Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[072]
Wongofu na Kweli
(Toleo
La 2.0 19941015-19980725-20090606)
Dhana ya uwongofu ukiwa kama mchakato wa kugeuka kutoka maovuni na upotofu
inaonekana kuwa ni fundisho la muhimu na la msingi kwa Kristo.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1994, 1998, 2009 Wade Cox)
(tr. 2015)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Dhana ya wongofu imechukuliwa kutoka kwenye ile ya kugeuka kutoka kwenye
makosa, na kuisikiliza kweli, na kuelewa kutoka moyoni.
Isaya 6:10 Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho
yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa
mioyo yao, na kurejea na kuponywa.
Isaya 6:10 Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao,
ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao,
na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.
Dhana hii imenenwa tena na Kristo.
Mathayo 13:15 Maana
mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho
yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao,
Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Marko 4:12 ili
wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije
wakaongoka, na kusamehewa.
Kweli ile inayoendelea kutoka kwa Mungu
ikiwa kama jambo muhimu ya kazi na matendo ya mwanadamu kwa kuzivunja sheria na
matendo ya dhambi.
Zaburi 19:7 Sheria
ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia
mjinga hekima.
Huu ni mwanzo wa dhana ambayo kwenye Agano Jipya ni msingi nay a muhimu kwa
wokovu. La muhimu sana ni kwamba inahitaji matendo kwa mtu kuweka msingi wake
kwenye kweli iliyofunuliwa ya Mungu. Mungu pia anaweka hilo wazi sana au kuwa
dhahiri kwamba mchakato inathibitiwa. Watu walikuja kwa Mungu wakitegemea uwezo
wao wa kufanya kwa mujibu wa kweli yake na kuifanya iwe lazima na muhimu kwa
maisha yao.
Uhuhimu wa kweli hii umeendelezwa na Yakobo.
Yakobo 5:19-20 Ndugu
zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine
akamrejeza; 20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye
dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi
wa dhambi.
Neno linalotumika kumaanisha wongofu kwenye lugha ya Kiyunani ni epistrepho(SGD 1994), ambalo maana yake ni kujirudi au kurudi tena. Neno hili linatumika kama neno kiini au chimbuko kwenye
Matendo 15:3 linalohusu wongofu wa Mataifa ambao ni epistrophe (SGD 1995) lenye maana ya kurejea au kujirudi kwa
maana ya mageuzi ya Wamataifa ing.
Matendo 15:3 Basi,
wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria,
wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.
Mchakato huu unatumika kwa neno la
Kiebrania kwenye Isaya, ambalo ni shoob (SHD 7725). Hili ni shina la msingi lenye maana ya: kugeuka na kurudi
nyuma. Kwa hiyo kweli ni lazima ipewe mara moja kwa mataifa yote ili kwamba
waweze kurejea kwenye kweli.
Uanzishaji huu kwenye kweli ulitokea chini
Nuhu na uanzishaji pya tena wa ulimwengu usio na uharibifu. Somo la msingi na
la maana ni kwamba watu hawataki kuijua kweli au kuufanyia kazi au kulazimishwa
kwenye kweli. Ndiyo maana dhana na watu ni kiunyume na hawahesabiki. Hakuna
kitu kilichoelezewa kiusahihi kwenye mawazo ya mtu aliyeongoka. Mchakato wa kumshambulia
mtu zaidi sana kuliko kutathimini kile kilichosemwa ni muhimu kwenye nia na
mawazo ya mtu asiyeongoka.
Yuda 9 Lakini
Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya
mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na
akukemee.
Namna hii ya fikra imefanyiwa mkazo kwene
Makanisa ya Mungu na muhimu kwa mchakato ya kutawala nia na mawazo ya watu yaliyoendelezwa
na dini za uwongo kwa kipindi kirefu.
Uwezo wa kuweka kikomo mbali na programu hii
umesaidiwa na Mungu kwenye mchakato wa wito ambao unahusisha na shurutisho kwa
msingi wenye mashiko wa ukweli, ni kama inavyodhihirika kwa mwongofu au kwenye
moyo wa mwongofu. Moyo ule usiopenda kuelewa na kutenda sawasawa na kweli ya
Mungu ni ya mtu asiyeongoka na asiyehitaji kuongoka. Mafundisho ya kweli ya
Mungu na makosa ya uvunjaji wa sheria na amri za Mungu ni sehemu ya mchakato.
Zaburi 51:13 Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako.
Zaburi 51:13 Nitawafundisha
wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako.
Mchakato wa wongofu
ni wa muhimu, mchakato wa kurejesha vitu vyote kwa Mungu. Kumrudia Mungu ni
mchakato wa kuwa sawa na mtoto mdogo.
Mathayo 18:3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe
katika ufalme wa mbinguni.
Neno “mwongofu” lililo hapa ni strepho (SGD 4762) ambalo maana yake ni: (kutiwa nguvu kwa) kutikiswa. Hivyo ina
maana ya kuongoka kwa kugeuka nyuma.
Kuwa kama mtoto hakuna maana kubadilika
hata uwezo wa kufikiri. Watoto wadogo wanajulikana kwa mambo mawili. La kwanza
ni maswali ya kidadisi yasiyokoma. Swali la “Kwanini” linarudiwarudiwa sana
kuulizwa watati wa utoto kuliko kipindi chochote kile kingine. Jambo la pili ni
uwezo au kiwango cha kuamini au imani kwenye kweli za kile kilichopo kwenye
wakati ule. Kwa hiyo, imani ni ufunuo wa Mungu kwenye Biblia sehemu kuhimu sana
ya kuelewa. Hii haiwezi kutokea kwa kukubalika kusikoweza kuonewa mashaka kwa
kile wanadamu wanachosema kuwa Biblia inasema, lakini, zaidi sana, kile ambacho
kwa hakika inasema. Mchakato wa kuifundisha kweli unaenda kwenye tafsiri pia.
Mchakato wa wongofu unahitaji toba kama
ilivyoelezwa huko mwanzoni.
Matendo 3:19 Tubuni
basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa
kuwako kwake Bwana;
Wakati wa kuburudika ni mchakato wa kuwaita wateule na kisha marejesho na
matengenezo mapya ya hii sayari. Kwa hiyo mchakato huu ni moja wapo ya kuielewa
dhambi na ndipo imetolewa fursa ya kutubu. Wongofu ni mchakato ambao unahitaji
mtu kujirudi kutoka kwenye makosa na dhambi. Hakuna mtu atakayebakia kwenye
makosa na dhambini na akadai kuwa ameongoka. Nia ya kubadilika na kuishinda
dhambi inawezeshwa na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, haiwezekani kuuishinda
ulimwengu pasipo uweza wa Roho Mtakatifu. Vita vilivyoko ni vita vya kiroho na
mwanadamu hanabudi kuwa chini ya bwana mmoja au kwa yule mwingine. Wanadamu
hawawezi kuuepuka mchakato huu; watapaswa ama wamtumikie Mungu au kutumikia
Malaika muasi. Ili kumtumikia Mngu mtu atalazimika kuongozwa na kweli.
2Yohana 1-4 Mzee,
kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke
yangu, bali na wote waijuao ile kweli; 2 kwa ajili ya hiyo
kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele. 3 Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa
Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo. 4 Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako
wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.
2Wathesalonike 2:10 na
katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali
kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. 11 Kwa hiyo
Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; 12 ili
wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika
udhalimu
Kama tutazifuata dhambi na uwongo,
tutapewa nguvu zaidi za udanyanyifu. Inatupasa ama kuwa waangalifu na kuipenda
kweli au tusifanye hivyo. Kama hatufanyi hivyo, basi tutapewa nguvu za kutenda
dhambi zaidi na na kuendelea kutenda dhambi na makosa zaidi.
Kuipenda kweli ni alama ya mteule aliye na
Roho ya kweli.
Yohana 14:17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni
wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani
yenu.
Yohana 15:26 Lakini
ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli
atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
Kwa hiyo kweli huendelea kutoka kwa Baba
kupitia Roho Mtakatifu, na inapaswa iendane na haki na utakatifu.
Warumi 1:18 Kwa maana ghadhabu ya
Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu
waipingao kweli kwa uovu.
Iwapo kama mteule mmoja anaijua kweli na
akawa haihubiri kwa watu – yaani anaificha kweli – hasira ya Mungu itamwagwa
kutoka mbinguni kwa ajili yake. Hii ndiyo sababu wateule, kama watendakazi wazijuao
siri za Mungu, wanahukumiwa kutokana nay ale wanayoyajua na kuyatenda. Mteule hawezi
kubakia kimya au azinyamazie na kuvumilia dhambi. Inawapasa wanene na kutenda.
Viuno vya mteule ni kipimo kwa ajili ya
kweli.
Waefeso 6:14 Basi simameni, hali
mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
Ukweli ni kwamba ni muhimu kuzijua silaha
za Mungu. Pasipo kweli hatuwezi kufana lolote kwa kuwa tutaongozwa nayo na
kuwaongoza wengine kwenye uwongo (soma jarida la Kweli (Na. 168)).
2Timotheo 2:15-25 Jitahidi
kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya
kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. 16 Jiepushe
na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika
maovu, 17 na neno lao litaenea kama donda-ndugu.
Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto, 18 walioikosa
ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya
watu kadha wa kadha. 19 Lakini msingi wa Mungu ulio
imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila
alitajaye jina la Bwana na auache uovu. 20 Basi katika
nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya
udongo; vingine vina heshima, vingine havina. 21 Basi
ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima,
kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema. 22 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na
imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. 23 Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu,
ukijua ya kuwa huzaa magomvi. 24 Tena haimpasi mtumwa
wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha,
mvumilivu; 25 akiwaonya kwa upole wao washindanao
naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli;
Maagizo yaliyo kwenye 2Timotheo ni muongozo wetu
sote. Ukweli ni malengo yetu na maazimio yetu. Kweli ni kile kitendo cha
kuutafuta utakatifu.
Tito 1:1 Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli ile iletayo utauwa;
Kweli itakuwa ni alama ya marejesho mapya.
Isaya 65:16 Hata
itakuwa yeye atakayejibariki duniani, atajibariki kwa Mungu wa kweli; naye
atakayeapa duniani, ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za kwanza
zimesahauliwa, na kwa kuwa zimefichwa machoni pangu.
Hakuna mtu anayeweza kuutoa uwezo wake wa
kiakili na kumpa mwingine. Wanahukumiwa na kweli na jinsi wanavyokenenda katika
kweli. Kwa hiyo hakuna Kanisa linaloweza kunena na kumuelekeza mtu kinyume na
kweli ya Mungu. Kama fundisho lolote la mtu litakuwa kinyume na Maandiko
Matakatifu, ndipo yeyote yeyote anayeyafuata mafundisho yale atatoa hesabu
mbele za Mungu. Kwa hiyo, kuielewa Biblia na kumjua yeye Mungu wa Pekee wa
Kweli na Mwanae, Masihi, ni muhimu kwa kuupata na kuhesabiwa kwenye uzima wa
milele (Yohana 17:3). Kwa hiyo hakuna Kanisa la Waamini Utatu litakalokuwa
kwenye ufufuo wa kwanza kwa kuwa wanapinga mafundisho kwa uwepo wao na
kuendekeza uwongo kwa kimyakimya. Wanawajibika kwa Mungu na wameondolewa kwenye
ufufuo wa pili ili kwamba maisha yao yaokolewe kwenye ufufuo wa pili, kama
alivyokuwa yule mzinzi kwenye kanisa la Korintho.
1Wakorintho 5:4-5 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho
yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; 5 kumtolea
Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya
Bwana Yesu.
Waebrania 10:26-27 Maana,
kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena
dhabihu kwa ajili ya dhambi; 27 bali kuna kuitazamia
hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
Uasi wa makusudi dhidi ya kweli ndiyo dhambi ya
makusudi inayotajwa hapa kwenye Waebrania. Kwa hiyo, ufufuo wa pili wa wafu
ndiyo njia pekee ambayo kwayo watu hawa wanaweza kuokolewa kwayo. Kisha
watahukumiwa na kuadibishwa mbali na uwongo na kwa Yule Malaika muasi, kwa kuwa
hawakuweza kutofautisha kwa kuipambanua kweli na uwongo kwenye mazingira ambayo
yanatupeleka hukumuni. Tunahukumiwa kwa uwezo tuliopewa wa kupambanua kati ya
kweli na uwongo sasa na kuenenda kwa mujibu wa uelewa wetu ule. Kama hatutaenenda
ndipo tutaingia hukumuni kwenye ufufuo wa pili wa wafu. Kwa maneno mengine,
tunaondolewa kutoka kwenye mchakato sasa na kutolewa kwa mungu wa dunia hii ili
kwamba mjaribu na mfanya maudhi aweze kuokolewa katika siku za mwisho.
Ni kweli tu ndiyo inaweza kutuweka huru. wateule wanaijua na kweli
inawaweka huru (Yohana 8:32). Kila mtu anapaswa kuenenda kwa uelewa. Inawapasa
kutubu ili kwamba dhambi zao ziweze kufutwa (Matendo 3:19).
Mchakato wa kuwatenga wateule kwa mujibu wa kweli, ya muhimu, unapasa
mgawanyo wa wateule.
1Yohana 2:17-27 Na
dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu
hata milele. 18 Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama
vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi
wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. 19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama
wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe
kwamba si wote walio wa kwetu. 20 Nanyi mmepakwa
mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote. 21 Sikuwaandikia
ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba
hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli. 22 Ni
nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga
Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. 23 Kila amkanaye
Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia. 24 Ninyi
basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo
mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya
Mwana, na ndani ya Baba. 25 Na hii ndiyo ahadi
aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele. 26 Nimewaandikia
haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. 27 Nanyi,
mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu
kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote,
tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.
Mchakato wa kutoka nje kwa wateule haumaanishi kwamba wateule wanastahili
kwenye utaratibu shirikishi—hawapo hivyo. Wateule wanatakiwa kujitenga wenyewe
na wale wasioipenda kweli. Wale wasioongozwa na kweli hawaipendi kweli.
Tunawajua wateule kwa kuwa wanaipenda kweli na hawachukuliwi na kuyumbishwa na
uwongo. Wanauweka upendo wa kumpenda Mungu Mmoja Wapekee na wa Kweli na Mwanae,
Masihi kwenye kipaumbele kuliko kitu kingine chochote. Watu hawa wataurithi
Ufalme wa Mungu.
Wateule ni mfano kwa ulimwengu kwa
kuipenda kwao kweli na kwa kupendana wao kwa wao.
Luka 22:31-32 Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta
kama vile ngano; 32 lakini nimekuombea wewe ili imani
yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Umuhimu uliopo hapa ni kutiana nguvu kula
mtu na mwenziwe. Shetani anauwezo wa kumpepeta kila mteule kama Mungu ataruhusu
hilo litokee. Kristo anaomba
na kutuombea sisi dua. Petro aliokolewa kwa msaada wa Kristo. Hakuwa ameongoka
hadi alipompokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste.
Matokeo ya mwisho ya mchakato ni kwamba
walioongezwa katika Israeli watakombolewa na kuenea kwa wongofu ni kwa
ulimwengu wote.
Isaya 1:27 Sayuni
itakombolewa kwa hukumu, na waongofu wake kwa haki.
Tunawajibu kwa Mungu kuufanyia kazi
wongofu wa watu wetu na wa ulimwengu. Tumeitwa kwa kusudi hili na kwa kazi hii.
Kama watu wanavyotiwa nguvu na Roho Mtakatifu wamewekwa huru kuelekea kwenye
lengo stahili. Wateule hawajitengi mmoja mmoja au kwa utaratibu wa ushirika wa
amoja. Wateule huipima na kuitawanya kweli. Wanaiskia sauti ya mchungaji na
kujuana kila mmoja. Watu wetu wamekabiliana, nab ado wanakabiliana na magumu makubwa
kwa ajili ya kweli ya Mungu. Tutiane moyo kila mmoja wetu na kusaidiana katika kweli.
q