Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[063]
Ufafanuzi kuhusu Esta
(Toleo la 3.0 19940824 – 20000 - 200090211)
Huu ni ufupisho wa kina wa
kitabu cha Esta. Maudhui yaliyomo kwenye kitabu cha Esta yana
maana kubwa kwa ajili ya Ukristo wa kisasa. Karatasi hii inatumia maelezo ya
Kirabbi na kuyaainisha kwa uwazi wa Ukristo wa
kibiblia, ambao unazalisha matokeo kadha yenye maana.
Christian
Churches of God
Barua Pepe: secretary@ccg.org
(Hati Miliki ©
1994, 1998, 2000, 2009 Wade Cox)
(tr. 2012)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakaotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia
yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Maelezo haya ni ya kitabu cha Esta. Ni hadithi ya ajabu kuhusu mwanamke aliye fanyika malkia wa Uajemi au inahusu kumiliki kwa Yesu Kristo kwa miaka Elfu au yahusu yote mawili. Kutokana na maelezo haya tutapata kwamba ni yote mawili yanasimuliwa katika hadithi hii. Inatufundisha jinsi sisi pamoja na wayahudi tutakavyoridhi Ufalme wa Mungu. Ni ulinganifu wa utimizo wa wakati au mpango wa wokovu wa wayahudi ilmuradi mfuatano huu ueleweke. Imefichwa kwa uangalifuzaidi haswa na wale marabbi wenyewe, kwa sababu ina habari isiyo ya kawaida. Kuna mambo kadha wa kadha yanayohitaji mafafanusi. Mfalme husika ni Ahasuero. Katika kitabu hiki Mungu hajatajwa popote Jambo hili si la kawaida kabisa, na maana yake ni kwamba uwezo wa mungu unatumika kupitia kwa Ahasuero. Hivyo basi hakuna haja Mungu kutajwa; kwani ufalme pamoja na utawala umo mikononi mwake aliyetumia uwezo wa Mungu. Ahasuero anaridhi nafasi hii katika hadithi hii, jinsi inavyofunua, hasa zaidi kwa mwonekano wa miaka elfu. Wahusika wenyewe wana umuhimu mkuu katika uhusiano kwa kanisa, kristo, jeshi lililoanguka na utaratibu wa wakati wa mwisho.
Ahasuero kwa ujumla anatambulika kama anayefanana na mfalme Xerxes aliyetawala tangu mwaka wa 485BC hadi 464BC. Neno la kihebrania Achashwerosh ni jaribio la kuwakilisha neno la kiajemi khshayarsha ambalo kwalo wayunani wanatokezea jina Xerxes (Taz. Soncino fn. to v.1). ni matamshi magumu na majina haya ni miandiko ya herufi nyingine zisizo za lugha yenyewe. Ni mfalme Xerxes aliyetawala baada ya Dario wa kwanza na kabla ya mfalme Arshatasta na aliyezuia ujenzi wa hekalu katika Ezra 4. Sura ya nne ya Ezra ina utaratibu wa ujenzi wa Hekalu. Ezra 4:4-5 inasema:
4 Ndipo watu wa nchi wakaidhoofisha mikono ya watu wa Yuda, wakawasumbua, walipokuwa wakijenga. 5 Wakawaajiri washauri juu yao, ili kuwapinga kusudi lao, siku zote za Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata wakati wa kutawala kwake Dario, mfalme wa Uajemi. Biblia Takatifu BT)
Hivyo walitatiza au kuzuia ujenzi wa hekalu wa katika utawala wa Koreshi hadi utawala wa Dario mfalme wa uajemi ambaye si Dario wa kwanza. Uyahudi wa sasa na ukristo wa kisasa una haki ya kuwa na haja imara katika kulikamilisha hekalu katika utawala wa Dario 1. Hekalu haikukamilishwa wala kamwe halingekamilishwa katika utawala wa Dario 1. Hicho ni kinyume cha moja kwa moja kwa maneno kamili ya Bibilia. Katika mstari wa 6 wa Esta 4 una sema:
6 Tena, wakati wa kutawala kwake Ahasuero, mwanzo wa kutawala kwake, watu wakaandika mashitaka juu ya wenyeji wa Yuda na Yerusalemu. (Biblia Takatifu BT)
Maelezo ya kirabbi juu ya ushupavu wa Esta yanasema alizuia ujenzi wa hekalu mwanzoni mwa utawala wake na kutangaza amri juu ya wayahudi katika miaka yake ya baadaaye (Taz. Midrashic Approach To Esther, p. 125). Na ndiyo sababu majaribio yamefanywa kufanya Ahasuero Cambyses aliyekuwa mwana wa Koreshi, ili yawiwane na ujenzi wa hekalu katika utawala wa mfalme Dario wa 1. Hata hivyo inaendelea katika fungu la 7:
Ezra 4:7-24 Na tena, katika siku za Artashasta, Mithredathi, na Tabeeli na mabaki ya
wenziwe, wakimwandikia Artashasta, mfalme wa Uajemi, salamu za heri; na
mwandiko wa waraka huo, ukaandikwa kwa herufi za Kiaramu, na kunenwa kwa lugha
ya Kiaramu. 8 Nao Rehumu, Bwana shauri, na Shimshai, mwandishi,
wakaandika waraka juu ya Yerusalemu kwa Artashasta, mfalme, kama hivi; 9 Rehumu, Bwana shauri, na Shimshai, mwandishi, na mabaki ya wenzao,
makadhi wa Kiajemi na madiwani wa Kiajemi; na Waarkewi, Wababeli, Washushani,
yaani, Waelami; 10 na mabaki ya mataifa, ambao Asur-bani-pali
mkuu, mwenye heshima, aliwavusha, na kuwakalisha katika mji wa Samaria, na
mahali penginepo, ng'ambo ya Mto; wakadhalika. 11 Hii ndiyo nakili ya waraka waliyompelekea mfalme Artashasta; watumishi
wako, watu walio ng`ambo ya mto wakadhalika. 12 Ijulikane kwa mfalme
ya kuwa Wayahudi, waliokwea kutoka kwako, wamefika kwetu Yerusalemu; nao
wanaujenga ule mji mwasi, mbaya; wamemaliza kuta zake, na kuitengeneza misingi
yake. 13 Basi, ijulikane kwa mfalme,
ya kuwa mji huu ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hawatatoa kodi, wala ada,
wala ushuru, na mwisho wake wafalme watapata hasara. 14 Na
sisi, kwa kuwa tunakula chumvi ya nyumba ya mfalme, wala si
wajibu wetu kumwona mfalme akivunjiwa heshima, basi tumetuma watu na kumwarifu
mfalme. 15 Ili habari zitafutwe katika kitabu cha tarehe za
baba zako; ndivyo utakavyopata kujua kwa kitabu
cha tarehe ya kuwa mji huo ni mji mwasi, wenye kuwadhuru wafalme, na maliwali,
na ya kuwa wenyeji wake wamefanya fitina katika mji huo zamani; ndiyo sababu
mji huo ukaangamizwa. 16 Twamwarifu mfalme ya kuwa mji huo
ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hutakuwa na sehemu ya nchi
ng'ambo ya Mto. 17 Ndipo mfalme akapeleka majibu; Kwa Rehumu,
Bwana shauri, na Shimshai, mwandishi na wenzao wengine waliokaa katika
Samaria, na penginepo ng`ambo ya mto, Salamu; wakadharika. 18 Ule waraka mlionipelekea umesomwa mbele yangu, nami nikaelewa na maana yake. 19 Nikatoa amri, na watu wametafuta habari; ikaonekana ya kuwa mji huu
zamani umefanya fitina juu ya wafalme, na ya kuwa uasi na fitina zimefanyika
ndani yake. 20 Tena walikuwako wafalme wakuu juu ya
Yerusalemu, waliotawala nchi yote iliyo ng'ambo ya Mto; wakapewa kodi, na ada, na ushuru. 21 Sasa toeni amri
kuwakomesha watu hawa kazi yao, mji huu usijengwe, hata
mimi nitakapotoa amri. 22 Tena jihadharini, msilegee katika
jambo hili; kwa nini madhara yazidi, na wafalme wapate hasara? 23
Hata nakala ya waraka huo wa mfalme Artashasta uliposomwa mbele ya
Rehumu, Bwana shauri, na Shimshai, mwandishi, na wenzao, wakaenda Yerusalemu
upesi, kwa Wayahudi, wakawakomesha kwa nguvu na kwa kuwashurutisha. 24 Hivyo kazi ya nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu ikakoma; nayo ikakoma
hata mwaka wa pili wa kutawala kwake Dario, mfalme wa Uajemi.
(Biblia takatifu BT)
Hivyo kwa urahisi sana, Ahasuero aliombwa jumbani mwa mfalme, (pia toka kwa ujasiri wa malkia) kuzuia ujenzi naye Arshtasta aliyemfuata, aliombwa pia na kulingana na bibilia katika Ezra 4:24, kazi ya nyumba ya mungu ilizuiwa hadi utawala wa Dario mwajemi, hivyo basi, kama vile usiku uliofuatia mchana, huyo Dario Mwajemi anayezungumziwa katika fungu la 24 hawezi kuwa Dario wa 1 aliyetawala kabla ya wafalme wawili Xerxes na Arshtasta. Maana yake ni kwamba majaribio yanafanywa kuzuia ujenzi wa hekalu hadi utawala wa mfalme aliyetawala awamu mbili kabla ya Arshatshata na mbele ya Ahasuero, mfalme aliye swala kuu hapa. Kuna maana katika kitabu cha esta yanayohusiana na ukamilishaji wa Hekalu la mfalme Suleimani ambayo ni muhimu.
Kanuni ya msingi wa majina ni muhimu.
kulikuwepo wafalme wengine walioitwa Ahasuero. Tafsiri ya maelezo ya kirabbi huelewesha maana ya maandiko haya.
Esta 1:1 Zamani za Ahasuero; naye huyu Ahasuero alimiliki toka Bara Hindi mpaka Kushi, juu ya majimbo mia na ishirini na saba; (Biblia Takatifu BT)
Orodha ya majimbo ni takribani zaidi ya mia na ishirini na saba. Dario wa 1 alimiliki juu ya ufalme huu naye akaugawanya kati ya maliwali mia na ishirini yanayoorodheshwa na maandiko kama mataifa mia na ishirini na saba kulingana na Marko na soncino. Katika Danieli 6:2 maliwali 120 wametajwa, hivyo tunashughulikia na uwezekano wa kuangalia mfuatano sio wa 127 bali ni watawala saba wakuu pamoja na maliwali 120. Hapo baadaye huenda huu ukawa ushaidi zaidi. Maeneo husika ni kushi hadi bara hindi, na bara hindi hapa ndio Hodu ya kihebrania na ndio ziwa la Indus. Kushi ilitekwa na kambisesi na Dario mfalme wa uajemi tangu 529 hadi 522 BC. Basi mambo haya yote yako tangu Kambesi na Dario. Hivyo tunamwangazia Xerxes alinyakua falme zilizoanzishwa tokea kushi na Ahasuero na majimbo chini ya Dario. Basi mfalme huyu ndiye aliye tawala baada ya Dario na ndiye Xerxes haswa.
Esta 1:2 siku zile mfalme Ahasuero alipoketi katika kiti cha enzi cha ufalme wake, huko Shushani ngomeni;
Esta 1:3 mwaka
wa tatu wa kumiliki kwake, ikawa
aliwafanyia karamu maakida wake wote na majumbe wake; wakuu wa Uajemi na Umedi,
watu wenye cheo na maakida wa majimbo, wakihudhuria mbele zake.
Esta1:4 Akawaonyesha utajiri wa ufalme wake mtukufu, na heshima ya enzi yake bora siku nyingi, maana siku mia na themanini. (Biblia Takatifu BT)
Hapa tunaangazia karamu ya siku mia na themanini (180). Karamu hizi za waajemi zilikuwa karamu za ukumbusho, nazo zilikuwa na anasa kupindukia sababu moja ya maagizo dhidi ya kufanya sherehe za kuzaliwa ni kwamba sherehe hizi zilikuwa desturi ya waajemi, swala hili pia limeangaziwa katika gazette la Siku za Kuzaliwa (No. 287). Walitoa kafara wakati huu wa karamu kubwa kwa miungu wa kigeni na kufanya shughuli za kila aina. Mwanzo na uadui kati ya Yuda na Waajemi ikihusishwa na sherehe hizi za kuzaliwa vilifanya msingi wa machukizo, yaliokuzwa miongoni mwa makanisa dhidi ya miandamo ya siku za kuzaliwa. Ukweli ni kwamba desturi hii inatokana na ibada za taratibu za As sryo-Babeli na ibada za Baali na Ista au taratibu za Easter.
Esta 1:5 Hata siku hizo zilipotimia, mfalme akawafanyia karamu watu wote
waliokuwapo huko Shushani ngomeni, wakubwa kwa wadogo,
muda wa siku saba, katika behewa la bustani ya ngome ya mfalme.
Esta 1:7 Wakawanywesha kileo katika vyombo vya dhahabu, na vile vyombo vilikuwa mbalimbali, na divai tele ya namna ya kifalme, sawasawa na ukarimu wa mfalme;
Esta 1:8 kunywa kulikuwa kama ilivyoamriwa, bila
sharti; maana ndivyo mfalme alivyowaagiza watumishi-wa-nyumbani, kila mtu
afanye apendavyo.
Katika siku hizo walioongozwa na watu maarufu. Tafsiri ya kirabbi ni kwamba walikubaliwa kunywa divai yao wenyewe na kunywa wapendavyo (Taz soncino). Kama tukio la mawazo ya kila namna yaliibuka toka kwa hili. Waajemi walikuwa wanywaji mashuhuri, Zenafoni aliongea juu yao, wao hunywa kiasi kwamba hawawezi kusimama kwa miguu yao, hivyo wao hubebwa. Ahasuero aliogopa machafuko wageni wake wakiisha kulewa. Taarifa za Xerxes zaonyesha kwamba hakushika ufalme kwa nguvu, bali dhana ni kwamba kuna maasi mbinguni sawa na tunavyoelewa na kwamba tatizo hili miongoni mwa jeshi lililoonekana katika utawala.
Esta 1:9 Tena Vashti, malkia, naye akawafanyia karamu wanawake ndani ya nyumba ya kifalme ya mfalme Ahasuero.
Esta 1:10 Hata siku ya saba, mfalme alipofurahiwa moyo wake kwa divai, aliwaamuru Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari, na Karkasi, wale wasimamizi-wa-nyumba saba waliohudumu mbele za mfalme Ahasuero, (Biblia takatifu BT)
Midrash inasema, hii inamwelekea Vashti malkia (Vashti maanake bora zaidi). Vashti aliwaandaa wanake nyumbani mwa mfalme, sio nyumbani mwa wanawake, kusudi la hili ni kuwadharau wanawake. Tunashughulika na jambo kwamba kuna mawazo ya kiroho katika jambo linalofanyika. Wanawake hapa wanatokeza wazo kuhusiana na kanisa au wanatumiwa kueleza au kutokeza wazo la kanisa na uhusianmo wake na jeshi lililoanguka. Vashti alipanga kuwafanya wanawake watende dhambi. Kulingana na midrashi maelezo ni kwamba mpango wa Ahasuero ulikuwa kuwafanya wayahudi watende dhambi na
……hivyo angeakikishiwa kwamba wataadhibiwa na Mungu na hwangerejeshwa katika nchi yao. Kwa hiyo alishindwa kuwakanya kuvunja Torati za sheria wasije wakasingingisia dhambi zao. Badala ya hayo aliwajaribu kufanya viburi katika karamu, walakini hakuwalasimisha kufanya hivyo (Soncino fn. To Esta 1:8)
Wayahudi wanaliona hili kama mfano wa kujaribu kuvunja hali uhusiano wao na Mungu. Wanaziona shughuli za Ahasuero katika mwelekeo na Vashti kama zisizofaa katika mfano wa kwanza ila hilo si kusudi lililo sawa la swala hili. Kusudi lilikuwa kuonyesha kuwa kuna mwanamke mteule, malkia pamoja na wafuasi wake, aliyechaguliwa kama aliye bora zaidi na kuwekwa katika ufalme kama mke wa mfalme. Hiyo ilikuwa Israeli, mkusanyiko na hivyo anawasilisha kusanyiko la Israeli lililotengwa liwe teule. Na sasa katika siku ya saba moyo wa mfalme ulipochangamka, aliwaamuru hawa wakuu saba. Huenda wazo la wale 127 linatokana na ukweli kwamba hawa wakuu saba walikuwa na amri ya uongozi juu ya maliwali 120, ila hii ni dhana tu.
Esta 1:11 wamlete Vashti, malkia, mbele ya mfalme, amevaa taji ya kifalme; ili kuwaonyesha watu na maakida uzuri wake, maana alikuwa
mzuri wa uso. (Biblia Takatifu BT)
Kiroho, wawakilishi saba wanaonekana kama watatoshelea wale malaika saba wa makanisa ya Mungu, walioamuriwa kuileta Israeli mbele za Mungu. Israeli hawakuja mbele ya Mungu. Israeli waliasi na kutenda dhambi.
Esta 1:12 Bali Vashti, malkia, alikataa kuja kwa amri
ya mfalme kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba; kwa hiyo mfalme akaghadhibika
sana, na hasira yake ikawaka ndani yake. (Biblia Takatifu BT)
Nao saba walionekana mbele ya mfalme wanaonekana kuhusisha manabii walioona uso wa Mungu; uwepo au malaika wa Mungu. Manabii saba (Samueli, Eliya, Elisha, Isaya, Yeremia, Ezekieli na Danieli), waliosimama uso kwa uso mbele ya Mungu kupitia kwa malaika wa uwepo, wahamuriwa kuaandaa Israeli baada ya musa tokea kipindi hicho kuendelea, kuleta Israeli mbele za Mungu kwa utaratibu unaofaa, ndipo Israeli ipate kutiwa taji kama taifa kiongozi wa dunia- kama malkia wa dunia. Israeli walikuwa na jukumu la kujitayarisha na kufanya hivyo.
Esta 1:13 Basi mfalme akawaambia wenye hekima, walio na elimu ya nyakati; maana ndivyo ilivyokuwa desturi ya mfalme kwa wote waliojua sheria na hukumu; (Biblia Takatifu BT)
Talmudi anawaelewa kama wanajimu, walakini maneno haya yanaenda sambamba na wote waliofahamu sheria na hukumu. Sheria na hukumu hutekelezwa kwa ufahamu wa sheria kupitia kwa roho mtakatifu. Hii ilitolewa katika sehemu ya kwanza ya njia ya manabbi. Soncino yasema pamoja na wote walifahamuo sheria na hukumu na bila shaka inamaanisha wale walio na uzoefu wa mifano ya kihistoria yenye nguvu za sheria. Hii inatokana na (ibn) mafafanuzi ya Ezra, ndivyo ilivyokuwa hali ya mfalme kwa wote waliofahamu sheria na hukumu, kwani wote wenye haki wana nguvu za sheria; iliyo utendaji wa haki. Hivyo wale wanao nguvu za Mungu hupendezwa pia- kwa wanaoifahamu haki, sheria na hukumu
Esta 1:14 na karibu naye wameketi Karshena, Shethari, Admatha, Tarshishi, Meresi, Marsena, na Memukani, wale maakida saba wa Uajemi na Umedi, waliouona uso wa mfalme, na kuketi wa kwanza katika ufalme; akawauliza, (Biblia Takatifu BT)
Hawa ndio manabii wakuu waliosimama mbele ya uso wa Mungu, kama ilivyotajwa hapo mwanzoni.
Esta 1:15 Tumfanyieje Vashti, malkia, kwa sheria, kwa sababu hakufanya kama vile alivyoamriwa na mfalme Ahasuero kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba? (Biblia Takatifu BT)
Hivyo Israeli hawakuwatii manabii. Israeli hawakujiandaa wenyewe kuja mbele ya mfalme. Israeli walijiweka uchi kwa mwenendo wao, jinsi Vashti kwa tabia yake alivyofanya pia. Mafafasi ya midrash yanasema kwamba alikuwa uchi na maelezo yanaelekea ukweli kwamba alivalia taji tu. Alikataa kuja kwa sababu ya jinsi alivyovalia naye alijiona mwenye uchi wake.
Kuna tafsiri mbili zinazosema alikuwa tupu, bali aliombwa kuonekana hivyo uchi akiwa tu na kilemba kichwani, na ndiyo sababu alikataa. Lakini alipojiangalia kwa kioo alijiona na ukoma usoni, ila hakuna mwingine aliyeona hivyo, naye aka kataa kuja kwani alijiona uchi wake mwenyewe kupitia kwa maaasi yake. Wafafanusi wa kirabbi wanafikia umbali huu, bali hawafanyi muunganiko kwamba ni Israeli kwa uasi wake ambao haustahili, akiwa amejiona uchi naye hangeenda mbele za Mungu. Hili lina maana kubwa. Marabbi wamefahamu swala hili kwa muda mrefu, huku wakiendelea kulizuia na midrash inaanza kupambanua katika hali zisizo za kibibilia, ili kuepuka ukweli kwamba walijionyesha kutokujiweza kuja mbele za Mungu katika hukumu. Memukani ndiye wa mwisho kati ya wale saba waliotajwa na inasemekana kwamba ni muhusika asiyejulikana na marabbi wanamtabulisha kama Hamani. Marabbi wanajaribu kuisukuma hoja kwamba alikuwa mpumbavu kwani aliongea kwanza, kwa kuwa mfafanuzi ya kirabbi yanasema kwamba mpumbavu tu ndiye huongea kwanza. Maelezo haya hutoka kwa megilla (meg. 12 B)
Hamani alikuwa na
sababu ya kumchukia vashti na sasa wanajaribu kumtafuta aliyemchukia vashti.
Hamani alikuwa mhagagi na Agagi alikuwa Mmaleki.
Tunashughukika na dhana za waamaleki dhidi ya Israeli.
Amaleki ndiye aliyewakabili wa Israeli kabla
hawajaingia katika nchi ya ahadi naye musa akasimama na kuinua mikono yake,
ndiposa wa Israeli wapate kuwashinda waamaleki, kabla ya kwenda katika nchi ya
ahadi. Hivyo basi tunaangazia dhana hii kwenye sehemu ya mwisho kabisa kabla
hatujaingia katika nchi ya ahadi; tukipambana na nguvu
za kishetani kwa umbo la Amaleki na ndiposa Yule Hamani Mwahagagi, Mwamaleki,
anawakilishwa hapa katika maangamivu ya Yuda. Hapo Marabbi wanasema kwamba kuna
mifano miwili- walioamriwa kuharibu wanakanani walimaanisha kuungana na wamaleki. Huu ni mfano wa tatu
wa waamaleki kujaribu kuwaharibu wateule. Tukio hili inaelekea maangamizi ya
mwisho; vita za mwisho kabla ya kwenda Israeli chini ya miaka elfu ya urejesho. Hii itakuwa tunapoendelea kupitia maandiko. Tunaangazia vita
vya mwisho wa wakati.
Hamani alikuwa mwamaleki katika taarifa hii sio kiajali. Kitabu cha Esta kinaongea juu ya uhalisi chini ya Shetani na Kristo, Kanisa dhidi ya ulimwengu kuingia hukumuni na kuitawala dunia. Hii ndiyo hoja ya vita vya siku za mwisho. Inapita kwa nguvu nyingi kwa vishindo vyake. Kutokana na maelezo kotoka midrash na Megillah kuna mafafanusi kadhaa kuhusu sababu iliyomfanya Hamani amchukie vashti; ila hakuna shaka kwa nini chuki ya wayahudi ipo kwa waamaleki hata leo. Waamaleki walikuwa maadui wa jadi wa waisraeli husi tunaangazia dhana ya maadui wa wateule hadi siku za mwisho. Vita vya mwisho zinachunguzwa katika kurasa mbali mbali za somo hili.
Hii hukumu ya vashti ililingana na sheria. Marabbi wanasema memukani aliongezea “kulingana na sheria” kwa sababu alijua kwamba Ahasuero hakutaka kumwua vashti. Hiyo ni kweli. Mungu hakutaka kuangamiza Israeli kwa uasi wake. Sheria iliyotolewa kwa Israeli na Israeli anahukumiwa kulingana na sheria. Hivyo vashti na maagizo ya Ahaseuro kwa mkono wa wasimamizi wa nyumba. Israeli hawakutii sheria kwa mkono wa wanabii. Hawakumtii Mungu.
Esta 1:16 Basi Memukani akajibu mbele ya mfalme na maakida, Huyu Vashti, malkia, hakumkosa mfalme tu peke yake, ila na maakida wote, na watu wote pia walioko katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero.
Esta 1:17 Kwa maana tendo hilo la malkia litajulikana na wanawake wote, hata waume zao watadharauliwa machoni pao, itakaponenwa ya kuwa mfalme Ahasuero aliamuru Vashti, malkia, aletwe mbele yake, bali hakuja. (Biblia Takatifu BT)
Linalosemwa ni kwamba wasi katika sehemu ya jeshi huenea na kuingilia jeshi zima, hivyo basi uasi katika Israeli uliwaathiri wote. Urejesho wa Israeli alikuwa hatua ya kimsingi katika kuondoka kwa sayari hii ya dunia. Israeli iliingizwa ndani ndiposa mataifa wapate kuingia. Walakini Israeli machoni pa Yuda hawakuona mataifa wakiletwa kwenye wokovu. Uhusiano kati ya Mungu na Israeli chini ya sheria unaelezwa katika gazette hizi Torati na Amri ya Kwanza [253]; Torati na Amri ya Tano [258] na Torati na Amri ya Saba ya Mungu [260] (cf. pia gazette hili Sheria za Mungu [L1] na maandishi mengine humo)
Israeli waliuona wokovu kama wao pekee yao hivyo wakajiona kwamba hawafai kuingia hukumuni. Na ndiyo sababu ya kuadhibiwa kwa Israeli, kwa maana ulimwenguhautaongoka kabla Israeli haijaongoka. Ulimwengu hauingii katika pumziko la miaka elfu hadi hapo Israeli itakapofikia pumziko hilo. Yuda atatazamishwa kuingia katika pumziko, ndipo ulimwengu uingie. Yuda atafanyika mkristo kwa upanga. Huu utakuwa upanga wa mungu na wa kweli, naye Mungu atayafungua macho yako katika siku za mwisho. Atalazimisha ufahamu wao na huyo roho atakapomwaga juu yao wataelewa, walakini hapa walikataa na kumpinga Mungu kwa hiari yao na kujionyesha kuwa hawafai kuingia katika ufalme wa Mungu
Esta 1:18 Hata na leo hivi mabibi wastahiki wa Uajemi na Umedi waliokwisha kuzisikia habari za tendo lake malkia watawaambia vivi hivi maakida wote wa mfalme. Hivyo kutatokea dharau nyingi na ghadhabu tele.
Esta 1:19 Basi mfalme akiona vema, na itoke kwake amri ya kifalme, nayo iandikwe katika sheria za Waajemi na Wamedi isitanguke, ya kwamba Vashti asifike tena mbele ya mfalme Ahasuero; na umalkia wake mfalme ampe mwingine aliye mwema kuliko yeye. (Biblia Takatifu BT)
Ilikuwa sheria ya wamedi na waajemi kwamba mfalme akitoa amri, kamwe isibadilishwe. Katika hali hii hoja inatokana na wazo kwamba kitokacho kinywani mwa Mungu hakirudi bure na ya kuwa Mungu akisha kuamuru na kuonyesha mapenzi yake, yanabakia kuwa hivyo. Hivyo basi mambo hufanyika kwa matamshi ya Mungu matakatifu, wala Mungu hakosei. Mungu hutoa amri kwa kinywa chake kuonyesha mapenzi yake nayo hufanyika kwa amri, hivyo basi amri takatifu hazibadiliki.
Esta 1:20 Basi mbiu ya mfalme atakayoipiga itakapotangazwa katika ufalme wake wote, nao ni mkubwa, wake wote watawaheshimu waume zao, wakubwa kwa wadogo.
Esta 1:21 Basi neno hili likawapendeza mfalme na maakida; naye mfalme akafanya sawasawa na neno lake Memukani.(Biblia Takatifu BT)
Heshima ipeanwayo kwa waume ni kwa sababu waweze kuwa bibi- arusi wa Kristo na bila shaka watu wote waingie karamuni kwenye sherehe ya ndoa ya mwanakondoo kama bibi arusi wa kristo. Hili hutendeka kwa utaratibu kama hapo awali, kupitia kwa wanawali wenye busara na wale wapumbavu katika ufufuo wa kwanza na wa pili. Hili lapaswa kufikiriwa ndiposa Israeli ikashughulikiwa ili hoja hii ifanywe. Chakula cha ndoa kilipeanwa kwa watu wengine vizuri kuliko wa Israeli; wokovu ulikuwa uwafikie wateule katika mataifa. Hilo ndilo kusudio.
Esta 1:22
Kwa maana alipeleka
nyaraka katika majimbo yote ya mfalme, kila jimbo kwa
mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake, ya kwamba kila mwanamume atawale
nyumbani mwake, na kuitangaza habari hii kwa lugha ya watu wake. (Biblia
Takatifu BT)
Wazo la kila watu kwa lugha yao ni kwamba barua au nyaraka zilizotumwa kwa kila jimbo na kila watu kwa lugha yao lilikuwa kiwakilishi cha Bibilia na nyaraka za Bibilia. Kwa sababu ya machafuko, ziliandikwa kwa lugha ya watu waliohusika, ili wokovu uwafikiye watu wote, mataifa yote. Katika mafafanusi ya kirabbi kuna; neno kilingana na lugha za watu. Ndiposa maana hasa ya sehemu ya pili ya maagizo inatolewa. Lugha nyingi zinazungumzwa katika utawala wa uajemi katika kipindi cha Xerxes. Wafafanuzi wa midrash na wale wa kiyahudi wanachukuliwa maneno haya kumanisha kwamba mume na mke wakiwa na makabila tofauti na lugha tofauti, wangemlazimisha mke kunena lugha ya mume. Hii ni taswira kwetu kupewa lugha mpya atakapokuja kristo. Sote tutalazimishwa kunena lugha ya mume wetu, bwana- arusi.
Kusudi lilikuwa kwamba desturi za mume zikihitilafiana na zile za mke, desturi la mume zilikuwa na nguvu kwa sababu kwa kweli desturi za Kristo zitashinda ulimwengu. Huenda Vashti alidai kwamba ilikuwa kinyume na desturi za watu wake kwamba malkia ajionyeshe mbele ya raia wake (hii ni kulingana na R.Ralbag). Pengine amri iliongezwa kwenye masimulizi ya tukio hili kuficha aibu ya mfalme (kulingana na ibn Ezra). Maelezo haya bila shaka yanamaanisha wokovu kuwezekana kupitia kwa nyaraka za bibilia kufikia mataifa yote na kwamba kila mtu aamue na nyumba yake mwenyewe na kunena kulingana na lugha ya watu wake mwenyewe. Dunia iligawanyika katika mnara wa babeli na mchafuko ukaingia ulimwenguni, ndiposa wokovu wapaswa kuujia ulimwengu katika lugha mbali mbali ndipo wokovu uwezekane kwa kila mmoja. Si kusudi la mwanadamu kwamba lugha zitofauitiane; iliitwa tu ndani mwao. (Taz pia ufunuo 14:6-7)
Esta 2:1
Baada ya hayo, hasira yake mfalme Ahasuero ilipotulia, alimkumbuka Vashti,
na vile alivyotenda, na yale yaliyoamriwa juu yake.(Biblia
Takatifu BT)
Hili wazo la Ahasuero kumkumbuka Vashti lilitazamwa na marabbi kama majuto, huku akitambua kwamba alitenda vyema kukataa kujionyesha uchi. Hivi si sawa. Haya maelezo ya kutenda vyema ni kwamba haelewi kinachohusishwa ndani ya Israeli wanapokataa kuja mbele za Mungu.
Maelezo ni kwamba Mungu mara zote atakumbuka kuna maelezo kadhaa katika zaburi yanayohusu hili, mahali tusipoweza kusahaulika naye Mungu ataturejesha, naye atatuinua na maelezo haya yanapatikana kwa manabii.
Esta 2:2 Basi watumishi wa mfalme waliomhudumu walimwambia, Mfalme na atafutiwe mabikira vijana wazuri;
Esta 2:3 naye mfalme aweke wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, ili wakusanye pamoja mabikira vijana wazuri wote waende Shushani ngomeni, kwenye nyumba ya wanawake mikononi mwa Hegai, msimamizi-wa-nyumba wa mfalme, mwenye kuwalinda wanawake; tena wapewe vifaa vya utakaso.
Esta 2:4 Naye yule msichana atakayempendeza mfalme na
awe malkia badala ya Vashti. Neno hilo likampendeza
mfalme, naye akafanya hivyo. (Biblia Takatifu BT)
Sasa awaye yote aweza kuona maendeleo kama na inavyotumika kwa Kanisa. Habari ilitumanwa kwa majimbo yote kuwaita wateule na kutayarishwa, wakiwa
mkononi mwa wasimamizi-wa-nyumba ya mfalme. Wateule walipeanwa kwa malkia wa makanisa na wasimamizi waliochaguliwa
kuwaandaa na ndio ulikuwa wajibu wa wachungaji wa Kanisa. Walipaswa
kuwatayarisha wateule ili wajionyeshe mbele za mfalme
(yaani Mungu), bila mawaa wala kunyanzi. Mambo haya hayakufanywa hivyo, ila ilikuwa ndio amri (cf. masomo Usafishaji Na Unyangoni [251]).
Waliondoka nje na kufanya kwa mfuatano kwa muda mrefu na mtu ataweza kuona jinsi kipindi hiki kinavyo kuwa.
Esta 2:5 Basi palikuwa na Myahudi mmoja huko Shushani ngomeni; jina lake Mordekai, bin Yairi, bin Shimei, bin Kishi, wa kabila ya Benyamini; (Biblia Takatifu BT)
Mordekai anavyo vidokezi viwili. Modekai anao msingi, kulingana na maelezo ya kirabbi, ya mera dachya inayomaanisha manemane safi pia ina kidokezi cha moarduk ndiposa kilichokuwa safi kilitumiwa vibaya. Katika hali ya kutajwa visivyo. Kwa hivyo dhana ni kuwa Mordekai alimaanisha manemane safi lakini nafasi yake imetumiwa vibaya. Alikuwa mwaka wa Jairi, mwana wa shimei, mwana wa kishi mbenyamani. Mbari hii inatokeza matatizo mengi Kishi alikuwa babu wa sauli wa kabila la Benyamini, walakini sauli hajatajwa hapa.
Sasa sauli ni mfalme wa Israeli na bora zaidi kuliko kishi. Hivyo mbona sauli haukutajwa hapa? Hivyo ukoo huu hauonekani vizuri. Ni muhimu kuzingatia majina na maana yake. Majina haya yana maana ya kiroho. Tunasoma kinachosemwa na mwafafanusi ya Talmud ni makabiliano ya midrash kwa esta kutoka kwa sincino uk 128
Zingatia 6: Mordekai kulingana na Midrash jina
hili linahusiana na Mera dachya ya kia Arama……………. manemane safi. Kama tu vile
manemani ndiyo kuu kwa viungo vyote vya kutokeleza
chakula ndivyo alivyokuwa Modekai mkuu wa wenye haki katika kizazi chake.
Na sasa tunazungumza kumhusu mfalme wa haki. Torah Temimah
aeleza kulingana na Talmud jina lake lilikuwa
Pelthahia tangu kuzaliwa. Jina Modekai alipewa baadaye.
Kwa kuwa jina hili linasisika kama la wamataifa Talmud
na midrash wanatafuta asili ya kiyahudi kuwajibikia jina hili. Kama ilivyotajwa kwingineko, mwanadamu aliyeitwa yesu kristo katika
kuzaliwa alikuwa Yoshwa au Yehoshwa yenye maana ya haki. Jina yesu limetoka kwa jina kiyunani lesous. Mfumo ulipatikana pia kwa Hyperborean celts, kama utatu wa mungu mwenye asili moja
kama Esus siyo kihebrania bali
ulitumika katika maandiko matakatifu ya wayahudi (Agano la kale kwa kiyunani). Jina la masihi lilibadilishwa. Sasa twende kwa mwana wa Jairi, maanake: mwana aliyeangaza macho ya Israeli kwa sala zake.
baadhi ya wafafanusi wa kirabbi wanasema kwamba hawa watolewa kama mbari ya Mordekai, lakini walikuwa wa mbali yake moja kwa moja, huenda hii ndiyo tafsiri ya kisawa. Ilifanywa hivyo na sababu kumwelekea masihi kama mwana aliyeangaza macho ya Israeli kwa dua zake.
Mwana wa shimei: inamaanisha: mwana ambaye mungu alisikia dua zake. Na mwana wa kishi maanake: mwana aliyebisha kwenye mlango ya rehema. Hii ilitokana na Yesu kristo- Nasimama mlangoni na kubisha. Alikuwa anabisha milango ya rehema ili rehema ienezwe kwa wanadamu wote kupitia kwa Israeli (cf. pia masomo Kristo na Koran (Nam. 163)) kwa maana za AI Tarikh the morning star).
Kwa hivyo majina haya siyo majina tu. Yanamwelekea Masihi na kazi yake. Mordekai ni mfano au chanzo cha Masihi katika Esta. Talmud huchukulia majina haya kuwa na maana ya kimahubiri- Talmud inasema hivyo- wala hawachukui hatua ya kufuatia ambayo ni kuongea juu ya masihi kwa sababu kuna matatizo ya namna zote katika kitabu hiki.
Sababu ya marabbi kutokumchukua Esta kwa mapana yake ni kwamba wanahukumiwa naye. Tunahitaji kufanya sauli. Kama ni
mbari ya Benjamini, Sauli alichukuliwa na Manothi Haleri kuondolewa kwa kusudi
kwani kwa kumhurumia Hagagi alisababisha Hamani kuzaliwa. Sauli ndiye
aliyemhifadhi Hagai Mmaleki, alipoaambiwa na Mungu
amwangamize, na kwa sababu hii Hagagi mwamaleki yu tayari kuangamiza Israeli
wakati wa utawala wa xerxes. Tunasoma katika Samueli, ambapo kitendo cha sauli
kinajitokeza kama kitendo cha huruma kwa mtu mmoja,
bali hiki kina matokeo miaka mamia baadaye, ambayo karibu sana inatokeza
maangamivu ya sehemu ya watu wa Israeli, watu wa uyahudi. Sasa hili
linarudishwakwa usambamba wa huruma inayoonyeshwa kwa
wakanaani na waamaleki katika mfano wa kwanza na karibu utaangamiza watu wetu
mwishowe.
Kabala hatujaingia katika nchi ya ahadi na kuingia umbo la miaka elfu moja, tutapitia katika maangamizi ya karibu, kwa sababu hatukufuta uovu mbali na watu wetu tangu mwanzo. Hatukutii amri za mungu kabisa na hili karibu litaiharibu sayari hii. Hilo ndio wazo litolewalo. Ndiposa hiyo aya ndogo katika 2:5 ni ya maana sana kuliko tu orodha ya majina.
Esta 2:6
ambaye kwamba amechukuliwa mateka kutoka Yerusalemu miongoni mwa wafungwa
waliochukuliwa pamoja na Yekonia, mfalme wa Yuda;
ambaye Nebukadreza, mfalme wa Babeli, alimchukua.
Ni nani aliyebebwa mbali; je ni Mordekai aliyebebwa mbali na Yerusalemu pamoja na mateka, waliochukuliwa pamoja na wayekonia, mfalme wa Yuda? Kama ni hivyo inamfanya kuwa na umri mkubwa. Hivyo tunamwangazia Mordekai mwenye miaka takribani 120 isiyo ya kawaida na tunapenda kumwangazia Zerubabeli alisimamishwa na hekalu kwa takribani miaka 120. Wakati huo tunaongea juu ya maisha ya Musa na pia juu ya mpango wa wokovu ukitumiwa kwa vitu vitatu.
Soncino yasema, jina husika linamwelekea nani; Mordekai au kishi? Hili ni mojawapo ya maswala nyeti katika kitabu cha Esta. Wanadhani yakuwa kishi ni babu wa moja kwa moja katika mbari hii- yaani baba yake, baba ya baba yake , na babu ya baba yake –aliyetekwa na asiye kishi babu ya sauli. Matumizi ya kihebrania yaonekana kana kudai kwamba inamaanisha Mordekai, ila umri wa Mordekai unaleta matatizo. Angelichukuliwa mateka hata akiwa mchanga pamaoja na Yekonia au Yehohakini mnamo 15/16 marehi 597BC (cf. Usomaji wa Sheria Kama Ulivyofanywa na Ezra na Nehemia [250]), angalikuwa na miaka 122 alipofanyika waziri mkuu katika mwaka wa 12 wa kutawala kwake Xerxes mnamo 474BC. Bila shaka alifurahia utumishi wa muda muzuri baadaye tokea 10:2. Ugumu huu umewaongoza wengi kutambua Ahasuero na Kambisesi, Dario au mmoja wa wafalme wa kwanza wa uajemi. Wengine wanalielekeza jina husika kwa kishi, ambaye basi angekuwa babu wa karibu wa Mordekai, babu wa babu yake wala si kishi wa kitabu cha samueli. Wahubiri wengi hufikiri kwamba “kuchukuliwa mateta” humanisha tu kwamba babu zake walitekwa na Nebukadrezza naye aliishi matekani kwa sababu ya kutekwa. Marabbi hata hivyo, waamwandikia Mordekai umri mkubwa zaidi isivyo kawaida, alikuwa mshiriki wa baraza kuu la makuhani manamo ilipokuwapo hekalu la kwanza naye aliishi kuona hekalu la pili kulingana na Yoseph ibn Nachmiash. Hivyo wanazungumzia mbari ya kudhania na kipindi cha wakati wa watu hawa. Bila shaka tunaangazia dhana ya vipindi vya umri ilioenea, vinayvohusiana na maisha ya musa, ujenzi wa hekalu na urejeshio wa watu na haya yote yanaangazia juu ya miundo ya wakati, inayohusiana na sikukuu za ukumbusho wa miaka pamoja na mpango wa wokovu.
Esta 2:7
Naye alikuwa amemlea Hadasa, yaani, Esta, binti wa
mjomba wake, kwa kuwa hana baba wala mama. Naye msichana huyu alikuwa wa umbo mzuri na uso mwema; nao walipokufa baba yake na mama
yake, yule Mordekai alimtwaa kuwa binti yake yeye. (Biblia Takatifu BT)
Marabbi wanajaribu kulikoroga / kuchanganya kidogo na kusema kwa kweli alimwoa. Sivyo inavyosema. Taratibu hii yote ni kwamba Hadassa alitayarishwa na kukuzwa kama binti wa mjomba Mordekai. Esta kama na alivyitwa baadaye, alikuwa binti ya mjomba wake na mjomba wa mwana wa wayahudi wa mbari ya Daudi naye alikuwa binti wa Israeli. Hili linatuambia kwamba tunaangazia dhana inayoenea mbele ya yuda. Kuna mambo kadhaa kumhusu Hadassa au Esta. Hadassa ni jina la kihebrania kulingana na mafafanusi ya soncino na Esta ni jina la alilopewa na mataifa. Hadassa limetoka kwa neno la kihebrenia myrtte na Esta linatoka kwa stara la kiajemi (yaani star from Meg. 13a) (ustara ni Ista linatoka kwa stara au mungu mke Easter mungu mke wa Ostarrichi au modern Australia tangu 996CE). Kulingana na wengine ni sayari venus (Rashi, Arush). Hivyo jina hili hutumika kama mwezi ama venus. Hii si ajali Kanisa linaitwa nyota ya asubuhi na Kanisa ni mwezi, unaozidi na kupungua na linaloelewa kwa mwana aliye Kristo. Ndio saba majina haya yanatumiwa.
Nyota ndiye Masihi ajaye hasa kutoka Israeli na kutoka kwa simba wa Daudi, lakini linapewanwa kwa Kanisa kusudi wawe wawili pamoja na mwezi na washiriki katika Nyota ya Asubuhi, iliyo uongozi wa sayari. Hiyo ndiyo maana yake
Esta 2:8 Basi ikawa, wakati iliposikiwa amri ya mfalme na mbiu yake, wasichana wengi wakakusanyika huko Shushani ngomeni mikononi mwa Hegai; Esta naye aliingizwa katika nyumba ya mfalme, mikononi mwa Hegai mwenye kuwalinda wanawake.
Esta 2:9 Yule mwanamwali akampendeza, akapokea fadhili kwake; naye akampa upesi vifaa vya utakaso, pamoja na posho zake, na vijakazi saba walio haki yake, wa nyumbani mwa mfalme. Pia akamhamisha yeye na vijakazi wake akawaweka mahali pazuri katika nyumba ya wanawake. (Biblia Takatifu BT)
Vilainishi hapa vinamaanisha chakula mwafaka. Kutoka kwa Soncino si virembesho bali ni chakula haswa kilichokuwa sehemu ya matayarisho (Tz Dan. 115), Neno la kihebrania ni sawa na lile la sehemu ya chakula katika 9119, 22 kulingana na ibn Ezra). Maelezo ya sehemu ya vilainishi ni kwamba walipewa vayakula maalum na hivyo kutayarishwa. Chakula bila shaka ni neno la Mungu na ujuzi wa sheria kwa njia ya Roho Mtakatifu.
Hoja inayofuatia inahusiana na wajakazi saba aliopewa na mfalme kutoka nyumbani mwake.
Ndipo kukawa na wajakazi saba waliopeanwa kwa Kanisa na hao wajakazi saba wa makanisa chini ya roho saba za Mungu, malaika saba na makanisa ya Mungu, “Nyumba ya wanawake” ni matumizi ya kanisa au utendaji wa kidini wa Israeli.
Esta 2:10 Walakini Esta hakudhihirisha kabila yake wala jamaa yake, kwa maana ndivyo alivyomwagiza Mordekai asiwadhihirishe.(Biblia Takatifu BT)
Sehemu kubwa ya Kanisa, Israeli hubakia kufichwa hadi siku za mwisho. Haijafahamika vyema. Kwa maana Mordekai amemwonya asiseme. Utaratibu huu wote siri za Mungu. Kuna mambo kadha wa kadha ya Kanisa yaliyofichwa kama sisri. Baadhi ya mafafanusi yanavutia sana kuhusiana na wajakazi saba kisha majina. Marabbi wanaeleza kutoka kwa Meg. Ba kwamba pamoja na wajakazi hawa angehesabu siku za juma hili ili kubainisha ni lini Sabato ingeanguka. Rashi anaeleza kwamba alimpanga majakazi mmoja kwa kila siku ya juma na alipofikiwa Yule wa sabato mara aonekanapo yuajua yeye kwamba sabato imekwisha ingia. Wanaigeuza hiyo kwa matumizi ya msingi wa kijuma. Wana chanzo/kifunguo ila hawaufungui mlango. Ufunguo huu ni kwa urejesho wa Sabato ya miaka elfu; kwa pumziko la Sabato ya Kristo, bali hawaiendelezi katika hali ya kimasihi.
Wahubiri huelezea maandiko mengine katika
Biblia kimasihi bali Esta hajaelezewa kimasihi
tunakuja kwa wazo la kanisa na kuondolewa kuhusiana na Esta kimasukudi.
Tunapopitia hayo, ‘alimwonya asiseme’ Mordekai sharti alifikiria kitu kama hiki. Esta angechaguliwa kama Malkia, ni kwa sababu tu
Mungu angetaka kumfanya chombo cha kusudi lake. Hiyo ni sawa Mungu alitaka kumfanya Esta, Kanisa, chombo cha
kusudi lake. Basi akifichuwa ukweli kwamba yeye ni
Myahudi, hivyo basi mhusika katika watumwa, atakejeli uteuzi wake na kwa hiyo,
uwezekano wa kufanyika chombo cha Mungu (kilingana na Ralbag, Tz sinano). Ndiyo
sababu siri za Mungu zilifichwa, kwani zingeelezewa na
kufunuliwa mapema kanisa lingetengwa nasi tungeuwawa. Basi
siri za Mungu zililificha kanisa hadi siku hizi za mwisho. Siri za Mungu
zinafichuliwa tu katika siku za mwisho ndiposa kanisa lisikejeliwe hadi lifikie
hali hii na idadi kamili ya wateule kuondolewa na
kuhifadhiwa. Ndiyo kazi yake. Ufafanuzi
huu unadokezewa katika Midrash. Alifikiria iliwezekanaje huyu mjakazi
mwenye haki aolewe kwa mtu asiye Mwisraeli. Huenda ni kwa sababu msiba mkuu ungewatokea Israeli naye
angewaokoa. Wanaelewa hili! Hii ni wazi kama kengele,
bali hawachukui hatua ya kufuatia. Ufiche huu mara zote umelaumiwa, kwamba ni vyema kunakili baadhi ya maelezo mengine mengi yake.
Rashi anaeleza kwamba hakutangaza asili yake ya kifalme( yaani alizaliwa kwa jamaa ya mfalme Sauli) ili mfalme afikirie kwa alikuwa kutoka jamii maskini na amfukuzie mbali. Ndivyo mawazo yao yalivyo. Walakini sivyo; hili lilifanyika hivyo ili kuwahifadhi wateule.
Esta 2:11
Na yule Mordekai akawa akitembea kila siku mbele ya ua wa
nyumba ya wanawake, ili ajue hali yake Esta, na hayo yatakayompata.
Hivyo ndivyo Kristo anavyoenda mbele ya kanisa kila siku ili azidi kuliangalia na kulilinda. Analileta kwake Mungu bila mawaa.
Esta 2:12 Basi ilipowadia zamu yake mwanamwali mmojawapo aingie kwa mfalme Ahasuero, hali akiisha kufanyiwa sawasawa na sheria ya wanawake miezi kumi na miwili; yaani, ndivyo zilivyotimia siku zao za utakaso, miezi sita kwa mafuta ya manemane, na miezi sita kwa manukato na vifaa vya utakaso wa wanawake;
Jina Mordekai limetokana na wazo la manemane safi naye Roho mtakatifu ameelekezwa kwa njia ya Kristo li kuwakuza wateule. Na ndiyo sababu wakapewa mafuta kwa miezi sita ya manemane halafu manukato mengineyo chini ya uongozi wa Kristo na jeshi.
Esta 2:13 mwanamwali huingia hivyo kwa mfalme; kila akitakacho hupewa kwenda nacho kutoka katika nyumba ya wanawake ili kuingia katika nyumba ya mfalme. (Biblia Takatifu BT)
Haya matayarisho ya wateule kwa muda ni kwamba mtu apate kusafika na wazo la utakaso na matayarisho yanafanywa katika hali ya kuendelea, pia kuna dhana nyingine katika siku hizi kutoka Abibu (Nisani) hadi Adari kwa sababu utaratibu hufuatia amri kutoka Nisan ya 13 hadi Adari ya 13, jinsi tunavyoona. Huanzia mwanzo wa mwaka mtakatifu na kumalizikia mwisho wa mwaka mtakatifu; hii siyo ajali. Maagizo haya yote yalifanyiwa ili kuikuza utaratibu wa wazo la mpango wa miaka elfu. Wakati utakapowadia wa wateule kwenda nyumbani mwa Mfalme, watapewa yote wanayoyatamani. Roho Mtakatifu ndiye wa kutamaniwa kuchukuliwa na watakatifu.
Esta 2:14 Huenda jioni, na asubuhi hurudi nyumba ya pili ya wanawake, mikononi mwa Shaashgazi, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda masuria. Wala haingii tena kwa mfalme, isipokuwa amempendeza mfalme, naye akaitwa kwa jina. (Biblia Takatifu BT)
Sasa hiyo ni kanuni ndani mwake. Kulingana na Soncino na mafafanusi nyumba hii ya pili ya wanawake ndiyo wangebakia ndani kwa maisha yao yote kwa ujane halisi. Hawangeruhusiwa kwenda ulimwenguni na kuolewa baada ya kuunganishwa na Mfalme. Ibn Ezra asema; Na baada ya mmoja kupatana na Mfalme-mara apewapo Roho Mtakatifu harudi tena kule nje ulimwenguni. Tunafungiwa. Sisi tu bibi-arusi aliyewekwa tayari kwa Kristo wala hatuendi tena kule nje ulimwenguni nasi hatuyachafui mavazi yetu. Wayahudi wanafahamu hivyo wala wengine wetu hatuelewi.
Esta 2:15
Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai,
ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila
vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona.
(Biblia Takatifu BT)
Uzao wa Esta ulijulikana hapa kuwa wa Abihaili, na hapo mwanzo ilisemekana hakuwa na baba wala mama. Hali ya kwanza ni uelekevu kwamba ni kweli wateule hawana kizazi au jamii. Ukuhani wao si ule wa Haruni, ni ule wa Milkizedeki. Hii yahusu Wahebrania. Wateule hawana baba wala mama. Hawahitaji kuwa makuhani kwa mfano wa Haruni. Hawahitaji kutoka kwa ukoo wa Haruni, hawahitaji kuwa wa kohanimu. Wao ni sehemu ya ukuhani wa Milkizedeki daima. Hivy ingawaje tuko na ukoo hatuna ukoo kwa kusudi la ukuhani.
Esta alipoingia kwa mfalme hakuhitaji kitu. Alisema alitosheka na kule alichokuwa nacho. Yote anipayo yatosha. Hakupungukiwa na kitu. Yote tupewayo kwa wokovu wetu tuwe sehemu ya wateule kama makuhani wa Mungu na sehemu ya ukuhani wa Milkizedeki tunapewa na towashi, na malaika wanaosimamia makanisa. Tumejiandaa na kufanywa tayari na hili lihitaji bidii yetu. Tumepewa kila tunachohitaji. Jinsi ya kujitayarisha wenyewe ni funzo. Tunayoyafanya katika juma nyumbani ni juu yetu. Tusiposoma hatutakuwa tayari nasi tutapungukiwa. Hatuna wakati wa kupoteza kwa masabato, tukipuuza mwendo wa taarifa. Tunapaswa kufanya kazi.
Esta 2:16
Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero, katika
nyumba ya kifalme, mwezi wa kumi, ndio mwezi wa Tebethi, mwaka wa saba wa
kumiliki kwake. (Biblia Takatifu BT)
Maana ya mwezi wa kumi Tebeti, katika mwezi wa saba wa utawala wake haifahamiki vyema. Kulingana na maelezo, majina ya miezi katika kitabu cha Esta ni yale yaliyorithiwa na Wayahudi katika Babeli na bado yanatumika (Yerushalmi Rosh Hashanah 1:2). Hii ilionekena katika mwaka wa saba muda mfupi baada ya kurudi kwake kwa aibu kutokana na ushidi katika vita vya kiyunani. Hivyo utaratibu ulikuwa msingi wa kukabili vita pamoja na kushindwa. Inaonekana kuwepo mfuatano wa wakati, ambao unaweza au usiweze kuhusiana na Biblia, walakini swala hili linahitaji uchunguzi zaidi.
Esta 2:17 Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti. (Biblia Takatifu BT)
Hilo basi ndilo jibu. Wateule hufanywa malkia badala, mahali pa Israeli wa kale pamoja na ukuhani wa Haruni.
Esta 2:18 Ndipo mfalme alipowafanyia karamu kubwa maakida wake wote na watumishi wake, yaani, karamu yake Esta; akafanya msamaha katika majimbo yote, akatoa zawadi sawasawa na ukarimu wa mfalme. (Biblia TAkatifu BT)
Na hii ndio mankuli ya ndoa ya mwanakondoo
Esta 2:19 Basi mabikira walipokusanyika mara ya
pili, Mordekai alikuwa akiketi mlangoni pa mfalme. (Biblia Takatifu BT)
Kuanzia 18, karamu ya Esta ni ile inayoitwa katika sherehe ya arusi ya Mfalme na Esta (Kutoka Lekach Tobi). Kufunguliwa kulingana na Talmud, ni kwamba Ahasuero aliyafungulia majimbo yake yote kutokana na ushuru kwa heshima ya Esta. Alitumai kwamba kwa heshima hii angefichua ukoo wake na watu wake. Ukweli ni kwamba kufunguliwa kulipitia kwa kanisa. Hii ni mara ya pili. Soncino inazungumzia fungu la 19 hili ni mojawapo ya maneno kaitka kitabu hiki, lililo gumu mno kulielewa. Mbona kukutanika kwa mara ya pili kwa wanawali.
Kulingana na tafsiri ya Kirabbi kusudi lake lilikuwa kuamsha wivu wa Esta na kwa hivyo achochewe kutangaza ukoo na mwanzo wake. Wengine hudokeza kwamba hawa ndio wanawali ambao hawakupatana na mfalme waliokusanywa toka mahali walikowekwa na kupelekwa nyumbani (Yosef Lekach). Wengine hueleza kwamba hawa wajakazi walikuwa wasichana waliokusanywa ili wamhudumie Esta nyumbani kwake. Ilikuwa desturi kuchagua watu wapya wakumhudumia Malkia mpya. (kutoka kwa Rokeach). Katu haimaanishi hivyo. Kusanyiko la pili ni la wanawali. Mmoja ndiye mteule, aliyetengwa na kuolewa na hili hufanyika katika Pentekoste.
Kipindi cha makanisa saba kilipokua kila mmoja wetu alijiondoa na wakati wa pili ni mankuli ya ndoa ya mwanakondoo atakapokuja tena Masihi na kutukuza. Mankuli ya ndio yenyewe yako katika sehemu mbili. Wanasema kwamba hawa ndio wanawake walioenda nyumbani. Huo ni mfano wa wanawake werevu na wapumbavu unaorudiwa hasa katika maelezo ya marabbi. Kuna baadhi ya wanawali waliotumwa nyumbani kisha wakarejeshwa. Hili halimfanyi Esta, ambaye ni Kanisa kuona wivu. Hawa ni masalio tu wa kanisa wanaoingizwa ndani kama wanawali wapumbavu katika ufufuo wa pili. Kuna ndoa mbili; kuna fufuo mbili na nafasi mbili anazopewa Yesu Kristo chini ya Mungu. Na ndiyo sababu hawawezi kuelewa, kwani hawaelewi kazi ya wateule, nao waisema. Wanaelewa kwamba mambo haya yalihusiana na mafungu wawili ya wanawali na yanahusu kazi mbili, ila katika Kanisa halieleweki hata. Inaonekana kwamba Yuda hawezi kukifungua kitabu hiki hadi siku za mwisho. Ufahamu wa Yuda wa kitabu hiki unaonekana kuwa kazi ya ujumbe wa Malaika wa kwanza kabla ya uharibifu wa muundo wa kibabeli na malaika wa pilli na siku za mwisho za mnyama katika ujumbe wa malaika wa tatu (Ufunuo 14:6-10) (Taz. Masomo haya Ujumbe wa Ufunuo 14 (No. 270).
Mordekai anakaa langoni mwa mfalme. Mafafanusi ya kirabbi yasema maana yake ni lango kuu lililojengwa kwenye handaki ya jumba la mfalme. Malango sawa na hayo yametumika mara zote kule mashariki kama mahakama ya haki na mahala pa kukutania kwa majadiliano na kubadilishana mawazo.
Yalikuwa mabomba ya vijiji vya mashariki kulingana na Midrash. Esta anamuusia Ahasuero kumhusisha Mordekai kama msiri wa kifalme kuandamia hakuhani wa wafalme waliotangulia, walipompendekeza Danieli kwa nafasi hii. Kwa nini Kristo akafanya Masihi? Ni kwa ajili yetu. Mungu alimteua Kristo na kumtenga kama kuhani mkuu naye akatufunulia siri za Mungu. Hii ina maana kwamba Kristo aliketi langoni pa Mfalme kwa ajili ya wateule.
Esta 2:20
Esta alikuwa hajadhihirisha jamaa yake wala kabila yake, kama
vile Mordekai alivyomwagiza; kwa maana Esta alikuwa akiyashika maagizo ya
Mordekai, vile vile kama wakati alipolelewa naye. (Biblia Takatifu BT)
Tunatii amri ya Yesu Kristo. Mafafanusi ya Kirabbi yanasema Esta hakuwa ametambua ukoo wake; kusudi la mwingilio wa maneno hayo mahali hapa, ilikuwa kujulisha wazi kwamba Mordekai hakujulikana kama mkoo wa Malkia, na hivyo maadui hawangemkabili. (Yalkut Me'am Lo'ez). Marabbi wanelezea kwamba pamoja na juhudi za Ahasuero za kuamsha wivu wake, esta bado hakutambua ukoo wake. Ukweli wa mambo ni kwamba mahusiano kamili ya wateule hayajulikani katika siku za mwisho na yanafichwa makusudi wala marabbi hawaelewi maelezo haya. Walakini wanafikia swala moja Inaonekana tu jinsi wanavyofikia karibu kisha wanageukia mbali na miisho.
Esta 2:21 Ikawa siku zile, Mordekai alipokuwa akiketi mlangoni pa mfalme, wawili katika wasimamizi wake mfalme, Bigthana na Tereshi, wangoje mlango, walighadhibika, wakataka kumpelekea mikono mfalme Ahasuero. (Biblia Takatifu BT)
Tunazungumza juu ya maasi ya jeshi. Tunasema kuhusu wawili wa makerubi walioasi. Hawa wanaangaziwa katika shetani na Aeoni; muundo wenye kichwa cha simba.
Esta 2:22 Basi Mordekai akapata kulijua jambo hilo, naye akamjulisha Esta, malkia; naye Esta akamwambia mfalme habari hiyo kwa jina la Mordekai.
Esta 2:23 Na jambo hilo lilipochunguzwa, na
hakika ikapatikana, hao wote wawili wakatundikwa juu ya mti. Hayo
pia yakaandikwa katika kitabu cha taarifa mbele ya mfalme. (Biblia
Takatifu BT)
Kwa maneno mengine waliondolewa katika kitabu cha uzima cha mfalme. Walilaaniwa. Yeye aangikwaye mtini amelaniwa. Hiyo ndiyo dhana husika. Waliondolewa kazini.
Esta 3:1 Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimwongezea cheo Hamani bin
Hamedatha, Mwagagi, akampandisha, akamwekea kiti chake juu ya maakida wote
waliokuwapo pamoja naye. (Biblia Takatifu BT)
Hili linaturudisha kwenye wazo la kupandishwa cheo kwa watumishi wa Shetani, Hamani na waamaleki, nguvu au majeshi ya dunia ambayo kwa kweli ni Hamani mwenyewe-Hamani anfanyika adui wa kutambulika. Ndiposa tunao wazao wa adui na adui kufanyika mhusika. Mfalme wa Tiro alikuwa sawa na Shetani. Ndiposa hapa Hamani anakuwa adui na tutaona hapo baadaye, anavyokuwa adui na anahusiashwa kama adui katika fungu hili.
Esta 3:2 Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia.
Wazo hili basi litatupeleka hadi vita vya nyikani, Kristo alipokabiliwa na shetani naye akakataa kuinama na kumwabudu shetani, ingawaje uongozi wa sayari umekabidhiwa shetani. Shetani ndiye aliyekuwa nyota ya Asubuhi ya Sayari alikuwa kiongozi wa dunia kutoka Waefeso 2:2 (cf 2Wakorintho 4:4) ila Masihi kama Mordekai ulitumwa alitumwa na Mungu ili apambane na Shetani, naye akapokea uongozi wa Sayari kwa shughuli zake. Kutoshindwa kwake na shetani kuonyesha katika mawazo husika hapa.
Esta 3:3 Basi watumishi wa mfalme walioketi
mlangoni pa mfalme wakamwambia Mordekai, Mbona wewe waihalifu amri ya mfalme?
Esta 3:4 Ikawa, waliposema naye kila siku
asiwasikilize, wakamwarifu Hamani, ili kuona kama
mambo yake Mordekai yatasimama; maana alikuwa amewaambia ya kuwa yeye ni
Myahudi.
Esta 3:5 Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana.
Esta 3:6 Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai.
Esta 3:7 Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari.(Biblia Takatifu BT)
Walipiga puri, kura, hili lina maana ya kidini. Sio shughuli ya kupingana kwa fedha. Kupiga kwa kura kulikuwa zoezi la kidini nao walipiga kura dhidi ya watu wa Mordekai. Walipiga kura dhidi ya kanisa na huu ni mpangilio uliondelea kuanzia Abibu (NIsani) hadi Adari, kwa mwaka mtakatifu wote. Kila mwezi wa mwaka mtakatifu walipiga kura; walikuwa kwa mashambulizi ya kiroho kuamua ni lini wangeangamizwa.
Esta 3:8 Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.
Ndivyo na mamlaka hii, iliyowekwa chini ya nguvu za Mungu, na mamlaka yote hutoka kwa Mungu, inaombwa kuwafagilia mbali wateule. Maelezo mengine yanahitajika juu ya kupiga kura na sheria mbali mbali kulingana na mafafanusi ya kirabbi. Soncino inasema juu ya “Puri” kwamba hakukuwa na neno kama kura. (Puri) limetokana na waajemi, lakini katika Accadiani Puri ndiyo kura hasa, kwa kawaida vipande vya mbao ambavyo mwaguzi angevipiga mbele ya mwenye kuuliza na kuamua wakati wa heri wa tukio kwa dalili zinazokuja juu ya vile vipande vya mbao (Daath Mikra). Vipande kama hivyo vilipatikana katika magofu ya jumba la Suza. Kila moja ilikuwa na upana wa 1cm x 4 1/2cm kwenda juu. Hata idadi ilionyesha jawabu kamili na vile visivyo vya kawaida havikuwa kamili (Soncino Marcus). Sasa wanaonekana walienda siku kwa siku na mwezi kwa mwezi. Hamani anaonekana alifuata utaratibu huu wa kujaribu kupiga kila siku kwa miezi yote. Kwa maneno mengine basi kuna utaratibu wa kuendelea kushambulia siku kwa siku na mwezi hata mwezi, uliofuatwa mapema. Wakati unaonyesha kwamba uliweka tangu mwanzo.
Hamani alishangilia akisema, “kura yangu imeangukia mwezi ambao Musa alikufa”, wala hakujua kwamba Musa pia alizaliwa katika mwezi wa Adari kutoka Tamuld. Wazo hili lina maana kwa hoja waliyojaribu kufanya kuhusu kifo cha Musa. Uharibifu wa Israeli unahusiana na kifo cha Musa kwa sababu Israeli wataanzisha sheria chini ya Masihi na Musa alikuwa taswira ya sheria kama chombo chake.
Shetani, kwa miundo ya kidunia anawakilishwa na waamaleki, alijaribu kuiharibu Israeli tangu wakati wa Musa. Musa alikufa katika kile kipindi cha mwisho kabla hawajaingia katika nchi ya ahadi na Israeli wakaomboleza kwa siku 30.
Kwa hiyvo tunazungumza kuhusu kura ya kifo cha Israeli na utaratibu wa kimasihi. Siku za mwisho 30 ni vita vya waamaleki ili kuangamiza Israeli. Kanuni zilikuwa kwamba maangamizi yaliimarishwa na kura, na katika siku za mwisho, kuna jaribio kuangamiza Israeli. Kutokana na upotovu wa ufahamu wa maisha na unabii. Mafafanusi ya Marabbi yanamzungumzia Hamani, juu ya watu Fulani waliotawanyika ng’ambo kama uchongezi. Chuki yake kwa Mordekai iliuwa kama uchongezi kwa Wayahudi wote, hivyo kwa maneno mengine, wateule wangeuawa kwa sababu ya Mordekai. Hii ni chuki kwa ufalme wa Masihi inayosababisha tendo baya juu ya wateule. Bila masihi hakuna hitaji kwa wateule, na bila ufalme mpya pamoja na kibadala. Tamuld inasema kuhusu Hamani kwamba hakuna aliyefahamu vizuri kuliko yeye jinsi ya kuchongea. Mmoja tu ndiye muhtasari wa uchongezi naye ni Shetani. Ndiye muumbaji wa mashtaka yanayoibuka na hizi ndizo dhana zinazoangaziwa. Wazo hapa kwamba sheria zao ni tofauti linahusu mwenendo wa watu chini ya sheria, ambayo ni tofauti sana na sheria ambazo Shetani aliweka kuiendesha sayari. Tunalo wazo la upotovu katika sheria na kwamba mashtaka yanafanywa kwamba watu hawa wako chini ya sheria tofauti kuliko ile itokanayo na shria ya Mungu. Hamani anasema watu hawa hawatatii sheria zilizowekwa na Mordekai ametoa, ukipenda, utaratibu wa sheria. Kwa usawa zaidi, Israeli, ikifuatiwa na Wayahudi wamepewa utaratibu wa sheira na malaika wa uwepo, unaotokana na asili ya Mungu, na bila shaka ni tofauti na ulimwengu unaozunguka. Ni taarifa ya kweli wala si mashtaka ya hukumu.
Esta 3:9 Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme.
Malipo haya ni ya kushtua sana kwa kiasi chake. Talanta elfu kuni za fedha zilikuwa sawa na pauni million tatu na elfu mia sita maelezo yanayohusu hii hesabu ni kwamba, yenye thamani mara nyingi kuliko leo hii, ikiwiwanishwa na ukubwa wa thamani ya pesa ilisawazishwa na thamani ya ushuru wa mwaka wa fedha ya ufalme wote wa Uajemi kulingana na Herodutus. Pengine Hamani alitarajia kupata hii yote kwa kuwanyang’anya wayahudi waliotarajia kuwaangamiza. Na ndiyo sababu alitarajia kuwafanya chambo kwa kuwaharibia mbali. Pia ingewezekana alipe kiasi hiki kutoka kwa mali zake, kwani alikuwa mashuhuri kwa mali na utajiri (Kulingana na Ralbag). Marabbi pia wameibuka na usawa wa wingi wa pesa kwa usawa wa 165, ambao ni muundo wa kihesabu wa miti ya kuwanyongea watu waliohukumiwa kisheria, ndipo kungekuwako uzito wa kisawa kwa maangamizi ya watu. Uchunguzi wa Marabbi huenda ukang’amuliwa kwa hesabu na wingi wa idadi kwa mifuatano.
Taz. pia
http://www.ccg.org/domain/holocaustrevealed.org/.
Esta 3:10
Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa
Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi.
Hivyo pete hii ilikuwa muhuri wake. Soncino anasema ‘urithi ambao kwao Hamani alipewa mamlaka yote kufanya kwa niaba ya mfalme.Alikuwa na mamlaka ya kufanya kwa niaba ya Mfalme na baadaye haya pamoja na kazi yahamishwa kwa Mordekai. Pete ya muhuri alipewa Shetani, naye Mungu. Alipewa uwezo juu ya Sayari hii, alifanywa Mungu wa dunia hii (Theos au Elohim).
Esta 3:11 Kisha mfalme akamwambia Hamani, Hiyo fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo vema.
Amerudishiwa fedha. Mfalme alimrudishia fedha yake.
Alisema umewapata na fedha unazo, watendee unavyoona vyema kwako. Angaliichukua fedha angewauzia hao watu. Malipo hayo hayakukubaliwa. Hii ilikuwa hukumu naye akampa fungu Hamani, Shetani ili kuonyesha matokeo, Mungu alimhukumu Shetani kwa jinsi alivyowatendea watu. Ndioyo sababu pesa hazikuchukuliwa katika hadithi hii. Mungu pia alimpa Shetani watoto wa Ayubu na Kurusu kuangamizwa kwao kwa matumizi ya siku kuzaliwa kwao kama sanamu chini ya taratibu za Assyro-Babeli (cf masomo Siku za kuzaliwa (Nam. 287). Hapa katika hadithi, wafafanusi wa kirabbi husema kwamba Ahasuero sawa na Hamani aliwachukia wayahudi kimakusudi alifikiria katika mistari hii waweza tu kujihifadhia fedha hizi na ufanye yakupendezayo. Walakini kiroho sivyo ilivyo.
Esta 3:12 Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa,
siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani
alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila
jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa
lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete
yake.
Esta 3:13 Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara.
Kwa hivyo tuna kanuni ya kupga kura, wamepitia kila siku ya mwaka mtakatifu wala hawakupata
kura ya kuwapendelea. Na bado ilitengwa kwa kura
kwamba ilikuwa ni mwisho wa masiku; mwisho wa mwaka mtakatifu kwenye siku ya
kumi na tatu ya mwezi maangamizi yangetekelezwa. Hivyo utaratibu wote umetengwa
tangu mwanzo wa ulimwengu kwamba watu hawa wasitufikie
mpaka siku za mwisho na hiyo ndiyo dhiki na muhuri wa 5 (cf pia Outline Timetable of the Age (Nam. 272)
na Significance of the Year 2000 (Nam. 286)).
Esta 3:14
Nakili ya andiko,
ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa
mataifa yote wawe tayari siku ile ile.
Esta 3:15 Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni.
Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji
wa Shushani ukafadhaika.
Shushani uliwa mji wa
kale uliotangulia Wamedi na waajemi (ona gazette Kuanguka kwa Misri: Unabii wa
Mikono Iliyovunjika ya Farao [036] Phase 1 - Part 1 & 2). Soncino anasema kwamba maneno mfalme pamoja na
Hamani waliketi chini kunywa ndicho kipande mwafaka cha kinyume ya wazi. Amri
zimetolewa kuwaangamiza wanadamu maelfu makumi, na
huku mfalme na mwandamizi wake mkuu kwa ukatili wana furahia karamu (Dera Pashra)
Esta 4:1 Basi Mordeikai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja na majivu, akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.
Esta 4:22 Pia akafika hata mbele ya mlango wa mfalme;
maana hakuna awezaye kuingia ndani ya mlango wa mfalme hali amevaa magunia.
Mtu hangeweza kwenda langoni pa mfalme na mavazi ya magunia. Mordekai alisimama kwa niaba ya wateule na kujinyenyekeza. Alivalia vazi la kibinadamu. Alijifanya mwanadamu na kujinyenyekeza hata mauti. Hii ni hadithi ya Masihi. Hakuna awezaye kwenda mbele ya lango la mfalme. Hakuna awezaye kwenda mbele za Mungu kwama mwanadamu. Haiwezekani kumwona, au kumkaribia kwa sababu vazi, dhambi na utu wa kufa inatufanya tusifae. Mungu ni Roho na haiwezekani kumwona asemavyo Paulo katika 1 Timotheo 6:16: Mungu tu amevaa kutokufa hakuna mtu aliyemwona au atakayemwona Mungu Yohana 1:18 pia inasema; hakuna mtu awaye yeyote aliwahi kumwona mungu.
Esta 4:3 Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu.
Esta 4:4 Basi wajakazi wake Esta, na wasimamizi wake wa nyumba, wakamjia, wakampasha habari; naye malkia akahuzunika mno; akampelekea Mordekai mavazi, ili kumvika, na kumwondolea gunia lake; walakini yeye asikubali.
Esta 4:5 Kisha Esta akamwita Hathaki, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa mfalme, aliyemwagiza amhudumu Esta, akamtuma kwa Mordekai, ili ajue mambo hayo, na maana yake ni nini.
Esta 4:6 Basi yule Hathaki akatoka nje kumwendea Mordekai kwenye uwanda wa mji ulipo mbele ya mlango wa mfalme.
Esta 4:7 Naye Mordekai akamweleza yote yaliyompata, na hesabu ya fedha Hamani aliyoahidi kulipa katika hazina ya mfalme, ili Wayahudi waangamizwe.
Kumbuka Kristo alimwambia Petro kwamba shetani alimwomba amchekecheke. Shetani alikuwa na uwezo wa kuwatenda wateule. Kristo anamwambia Petro kwamba Shetani alimwomba Mungu kwamba apewe Petro ili apate kumpepeta na kumlainisha na kumshughulikia, hivyo kumwonyesha hatoshi. Hilo linatudhihirishia kwamba Shetani sio tu kitu. Anao uwezo wa kumfikia Mungu na ni mshtaki wa ndagu zetu naye Kristo anasimama mahali petu. Anasema watu hawa Mungu amempa watafanya kazi hii naye anaweza kuwapata watu hawa huko. Shetani anasema hapana hawezi, watu hawa hawafai kuongoza na kuwa sehemu ya muundo. Ubishi ni kuhusu hilo. Wako mbali mbali na hawapaswi kuwa miongoni mwa muundo. Mungu anaeleweka visivyo. Uasi ulikuwa juu ya hayo tu mahali pa kwanza.
Esta 4:8 Pia akampa na nakili ya andiko la mbiu ya kuwaangamiza, iliyotangazwa
Shushani, ili amwonyeshe Esta, na kumweleza; tena amwagize aingie kwa mfalme,
kumsihi na kuwaombea watu wake.
Huu ndio wajibu wa Kanisa. Tunapaswa kujitayarisha wenyewe kwenda mbele za kiti cha neema kwa ujasiri. Wazee ishirini na wane wa Ufunuo 4 na 5 wamepewa majukumu ya kuchunguza maombi yetu katika mabakuli ya dhahabu. Wanayaweka mbele za Mungu nasi ndo tunawaombea watu wetu. Tunapokoma kuwaombea watu wetu wataharibiwa.
Esta 4:9 Basi Hathaki akaja, akamwambia Esta maneno ya Mordekai.
Esta 4:10 Ndipo Esta akasema na Hathaki, akamtuma tena
kwa Mordekai, kusema,
Esta 4:11 Watumwa wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu ye yote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini.
Wazo hili ni mwito wa wateule. Hatuwezi kuingia mahali patakatifu pa patakatifu ispokuwa tumeitwa na tukienda hapo pasipo kuitwa tutakufa. Hiyo ndiyo adhabu iliyowekewa kwa Israeli. Ni Haruni tu aliyeruhusiwa kuingia na mara moja tu kwa mwaka naye alifanya upatanisho kwa ajili ya watu wa Israeli. Tumeitwa na kuchaguliwa na kuteuliwa na kutayarishwa, nasi tunaweza kuiingia patakatifu pa patakatifu kwa misingi ya kisiku ili kuwaombea watu. Hata hivyo sharti tujitayarishe na mavazi yetu yasipofaa na tukiwa hatuko sawa kiroho na tuende mbele ya Mungu tutakufa. Wale walao pasaka isivyofaa pasipo kuuelewa mwili watakufa wakati mwingine kihalisi (1 Wakorintho 11:28-32)
Esta 4:12 Basi wakamwambia Mordekai maneno ya Esta.
Kipindi cha siku 30 tunachopata katika mafungu hazikosi maana. Kulikuwa maombolezo ya siku 30 kwa ajili ya Musa, ambayo yalihusiana na siku za mwisho.
Kristo hakufaa kuingilia na
kutayarisha neno la Mungu na kutangaza ujumbe hadi alipotimiza miaka 30.
Alihubiri miaka mitatu wakati wa huduma ya Yohana
mbatizaji na miaka miwili katika huduma yake mwenyewe (cf masomo Kupima Wakati wa Kusulubiwa na
Kufufuka [159]).
Esta 4:13 Naye Mordekai akawaagiza wampelekee Esta jibu la kusema, Wewe usijidhanie kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote.
Hakuna mahali pa salama (Taz. Masomo Mahali pa Kimbilio (Nam. 194)). Hakuna atayetoroka nyumbani mwa mfalme kuliko watu wengine. Ndivyo Kristo (Mordekai) asemavyo kwa wateule (malkia Esta). Hautaepukana na hili. Hautaendelea kuwapo na watu hawa wakifa. Unapaswa kufanya kazi, kuomba na kufanya kuwaokoa watu wako. Ndiyo maana ujumbe uliotoka kwa mafundisho ya madhehebu- mahali pa salama au kunyakuliwa ni uzushi (Tazama pia Miaka elfu moja na Kunyakuliwa (Nam. 95). Fundisho kama hilo lilishindwa kuwaandaa watu na hatuifanya kazi yetu. Tunapaswa kuifanya kazi.
Esta 4:14 Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?
Mungu atamwinia mtu mwingine. Mawe ya njia yatapiga kelele tusipopiga sisi. Tusipoifanya kazi yetu, Mungu atatuharibu tu na kuinua kitu kingine atakavyofanya na anavyofanya sasa. Tunajuaje kwamba hatukuitwa kufanya hivi tu: kwamba tulikuja kwa ufalme wetu wa kifalme; kwamba tulifanywa wafalme na makuhani; kwamba sisi tu washiriki wa ukuhani na Milkizedeki kwa wakati huu?
Esta 4:15 Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai,
Esta 4:16 Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.
Hivyo kuna utaratibu uliotengwa kiasi kwamba kwa muundo wa Sayari hii ni kinyume na mapenzi ya dunia, tunatakiwa kwenda kwa Mungu ili tuweze kutatua matatizo. Nikiangamia- ni njia ya kusema mapenzi ya Mungu yafanywe.
Esta 4:17 Basi Mordekai akaenda zake, akafanya yote kama vile Esta alivyomwagiza.
Hivi si kwamba neno hapa limeamuriwa bali, wazo ni kwamba Kristo yuko kazini kila siku, kulingana na maombi ya dua za watakatifu. Tunapofanya kazi, na kuomba na kutafuta na kuelekezana sisi kwa sisi na kumwomba Kristo, ndipo jeshi la malaika linavyotusaidia. linaweka uwezo mikononi mwetu usioeleweka. Na ndivyo maana Kristo alisema tunaweza kuhamisha milima na kuitupa baharini tukiwa na imani. Hivyo ina maana kwamba tunaweza kubadili utaratibu ulioewekwa wa mambo kwa imani. Esta
Esta 5:1 Ikawa siku ya tatu Esta alijivika mavazi yake ya kifalme, akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuielekea nyumba ya mfalme; naye mfalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi katika nyumba ya mfalme, kuuelekea mlango wa nyumba.
Mawazo haya ni ya
ujenzi pia ya ishara ya Yona tunapoona siku tatu za huduma ya Masihi kama
kanuni ya Kanisa kutayarishwa pia katika siku za mwisho kuna kipindi kingine
wakati wa mashahidi, ambao juu yao wokovu wa sayari hii unategemezwa. Jumbe za
malaika wa kwanza, wa pili na wa tatu, zinaweka utaratibu wa shughuli ya siku
za mwisho (cf masomo Ishara
ya Yona na Historia ya Ujenzi mpya wa Hekalu [013]; Mashahidi (Pamoja
na washahidi wawili (Nam.135); Jumbe za Ufunuo 14 (Nam. 270) na Pope wa Mwisho: Kutathimini Nostradamus and malachy (Nam. 288)).
Kanisa halitajikalia tu katika siku za mwisho huku mashahidi wakizungumza katika Yerusalemi; Kanisa halitaenda likizoni. Tutakuwa kwa magoti yetu katika mavazi ya magunia na majivu tuykijifunga na kuomba na kutayarisha sayari hii ndipo tusiharibiwe. Ni kazi ngumu. Sio mzaha wala haitakuwa mzaha. Ukweli ni kwamba si kikosi cha mtu mmoja. Kristo hakuifanya peke yake na mashahidi hawataifanya peke yao. Hatima ya makanisa inategemea wateule na sio tu huduma. Taifa linatutegemea pamoja na maombi yetu na kufunga kwetu pia uchunguzi wetu. Kuna kidogo chenye thamana kinachofanywa kwa ajili yake.
Esta 5:2 Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo.
Ni kwa kafara ya Kristo tuliwezeshwa kuingia na kuigusa fimbo ya dhahabu. Tuliingia patakatifu pa patakatifu na kuigusa fimbo ya dhahabu. Kufika wakati huo, haikuruhusiwa kufanyika hivyo.
Esta 5:3 Mfalme akamwambia, Malkia Esta, wataka nini? Nayo ni haja gani uliyo nayo? Utapewa hata nusu ya ufalme.
Hii inachukuliwa kama zawadi kitendo cha sifa tukufu, amabacho hakingezingatiwa kulingana na soncino na mafafanusi ya kirabbi. Hata hivyo siyo maana ya kabisa. Nusu ya ufalme ilikwisha ondolewa kwa njia ya uasi. Kati ya miungu kumi na wawili walioanguka na ni nusu ya ufalme ndiyo ingepeanwa kwa wateule. Kanisa lingeirithi sehemu hiyo ya ufalme ambayo jeshi lililoanguka lilinyakua. Kwa hivyo theluthi ya ufalme iliangukla Mumngu walakini kwenya daraja za juu ilikuwa hata ya nusu ya baraza. Kidokezi cha nyongeza ni kwamba jamii ya wanadamu inaongezea kiasi kwa jeshi la malalika, ndiposa yasiwe maneno matupu. Hatujui idadiyake; hatujui hesabu yake kwa sababu hatujaichukuwa. Hatuna haki ya kujua, ila maelezo haya hata nusu ya ufalme yanaonyesha kiasi kinachohisika. Maumbile ya kimwili yatasawazishwa na maumbile ya kiroho sawa na maelezo ya Mji wa Mungu (Nam. 180).
Esta 5:4 Esta akasema, Mfalme akiona vema, na aje leo, mfalme na Hamani, kwenye karamu niliyomwandalia.
Esta 5:5 Basi mfalme akasema, Mhimize Hamani, ili
ifanyike kama Esta alivyosema. Hivyo mfalme na Hamani
wakafika katika karamu ile aliyoiandaa Esta.
Esta 5:6
Basi mfalme
akamwambia Esta pale penye karamu ya divai, Dua yako ni
nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utafanyiziwa.
Esta 5:7 Esta akajibu, na kusema, Dua yangu ni hii, na haja yangu ni hii,
Esta 5:8 Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunifanyizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema.
Hivyo tuna kazi mara mbili. Wanakuja siku ya kwanza kwa karamu ya mvinyo, na kuna nyingine kama hiyo kwa siku ya pili. Hivyo tunaangazia siku mbili zinazohusika katika mwaliko. Utaratibu huu kwa siku mbili, mankuli ya ndoa na karamu mbili, yanafunika mawazo tena ya fufuo mbili. Pia inafunika wazo la hukumu. Kwenye karamu ya pili , sura ya pili, tunaangazia ufufuo wa wafu, hukumu ya malaika na hukumu ya jeshi lote. Ndipo Kanisa lina msafara tayari na Shetani anaitwa hukumuni chini ya uongozi wa Mungu. Haya yanaelezwa katika Masomo Ufufuo ya Waliokufa [143]; Hukumu Ya Mapepo (Nam. 80); Uwongo wa Ufufuo wa Tatu (Nam. 166); Nafsi (Nam. 92) na Makanisa Ya Wakristo Wa Mungu [199].
Esta 5:9 Basi Hamani alitoka siku ile kwa furaha na ukunjufu wa moyo; lakini Hamani alipomwona Mordekai mlangoni pa mfalme, ya kwamba hasimami wala kutetemeka mbele yake, alijaa ghadhabu juu ya Mordekai.
Esta 5:10 Walakini Hamani akajizuia, akaenda zake nyumbani kwake; akatuma kuwaita rafiki zake na Zereshi mkewe.
Esta 5:11 Naye Hamani akawasimulia habari za fahari ya mali zake, na wingi wa watoto wake, nayo mambo yote pia ambayo mfalme amemfanikisha katika hayo, na jinsi alivyompandisha juu ya maakida na watumishi wa mfalme.
Wana kumi ni wale tu wa Zereshi bila shaka kulingana na mafafanusi ya kirabbi. Kwa hakika alikuwa na ongezeko la wana kwa masuria pia.
Esta 5:12 Zaidi ya hayo Hamani akasema, Naye malkia Esta
hakumkaribisha mtu ye yote pamoja na mfalme katika
karamu aliyoiandaa, ila mimi peke yangu; hata na kesho pia nimealikwa naye
pamoja na mfalme.
Maeleza haya ni ya kujenga hadithi ya kile kinachomtendekea Hamani. Maana ni kwamba mfuatano huu unaendelezwa ndiposa Kanisa lisghughulike na watu hawa walio na hitaji. Au hamjui kwamba mtawahukumu malaika (1 Wakor 6:3). Hii ni wazo kwamba wale watu watawekwa chini yetu (cf pia masomo Kuwepo Kwa Yesu Kristo [243].
Esta 5:13 Bali haya yote yanifaa nini, pindi nimwonapo yule Mordekai, Myahudi, ameketi mlangoni pa mfalme?
Esta 5:14 Basi Zereshi mkewe akamwambia, na rafiki zake wote, Na ufanyizwe mti wa mikono hamsini
urefu wake, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake;
ndipo utakapoingia kwa kicheko pamoja na mfalme karamuni. Basi
neno likampendeza Hamani, akaufanyiza ule mti.
Esta 6:1Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru
aletewe kitabu cha maandiko ya taarifa, nayo yakasomwa mbele ya mfalme.
Esta 6:2 Ikaonekana kuwa imeandikwa ya kwamba Mordekai aliwachongea
Bigthana na Tereshi, wasimamizi wawili wa mfalme,
katika hao waliolinda mlango, waliotaka kumtia mikono mfalme Ahasuero.
Esta 6:3 Mfalme akasema, Je! Ni heshima gani au jaha
gani Mordekai aliyofanyiziwa kwa ajili ya hayo?
Watumwa wa mfalme waliomhudumu wakamwambia, Hakuna
alilofanyiziwa.
Esta 6:4 Mfalme akasema, Yupo nani behewani? Ikawa Hamani alikuwa ameingia
katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aseme na mfalme,
ili kumtundika Mordekai juu ya mti ule aliomwekea tayari.
Kwa hivyo tunaongea kimsingi kuhusu kanuni hapa za wateule na ukweli kwamba Israeli iliabudu sanamu. Shetani alifurahia kwamba israeli iliabudu sanamu. Pia kuna kitu kirefu cha mwaliko. Swala ni kwamba shetani aliendelea kudharau Israeli na Israeli ilipelekwa utumwani. Israeli ilitawanyika kabisa. Masihi pia alikuwa mmoja wa jeshi tiifu. Shetani alikuwa mmoja wa wale viongozi wawili wa jeshi lililoanguka aliowafanya kuasi na kuanguka kutoka kwa neema. Tunaona israeli ilipelekwa utumwani na Yuda pia kwa sababu ya sanamu. Wazo ni kwamba walialikwa ndani. Shetani pia alikuwa ndani. Mordekai aliwekwa basi alivyowekwa kristo. Hili linaonyeshwa na ukweli kwamba Hamani alikuwa anaenada kumwangamiza Mordekai. Hili ni mithali kuhusu maangamizi ya Yesu kristo na shetani kwa kumwagika kwa hasira msalabani.
Esta 6:5 Basi watumwa wa
mfalme wakamwambia, Tazama, Hamani yupo, amesimama behewani. Mfalme
akasema, Na aingie.
Esta 6:6 Basi Hamani akaingia. Mfalme akamwambia, Afanyiziwe nini yule ambaye mfalme apenda kumheshimu? Hamani akasema moyoni mwake, Ni nani ambaye mfalme apenda kumheshimu kuliko mimi?
Hii inaonyesha majivuno na nafasi ya kusema kwamba hakuna mtu mwingine kuliko mimi. Hiyo ni nafasi alioshikilia shetani kama kerubi afunikaye. Alijipandisha juu kuliko kila mshiriki wa Baraza la Mungu. Kerubi afunikaye, walakini alijaribu kuupanda mlima wa Mungu Alijaribu kujilinganisha kwa Mungu. Kristo hakufanya hivyo. Hii ndio kanuni ya majivuno yaliyohusika (na inaonkana Wafilipi 2:6).
Esta 6:7 Basi Hamani akamwambia mfalme, Yule ambaye mfalme apenda kumheshimu,
Esta 6:8 na aletewe mavazi ya kifalme ambayo mfalme amezoea kuyavaa, na farasi ambaye mfalme humpanda mwenyewe, ambaye ametiwa taji ya kifalme kichwani;
Farasi huyu anayeendeshwa na mfalme nii nguvu za Mungu na Masihi yuaja kwa farasi mweupe katika siku za mwisho, kuonyesha nguvu za Mungu kwa njia ya Roho mtakatifu.
Esta 6:9 na yale mavazi na yule farasi akabidhiwe mkononi mmojawapo wa maakida wa mfalme aliye mstahiki; ili makusudi amvike yule ambaye mfalme apenda kumheshimu, na kumrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, na kupiga mbiu mbele yake, kusema, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu.
Esta 6:10 Basi mfalme akamwambia Hamani, Hima! Twaa
mavazi na farasi kama ulivyosema, ukamfanyizie vivyo
hivyo Mordekai, Myahudi, aketiye mlangoni pa mfalme; lisipungue neno lo lote
katika yote uliyoyasema.
Esta 6:11 Ndipo Hamani alipoyatwaa mavazi na farasi, akamvika Mordekai yale mavazi, akamrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, akapiga mbiu mbele yake, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme penda kumheshimu.
Tunalo wazo hapa kwamba Masihi anahitimu kwa badala ya Shetani kama nyota ya asubuhi. Ametukuzwa na mfalme juu ya Shetani na amefanya Shetani akubali ukweli kwamba Kristo amehitimu kuwa badala yake. Bila shaka Shetani sasa anfahamu kuwa Kristo ndiye atakayekuwa nyota ya asubuhi na kwamba muda wake ni mfupi. Hiyo ndiyo utendaji wa uasi wa jeshi naye amefanywa kukubali ukweli huo. Hili linamghadhibisha joka.
Esta 6:12 Kisha Mordekai akarudi kwenye mlango wa mfalme. Bali Hamani akaenda mbio nyumbani kwake, mwenye msiba, na kichwa chake kimefunikwa.
Kristo alienda kwa nyumba ya mfalme. Kanuni hii ya Hamani kukimbilia nyumbani kwake, akiomboleza na kufunika kichwa chake ni ishara ya kuomboleza kutoka 2 Samuweli 15:10. Targum ana zingatia ukweli huu. Kinachowakilishwa ni kwamba, Hamani akifunika kichwa chake naye akawekwa na kufungwa sawa na anavyofungwa kwa miaka elfu. (Ufunuo 20:2)
Esta 6:13 Basi Hamani akawasimulia Zereshi mkewe na rafiki
zake wote kila neno lililompata. Kisha watu wake wenye hekima na Zereshi mkewe wakamwambia, Ikiwa huyu Mordekai, ambaye
umeanza kuanguka mbele yake, ni wa uzao wa Wayahudi, wewe hutamweza, bali
kuanguka utaanguka mbele yake.
Hivyo ukiwa mwana wa Mungu, ukiwa wa mbari ya Daudi waweza kufanya X, Y na Z Shetani aliyumia maneno hayo dhidi ya kristo jangwani.
Esta 6:14 Hata walipokuwa katika kusema naye,
wasimamizi-wa-nyumba wa mfalme walifika, wakahimiza
kumleta Hamani katika karamu ile aliyoiandaa Esta.
Esta 7:1 Basi mfalme na Hamani walikuja kula karamu pamoja na malkia Esta.
Esta 7:2 Mfalme
akamwambia Esta tena siku ya pili pale pale penye karamu ya divai, Malkia Esta,
dua yako ni nini? Nawe utapewa; na
haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utafanyiziwa.
Esta 7:3 Ndipo malkia Esta alipojibu, akasema, Mfalme, ikiwa nimepata kibali
machoni pako, na mfalme akiona vema, nipewe maisha
yangu kuwa dua yangu, na watu wangu kuwa haja yangu.
Esta 7:4 Maana tumeuzwa, mimi na watu wangu, ili tuharibiwe, na kuuawa, na kuangamia. Kama tungaliuzwa kuwa watumwa na wajakazi, ningalinyamaza; ila hata hivyo msiba wetu haulinganishwi na hasara ya mfalme.
Fungu hili ni gumu mno. Wafafanusi wa kirabbi wanasema ni fungu gumu kutafsiri, kwani tunazungumza juu ya adui hapa. Tutachunguza kanuni hizi. Ombi hapa ni kwamba Esta anasema kuwa sisi (wateule) tumeuzwa tuangamizwe. Tungelipelekwa utumwani wanaume kwa wanawake, tuwe watumwa. Mimi (yeye akiwakilisha Kanisa) nisingesema kitu, kwani wajibu wetu ni kwa watumishi wa Mungu. Tu watumishi wa Mungu, ambapo israeli ilikuwa tu mtumwa wa Mungu. Musa alikuwa mtumishi wa Mungu, ambapo Kristo alikuwa mwana wa Mungu, hivyo basi Kristo alikuwa na cheo kikubwa kuliko Musa katika serikali. Katika ufunuo, Musa pia tunapewa uana. Na sasa ikiwa uana ulivuliwa kwetu kama Kanisa nasi tukarudishwa tu utumwa, nani basii atakayekataa? Mbona tukatae kuwekwa kwa ufunuo wa pili kwa sababu tutakuwa tu watumwa wa Mungu? Huo si mkatao halali. Hata hivyo, lengo siyo kutuweka kwa ufufuo wa pili, bali kutuangamiza kama jeshi la kiroho. Na ndiyo maana tunapambana na shetani. Lengo la adui ni kutuangamiza kama jeshi na kumondoa Mungu na kuchukuwa mamlaka juu ya dunia nzima. Ndiyo maana ya fungu hili (kitabu hiki): ningalinyamaza ila hata msiba wetu haulinganishwi na hasara ya mfalme. Hatunyamazi kwa sababu adui huyu ni mdogo kuliko Mungu wetu hasi twamtumikia Mungu wetu. Adui hafai daraja hiyo hivyo twampiga ili kulinda serikali na Mungu wetu. Ndiposa twaenda mbele na kuimarisha uhusiano na Mungu kupitia kwa Yesu kristo ili adui apate kushindwa.
Esta 7:5 Ndipo mfalme Ahasuero aliponena, akamwambia malkia Esta, Ni nani huyu, tena yuko wapi, ambaye moyoni mwake alithubutu kufanya hivi?
Esta 7:6 Esta akasema, Ni mtesi, tena ni adui, ndiye huyu Hamani, mtu mbaya kabisa. Mara Hamani akaingiwa na hofu mbele ya mfalme na malkia.
Esta 7:7 Mfalme akaondoka katika ghadhabu
yake kutoka kwenye karamu ya divai, akaingia bustani ya ngome. Hamani naye akasimama ili ajitakie maisha
yake kwa malkia Esta; kwa kuwa aliona ya kwamba amekusudiwa madhara na mfalme.
Mwishowe mapepo yanatuomba kwa sababu tunayahukumu. Yanahukumiwa na matendo yetu kutoka 1 Wakorintho 6:3 . au haujui kwamba mtawahukumu malaika? Wataomba na kusihi huruma toka kwa Yesu Kristo pamoja nasi. Hayo yahusu hayo yote. Swala la huruma tutaombwa sisi.
Esta 7:8 Kisha mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ngome hata mahali pa karamu ya divai. Ikawa Hamani amejitupa chini penye kitanda alipokuwapo Esta. Mfalme akasema, Namna gani! Je! Atamfanyia malkia jeuri hata machoni pangu nyumbani mwangu? Na neno lilipotoka kinywani mwa mfalme, wakamfunika uso Hamani.
Kujilaza kuna maana. Shetani amechukua kitanda cha Esta na mshirika wa kitanda hicho na ndiyo Kristo anasema katika Ufunuo wa watu Thiatira, kuwa atawatupa wale wa Kanisa hilo kitandani pamoja na Yezebeli. Ndiposa tunakabiliana na mcanganiko wa dini za uwongo.
Mwonekano wa Hamani akilazimisha Esta ni Ule wa kulazimisha Kanisa, kulibaka Kanisa.
Esta 7:9 Ndipo aliposema Harbona, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa wale waliohudhuria mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema, Mtundikeni juu yake.
Mahali pa Harbona kama malaika wa Bwana aliyemfunga shetani panaelezewa katika masomo Ufafanusi Kuhusu Esta sehemu ya II: Kuokolewa tokana na Utimvi katika Siku za Mwisho (Nam. 63B).
Esta 7:10 Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.
Hivyo msiba alioandaliwa Kristo pamoja na jeshi unamgeukia Hamani, au Shetani, adui
Esta 8:1 Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akahudhuria mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu.
Nyumba nzima, sehemu yote ya nyota ya asubuhi, sayari inapeanwa, inachukuliwa toka kwa Shetani- Nyota moja ya asubuhi na kupeanwa kwa Kristo na Kanisa nasi twashiriki katika Nyota ya Asubuhi na uongozi wa sayari.
Esta 8:2 Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani.
Kristo amewekwa msimamizi wa nyumba na kupewa pete ya muhuri ya uongozi wa sayari hii kwa ajili ya wateule. Ndiyo Paulo anasema pia na pia Yohana anasema. Kusudi zima la Agano jipya ni kwamba Kristo amefanywa nyota ya asubuhi naye amepanda daraja kama kuhani mkuu wa wateule.
Esta 8:3 Tena Esta akasema na mfalme mara ya pili, akaanguka miguuni pake, akamsihi kwa machozi ayaondoe madhara ya Hamani, Mwagagi, na shauri alilowafanyia Wayahudi.
Esta 8:4 Ndipo mfalme alipomnyoshea Esta fimbo yake ya dhahabu. Basi Esta akaondoka, akasimama mbele ya mfalme.
Esta 8:5 Akasema, Mfalme akiona vema, nami nikiwa nimepata kibali machoni pake, na neno likionekana jema mbele ya mfalme, nami nikimpendeza machoni pake, iandikwe kuzitangua barua za Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuziandika ili kuwaangamiza Wayahudi walioko katika majimbo yote ya mfalme..
Esta 8:6 Kwa maana niwezeje kuyaona
mabaya yatakayowajia watu wangu? Au niwezeje kuyatazama maangamizo ya jamaa zangu?
Esta 8:7 Mfalme Ahasuero akawaambia malkia Esta na
Mordekai, Myahudi, kusema, Tazama, nimekwisha kumpa Esta nyumba yake Hamani,
naye mwenyewe wamekwisha kumtundika juu ya mti, kwa sababu aliwatia mikono
Wayahudi.
Esta 8:8 Basi waandikieni Wayahudi pia vyo
vyote mpendavyo, kwa jina la mfalme, mkatie muhuri kwa
pete ya mfalme; kwa kuwa andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa
muhuri kwa pete ya mfalme hakuna awezaye kulitangua.
Kitendo iki kinatokana na mapenzi ya Mungu. Ndipo Ufunuo inasemai wali na synagogi la Shetani, wanaojiita wayahudi wala sio nitawafanya kuwainamia na kuwasujujiita (ibada hapa ni hali ya kuikubali mamlaka)
Matendo yataficha wazo la uyahudi wa kweli ni nini wokovu wa kweli pamoja na nafasi ya Israeli ni nini. Hii ni tohara ya Roho na ni kwa njia ya Roho Mtakatifu na wateule. Siyo kwa njia ya Talmud.
Esta 8:9 Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na maakida na maliwali, na wakuu wa majimbo toka Bara Hindi mpaka Kushi, majimbo mia na ishirini na saba, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao.
Si ajali kwamba litafanyika katika sivani. Jambo lifanyikalo katika mwezi wa sivani kwa ujumla ni pentekoste nah ii ni sherehe ya Kanisa baada ya matarisho yake. Kukiwa na mawazo mengine yakuzwayo kwa sivani ni nadra.
Esta 8:10 Akaandika kwa jina la mfalme Ahasuero, na kutia muhuri kwa pete ya mfalme, akazipeleka barua kwa matarishi, wamepanda farasi, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, ndio waliozalishwa katika zizi la mfalme.
Esta 8:11 Katika barua hizo mfalme aliwaruhusu Wayahudi wakusanyike katika kila mji na kuzisimamia maisha zao, kuangamiza, na kuua, na kulifisha jeshi lote la watu na la jimbo watakaowaondokea, wao na wadogo wao na wanawake; na kuyachukua mali yao kuwa nyara;
Hili ni wazo la matarishi waliopanda farasi. Tunaangazia wazo la maendeleo haya hadi maangamizi ya mwisho katika ufunuo.
Esta 8:12 siku moja, katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari.
Esta 8:13 Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote, na kwa Wayahudi, wawe tayari siku ile ile kujilipiza kisasi juu ya adui zao.
Esta 8:14 Matarishi wakaondoka, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, huku wakihimizwa na kusukumizwa kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni.
Tunajitayarisha; hali imebadilika. Barua zilizo nyzraka za agano jipya na kitabu cha Ufunuo vimedokezea mwisho toka kwa hali hii. Baada ya kanisa kupewa choc hake na kupewa mitume na manabii, Ufunuo unakuzwa/ kuendelezwa kama kazi ya mwisho. muundo wote unaonyeshwa, kama ulivyo badilishwa mpango a wokovu. Masihi atakuja mwishoni dalili za mbinguni na kutawala. Hali imebadilishwa siku ya ghadhabu ya bwana ni dhana inayoendelezwa hapa ambapo uharibifu unatafutwa kusukumiwa wateule kwa kweli inatumiwa kukabiliana na sayari hii (cf pia masomo Siku Bwana pamoja na Nyakati za Mwisho (Nam. 192).
Esta 8:15
Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi
ya samawi na nyeupe, mwenye taji kubwa ya dhahabu, na
joho ya kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa
Shushani wakapaza sauti, wakashangilia.
Samawati ni nyeupe si ajali. Samawati na nyeupe huismamia ukweli na usafi kama vazi la kifalme. Kuvalia kwa unyenyekevu (magunia na majivu) kunasimamiwa na vazi la upatanisho kwa utaratibu, Masihi wa Haruni naye akauwawa. Ambapo alijitoa kafara kusulubishwa, hasa anaendelea mbele kama mfalme masihi na upanga wa kweli juu ya farasi mwenye uwezo wa Mungu. Tunaangazia pia taji kubwa ya dhahabu
Na vazi ya kitani nzuri na Zambarau vikuwa ishara ya ufalme kama mfalme Masihi.
Esta 8:16 Ikawa nuru na furaha na shangwe na heshima kwa Wayahudi.
Esta 8:17 Na katika kila jimbo, na kila mji, po pote palipowasili amri ya mfalme na mbiu yake, Wayahudi wakapata furaha na shangwe, karamu na sikukuu. Hata wengi wa watu wa nchi wakajifanya Wayahudi, kwa kuwa hofu ya Wayahudi imewaangukia.
Tunaangazia nabii katika Isaya; tunayaangazia mawazo ya mataifa kuingia Yuda. Waisraeli wote wanarejelea shida ya watu kumi kushika mavazi ya Myahudi, wakisema: “Tunasikia Bwana yu pamooja nawe”. Dhana hizi zilikuwa kwamba kwa ufahamu wao wanafanyika wayahudi; wanafanyika washirika wa wateule.
Esta 9:1 Hata ulipofika mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, siku yake ya kumi na tatu, amri ya mfalme na mbiu yake ilipowadia kutekelezwa; ambayo siku ile adui za Wayahudi walitumaini kuwatawala, bali kumebadilika kinyume, hata Wayahudi waliwatawala wale waliowachukia;
Esta 9:2 siku ile ile Wayahudi wakakusanyika mijini mwao katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero ili kuwatia mikono wale watu waliowatakia hasara; wala asiweze mtu kuwazuia, kwa kuwa hofu yao imewaangukia watu wote.
Watatawanyika katika makabila nao wataokea siku za mwisho kama simba vijana jinzi mafungu yanavyosema. Yuda atapigana Yerusalemu (Zak 14:14). Isaya 66 inaonyesha jinsi urejesho wa siku za mwisho utakavyofanyika duniani. Israeli watatafutwa na kurudishwa. Sabato na miezi mipya itarejeshwa (Isaya 66:23), sawa na sikukuu zitakavyorejeshwa (Zak 14:16-19)
Esta 9:3 Nao maakida wa majimbo, na majumbe, na maliwali, na wale waliofanya shughuli ya mfalme, waliwasaidia Wayahudi; kwa sababu hofu ya Mordekai imewaangukia.
Esta 9:4 Maana Mordekai alikuwa mkuu nyumbani mwa mfalme, na
sifa yake imevuma katika majimbo yote, kwa kuwa huyo Mordekai amezidi kukuzwa.
Na ufalme wa Masihi utadumu milele.
Esta 9:5 Basi Wayahudi wakawapiga adui zao wote mapigo ya upanga, na machinjo, na maangamizo, wakawatenda kama wapendavyo wale waliowachukia.
Esta 9:6 Hata huko Shushani ngomeni Wayahudi wakawaua watu mia tano, na kuwaangamiza.
Esta 9:7 Wakawaua na Parshandatha, na Dalfoni, na Aspatha,
Esta 9:8 na Poratha, na Adalia, na Aridatha,
Esta 9:9 na Parmashta, na Arisai, na Aridai, na Waizatha,
Esta 9:10 wana kumi wa Hamani bin Hamedatha, adui ya Wayahudi; walakini juu ya nyara hawakuweka mikono.
Hilo ni funda au mego kwa mila inasemekana yote kwa dakika moja na imeorodheshwa katika vitabu vya kimasoreti hivyo. Masora anataja majina ya wana kumi wa Hamani yaandikwe katika safu kwenye mkono wa kuume upande wa ukurasa pamoja na vav yaani hiyo na mkono wa kushoto. Hii bila shaka inatokana na mila kwamba hao kumi walitundikwa mtini mrefu mmoja juu ya mwingine. Pia ni desturi ya masomo ya Megilla juu ya Puri kuyasoma majina ya hao wana kumi kwa dakika moja kwa sababu wote walikufa pamoja kulingana na Targam. Hiyo siyo ajali. Wana kumi wa Hamani walisimamia kanuni ya serikali ya khimaya ya siku za mwisho. Tunakabiliana na muundo huu hadi mwisho.
Wana kumi wa
Hamani wameorodheshwa wote kwa dakika moja, kwa sababu wanaunda muungano wa
wafalme kumi katika siku za mwisho. Ndiyo sababu wote wako pamoja katika Masora
na maana ya muundo kushikamana pamoja. Wote wanaangamizwa pamoja jinsi
walivyopokea nguvu zao pamoja katika siku za mwisho katika utawala wa mnyama. Kitabu hiki ni juu ya
hiyo. Hiyo ndiyo sababu watu hawa wanajua mwishowe kwamba matokeo ya mwisho wa muundo wa kishetani ni serikali ya kubahatisha
iliyoanzishwa tangu matokeo ya wababeli, mwishowe ni muungano wa wafalme kumi
katika siku za mwisho. Mafafanusi ya kirabbi yanaelewa wazi kwamba mafungu haya
yanahusiana na sanamu ya mnyama katiaka Danieli sura
ya 2. Hakuna tashwishi kwamba marabbi wanafahamu kuwa ni
ile sanamu inayozingatiwa katika kitabu cha Esta. Kwa hiyo tunao utaratibu wa kuendelea wa ukuaji wa utawala chini ya Nebukadrezza,
akiwa kichwa cha dhahabu kuelekea kwa fedha ya wamede na waajemi, kuja kwa waamaleki
wanowakilisha tu sehemu ya kijeshi ya serikali hii, yaani majeshi ya kishetani
yanayohusika, yaonekanayo chini ya kila himaya na kukua kuelekea tawala nyingi.
Bila shaka kwamba hawa wana kumi, wakiwa matokeo ya mwisho ya serikali ya
kishetani, wanaangamizwa kwa dakika moja katika siku
za mwisho ni ufahamu wa maangamizi ya mwisho ya serikali ya kishetani,
wanaangamizwa kwa dakika moja kaitika siku za mwisho ni ufahamu wa maangamizi
ya mwisho ya utawala wa mnyama na vilole kumi vya Danieli 2. Hizi ndizo zile
pembe kumi tuzionazo katika ufunuo kwenye vichwa saba
vyenye pembe kumi. Yote mawili yanahusiana na jambo
joma. Ni viwango vya mwisho vya utawala wa mnyama,
aliye wa serikali ya kibabeli, inayozungukia kipindi chote cha mataifa. Na
ndiyo maana maelezo haya yanatolewa juu ya ua wa nje.
Hamani anakuja kwa ua wa nje kwa sababu anaruhusiwa
kuingia ndani. Yerusalemu wamepeanwa kwa mataifa na ua
wa nje unakanyagwa kwa miezi 42. Hilo ndilo wazo jingine linalojitokeza kwa fungu hili. Wale
wanaume 500 kimila wanaorodheshwa kama wa nyumba ya
Hamani yaani nyumba ya Shetani. Hilo lawiwana basin a tafrija ya wengine 500
chini ya wateule watakaoichukua nafasi yao. Huku
kutawaza kwa Krisot kwa wale 12, na wale 30, 70 mpaka kwa wale 144,000 yote
yana maana maalum kwa sehemu za majeshi, ambapo wanayachukua majukumu na
mamlaka ya jeshi lililoanguka. Wote wanateuliwa na wote
wanachaguliwa na kutawazwa kama wafalme na makuhani ndani ya utaratibu.
Hakuna nyara. Hakuna atakayechukuliwa mateka na wateule
kati ya watu wa serikali ya kishetani kuingia katika miaka elfu. Hakuna nyara itaguswa mafafanusi yalisema kwamba juu ya nyara
hawakuweka mkono wao. Wayahudi walikuwa tu na
wazo moja, kinga ya nafsi na kipande hiki cha habari kinasisitiza ukweli
(Eslkol Hakofer). Kilicho na maana ni kwamba kwa
salama ya wateule hakuna kitu katika serikali ya Shetani kinatekwa nyara ili
kuingizwa katika ufalme wa Masihi yote yanaachwa nyuma.
Esta 9:11 Siku ile mfalme akaletewa hesabu ya hao waliouawa huko Shushani ngomeni.
Esta 9:12 Mfalme akamwambia malkia Esta, Wayahudi wamewaua watu mia tano hapa Shushani ngomeni na kuwaangamiza, pamoja na wana kumi wa Hamani, je! Wamefanyaje basi katika majimbo ya mfalme yaliyosalia! Basi, una nini uombalo? Nawe utapewa; ama unayo haja gani tena? Nayo itatimizwa.
Esta 9:13 Ndipo Esta aliposema, Mfalme akiona vema, Wayahudi walioko Shushani na wapewe ruhusa kufanya tena kesho sawasawa na mbiu ya leo,
na hao wana kumi wa Hamani watundikwe juu ya mti ule.
Esta 9:14 Mfalme akaamuru vifanyike vivyo hivyo, mbiu ikapigwa huko Shushani,
wakawatundika wale wana kumi wa Hamani.
Esta 9:15 Basi Wayahudi wa
Shushani wakakusanyika tena siku ya kumi na nne pia ya mwezi wa Adari, wakawaua
watu mia tatu huko Shushani; walakini juu ya nyara hawakuweka mikono.
Hivyo, siku ya pili 300 waliuwawa wala nyara hazikuchukuliwa.
Esta 9:16 Nao Wayahudi wengine waliokaa katika majimbo ya mfalme walikusanyika, wakazishindania maisha zao, wakajipatia raha mbele ya adui zao, wakawaua waliowachukia, watu sabini na tano elfu; walakini juu ya nyara hawakuweka mikono.
Hapa tunasungumusa juu ya pumziko la Sabato. Katika himaya nzima waliwaua watu 75, 000.
Esta 9:17 Hii ndiyo siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari; na siku ya kumi na nne ya mwezi huo wakapumzika, wakaifanya kuwa siku ya karamu na furaha.
Esta 9:18 Lakini Wayahudi wa Shushani walikusanyika
siku ya kumi na tatu ya mwezi huo, na siku ya kumi na nne pia; na siku ya kumi
na tano ya mwezi uo huo wakapumzika, wakaifanya kuwa siku ya karamu na furaha.
Hivyo walifikia mwisho wa mwezi. Kufikia mwisho wa mwezi wa Adari waliafikia lengo lao.
Esta 9:19 Kwa sababu hii Wayahudi wa vijijini, wakaao
katika miji isiyo na boma, huishika siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, kuwa
siku ya furaha na karamu, sikukuu ya kupelekeana zawadi.
Hili wazo la kutuma zawadi wao kwa wao na lile la miji isiyo na kuta yanahusiana na kutulia kwa Israeli, kwa kuwa maamuzi au misimamo ya miji yenye kuta na ile isiyo na kuta haijatimika, na mtu angefikiria,wakati wa Xerxes katika utumwa wa Babeli. Msimamo wa kirabbi wa miji yenye kuta na ile isiyokuwa nazo chini ya karamu ya Puri inaamuliwa kutoka kwa miji iliyokuwa na kuta na ile isiyokuwa nazo wakati ta Yoshua. Hili lina maana kuu kwa sababu linasiwanisha hesabu. Hesabu ya nje ya Isreaeli ingelikuwa kubwa ingelikuwa hapo baadaye kuliko sasa, walakini haitimizwi kulingana na utaratibu huu. Inafanywa kama wakati wa Yoshua Israeli ilipotekwa kwanza. Hivyo basi tunazungumzia kukabili kwa nchi takatifu katika kujenga ndani ya sura ya pili, tukitumia urithi wa kwanza wa Waisraeli kujenga mawazo ya urithi wa pili wa Israeli. Haya ni maisha yaliyoenezwa. Ufahamu wa mamlaka za kidini wakati wa kipindi hiki ni kwamba yalianziwa nyakati za siku za Yoshua. Hili ni muhimu sana. (cf Taz. pia Kwanguka Kwa Yeriko [142]).
Esta 9:20 Basi Mordekai aliyaandika mambo hayo; naye akapeleka barua kwa Wayahudi wote waliokaa katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero, waliokuwa karibu na waliokuwa mbali,
Esta 9:21 kuwaonya wazishike siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, na siku ya kumi na tano yake, mwaka kwa mwaka,
Huu ni unabii unaokwenda kwa uongozi wa Kristo.
Esta 9:22 ambazo ni siku Wayahudi walipojipatia raha mbele ya adui zao, na mwezi uliogeuzwa kwao kuwa furaha badala ya huzuni, na kuwa sikukuu badala ya kilio; wazifanye siku hizo ziwe za karamu na furaha, za kupeana zawadi na za kuwapa maskini vipawa.
Esta 9:23 Nao Wayahudi wakakubali kufanya kama walivyoanza, na kama Mordekai alivyowaandikia;
Esta 9:24 kwa sababu Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi wote, alikuwa amefanya shauri juu ya Wayahudi ili kuwaangamiza, akapiga Puri, yaani kura, ili kuwakomesha na kuwaangamiza pia;
Esta 9:25 bali mfalme alipoarifiwa, aliamuru kwa barua ya kwamba hilo shauri baya alilolifanya juu ya Wayahudi limrudie kichwani pake mwenyewe; na ya kwamba yeye na wanawe watundikwe juu ya mti
Huo ni utaratibu wa hukumu. Unavyotafuta kuwaangamiza wateule utaangamizwa wewe mwenyewe. Utaratibu huu unazidi kuendelea kwa kipindi cha siku za mwisho na unatumika moja kwa moja kwa wale mashahidi wawili katika kipindi kinachotangulia mwanzo wa miaka elfu. Muda huu utafupishwa ili kuwaokoa wale wanaomngojea Masihi kwa hamu.
Esta 9:26 Hivyo wakaziita siku hizo Purimu, kwa jina la
Puri. Basi, kwa ajili ya maneno yote ya barua hiyo, na
kwa yale waliyoyaona wenyewe juu ya jambo hilo, na mambo yenyewe yaliyowajia,
Esta 9:27 Wayahudi wakaagiza na kutadariki juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, na juu ya wote watakaojiunga nao, isikome, ya kwamba watazishika siku hizo mbili sawasawa na andiko lile, na kwa majira yake kila mwaka;
Esta 9:28 siku hizo zikumbukwe na kushikwa kwa vizazi vyote na kila jamaa, katika kila jimbo na kila mji; wala siku hizo za Purimu zisikome katikati ya Wayahudi, wala kumbukumbu lake lisiishe kwa wazao wao.
Huo ni utendaji wa Wayahudi kuagizia kila mmoja aunganaye na Yuda. Huu unatwambia kitakachotendeka kwa sherehe ya Purimu Masihi anapotoa amri zake kwenye urejesho.
Esta 9:29 Ndipo malkia Esta, binti Abihaili, pamoja na Mordekai Myahudi, alipoandika kwa mamlaka yote kuithibitisha barua hii ya pili ya Purimu.
Esta 9:30 Akapeleka barua kwa Wayahudi wote katika majimbo yote mia na ishirini na
saba ya ufalme wake Ahasuero, maneno ya amani na kweli,
Esta 9:32 Amri yake Esta
ikayathibitisha mambo hayo ya Purimu; ikaandikwa katika kitabu.
Kwa hivyo, Kanisa litajiagizia sherehe ya Purimu chini ya Masihi. Sherehe ya Purimu itatunzwa wakati wote wa miaka elfu, ila itaongezwa wakati wa miaka elfu.
Esta 10:1
Basi mfalme
Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya
bahari.
Esta 10:2 Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika kitabu-cha-taarifa cha wafalme wa Umedi na Uajemi?
Esta 10:3 Kwa maana Mordekai Myahudi akawa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwatafuta watu wake wema, na kuiangalia hali njema ya wazao wao wote.
Mwisho wa kitabu cha Esta ni wa maana sana. Mfalme aliwekea nchi ushuru Mafafanusi yanasema haya tokea kifungu cha kwanza. Sura hii ni mwisho au nyongeza kwa kitabu inayosisitiza nguvu za Ahaseuro na utukufu uliokuwako hapo ukiangazwa kwa Mordekai kama waziri wake wa kwanza. Hili halionyeshwi na mkondo mkuu wa Ukristo au Uyahudi, kwani linajenga utiifu kamili wa Yesu Kristo. Wahubiri wakristo hawawezi kukabiliana nalo wala wahubiri wa kiyahudi hawawezi kwa kuwa linamwimarisha Kristo kama waziri mkuu kwa usawa na badala ya Shetani. Wazo ni kwamba Ahasuero pamoja na Mordekai waziri wake mkuu walifaulu kaitka kuteka majimbo mengi hadi alipoweza kukubali ushuru au sifa kutoka kwa nchi za karibu na Ufalme wake, sawa na visiwa vya mbali vya bahari kulingana na Malbim.
Kwa kuwa neno la kihebrania kila mahali linamaanisha kazi ya lulazimimshwa tafsiri mwafuaka ni kukalifu. (Taz. Or. Hachaim, Kutoka 1:11)
Kulingana na Targum inahusisha ushuru wa kichwa (Kutoka Aruk) Targum husema ni ushuru wa kichwa. Ushuru wa kichwa ni nini? Ni ushuru unaochokuliwa siku ya upatanisho kama ushuru wa hekali. Kinachofanyika ni kwamba Kanisa chini ya Masihi linatoa ushuru wa hekalu na pia kwa siku ya upatanisho, kwa watu wote katika majimbo yote ya himaya. Utaratibu wa ushuru wa upatanisho unamaanisha kwamba kila mtu atingizwa chini ya ufalme wa Mungu na wokovu unaenezwa kwa watu wote chini ya malipo ya ushuru wa hekalu wakati wa upatanisho. Ushuru huu una maana kwamba wokovu hauendi tu kwa watu wa mataifa kupitia kwa wateule na Kanisa bali unakuwa ni malipo ya kuagizwa juu ya mataifa yote yanapokuja chini ya uongozi wa Yesu Kristo Wakati wa mwisho. Hiyo ndiyyo maana ya sura ya ziada ya kitabu cha Esta.
Sasa tunaona kitabu cha Esta si hadithi ya mwanamke aliyefanyika malkia wa Uajemi. Mara tukikielewa kitabu cha Esta tunakielewa kwa kina kitabu cha ufunuo kama kinavyokua katika Agano jipya. Umbo lote, lililojengwa kupitia kwa Yesu Kristo, linaibuka na Kanisa moja kwa moja ili kuiokoa sayari.
q