Makanisa ya Kikristo ya Mungu

 

 

[L1]

 

 

 

Sheria za Mungu

 

(Toleo la 1.0 19990525-19990525)

 

Agizo la Usomaji wa Sheria za Mungu katika mwaka wa Sabato wakati wa Sikukuu ya Vibanda, kufafanua utaratibu wa Sheria za Kibiblia na za Manabii, umejumuishwa kwenye mlolongo huu wa majarida haya yaliyopangiliwa vema yenye ku tuama kwenye Amri Kuu Mbili. Kwa mujibu wa kimaandiko ya Biblia, inatakiwa kusomwa kwa kila mtu anayedai kuwa ni mwanafunzi wa Biblia.

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

(Copyright © 1999 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

This paper may be freely copied and distributed provided it is copied in total with no alterations or deletions. The publisher’s name and address and the copyright notice must be included.  No charge may be levied on recipients of distributed copies.  Brief quotations may be embodied in critical articles and reviews without breaching copyright.

 

This paper is available from the World Wide Web page:
http://www.logon.org and http://www.ccg.org

 

 


Sheria za Mungu [L1]



Agizo la Kusomwa kwa Sheria za Mungu  katika mwaka wa Sabato wakati wa Sikukuu ya Vibanda, kufafanua utaratibu wa Sheria za Kibiblia na za Manabii, umejumuishwa kwenye mlolongo huu wa majarida haya comprehensive  yanayotuama kwenye Amri Kuu Mbili. Kwa mujibu wa kimaandiko ya Biblia, inatakiwa kusomwa kwa kila mtu anayedai kuwa ni mwanafunzi wa Biblia.

 

"Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii. Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii." (Yesu Kristo; Mat. 22:37-40).

 

Amri Kuu ya Kwanza ya Mungu [252]

Kifungu hiki cha maandiko (au aya) kinaonyesha utaratibu wa mpangilio wa Biblia kuhusiana na Sheria na Manabii.

 

Sheria na Amri ya Kwana ya Mungu [253]

Kifungu hiki cha maandiko kinaonyesha mwanzo wa Sheria na amuhimu wake kama kigezo cha masuala ya imani, inayoitwa ya Mungu Mmoja wa pekwe wa kweli.

 

Sheria na Amri ya Pili ya Mungu [254]

Kifungu hiki cha maandiko kinaielezea Biblia kwa mtazamo wa Ibada ya sanamu na tendo la kuabudu sanbamu za kuchongwa kwa kutumia tafsiri za Kibiblia na utaratibu wake.

 

Sheria na Amri ya Tatu ya Mungu [255]

Kifungu hiki cha maandiko kinaelezea kuhusu Jina la Mungu na ulinzi wa mamlaka yake aliyonayo katika Sheria za Mungu kama ilivyofunuliwa kwenye Maandiko Matakatifu.

 

Sheria na Amri ya Nne ya Mungu [256]

Kifungu hiki cha maandiko kama kinaonyesha utaratibu jinsi Sheria inavyohusiana na utaratibu wa Sabato na utaratibu wa Kalenda na Unabii wa Biblia.

 

Amri Kuu ya Pili ya Mungu [ 257]

Amri hii Kuu ya Mungu inashikamanisha ukumbushiaji wa Sheria na Manabii ikizifafanua amri zile sita za Mwisho.

 

Amri ya Tano ya Mungu [258)

Amri ya Tano ya Mungu inahusiana na mfumo wa jamii na wa taifa na unafafanua kuhusu Sheria za Biblia na wajibu uhusuo pande zote.

 

Amri ya Sita ya Mungu, (Na. 259]  

Amri ya Sita ya Mungu inafafanua au kuelezea kuhusiana na usafi au utakaso wa maisha na haki ya kutoa uhai kuhusiana na isemavyo Sheria ya Mungu.

 

Sheria na Amri ya Saba ya Mungu [260]

Sheria kuhusiana na Amri ya Saba ya Mungu inasimamia kuweka mkazo unaokataza mambo ya uasherati na uzinzi na kuweka utaratibu wa mwenendo na maadili ya jamii za wanadamu.

 

Sheria na Amri ya Nane ya Mungu [261]

Sheria kuhusiana Amri ya Nane ya Mungu inasimamia haki zote za raslimali za mtu kwenye jamii yake.

 

Sgeria na Amri ya Tisa ya Mungu [262]

Kuhusu Amri hii ya Tisa inasimamia kanuni ya mfumo au utaratibu unaohusiana na mambo yahusuyo haki na kweli ndani ya jamii zote.

 

Sheria na Amri ya Kumi ya Mungu [ 263]

Andiko linalohusika na Amri ya Kumi ya Mungu inauinua utaratibu wa Sheria kutoka kwenye hali ya kimwili hadi kufikia kwenye kiwango cha kiroho na linafungamanisha Sheria na Manabii wa Roho wa Mungu.

 

Baadhi ya Majarida yanayounga mkono Aya hizo ni haya yafuatayo:

Wateuke kama Miungu Wadogo [001]

Mungu Tunayemuabudu [002]

Msalaba: Chanzo chake na Maana yake [039]

Kalenda ya Mungu [156]

Jukumu la Amri ya Nne ya Mungu Katila Historia ya Makanisa ya Mungu ya Watunza-Sabato, [170]

Utoaji wa Zaka [161]

Utakaso wa Hekalu la Mungu [241]

Uwepo wake Yesu kutoka Mwanzoni [ 243]

Utakaso na Tohara [ 251]

 

Hebu na tusikie mwisho wa mambo yote;

"Hii ndiyo jumla ya maneno;  yote yamekwisha kuwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake. Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu" (Mhu. 12:13) "Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, nakuwa na  ushuhuda waYesu…" (Ufu. 12:17; sawa  na  14:12)

 

 

 

 

 

 

q