Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[021K]
Ufafanuzi
wa Kitabu Cha Zekaria
(Toleo
La 2.5 20060820-20120114-20140905)
Kitabu cha Nabii Zekaria
ni cha muhimu sana ili kujua fundisho la Marejesho Mapya au Kufanywa Upya kwa
taifa la Israeli kutakakofanywa na Masihi katika Siku za Mwisho. Angalia pia
Sehemu ya II ihusuyo hatima ya Israeli na Yuda itakavyokuwa katika Siku za
Mwisho kwenye maandiko ya Zekaria na kwenye Agano Jipya.
(Sheria ya
Haki Miliki © 2006, 2012, 2014 Wade Cox)
(tr. 2012)
Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na
kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu
Jarida hili
linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org
Ufafanuzi wa Kitabu cha Zekaria
Utangulizi
Nabii Zekaria (maana
ya jina lake ni Aliyekumbukwa na Yahova)
alikuwa mwana wa Berekia (Aliyebarikiwa
na Yahova) na ni mjukuu wa Ido.
Alitoa unabii wake
kipindi cha utawala wa Dario Mwajemi au pia anaitwa Dario II wa Uajemi wakati
wa ujenzi wa Hekalu. Unabii alioutoa katika kipindi chote cha tangia ujenzi wa
Hekalu la Pili hadi kukamilika kwake kulikofanywa kwa kulipaka rangi na
kulipamba na aliendelea kutabiri hali itakavyokuwa tangia hapo hadi kuteketezwa
kwa Hekalu hili. Kwa hiyo, unabii wake unaendelea hadi kufikia kipindi cha
Masihi na ujenzi wa Kanisa la Mungu, ambalo ni Hekalu la Kiroho, na aliendelea
kuyataja mambo yatakavyokuwa hadi kipindi cha kurudi kwake huyo Masihi. Pia
inahusika na matengenezo ya mfumo wa uongozi utakavyokuwa mjini Yerusalemu katika
kipindi cha utawala wa Milenia wa Masihi. Ni kazi ya muhimu sana katika Siku za
Mwisho na kwa mataifa yatakayoishambulia Yuda.
Mpangilio wa
kitabu umegawanyika kwenye vipengele vifuatavyo:
Sehemu ya 1 A.
1:1-6 Unabii alioutoa katika Mwaka wa 2 wa Dario
B. 1:7-6:15 Unabii Kwa Njia ya Alama za Maono (Maono ya mambo Saba)
C. 7:1-8:23 Unabii wa tangia Mwaka wa 4 wa Dario
Sehemu ya 2 A.
9:1-10:12 Mzigo wa Kwanza Unafumbuliwa
B. 11:1-17 Unabii kwa njia ya Alama au Ufunuo
C. 12:1-14:21 Mzigo wa Pili Unafumbuliwa
Kipindi cha Dario na Manabii
Inadhaniwa kuwa Dari
II alitawazwa kuwa mfalme kwenye kipindi cha miaka ya 424 au mapema 423KK. Tangazo
la kuanza ujenzi wa Hekalu alilifanya mwaka 422KK (Ezra 6:1 na 4:24) (huenda ulikuwa
ni mwaka wake wa pili wa utawala wake). Majuma 70 ya miaka yalitangulia kabla
ya kufika siku hii. Kwa mujibu wa Ezra sura ya 5, inaonekana kuwa manabii Hagai
na Zekaria walitabiri kwenye miaka ya 423KK na 422KK. Majuma 70 ya miaka
ilitangila na kupita tangu mwaka 423/22KK (ambacho ni kipindi cha mwaka wa
kwanza wa Yubile mpya). Ujenzi huu wa Hekalu ulikamilika katika mwaka was ita
wa utawala wa Dario Mwajemi (Ezra 6:15) siku ya 3 Adari sawa na Machi ya mwaka 418KK.
Dario alikufa katika kipindi cha mwishoni mwa mwaka 405 katika kipindi cha
majira ya baridi ya mwaka 404 (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya
wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the
Reconstruction of the Temple (No. 13)]: Kwa jinsi hii twaweza kusema kuwa kazi ya
upangaji wa miaka aliyoifanya Bullinger imekosewa kwa jinsi inavyofanana na
nyongeza ya maandiko iliyowekwa.
Kwa hiyo, unabii
huu unatuama kwenye kipindi cha ujenzi wa Hekalu na unafanya kuwa ni sehemu muhimu
ya dhana ya Ufunguo wa Daudi iliyo kweny maelezo ya unabii huu na maongozi
yanayotupeleka kwenye Siku za Mwisho na majenzi mapya ya mwisho ya Hekalu (soma jarida la Sheria za Wafalme: Sehemu ya II; Sulemani na Ufunguo wa Daudi (Na. 282C)
[Rule of the Kings: Part III: Solomon and the Key
of David (No. 282C)].
Sehemu ya kwanza
inaonyesha mwanzoni mwa ujenzi na inaishia mwaka wa 2 wa ujenzi huu na kuachia
njiani mwa tukio hili. Sehemu ya pili inaonyesha sehemu ya pili ya ujenzi huu.
Kwa hiyo, kila sehemu inajiri kipindi cha miaka miwili kati ya mine iliyotumika
kwa ujenzi huu na kwenye unabii imetajwa kuwa ni kipindi cha marejesho ya taifa
la Israeli a Yuda wakati wa utawala wa Msihi, na kanisa lililotajwa hapa kwenye
maandiko ni lile litakalotawala na Masihi kipindi hiki cha Milenia huko mjini
Yerusalemu.
Kwenye unabii
wake Hagai anahusisha kipindi hiki kama tulivyojionea.
Ezra na Nehemia
walikuwa hawajarudi bado, jambo walilolifanya kwenye siku za utawala wa Artashasta
II mwishoni mwa kipindi cha majuma saba ya miaka. Artashasta II ndiye aliyetoa
tangazo la kwa ajili ya Hekalu na Nehemia akalijenga. Ezra alifariki mwaka 323KK
ambao pia ni mwaka aliokufa Iskanda Mkuu (Alexander the Great). Mkakati wa
kuyachunguza maandiko maarufu kama “canon” uliafanywa mwaka 321 na hatimaye
ulitangazwa kusitishwa.
Zekaria, sura ya 1
Sura ya 1 inahusika
na kuanzishwa kwa huduna ya kinabii na kipindi tajwa ambacho mji ungefanyiwa
marejesho lakini ukiwa hauna amani, na kwahiyo Hekalu lisingeweza kujengwa. Mungu
aliwakasirikia Yuda kwa kuwa hawakuwafundisha kanuni zake na Amri za Mungu
vizuri, na pia hawakuzitenda. Dunia ilikuwa na amani lakini Nyumba ya Yuda
hawakuwa na mapumziko ya amani kwa muda wa miaka saba. Mungu hakupendezwa na mataifa
wasiyo Waisraeli pia ambayo walijihisi kuwa wako salama. Ni kama tunavyojionea
kwenye maandiko, alikuwa amewakasirikia kidogo bali walijiongezea hasira yake
jambo lililopelekea wakutane na hukumu kali na mateso, mambo ambayo Mungu
hakuwaambia wafanye. Kisha zile pembe nne zilizofanya hila ya kuwatawanya Yuda,
Israeli na Yerusalemu zilishughulikiwa, na mafundi seremala wanne ambao ni
watumishi wa Mungu walikuja kuwatawanya waende kwenye zile pembe nne
zilizofanya hila ya kuwatawanya na kuwagawa Yuda.
Jina hili
la Bwana wa Majeshi au Yahova Sabaioti limeandikwa mara hamsini
na tatu kwenye kitabu hiki: mara arobaini na nne kwenye sura ya 1 hadi 8 na mara
tisa kwenye sura za 9 hadi 14. Mara zote ishirini na tisa zilizoandikwa
imehusianishwa na maneno yenye msisitizo ya Yahova Sabaioti pale inaposema
“Asema Bwana wa Majeshi” ni sawa na kusema kwamba maneno haya yamesemwa na
kuthibitishwa Yahova Sabaioti. Usemi wa “Asema Bwana” unamaana sawa na kusema “Haya ni Maneno yaliyothibitishwa
na Yahova” au Matamshi ya Yahova.
Mpangilio wa
jinsi maono aliyoyaona mara nane hadi kwenye Zekaria 6:15 yanaonyesha mambo
yafuatayo:
Maono ya 1 (Zekaria
1:7-17) Jeshi Lisiloonekana na Farasi Mweusi.
Maono ya 2 (Zekaria
1:18-21) Maadui wa Nje au Pembe Nne
Maono ya 3 (Zekaria
2:1-13) Kusudi la Yahova kwa mwanadamu linaonyeshwa.
Maono ya 4 (Zekaria
3:1-10) Kuonekana kwa Yoshua ambaye ni Chipukizi.
Maono ya 5 (Zekaria
4:1-14) Mpango wa Yahova unaonekana kwenye Kinara cha Taa
Manono ya 6 na 7
(Zekaria 5:1-4, 11) Maadui wa Nje, Gombo Lirukalo na Efa
Maono ya 8 (Zekaria
6:1-6) Magari ya Vita, Farasi
Kwa kuhitimisha, (Zekaria
6:9-15): Inaishia kwa kumfananisha Yoshua ambaye ni Chipukizi.
Mpangilio
uliowekwa ni ule wa Israeli na mtawanyiko wao. Wamataifa wanakuwa ni milki ya
Israeli kwenye kipindi hiki cha mwisho Yahova anatangaza nia yake ya kuingilia
kati mambo yalivyo mjini Yerusalemu (aya za 16,17; Isa. 40:1-5). Mtu aliye
kwenye sura ya 1 ni Adonai wa aya ya 9 na ni Malaika wa Yahova kwenye aya za 11,12
na tunaona jinsi nabii alivyoambiwa kwenye jibu lake. Wale wapanda farasi wote
wanayeoonekana kwenye aya ya 8 wanatoa habari zao kwa kiumbe hiki ambaye ni Adonai
wa Israeli anayetajwa kwenye Kumbukumbu la Torati 32:8. Neno “miongoni” linahusiana
na sura ya 6:1.
Zekaria 1:1-21 inasema: 1Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa mfalme
Dario, neno la BWANA lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Iddo,
kusema: 2“BWANA aliwakasirikia
sana baba zako wa zamani. 3Kwa
hiyo waambie watu: Hivi ndivyo BWANA Mwenye Nguvu asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’
asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘Nami nitawarudia ninyi,’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 4Msiwe kama baba zenu, ambao manabii
waliotangulia waliwatangazia: Hivi ndivyo BWANA Mwenye Nguvu asemavyo:
‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini
hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asema BWANA. 5Wako wapi baba zako sasa? Nao
manabii, je, wanaishi milele? 6Je,
maneno yangu na amri zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu, hayakuwapata
baba zenu?’’ “Kisha walitubu na kusema, ‘BWANA Mwenye Nguvu ametutenda
sawasawa na njia zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama alivyokusudia
kufanya.’
Miezi mitatu
baadae sehemu ya kwanza iliisha.
7Katika siku ya
ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja,yaani mwezi uitwao Shebati, katika
mwaka wa pili wa kutawala kwake mfalme Dario, neno la BWANA lilimjia nabii
Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Iddo. 8Wakati
wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu!
Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake
walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe. 9Nikauliza, ‘‘Hivi ni vitu gani bwana wangu?’’ Malaika aliyekuwa
akizungumza na mimi akanijibu, ‘‘Nitakuonyesha kuwa ni nini.’’ 10Kisha yule mtu aliyesimama katikati
ya miti ya mihadasi akaeleza, ‘‘Ni wale ambao BWANA amewatuma waende duniani
kote.’’ 11Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika wa BWANA, aliyekuwa
amesimama katikati ya miti ya mihadasi, ‘‘Tumepita duniani kote na kukuta
ulimwengu wote umepumzika kwa amani.’’ 12Kisha
malaika wa BWANA akasema, ‘‘BWANA Mwenye Nguvu, utazuia mpaka lini rehema
kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?’’
Sehemu
ya pili inaonyesha kipindi cha taabu. Pia inaonyesha kurejea kwenye sura ya 7:9; Zaburi102:13; Isaya 14:1; 49:13. maandiko
haya hayalihusu Kanisa ambalo ni mama yetu sote, bali zinauhusu mji wa Yeruralemu
wenyewe.
13Kwa hiyo BWANA
akazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami. 14Kisha malaika yule aliyekuwa
akizungumza nami akasema, ‘‘Tangaza neno hili: Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu
asemalo: ‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na Sayuni, 15lakini nimeyakasirikia sana mataifa
yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu,
lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.
Kwahiyo, Mungu
anawashughulikia Yuda, lakini mataifa yaliyoongeza maumivu wakati walikuwa
hawana la kufanya na hivyo walimchukiza Mungu na atawashughulikia.
Sehemu hii
ilikuwa inatazama mbele kwenye mtawanyiko mwingine. Hapa anaongelea kuhusu nyumba
yake inayojengwa juu yake, ambayo kwa sasa inaendelea kujengwa. Hata hivyo, tutajionea
jinsi unabii huu unavyoendelea hadi kwenye kipindi cha milenia moja na nusu na
kinaendelea hadi kwenye vipindi viwili vya kuja kwake Masihi na hadi alipokufa.
Mji wa Yerusalemu
utapimwa kwa nia ya kuweka tena utaratibu ufaao kwenye jingo hili. Tendo hili
litafuatiwa na Upimaji wa Hekalu ambalo ni Kanisa tuliloliona kwenye
Ufunuo 11:2.
16‘‘Kwa hiyo, hivi ndivyo
asemavyo BWANA: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu
itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa Yerusalemu,’ asema BWANA
Mwenye Nguvu. 17“Endelea
kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Miji yangu
itafurika tena usitawi na BWANA atamfariji tena Sayuni na kumchagua
Yerusalemu.’’’ 18Kisha
nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne! 19Nikamwuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini
hivi?’’ Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na
Yerusalemu.’’ 20Kisha BWANA
akanionyesha mafundi wanne. 21Nikauliza,
“Hawa wanakuja kufanya nini?’’ Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya
Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja
kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao
dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.’’
Hapa Mungu
anaonyesha kwamba atashughulikia pembe hizi au mamlaka ya wale wote
waliowaumiza na kuwatesa Yuda na Israeli na Yerusalemu. Hii haina uhusiano
wowote na Kanisa (kama anavyosema Bullinger, kwenye ufafanuzi wake wa Biblia
iitwayo Companion Bible anapoitafsiri aya 16). Mamlaka hizi nne
yanajichomoza ili kuyapiga vita mataifa yatakayoishughulikia, kwa nia ya
kuyafanyia vitisho.
Zekaria, sura ya 2
Sura hii ya 2 inaonyesha
kuwa Yuda wataongezeka na Mungu atakuwa ni ukuta wa moto utakaowazunguka na na
utukufu wake utakuwa katikati yao. Andiko hili linaonysha kwamba Mungu, yaani Yahova,
Bwana wa Majeshi, alimtuma Yahova ambaye ni Mungu wa Israeli aende mjini
Yerusalemu ili akaulinde (Zekaria 2:8). Mataifa mengi yatajiunga na Bwana katika
siku ile na watakuwa watu wake Mungu na Yahova atakuwa kati yao. Mungu
ataimiliki Yuda, ambayo ni milki yake kwenye Nchi Takatifu na ataupenda na
kuuchagua tena Yerusalemu (kana isemavyo Kumbukumbu la Torati 32:8).
Zekaria 2:1-13 inasema:
Kisha nikatazama juu, pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia
mkononi mwake! 2Nikamwuliza,
“Unakwenda wapi?’’ Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.’’
3Kisha malaika aliyekuwa akizungumza
nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye 4na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa
mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo. 5Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto
kuuzunguka,’ asema BWANA, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’ 6“Njoni! Njoni! Kimbieni mtoke katika
nchi ya kaskazini,’’ asema BWANA, “Kwa kuwa nimewatawanya kwenye pande nne za
mbingu,’’ asema BWANA. 7“Njoo,
Ee Sayuni! Kimbia, wewe uishiye ndani ya Binti Babeli!’’ 8Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo BWANA
Mwenye Nguvu: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa
yaliyokuteka wewe nyara, kwa kuwa ye yote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya
jicho lake, 9hakika nitauinua
mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo mtakapojua ya
kwamba BWANA Mwenye Nguvu amenituma. 10“Piga
kelele na ufurahie, Ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni
mwenu,’’ asema BWANA.
Kumbuka hapa
kwamba Yahova ambaye ni Bwana wa Majeshi atakuwa anaishi Yerusalemu. Anasema
kwamba hatimaye tutajua kwamba Bwana wa Majeshi amemtuma. Kwa maneno mengine ni
kusema kwamba huyu Yahova sio huyu Yahova ambaye ni Bwana wa Majeshi asemwaye
kwenye Zaburi 45:6-7 na Waebrania 1:8-9 aliyetumwa na Mungu kwa Israeli. Bali
ni Yahova aliyepewa Israeli kuwa ni urithi wake kama isemavyo Kumbukumbu la torati
32:8 (pia soma Biblia ya RSV ili kupata maana halisi). Maneno yasemayo “mboni
ya jicho langu” yalibadilisha na kusomeka “jicho lake” kazi ambyo ilifanywa na Wasoferim
waliodai ni kwa sababu za kielimu ya kianthropolojia. Yahova ambaye ni Bwana wa
Majeshi alimtuma huyu Yahova kwa “Utukufu wake Mwenyewe”.
Maonyo yametolewa
dhidi ya wale wote wanaoishi na kumrithia binti wa Babeli wakiepuka kutoka
pande ya Kaskazini. Zekaria anaongelea mambo yatakayotokea siku za baadae sana.
Babeli itakuwa imeshaanguka tayari kipindi hiki na ni somo kwa dola za Wamedi
na Waajemi na imekuwa hivyo kwa karne sasa. Anaongelea kuhusu Siku za Mwisho na
binti Babeli anatajwa pia kwenye sehemu nyingine na Kanisa.
Tunajua kuwa hiki
ni kitu muhimu kwa kuwa ni unabii na kisha inatangaza umoja wa mataifa mengi na
hata Yuda, mambo ambayo hayajatokea bado hata kwa matukio ya kwanza. Anasema
kuwa atakaa kati yao nao watajua kwamba Bwana wa Majeshi amemtuma yeye kwao.
Mtu huyu anaweza kuwa ni Yesu Kristo atakayekaa kati yao hapo ajapo tena.
11“Mataifa mengi yataunganishwa na BWANA siku hiyo, nao watakuwa watu
wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwamba BWANA Mwenye Nguvu amenituma
kwenu. 12BWANA atairithi Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na atachagua
tena Yerusalemu. 13Tulieni mbele za BWANA, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka
kutoka makao yake matakatifu.”
Kumbuka maelezo
yasemayo kuwa ataimiliki Yuda na kuifanya kuwa ni sehemu yake. Israeli ni milki
yake lakini Yuda ni kabila la Masihi. Mtu huyu, Yahova wa Israeli, anaweza kuwa
ni Yesu tu ambaye ni Kristro na Masihi.
Zekaria, sura ya 3
Kwenye sura ya 3
ya Zekaria, Bwana Mungu anaonyesha jinsi utakavyokuwa mwanzo wa siku za mwisho pamoja
na jinsi atakavyokuwa Kuhani Mkuu atakayekuwa anaitwa Yoshua, kama alivyofanya
Masihi ambaye alionekana kama Chipikizi. Shetani amekaa mkono wake wa kulia
akikusudia kumzuia na sio kumsaidia. Yoshua amepewa mavazi safi na meupe na
mavazi yake ya zamani yameondolewa mbali. Wafuasi na ambao pia watumishi wa
Kuhani Mkuu walioketi mbele yake ni watu wanaofanya mambo ya kushangaza. Bwana
Mungu anasema kwamba atalileta Chipukizi ambaye ni Masihi. Bwana Mungu anasema
kwamba jiwe lililowekwa mbele ya Yoshua lina macho saba kwenye jiwe moja
hilihili, ambayo inamaanisha pia kwamba kuna macho saba kwenye kila jiwe moja,
na tunajua kuwa maandiko yanatuambia kuna roho saba za Mungu ambazo
zinawakilisha pia malaika saba wa makanisa saba ya Mungu na kuna vinara vya taa
kwenye makanisa haya yote saba.
Ni Mungu ndiye
anayeyafanya mawe haya na kuyaweka macho saba, ambayo inamaanisha pia kuwa ni
roho saba. Mungu anayaondoa maovu ya nchi kwa siku moja tu. Alifanya hivyo
kupitia kwa Masihi na kuweka roho saba kwenye makanisa saba.
Aya ya 10 inasema:
‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu
wake na mtini wake,’ asema BWANA Mwenye Nguvu.
Jambo hili linaashiria
kuanzishwa kwa makanisa ka kipindi chote na kutuleta kwenye ile Siku ya Bwana,
siku ambayo imetajwa pia kwenye aya ya 10 kama: “Katika siku hiyo”.
Zekaria 3:1-10 inasema: Kisha akanionyesha Yoshua kuhani mkuu akiwa
amesimama mbele ya malaika wa BWANA, naye Shetani amesimama upande wake wa
kuume ili amshitaki. 2BWANA
akamwambia Shetani, “BWANA akukemee Shetani! BWANA, ambaye ameichagua
Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa
kwenye moto?’’ 3Wakati huu,
Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. 4Malaika akawaambia wale waliokuwa
wamesimama mbele yake, ‘‘Mvueni nguo zake chafu.’’ Kisha akamwambia Yoshua,
‘‘Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.’’ 5Kisha nikasema, “Mvike kilemba
kilicho safi kichwani mwake.’’ Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na
kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa BWANA akiwa amesimama karibu. 6Malaika wa BWANA akamwamuru Yoshua: 7“Hivi
ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na
kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya
nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa. 8 ‘‘‘Sikiliza, Ee Yoshua kuhani mkuu,
pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu ishara ya mambo
yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi. 9Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya
jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema BWANA Mwenye Nguvu,
‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja. 10“‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae
chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema BWANA Mwenye Nguvu.
Ni hakika kabisa
kwamba Kuhani Mkuu wa Israeli ni lazima aendane kwa mujibu wa Torati ama Sheria
za Mungu. Kazi hii ndiyo aliyoitoa Mungu na kumpa Yoshua, aliye Kuhani Mkuu wa
Israeli. Na kama hataifuata Torati hii ya Mungu basi hafai kuwa Kuhani Mkuu.
Zekaria, sura ya 4
Sura hii ya 4 inaendelea
kwa kuwaelezea Mashahidi wasimamao upande mwingine wa vile vinara saba vya taa
vinavyowaka kwenye kinara chake. Kupitia Zekaria, Mungu anasema hivi: “‘Si kwa nguvu, wala si
kwa uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu.” Hawa ndio Mashahidi Wawili wanaosimama
mbele za Bwana wa dunia nay ale macho saba ni roho saba za Mungu zinzoenda huku
na huko duniani kote. Huyu sio Shetani anayetajwa kama “Mungu wa dunia hii” (2Kor.
4:4) bali ni Masihi ambaye atachukua nafasi yake. Hii ndio sura inayoielezea sana
Siku ya Bwana na Ushindi wa Mashahidi wake utakavyokuwa kwenye Siku za Mwisho.
Zekaria 4:1-14 inasema: Kisha
malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka
katika usingizi wake. 2Akaniuliza,
“Unaona nini?’’ Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina
bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta
mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake. 3Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa
bakuli na mwingine upande wa kushoto.’’ 4Nikamuuliza
malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?’’ 5Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu
gani?’’ Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.’’ 6Kisha akaniambia, “Hili ni neno la BWANA kwa Zerubabeli: ‘Si kwa
nguvu, wala si kwa uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 7‘‘Wewe
ni kitu gani, Ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi
tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele
wakisema, ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’’ 8Kisha neno la BWANA likanijia: 9‘‘Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa hekalu hili, mikono yake
pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwa BWANA Mwenye Nguvu amenituma mimi kwenu.
10‘‘Ni nani anayeidharau siku ya
mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli.
“(Hizi saba ni macho ya BWANA ambayo huzunguka duniani kote.)’’ 11Kisha nikamwuliza yule malaika, “Hii
mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni
nini?” 12Tena nikamwuliza, “Haya
matawi mawili ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya dhahabu inayomimina
mafuta ya dhahabu ni nini?’’ 13Akajibu,
“Hujui kuwa haya ni nini?’’ Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.’’ 14Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili
ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.’’
Mashahidi hawa wawili watakuja mwishoni mwa matukio haya
na hawajafananishwa na mtu mginine yeyote tangu hapo hadi leo.
Zekaria, sura ya 5
Gombo la Bwana
lililoko kwenye Torati ya Mungu, litapeperuka na kuingia kwenye majumba ya wezi
na waongo na litatoa ushuhuda dhidi yao na kuwatawanya na kuwakomesha na
kuziteketeza nyumba zao kwa mawe na kwa matofali.
Umuhimu wa
kuitunza na kuiamini Torati utarejeshwa upya na Mashahidi hawa wa Mungu katika
Siku za Mwisho. Sura ya 5 inafuatia moja kwa moja kwenye kipindi kinachowaelezea
wao kwenye Sura ya 4 na haiyarudii mambo ya nyuma. Hali hii bado haijafanyika
hadi sasa.
Mashahidi hawa wa
Bwana waliharibiwa na kufanywa kuwa kama efa isiyofaa na kuwekwa mdomoni mwa
mwanamke anayeishi kwa kutenda matendo machafu, na mkate huu wa efa
ukachukuliwa na kupelekwa katika nchi ya Shinari, ambayo ndiyo Babeli.
Ndiyo maana ya
kutokea kwamba, mfumo wa dini ya uwongo ukapata nafasi ya kuwa msemaji na kutoa
unabii wake, na kuchukuliwa kwenye mfumo potofu wa dini ya Babeli na kisha
watahukumiwa katika Siku za Mwisho. Hawa ndio wale waantinomia wanaofundisha
leo kuwa Torati na Amri zote za Mungu zimeondolewa na hazima umuhimu tena siku
hizi.
Zekaria 5:1-11 inasema: Nikatazama tena, mbele yangu kulikuwa na kitabu
kilichoruka! 2Akaniuliza, “Unaona nini?’’ Nikamjibu, “Naona kitabu
kinachoruka chenye,urefu wa dhiraa ishirinia na upana wa dhiraa kumib.’’ 3Akaniambia,
“Hii ni laana inayotoka kwenda juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale
yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila mwizi atahamishwa, pia kufuatana na
yaliyo upande wa pili, kila aapaye kwa uongo atahamishwa. 4BWANA Mwenye Nguvu asema, ‘Nitaituma
hiyo laana, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi na nyumba ya huyo aapaye kwa
uongo kwa jina langu. Itabaki katika nyumba yake na kuiharibu, pamoja na mbao
zake na mawe yake.’’’ 5Kisha
yule malaika aliyekuwa akizungumza nami akanijia na kuniambia, “Tazama juu uone
ni nini kile kinachojitokeza.’’ 6Nikamwuliza,
“Ni kitu gani?’’ Akanijibu, ‘‘Ni kikapu cha kupimia.’’ Kisha akaongeza kusema,
‘‘Huu ni uovu wa watu katika nchi nzima.’’ 7Kisha kifuniko
kilichotengenezwa kwa madini ya risasi kilichokuwa kimefunika kile kikapu,
kiliinuliwa na ndani ya kile kikapu alikuweko mwanamke ameketi! 8Akasema, ‘‘Huu ni uovu,’’ akamsukumia
ndani ya kikapu na kushindilia kifuniko juu ya mdomo wa kikapu. 9Kisha nikatazama juu na mbele yangu,
walikuwepo wanawake wawili, wakiwa na upepo katika mabawa yao! Walikuwa na
mabawa kama ya korongo, nao wakainua kile kikapu na kuruka nacho kati ya mbingu
na nchi. 10Nikamwuliza yule
malaika aliyekuwa akizungumza nami, ‘‘Wanakipeleka wapi hicho kikapu?’’ 11Akanijibu, ‘‘Wanakipeleka katika
nchi ya Babeli na kujenga nyumba kwa ajili yake. Itakapokuwa tayari, kikapu
kitawekwa pale mahali pake.’’
Zekaria, sura ya 6
Zekaria 6:1-8 inaelezea
kiindi ambacho malaika saba wanaotajwa pia kwenye Ufunuo 7:1-3. Malaika hawa
wanne wanaonekana wapo kwa pea iliyopanda farasi Mwekundu, Mweusi na Mweupe nay
ule wa nne anaonekana amepanda gari lililotengenezwa kwa vitu mchanganyiko wa rangi
za Zambarau au Dam una Hudhurungi (iliyonakshiwa
kwa kupakwa neno linalotokana na Kifaransa gris au chuma chenye rangi ya hudhurungi).
Yule aliyempanda
farasi mweusi anaelekea upande wa kaskazini mwa nchi, na yule mweupe anaelekea
magharibi, na yule wa rangi ya hudhurungi
au kahawia-kidogo anaelekea kusini
mwa nchi, anaenda huku na huko duniani.
Neno la kuisimamisha roho yangu upande wa kaskazini
wa nchi linamaanisha “kunikasirisha [kunikasirisha] nisistarehe kwenye roho
yangu (kama alivyoandika Bullinger, kwenye Biblia yake maarufu kama Companion Bible). Kwa hiyo, Mungu
anataka kuishughulikia Nchi ya Kaskazini. Hekalu la Bwana ni lazima lijengwe na
litajengwa na watu watakaotokea nchi ya mbali (kama inavyosema Isaya 60:10) na ni
Chipukizi aitwaye Yoshua, Kuhani Mkuu atakayelijenga Hekalu. Kwa hiyo,
anatakiwa awe na Masihi aitwaye Yoshua, ambaye maana yake ni wokovu au Mwokozi. Hii itakuja kutokea ikiwa tu kama tutakaza mioyo yetu
kumsikiliza na kumtii Mungu.
Zekaria 6:1-15 inasema: Nikatazama juu tena, nikaona mbele yangu magari
manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba! 2Gari la kwanza lilivutwa na farasi
wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, 3la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na
farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. 4Nikamwuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, ‘‘Hawa ni nani
bwana wangu?’’ 5Malaika
akanijibu, ‘‘Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa
dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. 6Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya
kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya
kijivu linaelekea kusini.’’ 7Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa
wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, ‘‘Nenda duniani
kote!’’ kwa hiyo wakaenda duniani kote. 8Kisha
akaniita, “Tazama, wale wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha
Roho yangu katika nchi ya kaskazini.’’ 9Neno
la BWANA likanijia kusema: 10‘‘Chukua
fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa yaani Heldai, Tobia na Yedaya
ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa
Sefania. 11Chukua fedha na
dhahabu utengeneze taji, nawe uiweke kichwani mwa kuhani mkuu Yoshua, mwana wa
Yehosadiki. 12Umwambie, hili
ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi,
naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga hekalu la BWANA. 13Ni yeye atakayejenga hekalu la
BWANA, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye
atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao
wawili.’ 14Taji itatolewa kwa
Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya hekalu
la BWANA. 15Wale walio mbali
sana watakuja na kusaidia kulijenga hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kwamba
BWANA Mwenye Nguvu amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii BWANA, Mungu
wenu kwa bidii.’’
Huyu Chipukizi amepewa
heshima ya kifalme katika Israeli na kuhani atasimama kwenye kiti chake cha
enzi. Kutakuwa na amani kati yao. Unabii huu unahusu siku zijazo kipindi
ambacho Chipukizi huyu atajenga Hekalu lake akiwa na heshima ya kifalme na
akiwa ni mtawala atawalaye kama kuhani pia, na mtu huyu ni lazima awe Masihi
tu. Taji ya kifalme itakuwa kwenye Hekalu la Bwana. Wateule watatawala na Mungu
na taji za kifalme watavikwa ili watawale. Hii ndiyo ahadi lililopewa Kanisa la
Wafiladelfia kwenye Ufunuo sura ya 3.
Usemi usemao kuchipushwa
kwa chipukizi la Yemach ... yizmach ambayo maana yake ni
kusema kwamba chipukizi litachipuka.
Bullinger anauona ukweli huu pia na kwenye kitabu chake ameruka maandiko fulani
alipokuwa anaelezea hili.
Zekaria, sura ya 7
Katika kipindi
hiki cha miaka saba Israeli hawakufunga saumu wala kuomboleza kwa ajili ya
kutubia matendo yao ya kuenenda kinyume cha Torati ya Mungu. Na kwa mafungo yao
ya mwezi wa Tano na Saba hawakufunga saumu ili kumtii Mungu. Kumbuka kwamba
saumu ya siku ya 10 ya mwezi wa Abu waliyoifanya ili kuomboleza kwa ajili ya
kuteketezwa kwa Hekalu ilianzhishwa katika Yuda kipindi hiki (kama isemavyo Yer.
52:12,13). Neno la Bwana lilikuwa ni kufanya hukumu ya haki na kuonyesha rehema
na huruma kwa kila mtu na jirani yake, na kutowadhulumu wajane na kwa yatima
waliofiwa na baba zao na kwa mgeni na kwa maskini na kuwaasa kusiwe na mtu
miongoni mwao mwenge kumuwazia moyoni mwake mabaya ndugu (Zekaria 7:9-10). Lakini
hawakusikia bali wakazifanya shingo zao kuwa ngumu na kuziba masikio yao ili
wasisikilize. Waliifanya mioyo yao kuwa migumu kama jiwe, na kama mwamba, ili
wasizisikilize Sheria za Mungu na wasiyasikilize maneno ambayo Bwana wa Majeshi
aliyoyaleta kwao akiwatumia manabii zake
aliowapeleka kwao hapo kabla. Kwa ajili hiyo hasira kali kutoka kwa Bwana wa
Majeshi iliwaangukia (Zekaria 7:11-12).
Mungu anasema
kwamba itakuja kutokea kwamba, kwa kuwa wanakaza kuyaziba masikio yao ili
wasisikilize Amri za Mungu alizozileta kwao kwa kupitia manabii waliotangulia,
basi Mungu naye atafunga masikio yake asiwasikilize,, na Mungu akawatawanya
watoke na waende mbali kwenye mataifa yote ya dunia ili ardhi yao ibaki kuwa
ukiwa. Na kwa jinsi hiyohiyo ndivyo Mungu atawahukumu wale wote wanokataa kulisikiliza
Neno lake yeye ambaye ni Bwana na na Amri za Mungu katika Siku za Mwisho.
Zekaria 7:1-14 inasema: Katika mwaka wa nne wa utawala wa mfalme Dario,
neno la BWANA lilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu. 2Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma
Shareza na Regam-meleki pamoja na watu wao, kumsihi BWANA 3kwa kuwauliza makuhani wa nyumba ya
BWANA Mwenye Nguvu na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi
wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?” 4Kisha neno la BWANA Mwenye Nguvu
likanijia kusema: 5“Waulize watu
wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na
wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu? 6Na mlipokuwa mkila na kunywa, je,
hamkuwa mnasheherekea kwa ajili ya nafsi zenu? 7Je, haya sio maneno ya BWANA aliyosema kupitia manabii
waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika
hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefala zikiwa zimekaliwa na
watu?’’’ 8Neno la BWANA likamjia
tena Zekaria: 9“Hivi ndivyo
asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na
huruma ninyi kwa ninyi. 10Msimwonee
mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi
kwa ninyi.’ 11“Lakini wakakataa
kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao. 12Wakaifanya mioyo yao migumu kama
jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo BWANA Mwenye Nguvu
aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo BWANA
Mwenye Nguvu alikasirika sana. 13‘Wakati
nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asema BWANA
Mwenye Nguvu. 14‘Niliwatawanya
kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa
wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au
kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’’’
Katika Siku za
Mwisho, Mungu atashughulika na mabaki ya Israeli. Unabii huu uko kwenye sehemu
ya pili au ya mwisho maono ya sehemu ya kwanza. Inauonyesha mtawanyiko
unaofuatia na jinsi Yuda utakavyoachwa unaangamia na jinsi Hekalu
litakavyoangushwa na kuangamizwa ambalo walikuwa kwenye mchakato wa kulijenga. Jambo
la kujifunza hapa lilikuwa ni rahisi sana. Ni kwamba walitakiwa kuzishika tu
Amri za Mungu na Agano lake vinginevyo wangechukuliwa tena kutumikia adui zao.
Hekalu hili linawahusu wale tu wanaolituza Agano na kuzishika Amri za Mungu.
Zekaria, sura ya 8
Katika sura ya 8
Zekaria anaonyesha jinsi Mungu anavyoharakisha kurejea Sayuni na kuwakusanya
watu wake kutoka nchi liyo upande wa mashariki na wa magharibi. Watarudi na
kukaa mjini Yerusalemu kwa hali isiyo na hofu na haki. Kabla ya marejesho ya
mwisho hakukuwa na amani na Mungu alimfanya kila mmoja wao amchukie jirani
yake. Lakini katika Siku za Mwisho ataifanya dunia itoa matunda yake na Mungu
atautendea mema mji wa Yerusalemu na Yuda. Pia Mungu ataifanya upya Jerusalemu
na Yuda ili wasiwe laana tena kwa mataifa (Zekaria 8:10-15).
Hivi ndivyo
tunavyotakiwa kufanya. Tunatakiwa kusema kweli kwa majirani zetu na kutoa hukumu
ya haki na kuwa na amani malangoni mwetu. Tunatakiwa kuwapenda majirani zetu na
tusifanye viapo vya uwongo. Yuda watakomesha saumu ya mwezi wa Nne (siku ya 9 wakati
mji ulipobomolewa); mwezi wa Tano (siku ya 10 Abu, wakati Hekalu na Nyumba
zilipochomwa moto); mwezi wa Saba (siku ya 3 mwezi Tishri wakati alipouawa kwa
kuchinjwa Gedalia na Ishmaeli mwana wa Nethania (Yer. 40:8; 41:1-3, 15-18) na
mwezi wa Kumi (siku ya 10 Tebethi) wakati mfalme wa Babeli alipokuja kuuhusuru
yaani kuuteketeza mji wa Yerusalemu (Ezekieli 24:1-2)) (Zekaria 8:19). Hizi ni saumu zilizotungwa tu na wanadamu
na sio saumu alizoziamuru Bwana Mungu.
Katika
siku hizo, kipindi cha mwisho kabisa cha zama hizi, watu watashika upindo wa
yeye aliye Myahudi anayetoka mbali na taifa na lugha yao, kutoka nchi ya mbali
ya dunia nao watakuja Yerusalemu ili kuomba kwa Bwana wa Majeshi (kama
ilivyoandikwa kwenye Mwanzo 26:28; Isaya 2:3; Mika 4:2). Watu wa Mungu, (yaani
Israeli) watarejeshwa na kufanywa upya.
Zekaria 8:1-23 inasema: Neno la BWANA Mwenye Nguvu likanijia tena. 2Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye
Nguvu: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni, ninawaka wivu kwa ajili yake.” 3Hiii ndilo asemalo BWANA: “Nitarudi
Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli,
mlima wa BWANA Mwenye Nguvu utaitwa Mlima Mtakatifu.’’ 4Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Kwa mara nyingine tena
wazee wanaume kwa wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za
Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake. 5Barabara za mji zitajaa wavulana na
wasichana wanaocheza humo.’’ 6Hili
ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa
mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?’’ asema BWANA
Mwenye Nguvu. 7Hili ndilo
asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na
magharibi. 8Nitawarudisha waje
kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao
kama Mungu wao.’’ 9Hili ndilo
asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya
yanayozungumzwa na manabii ambao walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa
nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu, mikono yenu na iwe na nguvu ili hekalu liweze
kujengwa. 10Kabla ya wakati huo,
hapakuwepo na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli
yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu
adui wa jirani yake. 11Lakini
sasa sitawatendea mabaki ya watu hawa kama nilivyowatenda zamani,’’ asema BWANA
Mwenye Nguvu. 12“Mbegu itakua
vizuri, mzabibu utazaa matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na mbingu
zitadondosha umande wake. Vitu hivi vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi
wao. 13Jinsi mlivyokuwa kitu cha
laana katikati ya mataifa, Ee Yuda na Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi
mtakuwa baraka. Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na nguvu.’’ 14Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye
Nguvu: “Kama nilivyokuwa nimekusudia kuleta maangamizi juu yenu, wakati baba
zenu waliponikasirisha na sikuonyesha huruma,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu, 15“Hivyo sasa nimeazimia kufanya mema
tena kwa Yerusalemu na Yuda. Msiogope. 16Haya
ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, mtoe hukumu ya kweli
na haki kwenye mahakama zenu, 17usipange
mabaya dhidi ya jirani yako, msipende kuapa kwa uongo, nayachukia yote haya,’’
asema BWANA. 18Neno la BWANA
Mwenye Nguvu likanijia tena. 19Hili
ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Saumu za miezi ya nne, tano, saba na kumi
itakuwa sikukuu za furaha na za shangwe kwa Yuda. Kwa hiyo uipende kweli na
amani.’’ 20Hili ndilo asemalo
BWANA Mwenye Nguvu: “Mataifa mengi na wakazi wa miji mingi watakuja, 21na wenyeji wa mji mmoja watakwenda
kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihi BWANA, na
kumtafuta BWANA Mwenye Nguvu. Mimi mwenyewe ninakwenda.’ 22Pia watu wa kabila nyingi na mataifa
yenye nguvu yatakuja Yerusalemu kumtafuta BWANA Mwenye Nguvu na kumsihi.’’ 23Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye
Nguvu: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa,
watang’ang’ania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe
kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’ ’’
Zekaria, sura ya 9
Tunaanza sasa
Mzigo wa Kwanza wa sehemu ya Pili. Hi sasa ni kipindi cha mbali kijacho.
Kwenye Zekaria
sura ya 9 hadi 11, maafa yaliikumba miji ya Tiro na Sidoni na Gaza na Akroni na
Ashikeloni na Ashidodi na Damscus, na kwenye nchi zinazoizunguka nchi ya Shamu,
na nchi yote la Lebanoni, ambayo imetajwa na kushughulikiwa kwa namna rahisi.
Watamwabudu Mungu
huko Yerusalemu na Yuda, na watatawala mchi ya Israeli. Watakabiliwa na
maangamizo yatakayowafikisha kwenye wongofu na matengenezo mapya. Mungu ataweka
makazi yake mjini Yerusalemu na kufanya vita dhidi ya jeshi hili lililokuja
kinyume na mji huu (Zekaria 9:1-8).
Imeandikwa
kwamba, katika kipindi hiki: Shangilia sana, Ee Binti
Sayuni! Piga
kelele, Binti Yerusalemu! Tazama, mfalme
wako anakuja kwako, ni mwenye haki naye ana wokovu, mpole naye amepanda punda, mwana punda, mtoto wa punda. (Zekaria 9:9). Matukio yaliyoandikwa
kwenye herufi nzito yanaonekana pia kwenye Agano Jipya na yamenukuliwa kutoka
huko na pia yametabiriwa kwenye Mika 5:2 na yameandikwa pia kwenye Mathayo 2:1 na
21:5. Hay ani maandiko yaliyoandikwa kotekote. Aya ya 10 inaendelea kwa
kuelezea unabii wa Kuja kwa mara ya Pili kwa Masihi, akiwa na hukumu ya haki na
wokovu, akiwa amepanda gari akitokea kwa Efraimu na farasi kutoka Yerusalemu na
uta wa vita. Masihi ataleta amani kwa mataifa wasio Wayahudi na utawala wake
utaenea toka upande huu wa bahari hadi kwenye upande wa pili wa bahari na
kutoka kwenye mto hadi hadi pande ya mwisho ya dunia. Mungu anasema kwamba
atauchukua Sayuni na kuweka agano la damu na kuwafungulia wafungwa kutoka
shimoni ambako hakuna maji (Zekaria 9:11-12). Huu utakuwa ndiyo wongofu wa Yuda
na Efraimu. Maandiko yanaonyesha kuwa watatumwa kwa wana wa Yavani, ambao wanaaminika
kutoka kwenye jamii ya Wayunani tangu mwaka LXX lakini Waebrania wanatamka yavan, usemi unaoeleweka kuwa ni
Wayunani-Ioni wa kale, na sio Wayunai wa siku hizi. Na hawatokani na wakazi wa
siku hizi wan chi hii ya Uyunani, maarufu kama Ugiriki siku hizi na ambao sio
wana wa Yavani kwa namna yoyote (kama ivyoandika kwenye Mwanzo 10:2,4; Isaya
66:19; Ezekieli 27:13; Danieli 8:21; 11:2; Yoeli 3:6; tazama jarida la Kimbuko la Asili
la Mataifa (Na. 265) [Genetic Origin of the Nations (No. 265)] na
Vita ya
Hamoni-Gogu (na. 294) [War of Hamon-Gog (No. 294)].
Watapata nguvu
mpya na Bwana atawafanya kuwa imara na watawatiisha maadui zao kwa Roho
Mtakatifu aliye asili ya wongofu wao.
Lebanoni na fahari
yote ya Yordani vitaletwa. Bwana anasema atalilisha kundi la kondoo wa
kuchinjwa. Kwenye sura ya 11, Mungu anaonyesha jinsi jambo hili litakavyokuwa
na jinsi atakavyoingilia kati na kulilisha kundi. Kwenye sura hii Mungu anawaonya
wanaozitumikia vinyago na kufanya ibada ya sanamu na anaelezea jinsi hukumu yao
itakavyokuwa kwa dhambi waliyoifanya ya kuwaacha na kuwatelekeza kondoo na
kuharibu umoja wa watu. Hii ni moja ya mambo yatakayofanyika kwenye Ujio wake
wa Kwanza kipindi ambacho watumwa wa Uzuri na Njuga walizofungiwa
zitakapovunjwa na wachungaji wale ambao walikulia na kuendelea kuwa kwenye
Kanisa kengeufu linalowawinda masikini na kuwakokota kwa kwato zao
watakapoadhibiwa (kama ilivyoandikwa kwenye Ezekieli 34:1-22).
Zekaria 9:1-17 inasema: Neno la BWANA liko kinyume na nchi ya Hadraki na
Dameski itakuwa mahali pa kupumzika, kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote
za Israeli yako kwa BWANA, 2pia
juu ya Hamathi inayopakana nayo, juu ya Tiro na Sidoni, ingawa wana ujuzi
mwingi sana. 3Tiro amejijengea ngome
imara, amelundika fedha kama mavumbi na dhahabu kama taka za mitaani. 4Lakini Bwana atamwondolea mali zake
na kuuangamiza uwezo wake wa baharini, naye atateketezwa kwa moto. 5Ashkeloni ataona hili na kuogopa,
Gaza atagaagaa kwa maumivu makali, pia Ekroni, kwa sababu matumaini yake
yatanyauka. Gaza atampoteza mfalme wake na Ashkeloni ataachwa pweke. 6Wageni watakalia mji wa Ashdodi, nami
nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. 7Nitaondoa
damu vinywani mwao, chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao. Mabaki yao
yatakuwa mali ya Mungu wetu, nao watakuwa viongozi katika Yuda, naye Ekroni
atakuwa kama Wayebusi.
Kuanguka kwa miji
ya Tiro na Sidoni, kwa sehemu kulifanywa na Wababelonia. Hata hivyo, tukio hili
lilitokea siku nyingi zilizopita wakati ilipokuwa inaandikwa. Unabii iliangalia
mambo yanayokuja baadae kwa Wayunani na Warumi na kisha baadae kidogo kwa
Waarabu na Wapigania dini (Wakrusedi) na sasa unajiri kwenye Siku hizi za
Mwisho. Ufafanuzi uliofanywa hapa umefanywa kwa sehemu tu na wala sio wote, na
kwenye Siku za Mwisho tunajionea wenyewe haya yakifunuliwa na kuwekwa wazi na
tukishukudia kwa macho yetu..
Ahadi ziliyoko
hapa ni kwamba mataifa haya yatakuwa ni sehemu ya Israeli na yatakuwa ni
majimbo ya inchi hii ya Israeli na uukufu au uzuri wao utakuwa ni utukufu wa
Bwana, Mungu wa Israeli. Wayebusi walikuwa ni wakazi wa zamani wa mji wa
Yerusalemu na mahali alipokuwa anatwangia ngano yaani shinikizoni kwa Arauna
ndipo palipokujakuwa hatimaye ndipo Hekalu la Mungu lilipojengwa. Uweza wa kijeshi
wa Wafilisti uliondolewa na utawala wao uliondolewa kutoka Gaza maeneo mengine
muhimu yaliyokuwa sehemu nyingine ya Wafilisti yaliondolewa au yalifanywa yawe
na watu mchanganyiko kama ilivyokuwa mji wa Ashdodi. Hivi ndivyo yanavyosema
maandiko na maandiko hayawezi kutanguka.
Mungu atatuambia
kwamba hatimaye Masihi atakuja Yerusalemu kama alivyokuja kwa nguvu na ushindi
akashinda nguvu za dhambi na mauti. Andiko haliishii hapa tu bali linaendelea
kuwaelezea Efraimu naYuda kwa pamoja, ambao ndivyo watakavyokuwa katika Siku za
Mwisho. Israeli walikuwa wameshaenda utumwani tangu mwaka 722KK na hawakurudi.
8Lakini nitailinda
nyumba yangu dhidi ya majeshi ya wanyang’anyi. Kamwe mdhalimu hatashambulia
watu wangu tena, kwa maana sasa ninawachunga. 9Shangilia sana, Ee Binti Sayuni! Piga kelele, Binti Yerusalemu!
Tazama, mfalme wako anakuja kwako, ni mwenye haki naye ana wokovu, mpole naye
amepanda punda, mwana punda, mtoto wa punda. 10Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu na farasi wa vita kutoka
Yerusalemu, nao upinde wa vita utavunjwa. Atatangaza amani kwa mataifa. Utawala
wake utaenea kutoka bahari hadi bahari na kutoka mto Eufrati hadi mwisho wa
dunia. 11Kwako wewe, kwa sababu
ya damu ya agano langu nawe, nitawaacha huru wafungwa wako watoke kwenye shimo
lisilo na maji. 12Rudieni ngome
yenu, Enyi wafungwa wa tumaini, hata sasa ninatangaza kwamba nitawarejesheeni
mara dufu. 13Nitampinda Yuda
kama nipindavyo upindi wangu, nitamfanya Efraimu mshale wangu. Nitawainua wana
wako, Ee Sayuni, dhidi ya wana wako, Ee Uyunani na kukufanya kama upanga wa
shujaa wa vita. 14Kisha BWANA
atawatokea, mshale wake utamulika kama umeme wa radi. BWANA Mwenyezi atapiga
tarumbeta, naye atatembea katika tufani za kusini, 15BWANA Mwenye Nguvu atawalinda, wataangamiza na kushinda kwa mawe
ya kutupa kwa kombeo. Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo, watajaa
kama bakuli linalotumika kunyunyizia kwenye pembe za madhabahu. 16BWANA Mungu wao atawaokoa siku hiyo
kama kundi la watu wake. Watang’ara katika nchi yake kama vito vya thamani
kwenye taji. 17Jinsi gani
watavutia na kuwa wazuri! Nafaka itawastawisha vijana wanaume, nayo divai mpya
vijana wanawake.
Andiko hili
linaelekea mbele hadi kwenye Siku za Mwisho wakati Masihi atakaporudi kwa nguvu
na utukufu na kuyatiisha mataifa. Anautumia uweza wa Yuda na wa Efraimu kuyatiisha
mataifa, na hivi ndivyo ilivyotokea hasa tangia mwaka 1916 na kuendelea (tazama
jarida la Kuanguka
kwa Misri: Unabii Juu ya Mikono Iliyovunjika ya Farao (Na. 36) [The Fall of Egypt: The Prophecy of Pharaohs Broken Arms
(No. 36)]. Hata hivyo, watalazimishwa kwa amani.
Zekaria sura ya 10
Mzigo wa Kwanza
unaendelea hadi kufikia andiko la sura 10:12. Hata hivyo, sura nyingine mbili
zinazofuatia zinashughulika kuelezea kuhusu dini ya uwongo. Mungu anawaaambia
kuwa wanataka baraka zake na sio za terafi, ambaye ni mungu-sanamu ambaye tunaweza
kumuona hata leo akiwa na umbo la mwanamke akiabudiwa kama mungu-mke ambaye
anajulikana kama “Bikira Mariamu” au pia anatumika kwenye dini ya Buddha na
sehemu nyingi nyingine akijulikana kwa majina tofauti tofauti.
Waonaji wanajimu huona
uwongo na waota ndoto hukosea wanapotafsiri ndoto zao. Watu hudanganywa na
kupotoshwa na dini za uwongo kipindi hiki kinaedelea hadi mwishoni. Wachungaji
watahukumiwa kwa ajili ya yale waliowafanyia Yuda na Israeli na walivyowafanyia
wateule wa Mungu. Yuda wamewekwa kando ili kuonysha kuwa watarejeshwa upya na dini
ya uwongo itaondolewa mbali na kukomeshwa kabisa. Yuda watarejeshwa upya na Yusufu
watatiwa nguvu. Hata hivyo, tunapaswa kuelewa kuwa wao ni kina nani kwanza kabla
ya kuona kile ambacho Mungu anakwenda kufanya. Kabila hili la Yuda na nyumba ya
Yusufu wako Marekani kwa sasa na kwenye mataifa ya Jumuia ya Madola ya
Waingereza, isipokuwa kwa dakika moja wanajulikana kama Makabila Kumi
Yaliyopote ya Israeli, ambao nim ara kumi zaidi ya vile wanavyojulikana kama
Wayahudi leo kwenye mataifa hayo. Kuna Wayahudi wengi nchini Marekani peke yake
kuliko walivyo nchini Israeli kwenyewe na wengi wako Marekani na kwenye Mataifa
yaliyo kwenye Jumuia ya Madola kuliko walivyo hahala pengine popote duniani.
Hawa wote ni taifa kamili na kweli la Israeli leo, bila kuwahesabia wale
wanaojulikana kuwa na nasaba ya uzawa kwa Israeli wa kale.
Zekaria 10:1-12 inasema: Mwombe BWANA mvua wakati wa vuli, ni BWANA
atengenezaye mawingu ya tufani. Huwapa watu manyunyu ya mvua, pia mimea ya
shambani kwa ajili ya kila mtu. 2Sanamu
huzungumza udanganyifu, waaguzi huona maono ya uongo, husimulia ndoto ambazo si
za kweli, wanatoa faraja batili. Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo
walioonewa kwa kukosa mchungaji. 3“Hasira
yangu inawaka dhidi ya wachungaji, nami nitawaadhibu viongozi, kwa kuwa BWANA
Mwenye Nguvu atalichunga kundi lake, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama
farasi mwenye kiburi akiwa vitani. 4Kutoka
Yuda litatokea Jiwe la pembeni, kutoka kwake vigingi vya hema, kutoka kwake
upinde wa vita, kutoka kwake kila mtawala. 5Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa wanaokanyaga barabara za matope
wakati wa vita. Kwa sababu BWANA yu pamoja nao, watapigana na kuwashinda
wapanda farasi. 6“Nitaiimarisha
nyumba ya Yuda na kuiokoa nyumba ya Yosefu. Nitawarejesha kwa sababu nina
huruma juu yao. Watakuwa kama watu ambao sijawahi kuwakataa kwa sababu mimi
ndimi BWANA, Mungu wao, nami nitawajibu. 7Waefraimu watakuwa kama mashujaa, mioyo yao itafurahi kama kwamba
ni kwa divai. Watoto wao wataona na kushangilia, mioyo yao itafurahi katika
BWANA. 8Nitawapa ishara na
kuwakusanya ndani. Hakika nitawakomboa, nao watakuwa wengi kama walivyo kuwa
mwanzoni. 9Ijapokuwa
niliwatawanya miongoni mwa mataifa, hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali
watanikumbuka mimi. Wao na watoto wao watasalimika katika hatari nao watarudi. 10Nitawarudisha kutoka Misri na
kuwakusanya toka Ashuru. Nitawaleta katika nchi ya Giliadi na Lebanon, napo
hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha. 11Watapita
katika bahari ya mateso, bahari iliyochafuka itatulizwa na vilindi vyote vya
mto Nile vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitashushwa na fimbo ya utawala ya Misri
itatoweka. 12Nitawaimarisha
katika BWANA na katika jina lake watatembea,’’ asema BWANA.
Pia kumbuka kuwa
nchi ya Gileadi na Lebanoni zimehifadhiwa kwa ajili ya Efraimu na kama sehemu
ya Israeli yote kuu. Mungu anajiandaa kwa kipindi hiki hata sasa. Lebanoni
itajumuishwa kuwa kama sehemu ya taifa hili la Israeli na wataishi kwa amani.
Zekaria, sura ya 11
Kisha Mungu
anaitaja Lebanoni kwenye unabii huu kwa njia ya ishara. Kwa hiyo
wanahusianishwa na kundi na vilio vya wachungaji. Matukio haya yote yanahusishwa
na Siku za Mwisho. Vipindi vyote vya kuhusishwa kwa Gileadi na Lebanoni na
Israeli na Makanisa ya Mungu vimefungamanishwa pamoja kwenye mlolongo mmoja na
Mungu anashughulika na wote hawa.
Zekaria 11:1-17 inasema: Fungua milango yako, Ee Lebanoni, ili moto uteketeze mierezi yako! 2Piga yowe, Ee mti wa msonobari kwa kuwa mwerezi umeanguka, miti ya fahari imeharibiwa! Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani, msitu mnene umefyekwa! 3Sikiliza yowe ya wachungaji: malisho yao manono yameharibiwa! Sikia ngurumo za simba, kichaka kilichostawi sana cha Yordani kimeharibiwa! 4Hili ndilo asemalo BWANA Mungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa. 5Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘BWANA asifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii. 6Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,’’ asema BWANA. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.’’
Kipindi hiki
kimeendelea kwa muda mrefu sana na mfumo wa uwongo uliinuka na kuitawala dunia
na wafalme ambao walifanyanao uzinzi. Hii ndiyo dini tunayoitajwa kwenye kitabu
cha Ufunuo kuwa ni Babeli ya Siri. Hakuna mtu ambaye Mungu ameweza kumwokoa
kutoka mkononi mwao kwa ajuli la ukengeufu wao.
Dini ikafanyika
kuwa ni biashara huku ikienea na kuwalaghai watu wake yenyewe. Mungu akakomesha
mpango wa Neema na Ushirikiano au Umoja.
7 Kwa hiyo
nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana.
Kisha nikachukua fimbo mbili moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami
nikalilisha kundi.
Kwa muda wa mwezi
mmoja tu Mungu akawaondolea mbali wachungaji wake watatu. Jambo hili limeongelewa
vizuri kwenye jarida la Kulipima Hekalu (Na. 137) [Measuring the Temple (No. 137)]. Huu ni mwaka wa tatu wa siku za mwisho
zinazoitwa kama ni ya “Maombolezo ya Musa”. Kundi lile linajiangamizwa lenyewe
na wale wanaonyenyekeana na kutetemekewa kwa kuogopana na wanaositakiana
mashitaka ya uwongo na kushutumiana. Kisha andiko hili linarejea nyuma na kushughulika
na Masihi na mshahara wake atakaolipwa kwa ajili ya mwenendo wake kwa vipande
thelathini vya fedha.
8Katika mwezi mmoja
nikawaondoa wachungaji watatu. Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa
nao 9nikasema, “Sitakuwa
mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale
waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.’’ 10Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja,
kutangua agano nililofanya na mataifa yote. 11Likatanguka siku hiyo, kwa hiyo waliodhurika katika kundi
waliokuwa wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno la BWANA. 12Nikawaambia, “Mkiona kuwa ni vema,
nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.’’ Kwa hiyo wakanilipa vipande
thelathini vya fedha. 13Naye
BWANA akaniambia, “Mtupie mfinyanzi,’’ hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa
hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha na kumtupia huyo mfinyanzi
katika nyumba ya BWANA
Mkataba wa ushirikiano
hatimaye ulivunjika kati ya Israeli na Yuda. Hadi kufikia kipindi kile Israeli
walikuwa upande wa kaskazini walikopelekwa lakini wengi wao wanaushirikiano
bado na Yuda. Hata hivyo, Yuda waliangamizwa na kutawanywa na katika karne
hiyohiyo Waajemi na Warumi waliidhoofisha Israeli na washirika wake na wakaenda
Ulaya. Ushirikiano wao ukaisha. Hali hii iliendelea kwa kipindi cha miaka 1800
hadi kwenye karne ya Ishirini wakati Mungu alipoanza kushughulika tena na
Israeli na Yuda.
14Kisha nikaivunja
fimbo yangu ya pili iitwayo Umoja, kuvunja udugu kati ya Yuda na Israeli! 15Kisha BWANA akaniambia, “Vitwae tena
vifaa vya mchungaji mpumbavu. 16Kwa
maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea,
wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye
afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao. 17“Ole wa mchungaji asiyefaa,
anayeliacha kundi! Upanga na
uupige mkono wake na jicho lake la kuume! Mkono wake na unyauke kabisa, jicho
lake la kuume lipofuke kabisa!”
Mnamo mwaka 1916 Mungu
alianza kushughulika na Misri na kuirudisha Nchi Takatifu kwa mkono wa Efraimu mwaka
1917 Yerusalemu ulitwaliwa na nchi asilia ya Wayahudi ikatangazwa kwenye kile
kilichojulikana kama ni Azimio la Balfour. Mwaka 1948 Israeli ikatangazwa kuwa ni nchi huru na
ikapigana vita yake ya kwanza. Mwaka 1944 Lebanoni ilijitangazia uhuru wake
lakini katika mwaka 1948 ilijihusisha na mgogoro wa wakimbizi wa Kipalestina ambao
ulishuhudia wengi wao wakikimbilia huko Tiro na maeneo mengine ya Lebanoni. Miaka
saba ya Misri ilienda tangia mwaka 1916 hadi 1996. Kanisa la Mungu lilikuwa
likijikusanya upya kwa kipindi cha miaka arobaini muda huu wa kuanzia mwaka 1927
hadi 1967. Hawakushughulikia vizuri na masuala ya kundi la watu wa Mungu na
waliweza hata kutupwa kwenye mifumo ya wachungaji hawa wanaoabudu na kutumikia
vinyago na mnamo mwaka 1967 walijiingiza kwenye mfumo wa siku za mwisho na
mataifa ya Israeli hali iliyowalazimu kuwepo kwa mujibu wa ulivyosema unabii
bali walishindwa kutoa huduma vizuri. Mzunguko mmoja wa miaka kumi na tisa
uliruhusiwa (soma jarida la Miaka Arobaini ya Toba (Na. 290) [Forty Years for Repentance (No. 290)] na Unabii wa Uwongo (Na. 269) [False Prophecy (No. 269)].
Israeli na Tiro na
Lebanoni na Gileadi wote walipewa miaka sabini tangu mwaka 1948. katika miaka
hiyo mataifa mengine pamoja na kundi la Makabila Kumi wameendelea kubweteka na
kuishi maisha yasiyo na utaratibu wala mpangilio.
Kumbuka mikono
miwili inayotajwa kwenye unabii wa Mikono Iliyovunjika ya Farao (Na. 36) [Pharaoh’s Broken Arms (No. 36)]. Mikono hii miwili ilikuwa ni kipindi cha miaka
arobaini kilichodumu tangu mwaka 1916 hadi 1996. Walitawanyika tangu kipindi cha
mwanzo kwa miaka 2520 au kinachoitwa pia kama cha “mara saba”. Kwa hiyo
tunajionea pia mikono mingine miwili ambayo inayomaanisha zama ya kipindi cha
miaka arobaini cha mataifa haya cha kuanzia mwaka 1948 hadi 2028, ambcho ni
kipindi kilichowekwa kwenye mfumo mzima wa kuanzishwa kwa mfumo mzima wa
Milenia. Kuanzia kipindi cha mwaka. 2018 hadi 2028 tutajionea mwisho wa
kutiishwa kwa mataifa na mchakato wa kuanzishwa kwa mfumo wa milenia.
Mwaka 1967 mwanzo
wa mfululizo wa vita ulianza nchini Israeli na sambamba yake, hali ya ukengeufu
kwenye Kanisa la Munu uliendelea. Waliendela kuondoa maadhimisho ya kweli ya
Pasaka na wakaendelea na mafundisho ya uwongo. Waliyaacha mafundisho ya kweli
yenye uzima na kufundisha hadithi za uwongo. Fundisho lau kuhusu asili chanzo
ya Mungu likaendelea kufundishwa kuwa yeye anakamilika uungu wake kwa kujumlisha
Nafsi Mbili yani Udithei na waliwafundisha watu wao kushikilia hivyo na
kuyakataa mafundisho sahihi kuhusu jambo hili. Mnamo mwaka 1997 kipindi cha
Utimilifu wa Mataifa kilifungwa na kipindi cha miaka thelathini ya mwisho cha
kutiishwa kwa mataifa kilianza (soma jarida la Miaka Thelathini ya Mwisho: Pambano la
Mwisho (Na. 219) [The Last Thirty Years: the Final Struggle (No. 219)].
Mnamo siku ya 1 mwezi
wa Abibu 2008 ikiwa ni miaka wa arobaini ya watu hawa ikiwa imekamilika na
kisha mlolongo wa mwisho ukiwa unaendelea. Mungu amesema kwamba atautumia mji
wa Yerusalemu katika mkakati wakewa kuyashughulikia mataifa.
Zekaria, sura ya 12
Zekaria sura ya
12 inaelezea kuhusu Yuda na Yerusalemu watakavyokuwa katika Siku za Mwisho.
Inasema kuwa Yerusalemu itakuwa ni jiwe kuu na mzigo au kongwa kwa watu WOTE.
Wale wote watakaojiunga nao kwa kujipendekeza watakatwa vipande vipande
ingawaje watu wote wa dunia wataungana pamoja ma kuweka mikakati kadhaa kinyume
chao. Mungu ansema kuwa katika siku hiyo atampiga kila farasi kwa mapigo makuu
sana na atawapiga wapanda farasi wao kwa wazimu. Siku hiyo Mungu atafungua
macho yake kuuelekea na kuwatazama Yuda. Kwa hiyo, atawachukulia kwa moyo wa
upendeleo na atawapiga farasi wa watu hawa ambao ni maadui zao kwa upofu, jambo
linaloasiria kuwa kama bahati nzuri kwa kipindi hiki kwa hawa Yuda. Jambo
litakalowafanya washindwe kuamua mambo watakayoyachukua na kuanzisha mikakati
ya maana na mipangilio yenye manufaa (Zekaria 12:3-4). Katika Siku za Mwisho
viongozi wa Yuda watakuwa kama moto ulao kwa watu wote watakaokuwa upande wa
kulia na wakushoto kwao. Watawategemea wakazi wa Yerusalemu watakaokuwa na
Masihi na mikakati ya Bwana wa Majeshi, Mungu wao. Kwa hiyo, mashambulizi dhidi
ya Yerusalemu yataendelea kama yalivyo hadi kipindi Atakaporudi Masihi. Wateule
wataishi kwenye mji huu wa Yerusalemu pamoja naye na na watakuwa ni faraja na
nguvu ya wakazi wa Yuda na kuwazunguka.
Zekaria 12:7 inaonyesha
kuwa Yuda inaokolewa na wenyeji wa Yerusalemu ili kwamba Yerusalemu isijitukuze
dhidi ya Yuda. Zekaria 12:8 inasema kwamba: tates that: Katika siku hiyo
aliyedhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa
kama Mungu [elohim] kama Malaika wa BWANA akiwatangulia [au mbele ya macho
yao]. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba watakuwa Elohim kama Kristo alivyo
kichwa chao na Elohim. (soma jarida la Wateule Kama Elohim (Na. 1) [The Elect as Elohim (No. 1)].
Hivyobasi, Mungu
anasema (kwenye aya ya 9) kwamba: “Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa
yote yatakayoushambulia Yerusalemu.”
Zekria 12:10 ni
unabii wa kitaswira au unaopingana na taswira. Atakaporudi Masihi watamtazama
wale waliomchoma; kwa maneno mengine ni kusema kwamba, huyu ni Masihi waliyemuwamba
mtini na kumchoma kwa mkuki. Kulikuwa na uchungu mjini Yerusalemu wakati wa
kutoa dhabihu, na ndivyoitakavyokuwa tena wakati watakapogundua kikamilifu kuwa
kile walichokifanya kinawahusu wote yaani Yuda na Walawi, na hasahasa wa nyumba
ya Daudi kupitia kwa Nathani na Yuda, na kwa nyuma ya kikuhani ya Shimei na
Lawi, kwa mzaliwa wao wa kwanza ambaye ni Masihi. Maombolezo makuu yaliyotangulia
yalikuwa ni ya huko Hadadrimmon (kwa sasa inaitwa Rummane) magharibi ya Esdraelon
karibu na Megido ambapo Mfalme Yosia aliuawa na maombolezo haya hayakutarajiwa.
Kwa maneno mengine ni kusema kwamba, hata yalikuwa ni maombolezo muhimu zaidi
ya yote katika historia ya Israeli, na manasababishwa na tendo lao la kufahamu
kile walichokuwa wanakifanya na kile walichikikosa au kupungukiwanacho kwa
kipindi kirefu.
Zekaria 12:1-14 inasema: Hili ni neno la BWANA kuhusu Israeli. BWANA, Yeye
azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani
yake, asema: 2‘‘Nitakwenda
kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kulewalewa kwa mataifa yote yanayoizunguka.
Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia
Kumbuka kuwa
Yudaea itaharibiwa wakati maadui watakapouzingira mji wa Yerusalemu. Wale wote wanaojipendelea
na kujikinai wataharibiwa kabisa kwa mangamizi makuu.
3Katika siku hiyo,
wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya
Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu
kulisogeza watajiumiza wenyewe. 4Katika
siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye kwa uenda
wazimu,’’ asema BWANA. 5Kisha
viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa
sababu BWANA Mwenye Nguvu ni Mungu wao.’
Juda watajionea
jinsi mji wa Yerusalemu umetiwa nguvu kwenye uwezo wao wa kiroho kwa kupitia
nguvu za Mungu. Hii itakuwa ni sehemu mojawapo itakavyokuwa baada ya toba yao.
6“Katika siku hiyo
nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni,
kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote
yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake. 7“BWANA atayaokoa makao ya Yuda
kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa
zaidi kuliko ile ya Yuda.
Kumbuka kwamba
utukufu wa nyumba ya Daudi na utaratibu wa kiuongozi wa Yerusalemu hautaweza kujitukuza
dhidi ya Yuda, kwa jinsi Yuda itakavyopata ushindi kwenye kipindi hiki.
Hii ni siku ya
kurudi kwa Masihi: yaani Siku ya Bwana.
Wateule watakuwa
kama miungu wadogo siku ile. Watakatifu watakuwa wamefufuka na kuwa watawala au
wana wa Mungu na watakuwa kama miungu wadogo, wakiwa ni Wajumbe wenye ujumbe wa
Bwana vichwani mwao, na kumsaidia kazi zote Masihi aliye ni mzaliwa wa kwanza
wa wafu wote (soma jarida la Mteule kama Elohim (Na. 1) [The Elect as Elohim (No. 1)].
8Katika siku hiyo, BWANA atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba
aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi
itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa BWANA akiwatangulia.
Kutoka siku hiyo
Kristo atayaleta mataifa yote hadi Megido.
9Katika siku hiyo
nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoushambulia Yerusalemu. 10“Nami nitamiminia roho ya neema na
maombi juu ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu. Watanitazama mimi, yule
waliyemchoma, nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na
kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. 11Katika siku hiyo kilio kitakuwa
kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadadrimoni katika tambarare ya Megido. 12Nchi itaomboleza, kila ukoo peke
yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa
nyumba ya Nathani na wake zao, 13ukoo
wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao, 14na koo zote zilizobaki na wake zao.
Jamii za Daudi
kupitia Nathan na Lawi kupitia Shimei (Luka 3) ni familia za Masihi katika Yuda
walioshuhudia Masihi aliuawa.
Kwa hiyo, dhambi
za Yuda zitaponywa.
Zekaria, sura ya 13
Sura ya 13 inaema
kwamba katika siku hiyo chemichemi zitafunguka kwenye nyumba ya Daudi na kwa Yerusalemu
kwa ajili ya dhambi na unajisi. Wakati hili likitokea vinyago vyote
vitaondolewa kutoka Yerusalemu na katika Israeli yote na manabii watakatiliwa
mbali kwa kuwa Roho Mtakatifu atakuwa amemwagwa kote kwa kiasi kikumbwa sana
kiasi kwamba unabii hautahitajika tena kabisa, na wale wanaojifanya kutabiri
kwa jina la Bwana watakufa (Zekaria13:3).
Kama mtu hataiona
Yerusalemu, itakuwa ni vigumu kuigundua ibada ya sanamu hapo pamoja na vinyago
na alama zake na mahali palipo na uwongo na mafundisho mapotofu na yale ya
uwongo kila mahali. Watu hudhania kuwa wanamtumikia Mungu wanapojinyenyekesha
na kuvibusu mawe na vinyago na huku wakijipigapiga vifuani mwao.
Wakati Mungu
alipouondoa uwongo huu toka Yerusalemu na kumwaga Roho wake Mtakatifu manabii
watanya kazi ya ukulima na ufugaji. Zekaria 13:7 inaelezea yale yaliyofanyika
siku za nyuma katika kuuawa kwha Masihi na kutawanyika kwa wateule katika
kukamilisha unabii wa Isaya 53:5-10. Kondoo wataona theluthi mbili wakifa na theluthi
waliobakia watatawanyika na kusafishwa kwa kupitishwa kwenye moto (13:8-9).
Zechariah 13:1-9 Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa
nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi. 2“Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali
majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asema BWANA Mwenye
Nguvu. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi. 3Ikiwa yupo ye yote atakayeendelea
kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘ni lazima ufe, kwa
sababu umesema uongo kwa jina la BWANA.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe
watampasua tumbo. 4“Katika
siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la
kinabii la nywele ili apate kudanganya watu. 5Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima, ardhi imekuwa kazi
yangu tangu ujana wangu.’ 6Ikiwa
mtu atamwuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni
majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu. 7“Amka, Ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu, dhidi ya mtu aliye
karibu nami!” asema BWANA Mwenye Nguvu. “Mpige mchungaji, nao kondoo
watatawanyika, nami nitageuza mkono wangu dhidi ya walio wadogo, 8katika nchi yote,’’ asema BWANA,
“Theluthi mbili watapigwa na kuangamia, hata hivyo theluthi moja watabakia
ndani yake. 9Hii theluthi moja
nitaileta katika moto, nitawasafisha kama fedha isafishwavyo na kuwajaribu kama
dhahabu. Wataliitia jina langu nami nitawajibu, nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’
nao watasema, ‘BWANA ni Mungu wetu.’ ’’
Mungu atausafisha
kama isafishwavyo dhahabu mji wa Yerusalemu na wakazi wake.
Zekaria, sura ya 14
Zekaria 14 inaendelea
kuitaja Siku ya Bwana (soma jarida la Siku ya Bwana na Siku za Mwisho (Na. 192) [The Day of the
Lord and the Last Days (No. 192)].
Muda mfupi kabla
ya kuja kwake Masihi, mji wa Yerusalemu utatwaliwa na na nusu ya wakazi wake watachukuliwa
utumwani, lakini nusu nyingine watabakia ndani yake na hawataondolewa humu.
Kisha Bwana atawapigania na kuwaadhibu mataifa haya. Masihi atasimama juu ya
Mlima Sayuni na mlima huu utagawanyika vipande viwili, ukielekea pande mbili za
mashariki na kusini na kufanya bonde litakalotokea mashariki na kuelekea magharibi
na bonde hili litakuwa na kikomo chake kitakachoitwa Azal (Kwa mujibu wa
kitabu cha fafanuzi cha SHD 682 kutoka kifungu cha 680, neno hili atsel linamaana ya uungwana).
Zekaria 14:1-21 inasema: Siku ya BWANA inakuja ambayo nyara zilizotekwa
kwenu zitagawanywa machoni penu. 2Nitayakusanya
mataifa yote huko Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa, nyumba
zitapekuliwa na wanawake watanajisiwa. Nusu ya mji watakwenda uhamishoni,
lakini watakaobaki hawataondolewa kutoka mjini. 3Kisha BWANA atatoka na kupigana dhidi ya watu wa yale mataifa,
kama apiganavyo siku ya vita.
Milima
inayoelezewa kwenye aya ya 5 ni milima miwili iliyotokana na Mlima wa
Mizeituni. Tetemeko hili pia linalotajwa kwenye kitabu cha Amosi sura ya 1.
Siku ile, elohim wa Israeli atakuja na watakatifu wote pamoja naye (Zekaria
14:5). Masihi atakuwa mfalme atayayetawala dunia hii yote na jina lake litakuwa
moja. Mji wa Yerusalemu utakuwa tambarare kutoka Geba, eneo lililo na umbali wa
takriban maili sita kaskazini mwa Yerusalemu hadi Rimmon, ambao unaitwa pia Khan
Umm er Rumamin (sawa na inavyosema Nehemia 11:29). Mji huu ni wa Ain Rimmon (En
Rimmon, Yoshua 15:32). Hapo mwanzo mji huu walipewa kabila la Simeoni (Yoshua
19:7; 1Nyakati 4:32). Uko kusini mwa Yudea kwenye wilaya ya Negebu karibu na Beer-sheba. Eusebius anaielezea
hii kuwa ni kijiji kikubwa kuliko vyote miongoni mwa vile vya Wayahudi, maili
za Kirumi kumi na sita upande wa kusini mwa Eleutheropolis katikati ya Darome (upande
wa kusini ya Yuda). Khirbet er-Ramin iko maili tisa Kaskazini
Mashariki mwa Beer-sheba. Beer-sheba iko eneo la jumla ya maili ishirini na
nane Kusihi Magharibi ya Hebron na Hebron iko maili kumi na tisa kusini mwa
Yerusalemu, n ani maili thelathini na nusu Kusini Magharibi mwa
Bethhlehemu. Kwa hiyo, hili bonde linalojumuisha uwanda wa Yerusalemu lina
urefu wa maili arobaini na nne (au kilometa 66) urefu wake na linafunika eneo la
vilima vya kusini ya nchi ya Yuda. Matukio ya jiolojia kwa hiyo ni makubwa
sana.
4Siku hiyo miguu yake
itasimama juu ya Mlima wa Mzeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa
Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde
kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini. 5Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde
hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia
tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha BWANA Mungu wangu
atakuja, nao watakatifu wote pamoja naye.
Tunaona hapa
kwamba kuwa kurudi kwa Masihi aliwa na utukufu mkuu au akiwa ni Mtakatifu Ajaye.
Hili ni Kanisa pia.
6Siku hiyo hakutakuwepo nuru,
baridi wala theluji. 7Itakuwa
siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na BWANA. Jioni
inapofika nuru itakuwepo. 8Siku
hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari
ya mashariki na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi, wakati wa kiangazi na
wakati wa masika.
Ziwa kubwa
lililochini kwa chini lililogundulika hivi karibuni nchini Israeli litaunda
mfumo msingi wa maji kwenda nje kuelekea upande wa magharibi na upande wa kusini
mashariki.
9BWANA atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepo BWANA
mmoja na jina lake litakuwa jina pekee. 10Nchi
yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu,
itakuwa kama Arabaa. Lakini
Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi
mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa
Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme. 11Utakaliwa na watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu utakaa
salama.
Kwa hiyo, Ktisto
akiwa kama Mfalme, na Kanisa, watatawala kwa pamoja kutoka Yerusalemu kwa
kipindi cha miaka elfu moja (soma Ufunuo 20).
Watu wanaopigana
na Yerusalemu watateseka kwa tauni wakati kwamba miili yao na macho yao na
ndimi zao aitaliwa kwa kadiri watakavyokuwa wakisimama. Wote watawainukia
kinyume majirani zao na watauana. Utukufu na utajiri wa mataifa wafanyao hivyo,
utapelekwa.
12Hii ndiyo tauni
ambayo BWANA atapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu:
Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza
kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao. 13Katika siku hiyo BWANA atawatia wanaume hofu kuu. Kila mwanaume
atakamata mkono wa mwenzake nao watashambuliana.
Kumbuka kuwa hata
Yuda wataupiga vita mji wa Yerusalemu kabla ya kipindi cha kuongoka kwao siku
za mwisho.
14Yuda pia atapigana
katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu
utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na nguo. 15Tauni ya aina iyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia na punda
nao wanyama wote walio kwenye kambi za adui.
Baada ya tukio
hili, au vita kuu ya kipindi cha mwisho, kila ammoja miongoni mwa walioachwa
wamataifa atakayekuja kinyume na Yerusalemu kutoka mahali popote duniani,
watatuma wawakilishi wao mjini Yerusalemu, mwaka hadi mwaka ili wakamwabudu
Bwana wa Majeshi na kuishika Sikukuu ya Vibanda. Na wale wote ambao
hawatakwenda huko, mvua haitanyesha kwao kwa kajira yake sahihi na
watasumbuliwa na tauni au magonjwa ya Misri. Mkakati wa kilimo cha umwagiliaji
hautawaokoa watu hawa waasi. Kwa hiyo, tendo la kuzidharau na kutozishika Amri
na Sheria za Mungu na kutozishika Sikukuu zake kutawasababishia maafa na
misiba. Njuga za farasi wao zitakuwa zikilia “utukufu kwa Bwana” na vyungu vilivyo
kwenye Nyumba ya Bwana vitakuwa kama mabakuli yaliyo mbele ya madhabahu. Wale
watoao sadaka na sadaka zao watazipika nyama ndani yake kwa utakatifu (Zekaria
14:16-21). Mtindo na imani ya kutokula nyama bali mbogamboga tu hautakuwa ndio
mshika dau kwenye kipindi hiki cha Milenia (soma jarida la Imani ya Kutokula Nyama bali Mbogamboga
Kwenye Biblia (Na. 183) [Vegetarianism in the Bible (No. 183)].
16Kisha walionusurika
katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda
Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu na kuadhimisha
Sikukuu ya Vibanda. 17Ikiwa
taifa lo lote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme, BWANA Mwenye
Nguvu, hawatapata mvua. 18Ikiwa
watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua. BWANA ataleta juu
yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha
Sikukuu ya Vibanda. 19Hii
itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayatakwenda
Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 20Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa
maneno haya: SIKU TAKATIFU KWA BWANA, navyo vyungu vya kupikia katika nyumba ya
BWANA vitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu. 21Kila chungu kilichoko Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwa
BWANA Mwenye Nguvu na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu
hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyibiashara katika nyumba
ya BWANA Mwenye Nguvu.
Ezekieli sura za 26
na 27 zinaielezea pia Tiro na maafa yanayoungojea mji huo. Ulishambuliwa na
Wababelonia, na pia ukashambuliwa na Wamakedonia na Wayunani. Ukafanywa kuwa ni
makao makuu ya shughuli za uvuvi kwa karne nyingi, lakini maandiko yanasema
kuwa utaangamia na kupotea kwa kusombwa na mawimbi ya maji. Hapa tunajionea
piwa kwamba merikebu za Tarshish zitatumika kama vivuko vya wafanyabiashara
watakaozitumia pia kama meli za kivita. Yavani, Tubali na Mesheki yalikuwa ndio
mataifa yaliyofanyao biashara na watu wa Tiro, kwa hiyo walikuwa ni watu wenye
nasaba asilia ya Kiyafeti zaidi kuliko ya Kihamu nah ii ndio sababu ya wao
vipimovyao vya nasaba ya damu (YDNA) zinasomeka zaidi kwa kuonekana kuwa wao ni
wa kundi la K2 na sio wa E3. Ezekieli 28 inamtaja Shetani ikimfananisha kwa
kumuita kuwa ni Mfalme wa Tiro.
Lolote kati ya
mataifa haya yanayotoa wito wa kuliangamiza taifa la Israeli litakatwa vipande
vipande. Na hii inajumuisha wale wote watakaotafuta kuwasaidia wengine katika
maangamizo yake kama mataifa tunayoyaona sasa wakiwatuma wengine kuishambulia. Iran
na Iraq watalipa gharama pia. Mataifa haya yanayojipendelea na kujiamini
yenyewe kwa ajili ya jambo hili yatadanganyika na kujaribu kuushambulia mji wa
Yerusalemu. Vita ya kidini ambayo inakuja hivi punde na itakayopelekea
kuanzishwa kwa Vita Kuu ya III ya Dunia ambayo itakuwa ni ya hatari sana.
Miaka ishirini
kabla ya vita ya mwaka 1967, tarehe 15 Mei 1947, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
lilipiga kura ya kuunda Kamati Maalumu kuhusu Palestina (maarufu kama UNSCOP), ambalo
lilianza kazi yake rasmi na kuendelea kwa ajili ya kuanzishwa ka Taifa la Israeli.
Jambo hili lilifanyika miaka thelathini baada ya Azimio la kwanza la Balfour la
Waziri Mkuu wa Uingereza aliyeitwa Balfour lililolenga kuanzishwa kwa laita
asilia la Kiyahudi mwaka 1917. Azimio la pili la Balfour lilitilia maanani lengo la kikatiba la kuanzishwa
kwa Australia. Hatahivyo, azimio la Umoja wa Mataifa lilichelewa sana kuweza
kuikoa Yuda kutoka kwenye Mauaji Makuu na Yakuangamiza maarufu kama Holocust.
Na kama ilivyotokea,Yuda walilazimika wapigane kiume ili kuanzishwa kwake.
Kwa mujibu wa
utaratibu wa mzunguko wa kipindi cha miaka sabini, kutawezekana kuwa na mwaka
kwa mwaka unaowiana kati ya hatari inayotokana na Vita Kuu ya II ya Dunia
iliyopiganwa kipindi cha miaka ya 1936-1945 na kwenye kipindi cha miaka ya 2006-2015
ambacho kitashuhudia dalili za maafa na mauiaji ya Vita Kuu ya III ya Dunia.
Tangu vita za
mwaka 1967 hadi 2007 ni kipindi cha miaka arobaini na kumekuwa hakuna toba
yoyote hadi leo, na hata hakuna dalili hiyo wakati hali halisi ya mambo ni kwamba
inakaribia kutokea. Maandiko hayawezi kutanguka. Hata hivyo, ni matumaini
kwamba watu hawa wanaweza kutubu, lakini hawajachahua kufanya hivyo. Miaka hii
sabini tangu mwaka 1948 inaishia mwaka 2018. Miaka themanini ya vipindi viwili
vya pamoja vya miaka arobaini arobaini inaishia kwenye mwaka wa kwanza wa
Yubile ya Milenia ya mwaka 2028. Kati ya miaka ya 2006 na 2018 utaratibu au
mfumo wote wa vita utaendelezwa. Tangia mwaka 2006 tunajionea matatizo yakianza
na Mungu anashughulikia na nchi za Lebanon na Iraq. Vita hii itaendelea na
kuenea hadi Syria na Iran.
Hatua za kijeshi
zinazochukuliwa dhidi ya Israeli hazina maana yoyote. Majeshi hayawezi kuwa na
mbinu nzuri au ubunifu mzuri wa kuweka uzani wa kufanikisha mikakati ya
operesheni za kivita.
Tendo la Umoja wa
Mataifa la kuilaani IsraeIi, limeifanya lijiweke lenyewe kwenye kundi hili na
utapatwa na maafa hayohayo, na kama muundo wake unavyokusudia kumiliki mahala
palipoachwa akiba na Masihi na watu wake.
Bado hatujachelewa
sana kufanya toba na kufanyika wapya.
q
Kuna maswali mengi yanayoulizwa kuhusu jinsi gani ya kuwatambua hawa Yuda na maelekezo ya Kibiblia kuhusu wale wanaojiita Wayahudi kumbe sio na jinsi ya kuwajua watu hawa. Unabii kuhusu mtiriririko wa mwendo wa Kanisa tangu kipindi cha Wasminarna hadi kipindi cha mwisho cha Kanisa la Wafiladelfia. Mateso haya yalikuwa ni kwa ajili ya kurefusha kipindi cha makanisa kutoka kipindi cha Wasmirna hadi cha mateso ya Diocletian hadi kuja kwa Masihi na sio ufafanuzi tu utokanao na maeneo mawili ya kitabu cha Ufunuo yanayohusu makanisa mawili. Maandiko haya yameelezewa pia kwenye maandiko mengine ya Agano la Kale pamoja na kazi za Bwana na mfumo wa dini ya uwongo ambao utabidi uingie huko Yudea. Unabii huu umeonyeshwa pia kwenye kitabu hiki cha Zekaria miongoni mwa maandiko yaliyo kwenye Agani la Kale.
Kwenye maeneo haya mawili tunaona kunasemwa
kwamba kuna wale wanaojiita kuwa ni Wayahudi lakini sio bali ni wa Sinagogi la
Shetani. Watu hawa wanaenda kufanywa watokee na wawepo kwenye kanisa na
hatimaye kujitukuza wenyewe dhidi ya Kanisa la Mungu na kujifanya waonekane kuwa
wao wamependwa na kukubalika na Masihi na Mungu na kwamba wamekabidhiwa mamlaka
ya kuwasimamia na kuwaongoza watu hawa wote.
Ufunuo 2:8-11 inasema: 8‘‘Kwa
malaika wa kanisa lililoko Smirna andika: Haya ndiyo maneno yake Yeye aliye wa
mateso yatakayokupata. Nakuambia Shetani
atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa
siku kumi. Uwe mwaminifu, hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. 11Yeye aliye na sikio na asikie yale
ambayo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatadhuriwa na mauti ya pili.
Ufunuo 3:7-13
inasema: 7‘‘Kwa
malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika : Haya ndiyo maneno Yake Yeye
aliye mtakatifu na wa kweli, Yeye aliye na ufunguo wa Daudi. Anachokifungua
hakuna awezaye kukifunga, wala anachokifunga hakuna awezaye kukifungua. 8Nayajua matendo yako. Tazama,
nimeweka mbele yako mlango uliofunguliwa, wala hakuna awezaye kuufunga. Ninajua
kwamba una nguvu kidogo lakini umelishika neno Langu wala hukulikana Jina
langu. 9Nitawafanya wale wa
sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni
waongo, waje wapige magoti miguuni pako, nao watajua ya kwamba nimekupenda. 10Kwa kuwa umelishika neno la saburi
Yangu nitakulinda hata utoke katika saa ya kujaribiwa inayokuja ulimwenguni
pote ili kuwajaribu wote wakaao duniani. 11Ninakuja upesi. Shika
Hatahivyo, twaweza kujiuliza kuwa ni kinanani hao na wakowapi? Je, wametoka wapi na wanataka kuwa ni kina nani wao? Je, hii inahusianaje na maandiko matakatifu ya Agano la kale na tunawajuaje watu hawa?
Dhana au fikra iliyoko kwenye Makanisa ya
Mungu yaliyoko Uingereza kuhusu Waisraeli na kuhusu Waprotestanti wa Kizungu imekosewa
kabisa na utaratibu wa vinasaba vya uzao wa watu (DNA) unadhihirisha makosa
Ukweli wa mambo ni kwamba kiasi cha chini
ya 28% ya Wayahudi kwa kweli ni Wasemiti kiasi kingine kinatokana na wana wa
Ibrahimu pia. Kwenye kipindi cha mateso cha Diocletian (kilichodumu kwa
takriban miaka 284-305), ambayo ni kuanzia mwaka 303- 311 kilichoendelea baada
ya usitishwaji wake katika mwaka 305 hadi lilipotolewa tangazo la Azimio la Kuvumiliana
mwaka 311; lililoendelelea hadi kuinuka
au kuanza kwa Uislamu mwaka 632BK, Wayahudi walikuwa na nguvu na madaraka huko
Uarabuni na wamewaongoa watu wengi na kujiunga na wao kutoka kwenye makabila ya
Kiarabu. Wamewaongoa Waedomu na Wana wa Esau kabla ya kipindi cha utawanyiko
wao walivyoenda utumwani. Walilitesa kanisa na kujaribu kulimaliza kabisa
lakini kanisa lilidumu kuwa imara katika kipindi cha muanza kwa Uislamu
ulioanza na baraza la watu kumi na mbili huko Uarabuni likiongozwa na Muhammad
(soma jarida la Utambulisho wa Kitabi cha Ufafanuzi wa Koran (Q1) [Introduction to
the Commentary on the Koran (Q1)].
Wayahudi walirudi nyuma na kujifanya kuwa ni Waarabu na kuingia Uislamu,
ingawaje wengi wao hawakufanya hivyo.
Zaidi ya 25% ya Wayahudi ni Waba wa Hamu bila kujali kaqma wana nasaba ya Kikanaani au Kimisri waliotokana na Mchanganyiko Mkubwa wa Wakanaani waliochukuliwa na kuingizwa kwenye jamii ya Israeli na kutumikishwa huko.
Takriban 52% ya Walawi wa Kiashkenazi kwa kweli wana alama ya nasaba damu ya R1a inayoonyesha kuwa ni wana wa Yafeti, ambao huenda wanatokana na waongofu wa Kikhazari walioingia kwenye jamii ya Kiyahudi mwaka 740BK. Idadi kubwa ya watu hawa wana alama ya nasaba damu ya R1b ambayo ni ya Wahiti walioendelea kudumu kwenye mtiririko ya uzao wa kifalme wa Mfalme Daudi pi, hususan kwenye mlolongo wa uzao wa Dayan na Salathiel (soma jarida la Wahiti Kwenye Nyumba ya Daudi (Na. 67c) [Hittites in the House of David (No. 67c)].
Hii ndiyo sababu kwa imani ya Kiyahudi kutoamini Ubatizo na haizishiki amri za Mungu na kuifuata Kalenda potofu ya ukengeufu wa Kibabelonia ambayo ilikuwa haitumiki kwenye utaratibu wa Hekalu na ambayo iliingizwa kwenye dini ya Kizayuni mwaka 358BK na mtu aitwaye Hillel II aliyeiingiza ikiwa kinyume kabisa na utaratibu na amri za Mungu na wanavyotakakiwa kuitunza wateule, bila kujalisha kuwa wao ni Wayahudi au la. Yeyote anayeishika Kalenda ya Hillel itokanayo na itikadi ya Kizayuni hazitii amri za Mungu na atakuwa na kujibu kwa kupotosha watu wao jambo hili miongoni mwao ni Makanisa ya Mungu yaliyotokana na mfarakano wa Armstrong na yale ya Wayahudi wanaomwamini Masihi. Karibu wote miongoni mwao hawaishiki Kalenda ya Mungu (soma majarida ya Kalenda ya Mungu (Na. 156) [God’s Calendar (No. 156)]; Kalenda Na Mwezi: Uhairishaji au Sikukuu? (Na. 195) [The Calendar and the Moon: Postponements or Festivals? (No. 195)] na Jinsi Kalenda ya Mungu Ilivyobadilishwa Katika Yuda (Na. 195B) [Distortion of God’s Calendar in Judah (No. 195B)].
Kipindi kile ambacho Mashahidi watakapokuja na kuamsha nia na hamasa ya watu kuona umuhimu wa kuzishika amri za Mungu, ndipo Wapalestine/Israeli hawa watakuwa ni wakwanza kusafiwa kutokana na ukengeufu huu. Wayahudi ambao hawabatizwi na wanaoshika Kalenda ya Hillel wataondolewa. Pia Wayahudi wale ambao hawatubu, pamoja na wale wa nasaba-damu ya Yuda wataondolewa pia wasipotubu.
Hata hivyo, ugumu wa mioyo ulioko kwenye mioyo
ya Yuda utaondolewa na watatubu na hata wale wanaosema kuwa wao ni Wayahudi kumbe
sio ila wana tu ile nasaba-damu ya kijamii ya Kiyahudi inayosomeka kwa
kushabihiana
Muundo wa jinsi itakavyokuwa Yuda na Yerusalemu tangia kipindi cha utawanyiko wake hadi kufikia Siku za Mwisho umeelezewa vyema kwenye jarida la Ufafanuzi wa kitabu cha Zekaria (Na. 021K) [Commentary on Zechariah (No. 021K)].
Kwenye andiko hilo, hususan kwenye sura ya 2, tunaona kwamba Mungu wa Pekee na wa Kweli, Yahova wa Majeshi amemtuma mwnae wa pekee kwa mamlaka yake Yahova, aliye Bwana wa Israeli ilia je na kuulinda mji wa Yerusalemu na kuufanya upya. Taifa hili lilikwenda utumwani kwa sababu ya maovu yake na kuzivunja kwao Amri za Mungu na mfumo wa Hekalu jambo ambalo wanaendelea kufanya hivyo hadi leo. Kutoka kwenye Sehemu ya I hapo juu tuliona kwamba kwenye Zekaria Sura ya 1 inatanguliwa na maonyo na wito wa kumrudia Bwana wa Majeshi kwenye sehemu ya kwanza (Zekaria 1:1-6).
Kwenye maono ya pili (katika Zekaria 1:7) Mungu anaonyesha farasi watakaofanya kazi zao kuiadhibu dunia wakitumwa na Bwana, Mungu kipindi ambacho dunia itakuwa kwenye mapumziko kwakuwa dunia imeutendea vibaya mji wa Yerusalemu na Yuda kipindi kichokuwa hakiitajiki kwao kuufanyia hivyo. Kwa hiyo, baada ya miaka sabini Mungu alianza kufanya kazi lakini Yuda na Yerusalemu hawakutubu na walifanywa upya ili kutimiza mchakato wa kurudi kwa Masihi kuendane sawa na jinsi unabii ulivosema.
Mungu atafanya kazi zake ili kuwezesha
ujenzi wa hekalu ili kuufanya mfumo wake uanzishwe kwa ajili ya kutengeneza
ujio wa Masihi. Baada ya
Katika Zekaria 2:1-13 tumeona anatajwa Mungu wa Pekee na wa Kweli ambaye ni Yahova, Bwana wa Majeshi akimtuma Masihi kuurejesha upya mji wa Yerusalemu na kuufanya kwa maranyingine tena kuwa Mji Wake Mtakatifu na Yuda kuwa ni miongoni mwa sehemu iliyo Ardhi Takatifu.
Kwenye maandiko haya
ya Zekaria tunaona maendeleo ya mfumo wa Kibabelonia katika Israeli na hususan
katika Yuda.
Kwenye jarida la
Ufafanuzi wa kitabu cha Zekaria Sehemu ya 1 hapo juu linatakiwa lisomwe kwa
undani
Sura ya 5 inajikita
na kuwa maalumu kuelezea jinsi Yuda na Israeli walivyofanya maovu na kujiharibu
kwa kujichanganya na mifumo ya Kibabeloni kupitia kwenye muundo wa dini ya
uwongo. Tunaona jinsi walivyojenga nyumba kwa kufuata mfumo wake na kuweka efa
chini yake. Sura ya 6 inamtaja mtumishi wa Mungu ambaye ni Chipukizi
litakalotengeneza na kurejesha tena Hekalu na kuketi kwenye Kiti cha Enzi na
kuhani atakayemweka na kutakuwa na amani. Hali hii itatokea kwenye kipindi
ambacho dunia itakuwa kwenye amani. Na
Zekaria 6:9:15 inasema: 9Neno la BWANA likanijia kusema: 10‘‘Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa
watu waliohamishwa yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli.
Siku iyo hiyo nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa Sefania. 11Chukua fedha na dhahabu utengeneze
taji, nawe uiweke kichwani mwa kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadiki. 12Umwambie, hili ndilo asemalo BWANA
Mwenye Nguvu: ‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye atachipua kutoka
mahali pake na kujenga hekalu la BWANA. 13Ni
yeye atakayejenga hekalu la BWANA, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki
katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo
patakuwa amani kati ya hao wawili.’ 14Taji
itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu
ndani ya hekalu la BWANA. 15Wale
walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga hekalu la BWANA, nanyi mtajua
ya kwamba BWANA Mwenye Nguvu amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii
BWANA, Mungu wenu kwa bidii.’’
Tazama kwamba Malaika wa Bwana ambaye ni Yahova wa Israeli anasema kwenye aya ya 15 (na msisitizo umeongezewa) kwamba wale waliombali watakuja kusaidia ujenzi wa Hekalu nasi tutajua kuwa Bwana wa Majeshi amemtuma kwetu. Hapa wanaelezewa wateule wa Mungu walio kwenye hali ya utawanyiko ambao ndiyo nyumba yote ya Mungu walio wateule kwenye Mwili wa Kristo, ambao ndio Hekalu la Mungu.
Kisha sehemu inyofuatia inaendelea kuelezea
utawanyiko wa watu usababjshwao na utovu wao wa kutowatii manabii wa Bwana wa
Majeshi aliowatuma kwao na ndipo alipowatawanya kwa upepo wa kisulisuli (Zekaria
7:1-14). Kwenye sura ya 8 neno la Bwana wa Majeshi lilitumwa tena kwa Zekaria
na tunaona kuwa Yahova, Bwana wa Majeshi anawaambia tena lakini ni huyu Yahova,
Bwana wa Majeshi ndiye anayewarudisha Sayuni na kwenda kukaa katikati ya mji wa
Yerusalemu. Na Yerusalemu utaitwa kuwa ni mji wa Kweli na Mlima wa Bwana au
Yahova wa Majeshi, Mlima Mtakatifun (
Kwa hiyo,
maandiko haya yanaelezea kuhusu kurejeshwa upya tena kwa Israeli na Yuda kutoka
kwenye utawanyiko wao na matokeo yake ya mwisho ya marejesho haya kwao na kwa
Yerusalemu ni toba ya mataifa
Kwenye kipindi
hiki cha marejesho ya mwisho kutakuwa na maangamizi na maafa makuu kwa kiasi
kisichowahi kushuhudiwa kwenye mchi ya Shamu (
Sura ya 10 inatuelezea
kuwa tunapaswa kuomba mvua kwenye kipindi chake cha Mvua Nyingi (
Kundi la kondoo
limeenda kusiko na mwelekeo bila ya wachungaji (Zekaria 10:2). Mungu
aliwaadhibu wachungaji pia na mbuzi (wale ambao sio miongoni mwa wateule wa Mungu),
(aya ya 3). Kwenye mmwagiko huu, Roho Mtakatifu anamwagwa juu ya watu wa Yuda
na Mungu wa Pekee na wa Kweli, Bwana wa Majeshi na atawandaa kwa vita
itakayotokea kwenye kipindi hiki cha mwisho. Wale wanaoitwa Wayahudi wenye itikadi
kali wataondolewa na makuhani wao wataondolewa na taifa la Yuda litaanzishwa
ili lishughulike na dunia kwenye wongofu wao. Wayusufu watahuishwa tena pia na
kuletwa kwenye imani ya kweli na Mungu atawarejesha tena ili “kuchukua nafasi
Kwa sasa mambo haya yanatokea huko Misri na Ashuru ambao watatiishwa chini na kuandaliwa kwa kazi yao kwenye Ufalme wa Mungu (aya ya 11) na watatiwa nguvu katika Bwana na watatembea juu-chini na kotekote kwa jina lake (aya ya 12).
Mambo haya yote yanaanza kutokea sasa na yataletwa na kuonekana hivi karibuni.
Sura ya 11 inaelezea
kuhusu mchakato wa kuvunja kwa umoja wa Israeli na Yuda na kukomeshwa kwa
ukuhani na mafundisho
Sura ya 12 inaelezea mzigo wa wito ulio kwenye neno la Bwana kwa Israeli.
Ataufanya Yerusalemu kuwa ni kikombe cha kutetemesha kwa wale wote wanaojifunga
wenyewe kwake na kwa wote watakaouzingira Yuda na mji wa Yerusalemu. Wale
wanaoushambulia watateketezwa. Wakazi wa Yerusalemu wa Yerusalemu wataongoka na
kurejeshwa kwa uweza wa Bwana Mungu wao. Wakuu wa Yuda watawatumia watu wa
Yerusalemu kuwa ni nguvu na kinga yao wakiwa wamepata uweza huo kutoka kwa
Bwana wa Majeshi (12:5-6). Yuda wataokolewa kwanza ili kwamba Yerusalemu na
nyumba yote ya Daudi wasijitukuze kwa ajili hii (12:7). Siku hiyo Bwana atawalinda
wenyeji wa Yerusalemu, na yeyote mwenye mshangao na hadithi miongi mwao atakuwa
kama Daudi, na nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, au kama Malaika wa Bwana
mbele yao (au vichwani mwao) (12:8). Andiko hili linaongeleza moja kwa moja
kuhusu Ufufuo. Daudi ameshakufa na tena tunaambiwa kuwa yeye na nyumba ya Daudi
watakuwa ni miungu wadogo kama
alivyo Malaika wa Bwana kichwani
mwao ambaye ni Masihi na mtu wa Rohoni au mwana wa Mungu.
Kwa hiyo imeandikwa:
‘Nimesema kuwa, ninyi ndinyi miungu?’na Kristo hatimaye
akajitangaza kuwa ni Mwana wa Mungu (Yohana 10:34-36).
Kutoka kipindi hiki kutakuwa na chemichemi zitakazofunguliwa
kwa ajili ya wale watakaopenda kuongoka na ubatizo ili waweze kuingia kwenye
Nyumba ya Bwana, na ulimwengu wote utaanza kuongoka. Sura ya 13 inaendelea
kuelezea wazo hili (13:1). Tangu
siku ile hakutakuwa na majina mengine tena ya vinyago au ya mapepo
yatakayokumbukwa (aya ya 2a). Pia manabii wote na roho zote chafu zitaondolewa katika Israeli. Mfumo wa
dini ya uwongo utaondolewa pia pamoja na waalimu wake wa uwongo (aya ya 2b).
“Manabii” watakoma au hawatakuwepo kwa kulazimishwa na watu wao wenyewe na
watajitangaza kuwa ni wafugaji na kusema kwamba walifundishwa kutunza akiba kwa
ajili ya vijana wao (aya ya 3-5).
Kwa sehemu zote mbili wataondolewa mbali na theluthi moja itabakia na theluthi
moja nyingine iliyobakia watasafishwa kwenye moto na watatakaswa ili wamtumikie
Mungu na (Zekaria 13:8-9).
Ili kufanikisha hilo, tunajionea kwenye Sura ya 14 kwamba Bwana Mungu
atayainua mataifa dhidi ya Yerusalemu na mji utatekwa na kuchukuliwa, nyumba
zitachomwa moto na wanawake watatekwa na kufanywa vibaya na nusu ya mji
watakwenda utumwani na watakaosalia hawataondolewa kwenye mji. Hivyo basi Mungu
atausafisha Yerusalemu na wale wasio na imani na waongofu. Na katika kipindi
hiki, Yahova ambaye ni Masihi, elohim wetu atarudi pamoja na wateule wote na
atasimama kwenye Mlima wa Mizeituni. Mlima utagawanyika vipande viwili na bonde
kuu la takriban k.m. 66 litafanyika upande wa Kaskazini na Kusini na mji wa
Yerusalemu utakuwa katikati yake kama ilivyoelezewa kwenye Sehemu ya I (aya ya
4-5).
Kipindi hiki kitakuwa ni cha taaruki kubwa na huenda kitakuwa pia cha vita
vitakavyopiganwa kwa silaha za nyukilia. Wale waliochwa kama Wayahudi
walioongoka watapigana wakiwa mjini Yerusalemu na utajiri wa mataifa
utakusanywa na watapewa wao (14:14). Tangu kipindi hiki na kuendelea mataifa
yote yaliyoupinga na kuupiga mji wa Yerusalemu watatuma wawakilishi wao waende
Yerusalemu kila mwaka ili kuitunza Sikukuu ya Vibanda. Na wale wote ambao
hawatawatuma wawakilishi wan chi zao, mvua haitanyesha kwao kwa majira yake
mwafaka na watadhikika kwa magojwa ya tauni ya Wamisri (Zekaria 14:16-19). Hekalu za Sayuni litakuwa Takatifu na kitu
cha kupendeza na muhimu sana huko Yerusalemu na katika Yuda na patakuwa ni
mahali patakatifu kwa Bwana wa Majeshi. Mfumo utakaoanzishwa pale utakuwa
umefanywa vizuri na kwa uangalifu sana na sadaka za kuteketezwa au za kuchinja
wanyama zitafanyika kwa usimamizi makini wa makuhani tena kama ilivyokuwa
zamani. Maneno haya yanatoka kwenye Maandiko matakatifu, na Andiko halitanguki (Yuhana
10:35).