Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[076B]
(Toleo La 2.0 20090909-20110724)
Jarida hili litafanya marejeo katika
kuyapitia machapisho ya Kanisa lililojulikana kama Worldwide Church of God
(WCG) na litamulikia makosa yaliyokuwepo kwenye kanisa hili kuhusu imani ya
Uditheism, ambayo ni aina ya imani ya kuadubu miungu mingi ya kipagani na
ambayo hata sasa inaendelea kufundishwa na watumishi walio kwenye makanisa
chipukizi ya kanisa hili la WCG hata leo. Matumishi na wahubiri hawa
wameshindwa kuyashinda makosa haya kutoka kwenye uelewa wao kuhusu asili ya
Mungu na ya Kristo, na uhusiano walionao mmoja kwa mwigine. Uelewa potovu
uliopo kwenye makutaniko ya watumishi hawa unatokana na fundisho hili la
uwongo. Baadhi ya makanisa yaliyotoka kwenye Kanisa hili yanajaribu kuyarudisha
upya mafundisho haya mapotofu kwa kudai kwamba Kanisa hili la WCG ililikuwa la
mrengo wa mafundisho haya ya Kibinitarian, kama inavyodaiwa kuwa kanisa la
kwanza liliamini hivyo. Madai haya ni ya uwongo na yakulisingizia tu kwa namna
zote mbili. Wandishi wa jarida hili wamekuwa wakifuatilia zamba za mbalimbali
zililopitia kanisa kwa kipindi cha takriban miaka 130 iliyokuweko nyuma na
kabla ya kuanzishwa kwa kanisa la WCG, machipukizi yake na Makanisa mengine ya
Mungu.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Copyright © 2009, 2011 Wade Cox, Arthur Hartman, Tom Schardt, Jeremy Hatchett,
Donovan Schricker)
(Tr. 2013)
Masomo haya yanaweza kunukuliwa na
kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au
kufuta maneno. Jina la
mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni lazima iwekwe
pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa nakala yoyote
atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja
ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Uditheism
Utangulizi
Imani na mfumo wa
kanisa lililojulikana kwa jina la The Worldwide Church of God (WCG)
uliendelezwa kwenye zama za karne ya 20 kwa kutumia mahubiri na maongozi ya
Herbert Armstrong. Yeye pamoja na wahudumu wenzake waliosaidiana-naye
waliendeleza mafundisho yanayosema kwamba asili ya Mungu ni ya Kiditheist na
wakaliekeza Kanisa la Mungu kwenye mafundisho haya ya uwongo, na wale
waliobakia kuwa ni masalia ya Kanisa hili la WCG siku hizi hawaendelezi tena
kabisa kile ambacho ndicho asili ya imani hii ya Kiditheism na kujua jinsi
imani hii ilivyoathiri uelewa au fikra zao juu ya Mungu, na ukweli ulioko
kwenye Maandiko Matakatifu. Walianzisha maundisho mengi ya uwongo yanayosema
kuwa viumbe wawili wenye hadhi na uweza sawa, au wakio katika mwonekano wa kila
mmoja peke yake. Yaani viumbe kamili kila mmoja wao, walio kwenye familia ya
Mungu walijadiliana siku nyingi zilizopita za kihistoria na wawakubaliana
kwamba mmoja wao akubali kuwa na cheo cha uwana au mtoto wa huyu mwingine na
ili kwamba atolewe sadaka ya ondoleo ya dhambi za wanadamu, na kwamba Mungu
hajafanyika kuwa “Baba” hadi pale Kristo, Mwanawake, alipozaliwa na mwanamke
fundisho hili ni la uwongo wa dhahiri kabisa, na linaleta mkanganyiko wa
Maandiko Matakatifu.
Teolojia
unyofundisha Asili ya Mungu kwenye Biblia na kwenye Makanisa ya Mungu
vimeendelea kuwa ni msisitizo juu ya Mungu mmoja au Uunitariani kwa kipindi cha
Milenia Mbili zote hadi sasa.
Uwepo wa Kristo huko nyuma kabla ya kuzaliwa kwake umekuwa ni jambo linaloaminiwa kwenye makanisa na jamii zote za makanisa. Wa Unitariani wenye Itikadi Kali wameanza kujitokeza ama kuchipuka, kama kina Anthony Buzzard kutoka kwenye Makao Makuu ya Kanisa la Mungu yaliyoko huko Marekani (soma jarida la Uwepo Kabla wa Yesu Kristo (Na. 243) [The Pre-existence of Jesus Christ (No. 243)].
Inaeleweka kwamba Kristo alipewa mwili wake wa kiroho kwa kutii wake Mungu na akaonekana kwenye mwili wa kibinadamu kwa kutungishwa mimba tumboni mwa Mariamu sawa na ilivyotabiriwa ili kizaliwe kiumbe kitakachoweza kutuokoa. Hili lilionekana kuwa ni fundisho kuu la msingi kwenye kitabu cha Wafilipi 2:6-11 inaposema kwamba ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Kwa kupitia tendo hili, basi alifanyika kuwa Monogenes Theos, au aliyezaliwa na mamlaka ya Kimungu, na uweza wote wa kuwaokoa wanadamu wote.
Waamini Utatu au Watrinitariani wamekuwa kilamara wakitafuta jinsi ya kuandika tena andiko hili ili kulifanya lionekane na kusomeka kuwa alikuwa yu sawa kabisa na Mungu na kwa ajili hii lilitafsiriwa kimakosa lakini kwa makusudi kwenye nakala ya Tafsiri ya Mfalme Yakobo (KJV) kuwa: alidhani sio unyang’anyi kuwa sawa na Mungu. Makosa haya yalitanguliwa na mpenyezo wa imani na ibada za kumuabudu mungumke Easter au Ishtar, na kuingizwa kwa mafundisho ya mungu Attis na ibada za kuliabudu mungu zilivyoingizwa kwenye Ukristo tangu mwaka 154 BK huko Roma (soma jarida la Upotoshaji wa Kimafundisho wa Wabinitariani na Watrinitariani Kutokana na Teolojia ya Kwanza Kuhusu Uumgu (Na. 127B) [Binitarian and Trinitarian Misrepresentation of the Early Theology of the Godhead (No. 127b)].
Imani hii ya Kibinitariani haikukubalika kamwe kuwa ni fundisho kwenye Makanisa ya Mungu hadi kipindi cha kuingizwa mafundisho ya uwongo na ya uzushi kwenye Makanisa ya Mungu kwenye kipindi cha zama za mwisho za karne ya ishirini. Inaonekana kwamba ni kwa kutokana na hali ya kutoelewa kabisa kulikumba vuguvugu la Waprotestanti wa Marekani na kutokana na watu ambao hawakuyatubia kabisa mafundhisho haya ya uwongo na kisha wakaingia kwenyye Makanisa ya Mungu wakiwa wanatokea kwenye imani hizi za Kitrinitariani, ndio walioyaendeleza mafundisho haya.
Katika kipindi cha karne ya kumi na tisa, imani ya Kiunitariani kuhusu Mungu ndiyo iliyokuwa inajulikana kwa urahisi na wazi kabisa na ndiyo ilikuwa ikifundishwa na kuaminika ilimwenguni kote miongoni mwa waumini wa Makanisa ya Mungu ya Watunza Sabato wa Kibaptist na Vuguvugu la Waadventists. Waadventista walikuwa nawajulikana kama Waariani kutokana na mtazamo wa kimakosa ambao watu walikuwa wanaelewa vibaya kuhusu mafundisho yake kwa jinsi yalivyopotoshwa na Watrinitariani. Waadventista walienda mbali zaidi kiasi hata cha kuamini kuwa Kristo ndiye yule Malaika Mkuu, Mikaeli, na kwamba alikuwa ni huyu Malaika Mikaeli ndiye alikuwa Mfalme Mkuu aliyesimama upande wa taifa la Israeli (Danieli 10:13,21; 12:1). Kikundi kidogo sana cha masalia ya waumini wa Kanisa hili la WCG nchini Uingereza wanaendelea kufundisha na kuamini hivi pia, bali wanajaribu kuweka madai ya kuchanganya Malaika Mikaeli na Uditheist na kumtenganisha kutoka kwa wana wengine wa Mungu kwenye kundi la Malaika
Waadventista waliingiliwa na Majesuit na baada ya kifo cha Uria Smith mwaka 1931, ndipo walianza kuchukua hatamu za kuongoza vuguvugu hili la Waadventista, na hadi kufikia mwaka 1978 wakafanikiwa kulibadilisha rasmi vuguvugu hili la SDA na kuwa kwenye mishemishe za mafundisho ya uwongo (mishemishe ai mishmash) ni neno mishmash linatokana na neno la Kiebrania michmash) ya mafundisho ya potofu na nabii za uwongo, ambazo zinajumuishwa pia na mafundisho mapotofu ya nabii wao mke, Ellen G. White.
Nabii za uwongo za mashahidi wa Yehova na za wa SDA na za Herbert Armstrong vimefafanuliwa kwenye jarida la Unabii za Uwongo (Na269) [False Prophecy (No. 269)].
Kanila la Worldwide Church of God lilikuwa na udhaifu mkubwa na usio sahihi katika kuelewa Asili ya Mungu na liliendelea kufundisha mafundisho haya yasiyo sahihi na kwa mara nyingi. Mafundisho yake yalilenga kubomoa ukweli ulio kwenye uelewa wa wazi maelezo na mafundisho ya Waamini Mungu Mmoja au Waunitariani, kazi waliyoifanya kwa kupitia mafundisho yao ya Elimu kwa Njia ya Posta ya mafundisho ya Biblia ambayo yaliwapofusha watu kwenye imani ya miungu mingi ya Kiditheism na nyinginezo.
Baada ya kuvunjika na kuparaganika kwa Kanisa hili la WCG ndipo ilipoanza kufundishwa na wanateolojia waliojichagua wenyewe kuwa imani iliyokuwa inafundishwa na WCG ilikuwa ni ya Kibinitariani na hili ndiyo ilikuwa fundisho asilia lililoonekana kufanana na Biblia. Madai hay ni ya uwongo na yaliendelezwa na kukuzwa kiasi cha kufikia kuwa ni agenda ya watu wanaoonekana wanajaribu kuwarudisha pamoja waumini wa Makanisa ya Mungu na kuwapeleka kwenye mafundisho ya Utrinitariani, mahali ambapo waliitwa watoke walipokuja kwenye kanisa la WCG. Mafundisho haya haya ya uwongo ndiyo yaliingizwa kwenye kanisa linguine liitwalo Church of God (Seventh Day) kwenye Makao yao Makuu huko Denver mwaka 1995. Jimbo la Caldwell na kanisa lake walikuwa ni Waunitariani na ikatokea kwamba Mungu akawaruhusu kuituza kalenda ya kweli inayotokana na mwonekano wa mwezi mwandamo. Inaonekana kwa kufuatilia ukweli wa kihistoria kwamba hakuna Kanisa lolote la Mungu na lenye mafundisho mapotofu kuhusu asili ya Mungu linaloweza kuishika kiusahihi kalenda hii ya Hekaluni. Inaonekana kwamba ni wale tu wanaofuata mfumo wa Kibiblia wa Kiunitariani ndio pekee wameruhusiwa kuishika kalenda hii ya Hekaluni. Baraza Kuu la Makao Makuu ya Kanisa kwa kweli lipo kwenye mrengo wa Uunitariani wenye Itikadi Kali na huku wakikataa uwepo wa mwanzo wa Kristo na halikuweka msingi wake kwenye mafundisho makuu ya kiteolojia.
Haya hivyo, wao ni masalia ya Makanisa ya Mungu na ambayo yamejichanganya kwa kukosa kwao matumaini na baadhi yao wamejiingiza kabisa kwenye mishemishe za kimafundisho yanayowapigavita Waunitariani na kuupa mashiko Uditheism na pia kutoka kwenye Ubinitarianism na kwenda kwenye Utrinitariani. Kuna baadhi ya Waunitariani wachache sana wanaoukubali uwepo wa Kristo huko nyuma, lakini watu kama hawa ni wachache sana.
Nia ya jarida hili ni kuonyesha kuwa Armstrong alikuwa na makosa na kwamba imani na mfumo mzima wa WCG ulikuwa ni wa Kiditheist, na kwamba vikundi vyote vilivyotokana na kanisa lake kama vile LCG kwa kweli ni wa imani hii ya Kiditheist na hata wengine wao wanaojiita UCG ni watu walipoteza matumaini na wamechanganyikiwa wasielewe la kufanya kuhusu jambo hili na wanataabika sana na msimamo wa Kanisa la Mungu la Siku za Mwisho.
Na ni kwa sababu hii ndivyo kwamba Mungu ilimbidi awashughulikie na kuwatawanya. Kwa sasa anafanya kazi ya kuyaweka pamoja Makanisa ya Mungu yawe kwenye mafundisho ya kweli nay a uzima yakiwa kwenye muunganiko wa CCG nah ii itaendelea kukua.
Hebu sasa na tuuone Uditheism wa WCG na uingiaji wa mafundishho haya ya uwongo na uzushi na yanavyooelezewa kuwa yapo kinyume kabisa na Maandiko Matakatifu.
Kumbuka kuwa Mungu amempa mwana awe na uzima ndani yake. Hii inamaana kuwa Kristo hakuwa nao uzima huu kutokana na uwezo wake mwenyewe (Yohana 5:25-29; pia tazama Wakolosai 1:15-16).
Uditheism
Makosa
ya kwanza nay a msingi ya Herbert Armstrong
Kwa mujibu wa kitabu cha Herbert W. Armstrong cha “Umuhimu wa Utu wa Mwanadamu [The Incredible Human Potential” (TIHP)], kwenye ukurasa wake wa 68 anasema chini ya kifungu kinachosema “Ni kwa Jinsi Basi Mungu Alivyopanga Kujiongeza Mwenyewe?” anasema kwamba “Tangu milele yote Baba na Neno ambaye hatimaye alikuja kuwa Yesu Kristo walikuwa na uwepo sawa wa kuishi.”……….
Tunaona hapa kuwa kosa la msingi na la kwanza kuhusu uwezo sawa wa kuwepo na usawa linaanza kuonekana.
Kwenye kifungu cha pili cha uandishi wake anasema: “Ilianzaje hadi ikawa hivi, ni kwa zaidi ya watu wawili tu – Mungu na Neno – wakiwa kwenye familia ya Mungu? Mungu hamtaji kuwepo mwingine yeyote. Walikuwa peke yao, yaani “Neno” ambaye ni Mwana wa Mungu na Mungu Baba yake kwa wakati ule? Hakuna mahali popote panaposema hivi.”
(Soma Mithali 30:4-5 ambapo kwa kweli anaelezea tofauti ambapo jina la Mungu linatolewa).
Kwa hiyo tunajionea makosa ya kiuandishi ya Armstrong, ambayo yanamwingiliano na teolojia yake ya uwongo na ambayo haya ni madai yake ya uwongo kusema kwamba kulikuwa hakuna wana wengine wa Mungu katika kundi la Malaika hadi pale Kristo alipotungwa mimba yake na kuwa na mwili wa kibinadamu kwenye tumbo la Mariamu.
Somo la 13 lwenye mfululizo wa Masomo yake ya Kujifunza Biblia kwa Njia ya Posta kutoka kwenye chuo chake cha Ambassador College Bible Correspondence Course, ukurasa wa 6, kunapanaposema kuwa Ayubu 38:4-7, “Kwenye aya ya 7 neno la kibiblia kuhusu “nyota ya alfajiri au ya asubuhi” na “wana wa Mungu” inamaaisha “malaika.”
Inaendelea kuelezea ufafanuzi kuhusu Ayubu 1:6, anasema: “Malaika wanatajwa hapa kama ‘wana wa Mungu’ ni kwa mtazamo tu wa kwamba Mungu ndiye Muumbaji. Hakuna uhusiano mwingine zaidi wa baba na mwana kama alionao Yesu na Mungu Baba yetu. Malaika sio wana wa pekee na hawajajazaliwa na Mungu, kama alivyokuwa Yesu Kristo (Waebrania 1:5) – bali wao waliumbwa.”
“Malaika ni viumbe walioumbwa mmoja mmoja. Hawawezi kamwe kufanyika kuwa wana pekee wa Mungu Baba kwa kupitia kwa Roho wake Mtakatifu au wazaliwe kutoka kwenye Familia yake kama wanavyoweza kuzaliwa wanadamu ……..Bali malaika watabakia milele kuwa ‘wana wa Mungu’ kwa maana ya kwamba Mungu alimuaumba kila malaika mmoja mmoja, na akiwa ni kiumbe wa kiroho na asiyekufa.”
Kwenye kitabu hiki kiitwacho “Siri za Nyakati (Mystery of The Ages)” au (MOTA) ukurasa wa 43, Armstrong, anaielezea familia ya Mungu akisema “Familia ile inaundwa sasa kwa Mungu Baba, na Yesu Kristo Mwanawake, na wanadamu wengi wakipekee tayari sasa ni wana pekee wa Mungu (Warumi 8:14, 16; 1 Yohana 3:2), wanaofanyika kuwa ni Kanisa la Mungu.”
Kwa hiyo, malaika kwa mujibu wa mafundisho ya Armstrong ni viumbe wanaotokana na daraja dogo la uumbaji, na hawako kwenye viumbe na wana wa Mungu wa kiroho walioumbwa na wasiokufa ambao wateendelea kubakia nje ya muundo wa familia ya Mungu, na ambao hawawezi kuwa na uhusiano wa baba na mwanawe na Mungu Baba. Maelezo rejea yake yanaweza kuonekana kutoka kwenye muundo wa Mji wa Mungu (soma jarida la Mji wa Mungu (Na. 180) [The City of God (No. 180)].
Mafundisho haya yanaonyesha ukosefu mkubwa
wa uelewa wa Maandiko Matakatifu. Kwenye Ayubu 1:6, 2:1 na 38:4-7 tunaambiwa
kuna wana wengi wa Mungu waliokuwepo kabla ya uumbaji na Shetani akiwa ni mmoja
wapo. Ayubu anamwelezea mwokozi kuwa ni mmoja wa Jeshi kuwa la maelfu ya
Malaika (watawala) (Ayubu 33:23). Kazi hii inaonyesha kwamba kulikuwa na wana
wengi wa Mungu na Nyota wengi wa Alfajiri kipindi cha nyuma cha kabla ya
kuwekwa kwa misingi ya dunia. Zaburi inatuonyesha kwamba kulikuwepo na wana wa
Mungu na ambao walikuwa ndio Jeshi hili kubwa la Malaika na Kundi hili liliitwa
elohim na Kristo anawakiri watakatifu
wake mbele ya baraza hili la hawa elohim (kwa mujibu wa Zaburi 82:1). Zaburi
inasema wengine wameanguka na watakufa kama mwanadamu mwingine yeyote (Zaburi
82:6). Andiko hili linawahusu Jeshi zima lote la aiina mbili zote, yaani kwa
wale wa kiroho na wa kimwili. Mithali 30:4 inauliza swali muhimu kuhusu kazi za
Mungu na kwenye sura ya 30:5 linapatikana jibu kuhusu jina la Mungu wa Pekee na
wa Kweli na jina la Mwana wake. Neno linalopatikana kwenye mstari wa kwanza linasema: kila neno la ELOAH ni kamilifu.
Kutokana na Ezra sura ya 4 hadi ya 7 tunajua kwamba Eloah ni Mungu wa Hekalu na
ni kwa Torati yake na Hekalu lake na ndipo tunajua kuwa anaye mwana. Jina la
Eloah ni la umoja linajulikana kuwa halina namna ya kuliita kwa uwingi kwa
namna yoyote ile. Linatokana neno la lugha ya Kiaramu cha Kimagharibi na
Kikaldayo la Elahh lenye maana sawa na neno la Kiebrania la Eloah na linatumika
pia kwenye kitabu cha nabii Danieli kwenye Agano la Kale. Neno hili liliunda
msingi wa Kiaramu cha Kimashariki
ambacho kimesababisha kuwepo kwa neno la Kiarabu la ‘Allah’. Najina ya elahhin
na elohim yalikuwa na maana moja na yalijulikana siku za kale yakitaja wana wa
Mungu. Danieli anaashiria kuelewa vizuri kwa mujibu wa uandishi wake.
Sio kwamba imani
ya Armstrong ilikuwa haijui maana ya majina haya. Hapana. Kwenye somo lake la 8
la Mafundisho yake marefu ya kozi ya Biblia kwa Njia ya Posta, jina hili la
Eloah limetajwa na kukubali kuwa linatokana na asili ya umoja wa jina la Mungu
ambalo linakuwa elohim. Hata hivyo, kwenye sura hiyohiyo wanajikuta kuangukia
kwenye makosa au madanganyo ya kuamini Uditheist.
Mfano mwingine wa
kuwaonyesha kuwa wanajua na kuwa ni kwa makusudi tu hawakuamua kufuata ukweli
ni maandishi ya makala aliyoiandika Herman Hoeh kwenye kigazeti kiitwacho
Ukweli Uliodhahiri (the Plain Truth) aliposema:
Sehemu ya Agano la Kale Haikuandikwa kwa Kiebrania!
Kunabaadhi wanaopinga kuwa tusiyatafsiri majina ya
Kiebrania yaliyoandikwa kumtaja Mungu. Lakini ikumbukwe ushuhuda wa Biblia!
Kwenye Agano la Kale jina la Kiingereza “Mungu” mara zote linamaana ya maneno
ya Kiebrania ya El, Eloah, na Elohim. Ukumbukwe kwamba maneno haya yana maana zaidi ya
tunavyotaja majina ya Mungu kama vile YHWH (Zaburi 69:30; Isaya 9:6 – pia tazama kiboksi
kinacholielezea zaidi, Mungu ana Majina Meingi sana”).……..inatarajiwa kutoka
kwa “Mungu Asiyejulikana”, Nov/Dec 1972 PT na H. Hoeh.
Makala hii
inawajua pia Elahh na Allah’ wanaotokana na muundo huu wa kiuandishi. Dalili
kuu ya uelewa huu kwa mjadala uliopo kati ya Wakristo na Waislamu uligunduliwa
na kupotezewa. Teolojia yao ya miungu miwili ikaonekana kuwa haina maana kabisa
katika kuwasiliana na kushirikishana imani na Waislamu wa namna yoyote ile.
Armstrong na
watumishi wake walionekana kutokuwa na habari kabisa na kile ambacho maandiko
ya Biblia yanachokionyesha na kuwa yanawasuta wao kwa uwongo, na kwamba hakuna
kabisa mlingano wowote wa maandiko haya kutoka kwenye maandiko yao. Wanaonekana
kuwa wamelitunga tu fundisho hili. Na halionyeshi kuwa lilikuwepo kwenye
Makanisa mengine yoyote ya Mungu yaliyokuwa hapo nyuma kabla yake huyu
Armstrong.
Kwa kuendelea,
Armstrong anasema: “Ili kuwa na Mwana wa Mungu kwa wakati ule wa kabla ya
historia, Mungu angelazimika kufanya mpango wa mapema wa kuwezesha kuzaliwa kwa
huyu Mwana wake. Na huyu Mwana, kwa jinsi hii angeweza kuwekuwepo kipindi hiki
cha kuzalliwa kwake. Bali huyu Neno (Logos), ni Neno alikuwa kama Mungu,
anayeishi milele.”
Hii inaonyesha
kiini hasa ambacho kwacho alijikuta akiyakumbatia mafundisho ya uwongo na
kuwadanganya wengi kwenye Makanisa ya Mungu ambayo yaliyaamini na kuyapokea
mafundisho yake haya yasiyo na mashiko yoyote.
Ili kufanyika kuwa
Mwana wa Mungu kipindi cha huko nyuma kabla ya kuzaliwa kwake, kungemaanisha
kuwa basi yeye asingeweza kuwa ni wa kuishi milele na ingemlazimu awe na uzima
mara tu baada ya kuwepo kwake Mungu. Biblia inaonyesha hili kuwa ni suala lenye
kuzua mjadala kwenye maeneo mengi na maandiko pia. Armstrong alikuwa anajaribu
kurejea kwenye imani ya waamini Utatu au Watrinitari wa Kimarekani na
anaonekana kuwa hakujua kabisa kile alichokuwa anakifanya au alichukuwa anasema
kuhusu jambo hili.
Makosa ya
teolojia hii yalifikia kiwango cha kukufuru. Kwenye toleo la gazeti la Good
News (Habari Njema) la Septembea/ Octoba 1990 kwenye makala iliyoandikwa na K.
Neil Earle kuliandikwa makala iliyowapotosha wasomaji wake kutokana na mahubiri
ambayo makala hii iliyanukuu yaliyohubiriwa na maafisa wa Australia na Marekani
wa kanisa hili la WCG, na yalichukuliwa kana ni kitu cha kipuuzi na kufuru
kubwa na ndiyo hasa ilionyesha udhaifu wa kanisa la WCG na fikra zake za
Kiditheist.
Earle anasema
kwenye makaia yake hii anasema kwamba: Kuanzia
Hapa Hadi Milele (ukurasa wa 7), kwa
hiyo hata kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu, msemaji mkuu aliyepewa jukumu hili
kwenye familia ya Mungu alikubali kufanyika mwili (Yohana 1:1-3, 14) na akafa
ili kulipa fidia ya makosa yetu tuliyoyafanya kwa makusudi. (Warumi 5:8-10).
Kauli hii
ilichukuliwa kama kitu cha kipuuzi mkubwa na maafisa wa kanisa huko Australia
na Marekani kwa kutangaza kuwa Mungu alijadiliana na Kristo na wakaafikiana ni
nani kati yao aje hapa chini duniani ili afe na kutolewa sadaka kwa dhambi za
ulimwengu. Mwinjilist Gerald Waterhouse wa WCG aliyekwenda Australia kuishika
Sikukuu ya Vibanda mwaka 1991 katika mji wa Canberra ACT na kutoa mahuribi
aliyasema mahubiri haya ya kufuru ya kwamba waziwazi. Kumbuka kwamba Mungu
alirejea kwenye familia ya watu wawili na Kristo kuwa ndiye alikuwa ni msemaji
mkuu kana kwamba Mungu wa Pekee na wa Kweli anamapungufu fulani kwenye utendaji
wake wa kazi. Hii ni kinyume kabisa na inavysema Yohana 1:18. Pia inakana kile
kinachomaanishwa kwetye Wakolosai 1:15 ambapo inamuelezea Kristo kuwa ni Ishara
ya Mungu asiyeonekana, na ni mzaliwa wa kwanza wa kila kiumbe. Mtu angeweza
kudhani kwamba andiko lililo kwenye Ufunuo 3:14 kuwa ni usemi unaotafsirika.
Hili sio wazo
jipya kwenye kanisa hili la WCG. Kwenye makala iliyoandikwa na Garner Ted
Armstrong yenye kichwa cha somo kisemacho Je,
Ni nani – Ninini – Alikuwa Yesu Kabla Hajafanyika Kuwa Mwanadamu? (Gazeti
la Habari Njema au Good News, la mwezi Novemba/ Desemba 1972, kurasa za 14-16),
Mungu wa Agano la Kale alijifanya kuwa ni Yesu Kristo na akasema kuwa neno Yahova kwenye Agano la Kale halimtaji
Mungu Baba bali wakati wote linamaanisha Jesu Kristo. Maelezo haya yamenenwa
kwa namna moja inayolingana. Hawakuonekana kuwa wanagundua kwamba neno Yahova lilikuwa linamaanisha idadi ya
viumbe na kwamba hakukuwa na utumiaji wa neno Yahova. Wakati huyu Yahova wa
Majeshi anapotumiwa mara zote inamaanisha Baba. Neno Yahova (SHD 3068) linaweza
kumaanisha kwa mtu yeyote ambaye ni mjumbe wa Mungu. Ni nafsi ya tatu ya muundo
wa vebu Hayah na linamaana ya Asababishaye Iwe (soma nakala ya Biblia
ya New Oxford Annotated Bible RSV iliyoweka kikumbushi ‘f’ kwenye Kutoka 3:14).
Kama inavyojadiliwa wametajwa wane kwenye Mwanzo 18-19 kwenye maangamizi ya
Sodoma na Gomora. Jina linguine la Mungu ni Yahovi (SHD 3069). Jina hili mara
zote linasomwa na Wayahudi kama Elohim na neno Yahova linasomwa kuwa ni Adonai
kwa kuepuaha kuwachanganya watu wawili. Jina Yahovi linamuelezea Baba.
Ilikuwa ni kwa
sababu hii ndipo neno Yahova lilibadilishwa na Sopherim mwaka 134 na
likawekwa kwenye Agano la Kale kwenye Maandiko ya Masoretic (MT) ili
kuwabadilisha watu wawili hawa.
.
Kanisa la WCG
lilionekana kuwa halikuwa na habari ya mpangilio huu na ugeuzaji wa maandiko
uliofanyika kwenye maandiko haya ya MT na likatangaza tu kwamba kuamini hivyo
ni makosa.
Armstrong
aliendelea kuamini kuwa Yohana 1:1 iliitangulia Mwanzo mara zote.
Yohana sura ya
kwanza inamzungumzia Monogenes Theos au Mwana pekee wa Mungu 1:18, ambaye
alikuwa kwenye moyo au nia ya Baba, akimtaja. Hawa walikuwa ni elohim wengi au
wana wa Mungu ambao kwao Kristo ndye alikuwa ni mwana wa pekee na ni prototokos au wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu.
Fundisho
linalosema kwamba kulikuwa na viumbe zaidi ya Mungu huko nyuma nip tofu na inatokana
na imani ya kuabudu miungu mingi. Hili sio fundisho la Kikristo. Kumekuwa na
mifano mingi kwenye historia, kama vile imani ya wa Zoroastrian na ya Waamini
mingu wawili maarufu kama ya Manichean Dualism, bali imani hizi kila mara
ziliamini na kudai kuwa kulikuwa na mashindani kati ya mungu mwena na mungu
mbaya wakigombea ubora au ukuu. Lebo ya mamlaka. zuri t these systems Manichean
Dualism iliwwekwa kwenye utepe wa mavazi ya Wakatoliki ili kuyashughulikia
baadhi ya Makanisa ya Mungu kwa kuwa walidai kwamba nguvu za uumbaji pia anazo
Shetani kipindi cha ulimwengu uliokuweko kabla ya Tohu na Bohu walioandikwa
kwenye Mwanzo sura ya kwanza. Ni kama kadiri Sayansi insvyoendelea kukua
kiwango chake, mtazamo huu unaonekana kuwa sahihi na inawaelezea Wanefili,
ambao Augustine wa Hippo alikataa na kuwanena kuwa walikuwa ni watoto
waliozaliwa na Malaika Walioasi. Wakatiliki wameendelea kuuamini uwongo huu.
Armstrong
alilijua hili, na ndivyo ilivyokuwa kwenye huduma yake pia. Mmoja wao alitajwa
kuwa ni Mditheism wa dini ya waabudu jua iliyokutikana kwenye Mayans ya kale
huko Guatemala na inaonekana kufikirika kuwa walikuwa sahihi. Walikuwa na imani na muundo sawa na tabia
au desturi za Waamerika wanaoishi pande za Kati na Kusini mwa bara hilo.
George L. Johnson
aliandika mengi kuhusiana na Asili ya Mungu na akaitaja hii miungu ya wa Mayan
mwaka 1973 kipindi kijupi tu baada ya Garner Ted Armstrong kuiandika makala
hii.
http://cog-ff.com/PDF/is-god-a-trinity.pdf
mwandishi na mtunzi George L. Johnson kutoka Ambassador College Press Pasadena, California 1973.
Kwenye kurasa zake za 21-22 kweny kifungu kisemacho “Krristo hakuumba” anaandika maneno yanayotofautisha kati ya Kristo na Malaika wengine ambayo kwa kiini chake kwa Mafundisho ya Wabinitarian / Watrinitarian ambayo yametokana na mafundisho yaliyokuwa yakifundishwa kwenye Shule ya wa Alexandria kati ya miaka ya 170 na 325 BK. Kwenye kurasa za 24-25 zinahusisha miungu yaw a Mayan Tepeu, ambaye ni mungu wa mawingu na ni mmoja ya miungu waumbaji ambaye liyehusika na majaribio yote matatu ya kumuumba mwanadamu na Gucamatz mungu mwenye mwonekano wa joka lenye manyoya ambao walifananishwa na Mungu Baba na mwanae Yesu Kristo. Johnson anaonekana kufikiria kwamba sadaka ya kuwatoa kafara wanadamu ya hawa Mayans ilikuwa na maana fulani zaidi.
Ukweli ni kwamba Armstrong, akiwa anasaidiwa na huduma hii, aliipa nafasi imani hii na akaamini kuwa Mungu ni muunganiko wa viumbe wawili na kisha akamuita Mungu kuwa ni familia ya watu wawili. Alidai kwamba hakukuwa na wana wa Mungu hapo kabla hadi pale alipokuja Kristo na kuzaliwa mwanadamu. Ni kama tunavyojua sana kwamba huu ni uzishi tu na ni ukosefu mkubwa wa kuyafasiri Maandiko Matakatifu.
Bado na watu waliomfuata waliendelea kuyapotoa Maandiko na hata kuzidisha kuyapa mashiko zaidi matundisho yake mapotofu ya kujitungia mwenyewe. Mtu anayekumbwa na kuyaamini mafundisho haya mapotofu ni hasa yule ambaye haisomi Biblia na anayebakia tu kwenye majisifu yasiyo na maana akijiona bora kuwapita wengine.
Armstrong alisema kwenye kitabu chake cha “Siri za Nyakati (Mystery of the Ages)” kwenye kipengele cha Siri ya Kanisa (Mystery of the Church) kwamba:
Kwanini
ilifanya kuwa ni muhimu kwa Yesu kuwa Mungu halisi aliye kwenye mwili wa
kibinadamu? (sic). Kwa kuwa Mungu alikuwa ndiye Muumbaji wa watu wote. Kwenye
Waefeso 3:9 imefunuliwa kwamba Mungu aliviumba vitu vyote kupitia Yesu Kristo.
Mabishano haya yanatuama kwenye dhana inayotokana na falsafa za Kiyunani zilizotumika na Wakatoliki ili kuitambilisha imani ya Utatu. Suala lenyewe ni kwamba ni Mungu peke yake ndiye anayeweza kuwawapatanisha wanadamu kutokana na aina yoyote ya dhabihu isingeweza kutosha. Mjadala unahusu uweza wa Mungu. Dhambi ni lile tendo la kuzivunja amri au kuasi (1Yohana 3:4) na inapelekea kuwa ni deni kwa mujibu wa torati. Ilikuwa ni kwa sababu ya deni lile ndipo alisulibiwa mtini kwa mauti na kifo chake Kristo, kama tunavyoambiwa kwenye Wakolosai 2:14. Kifo cha Kristo kilifuta chierographon yetu au bili za madeni yetu kutokana na torati. Aliyafuta yote kwa kuwa Mungu alisema kwamba kwa kufanya hivyo ndipo angetufutia madeni yetu. Ilimpasa athibitishe kitu ili akubalike kutawala. Mungu angeweza kukichagua kitu chochote kiondoe madeni haya. Hadi kufikia mwaka 30 BK ndipo alipoipokea dhabihu na kumuamuru Kristo aweke utaratibu wa kuitoa sadaka hii. Alikuwa ni huyu Kristo ndiye aliyempa Munsa Torati ya Mungu na ndiye aliyewaongoza Israeli jangwani (1Wakorintho 10:4). Hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu kamwe na wala aliyewahi kuisikia sauti yake kabisa. Kristo alisema hivyo yeye mwenyewe.
Ni mapema kiasi gani basi wazo hili liliingia na kuendelezwa kwenye makanisa ya RCG/WCG? Fundisho lisilo na mashiko liliingizwa kwenye makala isemayo “Je, Yesu ni Mungu?” [kwenye Gazeti la Ukweli Mtupu (Plain Truth), la mwezi Februari 1950, ukurasa wa 3ff.; soma habari zake kwenye nakala iliyoambatanishwa hapo chini.)
Zaburi inaonsha kwamba David alijua kwamba Mungu wa Israeli alikuwa ni kiumbe ambacho ndiye alikuwa Mungu mwenyewe na asiyehitaji wa kumsaidia (Zaburi 45:6-7). Kunaweza kusiweko mashaka kuamini kwamba kiumbe huyu alikuwa ni Kristo, kama ilivyo kwenye Waebrania 1:8-9 na inavyosema kwamba alikuwa Kristo. Kwa usemi wa Kibilia, Mungu ni kiumbe anayewajibika na uwepo viumbe au vinginevyo atakuwa ni Mungu wa uwongo. Na kwa hiyo inategemeana na umuhimu au ukweli wa jambo lenyewe, kuona kuwa kama ni Mungu wa Israeli kuwa ndiye Mwana wa Mungu na kuwa ana Mungu na kama alikuwa na Mungu wakati Daudi alipokuwa akiyasema haya kwenye Zaburi hii akiongozwa na Roho Mtakatifu, na kwamba huyu Mungu mdogo ni uzao wake yeye mwenyewe Mungu na ndipo angeweza kabisa kuwa na umilele sawa na kumbe Yule. Biblia inasema wazi sana kwamba kulikuwa na viumbe wengi wa namna mbalimbali wanaoitwa elohim kabla ya uumbaji na viumbe wengine wengi walioitwa Yahova kabla ya kuzaliwa kwa Kristo. Zaburi 45:6-7 na Waebrania 1:8-9 zinasama wazi kwamba Mristo ana wafuasi au wenzake huko juu ambaye kwao aliinuliwa juu kutokana na maisha yake ya kibinadamu na kifo chake. Mwanzo sura ya 18 na 19 zinaonyesha wazi kabisa na kusisitiza kuwa kulikuwa na Yahova wanne kwenye maangamizo ya Sodoma na Gomora. Watatu walikuwako duniani. Mmoja alikuwa na Ibrahimu na wawili wengine walikuwa pamoja na Lutu na wa nne alikuwa mbinguni na ndiye aliyeinyeshea moto miji ile kutoka mbinguni (soma jarida la Malaika wa YHVH (Na. 24) [The Angel of YHVH (No. 24)].
Matendo 7:35-38 Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti. 36 Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arobaini. 37 Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye. 38 Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.
Na Mwamba ule ulikuwa ni Kristo (1Wakorintho 10:4).
Wanahistoria wanaojulikana au wasiojulikana
kabisa kusema kwamba teolojia ya kwanza ya Kanisa ilifanywa na watu wenye
mtazamo mdogo kuhusu Kristo. Wayahudi walimuelewa alichokuwa anakisema wakati
Kristo alipowaambia kuwa yeye alikuwa ni Mwana wa Mungu (Yohana 10: 34-36). Hivyo basi haiwezekani kuwa walikuwa hawajui kwamba
Baba alitajwa kwenye Agano la Kale na kwamba mwana wa Mungu ni Yahova wa Israeli.
Mungu
aliyefanyika kuwa ni Yesu Kristo alikuwa ni Mungu wa Agano la Kale na Mungu
Baba alikuwa nyuma ya utendaji wa mambo kwenye Agano la Kale akiyafanya hayo
yote kupitia kwa Kristo.
Madai haya yalifanyika mara nyingi kwenye sehemu kubwa ya huduma yake. Madai ya msingi inaonekana kuwa ni yale ambayo Agano la Kale liliyataja kuwa Mungu ilimaanisha Yesu Kristo, akiwa kama Baba aliyedhaniwa kuwa alikuwa hajafunuliwa hadi pale Kristo alipoanza huduma yake.
Madai ya Armstrong kwamba Mungu alikuwa hajafunuliwa kwenye Agano la Kale ni ya uwongo kabisa. Zaburi 110 inaonyesha kwamba ili kuwa hivyo, kama ilivyofanya Zaburi 45. Zekaria 2:8-10 inaonyesha kwamba Bwana wa Majeshi alimtuma Yahova wa Israeli aishi katikati yao. Ni kwa namna hiyohiyo, Mungu hujifunua kwa kupitia nanii Zekaria kwamba kiumbe aliye kwenye kichwa cha Nyumba ya Daudi na Kanisa ni Malaika wa Bwana (Zekaria 12:8).
Uongozi wa Hekalu ulijua sana kwamba kiumbe aliyekuwa akiwaongoza jangwani hadi Sinai alikuwa ni Malaika wa Bwana. Walijua kwamba mwana wa Mungu aliwachukulia Israeli kuwa kama milki yake na mmoja wa Malaika nah ii ndiyo maana walilibadili andiko la Kumbukumbu la Torati 32:8 (kwenye fasiri ya MT) ili isomeke hivi: Wakati Mwenyezi Mungu alipoyagawia mataifa urithi wao, Wakati alipokuwa anawatenga wana wa Adamu, pia aliwagawa watu kwa jinsi sawa na idadi ya wana wa Israeli. Tunajua pasi na shaka kwamba andiko hili lilisomeka hapo mwanzo “sawasawa na idadi ya wana wa Mungu”, na tafasiri ya Septuagint inasomeka kuwa malaika wa Munngu.
Biblia ya RSV imelisahihisha andiko hili na jambo hili lilijulikana kipindi ambacho Armstrong aliandika lakini alionekana kujifanya kama hakuwa analielewa hili. Gombo maarufu lijulikanalo kama The Dead Sea Scrolls (DSS) limethibitisha usomaji huu. Hawa elohim walikuwa wote wana wa Mungu na walikuwa sawa na Malaika wa Mungu. Madai aliyoyatilia mkazo Armstrong yalikuwa ni ya uwongo mkubwa sana kwa namna yoyote ya kimtazamo na kimjadala.
Inaonekana kuwa Armstrong hakuwahi kuzisoma sura hizi au vitabu hivi kwa undani sana. Na pengine hakuvielewa au kuvitumia kwenye uandishi wake na kwenye huduma yake na akavichambua tu yale waliyokuwa wakiambiwa bila kuyafanyia uchambuzi au kuyafikiria kwa kina. Mtu mmoja alisema kwamba alikuwa ameambiwa na mtumishi alikuwa na “akili sana kiasi cha kuweza kudumu kwa muda mrefu kwenye kanisa la WCG.” Kilichikuwa kinaonysha uadilifu wao.
Mahsmbulizi ya Armstrong juu ya Uweza wa
Kutoshindwa na chochote wa Mungu
Kwenye uandishi wa vitabu vhake vyote viwili, yaani cha Siri za Nyakati [Mystery of the Ages (MOTA)] na Umuhimu Mkubwa wa Mwanadamu [The Incredible Human Potential (TIHP)] Armstrong alidai kwamba Malaika hawawezi kufa.
Anasema kwenye kitabu chake cha (TIHP, 1; ukurasa wa 59):
Hukumu kwa ajili ya dhambi ya Malaika haikuwa kifo – kwa kuwa Mungu amewaumba kwa hali ya kuwa ni viumbe wa kiroho wasioweza kufa. Kile ambacho Mungu amewapa ilikuwa ni hii dunia iwe ni makao yao na kuwapa fursa ya kufikia kiwango cha kuusafisha au kuupamba na kuumiliki ulimwengu wote.
Wazo na fundisho hili ni uwongo mkubwa wa shetani kusema: “hakika hutakufa.” Ni namna nyingine ya fundisho la imani ya roho isiyoweza kufa.
Anaendelea na madai yake kwenye kitabu chake cha Siri za Nyakati [Mystery of the Ages (2, ukurasa wa 114)] kwa kusema:
Viumbe
wa kiroho, wanapokamilika tu kuumbwa (na kwa kuwa theluthi moja ya malaika
walioasi na kuwa mapepo), wasingeweza kubadilika tena! Roho inapokuwa
inakamilika kuuumbwa kwake tu, inakuwa na uwezo wa kuishi kiuendelevu na
inaishi milele – haiwezi kubadilika. Bali mwli wake asilia unaendelea
kubadilika.
Kisha kwenye paragrafu inayofuatia, anafanya maelezo ambayo yanayaonyesha yale aliyotangulia kuyasema yaonekane kuwa ni upuuzi.
Kwa
kupitia mpango kabambe wa Mungu kwa viumbe wake wa kiroho, wanaopaswa waonekane
baadae, umekuwa ni mpango kabambe wa Mungu na huyu Neno ambaye ni neno
alijigawanya mwenyewe kwa utukufu wake wa kimungu, na kwa kipindi chake muafaka
alichukua asili ya mwili wa kibinadamu akwa ni Yesu Kristo ili kufanya
iwezekane kwa mtembeo wa kiroho wa uumbaji wa mwanadamu—Mungu AMEJIONGEZA
MWENYEWE! Ni nini MPANGO KABAMBE katika UKAMILIFU
wote wa ukamilifu wa uumbaji! Ni MKUU kiasi gani Mungu wetu, kwenye fikra,
kusudio lake la kimpango, uundaji pamoja na UUMBAJI – kutoka kwenye umbile dogo
la kinasaba mbegu au kidudu hadi kuwa jua kubwa, kulishusha ukubwa jua letu
kubwa hadi kuwa kitu kidogo kisicho na maana!
Na umuhimu wa uliopo wa mwanadamu ni kule MUNGU MKUU NA MWENYENGUVU alivyo, ndani ya mwanadamu, akijiongeza mwenyewe – mwanadamu anaweza kuzaliwa kwenye FAMILIA YA MUNGU (mkazo umewekwa)
Ni fundisho la
uwongo kwa sababu zifuatazo:
1. Inapinga ile Sifa ya
Mungu kuwa ni wa Uweza wa Yote na asiyeshindwa na jambo lolote (Omnipotence) na
kumfanya kuwa hawezi kuthibiti mambo ambayo yeye mwenyewe aliyaumba.
2. Inapinga pia sifa ya
Mungu ya Uweza wa Kujua Kila Jambo (Omniscience) na kwenye hilo Armstrong
anadai kwa nguvu zote kwamba kwa kweli Mungu hakujua kuwa Shetani na theluthi
moja ya Malaika walikuwa wanataka kuasi au kama wangemuasi licha ya kujua
umuhimu wa dhabihu ya ondoleo la dhambi ya Kristo na kwamba ilikuwa imepangwa
kutolewa tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia. Ili kujilinda na mashambulizi haya
Armstrong alidai kwamba Mungu alichagua msimamo wa kutoyajua hayo kwa kusudi la
kulinda uhuru wa kujiamulia jambo linaloonyesha ni ukosefu mkubwa sana wa
kuelewa ama kuelewa vibada maana iliyopo kati ya uhuru na uamuzi na kumfanya
awe ni Mungu mwenye kigeugeu na aiyeeleweka msimamo wake.
3. Kwa kutoelewa kwake
matokeo yaliyojitokeza baadae, kunamfanya Mungu asiwajibike na wala kuwa na
uwezo na viumbe aliovyoviumba wakiwemo hawa Malaika na akiwa hajui maafa yao na
kushindwa kuingilia kati na kuwathibiti. Pia kunaondoa sifa nyingine ya wema wa
Mungu kwa namna mbalimbali nyingine kadhaa.
4. Inaondao pia maana ya
kifo na dhabihu ya Kristo kwa madai kwamba Roho haiwezi kufa, kana kwamba
Kristo alikuwa ni roho isiyoweza kufa, na kwa hiyo hatuna wokovu.
5. Kwa kweli inapingana
na Maandiko kwa namna nyingi sana na nukuu zake.
Kanisa hili la
WCG pia linadai kwamba ukatili wa Mungu ni miongoni mwa yaliyo kwenye
mafundisho yao kadhaa ya kanisa.
Matumizi mabaya
ya andiko la Ufunuo 20:13 linalosema juu ya Ufufuo wa Tatu wa wafu watakaotupwa
kwenye Ziwa la Moto ambayo ni adhabu atakayoweza pia kufanyiwa mtu yeyote atakayethubutu
kumuonea shaka Armstrong au atakayeondoka na kuliacha kanisa lake kwa ajili ya
kutoamini juu ya fundisho lake hili la ukatili kisasi cha kumungu ambayo kwamba
kila mtu wa wadhiwa wowote mwenye tabia na mwajibiko wa kumpinga (soma jarida
la Dhana ya Uwongo Kuhusu Ufufuo wa Tatu (Na. 166) [Fallacy of the Third
Resurrection (No. 166)].
Kwa jinsi hii
alikuwa na hukumu ya milele kwa malaika Walioasi. Teolojia yake ilikuwa ilikuwa
finyu sana nay a hatari kama ya Kanisa Katoliki la Roma aliyoikataa.
Kwenye Gazeti la Good News la Julai 1974, kuna makala iliandikwa na Robert
Kuhn akisema:
Kuna muda mwingi uliopo
ikiwa maudhi yataendelea—hata kwa kiasi kidogo—tungeweza kuwa kwenye matatizo
makubwa. Umilele ungekuwa ni jehanamu
halisi! Kwa ukweli wa mambo hili ndilo hakika janga lililobakia kwa Shetani na
mapepo yake. “ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni
nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.” (Yuda 1:13
Ni kitu gani hiki
anachofikiria akilini mwake na kuota nyozi hii isiyo na mashiko yoyote ya
kibiblia na kudai kuwa ni Mungu? Matokeo ya matumizi mabaya ya fundisho hili ni
kuwa na huduma isiyoheshimika na kuwa na waumini wenye kulaumiwa au kutoaminika
lakini wanaojihesabia hakim no wenyewe. Matokeo ya mwisho yalikuwa ni kuharibu
imani ya watoto wao na waumini wenzaao na kuwaweka mbali na imani.
Miungu Wawili wa Kweli na Mwonekano wao katika
mwili
Sasa inaweza
kupingwa kwa niaba ya Armstrong kwamba Kristo alikuwa ni mmoja kati ya Miungu
wa kweli wawili, na ambao wote wawili walikuwa na uweza wa kutokufa, na kwamba
alikuwa na uwezo wa kufa wakati Malaika walipokataa kufanya hivyo. Na kwa hiyo
asingeweza kuwa na uweza wa kutokufa.
Tatizo ni kwamba
Biblia imeweka wazi sana kuna Mungu mmoja tu aliye Wapekee na wa Kweli na
kwamba alimtuma Yesu Kristo, na kuujua ukweli huu na kuwajua watu hawa hivyo ni
muhimu sana kwa ajili ya kuupata uzima wa milele (Yohana 17:3).
Madai ya kwamba
Mungu amejifunua katika mwili ni ya uwongo na yaliingizwa kwa kughushiwa kwenye
Codex A kwenye 1Timotheo 3:16 na yakaendelezwa tena kwenye tafsiri ya KJV.
Inatuama kwenye neno linalomaanisha Mungu lililofanyizwa kwenye nyaraka za
Kiyunani, ambazo zimeongezwa na waandishi kwenye makala mbalimbali.
Bullinger
aliandika kuhusu ukweli huu na alinukuliwa kwenye maandishi ya chini ya Biblia
ya R.V. na kwahiyo hakuna udhuru kwa Armstrong na kikundi chake akiwa hana
habari juu ya ughushaji huu. Hila hii ya kughushi ilinukuliwa pia na huduma ya
kanisa lake la WCG anapojaribu kuikaribisha na kuiingiza imani ya Utatu, na kwa
watumishi wanaohudumu kwenye huduma nyingine zilizotokana na kanisa hili.
Mtume Paulo
ameweka wazi sana, mtu anaweza kufikiri kwamba kile alichokisema kwenye
1Timotheo 6:16, alikuwa anasema habari za Mungu:
ambaye yeye peke yake
hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna
mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata
milele. Amina.
Biblia imeweka
wazi sana kwamba ni Mungu tu mwenye uwezo wa kuishi pasipokufa ndani yake.
Hakuna mtu aliyewahi kumuona yeye na wala hakuna atakayeweza kumuona.
Aliumaanisha uweza huo kwa cheo cha Kristo na ataweza kuwa hivyo kwa Watakatifu
wote wa namna mbili, yaani wa Kimwili na Kiroho. Hawajui kuwa wanauweza mkubwa
wa kutokufa.
Kristo alionekana
wazi kote kueili, yaani siku za Agano la Kale na akiwa kama mwanadamu. Kristo
alikufa. Mungu hawezi kufa. Anawashirikisha uweza huu wa kutokufa Malaika wote.
Kwanza kabisa, Mungu alimshirikisha uweza huu Kristo, jambo alilolifanya wakati
alipopaa mbinguni. Hatimaye atawashirikisha mateule wote kipindi chake
alichokiweka baadae.
Ingekuwa wazi
sana kuona kwamba mtu mwenye akili za wastani tu kujiuliza kwamba iwapo kama Kristo
angekufa, basi Malaika wengine waliobakia wangekufa pia, kwa kutumia mchakato
huohuo au zaidi. Hiki ni kitu ambacho Biblia inakisema kabisa kuwa kitatokea.
Tumejionea andiko
la Zaburi 82:6-7. Kwenye aya yake ya 7 imeandikwa: Lakini
mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
Kristo alilitumia
andiko hili akimjibu Kuhani Mkuu alipojitangaza kuwa ni mwana wa Mungu.
Andiko hili kwa
kweli linawahusu Wateule wote bali kuwa ushahidi mwingine kwenye Maandiko
Matakatifu unaosema kwamba Roho yaweza kufa?
Kristo ni mfano mmojawapo. Matukio yalikuwa ni kwamba Kristo alijitoa kwenye ulimwengu wa roho na akaenda kwa Mungu ambaye hatimaye alimfanya kuwa zaigoti au kiumbe kichanga kwenye tumbo la Mariamu.
Kwa hiyo alikuwa ni roho ndiye aliyepunguza umbo la mwanadamu na hatimaye kufa na kufufuka. Na hii ndiyo maana tunaona kwa wazi sana kwenye Maandiko Matakatifu kuhusu Shetani na Malaika walioasi.
Roho Mtakatifu anasema kupitia kwa nabii
Isaya kwamba itatokea. Isaya
sura ya 14 inamtaja Shetani kuwa ni Lusifa.
Isaya 14:9
inaonyesha kwamba Sheol au kaburi litamwachia ili aweze kwenda kukutana naye
kipindi atakapokuja. Kwenye aya ya 10-11 inasema: “Hao wote watajibu na
kukuambia, Je! Wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi!
Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza
wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika”.
Ili kuondoa
mashaka yote kwa yeye tunatemnena, aya ya 12-14 inamwonyesha kiumbe na kile
alichojaribu kufanya.
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya
alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha
mataifa! 13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka
mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu
ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa
kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu
Kitu kisicho cha
kawaida ni kwamba watumishi hawa walinukuu hili kama wanamtaja Shetani na
lakini hawakusoma andiko lote la sura hii, ambayo inasema wazi kwamba Shetani
atauawa. Na kutopwa kuzimuni na kungojea Ufufuko. Ni Ufufuo wa Pili tu ndio
ungemaanisha kama wafalme wa Mataifa wangehusishwa, nah ii inaonekana wazi
kwamba hawatakuwepo kwenye Ufufuo wa Kwanza.
Ili kuondoa
mashaka yoyote, Ezekieli 28:14-18 inamwonyesha Shetani kuwa ni kama kerubi
mtiwa mafuta aliyefunikwa ambaye alitembea juu ya Mlima wa Mungu na ambaye
alikuwa mkamilifu hadi alipotenda dhambi na Mungu akamtupa hapa chini. Mungu
anasema ataagiza moto na uje juu yake na kumuangamiza awe majivu, na ndipo
Shetani atauawa na kufufuliwa kama mwanadamu na andiko liko wazi kuelezea jambo
hili. Maandiko Matakatifu hayatanguki (Yonana 10:34-35).
Huduma hii hii
inalielea maandiko haya na linasema wazi kwenye mahubiri yanayotolwa mara kwa
mara kuwa linamtaja Shetani, bali wao hawasomi au halifafanuliwi au linaonekana
kuelewa kwa lugha ya wazi na makusudio ya maandiko haya.
Upuuzi ulio
kwenye imani hizi zote mbili, yaani Wbinitariani na Utrinitariani umeelezewa
vizuri kwenye jarida la Ubinitatiani na Untrinitatariani (Na. 76) [Binitarianism and Trinitarianism
(No. 76)]. Inawezakusemwa kwa usalama kabisa kwamba
neno Ubinitariani halikuwa linatumika wala kueleweka na huduma au
washirika wa WCG hadi ilipotumika na kuelezewa na majarida ya CCG.
Sababu za msingi
za kuamini imani hii ya miungu wengi ya Armstrong zilipelekea idadi kubwa yao
kuwa ni wenye kuitete kwa utii mkubwa na kuanza kudai kwamba kanisa la kwanza
lilikuwa ni la Kibinitariani na kwamba kanisa la WCG na mengine mengi
yaliyotokana na kanisa hili yanashikilia kuwa fundisho asilia la kwanza. Uwongo
huu umeungwa mkono na waandika vitabu wa Kitrinitariani kwenye imani ya
Kiadventista wakijaribu kutafuta sababu za msingi za kuamini kuwa imani hii ya
Utrinitariani ilikuwepo kwenye Kanisa la kwanza. Larry Hurtado ni miongoni mwa
watetezi wa imani hii. Watetezi wa Utrinitariani kwenye makanisa ya LCG na UCG
wamefuata mstari huu wa mabishano licha ya kujua kwamba ni fundisho la uwongo
na la bandia.
Ubinitariani
ulianzia katika ibada za kuabudu jua na dini nyingine za siri za mungu Attis
huko pande za Magharibi, na mungu Adonis aliyeabudiwa na Wayunani na
Osiris/Isis aliyeabudiwa na Wamisri.
Ni Ukristo peke
yake ndio ulikuwa na kundi la kweli lililoshindana nao huko Roma nalo lilikuwa
ni dini ya Attis. Katikati ya karne ya pili (154/5 KK) askofu wa Roma,
Anicetus, alianzisha kuadhimishwa kwa sikukuu ya Easter kwenye kanisa huko
Roma. Jumapili iliingizwa kwa
hila sambamba na ibada Sabato tangu mwaka 111 BK.
Teolojia mafunzo
ya teolojia kufundisha wau kuhusu Attis yalikaziwa sana, na wanaoamini Ukristo
waliamini vitu mchanganyiko na mafundhisho haya ya uwongo ya Ubinitariani. Mara
tu baada ya kuingizwa sikukuu ya Easter teolojia ilibidi iendelezwe kwa kiasi
cha kuwa isomeke mno na kuwashawishi wanaomwabudu huyu mungu Attis. Mchakato
huu haufundishwi kwenye chuo chochote like cha kanisa isipokuwa kanisa la CCG
peke yake ndilo linaloliweka wazi mahali ambapo Watrnitariani walipoyapata
mafundisho hayo. Ilikuwa ni huyu Attis ndiye aliyeuawa wakati wa Easter.
Aliiuawa kwenye mti wa msonobari. Ni tukio hilli ndilo lililosababisha chanzo cha kupamba miti siku ya tarehe
24 Desemba. Ni mungu jua asiyeonekana ndiye anayeabudiwa pale siku hii ya
tarehe 25 Desemba. Ni yeye ndiye aliyefufuliwa na mungu mke mama yake ile siku
ya Jumapili. Yeye pia alikuwa na mapenzi kama huyo Easter, ambaye pengine
huitwa Rhea, au Cybele na majina mengine mengi. Hakuna Mkristo alisia
angaliyeweza kuusimamisha mti huu na hivyo wakashikilia ukweli kwenye jambo
najisi na lisilo safi wala haki na kuwafundisha watu wao uwongo.
Wengi miongoni
mwao kwenye Makanisa ya Mungu ni watu wafuatilia mambo ya bahati ama ni
Watrinitariani moja kwa moja wa dhahiri ambao lengo lao kubwa ni kuliharibu
Kanisa la Mungu.
Teolojia ya mungu
Attis ilianza kufundishwa kwa kujiiba kuanzia Roma na Alexandria. Mchakato na
teolojia vimeelezewa kwa kina kwenye jarida la Tafsiri Potofu Ya Ubinitariani na
Utrinitariani wa Teolojia ya Mwanzoni ya Kanisa la Kwanza (Na. 127B)
[Binitarian and Trinitarian Misrepresentation of the Early Theology of the
Godhead (No. 127b)].
Ubinitariani
unadai kwamba Mungu alijifanya mwenyewe kuwa wa kuabudiwa na ndiye aliyafanyika
kuwa mwana wake. Tusiwachanganye na Wasabelliani. Mafundisho ya Wasabelliani
yalipaswa yakataliwe kwa kuwa yaliondokana na imani ya Ubinitariani ambayo
ilikuwa ni muhimu kwenye imani ya mungu Attis. Mtazamo huo unashikilia kuwa
Baba, Mwana na Roho Mtakatifu walikuwa wakitenda mambo kiutofauti au mwonekano
wamtu huyohuyo. Hata hivyo Attis alikuwa akijulikana kuwa ni kiumbe kilicho
tofauti aliyetokana na Baba kujifanya kuwa ni Mungu mmoja.
Ilikuwa ni kutokana
na fundisho hili ndilo lililoanzisha imani ya Utatu na iliendelea tangu mwaka
170 hadi ilipochukuliwa na kutiliwa mkazo na mtaguso wa Nicaea mwaka 325.
Lilidumu kwa kipindi cha miaka miwili na hatimaye lilitangazwa kuwa ni fundisho
la uwongo na uzushi mwaka 327 na Waunitarian wanaoifuata Biblia walirejeshwa
upya na Constantine. Walibakia madarakani hadi Theodosius alipochaguliwa kuwa
mfalme mwenza na Gratian na Mtaguso wa Baraza Kuu la Kanisa ukaitishwa kwa
kikao buko Constantinople mwaka 381 na imani Utatu au Utrinitariani
ikapitishwa. Makosa haya yalisababishwa kuanzishwa na kuenea kwa Uislamu na
yakapelekea kukomeshwa kabisa kwa Ukristo unaofuata Biblia. Na hii ndiyo
itakayosababisha mapigano au vita vya siku za mwisho. Waunitariani wanaofuata
Biblia waliitwa Waariani ili
kutenganisha uhalisia wao mbali na Wabinitarian/Watrinitarian wazushi (soma
jarida la Tafsiri Potofu Ya Ubinitariani na Utrinitariani wa Teolojia ya Mwanzoni ya
Kanisa la Kwanza (Na. 127B) [Binitarian and Trinitarian Misrepresentation of
the Early Theology of the Godhead (No. 127b)].
Ubinitariani sio
fundisho la Ukisto. Linatokana na uzushi wa wapagani ambao hauna sehemu kwenye
Kanisa la Mungu na wale wote wanaoutukuza wanapaswa waonekane kuwa ni waabudu
sanamu.
Na ndivyo ulivyo
pia hata Uditheism ni fundisho la kizushi la kipagani na ambalo halina sehemu
yake kwenye Kanisa la Mungu pia. Huduma ama kanisa linalotukuza fundisho hili
linapaswa kutubu ili kuwafanya wawe na sshemu kwenye Ufufuo wa wafu.
Ni sababu kubwa
iliyomfanya Mungu aliangushe Kanisa la WCG na kuyafanya machipukizi yake
yashindwe pia.
Tangu Januari
1946, wakato Armstrong aliposema kwenye uandishi wa wasifa wake kwamba mfuo na
imani ya kanisa la WCG vinaanza na kuwa ni mwanzo rasmi wa kuanza kazi kwake
ulimwenguni kote, hadi mwaka 1986, ambao ni miaka 40 kamili, alipokufa, Kanisa
hili la Mungu lenye kiwango cha zama za Wasardi limeondolewa kwenye utendaji
kazi wa huduma ulimwenguni kote na kuyaacha machipukizi yake yakiendelea
kugombana huyu na Yule wakigombea waumini wanaotoa zaka na wanajulikana kuwa
wengi wao wako huko nchini Marekani peke yake.
Maafa au Msiba Mkubwa
Unaendelea
Fundisho hili la
Kizushi la Waditheist limechukuliwa kwenye kiwango kinachodaiwa kuwa ni
hitimisho lenye maana la kiafundisho na bila shaka liliwezesha kuzuka kwa imani
ya Kiantinomia ya Kinostiki wanaomsifu mungu wao Attis wa Kibinitariani na
wakimpenda.
Kinachofuatia ni
kuendelea kwa mabishano ya Armstrong kwamba Mungu huyu Mmoja na Wapekee ambaye
pia ni Baba wa wote hakutajwa kwenye Agano la Kale. Mtu mmoja ameichukulia hii
kwenye hitimisho la kwamba kwa kuwa Baba hakutajwa kwenye Agano la Kale, basi
Amri ya Kwanza ilimaanisha kumhusu tu Yesu Kristo kwakuwa yeye ni mungu wa Agano
la Kele. Licha ya kuwa ni uwongo wa wazi tu bali inaonyesha hali ya
kuwachukulia kimakosa pasipofuata viwango vyake kimafundisho na kule
ingalikoelekea na kuwapeleka.
Iliyochukuliwa
kutoka kwenye makala ya:
MUNGU KWENYE AGANO LA KALE NA UELEWA
WA WAYAHUDI
Mtunzi
na Mwandishi: Frank W. Nelte
Tarehe:
Machi 1994
Kipengele
namba:
“4)
Mitume wote walikuwa Wayahudi, na walikua na kulelewa wakimuamini Mungu mmoja,
bali badi bado walikuwa na wakati mgumu kuelewa vyema kuhusu Mungu Baba. Ni kwa
nini? Sehemu ya majibu yanatuama kwenye ukweli kwamba Mungu wa Agano la Kale,
Israeli HAKUWA Mungu Baba! Kimsingi Baba hakujulikana kwenye nyakati za Agano
la Kale.
Mungu
aliyewaongoza Israeli kutoka Misri na hatimaye jangwani na kishwa kwenye
historia yao yote alikuwa ni Yesu Kristo. HAKUWA Mungu Baba. Hiki ni kitu
ambacho Kanisa la Mungu limekielewa tangu kipindi cha Bwana Armstrong.”
Hii
huenda inaweza kuwa ni sahihi ni kwa hilo tu kwa kuwa Herbert Armstrong ana
mafundisho kama haya ya uwongo na yenye harufu ya ibada za sanamu
yiliyoendelezwa, kazi inazidi kuendelea mbele pamoja na muendelezo wa kufuru
dhidi ya Amri ya Kwanza:
“5)
kumbuka kwamba Kutoka 20 kwa kweli inasema kwamba:
Mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni Bwana,
Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.Usiwe na
miungu mingine ila mimi. (Kutoka 20:1-3)
A) NI
NANI aliyekuwa anayasema maneno haya? Jibu ni YESU KRISTO!
B) NI
KWA KINSI GANI basi Kristo alijitambilisha mwenyewe kwa Israeli? Jibu ni kwamba
"YHWH, Elohim wako aliyewatoa Israeli kutoka Misri".
UTAMBULISHO HUU NI WA MUHIMU SANA!
C)
KWANINI utambulisho huu uunganishwe kwenye amri 10?
D)
KUTOKA 20:3 inamaana gani kwani hasa? ... "Usiwe na miungu mingine ILA
MIMI”? NI NANI anayesema maneno haya?
Je.
Ni Yesu Kristo ndiye Anayesema maneno kwenye aya hizi akisema: ‘Usiwe na miungu
mingine ila Mungu Baba? HAPANA, hivyo sivyo alivyosema! Kristo aliwaambia
Israeli: ‘ila MINI’!
Je,
yunaweza kuyashikilia maana halisi ya Kutoka 20:3? Israeli hawakuwa na habari
kuwa kulikuwa na “Mungu Baba.” Alikuwa hajafunuliwa bado na Kristo. Yesu Kristo
mwenyewe alikuwa analiongoza taifa la Israeli, na aliwaambia wasiwe na miungu
mingine ila yeye, Yesu Kristo. Alipenda kujifunua mwenyewe kwao kama ‘YHWH,
Elohim wako’ aliyewatoa mtoke utumwani Misri.
E) Je, ilikuwas hapa Kristo
anajukweza mwenyewe zaidi ya Mungu Baba kwa kitendo chake cha kuwaambia wana wa
Israeli wamwabudu yeye, Yesu Kristo? HAPANA, sio kabisa! Mungu Baba na Yesu Kristo waliamua na
kukubaliana kwamba:
-
Kristo ndiye awe mwenye kushughulika na wanadamu au watu hawa;
- Kristo
ndiye atakayewashughulikia wanadamu hadi pale mpango wa wokovu ukamilike;
-
Kristo atajifunua kwa Israeli;
-
Kristo angetangulia kwa ujio wake wa kwanza, akishikilia uwepo wa Baba uliofichika
katika Israeli kwa ujumla;
-
Nyakati za Agano la Kale Kristo angefunua tu uwepo wa Baba yake kwa wateule
wachache tu waliochaguliwa kila mmoja peke yake na kwa sababu za msingi za
Mungu;
- Ni
katika ujio wake huu wa kwanza ndipo Kristo angejifunua uwepo wa Mungu Baba kwa
wanadamu;
-
Bali ni mara tu baada ya mpango wa wokovu ulipohitimishwa, ndpo Mungu Baba
alipokuja kwenye mawaziliano na wanadamu na ...’kuwa Mungu wao’.
Kiini
msingi cha ayah ii ni kwamba hadi pale ambapo Kristo kwa kweli ataukabidhi
ufalme kwa Baba, yeye ndiye atakayeshika maongozi haya kikamilifu, akiyaendesha
mambo kama “‘Mhusika Mkubwa’, kwa niaba ya Baba.”
Kumbuka kuwa imeshindikana kabisa kupatikana maeneo yote
yaliyoorodheshwa hapo juu jambo linaloonyesha kuwa huu ni mtazamo mpotofu. Ni
kama vile kwamba hawana uwezo wa kuweka uzani sawa wa kimaandiko. Huyu
mwandishi anaonekana kuwa hajui lolote kuhusu huyu Yahova mdogo wa Israeli ambaye ni
mmoja ya wana wa Mungu waliotajwa kwa uwazi hasa kenye Kumbukumbu la Torati
32:8. Pia mwandishi hajui lolote kuhusu ughushaji uliofanywa kwenye tafsiri ya
MT na baraza la Sopherim kwenye andiko hili. Na wala haionekani kuwa anayajua
mambo mengi yaliyoandikwa kuhusu Baba na wana wa Mungu kwenye maandiko ya Agano
la Kale.
Anaendelea
mbele kwa kusema:
“6)
Huyu Mungu ambaye wana wa Israeli walikuwa wanamuomba dua zao siku za Agano la
Kale alikuwa ni Yesu Kristo. Alikuwa ndiye aliyewaokoa na kuwaongoza na
kuwasaidia na pia kuwaadhibu. Kadri vipindi vilivyopita alitambulishwa ama
kujulikana kuwa “ni Mungu aliyewatoa watoke Misri”. Utambulisho huu
uliojulikana sana ndio ulitumika sana kipindi chote cha Agano la Kale. Kwa
kuongezea tu ni kwamba mbali ya Kutoka 20:2, kuna aya nyingine 40 ambazo kwamba
namna ya kumtambulisha Mungu wa Israeli imetumika:
Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda
Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami
nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele
sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi; (Waamuzi
2:1)
Lakini
kwakuwa Israeli HAWAKUJUA kwamba kuwakwakweli kulikuwa na Mungu mwingine
aliyekuwa ‘mkuu’ kuliko Yesu Kristo, haimaanishi kuwa huyu Mungu Baba hakuwepo
na akiwa ni Kiumbe aliye mbali kwenye kipindi kile cha Agano la Kale/
kumbukumbu la Torati 29:29, ilikuwa imeshatolewa tayari kwa nabii Musa,
akituambia:
Hii
inatuambia kwamba Mungu hakupenda kuyafunua mambo fulani ya ‘siri’ kwa watu
siku sile za Musa. NI KWA NINI? Je, mambo hayo ya ‘siri’ ni kama YEPI? Je, hayawezi kuwa ni
pamoja na hili la wasifa wa Mungu Baba linalosemwa (kwa msisitizo) kwamba” ‘Kwa
kipindi hiki huhitaji kujua kuwa mimi naishi. Nimeamua kwamba nitajifunua
mwenyewe uwepo wangu kwa wanadamu kwa ujumla kipindi ambacho Mwanangu atakapo
atakapokuwa ameitimiliza kazi yake duniani? Na kwa hiyo Kristo alikuja au
kumjulisha kwa watu wamjue kuwa yeye ni Baba, jambo ambalo Agano Jipya ndivyo
linavyotuambia, je, ni kweli?
Hebu
ziangali kwa Amri hizi Kumi tena! Hebu soma Kutoka 20:1-3! Kisha zipietie zile
aya 40 hapo juu ambazo zinamtambulisha Mungu wa Israeli. Utaona kwamba Yesu
Kristo pekee ndiye Mungu pekee waliokuwa wanamjua Israeli. Hawakuhitaji KUJUA
uwepo wa Baba. Ni kwa nini hawakuhitaji? Kama walikuwa hawakuwa na moyo au nia
ya kumtii Mungu waliyekuwa wanamjua, ambaye ndiye aliwaleta kutoka Misri...
Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa
kunicha, na kushika amri zangu zote sikuzote, wapate kufanikiwa wao na watoto
wao milele! (Kumbukumbu la Torati 5:29)
...
kwa hiyo kungekuwa na maana gani kuwatambulisha uwepo wa Mungu Baba? Wangeweza
kumkataa hata huyo Baba pia.”
Anaonekana
kwa wazi kabisa kwenye maandiko kadhaa mbalimbali ambako kote wametajwa, kama
vile Mithali 30:4-5 au Zekaria 2:8-9; au walipojitokeza wengi kwenye suala la
Ayubuna aya kadhaa zilizo kwenye Kubukumbu la Torati au Zaburi, kama vile
Zaburi 45, au mahali panapoonekana wazi kwenye Zaburi 110, au kwa suala la
Elyon kama Mungu Aliye Juu sana, au kwenye Zaburi nyingine nyingi
zinazomuonyesha huyu Mungu Mkuu na Aliye Juu sana na aliye kwenye makutaniko ya
Elohim. Na wala haonyeshi kama anafahamu maana ya Eloa na uwingi unaoonekana
hapa wa jina hili na mahala pake kwa elohim kama wana wa Mungu. Bali inaonekana
hapa kama mwandishi hajui kabisa kuisoma Biblia.
Matumizi
ya maneno Elohim kama Elohim wa Majeshi na wana wa Mungu wakati Kristo
anapochukua mahala pake miongoni mwao au mahali ambapo Ha Elohim Mungu aliye
juu ya wote hawa kwenye Zaburi 82:1,6; 86:8; 95:3; 96:4,5; 97:7,9; 135:5;
136:2; 138:1.
Hatimaye
anaendelea kuongeapumba kama ifuatavyo:
“8)
Ndiyo maana ukweli kwamba kulikuwa na Viumbe WAWILI katika Miungu mmoja wenye
uhusiano wa karibu sana kila mmoja kwa mwenziwe, na ambao wapo kwenye mchakato
wa kuendeleza uhusiano wa Kifamilia, ambao ni kwa kiasi kidogo sana umeelezwa
kwenye Agano la Kale.
Na
kwenye Zaburi 45:6-7
Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele,
Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa
hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako. (Zaburi 45:6-7)
Ingawaje walijua vema sana kuwa walikuwa wanashughulika
na Mungu mmoja, bali walikuwa wanashindwa kuelewa ama kuelewa vibaya bado
Maandiko mengi na waliyatafsiri kimakosa. Hii ni pamoja na kutafsiri vibaya
maana iliyo kwenye Kumbukumbu la Torati 6:4. Pia inajumuisha Maandiko mengi mengine. Yesu Kristo
ailema kwenye Mathayo 22:29.
Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui
maandiko wala uweza wa Mungu. (Mathayo 22:29)
Kwa
hiyo, uelewa wa WAYAHUDI juu ya asili ya Mungu kwenye Agano la Kale sio kitu
cha muhimu sana kwa njia moja au nyingine! Inaonekana dhahiri sana kwamba
WALIKOSA uelewa kwa kiasi kikubwa sana.
Ni
uelewa ambao Mugu alimfunulia Bwana Herbert W. Armstrong na alilifundisha hivyo
Kanisa la Mungu. Hakuna Andiko linalochanganya uelewa huu. Ni fikraza kibinadamu tu za
wanafalsafa wa zamani ndio naoendelea kwenye uelewa aina hii. kwa sababu,
walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea
katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa
wenye hekima walipumbazika; (Warumi 1:21-22)”
Ni kwa namna gani basi kila anayelifikiria taifa atasoma
Zaburi 45:6-7 na akadhani kwamba Biblia iko kimya juu ya viumbe wawili ambao
mmoja wao ni mdogo kwa mwingine, na sitajwe kwenye Agano la Kale? Hii
imesababisha Waebrania sura ya 1 hususan inarudia umuhimu wa muundo wa Zaburi
hii na kumuonyesha cheo cha udogo wa Yesu Kristo, na inatumia neno la Kiyunani
la metaxous ambao kwa hakika lina
maana ya wenza au washirika na
kuitafsiri kwa Kiebrania kwenye Zaburi 45 ikimaanisha wenza. Ni nini ambacho
kiko hata kwenye zaidi ya ulaghai wa kiakili ni kwamba mwandishi huyu anajaribu
kudai kwamba neno lililo kwenye Kiebrania halimaanishi wenza au washirika wa
pamoja wakati kwamba neno hilohilo metaxous
linatumika kulitfsiri neno lililo kwenye LXX. Halina maana nyingine zaidi
mshiriki-mwenza, au rafiki au mshirika. Kuna wana wengine wa Mungu. Inaonekana
kwamba watu hawa watasema kitu chochote zaidi ya kuwakubali kuwa nabii wao wa
uwongo alikuwa ni mwongo wa mambo yote mawili, yaani kiteolojia na kinabii.
Ni
kama ilivyosemwa hapo juu, Wayahudi walielewa kile alichokuwa anakisema wakati
Kristo alipokuwa anatangaza kuwa yeye ni Mwana wa Mungu (Yohana 10: 34-36). Kwa
hiyo haiwezekani kuwa walikuwa hawajui kuwa Baba alitajwa kwenye Agano la Kale
na kwamba mwana wa Mungu alikuwa ndiye Yahova wa Israeli. Na hii ndio maana
walimshitaki kwas kosa la kukufuru na walimuua.
Mafundisho
ya uzushi ya Waditheist na Wabinitariani yanatakiwa yawekwe wazi na kuonyeshwa
wazi kwenye Makanisa ya Mungu.
Kuumbwa kwa Wana wa
Mungu
Tunapokuja
kwenye suala hili la Wana wa Mungu, Wabinitariani/Watrinitariani/Waditheist wwanakabiliwa na tatizo kubwa kwenye
Agano la Kale na kwa hili wana wa Mungu walijulikana wote kama Kutaniko la
Malaika wa Mbinguni au Baraza la Elohim.
Mfumo wa udogo au usaidizi wa Yahova wa Israeli ulionekana kama kiumbe
aliyefichwa na kuagizwa kwa Israeli akiwa kama mmoja ya wana wa Mungu kwa kuwa
haikukubalika kwenye kipindi kilichofuatia mwaka 170 BK muundo wa Wabinitariani
wa Wakristo wa Roma ulituama kwenye imani ya mungu Ishtar na imani juu ya mungu
Attis, na pia Adonis na Osiris, Mithra na Baali wa huko Mashariki ya Kati.
Tangu mwaka 170 BK wanateolojia wa Kanisa walianza kuingiza mafundisho ya kutofautisha
kati ya Kristo kama Mwana wa Mungu na Malaika wa Mbinguni wakiwa nao kama wana
wa Mungu. Waliingiza wazo la kwamba wana wa Mungu walikuwa ni Malaika na ni
viumbe walio tofauti mbali na Kristo ambaye ndiye alikuwa mwana wa Mungu na
mbaye alikuwa hajaumbwa. Mtazamo wa imani hii ya Wabinitariani umechukuliwa
kutoka kwenye ibada za mungu Attis na uliingizwa kwenye Ukristo na ukaendelezwa
kwenye imani ya Wabinitariani kiasi kwamba ndipo Kristo aliinuliwa juu zaidi ya
Malaika kuwekwa kwenye sehemu sawa na Mungu akitofautishwa na Malaika na kisha
ilitanguliwa na madai y kwamba Kristo aliwaumba Malaika jambo lililosababishwa
na usomaji kimakosa wa nyaraka za Mtume Paulo kwenye Agano Jipya.
Mafundisho
haya ya kizushi yaliendelezwa hadi kwenye Mtaguso Mkuu wa Nicaea na yalidumu
kwa kipindi cha miaka miwili na hatimaye yakatupwa nje pamoja na wafuasi wa
Athanasias hadi yaliporudishwa tena na kushamirishwa mwaka 381 BK. Hatimaye
imani ya Utatu ilishika kasi na kile kilichojulikana kama kanuni au maazimio ya
Nicaea viliundwa na kufanyizwa kutoka kwenye Baraza la Mtaguso Mkuu wa
Constantinople mwaka 381 na kupewa meno zaidi kutumika tangu mtaguso wa
Chalcedon mwaka 451. Hebu na tuwe wazi hapa kwa kitu kimoja. Mafundisho haya ya
uzushi hayakuwepo kabisa na wala hayakuwa ni sehemu ya fundisho la Makanisa ya
Mungu hadi kipindi Herbert Armstrong alipoingiza imani na mafundisho ya
Uditheism kwenye kile kilichojulikana hapo mwanzo Radio COG na WCG kwenye karne
ya ishirini. Makanisa yaliyochipuka baadae baada ya kifo chake yaliendeleza
Ubinitariani baadae wakijaribu kujionyesha kuwa wanayafuata kikamilifu
mafundisho ya Armstrong na kuendeleza mvimbo wa msingi wa Utrinitariani na
kuufanya uendelee.
Historia
ya jinsi Mafundisho haya yalivyoendelezwa tangu mwaka 170 BK imefafanulia
kwenye jarida la Makosa ya Tafsiri ya Wabinitariani
na Watrinitariani ya Teolojia ya Mwanzo ya Uungu (Na. 127B) [Binitarian and Trinitarian Misrepresentation of the Early
Theology of the Godhead (No. 127b)].
Hila
na kughushi kwenye Kumbukumbu la Torati 32:8 kilikofanywa kwenye tafsiri ya MT
kulipaswa kuelezewe kwa wazi mara tu baada ya kugundulika kwake na wanazuoni
waliogundua ukwepeshaji maana kwenye tafsiri hizi za MT na LXX na kisha kulikuta
andiko hili kwenye Vitabu vya Musa au Torati huko Yudea kwenye kipindi kama
Kristo aliyeonyeshwa kwenye LXX alikuwa sahihi na halisi na walipaswa
kushughulika nayo.
Andiko hilo
linaonyesha kwamba wana wa Mungu wa elohim wa Malaika wa Mbinguni ameweka mataifa
na Yahova huyo ameichagua Israeli iwe urithi wake. Taifa la Yuda kipindi cha
Kristo lilielewa vema kuwa Yahova wa Israeli alikuwa ni Mwana wa Mungu, nah ii
ndoyo sababu iliyofakasirisha na kumuua Kristo alipotangaza kuwa yeye mwenyewe
ndiye huyo Mwana wa Mungu. Uhusiano huu ulieleweka kipindi cha Kristo na cheo
cha usaidizi cha elohim wa Israeli kilichotangazwa kwenye Zaburi 45:6-7 akiwa
kama ni aliyetiwa mafuta na Elohim wake au Mungu wake kwa mafuta ya furaha ama
ya shangwe na kuwa juu kuliko washiriki wenzi wake wote. Tunajua kwamba huyu
alikuwa ni Kristo kutokana na alivyoandikwa kwenye Waebrania 1:8-9 na aya
nyingine nyingi kwenye Maandiko Matakatifu. Aya inayofuatia inaonysha jinsi
Watrinitariani walivyojisikia vibaya kutokana na andiko hili na jinsi
walivyojaribu kuiendeleza aya hii na kuifanya ionekane kuwa inamtaja Baba,
jambo ambalo haliwezekani na linaukangavya muundo mzima wote wa Israeli wa
Kiroho ambao ni mwili wa Kristo. Ni sahihi sana kuamini kuwa Elyon ni Baba na
ni Mungu Mwenyezi aliyeyatenga mataifa. Kuna Mungu MMOJA tu na Mwenyezi Aliye Juu ya Yote. Vinginevyo, kwa lugha na
kimaantiki basi, asingeweza kuwa ndiye Mungu Mkuu na Mwenyezi na jina Elyon
lisingekuwa na maana yoyote (kama
inavyosema Yohana 17:3).
Nukuu kutoka NET © inasema
Wakati Mwenyezi Mungu 1
alipowapa mataifa urithi wao, alipoigawa kwa wanadamu, 2 aliweka
mipaka ya milki za watu, kulingana na idadi ya washikiri wa baraza la mbinguni.
3
NET ©
Notes |
1 tn neno la Kiebrania עֶליוֹן (’elyon) ni kifupisho cha jina kamili la Mungu wa Mbinguni, yaani El Elyon,
ambalo maranyingi limetafsiriwa kama “Mungu Mwenyezi” (na ndivyo lilivyo
kwenye tafsiri za NCV, CEV) au kitu kilicho sawa nalo. Jina hili kamilifu (au
cheo) huonekana kwenye Mwanzo 14 peke yake, kwa mambo mawili
yaliyosambamba Zaburi 73:11; 107:11; nk. Hapa iko wazi sana
kwamba Elyon ndiye atakayefanya hivi pamoja na mataifa kwa ujumla wakati
kwenye aya ya 9, kwa mwonekano kinyume, neno Yahwe linahusiana
kwa wazi kabisa na Israeli. Tazama kitabu cha T. Fretheim, NIDOTTE
1:400-401. Cheo hiki kinaashiria Mungu kama mtawala mwenye mamlaka wa hii dunia,
ambaye amewekwa juu ya kiti cha enzi juu ya tawala zake zote. 2 tn Heb “wana wa mwanadamu” (na kwenye tafsiri
ya NASB); au “wana wa Adamu” (kama kwenye KJV). 3 tc Heb “wana wa Israeli.” Wazo hapa huenda,
ni kwamba, Israeli alikuwa ni mlengwa wa makusudio ya Yahweh na kwa mataifa
mengine yote yalifanyika na kugawanywa kwa mujibu wa jinsi walivyohusiana na Israeli.
Tazama makala
ya S. R. Driver, Kumbukumbu la Torati (ICC),
355-56. Kwa tafsiri ya MT neno יִשְׂרָאֵל בְּנֵי (bÿney
yisra’el, “wana
wa Israeli”) Kwenye gombo la Qumran kumeandikwa “wana wa Mungu,” wakati
kwenye LXX inasomeka ἀγγέλων θεοῦ (angelwn
theou, “malaika
wa Munu”), ikiandikwa na kumaanisha בְּנֵי אֵל (bÿney ’el) or בְּנֵי אֵלִים (beney ’elim). “Wana wa Mungu” na
bilashaka kwa usomaji asilia; wa MT na LXX kila moja ina tafsiri yake
tofauti. MT inadhani kwamba usemi wa “wana wa Mungu” uliotumika kuwataja
Israeli (kama Hos. 1:10), wakati kwenye LXX
inadhani kwamba neno hili linamaanisha kulitaja jeshi la malaika wa mbinguni
(Zaburi 29:1; 89:6; sawasawa na ilivyoandikwa
kwenyc Zaburi 82). Neno hili linatathmini
pia ki Ugaritic, ambapo panataja kutaniko la mbinguni la Mungu El. Kwa mujibu
wa mtazamo wa baadae, ambao umeashiriwa kwenye tafsiri hii, Bwana alipeleka
ujumbe ili hukumu mataifa kwa jeshi la malaika (sawa na Danieli 10:13-21), huku akijichagulia yeye
mwenyewe Israeli, ambao kwamba aliwatawala yeye mwenyewe moja kwa moja. Kwa
kujilinda na mtazamo huu uliopo hapa, soma makala ya M. S. Heiser, “Kumbukumbu
la Torati 32:8 na Wana wa Mungu,” BSac
158 (2001): 52-74. |
Kumbuka,
mtazamo wa huyu Yahova kuwa ni Elyon hapa sio sahihi na maelezo ya Kristo
mwenyewe yanaonyesha kwamba kwenye Yohana 10:34-36. Andiko lililo kwenye
Zekaria 2:8-9 na pia 12:8 yanaonyesha kuwa walikuwa Yahova wawili
waliohusishwa. Mmoja wao ametumwa na mwingine a,baye ni Yahova wa Majeshi
ambaye hawezi kuwa ni huyu Yesu Kristo. Ni mtendakazi pamoja na Yahova ndiye
aliyetumwa ili kuwaokoa Israeli na Yerusalemu kama tunavyojua kutokana na
Maandiko yote ya Agano Jipya.
Vipengele
hivi na wasaa wake wakati wote vilieleweka na Makanisa ya Mungu hadi kipindi
ambacho Armstrong aliingiza imani ya Kiditheist kwa mbinu za kuwafundisha watu
wafundisho ya kizushi. Na ndipo sote tumekumbwa na wazimu wa mijadala na
mabishano na watu waliofundishwa kwenye huduma yake hii.
Kioja
hiki cha mafundisho asili yake yalianzishwa na waabudu mungu Attis na ambayo
hatimaye yaliingizwa na kuaminiwa na wahubiori wa zamani wa kanisa la WCG na
mengi ya madundisho haya ni ya uzushi tu na yametiliwa chumvi. Mmoja ya
mabishano haya yaliendelezwa zaidi na viongozi na wazee wa kanisa ambao
waliyapinga kufichouficho kwenye makanisa yaliyokuwa kwenye maeneo yao. Mmoja
wa walioyapigia chapuo sana na aliyejulikana sana alikuwa ni Frank Nelte,
aliyefuatilia sambsamba na msitari wa Ubinitarian wa huyu mungu Attis ambaye
anageuzwa na kumjulisha kama Kristo na siyo tu kwa namna tulivyoona akiwa kuwa
ndiye mlengwa kwenye ile Amri ya Kwanza, bali pia ni muumbaji wa Jeshi la
Malaika wa Mbinguni ambao kwenye fikra za Armstrong kwamba baba hakutajwa
kwenye Agano la Kale, jambo ambalo ni uzushi wa wazi sana.
Alipokuwa
akijibu makala kadhaa za UCG kuhusu Shetani, Frank Nelte aliendeleza mabishano
haya ya kipuuzi kwa kumtaja Kristo kuwa ni Nyota ya Asubuhi na kwa kuwa Shetani
alitajwa kuwa ni Lusifeli na mwana wa Asubuhi na kwa hiyo yeye ndiye alikuwa
ndiye aliyemuumba Shetani.
Kwa
vyovyote vile ni kwamba yeye alikuwa ni mwana wa Mungu na hakuyakataa maneno
aliyosema Shetani alipokuwa akimjaribu nyikani na wala Kristo hakudai kuwa
alimuumba Shetani, jambo ambalo kwamba kama angekuwa amemuumba Shetani angesema
kuwa “Mimi ni Mungu wako,” ambalo tunajua kutoka kwenye Zaburi 45 sio yeye na
pia tunajua kupitia Zaburi 110 kwamba Mungu Mmoja Wapekee na wa Kweli ndiye
aliyemfanya aketi mkono wake wa kuume hadi atakapowafanya maadui zake wawe
chini ya miguu yake. Bali Kristo alimwambia Shetani kwamba inatupasa kumwabudu
Bwana Mungu wako na yeye ndiye utakayemtumikia peke yake. Uditheism wa
Armstrong umepelekea kuwepo kwa makosa na uzushi mwingi wa kiteolojia kwa
wafuasi wake ambao hawakuwahi kamwe kuwa waumini wa Makanisa yoyote ya
Mungu. [Soma makala za Frank
Nelte: "Jibu
kwa Maelezo ya UCG kuhusu Jina Lusifeli. (A Response to the UCG Statement
on the Name Lucifer.")]
Katika juhudi zake za kuutetea msimamo wa Armstrong juu ya Uditheism, Frank Nelte anajaribu kumtenganisha Kristo kutoka
kwenye kundi la wana wa Mungu, kama walivyofanywa Wabinitarian waabudu mungu Attis huko
Roma tangu mwaka 170 hadi 325 ili tuutetea au kuuficha upotofu na uwongo wao.
Hitimisho lake ni mwamba kwakuwa Shetani
ameonyeshwa kama "mwana wa asubuhi" au "mwana
wa mapambazuko" kwenye Isaya 14:12, na Kristo anatajwa kama "Nyota ya Asubuhi" kwenye Ufunuo
22:16, kwa hiyo, Jesu Kristo alimuumba Shetani kwa kuwa anatajwa huyu Shetani
kuwa ni "nyota ya asubuhi." Ukweli ni kwamba kulikuwa na nyota wengi
wa Asubuhi
tangu kuwekwa kwa misingi ya hii Dunia wakati Eloah alipokuwa anaiumba na
waliopotea kwenye uasi au wasioendana na matakwa yake (sawa na ilivyo kwenye Ayubu
38:4-7). Hakuna madai yoyote kwenye
Biblia yanayosema kwamba Kristo aliwaumba wana wa Mungu. Anataja kuwa yeye ni
mwana wa Mungu na wala sio baba na hakuna mwingine, na hakuna hata Mwanazuoni
au Msomi yeyote yule wa Biblia wa Kitrinitarian anayeweza kufanya madai kama
hayo, ingawa kuna Watrinitarian wengi walio kenye “dini za kibiashara” huko
Marekani wanaoweza kusema kitu kinachoashiria hivyo.
Kimsingi Frank anasema kuwa jina hili "Lusifeli"
ni neno lililobuniwa linalotokana na tafsiri ya Kilatini ya Vulgate na
mwaandishi wa UCG hayajui maana yake kwa nini inatumika katika kumtaja Shetani.
Ndipo Frank anajaribu kutunga maana inayoashiria huenda ndiyo maana yake asilia
ya neno hili "Lusifeli" kwa Kiebrania na jinsi jina hili linavyoendana
kutoka kwenye Kiebrania hadi kumuita Shetani kwenye Isaya 14 na Ezekieli 28. Ndipo
anafananisha jina hili “Lusifeli” na neno la Kiyunani "Phosphoros" lilipo
kwenye 2Petro 1:19 kama linavyomweleza Kristo. Anasema:
"MATUMIZI HAYA YA JINA “LUSIFELI” KUWA YAMETUMIKA
KUMUITA YESU KRISTO KWENYE 2PETRO 1:19 KUMEACHWA KABISA KWENYE MTAZAMO NA
MAELEZO YA KANISA LA UCG!"
“Maelezo ya UCG
kuwa neno la Kiyunani “phosphoros” na lile la Kilatini “lucifer” yote mawili
yanamaana moja tu ya sayari ya Venus kimsingi ni kweli, bali yametumika vibaya!
Nia ya kuyajumuisha maneno hayo kuhusu Venus ni kupata uhakikisho wa kutumia
neno hilihili moja katika kumtaja “lusifeli” na Shetani, bali pasipo kulitaja
moja kwa moja. Ni suala tu la kujaribu kulihalalisha jina “lusifeli” kuwa ni
Shetani kwa kupitia mlango wa nyuma!”
Kisha kwenye hitiminho lake Frank Nelte kwa kweli
anaonekana kutofautiana na mtazamo wa Uditheism wa
Armstrong. Anasema:
“Hata
hivyo, IKIWA uitaji “mwana wa asubuhi” ni mwonekano sahihi wa naama
iliyokusudiwa. NDIPOSA uitajiwa wa “MWANA wa asubuhi” basi unatueleza sisi
kwamba “heylel” ALIZALIWA au ALIUMBWA na mtu mwingine ambaye hapa anatajwa kama
“Asubuhi”. Ni Yesu Kristo ndiye anayetajwa kwenye 2:28 kama “Nyota ya Asubuhi”
na kwenye Ufunuo 22:16 anatajwa kuwa ni “Nyota Ing’aayo ya Asubuhi”. Kwa hiyo uitaji kuwa “MWANA wa Asubuhi” kwenye Isaya 14:12
kuna maana tu ya kwamba Shetani ALIUMBWA NA YESU KRISTO. Wakati Mungu mwenyewe
amesema kwenye Isaya 14:12, hivi
karibuni Mungu alikuwa hafikirii juu ya sayari hii ya Venus!”
Totauti
yake ya kimawazo na maelezo haya ya Armstrong ni ujanja tu kwa kweli na hayana
maana. Tunajua sote kwamba Shetani alikuwa ni miongoni mwa wana wa Mungu
waliokuja mbele za Kiti cha Enzi cha Mungu na wametajwa hivyo kwenye Ayubu 1:6,
2:1, 38:4-7. Shetani alikuwa ni kerubi lililofunikwa nay eye mwenyewe alikuwa
ni Nyota ya Asubuhi na ni Nyota ya Alfajiri ya sayari na anaendelea bado kuwa
ni Nyota ya Asubuhi ya sayari hii, lakini watu hawa hawaonekani kama
wanalielewa hili. Pia ametajwa kuwa ni “mungu wa dunia hii” (limetumika neno
theoi kwa elohim; 2Wakorintho 4:4) na hili halipingwi na yeyote miongoni mwa
watumishi kwenye Makanisa ya Mungu.
Ukweli
ni kwamba wanapinga kwa kutumia mambo ya kubuni au uzushi na wote wawili, yaani
Wabinitarian na Waditheist wanapinga kwa kutumia mafundisho ya kuzua. Moja ni
kwamba kulikuwa na Miungu wawili tangu mwanzo na yule mmoja aliyefanyika kuwa
Baba alikubali kumruhusu mwingine aje hapa chini na afanyike kuwa mwanawe.
Wanapinga kimakosa kusema kwamba hakutajwa hivyo kwenye Agano la Kale.
Wabinitarian wanadai kwamba mmoja alitokana na mwingine kama kumbe
kilichotokana na utu wa sili ya kimbinguni na kufanyika kuwa ni mwana wa wake
kwa njia ya dhana fikirika ya mawazoni. Kwa mafundisho haya ya uwongo na
kizushi wote wawili wanafuata mafundisho ya namna moja tu ya kumuabudu mungu
Attis na ni mafunndisho ya kizushi ya kipagani.
Wasikudanganye
kabisa. Na ndiyomaana wamekufa na hawapo kabisa miongoni mwa walio kwenye Mwili
wa Kristo wanaokwenda kufufuliwa kwenye Ufufuo wa Kwanza.
Ukweli wa mambo ni kwamba Lusifeli alikuwa ni Mbeba Nuru
kipindi kabla hajawa Shetani. Tazama na kulisoma jarida la Lusifeli: Mbeba Nuru na nyota ya Asubuhi (Na. 223) [Lucifer: Light Bearer
and Morning Star (No. 223).]
Kumbuka:
Nyongeza
iliyoambatanishwa hapo chini ni makala inayotokana na machapisho ya Kanisa la
Worldwide Church of God yakisema yafuatayo:
1)
Je, Yuko Wapi Mungu Baba kwenye Agano la Kale?
[Gazeti la Good News, (Habari Njema), la Julai 1974]
2)
Je, Yesu ni Mungu? [Gazeti la The Plain Truth (Ukweli
Mtupu)], Toleo La XV, Namba 1, Februari
1950)
q
32 Ukweli
unaoshangaza ni kwamba watu walioishi
ziku za Agano la Kale walikuwa na uelewa mdogo sana juu ya Mungu Baba. Bali
yeye alikuwepo na kwa kweli ametajwa mara-kadhaa. Moja
ya sababu zilizomfanya Kristo aje duniani kama mwanadamu ilikuwa ni
kumdhihirisha Baba (Yohana 1:18; 5:37; 8:19; 14:7; Luka 10:22). Asingeweza
kumdhihirisha iwapo kama Mungu wa Agano la kale ambaye ndiye Waisraeli walimjua, alikuwa ni Baba. Tena
basi kisababisho cha kwanza cha kuwepo kwa Mtu ambaye hatimaye alikuwa ndiye
Baba kinapatikana kwenye sura ya kwanza kabisa ya ya Biblia. “Mungu akasema, Na
tumfanye [sio mimi] mtu kwa mfano wetu, kwa
sura yetu;....” (Mwanzo 1:26). Hii haiashirii “uwingi wa mwenyezi” kama wasomi
na wanazuoni wengine wanavyofikiri). Kwenye aya ya 2
tumepewa jina linguine la “Bwana [YHVH]
Mungu”” kama mshiriki mlengwa wa matendo na maneno wa hii “sisi.” Kumbe huyu
–Wamilele (ambayo naiyo maana ya
neno YHVH)—ndye kila mara ndiye anayeshughulika na wanadamu kama ujumbe wa
Biblia unavyosema. Kwenye Mwanzo 14:18, tunamkuta Mtu huyu akiwa kama “mfalme
wa amani na haki” (Melkizedeki kwenye
Waebrania), “mfalme wa Salemu” (amani). Thibitisho? Usemi unaotumika hapa ni
wa kumuelezea Melkizedeki huyu “kumeshuhudiwa kuwa anaishi”—kuwa ni wamilele (Waebrania 7:8). Kwa uthibitisho zaidi
wa mwonekano huu wa Melkizedeki, msomaji anakaribishwa kuagizia jarida letu
linalotolewa bure linaloitwa “Usiri kuhu Melkizedeki Umetatuliwa”. Jambo la kuliangalia hata hivyo ni kwamba, Melkizedeki,
YHVH, ndiye ambaye hatimaye alikuwa ni Jesu Kristo, aliyefanyika kuwa Mungu
Mwana, ambaye kwa wakati ule alikuwa ni Kuhani
(linganisha na Waebrania 7:1 na aya nyingine zinazofuatia na Waebrania
8:1), wa “Mungu Aliye Juu Sana”.(Mwanzo 14:18-22). Sasa, ni nani huyu basi
aliyejulikana kama Mungu Aliye Juu Sana, mtu ambaye alikuwa ni kuhani? Basi
Yesu mwenyewe na ajibu: “…Baba ni MKUU kuliko mimi. (Yohana 14:28).
|
GAZETI LA GOOD NEWS (HABARI NJEMA), JULAI 1974 JE, YUKO
WAPI MUNGU BABA KWENYE AGANO LA KALE? Ni kweli, Lakini hebu na tupate uhakika. Je, alikuwa ni Yesu
Kristo gani mwana wa “na nguvu zake Aliye juu
zitakufunika kama kivuli;” malaika alimwambia
Mariamu kabla hata Jesu mimba yake haijatungwa kwamba “kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa
kitakatifu, Mwana wa Mungu … Huyo atakuwa mkuu,
ataitwa Mwana wa Aliye juu,” (Luka 1:35,32).
Luka 8:28 na Marko 5:7 zinathibitisha kuwa Yesu ni
“Mwana wa Mungu Aliye Juu Sana” na Mwana wa Mungu Aishie Juu Sana”. Baba ametajwa mara mbili
zaidi kwa jina hili kwenye Agano Jipya—Matendo 7:48 na 16:17. Ni nani basi Yesu anayetuambia tumuombe dua zetu? Ni
Baba (Mathayo 6:9). Na ni nani ambaye Daudi alikuwa anamuomba? “Nitamwita
MUNGU Aliye juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu.” (Zaburi 57:2). Na tena “Nitamshukuru Bwana
kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu” (Zaburi 7:17). Ndiyo, inawezekana kuwa kwa hakika Daudi alimjua Yule
ambaye hatimaye atakuwa Baba (kumbuka, asingeweza kumuitwa Baba na huku akiwa
bado hajawahi kuwa na Mwana. Melkizedeki, YHVH alikuwa hajawa Mwana bado).
“Neno la Bwana [YHVH] kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata
niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako” Zaburi 110:1; Waebrania 1:13 Daudi aliimba, “Bwana alipiga radi toka mbinguni, Naye
Aliye juu akaitoa sauti yake” (IISamweli 22:14). |
Je, Musa pia alilijua hilo? “Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya hesabu…” Kumbukumbu la
Torati 32:8). Nebukadneza mpagani kwa hakika asingeona ni vigumu
kuwaamini washiriki wawili walio mbalimbali lakini pamoja kwenye familia ya
Mungu. Wababelonia waliabudu miungu mingi sana ya uwongo. Baada ya
Nebukadneza kusababisha watu watatu
wafungwe na watupwe kwenye tanuru la moto, hatimaye alichungulia ndani na
kuwaona “Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa,
wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni
mfano wa mwana wa miungu.” (Danieli 3:25-26). Nabii Danieli aliona kinabii kurudi kwa ufufuo na kupaa
mbinguni kwa Kristo na kwenda mbinguni kwa Baba ili akaupokee Ufalme (pia
soma Luka 19:11,12,15): “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja
aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo
mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa
mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na
lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita
kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa” (Danieli 7:13-14). Huyu “Mzee wa Siku” anayetajwa
hapa anamaanisha ni Baba ingawaje kwenye aya ya 9 inaonyesha kuwa Mwana
anaweza pia kuitwa “Mzee wa Siku” sawa tu na anavyoweza kuitwa Wamilele [YHVH]. Huenda hata manabii wanaweza kuwa na fununu kidogo
zinazoonyesha kuwa Mungu alijulikana kama familia: “Ni nani aliyepanda mbinguni
na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani
aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za
nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?” (Mithali
30:4). ---Lawson Briggs |
P3 Mpendwa wa Alabama anauliza: “Je, Yesu ni Mungu? Na je, Yesu ndiye Yahova Baba wa
Milele? Je, kuna Mungu mwingine zaidi ya huyu Mmoja? Tafadhali Nifafanulie.” Maswali haya ili kuyajibu kwa kina yanahitaji makala
iandikwe ukurasa mzima. Na makala kama hiyo itayaonekana ikiendelezwa kwenye
nakala zijazo za Gazzeti hili la PLAIN TRUTH. Jibu litakalotolewa kwenye
kipande hiki cha makala litakuwa ni fupi na litakosa maelezo ya kina
kufafanua. Ndiyo, Yesu ni Mungu, vinginevyo asingeweza kuwa
Mwokozi wa wanadamu.1). Iwapo kama Yesu angekuwa ni mwanadamu tu basi kifo
chake kingekuwa cha kutoa dhabihu ya kulipa deni la adhabu ya kumfanya
mwanadamu mmoja aliyeichukua adhabu ya kosa kwa kuvunja au kuiasi Torati ya
kiroho ya Mungu. Kwa kuwa ni Mungu Baba ndiye aliyeumba vitu vyote kupitia
kwa Yesu Kristo. (Waefeso 3:9) na kwa kuwa vimhusuvyo mwanadamu
viliyanywa na Yesu Kristo (Yohana 1:1-5 pamoja na aya ya 14; na aya ya 10;
1Wakorintho 8:6; Wakolosai 1:12-19). Yeye ndiye Muumbaji na kwa hiyo ni
Mungu, na maisha yake aliyoyatoa yana thamani kubwa kuliko kiasi chochote cha
mlinganisho wa ya wanadamu wote. (2). Maisha pekeyake yanaweza kuanzisha maisha mengine. Hii ndiyo kanuni ya ki-Biokemia kwa
kuwa Uzima wa Milele ni ZAWADI kutoka kwa Mungu, basi ni Mungu tu mwenye kuwa
na uweza wa kutokufa ndiye
anayeweza kuutoa uzima huu. Na kama Yesu angekuwa ni mwanadamu tu, basi
tusingeweza kuupata uzima wa milele kupitia kwake na asingeweza kuwa Mwokozi.
Wanadamu hawezi kuwa na uzima wa milele ndani yake mwenyewe, lakini kama
Mungu alivyo kuwa “Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo
hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake” (Yohana 5:26 na 1Yohana
5:11-12). Kwa upande mwingine lakini, Yesu ni mwanadamu pia. Kwa
kuwa ni mwanadamu ndiye aliyeziasi Sheria za Mungu ambaye yuhai wakati wote
((Yohana 1:1-2) ndipo kwa kweli alifanyika
kuwa mwanadamu katika mwili (aya ya 14). Yeye aliyekuwa Mungu hakika akafanyika kuwa mwanadamu mwenye mwili
(1Yohana 4:2-3). Alitungwa mimba na kuzaliwa na bikira Mariamu (Mathayo 1:18,
16, 23; na 2:2). Hakufanyika kuwa mwili tu, bali alifanyika pia kuwa mwanadamu kimwili na damu. (Waebrania 2:14). Yesu aliijiita mara kwa mara kuwa ni Mwana wa ADAMU, na
pia Mwana wa MUNGU, (Mathayo 16:13-17). Yuko SAWA na Mungu (Wakolosai 2:6). Aliitwa Mungu (Yuda 1:24-25; Tito
2:10,13). Kwa hiyo yeye ni Mungu.
Biblia ina nukuu nyingi kuhusu jambo hili na zilizo hapo juu ni chache tu
kati ya nyingine nyingi zinazoshuhudia. Ndiyo, Yesu ni “Yehova” ingawaje neno hili
limetafsiriwa vibaya kwenye Biblia ya Kiingereza ya Reversed Version. Jina
asilia la Kiebrania lina consonanti “YHVH”. Lilipoandikwa kwa Kiebrania,
vokali ziliachwa na zilisikika kwenye matamshi tu. Kwa hiyo, jina hasa
lilikuwa halijulikani. Bali kwa leo inadhaniwa kuwa lilikuwa ni “Yahwe”. Maana yake kwa Kiingereza ni
“WAMILELE” au “MWENYE KUISHI MILELE” au “ANAYE KUISHI NA KUDUMU KWA UWEZA
WAKE MWENYEWE PASI KUTEGEMEZWA”. Ilistahili kuwa “Yahwe”, au |
GAZETI LA PLAIN TRUTH (UKWELI
MTUPU), Februari 1950 Je, Yesu ni Mungu? ni kama ilivyozoeleka kuitwa “Yehova”, au ni kama
ilivyoandikwa kwenye Biblia ya Authorised Version “BWANA” wa Agano la Kale ni
Mungu Baba wa Yesu Kristo. Haya ni makosa makubwa
sana! “Yahwe
alikuwa ni Mungu wa Israeli. Na ndiye aliyekuwa anajulikana kuwa ni Mungu
pekee kwenye ibada za Israeli. Wao hawakumjua Mungu Baba. Kwenye Mwanzo 1 jina la Kiebrania lililotumika
kutafsiri jina “Mungu” ni “Elohim”. Hili ni jina lenye umoja wenye muunganiko na
wengi ndani yake kama tunavyotaja “kanisa” au “familia”. Kanisa na familia
vinajumuisha watu wengi ndani yake, zaidi ya mmoja, lakini bado linaitwa
kanisa au familia moja. Kwa mtazamo wa aina hii jina “Elohima” linaashiria
wote wawili, Mungu Baba na Yahwe ambaye ni “Logos” au NENO la Mungu ambaye
kwao Roho anatokea, Roho Mtakatifu ambaye ni UZIMA, KITU HALISI na UWEZA wa
Mungu. Yesu analipokuwa akiliombea
Kanisa alisema kwamba waumini wake wote wawe “kitu KIMOJA” (Yohana 17:11,
21). Kanisa ni Mwili MMOJA, lakini limeundwa kwa waumini wengi (1Wakorintho
12:12). Na mume na mke ni MWILI MMOJA, lakini wanaonekana kuwa ni watu wawili
walio mbalimbali. Kwa hiyo Kristo na Mungu Baba ni Mungu MMOJA, na sio Miungu miwili, na—“ELOHIM” Mmoja. Na ndio maana Elohim
alisema “NA tumfanye mtu kwa mfano WETU” (Mwanzo 1:26). Yahwe alikuwa ndiye “NENO” au
msemaji wa ofisi ya Uungu—mshiriki wa pili. Mara tu baada ya Mungu kuanza
KUONGEA na wanadamu, ilikuwa ni yuhu “Yahwe” ndiye aliyekuwa akiongea nao
(imetafsiriwa “BWANA” kwenye tafsiri ya Authorised na “Yehova” kwenye tafsiri
ya Revised Version). Tazama kwenye Mwanzo 2:16, 18, nk, na pia tazama kwenye
Kutoka 20:2, nk—kila mara inasema “Yahwe” kwenye tafsiri asilia ya Kiebrania
“NENO” aliyefanyika mwili. Ili kuthibitisha hili kunahitaji masomo ya kina na
yatakayogharimu kurasa nyingi kwa mamia ili kuthibitisha hili. Ili kuthibitisha kiufupi,
fananisha na Isaya 6:1-3 na 10 na Yohana 12:39-41; Isaya 8:13 na 1Petro
2:7-8; Isaya 40:3 na Mathayo 3:3 na Marko 1:3. Yohana alitengeneza njia kwa
ajili ya “Yahwe” (Isaya 40:3) ambaye ndiye Kristo (Marko 1:12-15) kwenye
Ufunuo 1:17, 8 na 22:13, Yesu Kristo (pia tazama Ufunuo 22:16 kwa uthibitisho
kuwa alikuwa ni Yesu aliyekuwa anasema) alijiita kuwa yeye ni “Alfa na Omega,
Mwanzo na Mwisho, wa Kwanza na wa MWisho”. Kwenye aya zilizo kwenye Isaya
44:6 na 48:11-12, (aya za 17-18 zinaonyesha kuwa ni Yahwe aliyekuwa akinena)
na Isaya 41:4, YAHWE ni wa Kwanza na wa Mwisho |
Kwenye 1Wakorintho 10:1-4
“MWAMBA” wa Agano la Kale ulikuwa ni Kristo. Kwenye Kumbukumbu la Torati
32:3-4; IISamweli 22:2-3, 32; na Zaburi 18:1-2; “MWAMBA” huu huu ni Yahwe.
Wakati Musa alipokuwa anaongea na YAHWE, na kumuuliza jina lake, (Kutoka
3:4-5, 13), alimjibu kuwa jina lake ni MIMI NIKO (aya ya 6 na 14) na YAHWE (aya ya 15). Pia tazama
Kutoka6:2-3. Kwenye Yohana 18:5-8, mara tu baada ya Yesu kujitambulisha kwa
makutano walioongozwa na Yuda kuwa yeye ni “MIMI NIKO” (kiponauni cha “yeye”
kwenye uandishi mlalo kimeongezwa pasipo uvuvio, na hakikuwepo kwenye nakala
asilia za mwanzoni), ndipo walirudi nyuma na kuanguka chini. Tena kwenye
Yohana 8:56-58, Yesu aliijiita mwenyewe “MIMI NIKO”. Pia kwenye Ufunuo 1:10
na mahali pengine. Mtu mwenye Uungu ambaye ndiye MKOMBOZI wetu ni
Yesu Kristo (Yohana 4:42, Wagalatia 3:13, Wafilipi 3:20, Tito 2:10-14, Luka
1:58-59, nk, nk. Yesu Yule ndiye YAHWE, tazama kwenye Isaya 49:7; Isya 60:16;
ambapo panasema pia kuwa yeye
“Mwenyezi wa Yakobo”—(kwa hiyo, kuwa ni WA Yakobo kunamaanisha mwana, au uzao
wa Yakobo)—Mwenyeenzi wa wana wa Yakobo. Pia kwenye Isaya 48:17 inasema YAHWE
ndiye Mkombozi, na Mtakatifu wa Israeli—Ndiye
aliye Mtakatifu wa Israeli! Ni sawa na ilivyoelezewa kwenye Isaya 43:14.
Kumbuka pia aya inayofuatia (15), YAHWE ni Mtakatifu wa Israeli, Muumbaji wa
Israeli, Mfalme wa Israeli. Sasa tega usikivu wako kwenye Matendo 3:14 ambako
ni Kristo waliomkataa Wayahudi alikuwa ni huyuhuyu “MTAKATIFU—YAHWE! Pia tazama Matendo 2:27 na Marko 1:24. Je, Daudi mchungaji alikiwa ni nani?—Zaburi 23:1,
YAHWE. Kwenye Yohana 10:11, Yesu alisema kuwa yeye alikuwa ni mchungaji. Pia
Waebrania 13:20, na 1Petro 2:24-25, na 5:2-4. Ni YESU KRISTO anayekuja tena
Kimwili na akiwa Mfalme wa Wafalme kutawala, kuja KUYAFANYA MAMBO YOTE UPYA,
(Ufunuo 19:13, 15; 17; 14; 1:5; na Matendo 3:20-21). Mchungaji Mkuu anayekuja
KUTAWALA akiwa kama MFALME wa Mfalme wote ni YAHWE—Ezekieli 34:11, 30-31; na
sasa weka mtazamo wako kwenye Isaya 2:1-4 na Mika 4:1-4— Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana
[YAHWE] utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu
wa mataifa watauendea makundi makundi.Na mataifa mengi watakwenda na kusema,
Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu ‘YAHWE] wa Yakobo;
naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana
katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu Naye atafanya
hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu
walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu;
taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena
kamwe. Bali
wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana
mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimesema hivi. |