Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[061]
Tasira
(Toleo La 2 19940923-19980523) Audio
Harida hili linaelezea
aina ya hasira zilizotajwa kwenye Biblia na namna ya jinsi tunavyoweza kutenda
na jinsi tunavyoweza kutumia hasira kwenye maisha yetu ya Kikristo.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati
Miliki © 1994, revised 1998
Storm Cox)
(Tr. 2015)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu
bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na
tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa
mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza
kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka
maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Tasira
Hasira ni Nini?
Neno lenye maana ya hasira kwenye Biblia ni
harah lenye maana ya "kupatwa na hasira au kukasirika". Kwa hiyo ni shina la neno au vebu. Neno
hili linaonekana mara 92 kwenye Biblia. Kamusi ya. Vines Expository Dictionary
inasema;
Kimsingi, neno hili
linataja kuhusu kuwaka hasira kama ilivyo kwenye Yona 4:1. Kwa maana ya
kiusababu, neno hili harah linamaana
ya "kujikuta na muwako kwa kazi" au "kwa kumaanisha bidii ya
kazi"(Nehemia 3:20).
Hasira ni neno la
muwako, hata hivyo, maana ya neno linatokana na bidii ya kazi, ambayo ni
hamasa. Hasira inatumotisha, na aina mbili za hamasa zinazotufanya kufanya
zaidi ya wengine wowote na kuogopa na kuona hasira. Zitatuhamasisha kutenda.
Hofu inaweza kutudhoofisha sisi, il hasira inaweza kutotoa kwenye hofu hii.
Kama tukiiangalia hasira kwa uzito mzuri, wakati kunapokuwa na wakati wa kuwa
na hasira, kisha tunaweza kuona kuwa inaweza kutupa uhalisia wa kazi.
Nauni ya neno
hasira ni haron au kuwaka hasira. Neno hili limejitokeza mara 41 kwenye Biblia na linajiri
kila kipindi. Neno
linahusiana tu na hasira ya mbingu au hasira ya Mungu, ambayo inasababisha
maswali kadhaa. Kama ni vibaya kuwa na hasira, kisha ndipo Kristo na Mungu
watakuwa walitenda dhambi walipofanya hasira? Hapana! Kwa kweli, kuna aina mbili
za, na moja tunayohitaji kuijua na kuitumia, ni ile hasira sahihi, na yatupasa
kuifukuza hasira mbaya kutoka mioyoni mwetu.
Mwanzo 4:1-3 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata
mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. 2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili.
Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. 3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya
ardhi, sadaka kwa Bwana.
Tunaiona hadithi ya Kaini na Abeli. Haya ni msisimko wa
kwanza wa mawazoni kimatendo. Tunaona hapa uwepo wa halisi wa kwanza wa kiburi
kwa mwanadamu. Kaini hakupenda kukataliwa, na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Nia yake
na roho yake havikuwa sahihi, na Mungu aliikaraa sadaka yake. Kunafanya maswali
mengi sana kama vile ni kwa nini hasira na roho mbaya ya Kaini iliachwa
kuendelea kama ilivyokuwa, na ni nguvu gani zilizokuwa zinamwenyesha na
maishani mwake wakati ule. Kama utayafuatilia matendo ya Kaini baada ya kumuua
Abeli, yanaleta maswali mengi sana kama tujiulizavyo kwanini alifanya hivyo?
Kile alichokuwa anakifanya ndicho kilichomfanya kuendeleza nia aliyokwisha
kuwanayo?
Mwanzo 4:6-7 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una
ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 Kama
ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea
mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Mungu namuonya
Kaini. Anaiona hasira ndani yake na anamuonya kwa kumwambia kwamba,
"ishinde, vinginevyo nitakuadhibu". Inakutamani, ila unapaswa
kuishinda. Kaini anaanza kutenda dhambi na anafikiri kwa mintaarafu ya
dhambi, na Mungu anamuonya kwa kumtaka aishinde.
Mwanzo 4:8 Kaini
akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini
akamwinukia Habili nduguye,akamwua.
Tunaona maana au
sababu za kuendelea kuwa na moyo wenye hasira hadi kuua. Hivyo ndivyo ilivyo
hasira. Ni mauaji, na wakati wote tunapowaonea hasira wanadamu wenzetu,
tunatenda dhambi ya mauaji mioyoni mwetu. Hasira ni kichocheo au chanzo cha
mauaji, na kwa hiyo wakati wote tunapopatwa na hasira, yatupasa tujue na kufikiri
kwamba matokeo ya kuongezeka hamasa hii ni kuua.
Mwanzo 4:9 Bwana
akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi
wa ndugu yangu?
Anamdanganya ili
kujificha, na ndipo tunaona kwamba mojawapo ya tendo lililoletwa na hasira
kwake ni uvunjifu wa amri mbili kwa kipindi kifupi tu.
Mwanzo 4:10-14: Akasema,
Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi,
iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake;
utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani. 13 Kaini
akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa
ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na
kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua
Kuna dhana fulani
za namna kadhaa kwenye kwenye vifungu hivi zinazofanya maswali tunayohitaji
kuyatilia maanani au kuyafikiri. Abeli amekufasasa, na sasa ni Adamu, Hawa na
Kaini wamebakia hai, ila Kanini akiwa anawahofia watu waliokuwa wanataka
kumuua. Kwa hiyo, tunashughulika na watu wengine zaidi ya hawa watatu tuwajuao
kuwa walikuwepo duniani. Ni kwanini walitaka kumuua Kaini? Ni kwanini
ilimlazimu Mungu amuweke Kaini alama ya kumnusuru, ili kwamba watu
wakimuonanayo wasimuue? Ni wazi kwamba alikuwa bado anashughulika na watu
walewale wenye tabia ya hasira, na mtazamo wangu ni kwamba watu hao walikuwa
wanawasiliana na Kaini kabla ya kifo cha Abeli (kama lisemavyo jarida la Wanefili (Na. 154.
Ni nani
alimfundisha Kaini jinsi ya kuua? Ni nani aliyemfundisha kukasirika?
Hadithi ya Kaini,
Abeli na Adamu ni hadithi na namna ya kibinadamu inayofananishwa na Malaika waasi.
Wana wawili wa Mungu wamewakilishwa kwa wana wawili wa Adamu. Abeli
anamwakilisha Kristo na Kaini anamwakilisha Shetani – uasi wenye chanzo cha
kiburi hichohicho na ukataaji huohuo wa kumkataa Roho wa Mungu kulikompelekea
Shetani kufanya kitendo cha uasi. Ndipo alitupwa duniani. Tunaona kwamba hasira
ilioonekana ulikuwa ni mchakatu tu wa kuiondolea mbalia sheria au Torati ya
Mungu, na roho ya uelewa ambayo Mungu ametupa. Wa kwanza kufanya jivyo alikuwa
ni Shetani kwa uasi wake. Mungu alituonyesha wazi sana kuwa dhana inaweza
kutolewa kwa namna yoyote ya maisha yetu, na yatupasa kuonyesha chanzo cha
michakato ya mawazo haya yaliyo kinyume au mabaya yanapotujia mioyoni mwetu.
Kaini alikuwa mtu mwenye wivu, aliyejipendelea mwenyewe na mwenye kiburi,
na hakuwa mtu wa kukubali kukosolewa na Mungu. Kiburi ni chanzo kikubwa sana
cha kumsababishia mtu kupatwa hasira. Mtu mwenye kiburi anapata hasira kwa mtu
yeyote, kwa kuwa anahoja ya juu sana na kujiona bora zaidi, na kama utaiathiri
hiyo hoja au hali yake, basi atakasirika sana. Hapendi kukosolewa.
Kutoka 10:1-11 Bwana
akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao; kwa kuwa mimi nimeufanya moyo wake
mzito, nipate kuzionyesha ishara zangu hizi kati yao; 2 nawe
upate kusema masikioni mwa mwanao, na masikioni mwa mjukuu wako, ni mambo gani
niliyotenda juu ya Misri, na ishara zangu nilizozifanya kati yao; ili mpate
kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana. 3 Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, Bwana, Mungu wa
Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape
watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie. 4 Au,
kwamba wakataa kuwapa hao watu wangu ruhusa waende zao, tazama, kesho nitaleta
nzige waingie ndani ya mipaka yako; 5 nao wataufunika
uso wa nchi, mtu asipate kuona hiyo nchi; nao watakula mabaki ya hayo
yaliyopona yaliyowasalia baada ya ile mvua ya mawe, watakula kila mti umeao kwa
ajili yenu mashambani; 6 na nyumba zako, na nyumba za
watumishi wako, na nyumba za Wamisri wote zitajawa na nzige; mfano wake baba
zako wala baba za baba zako hawakuona, tangu siku walipoanza kuwapo juu ya nchi
hata hivi leo. Basi akageuka na kutoka kwa Farao. 7 Ndipo
watumishi wa Farao wakamwambia, Mtu huyu atakuwa tanzi kwetu sisi hata lini?
Wape hawa watu ruhusa waende zao, wamtumikie Bwana, Mungu wao; hujatambua bado
ya kuwa Misri imekwisha haribika? 8 Musa na Haruni
wakaletwa tena kwa Farao; naye akawaambia, Nendeni, mkamtumikie Bwana, Mungu
wenu; lakini ni kina nani watakaokwenda? 9 Musa
akamjibu, Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu,
tutakwenda na kondoo zetu na ng'ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia Bwana
sikukuu. 10 Lakini akawaambia, Ehe, Bwana na awe
pamoja nanyi, kama nitakavyowapa ruhusa kwenda zenu pamoja na watoto wenu;
angalieni, kwa kuwa pana uovu huko mbele yenu. 11 Sivyo;
endeni ninyi mlio watu wazima, mkamtumikie Bwana; kwa kuwa ndilo jambo mtakalo.
Nao walifukuzwa usoni pa Farao.
Farao kwa kuwa alikuwa mtu mwenye kiburi alimkasirikia Musa.
Kutoka 10:10-16 Lakini akawaambia, Ehe, Bwana na awe pamoja
nanyi, kama nitakavyowapa ruhusa kwenda zenu pamoja na watoto wenu; angalieni,
kwa kuwa pana uovu huko mbele yenu. 11 Sivyo; endeni
ninyi mlio watu wazima, mkamtumikie Bwana; kwa kuwa ndilo jambo mtakalo. Nao
walifukuzwa usoni pa Farao. 12 Bwana akamwambia Musa,
Nyosha mkono wako juu ya nchi ya Misri kwa hao nzige, ili wakwee juu ya nchi ya
Misri, waile mimea yote ya nchi, yaani, vyote vilivyosazwa na ile mvua ya mawe.
13 Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya
Misri, na Bwana akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na
usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige. 14 Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua
ndani ya mipaka yote ya Misri, walikuwa wabaya mno; hawajakuwapo nzige kama hao
majira yo yote, wala baada yao hawatakuwa wengine jinsi hiyo. 15 Kwa kuwa waliufunika uso wote wa nchi, hata nchi iliingia
giza; wakala mimea yote ya nchi, na matunda yote ya miti yaliyosazwa na ile
mvua ya mawe; hapakusalia hata jani moja, mti wala mmea wa mashamba, katika
nchi yote ya Misri. 16 Ndipo Farao akawaita Musa na
Haruni haraka; akasema, Nimemfanyia dhambi Bwana, Mungu wenu na ninyi pia.
Tunaona toba ya muda mfupi, lakini somo lilikuwa halijasomwa bado.
Kutoka 10:17-26 Basi sasa, nawasihi,
nisameheni dhambi yangu mara hii moja tu, mkamwombe Bwana, Mungu wenu,
aniondolee kifo hiki tu. 18 Akatoka kwa Farao, na
kumwomba Bwana. 19 Bwana akaugeuza upepo wa magharibi
wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka katika Bahari ya
Shamu; hakusalia hata nzige mmoja ndani ya mipaka yote ya Misri. 20 Lakini Bwana akaufanya ule moyo wa Farao uwe mgumu,
asiwape wana wa Israeli ruhusa waende zao. 21 Bwana
akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, kuwe giza juu ya nchi ya
Misri, watu wapapase-papase gizani. 22 Basi Musa
akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; kukawa na giza nene katika nchi yote
ya Misri muda wa siku tatu; 23 hawakupata kuonana mtu
na mwenziwe, wala hakuondoka mtu mahali alipokuwa muda wa siku tatu; lakini
wana wa Israeli wote walikuwa na mwanga makaoni mwao. 24 Farao
akamwita Musa, na kumwambia, Haya, nendeni, mkamtumikie Bwana; kondoo zenu na
ng'ombe zenu tu na waachwe; watoto wenu nao na waende pamoja nanyi. 25 Musa akasema, Ni lazima utupe mikononi mwetu na wanyama
wa dhabihu na wa sadaka za kuteketezwa, ili tupate kumchinjia Bwana Mungu wetu
dhabihu. 26 Makundi yetu pia watakwenda pamoja nasi;
hautasalia nyuma hata ukwato mmoja; kwa maana inampasa kutwaa katika hao tupate
kumtumikia Bwana, Mungu wetu; nasi hatujui, hata tutakapofika huko, ni kitu
gani ambacho kwa hicho inatupasa kumtumikia Bwana.
Israeli walikuwa ni wateule wa Mungu, na kwa hiyo iliwapasa waende na Musa.
Hakukuwa na mjadala, na jambo hili lilikuwa ni pigo kubwa kwenye kiburi cha
Farao. Uamuzi wake wote ulikuwa ni aende na kuwashambulia na kuwaua Israeli
wote kwenye Bahari ya Shamu. Kwa hiyo, tunaona tuyafanyapo mapenzi ya Mungu,
tunawashinda wale walio kinyume chetu. Tunafanya kitu hichohicho kwa makundi
yote yaliyo na nguvu au uweza kwenye ulimwengu wetu huu, kwenye mifumo ya
kisiasa na kwenye mifumo yetu ya kanisa. Tunawakasirisha watu hao, na Kristo
anaposema Heri wenye kuudhiwa kwa
ajili ya haki, ni kwa kuwa tunaushambulia umfumo mzima wa muundo wa
dini za ulimwengu kwa kusimamia kile tunachokifanya.
Hesabu 22:21-30 Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na wakuu wa Moabu. 22 Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa Bwana akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye. 23 Na yule punda akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, na upanga wake mkononi mwake amekwisha kuufuta; punda akageuka upande ili kuiacha njia, akaingia shambani. Balaamu akampiga punda ili kumrejeza njiani. 24 Kisha malaika wa Bwana akasimama mahali penye bonde, katikati ya mashamba ya mizabibu, tena penye kitalu upande huu na kitalu upande huu. 25 Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajisonga ukutani, akamseta Balaamu mguu wake, basi akampiga mara ya pili. 26 Malaika wa Bwana akaendelea mbele akasimama mahali pembamba sana, hapakuwa na nafasi ya kugeukia mkono wa kuume, wala mkono wa kushoto. 27 Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake. 28 Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi? 29 Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi. 30 Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La!
Tunaiona
tena hasira wakati kiburi chake kinapoumizwa. Punda alimdhihaki na
aliachwa amjaribu. Alijaribiwa kwa namna hiyo, na hatua yake ya kwanza ilikuwa
ni kukasirika. Hatua ya pili ilikuwa ni kuua. Tunaona mchakato, na tabia
ya uharibifu ya hasira.
Mathayo 2:13-15 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. 14 Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri; 15 akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwanangu.
Wakati Herode alipogundua kuwa
alikuwa amedanganywa au kukwepwa na Mamajusi, alikasirika. Alitoa amri ya
kuwaua watoto wote wakume wa Bethlehemu na maeneo ya karibu nao waliokuwa na
umri wa miaka miwili na chini ya hapo, sawasawa na kipindi alichojifunza kutoka
kwa wale Mamajusi, kisha tunaona pia hapa kwamba kiburi chake tena
kilishambuliwa, na uamuzi wake wa kwanza ulitokana na hasira, ulikuwa ni kuua.
Alifikia uamuzi wa kuua kila mtoto aliye chini ya umri wa miaka miwili.
Unaposhambulia kiburi cha watu, watakujia kwa hasira na wanaweza kukuua kabisa.
Hasira ni kitu kinachoenda sambamba na mauaji, nii uuaji; wa wazi na wa rahisi
sana. Tumeona hayo kwa mifano mitatu sasa.
Kiburi
kinachochanganyika na mamlaka, ni tatizo kubwa na hatari sana.
Danieli 3:10-15
Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu atakapoisikia sauti ya panda,
na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma,
ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu; 11 na
kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa katika tanuru ya moto uwakao. 12 Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya
wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee
mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu
ya dhahabu uliyoisimamisha. 13 Basi Nebukadreza akatoa
amri kwa hasira na ghadhabu, waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego.
Basi wakawaleta watu hao mbele ya mfalme. 14 Nebukadreza
akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa
makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu
niliyoisimamisha? 15 Basi sasa, kama mkiwa tayari
wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na
santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu
niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika
tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono
yangu?
Tuna wazee wa imani zetu waliounda mifumo iliyo tofauti na kinyume kabisa
na utaratibu wa Mungu, na watu watatu wa Mungu walisimama kupinga, na walikataa
kuipigia magoti miungu hii migeni. Tunamuona mtu mwenye mamlaka makubwa, mtu
mwenye kiburi sana, ambaye alikuwa na mamlaka alishambuliwa, lakini si katika
mwili au kwa maneno ua kutamkwa, bali ni kwa kuweka msimamo tu wa kukataa
kukubaliana nayo. Utaratibu huu wote ulitiliwa mashaka, na kwa kuuliza kwake
hivyo ndipo swali hilo lilipelekwa kwenye baraza la utawala wa Nebukadneza.
Ndipo hasira pamoja na tishio la kufa vikatangazwa.
Hii ni mifano ya kibiblia ya hasira ya mwanadamu. Kuna hasira leo, na
tutaioja mfano wake kwenye michezo. Matendo ya michezoni ni mfano wa mambo
haya. Tunashuhudia mapigano yakitokea kwenye michezo ya mpira wa miguu, mpira
wa kikapu, michezo wa mpira wa kikapu huko Marekani, nchi inayochukuliwa kama
kioo cha mchezu huu, na watu wanapifkia hatua ya kupigana. Watu hawa
wanafanyika kuwa kama mfano wa kuigwa na watoto wetu. Mtu mwenye hasira zaidi,
mkaidi na mgomvi zaidi utamuona kwenye viwanja vya mpira, ndivyo unavyopata
heshima zaidi. Ndivyo alvyo Shetani hapa duniani anageuza mambo. Mashujaa wetu
ni Arnold Swartzeneggers wa ulimwengu, wenye maneno na hasira kali ya kuifanya
iwe ni kitu kilicho kizuri sana, chenye kusisimua na kikubwa. Inatutawala.
Inatutawala sisi sote, na inatoka kwenye matangazo yetu, mitindo yetu na
mapambo yaliyo kwenye jamii zetu, ambayo kwamba magenge ya kiuni ya mitaani na
vijana wetu, wateja wote wa vitu vyote vinavyoanza kujitokeza na kuunda nguvu
kubwa kwenye mitaa ya ulimwengu wetu wa leo.
M6ara tu baada ya mwanasoka mashuhuri wa Kiaustralia alipotiwa mbaroni kwa
kuuza silaha za kijeshi. Mtu huyu alikuwa ni mwenye kiwango cha juu sana cha
weledi wa kucheza soka, na wa6toto 6waliokuwa wanakua kwenye viunga vya
magharibi mwa mji wa Sydney walimuona mtu huyu ambaye kimsingi alitangazwa kuwa
amekamatwa, lakini ilikuwa ni vizuri sana kutumia silaha za bunduki za kijeshi,
na alikuwa anawauzia watoto bunduki za rashasha kwenye mitaa ya mji wa Sydney. Sielewi
ni kwa namna gani Mungu anakwenda kuhukumu jambo hili, bali watu 6hawa walikuwa
wamesifiwa sana, na ukiukaji wao wa sheria na fujo walizozifanya vilitangazwa
sana kwenye vituo vya runinga. Watu hawa hawakuhojiwa kabisa na wala kuulizwa
maswali, na kila kiongozi hakuwataka watu hawa wajihoji na kujiulizwa kwa
walichokifanya.
Aina nyingine ya hasira ambayo tumeiona, ni shambulio la binafsi. Tuliiona
hii wakati tulipoamua kuwa hatutakwenda sambamba wala kuchukuliana na
mabadiliko ya k6imafundisho kwenye makanisa ambayo sisi tulikuwa waumini wake.
Tuliweka msimamo na sote tulikumbana na shutuma za kila mmoja wetu mmoja mmoja,
kwa kufanya kwetu hivyo. Ni haaira ambayo waliihisi wengine, kwa kuwa kama tuko
sahihi, basi wao wanakosea. Inawafanya wawake hasira, kwa kuwa walipaswa
kubadili jinsi wanavyofikiri na jinsi wanavyofanya.
Kama uko kwenye mazingira ya shule, na unakwenda kufanya kitukilicho
tofauti na kundi linguine lililobakia, utapata mwitikio kwa kufanya kwako
hivyo. Kile unachokifanya ni kupunguza nguvu zao. Watakushambulia, pasi kujali
kile unachokisema, au unachikiwazia. Andiko la Luka 4 ni mfano mzuri:
Luka 4:14-30 Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda
Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando. 15 Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao,
akitukuzwa na watu wote. 16 Akaenda Nazareti,
hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa
desturi yake, akasimama ili asome. 17 Akapewa chuo cha nabii Isaya,
akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 18 Roho
wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari
njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona
tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka
wa Bwana uliokubaliwa. 20 Akakifunga chuo,
akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi
wakamkazia macho. 21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya
yametimia masikioni mwenu. 22 Wakamshuhudia wote,
wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye
mwana wa Yusufu? 23 Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia
mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba
yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe. 24 Akasema,
Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake
mwenyewe. 25
Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika
nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na
miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; 26 wala Eliya hakutumwa
kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. 27 Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli
zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu. 28 Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia
hayo. 29 Wakaondoka wakamtoa nje ya mji,
wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate
kumtupa chini; 30 lakini yeye
alipita katikati yao, akaenda zake.
Walitaka kumuua Kristo, mwana wa Mungu, lakini kwa kweli hawakuweza. Kile
alichofanya Kristo kilikuwa ni kusema kweli tu, nao walimchukia kwa hilo. Hili
lilikuwa ni shambulio la mtu binafsi. Kama mtu anasema kweli ndipo ajue kuwa
atachukiwa kwa hilo. Hasira inayokaa kwa watu hawa ni kutu ambacho ambacho sisi
sote tunakwenda kupingana nacho. Jinsi tunavyomudu kuizuia, na tusijiachiwe
kuendeshwa nayo mioyoni mwetu, na ndivyo tunavyouelewa ule usemi wa kwamba
chuma hukinoa chuma. Tunapoujua mchakato mzima wa hasira hii, ni wapi hasira
hii iliyoletwa inakotupeleka, basi tutaishughulikia kuipooza na kuikomesha
kabisa kwa haraka sana.
Maranyingi Mungu anatumia hasira na chuki ili kupeleka mapenzi yake kama
tulivyoona kwenye maisha yetu sisi wenyewe. Wakati mwingine anatumia hasira za
watu wengine ili kutuadhibu na kufanya uhusiano wetu na yeye uwe ni wa
kutegemeka na wa kueleweka. Mungu hutumia hasira za wengine ili kuturudisha
kanisani. Yatupasa kuona kwa upande mmoja kwamba roho ya hasira tuliyoiona kwa
watu wakati ule haikuwa roho utimamu wa mawazo na akili.
Watu wa dunia hupenda kuchagua makanisa waliyomo ndani yake, yatokanayo na
hali ya kujisikia kwao au kulingana na hali zao, na wanafanya hivyo ili
kuhalalisha hali yao ya kujisikia kimadaraja au ubora.
Kanisa la Waathanasian lililokuwa likihudumu huko Roma lilibadilisha Imani
ya Kikristo ili kuhalalisha hali yao ya kujisikia wako bora kuliko imani ya
Wayahudi. Shetani alitumia hali hiyo ya ubaguzi na wengine kujiona bora zaidi
kwa kuondolea mbali hata Sabato na Siku nyingine Takatifu za Mungu.
Waliufanikisha mkakati huu kwa dhana yao ya kuwapinga na kuwaona duni
Wasemitiki. Wakaianzisha dini yao wenyewe ili kuhalalisha ubaguzo wao (soma
majarida ya Chimbuko la Krismas na Easter
(Na. 235); Ndama wa Dhahabu (Na. 222);
Mafundisho ya Kizushi Kwenye Kanisa la Mitume (Na. 89); Msalaba: Chimbuko
Lake na Maana Yake (Na. 39); Teolojia ya Kwanza ya Uungu (Na. 127); Jaribio la Matendo na Sherka - au MMT (Na. 104); Mwendelezo wa
Mtindo wa Uplatoni-Mamboleo (Na. 17).
Dini nyingi au imani za siku hizo zimejengwa juu ya mbaguano wa wahusika.
Watu hupenda mafundisho kwa kuwa yanafaa na kusaidia maisha ya anayeyaamini au
ni kwa sababu wanampenda mtu fulani kwenye dini yao. Watu wengi hulitafuta
kanisa kwa kulinganisha na kufikishwa kwenye mahitaji yao na kisha
huyashambulia makanisa mengine kwa kuwa hawayafikii mahitaji na ndoto zao
fulani walizozitarajia.
Hii sio njia bora ya mtu kulichagua kanisa. Hii inamfanya mtu awe kwenye
hali ya kuwajibika kuamua na sio kitu kinginecho. Suluhisho la kweli ni kwa mtu
kuzitafakari Sheria na kuifanya Biblia kuwa ni kitu kinachoweza kumuamria
mtindo wa maisha ya mtu. Kisha ndipo mtu ana jozi ya kanuni ambazo kwazo
anazitumia kufanyia maamuzi.
Kama utalichagua kanisa au kitu chochote au mwanadamu, ndipo utafungiwa
kwenye uelewa ule tu kama ulivyo bila kuwa na msingi. Hasira kuu zaidi hutokana
na watu wanaoshughulika na maisha yao ya kiroho kwa namna hiyo.
Ndipo mtu anajikuta akiwa kwenye hali ya jakamoyo la kisaikolojia
inayomlazimisha mtu kuyumba kutoka kwenye hatua moja ya rejea hadi nyingine na
kumlazimu mwinine apingane na vipengele hivyo (mara nyingi ni kutokana na
uhalali). Ni vigumu sana kufidia au kurudisha mawazo au ushauri wa mtu. Kama
maamuzi yetu yote yanaendana sawa na neno la Mungu, basi hatuwezi kuikuza
hasira hii ya kibinadamu.
Madhaya Yatokanayo na Hasira
Ayubu 5:2 Kwani
hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga.
Zaburi 37:8 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
Zaburi 37:8 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
sababu ya dhuluma yake yule mwovu. Kwa maana wananitupia uovu, Na kwa ghadhabu wananiudhi.
Zaburi 76:10 Maana
hasira ya binadamu itakusifu, Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.
Mithali 6:34 Maana wivu ni ghadhabu ya mtu; Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi.
Mithali 12:16 Maneno ya waovu huotea damu; Bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa.
Mithali 14:17 Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa.
Mithali 14:29 Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
Mithali 15:1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
Mithali 15:18 Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.
Inaweza kuendelea mbele kwa mbele. Tumepewa mifano kwenye Zaburi yote na
Mithali. Kuna mithali nyingi zinazoelezea hasira. Kwa kujisomea vitabu hivyo,
tunaweza kuyajua madhara yanayosababishwa na hasira. Kisha tunasoma mambo
mengine mengi.
Kutoka 22:24 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.
Kutoka 33:5Bwana akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli, Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa vueni vyombo vyenu vya uzuri ili nipate kujua nitakalowatenda.
Hesabu 11:1 Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa Bwana; Bwana aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa Bwana ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago.
Hesabu 11:10 Basi Musa akawasikia watu wakilia katika jamaa zao zote, kila mtu mlangoni pa hema yake; na hasira za Bwana zikawaka sana; Musa naye akakasirika.
Hesabu 11:33 Kisha hapo hiyo nyama ilipokuwa ikali kati ya meno yao, hawajaitafuna bado, hasira za Bwana ziliwaka juu ya watu, Bwana akawapiga watu kwa pigo kuu mno.
Yoshua 23:16 Hapo mtakapolivunja agano la Bwana, Mungu wenu, alilowaamuru,
na kwenda kuitumikia miungu mingine, na kujiinamisha mbele yao, ndipo hasira ya
Bwana itakapowaka juu yenu, nanyi mtaangamia upesi katika nchi hii njema
aliyowapa.
Tumesoma tu kwenye Mithali na Zaburi kuhusu madhara yanayosababishwa na
hasira na jinsi hasira mbaya ilivyo. Tumejionea mifano, na bado kuna aya nyingi
sana zinazoelezea hasira ya Mungu. Kwa kweli, tunaizungumzia hasira nyingine,
na hasira hiyo inaitwa haron ambayo
tumeiongelea tangu mwanzoni, ni hasira ya kimungu, hasira iwakayo. Kwa hiyo
kwani tunasema kwamba ni vyema sana kwa Mungu na Kristo kukasirika, ila si
vizuri kwa sisi kufanya hivyo kwa kuwa Mungu ni Mungu tu? Hiyo ingekuwa ni sawa
na kusema. “kwakuwa mimi ni mtume, au “Mimi ni mtumishi kwa hiyo niko juu ya
sheria”. Ni sawa tu na kuwaza kwamba, kama kuna mazingira fulani ambayo Kristo
au Mungu anaweza kukasirika, kwa hiyo mtazamo ni kwamba, basi kuna wakati
tunaoruhusiwa hata sisi wanadamu kukasirika. Tunapotoa maana ya hasira. Inakuwa
ni wazi na dhahiri kuwa inaonekana kana kwamba wivu wa kazi. Kazi au kitendo
kinachoongelewa ni wivu au juhudi ya kuifanya kazi ya Mungu. Hasira kwa ajili
hiyo yaonekana kuwa itatupa sisi wivu au bidii ya kuitanya kazi ya Mungu.
Ikitumika vizuri inakuwa ni zana yenye nguvu kwa ajili ya mema.
Mathayo 21:1-16 Hata
walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo
Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia, 2 Enendeni mpaka kijiji kile
kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye;
wafungueni mniletee. 3 Na
kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka.
4 Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, 5
Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda
punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda. 6 Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya
kama Yesu alivyowaamuru, 7 wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo
zao juu yao, naye akaketi juu yake. 8 Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza
nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani. 9 Na
makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana,
Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu
mbinguni. 10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema,
Ni nani huyu? 11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya
Galilaya. 12 Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza
na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa
wakiuza njiwa; 13 akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala;
bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi. 14 Na vipofu na viwete
wakamwendea mle hekaluni, akawaponya. 15 Lakini wakuu wa makuhani na waandishi
walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni,
wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika, 16 wakamwambia, Wasikia hawa
wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto
wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?
Kwenye aya ya kumi na mbili, Yesu hakufurahishwa alipokuwa anafanya hivyo.
Usiingie ndani ukiwa unacheka na kupindua mambo, na kuwafukuza watu watoke
kwenye sinagogi. Alikasirika. Alikasirika kwakuwa hekalu lake, pake pa kufanyia
ibada palikuwa pamenajisika. Kwa dakika tu kama unapenda kuwa kwenye mchakato
wa kuwafukuza watu hawa, kwa kukasirika kutokana na hasira itokanayo na
kulinajisi huku, alianza kuwapinya watu kwanza. Hii ilikuwa ni ya moja kwa
moja. Hakuwa amewakasirikia watu hawa. Alichukizwa na matendo yao. Tumeamriwa
kuchukia dhmbi, na sio kuwachukia wenye dhambi.
Wazo hili la kulisafisha Hekalu, ni mlinganisho kwetu sisi kwa kuiondoa
dhambi maishani mwetu. Kristo hakujiondolea dhambi yeye mwenyewe kama mfano
wetu. Hakuwa na dhambi wala waa lolote maishani mwake yote. Alikwenda hekaluni,
kwenye sinagogi na kuisafishiliambali sumu iliyokuwa kwenye sinagogi, bali na
kuyasafisha matendo yao. Huu ni mfano na ni lazima au kazi itupasayo kuifanya.
Nasi pia, yatupasa kujitahidi kuyaondoa matatizo yetu kutoka kwenye mifumo na
taratibu zetu, na kutoka ndani ya mifumo ya maongozi yetu ya kibiblia, yaani,
kanisa (sawa na yasemavyo majarida ya Kulitakasa
Hekalu la Mungu (Na. 241); Marejesho
Mapya ya Yosia (Na. 245); Sikukuu za Mungu na Jinsi Zinavyohusiana na
Mchakato wa Uumbaji (Na. 227).
Sababu ya kila moja hapa ni Makanisa ya Kikristo ya Mungu ni kwa sababu
walitaka hilo tu, ili kuondoa makosa na dhambi katikati yao. Wakati ulipokuwa
unaishi visiwani kwenye makanisa yako ya zamani, na mabadiliko ya kimafundisho
yakiwa yanafanyika, na aina zote za mawazo tofauti yakiwa yanaletwa, unapatwa
na hasira. Tuliona kwamba neno la Mungu lilikuwa linanajisiwa, na tulikuwa
tumechochewa na matendo, na tulipatwa na wivu. Ni hasira ile ndiyo iliyotufanya
sisi sote hapa. Hatumchukii mtu yeyote wa kanisa lolote lile. Hatuwachukii.
Bali tunachukia kuona kwamba mafundisho haya mapotofu yangali yanaendelea bado.
Kama inaketi kanisa lolote, na ukijua kuwa kuna mambo mengi mapotofu tu
yanayohubiriwa, nawe wala husimami, na kuacha kuwapa wabadilisha fedha hawa,
kwenye meza zao, ndipo hakika hutimilizi agizo kuu alituagiza Kristo na
kukutuma kwalo. Mungu anaiachia hasira ya dunia ili ijiangamize yenyewe, na hii
ni sehemu hukumu ya watu wote. Inaua asilimia tisini au zaidi ya wakazi wa
dunia nayo imeruhusiwa itokee kwa sababu ya hasira ya Mungu, kwa kuwa sheria
zake zimeachwa na kupuuziwa na watu kuzishika. Ndipo Kristo anasema hapa kwamba
anapolisafisha hekalu, ni kana kwamba wewe unayaokoa maisha, kisha naipo haron; inakasirika kwa ajili ya
kuzihalifu sheria. Hii ndiyo aina ya hasira tunayopaswa kuwanayo, wazo hilo la
kuichukia dhambi, na litatuchochea kufanya kitendo.
Tunalolifanya ni kutenda kazi, na kuyafanya matatizo haya kwenye hisia za
watu. Kama upo kwenye kanisa linalohubiri mafundisho ya uwongo, basi unawajibu
wa kuwaandikia watumishi wako na kuwaambia kuwa umekasirishwa jinsi
wanavyoihalifu sheria.
Watu wengi kanisani wameuendelea mchakato huu, na huo ni ushuhuda wa kwenye
dhana ya kwamba kuendelezwa kwake hapa. Kitu kimoja kilichodhahiri ni kwamba
tunashutumiwa sana tunapousema ukweli. Watu hawasemi kile tunachokisema, bali
wanatushutumu kama mmoja mmoja. Hii ni sehemu ya jinsi hasira ya mwanadamu
ilivyotenda kazi hapo kabla. Ni rahisi sana kuipata kwa mazingira kama haya.
Kwa kuonyesha udhaifu wa wengine, watu wanaweza kuhalalisha hali walizonazo..
Hivi sivyo tulivyo sisi hapa. Hatuhusiki na watu wafanyao hivyo, kwa kuwa
huo sio Ukristo; si mtazamo tunaojaribu kuendeleza. Kuna wakati wa kukasirika,
na kuna hasira mbovu pia. Mungu anakasirika wakati anapoona sheria zake
zikihalifiwa au kuvunjwa, na sisi tunapaswa kuchochewa na ukweli huo. Tusione
haya kuwa na hasira, wakati tuonapo sheria zikivunjwa au kuhalifiwa zisishikwe.
Sisi, kwa mfano wa Kristo, na tumepewa kazi na majukumu kuona kwamba sheria
zinashikwa.
q