Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[047]
Shofa na Tarumbeta ya Fedha
(Toleo La 1.5 20030308-20130905)
1Wakorintho 14:8 inasema: “Kwa maana baragumu ikitoa sauti isiyojulikana,
ni nani atakayejifanya tayari kwa vita?”. Dhana hii ni yakufurahisha sana
kwenye kanuni ya kuwafikia watu walioko mbali. Baragumu au tarumbeta ina historia ndefu nay a
siku nyingi sana kwenye Kanisa. Kwa hiyo umuhimu wake utaelezewa na kufanyiwa
tathimini kwenye jarida hili. Ni wajibu wetu kutoa ujumbe ulio wazi kwa watu
ili waweze kujua la kufanya.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 2003, 2013 Storm Cox, ed. Wade Cox)
(tr. 2014)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na
kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au
kufuta maneno. Jina la
mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe
pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote
atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja
ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Shofa na Tarumbeta ya Fedha
Hapo mwanzo Mungu
muumbaji, Baba yetu alikuwepo; ni wa milele na mwenye uweza na nguvu nyingi;
asili na tabia zake ni Njema na kutokana na yeye Torati na sheria zote
zimetokea kama maelekezo yenye maana na yenye mashiko. Baba yetu akiwa kama
mtendaji wa mapenzi yake alichagua kuumba Neno la Mungu, pia na wana wengine wa
Mungu ambao ni Elohimu. Neno la Mungu akawa ndiye wa kwanza katika uumbaji wa
Mungu ambaye kwa yeye uumbaji wote ulifanyika. Tangu mwanzo, Torati, mpango na
viumbe wa aina ya malaika, waliumbwa na kufanywa wawepo. Hatimaye, malaika
wakiwa katika maongozi, walisaidia kuuumba ulimwengu uliopo na hatimaye
mwanadamu. Soma majarida ya Kusudi la Uumbaji na Kutolewa Dhabihu kwa Kristo
(Na. 160); Malaika wq YHVH (Na. 24); Mungu Tunayemuabudu (Na. 2) na Uwepo wa Yesu Kristo Kabla ya Kuzaliwa
Kwake Kimwili (Na. 243).
Mpango wa Mungu
ulikuwa ni kuwa na kiumbe mmoja chini yake, akifanya kazi kama nguvu isiyoungana
na yenye uweza mkubwa, ili kuudhihirisha mpango wake mkuu. Kwa bahati mbaya, hila
mbaya za malaika mkuu zilijitokeza ambazo zilishuhudia theluthi moja ya malaika
wake aliowaumba wakijiunga kwenye hila hizi za muovu zilizo kinyume na mamlaka
au serikali ya Mungu, na kutafuta kudunisha na kuwaharibu viumbe wa Mungu.
Dhana hii
imetolewa mfano kwenye Biblia kwa tarumbeta fulani mbili maalumu, yaani Shofa
au huitwa pia Keren (au Hoval au Pembe
za Kondoo mume) na kwa tarumbeta mbili za fedha zijulikanazo kama hazozarahs (Hesabu 10).
Tafsiri ya lugha
ya Kiingereza ya Biblia imeonyesha uelewa wa asili na utaratibu au mfumo wa
viumbe wa aina ya malaika. Uvivu na uzembe waliofanywa wa Eloa na Elohimu kama Mungu
umeonyesha uelewa muhimu. Kwa jinsi hiyohiyo kukosea kutenga makundi ya zana za
upepo zote kwa alama ya baragumu, au kwa kiwango cha chini, buruji, imeonekana.
Jarida hili litatathimini zana hizi na kutumaini kutoa mwanga wa namna fulani
kwenye uweza muhimu walionao, pamoja na tumaini la Mungu na watumishi wake ambao
wanawawakilisha.
Wazo la kwanza la
kuhusu pembe ya dume la kondoo au Shofa limetolewa kwenye kitabu cha Mwanzo,
kama ilivyoeleweka kwenye kitabu cha fasiri kijulikanacho kama Encyclopedia
Judaica, kuhusu alipopewa Ibrahimu kondoo akiwa kama sadaka badala ya kumtoa
mwanae Isaka. Sadaka ya Isaka ilikuwa ni hadithi iliyotolewa kuwa ni mfano
ashirio wa sadaka ya Kristo alipokuwa ale mtini, kwa ajili ya ukombozi wetu.
Kwa jinsi hiyohiyo sehemu ya habari hii imeelezewa pia kwenye vifungu vya
maandiko ya Kiislamu pia, kama sadaka ya Ishmaeli kutoka kwenye Korani (soma
jarida la Mwanzo 22, Imani ya Kiyahudi, Uislamu na Sadaka ya
Isaka (Na. 244)).
Hadithi zote
mbili (na hasahasa maandiko ya Biblia) ni mfano elekevu wa mlolongo wa Pasaka,
ambapo kondoo asiye na waaa alichukuliwa, kuchinjwa na kuliwa. Mifupa na nyama
iliyobakia hazikutakiwa wawenazo hadi asubuhi. Vitu vingine vilikuwa ni pembe
za kondoo asiye na hila wala mawa. Pembe hii ni inamuashiria Mungu Baba, na
asili yake ya Sheria, ambazo zimewekwa nay eye. Ni ishara pia a asili ya
umilele wa Mungu. Mlango ujao na ushindi ambao Mungu atakuwanao, na hatima ya
uumbaji, na utii kwa Mungu Mmoja na wa Pekee wa Kweli.
Utajwaji wa
kwanza wa hii Sofa umeanzia kwenye kitabu cha Kutoka sura ya 19. Tunasoma:
Kutoka 19:9-13 Bwana akamwambia Musa, Tazama, mimi naja kwako katika wingu zito ili watu hawa wasikie nitakaposema nawe, nao wapate kukuamini wewe nawe hata milele. Musa akamwambia Bwana hayo maneno ya watu. 10 Bwana akamwambia Musa, Enenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao, 11 wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu Bwana atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote. 12 Nawe utawawekea mipaka watu hawa pande zote, ukisema, Jihadharini, msipande mlima huu, wala msiuguse, hata mapambizo yake; kila mtu atakayeugusa mlima huu, bila shaka atauawa. 13 Mkono wa mtu awaye yote usimguse mtu huyo, ila hakika yake atapigwa kwa mawe, au kupigwa kwa mkuki; kwamba ni mnyama au kwamba ni mwanadamu, hataishi. Hapo panda itakapotoa sauti kwa kufuliza ndipo watakapoukaribia mlima.
Tarumbeta
inayoelezewa hapa inamaanisha Shofa. Neno lililotumika hapa ni Yobel, ambalo linamaanisha mlio
unaotokana na mpulizo wa pembe.
Kutoka 19:14-19 Musa akatelemka mlimani akawaendea watu akawatakasa, nao wakafua nguo zao. 15 Akawaambia watu; Mwe tayari siku ya tatu; msimkaribie mwanamke. 16 Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka. 17 Musa akawatoa hao watu katika kituo, akawaleta ili waonane na Mungu; wakasimama pande za chini za kile kilima. 18 Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu Bwana alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuu, mlima wote ukatetemeka sana. 19 Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti.
Shofa au pembe ya
kondoo haipigwi na wengine wowote zaidi ya wale walio kwenye kusaniko. Ilikuwa
inatoa sauti kubwa na ndefu. Ilikuwa inapigwa na malaika ili kutangaza uwepo wa
Malaika wa Yahova, alipokuja kama mwakilishi wa Baba. Shofa na upigaji wake ni
tangazo la uwepo wa Mungu na mamlaka yake unaotokana nayo. Kutokana na
utangazaji huu Sheria au Torati ulipotolewa na kupewa nabii Musa kupitia Kristo
kutoka kwa Mungu Baba. Wazo hili ni uendelezo wa yule aliyeelezewa kwenye utangulizi.
Nao ni Mungu na Kristo wanaotengeneza Sheria na kuziwezesha zionekane au
kuthihirika mapema kabla ya uumbaji wa dunia ulivyopangiliwa. Kwa hiyo, Torati
ilitolewa kwenye vitabu vya Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la Torati. Hii
ilikuwa ni mapema kabla ya kuwakusanya watu kulikoelezewa kwenye kitabu cha
Hesabu.
Ni kama Mungu
anavyochagua kujiwakilisha mwenyewe kwa kupitia shofa, anachagua kutupa sisi
pembe yetu ili kujiwakilisha sisi wenyewe. Anatupa sisi hilo kwenye Hesabu sura
ya 10.
Hesabu 10:1-2 Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia, 2 Jifanyie tarumbeta mbili za fedha; utazifanya za kazi ya ufuzi; nawe utazitumia kwa kuwaita mkutano wakutane, na kwa kusafiri kwao yale makambi.
Wazo la
kutengeneza tarumbeta mbili za fedha, kutoka kwenye kipande kimoja cha fedha,
linaelezea mambo mawili ya uumbaji. Pande mbili za uumbaji wa kimwili na kiroho
zilizo kwenye mpango mmoja.
Hesabu 10:3 Na hapo watakapozipiga hizo tarumbeta, mkutano wote utakukutanikia wewe, hapo mlangoni pa hema ya kukutania.
Wakati
zinapopigwa zote mbili viumbe wote wanaitwa kukusanyika; wote wawili, yaani
malaika na wanadamu, wakusanyike kwenye nyumba ya Mungu.
Hesabu 10:4 Nao wakipiga tarumbeta moja tu ndipo wakuu, walio vichwa vya maelfu ya Israeli, watakukutanikia wewe.
Hapa
wazo hili la viumbe wa aina ya malaika wakusanyike pamoja na wanadamu
linawakilishwa kwa kuitumia pembe kwa wafalme, daraja la kwanza la ngazi za
kiserikali ya viumbe, na baragumu la pili ni kwa viumbe wa daraja la pili.
Hesabu 10:5-12 Tena hapo mtakapopiga sauti ya kugutusha sana, marago yaliyoko upande wa mashariki yatasafiri. Tena hapo mtakapopiga sauti ya kugutusha ya pili, marago yaliyoko upande wa kusini watasafiri; 6 watapiga sauti ya kugutusha kwa ajili ya safari zao. 7 Lakini mkutano utakapokutanishwa pamoja mtapiga, lakini hamtapiga sauti ya kugutusha. 8 Wana wa Haruni, makuhani, ndio watakaopiga hizo tarumbeta; nazo zitakuwa kwenu ni amri ya milele katika vizazi vyenu vyote. 9 Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za Bwana, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu. 10 Tena katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu zilizoamriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 11 Ikawa mwaka wa pili, mwezi wa pili, siku ya ishirini ya mwezi, hilo wingu liliinuka kutoka pale juu ya maskani ya ushahidi. 12 Wana wa Israeli wakasafiri kwenda mbele, kwa safari zao kutoka jangwa la Sinai; na hilo wingu likakaa katika jangwa la Parani.
Kwenye aya ya 8 Mungu
anatuamuru sisi kuzipiga tarumbeta hizi kwenye Siku zetu Takatifu ikiwa ni amri
ya milele katika vizazi vyetu vyote.
Kufuatia na
utengenezaji wa baragumu hizi na kuzifanya kuwa ni ishara kwa viumbe na kufanya
ishara ya kuwaitia wanajeshi, wingu lilishuka kwenye hema ya kukunia. Wingu
hili liliwekwa juu yao Israeli walipokuwa wanatoka nje ya nchi ya Misri. Kwenye
Kutoka 19:9 unasoma:
Kutoka 19:9 Bwana akamwambia Musa, Tazama, mimi naja kwako katika wingu zito ili watu hawa wasikie nitakaposema nawe, nao wapate kukuamini wewe nawe hata milele. Musa akamwambia Bwana hayo maneno ya watu.
Wingu hili
lilikuwa ni wingu la ulinzi ambalo liliuacha mkutano na kuondoka baada ya kuupa
mkutaniko utaratibu wa kimaonyo, na utaratibu wa kuwaita warudi nyuma kwa wingu
hilo wakati mataifa na makabila yalilihitaji. Kitendo cha kuacha kuzipiga pembe
hizi kilimaanisha kuwa ulimwengu wa malaika usishirikishwe kwa kuletwa kwenye
vita na kuungana nasi, ili kupigana na adui zetu wakiwa nasisi na kutulinda
kutokana na maadui zetu.
Tarumbeta
ziliamriwa pia kupigwa juu ya sadaka za kuteketezwa. Utaratibu wa kutoa sadaka
alipewa Adamu na ulieleweka na familia tangu hapo hadi kufa kwa Kristo.
Utaratibu wa kutoa sadaka ulifanyika ikiwa ni kama alama ya mchakato ulioendelea
na wanadamu katika mpango wa Mungu. Ni kwa kuweka hivyo tu kunamaanisha kuwa ni
mjadala mgumu kwenye hewa gasi ya unajisi iliyoongezewa. Mnyama aliyesafi hufa
na hatimaye anachomwa moto na kuungua, au anaunguzwa kwenye tanuru la moto kama
fedha pamoja na takataka za chuma zinazobakia majivuni, na roho ikiungana na
ulimwengu wa roho ili kuwakilisha kwa Mungu “kama manukato yenye harufu ya
kupendeza”. Upigaji wa tarumbeta za fedha ulikuwa ni tangazo la mchakato wa tafsiri
na muunganiko na Baba. Sauti iliyopigwa ilizifanya sadaka zikumbukwe. Pasipo
upigaji wa hizi pembe, mchakato wa utoaji wa sadaka unakuwa haujakamilika, au
unafanya usiwe na maana.
Kwa hiyo, Mungu
anafanyiwa mfano kwa shofa, viumbe wa aina ya malaika kwa upigaji mmoja wa
tarumbeta ya fedha. Hii imeelezewa vyema na Daudi kwenye Zaburi 47:5:
Mungu (SHD 430) - Elohim
Amepaa – Ameinuliwa juu
Kwa kelele (SHD 8643) – teruwah(kelele – za shangwe, sauti ya vita kama sauti ya baragumu) yaani, sauti inayotokana na Hazozara
Bwana (SHD 3068)-Yehova (Mungu Baba)
Kwa sauti ya Baragumu (SHD 7782) – Shofa
0768868333Tunaposoma
Sefania 1:16 tunaona dhana hiyohiyo iliyotumika kuhusianisha na hii.
Sefania 1:16 Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.
Kuitafsiri hii
kiusahihi tulipaswa kusoma hivi:
“Siku ya Shofa teruwa (chatsotsserahalarm) juu ya buruji na kuta za miji zilizo ndefu sana.”
Kwa hiyo Zaburi
47:5 ingepasa isomeke hivi:
Tunamtukuza Elohim
kwa mlio na Yehova kwa shofa.
Tutashughulika na
umuhimu wa hii hivi karibuni.
Baadae tutatathimini
alama ya umuhimu ya upigaji wa shofa pamoja na baragumu za fedha. Kwanza
kabisa, tunaiona mifano ya matumizi ya shofa kwenye Biblia.
Huenda
unaojulikana sana na wa wazi sana uliofanyika kuhusu matumizi ya shofa umeelezewa
kwenye kitabu cha Yoshua, kwa habari ya Yeriko. Hii ni hadithi kubwa
inayoonyesha uweza wa Mungu. Hadithi hii inaweza kueleweka vizuri ukisoma
jarida la Kuanguka kwa Yeriko (Na. 142).
Matumizi yanayojulikana
sana ya shofa yalikuwa ni vitani. Baragumu za fedha zilipigwa kwa watu, na
kutakiwa wajilinde vitani wakati wa mashambulizi ya maadui, na kutokana na
machafuko ya kila siku ambayo watu waliyavumilia. Upigwaji wa shofa vitani
ulikuwa na sababu mbalimbali. Vita ambavyo shofa ilipigwa, vilikuwa ni vita
ambavyo Mungu aliruhusu vipiganwe, na lilikuwa ndilo jambo la kwanza na la msingi
la mpango wake na maongozi yake kwenye maeneo hayo kwa wakati ule.
Neno shofa ni la namba 7782 kwenye kamusi ya
SHD na ni Maandiko Matakatifu yanayofanana yanayomaanisha neno hilihili la
shofa linalotathiminiwa.
Tunaelewa sasa
maana na matumizi ya aina zote mbili za uandishi wa pembe. Na hata kabla hatujaangalia
kwenye upigwaji wa pembe hizi kwa pamoja, hebu na tutazame kwanza kwenye Danieli
3. Hapa inatupa taswira ya kupendeza kwenye uelewa na umuhimu ambao watu
walikuwanao kwenye falme zote, na kwenye uhusiano uliopo kati ya Mungu na sauti
au milio ya pembe hizi.
Kama tujuavyo,
jina la Kiebrania la aina ya shofa zaidi ya kuiita shofa lilikuwa keren (au pembe) e yovel au pembe ya kondoo. Sasa hii keren ilikuwa ni pembe tu, na inawezekana sana ilikuwa ni ya namna
ya shofa, ambayo ilitokana au kutengenezwa kutokana na chuma kwa mikono ya
wanadamu, na ampayo iliifanya kimapokeo na kiimani kuwa najisi na kutoweza
kufikia kiwango cha “shofa”.
Tunasoma hivi
kwenye Danieli 3:
Danieli 3:1-15 Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. 2 Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha. 3 Ndipo maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. 4 Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi, 5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. 6 Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuru ya moto uwakao. 7 Basi wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha. 8 Basi baadhi ya Wakaldayo wakakaribia, wakaleta mashitaka juu ya Wayahudi. 9 Wakajibu, wakamwambia mfalme Nebukadreza, Ee mfalme, uishi milele. 10 Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu; 11 na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa katika tanuru ya moto uwakao. 12 Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. 13 Basi Nebukadreza akatoa amri kwa hasira na ghadhabu, waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Basi wakawaleta watu hao mbele ya mfalme. 14 Nebukadreza akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? 15 Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu?
Neno Keren au pembe limetafsiriwa kama
kimondo. Pembe inayoongelewa hapa ni kifaa cha kwanza kabisa kuliko zote. Zana
nyingine zote zinapigwa ili kushirikiana na pembe kama Mfalme Daudi
alivyoziweka (Zekaria 13). Kile Nebukadneza alichotafuta kukifanya hapa ilikuwa
ni kutengeneza sanamu, Mungu wa uwongo. Kwa kupigwa kwake shofa kwa kutumia
pembe iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu kulimaanisha walitengeza sanamu,
wakalazimishwa watu wapige magoti na kuviabudu; ni nakala kamili ya imani na
ibada ambayo Mungu aliianzisha kwa kutumia shofa kama imani yake. Utekelezaji
wa amri hii yanashangaza.
Hebu na tutathimini
sasa mifano iliyotolewa kwenye Biblia kuhusu matumizi tarumbeta za fedha na
shofa kwa pamoja.
Kwanza
tutatafakari kwa kujionea kwenye 1Nyakati sura ya 15.
1Mambo ya Nyakati
15:1-29 Basi Daudi akajifanyia nyumba katika mji wa Daudi; akapaweka tayari
mahali kwa ajili ya sanduku la Mungu, akalipigia hema. 2 Ndipo
Daudi akasema, Haimpasi mtu awaye yote kulichukua sanduku la Mungu, isipokuwa
Walawi peke yao; kwa kuwa hao ndio aliowachagua Bwana, ili walichukue sanduku
la Mungu, na kumtumikia daima. 3 Basi Daudi
akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu, ili kulipandisha sanduku la Bwana,
mpaka mahali pake alipoliwekea tayari. 4 Daudi
akawakutanisha wana wa Haruni, na Walawi; 5 wa wana wa
Kohathi; Urieli mkuu wao, na nduguze mia na ishirini; 6 wa
wana wa Merari; Asaya mkuu wao, na nduguze mia mbili na ishirini; 7 wa wana wa Gershoni; Yoeli mkuu wao, na nduguze mia na
thelathini; 8 wa wana wa Elsafani; Shemaya mkuu wao,
na nduguze mia mbili; 9 wa wana wa Hebroni; Elieli
mkuu wao, na nduguze themanini; 10 wa wana wa Uzieli;
Aminadabu mkuu wao, na nduguze mia na kumi na wawili. 11 Tena,
Daudi akawaita Sadoki na Abiathari makuhani, na hao Walawi, Urieli, Asaya,
Yoeli, Shemaya, Elieli, na Aminadabu, 12 akawaambia,
Ninyi ni vichwa vya mbari za baba za Walawi; jitakaseni, ninyi na ndugu zenu,
ili mlipandishe sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli, mpaka mahali pale
nilipoliwekea tayari. 13 Kwani kwa sababu ninyi
hamkulichukua safari ya kwanza, Bwana, Mungu wetu, alitufurikia, kwa maana
hatukumtafuta sawasawa na sheria. 14 Basi makuhani na
Walawi wakajitakasa, ili wapate kulipandisha sanduku la Bwana, Mungu wa
Israeli. 15 Na wana wa Walawi wakalichukua sanduku la
Mungu mabegani mwao kwa miti yake, kama vile Musa alivyoamuru, sawasawa na neno
la Bwana. 16 Kisha Daudi akamwambia mkuu wa Walawi,
kwamba awaagize ndugu zao waimbaji, pamoja na vyombo vyao vya kupigia ngoma,
vinanda, na vinubi, na matoazi, wavipige na kupaza sauti kwa furaha. 17 Basi Walawi wakamwagiza Hemani mwana wa Yoeli; na wa
nduguze, Asafu mwana wa Berekia; na wa wana wa Merari ndugu zao, Ethani mwana
wa Kishi; 18 na pamoja nao ndugu zao kwa cheo cha
pili, Zekaria, na Yaasieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu; na
Benaya, na Maaseya, na Matithia, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na
Yeieli, mabawabu. 19 Hivyo hao waimbaji, Hemani,
Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu; 20 na Zekaria, na Yaasieli na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni,
na Eliabu, na Maaseya, na Benaya, wenye vinanda vya sauti ya Alamothi; 21 na Matithiya, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na
Yeieli, na Azazia, wenye vinubi vya sauti ya Sheminithi, 22 waongoze.
Na Kenania, mkuu wa Walawi, alikuwa juu ya uchukuzi; yeye aliusimamia uchukuzi,
kwa sababu alikuwa mstadi. 23 Na Berekia na Elkana
walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku. 24 Na
Shebania, na Yoshafati, na Nethaneli, na Amasai, na Zekaria, na Benaya, na
Eliezeri, makuhani, wakapiga baragumu mbele ya sanduku la Mungu; na Obed-edomu
na Yehia walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku. 25 Basi
Daudi, na wazee wa Israeli, na maakida wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha
sanduku la agano la Bwana kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu; 26 hata ikawa, Mungu alipowajalia Walawi waliolichukua
sanduku la agano la Bwana, wakachinja ng'ombe saba, na kondoo waume saba. 27 Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi
wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na
waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani. 28 Ndivyo
Israeli wote walivyolipandisha sanduku la agano la Bwana kwa shangwe na kwa
sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa
vinanda na vinubi. 29 Hata ikawa, sanduku la agano la
Bwana lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani,
akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia; akamdharau moyoni mwake. (Tafsiri ya The King James Version, (Cambridge: Cambridge)
1769.
Aya ya 28 ya sura
hii imetafsiriwa vibaya sana ikionyesha matukio ambayo yanajulikana vyema. Aya hii
ilipaswa itafsiriwe kama hivi:
Ndipo Israeli wote wakalileta sanduku la agano la Bwana na Teruwa (Mlio), na pamoja na sauti ya shofa pamoja na baragumu za fedha.
Upigaji huu wa
kugutusha unaonyesha kwamba Daudi alikuwa anawaunganisha tena watu wote warudi
kwa Mungu kwa unyenyekevu. Shofa inatangaza uwepo wa nguvu za Mungu ndani ya
sanduku la agano, na tarumbeta za fedha, zinapigwa ili kuwaita watu na malaika
wakutanike pamoja kama nguvu iliyoungana.
Binti wa Sauli
alimdharau Daudi alipokuwa anaacha madaraka ya Sauli, na kuviacha vitu nyuma
kwa utaratibu na nia sahihi, ambayo yalipaswa kuwafaidia watu wa Mungu.
2Nyakati 15 inatuambia
hadithi inayofanana kama hivi:
2Nyakati 15:1-19 Ndipo roho ya Mungu ikamjia Azaria mwana wa Odedi; 2 naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; Bwana yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi. 3 Basi tangu siku nyingi Israeli wamekuwa hawana Mungu wa kweli, wala hawana kuhani afundishaye, wala hawana torati; 4 lakini walipomgeukia Bwana, Mungu wa Israeli, katika msiba wao, na kumtafuta, akaonekana kwao. 5 Hata na zamani zile hakukuwa na amani kwake atokaye, wala kwake aingiaye, ila fadhaa kubwa juu yao wote wakaao katika nchi. 6 Wakavunjika-vunjika, taifa juu ya taifa, na mji juu ya mji; kwani Mungu aliwafadhaisha kwa shida zote. 7 Nanyi jipeni nguvu, wala mikono yenu isilegee; kwa maana kazi yenu itakuwa na ijara. 8 Naye Asa alipoyasikia maneno hayo, yaani, unabii wa mwana wa Odedi nabii, akatiwa nguvu, akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi ya Yuda na Benyamini, na katika miji aliyoitwaa milimani mwa Efraimu; akaifanyiza tena madhabahu ya Bwana, iliyokuwako mbele ya ukumbi wa Bwana. 9 Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu, na wa Manase, na wa Simeoni; kwa kuwa walimwangukia wengi katika Israeli, walipoona kwamba Bwana, Mungu wake, alikuwa pamoja naye. 10 Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwake Asa. 11 Wakamchinjia Bwana siku ile, katika nyara walizozileta, dhabihu za ng'ombe mia saba, na kondoo elfu saba. 12 Wakafanya agano, ya kuwa watamtafuta Bwana, Mungu wa baba zao, kwa mioyo yao yote, na kwa roho zao zote; 13 na ya kwamba ye yote asiyemtafuta Bwana, Mungu wa Israeli, atauawa, akiwa mdogo au mkubwa, kwamba ni mwanamume au mwanamke. 14 Wakamwapia Bwana kwa sauti kuu, na kwa kelele, na kwa mapanda, na kwa baragumu. 15 Na Yuda wote wakakifurahia kile kiapo; kwani wameapa kwa moyo wao wote, na kumtafuta kwa mapenzi yao pia; naye ameonekana kwao; naye Bwana akawastarehesha pande zote. 16 Hata na Maaka mamaye Asa, mfalme akamwondolea daraja yake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake, akaiponda, akaiteketeza penye kijito cha Kidroni. 17 Lakini mahali pa juu hapakuondolewa katika Israeli; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu siku zake zote. 18 Akavileta nyumbani mwa Mungu vitu alivyovitakasa babaye, na vile alivyovitakasa mwenyewe, fedha, na dhahabu, na vyombo. 19 Wala hapakuwa na vita tena hata mwaka wa thelathini na tano wa kutawala kwake Asa. (Tafsiri ya King James Version, (Cambridge) 1769).
2Nyakati 15:14 ilipaswa
itafsiriwe kama hivi:
Na walimuapia Bwana kwa sauti kuu wakisema,
Na kwa kelele, (SHD 8643) – teruwah (mlio)
Pamoja na baragumu, (SHD 2689) – Hazozarah (baragumu za fedha)
Na pamoja na buruji.(SHD 7782) - Shofa
Hadithi ya Asais ni
ya muhimu na inafanya taswira hali tunayoijua leo. Israeli walikuwa kwenye
kipindi kirefu wakiwa hawana “huduma ya kuwafundisha” na hawakuwa wanamjua
Mungu wa Pekee wa Kweli. Walikusanika pamoja na kuingia kwenye agano na Mungu
kama mbinu za kurejesha uhusiano na muunganiko. Shofa ilipigwa ili kuashiria kuwa
Mungu ni wa milele, na walikuwa wanyenyekevu kwenye mamlaka yake. Baragumu za
fedha zilipigwa ili kuwaita watu wakusanyike pamoja pamoja na malaika wawe wote
pamoja. Maana yake imepotea na uelewa uliopotea.
Sisi pia tumeingia
kwenye agano jipya na kuangalia mbele tukitarajia muunganiko wake. Daudi
alifafanua dhana hii kwenye Zaburi 98 na inapaswa itafsiriwe kama hivi.
Tunasoma hivi:
Zaburi 98:1-9: Zaburi
Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. 2 Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. 3 Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. 4 Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. 5 Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. 6 Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana. 7 Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. 8 Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha. 9 Mbele za Bwana; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili. (Tafsiri ya King James Version, (Cambridge) 1769.
Kwa Baragumu
(SHD 2689) – Hazozarah (baragumu za fedha)
Na kwa sauti ya buruji (SHD 7782) - Shofa
Piga kelele za furaha mbele za Mfalme.
Hapa Daudi anaweka
taswira ya wakati atakaporudi Kristo, na viumbe wote watashikamana chini ya
serikali moja ya Mungu. Ndipo upigaji wa kugutusha wa papo kwa papo wa zote mbili
kwa pamoja utafanywa. Wazo hilihuili moja tuliliona hapo nyuma mapema kwenye Sefania
1:16.
Nabii anaangalia
mbele hadi kwenye kipindi ambacho mambo yote ya viumbe wa aina zote mbili, malaika
na wanadamu, watakusanyika pamoja wakiwa wamoja tena.
Tukio hili
linalokuja tulipewa kwenye Mambo ya Walawi kama siku takatifu. Ni siku takatifu
ambayo tumeamriwa kuzipiga shofa zote mbili na tarubeta za fedha kwa pamoja,
ili kuadhimisha kipindi hiki kinachokuja cha ushindi na kuungana.
Walawi 23:24 tunasoma:
Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, kutakuwa na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa kuzipiga baragumu, ni kusanyiko takatifu.
Ilipaswa itafsiriwe
hivi:
Walawi 23:24:
Nena na wana wa Israeli, uwaambie,
Mwezi wa saba, -Tishi
siku ya kwanza ya mwezi,- mwandamo wa mwezi,
mtakuwa na Sabato
Siku ya kuikumbuka ya kupiga panda (SHD 8643) – teruwah yaani piga makelele kwa kuzipiga baragumu kama ilivyo kwenye Zaburi 47:5.
Andiko hili
halionyeshi kuwa ni baragumu, wala shofa wala hazozara. Kutoka kwenye andiko la
Zaburi 81:3, tumeamriwa kupiga aina zote mbili za baragumu kwenye siku hii,
kukiashiria umoja na mshikamano wetu na (Yehova, Baba yetu) kwa shofa, na elohim
(viumbe, jamii ya malaika na wanadamu walioko duniani), ni hazozara wawili.
Madai ni kwamba
Mambo ya Walawi 25 inaamuru kupigwa shofa katika Siku ya Upatanisho kila mwaka.
Hili ni kosa kama kwenye Mambo ya Walawi 25 inapoutaja mwaka wa yubile.
Biblia iko wazi
kuhusu wakati na jinsi baragumu hizi zinatakiwa zitumike, na zina sehemu muhimu
sana ya kutuelekeza mchakato na mwenendo wetu wa kidini na wajibu wetu.
Kitabu cha Ufunuo
kinaelezea kuhusu wakati wa mwisho ambapo malaika watazipiga baragumu z Mungu,
ili kuamuru matukio yatakayopelekea ujio wa pili wa Masihi.
1Wakorintho 15:52
inaielezea sauti ya shofa, kwa kusema kuwa “kwa dakika moja, kufumba na
kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu
watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.”
Tangu ilipokuwa
inatolewa Torati wakati wa Musa, hadi kwenye hukumu ya mwisho na ufufuo wa
viumbe wote na wa mwisho wa Mungu, shofa itapigwa ili kuanza, na shofa itapigwa
ili kuhitimisha. Ni kama kengele inavyolia ili kuashiria kuwa shule imeanza, na
ule upigaji uliotumika kupigia ikitoa mwito, nayo shofa itapigwa ili kuwaashiria
viumbe kwenye matendo na mabadiliko.
Ni wajibu wa
Kanisa kupiga baragumu na kuhubiri jumbe zinazoeleweka. Ni wajibu wetu
kuwaelekeza watu siku na mahali tunapokutanika na mahali tunapofanyia ibada na
jinsi ya kuabudu na matendo yetu. Ni wajibu wetu kusikiliza na kuitambua sauti
ya na kufuata maelekezo yake.
Inatupasa kila
mara kuwa tayari kulikuliko tulivyokuwa huko nyuma kulisikiliza baragumu
lililonenwa kwenye 1Wathesalonike 4:16-17.
“Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka
mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu;
nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa
pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja
na Bwana milele.”
AMINA
q