Makanisa ya Kikristo ya Mungu

 [068]

 

 

 

Uanzishwaji wa Shirika Liitwalo Makanisa ya Kikristo ya Mungu

(Toleo 2.0 19960308-20040704)

 

Kwa ajili ya ongezeko la watu kulipenda kanisa letu tumeona ni mudimu kuelezea jinsi na sababu au lengo la kuanzisha kanisa hili la CCG, ili kwamba mambo mengi yaliyoelezewa yaweze kufuatwa na watu wale wanaosoma habari zetu.

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

 

(Copyright ã 1996, 2004 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

http://www.logon.org and http://www.ccg.org

 


Uanzishwaji wa Shirika Liitwalo Makanisa ya Kikristo ya Mungu


 

Shirika hili liitwalo Makanisa ya Kikristo ya Mungu ambalo kwa Lugha ya Kiingereza linajulikana kama Christian Churches of God lilianzishwa mnamo mwaka 1994 na kuanza kutoa huduma zake siku ya 1 Nisan 1994. Maswali yamekuwa yakiulizwa mara kwa mara kwa watu wanaopenda kujua sababu hasa za kuanzishwa kwake. Majaribio kadhaa yamekuwa yakifanywa yenye nia ya kulikomesha au kuyapuuzia mambo yahusuyo tofauti ya kitabia, au kwa namna nyingine, kuepuka jambo halisi lililopelekea kuanzishwa kwake. Tunaendelea kuwepo kwa kuwa kwa sisi wenyewe tu, bila Mungu hatuwezi kupata fursa iliyopo.

 

Kanisa liliundwa na idadi kadhaa ya waumini waliobatizwa waliotoka kwenye shirika linaloitwa Kanisa la Mungu au kwa Kiingereza huitwa Church of God, wengi kati yetu tukiwa tukiwa tumekuwa ni washirika wa Kanisa lililojulikana kama Kanisa la Mungu Lililoenea Ulimwenguni Kote au kwa Kiingereza liliitwa kama tha Worldwide Church of God. Kadiri miaka ilipokuwa inaendelea kupita ndipo washirika walipozidi kujiunga wakitokea kwenye makanisa mengine kadhaa vile vile. Idadi kubwa ya watu kutoka nchi au mataifa mbali mbali duniani ambao hawajawahi kuwa washirika au kufahamu chochote kuhusiana na Kanisa hili la zamani yaani WCG, ingawaje wengi bado hujiunga kwenye kanisa hili yaani CCG wakitokea kwenye matawi fulani fulani.

 

Kama tuonavyo jinsi watu wengi wanavyojua, kwamba kanisa hili la zamani liitwalo the Worldwide Church of God (hapo mwanzo lilijulikana kama Radio Kanisa la Mungu yaani, Radio Church of God) ambalo liliundwa kutokana na kanisa lingine lilijulikana kama Kanisa la Mungu (la Kisabato) kwa Kiingereza likijulikana kama the Church of God (Seventh Day) baada ya kuganyika au kufarakana kwa kanisa hili mnamo mwaka 1940. Makanisa haya yote mawili yalikuwa ni ya mrengo wa Kiunitariani katika muundo wao katika mafundisho yao ya hapo mwanzoni. Kanisa lilikuwa ni la Kiumitariani kwa kipindi cha takriban miaka elfu moja na miatisa iliyopita. Kanisa limepita kwenye mateso kwa ajili ya kufuata na kuamini fundisho hili kiasi cha kupitia kwenye majaribio ya kukomeshwa kwa kipindi cha miaka mingi sana. Kanisa wakati wote limekuwa likifundisha kwamba kuna Mungu Mmoja tu wa pekee na wa Kweli, na kwamba Yesu Kristo ni Mwanawake (Yoh. 17:3; 1Yoh. 5:20). Kristo sio yule Mungu wa Pekee wa Kweli ambaye ni Baba (Yoh. 5:26). Mungu Wapekee na wa Kweli ndiye pekee hawezi kupatikana na madhara au kufa (1Tim. 6:16) na hakuna mtu awezaye kumuona na wala hakuna mtu aliyewahi kumuona (Yoh. 1:18; 1Tim. 6:16) (pia tazama jarida lisemalo Theolojia ya Mwanzoni kuhusu Uungu [127].

 

Kuanzia kipindi cha takriban mapema ya 1955 kumekuweko vuguvugu la mara kadhaa ndani ya kanisa lile kongwe la zamani la WCG lililohukika na watu wakijiuliza na kuulizana maswali kuhusiana na fundisho linalo husu imani ya Mungu mmoja maarufu kama Unitarian wakitaka kujua msimamo gani lilokuwanalo kanisa kuhusiana nayo, na ambavyo walijaribu kulichukua kanisa na kulipeleka kwenye muelekeo wa kuamini Utatu. Hali hii inaonekana kuwa ilipata msukumo wa moja kwa moja na Herbert Armstrong mwenyewe, huenda ilitokana kwa sababu fulani ya shinikizo kubwa kutoka kwa watu fulani. Baada ya mwaka 1955 baadhi ya majarida yao ya kufundishia mambo ya msingi ya kiimani, kama vile lile lisemalo Je, Yesu ni Mungu?,   lilionakana linaanza kuweka makala zenye mtazamo wa kitheolojia kwa niaba yake na kwa jina na idhini ya Kanisa hili kongwe la the Worldwide Church of God, ambayo ilikuwa ni wakianza kuisemea kinyume au kuipinga misingi ya kitheolojia ya Kiunitarian ya iliyokuwa ikiitwa Radio Kanisa la Mungu. Makala kama hizi zilitolewa na kuchapisha mtazamo wa kitheolojia zikiliwalilisha kanisa hili kongwe la theWorldwide Church of God jambo ambalo lisingewezekana kupata suluhu wala kuvumilika na misingi ya kiimani ya kanisa la Kiunitarian, na ni jambo linaloonekana kama lilipuuzia historia ya imani ya mafundisho ya theolojia ya Waunitarian ambayo yaliliunganisha kanisa kipindi kile lilipoanzishwa kwa mara ya kwanza. Wasshirika wale wa kanisa lile kongwe la the Worldwide Church of God waliobakia wakiishikilia kweli ya msingi wa muundo thabiti wa imani ya kimungu ya Uunitarian hawakufurahishwa na mwelekeo huu mpya wa kitheolojia ambao kanisa hili la the Worldwide Church of God lilikuwa likielekea kuushikilia.  Theolojia hii iliibadilisha kabisa imani ya misingi ya Uunitarian hata hivyo iliendelea kudumu kwa nguvu zote, na yapata kama mwaka 1994, kanisa lile la the Worldwide Church of God lilijitangaza kuwa ni la Kiutatu kwa kujitangaza kabisa kiwazi wazi.

 

Watu wanaounda bazaar la bodi ya uongozi wa Makanisa ya Kiristo ya Mungu maarufu kama the Christian Churches of God katika kikao chao cha uzinduzi walikuwa wamebakia kwenye ushirika na upenzi wa kanisa lile kongwe la the Worldwide Church of God licha ya kutangazwa kwa kujiunga kwake kwenye imani hii potofu na baadhi yao wenye kuamni utendaji kazi wa miungu miwili yaani Ubinitarian/Ditheist ambayo walimshawishi Herbert Armstrong. Wakati ambapo liliendeshwa hakukuweko kamwe na mtu yeyote aliyekuwa akiombwa zaidi ya Baba Mungu kwa jina la Kristo utaratibu ambao ulikuwa ni sahihi sana, na hakukuwa na mgongano uwaowote wa kiimani uliojitokeza. Ilikuwa pia ni dhahiri kwamba watu wengi miongoni mwao wale waliokuweko kanisani walikuwa ni waabudu wanadamu. Makanisa mawili yalianzishwa kutokea kwenye kanisa hili kongwe la the Worldwide Church of God kwa sababu ya mabadiliko yanayoendelea kuanzia miaka ya 1987-1991. Watu wetu hawajajiunga kwenye makanisa yao kwa kuwa yaligundulika kuwa yalikuwa na makosa makubwa. Zaidi ya yote, ni kwamba yameundwa kwa kufuata mfumo wa kikampuni yakimilikiwa na kuongozwa na kikundi kidogo cha watu binafsi.

 

Mwanzoni kabisa Herbert Armstrong aliunda muungo wa kanisa wa kishirikisho akiwa na maana nzuri sana na hatimaye akalibadilisha kuwa ni shirika la kibinafsi linalomilikiwa na yeye mwenyewe peke yake kwa kutumia mbinu ya kile alichokifanya kuwa ni maamuzi ya kura ya maoni iliyokuwa imepigwa na kupitishwa. Mashirika haya yaliundwa ama kuanzishwa yakitokea kwenye kanisa hili kongwe la WCG ambayo pia yale yale yaliendelea kufuata makosa yale yale ya muundo wa umilimiliki pia. Lengo la kwanza na lamsingi lilikuwa kwamba waweze kuingiza imani ya Kibinitarian au pia huitwa Ditheist. Makosa haya yalikuwa makubwa kwenye njia yao kama ilivyokuwa katika imani ya Kitrinitariani.

 

Washirika waliounda shirika hili maarufu kama Christian Churches of God walikabiliana na mlolongo wa mambo waliyotakiwa wayafanyie uchaguzi. Ni dhahiri kabisa kwamba ilikuwa wangeweza kujiunga kwenye makanisa yaliyokuwepo kwa sababu zozote zingalizoweza kuliharibu kanisa lile kongwe la Worldwide Church of God na kwa sababu ya kupokea kwa makosa kwao.

 

Kanisa hili halikuiona njia nyingine zaidi ya kuamua kuunda ama kuanzisha shirika hili linaloitwa Makanisa ya Kikristo ya Mungu, maarufu kama Christian Churches of God na kuendelea na maelekezo ambayo Kanisa lilipewa na Yesu Kristo mnamo mwaka 30 BK.

 

Mchakato endelevu wa uanzishwaji na uamuzi wake

Washirika wa CCG kapo mwanzo walitaka kuanzisha shirika lingaliloweza kumilikiwa na waumini wenyewe, na kila mmoja miongoni mwao awe na haki ya kupiga kura ili kufanya maamuzi ya mambo ya kanisa.

 

Waliapa kutorudia tena kuiachilia huduma binafsi iwaibe au kuwapokonya Kanisa lao kutoka kwao kwa kutumia njia za udanganyifu na mafundisho mapotofu ya uongo. Kwa moyo mmoja kabisa ikaamuliwa kuliweka Kanisa katika Matamko ya Ukiri wa Msingi wa Imani uliowazi sana na yasiyo na utata kueleweka na Katiba iliyoandikwa kwa wazi sana na bila utata pia.

 

Iliamuliwa kwamba lika mtu ajaye Kanisani atalazimika kuendelea kuamini na kudumu kwenye mambo haya yote mawili muhimu ya Kanisa yaani Katiba na Matamko ya Ukiri wa Imani kwa pamoja. Utaratibu au mchakato wa kubadilisha mambo haya ili kuyafanyia marekebisho ulitolewa namna yake na kuelezewa kwenye Katiba.lakini mtazamo mzima wa uungu wa Mungu mmoja kama ulivyofundishwa na Kanisa la kihistoria la karne ya kwanza ulilindwa kwenye katiba ili kwamba asije akatokea mtu mwingine huko mble akaanzisha ama kuingiza imani za Kibinitarian, Ditheism ama Utrinitariani kwenye Kanisa La Mungu, na hata katika kanisa letu la CCG.

 

Idadi ya wapigakura ilichukuliwa na Kanisa kwa kipindi kifupi cha miaka ya mwanzoni ili kuuwekea mkazo utungaji wa Katiba (kama inavyoonekana kwenye jarida [A2] na kufanya baadhi ya mabadiliko madogo madogo kwenye Matamko ya Ukiri wa Misingi ya Imani ya Kikristo  (kama inavyoonekana kwenye jarida [A1].

 

Ilitokea dhahiri na kwa haraka kwamba kilikuwa ni kipindi kigumu kilichohusishwa kwa watu wanakikumbuka walikubaliwa kupiga kura ya uanachama na kwamba marekebisho yamekubaliwa kwa utaratibu wa Baraza la Kanisa la Ulimwenguni kote mnam mwaka 1998. Mnamo katika miaka ya 1996 na 1997 Utaratibu wa muundo wa makanisa katika nchi za Marekani na Canada na kwingineko barani Ulaya, waliviona vikundi vikihudhuria Kipindi cha Usomaji wa Sheria za Mungu katika Mwaka wa Sabato wa 1998. Tendo hili la Usomaji wa Sheria ni la lazima kufanyika katika Mwaka wa Saba wa mzunguko unapotimia (kwa mujibu wa Kumbukumbu la Torati 31:10–13). Maafisa wa Kanisa wanateuliwa na kuwekwa kwa njia ya kupigiwa kura, kama idadi itazidi waliohudhuria, kwa mabaraza ya kitaifa na ya kimataifa wakati wa Sikukuu ya Vibanda. Mabaraza ya Kitaifa yote huweka na kusimika maafisa wake kwenye Idi ya Pasaka na Mikate isiyotiwa Chachu. Wawakilishi hawa hatimaye watakwenda kuhudhuria kikao cha Baraza la Halmashauri kuu ya Ulimwengu wakati wa Sikukuu ya Vibanda.

 

Mwangalizi Mkuu wa Kanisa hili Ulimwenguni anayeshikilia maongozi kwa sasa ni Wade Cox kutoka Australia na James Dailley kutoka Canada, wanawekwa kwa kufuata vipindi vya mzunguko wa Sabato kwa ajili ya kuimarisha sehemu yao ya kwanza wa utendaji wake kazi kimataifa. Kipindi chao cha utendaji kazi kitaishia mwaka 2012. Mwangalizi huyu Mkuu wa Kanisa, ni Mustralia ambaye wasifa wake kielimu na kiutendaji ni kwamba yeye ni mtu aliyebobea katika masomo ya falsafa kwa upande wa mambo ya Dini na Maadili, na kwenye Mambo ya Sheria za nchi, alifanywa kuwa ni mhariri mkuu wa machapisho yatolewayo na CCG na ni mwanatheolojia mkuu na aliyebobea tangu mwaka 1994. Ameshikilia jukumu hili tangia alipopewa na Baraza Kuu la Halmashauri Kuu ya Ulimwengu. Maafisa hawa wote wawili wanaongozwa na Katiba pamoja na Matamko ya Ukiri wa Imani. Na wanalazimika kuisisitiza waikubali. Kwa hiyo usimamizi wa shughuli za machapisho mbali mbali pia umewekwa kwao. Hawana fursa ya kujiamulia kufanya mambo kama wanavyoona wao. Kila mmoja wao anauwezo wa kikatiba wa kupiga kura ya turufu katika jambo linalohusiana na mabadiliko au marekebisho ya kimafundisho kuhusu asili ya Mungu.

 

Maafisa hawa wanachaguliwa kwa kupigiwa kura kwa mujibu wa inavyosema Katiba. Mwangalizi Mkuu ambaye anasaidiwa na mtu mwenye cheo cha Makamu wa Mwangalizi Mkuu, anao uweza wa kumteua na kuanzisha makanisa kwa kipindi cha miaka saba na kusimika au kuanzisha huduma mpya kwenye Kanisa.

Makatibu Wakuu watatu wameteuliwa na Waangalizi hawa Wakuu. Kwa kawaida wanateuliwa kutokana kama walifanya au walikuwa wakihudumu kama huduma ya makatibu wa taifa ao maafisa wa kanisa la taifa miongoni mwa makanisa yetu. Wanateuliwa kwa vile wanavyoonekana kuwa wanastahili bila kujali jinsia zao kama ni wanawake au wanaume, wanaweza kuteuliwa kutumika kushikilia majukumu hayo. Wanatakiwa kustaafu wakiwa na umri wa miaka 70 kwa mujibu wa vile inavyosema Katiba.

 

Baraza la Wazee la Halmashauri Kuu ya Ulimwengu linatokana na hawa wenyeviti wa taifa walioteuliwa na wawakilishi wa Majimbo waliochaguliwa ama kuteuliwa na Baraza la Halmashauri Kuu ya Ulimwengu. Ni maafisa hawa ndio wenye wajibu mkuu wa kusimamia mafundisho wakiwa chini ya uenyekiti wa Mwangalizi Mkuu.

 

Wanachama wa mabaraza ya kitaifa na wa Baraza la Halmashauri Kuu ya Ulimwengu hawawezi kuwekwa kwenye hesabu ya watu wanaolipwa mishahara ama kuajiriwa na Kanisa. Wanahesabiwa kupewa posho iliyo sawa na malipo ya mwangalizi, na anaweza kuajiriwa kwenye shughuli nyingine iwayo yote. Kwa hiyo hii inafanya kuwa migongano ya kimaslahi ipungue kutokea.

 

Makanisa yamekuwa yakianzishwa na idadi kubwa inaungana kwenye mataifa mbali mbali, katika nchi zilizoko kwenye mabara ya Amerika, Ulaya, Africa, na Asia na pia huko katika nchi zijulikanazo kama za Australasia au Mashariki ya Mbali ambako kanisa hili la CCG ndiko lilikoanzia kwa mara ya kwanza.

 

Baadhi ya watu, na mara chache makanisa yote, kwa bahati mbaya na kwa masikitiko sana kusema kwamba imelazimika waondolewe kutoka kwenye ushirika wa kanisa kwa sababu ya kushindwa kwao kudumu kwenye mafundisho na maadili yalitopo kwenye Katiba ya Kanisa au kushindwa kwao kudumu kwenye maelekezo ya kimaadili ya Kanisa. Kanisa halitakubali kulegeza msimamo wake eti kwa kutaka liwe na idadi kubwa ya watu.

 

Kila mmoja wetu anawajibika kuielewa na kuchukua hatua ya kuamua kubakia kwenye maelekezo ya Matamko ya Ukiri wa Imani na ya Katiba. Kama hawatakubaliana nayo, watakuwa wanamaanisha kuwa wameamua kujiondoa, basi na waondoke kwa amani. Kwa njia hii, basi kanisa linaunganishwa watu wanakubaliana na mafundisho na kuabudu pamoja kwa amani.

 

Watu hawatatengwa kutoka kwenye ushirika wa kanisa hivihivi tu bali ni lazima kuweko na mazingira maalumu yanayotosheleza, na wanaweza hata kupigiwa kura ama kutolewa ushahidi mbele ya baraza la halmashauri ya Kanisa.

 

Kuna utaratibu unaotumika kufuata kwa ajili ya kushughulikia mtazamo wa kuingiza mafundisho mapya, na yanayoweza kuendelezwa na mtu awaye yote kwenye kutaniko lolote moja wapo. Karatasi au nyaraka ule wa maoni unatakiwa kuletwa kwa makatibu wa kitaifa na zitolewe kwenye mabaraza ya kitaifa kwa ajili ya kuyajadili.

 

Iwapo kama itaonekana kuwa inastahili, basi zitapelekwa kwenye Baraza la Halmashauri Kuu ya Ulimwengu kwa kulitazama zaidi jambo hilo na Kamati Kuu ya Utendaji, na kisha hapo kupelekwa kwenye, Baraza au Bodi ya Wazee. Kama itakataliwa, jambo hilo bado litapelekwa kwenye Baraza la Halmashauri Kuu ya Ulimwengu ambao huenda wanaweza kutokubaliana na maamuzi ya kikao cha baraza la kitaifa, yanayoshauri kufanyika kwa marekebisho, au kwamba lipigiwe kura jambo hili. Kama likifikiriwa kikamilifu sana na ushuri ukahitaji kufanywa na Kanisa wa kubadili nakala za uanzishwaji, basi kura za wanachama wote zitapigwa. Na kama itaonekana kuwa imeshinda kwa kupata kura nyingi za wapiga kura kwa mujibu wa Katiba yetu inavyoelekeza, ndipo basi, nakala za msingi za Kanisa zitafanyiwa marekebisho.

 

Nguvu ya kura ya turufu inahusiana kutumiwa kwa masuala ya mafundisho ya umoja wa Mungu, ambao unalindwa kwenye Katiba. Uvunjaji wa kanuni ya kuabudu ama kuabudiwa kwa Mungu Mmoja na Wapekee wa Kweli hakutaweza kufanyiwa mzaha au kuchukuliana na mtu anaye kwenda kinyume na kanisa CCG, popote pale lilipo.

 

Uhusiano na Mwili wa Kristo

Kuna idadi kubwa ya makanisa yaliyoundwa ama kuanzishwa kuwanzia mwaka 1994, lakini kila moja kati yake yana matatizo ya kiuongozi na kimafundisho yaliyosababisha kugawanyika kwa kanisa lile kongwe la WCG kwa mahali pake palepale.

 

Makanisa mengine ya Mungu yamepuuzia na yanafanya mambo yale yale yaliyosababisha kuvunjika kukubwa kwa kwa kanisa lile kongwe la WCG. Watu kutoka mashirika haya wanakuja kwetu na kujiunga na sisi kila wakati

 

Baadhi ya watu kutoka kwenye mifumo ya Kiulaya, ambao walikuwa ni sehemu ya Makanisa ya Mungu kwa kipindi kile cha Matengenezo ya kidini barani Ulaya, pia wanajiunga kwetu kwa sababu sisi tunaendelea kushikilia imani ya kweli ya siku za kwanza za Kanisa, na hatujaichanganya imani ya kweli juu ya Mungu mmoja ambayo ni Uunitarian iliyokuwa ikiaminiwa na kufundishwa kwa kipindi hiki chote cha kihistoria ya Kanisa la Mungu.

 

 

 

 

 

 

q