kuliweka upya agano lao la ubatizo. (Soma jarida la Ushirika wa Meza ya Bwana (Na. CB 135) [The Lord’s
Supper (No. CB135)]. Ni muhimu kwa
waumini waliobatizwa kushiriki kwenye mchakato huu wa utakaso wa kila mwaka
kama walivyo wenyewe kwenye ibada ya Ushirika wa Meza ya Bwana.
Awamu
ya Mwisho wa Kipindi cha Siku Saba (siku ya 15 – 21)
Mchakato
wa utakaso hauishii kwenye ibada hii ya adhimisho la Meza ya Bwana. Siku
ishirini na moja za utakaso zinaendelea hadi adhimisho la Sikukuu ya Mikate
Isiyotiwa Chachu na inaishia siku ya mwisho ya Sikukuu. Sikukuu hii inataswirisha
wokovu wa Israeli na sayari hii yote. Mungu anatuonyesha sisi kwamba kwa
kuwatoa kwake Israeli utumwani Misri, alikuwa anaenda pia kututoa sisi kwenye
utumwa wa dhambi. Siku za mwisho, Mungu atamkomboa kila mmoja kwenye utumwa wa
dhambi hapa duniani.
Siku
ya Kwanza ya Mikate isiyotiwa Chachu (siku ya 15) ni siku takatifu na siku ya
mwisho ya Mikate Isiyotiwa Chachu (siku ya 21) pia ni siku takatifu. Hii ni
awamu ya tatu ya kipindi cha siku saba cha utakaso. Ni kipindi ambacho Kanisa
linatakiwa kukusanyika pamoja, na kuhudumiana na kufanya kazi kwa pamoja kwa
wajibu wetu tuliojiwekea kwa Mungu na kwa kutumikiana. Tunasafiri na kwenda
mbali na nyumbani kwetu ili kujikumbusha kwamba tunapaswa kutoka mbali na Misri
ya kiroho (dhambi) na kuiendea njia ya Mungu ya uzima. Sababu inayofanya kipindi
hiki cha utakaso kiendelee hadi kufikia Idi ya Mikate Isiyotiwa Chachu ni
kwamba, ni fursa nzuri kwa Kanisa kujiandaa kwa urejesho wa nguvu za Roho
Mtakatifu siku ya Pentekoste.
Siku
Ishirini na Moja za Utakaso zinaanzia na Mwandamo wa Mwezi na zinaishia na siku
takatifu na maana yake yanaonyesha taswira ya mambo yatakavyokuwa Mwezi wa
Saba. Inajumuisha vipindi vitatu vya siku sabasaba vinavyoendelea kutoka kutakaswa
kwa mataifa (saumu ya siku ya 7 ya mwezi kwa ajili ya dhambi zilizofanywa kwa
kupotoshwa) hadi kwenye utakaso wa kila mtu mmoja mmoja (adhimisho la kuula
ushirika wa Meza ya Bwana siku ya 14 ya mwezi) na hatimaye, kipindi cha kipindi
cha siku saba cha kutakaswa kwa kundi zima kinachoitwa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kipindi hiki cha utakaso cha
kila mwaka ni cha muhimu kwetu ili kuonyesha upendo kwa majirani zetu, upendo
katika uhusiano wetu na Mungu/na sisi wenyewe, na kuuonyesha upendo Mwili wa
Yesu Kristo ambao ni Kanisa lake Mungu.
q