Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[CB28]
Jeshi la Mbinguni
(Nakala 1.0
20060715-20060715)
Mungu Mmoja wa kweli (Eloah) akawa Baba hapo alipoumba Wana wake wa Kiroho. Katika Somo hili tutaangalia kwa kifupi vyeo na kazi za asili ya Uumbaji wa Ulimwengu wa Kiroho.
Familia ya Mungu.
Christian Churches of God
PO Box 369,
WODEN ACT 2606, AUSTRALIA
Email: secretary@ccg.org
(Haki
milki © 2006, Makanisa ya Kikristo ya Mungu, ed. Wade Cox)
Somo hili linaruhusiwa kunukuliwa, na kusambazwa kwa yeyote mradi tu kama litanukuliwa kikamilifu, bila kubadilishwa au kuondoa namna halisi, Jina la Mchapishaji na anuani yake na tangazo la hati milki lazima vijumlishwe. Hakuna gharama yoyote ipaswayo kuchangiwa na mtumiaji na hairuhusiwi kuuzwa nakala zake kwa msomaji. Nukuu chache zaweza kuchukukuliwa katika makala zinazo tofautiana kimtazamo na kimaoni bila kukiuka maadili ya haki milki.
Somo hili linapatikana pia katika Tovuti zetu popote
Duniani
http://www.logon.org
na http://www.ccg.org
Jeshi la Mbinguni
Biblia
inatufundisha ya kwamba Mungu Mmoja wa kweli ni Mungu asiyeonekana kwa macho,
na hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote au kusikia sauti yake (Yn. 1:18;
5:37). Mungu (Eloah) ana uzima nafsini mwake. Kwa hiyo hakuhitaji kuthibitika
kwa kuonekana, maana Uzima hutoka kwake. Uzima pekee ni jambo la kushuhudia ya
kwamba Mungu Yuko na yu Hai, na ni uzima wa milele, maana kitu ambacho si hai
hakiwezi kutoa uhai. Uhai ni uzima utokao, mahali pale tu palipo na Uhai, na
Uzima. Hivyo Mungu ni Uzima, tena ni Uhai maana vyote hivi vinamshuhudia Yeye,
na vyote vyatoka Kwake (Yn. 5:26; 1Tim. 6:16). Daima alikuwako, na Daima
atakuwako, na Daima Yuko wakati wote. Mungu aliyeko na Aliyekuwako na
Atakayekuja, Mwenyezi. Kuna wakati Mungu alikuwa peke yake, lakini aliamua
kuzaa Familia kwa ajili yake Mwenyewe. Angalia Somo la Mungu ni Nani? (Na. CB1).
Kitu cha
kwanza kabisa kutoka kwa Mungu na ambacho yeye Mwenyewe alitoa kutoka kwake
alikuwa ni Roho Mtakatifu. Katika Roho Mtakatifu Uumbaji wote uliofuata baadaye
ukifungamana kwa Mungu kwa sababu hakuna chochote kilichofanyika pasipo Roho
Mtakatifu wa Mungu, na Roho Mtakatifu alitoka kwa Mungu. (Roho ndiyo itiayo
uzima, ni Roho tena ni Uzima. Kutoka hapo Mungu alizaa (aliumba) Wana wa Kiroho
katika uwezo wa Roho Mtakatifu na wote waliungana na Mungu katika Roho
Mtakatifu, na waliweza kutenda kazi sawasawa na Mapenzi ya Mungu kwa maana
waliongozwa na Roho Mtakatifu ambaye ni Roho wa Mungu aliyetoka kwa Mungu.
Ilikuwa ndiyo sababu ya Mungu kuwa Baba wa Wana wa Kiroho maana amezaa Wana
kwaa njia ya Roho mtakatifu (Ebr.12:9). Angalia Somo la Roho Mtakatifu ni nini? (Na.
CB3).
Hawa ni
Wana wa Mungu aliye Juu sana wote wanaitwa elohim (kutoka Zab. 82:1) kwa ngazi
za utendaji tofauti tofauti. Waliumbwa Wakamilifu, na kwa kuendelea kumtii
Mungu (Eloah). Na wataendelea kuishi milele kama Wana wa Kiroho wa Mungu.
Malaika ni nani au ni wa namna gani?
Malaika
ni wajumbe wa Mungu wanaotumwa kutenda kazi za Mungu. Wana wa Kiroho wa Mungu
hawakuitwa malaika mpaka baada ya Uumbaji wa Adamu. Kwa sababu kabla ya Adamu,
hakuna yeyote aliyehitaji kupelekewa ujumbe, kwa hiyo hapakuwa na sababu ya
kuwapo kwa wajumbe ambao ni Malaika.
Malaika
waliumbwa katika Roho na ni Roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale
watakaourithi Wokovu (Ebr. 1:14). Mungu aliwaumba Wana wake wa Kiroho kabla ya
Uumbaji wa nchi (Ayubu 38:4-7). Kuna zaidi ya malaika milioni 100 (Angalia Dan.
7:9-10; Mt. 26:53; Lk 2:13; Ebr. 12:22; Ufu. 5:11). Malaika wameumbwa katika
hali ya mmoja mmoja (individuals) ambao wana uhuru wa kuchagua, ambao ndiyo
unahitajika katika kukua kwa tabia.
Neno la
Kiebrania, mjumbe (messenger) katika Agano la Kale ni Malaika na linatafsiriwa
kama Malaika (angel) katika Biblia za Kingereza. Neno linatumika katika
kuonyesha wajumbe wa Kiroho waiotumiwa na Mungu. (Mwa. 32:1-2) na pia
lilitumika kwa wajumbe wanadamu waliotumwa na Yakobo (Mwa.32:3).
Katika
Agano Jipya, neno la Kigriki, mjumbe (messenger) ni aggelos, ambapo tunapata
neno katika kiingereza angel yaani malaika, au mjumbe. Neno hili pia linatumika
katika sehemu zote katika wajumbe wa kibinadamu na wajumbe wa Kiroho.
Mungu
alituma wajumbe mbalimbali. Kwanza kulikuwa na wajumbe wa manabii na wa
wanadamu (2 Nya. 36:15-16). Pili, kulikuwa pia na wajumbe wa Kiroho (malaika)
waliotumwa na Mungu kwenda kwa wanadamu kwa madhmuni ya kupeleka ujumbe maalumu
au kwa madhumuni ya kutenda kazi.
Kama
mawakili wa Mungu walitumwa duniani kutoka mbinguni, kuchukua au kuleta maamuzi
ya Mungu, juu ya wanadamu katika kutimiza adhabu ya Mungu kwa wanadamu, na
katika kuwafundisha wanadamu (kut.12:23; Zab. 104:4; 2 Sam. 24:16; 2 Fal.
19:35; 1 Nya. 21:16; Matendo 12:23; Ebr. 11:28; 1 Kor. 10:10).
Malaika
pia walichukua ujumbe wa Mungu kuwapelekea manabii wa Mungu na kuwalinda watu
wa Mungu (Zab. 34:7; 91:11; Dan. 6:22; Mt. 18:10; Ebr. 1:14). Malaika
walioonekana kwa wanadamu daima walikuwa katika umbo la kibinadamu (Mwa. 18:2;
19:1,10; Lk.24:4; Mdo. 1:10).
Wana wa
Kiroho wa Mungu pia wanatofautiana katika ngazi na katika uwezo wa utendaji,
(Zek. 1:9,11; Dan. 10:13; 12:1; Efe. 1:21; Kol. 1:16; 1 The. 4:16; Yuda 1:9).
Malaika wamepewa uwezo na nguvu ya utendaji (2 The.1:7); “wanaitwa wenye nguvu
na uwezo mwingi” (Zab.103:20). Ni “Watakatifu” (Lk 9:26), ni “Wateule” (1 Tim. 5:21).
Hawasitahili kuabudiwa au kusujudiwa (Kol 2:18; Ufu. 19:10).
Malaika
wengine wana mabawa na wengine wanafanana kama sanamu wakiwa na sura za nyuso
mbili, ambapo uso mwingine unaweza kuwa ni uso unaofanana na nyuso za wanyama
na uso mwingine unaofanana na wanadamu. (Eze. 1:4-14; Isa. 6:1-3) wanaweza
kubadilika katika maumbile yao na kufanana na maumbile ya kibinadamu
wanapoonekana kwa wanadamu (Ebr. 13:2). Wakati wote wana miili ya kung’aa na
wanavaa mavazi meupe (Mdo 1:9-11; 22:6-9; 2 Sam 22:13).
Wanadamu
hawaruhusiwi kumwona Mungu, kwa hiyo Malaika wanawasaidia wanadamu katika
kumjua Mungu Mmoja wa kweli, (Eloah).
Malaika katika Agano la Kale
Mjumbe
muhimu anayetumwa na Mungu anayeitwa “Malaika wa Bwana”, au “Malaika wa Mungu”
katika Biblia za Kingereza. Majina haya yenye vyeo hivi huitwa Malaika Maalumu
(au wajumbe) ambao wanamwakilisha Mungu. Alikuwa mara kwa mara anaitwa Yehova.
Watu wa
Agano la Kale walimtambua huyu Mjumbe au Malaika aliyetoka kwa Mungu kuwa
hakuwa Mungu Mmoja wa kweli. Walijua ya kwamba Mungu (Eloah) alijifunuwa na
kujidhihirisha kwao kwa kupitia kwa hao malaika wa Mungu, ambaye pia walimwita
Elohim. Wakati malaika wa Yehova alikuwa pamoja nao, ilimaanisha ya kwamba
Mungu (Eloah) alikuwa yuko pia pamoja nao. Malaika alisema na kutenda kwa niaba
ya Mungu Mmoja wa kweli.
Malaika
wa Yehova ambaye mara kwa mara alishughulika na wanadamu, alikuwa ni mungu
(god) wa Waisraeli (k.m. Elohim). Alimwakilisha (Eloah), Mungu Mmoja wa kweli
ambaye Waisraeli walimwabudu. Huyu Malaika wa Yehova, aliyeshughulika na
wandamu ndiye yeye ambaye baadaye alijidhihirisha, na kuwa mwanadamu Yesu
Kristo. Tazama katika Somo la Yesu ni
nani? (Na. CB2).
Hebu
tuangalie matukio mengine mengi, ambayo Malaika huyu, alionekana na kuzungumza
na wanadamu katika nyakati za zamani.
• Malaika
alizungumza na Hajiri mara mbili (Mwa. 16:7-13; 21:17-18)
• Malaika
alizungumza na Ibrahim (Mwa. 12:1-3; 22:11-18).
• Malaika
alizungumza na Yakobo katika ndoto (Mwa. 28:11-21; na 31:11-13; Angalia pia
Mwa. 32:24-30).
• Malaika
alimtokea na kuzungumza na Musa (Kut 3:1-6; 24:12-16).
• Malaika
katika mawingu (kut. 13:21; 14:24)
• Malaika
akiwa kama mhifadhi, Mlinzi na Mwokoaji (zab. 34:7; 35:5-6).
Biblia
inasema alikuwa ni Malaika wa Yehova, ambaye ni Yesu Kristo, ndiye aliyetenda
haya yote (Mdo. 7:30-38, 53; Gal. 3:19).
Mtume
Paulo alisema ya kwamba alikuwa ni Kristo ambaye, ndiye aliyewavusha wana wa
Israel katika bahari (1 Kor. 10:1-4). Paulo pia anamtambulisaha Malaika wa
Mungu kama Yesu Kristo katika Wagalatia 4:14. Tazama somo la Malaika wa
Yehova (CB24).
Matukio
mengine ambayo Malaika aliwatokea Wanadamu;
• Baalamu
na Malaika (Hes. 22:22-35)
• Yoshua
na Malaika (Yos. 5:15)
• Gidioni
na Malaika (Amu. 6:12-24)
• Wazazi
wa Samsoni na Malaika (Amu. 13:2-20)
• Daudi
na Malaika (2 Sam. 24:16-17)
• Eliya
na Malaika (1 Fal. 19:5-12 na 2 Fal. 1:15)
• Malaika
na Daniel (Dan. 3:24-25, 28)
• Malaika
na Zekaria (Zek. 1:9,13-14,18-21; 2:3; 4:1,4-5; 5:5,10)
Malaika katika Agano Jipya:
Tunaona
ya kwamba Malaika walimhudumia Yesu wakati alipokuwa katika nchi (duniani) (Mt.
4:11, Lk. 22:43). Malaika alimtokea Yusufu na kumwarifu habari za kuzaliwa
kwake Yesu (Mt. 1:20, Lk 1:26-38). Malaika walikuwepo katika ufufuo wa Yesu (Mt
28:2-8; Yn. 20:12). Na walizungumzia wakati wa kupaa kwakeYesu Kristo (Mdo
1:9-11). Malaika wanatoa huduma za
Kiroho kwa watu wa Mungu (Ebr. 1:14;
Mt. 18:10; Mdo 5:19; 8:26; 10:3; 12:7; 27:23).
Malaika hufurahi mwenye dhambi anapotubu (Lk. 15:10).
Katika
Agano Jipya, Kristo kama mwanadamu bado alitenda kama mtu aliye mdhihirisha na kumfunua Mungu. Na alitenda
kwa ukamilifu akifuata asili ya Mungu na tabia ya Mungu. Kama Mpatanishi kati
ya Mungu na Wanadamu, kumwona Yesu ni sawa na kumwona Mungu, na kusikia na
kumtii Yesu ni kumsikia na kutii Mungu (Eloah). Maneno aliyozungumza hayakuwa
maneno yake mwenyewe bali maneno ya Mungu yaliyotoka kwa Mungu. (Yn. 14:8-10)
Vyeo mbalimbali vya Jeshi la Mbinguni
Malaika
wana vyeo, uwezo na nguvu zinazotofautiana katika utendaji wa kazi
mbalimbali. (Zek. 1:7-11; Dan.10:13; 12:1;
1The. 4:16; Yuda 1:9; Efe. 1:22; Kol 1:16).
Enzi Utawala, Nguvu, Mamlaka,
Tunajua
ya kwamba Kristo alikuwa ni mzaliwa wa kwanza katika uumbaji, ambapo baada ya
hapo Mungu hakuumba Wana wake wengine bali katika Yesu Kristo aliumba (k.m. alitengeneza) enzi,
utawala (ufalme) mamlaka na Serikali.
Hizi ni katika mambo ya utawala wa kimwili na sio katika mambo ya utawala wa
Kiroho. Lakini vyote vyatokana katika Kristo (Kol.1:16-17 ).
Maserafi:
Kuna
maserafi na wana mabawa sita (angalia Isa. 6:2,6). Wana nguvu uwezo wa kuondoa
makosa yaletayo dhambi na kuwandaa manabii kwa kuwatakasa (Isa. 6:7).Kuwa na
mabawa sita inadhihirisha ukuu na uwezo
wao katika katika utendaji wao wa kazi mbalimbali.
Neno
maserafi ni neno la wingi wa neno saraph (SHD 8314) likiwa na maana ya mwenye kuchoma kwa moto. Kwa sababu ya nyoka
katika Hesabu 21:6,8 walikuwa na sumu inayochoma kama moto wakati wanapouma,
kwa hiyo wakaitwa maserafi. Kwa hiyo hawa maserafi ni “nyoka wa moto wa
mbinguni” (linganisha pia Kum. 8:15; Isa. 14:29; 30:6). Mungu aliwatuma
ili waweze kuwadhibu watu waliotenda dhambi. Maumbile yao walionekana kuwa kama
wandamu kwa vile walikuwa na nyuso, mikono na miguu juu ya umbile lao la kuwa
na mabawa. Wanawakilishwa kama wenye “kusimama wakati wote” juu ya wote. Mfalme
anaposimamisha enzi yake, tayari kwa kumhudumia.
Hawa
ndiyo Malaika Wakuu na wana nafasi muhimu sana katika Jeshi la mbinguni. Ni
Malaika wakuu ndiyo mara nyingi hutumwa katika nchi kuleta ujumbe wa Mungu na
maonyo kwa wanadamu na kwa manabii.
Katika kitabu cha Henoko kinataja majina
ya Malaika wakuu sita:
Mikaeli
(Mkuu wa sehemu mhimu sana ya wanadamu) Gabriel (Mkuu wa Majoka, Bustani na wa
Makerubi), Urieli Malaika Mkuu wa dunia na watu wakali) na Raphaeli (Malaika
Mkuu wa Roho za wanadamu), Ragueli (ambaye analipiza kisasi juu ya dunia na
mwangaza) na Saragaeli (Malaika Mkuu wa watoto wa wanadamu, ambao Roho zao
wametenda dhambi).
Kitabu
cha Henoko, sura ya 20, R.H Charles, 2002).
Malaika
hawa pia wanaitwa Malaika Walinzi.
Malaika Mkuu Gabriel:
• Alitafsiri maono ya Danieli (Dan. 8:16, 26; 9:20-27)
• Alitangaza juu ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji (Lk.
1:11-20)
• Alitangaza kuzaliwa kwa Yesu (Lk. 1:26-38).
Malaika Mkuu Mikaeli:
Mikaeli
Mwana mkuu wa Mfalme, ametajwa mara nyingi katika Agano la Kale.
• Katika
Daniel 10:13 ametajwa “Jemedari mkuu aliyekuja kunisaidia.” Angalia pia Daniel
12:1
• Yuda
1:9 Mikaeli Malaika Mkuu, anagombana na Shetani kuhusiana na Mwili wa Musa.
• Ufunuo
12:7-8 Mikaeli pamoja na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye
akapigana nao pamoja na malaika zake.
Hawa
maserafi wanatambulikana kama makerubi wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu
kama tunavyoona sasa.
Makerubi:
Kiti cha
Enzi cha Mungu kinazungukwa na wanyama wane wenye vichwa tofauti. Hawa ni
Simba, Ndama, Tai na Mwanadamu, wanatambulikana kama Makerubi (umoja Kerubi)
wako wanne katika jumla ya hesabu yao na wana mabawa sita wanakizunguka Kiti
cha Enzi cha Mungu (Ufu. 4:6-9). Waliubwa wakiwa wanne (tazama mwisho wa Biblia
ya Companion Uk 10). Maelezo ya makerubi yanaelezewa katika Ezekiel 1:5-14;
10:20; na Ufunuo 4:6-9. Ambapo wameumbika katika viungo mchanganyiko katika
Ezekieli wakiwa walinzi wa Yehova wa Israeli na wanaonekana wenye mabawa manne
katika viwiliwii vyao vya juu. Hapa hawajatajwa kuwa na mabawa mawili katika
miguu yao kama wale makerubi wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu, au wale wa
moto katika Agano la Kale. Idadi ya hao makerubi kuwa wanne inatokana na
Uumbaji. Wakati makerubi hawa wanapotumwa katika nchi, kwa ajili ya Yehova wa
Israeli, na kutenda kwa pamoja huwa na mabawa manne na wanatembea pamoja katika
gari daima wakiangalia sehemu moja. Makerubi wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha
Mungu wana mabawa sita kama maserufi.
Mfano wa
vichwa vya viumbe wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu wanatabulikana kama
makerubi katika Ezekieli 1:1-28. Angalia Somo la Maono ya Ezekieli (Na. 108).
Vichwa
vya wanyama vinaashiria vita vya Wana wa Israeli na mgawanyiko wa makabila
katika idadi ya 10 na 11. Angalia
Somo la Uumbaji wa Familia ya Mungu (Na. CB4).
Tangu
mwanzo kulikuwa na makerubi wanne, makerubi wawili wanakizunguka na makerubi
wawili wakisimama nyuma ya Kiti cha Enzi cha Mungu. Ezekieli 1:4-14 anaelezea
juu ya makerubi wane; na hii ndiyo idadi ya “viumbe wane wenye uhai” wanaotajwa
katika Ufunuo 4:6
Makerubi
wanatajwa katika kitabu cha Mwanzo 3:24 ambapo tunasoma ya kwamba Mungu
alimfukuza mwanadamu kutoka katika Bustani ya Edeni na kuweka Makerubi, na
upanga uwakao moto katika sehemu ya Mashariki ya Bustani ya Edeni, kumzuia
mwanadamu asirudi na kula tunda la mti wa uzima.
Katika 2
Samweli 22:11; Zab. 18:10 na Ezekiel sura 1,9 na 10 inaonekana ya kwamba uzima
wa milele umesimama juu ya makerubi wanne.
Tunaona
mifano ya Makerubi inavyotumika, katika Hema ya kukutania pamoja na kwenye
Hekalu. Wale waliyo katika Sanduku la Agano wanaitwa “Makerubi wa Utukufu” (Ebr
9:5), kutoka kwa hao Makerubi Utukufu wa Mungu unaoonekana hukaa kwao.
Makerubi
wawili walitengenezwa kwa dhahabu, na wakiangaliana na mabawa yao yakiwa yameinuliwa,
huwekwa juu ya sanduku la Agano (Kut. 25:17-20). Mungu (kwa kupitia katika
malaika wake aliahidi kuzungumza na Musa “kutoka kati ya Makerubi” (kut.
25:22). Mifano ya makerubi iliwekwa katika mapazia ya Hema ya kukutania
(Kut.26:1,31).
Mfalme Sulemani
alikukuwa na makerubi wawili waliotengenezwa kutokana na mbao za mzeituni, na
kuwekwa Hekaluni. Makerubi pia waliwekwa milangoni na kwenye sehemu za ukutani
katika Hekalu, na mifano ya makerubi iliweza kushonewa katika nguo zilizotumika
Hekaluni (1 Fal. 6:23-35; 2 Nya. Sura ya 3).
Ingawaje
Biblia inatwambia ya kwamba tusijifanyie sanamu ya kitu chochote cha mbinguni
au cha duniani (Kut. 20:4; Kum. 4:16), Wana wa Israeli waliamriwa kufanya picha
za makerubi katika kuta za hema ya kukutania. Hizi zilikuwa ni mifano tu na
hazikuwa za kuwabudiwa. Hema ya kukutania ambayo Musa alijenga na Hekalu
alilojenga Sulemani ilikuwa mifano halisi inayowakilisha mambo ya mbinguni.
Nyota ya Asubuhi
Nyota ya
Asubuhi, Nyota ya Mchana au Mleta Nuru ni sifa tu za Jeshi la Kiroho na wala si
majina yao (Ayubu 38:1-7).
Nyota ya
Asubuhi ilionekana kutenda kazi kama Makerubi. Nyota ya Asubuhi ya sasa,
Lusifa, alikuwa ni mmoja wa makerubi watiwa mafuta kabla ya kuasi kwake. Cheo
hiki alichokuanacho Lusifa, pamoja na mamlaka na nguvu ya Kishetani aliyonayo
kama mungu, (god) wa Sayari hii itaondolewa na kuvuliwa hapo Kristo atakaporudi
mara ya Pili. Tazama Ufunuo 22:16.
Mbali na
shetani na Kristo kuna viumbe wengine katika Jeshi la Kiroho wanaotenda kazi
katika cheo kimoja. Angalia Somo la Lusifa: Nuru ing’aayo na Nyota ya Asubuhi (Na. 223).
Katika Uumbaji wa Sayari, nyota za Asubuhi zilikusanyiaka pamoja na kuimba
pamoja, na kupiga kelele na kushangilia kwa furaha pamoja na Wana wa Mungu.
(Ayubu 38:4).
Je, Mungu ndiye aliyemuumba shetani?
Mungu
aliwaumba Wana wake wakiwa Wakamilifu na Watakatifu, lakini walikuwa na uhuru
wa kuchagua Kumtii Mungu au Kutomtii Mungu. Tunajua ya kwamba wengine kati yao
walitenda dhambi, na Biblia inawataja kama “Malaika walioanguka” (Mwa. 6:2,4;
Yuda. 1:6)
Lusifa
alikuwa amejaa hekima na alikuwa Mkamilifu katika uzuri wote, lakini aliingia
katika majivuno na kuwa asiyefaa kitu na kugeuka kuendelea katika njia ya
dhambi, (Ezekieli 28:12-15). Alifikiri angeweza kujiinua juu ya Kiti cha Enzi
cha Mungu (Isa. 14:12-14). Maasi yake yalishindwa na kutupwa chini, duniani
katika nchi (Lk 10:18; pia katika Ufu.12:7,9). Lusifa alishawishi theluthi ya
malaika kumfuata katika maasi yake. Ambao alifukuzwa nao na jina lake
likabadilika na kuitwa shetani, yule joka mkubwa (Ibilisi) na malaika
waliofuatana naye wanajulikana kama pepo wachafu (demons). Wote wanajulikana
kama “Jeshi lililoanguka”. Angalia
katika Somo la Shetani ni nani? (Na. CB60).
Mungu
hakuwaachilia malaika waliokosa bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo
vya giza, walindwe hata itakapokuja ile hukumu (1 pet. 3:18-20; 2 Pet. 2:4-5;
Yuda 1:6). Mapepo wengine wachafu, huzunguka zunguka katika dunia hii
wakitafuta watu ili wawameze (Ayubu 1:6-12; Lk 8:30-32).
Ni nini kitakachotokea kati ya shetani na
mapepo wabaya?
Kristo
alihitimu katika kumkomboa mwanadamu na jeshi lililoanguka. Alilipa adhabu na
fidia, pale msalabani kwa dhambi zetu zote (Kol.1:19). Ni Mapenzi ya Mungu ya
kwamba hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wapate kutubu (2 Pet. 3:9).
Kwa hiyo
ni dhahiri ya kwamba mapepo wabaya wote watahukumiwa katika Ufufuo wa pili wa
wafu. Na yule Ibilisi, ambapo watakuwa katika umbo la kimwili kama wanadamu
watakao fufuliwa. Watakuwa na nafasi ya kutubu na kubadilika kuwa wana wa kroho
wa Mungu. Soma Biblia inasema nini katika Isaya 14:11-17. Tunaona shetani
anatajwa kama mwanadamu anaetoka katika shimo katika msitari wa 14. Tunaelewa
ya kwamba Kristo kama Mwana wa kroho wa kwanza wa mwanzo alifanyika mwanadamu
na akafa katika kifo cha kimwili. Kwa hiyo hilo pia linawezekana kwa shetani na
mapepo. Walakini, katika matokeo ya dhambi ya shetani na mapepo hawatahachwa
bila kuadhibiwa. Jambo moja hawatarudishwa tena katika nafasi zao
walizokuwanazo kabla ya kuasi.
Mwisho wa Mwanadamu
Mungu ni
Roho na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho, Kwa hiyo Uumbaji wa kwanza wa Mungu
ulikuwa ni Uumbaji wa viumbe vya Kiroho (Yn. 3:6). Mtu wa kwanza aliumbwa na
Mungu, lakini alitoka katika mavumbi ya
ardhini, kwa hiyo aliumbwa kama kiumbe kinachoonekana katika mwili. (kiumbe
chenye mwili unaoonekana) pia akaitwa mwana wa Mungu (Lk 3:38). Uumbaji wa
kimwili katika umbo la mwanadamu ilikuwa ni uumbaji wa pili wa Mungu.
Kilichozaliwa
kwa mwili ni mwili, (Yn. 3:6) na mwili na damu haviwezi kurithi Ufalme wa Mungu
(1 Kor. 15:50). Lakini mwisho wa wanadamu ni kuwa ‘wana wa Mungu’, k.m kuwa
Wana wa Mungu wa Kiroho. Wote wanomjua Mungu Mmoja wa kweli na Yesu Kristo,
Mwanae aliyetumwa na Yeye, na kutubu na kubatizwa na kupokea Neema ya Roho
Mtakatifu wa Mungu wanayo haki ya kuwa Wana wa Mungu (Yn. 1:13; Rum. 8:14-15; 1Yoh 3:1).
Wale
watakaofufuliwa katika ufufuo wa kwanza watabadilika na kuvaa miili ya Kiroho
na kutawala kama warithi pamoja na Kristo katika kipindi cha miaka elfu moja ya
Mileniamu. Wale watakaofufuliwa katika ufufuo wa pili ambao ni ufufuo wa
marekebisho na hukumu, iwapo wataonekana ya kwamba wanafaa na kuhitimu kwa kuwa
na sifa yakuwa Wana wa Mungu, basi watabadilishwa na kuvikwa miili ya Kiroho.
Mpango wa
Mungu wa Uumbaji wa Familia yake, hautakuwa umekamilika mpaka baada ya
kumalizika kwa hukumu ya mwisho, na kubadilika kabisa kwa sayari yote (dunia).
Hapo sayari yote (dunia)itakapobadilika katika Uumbaji mpya yaani Mbingu Mpya
Na Nchi Mpya, wote watakuwa Wana wa Mungu kama Elohim katika Roho Mtakatifu,
wote watakuwa wamekamilika katika Umoja wa Uungu, kama Familia ya Mungu
waliyounganishwa katika Roho mtakatifu na kuungana na Mungu kama Familia ya
Mungu.
Kwa
maelezo zaidi na mafunzo zaidi soma somo la
Serikali ya Mungu (Na. 174)
Jinsi Mungu anavyokuwa Familia
(Na. 187)
Hukumu ya Pepo wachafu (Na. 80)
q