Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[073]
Samsoni na Waamuzi
(Toleo
La 2 19941022-20031011)
Matendo na maovu ya Israeli waliyoyafanya wakiwa kipindi cha uongozi wa
Waamuzi kulipelekea hatimaye kuinuka kwa Samsoni akiwa kama Mwamuzi wa Israeli
akitokea kabila la Dani. Habari hii imeelezewa kwa kina kwa mtazamo wa kiroho,
ukionyesha mlolongo wa matukio kama unavyochukuliwa na kufananishwa na
maendeleo ya Roho Mtakatifu kwa kila mtu kwa maelekezo ya Yesu Kristo na pia
kwenye Kanisa kama kundi. Hadithi hii ina mafundisho mazuri nay a kushangaz kwa
siku zetu za sasa kwenye uelewa wa matendo na kazi za Masihi na kwa Kanisa.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1994, 1998, 1999, 2003 WadeCox)
(tr. 2015)
Masomo
haya yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa
kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na
tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa
mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza
kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka
maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Waamuzi
Bwana aliwaingiza kwenye nchi ya ahadi Israeli wakiwa chini ya uongozi wa
Yoshua (wokovu)\mwana wa Nuni (uvumilivu). Israeli walimtumikia Bwana siku zote
za Yoshua na siku za wazee wa Israeli (mabaki ya wale Sabini) ambao waliishi na
kuhudumu baada ya Yoshua, aliyefariki akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi (Waamuzi
2:7-8). Vizazi vyote walikusanyika na mababa zao, yaani, walifariki (Waamuzi
2:10). Wana wa Israeli walifanya maovu baada ya hayo na wakamtumikia Baalimu au
Mabwana wengine (Waamuzi 2:11). Na hii ikafanyika kuwa ni tabia yao Israeli kwa
kanuni na sheria zao. Kuna maovu sita yaliyoorodheshwa na kuandikwa kwenye
Waamuzi 3:7,12; 4:1; 6:1; 10:6; 13:1. Kuwatumikia huku miungu mingine, wakiwemo
Baali na Ashtorethi, kulimkasirisha sana Bwana na kumchukiza na akawatoa
mikononi mwa waangamizi na mikononi mwa maadui zao ili wasiweze kuwashinda (Waamuzi
2:12-14). Wakati wowote walipokwenda vitani mkono wa Bwana ulikuwa kinyume chao
(Waamuzi 2:15). Walipelekwa utumwani na Mungu akawainulia Waamuzi wa kuwaokoa (Waamuzi
2:16).
Waamuzi 2:17-23 Lakini
hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu
mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile
waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za Bwana bali wao hawakufanya hivyo. 18 Na wakati Bwana alipowainulia waamuzi, ndipo Bwana
alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za
mwamuzi huyo; maana Bwana alighairi kwa ajili ya kuugua kwao kwa sababu ya watu
wale waliowaonea na kuwasumbua. 19 Lakini ikawa,
wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao,
kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha
matendo yao, wala njia zao za ukaidi. 20 Basi hasira
ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili wamelihalifu
agano langu nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu; 21 mimi nami tokea sasa sitalifukuza taifa mojawapo la hayo
aliyoyaacha Yoshua alipokufa; 22 ili kwa njia ya hayo
nipate kuwajaribu Israeli, kwamba wataishika njia ya Bwana kwenda katika njia
hiyo, au sivyo. 23 Basi Bwana akawaacha mataifa yale,
wala hakuwafukuza kwa upesi, wala hakuwatia katika mikono ya Yoshua.
Israeli waliachwa na kutawanyishwa kwenye mataifa mbalimbali yaliyobakia
yakiwakalia ili kwamba Israeli wajaribiwe kwa kupitia mataifa hayo (Waamuzi 3:1-4).
Waamuzi 3:1-11 Basi
haya ndiyo mataifa ambao Bwana aliwaacha, ili awajaribu Israeli kwa hao, yaani,
awajaribu hao wote ambao hawakuvijua vita vyote vya Kanaani; 2
ili kwamba vizazi vya wana wa Israeli wapate kujua ili kuwafundisha
vita, hasa wao ambao hawakujua vita kabla ya wakati ule; 3 aliwaacha
wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa
katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi. 4 Naye aliwaacha ili awajaribu Israeli kwa hao, apate kujua
kwamba watasikiliza amri za Bwana, alizowaamuru baba zao, kwa mkono wa Musa. 5 Basi wana wa Israeli wakaketi kati ya Wakanaani; hao
Wahiti, na hao Waamori, na hao Waperizi, na hao Wahivi na hao Wayebusi; 6 wakawaoa binti zao, na binti zao wenyewe wakawaoza wana
wao waume, na kuitumikia miungu yao. 7 Wana wa Israeli
walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakamsahau Bwana, Mungu
wao, nao wakawatumikia Mabaali na Maashtorethi. 8 Kwa
hiyo hasira za Bwana ziliwaka juu ya Israeli, naye akawauza na kuwatia mikononi
mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia; na wana wa Israeli wakamtumikia
huyo Kushan-rishathaimu muda wa miaka minane. 9 Kisha
wana wa Israeli walipomlingana Bwana, Bwana akawainulia wana wa Israeli
mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu. 10 Roho ya Bwana ikamjilia juu yake, naye akawa mwamuzi wa
Israeli; akatoka kwenenda vitani, naye Bwana akamtia huyo Kushan-rishathaimu,
mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda
Kushan-rishathaimu. 11 Nayo nchi ikawa na amani muda
wa miaka arobaini. Kisha Othnieli, mwana wa Kenazi, akafa.
Kila wakati mwamuzi aliyechaguliwa na kuwekwa na Bwana alipokufa, watu
waligeuka na kufanya maovu na kuandama ibada za sanamu. Hawa Waamuzi walikuwa
na Roho Mtakatifu, aliyejulikana kama Roho wa Bwana. Mfano wa jinsi hilo
lilivyofanyika umeonyeshwa kwenye hadithi ya Samsoni, ambao utaelezewa kwa kina
hapo chini.
Baada ya Othnieli (maana yake ni jeshi
la Mungu) ambaye alikuwa ni mwana wa Kenazi, ndugu wa Kalebu, kufa walitenda
dhambi tena.
Waamuzi 3:12-15 Basi
wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu tena mbele za Bwana; naye Bwana akamtia
nguvu Egloni mfalme wa Moabu juu ya Israeli, kwa sababu walikuwa wameyafanya
yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana. 13 Huyo Egloni
akakutanisha kwake wana wa Amoni na Amaleki; akaenda na kuwapiga Israeli, nao
wakauchukua huo mji wa mitende. 14 Wana wa Israeli
walimtumikia Egloni mfalme wa Moabu muda wa miaka kumi na minane. 15 Lakini wana wa Israeli walipomlilia Bwana, Bwana
akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye
shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa
huyo Ehudi.
Zawadi ambayo walimtumia Egloni, mfalme wa Moabu, ilikuwa ya namna ya sime iliyosimikwa
kwa Ehudi, mwana wa Gera, kwenye paja la kuume ya Mbenyami (Waamuzi 3:16).
Wabenyamini waliachwa wamepewa, jambo lililodaiwa kuwa ni upewaji dhaifu
kuliko zote. Mfano ni kwamba Mungu huathiri mpango wa ukombozi kwa kupitia vitu
dhaifu sana. Kutoka kwa vitu vidhaifu sana anawezesha kuwepo na uweza. Hii imeathiri
mara saba kwenye mfano kielelezo wa Waamuzi 1Wakorintho 1:27; 2Wakorintho 12:9.
Nazo ni:
· Mkono wa kushoto
(Waamuzi 3:21);
· Fimbo ya
kuswagia ng’ombe (Waamuzi 3:31);
· Mwanamke (Waamuzi
4:4);
· Msumari au kucha
(Waamuzi 4:21);
· Kipande cha
jiwe la jiwe la kusagia (Waamuzi 9:53);
· Wasimika hema na
tarumbeta (Waamuzi 7:20); na
· Mfupa wa taya la
punda (Waamuzi 15:16).
Bullinger (soma tafsiri ya Companion Bible, kwen.ye
Waamuzi 3:21) anashikilia kuamini kwamba mlolongo huu wa matukio uliendelea
kwenye nyakati zilizofuata kwenye harakati za Luther (mtoto wake mdogo), Calvin
(mwana wa mtengeneza mapipa), Zwingle (mtoto wa mchungaji, Melancthon (mtoto wa
armoureri) na John Knox (mtoto wa halisi wa mwenyeji). Kwa hiyo watano hawa
walionekana kama walifana idadi ya watu saba. Hitimisho ni huenda ni zaidi kwa
kufikia kuliko wale aliowaona Bullinger.
Ehudi alitoroka baada ya kumuua Egloni na
akawahutubia Israeli kutoka kwenye milima ya Efraimu.
Waamuzi 3:27-30 Ikawa,
hapo alipofika akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, ndipo
wana wa Israeli wakatelemka pamoja naye kutoka huko milimani, naye
akawatangulia. 28 Akawaambia, Niandameni mimi; kwa
kuwa Bwana amewatia adui zenu, Wamoabi, mikononi mwenu. Basi wakatelemka na
kumfuata, wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha Wamoabi, wala hawakumwacha
mtu kuvuka. 29 Wakati huo wakapiga katika Wamoabi watu
waume wapata kama elfu kumi, ambao wote walikuwa wanene, na wote mashujaa;
hakupona hata mtu mmoja. 30 Basi Moabu alishindwa siku
hiyo chini ya mikono ya Israeli. Nayo nchi ikawa na amani muda wa miaka
themanini
Kwa hiyo vizazi viwili vilipita. Baada ya Ehudi alifkuwepo
au kufuatiwa na Shamgari, mwana wa Anathi, aliyewaua Wafilisti mia sita kwa
taya au mfupa wa punda (Waamuzi 3:31). Wakati Ehudi alipofariki, baada ya Shamgari,
watu walifanya maovu tena machoni pa Bwana na aliwaokoa kutoka kwenye mikono ya
Wakanaani chini ya Yabini wa Hazori, ambaye ndiye alikuwa mkuu wa majeshi wa
Sisera na waliwatesa Israeli kwa mateso makubwa sana kwa kipindi cha miaka
ishirini (Waamuzi 4:1-3).
Debora, nabii mke wa Efraimu, aliyeishi katikati
ya Rama na Beth-eli aliwaamua Israeli wakati ule. Kwa maongozi ya Mungu,
alimuelekeza Baraka awakusanye watu wa makabila ya Naftali na Zabuloni ili
wakawaokoe Israeli.
Kimsingi, hapo mwanzoni Israeli walisalitiwa
kibiashara na Heberi (maana yake ni jamii
au jumuia au ushirika na pia ni mhamasishaji),
Wakeni, ambao ni wana wa Hobabu, babu yake Musa. Alijitenga mbali na Wakeni na
aliweka hema ya kambi lake kwenye nchi tambarare ya Zaanaimu (maana yake ni yaliyozolewa na kuondolewa) karibu na
Kedeshi (Naftali) (Waamuzi 4:11-12). Kulikuwa na amani kati ya watu wa Heberi, Wakeni,
na Yabini, mfalme wa Hazori (Waamuzi 4:17). Sisera akakimbia na kuelekea kwenye
hema za Heberi. Mke wa Heberi Yaeli alitoka nje kwenda kukutana na Sisera na,
baada ya kumpa ulinzi, alimuua kwa haraka kwa kumshindilia msumari kwenye
hekalu lake hadi chini sakafuni (Waamuzi 4:21-22).
Kwa hiyo, Mungu aliwanyenyekesha Wakanaani, na
kuwafanikisha Israeli. Wimbo wa Debora unaonyesha kwamba, Malaika wa mbinguni
walihusika kupigana vita hivi (Waamuzi 5:20). Vita tunavyopigana kwenye mchakato
huu sio vita vya kutumia silaha zinazoonekana, bali vinajumuisha uweza wa
Malaika wa mbinguni.
Ardhi ilipumzika kwa kipindi cha miaka arobaini (au kizazi kingine) na
kisha walianguka kwa kurudia tena kuabudu sanamu na Mungu akawafanya wawe
mateka kwenye mikono ya Wamidiani kwa miaka saba. Israeli waliishi mapangoni na
kwenye miamba ya milima. Wamidiani na Waamaleki na wana wa mashariki walikuja
wakiwashukia Israeli na kuharibu mazao na kuwaacha Israeli wakiwa hawana
chakula wala mifugo (Waamuzi 6:1-5). Israeli wakamlilia Bwana na waakatumiwa
Gideoni wa kabila la Manase. Hadithi ya Gideoni (maana ya jina lake ni kuuangusha mti au kukata na kuangusha chini na, kwa hiyo ni, mwangushaji au mtu shujaa)
au Yerubaali (maana yake ni Baali atashindana)
(Waamuzi 6:1 hadi 8:28) inaelezewa na kufundishwa kwenye jarida la Jeshi la Gideoni na Siku za Mwisho (Na. 22). Kiini cha hadithi hii kinahusika na
kufanya taswira ya siku za mwisho na kwenye hadithi ya kuondoa ibada za sanamu
na vita iliyojitokeza kila mara iliyofuatia, kutokana na ukweli wa kwamba Baali
anashindana katika siku za mwisho. Maana yake kwa wateule na ukengeufu wa siku
za mwisho kunahitajika masomo au mafundisho.
Gideoni alikuwa na wana sabini, ambao waliweka
taswira ya baraza la wazee. Mara tu baada ya kufa kwake Gideoni, Israeli
walitenda dhambi tena kwa kufanya ukahaba na muingu migeni. Jambo hili
lilijitokeza kila wakati ambapo mwamuzi alipokuwa anakufa. Israeli waliuacha
ujumbe wa Mungu na kugeukia ibada za sanamu, hadi pale walipomlilia Mungu na
akawainulia mwamuzi mwingine. Kila wakati mwamuzi alitoka kwenye kabila
linguine na alikuwa na mamlaka ya kitofauti na yale ya mwamuzi aliyemtangulia.
Haikuwahi kutokea kwamba mtoto wa mwamuzi amrithi huduma hii hata kwa sababu
iliyoonenaka kuwa ni njjema, au kwa kuamriwa na Mungu.
Abimeleki, mwana wa Yerubaali, au Gideoni aloyemzaa
na mjakazi wake (Waamuzi 9:18) alifanywa kuwa mfalme wa Shekemu, kwa watu wa
nyumba ya mama yake. Abimeleki akawatawala Israeli kwa miaka mitatu (Waamuzi
9:22). Utawala wa Abimeleki ni taswira ya jaribio la kwanza la kutwaa kwa nguvu
au kunyang’anya mamlaka baraza la kidini la Sanhedrin hadi kwenye kipindi cha
ufalme. Abimeleki alimuua kaka yake mwenyewe, wa sabini, ili ajitwalie utawala.
Abimeleki aliuawa na mwanamke aliyempiga kwa kipande cha jiwe la kusagia kutoka
kwenye mnara wa Tebesi. Ilivunja fuvu la kichwa chake na akamuomba mbeba silaha
wake amuue ili asisimangwe na watu kuwa aliuawa na mwanamke (Waamuzi 9:53-54). Kwa
jinsi hiyohiyo, huu ni mfano kwa Malaika ambapo Shetani, ambaye anafanya vita
ya sabini Malaika watakatifu, ameshindwa na mwanamke ambaye ni Kanisa lake
Mungu.
Baada ya Abimeleki, mwenye kuwashindia Israeli, alikuwa
ni Tolasoni wa Pua wa kabila la Isakari. Aliishi huko Shamiri kwenye Mlima wa Efraimu
na aliwaamua Israeli kwa miaka ishirini na tatu (Waamuzi 10:1-2). Baada ya Tola
alifuatiwa na Yairi, Mgileadi, aliyewaamua Israeli kwa miaka ishirini na miwili
(Waamuzi 10:3). Alikuwa na wana thelathini ambao waliendesha magari ya farasi.
Mlolongo wa mambo tunaouona ni kwamba Wokovu kwa njia ya Uvumilivu umerithiwa
kutoka na hukumu ya Malaika. Kulikuwa na jumla ya waamuzi kumi na wawili katika
Israeli baada ya Yoshua hadi kufikia zama za kuanzishwa utawala wa wafalme.
Yoshua alikuwa ni Kiongozi wa Vita wa Israeli chini ya Musa. Aliwaongoza
Israeli kuwaingiza Palestina na kufanikiwa kuiteka ardhi hii. Baada ya yeye
Waamuzi wa Israeli wanaonekana kama mwanzo wa utawala.
Hawa ndio waliohudumu kuwa waamuzi:
· Othenieli, mwana
wa Kenazi, mpwae Kalebu;
· Ehudi wa kabila
la Benyamini;
· Shamgari, mwana
wa Anathi;
[Baada ya Ehudi kufariki watu walitolewa kwenye mateso ya Yabini mfalme
wa Kanaani. Kwa jinsi hii Shamgari alikuwa sio mwamuzi wa moja kwa moja kama tunavyoona
kwenye Waamuzi 3:31-4:4].
· Debora nabii
mke, mke wa Lapidothi wa Efraimu (alimtumia Baraka wa Naftali alikuwa kiongozi
wa vita) (Waamuzi 4:4-7);
· Gideoni alikuwa wa
kabila la Manase;
[Abimeleki mnyang’anyaji, mwana wa Gideoni kwa mwanamke Mshekemu, alijifanya
kuwa mfalme wa uwongo. Hii ndiyo mana ya kuitwa mnyang’anyi. Hakuwa mmoja wa
wale waamuzi kumi na wawili ila alikuwa mfalme bandia na wa uwongo.]
· Tola, mwana wa Pua wa
kabila la Isakari, aliwaamua miaka ishirini na tatu (Waamuzi 10:1-2);
· Yairi wa Gileadi (Gadi
na Manase), aliwaamua kwa miaka ishirini na miwili (Waamuzi 10:3-5);
· Yepta Mgileadi, mwana
wa mwanamke kahaba (Waamuzi11:1), aliwaamua miaka sita (Waamuzi 12:7).
Yefta alihamasishwa na wana wa Gileadi, ndugu zake
kutoka kwa mke wa Kigileadi. Makiri, mwana wa Manase, alikuwa ni baba wa
Gileadi (Yoshua 17:1). Kwahiyo, mwamuzi wa Israeli hapa alikuwa ni mtoto wa haramu
wa mwanamke kahaba wa Gileadi. Wakati Wagileadi walipoingia kwenye matatizo,
wazee walimjia na kuomba msaada wake na kumfanya awe kiongozi wao (Waamuzi
11:9-11). Yefta aliwashinda na kuwatiisha Waamoni. Alikuwa ni Yefta huyuhuyu
ndiye aliyejipiz kiapo kilichomletea madhara binti yake kwamba atamtoa sadaka
kwa Bwana. Tafsiri ya Biblia iitwayo Companion Bible inaenda mbali kwa kudhani
kwamba kama sadaka yake ilivyokuwa isiyo sahihi, andiko linamtaja binti huyu
kuwa alikuwa ni bikira. Andiko lililo kwene Waamuzi 11:34-40 haiashirii hivyo
na tafsiri ya Soncino inaichukulia sadaka hii kuwa ni kama kitu kisicho na
maana yoyote kwa kweli. Kwa mjibu wa Talmud (Taan. 4a) na vyanzo vingine kadhaa
vya marabi, ikiwemo Targum, vinamchukulia kuwa alikuwa ni sadaka ya kutosha
kabisa kwa kweli. Kimchi alielezea kuhusu andiko lisemalo Sitoweza kurudi nyma kwamba kisheria kiapo hiki kilitanguka na
kingeweza kutanguliwa. Kwa mujibu wa Soncino:
Kile kijulikanacho
kama Midrash Rabbah (Mwisho wa huduma ya Kilawi) inahusiana kwamba angeweza
kwenda kwa Finehasi au Kuhani Mkuu angeenda kwake na ndipo kiapo chake
kngetanguliwa. Kila mmoja alisimama kwa uadilifu wake na kuwangojea wengine
wachukue hatua, na kati ya hawa wawili walipatilizwa. Wote wawili waliadhibiwa,
Utukufu au Uwepo wa Mungu ukaondoka kwa Finehasi na ukoma ukampata Yefta.
Fundisho la kujifunza hapa ni kwamba hakuna mtu
anayefungwa katika Israeli kwa kiapo ambacho kinavunja sheria ya Mungu. Kosa la
kuhani la kutochuku hatua na watu binafsi kuikana au kuiacha imani ni kuondoka
kwa Roho Mtakatifu kwa kila mtu binafsi mhusika. Wingu lijulikanalo kama Shekina
litakuwa kwa wale wanaoonyesha kuzaa matunda. Malumbano ya kwamba mtu
aliyejikita kwenye mashirika au vikundi, vinavyoenda kinyume na maagizo ya
Biblia, kwa kudhani kwamba kuna mtu aliyepewa mamlaka ya Mungu kupitia Roho
Mtakatifu ni ya uwongo kabisa. La muhimu sana zaidi, ni kwamba mtu anayeshindwa
kuenenda hivyo atakufa. Ugonjwa wa ukoma ni mbaya sana, ambao unaonyesha mfano
wa kuharibika au kuangamia kwa mwili wa kiroho. Malumbano ya hivi karibuni
kuhusiana na kutii na kujinyenyekeza kwenye makanisa yaliyokengeuka, au kufuata
utaratibu wa shirikisho, ni kitendo kibaya sana na kudhuru, kwa wote wawili,
makuhani wanaojua na kuelewa vyema kabisa na walio kwenye mafundisho hayo ya,
na watu wanaojidanganya wenyewe kwa kufuata ushauri kama huo. Makund yote
mawili, yaani ya makuhani na wazee watakufa.
Yefta pia alipitia kwenye vita ya ndani kwa sababu
ya makosa yake. Waefraimu wote walikusanyika kinyume chake na watu 42,000 wa Efraimu
waliuawa kwenye maeneo ya kingo za Yordani kwa kuwa walishindwa kulitamka
sawasawa neno Shibolethi bali zaidi sana tu wao walilitamka Sibolethi (Waamuzi
12:1-6). Shibolethi maana yake kijito kinachofuatia, ambacho ni kidogo, na pia
ni tawi au ni kama kichala cha mahindi.
Maana ya makosa hasiyoelezwa yanaonyesha huenda
kwamba taswira inayowatambulisha wateule inatolewa na kuna hasara kubwa katika
Efraimu kulikotokana na makosa yao ya kutochukua hatua. Munbu anawachukulia hatua kuwatetea na ana umuhimu
na ubora kwao. Wagileadi wanakuwa wakimbizi katikati au ndani ya Wamanase (Waamuzi
12:4-5) lakini watapewa uweza katikati yao wakiwa kama jeshi la Israeli. Tunajua
kwamba Wamanase, Wareubeni na Wagadi walipokea urithi wao ng’ambo ya Yordani, na
Wamanase walipewa urithi wa ziada katika Israeli. Mfano wa jambo hiili nii
kwamba Manase, Reubeni na Gadi walipokea urithi nje ya Israeli. Makabila ya Gadi
na Manase yote mawili yaliishi katika nchi iliyojulikana kama Gileadi, upande
wa mashariki mwa Yordani.
Waamuzi waliofuatia ni:
· Ibzani wa
Bethlehemu, aliyewaamua miaka saba. Alikuwa na wana thelathini na mabinti thelathini
kutoka nje kwa wanawe (Waamuzi 12:8-10). Hii ni taswira ya baraza la ndani.
· Eloni wa Zebuloni,
aliwaamua miaka kumi (Waamuzi 12:11).
· Abdoni, mwana
wa Hilleli Mpirathi wa Efraimu, aliwaamua kwa miaka minane. Alikuwa na wana
arobaini na wapwaze thelathini walioendesha magari ya farasi sabini (Waamuzi
12:13-14). Hii ni taswira ya baraza
lote kamili la waliorejeshwa sabini.
Baada ya hii, wana wa Israeli walitenda dhambi na Bwana akawatia mikononi
mwa Wafilisti kwa kipindi cha miaka arobaini, kama alivyofanya huko nyuma na
Wamoabi (Waamuzi 13:1). Wakati wa kipindi hiki, Samsoni alikuwa mwamuzi.
Waamuzi wawili wa mwisho wameendelea hadi kwenye 1Samweli ambao ni Eli na Samweli
na ndio walikuwa ni waamuzi wa mwisho wa Israeli. Samweli alikuwa nabii na
mwamuzi katika Israeli, ambaye alimtia mafuta Sauli awe mfalme na kutimika chini
yake au kipindi chake, lakini kwa hakika hakuhesabiwa au kujumuishwa miongoni
mwa wale waamuzi kumi na wawili. Baada ya kufariki Eli ndipo mfumo wa utawala
wa kifalme ulianza.
Samsoni
Waamuzi 13:1-25 Wana
wa Israeli wakafanya tena yaliyo mabaya mbele za macho ya Bwana, Bwana akawatia
katika mikono ya Wafilisti, muda wa miaka arobaini. 2 Palikuwa
na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe
alikuwa tasa, hakuzaa watoto. 3 Malaika wa Bwana
akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini
utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume. 4 Basi
sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho
najisi; 5 kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa
mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa
mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya
Wafilisti. 6 Ndipo yule mwanamke akaenda akamwambia
mume wake, akisema, Mtu wa Mungu alinijia, na uso wake ulikuwa kama uso wa
malaika wa Mungu, wa kutisha sana; nami sikumwuliza, Umetoka wapi? Wala
hakuniambia jina lake; 7 lakini aliniambia, Tazama,
utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala
kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa
Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.
Ukombozi wa Israeli ulifanywa na Malaika wa Yahova. Malaika huyu anaelezewa
kuwa ni Kristo (soma majarida ya Mteule Kama Elohim (Na. 1) ; Uwepo wa Zama ya Kabla ya Kuzaliwa Kimwili Yesu Kristo (Na. 243) na Maila wa YHVH (Na. 24)). Samsoni aliteuliwa na kutengwa mahsusi tangu kuzliwa kwake kuwa ni
mtakatifu kwa Bwana. Hii inatokana na dhana ya kukusudiwa na kujulikana kwa
wateule kulikofanywa tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia. Urithi wa Dani ulikuwa
ni kuwahukumu watu wake kama mojawapo ya makabila ya Israeli (Mwanzo 49:16) na Samsoni
alikuwa ni wa kwanza na mfano mkubwa wa jambo hili. Hata hivyo, unabii huu
haukuhitimishwa tni wa kwanza na tni wa kwanza na kwa Samsoni. Kulikuwako pia
mji wa Dani kaskazini mwa Palestina wakati wa Ibrahimu (Mwanzo 14:14), ambao ni
tofauti na huyu mtoto wa Lea aliyeitwa Dani na walio kwenye kabila lake la
Dani. Eneo hili la kale lilikuwa kaskazini mwa Gileadi. Waamuzi 18:30 inaelezea
ibada za sanamu za wenyeji wa Dani. Kujumuishwa kwa Dani na Ufraimu kwenye
Ufunuo 7:4 kama kabila la Yusufu, ni jambo linaloonekana wakati mwingine kama
hukumu kwa kabila la kwanza lililoingia kwenye ibada za sanamu (soma pia
Kumbukumbu la Torati 29:18-21; Mambo ya Walawi 24:10-16; 1Wafalme 12:30; 2Wafalme
10:29). Ni ili kuwawezesha kabila la Lawi waingie wakiwa jumla ya watu144,000 kama
makuhani.
Kufanywa kwa mwamuzi kuwa ni Mnazarayo au Mnadhiri toka kuzaliwa kwake, ni
alama pia ya mteule. Nadhiri za Mnazarayo zilikuwa zinadumu, na hazikuwa muhimu
sana kama za Masihi ambaye yeye mwenyewe hakuwa Mnadhiri. Kutokana na
kumbukumbu za Biblia, hakuna mahali panapoonyesha kuwa huduma ya Kristo
ilimlazimu aweke kiapo cha kuwa Mnadhiri. Elimu ya Samsoni pia ilikuwa chini ya
maelekezo na maongozi.
Aamuzi 13:8-18 Ndipo
huyo Manoa akamwomba Bwana, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu
uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo kumfanyia
huyo mtoto atakayezaliwa. 9 Mungu akasikiza sauti ya
Manoa; naye malaika wa Mungu akamwendea yule mwanamke tena alipokuwa anaketi
shambani; lakini mumewe, Manoa, hakuwapo pamoja naye. 10 Basi
huyo mwanamke akaenda haraka, akapiga mbio, na kumwambia mumewe, akisema, Tazama,
huyo mtu amenitokea, huyo aliyenijilia siku ile. 11 Basi
Manoa akainuka, akamwandama mkewe, na kumfikilia mtu huyo, akamwuliza, Je! Wewe
ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Naam, ni mimi. 12 Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia,
je! Huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini? 13 Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, Katika hayo yote
niliyomwambia huyo mwanamke na ajihadhari. 14 Asile
kitu cho chote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala
asile kitu cho chote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze. 15 Kisha Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana, Nakuomba,
tukuzuie, ili tupate kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako. 16 Lakini
malaika wa Bwana akamwambia Manoa, Ujapokuwa wanizuia, sitakula katika mkate
wako; na kwamba wataka kufanya tayari sadaka ya kuteketezwa, inakupasa
kumsongezea Bwana. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa Bwana. 17 Manoa akamwambia huyo malaika wa Bwana, Jina lako ni
nani, ili kwamba hapo hayo maneno yako yatakapotimia nipate kukutukuza? 18 Huyo malaika wa Bwana akamwambia, Kwani wewe kuniuliza
jina langu, kwa kuwa jina hilo ni la ajabu?
Neno kustaajabisha (limetafsiriwa
kamairi kwenye tafsiri ya KJV likonyesha kubadilisha maana halisi ya uhusiano) ni
jina la Masihi kwenye Isaya 9:6.
Waamuzi 13:19-25 Basi
Manoa akamtwaa yule mwana-mbuzi, pamoja na sadaka ya unga, akamtolea Bwana hapo
juu ya mwamba; huyo malaika akatenda la ajabu; Manoa na mkewe wakaangalia. 20 Kwa maana, ikawa, mara huo mwali wa moto ulipopaa juu
mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa Bwana akapaa katika mwali wa
moto wa madhabahu; nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakainama kifudifudi. 21 Lakini malaika wa Bwana hakumtokea Manoa tena, wala
mkewe. Ndipo Manoa alipojua ya kwamba ndiye malaika wa Bwana. 22 Manoa akamwambia mkewe, Hakika yetu tutakufa sisi, kwa
sababu tumemwona Mungu. 23 Lakini mkewe akamwambia,
Kama Bwana angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya
unga, mikononi mwetu, wala hangetuonyesha mambo hayo yote, wala hangetuambia
mambo kama hayo wakati huu. 24 Basi yule mwanamke
akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, Bwana
akambarikia. 25 Roho ya Bwana ikaanza kumtaharakisha
katika Mahane-dani, katikati ya Sora na Eshtaoli.
Jina Samsoni maana yake ni nuru au mwanga wa jua na kwa kupitia nuru
ya ulimwengu, Israeli wanapewa haki yao. Roho wa Bwana ndiye silaha ambayo
Samsoni alipewa nguvu zake kwaye. Nywele za Samsoni ndizo zilizoonekana kama
ishara ya nje ya nguvu zake au zilikuwa pia ni ishara ya kimwili aliyopewa
ikiwa kama ahirio la uwepo wa Roho Mtakatifu.
Kabila la Dani waliweka hema zao huko
Mahane-Dani au kwenye kambi ya Dani ambako ni Kiriyathi-yearimu katika Yuda/
kutoka hapo walikwenda na kuingia Efraimu na kuziondoa sanamu au terafimandi kutoka
kwenye nyumba ya Mika na kuanzisha uwekaji wa Laishandi kwenye sanamu ya
kuchongwa ya Mika katika nyumba ya Mungu katika wakati wote ambacho ilikuwa
huko Shilo na Yonathani mwana wa Gershomu mwana wa Manase, Mlawi, na wanawe
walikuwa ni makuhani hapo (Waamuzi 18:12-13, 30-31).
Mfano wa kwanza tulionao wa Samsoni ni
pale anapoomba aoe mwanamke wa Kifilisti na kuwaomba wazazi wake wampe binti huyo.
Mipango ya kuoa iliandaliwa na wazazi na hasahasa baba (Wanzo 21:21; 24:4; 34:8
Kutoka 21:9; soma kitabu cha Soncino, Daath Mikra). Mipango ya kuoa iliandaliwa
na baba ni taswira ya kutolewa kwa wateule kwenye arusi na Kristo. Kwa mujibu
wa kitabu cha Soncino, marabi waliamini na kufundisha kwamba kabla ya kuolewa
mwanamke anaweza kuwa mwongofu aliyetoka kwenye umataifa kama ilivyokuwa haimithiliki
kwamba Mnadhiri anaweza kuishi na mwanamke mmataifa asiye Muisraeli (Kimchion
12:4, Metsudath David). Ukweli ni kwamba wateule wote walikuwa ni Wamataifa
walioitwa na wakatoka kutoka kwenye imani za kimataifa na kuandaliwa kwenye
arusi kupitia kwa Roho Mtakatifu na Masihi mwamuzi aliyeonekana kimfano hapa
kama Mwamzi au wa Dani ambaye ni mwamuzi wa Israeli kama kabila hapa na kuwa
mwamuzi wa waamuzi wa kimwili.
Waamuzi 14:1-4 Samsoni
akatelemkia Timna, akaona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti.
2 Kisha akapanda, akawaambia baba yake na mama yake,
akasema, Nimemwona mwanamke huko Timna, mmojawapo wa binti za Wafilisti; basi
mnipatie, nimwoe. 3 Ndipo baba yake na mama yake
wakamwambia, Je! Hapana mwanamke hata mmoja katika ndugu zako, au katika jamaa
zangu zote, hata uende kumwoa mwanamke kwa hawa Wafilisti wasiotahiriwa?
Samsoni akamwambia baba yake; Mnipatie huyo, kwa maana ananipendeza sana. 4 Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili
ni la Bwana; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti
walikuwa wakiwatawala Israeli.
Hapa tuna usemi maalumu unaoonyesha kuwa alikuwa Malaika wa Yahova (aitwaye
Yahwe au Yehova) ndiye aliyekuwa anamtumia Samsoni kwa kujifungamanisha na
hatimaye kuwapiga Wafilisti. Watu hawa wanawakilisha Wamataifa ambao walipewa
mamlaka ya kuwatawala Israeli kwa utumwa wa Wababeloni, hadi pale nyakati za
Mataifa zilipohitimika. Akiwa kama Malaika wa Bwana aliwaokoa Israeli kutoka
mikononi mwa Wafilisti kwa kupitia Samsoni, na ndivyo hivyo atawakomboa Israeli
katika siku za mwisho kwa kupitia utaratibu wa hukumu ya watu waliochanganika
kati ya Wadani na Waefraimu (Yeremia 4:15) na mashahidi (Ufunuo 11:1-2) ambao watatangulia
ujio wake akiwa kama mfalme Masihi (sawa na majarida ya Maonyo ya Siku za Mwisho (Na. 44) na Mashahidi (wakiwemo Mashahidi Wawili) (Na. 135)).
Waamuzi 14:5-11 Ndipo
Samsoni na baba yake na mama yake wakatelemkia Timna, wakafika mashamba ya
mizabibu huko Timna; na tazama, mwana-simba akamngurumia. 6 Roho
ya Bwana ikamjilia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi,
wala hakuwa na kitu cho chote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na
mama yake aliyoyafanya. 7 Basi akatelemka na
kuzungumza na huyo mwanamke; naye akampendeza Samsoni sana. 8
Kisha baadaye akarudi ili kumtwaa, naye akageuka kando kuuangalia mzoga
wa huyo simba; na tazama, nyuki wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na
asali. 9 Akatwaa asali mikononi mwake akaenda mbele,
huku akila alipokuwa akienenda, akawafikilia babaye na mamaye, akawapa, nao
wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba. 10 Basi babaye akamtelemkia huyo mwanamke; Samsoni naye
akafanya karamu huko; kwa kuwa vijana ndivyo walivyokuwa wakifanya. 11 Basi ikawa hapo walipomwona, wakamletea wenziwe
thelathini, wawe pamoja naye.
Washirika thelathini ndio tena dondoo kwenye baraza la ndani la Malaika. Kitendo
cha kuchukua asali kutoka mwenye mwili wa simba kinawakilisha usafishaji na
chakula, ambao ni wa kitu kisichosafi na kilichonajisi chenyewe. Kitendawili
kilifanywa kwenye siku saba za sikukuu. Kafiri au kefhiri huyu au simba kitoto cha
simba mkamilifu na kubwa (kutoka guri,
hadi kefiri, hadi ariyehi hadi labi na kisha laishi)
anakuwa mkali zaidi kuliko anapozeeka. Desturi ya kuwa na sherehe za arusi kwa
kipindi cha siku saba inaandikwa na kuonyeshwa kwenye Mwanzo 29:27, kuwa ni
kama ilitendeka hata katika siku za Mababa waliotangulia nyuma yao huko Mesopotamia.
Wayahudi wanaendelea kufanya hivyo hata leo, kwa sababu ya maelekezo ya
mafundisho na imani za marabi (soma Soncino, p. 271). Sikukuu inayowakilisha
taswira ya arusi ya Mwanakondoo inaadhimishwa mwezi wa saba uitwao wa Ethanimu
au Tishri.
Waamuzi 14:12-14 Samsoni
akawaambia, Mimi nitawategea ninyi kitendawili; kama mwaweza kunionyesha katika
hizo siku saba za karamu, na kukitambua, ndipo hapo nitawapa mavazi thelathini
ya kitani na mavao mengine thelathini; 13 lakini
msipoweza kunionyesha ndipo hapo ninyi mtanipa mimi mavazi thelathini ya kitani
na mavao mengine thelathini. Basi wakamwambia, Haya, tega kitendawili chako,
ili tupate kukisikia. 14 Naye akawaambia, Katika huyo
mwenye kula kikatoka chakula, Katika huyo mwenye nguvu ukatoka utamu.
Kuna mlolongo wa mambo yanayoonyesha uwezekano kwenye andiko hili. Mavazi
yavaliwayo na wahudumu wa baraza la katikati yameandaliwa kwa ajili ya kumuwakilisha
elohimu. Simba mfu ni wazo au dhana ya mrejeo wa mmeguko mpya na hari ya kupenda
vita waliyonayo Malaika walioasi. Uangamivu wake utasababisha kwenye mavazi
mapya na kuondolewa kwa machungu ya uasi. Mwamuzi ni mtumishi wa siri za Mungu.
Wateule wamepewa uwezo wa kuzijua siri hizo pia, kama wakiwa tayari na ni
muhimu au lazima kuudhihirisha mpango wa wokovu. Wamataifa wanatamani kuzijua
siri hizi na wanabakia kwenye mtafaruku wanaposhindwa kuzielewa au kuthibiti
mchakato. Na ndiyo maana wanatafuta na kufanya kila liwezekanalo kumwangamiza
bibi arusi wanapokuwa wamekanganyika.
Waamuzi 14:15-20 Ikawa
kwa siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, Mbembeleze mumeo, ili atuonyeshe
hicho kitendawili, tusije tukakuteketeza moto wewe na nyumba ya baba yako; je!
Mmetuita ili mpate kuichukua mali yetu? Je! Sivyo? 16 Basi
mkewe Samsoni akalia mbele yake, akasema, Wewe wanichukia tu, wala hunipendi;
wewe umewategea kitendawili hao wana wa watu wangu, nawe hukuniambia mimi. Naye
akamwambia, Angalia, sikumwambia baba yangu wala mama yangu, nami nikuambie
wewe? 17 Naye akalia mbele yake hizo siku saba, wakati
ulioendelea karamu yao; basi ikawa siku ya saba akamwambia, kwa sababu alikuwa
akimsisitiza sana; naye akawaambia wale wana wa watu wake hicho kitendawili. 18 Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua
kuchwa,Ni kitu gani kilicho tamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu
kuliko simba? Naye akawaambia, kwamba hamkulima na mtamba wangu,Hamngekitambua
kitendawili changu. 19 Roho ya Bwana ikamjilia juu
yake kwa nguvu, naye akatelemkia Ashkeloni, akapiga watu waume thelathini
katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili
mavao hayo. Hasira zake zikamwaka, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake. 20 Lakini huyo mke wa Samsoni aliozwa mwenzake, ambaye
alikuwa amemtendea kama rafikiye.
Mtamba ni taifa la Israeli, limewakilishwa pia
na dume la ng’ombe la Efraimu. Mtamba mwekundu huwatakasa makuhani (soma jarida
la Masihi na Mtamba wa Ng’ombe Mwekundu (Na. 216)). Mtamba aliyefundishwa wa Hosea 10:11 anafananishwa
pia na Misri kwenye Yeremia 46:20. Efraimu na Yuda watawekwa kwenye kongwa
sawasawa na unabii ulio kwenye Hosea 10:11. Israeli walijifunga kwa kuweka agano
na Mungu walipokuwa jangwani, lakini walilivunja na kumgeukia mungu wa
urutubisho aliyeitwa Baali walipofika Kanaani. Ndiyo maana andiko hili
linaelezea juu ya kulima kwa kutumia mtamba wa ng’ombe wa Mwamuzi. Kwa sababu
hii Israeli amefanywa kuwa tasa kwa mujibu wa Hosea 9:11 nk.
Kujipatia siri kwa njia ya uwongo na
ulaghai, kwa lazima, kunajumuisha na maangamizo ya watu wake mtu mwenyewe.
Mavazi ya watu thelathini yanahusiana na karama au kipawa cha Mungu ambacho
hakiwezi kupatikana kwa njia ya ulaghai.
Mke ambaye alikuwa sio mwaminifu, alikuwa
amepanga sawasawa na maagizo ya sheria zilizoanzishwa na Malaika walioasi, kwa
kuchukua nafasi ya torati ya Mungu. Maandiko ya kisheria yanayowekewa maswali
ni yale yajulikanayo kama Sheria za Hamurabi
seksheni za 159, 163 na 164. Mpangilio wa mwanamke kulifanyika kwa mujibu sawa
na sheria hizi zinavyosema, ambazo zimewekwa kwa nia ya kuchukua pahala pa zile
za Mungu na ambazo zilikuwa zimeangamiza na kuwadhuru watu kwenye sehemu ya
kwanza. Kwa hiyo, desturi ya kuingilia kati kwa Wamataifa na wito wa wateule.
Hii ilifanya matokeo kupoteza kwa mahali pa mke wa kwanza wa Samsoni, kama
tunavyoona kwenye andiko lililo kwenye aya inayofuatia.
Waamuzi 15:1-2 Lakini
ikawa baadaye, wakati wa mavuno ya ngano Samsoni akaenda kumtazama mkewe,
akamchukulia mwana-mbuzi; akasema, Nitaingia chumbani kwa mke wangu. Lakini
baba yake mwanamke hakumwacha kuingia. 2 Baba yake
akasema, Hakika mimi nalidhani ya kuwa umemchukia kabisa; basi nalimpa rafiki
yako. Je! Ndugu yake mdogo mzuri kuliko yeye? Tafadhali, mtwae huyo badala
yake.
Hii inasanyiza jambo kwa awamu inayofuatia
ya harakati za hukumu. Ndoa ya Wamataifa inaendelea. Hapa tuna mfano wa kwanza
wa matumizi ya Roho Mtakatifu. Hili ni pendo la kwanza la mlolongo huu wa
matukio. Huu ni mwaka wa Waefeso na mzunguko – unaofanyiza mwaka wa kwanza wa
kipindi cha miaka saba na mzunguko wa kwanza wa mizunguko saba ya Yubile. Awamu
na hatua za mwonekano wa uthihirisho wa Roho Mtakatifu kwa Samsoni, hufuatia
hatua za mfano wa mti kama ulivyotolewa na Kristo kwenye Luka 13:8.
Luka 13:6-9 Akanena
mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu;
akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. 7 Akamwambia
mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta
matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? 8 Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata
niupalilie, niutilie samadi; 9 nao ukizaa matunda
baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.
Mchakato huu hu0ndelea kwa miaka mitatu.
Kisha wa nne mi mmoja wa urutubisho na kulazimishwa kukua. Wa tano ni mmoja ya
wa neema na wa sita ni mmoja wa majaribu. Wa saba ni ule wa mapumziko ya
Sabato. Kwa hiyo sheria ililazimishwa na mchakato unaanza tena kwa kiwango cha
juu sana. Mchakato wa mwaka wa saba unaweza kushuhudia kuondolewa au kuzimishwa
kwa waonyesha nia, ambao kwa hiyo wameitwa lakini hawajachaguliwa. Kupungua kwa
upendo wa kwanza kunafuatia pia kama hatari iliyotofauti wa mchakato huu wa
mwanzo. Mchakato huu umeonekana pia kama hatua saba za Kanisa, kwa kupitia
makanisa saba ya Mungu yaliyo kwenye Ufunuo 2 na 3.
Waamuzi 15:3-8 Samsoni
akasema, Safari hii nitakuwa sina hatia katika habari za hawa Wafilisti, hapo
nitakapowadhuru. 4 Samsoni akaenda akakamata mbweha
mia tatu; kisha akatwaa vienge vya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia, akatia
kienge kati ya kila mikia miwili. 5 Alipokwisha
kuviwasha moto vile vienge, akawaachia mbweha kati ya ngano ya Wafilisti,
akayateketeza matita, na ngano, hata na mashamba ya mizeituni. 6 Ndipo Wafilisti wakasema, Ni nani aliyetenda hivi?
Wakasema, Ni huyo Samsoni, mkwewe yule Mtimna, kwa sababu alimchukua mkewe
akampa mwenzake. Wafilisti wakaenda wakamteketeza yeye na baba yake kwa moto. 7 Samsoni akawaambia, Ikiwa ninyi mnafanya mambo kama hayo,
hakika nitajilipiza kisasi juu yenu, na baadaye nitakoma. 8 Akawapiga
upeo, mapigo makuu sana, kisha akatelemka akakaa katika ufa wa jabali la Etamu.
Hapa, tunakutana na hadithi hiyohiyo ya Gideoni, ambapo mienge inatumika
katika kuwaangamiza Wamataifa. Mbeha mia tat uni sawasawa na wanaume wa vita
mia tatu wenye silaha za kuchomea maadui kwenye hadithi ya Gideoni. Hapa huyu
ni Roho Mtakatifu kwa mikono ya Kristo akimtumia mwamuzi wa Dani kuwaanzaa wao.
Kutajwa kwa bustani za mzeituni kunahusu matumizi ya neno litumikalo kwa ajili
ya ukuhani. Dini na imani potofu za Wamataifa yamejumuishwa na neno la Mungu,
mikononi mwa mteule. Na ndiyo sababu mke wa Mwamuzi aliteswa na walichomwa moto
hadi kufa, kama walivyokuwa wale waliokuwa kwenye mstari wao wa kiuzawa, kwa
ajili ya makabila yaliyofichika ambayo kwayo idadi ya wale 144,000 wanachukuliwa
au kutokana nayo.
Kwa sababu hii Wamataifa ndipo waliishambulia Yuda.
Waamuzi 15:9-13 Basi
Wafilisti wakapanda wakapiga kambi yao katika Yuda, wakajieneza katika Lehi. 10 Watu wa Yuda wakasema, Mbona mmekuja kupigana nasi?
Wakasema, Tumepanda ili kumfunga Samsoni, kumtenda yeye kama alivyotutenda
sisi. 11 Ndipo watu elfu tatu wa Yuda wakatelemka hata
ule ufa wa jabali la Etamu, wakamwambia Samsoni, Je! Hujui ya kuwa Wafilisti
wanatutawala? Ni nini hii, basi, uliyotutenda? Akawaambia, Kadiri ile
walivyonitenda mimi, ndivyo nilivyowatenda wao. 12 Wakamwambia,
Tumeshuka ili kukufunga, tupate kukutia katika mikono ya Wafilisti. Samsoni
akawaambia, Niapieni ya kwamba ninyi wenyewe hamtaniangukia. 13
Wakamwambia, wakisema, Vema, lakini tutakufunga sana, na kukutia katika
mikono yao; lakini hakika hatutakuua. Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya,
wakamchukua kutoka huko jabalini.
Kwenye mfano huu mwamuzi wa Israeli alitokana na Yuda, kwa kuwa walishambuliwa
na Wamataifa, kwa nia ya kulitokomeza kabila ambalo kwalo walitokea ama
kuchipukia. Masihi aliruhusu afungwe mkatale na kumtoa ili auawe. Hata hivyo,
alirejeshwa kwa kufanywa upya na kurudishiwa uweza au nguvu zake tena kwa uweza
wa Roho Mtakatifu, kama atakavyokuwa katika siku za mwisho atakaporudi akiwa ni
mfalme.
Waamzi 15:14-17 Alipofika
Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya Bwana ikamjia
kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani
iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake. 15 Naye akaona mfupa mbichi wa taya ya punda, akautwaa,
akapiga watu elfu kwa mfupa huo; 16 Samsoni akasema,
Kwa taya ya punda chungu juu ya chungu, Kwa taya ya punda nimepiga watu elfu. 17 Ikawa, alipokuwa amekwisha kunena akautupa ule mfupa wa
taya mkononi mwake; na mahali pale pakaitwa Ramath-lehi.
Hivyo basi, ingawa jambo hili wokovu ulifanyika. Ulinzi wa wateule
unafuatiwa na wokovu ule.
Waamuzi 15:18-20 Kisha
akaona kiu sana, akamwita Bwana akasema, Wewe umetupa wokovu huu kwa mkono wa
mtumishi wako; na sasa nitakufa kwa kiu, na kuanguka katika mikono ya watu
wasiotahiriwa. 19 Lakini Mungu akapasua mahali penye
shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokwisha kunywa, roho yake
ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore, napo pa
katika Lehi hata hivi leo. 20 Naye akawa mwamuzi wa
Israeli: katika siku za Wafilisti muda wa miaka ishirini.
Hapa, tunaona mchakato wa hukumu
ukianzishwa. Hukumu hii ya miaka ishirini uliofuatiwa na mfuatano huu wa
matukio. Ndipo anguko la Wamataifa limeonyeshwa pia, kwa kupitia watu mia tatu
pamoja na Gideoni. Mchakato huu unaweza kuchukuliwa kama taswira ya mambo hadi
siku za mwisho. Kwa hiyo mchakato huu ni endelevu kutokana na mlingano
uliorudiwa. Mfano linganifu wa kuugawanya mwamba kwa kipigo huko Lehiisi pia ni
alidurufu harakati za Masihi, kukifanya iwezekane kuwepo kwa mito ya maji
yaliyo hai kutoka kwenye mwamba ambao ni Mungu.
Hadithi ya Samsoni na Delila inajulikana
sana lakini haieleweki vizuri. Anguko la Samsoni lilitokea mwishoni mwa kipindi
chake akiwa kama Mwamuzi wa Israeli, ambapo kinadhararia angeweza kuwa na nguvu
zaidi kwa njia ya kukua katika Roho Mtakatifu. Mwaka wake wa ishirini kwa kweli
ulikuwa ni mwaka wa tatu wa majaribu kwenye mfumo wa Jubile. Mchakato ulianzia kwenye
mwaka wa kumi na tisa. Hadithi hii hata hivyo, inachukua mzungujko kamili
kuendeleza. Kwenye awamu ya kwanza alitupwa kwenye ibada ya sanamu ya
kiuhusiano na mpagani. Uhusiano huu ulianza kwa mwongozo na maelekezo ya Roho Mtakatifu,
kama ilivyokuwa hapo kwanza. Lengo hasa lilikuwa ni kuuleta nyumba yote ya
nyumba ya Wamataifa. Huu kwa kweli ni mchakato kamili kama utakavyoonekana mwishoni
mwa Yubile ishirini za Milenia, wakati Shetani atakapokuwa amefunguliwa tena na
mataifa yatakapomilikiwa tena na Malaika waasi, na wakianzisha tena dini potofu
na za uwongo. Uwakilishi wake unajiri pia na Kanisa katika siku za mwisho kama utakavyokuwa
chini ya kahaba.
Waamuzi 16:1-3 Samsoni
akaenda Gaza, akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake. 2 Watu
wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira,
wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema,
Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua. 3 Basi
Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku, akaishika
milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing'oa pamoja na komeo lake,
akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.
Hapa, Roho Mtakatifu yuko pamoja naye. Samsoni anaanza kujiamini kwa nguvu
zake ambazo amepewa. Wamataifa
walichukizwa na nguvu ambazo zilikuwa zilimfanya amudu kuwa kwenye kiwango cha
Roho Mtakatifu. Mwonekano wa Samasoni tangu kuzaliwa kwake ulijulikana kama
mfano kwamba Kanisa linaweza kufanya kazi vizuri likiwa na mchanganyiko au na
mtu binafsi watakatifu.
Waamuzi 16:4-12 Ikawa
baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake
akiitwa Delila. 5 Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea,
wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi
tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu
fedha elfu na mia moja. 6 Delila akamwambia Samsoni,
Tafadhali uniambie asili ya nguvu zako nyingi, na jinsi uwezavyo kufungwa, ili
uteswe. 7 Samsoni akamwambia, Wakinifunga kwa kamba
mbichi saba ambazo hazijakauka bado, hapo ndipo nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama
wanadamu wenzangu. 8 Ndipo wakuu wa Wafilisti
wakamletea kamba mbichi saba zisizokauka, naye akamfunga nazo. 9 Na yule mwanamke alikuwa na watu katika chumba cha ndani,
wakimwotea. Basi akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Ndipo akazikata zile
kamba kama vile uzi wa pamba ukatwavyo ukiguswa na moto. Basi hiyo asili ya
nguvu zake haikujulikana. 10 Delila akamwambia
Samsoni, Tazama, umenidhihaki, na kuniambia uongo; sasa tafadhali, niambie,
waweza kufungwa kwa kitu gani? 11 Akamwambia
Wakinifunga tu kwa kamba mpya ambazo mtu hakufanya kazi nazo, hapo ndipo nitakuwa
dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. 12 Basi
Delila akatwaa kamba mpya akamfunga nazo, akamwambia, Wafilisti wanakujia,
Samsoni. Na wale wenye kuotea walikuwa katika chumba cha ndani. Naye akazikata,
akazitupa kutoka mikononi mwake kama uzi.
Mchakato umeendelea kutoka kwenye vigingi vya shungi hadi kamba. Jaribu
linakuwa gumu zaidi kadiri linavyoendelea mbele. Saba ni tarakimu ta ukamilifu.
Kuna mizunguko saba ya Yubile ambayo kwayo mchakato huu unarudiwa.
Waamuzi 16:13-14 Delila
akamwambia Samsoni, Hata sasa umenidhihaki, umeniambia maneno ya uongo; niambie
sasa, waweza kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia, Ukivifuma hivi vishungi saba
vya nywele za kichwa changu katika mtande wa nguo. 14 Basi
akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka
usingizini, akaung'oa ule msumari, na ule mtande.
Hapa mchakato unakaribia kwa ukaribu na ukweli. Majaribu matatu ambayo
aliyapitia yalikuwa chini ya ulinzi wa Mungu. Samsoni alikuwa anaanza
kujiamini, na kudhani kwamba nguvu alizokuwanazo zilikuw ni zake yeye mwenyewe,
na sio za Yule Malaika wa Bwana, ambaye ndiye Masihi, aliyemuwezesha Roho Mtakatifu
aliyekuwa ndani yake. Mchakato huu wa majaribu ulidumu kwa kipindi cha miaka
mine ya kukua na kuhitimika. Mwaka wa kwanza wa ndoa kwa mujibu wa torati
humzuia mtu kwenda vitani.
Mwaka wa tano wa neema unamuandaa mtu kwa
ajili ya mwaka wa sita wa majaribu. Ata hivyo, mchakato wa majaribu huanza
katika Mwaka wa Neema na huishia kwa mavuno maradufu ya mwaka wa sita wa
mavuno. Kwenye Mwaka wa Neema ishara za kushindwa
kwetu kuamini zinatolewa ama kuonyeshwa dhahiri na Mungu anautumia mwaka huu
ili kuanzisha mchakato wa kuwapitisha watu kwenye kipindi hiki kigumu
nauthibitisho au kuwahesabia haki kila mmoja wao. Kila mwaka mchakato huu huanza
na kuelekea kwenye majira ya Pasaka, na Mlo wa Meza ya Bwana, Uoshanaji wa
miguu na, na Sakramenti ya Pasaka ambayo kwayo dhambi zetu zimesamehewa kwa
mwaka mwingine. Hatahivyo, Mwaka wa Tano wa mzunguko ni wa muhimu sana kwa
namna yake na watu wengi wanajaribiwa kiimani katika mwaka huu. Zile dhambi
zilizoachwa kutiliwa maanani hadi sasa zinaletwa mbele machoni na kwenye matukio
mengi, watu wengi mmoja mmoja wanaondolewa kabisa kutoka Kanisa la Mungu kwa
ajili ya dhambi zisizotubiwa na kubwa.
Mungu atawashughulikia pia watu kwa mtazamo kwamba ni
muhimu kwenye mzunguko wa miaka ya Sabato na kwamba hapendi kuwaacha bila
kuwarudi kwa ajili ya mzunguko unaofuatia. Vishinda saba vya ufungaji nywele wa
Samsoni vinafanya taswira ya mizunguko saba na Malaika wa Makanisa saba wayasimamiao
ambao ni Kristo.
Waamuzi 16:15-20 Mwanamke
akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami?
Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. 16 Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku,
na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa. 17 Ndipo
alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya
kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa
mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu,
nitakuwa kama wanadamu wenzangu. 18 Delila alipoona ya
kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa
Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo
moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha
mikononi mwao. 19 Naye akamlaza usingizi magotini
pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa
chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka. 20 Kisha
akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema,
Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa Bwana
amemwacha.
Kifungu hiki cha mwisho ni cha muhimu sana kukitilia maanani. Hakujua kuwa Bwana alikuwa amemwacha inaashiria
kwamba umuhimu wa kujali masharti ya kiroho chetu sisi wenyewe unapungua kwa
kiasi kikubwa sana kwa wateule. Bwana alimuacha Samsoni kwa njia ya kumfanya
Samsoni awe na mawazo ya kujiamini kupita kiasi, lakini ni kwa njia ya Roho
Mtakatifu tu ndipo Samsoni angeweza kuwashinda Wamataifa. Siri ya nguvu zake
ilitunza na kubakia kuwa siri hadi siku ya mwisho alipoitoboa mwenyewe.
Inafunuliwa ili kumjaribu huyu teule na kuwahukumu Wamataifa na ili kuivunja na
kuiharibu imani yao na dini yao iwe si kitu. Wamataifa walichukua uweza na
kumshinda mwamuzi wa Israeli na, ndio akaondokwa na uweza au nguvu za Roho
Mtakatifu. Walimng’oa macho yake na ha kuweza kuona tena, kama walivyofanywa
Yuda na watu wengi wa mataifa hilo, hadi pale watu wapatao 144,000 walichukuliwa
na watu wengi walijaribiwa kwenye adha ya dhiki kuu. Uweza na utawala wa Mnyama
utaendeleza jambo hili.
Waamuzi 16:21-31 Wafilisti
wakamkamata, wakamng'oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa
vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza. 22
Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya
kunyolewa kwake. 23 Kisha wakuu wa Wafilisti
wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana
walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu. 24 Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana
walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi
yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu. 25 Ikawa
mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo.
Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya
nguzo mbili. 26 Samsoni akamwambia yule kijana
aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate
kuzitegemea. 27 Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu
waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari
palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni
alipocheza. 28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee
Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee
Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu
mawili. 29 Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za
katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake
wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto. 30 Samsoni
akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile
nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale
watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati
wa uhai wake. 31 Ndipo ndugu zake, na watu wote wa
nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora
na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa
mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini.
Uweza wa Mungu wenyezi ulionekana kwenye
mchakato huu wa marejesho mapya ya Roho Mtakatifu, ambao ulionekana kwa kupitia
nywele zake. Ndipo kupitia kwa mtu kipofu ambaye hapo zamani alikuwa anaona,
ndipo dola au utawala wa dunia utaangushwa chini. Na ndiyo mana kwamba kipindi
au zama ya mwisho ya Kanisa, Walaodikia ambao ni wenye mashaka, na maskini, vipofu
na wa uchi. Inataniwa na Wamataifa kwa kuwa limechukuliwa utumwani kwa ajili ya
tama zake na ulafi ua uroho wake. Ndipo kutokana na ukengeufu wake mdogo na
mfumo wake dhaifu, bado kutakuwa na wateule wachache ambao watamshinda na kumpondaponda
na kumwangusha chini MUNGU wa Wafilisti na kuvunja nguvu zao, ili kwamba ufalme
mpya uweze kuanzishwa. Vinyago na ibada za sanamu kwenye nyumba ya Mungu za huko
Shilo, chini ya makuhani wake wakengeufu, vitaondolewa na mahala ake
patachukuliwa na Hekalu Jipya la Masihi la huko Yerusalemu.
Yubile na
mizunguko ya miaka saba katika nyakati za mwisho
Tunaona uhusiano ulipo kati ya mizunguko ya miaka saba kwenye maisha ya
Samsoni, kama unavyotenda kazi kwa kila mmoja chini ya Yesu Kristo na kama
Kanisa lililo chini ya maongozi ya Kristo na Roho Mtakatifu. Kila mtu anaenenda
kwa mzunguko wa maendeleo kwa kipindi chake cha miaka hamsini cha maisha yake,
kama ilivyoelezewa na kulinganishwa na Yubile. Kwa hiyo, mtu ni Yule aliyefikia
utu uzima akiwa na umri wa miaka ishirini na anaendelea hadi miaka sabini au
Yubile kamili.
Kanisa limeamriwa kutilia maanani hilo kama lilivyoanzishwa likiwa kama
mwili chini ya Yesu Kristo. Mwili huu umewekewa utaratibu kwa mujibu wa
mlolongo na utaratibu wa Yubile arobaini jangwani. Tunajua wakati utaratibu wa
Yubile umo na umeandikwa kwenye maandiko ya Biblia (soma majarida ya Maana ya Maono ya Ezekieli (Na. 108); Usomaji wa Torati Ulivyofanywa na Ezra na Nehemia (Na. 250)). Miaka
saba ya mzunguko ni hii 1998, 2005, 2012, 2019, 2026 pamoja na Yubile ya mwaka
2027/28 na mwaka wa kwanza wa mzunguko ujao utakaokuwa ni mwaka mtakatifu wa 2028/29.
Na kwa hiyo unafuatiwa na miaka ya mateso na dhiki kwa Kanisa kuanza na
pamoja na mwaka wa tano na wa sita ya mzunguko na miaka mingine ya Sabato na ya
Mapumziko nay a Usomaji wa Torati. Kwa hiyo, kila Kanisa linajaribiwa na
kuchekechwa na kila taifa linajaribiwa kwa msingi wa mzunguko wa miaka ya
Sabato. Kwa hiyo, miaka ya 1996/97/98,2003/04/05, 2010/11/12,2017/18/19 na 2024/25/26
ilikuwa au inaendelea kuwa ni miaka ya kujaribiwa na kuchekechwa kwa Kanisa na
kwa mataifa. Kwa utaratibu wa usomaji wa torati kwa kipindi cha zaidi ya miaka
mingine thelathini, kila mzunguko utashuhudia kukaziwa kwa hukumu na matokeo
mabaya au mateso kwa Kanisa na kwa taifa, na muongezeko mkubwa wa mateso na
dhiki kuu hadi dunia itakapokuwa imeangamia kabisa mwaka 2025. Katika mwaka
huo, mataifa yote yatapaswa yawe chini ya hukumu ya Masihi na kuletwa kwenye mamlaka
kamili ya Masihi. Mwaka wa kwanza wa Yubile ya kwanza utakuwa mwaka 2028/29. Masihi
atatawala dunia kwa kutumia mtindo wa agizo jipya la ulimwenguni kote kutoka Yerusalemu,
kwa amri na torati ya Mungu tangu itakapofanywa upya na marejesho.
Joka ataangukia usoni na Sinagogi la Shetani litaonekana wazi likiabudu
machoni pa wateule. Wateule watafanyika kuwa nguzo kwenye Hekalu la Mungu na
hawataondoka kabisa kutoka hapo. Watakuwa na jina la Mungu na jina la Mji wa
Mungu na jina jipya la Kristo. Shika sana ulichonacho asije mtu akaitwa taji
yako (soma Ufunuo 3:8-13).
Hadithi ya Samsoni kwenye hekalu ya Joka ni awamu ya mwisho ya hadithi ya
Samsoni, wakati alipoondolewa kwa ubatili wake mwenyewe, alishinda na
kujitiisha Hekaluni. Hadithi hii kwa kweli ni habari ya kanisa la Walaodikia
katika siku za mwisho. Inaonesha taswira kurejea kwa wale walio kwenye madaraja
ya vyeo vyake wanaofanya matengenezo kwa msaada wa Roho Mtakatifu, na
kuuangusha mfumo na imani ya Mnyama. Marejesho yale yanatokea katika siku za
mwisho wakati Kanisa litakaposhindwa na wale walio wateule wake (kama asemavyo
Danieli) kuwa watashindwa na nguvu za Mnyama na dini yake. Hata hivyo, kanisa
linafanya marejesho ya imani ya kweli na kutoka kwenye harakati hizo Kristo
atakuja kuwaokoa wale wanaomsubiri kwa hamu kubwa. Hili Hekalu la Joka ni imani
na dini potofu ya huu ulimwengu, na kwamba mfumo na imani yote itaangushwa
chini na kuangamizwa.
Vishinda saba vya nywele za Samsoni vinawakilisha roho saba za Mungu na
nyakati saba za makanisa, kwenye mchakato wake wa maendeleo, yakielekea kwenye
hatua ya yeye kuwa maskini, mwenye mashaka, kipofu na uchi, akakamatwa na
Wafilisti (mungu wa dunia hii), akashindwa na kuletwa ndani akafanyika kama
kichekesho na acheze mbele yao kwenye Hekalu la Dagoni (Waamuzi 16:25). Ni
mwisho ule, kiwango cha chini zaidi cha Kanisa nipo Kanisa litapata nguvu za
Roho Mtakatifu, na kumuangusha chini na kumwangamiza mungu wa dunia hii na dini
yake yote na imani yake ambayo inafanya juhudi ya kulikomesha au kuliangamiza.
q