Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[CB23]

 

 

 

 

Siku za Ibada za Shetani

(Toleo La 2.0 20030312-20061223-20140209)

 

Watu wengi sana duniani wanaadhimisha sikukuu za Krismas, Easter na Mwaka Mpya, lakini je, kuna msingi wowote wa kimaandiko unaotuamuru kuzishika sikukuu hizi? Na kama hakuna, je, tunaweza basi kuziadhimisha Siku za Mungu sambasamba na huku tukizishika sikukuu hizi za uwongo na potofu za kidini?

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

 

(Hati Miliki © 2003, 2006 Diane Flanagan, ed. Wade Cox)

(rev. 2014)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.

 

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 


Siku za Ibada za Shetani


 

Ibada ya Kweli

Watakatifu wa Mungu ni wale wanaozishika Amri za Munguna Ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12; 22:14). Wanamuabudu Mungu Mmoja wa Pekee na wa Kweli (Kum. 6:4; Yohana 1:18; 17:3; 1Timotheo 6:16; 1Yohana 5:20). Wanazitii Sheria na Torati yote na wanamuabudu Mungu kwa siku zake sahihi zilizoagizwa kwa namna ambayo ameiamuru Mungu.

 

Namna potofu ya kuabudu

Shetani Mfalme wa mamlaka ya uweza wa anga (Waefeso 2:2). Hii inamaana kwamba Shetani ana uwezo wa kushawishi fahamu na uelewa wa watu na fikra zao. Shetani anapenda kugeuza na kupingana na Mipango ya Mungu. Kwa kweli, Mungu hatakubali hilo litokee. Lakini kwa kipindi cha miaka 6,000 ambayo Shetani ameruhusiwa kutawala hapa Duniani ,Sameanzisha mafundisho mengi sana ya uwongo, na kwa kufanya kwake hivyo amewapata watu wengi sana.

 

Kumbadili Mungu tunayemuabudu

Shetani ameweka mchanganyiko wa sehemu ya ukweli na uwongo. Au amechukua imani na desturi za kipagani za kale na kuyachanganya na kiasi fulani cha ukweli. Shetani amewafanya pia watu waamini kwamba Mungu anakamilika kwa muunganiko wa viumbe watatu, imani inayoitwa ya Utatu. Tunajionea wazi kabisa kutoka kwenye Timotheoy 6:16 inasema wazi kabisa kwamba kuna Mungu Mooja tu wa Pekee na wa Kweli (soma jarida la Mungu ni Nini? Na. CB 1 [Who is God? (No. CB1)]. Ni huyu Mungu wa Pekee na wa Kweli ndiyw tunayemuabudu kwenye zile siku alizozitenga na kuzibarikia kuwa ni Siku Takatifu na kutuamuru tumfanyie makusantiko Matakatifu. Ingawa Shetani aliumbwa mkamilifu, aliasi. Alimuasi Mungu na kujaribu kukitwa Kiti cha Enzi cha Mungu (Isaya 14:13). Alipokuwa ameumbwa kwanza jina lake lilikuwa ni Lusifeli, ambalo linamaansisha Mleta Nuru, lakini Mungu alilibadilisha na akaitwa Shetani, ambalo maana yake ni Mshitaki au Mlleta mashitaka (1Petro 5:8; Rev. 12:10). Ili kujifunza zaidi

 

 

kuhusu uasi huu, soma jaridea la Uumbaji wa Familia ya Mungu (Na. CB4 [The Creation of the Family of God (No. CB4)].

 

Kwa vipindi fulani mbalimbali Shetani amefanya mjaribio mbalimbali ili kuusimamisha Mpango wa Mungu. Mara tu baada ya kifo cha Kristo, Shetani alianzisha dini na imani mbalimbali zilizonuia kukomesha ushikaji wa Sheria au Torati. Ndipo aliweka mafundisho yanayobadilisha asili ya Mungu tunayemuabudu, na kujumuisha mafundisho mengine yanayotokana na imani za kale za kipagani na kuyaingiza kwenye Ukristo. Wapagani ni watu wanaoabudu miungu mingi mbalimbali, lakini hawana uhusiano na Mungu wa Pekee wa Kweli (Eloa). Kwenye maeneo mbalimbali ya duniani miungu hawa wengi wa Utatu (imani ya miungu wanaojumuisha viumbe watatu) wanaabudiwa. Kwenye kipindi cha zamani sana kabla ya kufa kwa Kristo, imani hii ya Utatu ilifanikiwa kuingizwa kwenye Kanisa Katoliki la Roma  

 

Watu wengi sana leo wanaamini kuwa Mungu anatokana na muunganiko wa viumbe watatu kwa kile kinachoitwa—Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Huu ni uwongo mkubwa sana. Bali kuna Mungu Baba mmoja, na ndiye Muumbaji wa vitu vyote na ni yeye tu peke yake ndiye tunayetakiwa kumuabudu. Pia kuna Yesu Kristo, Mwanae, ambaye alikuja hapa Duniani akiwa kama Malaika wa Yahova na kuongea na nabii Musa na manabii wengine, kama Biblia inavyotuambia. Hatimaye, Kristo alitwaa mwili wa kibinadamu na akafanya ishara mpya kwa njia ya maadhimisho ya Pasaka. Akafanyika kuwa ni sadaka kamilifu na takatifu ambayo iliwapatanisha na Watakatifu kwa Mungu Baba. Soma jarida la Mungu ni Nini? Na. CB2) [Who is Jesus? (No. CB2)].

 

Roho Mtakatifu ni uweza tu wa Mungu. Anatusaidia kuwasiliana na Mungu na anatusaidia pia kuyajua mapenzi ya Mungu na anayotaka tuyafanye. Lakini hii isitufanye sisi tumruhusu mtu yeyote ajaribu kutudanganya kwa kutuambia kwamba miungu hii mitatu inafanya jumla ya Mungu mmoja. Shetani hajali jinsi anavyowapotosha watu mbali na Mungu wa Kweli. Soma jarida la Roho Mtakatifu Ninini? (Na. CB3) [What is the Holy Spirit? (No. CB3)].

 

Kuibadili kalenda na mwanzo wa siku

Mungu anatuambia kwamba mwaka mpya unaanzia mwezi wa Abibu, mwezi ambao wana wa Israeli walitolewa utumwani Misri (Kutoka 13:4). Kwenye kalenda ya Kirumi huu ni mwezi wao wa Machi au Aprili kutegemea na mwaka ulivyo. Ili kuelewa kikamilifu kuhusu Kalenda, soma jarida la Kalenda Takatifu ya Mungu (Na. CB20) [God’s Sacred Calendar (No. CB20)]. Kalenda ya kale zaidi ya Kirumi pia mwaka wake ulikuwa unaanza mwezi wa Machi/Aprili. Kwa kipindi kifupi tu, Shetani alifanikiwa kuwashawishi karibu watu wote duniani kubadilisha mwanzo wa mwaka hadi kwenye mwezi wa Januari, kama unavyojulikana leo kwenye kalenda ya Wagregoriani.

 

Karibu miezi yote ya mwaka mzima imeitwa kwa majina ya miungu ya kipagani, watawala au idadi ya miezi kutokea mwezi wa kwanza wa kalenda:

 

  1. Januari unatokana na jina Janus, ambaye ni mungu wa kale wa Warumi.
  2. Februari unatokana na neno Februaries, kwa kuwa shughuli za ida ya utakaso ya Warumi ilikuwa inafanyika tarehe 15 ya mwezu huu.
  3. Machi unatokana na neno Mars, ambaye ni mungu Vita. Hapo kale, Warumi, pamoja na watu wa ulimwenguni kote walianza mwaka mwezi huu wa Machi.
  4. Aprili unatokana na neno Aprilis, ambapo atdhi inafunuliwa tayari kwa kuchipusha mazao na mimea.
  5. Mei unatokana nan neno Maia, ambaye ni mungu mke wa makuzi au maongeo.
  6. Juni unatokana na neno la Kilatini Junius (la mungu mke aliyeitwa Juno). Yuhu ni mungu mke mwenye nguvu za uzazi wa Dola ya Warumi na ni miongoni mwa miungu mitatu iliyokuwa inaabudiwa na kuunda itikadi ya utatu.
  7. Julai unatokana na neno la Kilatini Julius (jina alilokuwa anaitwa Kaisari Yulio au Julius).
  8. August unatokana na jina Augustus, aliyekuwa Kaisari wa Kirumi.
  9. Septemba unatokana na neno la Kilatini Septim lenye maana ya saba, kwa kuwa hapo mwanzoni ulikuwa ni mwezi wa saba kwenye kalenda ya Warumi. Siku hizi ni mwezi wa 9. Miezi miwili iliyopewa majina ya Makaisari iliongezwa.
  10. Octoba unatokana na neno Octo linalomaanisha nane; ni mwezi wa 8 wa Kalenda ya kale ya Warumi ambayo mwezi wake wa kwanza ulikuwa unaanzia Machi. Huu ni mwezi wa 10 wa kalenda ya Wagregoriani.
  11. Novemba unatokana na neno Novem ambayo inamaanisha tisa; ambao ni mwezi wa 9 wa Kalenda ya kale ya Warumi. Ni mwezi wa 11 wa kalenda ya Wagregoriani.
  12. Desemba unatokana na neno Decem inayomaanisha kumi; ambao ni mwezi wa 10 wa Warumi wa kale. Ni mwezi wa 12 sasa.

 

(Hii hi kwa mujibu wa Kamusi ya kitabu cha Fafanuzi kiitwacho The Living Webster Encyclopedic Dictionary of the English Language 1977.)

 

Mungu anatumia hesabu au idadi ili kuitambulisha miezi yake (Kutoka 12:2; 13:4; 2Nyakati 30:2; Nehemia 8:2). Katika kipindi hiki tutaona majina yaliyotumiwa kuitaja miezi kwenye Kalenda ya Mungu. Majina haya yana asili ya Kikanaani au Kibabelonia na yaliingia kwenye lugha ya Kiyahudi.

 

Mungu anatumia pia idadi katika kutambulisha siku za juma. Siku iliyotajwa kwa jina tofauti ni Sabato tu. Sabato ni siku ya saba ya juma, lakini imetajwa kuwa ni Sabato.

 

Mfumo wa Shetani pia unatumia majina ya miungu kwenye majina ya siku za juma:

 

  1. Sunday (Jumapili) inatokana na neno Sunnandaeg la Kiingereza cha Zamani, ambalo maana yake ni siku ya mungu jua. Zamani iliadhimishwa kuwa ni siku ya kuliabudu jua au kumuabudu mungu jua.
  2. Monday (Jumatatu) inatokana na neno Monandaeg la Kiingereza cha Zamani linalomaanisha ni siku ya mwezi mwandamo.
  3. Tuesday (Jumanne) inatokana na neno Tiwesdaeg la Kiingereza cha Zamani linalomaanisha siku ya mungu Tiw, ambaye ni Mars wa pande za kaskazini au mungu wa vita.
  4. Wednesday (Jumatano) inatokana na neno Wodnesdaeg la Kiingereza cha Zamani linalomaanisha Woden au bidhaa ya miti.
  5. Thursday (Alhamisi) ilikuwa ni siku iliyowekwa wakfu kwa Thor, mungu wa Ngurumo au Radi wa Waskandinavia wa kale.
  6. Friday (Ijumaa) inatokana na neno Frigedae la Kiingereza cha Zamani ambayo ni siku iliyowekwa wakfu kwa Frigga au Freya, mungu mke wa Wateutoni.
  7. Saturday (Jumamosi) inatokana na neno Saeterdaeg la Kiingereza  cha Zamani lenye maana ya siku ya mungu Saturn. (ibid.)

Kumbuka: O.E. = ni badala ya Kiingereza cha Zamani.

 

Kama tunavyoona kwamba Shetani aamejaribu kubadilisha vitu na mambo yote ambayo Mungu ameyapanga ili sisi tuweze kujua ni kipindi gani kilicho sahihi kumuabudu. Kitendo cha kuabudu siku isiyopangwa au kuamriwa hakimaanishi wala kuonyesha kuwa tunamheshimu au kumuabudu yeye Mungu Baba yetu na kuzitii Amri zake.

 

Biblia inatuambia kwamba siku inaanzia majira ya kuzama jua (Walawi 23:32; Nehemia 13:19; Matendo 27:27-33). Siku nyingi sana zilizopita watu walijua kwamba siku ilianzia muda jua linapozama giza likianza. Lakini Shetani alimudu kunpata mtu wa kuongoza mkakati huu wa kubadilisha majira ya kuanza kwa siku. Hivi sasa siku inaanzia usiku wa manane. Hili ni jaribio lingine la Shetani katika kuwachanganya watu na kuichanganya siku wanayopaswa kumfanyia ibada Mungu.

 

Kama hatutamuabudu huyu Mungu wa Pekee na wa Kweli katika siku alizoziweka na kutuamuru, basi tujue kwamba tunamuasi au hatumpi heshima yake yeye Mungu!

 

Kuibadili Sabato

Kwa kujaribu zaidi kuuharibu Mpango wa Mungu, Shetani alijaribu kuzibadili siku ambazo tulipaswa kumfanyia Mungu ibada. Na ndiyo maana wengine wanasema kwamba siku tunayopaswa kumuabudu Mungu ni Jumapili. Siku za kale, watu waliliabudu jua siku hii kwa kuwa kilikuwa ndiyo kitu wanachikiona na walijua kwamba jua lilikuwa ni la mihimu sana katika kuwapa uhai wao na mazao yao. Siku hii ya Jumapili ilikuwa rasmi kwa kuliabudu jua. Tangu ksrne ya pili, ibada hii ya kuliabudu jua ilianza huko Roma sambamba na ibada ya Sabato. Katika kipindi cha takriban karne ya 3 na 4, watu fulani walijaribu kuibadili Sabato na kuitukuza Jumapili na waliwashawishi wengine kuukubali na kuueneza uwongo huu. Soma jarida la Siku ya Sabato (Na. CB21) [The Sabbath Day (No. CB21)].

 

Kuingiza sikukuu za upotofu zichukue mahala pa Siku Takatifu za Kila Mwaka Zilizoamriwa na Mungu

Karibu sikukuu zote za zinaendana na majira ya kukua mazao. Miaka imegawanywa kwa kufuatia vipindi vya ikwinoks, vya usiku kuwa mrefu cha solstices na siku za robo mwaka. Kipindi cha ikwinoks kinatokea wakati jua linapopita kwenye mstari wa ikweta na siku hii masaa ya usiku na mchana yanalingana urefu wake duniani kote. Ikwinoks ya majira ya baridi inatokea mnamo tarehe 21 Machi na ile ya majira ya joto inatokea Septemba 23. Majira haya ya solistais yanakuwa jua linapokuwa mbali sana kutoka kwenye mstari wa ikweta. Linafika upande wa kaskazini zaidi ya dunia tarehe 21 Juni, ambayo ni siku ndefu zaidi ya mwaka kwa upande Ukanda wa Kaskazini, na Desemba 21, ambayo ndiyo siku fupi zaidi ya mwaka kwenye Ukanda wa Kaskazini. Kwenye Ukanda wa Kusini, siku ndefu kuliko zote ni tarehe Desemba 21 na siku fupi zaidi ya zote ni Juni 21. Siku zinazoangukia robo ya mwaka zinakuwa ni kati ya siku ya usiku mrefu zaidi maarufu kama solstice na kila cha ikwinoksi.

 

Ikwinoksi ya Majira ya Baridi ya March 21 na Maadhimisho ya Ostra/ Easter

Ni kama lilivyofanywa jaribio la kuibadili siku ya Sabato na kuwa Jumapili, baadhi ya watu walijaribu kuibadili Pasaka na kuiadhimisha Easter. Kwa kweli, jaribio la kuibadili siku ya Sabato kuwa Jumapili lilifanyika kutokana na imani  na taratibu za zamani za kipagani, ambayo iliendana au kuhitinishwa na maadhimisho ya Easter. Easter ni sikukuu ya kipagani ya mungu Ishtar au Ashtorethi. Mungu mke huyu alikuwa na majina mengi sana mbalimbali kokote kule duniani. Baadhi ya majina yake ni: Cybele, Shingmoo, Isis, Diana, Nuria, Vensus, Nana, na Disa. Kwenye Kiingereza cha Zamani, alijulikana kwa jina Easter, na hapa ndipo jina la Kiingereza la sikukuu hii lilitokana kwayo.

 

Sungura wa  Easter ilikuwa ni takatifu kwa mungu mke huyu na kuangua mayai ya watoto wema. Easter inaashiria maisha mapya na alama yake ni sungura wengi, mayai na vinginevyo. Ni wazi kabisa kwamba Biblia haisemi wala kutuamuru sisi tuiadhimishe sikukuu hii ya Easter. Baadhi ya watu wamekwenda mbali kiasi cha hata kubadili maandiko fulani ya Biblia kwa kujaribu kuwashawishi watu kuiadhimisha sikukuu hii ya Easter. Kwenye Biblia ya Kiingereza Tafsiri ya Mfalme Yakobo maarufu kama the English King James Version of the Bible (KJV), Matendo 12:4 imeandikwa kimakosa na upotoshaji wa makusudi kwa kuliandika neno "Easter". Mtu akiangalia na kulinganisha na tafsiri nyingine kama vile ya Revised Standard Version (RSV) au nyinginezo zilizotafsiriwa kiusahihi unaweza kuipata maana halisi ya neno liliortumiwa.

 

Visingizio vya kusema kwamba eti Kristo alifufuka kutoka kwa wafu siku ya Jumapili alfajiri ni jitihada tu za kurudisha upya mapokeo ambayo kwamba makuhani wa Easter walikuwa wanafanya ibada ya kuliabudu jua siku hiyo. Desturi ya kuila nyama ya paja la nguruwe wa Easter inaonekana kutokana na viumbe wa zamakale ambaye alikuja kuwa ni mungu Tammuzi, ambaye aliuawa na dume la nguruwe pori, ambaye ni nguruwe. Mungu anatuambia nguruwe ni mnyama najisi kwetu na tusimle. Tafadhali soma ba kujifunza zaidi kwenye jarida la Sheria ya Vyakula ya Biblia (Na. CB18 [The Biblical Food Laws (No. CB19)].

 

Attis alikuwa mungu mwingine aliyekuwa na mfanano mkubwa na Kristo. Kulizuliwa uzushi kwamba Attis alizaliwa pasipo kuwa na Baba, na kwamba alikuja kuwakomboa watu wake, alisulibiwa kwenye mti wa msonobari, akazikwa na kufufuka siku ya 3 toka kwa wafu.  Kifo cha Arris hapo zamani kilisherehekewa tarehe 25 Machi. Kwa kweli walikuwa na maadhimisho ya juma zima yaliyoitwa Hilaria (kwa mujibu wa Barbara Walker, The Woman’s Encyclopedia of Myths and Secrets, New York: Harper Collins, 1983, pp.267, 268, 403). Maadhimisho haya yalibadilishwa na kuitwa maombolezo ya mateso ya kusulibiwa ya Ijumaa hadi ufufuo wa Jumapili, shamrashamra zilizopamba moto sana na tunazozijua siku hizi na ambayo yamepewa jina la uwongo la Ukristo.

 

Kipindi cha Lenti

Kwa imani ya Makanisa Makongwe, kipindi kinachojulikana kama Lenti kinaanzia siku wanayopakazwa Majivu kwa imani ya kidini ya Jumatano hadi mwishoni mwa maadhimisho ya Easter siku ya Jumapili. Kipindi hiki cha Lent kinamaanisha siku 40 za kujitafakari kwa maandalizi ya Easter. Watu wengi wanaiadhimisha Lenti kwa kufunga, kutoa sadaka, kujinyima kula baadhi ya vyakula na kujinyima na kiburudisho, nk.

 

Hata hivyo, wale wanaoifuata Kalenda ya kweli ya Mungu wanajua kwamba maadhimisho haya ya Lenti ni upotoshaji unaokusudia kufunika maandalizi ya Mwezi wa Kwanza (Abibu) kipindi tunachojiandaa na kuiadhimisha Pasaka kwa mujibu wa Torati ya Mungu. Imani ya kipagani iliichukua hii kama ilivyofanya kwa Easter pamoja na sikukuu nyingine nyingi \zilizoanzishwa na wanadamu.

 

Mardi Gras

Haya ni maadhimisho yanayofanyika kwa mapambo ya rangi yanayofanyika Jumanne inayotangulia Maombolezo ya Kwaresma, siku inategemeana na tarehe itakayoadhimishwa Easter. Maadhimisho yanafantika mwishoni mwa sherehe ndefu ya inayoanzia tarehe 6 Januari au Usiku wa Ishirini. Mardi Gras ni neno la Kifaransa ambalo maana yake ni Jumanne Nene. Neno hili linatokana desturi ya kumswaga ng\ombe dume kwenye mitaa ya mjini Paris siku ya Jumanne inayotuatia Kwaresma.

 

Sherehe hizi za Mardi Gras yanaenda hadi nyuma kwenye desturi za zama za Warumi wa kale za kufunga ndoa kabla ya kipindi cha kufunga saumu. (kwa mujibu wa jarida la World Book Encyclopedia, 1989 Ed.)

 

Jumatano ya Majivu

Maadhimisho haya ya Jumatano ya Majivu yanayofanywa na makanisa kale makongwe, kunakuwa na majivu ambayo waumini wake wanapakwa kwenye vipaji vya nyuso zao na makasisi wao au wahudumu waliochaguliwa kufanya kazi hiyo. Wanavyos3ema wenyewe ni kwamba ibada na tendo hili vinalenga kuwawakumbusha waumini wao kuwa maisha yao hapa duniani ni mafupi na umuhimu wa wao kujindaa kwa kifo kinachokwenda kuwafuatia.

 

Lakini ibada hii haitokani na mapokeo wala imani ya Kanisa la kwanza bali chanzo chake kinatokana na imani za kipagani iliyochukuliwa na kuingizwa pamoja na maadhimisho ya Easter katika karne ya pili. Maadhimisho au ibada hii ya Jumatano ya Majivu haina uhusiano wowote na maagizo ya kwenye Biblia. Mwanzoni kabisa Jumatano hii ya Majivu ilikuwa ni siku ya kumuombolezea mungu aliyekufa na kifo cha kuteswa kipindi hiki cha pilikapilika za sikukuu. Ni wakati walipokuwa wanachoma matawi ya mitende ndipo hapo ndipo majivu haya yalipotokea.

 

Siku ya Wajinga ya mwezi Aprili

Sherehe za Hilaria ziliishia mwezi Aprili tarehe 1. Siku hii watu walienda huku na huko waliwa na hali ya kujibadili mwonekano wao na kwa ujumla watu wangeweza kusema au walifanya kitu chochote walichotamani kukifanya (ibid., pp.79,403).

 

Siku ya Mei 1 au ya Belatine/ Mei Dei

Huko Ujerumani, siku hii ilijulikana kama Walpurgisnacht, huko Ireland na Scotland ilijulikana kama Beltaine au Baltein, siku ambayo mungu Baali, Beli au Balder alipochomwa moto na kuteketezwa sanamu yake. Wakati mwingine siku hii iliadhimishwa kwa mtu kuchaguliwa na kukatwa na kutupwa achomwe moto mahali palipokuwa panaitwa tanuru la tita la Baler kwenye maeneo ya mashambani ya nchi za Scandinavia (ibid., pp. 624-626). Wengi wa wasomaji wangu mnakumbuka kuhusu alivyotajwa Baali kwenye Maandiko Matakatifu.

 

Zamani sana hata Israeli walimtumikia huyu Baali. "Wakaziacha amri zote za Bwana, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali." (2Wafalme 17:16). Soma pia Waamuzi 2:13.

 

Lakini Mungu alimwambia nini nabii Eliya? "Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali" (Warumi 11:4). Sisi pia tunapaswa kuwa ni miongoni mwa hao waliobakia kuwa waaminifu kwa Mungu wa Pekee na wa Kweli na tusiojitoa kuiabudu miungu mingine wala kuitumikia.

 

Hiki ndicho kipindi ambacho mungu mke wa uchawi na ushirikina alikuwa anafikia kilele chake cha uweza wake wote. Mabiwi makubwa yaliwashwa ili kumkaribisha huyu mungu mke. Nabii Yeremia anatuambia kwamba wakati mwingine mioto hii iliwashwa kwa minajiri ya kutolea kafara za watu, “nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu" (Yeremia 19:5). Tunajua kwa wazi kabisa kwamba hii haikuwa Kanuni wala maagizo ya Mungu wala sio napenzi yake.

 

Uchezaji wa Mziki unaojulikana kama Maypole ni alama iliyoashiria alama ya urutubisho na ngoma. Ngoma hii ilichezwa kwa kipindi kirefu kwa kuingiliana wachezaji wakiashiriana mambo maovu. Mziki au ngoma hii ya Maypole ilitokana na wachezaji waliojipangwa sawasawa Upande wa Kuume na Kushoto, ambako wanaume na wanawake walipita katikati na kutoka kwenda kwenye duara walizozifanya huku walipeperusha vitambaa juu walivyovifunga kwenye vinara vidogovidogo (Walker, ibid., pp. 25,26).

 

Solstaisi ya majira ya hari ya Juni 21 au Litha ya Majira ya Katikati ya hari

Sherehe ya solstaisi ya majira ya hari ilikuwa kama ya ikwinoksi za majira ya machipuko. Matita ya nyasi yalichomwa usiku kucha ili kulitia moyo jua lirudi. Kulikuwa na michezo ya mashambani na iliyopangiliwa kwa mistari.

 

Siku ya Uhuru ya Julai 4 huko Marekani

Hii ni siku nyingine ya utoaji kafara kwa kalenda ya kipagani. Ilipelekwa kwenye siku hii ya tarehe 4 Julai ili ikidhi matakwa ya kalenda ya wachawi au washirikina wa kale waliojulikana kama Wiccan, ambayo ilikuwa ni siku ya kutoa kafara za watu au wanadamu.

 

Siku ya August 1 ya Lughnasad / Lammas

Lammas maana yake ni Sikukuu ya Mikate. Lilikuwa ni jina la Mkristo la mpagani Lugnasad, Mceltiki "Michezo ya Lug" (ibid., pp. 556-556). Lug alikuwa mungu wa nafaka aliyetolewa kafara na kufufuka ili ampe heshima heshima Mama wa Mavuno mwanzoni mwa mwezi August.

 

Ikwiniks ya Majira ya Hari au Mabon ya Septemb 21

Hii ni siki nyingine ya kipagani ya uroaji wa kafara iliyokuwa kwenye kalenda ya kipagani.

 

Halloween ya Octoba 31 – Siku ya Roho Zote ya Novemba 1

Halloween au Siku ya Mazimwi ilikuwa ni ile iliyokuwa inaitwa kwenye nakala za Wakristo wa Damhain kuwa ni sikukuu ya madhehebu ya Kiceltiki na ni sikukuu ya wafu. Iliitwa na Aryan Lord kuwa ni ya Wafu. Wazo la wapagani lilitaka kuifanya kuwa ni ya kipindi fulani maalumu tu cha majira ya "mavunjiko" iliyofunguliwa ya majira ya frabic yaliyo kati ya “ulimwengu wa wafu na mazimwi” na ulimwengu wa walio hai (ibid., pp. 371-372). Tunajua kutokana na Maandiko Matakatifu kwamba sehemu walioko wafu ni pale wanapolala (Mathayo 9:24; Luuka 8:52); na kwamba hakuna wanachokijua (Mhubiri 9:5); na kwamba wako kimwa (Zaburi 115:17); na kwamba wako gizani (Zaburi 143:3). Hapo kale sana, watu wengi waliamini kuwa roho haifi. Hii ilimaanisha kuwa wangeishi milele wakiwa kwenye mwili wa kiroho (mizimu). Hata sasa bado watu wanaamini uwongo huu. Alama kama za kunguru, popo nap aka ni ishara zinazofafa na maroho haya.

 

Siku ya utoaji shukurani

Alama ya pembe yenye kumwaga tunu, inayoonekana kwenye wazi kwenye maadhumisho haya ya Siku ya utoaji shukurani huko Marekani, ilikuwa hapo kwanza inaashishia pembe ya Mama Mkuu akiwa kwenye umbo lake la ng’ome au la mbuzi. Majina yake yalikuwa ni Io, Ceres, Hera, na Hathor. Waliamini kwamba kila jambo jema lilitokea kwenye pembe yale tukufu, ambayo ilikuwa ni ishara ya maombi aliyokuwa anaombwa huyu mungu mke. Cornucopias bado wanaonekana mara kwa mara kama mapambo ingawa watu wengi hawajui maana yake ya kipagani na kwamba hii ni sikukuu takatifu ya dini ya kipagani (ibid., p. 90). Siku asilia iliyokuwa imewekwa kusherehekea siku hii ya Utoaji shukurani ilibadilishwa na kupangiwa siku hii kwa

kukidhi sababu za kipagani na dini inayoendesha mambo kisirisiri ya Wamarekani tangu zamani.

 

Krismas  

Biblia haituambii wala kutuamuru kuiadhimisha sikukuu yoyote katika mwezi wa 11 au mwezi Desemba. Lakini kwa mara nyingine tena, Shetani aliingiza sikukuu hii ya kipagani iliyojulikana hapo mwanzoni kama Saturnalia, na kuiunganisha kwa kisingizio kinachodaiwa kuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Kristo na hadithi za Santa Claus. Soma jarida la Sababu Zinazotufanya Tusisherehekee Krismas (Na. CB24) [Why we don’t celebrate Christmas (No. CB24)].

 

Kuna taratibu nyingi za kidini ya kipagani zilizofungamanishwa kwenye kajira haya ya solstaisi ya majira ya baridi iliyoanzishwa kipindi cha maelfu ya miaka iliyopita.

 

Sikukuu ya Mwaka Mpya

Kwenye kalenda ya kale ya Warumi, Mwaka Mpya ulikuwa unaanzia siku iliyojulikana kama Ides, ambayo ni katikati ya mwezi ya Machi. Kwa ujumla siku hii iliaminiwa kuwa ni siku ya kufanya sherehe au tafrija mbalimbaloi za maporini na kunywa na kulewa bila mipaka kwa kuwa walikuwa wanausherehekea ujio wa Mwaka Mpya ambao kwamba ungeweza kuwasamehe makosa na dhambi zao zote walizozifanya huko nyuma. Hadi siku hizi huko Ulaya, kipindi cha kabla ya Lenti kinaadhimishwa kama cha tafrija za maporini kutenda dhambi na maovu yote mbalimbali. Baada ya kubadilika kwa kalenda ya Warumi, Siku hii ya Mwaka Mpya ilisherehekewa baada ya solstice ya majira ya baridi na inaangakia kipindi cha mungu Januas. Janus alikuwa ni mungu aliyekuwa na vipaji viwili vya uso au sura mbili, moja iliangalia mbele na nyingine myuma na hakuwa na kisogo. Walimtukuza kama Mama wa Majira na Nyakati, aliyekuwa anatawala Vitu vya Kimbinguni akiukinga na kuuzuia Upepo unaotokea pande za Kaskazini ambao watu walikuwa wanauogopa (ibid., p. 208).

 

Februari 1: Siku ya Imbolg/ya Kuwasha Mishumaa/ Siku ya Ground hog

Hapo kale, siku hii ya Kuwasha Mishumaa ilikuwa inaadhimishwa na Warumi ikilenga kumtukuza mungu Juno Februata waliyemuita kuwa ni mwanakme bikira wa Mars. Waumini wa dini hii ya kipagani walikwenda kuhiji mjini Roma ambako waliuzunguka wakiwa wamebeba mishumaa mikononi mwao wakimuomba na kumtukuza mungu Februa. Waceltiki walimuita Imblog, lakini ni huyuhuyu (ibid., p. 171).

 

Tabia za wanyama zilichukuliwa kama dalili njema au ishara ya hali ya hewa (Sam Epstein, Spring Holidays, Champaign, Illinois. 1964, pp. 5-11). Kwa hiyo yale maadhimisho ya siku ya nguruwe pori, yanayoadhimishwa Marekani yanamaanisha sherehe hii na chanzo chake ni ya kipagani.

 

Siku ya Valentine, February 14

St. Valentine alichukuliwa kama ni kiranja wa wapendanao, desturi iliyounganishwa na imani ya kale iliyotiliwa chumvi kwamba pia kuna ndege wanaoruka kwa kufuatana wawiliwawili siku hii ya Februari 14. Au iliweza kuunganishwa na sherehe ya kipagani ya mungu wa urutubisho, Lupercalia. Hii ilikuwa ni sherehe ambayo wanaume vijana waliwachagua wachumba wanawake kwa kuandika majina yao na kuwaahidi kushirikiana nao kingono na mambo mengineyo yote (kwa mujibu wa kamusi ya Oxford Australian Reference Dictionary).

 

Siku ya Mtakatifu Patrick

Kila tarehe 17 Machi ilikuwa inahusishwa na wa Leprechauns ambao walikuwa ni watoto wanavaa nguo za kijani na ambao walisababiha matatizo. Kijani inaashiria rangi asilia. Washillelagn au Washillelagh walikuwa ni watumishi au wanachama wenye sauti kwenye kundi la wabuni mambo yanayotumiwa na watu lakini yenye maana za kisiri maarufu kama Occult. Ilijulikana pia kama fimbo yenye manyoya, pembe ya mnyama wa ajabu mwenye umbo la farasi ainayeitwa unicorn, Pembe ya Moloch na Pembe ya Wataliano. Sufuria au majungu makubwa yalitumika na wachawi kwa jinsi zilivyotengenezwa na zinavyoashiria kwa Baraka za kifedha za Moloch.

 

Maadhimisho ya siki ya kuzaliwa

Maandiko Matakatifu yanasema kwamba siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa (Mhubiri 7:1). Hakuna mahali kwenye Biblia paliposema wala kuagiza watu kusherehekea siku ya kuzaliwa. Na kwa kweli, mifano iliyoko kwenye Biblia inaonyesha kwamba haturuhusiwi kuadhimisha siku za kuzaliwa (Mwanzo 40:20; Ayubu 1:4; Mathayo 14:6; Marko 6:21). Biblia ya Shetani imeorodhesha ikionyesha kwamba siku mtu anaposherehekea kuzaliwa kwake anapanda daraja na kuwa kama mungu mdogo. Ingawa tunaweza kuwa waumini tuliohesabiwa kwenye Familia ya Mungu, tujua kwamba hatu wezi kabisa kuwa mingu sawa na Mungu kwa kuwa Mungu ni Mungu tu. Kitendo hiki cha kusherehekea siku ya kuzaliwa ni mojawapo ya uwongo mwingine alioutunga Shetani unaokusudia kumkufuru Muumba wetu.

 

Tendo linguine linalofanyika sambamba na sherehe hii ya kuzaliwa ni kuwekwa kwa kitu kinachoitwa Piñata. Hii pia inatokana na asili ya kipagani na hatupaswi kuwa matendo kama haya. Hapo mwanzoni kabisa, hii Piñata ilitengenezwa kwa umbo la nguva jike, ingawa haitengenezwi kila mara kwa umbo hili la nguva jike siku hizi. Wakati mwingine inatengenezwa na nyota inayoonekan kwa namna sita mbalimbali. Nyota hii inayomwakikisha mungu inatokana na chanzo kilekile walichomchukulia huyu nguva jike. Hii ni miungu ya kipagani.

 

Nguva jike alipingwa kwa fimbo ili kumvunja Piñata au kifurushi cha mbegu, ambacho alikuwa nacho, ili kuzifanya mbegu zimwagike chini ya Ardhi na ndipo ziweze kuota. Na ndiyo sababu Piñata inamseto wa pipi/peremende zinazoashiria mbegu.

 

Katika siku za kale, waliweka ngozi ya mwandamu na kuipiga. Mara nyingi sherehe hizi ziliendana na utoaji wa kafara za wanadamu.

 

Siku ya Wamama na ya Wababa

Dini inayosisitiza usawa wa kijinsia kwa Wamama na Wababa na kufana maadhimisho kwa kutenga siku maalumu za watu hawa ilianziishwa na Warumi. Ni miongoni mwa dini zinazoadhimisha mambo ya urutubisho, ambayo iliwakilishwa na imani ya Utatu. Mungu wa Utatu wa Warumi alikuwa kwenye muunganiko wa Utatu na Jupita ambaye alikuwa anaashiiwa kwa umbo la mwanaume mwenye uzazi mwingi aliyeonekana kwa ishara ya Genii, au muunganiko wa watu wenye akili nyingi wa Dola ya Rumi. Mungu mke Juno alionekana kwa umbo la mwanamke mzazi. Kitu cha tatu kilikuwa ni kile Kisule kinachoonekana kimezunguka kichwa kwa juu kilichotokana na imani ya watu wa Mashariki na kimewezesha kuleta ushawishi kwa mungu mke alikuwa bikira aliyeonekana kuungana na miungu wengine wawili walio kwenye muundo huu wa kiutatu. Imani hii inawakilisha nguvu au uweza wa kiroho alionao Lusifeli. Na hii ndiyo sababu inayofanya kuwekwe madoli ya kike yenye mabawa kwenye miti ya Krismas

 

Siku hizi za Wamama na Wababa za siku hizi zinatofautiana kutoka taifa moja hadi lingine. Sehemu kubwa ya maadhimisho haya yanafanyika kibiashara, bali baadhi yake yanaendana sawa na chanzo chake asilia cha upagani uliokuwa kwenye dini za kale kabisa.

 

Hitimisho  

Kuna sikukuu nyingine nyingi ambazo hatupaswi sisi kuziadhimisha. Kama tukiwa hatuna hakika na sababu za maadhimisho ya siku au sikuu yoyote ile, basi na tuwaulize wazazi wetu watuambia maana hasa ya maadhimisho ya siku ile ili tuone na kuamua iwapo kama haina madhara yoyote kwetu kuziadhimisha.

 

Kumbuka kuwa tunapokuwa na hata mzazi mmoja tu aliyeamini na kubatizwa na anamwamini Mungu wa Pekee na wa Kweli, basi watoto wote tunatakaswa, au tunatengwa mbali na maasi ya dunia (1Wakorintho 7:14). Kile wanachotufundisha wazazi wetu walioamini au wanachotuambia na kutuadibisha kwa mujibu wa Biblia ndicho kitakachotulinda dhidi ya yale tunayofundishwa na dunia.

 

Tunapaswa kijiepusha kujifunza njia za mataifa.

Yeremia 10:2 Bwana asema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni; maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo. 

 

Ni jukumu letu kumfundisha kila mmoja wetu ajifunze kumcha na kumuabudu Mungu kwa usahihi zaidi na kwa kila mara yale tunayojifunza na kuyaamini husuan juu ya Siku zake Takatifu zilizoamriwa na kwa nyakati zake za kuziadhimisha. Soma jarida la Siku Takatifu za Mungu (Na. CB22) [The Holy Days of God (No. CB22)].