Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[CB12]
Isaka:
Mwana
wa Ahadi
(Toleo 2.0 20031120-20070126)
Na Bwana akamtendea Sara alivyomhahidi. Sara akawa mja mzito na kajifungua mwana wa Abrahamu katika umri wake mzee, wakati ule ule ambao Bwana alimhahidi. Nakala hili limetolewa kutoka mlango wa 7 na 8 ya hadithi ya Bibilia volume 1 na Basil Wolverton, limechapishwa na chuo cha Ambassador na NIV Study Bible.
Christian Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Copyright ã 2003, 2007 Christian
Churches of God, ed. Wade Cox)
(Tr. 2009)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Isaka:
Mwana wa Ahadi
Baada ya kuharibiwa wa miji yordani. Abrahamu alielekea kusini magharibi mahala panapojulikana kama Gerar. Kama mUngu alivyo hidi mwana angezaliwa kwa Abrahamu na Sara Malaika alikwisha waambia watamwita Isaka. Abrahamu alikuwa na umri 100 wakati ambapo Isaka alizaliwa na Sara alikuwa na umri wa Miaka tisini 90 (Mwanzo 21:13).
Nyakati hizo ilikuwa ni mila kusherekea kwa ajili ya mtoto kati ya maika miwili n atatu. Isaka alipofika umri huo, Abrahamu aliandaa karamu kwa kuwa mwanawe alikuwa ameondoka utotoni na kuwa mvulana mchanga. Kwa kuwa alikuwa mtu aliyeheshimika sana, Abrahamu aliwaalika watu wa maana katika sherehe pengine hata mfalme wa Gerar.
Hagar na mwanawe Ishmaeli walipoona jinsi Isaka alipendwa na wengi walimwonea kijicho. Ismaeli alikuwa mwanawe wa kwanza wa Abrahamu na Hagar aliona chuki n awivu kwa kuwa Ishmaeli hakutazamiwa na wengi alipokuwa umri ule wa Isaka (Mwanazo 21:8-9). Wakati wa chakula cha usiku, Hagar na Ishmaeli walimrusha Isaka maneno mabaya. Mamake Isaka alikasirika alipowasikia.
Ishmaeli Aondoka
Ingawa Sara ndiye aliyemwambia Abrahamu azae na mtumishi wake Hagar, hakufurahia Hagar na ishmaeli kuishi naye na Abrahamu pahala pamoja. Alikwenda kwa Abrahamu na kumwaambia awafukuze Hagar na Ishmaeli. Huu ulikuwa ni shida kwa Abrahamu aliye jua hapange kuwa na furaha nyumbani pake ikiwa wanawake wale wawili wangechukiana au kuoneana wivu.
``Fanya atakayo Sara akatamani na kuwafukusha mbali’’, Mungu aliambia Abrahamu. ``Usi huzunike kwa ajili ya hiyo kwa kuwa nitawalinda, Isaka na sio Ishmaeli, atakuwa mwanao lakini kwa kuwa Ishmaeli nitafanya taifa nzima!’’ (Mwanzo 21:10-13).
Ahadi hii ilimtuliza Abrahamu. Akamheshimu Mungu. Awali keshoye akaanda kutoka kwa Hagar na mwanawe Ismaeli. Ambao alitazamia wata fika pahali watakapopumshika kutokana na jua kali la mchana. Pengine alitazamia hawatatembea sana ili kupata watakapoishi.
Ingawa kulikuwa na kibandi asubuhi. Hagar na Ishmaeli walichukua chakula na maji na wakaanza mwendo kwa miguu Hagar aliyekuwa Mmisri, alitoka na mwanawe kupitia jangwani mpaka kusini, pengine akitarajia kurudi Misri (Mwanzo 21:14). Aliamini ikiwa watafika barabara ya Misri wangelipata farasi ambaye angewapeleka kusini magharibi.
Halikufanyika kwisha alivyotarajia. Hagar alishindwa kupata njia ya farasi mchana wali kunywa maji yote kwa sababu kulikuwa na jua kali. Kutokuwa na kivuli lilikuwa motop hata katikati ya mchana Ishmaeli alianguka kwa ule mchanga vyakula na vibu kusimama tena. Kwa kuwa kijana alihitaji vyakula na vibu rudisho. Kuliko jinsi mamake alivyo hitaji ambaye aligundua kuwa ikiwa hatapata maji mara moja mwanawake angeuawa kwa kiu, kwa muda mrefu.
Hagar alisikitika. Hakukuwa na uwezekano wa kupata maji jangwani kwani kulikuwa na mchanga na mawe tu. Katikati ya mchana jua ulipokuwa mkali zaidi Ishmaeli alikuwa amekwisha anza kupoteza fahamu. Hagar alijaribu kumlaza kwenye kivuli kidogo jangwani. Akamwacha pale na ili asiyasikie na kutembea mbali hadi pahali hakuwesha kusikia maumivu yake. Hiyyo na kilio chake ndio kulikuwa sauti mbili jangwani kwa uchungu wa jangwani.
Ishmaeli aokolewa
Baada ya muda kulisikika sauti tofauti. Ilikuwa sauti ya malaika wa Bwana akinena na Hagar! ``Usijali kwa ajili ya mwanao Hagar’’ malaika akamwambia. ``Nenda kamsaidie. Mungu atalifanya taifa kuu kutokana na Ishmaeli‘’ (Mwanzo 21:17-18).
Hagar alitazama juu. Hakumwona mnenaji, lakini aliona kitu ambacho hakuwa amekiona mwanzoni. Ilikuwa kisima cha maji safi, sawa ilichotoka katika mchanga ambao ilikuwa muda kidogo kutoka pahali alipokuwa. Hagar alikimbilia maji ilo, na kujasha kiriba chake, na kwa shukrani alikimbilia kuweka zingine kwa paja la Ismaeli na kuweka zingine kwa ulimi wa Ishmaeli.Kwa Maana Mungu aliahidi Abrahamu kuwa ataulinda Ishmaeli na mamake. Alianza kwa kuokoa maisha yao jangwani.
Baada ya Ishmaeli kuamkua, yeye na mamaye hawakuweza kupata njia ya farasi. Walitembea kusini mashariki mpaka jangwa walikoishi. Ishmaeli akawa shupavu kwa uwindaji na aliweza kuwinda ndege na wanyama, kwa kitoweo chao wawili. Waliendelea kuishi jangwani kwa miaka mingi mpaka akawa kama mnyama pori (Mwanzo 16:12). Hagar alijaribu kumlea kama wake za Misri wanavyo fanya (Mwanzo 21:21). Ishmaeli na mkewe wakawa na watoto, na wale watoto wakawa na wao pia wakawa na wanao. Kwa muda taifa zima lilifanywa kutoka kwa Ishmaeli, jinsi Mungu alivyokuwa ametabiria.Leo tunajua hao watu kama ni wa Arabu.
Miaka na miaka Abrahamu alionyesha utiifu kwa Mungu na hivyo alionyesha ni mtumishi wa kweli wa Mungu. Mungu alipanga kumjaribu mara moja tena ambayo ingekuwa ngumu zaidi ya yale yote. Wakati ule aliishi pahali palipoitwa Beersheba, kasakasini mwa mahali ambapo Hagar na mwanawe waliendea jangwani. Hapo, Isaka alilelewa. Abrahamu alimshukuru Mungu kwa kuwa alimpea mwana mzuri. Alistaajabika siku moja aliposikia Mungu akisema: ``Kuchua Isaka katika ardhi ya Moria na kumtowa yeye kama sadaka ya kuteketeshwa’’ (Mwanzo 22:2).
Abrahamu angechagua kutoa uhai wake, lakini hilo lilikuwa kinyume na alichoambiwa na Mungu. Abrahamu alijua mtu hangefanya vyema zaidi kuliko kumtii aliyemuumba, hata awe ni ngumu kiasi gani. Hivyo alianza kufuata maagizop ali vyokuwa akiambiwa.
Lakini kabla ya Abrahamu kumchinja mwanawe Bwana akamwambia: ``Usimumize Isaka kwa kuwa umekubali kumtoa mwanako, najua umeniogopa!’’ (Mwanzo 22:10-12).
Abrahamu alijua Mungu alikuwa akinena naye kupitia kwa malaika. Alipiga magoti na kudondoza na machozi ya furaha na shukrani kwa kuwa Mungua hakumuacha amuue mwanawe. Hapo ndipo alipomwona kondoo katika msitu uliokaribu. Abrahamu alijua kuwa Mungu alikuwa amempea mnyama wa kuteketezwa badala ya mwanawe Isaka (v.13).
Isaka pia lazima
alishukuru wakati ambapo babake alimfungua kamba yaliyomfunga. Kwa maelezo
zaidi ya hadithi hii tazama nakala Abraham
and Isaac: A Faithful Sacrifice (No. CB11).
Pengine Mtu aweza dhani kuwa hii ilikuwa ukali kwa Mungu kumfanya Abrahamu karibu amuue mwanawe Isaka. Mungu si mkali. Ni mpendevu na mwenye huruma. Saa zingine hupeana majaribio makali kwa wanao mtii. Hii ni kudhibitisha utiifu au hekima kama vile walimu na wazazi hupeana mtihani kujua ni ipi mtoto amesoma.
Imedhibitishwa kuwa Abrahamu alimpenda muumbaji wake juu ya chochote au yeyote, hata mwanawe. Abrahamu alionyesha imani kuu kwa kile alichotaka kukifanya. Dhibitisho ulikuwa nzuri kwa Abrahamu na mfano mwema kwa Mamilioni ambao baadaye watasoma tukio hilo. Yaashiriwa pia kwa wakati miaka elfu mbili baadaye ambapo Mungu mwenyewe angemtoa mwanawe wa kipekee, Yesu kuuwawa kwa ajili ya dhambi na maovu za wanadamu.
Vizazi vya Abrahamu waahidi maisha mwema
Kabla ya Abrahamu na Isaka kuteremka chini, Bwana alinena na Abrahamu. ``Kwa kuwa ulikubali kumtoa mwanao kwa wangu’’, Mungu alihaidi, akinena kupitia Malaika, ``Kwa kweli nitakubariki. Vizazi vyako watakuwa wengi kama nyota ya mbinguni na kama mchanga iliyo kando ya bahari. Wataweza kuwashinda maadui wao. Mataifa yote ya ulimwengu wata taka kuwa kama wale walitoka kwako. Hizi zote zitafanyika kwa kuwa umenitii!’’
Baada ya Abrahamu na Isaka kurudi pahali ambapo wal; e watumishi wawili walikuwa wakimgonja, walirudi mpaka Beersheba.
Baadaye Abrahamu alihama Hebron kasakasini mwa sehemu ya nchi ya kanaani. Hapo Sara aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 127. Huyu mama wa Mamilioni ya watu wanaoishi dunianai na ulimwengu na alizikwa katika hema katikati ya uwanja ambao ilikuwa ya Abrahamu.
Karibu miaka tatu baada ya mke wake Sara kufa, Abrahamu alianza kufikiria jinsi Isaka angeweza kuowa. Isaka alikuwa na umri wa miaka 40. Abrahamu alionelea kuwa Isaka asiowe kati ya wana wa Kanaani ambao walikuwa waabudu sanamu.
Abrahamu alimuagiza mtumishi wake mkuu awachukue watu, ngamia na chakula kwa tayarisha safari ya kwenda Mesopotamia, Hilo ndio ilikuwa ardhi asili ya Abrahamu, na kuleta mke kwa Isaka kutoka kati ya watu wao (Mwanzo 24:3-4). Ilikuwa kimila wakati huo,kama ilivyo katika nchi zingine sasa,kwa wazazi kuwachangulia wanao na wasichana wachumba wao.
Abrahamu alijua kwa uhakika kuwa bado kulikuwa na watu wengi Mesopotamia ambao walimuabudu Mungu.Alikuwa na ndunguye Nahor aliyeishi huko na alikuwa na familia kubwa (Mwanzo 22:20-24). Alijua ingempendeza Mungu kwa Isaka kumuowa mchumba kutoka katika familia yake (Lakini sio jamaa wa karibu) badala ya mwabudu sanamu kama mchumba.
Mtumishi wa Abrahamu Ampata
Rebeka
Baada ya siku kadhaa ya safari kaskazini mashariki, mtumishi wa Abrahamu na farasi iliwasili jioni moja katika kisima nje ya mji wa Nahor (Mwanazo 24:10). Kwa siku huo wanawake ndio walioteka maji visimani. Mtumishi wa Abrahamu aliomba kuwa mioungoni mwao wangempata mchumba mwema kwa ajili ya mwana wa tajiri wake. Aliomba kuwa Mungu angemchagua mchumba huyo kwa kumfanya ajitolee kumtekea yeye na ngamia zake maji. Hii ingeonekana kuomba vitu vingi kutoka kwa Mungu. Nani angekubali kuchota maji kwa ngamia kumi walio na kiu?
Lakini hata kabla mtimishi haja maliza kuomba, msichana nzuri alimtokelea haki karibia kisima. Alipokuwa akiteka maji, mtumishi wa Abrahamu alimjia na kumwomba maji anywe. Mara moja alimpa maji kutoka ka kikombe (Mwanzo 24:11-15). ``Kunywa, bwana wangu,’’akasema.`` Hii yaweza kuwa majibu maombi yangu’’ alifikiri mtumishi yule. ``Ame kubali kunipa maji lakini hatakubali kutaka taabu zangu’’. Mtumishi wa Abrahamu alishutuka msichana yule alipomuambia `` Nitafurahi kuwachotea ngamia zako maji pia! nitawapa kadri ya watayoweza kunywa.
Huu ulikuwa jibu mara moja kwa maombi aliloomba dakika chache tu awali. Mtumishi yule alikuwa na uhakika kuwa yule ndiye aliyokuwa mchumba wa Isaka. Kwa kumlipa alimpoa pete ya dhahabu iliyokuwa na uzito wa nusu shekeli na bangili ya dhahabu uliokuwa na uzito wa shekeli 10 (Mwanzo 24:22).
Shekeli Kumi uliashiria malipo ya uhuru ya mwana mke dada aliye kati ya miaka tano na ishirini. Malipo ya uhuru ya watu ulikuwa sheria na wala haukuwa mzigo (Walawi 27:1-8) nusu shekeli yaonyesha shekeli ya mahali Hekalu kama usuru jinsi ilivyo tajwa kwenye upatanisho takatifu (Kutoka 30:11-16). Kristo alilipa garama yetu, alipokufa kwa ajili yetu.Bangili na henni yaashiria kama upatanisho (Hesabu 31:49-50).
Alipomuuliza jina lake, alipokea mshutuko lingine. ``Mimi ni Rebeka‘’, alimwambia. `` Mimi ni bintiye Bethueli, Mwanawe Nahor.’’
Nahor alikuwa nduguye Abrahamu, sasa mwanamke msichana alikuwa sangazi ya Isaka! Ilikuwa habari njema kwa Mtumishi kwa kupata mchumba ambao ni jamaa ya Abrahamu, na kwa yule aliye jua Mungu moja ya kweli. Mtumishi wa Abrahamu mara moja akashukuru Mungu kwa kumzaidia.
Labani amualika mgeni
nyumbani
Rebeka alikimbia nyumbani kuwaeleza kwa furaha familia yake kilichotendeka na ili kuwaonyesha yale bangili na pete. Kama nduguye Labani alipoona yale mapambo yenye bei ghali na kuisikiza hadithi ya Rebeka, aliharakisha mpaka pale kisimani kumualika mtumishi wa Abrahamu nyumbani kwake (Mwanzo 24:29-31). Mtumishi wa Abrahamu alishukuru kwa mwaliko ule, lakini kabla hajai kubali aliahakikisha watu waliokuwa naye walipimzisha na kuwapa chakula za kuwatengezea wake ngamia pahali pa kulala kisha yeye na watu wake walipewa maji ya kuosha miguu. Hii alikuwa desturi muhimu kwa walio ishi jangwani ambapo palikuwa na vumbi na kulifanya watu kuchoka.
Kisha walipewa chakula, lakini watumishi wale hawangekula mpaka walipomwelezea mwenyeji sababu yao kuja (v. 33). Akawaeleza familia ya Rebeka kilichokuwa kimemtendekea Abrahamu kuanzia siku alitoka Harani miaka mingi zilizo pita. Aliwaambia jinsi Abrahamu alivyomtii Mungu kati ya watu wasiomtii Mungu na jinsi Abrahamu alivyotajirika na babake mpendwa mwana mtiifu Isaka.
Wakati ambapo mtumishi yule aliwaambia kuhusu ombi lake kuhusu mke mwema kwa Isaka na jinsi Rebeka alivyotimiza ombi lile, familia ya Rebeka alijua Mungu ndiye aliyemuelekeza kwa Rebeka.
``Tume amini kuwa ni matakwa ya Mungu kuwa Rebeka awe mchumba wake Isaka ‘’ Walimwambia mtumishi (v. 50).
Mtumishi alifurahia kusikia hivyo na tena akamshukuru Mungu kisha akaamrisha Rebeka aletwe dhahabu, fedha na nguo nzuri na zawadi kwa familia yake (v. 53). Zawadi zile za mali zilizopeanwa kwa Rebeka na familia yake ilionyesha kuwa familia yake ya baadaye ni tajiri. Kisha mwisho wote walisherekea ikiwa msomaji atafikiria kuwa ilikuwa sihaki kwa Rebeka kwa kuwa haki changia kwa mipango hayo yote, lazima ikumbukwe kuwa wakati huo wake wakichaguliwa kwa njia tofauti tofauti. Rebeka alikuwa ametoshelezeka na mwenye furaha. Ingawa hakuna amemuuona Isaka. Kilicho cha muhimu zaidi ni kuwa Mungu ndiye aliyekuwa mwenye mipango hayo ambayo ungeonelea waliohusishwa walikuwa na furaha.
Asubuhi iliyofuata familia ya Rebeka waliuliza ikiwa ataweza kukaa siku kadhaa nyumbani. Mtumishi wa Abrahamu akawakumbusha kuwa Mungu alimwelekeza kwa Rebeka haraka na hakuna sehemu ya mpango ungehairishwa. Rebeka akasema alikuwa tayari kutoka mara moja kwa hiyo waka funga safari ya kurudi katika safari ya kurudi msafara wa ngamia uliongezeka kwa ajili ya ngamia walioongezwa waliobeba Rebeka, mtunzi wake na watumishi wake. Familia ya rebeka iliuzunishwa kumwona akienda lakini walikuwa na raha kujua alimpata mchumba mwema kuwa bwanawake (vv. 55-61).
Isaka amuona Mchumbake
Masiku baadaye, Isaka alipokuwa akitembea uwanjani, aliona msafara wa farasi ukikaribia alienda kuilaki na matumaini ya kuwa alikuwa yule Babaye aliyemtuma Nahor.Wakati Rebeka alipomwona mwanaume akiharakisha kwao aliuliza ni nani. Kwa kuambiwa kuwa yule ndiye angemuona aliridhika, alivaa haraka haraka kabla ya kushuka kutoka kwa ngamia kumpokea Bwanake mtarajiwa (v. 65).
Isaka na Rebeka walifunga ndoa muda mfupi baada ya kukutana. Kwa kuwa walikuwa na Baraka za Mungu, walifurahia (v. 67). Kupitia kwao muumbaji alipiga hatua kwa kuanzisha taifa litalofanya kazi ya maana katika ulimwengu kupitia vizazi.
Miaka thelathini
na tano baadaye, katika umri wa miaka 175 Abrahamu akaaga dunia (Mwanzo
25:7-8). Wana wawili wa Kwanza Ishmaeli na Isaka walimzika baba yao katika
kaburi lile alilozika bibiye wa kwanza Sara (Mwanzo 25:9-10) tazama nakala Ahraham and Sarah (No. CB10).
Ingawa Isaka na Rebeka walifurahia ndoa yao, miaka ilipita bila ya kupata watoto. Walihaibishwa sana mpaka mwishoni Isaka akamwomba Mungu awatumie mwana (Mwanzo 25:21). Mungu akayjibu maombi yao. Baada ya miaka ishirini ya ndoa, Isaka na Rebeka walijua kuwa mwisho wngekuwa wazazi.
Wakati mwingine Rebeka tesheka maumivu ya siyo yakawaida kwa hiyo aliomba kwa uponyaji. Mungu alimuambia labda kwa ndoto au maono, kuwa angeweza mwanzo wa mataifa mbili. Taifa moja angekuwa na nguvu kuliko lingine, aliamimbiwa, na kifungua mimba angemtumikia mwenzake. Mungu akampa nguvu kuendelea alivyo mpaka alipowazaa mapacha na kuwa mama wa pacha wanaume. Wakwanza kuzaliwa aliitwa Esau. Na wapili aliitwa Yakobo (Mwanzo 25:22-26).
Isaka na Abimaleki
[Tazama: kutoka hapa kwa The NIV Study Bible ilitumika kusashiria na maana]
Kulikuwa na kuangazi katika nchi na Iska akamuendea mfalme Abimaleki wa Gerar.Huu ulikuwa kiangazi tofauti na ule wa wakati wa Abrahamu alipo enda Misri (Mwanzo 12:10). Bwana akamtokea Isaka na akamwambia asiende Misri .
``Kaa katika nchi hii kwa muda kidogo,na nitakuwa nawe na kukubariki. Kwa maana kutoka kwako na kwa kizazi chako nita wapaa ardhi hii yotenita kaa nyuma ya haadi niliyo fanya kwa babako Abrahamu. Nita fanya vizazi vyako mengi kama nyota ya mbinguni na nita wapaa ardhi hii yote, na kupitia kizazi yako nita bariki taifa zote za dunia, kwa maana Abrahamu alinieshimu na kuogopa amri zangu, sheria na hangizo langu’’ Sasa Isaka alikaa Gerar (Mwanzo 26:3-6).
Sasa kama Sara, Rebeka alikuwa mrembo. Hivyo waume wan chi ile walipomuuliza Isaka kuhusu bibiye alisema ``Ni dadangu ‘’ aliogopa kusema ni mkewe kwa kuwa alidhani wale watu wangemuua na kumchukua mkewe lakini, baada ya Isaka kuwa pale muda mrefu, mfalme aliangalia nje ya dirisha lake na akamuona Isaka akimpapasa mkewe. Kwa hivyo alitumana Isaka aitwe ``Ni mkeo wa kweli! kwa nini ulisema ni dadako?’’
Isaka akamwambia mfalme aliogopa atauwawa kwa ajili ya Rebeka. Hivyo Abimaleki alikasirika kwa kuwa moja wa watu wale wangemchukua Rebeka kama mke. Sasa Hivyo akapeana amri kuwa yeyote atakayemshika Rebeka atauwawa (Mwanzo 26:7-11).
Ni jambo la kufarahisha kwamba babake Isaka, Abrahamu alifanya vivyo hivyo alipoenda Misri. Alidanganya kuwa Sarai mkeo alikuwa dadake. Kama Isaka, alidhani kuwa uongo huo ungeokoa maisha yake (Mwanzo 12:11-14). Wote wange muanmini Mungu kuwalinda kwa kuwa tayari alikuwa ameahidi kufanya hivyo.
Isaka alipanda mimea na baada ya muda alitajirika, na akazidi. Alikuwa na mifugo mengi na watumishi ambao walikuwa Wafilistia walimwoneajicho na wakaanza kumchukia. Baadaye Abimaleki alimtukuza Isaka kuwa alikuwa maarufu zaidi (Mwanzo 26:12-16). Kama Mungu alivyoweka ahadi .na kuyatimisha agano lake watu wake walibarikiwa na walionwa kama tisho kwa wengine katika nchi walipoishi.
Kwa hivyo Isaka alitoka na akaishi katika bonde la Gerari. Akafungua visima vilivyofungwa ambavyo babake aliuwacha. Watumishi wa Isaka walichimba bonde na wakapata kisima chamaji masafi. Lakini wale wachungaji wengine waka wagombanisha kuwa maji hilo ni yao. Hivyo akaiita kisima kile Esek kwa sababu walingangania naye. Kisha wakachimba kisima lingine na waka ngangania pia akaiita Sitnah.Aliendelea na kuchimba lingine na hakuna aliye ngangania hiyo. Aliita Hiyo Rehoboth, kusema,`` Kwa kuwa Munguametufanyia nafasi an tutazidi katika nchi’’ (Mwanzo 26:17:22).
Baadaye Isaka akaenda Beersheba. Hapo Bwana akamtokea na akasema,`` Mimi ndiye Mungu wa babako Abrahamu. Usiogope kwa kuwa niko nawe; nitakubariki na nitazidisha kizazi chako kwa ajili ya mtumishi wangu Abrahamu’’ (Mwanzo 26:23-24).
Isaka akajenga dhabahu pale na akaliitia jina la Bwana. Hapo akafunga weka hema lake na pale watumishi wake wakachimba kisima. Punde Abimaleki alikuwa amemjia na watu wake kutoka Gerari. Ambao Isaka aliuliza: `` Mbona mwanijia, nanyi mlinichukia mkanifukuza kwenu?’’ (Mwanzo 26:25-27).
Wakajibu: ``Hakika tuliona ya kwamba Bwana alikuwa pamoja nawe;nasi tukasema, na `tuapianeagano na ulewano kati yetu. Wacha tufanye kwa fanya kibaya, na iwapo sisi hatuko gusa wewe wala hatukutendea ila wema tutakuacha uende zako kwa amani ‘. Na sasa umebarikiwa na Bwana‘’ (Mwanzo 26:28-29).
Isaka akaandaa karamu kwa ajili yao na wakala na kunya. Karamu hiyo ilikuwa yakuonyehsa urafiki baina yao kama chama cha agano. Mapema siku iliyofuta waliapiana na agano kwa kila mmoja. Halafu Isaka akawaacha kwa amani wakichukua mwenendo wao. Siku watumishi wa Isaka walienda kumwambia kuwa walikuwa wamepata maji mengi zaidi. Alikiita kile kisima Shibah na mpaka wa leo jina la jiji hilo inaiitwa Beersheba (Mwanzo 26:30-33).
Baraka za Isaka inaendelea
Waba wa Isaka walikua na Esau alikuwa mwindaji mashohoni na Yakobo alikuwa mtulivu aliyekaa hemani. Isaka alimpenda Esau zaidi na Rebeka alimpenda Yakobo zaidi (Mwanzo 25:27-28), sasa kila mzazi alikuwa na mwana ampendayo zaidi. Ingawa, wazazi wanapenda wanao zote sana, zazingine wana weza kuwapa nehema kwa mmoja kuliko mwingine.
Esau ndiye aliyekuwa kifunga mimba kwa hiyo alikuwa mkuu kulingana na tamaduni na ahadi. Tamaduni hii pia alijumilisha kuridhi wa haki ya kifungua mimba. Hii yamaanisha Esau alikuwa na haki ya sehemu mara mbili ya vitu vya babake. Chini ya kaza Esau alimuusia haki ya kuzaliwa kwa nduguye mdogo Yakabo. Hivyo Esau akaidharahu haki ya kuzaliwa wa kwanza na Yakobo (Mwanzo 25:29-34).
Yakobo na mamaye wakapanga
kuchukua Baraka za Mungu kupewa Yakobo.Mungu alikwisha ahidi Rebeka kuwa mwanao
wa kwanza angemtumikia yule mdogo, basi angekuwa na imani kuwa Muingu atatenda
jinsi ameahidi (Mwanzo 25:23). Kwa sababu ya damu mbaya iliyokuwa kati ya wale
ndugu wawili, Yakobo alifukuzwa mbali kwa ajili ya usalama na kumtafuta mke.
Kwa mengu kuhusu hadithi ya wana wa Isaka Tazama nakala Jacob: The son of Isaac (No. CB13).
Yakobo baadaye ali fanya amani na nduguye Esau na akamjianyumbani kwa babake Isaka katika Herbon ambako Abrahamu na Isaka aliishi. Baada ya Isaka kuishi miaka 180 aliaga dunia ``akakusanyika kwa watu wake, wazee na waliokuwa na siku kadhaa.’’ Na wanawe Esau na Yakobo wakamzika (Mwanzo 35:27-29).
q