Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[080]
Hukumu ya Mapepo
(Toleo
La 4.0
19941203-20060625-20100606)
Jarida hili linaelezea kuhusu kipindi cha mwishoni mwa utawala wa millennia
wa Kristo wakati mapepo yatakapohukumiwa kwa makosa waliyowafanyia wateule kwenye
kipindi cha mwisho wa Milenia. Mchakato wa hukumu unamambo fulani ya kushangaza
yatakayohitimisha kwayo yanayohusu hukumu na adhabu watakayopewa mapepo kwa
mtazamo wa kwamba mwingiliano holela wa asili na sifa au heshima ya Mungu.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki © 1994, 1999, 2006, 2010 Wade Cox)
(Tr. 2013)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Hukumu ya
Mapepo
Malaika wa
Makanisa ya Mungu
Muundo wa ujenzi
wa Hekalu unatuambia mengi kuhusu mtazamo wa kisayansi ya kiilimwengu au
cosmolojia ya Kiebrania kuhusu ulinzi wa sayari na ambao umepelekea kuwapa
wajibu malaika na hukumu. Kwa mfano, kwenye Ezekieli 41:18-19, wanaonekana
makerubi kuwa wako wa aina mbili, kama vile mwenye kichwa cha mwanadamu na
mwenye kichwa cha samba au Æon.
Kwa hiyo
maeneo mawili yanayodhibitiwa na viumbe hai wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha
Mungu, yamepewa wajibu mkubwa wa kusaidia maendeleo ya Israeli kwa mujibu wa
nabii Ezekieli, walionekana kuwa ni mfumo wa kimalaika au kibinadamu, ambao
kwamba Shetani alikuwa ndiye Yule kerubi wa kwanza mwenye mbawa zinazofunika na
pia ni mfumo wa Æon, sehemu ya kile ninachoonekana kuwa aliuasi. Jambo hili
limeongelewa sana kwenye kitabu kisemacho Tatizo
la Uovu na Imani za Siri (The
Problem of Evil and Mysticism).
Huyu kerubi aliyefunika mbawa anaaminika kuwa Elohim bali wanajulikana pia kama
Malaika. Malaika wa YHVH pia alijulikana kama Masihi (tazama majarida ya Malaika wa YHVH (Na. 24) na Mungu Tunayemwabudu
(Na. 24) The Angel of YHVH (No. 24) and [The God We Worship (No. 2)]. Kitabu cha Ufunuo kinaonekana kumtaja Masihi
kama Malaika pia. Kwenye Ufunuo 1:1 Malaika anatoa ujumbe au Ufunuo, ambao
unatoka kwa Mungu akapewa Kristo.
Kwenye Ufunuo
1:10-20 inaonekana wazi kabisa kwamba Kristo ndiye anayetajwa kuwa ndiye
anayeufafanua ule ujumbe. Ngazi za kimadaraka zinaonyesha kwamba Kristo ni
Malaika au Kichwa cha Makanisa ya Mungu. Kila moja ya makanisa haya
madogomadogo, ambayo idadi yake yako saba yaliwakilishwa na alama ya kinara cha
taa, kinachowaka kwa kutegemea mafuta ya roho (Zekaria 4:2). Makanisa hayo saba
ni: Efeso,
Smirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia, na Laodikia. Yanasimamiwa na Malaika wadogo ambao
waliandikiwa na kupewa zile nyaraka za Ufunuo 2 na 3. 1Timotheo 5:21 pia
panaonekana kugusia kuwataja Malaika wa Makanisa ambayo Mtume Paulo anasema
kuwa:
Nakuagiza mbele za
Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo
pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.
Ni kweli kabisa
kwamba Mtume Paulo hapa anawajumuisha maaika wema na watiifu kuwa ni sehemu ya wateule
na kwamba ahadi inaendelea hadi kwenye muundo wa wote wawili yaani wanadamu na
malaika.
Waandishi wa
mambo ya kidini wanaamini kwamba kulikuwa na malaika msimamizi wa makanisa
haya. Nao ni pamoja Origen (Hom. Aliye kwenye Luka 13:23), Gregory wa Nazianzus
(Or. 42), Basil (Linganisha na Isaya 1:46), Gregory wa Elvira (Tract.16),
Hyppolytus (De Antichr. 59), na Eusebius (Linanisha na Zaburi 47:50). Ili kujua
kwa kina angalia pia kitabu cha Jean Danielou, cha Malaika na na Shughuli zao [The Angels and their Mission),
(Westminster, Md, kilichochapishwa na Newman Press, 1953)] na kitabu kingine
cha Wink, T, cha Uweza au The Powers, Vol. 2: na kingine cha
‘Unmasking The Powers’ (Fortress Press, Philadelphia, 1987 p. 192). Kwa
bahati mbaya sana, teolojia ya kipatristiki hatimaye imekuwa na mwingiliano
mkubwa na Mafundisho ya Dini za Siri ambazo kwenye kipondi cha Gregory wa
Nazianzus, elimu ya cosmolojia ilienezwa ikijumuisha na mafundisho ya roho na
mizimu, pamoja na mafundisho ya kwenye kwenye Yerusalemu ya Mbinguni (Or. 32 na
pia Basil Ep. 2.238).
Imani ya kuwa na
malaika mlinzi na wakuwaongoza wanadamu imeenea sana na inaingia akilini na
kuaminika. Maelezo kamili ya mgawanyo wa uweza au mamlaka za malaika yametolewa
kwenye kitabu cha Wink, cha The Powers, Vols. 1 na 2 (hususan Vol. 2);
na cha Wagner et. al., Territorial
Spirits (Sovereign World Limited, UK, 1991); na cha Dickason, cha Angels
Elect and Evil (Moody Press, Chicago, 1975). Dhana ya kuwa dunia
imegawanywa kwenye mamlaka yaliyo chini ya mamlaka za malaika ilienea na
kuaminiwa sana sio kwa Waisraeli peke yao na Agano lao, bali hata na mataifa ya
Wamataifa waliamini hivyo pia. Wink anasema hilo pia (n. 11 on ukurasa 196)
kwamba:
Mfalme Julian (d.
363) akiwa kwenye umri mkubwa sana alisema akiamini kwamba wanadamu wote wana
tabia mbalimbali, na lugha, na sheria au kanuni, zinazoendana na roho za wale
waliowatangulia. ‘Iwapo kama kuna mungu wa taifa anaowatangulia, na chini yake
kuna malaika na pepo na shujaa na kikundi fulani cha roho zilizoko pamoja
zikiwa kama wasaidizi na wakala wa nguvu kuu zilizo nyuma yake, hawakufanya
lolote la tofauti kwenye sheria na mataifa, sasa niambie, ni kigu gani zaidi
kilichafanywa na hivi vyote? (Jarida la Kinyume au Dhidi ya Wagalilaya (Against the Galileans 143 B).
watu jamii ya Demiurge 'wamewatenga watu kwa mlinganisho wa miungu mbalimbali,
ambao kazi yao kubwa ni kuyaangalia mataifa na kuyalinda mataifa mbalimbali na
miji yake. Kila mmoja wa miungu hii anatawala kwenye eneo lililomuangukia
kimgawanyo na lillyosawa na asili yake ilivyo. Kila taifa inafanya mambo yake
ama utamaduni wake sawa na jinsi linavyoongozwa na ungu anayelitawala’ (ibid., 115D).
Imani hii ya
kuamini kuna Jeshi la mbunguni linalotulinda
ni ya kale sana. Walinzi ('îyr)
lilikuwa ni jina walilopewa Jeshi la malaika kutokana na imani ya kidini au
walinzi wa Kikaldayo (Danieli 4:13,23), na pia alipewa
mtu anayetoa amri ya kufanya mambo yaliyo kwenye taratibu za kisheria (Danieli
4:17; ila usichanganye na yaliyoandikwa kwenye Yeremia 4:16). Kristo anatajwa
kuwa ni Kiumbe aliyewezesha uweza na mamlaka ya Viumbe hawa.
Malaika Mkuu
Mikaeli anatajwa kuwa ni Malaika au Mfalme Mkuu (sar) asimamaye kwa upande wa
Israeli (Danieli 12:1). Uelewa ulikuwa ni kwamba Israeli walikuwa wamechaguliwa
na kusimama peke yao kati ya mataifa. Andiko
lililoko kwenye Walawi 5:6 linasema (Malaika wa YHVH, ambaye baadhi ya
makundi wamemtambilisha kama Mikaeli):
Mimi ni malaika
anayeliombea mataifa la Israeli ili wasipigwe na kuangamizwa kabisa, na kila
roho chafu inayoishambulia (APOT) (pia kumbuka alivyoandika Wink, ukurasa wa
197).
Muundo wote mzima
wa kiroho wa dunia ulisimama kinyume na taifa hili teule, kadiri mungu (theos) wa dunia
hii, Shetani Azazeli, na Jeshi lake lote lililoasi waliotupwa hapa duniani na wakiyamiliki
na kuyaongoza mataifa, ambako waliruhusiwa wakae wakiwa chini ya Mwenyeji wao
wa kwanza kuasi tangu uumbaji Adamu. Hii ndiyo maana ya iliyomaanisha lile neno
mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Haikuwa
na maana ya ujuzi tu bali ilimaanisha uwezo wa kaamua kufuata mwelekeo gani.
Origen analijua hili. Origen aliamini kwamba malaika wa mataifa wangeweza
kuongoka.
Ikiwa mwanadamu
anaweza kuheshimu na kupita kutoka kwenye upotoe na kutoamini na kuwa mwamini,
ni kwa nini basi tunasitasita kusema kilekile kuhusu Uweza? Kwa upande wangu,
nathani kwamba imekuwa ikitokea wakati mwingine baadhi ya hawa wenye Mamlaka
kuongoka Kristo alipokuja, na ndiyo maana baadhi ya miji na hata mamataifa yote
walimkubali na kumwamini Kristo kwa utayari sana kuliko mengine (Wink, p. 197
sawa na ukilingan9isha na Yohana 18:59).
Origen anaamini
kuwa Yule mtu wa Makedonia
aliyemtokea Mtume Paulo kwenye maono akimuoma amsaidie kwenye Matendo 16:9
alikuwa ni Malaika wa Makedonia aliyekuwa anahusika na kuwajibika kuwapatia
mahitaji yao yote mema ya kila namna (Hom. Kwenye Luka, 12). Na Origen anaamini
hapa kama hivit:
Kabla ya kuzaliwa
kwa Kristo malaika hawa walikuwa na maana ndogo kwa wale walioamriwa
wawahudumie na mambo yao yalikuwa hayakubaliki na kufuatiliwa kwa mafanikio.
Daniélou
ameandika kwa kina sana kwenye kitabu chake chenye kichwa cha somo (The
Angels and Their Mission, (Malaika na Kazi Zao), Westminster, Md, Newman
Press, 1953, pp. 15ff., 232: na chanzo kingine ni Les
sources juives de la doctrine des anges des nationes chez Origène, Recherches de Science Religieuse 38
(1951, pp. 132-137).
Toba
watakayoifanya Malaika hawa waasi ni kipindi kikuu sana kwenye swali la Uweza
wa Mungu wa Kujua Kila Jambo. Mawazo ya Origen kuhusu tukio hili na nafasi ya
hawa Malaika waasi kutubu na kuongoka yanachukuliwa kuwa yana maana iliyo
sahihi katika mwendelezo wa falsafa ya Biblia. Jambo hili limeelezewa kwa kina
kwenye kitabu kinachoitwa The Problem of
Evil (Tatizo la Uovu). Mtazamo na kinachoelezwewa kwenye Biblia ni kwamba
ni Shetani tu ndiye atakaye hukumiwa (1Wakorintho 6:3). Ishara ya anguko la
Adamu hasajasa inaonekana kwenye Mwanzo 3:15 wakati nyoka alipowadanganya
akijichanganya na mwanadamu, akijifanya kuwa sio miongoni mwa Malaika waasi na
akamdanganya kwanza mwanamke na kumpotosha. Andiko hili linaendelea kueliezea
tukio hili ikitumia nafsi ya umoja kwa wanamke (hapa inadhaniwa kwamba ilikuwa
inamhusisha na kumtaja Masihi) kuwa ndiye kisigino cha wanadamu na kichwa cha
huyu nyoka kita pondwa kwa miguu au kwato
na (SHD 7779) inafasiri maana yake
kuwa kukiachanisha, au kukichoma kwa lugha ya mfano ni kukikomesha na kukishinda kabisa kwa:-
kukivunja, kukiponda au kukifunika. Kisigino
cha mwanadamu kinaumia na kichwa cha huyu joka kimepondwa. Lakini huyu
mwanadamu hajaumia maumivu ya kudumu. Neno lililotumika halionyeshi dalili ya
kukomesha au kumuondolea mbali mtu mmoja dhidi ya mwingine. Kwahiyo mgawanyo
unaweza kusuluhishika na Malaika (pengine zaidi kuliko kwa Shetani) hata
akitubu.
Hukumu ya
Malaika
Kuhusu mhusika
atakayewahukumu hawa Malaika umekuwa ni mjadala uliodumu kwa muda mrefu sana.
Wakristo wa leo hawaelewi mlolongo sahihi wa hukumu ya hawa Malaika waasi, kwa
sababu ya kutouelewa mchakato mzima wa kifo na ufufuo nay a uzima wa milele, wa
wote wawili yaani wa wanadamu na wa Malaika. Wakristo wa leo wamejikuta
wakiangukia kwenye makosa makubwa kutokana na kulitafsiri vibaya andiko la
1Wakorintho 6:2-3.
1Wakorintho 6:2-3 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu
ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata
hukumu zilizo ndogo? 3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana
mambo ya maisha haya?
Je, ni malaika
wapi wanaokwenda kuhukumiwa? Kwa mujibu wa andiko hili inadhaniwa kwamba
Malaika watiifu wanaotajwa tu hapa na kwamba mapepo hawawezi kutubu. Hii sio
kweli kabisa. Hukumu inaweza kuwahusu tu Malaika walioasi na hawawezi kuwa wale
watiifu kwa Mungu.
Ni lini
tunapowahukumu basi? Haiwezikuwa ni mwanzoni mwa kipindi cha Milenia kwa kuwa
tutakuwa hatujafanya lolote na wanaweza kuhukumiwa tu kwa matendo yetu tukiwa
kama wana wa Kiroho wa Mungu. Hii inamaana kwamba wanasehemu kwenye Ufufuo wa
Pili wa wafu. Na hapa ndipo tutakapowahukumu. Kama watakuwa wamekwisha hukumiwa
basi itakuwa ni kinyume chake.
Kwenye awamu ya
kwanza ya Ukristo toba ilikuwa ni kitu cha lazima kufanywa. Tendo la kuangukia
au kutupwa kwa Malaika kuzimuni lafaa lifafanuliwe kwa kuzingatia maelezo
yafuatayo.
Isaya 14:1-32 inasema: Maana
Bwana atamhurumia Yakobo, atamchagua Israeli tena, naye atawaweka katika nchi
yao wenyewe; na mgeni atajiunga nao, nao wataambatana na nyumba ya Yakobo. 2 Na hao mataifa watawatwaa na kuwaleta mpaka mahali pao
wenyewe, na nyumba ya Israeli watawamiliki, na kuwafanya watumishi na wajakazi
katika nchi ya Bwana; nao watawachukua hali ya kufungwa watu wale waliowafunga
wao, nao watawamiliki watu wale waliowaonea. 3 Tena
itakuwa katika siku ile, ambayo Bwana atakupa raha baada ya huzuni yako, na
baada ya taabu yako, na baada ya utumishi ule mgumu uliotumikishwa; 4 utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na kusema,
Jinsi alivyokoma mwenye kuonea; Jinsi ulivyokoma mji ule wenye jeuri! 5 Bwana amelivunja gongo la wabaya, Fimbo ya enzi yao wenye
kutawala. 6 Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu, Kwa
mapigo yasiyokoma; Aliyewatawala mataifa kwa hasira, Ameadhibiwa asizuie mtu. 7 Dunia yote inastarehe na kutulia; Hata huanzilisha kuimba.
8 Naam, misunobari inakufurahia, Na mierezi ya
Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti
aliyetujia. 9 Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili
yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio
wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao
vya enzi. 10 Hao wote watajibu na kukuambia, Je! Wewe
nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi! 11
Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza
wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. 12 Jinsi
ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi
ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe
ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu
kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za
mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu,
Nitafanana na yeye Aliye juu. 15 Lakini
utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo. 16 Wao
wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye
aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme; 17 Aliyeufanya
ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?
18 Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima,
Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe; 19 Bali wewe
umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Kama vazi
la wale waliouawa, Wale waliochomwa kwa upanga, Wale washukao mpaka misingi ya
shimo; Kama mzoga uliokanyagwa chini ya miguu. 20 Hutaungamanishwa
pamoja nao katika mazishi, Kwa maana umeiharibu nchi yako, Umewaua watu wako;
Kizazi chao watendao uovu hakitatajwa milele. 21 Fanyeni
tayari machinjo kwa watoto wake. Kwa sababu ya uovu wa baba zao; Wasije
wakainuka na kuitamalaki nchi, Na kuujaza miji uso wa ulimwengu. 22 Nami nitainuka, nishindane nao; asema Bwana wa majeshi;
na katika Babeli nitang'oa jina na mabaki, mwana na mjukuu; asema Bwana. 23 Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungu, na maziwa
ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema Bwana wa
majeshi.
Maandiko yaliyotiwa wino mzito yanabeba
ujumbe wa kupunguzwa kwa Shetani kwenye kima cha shimo. Ukweli ni kwamba
alitupwa kaburini kwake (kaburini)
kama tawi lisilotakiwa (aya ya 19,
Biblia ya Interlinear Bible). Mzoga uliokanyagwa kwa miguu unaoelezwa hapa
uliandikwa peger kwenye kamusi ya (SHD 6297), ambao unamaanisha mzoga mtepetevu uliooza, wa ama wa
mwanaume au wa mnyama na kwa lugha ya fumbo inamaanisha ni aina ya kitu
kilichutukuka sana cha ibada za sanamu. Kitu kiovu kinachotajwa hapa
hakijajumuishwa kwenye mazishi yanayodaiwa kufanywa kwa sababu ya maovu.
Amefananishwa na mfalme wa Babeli (maana
yake ni machafuko na dini za ulimwengu) lakini ni Lusifeli, Nyota ya Mchana
ambaye anatajwa kama (kwenye aya ya 4). Na watu watamtazama na kusema; Je, huyu ndiye
yule MTU aliyeitetemesha dunia (aya ya 16). Amekufa na hajalazwa kwenye kaburi lake.
Hakujumuishwa na wafalme wa dunia kwenye mazishi kwa sababu alikuwa ameiharibu
dunia na kuwauwa watu (aya za 17-20). Hii inaweza kuwa ni vita tu ya mwishoni
mwa Milenia wakati dini yote alitoianzisha na kuishamirisha itakuwa imekomeshwa
sambasamba na “watoto” wake (aya ya 21). Andiko linaonyeha kuwa ni Bwana ndiye
atakayeyakomesha mataifa na bwana atawajibu wajumbe wa mataifa na watu wake
watafut mahali pa kukimbilia. Anaongelea kuhusu kushughulikia wenyedhambi siku
ya hukumu.
24 Bwana wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu
kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo
itakavyotokea; 25 kwamba nitamvunja huyo Mwashuri vipande vipande
katika nchi yangu, na juu ya mlima wangu nitamkanyaga chini ya miguu yangu;
ndipo nira yake iliyo juu yao itakapoondoka, na mzigo wake utatoka mabegani
mwao. 26 Hilo ndilo kusudi lililokusudiwa duniani mwote, na
huo ndio mkono ulionyoshwa juu ya mataifa yote. 27 Maana Bwana wa
majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni
nani itakayeugeuza nyuma? 28 Ufunuo huu ulikuja mwaka ule alipokufa
mfalme Ahazi. 29 Usifurahi, Ee Ufilisti, pia wote, Kwa sababu fimbo
ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, na uzao
wake ni joka la moto arukaye 30 Nao walio maskini kabisa watakula, Na
wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako
watauawa. 31 Piga yowe, Ee lango; lia, Ee mji; Ee Ufilisti, pia
wote, umeyeyuka kabisa; Maana moshi unakuja toka kaskazini, Wala hakuna
atakayechelewa katika majeshi yake. 32 Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani?
Ya kuwa Bwana ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika
watu wake wataona kimbilio.
Ili
kushughulika na hukumu ya mapepo wanatakiwa wapunguziwe kwa wanadamu, waliokuwa
amekufa na akawafufua na kuwapa miili wakawa hai hata kwenye Ufufuo wa Pili wa
wafu. Hawa ndio watakaohukumiwa kwa hukumu ya Krisis au ya jumla ya wote na
Roho Mtakatifu kwenye ubatizo. Dini na mifumo yao ya zamani na maroho
zitatumika kuanzisha kumbukumbu za Ziwa la Moto.
Watapewa majina mapya na kufanywa upya kama wana wa Mungu kwa Roho
Mtakatifu kama walivyokuwa huko mwanzoni kabla ya anguko lao. Mpango wa Mungu
ni mkamilifu na haubadiliki.
Malaika waasi
wote watatupwa hapa chini kwenye shimo. Baadhi ya mapepo hawa watatolewa nje ya
shimo hili kwa kitambo ili wawadanganye wanadamu. Kujaribiwa huku kumelengwa
wafanyiwe wateule.
Mapepo wanamtii
Kristo na wateule tangu walipochaguliwa na kutumwa wale wanafunzi sabini (Luka
10:1,17-20).
Luka 10:17-20 Ndipo
wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa
jina lako. 18 Akawaambia,
Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. 19 Tazama,
nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala
hakuna kitu itakachowadhuru. 20 Lakini,
msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu
yameandikwa mbinguni.
Kwa mujibu wa
maandiko haya, anguko la Shetani limetajwa. Mapepo wana namna viwango mbalimbali
vya kujisikia uhuru.
Mathayo 8:28-32 Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya
Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali
mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. 29 Na tazama,
wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa
kabla ya muhula wetu? 30 Basi, kulikuwako mbali nao
kundi la nguruwe wengi wakilisha. 31 Wale pepo
wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la
nguruwe. 32 Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia
katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata
baharini, wakafa majini.
Maandiko
yaliyo kwenye Mathayo 8:28-32 na kwenye Marko 5:1-17 mara nyingi yanaonekana
kama yanajichanganya, bali kwa kweli haya ni matukio mbalimbali tofauti. Moja
linawahusisha watu wawili na linguine linamhusisha mtu mmoja. Idadi ya mapepo
ni kubwa. Kwenye matukio yote mawili mapepo wanaamriwa waende wakawaliingie
kundi la wanyama najisi na wanyama wanakufa. Kristo alifanikisha malengo mawili
kwa kushughulika kwake na mapepo hapa. Aliwatumia mapepo kwa kuwakinga Israeli
na wanyama najisi na kuwaondolea mapepo au roho chafu pia. Kwenye ukemeaji wake
wa kwanza roho hawa wachafu walijua kuwa walikuwa na kipindi kifupi sana na
walijua pia kwamba watakabiliwa na Kristo kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa
kipindi kile kilichowekwa. Na hapa kwenye Injili ya Marko tunaona kuwa ni mtu
mmoja peke yake aliyekuwa amepagawa na jeshi la mapepo na wanamsihi Kristo
asiwafukuze mbali na nchi ile. Kwa hiyo kulikuwa na namna nyingi mbalimbali
himaya waliyokuwa wamepangiwa.
Marko 5:1-17
inasema: Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. 2
Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka
makaburini, mwenye pepo mchafu; 3 makao yake yalikuwa
pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa
minyororo; 4 kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi
kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu;
wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Na
sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na
kujikata-kata kwa mawe. 6 Na alipomwona Yesu kwa
mbali, alipiga mbio, akamsujudia; 7 akapiga kelele kwa
sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha
kwa Mungu usinitese. 8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo
mchafu, mtoke mtu huyu. 9 Akamwuliza, Jina lako nani?
Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. 10 Akamsihi
sana asiwapeleke nje ya nchi ile. 11 Na hapo milimani
palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. 12 Pepo
wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. 13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia
katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia
baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. 14 Wachungaji
wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione
lililotokea. 15 Wakamwendea Yesu, wakamwona yule
mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile
jeshi; wakaogopa. 16 Na wale waliokuwa wameona
waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. 17 Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao.
Malaika
walioelezwa kuwa wataingia shimoni kuzimuni ni wale wenye uweza waliopewa na
Mnyama. Mashahidi wa nyakati za mwisho watapambana na nguvu za mapepo katika
siku za mwisho.
Ufunuo 11:1-14 inasema: Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja
akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo
humo. 2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala
usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi
arobaini na miwili. 3 Nami nitawaruhusu mashahidi
wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali
wamevikwa magunia. 4 Hao ndio ile
mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi. 5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao
na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. 6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe
katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na
kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo. 7 Hata
watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita
nao, naye atawashinda na kuwaua. 8 Na mizoga yao
itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri,
tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa. 9 Na watu wa hao
jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala
hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini. 10 Nao wakaao
juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa
wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi. 11 Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo
kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia
watu waliowatazama. 12 Wakasikia sauti kuu kutoka
mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui
zao wakiwatazama. 13 Na katika saa ile palikuwa na
tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba
wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza
Mungu wa mbingu. 14 Ole wa pili umekwisha pita, tazama
ole wa tatu unakuja upesi.
Mchakato wa zama
za Mataifa na kipindi cha maombolezo na ole cha miezi arobaini na miwili ni
kipindi hikihiki ambacho malaika wenye nguvu wane wataachiliwa watoke kwenye
shimo ili waue theluthi moja ya wanadamu. Malaika hawa waasi pia watakuwa na
malaika juu yao huko kuzimu shimoni.
Ufunuo 9:1-18
inasema: Malaika
wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi;
naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. 2 Akalifungua
shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa;
jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. 3 Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda
juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi. 4 Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi,
wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na
muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao. 5 Wakapewa
amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama
kuumwa na nge, aumapo mwanadamu. 6 Na siku zile
wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo
mauti itawakimbia. 7 Na maumbo ya hao
nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao
kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu. 8 Nao walikuwa na nywele kama nywele za
wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. 9 Nao
walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa
kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani. 10 Nao
wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi
mitano ilikuwa katika mikia yao. 11 Na juu yao
wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni,
na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.
Malaika wane
watasimama kwenye mto Frati, na wataachiliwa kwa kitambo kidogo katika siku za
mwisho. Hii ni vita ya
baragumu ya sita, itakayowaua theluthi ya wanadamu.
12 Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado
ziko ole mbili, zinakuja baadaye. 13 Malaika wa
sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za
madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu, 14 ikimwambia
yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne
waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati. 15 Wale
malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na
mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu. 16 Na
hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi;
nilisikia hesabu yao. 17 Hiyo ndivyo
nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii
kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao
ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na
kiberiti. 18 Theluthi ya wanadamu
wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho,
yaliyotoka katika vinywa vyao.
Mfumo huu wa
kidini utakaowajumuisha malaika kwenye himaya moja dhidi ya Jeshi la Malaika
ili kwamba uweza wao uzuiwe. Shetani hali kadhalika atakuwa ameingizwa na
kuzuiwa kwenye ahimo hili.
Ufunuo 20:1-15 inasema: Kisha
nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo
mkubwa mkononi mwake. 2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye
ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika
kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena,
hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
Kitu muhimu cha
kukijua hapa ni kwamba Shetani ametupwa kuzimuni kupisha utawala wa milenia wa
watakatifu. Nguvu hizi kwa mataifa ilizuiwa ila nguvu ile itarudishwa tena siku
au kipindi cha Milenia ili kushughulika na na mataifa. Tatizo kubwa sana kwa
mataifa kipindi hiki cha utawala wa Milenia itakuwa ni kwamba watakuwa na hali
ya kujiona wenye haki na watakatifu sana. Shetani ataachiliwa ili kuonyesha
kwamba wanahaki na kama walikuwa hovyohovyo pasi na utaratibu bila Roho na
walikuwa kwenye ushawishi wa kimaongozi na mwelekeo wa Malaika waasi.
Wateule watapewa
uongozi wa hii dunia na Kristo na hapa ndipo watafanya kazi ya kuhukumu. Wengi
wa wateule hawa wameuawa wakiwa mashahidi wa imani (Ufunuo 20:4).
4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu
yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya
ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule
mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso
zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka
elfu. 5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie
ile miaka elfu. 6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na
mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya
pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala
pamoja naye hiyo miaka elfu. 7 Na hiyo miaka elfu
itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8
naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu
na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya
watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. 10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika
ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao
watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
Wafu waliosalia
hawataishi hadi baada ya kipindi hiki cha miaka elfu kifike mwisho. Kwa hiyo,
hukumu itafanywa na wateule peke yao waliokuwa na sehemu kwenye Ufufuo wa
Kwanza. Hukumu ya mapepo na tendo la kumtupa Ibilisi (diabolos) kwenye Ziwa la Moto, pamoja na Mnyama na nabii wa uwongo
ni andiko gumu kueleweka. Mfumo wa kidini wa unabii wa uwongo sambamba na ule
wa mnyama vyote vitatupwa kwenye Ziwa la Moto pamoja na kifo, mauti na kuzimu
baada ya Ufufuo wa Pili wa wafu. Mambo haya yatakuja kuondolewa mbali pamoja na
wazo “dhana” au itikadi zake. Mambo haya yenyewe tu yanashughulikiwa sawa na
mpango wa Mungu.
11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na
yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao
hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama
mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine
kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo
yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa
wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika
kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
(imefafanuliwa kwenye jarida la Ufufuo wa Wafu (Na. 143) [The Resurrection of the Dead (No. 143)].
Azazeli mwenyewe ameikwisha hukumiwa tayari kama tunavyoona kwenye Yohana 16:10-13.
Yohana 16:10-13 kwa habari ya haki, kwa sababu
mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; 11 kwa
habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa. 12 Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini
hamwezi kuyastahimili hivi sasa. 13 Lakini yeye
atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa
maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena,
na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Hukumu ya Shetani alikusudiwa hasa kwa kuwahukumu Malaika walioasi. Shetani alishahukumiwa kwa matendo yake akilinganishwa na Kristo. Malaika waasi wanahukumiwa kwa matendo yao wakilinganishwa na wateule. Kila ngazi inahukumiwa kwa kuilinganisha na ngazi yake stahiki kwenye mpangilio wa wateule wakiwa chini ya Kristo. Hukumu ya Malaika hawa inajumuisha pamoja na kuondolewa kwenye nafasi ya mamlaka ambayo waliaminiwa na kupewa. Hata hivyo wao hawana la kufanya zaidi ya kuonekana wakirekebishwa na mchakato wa uongozi adilifu na marekebisho.
Katika maongozi sahihi na maelekezo, mapepo wanaweza kutubu. Upingaji wa kwamba hawawezi na kwamba wamekusudiwa kudumu kwenye mateso ya milele ni ya Kishetani na yanayolenga kufuta mawazo sahihi ya tabia za Mungu za Rehema na huruma na yanalenga kumfanya Mungu aonekane kuwa sio muumbaji mkamilifu.
Kwa uweza wake wa Kuelewa Kila Jambo Mungu alijua kwamba Malaika na wanadamu watatenda dhambi. Ingekuwa kwamba aliweka utaratibu ili kuwafanya Malaika wote waokolewe, basi utaratibu mzima usingekuwa na maana yoyote. Dhambi za Shetani zilikuwa ni kwa ajili ya kujihesabia haki na kujiona bora. Akataka ampindue Mungu na kuchukua cheo chake. Kristo akateuliwa ili achukue mahala pake na alifanya lile ambalo Shetani alipaswa kulifanya huko mwanzoni. Mlolongo huu unaonekana kwenye Wafilipi 2:1-11.
Wafilipi 2:1-11 inasema: Basi
ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi,
ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema, 2 ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi
mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. 3 Msitende
neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu
na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. 4 Kila
mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. 5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia
ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye yeye mwanzo alikuwa
yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha
kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana
utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu,
alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina
lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila
goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa
utukufu wa Mungu Baba.
Tazama jinsi
mlolongo ulivyo hapa:
1.
Kupewa uweza au karama za
Roho kwa upendo, kukemea kwa huruma, esteule wanie mamoja.
2.
Kisifanyike kitu chochote kwa
ubinafsi au kwa udanganyifu, bali ni kwa unyenyekevu, kuwaona wengine kuwa ni
bora kuliko nafsi yako.
3.
Kila mmoja atangulize maslahi
ya wengine.
4.
Hii ndiyo nia iliyokuwepo
ndani ya Kristo ambaye ingawaje alikuwa yu namna (morphe) ya Mungu hakujaribu kujifananisha na Mungu. Hakujaribu
kujifanya kuwa yu sawa na Mungu kama alivyojaribu kufanya Shetani hivyo.
Badalayake, Kristo alifanyika kuwa ni mtumishi na kujinyenyekesha hadi mauti.
Mungu aliridhia
kwamba Shetani alionyesha uongozi wake na utii lakini hakuwa mtiifu, Mungu
alimuondolea mamlaka yake ya kuwa Nyota ya Asubuhi na akampa wadhifa huo Kristo
(Ufunuo 2:28; 22:16). Nafasi hii anawashirikisha wateule.
Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi
iko isiyo ya mauti (1Yohana 5:17). Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi
(1Yohana 3:9). Kwakuwa dhambi ni uasi. (1Yohana 3:4). Dhambi ilivyotawala
katika mauti (Warumi 5:21). Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi
6:23). Kristo alikufa ili awe sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi mara
moja kwa wote akiwa ni Kuhani
Mkuu wa malaika na wateule (Waebrania 9:26; 13:11). Upatanisho huu haukuweza
kuzuiwa na mwanadamu, na Kristo akiwa ni Kuhani Mkuu wa Malaika, ikiwa ni
pamoja na mamlaka ya kimalaika. Ni sawasawa kabisa, hakutakuwa na upendeleo kwa
yeyote, kwa kuwa hiyo ni dhambi (Yakobo 2:9). Kwa hiyo, kuwaacha malaika bila
kutubu ni kuwapendelea kwa kuwa fursa hiyo imetolewa kwa wale walio ndani ya
Jeshi la Malaika. Mungu hawezi kutenda dhambi na kwa hiyo Mungu hawczi kuwa na
upendeleo kwa yeyote. Pia hawezi kumpendelea mtu atoapo hukumu (Mithali 24:23)
na kwa kweli hana upendeleo (Matendo 10:34). Kwa hiyo Malaika watatubu na
kuokolewa kwa dhabihu ya ondoleo la dhambi ya Kristo.
Toba ya Shetabi
ndicho huenda kitu cha kukionea mashaka. Imani kuwa anaweza kutubu inatoa
mashaka makubwa kwa kulinganisha na tabia zake zaidi kuliko tabia za Mungu. Hii
haijaorodheshwa kwenye hii ya maandiko. Toba ya mapepo inachukuliwa kuwa ya
namna ya kipekee aina yake na kwa kweli wengi wao wamekwisha tubu tayari.
Hukumu aliyopewa Shetani ilikuwa ni kwamba aliondolewa kutoka kwenye mamlaka yake.
Mapepo walioasi hawahukumiwa bado. Na wateule hawajaimaliza bado kazi au
majukumu yao ili kuwafanya wawe wamepimwa kikamilifu dhidi ya matendo yao kama
walinzi au waangalizi wa sayari hii.
Tunaweza
kuifananisha toba ya Shetani na mfano wa Mwana Mpotevu (tazama jarida la Kondoo Aliyepotea na Mwana Mpotevu (Na. 199) [Lost Sheep and the Prodigal
Son (No. 199)]; na pia kutoka kwenye ukweli wa kuwepo kwake
Shetani kwenye ufufuo wa wafu akiwa na umbo la mwanadamu, ambalo tunaliona
kwenye maandiko mengine yanayofuatia.
Jambo lililo wazi
ni kwamba Shetani ametajwa kuwa ni ni mtu na anatokea shimoni kuzimuni kwenye
Isaya 14. Uweza wake kama roho utaondolewa kutoka kwake kwenye kipidi cha
mwishoni mwa utawala wa Milenia baada ya kugunduliwa kipindi cha mwisho. Kutoka
kwenye Isaya 14 tunajionea kwamba mataifa yanaeleza kushangazwa kuona kuwa yeye
ni mtu aliyeweza kuyaharibu mataifa.
Mataifa wanamwambia Lusifeli kutokana na maandiko haya kwenye Isaya 14:10.
Je! Wewe nawe
umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi! (tafsiri
ya Interlinear Bible)
Andiko hili
linaelezea mambo mawili. Hatimaye neno mtu
linahudumia makusudio ya utambulisho kerubi lifunikalo ambavyo ndivyo
alikuwa yeye, liitwalo la kaskazini au lenye kichwa cha mwanadamu. Pili tunajua
kutoka na andiko hili kwamba Shetani atakwenda kuzimuni na kutaabika na mateso
na maangamizo yatakayoendana na hali ya mwili alionao. Angalia tena andiko la
Isaya 14:11-17.
Isaya 14:11-17
Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza
wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. 12 Jinsi
ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi
ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe
ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu
kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za
mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya
mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. 15 Lakini
utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo. 16 Wao
wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye
aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme; 17 Aliyeufanya
ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?
Shetani ndiye
aliyeondolewa kwenye mtandao wa nguvu za kiroho na nguvu zile ndizo
zinazochoche moto kwenye Ziwa la Moto. Kwa hiyo nguvu zimewekwa kutumika kama
kumbukumbu, moshi ambao utafumuka juu milele. Ukweli wa kwamba moshi utaendelea
milele haumaanishi kuwa viumbe walioko ndani yake watateseka kwa kuunguzwa
milele. Dhana hii sio ya kimungu na inapingana na tabia asilia za Mungu.
Kuyatamani mateso ya mwingine ni wazo lililo kinyume na ni ukengeufu kwa mujibu
wa mchakato huu. Njia ya kimungu imeelekezwa vema kwenye Injili zote. Mpende adui yako, Watendee mema wale
wanaokuchukia. Watendee mema wale wanaokuchukia. Wahurumie wale wanaokutendea
mabaya. Huruma za Mungu zadumu milele (Zaburi 136:24). Umilele huu
hautakuja hadi hukumu itakapotimia. Mambo makuu yaliyo kwenye Torati ni hukumu
na rehema. Hukumu inachukuliwa kuwa na maana ya marekebisho na kuadibisha.
Marekebisho haya pamoja na fursa iliyopo ya kutubu imetolewa kwa Shetani sawa
kama iliuvyotolewa kwa wengine wote.. yryr hapungukiwi na sifa ya kuwa ni
kiumbe aliyeumbwa na Mungu na ndugu yetu zaidi ya walivyo Malaika wengine wote
waasi. Shetani na Malaika wengine wote watafufuliwa na kusimama kwenye Kiti
Kikubwa Chaenzi Cheupe cha Hukumu. Watachukuliwa na kuhukumiwa sawa na wanadamu
wengine kwenye Ufufuo wa Pili wa wafu, pamoja na viumbe wengine wote ambao
hawakuwepo kipindi cha Krsto wakiwa ni viumbe walio kwenye ulimwengu wa roho
kipindi cha utawala wa millennia. Tunaona kwamba tukio hili linamjumuisha pia
Shetani.
Andiko hili ni
Andiko Takatifu, na Maandiko Matakatifu hayawezi kutanguka. Mapepo waliomba
awahurumie (Mathayo 9:27) na huruma ile itaendelea kwao, ili kuwaonyesha
malaika hawa kwamba umbaji wake wote ni mkamilifu. Ni mapenzi na makusudi ya
Mungu kwamba yeyote mwenye mwili asipotee, bali wote wafikilie toba (2Petro
3:9). Katika mwanzo wa uumbaji Shetani na Malaika wote walikuwa ni sehemu ya
waaminio. Keisto alisema kuwa yalikuwa ni mapenzi ya Mungu kwamba hata mmoja ya
wadogo hawa asipotee (Mathayo 18:14). Kama mmoja wa wadogo walioko kundini
akipotea hata kwa kiwango cha Nyota ya Asubuhi, Baba asingeweza kuonyesha
kupitia uweza wake wa Kujua Kila Kitu na
uweza wake wa Kujua Kila Kitu na Uelewa wake mkuu kuliko kiumbe mwingine yeyote
na pendo lake la agape? Je, ni lini Mungu aliwahi kukataa toba ya kiumbe
wake? Je, angeweza kuikataa toba inayoombwa na mteule wake? Dhambi
isiyosameheka ni ile ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Dhambi hii haimo miongoni mwa
ile ya kuzikana nguvu za Roho Mtakatifu zenye kumwongoa kumbe yeyote na kumrejesha
kwa Mungu. Mchakato huo unahusika na kuukana uweza na umoja wa Mungu kwa
Malaika unaosababishwa na hali ya kujihesabia haki.
Kwa hiyo andiko
lililoko kwenye Yeremia 10:11 linalosema kuwa Elahia (miungu) wata 'abad
(imetafsiriwa kama kuangamia) ina maana ya ya kukosa jinsi ya kukimbia akiwa amevunjika kuliko kuchukuliwa kutoka kuwepo kwake. Fursa ya toba ipo kwa viumbe wote
wa Mungu, kwa kuwa Mungu hana upendeleo (Warumi 2:11). Kama Shetani hawezi
kutubu, basi Mungu atakuwa ni mwenye upendeleo. Bali hayuko hivyo na kwa hiyo
hata Shetani anayo fursa ya kutubu. Mchakato wa toba yake utafanyika katika
kipindi cha miaka mia moja ile ya Ufufuo wa Pili wa wafu kilichoko kwenye
Ufunuo 20, ambacho kimetajwa pia kwenye Isaya 65:20. Kudai kwamba toba ya
mapepo imekataliwa ni kupotosha ukweli kuhusu tabia ya Mungu na ni mchakato ule
ule wa mawazo mapotofu ambayo yameiharibu sayari hii. Kristo ameushirikisha
mchakato huu kwa wanadamu.
Kristo alikufa
kwa ajili ya dhambi zetu
Ni fundisho kuu
la Biblia kuwa Masihi alikufa ili awaokoe wenye dhambi.
Kifo chake
kilichofanyika mara moja kilikusudia kuwaokoa wenye dhambi. Walipewa fursa ya
kutubu na kuletwa hukumuni.
Biblia inasema
pasi na kificho kuwa mapepo walimuomba Kristo awahurumie (kama tulivyoeleza
hapo juu). Agano Jipya inaeleza pia kwamba Kristo aliwaendea mapepo waliofungwa
kifungoni na akawahubiria baada ya kufufuka kwake.
Kama mapepo
hayawezi kutubu basi kusingekuwa na haja ya Kristo kwenda kuwahubiria kama
asingeweza kubadilisha chochote wala kufanya jambo la maana kwao ambayo ndiyo
kusudi la kuhubiri.
Pia ni madai ya
uwongo sana kwa baadhi wanaoamini kuwa kiumbe wa kiroho au pepo hawezi kufa.
Sababu ya 1. Iwapo
kama mapepo waliweza kutebda dhambi na hawakutubu basi ni lazima wangekumbana
na adhabu ya kifo na hakuna wokovu ungaliowezekana. Kwa hiyo viumbe hawa
wangekuwa wamependelewa na Mungu, tabia ambayo Mungu hanayo kama tulivyoona na
kujifunza hapo juu.
Sababu ya 2. Iwapo
kama roho haiwezi kufa basi imani ya kwamba Kristo ambaye alikuwepo tangu zamani
kabla ya kuzaliwa kwake kimwili asingeweza kufa. Bali Kristo alikufa na
alifufuka kutoka kwa wafu.
Kwahiyo basi,
kama Mungu alivyo na uweza wa Kufanya Kila Kitu pasi kushindwa, ndivyo ilivyo
kuwa mapepo wanaweza kufa kwa namna sawa tu na alivyokufa Kristo ndivyo
ilivyokuwa kumleta hapa chini duniani kwa wote wenye mwili na hatimaye kuzimuni
na hatimaye akafa na kisha akafufuka ili kuwahukumu.
Baada ya kufufuka
kwake Kristo alikwenda kwa Roho Mtakatifu kuwahubiria roho walioko kifungoni,
ambako ni kuzimuni. Roho hawa ni wale walioandikwa kwenye mwanzo 6:2,4 waliofanya dhambi ya uzinifu na binti za wanadamu na
walihukumiwa na kufungiwa huko kwa sababu hii (soma pia notisi za ufafanuzi wa
jambo hili kwenye Biblia ya The Companion Bible kwenye aya ya andiko
hili hapa chini na kwenye jarida la Nyongeza ya 23).
1Petro 3:18-22 Kwa maana Kristo naye
aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki,
ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni,
akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu
wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa;
ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. 21 Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku
hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za
Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. 22 Naye yupo
mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha
kutiishwa chini yake.
Inafuata, kama
usiku na mchana, ambao Kristo asingejisumbua kuwahubiri mapepo iwapo kama
wasingeweza kutubu na kama wasingeweza kuokoka.
Mapepo hawa pia
ni wale waliotajwa kwenye 2Petro 2:4 na Yuda 6.
2Petro 2:4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika
waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe
hata ije hukumu;
(Interlinear Bible)
Yuda 1:6 Na malaika
wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka
katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
Biblia ya NIV
imekosea kutafsiri andiko hili la 2Petro 2:4 na kutafsiri neno Tartarus kuwa ni
jehanamu, ambavyo sivyo kabisa.
Wamefungwa huko
hadi kipindi cha hukumu na tunajua kuwa itakuwa baada ya vita ya mwishoni mwa
kipindi cha Milenia.
Malaika walioasi wametupwa kuzimuni au shimo refu lisilo na mwisho wa kina
chake kipindi kirefu kilichopita wakingojea kuja kwa ukombozi wa Kristo siku ya
hukumu.
Sasa, kama
wamefungwa kwenye moto wa milele nasi wangekuwa wamekwisha hukumiwa tayari. Kwa
hiyo Biblia kwenye maandiko haya yangekuwa hayana maana na yangekuwa
hayajavuviwa. Neno liliikwenye andiko hili linaijata kuzimuni kama Tartarus,
ambalo ni shimo kubwa lenye kina kirefu chini na lisilo na mwisho wake lakini
linatumika kuwashikilia Malaika hawa waasi.
Kristo alifikia
vigezo stahiki vya kuwaokoa wanadamu na pia hata kwa hawa Malaika walioasi na
mamlaka zote za mbinguni na duniani ambao ni wametiishwa kwake.
Hitimisho
Mapepo hawana
uwezo na wako chini yetu na tutawahukumu kwenye Ufufuo wa Wafu. Kisha watapewa
mwili wa kibinadamu kwa jinsi ileile ya kama wanadamu waliofufuka wa namna
walivyoumbwa watakavyochuwa na kuwa na mwili wa kibinadamu tena kwenye Ufufuo
wa Pili . kisha watabadilishwa wote ili wafanye toba na kuadibishwa wale ambao
hawatatubu watakufa na kuchomwa kweny moto wa Jehanamu, ambalo ni shimo la
takataka ambapo ni sehemu yao ya hukumu na kifo.
Iwapo kama
tunashindwa kuhukumu kwa haki ndipo tutashindwa kuwapo pale kuwahukumu. Kuna
pande mbili tu za Ufufuo wa Pili wa Wafu: wa wale wanaohukumiwa na wa wale
wanaohukumu. Basi kama tutakuwa tumekwisha wahukumu tayari basi tujue kuwa tuna
upendeleo na kuwa ni wahukumu tusiozingatia haki. Na hatustahili kuwa ni sehemu
ya wale walio Nyumbani mwa Mungu kwa mtazamo na tabia aina hii.
Baba wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo!
Ni kwa kupitia
matendo yetu sasa ambavyo wanaweza kuhukumiwa. Tunaweka viwango kwa kaduri kwa
jinsi watakavyohukumiwa na kwa jinsi tunavyotenda dhambi ndipo wanapohesabiwa
haki. Na ndiyo maana Shetani anaitwa mshitaki wa watu wa Mungu.
Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? (Malaki 2:10)?
Je, angekuwa ni
mkatili kiasi gani na aliyekosa wema na huruma akiruhusu mmoja ya watoto afe
kwa ajili ya kulipa fidia ya mwingine? Lakini tunaamini kuwa Mungu bado hana
upendeleo. Wote miongoni mwa watoto wake wamepewa fursa ya kutubu kweny kipindi
hiki cha kuadibishwa na cha hukumu ya haki.
Kiumbe huyu Lusifeli ambaye alikuja kuwa Shetani ni roho. Anapaswa
kuangamizwa na afe kabisa. Kwa hiyo anatakiwa afe kama mwanadamu na kama Kristo
alivyokufa akiwa mwanadamu. Fundisho la kwamba roho haifi ni ya kishetani
inayoendeleza fundisho la roho isiyoweza kufa na inayoishi milele, fundisho
lililoimngizwa kwenye Makanisa ya Mungu na Armstrong na yameharibu fikra za
wapendwa waaminio na kuwajaza mawazo ya chuki. Kama roho haiwezi kufa basi
Kristo asingeweza kuwa mwokozi wetu.
Roho ile iliyoharibika na ni roho ya muovu, au ya kiibilisi au ya waabudu
mashetani, ambayo ni ya unabii wa uwongo nay a Mnyama ambao watatupwa kwenye
Ziwa la Moto kama walivyoelezewa habari zao kwa kina kwenye kitabu cha Ufunuo.
Kutoka kwenye kitabu cha nabii Ezekieli tunajua kwamba moto utashuka kutoka kwa
Shetani na utamuangamiza yeye mwenyewe akiwa na umbo la mwanadamu.
Ziwa la Moto ni ukumbusho ambalo limefanyizwa kutoka kwa roho hii
iliyochukuliwa kutoka kwenye kiumbe baada ya kutumiwa katika kumharibu katika
mwili wake wenye mwonekano.
Yeye ni kiumbe, aliyeumbwa na wala hana tofauti na viumbe wengine hapa duniani
waliowahi kufa na kuzikwa. Kwa hiyo yuko tayari kwa Ufufuo wa Pili wa wafu.
Kiumbe huyu mdogo au ukumbusho wa viumbe amemrudi Mungu aliye muumba kama
walivyo wenngine wote.
Mungu anapaswa kuwa kwenye uangalizi na uthibiti wa viumbe vyake. Kwa hiyo
tunapaswa kuamua matokeo ili tuwe na uweza wote usioshindwa kitu chochote.
q