Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[CB60]
Shetani
ni nani?
(Nakala
2.0 20060114 – 20070210)
Tunapofikiria juu ya shetani, Je tunakuwa tunafikiria juu ya kitu gani au shetani ni nini? Au ni nani? Je alikuja kutokea wapi? Madhumuni na makusudi yake ni nini? Je, Anatuathiri kwa namna gani? Na ni kwa nini shetani yupo? Je Ana mahusiano gani na Mungu?
Christian Churches of God
PO Box 369,
WODEN ACT 2606, AUSTRALIA
Email: secretary@ccg.org
(Haki
milki © 2006, 2007, Dale Nelson na Wade Cox)
(tr. 2008)
Somo hili linaruhusiwa kunukuliwa, na kusambazwa kwa yeyote mradi tu kama litanukuliwa kikamilifu, bila kubadilishwa au kuondoa namna halisi, Jina la Mchapishaji na anuani yake na tangazo la hati milki lazima vijumlishwe. Hakuna gharama yoyote ipaswayo kuchangiwa na mtumiaji na hairuhusiwi kuuzwa nakala zake kwa msomaji. Nukuu chache zaweza kuchukukuliwa katika makala zinazo tofautiana kimtazamo na kimaoni bila kukiuka maadili ya haki milki.
http://www.logon.org
na http://www.ccg.org
Shetani ni nani?
Watu wengi wanamsimulia Shetani kwa namna nyingi, na ana majina mengi.Yeye ni Ibilisi Lucifa, mwovu sana mbaya mno mpotovu, giza nene. Ni wakili wa mambo mabaya, machafu na yale yote ambayo Mungu hayapendi na ambayo Mungu hawezi kuyatenda. Shetani anawakilisha uovu. Hasa kitu cha kuogofya, kitu cha machukizo, kitu cha kulaumu, na kitu cha kuharibu na kuleta maafa ya madhara ya milele kwa ajili ya kuurithi ubaya wa uovu wake. Sasa baadhi ya haya ni kweli na baaadhi si kweli. Sasa tuone Shetani ni nani na jinsi gaini anavyoweza kuingia katika Mpango wa Mungu.
Asili:
Tangu mwanzo Shetani hakuwa anaitwa Shetani, yaani hapakuapo na
kiumbe kilichoumbwa na kuitwa Shetani. Alikuwa ni “mwana wa asubuhi”
(Isa.14:12) yeye pamoja na jeshi lingine la mbinguni,waliumbwa wote wakiwa
wakamilifu katika njia zao zote ( Ezekieli. 28:14-19). Kulikuwa na amani na
umoja Mbinguni. Kisha mambo
yakaharibika. Biblia haiko wazi sana
juu ya swala hili ni nini hasa kulitokea na
kwa namna gani, ila uovu au kutokumtii Mungu kulioneka kwa Lucifa.
Mwishowe alifukuzwa kutoka Mbingini, pamoja na jeshi lake lote lililoasi,
wakafukuziwa mbali kabisa kutoka mbinguni na kutupwa, na wanazunguka zunguka
katika nchi (duniani). Angalia Somo la Familia ya Mungu (CB.4).
Kuna baadhi ya watu wanadhani na kufikiria ya kwamba sababu iliyomfanya Shetani atende uovu mbinguni ni kwamba aliona wivu Mungu alipo muumba Adamu. Kabla ya uumbaji mpya wa kimwili, Mungu tayari alikwisha kuwa na Familia ya kiroho katika wana wa Mungu (Malaika). Kwa hiyo aliona kwa nini Mungu alihitaji kuongeza Familia nyingine, hasa iliyo dhaifu ya kimwili?
Mafikirio haya ya Shetani yalitimizwa pale katika bustani ya Edeni, shetani alipofanikiwa katika majaribu yake ya kumdanganya Adamu na Hawa, na kufukuzwa katika bustani ya Edeni, wakafukuzwa mbele ya Mungu, Shetani pia ataadhibiwa kwa kuingilia au kujaribu kuharibu Mpango mpya wa Mungu wa uumbaji.
Isaya. 14:12 Jinsi ulivyoanguka kutoka Mbinguni. Ewe nyota ya alifajiri, mwana wa asubuhi ! Jinsi ulivyokatwa kabisa. Ewe uliyewaangusha mataifa !(KJV imetumika wakati wote)
Shetani amedhoofisha mataifa kama Adamu alivyofukuzwa kutoka katika Bustani ya Edeni kwa sababu ya ushawishi wa Shetani. Hebu fikiria lile taifa la Adamu na Hawa, lingekuwa na nguvu ya namna gani kama watoto wao wangeendelea kupata amani na utakaso wa Bustani ya Edeni.
Anguko:
Inaonekana Shetani
hakufahamu Mpango wa Mungu, na alifikiri ya kwamba yeye shetani angeweza
kufanya vizuri zaidi kuliko Mungu. Hii ndiyo ilikuwa dhambi kuu ya Shetani. Kwa
kufikiri hivi hakumwabudu wala kumsujudia
Mungu, lakini anamwona Mungu
kama sawa na yeye (Flp. 2:6) Angalia Somo la Amri kumi za Mungu (CB17).
Isaya 14:14. Nitapaa kupita vimo vya mawingu. Nitafanana na yeye Aliye Juu.
Kisha shetani alijaribu
kumthibitishia Baba, Mungu, ya kwamba yeye ni mwenye haki na Mpango mpya wa
Mungu wa uumbaji wa dunia pamoja na vitu vilivyomo sio Mpango sahihi. Tunaposoma katika kitabu cha Ayubu tunaona
ya kwamba, Shetani na wana wote wa Mungu (Ayubu. 1:7; 2:1-4). Wanajiudhurisha
kwa Mungu. Shetani anajaribu kuonyesha ya kwamba mwanadamu anapokuwa
hakubarikiwa na Mungu, atamkana Mungu kwa sababu ya kutokuishi vizuri. Mungu
alijua moyo wa Ayubu na ingawaje alimruhu Shetani kuharibu yote alikuwa nayo
Ayubu (familia yake, mji wake, na afya yake).Ilikuwa ni kwa sababu ya madhumi
maalumu ya Mungu. Safari hii madhuni
makubwa ya Shetani na ushuhuda wake ulithibitishwa kuwa ulikuwa ni uongo, na
wote tunajua uongo wa shetani, wana wengine wa Mungu na wote wanaosoma Biblia
wanajua uongo wa Shetani (Yeye alikuwa ni mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama
katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema
yaliyo yake mwenyewe kwa kuwa yeye ni mwongo, na baba wa uongo. Mateso yote
aliyoyapata Ayubu yalipopita, Ayubu alibarikiwa hata kupita alivyokuwa
amebarikiwa hapo kwanza, alibarikiwa
mara dufu. (Ayubu 1 na 2). Katika mambo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala
kumumwazia Mungu kwa upumbavu. Angalia Somo la Historia ya Ayubu (Na. CB54).
Kutoka Ufunuo 12 tunaona ya kwamba
Kristo, Mwana-Kondoo amefufuliwa na vita mbinguni vinaisha. kulikuwa na vita
Mbinguni, Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, naye akapigana nao
pamoja na malaika zake waliodanganywa na shetani.
Ufunuo. 12:9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae ibilisi na shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Shetani hana nafasi tena ya
kujihudhurisha katika mkutano wa Mungu na kuwashitaki ndugu zetu (watu wa
Mungu) moja kwa moja kwa kusema maneno mabaya, ya uongo kama alivyofanya wakati
wa Ayubu.
Madhumuni ya Shetani:
Ufunuo 12:12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari ! kwa maana yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
Kwa sasa Shetani anatambua ya kuwa
anayo kazi kubwa na ana kipindi kifupi sana. Ametupwa hata chini. (yule mkubwa,
yule nyoka wa zamani. aitwaye Ibilisi na shetani audanganyaye ulimimwengu wote,
akatupwa hata nchi na mlaika zake wakatupwa pamoja naye. Kama tukimtii Mungu na
kumpinga Shetani naye atatukimbia. Kwa hiyo lazima tufanye bidii hadi tushinde.
Dhambi iko inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yakupasa
uishide, Shida inayotupata ni kwamba wengi hatuelewi na kufahamu ulimwengu wa kiroho vizuri, kwa sababu sisi
sio sehemu yake, na Shetani amekuwa na vishawishi vikubwa sana juu yetu.
Shetani hatusaidii na wala hatatusaidia
kitu chochote. Kazi ya shetani ni kutufanyia mazingira magumu na kutukatisha
tamaa, ili aweze kuonyesha ya kwamba yeye ana haki, na Mungu ni mwenye makosa.
Shetani anatushawishi vipi?:
Asili ya shetani ni roho mchafu.
sio kitu kinachoweza kuonekana, lakini ni
kitu ambacho tunaweza kukifahamu kwa kusoma Biblia. Biblia ilitolewa
kama Neno la Mungu. Yesu Kristo alikuja kwetu kama mfano hai wa Neno la Mungu.
Ni katika kusoma Biblia tu, ndipo tunaweza kutambua mazuri na mabaya, kujua juu
ya utauwa, au kutambua haki na imani ya kweli, na yapi yaliyo ya shetani. Na ni
nini yaliyo Mapenzi ya Mungu. Sio jambo tunaloweza kulifahamu tangu
kuzaliwa au ambalo tukiwa tunazaliwa tunakuwa tunalifahamu.Wengi kati yetu tunafanya uchaguzi mbaya kwa sababu hatusomi Biblia na
kulifuata Neno la Mungu, sawa sawa na Mapenzi ya Mungu. Tazama Somo la Dhambi ni
nini?(Na. CB26), na Siku za kumwabudu shetani (Na. CB23).
Shetani ni roho mchafu na
anatushawishi kiroho, njia moja ya kumuona shetani ni katika mawazo yetu, akilini mwetu. Tamaa mbaya,
mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu. Shetani sio kitu
kilichoandikwa, sio kitu tunachoweza kukiona kwa macho, kukisikia, kugusa,
kuonja au kunusa. Mungu ni kama hivyo kwa namna fulani na malaika wote na hata shetani
pia.
Waefeso. 2:2 Ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumufuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi.
Maandiko haya yanaonyesha jinsi
gani shetani alivyo na ushawishi mkubwa sana kwetu. Ni mfalme wa uwezo wa anga.
Anajaribu kuteka mawazo yetu. Anatushinda pale tunapokuwa hatumtii Mungu. Kwa
maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na
mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili. juu ya mapepo wabaya katika ulimwengu wa
Kiroho. Mungu hawezi kutufanya sehemu ya Familia yake mpaka hapo tutakapokuwa
tumeamua kufanya uchaguzi wa kuwa sehemu ya Familia ya Mungu. Ni lazima tufanye
uchaguzi. Basi chagua uzima ili uwe hai wewe na uzao wako. Mungu anapenda na
anahitaji tuwe sehemu ya Familia yake. Mungu anapenda na anahitaji tumwabudu
Yeye tu. Watu wanaoshinda haya
hubatizwa na mwishowe kuwa katika sehemu ya Ufufuo wa kwanza, au iwapo watakua
hai wakati wa kurudi kwa Kristo mara ya pili, basi watabadilika na kuvaa miili
ya Kiroho. Kama watakuwa hajabatizwa bado hata wakati wakurudi kwa Kristo
katika mileniamu katika hali ya kimwili kama wafalme na makuhani. Kama Ayubu,
tutabarikiwa na kupewa heshima zaidi kama tukiyashinda majaribu yote bila
kudanganywa na shetani.
Mawazo yote ambayo siyo mapenzi ya
Mungu yatoka kwa yule mwovu Shetani. Hii ndiyo sababu Yesu Kristo alimwita
Petro “Shetani” katika Mathayo 16:23.
Mathayo 16:23 Akageuka, akamwambia Petro, nenda nyuma yangu, Shetani u kikwazo kwangu, maana huyawezi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Petro hakuwa shetani bali
alimwakilisha shetani, au alikuwa kama shetani pale aliposema maneno mabaya
ambayo hayakuwa mapenzi ya Mungu aseme hivyo. Mawazo ya shetani sio mawazo ya
Mungu. Tukiwaza mawazo ya kishetani ( mawazo mabaya, tamaa mbaya) basi tumekuwa
kama alivyo shetani. Tukiwaza mawazo ya Mungu na tukienenda na kutenda kwa
Mapenzi ya Mungu, basi tutafanana na Mungu, au kwa njia nyingine tunaweza
kusema tuko pamoja na Mungu, au tu Umoja na Mungu, au tuko ndani ya Mungu.
Luka 22:31 Akasema, Simeoni, simeoni, tazama, shetani amewataka ninyi apate kuwapeteta kama vile ngano.
Shetani hapendi tushike imani zetu
na kumtii Mungu na kuishi katika sheria za Mungu. Hilo shetani halitaki kabisa.
Sheria za Mungu ziko kwa ajili yetu sisi na ni njema. Tukiyakiri haya na
kutenda kazi moja kama kundi moja, tutajilinda na yule mwovu shetani
hatatugusa, wala hatatupepeta kama ngano kila mmoja akitawanyika peke yake.
Kukataa kutii na kukataa kuhifadhi na kutunza sheria na Amri za Mungu, hatuwezi
kuwa nuru ya dunia, au kwa mtu na mtu,
na hatutakuwa na manufaa kwa Mungu. Mashaka ya mtu na mtu na juu ya mambo
tuyatendayo yakiwa ya mashaka yaani yasiyo na uhakika na kutokuwa na uhakika
yaani kuwa na mashaka na Mungu, Shetani ameshinda.
Wema Dhidi ya Ubaya?:
Mema yote yanatoka kwa Mungu.
Wakati watu walipomwita Kristo “Mwema” alisema, “Hapana! usimwite mwanadamu
mwema”; Ni Mungu tu ndiye Mwema”.
Mathayo 19:17 kwa nini kuniuliza habari ya wema? .Aliye mwema ni mmoja.Lakini ukitaka kuingia katika uzima,zishike Amri.
Alichokuwa akisema ni kwamba sisi
sio wema na hatuwezi kuwa wema kwa juhudi za nafsi zetu wenyewe. Hata Kristo
mwenyewe hakuwa mwema kwa kujifanya mwenyewe
mwema, kila lililokuwa jema kwake lilikuja kwa sababu ya kufahamu ni
nini yalikuwa mapenzi ya Mungu kwake, kama kutunza Amri za Mungu. Alikuwa mwema
kwa sababu alitunza sheria za Mungu. Alikuwa mwema kwa sababu aliyafahamu
mapenzi ya Mungu na aliwashirikisha wengine. Wema wake haukutoka kwake; ulitoka
kwa Mungu.
Ni lazima tufuate mfano wa Kristo
na kumtukuza Mungu, na kumkiri ya kwamba mambo yote yatoka kwake na utukufu
wote na sifa zote lazima apewe yeye kutii na kushika Amri za Mungu. Haimanishi
ya kwamba tunarithi wema, au kwa lugha nyingine hatuwi wema kwa asili, au kwa
kuzaliwa au kwa kutenda matendo mema. Ni Mungu tu ndiye aliye na matendo mema.
Tunahitaji na ni lazima tuenende sawa sawa na mapenzi yake iwapo tunataka tuwe
wema.
Shetani anataka tumdharau na
kutomsikiliza Mungu na tuamini kama yeye anavyoamini, ya kwamba tunaweza kuishi
bila Mungu vizuri, ahsante sana. Hatumuitaji Mungu katika kuiendeleza jamii
yetu kwa furaha. Hivyo ndivyo shetani alivyomwambia Mungu, “Nipatie Ayubu na
atakukana kama nikimnyang’anya mali na vitu vyote ulivyo mbariki” Ayubu
Ayu 2:4 Shetani akamjibu BWANA, na kusema. Ngozi kwa ngozi, Naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
Shetani anasema ya kwamba
mwanadamu anafikiria maisha yake ni muhimu na bora kuliko kuwa na Mungu kwanza
yaani maisha kwanza halafu Mungu badaye. Ni kweli ya kwamba pasipo Mungu hakuna
lolote zuri linaloweza kutendeka licha ya kwamba bado tunaweza kuendelea kuishi
na kufanya kazi zetu, ingawaje maisha yetu hayawezi kuwa na furaha na amani.
Hii ndiyo sababu maisha ya historia ya Ayubu ni muhimu na ya maana sana kama
kichocheo katika wokovu wetu, bila kujali shida matatizo mbalimbali na majaribu
yanayoweza kutupata. Tukitambua na kujua ya kwamba hayo yote hayatokani na
Mungu. Usimkane Mungu kwa kusema maneno mabaya juu yake au kumdharau Mungu unapokuwa
katika matizo au shida mbalimbali kwa sababu mwisho wake huwa ni mazuri kama
tukishikamana katika Imani au kumtukuza Mungu Baba. Mwisho wa yote kwetu,
mapenzi ya Mungu ni kututakia mema yaani uzima wa milele.
Kumbuka ya kwamba shetani haamini
juu ya Mpango wa Mungu kwa ajili yetu, Lakini Kristo anaamini. Hii ndiyo sababu Kristo alijitoa awe kafara
(Sadaka). Shetani asingeweza, kwa sababu hafikirii ya kwamba sisi tunaweza kuwa
mpango wa sehemu hiyo kwa vyovyote vile. Kristo, aliye wa asili ya kiroho na
kibinadamu, ametufunga wote kwa pamoja, jeshi la kiroho na sisi wadamu (jeshi
la kimwili), yaani Kristo ametupatanisha sote kwa Mungu. Wote sisi (wa kiroho
na wa kimwili), kama wale wote ambao hawajamfahamu Mungu bado, na wale ambao
wanamfahamu, sasa wote wanaweza kuwa sehemu ya Familia ya Mungu kwa damu ya
Mwana - Kondoo, kama wakichagua au kuamua kuwa hivyo. Hii ndiyo sababu (Kafara)
Sadaka ya damu yake ni muhimu sana katika wokovu wetu. Maana Kristo alikuja
akawa hai tena kwa sababu hii awamiliki waliokufa na waliyo hai. Kristo
anatimiza yaliyo mapenzi ya Mungu kwa kila njia na shetani anajaribu kupinga na
kutenda kinyume chake.
Jinsi shetani anavyotenda kazi:
Mark. 4:15 Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja shetani, akaliondoa lile neno lililopadwa mioyoni mwao.
Iwapo shetani alimjaribu na
kumshawishi na kujaribu kumdanganya Yesu Kristo pale mlimani (Mk. 1:13). Je
hatuwezi kufikiria ya kwamba atafanya hayo hayo ya udanganyifu na kutujaribu
sisi pia?. Je hafanyi hayo hayo kwetu sisi kwa wakati huu?. Shetani anataka
tuwaze na kufiri kunyume na mapenzi ya Mungu, na haya yakitokea hatutakuwa
karibu na Mungu. Kufikiri kunyume na mapenzi ya Mungu ni kujitenga na Mungu.
Shetani anatumia hila nyingi sana kutufanya tuwe na mawazo tofauti na Mungu.
Shetani anaharibu mawasiliano ya mwanadamu na Mungu. Mchonganishaji wa
mwanadamu na Mungu. yeye alikuwa muaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika
kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake
mwenyewe, kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa uongo.
2 Wathesalonike 2:9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo.
Anatufanya tuamini pepo, uchawi,
mageuzi yenye kuendelea kutokea, kwa utaratibu
wa wanadamu (evolution) na miujiza, mambo ambayo hayatokani wala hayatoki
kwa Mungu, anatulazimisha kuamini chochote kile ili kutuchanganya akili zetu.
2 Wakoritho 11:14 Wala si ajabu. Maana shetani mwenyewe hijigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki,ambao mwisho wake utakuwa sawa sawa na kazi zao.
Shetani ana udanganyifu wa hali ya
juu sana, akifanya mazuri kuwa mabaya. Kuna makanisa mengi yanayohubiri imani
ambazo wanaziona kuwa ni nzuri, lakini swali
la kujiuliza, je hayo ndiyo mapenzi ya Mungu? Mungu anasema ya kwamba
“Na uzima wa milele ndiyo huu, wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu
Kristo uliyemtuma. Na kuonyesha ya kwamba tunampenda ni lazima tushike na
kutunza amri zake. Kanisa linaloshika na kutenda amri za Mungu ndilo
kanisa linalopaswa kufuatwa.Wengine
wanashika na kutunza amri sita za mwisho na wakati huo huo wanafundisha mpende
jirani yako, lakini amri za kwanza nne zinazotueleza tumpende Bwana Mungu wetu
na ndizo zinazoshuhudia upendo wa Mungu ambazo hawaziangalii. Shetani
amechanganya ulimwengu kwa udanganyifu wa hali ya juu sana, kiasi kwamba ni
vigumu kupata wenye imani wanaoamini juu ya mambo haya.
Usijione kama umepotea au kuogopa
kama vile majeshi, au jeshi la malaika ambalo ni waaminifu na ni wakiroho
wanapotulinda tunapowahitaji. Malaika ni wajumbe wa Mungu, kwa hiyo ni kwa ye
yote anayetuletea ujumbe kutoka kwa Mungu, kama vile mtu maalumu wa posta
anayetuletea barua kutoka kwa Mungu. Kirsto alikuwa ni Malaika Maalumu, Mwana
Maalumu wa Mungu aliyeleta ujumbe maalumu sana. Heshima aliyopewa ni kuu kuliko
heshima aliyopewa malaika yeyote kwa sababu kuna tofauti na shetani, Kristo
aliamini hukumu ya Mungu. Kwa sababu hiyo ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba
na jeshi lote la mbinguni wanamtii na kumpa heshima Angalia Somo la Jeshi la mbinguni.(Na.
CB 28).
Ufunuo 5:12 kwa sababu hii sasa ameketi katika mkono wa kuume wa Mungu akiwamilki malaika pamoja na sisi sote ni milki yake sote kwa pamoja tunampa heshima na utukufu na baraka.
Mpango wa Mungu:
Kristo atarudi tena mara pili, sio
kama tu kama kuhani wakati alipokuja mara ya kwanza, lakini pia kama Mfalme.
Anakuja kutimiza azima yake ya kuwa Mfalme. Itakuwa ya kwamba dunia yote italazimika
kushika na kutunza sheria za Mungu kuthibitisha ya kwamba ndiyo njia ya
utaratibu mzuri wa kuishi (Zek.
14:16-21). Hii haiwezi kutokea mpaka dunia yote itakapokuwa imeharibiwa, kwa
sababu ya kutojali kwa wanadamu wanaokaa duniani. Hii ndiyo sababu kuna vita,
ongezeko la joto duniani, magonjwa ya ajabu, mvua ya sumu n.k. haya yote
yasingetokea kama tungeshika na kuzitunza amri za Mungu nazo ni kumpenda Mungu
na jirani zetu, ambapo ni kushika na kutunza sheria zinazohifadhi mazingira na
watu wake. Kama Mungu atakatiza na kutengeneza
mapema, tutasema, naam, lakini tungeweza kuitengeneza: na tukawa
hatumhitaji kweli. Lakini ni lazima ijulikane wazi na kudhihirika katika dunia nzima ya kwamba pasipo Mungu
kutengeneza dunia hii, kazi za mikono ya binadamu ni bure. Ni Mungu tu ambaye
ndiye anayeweza kuibadilisha dunia hii. Katika muda wa miaka elfu moja.
Katika kipindi cha mileniamu, kitakuwa
kizuri sana na salama kabisa. Kila mtu atasahau yale ya nyuma yaliyopita. Kila
mtu atakuwa mkarimu na mwema: kila mtu atatunza sheria za Mungu kwa upendo na
furaha.
Ufunuo 20:2 Akamshika yule joka, yule joka wa zamani, ambaye ni ibilisi na shetani, akamfunga miaka elfu.
Shetani atafungwa na hataweza
kumshawishi mtu tena mwanadamu yeyote kwa muda miaka elfu moja kisha
atafunguliwa tena (Ufu. 20:7) mwisho wa hiyo miaka elfu moja. Na hiyo miaka
elfu itakapokwisha, shetani atafunguliwa, atoke kifungoni kwake; na kutambua ya
kwamba ameshidwa; ni mnyonge hawezi kupata nguvu pasipo Mungu, na kuna vita
vingine tena vitakavyotokea dhidi ya Mungu kama shetani atakavyowadanganya
nakuwashawishi watu tena kama anavyofanya wakati huu wa sasa. Tazama somo la Siku takatifu za
Mungu (Na. CB22).
Walakini, watu hawa wanaofanya
uchaguzi mbaya na kumkana Mungu hawapotei milele. Mungu ni wa rehema nyingi na
watafundishwa kama vile wengine watakavyofundishwa katika ufufuo wa pili. Kama
wakishidwa kuchagua kumwabudu Mungu na kumtii, ndipo watakapoadhibiwa katika
ziwa la moto wa milele ( Ufu. 21:8) ambayo ndiyo yatakuwa ni maangamizi ya mwisho
ya moto wa milele, kuzinu ambayo ni mauiti ya pili, k.m. watakufa milele, na
hawatasikia, hataona, hawatapata fahamu. Hawatafufufliwa milele kupata uhai wa
kimwili au wa kiroho. Lakini katika ukweli kwamba mapenzi ya Mungu ni kokolewa
kwa watu wote ni ishara ya kwamba huenda mtu yoyote hatapotea katika mauti ya
milele. Tazama somo la Ni nini kitakchotokea tutakapo kufa? ( Na. CB 29).
1 Timotheo 2:4 Ambaye hutaka watu wote
waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.
Mpango wa Mungu ni Mkamilifu,
Mungu ni Mwenye Mamlaka, mwenye Enzi zote, Mkuu wa yote (Omnipotence). Hii ina maana ya kwamba Mungu anajua vitu
vyote na anaweza kufanya yote atayakayo. Mpango wa Mungu ni kwamba wanadamu
wote wampende Mungu, wamwabudu na kumutumkia, na kuwa sehemu ya Familia yake.
Matendo 26:18 uwafumbue macho yao, na
kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru,waziache nguvu za shetani na
kumwelekea Mungu: kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao
waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.
Shetani anatupwa katika shimo
(Isa. 14:15-17). Na wale wanaomwona
washangaa na kustajabu ya kwamba huyu ndiye yule aliyeleta matatizo yote ya
duniani na huzuni na masikitiko yote. Ghafla anabadilika na kutokuwa tena yule
mnyama wa roho chafu ya kutisha na ya kuogofya ambaye hapo mwanzo alikuwa ni wa
kuogofya na wa kutisha, aliyeweza kusababisha watu waamini ya kuwa ndivyo
alivyo. Yeye ni mhongo aliyouadhibu uumbaji wa Mungu uliyofundishwa kumkili
Mungu katika nguvu zake ambaye Yeye ni Mweza.
Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
Hata hivyo shetani atatambua ya
kuwa Mungu alikuwa ni wa haki wakati wote. Hili neno “shetani” maana yake ni
mshitaki. Shetani ataacha kuwa mshitaki, hatakuwa shetani tena. Hatawashitaki
tena ndugu, kama alivyowashuhudia kwa uongo. Mashitaka yamekwisha lakini
yatakuwepo daima kama kumbukumbu. Adhabu gaini kwa shetani ! Mashitaka yake
hayatasahaulika. Yatakumbukwa daima kama aliyemvunjia Mungu heshima, na kwa
kuudan ganya ulimwengu. Atapata mateso yake kwa sababu atatambua makosa yake.
Msamaha wetu ni muhimu sana katika kurudisha utukufu na heshima yake na katika
maisha mema.
Mwishowe, kila mtu atamtambua
Kristo kuwa ni Mfalme na Kuhani Mkuu anayeunganisha dunia yote na kumwakilisha
Mungu. Jambo hili litakapokamilika vita kati ya mema na mabaya vitakuwa
vimekwisha. Ushawishi wa shetani utakuwa umekwisha. Mauti yamekwisha. Makanisa
ya uongo na manabii wa uongo na unabii wa uongo utakuwa umekwisha. Yote
yatakuwa yamekwisha; wote watatambua Mpango wa Mungu na watakuwa sehemu ya
Familia ya Mungu. Wote watakiri ya kwamba Mungu alijua yote, na anajua yote, na
daima atajua yote.
Kuwa Huru na Ushawishi wa Shetani:
Tuko vitani ( 2 Kor: 10:1-6). Na
tunahitaji tuvae silaha zote za Mungu ili tuweze kupata kuzipinga hila za mwovu
Shetani (Efe. 6:10-20). Tujifunge kweli viunoni, dirii ya haki kifuani,
kufungiwa miguuni utayari tupatao kwa injili ya amani, ngao ya imani, chapeo ya
wokovu, na upanga wa Roho, ambao ni neno la Mungu. Kuwa tayari kusoma Biblia,
kuomba na kufunga. Angalia somo la Maombi sehemu A
mwongozo wa mwalimu (Na. CB31).
Wala tusiache kukusanyika pamoja,
kama Mwili Mmoja katika Kristo. Ni adhabu kutengwa nje ya kundi.(1Tim. 1:20).
Tuwe na matumaini kwa mambo yajayo
na tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana (2 Kor. 4:16-18).
Kwa Mhutasari:
Kama historia ya mwana mpotevu
katika Luka 15:11-32, Shetani anauzunika kijana mdogo Adamu, anapokaribishwa na
kuungana na Mungu. Anapoungana na Malaika wote wanaposhiriki pamoja katika
Upendo wa Baba. Shetani anamkasirikia Mungu na anapanga mipango ya kuthibitisha
ya kwamba Mungu ana makosa.
Shetani amepewa muda mfupi wa
kudanganya ulimwengu, kama vile alivyopewa muda mfupi wa kumtesa Ayubu. Hata
hivyo wakati wote tunapaswa kusimama imara kuwa na kiasi na kukesha, tukijua ya
kuwa shetani ni (mshitaki wetu) Ibilisi kama simba aungurumaye, huzunguka
zunguka, akitafuta mtu ammeze. Ni lazima tumpinge na tusimame imara katika
imani (1 Pet. 5:8).
Mwishowe, ulimwengu (kama Ayubu)
hautamkana Mungu, ingawaje shetani anasema tutamkana.
Shetani amethibitishwa kuwa ni
mwongo, kila wakati mara zote shetani ni mwongo tu wala kweli haikai kwake.
Mwisho Mungu atakuwa katika
yote na ndani ya wote katika umoja,
upendo, amani na katika Familia yake yote. Wana wa Mungu (Malaika) watajua
mipaka ya utendaji wa wajibu wao bila ya kuathiri uumbaji wa Mungu katika
uumbaji wa Adamu mwadamu, na mwanadamu
(Adamu) naye atajua mipaka ya utendaji wa wajibu wake bila ya kuathiri uuumbaji
wa Mungu katika kuwako kwa malaika. Bila kuteegemea uzoefu wao au kutegemea
akili zao wenyewe,wote watatambua ya kwamba furaha yote imeletwa na Mungu. Huu
ndiyo Mpango wa Mungu na ndiyo maana shetani amerusiwa kuendela kutenda kazi
yake hivi sasa. Mungu anatawala yote. Ana Mpango. Ni Mkamilifu. Mpango wa
Mungu Utatimia. Usiwe na hofu.
q