Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[036_2]

 

 

 

Akungo la Misri Sehemu ya II:

Vita Vya Nyakati za Mwisho

 

(Toleo La 1.5 20110206-20141026)

 

Matukio yanayoendelea hivi sasa huko Misri hayawashangazi sana wanafunzi wanaosoma kwa bidii unabii wa Biblia kama mlolongo unaofuatia ni sehemu ya kipimo cha muda kinachoenda kutoka zama za Waashuru na Wababeloni kwenye Vita vya Carchemishi mwaka 605 KK ambapo Wamisri walishindwa na kuishia kwenye nyakati za kufungwa kwa kipindi kijulikanacho kama cha Nyakati za Wamataifa au Mataifa na mwanzo wa miaka thelathini ya mwisho kilichanzia rasmi tangu mwaka 1997 hadi 2027. Jarida hili linashughulika na mambo ya msingi na awamu inazofuatia baadae.

 

Christian Churches of God

PO Box 369, WODEN ACT 2606, AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

(Hatimiliki © 2011, 2014 Wade Cox)  

(tr. 2015)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

 

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


Anguko la Misri Sehemu ya II: Vita Vya Nyakati za Mwisho



Zaidi ya juma moja la kabla ya Mwezi Mpya wa Adari (1/12/33/120 au 3 Februari 2011) umuhimu uliwekwa kwenye fujo zilizofanyika huko Misri. Misri ni nchi muhimu sana kwenye historia ya Biblia na nafasi yake kwenye unabii inamaana sana, na inabakia kuwa na umuhimu hadi kwenye mlolongo wa matukio ya siku za mwisho. Yeyote anayeitawala Misri yupo kwenye utekelezaji wa mikakati ya Mfalme wa Kusini aliyenenwa na nabii Danieli na nafasi yake ni ya muhimu kwenye mchakato wa mchakato wa maukio yaliyotabiria kwenye Biblia. Unabii ulio kwenye kitabu cha nabii Ezekieli unaingiliana na ulio kwenye kitabu cha Danieli kinapoelezea mifumo au dini za Wababeloni na kipindi cha nyakati saba cha kufikia kwenye Nyakati za Mataifa na cha Vita vya Mwisho hadi kuifikia Siku ya Bwana (soma jarida la Siku ya Bwana na Nyakati za Mwisho (Na. 192)).

 

Mlolongo wa unabii wa Ezekieli na uhusiano wake na ule wa nabii Danieli vimeelezewa kwa kina kwenye jarida la Anguko la Misri:Uunabii Kuhusu Mikono Iliyovunjika ya Farao (Na. 036). Jarida hili limekuwepo kwenye wavuti kwa kipindi cha miaka 15 na liliandikwa mwaka 1994. Mnamo Februari 2011 idadi kubwa na isiyoweza kukadiriwa ya maelefu ya nakala kutoka kwenye lugha mbalimbali zilipakuliwa au kurudufiwa kwa hamu ya kutaka kujua hakika ya kile kinachotokea. Ndipo sasa watu wanaanza kugundua kuwa hii ni hatua ya mwisho ya kukamilisha historia. Kipindi hiki ni kile cha kuwaunganisha na kuwajumuisha pamoja Mfalme wa Kusini na kumsukuma au kumshurutisha Mfalme wa Kaskazini, jambo litakalopelekea kuongezeka kwa matukio yatakayopelekea hatimaye kuzuka kwa Vita Kuu ya III ya Dunia itakayoenea na kutambaa kuazia Afghanistan hadi Iraq, matukio ambayo yamekwishaanza tayari tangu mwaka 2001 na ambayo yataendelea hadi kufikia kiwango chake cha juu sana cha mapigano yatakayoibuka na kuendelea kutoka kwenye vuguvugu za makundi au jamhuri ya Kiislamu za pande za kaskazini na mashariki mwa Yerusalemu. Mlipuko huu na kuendelea kwake kutashuhudia maangamizo makubwa sana na yakutisha ya watu na mataifa. Unabii wa mwisho utahitimika na Masihi atachukua hatamu za kuiongoza na kuitawala hii dunia.

 

Kwenye jarida la Ufafanuzi wa Sura ya 7 ya Kitabu cha Danieli (Na. 299C) tulijionea tafsiri sahihi kuhusu Wanyama Waane na jinsi walivyojigeuza na kufanyika uwepo wa Mnyama wa Nne anayefuatiwa na Dola yene Vidole Kumi vilivyoonyeshwa na kuelezewa habari zake kwenye Danieli sura ya 2.

 

Hivyo basi, kama tunaelewa kile kinachotokea basi tutafuatilia kipindi kilichokusudiwa kuelezewa na unabii wa Anguko la Misri.

 

Kitendo cha kubadilishana mamlaka hakitatokea hadi nyakati zake zilizotabiriwa ziwasili. Kwahiyo, vita hivi vilikuwa na matokeo yake na walifana hivyo ili kwamba unabii na Maandiko Matakatifu yasitanguke. Hata hivyo, matokeo ya vita hivyo yalitumiwa kwa namna hiyo kama kuiandaa sayari kwa matokeo ya wastani wakati nyakati za kutimilika unabii zitakapofika.

 

Shetani alikuwa na kipindi chake maalumu alichopangiwa na kwamba kipindi chake cha miaka 6000 kinaishia mwaka 2027 na kitafupishwa ili kuiepusha dunia kutokana na kuangamia kabisa. Alitarajiwa na kanisa la Nyakati za Mwisho kujua kile Mungu alichokuwa anakwenda kuufanyia imani au mfumo ule.

 

Hebu na tuyaone basi baadhi ya makutio yaliyotokea tangu mwaka 1914. Tangu kushambuliwa na kuuawa kwa Archduke Ferdinand wa Austria tarehe 28 Juni 1914 huko Sarayevo na kutangazwa rasmi kwa Vita vya Serbia tarehe 28 Julai 1914 mambo yaliendelea kuporomoka tu na hatimaye dunia ikaingia kwenye vita.

 

Tarehe 1 Augusti ujerumani ilitangaza vita dhidi ya Warusi na Wafaransa na wakaishambulia Ubelgiji. 

Tarehe 4 Augusti 1914 Uingereza ilitangaza vita dhidi ya Wajerumani kutokana na kitendo chao hiki cha kuishambulia Ubelgiji.

Tarehe 5 Augusti 1914 Austria ilitangaza vita rasmi dhidi ya Warusi. Na Warusi, Waingereza na Wafaransa wakatangaza vita dhidi ya Waturuki.

Tarehe 26-28 Augusti 1914 Wajerumani walifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuwapiga na kuwashinda Warusi kwenye mapigano yaliyofanyika huko Tannenburg. Wajerumani waliishambulia pia Ufaransa na uingiaji wao huko Paris ulifanikiwa kwa vita au mapigano ya Marne. Waingereza waliingia Ufaransa na Mapigano ya huko Ypres yalipinganwa had miezi ya Oktoba-Novemba 1914. Hii ilianzisha au kusababisha vita kubwa/trench warfare upande wa mbele wa magharibi. Kwa hiyo tunaangalia hatua kuu na muhimu ya historia mapigano au vita na ile ya Dunia ya mwaka zama 1914 na ni kama kipindi kinachopelekea kuanza kwa vita au mapigano ya Carchemish mwaka 605 KK yapata miaka takriban 2,520 au kipindi cha nyakati saba zilizopita. Kumbuka kuwa, hitimisho kamili la kipindi cha miaka 2520 tangu Carchemish mwaka 605 KK kilikuwa ni mwaka 1916. Kwa hiyo miaka miwili ya mwisho ya mwandamano wa kwanza ilikuwa ni tangu mwaka 1914 hadi 1916.

 

Jarida la Anguko la Misri (Na. 036) lilsema kwamba: “Jambo lingine lilikuwa ni kuingilia mambo ya dunia hata kama yanaonekana kuwa ni madogo, lilikuwa ni Banki ya Uingereza ilipewa maklaka kuchapisha pesa za maratasi kwa kulingana na kikomo cha sheria halali. Kitendo hiki kilisababisha mchakatowa mporomoko wa kiumchumi, ambao utafikisha madhara yake kamili kwenye madeni ya kifedha na utumwa utakaosababisha na hali hiyo kuwakumba watu wote walio kwenye mataifa yanayozungumza lugha ya Kiingereza au nchi za Jumuiya ya Madola. Madhara yaliyotajwa kwenye Kumbukumbu la Torati 28 (soma jarida la Baraka na Laana (Na. 75)) ndipo hapo yatakapoonekana.” Ni kama tujuavyo sasa hii iliendelea kutokana na ukosefu wa mashindano ya kisiasa ya Wamarekani kwenye sheria yao ujulikanayo kama ‘Sheria ya Kulinda Muungano’ ya [Federal Reserve Act] ya Decemba 1913 iliyoanzisha uhusiano wa namna fulani wa mabenki ambayo yanamikiliwa na Wamarekani. Kwa kipindi chote cha tangu mwaka 1914 hadi 1996, sheria hii ya ‘the Federal Reserve Bank’ ilipelekea kumiliki utajiri wote na dhahabu zote vilivyohifadhiwa kwenye nchi yote ya Muungano wa Majimbo ya Marekani. Hadi kufikia mwaka 2008 nchi ya Marekani ilijikuta imefilisika kabisa na ikapelekea mabenki mbalimbali ya dunia kuanzisha kitu kinachojulikana kama Agizo Jipya Ulimwenguni [New World Order] chini ya itikadi Moja Ulimwenguni kote chini ya udhibiti wa Benki ya Dunia. Kwenye miaka ya 2009-10 walijaribu kujitwalia uthibiti wa mifumo ya kiuchumi ulimwenguni chini ya kigezo au mfumo usiochaguliwa wala kupendekezwa wa uthibiti wa uchumi wa Umoja wa Mataifa. Umoja wa Mataifa pia unatumia ulaghai wa kisayansi kuhusu hiki wanachokishadidia kuwa ni Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa kuogopa ukakati uliopo kwa mbali wa kuitaka dunia yote ijisalimishe na kumpa mamlaka yao yote Mnyama. Tukio hilo litatokea kama kitabu cha Ufunuo kinavyosema kuwa litatokea.

 

Kumbuka kuwa jarida la “Anguko la Misri” liliandikwa mwaka 1994 na kwa hiyo vita vya mwisho vilikuwa vinatarajiwa kutokea. Maneno yaliyo kwenye jarida hili yalionyesha kile kilichokuwa kinatarajiwa kutokea na kwa kweli, kilitokea na kinaendelea kutokea hatua kwa hatua.

 

“Vita ya I ya Dunia iliendeleza dhana na mbinu mkakati za vita vilivyoko sasa. Hawa hawakuwa kama mashujaa wa zamani walioingia Shimoni wakiwa na panga zao na ngao. Muhtasari mfupi tu wa hadithi au historia inaweza kuandikwa kama hivi.

Tarehe 18 Februari 1915. Kulifanyika ulipizaji kisasi kwa kuvunjwa kwa kikosi cha manowari za Kijerumani kulikofanywa na majeshi ya Waingereza, Ujerumani ilifanya ulipizaji wa kisasi kwa kukivunja kikosi cha manowari za Waingereza.

Tarehe 22 Aprili-25 Mei 1915. Vita ya pili ya Ypres ilishuhudia matumizi ya mabomu ya sumu yalifanywa na Wajerumani kwa mara ya kwanza.”

 

Vita ya Wenewe kwa Wenyewe ya Wamarekani ilikuwa ni mwanzo wa vita vilivyoko sasa vya matumizi ya silaha za atomatiki na zenye uwezo wa kuvunja na kuangamiza vitu vizito. Kitendo cha waabudu Shetani cha kuutumia mfumo na imani ya Kimasoni chini ya kiongozi wao Albert Pike, ulipanga mkakati wa vita tatu kuanzia mwaka 1871. Vita Kuu ya I ilikuwa ni uwanja wa majaribio wa silaha za kutisha sana na za maangamizi zaidi.

 

Mataifa ya Kisemitiki ya kati yaliundwa tena. Taifa la Israeli lilizaliwa tena kwa kupitia Azimio la Balfour la mwaka 1917 (Kulikuwa na Maazimio mawili ya Balfour mwaka 1917, la kwanza lilihusu nchi ya asili ya Wayahudi na la pili lilihusu msingi halali na wa kisheria wa kuanzishwa kwa taifa la Australia.) vita vya Wasemitiki/Wamisri/Waaryani vimeanza tena.

Tarehe 25 Aprili 1915. Majeshi ya muungano yalijipanga kwenye Peninsula ya Gallipoli lakini yalishindwa kuthlakini yalishindwa kuthibiti Malango ya Bahari ya Dardanelle. ANZAC inazaliwa.

Italia ilijiunga kwenye vita upande wa jeshi la mataifa ya ushirika.

Uingereza iliunda serikali ya umoja chini ya Asquith.

Mashambulizi mabaya ya majeshi ya ushirika ya Waingereza na Wafaransa yalishindwa.

Tahere 6 Septemba 1915 Bulgaria ilijiunga kwenye umoja wa mamlaka ya katikati.

 

Kipindi cha miaka 2520 ilikuwa juu na vita vya mwisho vilianza kwa nguvu. Kwenye jarida la Anguko la Misri:

“Tarehe 21 Februari hadi tarehe 16 Desemba 1916. Vita ya Waverdun ilishuhudia mashambulizi makubwa ya Wajerumani upande wa mbele wa kagharibi na hasara kubwa na yakutisha kwa sehemu au pande zote mbili.

Tarehe 20 Marchi 1916. Mapatano ya siri ya Waangosaxoni wa Kifaransa au Wasykes-Picot yalikunguwazwa kwa kuzuiwa na Dola ya Waturuki, ambayo hadi kuanza kwa vita hii walikuwa wamewajumuisha Wapalestina. Misri ilikuwa ni sehemu ya muundo huu wa kidola.

Tarehe 24 Aprili 1916 ilishuhudiwa kuibuka kwa maadhimisho ya sikukuu ya Easter huko Ireland iliashiria mabadiliko ya mamlaka ndani ya Visiwa vya Uingereza wenyewe.

Tarehe 31 Mei hadi tarehe 1 Juni 1916. Vita vya huko Jutland, ni kambi pekee ya majeshi ya majini yalianzisha mapigano kati ya Waingereza na Wajerumani yakikimbia na kushuhudia Waingereza wakipoteza wanajeshi wengi na Wajerumani wakiwapoteza askari wao pia.

Mashambulizi makubwa ya Mrusi aitwaye Brusilov yalishindwa.

Tarehe 1 Julai 1916. Vita vya Somme ilishuhudia matumizi ya kwanza ya vifaru kwa mara ya kwanza vikitumiwa na Waingereza.

Tarehe 27 Augusti 1916. Romania na Ureno zilijiunga kwenye vita kupigana na Wajerumani.

Marekani, huenda ilinufaika na vita, kwa kununua visiwa vya Virgin Islands. Ilipeleka majeshi yake huko Santo Domingo, Jamhuri ya Dominika na yakabaki huko hadi mwaka 1924.

Tarehe Februari 1917 ilishuhudia mapinduzi ya Urusi na kupinduliwa madarakani  kwa Tsar Nicholas.

Tarehe 11 Marchi 1917. Uingereza iliutwa mji wa Baghdad kutoka kwa Waturuki. Waturuki wa jamii ya Ghuz Turks, walioitwa hivyo kutokana na mstari wao wa kiuzawa wa Seljuks, waliishi huko Baghdad tangu karne ya 12 na waliwashinda kivita majeshi ya magharibi ya  Byzantine kwenye Mapigano ya Myrio-cephalum ya mwaka 1176. Hii ilifikisha ukomo wa uamsho wa wa Byzantines ulioanzia kushindwa kwa jamii ya Seljuks wa Rumi kwenye crusade ya kwanza ya huko Nicća na Dorylćum. Ushindi huu uliwafanya wapiganaji wa crusade kutembea kwa miguu wakipitia Syria na kuitwaa miji ya Edessa na Antiokia mwaka 1098 na kisha Yerusalemu mwaka 1099.”

 

“Maamuzi ya matokeo haya ya awamu hii yalianzia mwaka wa 1917.

Tarehe 6 Aprili 1917. Marekani ilitangaz vita dhidi ya Ujerumani.

Tarehe 31 Julai hadi 10 Novemba 1917. Ushindi wa Vita vya Passchendale, mashambulizi makubwa sana ya Waingereza, yalipingwa na mashambulizi ya nguvu mara mbili ya Wajerumani.

Tarehe 24 Octoba 1917. Vita vya Caporetto ilishuhudia kushindi vibaya wa Wataliano.

Mapinduzi ya mwezi Octoba yalishuhudia Bolsheviks akiiwapindua serikali ya kijimbo. Lenini akafanyika kuwa kamisaa mkuu na Trotsky akafanyika kuwa Kamisaa wa au Waziri wa Mambo ya Nje.

Ushindi wa mataifa shirika ya Jumuia ya Madola huko Mashariki ya Kati ulishuhudia Wapalestina wakitawaliwa na Waisraeli. Kisima cha nadhiri au cha ahadi cha Beersheba, kilitwaliwa na kikosi cha farasi cha Waaustralia kilichojulikana kama Light Horse kwenye shitaka kuu la mwisho walilolundikwia watu wanaoitumia lugha ya Kiingereza. Kutokana na hiyo, ndipo Azimio (la 1) la Balfour Lilitangazwa ili kutilia uwezekano wa kuwepo kwa taifa la Kiyahudi ndani ya ardhi ya Palestina.

Tarehe 9 Decemba 1917. Majeshi ya ushirika wa Jumuiya ya Madola yaliutwaa mji wa Yerusalemu. Mji huu ukawa chini ya milki ya Israeli tena baada ya miaka 1,847.

 

Hiki kilikuwa ndicho chanzo kikubwa cha vita kwa mtazamo wa kinabii. Ukumbusho wa vita umeainishwa kwa mujimu wa vipengele vikuu vifuatavyo.

Tarehe 3 Marchi 1918. Mkataba wa amani au mapatano ya Brest-Litovsk kati ya Urusi na Ujerumani yalipelekea Urusi kujingoa vitani.

Tarehe 15 Julai hadi 2 Augusti 1918 ilishuhudia kushindwa kukubwa kwa mashambulizi ya Wajerumani kwene Mapigano ya Marne.

Tarehe 16 Julai 1918 kulishuhudiwa kuuawa kwa Tsar mstaafu, Nicholas II na familia yake.

Tarehe 18 Julai 1918 kulishuhudiwa kuanza kwa mashambulizi ya majeshi ya Washirika. Ujerumani ililazimika kufanya mapatano.

Wataliano wapata ushindi mkubwa uliowalekea kusalimu amri majeshi ya Vittoria Veneto na Austria-Hungary.

Tarehe 9 Novemba 1918 kulishuhudiwa mapinduzi ya Ujerumani na kuacia madaraka kwa Wilhelm II. Mfumo wa utawala wa Jamhuri ukatangazwa.

Tarehe 11 Novemba 1918. Ujerumani ilikubali Kusimamisha kwa muda na Vita Kuu ya I ikaisha.

Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe huko Ireland ilianza.

Lenin akajinyakulia mamlaka ya serikali na utawa wa huko Bolshevik na vita vya wenyewe kwa wenyewe iliendelea hadi mwaka 1920.” (ibid)

 

Mambo haya yanaonyesha jinsi hatua hii muhimu nay a kipekee aina yake katika historia ilivyohusisha mataifa yaliyotajwa kwenye unabii na nyinginezo zaidi. Lengo lake lililo wazi kutokana na orodha hii ni kwamba tunakitarajia aina nyingine mpya ya vita ikiibuka ambayo itakuwa ni tofauti kabisa na aina nyingine zozote zilizopita. Na hasahasa, mchakato huu wa nyakati za mwisho ulikuwa ni wa kufanyiza uwezekano wa vita vya mwisho na kuanzishwa kwa Ufalme wa Mungu. Na pia mifumo ya kifedha iliyokuwa ikifadhili vita hivi ilikuwa ikimilikiwa au kuthibitiwa na mabenki yaliyoibuka ya kile kitakachokuja kufanyika kuwa ni Agizo Jipya la Ulimwenguni na utawala wa Mnyama wa Nyakati za Mwisho. Waliitumia migongano hii tangu mwaka 1914 ili kujiimarisha kwa kujiongezea na kujitwalia uwezo na mamlaka zaidi waliyopewa visivyo halali na Bunge la Marekani tangu Decemba 1913 kwa kile kilichofanyika kuwa sheria ya uhaini mkuu sana ambayo haijawahi kutokea kutungwa wakati mwingine wowote wa kudumu kwa ulimwengu.

 

“Historia ya mlolongo na matukio haya yameandikwa kwa ufupi kama ifuatavyo:

Mwaka 750 KK. Wanubi waliijumuisha Misri chini ya himaya ya Wanubi.

Mwaka 732 KK. Waashuru chini ya mfalme wao Tiglath Pileser III waliutwaa au kuuteka Damascus na kuifanya Israeli ikiwa kama ufalme wa Yuda kuwa nchi ya kuitoza na kukusanyia kodi kwenye eneo hili.

Mwaka 729 KK. Tiglath Pileser aliitwaa Babeli.

Mwaka 724-721 KK. Shalmaneser V aliitwaa Israeli. Mrithi wake Sargon II akayafukuza makabila kumi. Ufukuzaji huu ulikuwa ni zaidi ya ule alioufanya Araxes katika siku zake.

Mwaka 710 KK. Wacimmerians walishambulia kwa kuziharibu au kuziangamiza Urartu na Phrygia. Sargon aliuawa akiwa anapigana na Wacimmerians mwaka 705 KK na alirithiwa na Senakeribu.

Mwaka 696 KK. Waashuru waliutwaa mji wa Tarso.

Mwaka 687 KK. Kiti cha Ufalme wa Lydia upande wa magharibi kilichukuliwa na Gyges.

Ashuru sasa inamudu kuishinda na kuitwaa Misri na ikafanyika kuwa ni dola kuu nay a muhimu kwa upande wa magharibi mwa Asia.

Miaka ya 669-663 KK. Waashuru waliishambulia Misri na kuifanya Misri kuwa misaidizi wake wa kuaminika.

Jeshi la Misri ndipo likavunjika kwa maana ya msingi.

Mwaka 605 KK. Nebukadneza alimshinda Neko, aliyekwenda kuwasaidia Waashuru, kwene vita vya Karkemish. Jeshi la Misri lilifuatiwa kwenye mipaka ya Misri lakini Nebukadneza hakuingia kwenye nchi hii wala kwene ufalme wa Yuda (2Wafalme 24:7). Kipindi cha awamu saba za nakati kilianza.

Wamisri walifaulu kuishinda tena Gaza baada ya vita vya mwaka 601 KK na kwa ajili ya hiyo ushawishi wao uliongezeka huko Yerusalemu licha ya maonyo ya nabii Yeremia.

Mnamo mwaka 599 KK Nebukadneza aliwashinda Waarabu wa mashariki mwa Syria na Palestina.

Mwaka 598 KK aliamudu kuuhusuru kwa kuuzingira mji wa Yeerusalemu na akaushinda kwenye tarehe za 15-16 Marchi 597 KK.

Akarudia tena kuuzingira na kuuangamiza kabisa mji wa Yerusalemu mwaka 586 KK.

Yapata kama mwaka 567 KK. Misri ilijaribu kujiunga tena kurudisha utaifa wake na kumtawaza mfalme wao aliyejulikana kama Farao Amasis, aliyerithi kiti cha Hophra, akakabiliwa na Nebukadneza kwenye mwaka wake wa thelathini na saba (567 KK).

Mwaka 525 KK. Cambyses aliishambulia Misri na kuivunja mkono wake mwingine.

 

Mwiho wa awamu ya kwanza kulishuhudiwa kuhamishwa kwa mamlaka kutoka kwa watu wa jamii ya Wasetiki kwenda kwa Waayani waliowakilishwa na Wamedi na Waajemi. Makundi haya mawili yaliunganisha nguvu, ambao waliweka zamu za kutawala. Misri ilikuwa chini ya mamlaka ya makundi haya yote mawili. Mwisho ma kipindi cha muungano wao uliodumu kwa kipindi cha nyakati arobaini mbili za miaka ulikuwa ni mwaka 525 KK kwa kushambuliwa na Cambyses. Mzunguko wa mara saba uliodumu kwenye kipindi hiki cha ukomo uliaucha mwaka 1995/6 kuwa ni kama mwisho wa Awamu ya 2. 1996/7 ulikuwa mwaka wa Hamsini wa utawala wa Wayunani kwenye mzunguko wa mwaka wa Sabato wa miaka 2520 Kushambuliwa kwa Misri na Cambyses mwaka 525 KK. Mwaka huu ulikuwa mwisho wa Nyakati za Wamataifa. Mwaka 1997 ulikuwa ni mwaka wa mavuno mara dufu wa mwaka wa Sabato na ni mwaka wa kwanza wa Usomwa tena wa Torati ambako kulifanyika mwaka 1998. Mchakato wa utoaji maonyo ulikuwa umeanza.

 

Mkakati wa mwisho wa Agizo Jipya Ulimwenguni ulikuwa unaendelea kwenye miaka hii ya 1995 na 1997 kipindi cha Utimilifu wa Mataifa kilikuwa kinaishia kabisa na Agizo Jipya la Ulimwengu lilianza kuchukua mkondo wake na kutawala. Kati ya miaka ya 1997 na 2001 mkakati ulianza wa kuelekea kwenye Vita Kuu ya Dunia. Iraq ilishambuliwa na Marekani kwa kile kilichopewa jina la Oparesheni Dhoruba ya Jangwani kwenye Vita vya Kwanza vya Iraq. Mikakati ya Uibiti wa Kifedha au Kiuchumi ilianza kuandaliwa ili kuipeleka dunia kwenye utumwa wa kiuchumi uliotokea mwaka 2009.

 

Kuna maana yake fulani kwamba millennia ya pili tangu kuzaliwa kwa Kristo iishie mwaka 1996. Kristo asingeweza kuzaliwa kabla au baada ya mwaka 4 KK (uliopewa wa kifo cha Herode kati ya siku ya 1 na 13 Abibu mwaka 4 KK). Hivyo basi angekuwa amezaliwa mwaka 5 KK au mapema yake. Soma majarida ya Maana ya Mwaka 2000 (Na. 286) na Umri wa Ubatizo wa Kristo na Urefu wa Kipindi cha Huduma Yake (Na. 19).

 

Mfalme wa Kusini alikuwa ni Mwingereza kabisa na hatimaye, akashirikiana na Marekani na akachukua fursa ya kuwa mikono ya vita ya Mfalme wa Kaskazini kukifuatiwa na kuanzishwa kwa ushirika wa kijeshi wa NATO baada ya kuzishinda nguvu za mashoka za Axis. Misri ilikaliwa na kutawaliwa na Waingereza na mnamo mwaka 2520 wa awamu yao ya Kwanza ya kuikalia iliishia. Matukio yaliendelea cha chinichini na hatua ilibidi ichukuliwe kwa ajili ya vita vya mwisho.

Misri ya Sasa

Yubile ya 118 ilikuwa mwaka wa 1927 na mwaka wa Kwanza wa Yubile ya 119 ulikuwa ni mwaka wa 1928. Mwaka 1928 chama cha Udugu wa Kiislamu cha Misri kiliundwa. Wakati huu wa tangu hapo hadi mwaka 1953, Misri iliandaa harakati za kudai uhuru. Wanachama wa Udugu wa Kiislamu wamekuwa wakikandamizwa huko Misri tangu mwaka 1952 na waharati za dharura mavuguvugu ya kudai uhuru. Mwaka 1953 Misri ilijitangazia uhuru wake chini ya Gamal Abdel Nasser na mwaka 1956 Misri iliutwaa mfereji wa Suez Canal kutoka kwa Waingereza. Huu ulikuwa ni mwisho wa miaka 40 ya Mkono wa Kwanza na ilikuwa ni miaka 2520 au nyakati saba tangu dhana yake ya kupata uhuru kutoka kwa Madola ya Kaskazini takriban mwaka 565 KK. 

 

Misri ilipitia vipindi vingi vya kushambuliwa na kushindwa na Waisraeli tangu mwaka 1967 na kuendelea. Mwaka 1981 ilianza kutawaliwa na utawala wa kiimla wa Rais Hosni Mubarak. Kwa kipindi chote cha miaka 30 ya utawala wa chuma wa Mubarak, Misri ilijikuta ikijikandamiza yenyewe. Ilikuwa ni nchi ya utawala wa Kiislamu lakini haikuwa ya kihafidhina kama wafuasi wa Udugu wa Kiislamu walivyokata iwe na wajapata fursa ya kuitawala. Wamisri wa madhehebu ya Kikoptiki ambao wako takriban 10% tu nchini humo, walishurutishwa kuiacha imani yao asilia na wakageukia kwenye imani za Ukristo wa Ulaya na kumsaidia yeyote aliyekuwa anawapinga wanachama wa Udugu wa Kiislamu ambao wenyewe wana ushawishi na kuungwa mkono na 20% ya Wamisri wote. Na hadi sasa, wafuasi wa Udugu wa Kiislamu wapo kwenye miaka miwili ya kukandamizwa na kuteswa nchini humo. Wamebadilisha mwonekano wao kama mbinu yao ya kueleweka zaidi na wanaonekana sasa kuwa ni kama wanademokrasia zaidi na wasiokuwa na uhafidhina wa kidini sana. Lakini je, ni kweli ndivyo walivyo kutoka mioyoni mwao? Tutajua hayo hivi karibuni.

 

Hiyo hatahivyo inaonekana kuwa ni ulaghai tu na ndiyo maana walifikia hatua ya kupinduliwa na kisha kupigwa marufuku na kuhesabiwa kuwa ni kikundi cha kigaidi na jeshi lililojiunga pamoja na kisha kufanya mapinduzi na kuwaondoa madarakani. Mashitaka na migogoro inaendelea tangu mwaka 2014.

 

Taifa la Marekani lilikuwa linathibiti mambo na kuisaidia Misri wakati wote wa utawala ule wa chuma na wa kiimla wa Mubarak na kwa kweli wanaendelea kuiunga mkono Misri kwa kuipa misaada ya takriban vifaa vya ujenzi vya takriban bilioni 1.5 hadi 2 kwa matumizi ya kijeshi kil mwaka. Hata hivyo, Misri baada ya mapinduzi ilifanya makubaliano ya kimahitaji na Urusi kwa Mikono. Ushawishi wa Urusi katika Mashariki ya Kati ndipo unaanza kukua.

 

Mapinduzi yaliyoikumba Kaskazini mwa Afrika yakianzia Tunisia yaliyosababishwa na hali ya kutoridhishwa na hawa maimla wa Kiarabu na ubadhirifu wao uliowapelekea kuwa na ufisadi mkubwa na wa kupindukia kwenye nchi hizi. Hali ngumu ya kupanda bei ya vyakula kwa takriban 220% iliyowarudisha kwenye matukio ya ugumu wa maisha wa miaka ya 2007/8 kulichochea mlipuko wa hali hii ya waka. Hali ya dhuluma na maonevu nchini Tunisia na Misri kulichochea mapinduzi na ndivyo ilivyotokea. Marekani ilijitahidi kumsaidia rafiki yao Mubarak na sasa mkakati wa Marekani ni kuitimia haiba iliyonayo Umoja wa Mataifa ili kupata watu wa aina kama ya watu Dr. Mohamed El Baradei.

 

Tatizo ni kwamba El Baradei hauna watu wanaomuunga mkono wala hana ushawishi wa kutosha nchini Misri. Amekuwa akiishi nje ya Misri kwa miongo kadhaa na alijikuta akishindwa vibaya alipojaribu kujiunga kwenye upinzani. Ukweli ni kwamba hakukuwa na upinzani unalioeleweka kwa kuwa viongozi wake walikuwa wakitiwa mbaroni na kuteswa hata kuuawa au kupotezwa na utawala huu haramu na wa kiimla wa Mubarak. Mwingine amekuwa sasa amenyamazishwa pamoja na Udugu wa Kiislamu. 

 

Ukweli na hali halisi iliyopo ni kwamba Udugu wa Kiislamu walitangaza machafuko yao hapo zamani na walianza kwa mbinu iliyowapelekea waiachie nchi isiyoongozwa na sheria za kidini na kujikusanya wenyewe kama ni umoja wa wanataaluma wa Kimisri na kujipatia umaarufu. Kinajifungamanisha na vyama vya wanataaluma wa Misri, makazi ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kwene programu za kuhudumia jamii. Kimekuwa kikisaidia harakati za kidemokrasia na huku pia kikikosoa sera za mambo ya nchi za kigeni za Marekani. Marekani haipendi kukosolewa na kuna maoni na mitazamo ya namna nyingi kuhusu nini hasa wanachokikusudia. Haki za kidini za Marekani zinauona kuwa wahafidhina na wasipewe haki ya kutawala hawa wa Udugu wa Kiislamu kama hali mbaya na ovu sana. Wamarekani walio kweye mstari wa mbele watajitengenezea maadui kutokana na watu hawa.

 

Imekuwa ikizuiwa kuibuka au kuendelea bali imahifadhiwa kutendwa. Imetangazwa kuwa shambulio la kigaidi lililofanyika hivi karibuni kuwa ni kitendo cha woga. Imetakuwa kuwa waangalifu sana kuchukulia nafasi yake kuwa ni kama upinzani usio na maana au madhara kuwatumia vijana na watoto wadogo walichochewa ili kuendeleza. Kuna kamati za watu kumi wanaoongoza na kupanga harakati za kuenea kwa itikadi hii ya Udugu wa Kiislamu zilizoonyeshwa kwenye Kamati zao. Ndipo Englund kwenye aliliambia gazeti la The Washington Post kwamba: vikundi vinavyoendesha maandamano vimeunda kamati za watu za kushughulikia kuhujumu serikali; Udugu wa Kiislamu ni kikundi moja wapo. Wakati waangalizi wake wa nane wa kikanda walipotiwa mbaroni juma lililopita, hawakuchagua kutumia njia ya kujikusanya ili kujilinda, ili wasiharibu mpango wao na lengo lao kuu la kuondoka kwa Mubarak.

 

Itatafuta kuwatenganisha wanajihadi wafana fujo ili waweze kuwashambulia wapiga kura waungwana wa Kiislamu. Hivyo ndivo inavyokwenda kuwa. Hata hivyo, ni marafiki wa Hamas na Wairani waliiona hiyo kama fursa ya kuwaondoa watu wenye kasumba ya Kimagharibi huko Misri na kuitenganisha Israeli na Magharibi, jambo litakalopelekea kuzuka kwa vita. Kwa sababu zote zilizopo hapo juu, maoni kuhusu jambo hili ni mengi na yanatofautiana. Maoni yanayolenga kwenye mtazamo kwamba lengo lake kuu ni kumuondoa Mubarak na kuleta amani huko Misri kwa fikra kwamba wataichukua Misri na kuliunda taifa lililo kinyume na hata linaloipinga Marekani na Taifa adui. Historia inaonyesha kwamba watachukuliwa na mifumo hii ya Kaskazini katika Nyakati za Mwisho kwa vyovyote vile, baada ya mgogoro mkubwa.

 

Utawala wa chuma wa Mubarak iliutumia upinzani huu wa Waislamu kuhalalisha utawala wake wa kiimla. Ili watumia wafungwa kuwakandamiza waandamanaji hawa kwa nguvu na fujo. Mbinu ilikuwa ni kuwafungulia wafungwa viwanjani ili wawashambulie na kuwapora waandamanaji ili kuwadhalilisha waandamanaji na mpinzani yeyote. Polisi pia walikuwemo kwenye matendo haya. Mata kadhaa kulishuhudiwa pia kwamba mashambulizi yaliyofanywa kwenye vituo vya polisi na wasioathirika walishuhudia wafungwa waliachiliwa pia na wapinzani wakidhalilishwa pia kwenye matatizo haya makuu matatu. Wananchi sasa wanafanya shughuli za ulinzi na kuweka vizuizi kwenye mitaa na majimboni mwao ili kuzuia vitendo vya wizi na uporaji.

 

Vuguvugu la Udugu wa Kiislamu lilipigwa marufuku na Mubarak lisijihusishe kabisa na masuala ya kugombea kwenye uchaguzi na kwenye harakati zozote za kisiasa. Laniki bado kilijiungaunga chenyewe na kufanyika kuwa ni kundi kubwa lililoonyesha upinzani mkubwa nchini Misri na licha ya kupigwa kwao marufuku, wana wawakilishi 7 kwene bunge la Misri wanaoliunga mkono. Kilichangia (ingawaje sio kwa moja kwa moja) kumpelekea El Baradei iwe ni vigumu sana kwake wakati wa kuondolewa kwa Mubarak. Tatizo hasa lilikuwa ni kwamba hakukuwa na viongozi hasa na wa kweli kwenye upinzani na jeshi likalazimika kuchukua madaraka. Jeshi likasema kwamba halitawakandamiza waandamanaji na kwamba ni lazima Mubarak aondoke madarakani. Ukweli ni kwamba El Baradei hakuwa na wakumsaidia wala wafuasi na hivyo, Udugu wa Kiislamu wataendesha mkakati hadi kujiunga pamoja hadi kuupata uongozi. Adui halisi wa mchakato wa kidemokrasia ni ukweli kwamba Marekani ndiye kiongozi wa mkakati huu wa Agizo Jipya Ulimwenguni na mamlaka ya Kaskazini zitashurutisha uundwaji upya wa muundo wa Mashariki ya Kati.

 

Ofu waliyonayo Israeli ni kwamba vuguvugu hili la Udugu wa Kiislamu likichukua serikali na kuingoza Misri, sio tu kwamba itamaanisha kutakuwa na nguvu kubwa za Uislamu huko Gaza, bali pia na chama cha Fatah inayokaliwa na kuongozwa na Mamlaka ya Wapalestina. Israeli watajihisi kutishiwa. Wako tayari kuishambulia Iran hata sasa hivi na inasubiri tu kitu cha kuchochea. Uongozi kama huu kutoka Misri utawajumuisha pia Hamas na Hezbollah na kubalisha uwiano wa uongozi kuhusu Fatah. Hezbollah wapo kwenye hali ya kuwatupia maroketi Wairani kutoka Lebanon na sio kuwa wanawachukia Israeli peke yao, bali wanawachukia Wazungu pia. Hali kama hii inaufanya mkakati wa ujenzi wa vinu vya nyuklia wa Irani uwe wa hatari sana hata kwa miji mashuhuri iliyoko Ulaya. Shinikizo la maandamano ya Tunisia na Misri limekwisha onekana pia huko Syria na litaendelea kuenea hadi Saudi Arabia kwingineko. Usemi wa Wamarekani kuhusu demokrasi na huku wakiwakumbatia maimla na tawala zao dhalimu kwa sababu zao za kimamlaka.

 

Hofu kuu iliyopo ni kwamba Udugu wa Kiislamu unaweza pia kuvunja mikataba iliyowekwa kati ya Waisraeli na Wamisri mwaka 1979 iliyofanikiwa kuwekwa chini ya uongozi wa Anwar Sadat. Pia hii itaweza kuathiri utendaji kazi wa Mfereji wa Suez Canal. Inahofiwa pia kwamba wanaweza kuathiri mikakati iliyopo ya kupigana na kukomesha itikadi kali za kigaidi ulimwenguni kote. Uhusiano wao na Hamas unaonekana kama unaashiria kuwa maandamano yao ya kupinga hayaashirii usalama. Ni hali hiyohiyo ndiyo inayojitokeza huko Iran a watu hawataweza kurudisha nyuma nguvu za majeshi ya Waislamu yaliteka mahali. Misri itakumbana na maafa kama hayohayo. Tawala za kikatili na zisizo na hata chembe ya huruma za Waislamu wa madhehebu ya kishia pamoja na majeshi yao yenye roho ngumu ya vikozi vya Walinzi wa Jamhuri hawapasi kupuuzwa au kudharauliwa.

 

Vuguvugu la Kiislamu litakazia upinzani wake kupinga mifumo ya Kaskazini na utazipindua serikali zilizopo sasa zilizowekwa kama vibaraka wa Marekani na washirika wake. Tendo hilo litafanyika ili kuhalalisha uingiliaji wa kijeshi katika Mashariki ya Kati kwa kiwango kikubwa kuyakalia maeneo mengi kutoka Yerusalemu. Utawala wa Mnyama utayakalia maeneo mengi kutoka Gaza hadi Yerusalemu kwa kipindi cha miezi 42 cha mwishoni na cha Mashahidi Wawili (soma jarida la Mashahidi (Wakiwemo Mashahidi Wawili) (Na. 135)). Pia soma jarida la  Mwaka 2012 na Mpingakristo (Na. 299D) ili kuujua wakati unaokusudiwa.

 

Mchakato wa Vita vya Mwisho umeelezewa kwenye majarida ya Miaka Thelathini ya Mwisho: Harakati za Mwisho (Na. 219) na lile la Vita vya Hamon-Gogu (Na. 294). Majarida haya yanajumuisha unabii wa kipindi cha tangu mwaka 1997 hadi mwaka 2027 ambao pia ni mwaka wa yubile ya 120. Kwenye majarida hayo, mwanzo wa vita umeelezewa tangu mwaka 2001 wakati walipoanza kujihusisha na vuguvugu huko Afghanistan na mwenye mataifa yanayoishia kutamkwa “Stans” yaliyokuwa kwene ushirika wa iliyokuwa hapo zamani Soviet na kuendelea hadi Iraq na kisha kuihusisha Mashariki ya Kati kwa ujumla. Kila kitu kilichotajwa kwenye kile kitabu yapasa kithibitishwe zaidi hadi kifikie ukamilifu wenye usahihi kwa asilimia 100%.

 

Tutaendelea kufafanua na kulinganisha na hali ilivyo huko Kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati. Ni kama tulivyojionea mtiririko wa nyakati na matukio yake ilikuwa ni kulisukumia taifa la Misri kwenye vita vya mwisho na nyakati za mstari wa mwisho mwishoni mwa miaka 2520 tangua mashambulizi ya Cambyses huko Misri mwaka 525 KK, yaani mwaka 1996/7. Mlolongo huu wa matukio umeainishwa kwenye jarida la Anguko la Misri: Unabii Kuhusu Mikono Iliyovunjika ya Farao (Na. 036).

 

Kipindi cha mikono miwili mmoja kati yao ulivunjika mara mbili kinajitokeza kwenye tarehe muhimu ya vita ya Carchemish mwaka 605 KK. Miaka 2520 tangu mwaka 605 KK inaishia mwaka 1916. Tarehe hii ilishuhudia mgogoro mkubwa wa mwanzo wa Vita Kuu ya I na mapigano au upiganaji wake kama ilivyohusiana na kuendelea shemu zote mbili, yaani Ulaya na Mashariki ya Kati. Mfumo wa kifedha ulimwenguni pia uliwekwa kwenye umili wa binasfi tangu Decemba 1913 na tangu mwaka 1914 hadi 1916 dunia yote iliwekwa tayari kukabiliana na “Vita vya Nyakati za Mwisho” na vita hivyo viliandaliwa viendelee kwa kupitia awamu tatu zilizohusishwa na Vita Kuu ya I, ya II nay a III ya Dunia. mlolongo huu umeapangiliwa na waabudu Mashetani wakitumia jumuiya za siri zilizo chini ya uongozi wa Albert Pike. Mambo hayo yameelezewa kwa kina kwenye jarida la Mwaka 2012 na Mpingakristo (Na. 299D). Lengo hasa la mpango huu haukuwa ni kuanzisha tu tasisi au bodi ya utawala ya ulimwengu ambayo itakuwa chini ya Shetani akiwa ndiye kama mungu wake, ambavyo ni sawa kama Waabudu mashetani walivyokuwa wakiambiwa, bali ni kwa lengo la kumwangamiaza mwanadamu pia, ambalo ndilo lengo na kusudi hasa alilonalo ibilisi na mshitaki wa ndugu zetu.

 

Mwaka wa 1996/7 ulishuhudia mwisho wa kipindi kinachojulikana kama Kipindi cha Utimilifu wa Mataifa kilichonenwa kwenye Unabii wa Biblia na mwanzo wa kipindi cha miaka thelathini ya mwisho, au cha “Maombolezo ya Musa” yanayoonyesha kwa mfano wa siku thelathini za mwisho kabla ya Israeli hawajaingia kwnye Nchi ya Ahadi. Katika mwaka ule, makubaliano yalifikiwa ya kusalimisha mamlaka ya mataifa yote kwenye mfumo mmoja shirikishi chini ya uthibiti wa serikali moja duniani. Nchi za Jumuiya ya Madola zilizo chini ya Uingereza na Marekani zimekuwa zikiunga mkono wazo hili na kuwezesha uwezekano wa mfumo huu tangu kufanyika kwa makubaliano haya mwaka 1997 na wanapingana na katiba zao wenyewe pamoja na Sheria zinazosimamisha na kupinga uwepo wa kikatiba na ufalme. Ni uhaini na ni kuusaidia na kusaidi au kuungamkono uhaini.

 

Matukio mengi yaliyohusishwa ni yapo kwenye vifungo fumbo vya miaka thelathini kutokana na yale yaliyo kwenye tarehe muhimu sana. Tangu mwaka 1916, mwishoni mwa kipindi cha nyakati saba tangu mapigano ya Carchemish mwaka 605 KK, tumeshuhudia sehemu ya mwisho ya jaribio katika kukomeshwa kwa utawala wa Yuda na kwamba ile miaka thelathini iliishia mwaka 1946 na ilikuatiwa na kuanzishwa kwa taifa la Israeli. Kwa kipindi hikihiki chote tulijionea pia harakati za Wamisri. Harakati za kudai uhuru zilianza tangu mwaka 1951 na Hosni Mubarak aliinga kwenye huduma za kutumikia umma siku hizi akiwa chini ya Muhammad Naguib, rais wa kwanza wa Jamhuri na cha Gamal Abdel Nasser (rais wa pili mwaka 1956).  Mwaka 1952 vuguvugu la Udugu wa Kiislamu lilikandamizwa na kuzimwa huko Misri. Huu ulikuwa ni mwanzo uliofuatia watawala wote wa Afrika ya Kaskazini yote na Mashariki ya Kati wawe chini ya kasumba au vibaraka na uangalizi wa madola ya Magharibi pamoja na washirika wao. Kitendo hiki kimemudu kufanikiwa kwenye mataifa mengi kwa muda mrefu hadi kufanyika kwa mapinduzi ya Iran ya mwaka 1979. Maandamano yalianza mnamo Januari 1978. Mnamo Februari 1979 Shah aliondoka madarakani na kuikimbia nchi yake na ndipo Jamhuri ya Kiislamu ilianza rasmi chini ya Ayatollah Khomeini mwisho mwa mwaka. Hii ilikuwa ni miaka thelathini na tatu au vipindi viwili cha vya thelathini tangu mwaka 1916 jumlisha mitatu mingine. Mwaka 1976 ulikuwa ni mwaka wa Sabato na mwaka 1977 ulikuwa ni mwaka wa Yubile ya 119 (tangu siku ya Upatanisho ya mwaka 1976 hadi Siku ya Upatanisho ya mwaka 1977). Mwaka 1978 ulikuwa ni mwaka wa kwanza wa Yubile ya 120 ambayo ndiyo yubile ya mwisho ya utawala wa Shetani hapa duniani. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliruhusiwa ili kuanzisha nguvu kubwa ya Uislamu wa Kihafidhina utakaokuwa ndio msingi au chimbuko la vita vya mwisho na chanzo cha maangamizi na utumwa wa Mashariki ya Kati. Shah wa Iran (Uajemi) alisababisha hali ya watu kufikia kuhamasika kupenda kufanya mapinduzi, kwa kuwa alianzisha sheria iliyotoa amri kwamba mtu yeyote anayeshiriki kwenye harakati zozote za kumpinga apigwe risasi. Hii iliwalazimisha wapinzani wake kupatwa na hasira na kujaribi kutafuta ufumbuzi wake na hatimaye kufanyika kwa majaribio kadhaa ya mapinduzi kwa kila siku arobaini baada ya kipindi cha kuwaombolezea wale waliouawa kwa kupigwa risasi kwenye mkandamizo uliopita. 

 

Kuundwa tena kwa mfumo wa ulimwengu kulipangiliwa na washirika wa kile kinachojulikana kama Klabu ya Roma (the Club of Rome) mwaka 1956. Hiki kilikuwa ni kipindi cha miaka arobaini tangu mwisho wa nyakati saba au miaka 2520 tangu Vita ya Carchemish na kuanzishwa kwa utawala wa Babeli unaowakilishwa na “Kichwa cha Dhahabu” chini ya mfalme Nebukadnezar.

 

Mnamo mwaka 1956 ilikubalika kwamba Agizo Jipya la Ulimwengu lianze rasmi chini ya kanda saba za kibiashara. Kanada hizi za kiutawala zilitakiwa zijiunde na kufanya tawala kumi zenye nguvu zitakazoongozwa na viongozi kumi wasio wa kuchaguliwa na watakaounda mfumo mpya wa kiuchumi duniani. Kanda hizi kumi zingefanyika kuwa ni zile Pembe Kumi za Agizo Jipya la Muundo wa Dunia ambao ndio ungekuwa ni Dola ya mwisho ya “Vidole Kumi vya Chuma na Udongo.” Hii ndiyo itakayopelekea kuundwa kwa Dola ya Mnyama na Shetani ataipa uwezo wake dola hii. Itawageuka na kuiangamiza kabisa imani na Dini ya Waamini Utatu na pia atazikomesha dini na imani za Uislamu na Uzayuni wa Kiyahudi. Dola hii ya mwisho ya muundo wa Kibabeli ndiyo itakayongamizwa na Kristo atakapokuja.

 

Utawala wa milenia wa Kristo na watakatifu wake utaanzisha na utaongozwa kutoka Yerusalemu. Kabla ya kuja kwake Masihi (soma jarida la Ujio wa Masihi: Sehemu ya 1 (Na. 210A) kuna idadi kadhaa ya matukio ambayo ni lazima yatokee kwanza (soma majarida ya Mihuri Saba (Na. 140), Baragumu Saba (Na. 141), Maonyo ya Siku za Mwisho (Na. 044)). Mungu hafanyi kitu chache chochote bila ya kuwafunulia kwanza watumishi wake manabii. Kwa sababu hiyo ndipo ulimwengu unaonywa kwanza pia kwa njia mbili zote, yaani kupitia Kanisa lake Mungu na kwa Mashahidi wake. Umuhimu wa jambo hili umeonysshwa pia kwenye jarida la Mashahidi (Wakiwemo Wale Mashahidi Wawili (Na. 135).

 

Mungu amekuwa pia analiandaa Kanisa la Mungu ili liweze kumrejesha nandi kila mmoja anayetubu katika siku za mwisho na kumrudia Mungu na kubatizwa. Mchakato huu umeainishwa kwa kina kwenye jarida la Watano Kutoka Mbinguni (Na. 28).

 

Biblia iko wazi sana kwamba Dini ya Kahaba wa Babeli na Dini za Kisirisiri lazima vitaangamizwa na Mnyama mwenyewe. Mlolongo huu wa kimatukio umeainishwa kwa kina kwenye majarida ya Vita ya III ya Dunia Sehemu ya I: Dola ya Mnyama (Na. 299A) na lile la Vita ya III ya Dunia Sehemu ya II: Mwanamke Kahaba na Mnyama (Na. 299B). 

 

Iko wazi sana pia kwenye Danieli 11:40-45 kwamba Vita vya mwisho ni lazima vijumuishe mataifa ya mashariki na kaskazini kwa Yerusalemu na Mfalme wa Kaskazini atakwenda kuwaangamiza watu wengi kwa maangamizi makubwa sana. Kwenye maafa hayo ya moto mkubwa yatakayowaua theluthi moja ya wanadamu wataangamia na robo moja watakufa kwa tauni baada yake hadi Masihi na Vitasa vya Ghadhabu ya Mungu.

 

Baada ya mgogoro huo Mfalme wa Kaskazini, ambaye ndiye mwenye nguvu kubwa sana za kijeshi kuiliko dola nyingineyoyote duniani katika Siki hizi za Mwisho, atarudi kwenye makao yake makuu ambayo yataichukua sehemu yote kutoka Ukanda wa pwani ya Gaza hadi Yerusalemu ambako viongozi wake watamiliki na kuishi. Itamiliki na kuikalia Yerusalemu kwa kipindi cha siku 1263.5 au miezi 42. Wakati huo, mji huu utahubiriwa na Mwashahidi wawili ambao ni manabii wake Mungu.

 

Mwishoni kwa kipindi hiki cha siku 1260 Mashahidi wawili watashindwa na majeshi ya Mnyama. Ulimwengu utakurahia kushindwa huku na hawatawazika. Mwishoni mwa siu tatu na nusu watafufuliwa kwa sauti au tarumbeta ya Malaika Mkuu na ndipo Ujio wa Masihi utachukua mkondo wake. Huyu Masihi, Kristo, anayeitwa Issa kwenye Korani, atarudi ili kuufanya ulimwengu utawaliwe kwa sheria au torati ya Mungu. 

 

Hata hivyo, mataifa yaliyoko Mashariki ya Kati yatatiishwa na kunyenyekeshwa vizuri na Mfalme wa Kaskazini hata kabla ya haijatokea hivyo. Kwa hiyo, nchi za Kiarabu zitajiunda upya na chokochoko za kumsukuma Mfalme wa Kaskazini kama ilivyotabiriwa kwenye unabii wa Danieli, chini ya msukumo au uchocheo wa Misri na mataifa meingine ya Mashariki ya Kati. Misri inalengwa sana na unabii. Mchocheo au chokochoko zimekuwa zikiendelea kwa miaka mingi sana.

 

Vita hii ya mwisho ambayo imeanza rasmi mwaka 2001, itakuwa imeharakishwa na mataifa ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wakijaribu kumshinda na kumuangamiza Mfalme wa ukanda wa Kaskazini atakayetawala kutoka Ulaya. Imani au dini ya Kibabeli vimefananishwa na miji saba ya vilima, ambayo ni Babeli ya kisasa, iliyotokana na muundo wa iliyokuwa ikijulikana kama Dola Takatifu wa Kirumi na iliyoonyeshwa kwenye sura ya 2. Ni muungano wa kisiasa na wa kiuchmi ulioundwa kimfano kwenye Mapatano au Makubaliano ya Mkataba wa Roma wa mwaka 1956 pamoja na Vichwa vyake Kumi au kanda zake za kiuchumi.

 

Kwenye mwisho ule tunaweza sasa kuona hali ya kutorithirika na maandamano vikitokea kutoka Morocco hadi Yemen na yakiungwa mkono na Iran na wahafidhina wa Kiismalu kila mahali. Imefanywa itokee hivyo kutokana na ufisadi na uksefu wa uadilifu na kwa uvunjaji wa sheria za Biblia na Koran (Qur’an). Inaashiria kila kitu kuwa hakuna uadilifu na kupotoka, mambo yanayoukumba Umoja wa Mataifa na mfumo wa kisiasa wa Ulaya. Ni hivi karibuni tu ulimwengu mzima utakwenda kutekwa na kutumikishwa na na Dola hii ya Mnyama.

 

Nyakati hizi za mwisho pia watakatifu wake yeye Aliye Juu Sana watashindwa kutokana na ujinga, mafundisho potofu ya kizushi, rushwa na ufisadi, pamoja na uchoyo. Nguvu zao zinapungua na kuporomoka kwa namna nyingi sana mbalimbali.

 

Ifuatayo ni taasisi ambayo kwa sasa inasimama na mataifa ya Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati yakijipanga tayari kwa harakati hizi za mpambano wa mwisho kabla hawajaenda utumwani na kabla Masihi hajarudi kuwashughulikia.

 

Morocco

Chini ya Mfalme Mohammed VI Morocco, kama ilivyo Yordani, ni nchi ya kifalme iliyo na uwezo na utaratibu mzuri wa kuwasaidia watu wake, lakini mfumo wao wa kifalme umekuwa ukiwatumikia watu wake kwa ubadhirifu mkubwa sana wa kifisadi, wanaofanya wale walio karibu na mfalme na pia vina kikomo cha kuutumia uhuru wa kujieleza au wa kusema.

 

Tunisia na Algeria

Maandamano makubwa kusifika na kufanikiwa ya mitaani yaliikumba pia Algeria nchi iliyo na umuhimu mkubwa sana kwa Misri, na ni kama takriban siku kadhaa tu baada ya maandamano kulishuhudiwa Rais wa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali akiikimbia nchi.

 

Uimara na umahiri mkubwa wa utawala usiojali watu na wa kiimla ulisababisha ongezeko la hali ya kutorithika miongoni mwa wananchi wao wengi. Hii iliongezeka zaidi kwa ongezeko la mlipuko wa bei za vyakula. Hali hii ilisababishwa pia na nchi za Magharibi na mtindo wake wa kimaisha ya hali ya juu na ongezeko la fursa ya kizazi cha vijana. Ulimwengu wote wa Kiislamu una vijana wengi sana kuliko nchi za Magharibi na ungali unaendelea kuzalisha vijana wengi zaidi wakati ulimwengu wa Kimagharibi unapunguza idadi ya watu wake ili wasiongezeke sana.

 

Kile kisichoeleweka mara nyingi ni kwamba amri ya hali ya hatari imekuwa ikitumika nchini Algeria tangu mwaka 1992. Maandamano ya hadhara nay a watu wengi kwenye miji mkuu yamepigwa maufuku. Maandamano ya kawaida tu yamejitokeza kila mahali katika nchi hiyo. Hata hivyo, waandamanaji wakaibuka hapohapo na mara moja nchini kote Algeria kwa mara ya kwanza, pamoja na kwenye mji wao mkuu wa Algiers. Maandamano hayakuendelea kwa namna moja hiyohiyo kama ilivyotokea huko Tunisia. Huenda ni kwamba inatokana na mwitikio mdogo uliotokana na mkandamizo wa kijeshi, pia amoja na uingiliaji kati wa serikali wa kuthibiti mlipuko wa ongezeko la bei ya vyakula na bidhaa ninginezo kulisaidia kuyatuliza mambo.

 

Serikali ya Algeria ina utajiri unaoaminika unaotokana na uzalishaji na usafirishaji wa biashara yake ya gesi na mafuta. Hii inaiwezesha hata kuyakopesha mataifa mengine yenye uhitaji. Inajaribu kuondoa mangu’uniko kwa watu wake na kuwanyika wanaotaka kuanzisha manung’uniko kukosa sababu kwa kutumia kiasi kikubwa cha raslimali zake kwa kuanzisha na kuendeleza miradi yenye manufaa kwa umma. Hatahivyo, matatizo makubwa yamebaki kwa ajili ya ukosefu wa ajira, ufisadi, ubadhirifu na kutokuwa na mageuzi ya kisiasa.

 

Vita vya Algeria vilivyolipuka katika historia ya hivi karibuni, vinaifanya isiendelee mbele kinyume na ilivyotokea kwa jirani zao Tunisia. Siasa za Algeria za miaka ya 1990s zilitawaliwa na harakati zilizohusisha wanajeshi na wanamgambo wa Kiislamu. Mwaka 1992 uchaguzi mkuu uliokipa ushindi chama cha Kiislamu ulifutiwa matokeo yake. Kitendo hiki kilianzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopelekea umwagaji mkubwa wa damu ambapo zaidi ya watu 150,000 waliuawa. Hivyo, idadi kubwa ya Waislamu waliweza kuwekwa kwenye uangalizi wa wanajeshi walioingilia kati hali iliyojitokeza. Ukandamizaji huu unafikia viwango vikubwa vya watu kujisikia kutoridhika. Mafundisho ya uwongo na ya kizushi ya kidini ya wahafidhina wa Kiislamu hayaisaidii hali hii na wala haiusaidii mfumo wa kidini wa Kimagharibi na hasahasa Marekani kwa imani yake potofu nay a kizushi ya Mungu wa Utatu. Amani haiwezekani katikati ya imani mbili na hasa kama zote zitakuwa ni zenye mafundisho ya kizushi ya zisizotaka kupatana.

 

Libya

Kanali Gaddaffi ni kiongozi muimla na mwenye maauzi yap eke yake ya kiutawala ya kila taifa changa ambalo wastani wa umri wa kuishi kwao ni chini ya miaka 25. Wastani wa taifa wa umri wa kuishi unahusiana na karibia miaka 29.7 nchini Tunisia hadi miaka 17.89 huko Yemen. Hawa ni vijana na mataifa yenye vurugu na machafuko. Libya peke yake ina idadi ya watu milioni 6.5 ikitofautiana na Misri yenye takriban watu mlioni 84.5. hata hivyo, ni Misri tu ndiyo yenye wastani wa chini wa umri wa kuishi wa watu wake ambao ni miaka 24 ambao ni wa chini hata kulinganisha na Libya (tazama hapo chini). Uwezo au kiwango chao cha kukusanya majeshi ni jambo la kutilia maanani.

 

Libya inakataza kabisa kufanyika maandamano au hata aina yoyote ya maandamano. Hata hivyo, taarifa zimejitokeza za kuanza kwa vurugu kwenye jimbo la al-Bayda. Kuzuiliwa majumbani kumeisababisha serikali kutangaza ongezeko la matumizi kwenye majengo ya umma.

 

Kumbuka kwamba unabii wa Danieli 11 unasema kuwa nyakati za meisho Libya itakuwa kwenye hatua ya nguvu za majeshi yaliyojipanga yanayoitumikisha Misri (tazama hapo chini). Ndivyo hata kwa Ethiopia. Hii inaweza kuchukuliwa kuwa na maana kwamba mfumo wa mamlaka ya kidunia wa Kaskazini utaenea hadi Libya na Ethiopia na kuitumikisha Misri. Nahumu 3:9 inawaonesha wakiisaidia Misri na tafsiri ya Soncino inasema “hauatzake zote” ikimaanisha ama kuunganisha jeshi lake au kuliweka tayari kwa lolote litakalotokea.

 

Wakati wa kutolewa kwa unabii, “Libya” ilimaanisha nchi ya magharibi mwa Misri kwenye pwani ya bahari ya Atlantic ambako ndipo iliko sasa nchi ya Morocco.  Ndicyo pia, Ethiopia kama eneo kubwa lililotanuka linalojumuisha ardhi au nchi za kusini mwa Misri. Mito ya Ethiopia ilikuwa ni mto Mweupe wa Nile. Putu ilikuwa ni eneo la pande zote mbili za Bahari ya Shamu katika Yemen na katika Somalia na Eritrea.  Hivyo basi tunaweza kutarajia majeshi ya Kiislamu yakiibuka kutoka nchi za kusini mwa Misri na kuenea hadi Yemen.  Kwa sababu ya uhusika wao, watakujakuwa chini ya utawala wa Mnyama kwenye vita. Vikundi hivi vya kimakabila vimeelezewa pia kwenye jarida la Wana wa Hamu: Sehemu ya IV: Putu (Na. 45D).

 

Nafasi ya Misri kwenye vita hivi

Kama unabii unavyotuambia Misri itakuwa imetwaliwa na kuchukuliwa utumwani na viongozi wa Kaskazini na mkakati wa kiutawala wa Agizo Jipya Ulimwenguni na Umoja wa Mataifa. Mfumo wote kabisa wa kifedha na wa kiuchumi wa Misri utakuwa chini ya udhibiti wa mfumo huu wa Agizo Jipya la Dunia kama tunavyoona ilivyoandikwa kwenye Danieli 11:42-43.

 

Jaribio lolote la kujifanya kuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki ilikandamizwa. Hii ilitimilikaje? Matukio haya yanafunuliwa kama ifuatavyo.

 

Tarehe 25 Januari 2011 waandamanaji waliitisha maandamano ya kimapinduzi yaliyowavuta maelfu ya waandamanaji hadi katikati ya jiji la Cairo na miji mingine muhimu nchini kote Misri, tangua Alexandria hadi kwenye Mfereji wa Suez na pande za mbali za kusini. Tarehe 9 Februari 2011 vurugu za kusini kwenye mji wa chemichemi kulishuhudiwa vurugu zikiendelea ambako risasi za kweli zilitumika. Wafanya vurugu walijibu kwa kufanya mashambulizi ya kujilipiza na ya kujibizana na wakayachoma majengo saba makubwa nay a muhimu vikiwemo vituo viwili vya polisi. Jeshi likaifunga barabara ya kutoka Kairo kwenda pande za kusini. Waandamanaji huko Cairo wakaongezeka kupindukia tena na wakawa mara dufu. Idadi kama hiyo haijawahi kuonekana huko nyuma bado tangu vurugu ya kugomea ongozeko la bei ya mkate iliyofanyika miaka ya 1970 na hata haya yalizidi. Mbinu za kipolisi za kuyazima maandamano hayo kwa kutumia kuwamwagia majl ya kuwasha na kuwatisha kwa risasi za mipira zilishindwa na ikabidi wanajeshi waitwe kusaidia. Kitendo kilichofuatia baadae cha kuwapiga risasi za kweli kiliendelea kutopata ufumbuzi na kuliendeleza hali ileile ngumu kwa serikali kama ilivyotokea huko Iran kwenye harakati za kupinduliwa kwa Shah. Hata hivyo, Jeshi lilikataa wito wa kuchukua hatua kali ya kikatili ya kukomesha na kukandamiza maandamano haya na vurugu hizi huko Cairo. Matokeo yake yalikuwa ni kwamba kuanza kutumia mbinu walizozitumia mara nyingi za kuyashirikisha makundi ya wahuni na waovu waliofungwa jela na kuwaachilia kutoka magerezani wakijua kuwa wangewashambulia wafanya vurugu hawa. Walijaribu kufanya hivyo lakini matokeo yake walizidisha hasira za waandamanaji zaidi na zaidi.

 

Mamia ya watu walikufa kwenye majuma mawili ya mwanzoni ya vurugu. Maelfu walijeruhiwa. Vurugu zilipangwa kuendelea hadi Mubarak akaachia madaraka na uchaguzi huru ukaandaliwa kwa haraka. Katiba mpya lilikuwa jambo la msingi kudaiwa na wanaharakati hawa. Hiyo hata hivyo ilipangwa iandaliwe ili kuuwezesha mkakati wa Agizo Jipya Ulimwenguni lichukue utawala, ni kama inavyofanywa kwa njia za wizi na uhaini katika nchi nyingine za dunia zikiwemo Uingereza, Australia na Marekani na Canada pamoja na nchi z Ulaya kwa ujumla.

 

Maneno ya shutuma na miito ikasikika kutoka Marekani ya kutakiwa kuandikwa upya sera zake za mambo ya nje jinsi zinavyokwenda siku hadi siku. Hilary Clinton alimsaidia Mubarak na kisha hata Seneta Kerry akiwa kama mwenyekiti wa Kamati ya Mabo ya Uhusiano na Nchi za Nje alisema kuwa aendelee kutawala na kisha akaambiwa na Balozi wa zamani kwa niaba ya Rais Obama kwamba yampasa aende haraka Misri. Seneta McCain pia alisema kuwa wanataka ufanyike uchaguzi huru lakini la muhimu ni kwamba wasiwachague hawa wa Udugu wa Kiislamu. 

 

Nchi za Magharibi zikatoa matamko hayohayo dhidi ya Mubarak, wakisema kwamba kama yeye hataikomesha vurugu wangejionea wanaharakati wa Udugu wa Kiislamu wachukua madaraka najeshi la Waislamu lingeibuka. Hii kwa kweli umekuwa ni mkakati wa jumuiya za siri tangu kwaka 1871 ulioanzishwa na mpango wa Pike kama tulivyoonyesha kwenye jarida la Mwaka 2012 na Mpingakristo (Na. 299D).

 

Misri ilikuwa na machafuko kwa kipindi cha zaidi ya majuma mawili. Biashara au shughuli ya kutembelewa na watalii na utalii wenyewe ulipata mkwamo mkubwa.

 

Tarehe 10 Februari 2011 kile kilichoonekana kuwa hakuna namna nyingine zaidi ya utoaji wa makusudi wa waandamanaji ulifanywa na Mubarak, na utawala wake wa kikatili, kwa kutoa mfululizo wa matangazo yaliyoashiria kwamba Mubarak angefanya tangazo fulani siku hiyo la kuhitimisha na kuleta ufumbuzi wa jambo hili. Hii ilitanguliwa na tangazo lililotolewa na Baraza Kuu la Kijeshi lililotangaza kuwa lilikuwa upande wa wananhi wa Misri na kwamba inampasa Rais atangaze siku hiyo. Watu walitarajia kumsikia akitangaza kujiuzulu na kumpa madaraka yake Makamu wake wa Rais. Alijitokeza kwenye runinga na akafanya kitu cha tofauti kabisa na matarajio yao. Alitangaza nia yake ya kubakia bado madarakani hadi kwenye uchaguzi uliotarajiwa kufanywa mwezi Septemba, lakini yeye mwenyewe hakuweza kushindana nao. Matokeo yake yalikuwa ni kuwakasirisha waandamanaji. Zaidi ya waandamanaji milioni moja wakaingia mitaani wakimtaka ajiuzulu. Ndipo jopo la wanamapinduzi la wanajeshi likachukua madaraka na Mubarak akaachia madaraka rasmi tarehe 11 Februari 2011. Matengenezo mapya yakaanza.

 

Mgogoro na vurumai hizi vinaonekana ni mchakato uliopangiliwa kwa muda mrefu ili kwamba harakati za Kiislamu ziendelee kuenea ili kuhalalisha mkakati wowote wa vita utakaofanywa na Majeshi ya Kaskazini. Kile kinachofanywa na jopo la kijeshi la mapinduzi litaamua kukomesha ueneaji huu. Majeshi ya kiislamu yalisherehekea sehemu zote za Mashariki ya Kati.

 

Mungu amesema kinachokwenda kutokea kwenye Dola ya mwisho ya Mfalme wa Kaskazini na mfumo wa Kishetani ambao ataupa nguvu na uweza. Anguko la Misri lilipangiliwa tangu mwaka 1997 ambao ulikuwa ni wa anguko kuu la kiuchumi na la utawala ulimwenguni ulilolengwa kuingia rasmi kwenye Agizo Moja la Ulimwengu kwa kutumia ushirika wa kidini na uthibiti kamili utakaoyataka mataifa kuachia haiba au heshima ya mataifa yao kabisa. Mubarak alianza kutawala mwaka 1981 kwa kuwekwa na Wamarekani wakimuunga mkono, kitendo ambacho ni sehemu tu ya mpango huu. Unabii kuhusu Misri na mwisho wake baada ya miaka 2520 au nyakati saba tangu kushambuliwa kwa Cambyses mwaka 525 KK kulishuhudia Misri ilipangiwa na ilijiimarisha na kuingia kwenye moja ya kanda hizi kumi za mpango wa Agizo Moja Ulimwenguni na wakati ulipofika wakati wa kupangilia upya mabadiliko ya mwisho, walaghai wasimamao nyuma ya matukio wakaanzisha vurugu au machafuko kwa mazingira ya kuipotosha na kuiharibu sana jamii hali iliyowawezesha kutokea.

 

Kama ilivyofanyika kwenye nchi nyingine, wanaharakati wa Kiislamu walijikusanya ya hata kuzishinda serikali zilizokuwa madarakani kama walivyofanya huko Iran mwaka 1979 tangu mwanzo wa yubile ya 120 au walilazimika kuanzisha harakati za kijeshi zilizohakikisha kuwaona wakifanikiwaq kumwangusha au kumpindua mtu yeyote aliye madaarakani. Misimamo miovu ya kutotaka mapatano ya viongozi wan chi za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati vilisababisha ionekane hali hii ikiongezeka na kuendelea.

 

Matatizo yaliyojitokeza huko Afrika Kaskazini kama tunavyoona hapo juu yalienea pia huko Mashariki ya Kati.

 

Jordani  

Matatizo yanaendelea kuonekana huko Jordani kwa sababu ya ubadhirifu na ufisadi wa wale walio karibu na Mfalme Abdullah na kwenye uongozi wake wote. Maandamano makubwa yaliyofanyika nchini kote Jordani tarehe 1 Februari yalimlazimisha mfalme kuivunja serikali na kumchagua Bwana Maroof  Bakhit kuwa ni Waziri Mkuu mpya akiangizwa kufanya mabadiliko au mageuzi makubwa ya kisiasa. Hasira zao zilielekezwa kwenye umaskini na ukosefu wa ajira na pia kwa mtindo uliokuwepo wa kuwachagua Mawaziri Wakuu moja kwa moja na sio kwa uchaguzi wa wananchi. Nchi ya Jordani ina vuguvugu kubwa la upinzani wa Kiislamu – wanaoitwa Uisamu wa Mstari wa Mbele Kimatendo, maarufu kama Islamist Action Front (IAF) – ambalo limeanza hivyo lakini linadai kuwa halikusudii kumwondoa madarakani Mfalme Abdullah, aliye na wafuasi wengi na kuungwa mkono kukubwa na ni mtu asiyelaumiwa au kukosolewa kwa moja kwa moja kwenye vurugu hizi. Hata hivyo, inamesemekana kwamba haikubaliani na wazo la kumchagua Bwana Bakhit.

 

Maandiko ya Biblia yanasema kwamba nchi hizi zitaukwepa mkono wake: Edomu na Moabu na wana wa Amoni. Wau hawa na mikono yao ni hawa Wayordani wa siku hizi na pia ni sehemu ya Waisraeli walioko Palestina, wakiwa wote ni Wayahudi na Wapalestina. Waedomu walishindwa na kujumuishwa na Wayahudi na John Hyrcanus na Wamakabayo mnamo mwaka 160 KK.  Tutalijadili jambo hili hapo chini.

 

Syria

Syria inajishuhudia yenyewe kuwa haijatulia, ila ina miguu iliyochanganyika na udongo. Rais wa Syria Basher al-Assad aliyarithi madaraka yake kutoka kwa baba yake mwaka 2000. Baba yake, Hafez al-Assad, aliitawala Syria kwa kipindi cha miongo mitatu. Mwezi Januari aliliambia jarida la Wall Street Journal kwamba nchi yake ya Syria iko imara na salama kuliko nchi za Tunisia na Misri na kwamba hakuna fusra wala ndoto ya kufanyika mapinduzi ya kisiasa. Hii yaonekana kuwa ni mawazo ya kimapenzi tu. Wanaharakati wa Kisyria waliitisha siku malengo ila hawakuamsha wala kuhamasisha mapinduzi yaliyotarajiwa na Syria ni msaidizi mkubwa wa Iran na wa kuenea kwa harakati za Kiislamu. Mwaandamanaji wa huko waliutumia mtandao wa kijamii wa Facebook kueneza harakati zao za maandamano lakini ofisi iliyokuwa inashughulia kuendesha mtandao huu ulifungwa rasmi kwa nia nzuri yoyote iliyokubalika. Wanaharakati wanaandamana dhidi ya kile wanachokiona kuwa kama, mwendelezo wa utawala wa kifalme na mfumo wake wa kifisadi na utawala wa vitisho na ukatili. 

 

Nchi zote mbili, yaani Syria na Misri zimewahi kutawaliwa kwa sheria za hali ya dharura na zote mbili zipo kwenye mateso ya umaskini mkubwa na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira. Ingawaje uchumi umefunguliwa tangu alipoingia madarakani, bali uhuru wa kisiasa na wa kibinafsi umezuiwa na kupingwa marufuku kabisa. Hamasa na hisia ya kufanya mapinduzi bado ingalipo kwenye anga ya Kiarabu. Vikundi Vikuu vya upinzani vimefungiwa na kuna maelfu ya wafungwa wa kisiasa magerezani. Chama cha Baath kimetawala kwa karibu nusu karne, tangu mapinduzi ya mwaka 1963 nchini Syria na kuna ufisadi na ubadhirifu wa kukatisha tama, vilivyopelekea machafuko. Chama hiki kiliundwa mwaka 1947 na kimetawala katika nchi zote mbili, yaani Syria na Iraq hadi kilipogawanyika na kuwa maadui wawili kiitikadi.  Ni chama chenye muundo na itikadi za Ujamaa wa Kiarabu. Hata hivyo, jinsi kinavyofanya kwenye mkakati wa Agizo Jipya Ulimwenguni ni jambo la kusubiria tuone.

 

Yemen

Yemen ni nchi ya Kiarabu iliyo kwenye kundi la mataifa maskini sana duniani. Karibu nusu ya watu wake wanaishi kwa matumizi ya takriban $2 kwa siku.

 

Machafuko yaliyofanyika Tunisia yalipelekea kutokea kwa machafuko katika nchi za Misri, Jordani na huko Yemen. Tarehe 27 Januari 2011 makumi kwa maelfu ya Wayemen walifanya maandamano kwenye mji mkuu wan chi hii wa Sanaa walimtaka rais wao ajiuzulu. Rais alijaribu kupunguza jazba ya waandamanaji kwa kuamuru kupunguzwa kwa bei ya bidhaa kwa 50% kwene kodi yake ya mapato na bei ya bidhaa. Ingawa aliwatia mbaroni baadi ya waandamanaji, aliwaachilia wafungwa 36 kutoka gerezani akiwemo mwana harakati wa haki za binadamu Tawakul Karman. Ili kutoa hakikisho la uadilifu, kwa wakati huohuo alipandisha mishara ya wafanyakazi wa serikalini kumuondoa madarakani muadhimu mkuu wa jeshi.

 

Baada ya siku kadhaa ya maandamano, Rais Ali Abdullah Saleh alilitagazia bunge la nchi hiyo tarehe 2 Februari 2011 (baada ya miongo mitatu ya kuwa madarakani kama walivyo wengine wengi) kwamba hatataka kuongeza mhula mwingine wa kutawala na wala hata mtoto wake hatamani madaraka na kwwamba wala hatamrithisha utawala atakapoachia madaraka. Tangazo lake lilisababisha kulipua maandamano mengine makubwa ya kupinga nchini kote siku iliyofuatia. Wanaharakati wa upinzani walikataa nasaha zake na wakasema kuwa wataendelea mbele kwenye kile walichokiita kuwa ni siku ya mshikamano na ya shabaha. 

 

Mfululizo wa matukio

Danieli anatueleza kuwa: na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati. 41 Tena ataingia katika hiyo nchi ya uzuri, na nchi nyingi zitapinduliwa; lakini nchi hizi zitaokolewa na mkono wake, Edomu, na Moabu, na wakuu wa watu wa Amoni. 42 Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka. 43 Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibia na Wakushi watafuata nyayo zake. (Danieli 11:40-43). 

 

Kama ilivyoonekana hapo juu, Nahumu 3:9 inaonyesha Walibya wakiisaidia Misri na tafsiri ya Soncino inasema kwamba neno la Kiebrania kwa usemi huu wa “kwa hatua zake” inamaanisha ama kuunganisha jeshi lake kwa kupokea amri ya hali ya hatari na kuwa tayari wakati wote na kwa lolote.

 

Kwahiyo kutakuwa na muungano wa jumla kati ya Misri yote na ulimwengu wa Kiarabu na Wapalestina. Muungano huu wa Waarabu utaendelea hadi kumsukumia mbali Mfalme wa Kaskazini. Neno hili la “Kumsukumia Mbali” kwa usemi wa moja kwa moja ni “kubadilishana misukumo” ikimaanisha “shambulizi” au “kwenda vitani pamoja na.” Hii itahusisha mashambulizi yatakayoilenga imani na mfumo wa Kaskazini. Kitabu cha Ufunuo kinatuambia kwamba hii itahusisha kuangamizwa kwa mji wenye mundo wa mwisho wa Kibabeli ulioko juu ya vilima saba. Mji huo ni wa Roma na mabadiliko yake yataiathiri miji mikuu ya Ulaya na wanamapinduzi wa Kiislamu watashuhudia uharibifu mkubwa ukiikumba miji hii na watu wake.

 

Mfalme wa Kaskazini au washirika wanachama wa Ushirika wa NATO watapeleka majeshi yao yote yaliyo kwenye mataifa yote shirika ya umoja wa NATO na mkono wa vita vya Nguvu ya Mnyama na kushambulia na kuitiisha au kuikalia Mashariki ya Kati.

 

Kwenye hali hii ya kuikalia, ndipo majeshi ya Kiislamu ya pande za Mashariki na Kaskazini yatakusanyika dhidi ya Mfalme wa Kaskazini au mataifa shirika ya umoja wa NATO. Danieli 11:44 anaendelea: Lakini habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha; naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuharibu, na kuwaondolea mbali watu wengi.

 

Tafsiri ya Soncino inajaribu kubadilisha maana ya maandiko haya ya kuonysha kama ni tendo lililokwisha ita ikitumia tafsiri ya Bevan. Hata hivyo, hii haiwwezi kuwa sahihi kwa kuwa andiko linaonyesha wazi kuwa ni Nyakati za Mwisho. Wamekabiliwa na kuelewa kwamba Danieli sura ya 12 inaelezea kuhusu hatima ijayo ya kienyeji na zaidi kwamba sura ya 11 haifungamanishi wala kuunganisha tofauti hiyo. Wanalofanya hata hivyo ni kujua kwamba, kama tafsiri ya Bevan ambayo inaonyesha jambo hili kama kuutazama mji wa Yerusalemu kutoka Misri ambavyo ni uwongo, na kwamba ilimaanisha Babeli na Parthia. Parthia ilienea hata hadi Palestina wakati wa kilele chake cha zama yake ya kidola na ilienea hadi Caucasus na mashariki hadi huko Indus na ikajumuisha Uajemi na kwa kweli ilianzia huko Uajemi. Eneo iliyojumuishwa ni ulimwengu wote wa Kiislamu kutoa Iraq na Iran hadi Yemen hadi Kazakhstan na Afghanistan na Pakistan na Afrika ya Kaskazini.

 

Wakati mashambulizi ya Mashariki ya Kati yakiendelea, majeshi ya Kaskazini na Mashariki yatajiunga pamoja dhidi ya majeshi ya NATO na mgogoro huu utabadilika na kujikuta unakuwa wa kinyuklia na utaendelea hadi kujikuta ukifikia kwenye awamu ya kulipuka kwa Vita Kuu ya III ya Dunia.

 

Ushirika wa NATO wa Nguvu za Mnyama utashinda mgogoro huu, kwa kusababisha na kufanya maangamizi na uharibifu mkubwa sana, na watarudi kuyakalia makao yake makuu katika Palestina. Inaonekana kwamba Hamas watashuhudia uharibufu na maangamizi haya makubwa ya watu wake na ukaliwaji na mamlaka ya Makao Makuu ya NATO.

 

Danieli 11:45 anasema: Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataifikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.

 

Eneo linalohusishwa hapa ni kutoka pwani ya Gaza hadi Mlima Sayuni. Tafsiri ya Soncino inashikilia kwamba huu ni ukusanyaji wa mahema yanayounda makao makuu tiifu. Nauni ya neno la appëden (kasri) ni la Kiajemi asili yake na linaonekana hapa peke yake. Hivyo, tunazamia ukaliaji wa mwisho wa Mpingakristo na Nguvu za Mnyama za Agizo Kuu Jipya Ulimwenguni ukifanika kwa haraka sana kabla ya ujio wa Masihi na kuangamizwa kwa mfumo ulioko ulimwenguni ulio chini ya nguvu hiyo. Mgogoro huu umeelezewa kwa kina kwenye jarida la Vita vya Hamon-Gog (Na. 294).

 

Kwa kuwa atakuwa amesababisha maangamizi makubwa, Wafalme wa Mashariki hawatamsaidia na atangojea hadi wao wenyewe watakapoburutwa au kuchukuliwa kwa guvu hadi Megiddo watakako kwenda kushughulikiwa kinume chake. Hawatampokea wala kuumkubali Masihi na utawala wake wa kutoka Yerusalemu way eye na wateule wake.

 

Vita hivi vya Nyakati za Mwisho ni vyetu sisi. Mfumo wa Agizo Kuu Jipya Ulimwenguni utaangamizwa na mfumo wa kifedha au kiuchumi nao utaharibika pia. Ili kuelewa kuangamizwa kwa mfumo wa kifedha na madhara yake, itakupasa uisome Ufunuo 18 sambamba na andiko hili.

 

Danieli sura ya 12:1 anaendelea kwa haraka kusema: Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.

Aya ya 2 ndipo anaendelea kuelezea awamu za Ufufuo wa Wafu.

 

Inawezekana kusiwe na uwezekano wa kuonea mashaka kwamba hata sisi tunaweza kuwa kwenye Nyakati hizi za Mwisho wakati wa mwisho wa utawala wa Shetani na mwanzoni mwa utawala wa milenia wa Kristo utakaotokea Yerusalemu. Vita hivi vimefunuliwa kama vilivyotabiriwa kwa kipindi cha karibu miaka elfu mbili mia sita iliyopita. 

 

Ili kujua mlolongo wa matukio ya Yubile ya mwisho ya 120, hebu na tuiainishe au tuilinganishe yubile kwa kuilinganisha na utaratibu wa Kuhesabu siku za kuelekea siku ya Pentekoste kwa kutumia majina ya majuma kutoka kwene Kalenda ya Wasamaria.

Kuyahesabu na kuyataja majuma ya Hesabu kuelekea Idi ya Majuma

Utaratibu wa kuyataja majuma kwenye Uhesabuji wa Kuelekea Idi ya Majuma kama kulivyoonyeshwa kwenye kalenda ya Wasamaria kunawezekana kukafanyika kwenye Yubilee ya mwisho ya 120 kama ifuatavyo.

1. Miaka ya 1978-1984 "Juma la Kuivuka Bahari ya Shamu" (Kutoka 14:26-15:21);

2. Miaka ya 1985-1991 "Juma la kuyabadili maji ya machungu ya mara" [uchungu] (Kutoka 15:22-26);

3. Miaka ya 1992-1998 "Juma la kuwa huko elimu, walikozikuta chemchem kumi na mbili na mitende sabini" (Kutoka 15:27-16:3);

4. Miaka ya 1999-2005 "Juma la kushuka mana, iliyoanguka chini katikati yao kutoka mbinguni walipokuwa jangwani (Kutoka 16:4-36);

5. Miaka ya 2006-2012 "Juma la kupata maji yaliyotoka kwenye mwamba" (Kutoka 17:1-7);

6. Miaka ya 2013-2019 "Juma la mapigano na “Amaleki” (Kutoka 17:8-17);

7. Miaka ya 2020-2026 "Juma la kuwa Mlimani Sinai" (Kutoka 1:1 ff.).

(sawa kama alivyosema Sylvia Powels, kwenye kitabu chake cha The Samaritans [Wasamaria], kilichorekebishwa na Alan Crown).  

Andiko lililoko hapo juu limechukuliwa kutoka kwenye jarida la Jinsi ya Kuhesabu Hadi Pentekoste (Na. 173).

Siku ya 50 inayofananishwa na miaka ni mwaka wa Yubile wa 2027 kama inavyoashiriwa na Pentekoste ambavyo Pentekoste inauwakilisha mwaka wa Yubile

  1. Miaka ya 1978-1984 “Juma la kuivuka Bahari ya Shamu”

Tangu mwaka wa Kwanza wa Yubile, na mfano wa kuivuka Bahari ya Shamu, tunaanza kuona utambulisho na kuitwa kwa watu wa Mungu watoke kwenye dunia ili kujiandaa kwa awamu hii ya mwisho ya Makanisa ya Mungu. Mfumo na imani ya Sabato iliyojitangaza yenyewe kuwa ni waamini Utatu imeibuka kwa wingi sana kipindi hiki cha mwaka wa kwanza. Ilikuwa ikinyemelewa na imani ya Mungu wa Utatu ya Roma kwa kipindi cha miongo kadhaa tangu mwaka 1931 hadi 1978. Ndivyo ilivyokuwa pia kwa huduma nyingine za Makanisa ya Mungu yamekuwa yakinyemelewa na imani hizi za kizushi. 

 

  1. Miaka ya 1985-1991 "Juma la kuyabadili maji Machungu au Marah kuwa matamu"

Kusafishwa kwa Maji ya Mara kulishuhudia Makanisa ya Mungu yakibadilisha mikono na huduma zao ziliingia kwenye machafuko. Mwaka 1987 tulilishuhudia Kanisa likiandaliwa ili kupimwa na hiyo ilianza kwenye mwaka wa tatu wa mzunguko wa kalenda wa mwaka 1987. Mnamo mwaka 1991 kanisa lilifikia hatua yake ya mwisho na huduma ilishindwa. Wapendwa walipitia kwenye majaribu au hukumu na kisha wakatawanyika hadi kwenye awamu nyingine iliyofuatia, na wengi wao ni waliraruliwa tu kama riboni za nguo na huduma ile iliyoshindwa.

 

  1. Miaka ya 1992-1998 “Juma la kuwa huko elimu

Juma hili lilimaanisha utengano au utofauti wa uongozi wa kanisa na baraza la elohim. Kinara cha taa ilibidi kilichukuliwe kutoka kwenye imani ya Kanisa la Sardi. Mwisho na upeo au kilele cha imani ya Wasardi ulionekana na huduma zao wenyewe au jinsi walivyohudumukwa kuchagua jina la “Hai” ili kuonyesha kanisa la mwisho la mfumo na imani ile na kuhudumu kwake (kama ilivyoandikwa kwenye Ufunuo 3:1). Ndivyo pia lilivyokuwa imani ya kanisa la Walaodikia iliyoishia hapo na imani yao ikaanza kuondolewa.

 

Mwaka 1995 ulishuhudiwa kuwepo kwa kifaa kilichileta mabadiliko kwenye mbinu za uinjilishiaji kwenye Interneti. 

 

Mwaka 1998 Usomaji wa Torati ya Mungu kwenye Mwaka wa Sabato ulifanyika kwa mara ya kwanza baada ya karne nyingi kupita na kwamba utaratibu wa kuifuata kalenda ya Hekaluni na utaratibu wa kuiadhimisha miaka ya Yubile ulirejeshwa upya rasmi kwenye Makanisa ya Mungu tangu mwaka 1994.

 

  1. Miaka ya 1999-2005 “Juma la mana

Miaka ya 1999-2005. Kutoka tukio la Usomaji wa Torati, Mungu alianza kutoa mikate kutoka mbinguni na kulipa kanisa kwa kiwango kikubwa sana cha ubora na kuwatenga wale waliotuama kwenye Makanisa ya Mungu kwa jinsi watu hao walivyoitumia na kuenenda.

 

Mwaka 2005 Torati ya Mungu ilisomwa tena kwa mara ya pili baada ya karne nyingi kupita. Ushuhuda ulipelekwa hadi Afrika kwa mpangilio wa tahadhari kubwa sana na Mungu akaanza kushughulika na hilo kwa nguvu.

 

  1. Miaka ya 2006-2012 "Juma la kutoka maji kwenye mwamba"

Mwaka huu ulishuhudia mwagiko mkubwa sana wa Roho Mtakatifu kwa jinsi isivyowahi kutokea hapo kabla kwenye historia ya Kanisa la Mungu. Ongozeko la uweza wa kuuelewa unabii ulienea ulimwenguni kote. Tangia mwaka wa tatu, kama ilivyo kawaida, mabadiliko na ukuaji ulianza na Mwaka wa Tatu ongezeko liliombwa na kupokelewa. Tangu mwaka wa Nne ukuaji ulianza kutoka Kusini na Afrika ikafanika kuwa kituo kikuu cha Makanisa ya Mungu. Muungaiko wa Makanisa yote ya Mungu kulifanyika pamoja nay ale yaliyokuwa kwenye imani ya washika Sabato. Wito kwa mataifa mengi kwa hiyo kulifanyika.

 

Mnamo mwaka 2011 mapinduzi makubwa yaliendelea kutokea na kuongezeka na mwaka 2012 utakuwa ni Mwaka wa Tatu wa Usomaji wa Torati na ni mwaka muhimu sana utakaoshuhudiwa migogoro mingi kutokea.

 

  1. Miaka ya 2013-2019 "Juma la mapgano na 'Amaleki"

Mwaka huu utashuhudia vita vya Waamaleki vikiendelea kwa kiwango chake kamili na Makanisa ya Mungu na Wateule watajikuta wamejikita kwenye vita na mogogoro, ya namna mbili zote, yaani ya kimwili na kiroho, itkayosababishwa au kuletwa na wale wanaotaka kuwaangamiza. Kipindi hiki tunatarajia kuwaona Mashahidi wa Mungu na kurudi kwa Masihi kwa ajili ya Usomaji wa Nne wa Torati na vita kuu ya mwisho ya Armagedoni au vita ya Megido na kumwagwa kwa vitasa vya ghadhabu ya Mungu.

 

Shetani atatupwa Kuzimuni au kwenye Shimo refu lisilo na mwisho la Tartaros. Imani na mfumo huu wa kidini utakoma na kuagamizwa.

 

  1. Miaka ya 2020-2026 "Juma la kusimama kwenye Mlima wa Sinai"

Juma hili ki kipindi cha mwisho cha kuwakusanya watakatifu wakimngojea Masihi, kama walivyofanya huko Sinai wakati walipoongea naye uso kwa uso na walikuwa na viongozi wao waliochaguliwa kupitia makabila yao na Baraza la Wazee wa Israeli lilichaguliwa. Walipewa sheria autorati kwa mpangilio endelevu na viongozi wao walisomeshwa au kuelimishwa kwa kipindi cha zaidi ya miazi sita tangu mwezi wa Abibu hadi Eluli, ambapo Musa alipanda kwenda juu mara sita kushauriana au kuongea na Kristo (soma jarida la Mipando ya Musa (Na, 70)). Katika mwezi wa Saba waliishika sikukuu, na kwenye Mwaka huu wa Saba, Baragumu lilipigwa kwa ajili ya upatanisho wa mwaka wa Sabato. Mwaka wa Yubile ulianza, na marejesheano ya vitu yalifanywa.

 

Mnamo mwaka 2028 kipindi cha Milenia kitaanza na watu wote watarudi kwenye milki zao na ulimwengu utaongozwa na Kristo na Watakatifu kutoka Yerusalemu kwa kipindi kinachofuatia cha miaka 1000. Nabii Isaya anasema kuwa Misri itapigwa na kisha itafanywa upya wakati wa Masihi. Watapewa maarifa ya kuijua imani na Torati ya Mungu na Kristo.

 

Unabii huu unakutikana pia kwenye Isaya sura ya 19. Mungu anawaambia kwamba ataitendea Misri. Isaya 19:1-10 inaongelea kuhusu kuanguka na kushindwa kwa mawazo ya Wamisri. Utabiri huu au unabii huu unajiri kipindi cha miaka 2500 na unalinganisha kwa umakini unabii ulio kwenye vitabu vya Ezekieli na Danieli. Wamevunjika au kubwagwa chini na kutawaliwa au kukaliwa.

 

Isaya 19:1-10

Ufunuo juu ya Misri.

Tazama, Bwana amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake. [2] Nami nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme. [3] Na roho ya Misri itamwagika kabisa katikati yake, nami nitayabatilisha mashauri yake, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli, na kwa wachawi.

 

Mvunjiko haya yametokea, ili kuruhusu kukaliwa kutoka kwa Waashuru hadi na Wababeloni na Wamedi na Waajemi kisha na Wayunani na Warumi.

 

[4] Nami nitawatoa hao Wamisri na kuwatia katika mikono ya bwana mgumu; na mfalme mkali atawatawala; asema Bwana, Bwana wa majeshi. [5] Na maji ya baharini yatapunguka, na huo mto utakauka na kuwa pakavu. [6] Na vijito vya mto vitatoa uvundo, na mifereji ya Misri itakuwa haina maji mengi, itakauka; manyasi na mianzi itanyauka. [7] Vitu vimeavyo karibu na Nile, katika ukingo wa Nile, na vyote vilivyopandwa karibu na Nile vitakauka na kuondolewa na kutoweka. [8] Na wavuvi wataugua, na wote wavuao kwa ndoana watahuzunika, nao watandao jarife juu ya maji watazimia. [9] Tena wao wafanyao kazi ya kuchana kitani watafadhaika, na hao pia wafumao bafta. [10] Na nguzo za nchi zitavunjika vipande vipande, wote wafanyao kazi ya mshahara watahuzunika nafsini mwao.

 

Sehemu hii haijatimilika bado na kwa hiyo inaendelea. Kumbuka kwamba utimilifu wa mwisho wa unabii unayataja maji ya mto Nile kuwa yatakauka. Maafa yoyote yale ya namna hii hayajawahi kutokea. Ingawaje kumewahi kutokea matukio kadhaa ya ukame huko Misri na matatizo mengine mengi, ni wakati tu wa ujenzi wa Bwawa Kuu la Juu la lijulikanalo kama Aswan High Dam ndilo tukio lililostua.

 

Sababu ya matatizo mengi ni upuuzi au ujinga wa uongozi wa Wamisri na kwamba hajabadilika.

[11] Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, shauri lao limepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani? [12] Wako wapi, basi, watu wako wenye hekima? Na wakuambie sasa; na wajue mambo aliyokusudia Bwana wa majeshi juu ya Misri

 

Sababu ya hii ni mkanganyiko uliotuama katika Misri kwa kuabudu kwao sanamu na kushindwa kao kuyashika maagizo yaliyo kwenye Torati ya Mungu.

[13] Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu, wakuu wa Nofu wamedanganyika; na hao walio mawe ya pembeni ya kabila zake wameikosesha Misri. [14] Yeye Bwana ametia roho ya ushupavu katika moyo wa Misri, nao wameikosesha Misri katika matendo yake yote, kama mlevi aendavyo huko na huko akitapika. [15] Wala haitakuwako kazi yo yote katika Misri iwezayo kufanywa, ya kichwa au ya mkia, ya tawi au ya nyasi. [16] Katika siku hiyo Misri itakuwa kama wanawake; itatetemeka na kuogopa kwa sababu ya kutikiswa kwa mkono wa Bwana wa majeshi, autikisao juu yake.

 

Kipindi hiki kinaifanya nchi ya Yuda iwe tishio la Wamisri na hilo halijatokea bado na nyakati za hivi karibuni ambapo matukio ya nyakati yameenea kama tutakavyoweza kujionea.

[17] Na nchi ya Yuda itakuwa sababu ya utisho kwa Misri; kila mtu atakayeambiwa habari zake ataingiwa na woga, kwa sababu ya kusudi la Bwana wa majeshi, analolikusudia juu yake.

 

Kisha unabii unaendelea kwenye nchi ya Gosheni ambapo palikuwa ndipo mahali walipoishi au kukaa Waisraeli kabla ya tukio la Kutoka. Unabii unaitaja miji mitano iliyoko huko Heliopolis au Mji wa Jua. 

[18] Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia Bwana wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa uharibifu.

 

Eneo hili lilikaliwa tena na Wayahudi. Walichuikuliwa huko na Ptolemy na akaanzisha koloni kubwa huko Misri kwa hali ambayo hawajawahi kuwepo huko hapo kabla. Kisha unabii unaendelea mbele hadi kwenye karne ya pili KK wakati Onias IV Kuhani Mkuu alipolijenga Hekalu la Mungu huko Heliopolis.

[19] Katika siku hiyo itakuwako madhabahu katika nchi ya Misri kwa Bwana, na nguzo mpakani mwake kwa Bwana.

 

Ilikuwa ni kwenye Hekalu hili ndiko Kristo alipelekwa na Yusufu na Mariamu mwaka 5 KK ili kumlinda kutokana na Herode kati ya siku ya 1 na 13 Abibu mwaka 4 KK. Huku ni kutimiliza unabii ulionenwa na manabii wa Mungu wakisema: “Kutoka Misri Nimekuita mwanangu.”

 

[20] Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa Bwana wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia Bwana kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa.

Kristo alikufa ili awe mwokozi wa mataifa na atatumwa tena kuwapeleka Wamisri utumwani na kuwaokoa kutoka na mauti.


[21] Na Bwana atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua Bwana katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea Bwana nadhiri, na kuzitekeleza.

 

Andiko linaonyesha kuwa Masihi atajidhihirisha mwenyewe kwa Wamisri na wataongoka na kuikubali imani. Ni kweli kwamba Hekalu lililoko huko Heliopolis liliendelea kutoa sadaka za wanyama hadi lilipofungwa mwaka wa 71 BK kwa amri ya Vespasian. Hata hivyo, imani inayoelezewa ya wongofu unaokuja kufanyika baadae ni wa watakatifu na Masihi. Ili kufanya hivi ni lazima wavunjik mioyo yao kwa unyenyekevu na kufanwa upya. 


[22] Naye Bwana atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa Bwana, atakubali maombi yao na kuwaponya

 

Hii itatokea tu katia Nyakati za Mwisho atakapokuja Masihi.

 

[23] Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri. [24] Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa baraka kati ya dunia; [25] kwa kuwa Bwana wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu.

Baada ya Vita hivi vya Mwisho kukaribia, vitaenea tangu Misri hadi Ashuru. Ambao utaanzishwa na wao wenyewe na Israeli ni sawa tu na theluthi ya watu wa Mungu chini ya Masihi, kwenye Edeni mpya.

 

Eneo hili kutoka mto Nile hadi Mito ya Kaskazini na kutoka kwenye pwani mwa bahari ya Mediterranean hadi kule kunakojulikana sasa kama Jangwa la Uarabuni kulikuwa ndiyo eneo halisi na asilia la bustani ya Edeni. Unabii huu unaoihusu Misri na hasahasa Ashuru uliendelea kwa kipindi cha zaidi ya miaka 2200, tangu kujengwa kwa Hekalu la huko Heliopolis na Onias IV hadi kwenye maskani ya Masihi mwaka wa 5 KK, hadi kwenye marejesho ya tangu mwaka 2011-2025. Waashuru na Waisraeli watatembea mkono kwa mkono kutoka Kaskazini hadi Ashuru (sasa Iraq) na Israeli kwenye kipindi chote cha marejesho mapya ya milenia.  

q


 

 

 

 

 

 

 

Nyongeza

Ishara za kijamii za Mashariki ya Kati

nchi

idadi (milioni) wa

Umri wa kati

Jwasio na kazi (%)

Walio chini ya mstari wa umaskini (%)

Wanaotumia huduma za intaneti (milioni)

kwa hisani ya jarida la: CIA World Factbook/UN

Algeria

35.4

27.1

9.9

23

4.7

Misri

84.5

24

9.6

20

20

Jordan

6.5

21.8

13.4

14.2

1.6

Lebanon

4.09

29.4

Na

28

1

Libya

6.5

24.2

30

33

0.35

Morocco

32.3

26.5

9.8

15

13.2

Saudi Arabia

25.7

24.9

10.8

Na

9.6

Syria

22.1

21.5

8.3

11.9

4.4

Tunisia

10.5

29.7

14

3.8

3.5

Ukanda wa Magharibi & Gaza

2.5

20.9

16.5

46

1.3

Yemen

24.3

17.89