Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[076]

 

 

Imani ya Kibinitariani na ya Kitrinitariani

(Toleo La 5.0 19941112-20001202-20080503-20100714)

 

Jarida hili linashughulika kuyachambua mambo ya msingi wanayotuamanisha imani hizi zote mbili, yaani ya Wabinitariani na Watrinitariani. Chanzo kisichotokana na biblia kuhusu mafundisho yao na jinsi yalivyoanzishwa na na kuendelezwa kumechambuliwa pia. Jarida hili linatathmini mlolongo na hatua mbalimbali zilizotumika kuendeleza itikadi na imani hizi tangia ile ya Utatu ilivyoenezwa na ambayo imeainishwa kwa namna ambayo inayozua maswali kwa jinsi imani hii ya Utatu inavyokinzana na mafundisho yaliyo kwenye Agano Jipya nanayotokana kwenye Maandiko Matakatifu ya msingi.

 

Madai yanayotolewa na baadhi ya Makanisa ya Mungu kuwa Kanisa la Kwanza lilikuwa ni la kibinitariani hayana mashiko yoyote kabisa bali ni imani iliyozuka tu kipindi cha karne ya ishirini ambako ndipo yalibuniwa na kuingizwa.

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Barua Pepe au E-mail: secretary@ccg.org

 

 

 

(Hati Miliki ©  1994, 2000, 2008, 2010 Wade Cox)

(tr. 2013)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

 


Imani ya Kibinitariani na ya Kitrinitariani

 


Mjadala wa Kiteolojia na na Kifilosofia kwenye Kanisa la WCG na makanisa yake mwingine Yaliyoibuka kutoka ndani yake

 

Ni kwa zaidi ya kipindi zaidi ya miaka ishirini tumejionea matawi mengi ya makanisa ya Mungu yakiongeza mafundisho yasiyo na msingi wa kihistoria au hata pengine hata ikaonekana hatimaye kuwa ni mafundisho yasiyo sahihi na kuwa yameingizwa tu kama ukweli kwamba ni wanachama wa makanisa hayo yameyachukua kwa ukweli tu kwa kuwa walikuwa wameambiwa mambo haya na viongozi waliowataka kuwaamini.

 

Mambo yafuatayo ni ukweli:

 

1. Herbert W. Armstrong hakuwa na amechukua mafunzo kwenye taasisi yoyote yenye elimu inayotambulika, iwe kwenye Chuo chochote cha Kidini na akawa Mwanafunzi humo au Mwanafunzi wa Chuo cha Falsafa au wa elimu ya Dini au ya Kijamii au Maadili na wala hata hakujifunza kutoka kwa watumishi au viongozi wake wa juu na hata wale wanaodiriki kumuita kwa kumpa cheo cha “Dokta” Armstrong hawakuwa na msingi wowote wa mafunzo ya yoyote ya kielimu.

 

2. Hakuna mwanateolojia wa Makanisa makubwa ya Mungu aliyekuwa na sifa hii ya kuwa mkufunzi mbali na CCG. Mtu mmoja aliyekuwa sio mwanazuoni wa teolojia ya kanisa aliyedai kuwa alikuwa na ngazi ya uhitimu wa mafunzo kwenye teolojia ya kanisa la kwanza iakini uandishi wake hauashirii kuwa amepitia mafunzo hayo.

 

3. Mengi ya yanayosemwa na watu hawa hayaonyeshi kuwa ni kweli maana hayaonyeshi ukweli wa kihistoria.

 

4. Mengi ya waliyosema yamekosa mashiko au yamechukuliwa kutoka kwa waandishi wengine. Machapisho mengine kama kijarida chenye kichwa cha maneno cha Marekani na Uingereza Iliyo kwenye Jumuia ya Madola kwenye Unabii ni wazi kabisa kuwa wamechukua mawazo kutoka kwenye uandishi wa wengine (kwa jambo hili wamechukua kutoka kwa mwandishi J. Allen kutoka kwenye kitabu chake cha Fimbo ya Enzi ya Yuda na Haki ya Uzaliwa wa Kwanza).

 

5. Kila moja ya makanisa haya yaliyoptoka kwenye kanisa hili limejuluisha ndani yake watu wenye mawazo mbalimbali na tofauti kuhusu asili ya Mungu. Kwa mfano, kanisa la UCG na washirika wa kwaida ambao wanaamini mafundisho ya Waunitaria wenye Msimamo Mkali, Waditheisi, Wabinitariani na waamini Utatu ama Waunitariani. Makanisa mengine yaliyotokana na kanisa hili kama vile LCG na RCG yanajumuisha michanganyiko ya makundu haya haya. Pia kunamigongano inayoibukia ya kuhusu Kalenda.

 

Tafsiri ya majina ya makundi haya:

 

Imani ya Waunitariani mwenye Itikadi kali: Watu hawa wanaoitwa Waunitari wenye Itikadi Kali (Radical Unitarian0 wanapinga uwepo wa zama kabla ya kuzaliwa wa Yesu Kristo na pia wanapinga mafundisho ya kwamba Yesu alizaliwa kkutokana na Mungu kutoka kipindi cha kupata mimba kwa Mariamu (ambaye wao humuita Maria) (soma zaidi kuhusu imani hii kwenye jarida la (Chanzo cha Imani ya Uunitaria ya Itikadi Kali na Ubinitariani (Na. 076C) [Origins of Radical Unitarianism and Binitarianism (No. 076C)].

 

Uunitariani: Imani ya Kibiblia ya Kunitariani ni wale wanaoamini uwepo wa Mungu Mmoja na Wapekee wa Kweli na kumjua kwamba yeye ndiye aliyewaumba Malaika na ndiye aliyemtuma Yesu Kristo aje hapa duniani kwa wanadamu. Aina yoyote ya Wamonotheist au Waamini Mungu kuwa ni Mmoja na hana mshirika (kama ilivyofafanuliwa kwenye kitabu kinachoitwa Universal Oxford Dictionary art. neno ‘Unitarian'). Wamonist wanaondolewa kwa sababu maalumu kwenye maana ya neno hili.

 

Waditheisti: Mditheisti anadai kwamba kulikuwa na Miungu miwili ya kweli walioishi kipindi chote na kwamba wote wanaishi milele na wanahadhi sawa. Wazoroastriani na Wamanicheani wanasema kuwa walikuwa wanapingana. Mafundisho ya baadae ya Herbert Armstrong yanadaia kuwa mmoja kati ya Miungu hii alikubali kuja hapa chini Duniani na kuwa Mwana wa mwingine ili aweze kutolewa sadaka na ndiye aliyefanyika kuwa Kristo. Kristo huyu au Masihianaishi tu kwa ajili ya kazi aliyotakiwa kuifanya na alifanyika kutokana na uwepo wake kutoka huko nyuma kabla hajazaliwa. Mapema kabla yake alikuwa ni sawa na Mungu katika kuishi kwake, na mbali ya huyu mwingine aliyefanyika hatimaye kuwa ni Baba (imeandikwa kwa kina kwenye Kamusi ya Univ. Oxf. Dict.). hii kwa kweli ni aina ya imani ya miungu wengi. Fudhisho hili hatimaye liliandikwa na kuchaoishwa na kanisa hili la WCG kwenye Gazeti lililojulikana kama Good News Magazine mapema kabla ya adhimisho la Sikukuu ya Vibanda ya mwaka 1991 na liligawanywa kwa watu na kufundishwa na Gerald Waterhouse huko Australian Capital Territory (ACT) wakati huu wa Sikukuu ya Vibanda ya mwaka 1991 (soma jarida la Uditheism (Na. 076B) [Dditheism No. 076B)].

 

Umodalism: Ni mafundisho ya Kiyunani ya Wasabeliani ambayo yanautofautisha Utatu na kkuuweka kwenye “modali” peke yake, mfano, wanasema kwamba Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni watu watatu waliotofauti na wanaofanya kazi tofauti za Mambo ya Kimbingu (soma kamusi ya Univ. Oxf. Dict.).

 

Ubinitaria/Ubinitariani: Hii ni imani inayoamini Uungu wa wati wawili tu (kwa mujibu wa kamusi ya Univ. Oxf. Dict.), ilitumiwa na Loofs mwaka 1898 akiwa ni Mbinitari wa Kijerumani. Katika uelewa wa Makanisa ya Mungu. Mbinitari ni mtu anayeamini kwamba kuna Mungu mmoja anayeishi na ametume sehemu yake mwenyewe hapa Duniani, na abayo sehemu hiyo ndiyo huyu Kristo. Kiini na chanzo cha fundisho hili kinatokana na ibada za miungu Attis, Adonis na Osiris. Mtazamo huu kuhusu Uungu haukuingia kwenye Ukristo hadi kipindi kile kanisa lilipoanza kuadhimisha sikukuu ya mungu mke aitwaye Easter mwaka 154 BK na ilivyojiingiza kwa hila tangia mwaka 160 na kundelea mbele. Historia ya kuendelezwa kwake imeelezewa kwa kina kwenye jarida la Umakosa ya Ufundishaji ya Imani za Kibinitari na Utrinitari ya Teolojia ya Kwanza ya Uungu (Na. 127B) [Binitarian and Trinitarian Misrepresentation of the Early Theology of the Godhead (No. 127B)]. Ilianzishwa kwa kuchukuliwa kutoka kwenye imani za kipagani walipoketi kwnye Mtaguso wa Nikea (Nicaea) mwaka 325. Mfundisho msingi yajulikanayo kama Kanuni za Nikea ziliachiliwa mbali na kuchukuliwa kuwa ni mafundisho mapotovu na ya uzushi mwaka 327 BK na Waunitariani wanasemekana kuwa waliliongoza kanisa na walifanikiwa kufanya hivyo hadi mwaka 381 BK wakati imani ya Utatu ilipoibuka tena upya kwenye Mtaguso wa Constantinople. Kirk na Rawlinson (Ess. Trin. and Incarn.) wanaelezea jambo hili la Ubinitariani na kuendelea kwenye ukurasa wa 215 unaelezea kuhusu Ubinitariani wa Tertullian wa mawazo ya kwanza ya Wakatoliki (haya yamo kwenye kamusi ya Oxford English Dictionary Supplement, Vol. 1 A-G, p. 263).

 

Mtazamo huu ka hakika ni wa mafundisho ya Mpingakristo na ambayo yanalenga kutengamisha ubinadamu na mwili wa kimbinguni wa Kristo. 1Yohana 4:1-2 ilibadilishwa kutoka kwenye uandishi wake asilia na hawa waliokuwa wanapenda kumtofautisha Kristo kutokana na hali yake ya kimbinguni (haya yamo kwenye kitabu cha Socrates VII, 32, ukurasa 381.) (Inaweza kuwa iliandikwa upya na kitabu cha Irenaeus ANF, Vol. 1, fn. p. 443.)

 

Katika hili mwamjua Roho wa Mungu... Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo (sawa na ilivyoandikwa kwenye jarida la Smatamko ya Imani (Na. A1 toleo la 4, ukurasa wa 7 [Statement of Beliefs (A1) 4th ed., p. 7)].

 

Utrinitariani. A1. Ni imani inayoegemea au iliyoanzishwa kwa amri ya Utatu Mtakatifu. 2. Mwateolojia anayehusiana na imani ya Utatu; anayeaminika kwa mafundisho ya Utatu (kinyume chake ni Imani ya Mungu mmoja au Unitariani) 1656. 3 Ni Imani inayoweka mfumo wa Utatu: yaani vitu vitatu au muunganiko wa watu watatu. B. sb (na herufi kubwa ya T). 1 Ni mshirika au muumini wa dini inayofuata mafundisho ya Utatu; = Mathurin 1628 2. Mwanateolojia anayefundisha imani hii. Ni mtu anayeyashikilia au kuyaamini mafundisho haya ya utatu katika Uungu; mtu anayeamini Utatu 1706 Kwa hiyo, ni imani ya Utatu, mwamini Utatu (Univ. Oxf. Dict.  p. 2248).

 

Fundisho la Utatu halikuenezwa na kujulikana sana hadi kipindi cha Wakapadokia, wa Gregory wa Nyssa, Gregory wa Nazianzus na Basil. Waliyapa ujiko na kujulikana na yalipelekwa kwenye Baraza kuu maarufu kama Mtaguso wa Constantinople mwaka 381 BK. Lakini mapema kabla ya kipindi hiki fundisho hili lilikuwa halijulikani kwa Wakristo.

 

Baadhi ya wafuasi wa Armstrong wanajaribu sasa kudai kwamba yeye mwenyewe alikuwa ni Mbinitariani na kwamba yeye pamoja na huduma yake yote waliyaunga mkono mafundisho haya ya Kibinitariani. Hii siyo kweli kabisa. Armstrong na huduma yake walifundisha kwamba Mungu alikuwa ni familia inayohusisha viumbe wawili ambao wote walikuwa na hadhi na uweza sawa na wenye kuishi milele pasipo kuwa na mwisho na kwamba mmoja wao alikubali kuwa mwana wa mwenzake na akafa akiwa ni sadaka ili kuwakomboa wanadamu. Walifundisha kwamba wateule kutoka kwenye Makanisa ya Mungu watakuwa pia ni sehemu ya familia hii ya Mungu wakiwa kama miungu midogo elohim. Mwandishi wa habari hii amekuwa akiyasoma mafundisho yao kwa kipindi kirefu cha tangu mwaka 1964. Haina maswali kwamba watu hawa hawakuwa ni waamini mafundisho ya Kibinitaria na kwa kweli hadi mwandishi wahabari hii alipokuwa anahitimu mafundisho ya imani ya dini yao na kujifunza historia ya Makanisa ya Mungu, kamwe hakupata kuwaona wala kuwasikia na inaonekana pia kwamba hakuwahi hata kuwaona wakitumia neno hilo.

 

Mada sasa yanafanywa kwamba hawakulitumia neno elohim kabisa katika kuitaja hii imani ya Kibinitaria. Ni suala la ukweli kamili tu kwamba Kozi Ndefu ya Kujifunza Biblia ilifundisha kwa miongo kadhaa kwamba jina asilia na alisia na la kwanza la Mungu ni Eloa na kwamba jina hili lilikuwa ni la umoja na mwendelezo wa jiana hilo ni Elohim ambayo ilikuwa inamjumuisha Kristo kama mwana. Mgogoro mzima uliopo kuhusu nafasi ya wa Unitaria umeelezwa kwa kina kwenye Kozi (L. 8) (ambayo imebakia katika situ kwa kipindi cha miaka takriban arobaini na ilikuwa inatumika bado na Joseph Tkach Snr.) na katika familia ya Mungu ya Kidietheisti kwa nafasi inayoonyesha uzembe wa kiteolojia wa huduma kuu na mgongano ulio kwenye mitazamo yao. Walikuwa na wa Unitariani, Waunitariani wenye Itikadi Kali, Waditheisti na Watrinitariani kwenye huduma yao na walifundisha kwa nadra sana fundisho la Asili ya Mungu kwa kuwa ilikuwa ni jambo lililobishaniwa na kuzusha mjadala usio na jibu kulikosababishwa na teolojia yao yenye utata. Kile kilicho na uhakika ni kwamba Kanisa halikuwa la Kibinitariani kabisa isipokuwa kwenye kipindi chake cha mpito cha kufa kwake ndipo lilikuwa na watu waliojumuisha na kukubaliana na imani ya Kitrinitariani waliokuwa chini ya Tkach. Lilitumiwa na Watrinitariani, wanaoonekana kuwa huenda ama hawakuelewa na kuyatubia makosa yao, au walikuja kwenye Kanisa la Mungu kwa lengo la kuliharibu kwa makusudi. Kulikuwa na watu wengi wa aina hii nab ado wanaendelea kuifanya kazi hii masalia ya makanisa haya.

 

Makanisa ya Mungu hayakuwa ya imani hii ya Kibinitariani kwenye imani yao kwa ujumla kwa kipindi cha zaidi ya miaka efu mbili. Mtazamo huo ulianzishwa na Athanasian na yalikuwa ni matokeo ya imani yake na ambayo yalishika kasi sana kwa kipindi kifupi tu cha miaka miwili tangu mwaka 325 BK chini ya Constantine, na kisha ilishamirishwa zaidi mwaka 381 BK kwenye Mtaguso wa Constantinople. Constantine aliutangaza mfumo na imani hii ya Kiutatu na kuirasikisha mwaka 327 BK nay eye mwenyewe alibatizwa na akiwa na imani ya Kiunitariani hadi alipofariki. Alibatizwa na Eusebius wa Nicomedia. Watrinitariani wanawaita watu hawa kuwa ni wa Arians ili kuugeuza ukweli wa imani yao. Muundo wa Imani  uliletwa kwa Marafiki Wasabato kama ilivyoelezwa kwenye jarida la Jukumu la Amri ya Nne Kwenye Historia ya Makanisa ya Mungu Yanayoishika Sabato (Na. 170) [The Role of the Fourth Commandment in the Historical Sabbath-keeping Churches of God (No. 170)] iliyochapishwa mwaka 1996. Licha ya kuonywa sana hapo mwaka 1994, Kanisa la Mungu lijulikanalo kama The Church of God (Seventh Day) lilijitangaza kuwa la mrengo huu wa imani ya Kibinitariani mwaka 1995. Huko nyuma lilikuwa ni la Kiunitariani kama lilivyokuwa Kanisa la Sabato la Kibaptisti ambalo linajulikana kama the Seventh Day Baptist Church na ambalo lililitangulia hili. Muundo wa imani ya Kiunitariani wa zama za Makanisa ya Mungu ya kabla ya Matengenezo unaweza kuonekana kwa wazi sana kutoka kwennye kitabu kijulikanacho kama Wasabato wa Transylvania [Sabbatarians of Transylvania (CCG Publishing 1998)]. Madai yaliyoko kwamba LCG ni la Kibinitariani ni jaribio la kipindi cha mwisho la kujaribu kujiwekea umaarufu wa uwongo wa kihistoria na kutumia teolojia ya uwongo. Soma jarida la Uditheismu (Na. 76B) [Ditheism (No. 76B)].

 

Wayahudi wa Leo au Kalenda ya Hilleli

Kalenda ya Hilleli haikuwa inatumika kamwe kipindi zama cha Hekalu. Ililetwa na Hilleli II na marabi wawili wa Kibabeli mwaka 344 BK.  Hilleli aliitangaza na kuirasimisha kwenye dini ya Kiyahudi mwaka 358 BK. Hatimaye ilibadilishwa muundo wake kwenye karne ya 12 na Maimonides (Rambam) ili kurekebisha makosa yake. Hii siyo kalenda ambayo Kristto na Mitume waliishika. Imetuama kwenye imani na muundo wa Kibabeloni wa kufanyiwa marekebisho ili iende sawa na haiko sahihi na mara nyingi inapingana na ile iliyotumiwa ns kusminiks kes tsratibu za Hekaluni.

 

Baadhi ya watumishi wanaofuata mafundisho ya Armstrong wameutafsiri kwa makusudi muundo huu wa kalenda kuwa ulikuwa unatumika katika kipindi zama cha Hekalu. Huu ni uzushi wa kijinga na umethibitika kuwa ni uwongo uliofanywa na historia iliyotengenezwa kwa uwongo.

 

Utii

Iwapo kama Mungu ametupa sisi Kitabu cha Torati na kutuamuru kuwa tuzishike na kuzitakatifusha siku zilizoagizwa kwenye kitabu hiki na akatuagiza pia kuzishika na kuziadhimisha sikukuu zake na kuziadhimisha Yubile zake na kuzitakatifusha kiasi kihi; je, tunaweza kuruhusiwa tena kuzibadilisha siku hizi na kuibadilisha kalenda kwa mapenzi yetu sisi wenyewe?

 

Jawabu kwa aina hii ya mawazo ya kiujanja na yakibinadamu ni hapana. Kama watoto wetu walitumia aina hii ya mawazo au fikra kwetu tungelazimika kuwaadhibu.

 

Ni sawa tu na ilivyo hivyohivyo, uingizaji wa muundo dhana wa kiteolojia ya Waditheisi au Wabinitariani au Watrinitariani ni kosa linalostahili kuadhibiwa.

 

Hakua mwanateolojia aliyewahi kufanyamadai mengine zaidi ya kukubali kuwa Biblia haina muundo mwingine zaidi ya kuwa ni ya huu wa Kiunitariani. Wanateolojia maarufu na wanaojulikana na kuheshimika (kama kina Calvin, Harnack, Brunner) wanakubali kwamba Utheismu Kamilifu, Imani ya Kiyahudi, Biblia, na Uislamu vyote viko kwenye mrengo wa Kiunitariani (soma jarida la Kristo na Korani (Na. 163) [Christ and the Koran (No. 163)].

 

Kwa nini basi hata uwongo huu uliingia kwenye kanisa hili la WCG chini ya Armstrong na iliwezekana vipi kuendelea kuaminika hivyo? Jibu ni kwamba yaliingia kwa sababu ileile tu kama ilivyoingia kwenye imani inayoamini mambo ya Kisasa ya Kimodalismu na ambayo hatimaye ilikuwa ni ya Kibinitariani kwenye imani ya Warumi katika karne ya nne. Sababu ile ilijitokeza na kudai urasimisho ambao uliopotoshwa na ibada za kuabudu miungu ya uwongo ya Attis na Adonis na Dini ya Sirisiri ya kuliabudu Jua. Fundisho lisemalo kwamba Mungu ni muunganiko wa watu au viumbe wawili ambao ni baba na mwana, na kwamba huyu mwana alikuja hapa chini Duniani ili afanyike dhabihu, halitokani na Biblia. Bali lilikuwa ni fundisho la uwongo la miungu Attis na Adonis. Lilikuwa ni fundisho la miungu ya nafaka hasa mahindi na mafuta na divai au mvinyo, kama James Frazer alivyolitolea ufafanuzi na kuweka wazi kwenye kitabu chake cha Tawi la Dhahabu yaani The Golden Bough. Sanamu au mchoro unaomuonyesha Kristo amebebwa mikononi na Mariamu ambayo inaenea na kuaminika hivyo kuwa ni ya kweli, ni alama ya waamini Utatu au Watrinitariani inayomaanisha sanmu ya ubebaji iliyokuwa imechongwa kuashiria mungu Mke na mungu mdogo anayemfia mikononi (yaani Attis na Adonis) na ile alama ya msalaba inayoonekana kuzinga kichwani ilikuwa inaonyesha hali ya masikitiko aliyokuwanayo wakati wa vifo vyao. Walikuwa na nywele ndefu na za mwonekano wakike au kama za mwanamke kwenye michoro au picha zao, na ndivyo alivyokuwa wanaonekana makuhani wao waliohanidhiwa. Kristo hakuwa na nywele ndefu na alikuwa ni mwanaume kamili wa Kiyahudi, na wala hakuwa towashi wala hanithi wa aina ya mtu huyu wanayemuonyesha hawa Watrinitariani, na ambaye alikuwa ni mungu wa Wabinitariani aliyetambulishwa kwao na waibaji.

 

Ni sawa tu na makosa ya kufikiri tunayoyashuhudia yakifanywa kwenye wavuti za watu wanadai kuwa ni Makanisa ya Mungu.

 

Mwandishi mmoja aitwaye B. Thiel, Ph.D. (sio kwa taaluma ya teolojia, falsafa au mwanafunzi wa elimu ya kidini), aliyeandika akiwa kama ni mwandishi wa kujitegemea na aliyedai kuwa ni mshirika wa Kanisa liitwalo Living Church of God, ameandika makala mbili akikusudia kuwashawishi watu waamini kuwa Kanisa la Kwanza lilikuwa ni la imani ya Kibinitariani. Makala hizi zilikuwa na kichwa cha habari kisemacho:

“Ubinitariani: Mungu Mmoja, Watu au Viumbe Wawili Kabla ya Uumbaji” akaweka kwenye wavuti ya:

http://www.cogwriter.com/binitarian.htm na

U-unitariani:  Je, Imefundishwa kwenye Boblia na Ulikuwa ni Msimamo wa Kanisa la Kweli?” akaweka kwenye wavuti ya:

http://www.cogwriter.com/unitarian.htm

 

Majarida haya yote mawili yanatofautiana kidogo sana ila yana vifungu vinavyofanana na vinatumia maelezo yaleyale bila kupishana au kubadilika karibu kila neno limeandikwa kama lilivyo. Majarida haya yanaanza kwa utangulizi wa aina moja na kisha ameweka Kichwa cha Somo kisemacho Agano la Kale na halafu kwenye kifungu kile ametumia nukuu kutoka kwenye jarida moja kwa nia ya kujaribu kujionyesha kuwa anapembua kwa kina na kwa uangalifu mkubwa nafasi ya LCG ya kiimani na eneo la mwandishi huyu kwa kichwa cha habari cha jarida hili wakati ambapo kuna majarida mengi sana yanayoelezea somo linalohusu mahali pa Kanisa la kwanza kwa ufasaha na uwazi zaidi na kwa muonekano wa wazi zaidi yakionyesha. Uandishi alioandika Thiel kuhusu makosa makubwa ya utafsiri na jaribio lake la kuwataka viongozi wayapuuze na wasiyaamini maandiko ya Agano la Kale.

 

Thiel answajadili pia wale wanaodai kuwa ni sehemu ya Kanisa la Mungu na huku wakiikumbatia imani hii ya Utatu, kana kwamba hawako miongoni mwao, na ingawaje ujuzi huu wa kujieleza unaruhusiwa kwenye kifungu cha uandishi kiitwacho Filadel na Kipindi cha Zaidi ya Hapo ambacho kinaielezea zama ya Walaodikia ambayo “inawezekana kuwa yaweza kuwajumuisha Waunitariani waliochanganikiwa kiimani”. Kitabu hiki chenye mambo yenye utata na yasiyoeleweka vizuri kinanukuliwa kikiandikwa haya yafuaayo:

 

Piladelfia na Kuendelea

Kanisa linalofuatia kiurithi kwenye Ufunuo 3 lilikuwa ni la Filadelfia. Ni nje kabisa ya zama za Wasardi kwenye Kanisa la Mungu kwa wanaoamini mpangilio huu wa zama za Kanisa wanaami i kwamba zama hii ilikuwa ni ile ya kile kilichojulikana kama ni cha Redio ya Kanisa la Mungu, na kwa sehemu kubwa kilijulikana kama ni kipindi cha Kanisa la Mungu Ulimwenguni Kote, maarufu kama Worldwide Church of God (WCG) lililoongozwa na Herbert W. Armstrong. Sehemu kubwa ya masalia ya zama hii walijiunga na kuanzisha Kanisa lililojulikana kwanza kama Global Church of God na ndilo hili linalojulikana sasa kama Living Church of God (LCG). Mwanzoni mwa uandishi wa makala hii kililielezea kanisa hili la LCG kuwa ni la Kibinitaiani (kama ilivyonukuliwa kwenye makala za mwanzoni za kijarida hiki) ambayo ililielezea kuwa linaamini sawa na ilivyokuwa ikiamini Radio Church of God na ambayo ilikujakuwa WCG. Kwenye barua kwa malaika wa kanisa la Filadelfia, Bwana Yesu anasema, "hukulikana jina langu" (Ufunuo 3:8). Na hii ilikuwa na jambo la kufanya na masuala ya kimaongozi, nah ii inaweza pia kutofautisha ukweli wa kwamba sehemu ya kweli la kanisa la Filadelfia ni ya wale ambao hawajaukataa uungu wa Yesu (huenda, isiwapendeze baadhi ya wale wangaliopenda kuwa sehemu ya zama zinginezo).

Kanisa la mwinho kwenye mlolongo wa orodha ya Ufunuo 3 ni la Laodikia. Hii lilipaswa kuwa ni Kanisa kubwa na lenye nguvu katika nyakati za mwisho. Wakati kwamba sehemu kubwa ya matawi yake, machipukizi yaliyotokana na mafarakano, na yale yaliyo kivyakevyake yatakuwa ya imani hii ya Kibinitariani, na inawezekana kabisa kuwa huenda yanaweza kuwa na Waunitariani waliochanganikiwa kiimani, ingawaje hii inaweza kuwa ni jambo lenye kutilia mashaka sana (soma Matendo 4:12).

 

Mjadala huu wa mfumo wa zama za makanisa haya saba ya Ufunuo, uliendana na madai ya bwana Armstrong ya kwamba kanisa lake kuwa ndilo Kanisa la Mungu la Filadelfia na Kanisa linaloitwa siku hizi kama Church of God (7th Day) lilikuwa ni Kanisa la Sardi. Anaonekana kutojua au kupuuzia ukweli mkuu na wamuhimu sana wa jinsi Kristo alivyolaumu matendo ya Kanisa la zama za Wasardi ambayo yaliwafanya wawe na hali ya kuwa Hai lakini wakiwa wamekufa. Ni ukweli kwamba kanisa lake mwenyewe lijulikanalo kama Kanisa la Mungu Lililo Hai maarufu kama, Living Church of God, ndilo kanisa pekee katika historia lililochukua jina hili na Kristo anawaambia kwa wazi kabisa kuwa ni Wasardi na kwamba.

 

Utambilisho na nukuu zinazowaelekeza ni hizi zifuataza: 

Utangulizi

Mungu ni nini? Ni nani Mungu Mmoja? Je, Baba na Mwana Wote ni Mungu?

Makala hiii itajaribu kutoa ushahidi wa kibiblia na wa kihistoria kuhusu asili ya Mungu na ni kinyume kabisa na mafundisho ya Kiunitariani.

Makala hii itaichambua Biblia, mtazamo wa wa unitariani, na maandiko ya wanahistoria fulanifulani ili kutoa uhibitisho wa kibiblia na kihistoria ili kutona kama imani ya kiunitariani inaweza kuchukuliwa kuwa ni mtizamo sahihi katika mausla ya Uungu.

Wakati kwamba Uislamu ni dini kuu zaidi katika imani hii ya “kunitariani” yenye idadi kubwa ya waumini, bali makala hii itawalenga Waunitariani wanaojiita kuwa ni Wakrissto. (Sababu moja wapo inayowafanya Uislamu ukataliwu ama kupuuziwa ni kwa kuwa unafundisha kwamba kimsingi Biblia imeharibiwa maana yake na Wahayudi na Wakristo, na ndio maana kwenye Biblia hakuna hata neno moja linalouelezea uwepo wa Uislamu).

Makala hii pia itakwenda kuwajadili wale wanaojiita kuwa ni Kanisa la Mungu—lakini wakiendelea kukumbatia mafundisho haya ya kiunitariani.

 

Agano la Kale

Ili kuanza na hili tunapaswa tuanze na mwanzo wa Biblia:

Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi (Mwanzo 1:1, tafsri ya NKJV inaonyesha maneno ya pasipo kitumia kitu, au pasipo kitu, au pasipo kitu kingine).

Neno la Kiebrania lililotumika kumtaja Mungu hapa limeandikwa  'elohiym (au wakati mwingine linatamkwa elohim). Kwa hiyo ni kwa mara ya kwanza hapa Mungu anatajwa kwenye Biblia, na dalili hapa ni kwamba Mungu anatajwa kwa namna ya wingi ("mwonekano" kwa kuwa kwa sehemu nyingine 'elohim inaweza kumaanisha umoja).

Na ili kuhakikisha uwingi wa Mungu kuwa ulijulikana, ni kwenye Mwanzo 1:26 ambapo inasema,

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

 

Mwanzo 1:26 inaonyesha kwamba 'elohim hapo juu anajitambulisha kwa kusema “Sisi”. Neno Sisi linamaanisha pia uwingi.

Kwa hiyo, hakuna mashaka kabisa kuamini kuwa tangu mwanzo wa Biblia, uwingi wa Mungu ulionekana. Na hii inakubalika na pande zote mbili za wabinitariani na watrinitariani.

Hatahivyo, bado waunitariani wanadai (kushikilia yangu),

Hakuna shaka kwamba elohim ni neno linaloonyesha kuwa ni wengi na hawa ni wajumbe wanaopeleka habari au ujumbe na kwenye maandiko ya Biblia wanatajwa kuwa ni malaika na Kristo mwenyewe alikuwa ni Malaika wa Uwepo wake au Malaika wa YHVH. Ni upuuzi kudai kuwa katika kazi ya uumbaji hakuna malaika aliyehusishwa wakati Kristo mwenyewe ametajwa kuwa alikuwa ndiye yule Malaika wa YHVH. Na zaidi sana ni kwamba hakukuwa na dalili au ishara kuwa maneno ya uwingi yanayojumuisha waumbaji yalikuwa yanamaanisha mjumuisho wa Viumbe wawili ambao wote walikuwa na hadhi sawa ya uungu, yaani Mungu na Kristo. Hii ni dhana isiyo na mashiko wala ushahidi unaoiunga mkono na ambayo inapingana na isemavyo Biblia. Bali tunajionea tu kuwa ni nadharia tu iliyo na msingi wake kwenye fikra za kibinitariani, ambayo kwa kweli ni uptofu usiona maana na kitendo chao cha kukumbatia mafundisho haya kinapekekea washindwe kujinasua na imani nyingine ya Kitrinitariani. Makosa haya yalifanywa na kuindizwa kwenye Kanisa katika miaka takriban 30-40 iliyopita na wengene wameshindwa kutofautisha kati ya imani hizi. (Soma jarida la Ubinitariani na Utrinitariani Na. 76 [(Binitarianism and Trinitarianism (No. 76) (Toleo la 3.0 19941112-20001202). Hati Miliki 1994, 2000, Wade Cox, Christian Churches of God)].

 

Nukuu zinapuuzia fafanuzi za mwanzoni zinazoonyesha muundo wa jina la Mungu na uasili wake wa umoja.

 

Ni uzishi mkubwa sana kudai kwamba Kanisa la kwanza lilikuwa la imani hii ya Kinitariaani na tathmini ya majarida itaonyesha na kuthihirisha ukweli huu. Madai waliyonayo kuhusu Constantine na Mtaguso wa Nicaea ambayo wanajaribu kujengea hoja zao pia ni ya uwongo na wameyapata kutoka kwenye vyanzo visivyo halizi. Constantine alibatilisha Ubinitariani na maaskofu wao kwa kipindi cha miaka miwili na mnamo mwaka 327 alikuwa bado ni Myunitariani nay eye mwenyewe alibatizwa akiwa Myunitariani na Eusebius wa Nicomedia, ubatizo alioufanyiwa akiwa mahututi karibu na kufa kitandani kwake. Hakuna kamwe Mfalme aliyewahi kutawazwa kuwa mfalme akiwa ni Mbinitariani au Mtrinitariani na wala hakukuwa na imani hii kanisa hadi pindi alichotawazwa Theodosius ambaye aliwekwa na Gratian na akaitisha Mkutano wa Baraza Kuu huko Constantinople mwaka 381. Huko ndiko ile iliyokuwa inajulikana kama Msingi wa Imani wa Nikea (au Canons of Nicaea) ilipotezewa au ilifanyiwa marekebisho zaidi na nyingine kutupiliwa mbali na ilibidi zitungwe na kuundwa upya na kile kilichojulikana kama Misingi ya Imani au Canons ya Constantinople.

 

Ni wazi kabisa kwamba Kanisa la kwanza halikuwa ni la Kibinitariani ila lilikuwa ni la Kiyunitariani na kudai vnginevyo ni makosa na uwongo. Wanateolojia mashuhuri wanakubaliana pia kwamba hivi ndivyo ilivyokuwa (soma pia ukurasa wa Nyongeza kwenye jarida la Msingi wa Imani ya Imani ya Kikristo (Na. A1) [Statement of Beliefs of the Christian Faith (A1)]. Teolojia ni mafundisho yaliyotengenezwa au kutungwa na Wakatoliki yenye lengo la kuwashinda au kuikomesha imani ya Kibiblia juu ya Mungu mmoja ya Wayunitariani ili kuiwezesha na kuishamirisha imani na mafundisho ya kibinitariani ya Athanasian na yaliyolenga yaendelezwe hadi kufikia leo lao la kuwafundisha na kuwaaminisha watu imani ya Utatu au Utrinitariani ya Wacappadocians.

 

Rejea pia kwenye majarida ya Mafundisho ya Kwanza ya Imani ya Kikristo (Na. 88); Teolojia ya Mwanzo Kuhusu Uungu (Na. 127); Imani ya Waariani na Wasemi-Ariani (Na. 167) na Imani ya Kisociniani, Kiariani na Uyunitariani (Na. 185) [Original Doctrines of the Christian Faith (No. 88); Early Theology of the Godhead (No. 127); Arianism and Semi-Arianism (167) and Socinianism, Arianism and Unitarianism (No. 185)].

 

Nafasi Isiyo na Mashiko ya Utrinitariani

Watrinitariani walijaribu kukamata hisia na akili za watu ili waamini Mungu mwenye vichwa vitatu kwa kutumia neno la Wastoiki la hypostases au fumbo kuu na neno la Waplatoni ausia ambalo maana yake ni kilichopo na kinafanya kazi, uwepo wa kiumbe.

 

Neno hili hypostases likachukuliwa na kupewaa umuhimu mkubwa kwenye mafundisho ya Wakatoliki, kiasi cha kusababisha makufuru makubwa kuingizwa kwenye vikao vya Mitaguso ya Chalcedon na Constantinople II. Imani hii ilipelekea kutangazwa kwa kile walichokiita Monarchia na Circumincession. Tangazo hili lilisema kuwa Uungu ni kitu kilichotofauti bali sio mbalimbali kwa kweli ndiyo misemo iliyotungwa na hawa Monarchia na Circumincession. Ni jambo ambalo kifilosofia ni upuuzi linaloelezeka hivyo kwa lugha ya Kiingereza.matumizi ya hivi wanavyoviita wao hypostases na ousia kama misemo kunaonekana kuwa ni jaribio la kutofungamana kwake. Uungu unaaminika na Watrinitariani kuwa ni hypostases watatu katika ousia mmoja wakitumia maneno ya Kistoiki na Kiplatoniki ili kujaribu kutofautisha.

 

Baadhi ya Watrinitariani wanajaribu kupinga kuwa Mungu ni Kiumbe, wakitumaini kwa hiyo kumtambulisha wazo jipya na la ajabu la ziada ili kujilinda dhidi ya shutuma zinazoonekana kuwa hazina mashiko, ambavyo kwavyo wanajitetea kwa kutangaza kuwa mambo yote ni siri na fumbo kubwa.  Kitendo chao cha kukataa usemi wa kuwa Mungu ni Kiumbe na kwa Kristo ni kitendo cha dhahiri kuwa wanakataa uwepo wao, jambo ambalo ni upuuzi mkubwa. Kusema kwamba Mungu ni Mawazo Yaliyoenea tu Ulimwenguni Kote (au ni Roho Iliyoenea Ulimwenguni Kote) ni jambo linalouondoa uwepo asilia wa kimaumbile wa Mungu na ni kitendo cha kukana ukweli wa uwepo wa Mwana wa Mungu vinginevyo ni kwaamba uwepo wa Mwana ni dhana tu yenye kufikirika inayojulikana kama hypostases. Ni jina lenye utata tu ambalo halitoi ukweli wenye kufanyiwa msisitizo wa kuwepo kwa Mwana, na kisha mafundisho haya ni ya hayana mantiki kabisa na uvunjaji mkubwa na wamakusudi wa amri ya kwanza ya Mungu inayosema: Usiwe na elohim mwingine ila mimi.

 

Bwana hapa ni YHVH Eloheik (YHVH Mungu Wako) aliyetambulishwa kwenye Zaburi 45:7-8 kama Elohim aliyemtia mafuta Elohi wa Israeli. Kwa kumtukuza huyu mpatanishi wetu elohim, mmoja wa Wajumbe (Zaburi 89:7), hadi kwenye kiwango cha Eloa, Mungu Baba, kutakuwa tunaivunja amri ya kwanza. Na hii ndiyo dhambi aliyoitenda Ibilisi aliyetaka kujifanya kuwa yeye Eli wa baraza la Elohimu (Ezekieli 28:2).

 

Fundisho hili la Utatu wa Mungu limetuama kwenye mlolongo wa mambo ya kuokoteza ya uwongo yanayofanyizwa ili kuwezesha kuwayumbisha watu kiujanja. Kuna mambo kama vile:

a)   Kwamba elohim kama Uungu unaotajwa kuwa wa muunganiko wa wawili peke yao, ambao hawafanyi kuwe na tofauti yoyote kati ya Eloa na viumbe wengine wakiwemo Baraza la Mbunguni na Malaika (Danieli 7:9).

 

b)       Kwamba kuna viumbe wawili (na Roho) ambao hawawezi kutenganishwa kwa hali halisi wala kwa mawazo  na hawawezi kuchukuliwa kuwa ni Viumbe.

 

c)       Kwamba dhana ya uwepo wa Kristo huko nyuma kabla inaamini hakuwa kama Malaika wa YHVH.

 

d)       Kwamba Kristo alikuwa ni Mwana wa Pekee wa Mungu kabla ya uumbaji wa hii dunia (soma Ayubu 1:6; 38:7).

 

e)       Kwamba Kristo na Shetani walikuwa ndiyo Nyota wa Asubuhi peke yao (soma Ayubu 38:7; Isaya 14:12; Ufunuo 2:28; 22:16)

 

f)        Kwamba Kristo ni Mungu kwa mtazamo wa kwamba Mungu ni Mungu na sio mtu aliye chini ya mamlaka ya Mungu (Waebrania 1:9) aliyetumwa na Bwana wa Majeshi (Zekaria 2:10-11). Kwa hiyo amefanyika kuwa mlengwa kwenye ibada zetu na tunayepaswa kumuomba, jambo lililo kinyume kabisa na isemavyo Kutoka 34:14 na Mathayo 4:10, nk.

 

g)       Kwamba Kristo alikuwa ndiye Mwana wa Pekee na sio Mungu Pekee Aliyezaliwa na Mwana (monogenes theos & uion) (Yohana 1:18; 3:16; 1Yohana 4:9; pia tazama Luka 7:12; 8:42; 9:38; Waebrania 11:17 ili kufanya mlinganisho). Alikuwa ni mzaliwa wa kwanza (proototokos) wa viumbe vyote (Wakolosai 1:15) ambaye ni mwanzo wa uumbaji wa Mungu (Ufunuo 3:14, sio kama ilivyoandikwa kwenye NIV).

 

h)       Kwamba Kristo alikuwa na makao yake meingine mbali na hali ya uwepo wake wa kabla ya kuja kwake duniani ambako angeweza kujiombea kama Mungu. Fikra kama hii inapingana na inakataa kabisa ukweli wa tofauti aliyonayo ya Baba na Mwana na ukamilifu wa ufufuko wake. Ni mafundisho ya Mpingakristo (1Yohana 2:22; 4:3; 2Yohana 7).

 

i)         Kwamba Kristo na Mungu walikuwa na mapenzi sawa na kwamba Kristo hakuwa na mapenzi mengine tofauti ambayo kwayo alituwa na Mungu na kwa kupenda kwake mwenyewe na utii tofauti na iliyoandikwa kwenye Mathayo 21:31; 26:39; Marko 14:36 na Yohana 3:16; 4:34.

 

j)        Kwamba ule uasili wa Kimbinguni unakubali kuwa hauna maana au faida na wala hauna hasara kwa Kristo. Kwa kweli usemi huu unapinga uwezekano wa ufufuo wa watakatifu kama ulivyoelezewa kwenye 1Wakorintho 15, na kwenye ahadi za Biblia kwa wateule. Imani ya Utatu inatafuta kujenga hoja kwamba mwili wa kimbinguni waliopewa wateule unatofautiana na ule aliopewa Kristo.

 

k)       Kwamba Roho Mtakatifu ametolewa kwa kipimo tofauti na inavyosema Yohana 3:34 (Tafsiri ya RSV) na Warumi 12:6.

 

l)         Kwamba Kristo hangeweza kutenda dhambi (kutokana na mtazamo wa potofu wa kuhusu uweza wa miili ya kimbinguni unaokubaliana kuwa hakuna faida wala hasara zaidi ya vile kuwa wa uwezo wa Mungo wa Kujua kila kitu, ambaye alijua kwamba Kristo asingeweza kutenda dhambi).

 

m)     Kwamba Kristo alikuwa na mafungamano ya pamoja na Mungu kiasi kwamba alikuwa yuko sawa kwa kila kitu na alikuwa pia yuko sawa katika hali ya umilele na Mungu, kinyume na inavyotuambia Wafilipi 2:6 na 1Timotheo 6:16, zinazotuonyesha kwamba Mungu tu ndiye asiyeweza kufa. Umilele wa Kristo au uzima wa aioonion (1Yohana 1:2) na ule wa Viumbe wote, akiwemo Kristo, unatokana na umilele ule. Wote wawili, yaani Kristo na wateule wanaasili moja, Waebrania 2:11 (RSV) wanajipatia uzima wao wa milele kwa kupitia utii wao wenye masharti kwa Baba (Yohana 5:19-30) aliyetuumba sisi sote (Malaki 2:10-15). Kama Baba alivyo na uzima nafsini mwake, pia amempa Mwana awe na uzima nafsini mwake (Yohana 5:26), nasi tu warithi tuliokusudiwa kupewa uzima nafsini mwetu kwa mamlaka au weza wa Mungu.

 

n)       Kwamba wateule sio Wana wa Mungu kwa namna aliyonayo Kristo kuwa kwake Mwana wa Mungu na kwa hiyo sio warithi pamoja naye, ni kinyume ka ilivyoandikwa kwenye Warumi 8:17; Wagalatia 3:29; Tito 3:7; Waebrania 1:14; 6:17; 11:9; Yakobo 2:5 na 1Petro 3:7.

 

o)       Kwamba Mungu Mkuu Mwenyewe alishuka hapa chini katika mwili na kuishi pamoja na wanadamu (kupingana na madai ya waongo kwenye 1Timotheo 3:16 kwenye Codex A. Madai ya uwongo yalitupiliwa mbali kwenye KJV na yakawekwa kiujanja kwenye mhutasari wa NIV). Madai yakuwa kwamba Mungu Mwenyezi alishuka hapa duniani katika mwili yako kinyume kabisa na Yohana 1:18 (na Yohana 1:14 ambapo kulikuwa ni andiko la mfano tu yaani logos (au Memra) ambaye alikuwa mwili) na maandiko kadha wa kadha yanamtenga Kristo mbali na Mungu Mmoja wa Pekee na wa Kweli (Eloa au Theon, ambaye ndiye Baba Mungu), Mungu wa Yesu Kristo (Yohana 17:3; 20:17; 1Wakorintho 8:6; 2Wakorintho 1:3) anayesimama kwa jina lake mwenyewe (Mika 5:5).

 

Fundisho hili la Mungu kuwa ni Mmoja tu linaeleweka vibaya na waamini Utatu. Jina Shema (Kumbukumbu la Torati 6:4) linahitaji kulielezea kwa undani sana na muda hautoshi hapa (jisomee jarida la Yoshua, Masihi, Mwana wa Mungu (Na. 134) [Joshua, the Messiah, the Son of God (No. 134)]. Yule anayetajwa kwenye Kumbukumbu la Torati 6:5 anajulikana kama Mungu Mwenyezi, na ni Mungu aliyemtia mafuta Kristo awe Elohi wa Israeli kwenye Zaburi 45:7. Umoja wa Mungu ni sharti muhimu sana kwenye imani ya Waabudu Mungu mmoja, maarufu kama Monotheism, na ni agizo kuu linaloenezwa kuishi kwenye umoja wakiwa na nia moja mioyoni wakikubaliana na katika Roho na Uweza wa Mungu (1Wakorintho 2:4-14), ambayo ni kwa njia ya Kristo kwa Mungu (2Wakorntho 3:3-4).

 

Imani ya Utatu inakataa umuhimu wa umoja wanaouamini juu ya Mungu mmoja na imani hii kwa kweli ni ya kuamini na kuabudu miungu wengi. Imetokea hivo kwa kuwa watawala hawaelewi, yale yasiyo ya kiroho (1Wakorintho 2:8,14).

 

Maswali ya kuwauliza Watrinitariani

Iwapo kama Mungu ni mtu mmoja aliye kwenye nafsi tatu au hypostases, akiwa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, inawezekanaje mambo yafuatayo yatokee, yakiwa yameandikwa wazi kwenye Biblia?

 

·      Kwa Yesu Kristo apokee ufunuo kutoka kwa Mungu?

Ufunuo 1:1 inasema kwamba “Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;

 

Itawezekana vipi tena huyu Kristo aketi kwenye Kiti cha Enzi cha Baba? (Ufunuo 3:21) Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi..”

 

·      Iweje tena kichwa cha Kristo awe ni Mungu?

(1Wakorintho 11:3) Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu..

 

·      Iweje basi Kristo amlilie tena Mungu?

(Kama alivyofanya kwenye Mathayo 27:46; Marko 15:34): “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

 

·      Iweje tena Kristo apae juu kwa Mungu kama alivyofanya kwenye Yohana 20:17?

Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu..”

 

·      Iweje basi afundishe kuwa wote walio na Roho wa Mungu wawe Miungu?

Katika Yohana 10:34-36: “Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? 35 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); 36 je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?

 

Tamko la kwamba Maandiko hayatanguki linatolewa hapa ili kuonyesha kwamba tunapaswa kuwa miungu midogo yaani elohim na kwamba hatima yetu haitaweza kuvunjika au kushindwa. Itakuwaje basi Mungu amtenge Kristo mbali na wengine akiwa ni yeye mwenyewe na akatumwa ashuke hapa duniani akiwa yeye ni Mungu kukiwa hakuna wengine?

 

·      Iweje basi maandiko yaseme kwamba Kristo ameumbwa na Baba?

Kwa yeye kuwa mwanzo (arche – sio mtawala kama inayovyosema NIV) uumbaji wa Mungu (Ufunuo 3:14), “…naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. (Wakolosai 1:15).

Watrinitariani wanajaribu kudai kwamba maneno haya ya arche na proototokos ni ya kiwadhifa tu ili kukwepa hitimisho dhahiri linalofuatia kifungu hiki cha maandiko kikilinganishwa na 1Timotheo 6:16, inayoonyesha kwamba ni Mungu tu ndiye kwenye kuishi milele na asiyekufa.

 

·      Je, inawezekana kwa mtu kujiomba mwenyewe?

(Yohana 3:16) Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ...

 

·      Inakuwaje basi Baba awe ndiye yote katika yote?

(Waefeso 4:6) Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.

 

Kwa hiyo muandiko haya yanakataa dhana hii ya kwamba Baba yuko ndani ya Mwana na kwamba Mwana yuko ndani ya Baba. Mahusiano haya ya mwana na mzazi yanaendelea hadi kwa wateule pia.

 

Yesu ni Mwana wa Mungu Mwenyezi (Marko 5:7) ambaye ndiye Mungu na Baba (Wakolosai 1:3; 1Wathesalonike 3:11), akiwa ni tofauti mbali na Mungu ba Baba yetu (2Wathesalonike 2:16). Kwamba usemi wake wa kwamba Mungu ni Baba yake haumfanyi au kumaanisha kuwa yeye yu sawa na Mungu, kama ilivyokuwa imedaiwa na Mafarisayo kuwa alisema katika Yohana 5:18. Kwa hiyo madai ya Watrinitariani ni uwongo ule ule kama Kristo alivyoshitakiwa nao. Je, inakuwaje hivyo?

 

·      Iwapo kama kuwa hawa hypostases watatu, inawezaje basi kuwe na roho saba za Mungu (Ufunuo 5:6)? Je, macho haya saba yaliyo kwenye pembe saba za Mwanakondoo sio migawanyo saba iliyo mbalimbali au ni mamlaka zilizotumwa zitoke kwa maelekezo ya Kristo akiwa ni Mwanakondoo ili zimiliki Nchi?

 

·      Inawezekanaje kiumbe ajitoe sadaka atakayoipokea yeye mwenyewe?

(1Petro 1:19) bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.... ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu..

Warumi 5:15 inasema: Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.

.

Imani na tumaini letu ni kwa Mungu, na sio kwa Kristo, bali ni kwa kupitia huyu Kristo kwa njia ya Roho ambaye ndiye Roho wa Imani na Kweli.

 

·      Inawezekanaje kumbe ajiombe mwenyewe na/ au ajipe kitu mwenyewe?  Kwa mfano:

(Luka 11:13) “...Je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?

(Yohana 17:4) “...nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

(Yohana 17:9) “Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;

(1Yohana 5:10) … kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.

 

·      Inawezekanaje kiumbe kiwe kikubwa kuliko chenyewe?

(Yohana 14:28)Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.”

 

·      Inawezekanaje kiumbe kijigawe kwa jinsi inavyijua?

(Mathayo 24:36) “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.

(Ufunuo 1:1) Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi;

 

·      Inawezekanaje kiumbe kijiombe chenyewe?

(1Timotheo 2:5) Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;

 

(Wagalatia 3:20) Basi aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja.

(1Yohana 2:1)  ... tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,

(1Yohana 2:22) Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana.

 

·      Inawezekanaje kiumbe kijinyenyekeshe kwake chenyewe?

(Yohana 10:18) “...Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.

·      Inawezekanaje kiumbe kiyakatae mafundisho yake chenyewe?

(Yohana 7:16) “Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka.”

 

·      Inawezekanaje kiumbe kimoja kitofautiane kimatakwa na bado kiendelee kuwa kiumbe kimoja kile kile, Kristo amtii aliye juu yake ambaye ni Mungu?

(Mathayo 7:21)Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.”

(Mathayo 12:50) “Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.”

(Mathayo 26:39). “...akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.

(Marko 3:35) “Kwa maana mtu ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.”

(Yohana 4:34) “...Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

(1Wathesalonike 5:18) ... shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu..

 

·      Inawezekanaje kumbe mmoja Yule Yule awe ni msaidizi au mdogo na hapohapo awe sawa na aishi milele nab ado awe ni sehemu ya mfumo endelevu, ujulikanao kama mwili wa Kristo pasipokuwa na kiwango kilekile akiongezeka kwenye idadi yote ya mwili?

 

·      Inawezekanaje mtu ajiombe na kujiabudu mwenyewe huku akiwa hana tatizo lolote lile la kisaikolojia?

Mungu ndiye anayepaswa pekee kuabudiwa kama alivyoelezewa kwenye kitabu cha nabii Isaya na ikarudiwa na Kristo kwenye Mathayo 15:9: “....waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.

(Luka 4:8) “Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.”

(Yohana 4:21-23) “...Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.”

(Waefeso 3:14-15) Kwa hiyo nampigia Baba magoti,  ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.

 

·      Inawezekanaje mtu mwenye uweza wa kuwepo kila mahali kwa wakati mmoja aliye wa hypostases aje na kuondoka mwenyewe?

(Yohana 14:28) “Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.

(Yohana 16:27-28) “...na kusadiki ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba.”  

 

·      Sambamba na hilo, anawezaje kuwa ni mkubwa kuliko mwenyewe? Au anawezaje kuonekana na kisha akane kuwa hakuna aliyemuona?

(Yohana 6:46) “Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba.

(Yohana 5:37) “Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.

 

·      Inawezekanaje Mungu awe na umbo na asiwe na umbile?

 

·      Inawezekanaje mtu ajisikilize mwenyewe na kisha awe ndiye mtu wa kumuomba tunaposali?

(Yohana 11:41-42) “...Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.”

 

·      Inawezekanaje mtu awe dhaifu na hapohapo ajisaidie mwenyewe?

(Yohana 5:19) “...Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile

 

·      Inawezekanaje mtu ajikabidhi mamlaka mwenyewe?

(Yohana 12:49-50) “Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. 50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo..”

 

·      Inawezekanaje mtu ajinyenyekeshe kwake mwenyewe na kisha ajipe kitu mwenyewe?

(1Wakorintho 15:28) Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

(1Wakorintho 15:24) Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

 

·      Sawa na hilo, inawezekanaje mtu kujikabidhi mamlaka mwenyewe?

(Yohana 5:30) “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.

(Yohana 5:19) ... Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.

 

·      Inawezekanaje basi Kristo akabidhi Ufalme wa Mungu kwa Baba ikiwa wao ni mtu mmoja?

(Mathayo 26:29) “Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”

(Marko 10:15) Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa

(Luka 12:32) “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme..”

 

·      Inawezaje basi mtu aliyesawa awe na kitu cha kuhitaji kwa Baba ili akitwae tena wakati atakapoamriwa kufanya hivyo?

(Luka 22:29-30) “Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi; mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.”

 

·      Inawezekanaje basi wateule wawe warithi pamoja na Kristo ikiwa Kristo ni Mungu tayari akiwa na sifa ya Uungu wa milele? Ni nini basi au je, kuna chochote cha kurithi hapo?

(Warumi 8:17) ... na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; ...

 

·      Inawezekanaje basi mtu ajikiri au ajikane mbele zake mwenyewe?

(Mathayo 10:32-33) “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.  Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

 

·      Inawezekaje basi mtu ajipende au ajichukie mwenyewe na kwa kumaanisha kabisa pasipokuwa na matatizo ya kisaikolojia?

 

Maswali ya Watrinitariani kuhusu Asili ya Mungu na Kristo yanayoonyesha makosa ya uelewa, au yanayojaribu kuwapotosha Wasomaji wa Biblia

 

Swali la 1. Ni kwa nini Thomaso alimuita Yesu Mungu kwenye Yohana 20:28?

 

Jibu 1. Maandiko kwenye Yohana 20:28 yameelezwa vizuri kwenye jarida la Malaika (Na. 24) [The Angel of YHVH (No. 24)]  kwenye Kutoka 34:6 wakati Kristo anajitangaza kuwa ni: “Bwana, Bwana, mungu mwenye rehema na neema”. Andiko hili limerudiwa tena katika Zaburi 86:15 na uhusiano wake umetangazwa tena kwenye Zaburi 45:7-7 na Waebrania 1:8-9. Alikuwa ni elohim mdogo wa Israeli ambako kulikuwa na zaidi ya mataifa 72 (soma Kumbukumbu la Torati 32:8 (RSV, LXX, DSS). Kufuatia mtazamo huu hadi kwenye Waebrania 1:7-10 hapo chini inahusianisha nyuma kwenye Zaburi 2:9 na Ufunuo 2:27; na pia kwenye Waebrania  3:1,14. Vigezo vimeorodheshwa kwenye Luka 4:18 ambapo Roho wa Bwana alikuwa juu yake ili awahubirie maskini na kuwaachia huru mateka. Hii iliwezekana kwa kupitia Roho Mtakatifu akiwa amefanyika kuwa ni Mwana wa Mungu na kutumwa akiwa na Roho wa Mungu (sawa na Matendo 4:27; 10:38; 2Wakorintho 1:21).

 

Swali la 2. Ni kwa nini Yesu ameitwa Mungu kwenye Waebrania 1:8 na hii inamaana gani? Je, ni kwa namna gani basi yeye anakuwa ni mwakilishi wa Mungu?

 

Jibu 2. Maandiko yaliyo kwenye Waebrania 1:3 yanasema aliudhihirisha utukufu wa Mungu na kuchukua mwonekano ule ule wenye asili yake. Na hii ndiyo sababu anaitwa Nyota ya Asubuhi ambayo inatoanuru ya nguvu za jua na inamuashiria Roho Mtakatifu.

Waebrania 1:1-14 inasema: Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. 3 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; 4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao. 5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana? 6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu. 7 Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto. 8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. 9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio. 10 Na tena, Wewe,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za mikono yako; 11 Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu; Nazo zote zitachakaa kama nguo, 12 Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma. 13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? 14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

 

Waebrania inarudia kile kilichoandikwa kwenye Zaburi 45:6-7.

Kusudi la sura hii ni kutangaza kazi za Kristo kama ndiye aliyeinuliwa juu kwa ajili ya kitendo chake cha kuzaliwa kwenye tumbo la mwanadamu. Tafsiri hii ni madai ya uwongo kusema kwamba Kristo aliteuliwa na kufanywa kuwa ni mrithi wa vitu vyote.


Andiko hili limetafsiriwa kwamba: "Kwa yeye aliyeiumba dunia", ila huu ni uwongo kwa kuwa pale ilipoandikwa “neno” pametafsiriwa kwa makusudi kuwa “dunia” kwenye aya ya 2 ambayo kwa kwelis ni Aeonas au kingo za dunia na maongozi yake. Kristo hakuumba dunia. Bali aliyafanya mambo tangia zama ya Adamu. Mungu alimtuma Kristo akiwa ni prototokos kwa mwonekano wa kimalaika Mkuu ili awakomboe Kundi la watu wa Mungu na akawatuma malaika na roho wenye kuwatumikia wanadamu na walitumwa waende ili wanadamu waupokee wokovu. Kristo aliwekwa juu yao.


K risto alitumwa ili awakomboe wote wawili, yaani wanadamu na Malaika Walioanguka ambao kwao ndiko alikwenda kuwahubiria huko kifungoni kwao ambako kunaitwa pia Tartaros, kama tunavyosoma kwenye 1Petro 3:14-4:6: inaposema:

Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. 15 Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. 16 Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. 17 Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya. 18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. 21 Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. 22 Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.

 

1Petro 4:1-6 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. 2 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; 4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. 5 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. 6 Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.


Andiko hili linaonyesha kwa wazi sana kwamba Kristo ni elohim mdogo wa Israeli ambaye alikuwa ni mtumishi wa Baba Mungu na pia kiwa ni ndugu na wana wa Mungu ambao walikuwa ni Malaika.


Andiko linatafsiriwa kama: Aliudhihirisha Utukufu wa Mungu na kuwa na hali yake asilia akiishi hapa ulimwenguni kwa neno la nguvu zake. Andiko hili limegeuzwa hivyo kwa makusudi ili kufanya ionekane kuwa inakusudia kusema kuwa inashikiliwa na nguvu za Kristo bali inashikiliwa na uweza wa neno la Mungu. Na ambavyo ni kwamba “kuchukua vitu vyote kwa nguvu za neno lake (yaani Mungu)” (sawa na kitabu cha fasiri cha Marshalls Interlinear Greek English).


Mwandishi wa Waraka kwa Waebrania ameonyesha pia jukumu hili kwenye Waebrania 3:1-6.

Waebrania 3:1-6 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu, 2 aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu. 3 Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba. 4 Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu. 5 Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye; 6 bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho..


Katika Waebrania 3:2 inasema kwa wazi sana kwamba Kristo alikuwa mwaminifu kwake aliyemuumba. Neno la asili la Poiesanti maana yake “yule aliyemfanya au kumuumba” na imetafsiriwa tu kama aliyemtuma kwa mahali hapa pamoja pekee na mahali pengine imetafsiriwa kwa maana ya “kufanya” kwa sehemu zote mbilia za Agano Jipya la tafsiri ya LXX.

 

Pia soma kwenye jarida la Utangulizi Kuhusu Uungu (Na. 193) [Introduction to the Godhead (No. 193)].

 

Kwa ajili hii yeye alikuwa ni mzaliwa wa kwanza wa Uumbaji wa Mungu (Wakolosai 1:15) na Mwanzo (Arche) wa Uumbaji wa Mungu (Ufunuo 3:14).

 

Swali la 3. Ni kwa nini Mtume Yohana anasema kwamba Yesu nmdiye alikuwa Neno ambalo ndilo lilikuwa Mungu ambalo lilifanyika mwili (Yohana 1:1,14)?


Jibu 3. Neno hili “Neno” linatokana na neno lililoko kwenye lugha ya Kiyunani liitwalo Logos ambalo kwa Kiebrania huitwa Memra ambaye alikuwa ni msemaji wa Mungu. Yohana 1:1 imetafsiriwa kimakosa na kwa makusudi na hawa waamini Utatu. Kiusahihi, ilitakiwa isomeke hivi: Hapo mwanzo lilikuwepo neno na neno lilikuwa la Mungu na Mungu alikuwa ndiye hilo neno. Shina la uandishi marazote linamwelekeo wa lugha ya Kiyunani. Tafsiri ya Agano Jipya iitwayo The Concordant Literal limeruka kiini hiki cha shina walipokuwa wanatafsiri sehemu hii hivyo. Tafsiri nyingine inayoitwa The New World Translation imeweka kishina hiki lakini ikalibadili uratatibu wa neno la mwisho. Aya ya  14 inasema wazi kwamba huyo Memra akafanyika mwili na kuishi pamoja nasisi nasi tunauona utukufu wake kama wa mwana pekee ashukaye toka kwa Baba. Mantiki ya ayah ii inaelezewa kwenye Yohana 1:18 ambapo huyu monogenese theos, au mungu mdogo pekee kuzaliwa, ndiye pekee aliye kifuani mwa Baba na aliyenena au akitangaza. Neno “Yeye” limeongezwa na ni makosa au limewekwa kiujanya kwa nia ya kupotosha (pia soma jarida la
 Kwenye Maneno: Monogenes Theos kwenye Maandiko Matakatifu na Mapokeo (Na. B4) [On the Words: Monogenes Theos in Scripture and Tradition (No. B4)]. Mungu hayawahi kamwe kuooekana na yeyote mwenye mwili (Yohana 1:18, 6:46 1Timotheo 6:16).

 

Hili limefafanuliwa pia kwenye jarida la Uwepo wa Yesu Kristo Hapo Kabla ya Kuzaliwa Kwake (Na. 243) [The Pre-Existence of Jesus Christ (No. 243)].

 

Tofauti ya Viumbe imefanywa kwenye maandiko yaliyo kwenye Yuda 4 lakini yamegeuzwa na hawa waamini Utatu na wakaungwa mkono na Wabinitariani/Waditheist (soma Jibu la 13 hapo chini).

 

Swali la 4. Ni kwa nini usemi usemao "Liitie Jina la BWANA" (Kiebrania, YHVH, kama kwenye Zaburi 116:4) linatumika kwa Mungu tu kwenye Agano la Kale, na kutafsiriwa kwenye Biblia ya Kiyunani maarufu kama “the LXX” ikisomeka: "Liitie Jina la BWANA (Kiyunani, KURIOS)," ikimaamisha Yesu kwenye Agano Jipya (1Wakorintho 1:2) iwapo kama Yesu sio Mungu katika mwili?

 

Jibu 4. Swali hili linatokana na mafundisho ya uwongo na mapotofu yaliyopangiliwa kwa mchanganyiko wa maneno ya kweli. Swali hili linaonyesha kutoelewa tofauti iliko kwenye majina mawili haya, yaani Yahova (SHD 3068) na Yahovi (SHD 3069) na utendaji kazi wake ndani ya Watakatifu. Jina Yahova Malaika aliyewaongoza Israeli au yeyote Yule aliye miongoni mwa wana wa Mungu anayepeleka ujumbe kwa niaba yake Mungu au anayemwakilisha Yahova aliye Bwana wa Majeshi ambaye ni Eloa. Yahova ni nafsi ya tatu ya vebu, maana yake ni Yeye aliyesababisha na ikawa na inamaanisha au kuwahusu Viumbe wote walio katika mwonekano wa kilamaika ambao pia ni wajumbe wa Mungu (ambaye ni Eloa), ambaye ndiye Elyon (Mungu Aliye Juu Sana) au Yahova wa Majeshi maana yake ni Yahova mkuu ni Yahovi.

 

Tofauti iliyoko kati ya watu hawa wawili inaeleweka sana na wakati maneno haya mawili yanaposomwa kwa Kiebrania hawasemi Yahovi na Yahova, bali wanasema Elohim kwa 3069 na Adonai kwa 3068.

 

Maandiko yanaonyesha kwenye Mwanzo 18 na 19 kwamba wakati Mungu alipowatuma waende kwa Ibrahimu na Lutu walikuwa Malaika (Yahova) watatu walioonekana na mmoja wao akabaki na Ibrahimu na wale wawili wengine wakaenda kwa Lutu na kisha wakatangaza hukumu kweny mji ule na kisha wakaagiza moto ushuke kutoka mbinguni kwa Yahova (soma jarida la Makaila wa YHVH (Na. 24) [The Angel of YHVH (No. 24)].

 

Neno kurios lina tofauti iliyo sawa na lile la Kiyunani ila maana yake kiutendaji linaendana na viumbe wengi walioko kote kuwili, yaani mbinguni na wakibinadamu. Madai wanayoyafanya kuhusu maneno ya Kiebrania na kwamba uhusiano wake ni ya uwongo na inaonyesha kukosa kwao uelewa wa maandiko ya Agano la Kale na majina ya Mungu.


Swali la 5. Nikwa nini Mtume Yohana anasema kwamba Yesu alikuwa, "...kumuita kwake Mungu baba yake, kulimfanya awe sawa na Mungu" (Yohana 5:18)?

 

Jibu 5. Yohana 5:18 kwa kawaida inafanya marudio:

[18] Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.....

 

Andiko hili linaonyesha tofauti inayokutikana kwenye Zaburi 45:6-7 wakati malaika au elohim wa Israeli alipokuwa Mwana wa Mungu kutokana na maandiko haya. Alikuwa ni mwana wa Ha Elohim ambapo alijifanya mwenyewe kuwa ni elohim. Yeye ni malaika tu au elohim na mwenye Baba Mungu juu yake ambaye ndiye elohim wake. Alikuwa ni elohim lakini hakuwa ndiye Yule Mungu Mkuu, wa Pekee na wa Kweli. Usawa alionao ni kwamba alimudu kujifanya awe sawa na malaika au theos aliyewaongoza Israeli. Tofauti hii imefunikwa kwa makusudi na Watrinitaria na wakauficha ama kuugeuza ukweli wa tofauti hii. Mungu Mkuu na Wapekee na wa Kweli mara zote alijulikana na kuandikwa au kutajwa kuwa ni Ton Theon au Ho Theos kwa Kiyunani na mwenye waliochini yake malaika, na kwa kweli, malaika au elohim yeyote alijulikana ama kutajwa kama Theos (SGD 2316). Tofauti mbili zilizokuweko kati ya Ton Theon na Theos zote mbili zimeelezwa kwenye 2316 na zikichukuliwa kama ni mambo ya shutuma na uteuzi kwa kweli wakati Koine inapotumika kwa namna hii ili kufanya tofauti kati ya Eloa /elohim au Ha Elohim na Elohim au Yahovi/Yahova kwenye Kiyunani ambacho Watrinitariani wanapuuzia. Kwenye andiko hili inasema kwamba alikuwa ni yeye aliyemfanya Baba Ton Theon awe sawa na /Mungu Mkuu (Theos). Andiko hili lina watu wawili wanaoonekana Mungu, mmoja aliwa mkuu kuliko mwingine.   

 

Pia soma jarida la Zaburi 45 (Na. 177) [Psalm 45 (No. 177)]

 

Swali la 6. Ninini alichokisema Yesu hadi kikawapelekea Mafarisayo wadai kwamba Yesu alikuwa anajifanya au kujilinganisha na Mungu?

 

Jibu 6. Kwa mara nyingine tena ni kwamba tofauti iliyopo kati ya Ukuu na udogo uliopo kati ya Mungu na malaika Theoi (umoja) ulifahamika na waumini wa kanisa la kwanza na kwa Wayahudi na jambo hili lilifichwa na Wabinitariani na Watrinitariani ambayo ilichukuliwa kutoka kwenye robo ya mwisho ya karne ya pili huko Roma.

 

Pia soma jarida la Makosa ya Uelewa wa Teolojia ya Kwanza Kuusu Uungu ya Wabinitariani na Watrnitariani (Na. 127B) [Binitarian and Trinitarian Misrepresentation of the Early Theology of the Godhead (No. 127B)].

 

Swali la 7. Iliwezekanaje basi Yesu kuyajua mambo yote (Yohana 21:17)?


Jibu 7. Huu ni ujanja wa Watrinitariani tena unaotokana na makosa ya kutafsiri. Neno lililotafsiriwa hapa kwa maana ya kujua ni neno linalotamkwa oidas (eidos) (SGD 1491) ambalo maana yake ni kufahamu au kuyaona mambo yote. Na imefafanuliwa kwa kina kwenye kamusi ya SGD 1492 (lakini halionekani kwenye kitabu cha Strong kabisa kama 1492) ambavyo ni Eido yenye maana ya kujua lakini ikiandikwa eidos inamaanisha uwezo tu wa kuona au kuwa na mtazamo.

 

Yohana 21:17 imetafsiriwa na maneno mawili ya oidas na ginoskeis yenye maana ya kujua wakati neno lake la pili tu ginosko lina kanuni na matamshi hayo.

 

Kiusahihi inamaana ya kwamba “unapokea kila kitu na unajua kwamba nakupenda” Ni aina nyingine ya udanganyifu wa Watrinitariani kutumika kwenye maandiko ya Kiingereza.

 

Mathayo 24:36 "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake."

 

Majibu ya Kristo yalikuwa sio ya mtu mwenye kufahamu kila jambo na Ufunuo 1 inasema wazi kwamba ulikuwa ni Ufunuo wa Mungu ambao alimpa Kristo. Yeye hakujua ukweli wake na kwa hiyo hakuwa mwenye uwezo wa kujua kila kitu. Alipopewa maandiko haya alikuwa ameshafufuka tayari na alikuwa mbele za Mungu.

 

Yeye hayuko sawa na Mungu:

Mathayo 26:53 "Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?"

Iwapo kama Kristo angekuwa sawa na Mungu basi angewahubiria Malaika wake tu.

 

Baba ndiye anayejua majira na nyakati.

Marko 14:36: "Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe."

 

Uwezo wote aliokuwanao pamoja na wakujua mambo ulitoka kwa Baba na yeye Kristo alipewa tu sawa na kama walivyoruzukiwa watumishi wake manabii ambao waliwaeleza wanadamu. Hawako sawa, wala hawana umilele wote wawili, yaa ni Baba Mungu au Eloa ambaye ndiye aliye Mungu wa Pekee na wa Kweli na ndiye anayetuchagua kila mmoja wetu ili apewe Kristo na turuzukiwe Roho Mtakatifu. Na hatimaye tunafanyika kuwa na uhusiano mzuri na Baba kwa kupitia jina la Kristo.

 

Yohana 16:23-33 Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. 24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. 25 Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba. 26 Na siku ile mtaomba kwa jina langu, wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; 27 kwa maana Baba mwenyewe awapenda kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, na kusadiki ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. 28 Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba. 29 Basi wanafunzi wake wakasema, Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni mithali yo yote. 30 Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote, wala huna haja ya mtu akuulize; kwa hiyo twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu. 31 Yesu akawajibu, Je! Mnasadiki sasa? 32 Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. 33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu..


krristo alisema kwamba: “Mambo yote ninayowaambia ni ya Baba yangu.”

 

Mathayo 11:27 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.


Luka 10:22
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.


Yohana 14:26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Yohana 15:15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.


Swali la 8. Inawezekanaje basi Yesu awajue watu wote (Yohana 16:30)?

 

Jibu 8. Neno watu au wanaume halikuandikwa kwenye andiko lililoko kwenye sura ya 16:30 na neno lililotasfiriwa kujua ni wazee na oidas (SHD 1491) ambalo maana yake ni sasa tunaona ya kwamba unaelewa mambo yote. Hii ni aina nyingine ya makosa ya kitafsiri. Kiini au nia iliyokusidiwa iko wazi kama inlivyo hapo juu. 

 

Swali la 9. Inawezekanaje basi Yesu aweze kuwa kila mahali (Mathayo 28:20)?

 

Jibu 9. Andiko hili halisemi chochote kuhusu Kristo kuwepo kila mahali kwa wakati mmoja. Bali anachosema hapa ni kwamba atakuwa pamoja nasi hadi ukamilifu wa dahari, jambo ambalo kwa kweli limetimilika kwa kuja kwake Roho Mtakatifu ambaye pia amewezesha kuandikwa kwa maandiko hata matakatifu: kuamini vinginevyo ni makosa mengine ya kitafsiri.

 

Swali la 10. Inawezekanaje basi Yesu Kristo awe ndani yetu (Wakolosai 1:27)?

 

Jibu 10. Ndiyo! Anakaa ndani yetu kupitia Roho Mtakatifu ambaye ndiye uweza wa Mungu na aliyetumwa na Mungu (Eloa).
tunashiriki mwili na damu ya Kristo. Kristo anaishi ndani ya wale wanaoshiriki kuula mwili na damu yake.

 

Kwa njia ya ubatizo na kuwekewa mikono, wateule wanapewa fursa ya marejesho mapya ya kiroho ya kila mwaka kwa tendo hili la kushiriki Ushirika wa Mlo wa Bwana wa majira ya Pasaka. Kristo anaishi ndani yetu kwa kujielezea mapenzi yetu na uweza wa Mungu, Baba yetu. Maandiko makamilifu yanawezesha kupata uelewa kamili way ale anayoyapenda na kuyaagiza:

Wakolosai 1:20-29 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni. 21 Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; 22 katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama; 23 mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake. 24 Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake; 25 ambalo nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu; 26 siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; 27 ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu 28 ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. 29 Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu..


baba aliishi ndani ya Kristo kwa mtindo huo huo ambao kwao anaishi ndani yetu sisi. Wao ni wamoja kama sisi tulivyo na umoja na Kristo alipotupatanisha na kuwa tumekombolewa kwa njia ya dhabihu yake aliyoitoa kwa ajili yetu. Na yeye (Kristo) atatuwakilisha au kututambulisha kwa Baba ili kwamba yeye (BABA) awe yote katika yote na ndani ya yote.

 

Kristo anaishi ndani yetu kwa mapenzi ya Eloa ambaye ametupa sisi Kristo na aliyetupelekea roho Mtakatifu ili kwa yeye kazi yote ikamilike na kwa kupitia yeye tuweze kuzijua Risi za Mungu na turuzukiwe tunda la Roho Mtakatifu.

 

Mathayo 7:21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.


ni kwa kupia mapenzi ya Mungu tunafanyika kuwa warithi pamoja na Kristo na tunapewa uzima wa milele kama alivyopewa Kristo.

 

Swali la 11. Ni kwa jinsi gani basi Yesu anaweza kuwa wa milele (Mika 5:1-2)?

 

Jibu 11. Swali kama hili linatokana na dhana fikirika tu nay a kubuni inayotokana na upotoshaji wa maana iliyo kwenye andiko la Mika 5:1-3. Andiko hili limefafanuliwa kwa kutumia mamlaka ya Kiebrania kwenye jarida la Mika 5:2-3 (Na. 121) [Micah 5:2-3 (No. 121)]. Ni kama waamini Utatu wote wanavyorudiarudia pamoja na wa Binitariani na Waditheist wanavyofuliza kufundisha na kuamini, haya yote ni matokeo ya kushindwa kutafsiri vizuri tu.

 

Swali la 12. Inawezekanaje kuwa Yesu awe ndiye mtoa uzima wa milele (Yohana 10:27-28)?

 

Jibu 12.  Aya ya 29 inaendelea kufafanua jambo hili kwamba ni Kristo atoaye uzima wa milele kwa uweza na mamlaka ya Mungu. Tumefanyika kuwa warithi pamojanaye katika urithi wake. Andiko lile linaloelezea hili linapatikana kwenye Marko 10:17; Yohana 3:15; 17:2-3 (pia soma jarida la Uzima wa Milele (Na. 133) [Eternal Life (No. 133)].


Swali la 13. Anawezaje yeye kuwa Bwana wetu wa pekee na Bwana Mkubwa wetu (Yuda 4)?

 

Jibu 13. Yuda 4 ni andiko linguine lililokosewa walipotafsiri na ni hila za waamini Utatu au Watrinitariani.

 

Tafsiri ya RSV katika maandiko ya Kiyunani na Kiingereza ya tafsiri iitwayo Marshalls Greek English Interlinear inasema:

Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.

 
Andiko hili linaongelea kuhusu neema ya Mungu na pia hukusu bwana wetu wa pekee na mwokozi wetu Yesu Kristo (au bwana wetu wa pekee na mwokozi wetu Yesu Kristo kama maandiko mengine yanavyosema, kama ukisoma tafsiri ya Marshalls).

 

Tafsiri ya KJV unapoisoma, haionyeshi maandiko haya kuwa yanasema Bwana na Mungu wa pekee na Bwana wetu Yesu Kristo. Tafsiri ya Bullinger na mamlaka vinakubali kwamba maandiko haya hayasemi Bwana Mungu na kwa kweli neno Bwana ukweli ni neno despotes ambalo maana yake ni bwana mkubwa na sio Bwana.

 

Haya ni makosa mengine yenye mwonekano wa kughushi kuongeza neno Mungu mahali ambapo hakuna neno kama hilo kwenye maandiko asilia ya Kiyunani.

 

Swali la 14. Inawezekanaje Yesu aitwe Mungu mwenye Nguvu (Isaya 9:6) iwapo kama kuna Mungu mmoja tu anayeishi (Isaya 44:6-8; 45:5)?

 

Jibu 14. Bwana huyu amejibiwa ama kuelezewa ufafanuzi wake kwenye jerida la Isaya (Na. 224) [Isaiah 9:6 (No. 224)].

 

Kuna mabwana wengi au elohim au theoi. Zaburi 45:6-7 (Waebrania 1:8-9) inainyesha kuwa kuna Mungu mmoja pamoja na wasaidizi wake na hawa wasaidizi wana ndugu wengi. 

 

Mtume Paulo anasema kuwa kuwa theoi polloi akimaanisha kuwa kuna miungu mingi.

 

Isaya 9:6 anatumia neno El (SHD 410) na El inaweza kuwa na maana ya mtu mwenye nguvu au Mungu na inaweza kumaanisha yeyote kati ya Malaika au mwanadamu. 


Tafsiri ya LXX kuhusu Isaya 9:6 inamwita Kristo Malaika wa Shauri Kuu kwa hiyo tunaona hapa kuwa inamzungumzia Malaika wa Uwepo wake kwenye andiko hili. Watrinitariani kamwe hawapendi kutumia maandiko haya yanayothibisha na kueelezea ukweli ulio kinyume na vile wanavyosema vinginevyo wanaendelea kudai kuwa huu ndio usahihi na kudai kinyume chake kwa jinsi ambayo haisemi hivyo, kama Wafilipi 2:5-8 pale ambapo Kristo hakukusudia wala kupenda kutafuta awe sawa na Mungu, jambo ambalo ndilo ilikuwa dhambi ya Shetani.

 

Kwa Kiyunani inasema Megales Boules Aggelos. Neno la Kiyunani la aggelos aggelos kila mara limetafsiriwa kama ni Malaika kwenye Agano Jipya. Maana yake ni mjumbe lakini Watrinitariani peke yao hutafsiri hapa kama mjumbe pale tu inapomlenga Kristo. Wanapenda kuwa pande mbili zote.


Maandiko ya Kiebwania kwenye hii Isaya 9:6 yanasema ni El Mwenye Nguvu. Neno El linaweza kutumika kutaja Jeshi la malaika au mkubwa wao na pia linaweza kutumika kumtaja kiongozi wa wanadamu. Tafsiri ya LXX ilitumia neno aggelos katika kutafsiri huyu El Mwenye Nguvu (kwenye maneno ya SHD 3289 mshauri, SHD 410 El, na SHD 1368 Mwenye Nguvu).
Maneno haya hayanamaana ya kumtaja Mungu wa Pekee na wa Kweli, Eloa. Jina lake huhu ni Pele (6382). Kiyunani kilichaguliwa ili kuonyesha ukweli kwamba andiko hili lilikuwa linamtaja Mjumbe wa Mungu na anaelezwa kwa wazi kwenye Zaburi 45:6-7, na Waebrania 1:8-9 ambako anatajwa kuwa ni Kristo ambaye ni malaika mpole au elohim aliyewaongoza Israeli.

 

Swali la 15. Ni kwa nini Yesu aliitwa Mungu mwenye Nguvu (Isaya 9:6) na "Mungu" pia aitwe pia Mungu mwenye Nguvu kwenye Isaya 10:21?

 

Jibu 15.  Kuna watu wawili wanavyohusishwa. Wa kwanza hapo juu ni El na na Yule aliye kwenye Isaya 10:21 ameelezewa kwenye aya ya 23 kama Yahova wa Majeshi ambaye ndiye Mungu wa Pekee na wa Kweli, Eloa. Pia kuna mchanganyo wa jinsi ya kuita majina unaotokana na kutoelewa majina ya Kiebrania yaliyotumika. Tazama hapo juu.

 
Swali la 16. Aliwezaje Yesu kujifufua mwenyewe kutoka kwa wafu (Yohana 2:19-21)?

 

Jibu 16. Yohana 2:19-21 inalitaja Hekalu kuwa ni mwili wa ufufuo. Biblia inataja mahali pengine kwamba iikuwa ni Mungu ndiye aliyemfufua toka kwa wafu (soma Matendo 2:24,30; 26:8; 2Wakorintho 4;14; Waefeso 1:20, Waebrania 11:19).

 

Ni kweli alikuwa anasema kwamba mwili wake utafufuka baada ya siku 3.

SGD 1453

egeirw (egeírō)

+ Huenda elimu inayohusika na maneno ya asili ya kihistiria au Etimolojia wanahabari msingi wa 58 (ingawa wazo la kukusanya historia ya kimasomo ya mtu);

- Maana yake: kuamsha (kwa kupitisha au kwa kutopitisha), kama vile kumwinua (kimatendo kabisa kutoka usingizini, kutoka alipoketi au alipolala au kutoka kwenye magonjwa, kutoka mautini au kwa namna nyingine ya kimfano, kutoka mashakani, kutokana na mchoko, kutokana na maangamizi, kutoka kwenye hali isiyokuwepo)

+ KJV inatumia:--amsha, inua (juu), inua juu (tena, tena), amsha na inua juu, (amsha) (tena, juu), simama, inua juu.

Tazama matokeo kwenye Agano Jipya la Kiyunani hapa (See occurrences in the Greek New Testament)

 

Kristo alikufa. Mungu mkuu na muumba wa vyote Eloa ambaye ni Baba wa wote hawezi kufa. Ni dhahiri kabisa kuwa Baba alimfufua kutoka kwa wafu. Ni Baba ndiye aliyemtuma. Alisema kwamba naenda kwa Baba yangu...Namuomba Baba ALIYENITUMA nk. Kristo alikuwa muwazi sana kusema kwamba alitumwa NA Mungu.... na kwamba yeye hakuwa Mungu (Eloa).


Swali la 17. Aliwezaje basi Yesu kuumba vitu vyote (Wakolosai 1:16-17), wakati ni Mungu tu ndiye aliyeviumba vitu vyote kwa nafsi yake (Isaya 44:24)?

 
Jibu 17. Wakolosai 1:16-17 inasema kwamba Kristo aliumba viti vya enzi na usultani na mamlaka na tawala. Hakuumba Viumbe wanaoitwa wana wa Mungu wala Jeshi la Malaika walioko mbinguni.  

 

Mungu (ambaye pia ndiye Yahova Elohim) amenenwa kuwa ndiye muumbaji aliyeviumba vitu vyote (yaani El) (katika Mwanzo 1:1; 2:4;  Mwanzo 6:7 (akiwa ni Mungu Mkuu yaani Yahova apaswaye kuabudiwa na anauwezo wa kufanya maamuzi ya kuangamiza);

Kumbukumbu la Torati 32:6 (anatajwa kuwa ni Eloa na kwenye sura ya 32:15;17 yeye ni Mungu na Mwamba wa wokovu wetu);

Isaya 42:5 (El), 45:18 (Ha Elohim Muumbaji Yahova Mungu anatumia aina mbalimbali ya namna ya kumuita na anasema kwamba yeye hakuiumba dunia Tohu au iwe tupu kama ilivyokuwa kwenye Mwanzo 1:2);

Malaki 2:10 (Mungu mmoja aliyetuumba sisi sote); Marko 13:19 (Kristo anasema hapa kwamba Mungu ndiye aliyeviumba viumbe na uumbaji wote);

Wakolosai 3:10 Mtume Paulo anasema kwamba ilikuwa ni Mungu ndiye aliyeumba vitu vyote;

Waefeso 1:20 (Alionyesha uweza wake kupitia kwa Kristo na ndiye aliyemfufua kutoka kwa wafu);

Waefeso 3:9 (Mungu ndiye aliyeumba na ndiye alikuwa kinara wa Mipango iliyofichwa na Mungu aliyeviumba vitu vyote kwa Siri na fumbo na ndiye aliyevifanya vijulikane na watawala au wanaovitumia na kwa mamlaka ya mbinguni kwa njia ya kanisa sawasawa na mipangilio ya kila zama ambayo aliyafanya katika Kristo (kama ilivyoandikwa kwenye Marshalls Interlinear): huyu Kristo alikuwa ndiye kifaa kilichowezesha kupangilia katika zama zote, lakini kazi ya uumbaji ilikuwa ni ya Mungu wa Pekee na wa Kweli; pia soma Ufunuo 10:6).

 

Tofauti kati ya wawili hawa imeandikwa kwenye Tito 1:2,4.

 

Swali la 18. Anawezaje basi Yesu kuichunguza na kujua mioyo au mawazo ya watu (Ufunuo 2:23)?

 

Jibu 18. Kristo amepewa mamlaka ya kuyahukumu mataifa siku ya Ufufuo ule wa hukumu. Alipewa Roho Mtakatifu naye ndiye anayefanya kazi hii ya kuchunguza na kujua kila kitu. Uwezo wa kupambanua aina za Roho ni mojawapo ya karama na hukumu inatolewa kwa wateule wote kupitia kwa Roho Mtakatifu nasi tutauhukumu ulimwengu na malaika (1Wakorintho 6:2-3).


Swali la 19. Ni kwa nini Yesu aliabudiwa (Mathayo 2:2,11; 14:33; 28:9; Yohana 9:35-38; Waebrania 1:6) wakati anasema anayepaswa kuabudiwa ni Mungu peke yake (Mathayo 4:10)?

 

Jibu 19. Ni neno lilelile la Kiyunani ndilo lililotumika kuelezea kuabudu kila mahali. Neno lenyewe lililotumika proskuneo ambalo halimaanishi sawa na kitendo cha kuabudu kama Mungu.  

 

(Mathayo 2:2,11; Tafsiri ya The Kingdom Interlinear Translation ya Maandiko ya Kiyunani....tumekuja kumpa heshima yake anayostahili.
Diaglott....heshima anayostahili kupewa mtu
KJV...Kuabudu
Mathayo 2:11...Utiifu wa Kiheshima
Mathayo 14:33 Utiifu
Mathayo 28:9 Utiifu
Yohana 9:35-38 Utiifu
Waebrania 1:6 (4416 proskuneo) malaika wote wa Mungu na waonyeshe utii wao kwake.

 

Nukuu kutoka Kumbukumbu la Torati 32:43 ambayo kwenye fasiri ya Septuagint inasomeka "Na mfurahi enyi mbingu, pamoja naye, na malaika wote wa Mungu wamuabudu yeye.....wamtukuze, wampe heshima, wapige magoti mbele zake na wambusu mikono wakiielekeza kwake.”

 

KJV inatafsiri kuabudu.
Tazama Biblia iitwayo Companion Bible Appendix 137
proskuneo = kumuashiria mtu mwenyewe (kwa kuonyesha upande wa nyuma), kuonyesha heshima.

 

Katika Ufunuo 3:9 sinagogi la Shetani linakwenda kufanywa kuwa proskuneo kwa wateule na kwa tafsiri hii watafanywa watuabudu sisi jambo ambalo ni upuuzi. Maana halisi ni kwamba watatupa heshima tunayoistahili tukiwa kama makuhani na wafalme. 

 

Swali la 20. Kwenye Agano la Kale Mungu alionekana (Kutoka 6:2-3; 24:9-11; Hesabu 12:6-9; Matendo 7:2), wakati maandiko mengine yanasema kwamba hakuna mtu atakayewahi kumuona Mungu (Kutoka 33:20; Yohana 1:18). Kama alikuwa sio Baba Mungu Yule aliyeonekana kwenye Agano la Kale  (Yohana 6:46), basi walikuwa ni kina nani hawa walioonekana? Soma Yohana 8:58.

 

Jibu 20. Waliyekuwa wanamuona alikuw ni Malaika wa YHVH kama ilivyoandikwa kwenye jarida la Malaika wa YHVH (Na. 24) [The Angel of YHVH (No. 24)]. Ni kama tulivyojionea kwamba hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu kamwe. Maandiko yote yamefafanua kwa kina kwenye jarida hili.

 

Swali la 21. Sasa basi ni kwa nini Yesu alidai kuwa na jina la kimbinguni, "MIMI NIKO", akajiita hivyo mwenyewe kwenye Yohana 8:58? Soma Kutoka 3:14.


Kristo alisema kwa niaba ya Mungu kwenye Kutoka 3:14. Jina hili sio MIMI NIKO. Maneno haya kwenye Kiebrania yanaitwa ‘eyeh ‘asher ‘eyeh ambayo maana yake ni mimi (nafanyika) jinsi nitakavyo kuwa na linaelezea mfumo wa majina ya Mungu na Jeshi la malaika. Mungu ni Yahovi (SHD 3069) kama Ha Elohim na wale wanaonena kwa niaba yake wanaitwa Yahova (SHD 3068) ambaye ni nafsi ya tatu ya uandishi wa vebu yenye maana ya Anayesababisha kutokea. Kwa hiyo, Mungu Mmoja wa Pekee na wa Kweli atafanyika kuwa ni kitu ambacho anasababisha kitokee. Kiebrania kinasomeka na Wayahudi kama Elohim kwa Yahovi (SHD 3069) na Adonai kwa Yahova (SHD 3068) kwa hiyo tusimchanganye huyu Mungu wa Pekee na wa Kweli na wajumbe wengine ambao ni Malaika na yeye. Wakati Yahovi anapotajwa kama Yahova ni mara zote anaitwa Yahova wa Majeshi, jambo ili kummwonyesha au kumtambulisha yeye kuwa ni Mungu Mkuu na Wapekee, Eloa au Elyon; Mungu Aliye Juu Sana. 

 

Swali la 22. Bi kwa nini basi kwamba wote wawili, yaani Baba na Mwana wanatoa uzima (Yohana 5:21)?


Jibu 22. Ni kwa kuwa Mungu Baba, Eloa alitoa mamlaka yake kwa mwanaekama ilivyoelezewa kwenye Yohana 17:1-3 (soma jarida la
Uzima wa Milele (Na. 133) [Eternal Life (No. 133)].

 

Swali la 23. Ni kwa nini Yesu alijishuhudia mwenyewe (Yohana 8:18; 14:6)?

 

Jibu 23.  Mimi ndiye ninayejishuhudia mwenyewe, na Baba aliyenituma ananishuhudia.

 

Kamusi ya Strong's G3140 – martyreō: kuwa shahidi, kushuhudia, kama kuthibitisha kile ulichokiona au kusikia au ulichojionea kiuzoefu, au kwamba analijua kwa kuwa alifundishwa kwa kupitia ufunuo wa kimungu au uvuvio

a) kutoa (sio kurudi nyuma au kuacha) ushuhudia

b) kutamka au kutoa ushuhuda wenye staha, kutoa habari au taarifa njema

c) omba, sihi sana

 

tafsiri ya Biblia ya Authorized Version (KJV) Hesabu — Jumla: 79 AV — toa ushahidi 25, shuhudia 19, toa tathmini 13, ushuhuda 5, kuwa shahidi 2, shuhudia 2, kuwa na habari njema 2, shahidia 11.

 

Kwenye kila waraka halali au agano, shahidi anatia saini yakuwa”shahidi”. Wanashuhudia. Mtu yeyote pia anaweza kujihoji mwenyewe. Na hii haimfanyi mtu yeyote kuwa Mungu, Eloa wa Pekee. Haimfanyi yeye kuwa aishi kutoka umilele wake. Ni yeye anayejaribiwa katika kweli.

 

Yohana 14:6   Yesu akamwambia, Mimi ndiye njia ya kweli nay a uzima, na hakuna mtu atakayemuona Baba ila kwa njia ya mimi.

 

Anasema kwa wazi sana utofauti na kwamba yuko chini kuliko Baba kwa jinsi hii, na kwamba yeye amepangiwa kazi fulani sawa na kama tufanyavyo kwenye maisha yetu ya kila siku na hakuna anayeweza kuja kwa CEO isipokuwa ni kwa njia ya mwombezi aliyechaguliwa au afisa. Iwapo kama afisa Yule atadai kuwa yeye ni CEO au ana cheo sawa naye, basi atafukuzwa. Na hii ndio dhambi aliyoitenda Shetani ya kutamani kuwa sawa na Mungu jambo ambalo Kristo hakupenda wala kutamani kuwa hivyo wala kufanya (Wafilipi 2:5-8)

 

Swali la 24. Kwa nini Watrinitariani na Wabinitariani/ Waditheist wanaghushi au wanatumia maandiko mengi yaliyopindishwa maana yake kwenye Biblia?

 

Jibu 24. Kwa kuongezea yaliyoelezwa hapo juu na mifano yake ni kama ifuatavyo:

1Yohana 5:7 kwenye KJV (Receptus): hakuna mahali panapoupa mashiko Utatu kwenye Biblia yote na ndipo walipoighushi 1Yohana 5:7 ya tafsiri ya KJV na Receptus.

 

Kwenye 1Timotheo 3:16 tafsiri ya KJV inatumia maandiko yanayojulikana kuwa yameghushiwa ambayo yameghushiwa kutoka kwenye tafsiri ya Codex Sanaiticus na ughushaji huu uko kwenye michepuo miwili tofauti kwenye maandiko ili kufanikisha kuliweka neno ambaye linalotuama kwenye uingizaji wa herufi “O” kwenye neno Theta sigma likiwa kama ni kifupi cha neno Theos au Mungu jambo ambalo kwa kweli sivyo.

 

Bullinger anaonyesha maandiko yaliyoghushiwa kwenye maandiko haya ya ufafanuzi ya chini kwenye Biblia iitwayo th Companion Bible ambayo utaweza kujionea mara nyingi fafanuzi zake kama vile Maandiko Yaliyorukwa unaoonysha wazi kuwa ni kazi ya kughushi ya Watrinitaria.

 

Watrinitariani na Wabinitariani hawana msingi wala mashiko kwa teolojia yao ya kwenye Biblia na kwa hiyo wanatumia kughushi chochote wanachokiona kinaweza kuwasaidia, na Waprotestanti ndio wamekuwa wapenda uwongo wakubwa na wanaouunga mkono.

 

Hapa tunarudi kwenye malumbano ambayo yameonekana kwenye Maswali ya kuwauliza Watrinitariani kwamba wao na wenzao Wabinitariani hawawezi kwa kweli kuyajibu kwa kutumia mafundisho yao yenye utata. Kristo alimshuhudia Mungu na alisema kwamba alikuwa anajishuhudia mwenyewe. Kila mmoja wetu anajishuhudia mwenyewe kama wana wa Mungu kwa Roho Mtakatifu na tumetumwa na Roho Mtakatifu ili tukawashuhudie hawa wawili, yaani Mungu na Kristo na kanisa. Matendo yetu huishuhudia imani na kwa Mungu kwa kupitia Roho Mtakatifu.  

 

Yohana 15:23 inasema kwamba: Yeye anichukiaye mimi amchukia Baba pia. Hata hivyo hasemi hivyo kwa kuwa wao ni kiumbe mmoja kama tunavyoona kwenye Yohana 5:20: “Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu.”.

 

Tukiliona hili twaweza kujiuliza kuwa inawezekanaje basi kiumbe mwenye uwezo wa kujua kila jambo aonyeshwe kitu na kiumbe mwenzake mwenye uwezo huohuo wa kuelewa kila jambo? Basi lilikuwaje basi apewe kama ilivyo hapo juu (na Ufunuo 1:1), basi Kristo anaweza kuwa ni mtu mwenye uwezo huu wa kujua kila jambo?

 

Mungu ni roho. Yohana 4:24 inasema: Mungu ni roho; nao wamwabuduo halisi imewapasa wamwabudu katika roho na kweli. Jaribio la kulifanya andiko hili lisomeke Mungu ni roho halijasaidiwa na tafsiri yoyote ile ya maandiko na maana yake kwa jinsi ilivyotumiwa na yeyote miongoni mwa wanateolojia waliotwa ante-Nicene au tafsiri yao. Madai haya ni kutunga au kuingiza fundisho la kwamba hakuwa pekeyake na asili isiyobayana ya Mungu. Na kuwafundisha watu kuwa Mungu ni endelevu na yuo kwenye mfumo mpana na enevu. Na hii inaenda mbali zaidi ya Utrinitariani hadi kwenye Mchakato wa Teolojia.

 

Mungu anayo familia kama inavyosema Waefeso 3:14-16: “Kwa hiyo nampigia Baba magoti, 15 ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, ...”

 

Watrinitariani/Wabinitariani wanajaribu kumfanya Kristo na Mungu kuwa ni Mtu mmoja, au manadai ya kuwa Kristo ni Mungu kwa kuchukua mtazamo wa maandiko yaliyoghushiwa nay a uwongo tuliyoyaona hapo juu na tafsiri yenye makosa ya Yohana 1:1, ambayo kiusahihi zaidi ingesema: Hapo mwanzo kulikuwako Neno, nalo Neno lilikuwako kwa Mungu, (Theon) naye (Mungu wetu au theon) alikuwa neno.

 

Lakini nukuu na imani imewekwa kwenye andiko la Yohana 2:19 kama kigezo cha kwamba Kristo alikuwa ni Mungu kwa kuwa anasema:

Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.”

Makanusho ya madai haya yanapatikana kwenye Injili hii hii kwenye Yohana 10:18, ambapo Kristo anasema kwamba:

Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.”

 

Hakuna shaka kwamba Kristo ni mdogo kwa Mungu, mtiifu na ni mtumishi mnyenyekevu wa Mungu wa Pekee na wa Kweli. Yeye ni kaka yetu na mrithi pamoja nasi katika Ufalme wa Mungu. Lakini hata hivyo hatupaswi kumuabudu yeye au alama zake za kiroho. Kwa amri yake tunamwabudu Mungu na kuzitenda amri za Mungu. Kitendo cha kumuita Kristo Bwana kwa chenyewe tu hakiwezi kukuingiza kwenye ufalme wa mbinguni.  

 

q