Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu

[054]

 

 

 

Jina La Mungu Kwenye Uislamu

 

(Toleo La 1.0 20020126-20020126)

 

Kutoka Septemba tarehe 11 mwaka 2001 kumekuwa na kiasi kikubwa cha ufichaji wa habari na visingizio vya kitoto ikitokea kama matokeo ya kuelekea kwenye historia na midahalo huko Marekani, hususan kwenye mifumo na imani zake za kidini. Utumiaji wa jina la Mungu ni mojawapo ya mfano huo.

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

(Hatimiliki © 2002 Wade Cox)

(Imetafsiriwa Mwaka 2009; rev. 2017)

 

Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org na http://www.ccg.org

 

 


 Jina La Mungu Kwenye Uislamu

 


Ujinga wa kutokujua: Mwanzo wa chuki

Mara nyingi mtu anaweza kupumbazwa na kukerwa na kiwango kikubwa cha ujinda wa kutokujua wa imani za kidini za ulimwenguni humu. Kwenye majadiliano ya siku nyingi kumekuwa na kiwango kikubwa na kisicho cha kawaida cha kisingizio cha imani ya Kiislamu iliyotiliwa mkazo, au ni kama ni matokeo yake, ndipo mashambulizi ya kigaidi yanatokea kwenye imani za Waafghani chini ya Wataliban na mtandao wa Bin Laden majibu ya kimatokeo makubwa ya Washirika wao. Majarida mengi yamekuwa yakizungushwa ambayo ni ya uwongo sana, lakini tena yamewakilishwa kwa njia ya kimadai, ambaye ni mwanazuoni msomi wa Dini Zinazolingana mambo yake angeweza kucheka ayaonapo madai haya. Hata hivyo, idadi ya watu, ambao hawajajulishwa vya kutosha, wanakuwa wamechukuliwa kwenye maandishi au nakala za kidini.

 

Hadithi moja kama maelezo na alama au maandishi hayo yanahusu jina la Mungu au Allah kwa Kiislamu.

 

Tutaangalia baadhi ya madai yahusuyo mambo haya. Huenda tunaweza kupata ukweli kidogo na sababu kulingana na ukweli wa mambo yanayobishaniwa.

 

Chimbuko la Jina Allah

Dai mojawapo kuhusiana na jina hili la Allah ni kufanya mizunguko ifuatayo.

 

“Iwapo kama hii ingekuwa ni historia ya iliyothibitishwa, basi kitabu kidogo cha maandiko kingeeleza kwamba mungu wa Muhammadi alikuwa ni kazi iliyobuniwa na wanadamu. Saudi Arabia lilikuwa ni taifa la kipagani lililoabudu zaidi ya miungu 300. Mmojawapo kati ya miungu hiyo alikuwa ni mungu mwezi aliyejulikana kama al-ilah. Hadithi zinasema kwamba huyu mungu mwezi aliolewa na mungu wa jua na walizaa mabinti wawili, na hawa wawili nao waliabudiwa kama miungu midogo ya kike. Wakati Muhammadi alipodai kuwa ameonyeshwa au kupokea ‘maono’ yake na ‘ufunuo kutoka kwa Gabrieli’ alimchagua al-ilah kama ndiye mungu kujenga jeshi lake karibu. Muhammadi alilifupisha jina hili la al-ilah na kuwa Allah, na kumtangaza kwamba ni yeye peke yake ndiye anayefaa kuabudiwa. Alikataza na kupiga marufuku ibada za kuwaomba wale mabinti. Mpaka siku hii ya leo, sanamu ya mwezi mwandamo mchanga inaweza kuonekana mbele au juu au mahala popote muhimu kwenye kila msikiti, ikiwa ni ishara ya kukubali kwamba Allah alikuwepo na ni mungu wa mwezi. Haya yote yamekosekana kuandikwa kwenye maandiko ya makala ya Houghton-Mifflin”

 

Sasa machoni mwa malumbano haya ingeonekana kuwa ni hoja yenye kukubalika kwa wasiojulishwa na kwa kweli imeenea kwa baadhi kuwa ni mtazamo hakisi na sahihi.

 

Kumbuka mwandishi anashambulia maelezo na hoja za Houghton-Mifflin kwa kuwa hazina kile kinachowakilishwa kama ni ukweli unaothibitika. Inataka kudai na kutafuta maeneo ya kushindwa kwa watunzi ili kuonyesha amani hii ya thamani ya habari. Haishangazi kuona kwamba maelezo hayo hayana rejea kama hizi, kama madai hayo ni ya uwongo yote kabisa, kama tutakavyokwenda kuona.

 

Majina ya Mungu Mwezi na Mwezi Wake Jua

Jina la Mungu Mwezi hapo mwanzoni liilikuwa Sin alivyojulikana kwa Waisraeli. Waarabu walimpatia mungu huyu mume jina la Qamar na mwenzi wake walimuita Shamsi. Nabari zake kwa kina zinapatikana kwenye jarida la (Ndama wa Dhahabu (Na. 222)).

 

Mungu jua alikuwa ni mwenza wa kike. Majina tunayoyapata miongoni mwa Selti yanatokana na majina haya. Kwa mfano jina James, yaani Yakobo linatokana na aina ya jina hili la Shamus na linatokana na imani hii. Ndivyo ilivyo pia kwa miungu ya Milkomu na Kemoshi ya kipagani ya wana wa Lutu. Mungu Milkomu anahusiana katika jina la Malkomu.

 

Jina Al ilati linalozungushwa na kuenea kama tunavyoona hapo juu ni upotoshaji wa mmoja wapo kati ya miungu mike mitatu ya kike. Jina Al ilati ni muundo wa kizamani sana wa Mungu jua aliyetajwa kwenye maandiko ya Herodotus i. 131, iii, 8. Huyu alikujakuwa Al lati ama Allati na maana yake ni mungu mke. Alikuwa anaabudiwa na Waarabu wa peninsula ya Sinai na hasa hasa wa jamii ya Nabateani na Palmyrenesi. Herodotus anadai kwenye ukurasa wa pili kwamba ‘alilati na ‘arotalti ni miungu mikuu wa Waarabu. Noldeke (ERE I, ukurasa wa 661) kinatuofanya tulione jina kuwa ni kama mtindo wa kizamani sana wa jina Allati na kinalinganisha na jina Al’ilah, ambalo ni jina la kale la Allah. Kwenye vifungu vyote viwili vya Herodotus vinamuonyesha yeye na Ούρανίη na hivyo basi mungu mke mkuu wa kuheshimiwa na kustahili.

 

Maelezo ya uthibitisho kwamba al itati mungumke hahusiani na Allah ni taarifa iliyotolewa na Muhammadi mwenyewe kwenye Korani katika sura ya 1iii:19, ambapo anamwelezea al ilati kama ni mmoja wapo wa miungu mitatu ya mbinguni, Ali Lat, Al Uzza, na Manati kama wa tatu. Alikanusha uhusiano na mshikamano wao na kumuweka Allah kuwa ni kama Mungu mmoja wa Kweli. Kwenye Sura hii anaendelea mbele kwa kukanusha kuombwa na kuabudiwa au kutukuzwa kwa Sirius (Sura ya 1iii, 50) katika kuilaani imani ya  kwamba Siriusi mwenyewe alikuwa na nguvu za kimungu.

 

Al Lati pia anajulikana au kutajwa kwenye maelezo katika Safa kama LT na pengine HLT. Anajulikana kama ni Mama wa Miungu. Jina hili linaonekana wazi kutamkwa kama Hallati. Alipewa heshima kubwa na kutukuzwa miongoni mwa Warabu wa baadaye.

 

Mungu jua aliyechukuliwa jupokea heshima maalum kwa Wanabateanis na kutambuliwa na Strabo (784) pia ilijulikana kuwa Al Lat (ERE ibid.).

 

Dini potofu ilikuwa huko Ta’if hadi mashariki mwa Maka na kabila la Thaqif lilimwongelea yeye kuwa ni kama mkunga.

 

Dini potofu nuhimu ya nyakati zilizofuatia pia ilikuwa ni dini ya Al Uzza, ambayo ilikuwa ni ya kuiabudu sayari ya Zuhura yaani Venus. Jina hili kwa maana nyepesi limaanisha “Nguvu au Uweza”.

 

Manat huenda alihusiana na mungu wa Meni (Isaya 65:11). Manati alikuwa anaheshimiwa na kuabudiwa na kutukuzwa na kabila la Hudhaili karibu na Maka na hasa hasa miongoni mwa wakaazi wa Yathribi (Madina). Tukio la jina lake liko wazi kwamba dini hii potofu ilipatikana kwenye sehemu kubwa ya Saudi Arabia.

 

Kwa sababu hii Mtume Khasimu (aliyeitwa Muhammadi) alibidi ashambulie matendo ya kuiabudu miungu hii, Katika kulielezea tatizo alikiweka kipindi hiki cha kuabudu miungu katika nyakati za Nuhu na hivyo kuwahusianisha wao na imani zilizokuwa huko Babeli kama zinavyoonekana kwenye kitabu cha Mwanzo. Mingu iliyowekwa ilikuwa ni hii ifuatayo:

Yaghuthi (msaidizi) (Sura ya lxxi. 23)

(Robertson Smith anamwelezea mungu huyu na Ye’ushi mzee na babu wa Waedomu aliyetajwa kwenye Mwanzo 36 na mahali peinginepo pote kwenye Agano la Kale). Ni baadae tu kidogo tunaposikia kuhusu kinyago hiki cha mungu kikiwa kinahusiana kwenye makabila Yamen.

Ya’uq na Suwa (huenda linamaana ya mbakizaji) dini iliyokuwepo na kupata nguvu sana huko Yamen (Sura ya lxxi 20).

 

Hubal na Dhu Shara

Kuna miungu miwili ambayo inashabihiana sana na hoja au mjadala huu: Hubali na Dhu Shara.

 

Dhu Shara ama kwa usahihi zaidi ni Dhu ‘sh – Shara, ambayo maana yake ni “inayotokana na ash–Shara” ana uhusiano wa moja kwa moja na neno Ashera la kwenye Bibilia. Ni mungu ambaye alikuwa anaabudiwa na Wanabateani katika mji mkuu wao wa Petra. Alikuwa anaonyeshwa kwa tofali la pembe nne la jiwe jeusi lisilochongwa lenye urefu wa futi nne kwenda juu na upana wa futi mbili. Damu ya vitu vilivyotolewa sadaka ilimwagwa juu yake na mbele yake. Chini yake kulisimamishwa kiwiko cha dhahabu na maskani yote ilingarishwa na dhahabu na sadaka zilizopigiwa kura na za kuvutia (ERE makala ua 1, ukurasa wa 663). Rekodi au maandishi ya Kiyunani vinamuonyesha mungu huyu kuwa ni Dusares. Epiphaneus anasema kuwa sherehe au sikukuu ya Dusares ilisherehekewa huko Petra katika tarehe 25 Desemba ambayo iliyokuwa majira ya baridi wakati jua linapokuwa upande wa kaskazini kabisa mwa Ikweta. ERE inaelezea na kutambua jambo hili ni kama kuna muungano au uhusiano na ibada za jua (Ibid) (sawa na ilivyodadavuliwa kwenye jarida la Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235)).

 

Katikati ya nyumba ya dini potofu ya As shera (ambayo ni Miti au Kijimsitu) alitambuliwa na Dionysus. Muungano au uhusiano wa dini hii potofu na wala mbogamboga kwa kustarehe ni ule wa waabudu jua, ibada zilizofanyika kwa kuzuguka miduara. Miungu hii ilikuja omyeshwa kwa kuchongewa sanamu kwenye kabila la Dausi siyo mbali sana na Maka.

 

Jiwe jeusi la Dusaresi ama Dionysus mungu wa Wanabateani huko Petra lilichukuliwa na kupelekwa au kufanywa Ka’aba na kuganywa kwamba kitu cha kutumika kidini kama kigezo huko na hata Muhammadi alishindwa kuliondoa. Kidogo kidogo hatimaye likakuzwa habari na umuhimu wake na Hadithi za Kiislamu na kwenye ibada za mungu wa kipagani zikafanyika kuwa ni kitovu cha kutembelea mahujaji wa huko Maka.

 

Mungu wa pili ajaye kutoka Kaskazini alikuwa ni yule wa Hubali. “Amr b. Luhai anajulikana kuwa alileta sanamu zake hadi Maka kutoka Moabu (Ma’ab) na kuliweka katika Ka’aba. Mwanzoni lilikuwa katika muundo wa binadamu. Pamoja nail kulikuwa na mishale ya kufanyia ubashiri kwa njia za nguvu za mapepo.

 

Kabila la Kalbi la Wasyria wa Jangwani walilitumia jina la Habuli kwa kumwita mtu ama ukoo na pia walitumia Isafi na Na’ila, ambao walikuwa miungu mingine miwli waliojulikana sana huko Maka.

 

‘Amr. b Kuhai nachukuliwa kuwa ni mwakilishi wa Huza’a ambalo ndilo lilikuwa kabila waliokaa huko Maka kabla ya Makureshi (ERE ibid., ikuasa wa 664).

 

Hivyo basi tunaweza kusema au kuona kwamba kwamba Huza’a alianzisha dini za kipagani huko Maka ingawa Noldeke anachukulia kuwa haiwezekani kwamba ‘Amr. B Luhai anafaa kupongezwa na mwenendo huu lakini haelezi bayana sababu, akituacha tudhanie kwamba ilianza kabla yake.

 

Neno El lilitumika na Waarabu wa mwanzoni kama jina la kipekee la mungu akiwa ni kama Mungu kwa namna hiyohiyo lilivyotumika kwenye Bibilia. Neno hili likafanyika kuwa iyal kama muundo wa kiuwingi wa mtukufu.

 

Kwa namna hiyohiyo, neno la Bwana, Baali, kama Bwana likafanyika kuwa jina la mungu na inaonekana kuwa la kawaida hasa kwenye imani ya Kisemiti. Kivumishi ba’ila (kutatizwa) inamaanisha kwa hakika kumtwalia Mungu Ba’ali (huenda pia makusanyo au madeni au bili zetu).

 

Kwenye maelezo ya neno Hallah linalomaanisha Mungu kunaingia mtungo wa majina kadhaa ya kipekee ya Wanabateani na ya Waarabu mbalimbali wa Kaskazini wa nyakati za zamani na za mwanzoni sana na neno hili lilikuwa likitumika hata miongoni mwa wapagani waliokuwepo kipindi cha kabla ya kuanza kwa Uislamu na wapagani wa Kiarabu. Allah likafanyika kuwa limezoeleka kutumiwa kwenye matumizi ya maandiko kadha wa kadha yaliyokuwa ya muhimu ya wapagani wa Kiarabu. Kozani yenyewe inashuhudia kwa mtazamo wa kwamba zama za kabla ya Uislamu na wapani wa Kiarabu wenyewe walimchukulia Allah kama Kiumbe Mkuu. Walimrudia Allah wakati mambo na walipokuwa mashakani (Sura x, 23, xxix, 65, xxxi, 31). Viapo vya muhimu viliapwa kwa jina lake (S. vi, 109, xvi, 40, xxxv, 40). Anatambuliwa na wanadamu kama Muumbaji, na Mtoaji wa mvua (xxxi, 61ff). Makosa yao ni kwamba wanaabudu mingu mingine zaidi ya yeye; ijulikanayo kama miungu mitatu ya kike Al lati, Al Uzza na Manati ambao wanaaminiwa kuwa ni mabinti zake (xvi 59ff).

 

Miji ya Wawellhausan ina idadi kubwa ya vifungu ambazo kwamba Waarabu walioishi kabla ya Uislamu walimtaja Allah kuwa ni mungu mkuu. Kuna wengi sana hata kama tutawaondoa wengine nje kama mashaka bado wanabakia wengi wa kutufanya tusione shaka kuamini kwamba neno Allah ni neno lililokuwepo na limekuwa likitumika hata kipindi cha kabla ya harakati za Mahammadi.

 

Neno hilo ni jina la kawaida la Mungu wa Waarabu wote, wapagani na wengineo. Tena licha ya ushahidi huo kuthibitisha, Wellhausen bado anaendelea mbele akijaribu na kuanzisha muunganiko unaosema kuwa jina Allah linatokana na ibada ya Hubali wa Wamoabu. Hii inaonekana kuwa ni hombwe au mkanganyiko wa kidini usio na msingi kwenye ukweli wa kihistoria ambao mtu anaweza kuwa tayari sana kuuona. Kwa kweli ushahidi wenyewe unatofautiana sana. Ni kutoka kwa huyu Wallhausen ndiko hoja hizi za uwongo zinatokea (ERE ibid.).

 

Mkanganyiko kwenye unatokana na hatari iliyoko ya udogo au ufinyu wa maarifa wa baadhi ya misingi iliyopotoshwa na Wallhauseni.

 

Kwa kuwa tunarudiarudia kulikuta jina la mungu likifuatiwa na jina Alaha, au mungu, Wallhauseni ilipinga kwamba Warabu wa miaka ya baadaye yawezekana kuwa walichukua kiambishi cha jina Allah kuwa ni kama Mungu kwa idadi ya miungu tofauti na kwamba, kwa maana hiyo, kutoka kuwa kiunganisho peke yake hadi kuwa ni jina la mungu mkuu, ndipo yawezekana kuwa kidogokidogo likafanyika kuwa ni jina la Mungu Mkuu.

 

Hoja hii inaibua au kuzidisha hali ya kulipuuzia andiko la Biblia na mtindo wa kizamani wa ulimu ya lugha kuhusiana na majina ya Mungu kwa lugha za Kiebrania, Kikaldayo, Kiaramu na Kiarabu.

 

Chimbuko la Jina Allah

Wakati Ka’aba ilipokuwa inasafishwa nje ya Maka kulikuwa na vinyago au sanamu 167 hapo. Sanamu ya mfano wa samba miongoni mwa Waarabu ilihitajika sana, ingawaje iliwekwa kwa wingi kwenye miungu ya mitatu, na Siriusi. Mtindo mingi na taratibu wa ibada za kipagani vimeingizwa kwenye Uislamu kama tutakanyoona lakini haikuhusisha Jina la Mungu.

 

Mohammadi alitokea kwenye familia ambayo kwa sehemu kubwa ilikuwa ya Ukristo wa Kuamini Mungu Mmoja, yaani Uyunitarian na ilikuwa ni lengo lake kuonyesha mfumo ulio kwenye Biblia.

 

Alikusudia kuondoa miungu hii mitatu hadi wafikie kwwenye ibada ya Mungu mmoja wa kweli. Kwanza kabisa alinuia kukomesha ibada za kipagani kutoka kwenye makabila ya Kiarabu. Kisha alikabiliana na harakati za kiupinzani na kuubomoa mfumo wa Kiutatu, ambao ulikuwa umejiingiza ukitokea Mashariki kutoka Costantinople ukiwa kama kifaa cha imani ya Kirumi. Alikuwa pia na jukumu la kuwatoa na kuwaweka huru Waarabu kutokana na itikadi za kiastrokrasi na za kifalme za Kiyahudi, itikadi na fikra zilizokuwa zinatawala fikra za watu wa Mashariki ya Kati kwa wakati huo. Nyingi za ushawishi huu ulienea hadi kwa Wakhazaria na ndipo tulijioea uwongofu wa Wakhazaria, Waashikenazi wakiingia kwenye imani ya Kiyahudi katika karne iliyofuatia mnamo mwaka 740BK.

 

Muhammadi alianza kufundisha mnamo mwaka 610 BK na ilipofikia mwaka 632, Uislamu ulianzishwa rasmi baada ya kile kilichojulikana kama Hijra au kukimbia kutoka Maka mpaka Madina.

 

Ni ukweli kwamba misikiti ya Kiislamu ina alama ya mwezi mchanga inayoshikirishwa nayo lakini ni sawa tu na kama yafanyavyo Makanisa mengi ya Wakristo waamini Utatu pia. Hatahivyo, majina hayo hayana uhusiano wowote na jina la Allah. Ujenzi wa miskiti mingi unahusianishwa pia na kuweka kwa siri maziwa au matiti ya mungu mke upande wa juu ya mapaa na kitendo hicho ni cha kipagani moja kwa moja, lakini hii haihusiani sana na Mtume na kwenye Uislamu wa kweli.

 

Kama tunavyoona Al’ilah lilikuwa ni aina nyingine ya kuandika jina la Allah. Huyu hakuwa na uhusiano wowote kabisa na Mungu Mwezi na wala miungu mke aliyejulikana na kuabudiwa sana aitwaye Al ilat au Al Lat iwe kwa namna yoyote ile.

 

Lugha za Kiebrania na ya Kiarabu zinahusiana kwa njia hii. Kiebrania kilikuwa ni mwanzilishi wa mtindo wa Kiaramu cha magharibi, ambacho kiliongelewa baada ya zama za utumwa wa Babeli badala au mahali pa Kiebrania. Lugha ya Wasemiti ya Wakaldayo ikafanyika kuwa ni ya Waaramu wa mashariki na ndiko kilikotokea Kiarabu cha siku hizi.

 

Majina ya Mungu kwa Kiebrania yalikuwa:

Eloah (kwa namna ya umoja); na

Elohim (kwa wingi).

 

El ilikuwa ni kifupi cha uandishi na iliemaanisha uweza kama alionao mtu.

 

Majina ya Mungu kwa Kikaldayo yalikuwa:

Elohi (kwa umoja) (= Kiebrania. Eloah)

Elahhim (kwa wingi) (= Kiebrania, Elohim).

 

El ilikuwa na maana sawa. Kwa lugha zote mbili, yaani Kiebrania na Kikaldayo zinaonekana kwenye maandiko ya Biblia zikitumia mitindo hii. Kitabu cha Ezra kinaonyesha kwamba jina Eloah ni jina la cheo la Mungu wa Hekalu aliyeko Yerusalemu. Jina hili ni umoja na linakubali na kuthibitisha kutokuwa na aina yoyote ya uwingi. Linamtaja na kumrejelea Mungu mmoja na wa ukweli peke yake.

 

Kwenye Kiaramu cha mashariki, Elahh mmoja au wa pekee ailikuwa Allah kwa Kiarabu kwa namna hii. Elahh alitajwa kama Al Elahh au Mungu kwa umoja kama inavyoonekana kwenye maandiko ya Biblia na kwenye Kikaldayo. Kwa hiyo alikuja kuwa Al’ilah kwa muundo wa Kiarabu ambacho ndicho Kiaramu cha mashariki, herufi mbili za hh zinaelezwa kuwa ni kama kihamasisho au kiambishi cha herufi za mwishoni h cha Allah. Kwa hiyo, mtindo wa Kiarabu cha zamani uliokuwa Al’ilah ulikuwa unabadilisha sauti ya h mbili. Uislamu chini ya Muhammadi uliendeleza jina Allah kwa sababu lilikuwa la umoja na linakubaliana kutokuwa na uwingi.

 

Hakuna tashishwi kwamba jina Eloah wa Biblia na Allah wa Kiarabu lilitujia kutoka kwrmur lugha ya Kisemiti kupitia Kiebrania cha Kale na Kikaldayo cha Kale kwa kipekee na inamaanisha kitu hichohicho kimoja.

 

Jina Yahovah ni la kisheo au mamlaka linalomtaja au kumhusu Eloah kama muundo wa nafsi ya tatu ya kiambishi inayomaanisha “Anafanya Ikawa”. Mtazamo huu unathibitishwa na maandiko ya bangokitita kwenye maandiko ya Kutoka 3:14 katika tafsiri ya Annotated Oxford RSV. Jina lililoelezewa kwenye andiko la Kutoka 3:14 inamaanisha “Mimi Niko Ambaye Niko (‘eyeh ‘asher ‘eyeh sawa na Bulhinger fn kwenye tafsiri ya Companio Bible pia). Inaonyesha au kuelezea kitendo cha uumbaji kwa kujieneza mwenyewe na Mungu Mmoja, Wapekee na wa Kweli sawasawa na mapenzi yake na mipango yake. Kwa jinsi hiyo watu wote watafanyika kuwa wana wa Mungu.

 

Kwa hiyo ni jina linalotumika au kumhusu msemaji wa Mungu Mmoja wa Pekee wa Kweli ambaye anajulikana kama Yahovih (SHD 3069) au Yahovah ya Majeshi. Yahovah (SHD 3068) inatumika kuwataja miungu wadogowadogo au wasaidizi na wakati mwingine ni miungu wengi kwa wakati huohuo mmoja. Kwa maneno mengine ni kwamba wote hao wanatenda kazi kwa niaba ya Mungu mmoja wa Kweli, Eloah kama elohim. Kwa hiyo watu wote watafanyika kuwa miungu wa kiroho au elohim kama wana wa Mungu (soma jarida la Wateule Kama Elohim (Na. 1)).

 

Jina Yahovah limetumika kwa takriban viumbe mwanne, watatu wao wakiwa ni malaika au wajumbe wa Mungu wa Mbinguni kwa wakati huo huo kama tunavyoona kwa mfano kwa Ibrahimu na Lutu, na kuangamizwa kwa Sodoma na Gomora. Mambo haya yote yameelezewa kwa kina kwenye majarida ya Malaika wa YHVH (Na. 24); Majina ya Mungu (Na. 116); Uwepo wa Yesu Kristo Kwenye Kipindi cha Kabla ya Kuzaliwa Kwake Rasmi Duniani (Na. 243); na Ibrahimu na Sodoma (Na. 91).

 

Hii ni kutokana na hali ya kutojua chimbuko la majina kwenye lugha zake na shauku ya kudanganya kwa kujihesabia haki kamili kwenye imani ya Kikristo ambako tunaona makosa na udanyanyifu ukiibuka. Kutofahamu kwa Waislamu kumetuama kwenye mapokeo ya wanadamu ambayo yanaongoza hali ya chuki kwa kiasi kikubwa sana.

 

Kwa nini watu wanalishambulia jina Allah? Ni nini maana ya jina hili?

 

Tatizo halisi linatuama kutoka kwenye teolojia potofu na ya uwongo iliyouingia Ukristo na kutafuta meelezo yake leo yakifundishwa kwenye Makanisa ya Mungu.

 

Imani ya Utatu au Utrinitarian ilitokana na imani ya Kibinitariani na ni mwendelezo wake tu, ambayo ilijikuta ikiingizwa rasmi kwenye Halmashauri Kuu ya Mtaguso wa Nicaea mwaka 325 BK. Utrinitarian uliendelezwa na Wakapadokiani, Gregory wa Nysaa, Gregory wa Nizianzus na Basili. Teolojia hii iliingizwa mwaka 381 BK na iliuzinga Ukristo kiteolojia. Augustine wa Hippo naye alianzisha teolojia potofu akiianikiza kwa kutumia maandishi yake.

 

Makanisa ya Mungu yamekuwa hata hayana udhuru kwa upotofu huu. Waliiendeleza na kuikuza, chini ya Herbet Armstrong katika miaka ya karne ya ishirini, wakafundisha imani ya uditheism ambayo ilikuwa chanzo cha teolojia potofu iliyofundisha kuwepo wa miungu wawili wenye hadhi na mamlaka sawa. Waalimu hawa wa uwongo wanakabiliwa na utata wa maneno ya Biblia kuhusu jina Eloah kuwa ni jina la Mungu katika umoja na ambalo linaweza tumika tu kwa Mungu Mmoja wa Pekee na wa Kweli aliyemtuma Yesu Kristo (Yohana 17:3). Kwa hiyo ndipo wanakataa na kushambulia matumizi ya jina la Eloah kuwa ni kama Mungu wa Pekee wa Kweli. Wanafanya hivyo kwa kuhanganya majina ya Eloah na Allah, ambapo ni muunganiko sahihi, lakini wanadai kuwa linahusiana na za Mungu mwezi katika Uislamu kwa sababu ya mwingilio wa kipagani kwenye misikiti kulikofanywa na dini za siri. Ni kweli kabisa kwamba Uislamu, kama ulivyo Ukristo uliokuwepo kabla yake, umepotoka kwa kupaganishwa kwake lakini hiyo halina uhusiano wowote na matumizi ya jina Allah kwenye Ku’rani.

 

Makanisa mengine kama Kanisa la Mungu (la Siku ya Saba) wakati lilipoingiliwa na imani ya Utatu ama Utrinitarian huko Marekani lilianza kwa kukubaliana na Ubinitarian kama njia rahisi kwao na bila shaka litaishia kwenye Utrinitarian. Kanisa la Seventh Day Baptists bado wangali waamini Mungu mmoja yaani Wayunitarian ni kama walivyokuwa hivyo wakati wote kimsimamo kwenye Makao yao Makuu ya Kimataifa, lakini wamejikuta wakiingia kwenye Utrinitarian kwenye Halmashauri yao ya Kanisa la Marekani kuanzia katikati ya miaka ya sabini. Kiteolojia ni wadhaifu sana. Makanisa ya Mungu pamoja na kanisa la Seventh Day Baptists mwanzoni walikuwa waamini Mungu Mmoja au Wayunitarian kwa madhehebu mengine yote likiwemo kanisa la Waadventista Wasabato au Seventh Day Adventists. Armstrong aliwekwa wakfu na kukubaliwa kuwa mtumishi kwenye kanisa lijulikanalo kama Church of God (Seventh Day) wakati lilipokuwa bado ni la mrengo wa kuamini Mungu Mmoja au Uyunitarian mwishoni mwa miaka ya 1970.

 

Watu hawahawa wanakabiliwa sasa na ukweli wa kwamba wameanzisha mafundisho ya uwongo na kuyapotosha Makanisa ya Mungu kwa upotovu.

 

Ilikuwa kwa sababu hii katika karne za mwanzoni kwa kufuatia teolojia potofu ta Kitrinitarian kwenye Ukristo ndipo Uislamu ukasisitiza kumrejelea Mungu Mmoja, wa Pekee wa Kweli kuwa ni Allah, kuliko mungu wa uwingi ellahhim, kwa kuwa jina lenyewe linakubaliana kutokuwa na uwingi wa aina yoyote ile.

 

Badala yake linakubaliana na kuwaonyesha kwamba wamepotoka, waalimuwa wa Kibinitarian, Kiditheist na Kitrinitarian wa Makanisa kadhaa mbalimbali ya Mungu walianzisha malumbano wakiwekea msingi wake kwenye uwongo na kuwasingizia mambo ya uwongo wale waliopingana nao na kutoamini hoja na mafundisho yao. Matendo haya ni kinyume kabisa na Biblia na hata sasa kwenye Sheria za Marekani pamoja na za mataifa mengine pia.

 

Upotovu kadhaa wa teolojia hii umeainishwa kwa kina kwenye jarida lihusulo Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Uislamu (Na. 55).

.

Fikira ya kwamba Alla siyo Mungu wa kwenye Biblia, ambaye jina lake kwa kweli ni Yahweh kama inavyosemekana, ni fikira ambazo zimetokana na teolojia ya Majina Matakatifu zinazofundishwa au zilizotokea nchini Marekani na ni ya uwongo. Imeshindwa kuyajua majina ya Mungu yalivyo kwenye Biblia na nafasi au mahali pa Eloah – Elohim na tofauti yao hapa.

 

Kwenye makala au tahakiki moja tunakutana na fafanuzi au maoni ya kama vile

“Kwa watu wa Maandiko” ama “wa kitabu” Waislamu wameambiwa waseme. “Tuna imani kwa kile ambacho kimefunuliwa kwetu na kwa kile ambacho kimefunuliwa kwenu. Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja, na kwenu ninyi tumetulia” Kurani 29:46.

 Je Waislamu wavinamini vitabu vyote viwili, yaani Korani (Kurani) na Biblia?

Tunaona.

 

Sasa malumbano na hoja hii ni mwelekeo wa muhimu. Inaonyesha umuhimu wa kuiuliza Korani na kuona kuna tofauti ipi kati ya dini hizi mbili.

 

Kurani kwa hakika inamtaka Muislamu wa kweli kuvifuata vitabu vyote viwili, yaani Kurani na Biblia. Hii ina maana na nguvu sana na ingeweza kuwa ni uthibitisho wa kwa dini zingeweza kusuluhishwa na kwenda sambamba. Mfano wa dhana inayoyaacha Makanisa ya Mungu kwa wakati huu ni hii ifuatayo:

 

Asili ya Allah ni nini – Allah - wa Waislamu? Je, yeye ni sawa tu na Yahweh wa kwenye Maandiko Matakatifu?

Kama ilivyoripotiwa kwenye taarifa ya jarida lijulikanalo kama Battle Cry la Januari na Fenruari 2000, mlinganisho kati ya Allah na Yahweh, wakiwekea msingi wa kuionyesha Kurani na Biblia kwa ujumla, ni mafunzo ya kupinga tu.

Kinachojulikana na kukubalika: Allah ni mkuu, hana mfano wala mipaka, aliyetukuka sana na kwamba hakuma mtu anayeweza binafsi yake kumjua Allah. Yahweh, kwa upande mwingine ni kwamba alimtuma Mwana wake Yesu Kristo duniani ili kutuwezesha tumjue Mungu kila mtu nafsini mwake, Yohana 17:3 (kwa mujibu wa jarida la R Nickels la Uislamu na Wewe, Somo Na. 185).

 

Bibilia inasema wazi kwamba hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu kwamwe. Alichagua kujifunua mwenyewe kwa kupitia watumishi wake manabii na akamtuma Yesu Kristo. Mwandishi anaonekana kuwa hajui lolote kabisa kuhusu jina Eloah kwa jinsi linavyotumika kwenye Biblia. Pia anaonekana kutolijua kabisa neno Yahovah au Yaweh kwa vile anavyodai kuwa limetumika kuwaelezea au kuwahusu Malaika wa Agano la Kale, ambao mmoja wao, Mwamba wa kiroho ambaye alikuwa pamoja na wana wa Israeli Jangwani (1Wakorintho 10:4) ulikuwa ni Yesu Kristo.

 

Ezra anaonyesha, kwenye matengenezo na marejesho makuu kwamba Nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu ilikuwa ni Nyumba ya Eloah (Ezra 4:24) na siyo Nyumba ya ‘Yaweh.’ Ezra anamtambulisha Eloah kuwa ni Eloah wa Israeli. (Ezra 5:1). Manabii walikuwa ni manabii wa Eloah (Ezra 5:2). Yeye ni Eloah wa Wayahudi (Ezra 5:5). Yeye ni Eloah mkuu ambaye kwaye Nyumba ilijengwa (Ezra 5:8). Yeye ndiye Eloah wa Mbinguni na Duniani (Ezra 5:11). Alikuwa ni Eloah huyu ambaye mababu zetu walimkasirisha kwa hasira na akawapeleka utumwani (Ezra 5:12) Koreshi alitoa amri kwamba nyumba ya Eloah ikajengwe, na vyombo vya dhahabu na fedha viingizwe ndani yake (Ezra 5:13-17; 6:5).

 

Nyumba ya Eloah ililindwa na iliamriwa ijengwe na watawala wa dola kwa kuwa Eloah alikuwa amemchagua Koreshi aanzishe mchakato huu wa ujenzi. Dario II aliumalizia na Ahauswero II aliamuru mng’aro wake. Ezra na Nehemia waliurejesha upya utaratibu wa huduma za Hekalu na Ezra alifariki mnamo mwaka 323KK. Hakukuwa na mashaka kwenye mawazo ya mtu yeyote kwamba lilikuwa ni Hekalu la Eloah, Mungu wa Mbingu na Dunia. Sio mara moja tu jina Yahweh limetajwa kwa jambo hili. Kwa kweli, neno Yahweh linatokana na kosa la kimatamshi ya jina lenye kwenye kila tukio.

 

Kutoka hapo juu tunaona kwamba majina ya Eloah na Allah kama yanatokana na sehemu mbili tofauti zenye muundo na mfumo mmoja wa lugha Eloah na Allah ni Mungu huyuhuyu mmoja ambayo kutokana na huyo ndipo linatoa jina Allah. Kwa kupewa ukweli huu wa muhimu ndipo kwa hiyo tunaweza kwenda kwenye msimamo wa kawaida na kujenga uelewa uliosawa kwa pande mbili zote.

 

Allah ni muundo wa kijina wa Kirabu wa Mungu Mmoja wa Kweli, Eloah anayejieneza mwenyewe kufanyika kuwa elohim kwa kupitia watu aliowaita kwenye mfumo wake.

 

Kurani inashikilia kusema kwamba Wakristo wapo karibu sana na wao. Hawakubaliani na wala hawatakubaliana na mapokeo yoyote yanayojumuisha imani ya Utatu na Ubinitarian. Kimsingi wao wamekaza mtazamo wao kwa kutomkubali Mungu mwenye mjumuiko na viumbe wengine na mdahalo kama huu hauleti maana wala kutupeleka kwenye malengo yoyote zaidi ya kusababisha mafarakano na kuzidisha chuki miongoni mwetu.

q