Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[007]

 

 

 

 

Maana ya Alama za Tarakimu

(Toleo La 2.0 20000725-20000725-20070813)

 

Jarida hili linashughulika kwa kina kuelezea juu ya maana ya kiroho ya tarakimu kwenye Biblia.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Hati Miliki © 2000, 2007 Wade Cox)

(tr. 2015)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Maana ya Alama za Tarakimu


 


Tarakimu kwenye Biblia zina maana ya kiroho na hazimo kwa ajili ya kuhimisha tu mchakato wa kimahesabu.

 

Tarakimu ya Namba Moja (1) inamaanisha umoja au muungano na mwanzo, hususan wa uumbaji. Elohimu ni mmoja kutokana na mwendelezo wa kiuungu wa Eloa hadi Elohimu lakini ni wamoja kwa mapenzi ya Eloa.

 

Tarakimu ya Namba Mbili (2) inaony0sha utofauti. Kwanza kabisa, makubaliano kwenye ushuhuda yanahitimisha ushuhuda. Kwa hiyo basi, kila wakati kuna mashahidi wawili tu wanaohitajika ili kuwezesha kuadhibi dhambi na kufanya hukumu. (Soma jarida la Torati na Amri ya Nne (Na. 262).)

 

Tarakimu hii ya mbili inaonyesha mgawanyiko na hii inatokea kwamaana ya kuwa na mawazo ya kutangatanga nk, kwenye usemaji. Hii ilikuwa ni kazi ya siku ya pili ya uumbaji.

 

Tarakumu ya Namba Tatu (3) inaonyesha au kumanisha utimilifu kwa maana ya mistari mitatu ya umbo. Ilitumika pia kwenye mundo wa dini na imani ya kishetani ya mungu wa Utatu. Siku ya tatu ilihitimisha msingi wa muundo wote wa uumbaji. Siku za nne, tano na sita ni tarakimu shirika wa mchakato wa muundo wa mara tatu wa uumbaji tunaouona kutoka kwenye siku ya kwanza, ya pili nay a tatu.

 

Tarakumu ya Namba Nne (4) (3+1) inamaanisha au inamaanisha kazi uumaji na inafanya rejea yake kwa Dunia na vitu vinavyoonekana vilivyo kwenye umbaji.

 

Ni kwenye vifungu vinachofuatia vya nne, tanona vya siku ya sita kwenye utendaji kazi tunaouona kwenye muundo uliojengeka kwenye kile kilichowekewa msingi wake kwenye siku tatu za kwanza. Kwenye jambo hili likilinganishwa na hesabu ya mwaka mmoja kwa siku moja tunauona mfano wa mti. Siku tatu (au miaka mitatu) inaruhusiwa kulima na kisha kwenye mwaka wa nne vilichinbwa. Hakuna matunda yanayoruhusiwa kuliwa kipindi hiki. (Soma jarida la Samsoni na Waamzi (Na. 73) ili kupata maelezo zaidi kuhusu mfano huu.)

 

Tarakumu ya Namba Tano (5) inasimama kumaanisha Rehema za Mungu. Ikiwa kwenye mjmuisho wa kitarakim wa 4+1, ni kazi iliyochukuliwa na kufanywa na Roho Mtakatifu wa Mungu kwa amani ikielekea kwenye muimarisho au kuimarishwa kwenye majaribu. Kwa hiyo, mwaka wa hamsini wa mchakato na mfuatano wa matukio umechukuliwa na kuhesabiwa kikamilifu kwenye awamu hii.

 

Kwenye lugha ya Kiebrania, Bullinger anaonyesha kwamba neno Ha'aretz (Dunia) kwenye gematria – ambalo ni nyongeza ya thamani ya kibiashara ya herufi hizi kwa pamoja – ni uwingi wa nne, wakati ambapo Hashamayim (mbingu) ni mzidisho wa tarakimu tano. Gematria ya neno la Kiyunani Charis au Neema ni pia mzidisho wa tarakim tano. Namba Tano ni jambo lililotangulia kwenye upimaji wa Maskani.

 

Tarakumu ya Namba Sita (6) inajlikana kama Namba ya Kibinadamu. Mwanadam aliumbwa siku ya sita ya juma la uumbaji. Matumizi ya tarakim hii na mzidisho wake wowote kunahusiana na uumbaji na ni zao la mwanadamu na muundo wote wa uumbaji. Kwa hiyo, nambari au tarakimu zinazotuama kwenye tarakimu hii ya sita ni viwakilishi vya kazi iliyoanza mapema ya kabla mapumziko ya mwisho yaliyotolewa na Mungu. Pia ni ukamilifu wa kazi, ikiwa ni hitimisho la siku ya sita ya siku za kazi za Mungu. Masaa ya siku yamekuwa ni migawanyo pia ya siku sita. Na ndivyo ilivyo pia kwa dakika na sekunde zinazozidishwa kwa sita kwenye makumi.

 

Utendaji kazi wa sita haujakamilika na hauashirii au kuonekana kuwa haujakatazwa na Mungu. Athalia alikitwaa kiti cha ufalme wa Yuda kwa kipindi cha miaka sita. Tarakimu hii inazifanya zile zilizokwisha simama kuwa kwenye ya Mungu kama walivyokuwa kina Goliathi, Nebukadreza na baadae atakavyokuwa Mpingakristo na utawala wake.

 

Tarakumu ya Namba 666 ni ya alama ya Mnyama na utawala wake (ingawa kuna baadhi ya maandiko ya zamani pia yanasema namba 612). Alama ya dini na imani potofu za Kisiri ilikuwa ni tarakimu hii ya 666 kwa namna ya utambulisho wa kumtambulisha Isis. Nembo au alama yake ilikuwa ni SSS ambayo kimahesabu ilikuwa ni 666. Kwa hiyo alama ya Mnyama ni imani ya kidini ambayo msingi wake umewekwa kwenye dini za Siri na za waabudu  Jua ya Mabaali na Easter au Isis ambazo zilishamiri sana huko Mashariki ya Kati.

 

Kila imani ya kidini inaoamini maadhimisho ya ibada za Jumapili na kuiamini Easter yanaibeba alama ya Mnyama. Kila kitu kimewekwa kwa msingi wa tarakim hii ya namba sita na kuwekwa kwenye mzingiro wake.

 

Tarakumu ya Namba Saba (7) inamaanisha ukamilifu wa kiroho. Inaonyesha taswira ya kazi ya Roho Mtakatifu kama nguvu au uweza wa Mngu kama inayopigwa chapa ya nembo ya ubora. Ni alama ya uzima na inakigawanya kipindi cha ungezeko au uzazi mwingi kwenye maisha ya mnyama. Ni tarakim ya pumziko na ni mzunguko wa pumziko kwenye yubile. Inafanya pia taswira ya kipindi cha ujio wa Mungu kwenye pumziko na kurudi kwenye sheria au Torati yake, na ndiyo maana Torati inasomwa kwenye mwaka wa Sabato wa mzunguko.


Tarakumu ya Namba Nane (8) inamaanisha ufufuo au kufanywa upya kwa watu. Hivyo tunaona mwanzo mpya na utangulizi wake. Ni mwanzo mpya na hivyo ni ubeti wenye sauti nane kwenye muziki na inahusiana na rangi. Ni mwaka wa Yubile kwenye mzunguko wa mwisho wa kipindi cha mgawanyo wa saba kwa saba ukiwa kama mwaka wa nane, ukiwa ni wa hamsini na wa nane wa mzunguko ukipitiliza kwa sehemu tu (soma majarida ya
Torati na Amri ya Nne (Na. 256); Utoaji wa Zaka (Na. 161); na Jinsi Usomaji wa Torati Ulivyofanywa na Kina Ezra na Nehemia (Na. 250)).

 

Dhana ya siku ya nane inatokana pia na dhabihu ya Kristo iliyotolewa kama Mganda wa Kutikiswa. Kristo alifufuka kwenye siku ya ukamilisho wa juma mwishoni mwa siku ya Sabato na kipindi kilichojulikana kama Sabaton kwenye juma (soma jarida la Nyakati za Kusulibiwa na Kufufuka (Na. 159)).

 

Kristo alipaa kwenda kwa Baba akiwa kama Sadaka ya Mganda wa Kutikisa siku ya Kwanza ya Juma saa 3:00 asubuhi akionyesha mwanzo mpya wa uumbaji. Alirejea siku ile akiwa na Roho Mtakatifu na kuwavuvia wanafunzi kwa pumzi. Na ndiyo maana kuna juhusi kubwa sana inayofanywa na watu wa dibi ya kupinga adhimisho hili la Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa na kukubalika kwa Kristo kwa Mungu kwenye siku hii. Rejea pia kwenye jarida la Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa (Na. 106b).

 

Tarakimu inayomlenga Iesous (Yesu) ni 888 kwenye muundo wa kigematriki pia. Tarakimu hii inaonekana kwenye matukio mengi mbalimbali ya utendaji au kazi za Bwana.

 

Tarakumu ya Namba Tisa (9) inawakilisha hitimisho la mfululizo wa matukio au hokum. Ni hesabu ya 3 x 3 na ndiyo utaratibu kamili wa matukio. Tarakimu hii inakutikana kwenye mambo yote yahusuyo mambo ya hukumu.

 

Tarakumu ya Namba Kumi (10) inawakilisha ukamilifu wa kawaida na mwanzo mpya ukiwa kama mmoja kwenye mwandamano mpya wa mambo.

 

Tarakumu ya Namba Kumi na Moja (11) wakati mwingine inaonekana kama mkanganyo, lakini ni jambo lisilokamilika kama ilivyo kwa sehemu au nusu ya alfabeti za Kiebrania. Ia, ni moja iliyo nyuma ya kumi na kumi na mbili, tarakimu ya kipimo cha rerikali ya mbinguni.

 

Tarakumu ya Namba Kumi na Mbili (12) inawakilisha serikali ya Mungu pamoja na idadi nyingine kubwa ya uzidisho wa kumi na mbili zinazojitokeza kwenye resikali.

 

Inawakilisha Maskani na makuhani waliogawanyika kwa kufuata utaratibu wa mgawanyo wa makabila, ambao wao wenyewe wanawakilisha Ufalme wa Mungu. Tazama kwenye jarida la Mji wa Mungu (Na. 180).

 

Tarakumu ya Namba Kumi na Tatu (13) inaonekana kuwa ni tarakimu inayowakilisha hali ya kutamalaki au kuiwekea utaratibu migawanyo kwenye mndo wa serekali. Kwa mfano, kulikuwa na makabila kumi na mawili na la kumi na tatu lilikuwa ni la Lawi ambalo lilitumikia huduma za Hekalu. Kalenda 7a Mungu (soma jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156)) imegawanywa kwa miezi kumi na tatu kwenye kila miaka saba ya kipindi cha mzunguko wa miaka kumi na tisa.

 

Kwahiyo uasi na waasi wote wanatafuta jinsi ya kuchukua fursa ya utendaji huu kama kijalabu cha kumi na tatu au umiliki wake, na tarakimu ya namba 13 maranyingi imehusiana na uasi. Tunaweza kujionea hilo kwenye tukio la kwanza lililo kwenye Mwanzo 14:4 na la pili linathibitisha yale yaliyo kwenye Mwanzo 17:25. Dr. Bullinger anashindwa kujua au kulijua jambo hili kuhusu matendo ya Mungu kwenye kazi yake ya uandishi kwenye somo lililo kwenye sehemu ya Nyongeza 10 hata kwenye tafsiri ya The Companion Bible. Majina na tarakimu vinavyohusiana na harakati za uasi vinavyoonekana kuwa vimezidishwa kwa namba 13 vimehusishwa. Ni tarakimu ya nambari kuu na ambazo zimehusiana na dhana hiyo ya kazi za mwanadamu pasipo kuhitimisha na Mungu, isipokuwa ni kama ukweli ulioamriwa na Mungu kwenye imani iliyothibitika.

 

Tarakumu ya Namba Kumi na Nne (14) ni saba mara mbili nah ii inaifanya kuwa ni mfano au alama. Inapungua kwa tano wakati tarakimu zinapoongezeka.

 

Tarakumu ya Namba Kumi na Tano (15) ni kiwango cha neema iliyo mara tatu. Inatumika pia na imani ya kipagani kwenye elimu yao ya mambo ya tarakimu (kama zilivyokuwa ni tarakimu zote), na inapungua kwa tarakimu sita. Kwa hiyo tarakimu hii pia ni ya dini ya uwongo.

 

Tarakimu hii ya nambari 15 ni nambari au tarakim ya kipagani pia na inayotumika kwenye dini ya kipagani ya Kirumi. Tarakim au nambari ya Mapapa ni Chuo cha Mapapa cha huko Roma kilikuwa ni tarakimu hii ya kumi na tano. Imani au dini ya Siri ya kumuabudu Mungumke kwenye mpangilio wao wa kimaombi ulikuwa pia na jumla ya talasimu hizi 15. Hii imeonekana kuashiriwa kwenye kile kinachoitwa sasa Fumbo la Lozari, ambalo linaendelea bado hadi siku hizi. Desturi ya kimapokeo ya imani hii ya dini ya mungumke yalichukuliwa na kuhamishwa tu na kuvikwa matazamo uliojulikana kama maombi na imani ya Mariamu kwenye kipindi cha karne ya tano na ya sita.

 

Tarakumu ya Namba Kumi na Saba (17) inamaanisha mjumuisho wa Roho na utaratibu (10+7) na ni tarakimu au nambari kuu na ya muhimu ya kumi na saba.

 

Tarakumu ya Namba Ishirini na Mbili (22) ni tarakimu kamilifu nay a mwisho kwenye alfabeti za Kiebrania kwenye konsonanti, na inamaanisha ukamilifu.

 

Tarakumu ya Namba Ishirini na Nne (24) ni tarakimu ya muundo wa utawala kama viumbe wawili walioongezwa kwenye utaratibu au imani ambao msingi wao ni kwa wale kumi na mbili. Kuna migawanyo ishirini na mbili ya makuhani, kila miwili ikisimama kwa kabila moja. Kuwa Wazee ishirini na wanne au elohim mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu wakiwa kama Makuhani Wakuu wanaohudumu kwa kuwaombea watakatifu wa Mungu Aliye Juu Sana.

 

Tarakumu ya Namba Ishirini na Tano (25) ni 5 x 5 au rehema iliyoonekana.

 

Tarakumu ya Namba Ishirini na Saba (27) ni kipimo cha dhiraa 3 na matumizi yake yanahitaji kupimwa kikamilifu na kwa uangalifu mkubwa sana. Ni ashirio au taswira ya kitu kilicho mara tatu cha Mungu na Malaika kwa pamoja pamoja na Roho Mtakatifu.

 

Tarakumu ya Namba Ishirini na Nane (28) ni muundo wa Baraza la Makerubi na inahusiana na uumbaji.

 

Tarakumu ya Namba Ishirini na Tisa (29) ni tarakimu au nambari ya Baraza lililo chini ya Kristo na hukumu ya kimngu.

 

Tarakumu ya Namba Thelathini (30) (3 x 10) ni Halmashauri ya Baraza la Mngu kwenye utaratibu au agizo la mbinguni na serikali (soma jarida la Utawala wa Mungu (Na. 174)).

 

Tarakumu ya Namba Arobaini (40) (10 x 4) ni jumla ya mawazo-dhana ya kutia samadi kwenye mti na kwa hiyo ni kipindi cha matazamio. Kwa hiyo kipindi chote cha matazamio ni 40. Kinaweza kuwa ni cha siku kama ilivyo kwa suala la hukumu ya kila mtu kama tunavyoona habari ya Ninawi (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13)). Inaweza pia kuwa ni kwa kipindi kilicho kwenye majuma, kama tunavyoona kwa baadhi ya makuhani wanaohukumu watu.

 

Pia arobaini ni tarakim ya kizazi. Israeli ilikuwa ni zama ya kizazi cha jangwani walipokuwa Wakitoka utumwani. Miaka arobaini walipewa Yuda tangu mwaka wa 30 BK kwenye tukio la Kusulibiwa hadi siku ya 1 Abibu, mwaka 70 BK wakati ulipozingirwa mji wa Yerusalemu na Jeshi la Warumi lililoongozwa na Jemadari Tito.

 

Kipindi cha Yubile arobaini kimewekwa na kupewa mataifa yote ili yatubu na kuwaleta kwenye kuitumikia amri ya kimbinguni kwa ajili ya kipindi cha mwisho wa Milenia ya sita mnamo mwaka 2027.

 

Tarakimu nne kamilifu za 3, 7, 10 na 12 zina matokeo yaliyo kama matunda yake ya mara saba ya 2,520 (7 x 360). Tatakimu hiii ni ndogo sana kwenye hesabu za mzidisho wa kawaida wa tarakimu kumi zinazoongoza mpangilio wa kimahesabu, na zenye uwezo au zinazoweza kugawanywa kwa kila moja kwa tarakimu tisa bila kukumbushia (Bullinger, ibid.). kwa hiyo ni tarakimu ya ukamilifu wa nyakati.

 

Tarakumu ya Namba Sabini (70) ni tarakimu ya Mabaraza yote kamili ya sehemu zote mbili, yaani ya mbinguni na duniani, na yana nyongeza mbili kama Mungu na Kristo yakifanya kuwepo kwa kinachoijlikana kama Hebdomekonta[duo] au wale wanafunzi sabini na [mbili] wa kwenye Luka 10:1,17.

 

Tarakimu nabari sabini ilikuwa pia ni ya baraza la Sanhedrin au baraza la Wazee wa Israeli, ambalo lilikuwa na jumla ya watu sabini, pamoja na wengine wawili waliokuwa nje ya maskani waliofanya taswira au waliowawakilisha kina Eldadi na Medadi.

 

Mataifa pia walifanya jumla hii ya watu sabini, kama wana wa Mungu walivyochukuliwa kuwa na jumla ya idadi hii ya sabini kwenye mabaraza ambayo Sanhedrin ilikuwa ni nakala. Mataifa haya yapangwa kwa mjibu sawa na idadi ya wana wana wa Mungu; Mungu Aliye Juu Sana au Yahova wa Majeshi, aliyewafanya Israeli kuwa na Yahova mwingine (Kiumbe aliyefanyika baadae kuwa ki Kristo). Kumbukumbu la Torati 32:8 ililisema hilo kwenye maandiko ya kale. Yalibadilishwa na kupotoshwa baada ya kuanguka kwa Hekalu ili kupotosha ukweli hu. Tafsiri ya RSV peke yake ndiyo Biblia pekee iliyo na maneno sahihi kuhusu andiko hili lilivyoandikwa tangu kwenye nakala yake asilia na ambayo imerejesha ukweli huu.

 

Tarakumu ya Namba Mia Moja na Ishirini (120) (12 x 10) ni tarakimu ya serikali iliyoenea. Hii ni tarakimu iliyofuatia kwenye mwandamano wa matukio ya Kanisa.

 

Tarakumu ya Namba Mia Tatu na Sitini (360) ni wakati au kipindi muhimu au mwaka wa kinabii. Ni miezi kamili 12 yenye siku 30. Wakati huo unatumika kwenye unabii na unaweza kumaanisha kuwa ni mwaka, lakini inamaanisha pia kuwa ni miaka 360. Kwa hiyo, usemi wa “wakati, nyakati mbili na nusu wakati” inaweza kuwa ni miaka 1260 au miezi 42, yaani, ni sawa kama, miaka mitatu na nusu. Kwa kawaida ni miaka.

 

Tarakumu ya Namba Mia Tano (500) ni tarakimu inayofuatia tunayoiona kwenye rekodi za watu ambao Kristo waliwatokea baada ya Kufufuka kwake na kujitoa akiwa kama Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa.

 

Tarakumu ya Namba Elfu Moja (1,000) ni tarakimu ya Baaza la Nje lililohusiana na nafasi ya ukombozi (Ayubu 33:23).

 

Uzidishaji wa taraklm hizi kwa 1,000 unaeneza au kuzidisha amri na utaratibu au muundo wa Mungu.

 

Tarakumu ya Namba Elfu Tatu (3,000) lilikuwa ni ongezeko kubwa sana kwa Kanisa kwa siku moja na kunaashiria kufanyika kwa mbadala wa huduma ya makuhani tangu ilipopotea huko Sinai.

 

Tarakumu ya Namba Elfu Kumi na Mbili (12,000) ni tarakimu ya msingi ya viongozi muhimu na wakuu waliowekwa kwenye makabila wakiwa kama viongozi wakutumainiwa na wawakilishi au mawakala wa serikali ya Mungu. Makabila 12 yalipangwa kwa kundi la watu 12,000 kila moja na kufanya idadi ya watu 144,000.

 

Tarakumu ya Namba Mia Moja na Arobaini na Nne Elfu (144,000) ni zao la dhabihu kwa mwaka ikiunda baraza la wajmbe 72, wakiwa ni matokeo ya mundo mzima wote ulio nje ya Mungu na Kristo kwa kupitia Roho Mtakatifu.

 

Kuna Sabato 52 kwenye mwaka wa kinabii pamoja na Miandamo ya Mwezi Mpya 12 na dhabihu za Sikukuu saba au sadaka. Idadi ya jumla ya 71 pamoja na Sadaka ya Mganda wa Kutikiswa inafanya jumla ya wanadamu viongozi wakamilifu 72 au sadaka au sadaka kwa Mungu kwa kipindi cha zaidi ya Yubile arobaini za Kanisa kuwa jangwani. Idadi kamili ya watu 144,000 (soma jarida la Mavuno ya Mungu, Dhabihu za Miandamo ya Mwezi Mpya, na Wale 144,000 (Na. 120)).

 

Kusanyiko Kuu linahusiana na utoaji wa adaka za daima na hazihesabiki kwa kuwa Israeli hawahesabiki.

 

Hekalu aliloonyeshwa nabii Ezekieli linaonyesha kuwa nusu ya utaratibu utakaofanyika kwenye kipindi cha utawala wa millennia, itafanya mavuno haya yaendelee hadi kwenye Ufufuo wa Pili wa Wafu (soma jarida la Ufufuo wa Wafu (Na. 143)).

 

Mji wa Mungu umefanywa kwa uwanja unaolingana na idadi hii ya hawa 144,000 x 2 na Malaika. Soma jarida la Mji wa Mungu (Na. 180).

q