Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[083]
Korani Kwenye Biblia, Torati na Agano
(Toleo La Edition 3.0
20040828-20041122-20110503)
Kitabu cha Koran
kina ujumbe muhimu sana kuhusu Biblia au Maandiko Matakatifu na Torati na
Agano. Kitabu hiki cha Korani kinauthibitisha au kunga mkono ujmbe wa Biblia na
Torati na Ushuhuda na Agano la Mungu. Hakuna mtu anayedai kuwa yeye ni Mwislam
anaweza kuwa wa imani hiyo pasipo kukubaliana na Maandiko Matakatifu na Torati
ya Mungu kwenye ubatizo na uanachama au ushirika wa Kanisa la Mungu.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati
Miliki © 2004, 2011 Wade
Cox)
(tr.
2015)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Korani
Kwenye Biblia, Torati na Agano
Kumbuka: Muhammadi ni jina la
kanisa.
Ahmedi anatajwa kama Roho
Mtakatifu.
Jina la mtume lilikuwa Kasimu
(aliyeitwa hatimaye Muhammadi)
*************
Tumeona kuwa
Kristo alikuwa mlengwa muhimu kwenye Korani akijulikana kama Nyota ya Alfajiri.
Torati na Sheria za Mungu ilitolewa kwa Mababa wa imani na kwa nabii Musa na
kwa Kristo, kama tunavyoona kwenye Sura zake. Zile zinaofanya Madaraja ya
nyadhifa. Kwenye hizi Sura, kwenye Sura ya 61:5-6, Musa na Kristo kwa wazi sana
wanaonyeshwa kuwa ni kama manabii wawili wakuu sana wa Mungu. Kwanza kabisa,
Musa aliaminiwa kwa kupewa Torati ya Mungu na watu hawakumsikiliza. Kristo
alitumwa ili athibitishe yote yaliyofunuliwa mbele yake kwenye Torati na
kumtaja au kumrejea yeye anayestahili kusifiwa, Ahmedi, ambaye maana yake ni:
“Mwenye Kusifiwa au Mwenye Kustahili Sifa”. Huyu alikuwa ni mfariji wa Agano
Jipya, Roho Mtakatifu, lakini maandiko ya Hadithi yanadai kuwa lilikuwa ni jina
la Nabii wa Uarabuni. Mtu atauona utazamo hu ukielezwa kwenye tafsiri nyingi za
Korani na jina la Ahmedi maranyingi imetafsiriwa. Hata hivyo, Sura ya 5
inamtaja Roho Mtakatifu kuwa ni kama uweza wa Mungu kwenye maelezo ya 5:110,
ambaye alikuwa ndiye chombo au chimbuko ambalo alikuwa ameelekezwa pia.
Kristo ni mlengwa
akiwa kama chanzo au kiini au chanzo cha Ufunuo na uelewa wake. Kwa yeye aliwafunulia Torati au Taurati,
na Injili au Injeeli. Nyingi ya vifungu hivi vya maandiko zimeachwa bila
kutafsiriwa au kutafsiriwa vibaya au bila umakini, na sio kufanya uelewa
kirahisi, lakini kuhakikisha kuwa Waislamu hawaelewi na hivyo hivyo wasiongoke
kikamilifu. Hakuna tofauti kati ya Ukristo wa sasa na Maimamu. Lengo lao ni
kuihakikishia migawanyo na nguvu za kisiasa. Kwa kuwachanganya hawamhakiishii
mtu yeyote aelewe na ni bure. Wanazishika sheria za Mungu na Injili, na huku
bado ni hakika kuhusu kazi hizi zinazowapinga wanazuoni wa Hadithi wazipinge na
wakatae kuzitii. Korani inatamngaza Kristo kuwa ni kama Mhukumu na ni kwa
Torati ya Mungu aliyonayo ndipo ataitumia Kuhukumu.
[5.43] Na
huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati
yenye hukumu za Mwenyezi Mungu? Kisha baada ya hayo wanageuka. Na
hao si wenye kuamini.
Manabii wote na
waamzi wa watu wa Mungu walikuwa walinzi wan eno lililofunuliwa la Mngu, na
walinena sawasawa na sheria na ushuhuda wa Mungu (sawa na Isaya 8:20).
[5.44] Hakika
Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio
nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani
walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi
juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya
zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu,
basi hao ndio makafiri.
Ndivyo ilivyo pia
kwenye Injili ya Ufalme wa Mungu ilifunuliwa na Kristo iliongezwa kwenye Torati
ya Mungu, ambayo ndiyo imeelezewa. Huu ni msingi wenye mashiko wa Korani
yenyewe.
[5.46] Na
tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake
katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo
sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha
kwa wachamungu. (dhdi ya uovu).
[5.66] Na
lau kuwa wangeli ishika Taurati na
Injili na yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka
wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao
walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno.
Hakuna yeyote
anayeweza kuwa na imani bali ni Kanisa la Mngu, ambavyo ni Uislamu wa Mungu,
hadi wanapofuata Torati na Ushuhuda.
[5.68] Sema:
Enyi Watu wa Kitabu! Hamna lenu jambo
mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlio teremshiwa kutokana na Mola
wenu Mlezi. Na hakika ulio teremshiwa wewe kutokana na Mola wako Mlezi
yatawazidishia wengi katika wao uasi na ukafiri. Basi usiwasikitikie watu
makafiri.
Tabia ya Torati na Ushuhuda kwa kweli ilimlazimisha muasi
kupinga yaliyo kwenye maandiko, na kwa kweli kuongeza kwenye hali ya kutomiliki
na kutoamini kama tunavyoona imani na itikadi kongwe za Kiyahudi, Ukristo na
Uislamu. Hakuna mtu anayeweza kuwa na imani ya Kiislamu pasipo kuwa na Roho
Mtakatifu.
[5.110] Na
pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu
yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na
watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo
sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu;
na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa
idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo
wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi
mtupu!
Roho Mtakatifu anaweza kupatikana tu kwa njia ya ubatizo, ambaye Korani
inamtaja moja kwa moja kuwa ni wa Mungu.
Korani na Ubatizo wa Allah
Sura ya Ng’ombe
[2.138]
(Pokea) Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka
rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu Yeye tu..
Korani Tukufu, iliyotafsiriwa
na M.H. Shakir na kuchpishwa na Tahrike Tarsile Qur'an, Inc., mwaka 1983.
Tafsiri nyingine nyingi zimeorodheshwa hapo chini.
Pickthal: (Tunachukua vyetu) Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi
Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni
wenye kumuabudu Yeye tu..
Darabadi: Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani
aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye kumuabudu
Yeye tu.
Mohammed Asad: [Sema: “O Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi
Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni
wenye kumuabudu Yeye tu.
Yusufali: (Dini yetu ni) t Huko
ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi
kuliko Mwenyezi Mungu?
Ufafanuzi: Sibghah ص ب غ: maana ya
msingi yanaonyesha kidokezo cha kupaka rangi au rangi yenyewe; ni wazi kabisa
kwamba Waarabu na Wakristo wamechanganya rangi kwenye maji ya ubatizo,
wakimaanisha mtu aliyebatizwa aliyepata rangi mpya maishani mwake. Yusuf
Ali.
Neno “Sibghatun”
linamaana kutia rangi au rangi yenyewe, rangi (nauni). Kwa hiyo, maneno
yaliyotoholewa kutoka kwenye neno asili humaanisha: kupaka rangi, kutia rangi, kubatiza,
kutia ndani, kuzamisha, kupaka rangi, kuchukua tabia, mtindo, tabia asili,
gombo la sheria, dini.
Kwenye
Aya ya 138 ya Sura ya Al-Baqaraah ya Korani, tabia za Allah na Kitabu chake cha
Torati inaitwa Sibghaha
ya Allah.
Neno صِبْغَةَ limetoholewa kutoka kwenye Aya hii (aya) ikidaiwa kabisa kuwa ni kama
kitu muhimu kwa Wakristo kwamba “ubatizo” wa maji hauathiri badiliko lolote kwa
mtu.
Ni hili neno la Tahkalluq bi
Akhlaq Allaah, ambalo limetoholewa kuwa la tabia za Allah (za
Mungu), na kanuni pana na mhimu za imani,
zinazoonyesha matokeo yanayoonekana ya mabadiliko ya kweli na halisi moyoni na
ya kitabia. Ni kwa njia hii ya “ubatizo”, ambao kimsingi mabadiliko mema
yafanywayo na Roho Mtakatifu, ambayo yanawezesha au kufanya kuzaliwa kupya
kutendeke. Kwa mujibu wa matumizi ya lugha ya Kiarabu wakati mwingine inapokuwa
inakusudiwa kabisa kumtaka au kumlazimu mwanadamu kufanya kitu fulani vebu
inarukwa, kama ilivyo kwenye 2:138 na ni kitu chenyewe tu ndicho kimetajwa. Kwa hiyo,
kwenye tafsiri ya Aya hii (aya) ni lazima mtu aongeze vebu kama hiyo kama Khudhu yaani kudhania, au kuasili (Shahid
Bin Waheed)
Kutokana na
fafanuzi zilizo hapo juu tunaweza kuona kwamba wengine wanaelewa mabadiliko ya
kitabia yatokanayo na uongofu. Matokeo ya ubatizo ni kutoka kwenye matokeo ya
kila mara ya Roho wa Mungu.
Kutokana na andiko lililoko hapo chini, kilamtu anapaswa kuona kwamba
ubatizo ni sehemu ya imani ya kweli iliyotolewa na kupewa mtu mara moja tu na
ni ambayo bado inatakiwa kutunzwa na mwamini.
[2.136] Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale
tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na
Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii
wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao,
na sisi tumesilimu kwake.
Kwa hiyo, kuna
imani iliyotolewa mara moja tu na imani hii walipewa mababa wa zamani wa imani.
Hakuna muumini anayepaswa kuepuka au kuacha kufanya kitu kinachohitajika
kufanywa ili kutimiliza matakwa ya imani.
[2.137] Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi, itakuwa kweli
wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu
atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi.
Korani inaagiza
kuwa muumini atubu na kusilimu. Yeyote anayefundisha kinyume na mafundisho hayo
basi sio mwamini. Mafundisho ya Hadithi za kisasa yanafundisha kusilimu sio
kitendo cha muhimu, na wanatumia maandiko kuonyesha kuwa Allah anasilimisha
kuliko usilimishaji wowote unaofanywa wa kimwili unaohitajika, fundisho ambalo
ni kinyume kabisa na nia au lengo la Korani na Biblia. Ubatizo ni sharti la
mhimu kwa mteule ili aweze kuupata ufufuo wa kwanza wa wafu. Wale wanaofundisha
kinyume na hivyo, hawataweza kuuingia Ufalme wa Mungu na kwenye Bustani ya
Ufufuo wa Kwanza wa Wafu wenyewe, na wanawazuilia wote wanaowasikiliza
kutofanya hivyo.
[2.138]
(Pokea) Huko ndiko kupaka rangi kwa Mwenyezi
Mungu, na nani aliye mbora wa kupaka rangi kuliko Mwenyezi Mungu? Na sisi ni wenye
kumuabudu Yeye tu.
[2.139] Sema: Mnahojiana nasi juu ya Mwenyezi Mungu, naye ni Mola wetu Mlezi na Mola wenu Mlezi, na sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu? Nasi tunamsafia Yeye tu.
[2.140] Au mnasema kuwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub
na wajukuu zao walikuwa Mayahudi au Wakristo? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au
Mwenyezi Mungu? Na ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliye ficha
ushahidi alio nao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye
kughafilika na hayo myafanyayo. M.H. Shakir
Hadithi za Kiislamu zinasisitiza ushuhuda huu kuhusu usilimishaji wa Allah,
ambao hi dhambi zilizotendwa zamani, mwongofu mpya la washika maagano wanapaswa
kuupokea.
Hakuna mtu anayeweza kuongoa na kusilimisha vizuri kuliko Allah, hivyo
jinyenyekeze kwake.
Dini ile inayoitwa “Uislamu” watu wake hawaisomi Torati na Ushuhuda kama
vilivyoelekeza, uelewa kuhusu mambo muhimu yahusuyo ubatizo au kusilimu na umuhimu
wake ulepotea. Na hata wanadai kwamba Biblia ilikuwepo na kwamba hadi ulipofika
mwaka 632 BK wa kuanza huduma ya Mtume na imani yake, ndipo ilipotea. Wanafanya
hivyo ili kwamba waidharau Biblia na ili waiharibu imani. Mtume anawaita
waalimu hawa wa uwongo kuwa ni ngamia au punda waliobebeshwa vitabu vya
dhahabu. Wanazibeba kila siku na kwa bidii kubwa lakini hawaelewi chochote kwa
yaliyoandikwa ndani yake.
Biblia iliyosomwa na Mtume mwaka 632 bado ipo hadi siku hizi, na hakuna
hata yodi moja au neno lolote dogo lililoondolewa kutoka kwenye Torati. Maneno
ya Eloah au Allah hayarudi nyuma bure, au bila matokeo, kama tulivyoambiwa.
Kitendo cha kusilimisha cha Allah ni sakramenti ambayo iko bado na umhimu
wake muhimu kwa imani na hali ya kujitoa, na ni jambo ambalo Waislamu
wanalipuzia.
Korani inaonyesha kuwa Torati na Ushuhuda ni muhimu na ni lazima zifuatwe.
Torati na Injili
[2.63] Na tulipo chukua ahadi yenu, na tukaunyanyua mlima juu
yenu (tukakwambieni): Shikeni kwa nguvu haya tuliyo kupeni, na yakumbukeni
yaliyomo ndani yake ili mpate kujilinda. (dhidi ya uovu).
Torati inaendelea
kufundisha kuhusu sheria kuhusu vyakula pia. Kile Biblia inachofundisha na
kuamru kuwa ni sheria, kinakuwa ni sheria pia kwa Waislamu pia. Sheria
zilizoandikwa za Torati ni sheria pekee kwenye jamo hili. Sheria za baadae za
Wayahudi za Kashrut hazipaswi kufuatwa.
[2.168] Enyi watu! Kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala
msifuate nyayo za Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu aliye dhaahiri.
[3.93] Kila
chakula kilikuwa halali kwa Wana wa Israili isipo kuwa alicho jizuilia Israili
mwenyewe kabla haijateremshwa Taurati. Sema: Leteni Taurati muisome ikiwa nyinyi ni wasema kweli.
Mafundisho haya hapa yanaonesha kuwa baadhi ya
mafundisho ya uwongo kwa kweli yalitokea au kuanzishwa huko Misri, na sio
yalitoka Babeli kama ilivyodhaniwa hapo kabla. Haya yanaweza kuwa na misingi
yake fulani, kama mapokeo ambayo sio yaliyo kwenye msisitizo wa kibiblia ya
watu wa jamii ya Lemba wa Afrika Kaskazini, ambao kinasaba ni wa uzao wa
Wayahudi waliojiengua kutoka Yudea kipindi cha utumwa wa Warumi.
[5.5] Leo
mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula
chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema
miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla
yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati
wala kuwaweka kinyumba. Na anaye kataa kuamini bila shaka a'mali yake imepotea,
naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara.
[5.88] Na kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi
Mungu, halali na vizuri. Na
mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamuamini.
Kwenye Sura ya 5
tunaona sheria za vyakula zikisisitizwa mara kadhaa.
Sheria za vyakula
zinasisitizwa kwenye Korani na kuchukuliwa kama wajibu kwa Mungu.
[5.96] Nyinyi mmehalalishiwa kuvua vinyama vya
baharini na kuvila, kwa faida yenu na
kwa wasafiri. Na mmeharimishiwa mawindo ya wanyama wa bara maadamu mmeharimia
Hija. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mtakusanywa kwake.
Korani Sura ya
5:96 inaweka mwingiliano mgeni, kwa kile kilichooza cha samaki na kula samaki
aliye safi wakati kwamba kwenye shughuli za hija, haifanyiki kwa sababu ya
tofauti iliyopo kutokana na hali ya bahari. Hata hivyo, sio vibaya kufanya
mawindo au kucheza wakati wa hija. Hakuna sababu inayotolewa kwa makatazo
kwenye Korani, lakini inaonekana kutuama au kuweka msingi wake kwenye torati
iliyo kwenye Kumbukumbu la Torati 14:22-27, ambapo panahitaji maongeo ya nchi
yatolewe zaka na yachukuliwe kwenye misafara ya hija au mahali palipochaguliwa
kufanywa kambi ya sikukuu ikimaanisha kuwa sheria haijashikwa bado. Kama njia
ilikuwa ni mbali sana ndipo maongeo hayo yaliamriwa yabadilishwe kuwa fedha na
zachukuliwe hadi huko na vyakula na sadaka zilitakiwa zinunuliwe kutokana na
fedha zinazotokana na zaka. Kwa hiyo, kitendo cha kuwinda wakati wa hija au
sikukuu kulionyesha kwamba zaka haikuwa imekusanywa kiasi cha kutosha na
hakukuwa na umakini. Mchezo uliowakusanya kwa njia hii haukuwa sehemu ya sadaka
halisi na za kweli za Israeli au za Waislamu au za Mungu.
Makatazo yaliyo
kwenye maandiko ya Biblia yanakubalika pia na kuhusu mambo yahusuyo vita,
lakini kile kilicho safi na kilicho najisi vilibakia hivyohivyo.
Zaka pia inajiri
au inahusiana na vitu vilivyotekwa kutoka kwenye vita kama Ibrahimu
alivyoonyesha wakati alipomtolea zaka yake Melkizedeki. Lawi, akiwa bado
nyongani mwake, alimtole pia huyu Melkizedeki, ambavyo ilionyesha kuwa
Melkizedeki kuwa ni kama kuhani mkuu sana, akiwa ni urithi wa Lawi pia. Ndivyo
ilivyo pia, kwa Ishmaeli na Esau, na wana wa Ketura, walimtolea zaka zao Melkizedeki,
pia wakiwa kwenye nyonga za Ibrahimu, kukimaanisha kwamba wao pamoja na watoto
wao wote walikuwa wanamtii Kristo, na kuhani mkuu sana wa Kanisa la Mungu.
Neno mtume-nabii
lililotumika kwenye Sura ya 7:157 mara nyingi limetafsiriwa kama Mjumbe, mtume
kama kifungu kinachorudiwa ili kuficha maana yenye mwingiliano wa ndani kati ya
Korani na Biblia.
Ummi kwenye Sura
hii limerudiwa kama mtu aliyekuwa wala hawezi kusoma wala kuandika (kama
inavyosema Pickthall). Hata hivyo, andiko linasema “kwa yeye walikuta aliwa
ameandikwa chini na wao kwenye Torati na kwenye Injili”.
[7.157] Ambao
kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta
kaandikwa kwao katika Taurati na Injili,
anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana
waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao.
Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata
nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.
Wazo linaloaminika,
ni lile la mjumbe wa Kanisa la Mungu, anayehubiri maana ya kweli ya Biblia na
Torati ya Mungu, akiweka wazi tofauti iliyopo zilizopelekea kuonekana kuwa safi
na najisi.
[8.69] Basi
kuleni katika mlivyo teka, ni halali
na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe
na Mwenye kurehemu.
Maelekezo ya
imani kwenye kweli ni kuifuata Biblia, ambacho ndani yake kuna Vitabu
vinavyothibitisha kuwa ilikuwa imeandika kabla yao. Kwa hiyo Korani ni lazima
ikubalianenacho na itimize yale yaliyoandikwa kwenye Injili iliyoitangulia na
Torati, vinginevyo haitaweza kueleweka vema kwa kuisoma yenyewe tu peke yake.
Hakuna nabii anayeweza kupingana na sheria au torati na kile kilichofunuliwa
kabla yake kwenye maandiko na ushuhuda. Hakuna nabii au mtume anayefanya hivyo.
Ujumbe wa kila nabii ni ufafanuzi tu wa kile kilichopita kabla yake, na ufunuo
wa Mungu wa kuhusu kile kinachokwenda kutokea na kupita zake.
[5.48] Na
tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu
[Koran] hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu [Maandiko Matakatifu\] na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa
aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo
kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa
Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni
kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi
Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa
mkikhitalifiana.
Paulo anaeleza kuwa migawanyiko au
mafundisho ya kizushi vimeruhusiwa kuwepo miongoni mwetu ili kuwaonyesha
dhahiri wale waliokubaliwa na Mngu. Andiko hili ni rejea ya maelezo ya Mtume
Paulo, na migawanyiko inayotokana na makosa ya imani kwa imani kwa kushindwa
kufuata Sheria na Ushuhuda.
Andiko lililo kwenye Sura ya 3:50 linaeleza kuwa ushuhuda wa Kristo
unathibisha kuwa hii ilikuwa ni kabla yake kwenye Torati.
Jambo lililokatazwa lilikuwa ni kuongeza kwa kipindi cha ukuhani wa
Melkizedeki hadi kwenye kipindi cha Kanisa, ambapo hapo mwanzoni sana, katika
Israeli, ni kabila la Lawi tu ndilo waliruhusiwa au kupewa huduma hii.
Haimaanishi chochote kuhusu sheria ya vyakula.
[3.50] Na
ninasadikisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale mlio harimishiwa,
na nimekujieni na Ishara kutokana na Mola Mlezi wenu. Kwa hivyo mcheni Mwenyezi
Mungu na nit'iini mimi.
Hata hivyo,
anaelezea kuhusu sheria za vyakula kwenye Sura ya 3:93, ambapo panaamriwa
kwamba sheria ya biblia ya vyakula zinatofautiana kutokana na mapokeo au
desturi za Wayahudi, ambapo ni uamuzi wa mtu binafsi, ikiwa kama ni matokeo ya
maamuzi ya Waisraeli, ni sawa na ilivyokuwa kipindi cha kabla ya kufunuliwa
Torati. Kwa hiyo, kutokana na Korani, Israeli inajlikana kuwa waliama huko
Misri kuchukua baadhi ya makatazo au miiko ambayo haikuwepo kwenye Torati.
Imani ya Kiyahudi ina makatazo au miiko inayoonekana kama inafanana na imani za
siri, na mapokeo ya Wayahudi yanatuama kwenye mfano huo wa imani za Siri na za
Kimafumbo, na hayapo kwenye maagizo ya torati ya Mungu iliyotolewa huko Sinai.
[3.93] Kila
chakula kilikuwa halali kwa Wana wa Israili isipo kuwa alicho jizuilia Israili
mwenyewe kabla haijateremshwa Taurati.
Sema: Leteni Taurati muisome ikiwa
nyinyi ni wasema kweli.
Kwenye sura ya
5:43 tunaona kwamba Sheria ya Mungu ni msingi wa hukumu yote na mwamini ndiye
mtu Yule anayezifuata na kuzishika sheria na amri za Mungu na ushuhuda wake.
[5.43] Na
huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati
yenye hukumu za Mwenyezi Mungu? Kisha baada ya hayo wanageuka. Na hao si
wenye kuamini.
Korani
inashikilia kuwa manabii wanahukumiwa kwa Sheria au Torati ya Mungu.
[5.44] Hakika
Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu
na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na
wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha
Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali
niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu
kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.
Kwa hiyo, mtu
asiyeamini au kafiri ni Yule asiyejiheshimu mwenyewe, na kujitathmini kwa yale
yaliyofunuliwa kwenye Sheria na Ushuhua.
[5.46] Na
tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla
yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na
inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na
mawaidha kwa wachamngu. (dhidi ya uoavu).
Kristo alitumwa
kwenye nyayo za manabii na kuthibitisha kuwa kile kilichokuwa kabla yake
kilikuwa ni Torati. Hivyo basi, Korani inaungana na Injili na Agano Jipya
kwenye maandiko ya Agano la Kale na Torati ya Mungu. Korani imeelekezwa moja
kwa moja na kwa wazi kuwalenga Wakristo Waamini Utatu na wanaokataa kuitii na
umuhimu wa Torati na sheria za Mungu.
[5.66] Na
lau kuwa wangeli ishika Taurati na
Injili na yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka
wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao
walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno.
Mwongozo uliopo
hapa ni kwenye Sura 5:66 ni kwa kushindwa kwa imani kuishika pamoja na Torati
na Injili. Walishindwa kuichukua kutoka juu yao, yaani, kutokana na maongozi ya
Mungu na kutoka chini ya miguuni mwao, yaani, kutoka miongoni mwa wale wanaodai
kuwa ni Wakristo; kuna sehem muhimu na stahiki ya imani inayoishika na kuwa
kwenye kiwango sawa na kile cha imani asilia iliyotolewa mara moja tu na
iliyofuatwa na Kristo na Mitume. Hilo ni Kanisa la kweli la Mungu.
Kisha Korani
inaendelea mbele kuwatangazia wale wanaodai kuifuata imani hivi:
[5.68] Sema:
Enyi Watu wa Kitabu! Hamna lenu jambo
mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlio teremshiwa kutokana na Mola
wenu Mlezi. Na hakika ulio teremshiwa wewe kutokana na Mola wako Mlezi
yatawazidishia wengi katika wao uasi na ukafiri. Basi usiwasikitikie watu
makafiri.
Hapa Korani
inasisitiza kwamba yeyote anayedai kuwa na imani ni lazima aishike Sheria na
Ushuhuda. Lakini ni Sheria hii hii na Ushuhuda ambayo imekuwa kikwazo na
kupingwa na wale wanaodai kuwa ni watu wa imani, au wanaotaka kuiingiza na
kuitendea kazi kwenye matendo ya kipagani, kama walivyofanya waamini Utatu.
Wengi wanakulia kwenye mazingira ya kutoamini kwa kuwa wanapinga na kuyazuia
maelekezo ya Sheria na Ushuhuda. Hii ililengwa hapo mwanzoni kabisa kwa
Wakristo wa uwongo, bali sasa inahusika na Hadithi za Kiislamu pia, kwa hilo
hawazifuati Amri na Ushuhuda kama zilivyoelekezwa na Korani kabisa. Zaidi sana,
ni kwamba sheria na Ushuhuda hazipo kwa ajili ya Taureti (Torati) peke yake na
kwa ajili ya Injeeli au Injili tu, ambazo zinaonekana kuwa kama majina ya
kijeneriki. Kitabu cha Hekima kinaendana sambamba na Torati na Injili kwenye
maandiko yafuatayo ya Sura ya 5:110:
[5.110] Na pale Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin
Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako, na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu
kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo
kufunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura
ya ndege, kwa idhini yangu, kisha ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na
ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa
idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo
wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao: Haya si lolote ila ni uchawi
mtupu!
Kumbuka pia 7:157
hapo juu, inayoelekeza kuifuata Sheria au Torati na Ushuhuda. Korani
inaifungamanisha imani kwa wafuasi wa Eloah, Mungu wa Pekee na wa Kweli. Mungu
huyu wa Pekee na wa Kweli, Eloah. Huyu Nguvu au Lah, amewanunua waumini wote kwa madhumuni kamili
yaliyokusudiwa ya kuwapa uzima wa milele kwenye Ufufuo wa Wafu, ambao unatajwa
na kufananisha na Bustani ya Paradiso. Tunaja kwamba kuna Bustani mbili za
Paradiso, ni hizi zinawakilisha aina mbili za ufufuo wa (soma jarida la Kristo na Korani (Na. 163)).
[9.111] Hakika
Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata
Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni
ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati
na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi
furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa,
Jina lililoko
hapa ni la Muhammedi, lakini tunaongea habari za Kanisa hapa na sio kuhusu
Nabii. Sura ya Al Hujarat inachukua jina lake kutoka kweye aya ya 4, Ahadi
ya Kipekee ya Binafsi ambapo hali
isiyo na umakini inawakumba waaminio.
Sura hii inaeleza
kwa wazi kabisa kwenye Kanisa na jina la “Muhammedi” linalenga kwenye bodi au
kundi zaidi kuliko kumkusudia mtu. Ndipo watafsiri waliongeza jina Muhammedi
kwa sehem nyingine mbalimbali. Limewekwa mahali ambapo hapahusiki kwenye
maandiko asilia au limeongezwa kwenye maandiko ya zamani sana. Kutumika kwa
jina au neno Muhammedi mara nyingi kunajitokeza kuwa ni neno la kijenerikali au
la jumla na linataja kikundi, ambacho kinaweza kuwa ni Kanisa la Mungu tu, peke
yake.
[48.29] Muhammad
ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri,
na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila
na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya
kusujudu. Huu ndio mfano wao katika
Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake,
kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake,
ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi
Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira
mkubwa.
Alama ya usoni
mara nyingi inaonekana miongoni mwa wale wanadai kuwa wenye kuamini ikiwa kama
alama ya hisia au unyenyekevu wao. Wameweza kufanya hivyo kwa kujisugua sana
ardhini vipaji vya nyuso zao kwenye mazingira ya kusujudu na maombi, ambayo
wanafanya hivyo kwa kurudia rudia kama wanavyofanya wapagani wasioamini.
Kwenye Sura ya
61:6 tunaona kwamba Kristo anatajwa kuwa ni mjumbe au mtume wa Mwenezi Mungu. Habari njema ya Ahmedi ilikuwa ya
kwamba “Mfariji” alikuwa analetwa Kanisani. Roho Mtakatifu akatokea akiwa na
nguvu au uweza wa Mungu akiwa kama mjumbe au mfariji wa Kanisa siku ya
Pentekoste ya mwaka wa 30 BK, lakini nguvu zake zilikataliwa au uweza wake
ulidhihakiwa na wengi. Andiko hili linaloshabihiana na la Matendo Sura ya 2.
Hadit imepotosha kwa makusudi nia iliyokusudiwa ieleweke kimaandiko.
[61.6] Na
Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa
Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja
Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja
zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!
Itikadi ya
kiimani imeelezwa kuwa ni kufanyika kuwa safi kwa kila mmoja miongoni mwa
wateule kabla ya kufa kwao. Kristo mwenyewe anachukuliwa kuwa ni shahidi wa
wale wote wanaodai kuwa wenye imani, na huku wakiwa hawalitii neno la Mngu.
[4.159] Na
hawi katika Watu wa Kitabu ila hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake. Naye
Siku ya Kiyama atakuwa shahidi juu yao.
Walioitwa kwenye
Kanisa la Mungu ndio wanaoonekana kuwa ni wenye imani linapoitwa, na kuletwa
kwenye uelewa halisi na sahihi kabla ya kufa kwao.
Korani na Agano
Agano la Mungu limefungamanishwa kwene Korani na imani. Kwa hiyo, hakuna
amtu anayeweza kuwa na imani na akakana au kulikataa Agano, au akataka kuenenda
kinyume nalo.
[2.27] Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha
ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya
uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara.
Agano la Mngu
linajulikana kuwa limewekwa na Wana wa Israeli pamoja na Mungu.
[2.40] Enyi
Wana wa Israili! Kumbukeni neema yangu niliyo kuneemesheni, na timizeni ahadi
yangu, na Mimi nitatimiza ahadi yenu, na niogopeni Mimi tu.
Agano la Mungu lilifanywa
kwa kupitia manabii. Manabii wale wanaonena sawasawa na Sheria na Ushuhuda ni
lazima wasaidiwe. Wanalithibitisha kwa kulifanya imara Agano na kwa hiyo nabii
ni shahidi dhidi yao.
[3.81] Na pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi kwa Manabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikima, kisha
akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini na
mumsaidie. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agizo langu juu ya hayo?
Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi katika
kushuhudia.
Agano la Mungu
linaunganisha kundi linalolisika. Hilo ni Kanisa la Mungu, ambalo ni Al
Islam au Wanyenyekevu Waliojitoa kwa Mungu.
[3.103] Na
shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi
Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu
iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha
nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto,
naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili
mpate kuongoka.
Waaminio
wamekombolewa kutoka mautini na kupewa fursa adhim ya wokovu. Agano hilo
lilifanywa na Waisraeli na kisha na Kanisa, lakini wengi walilikiuka na
kuliacha Agano hili la Mungu kwa fedha au mali tena na kufanyika kuwa Kanisa la
uwongo kwenye mabaraza ya yaliyokaa vikao vyao katika Karne ya Nne,
wakijichukulia wenye imani za kuabudu sanamu kwa kujipa mamlaka au uweza wa
muda mfupi.
[3.187] Na
pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana
na walio pewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha,
walikitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwacho thamani duni. Basi ni
kiovu hicho walicho nunua.
Kwa hiyo, ujumbe
wa Uislamu uliwalenga Wakristo waamini Utatu ikiwataka wairudie imani
waliyopewa mara moja tu.
[5.15] Enyi
Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo
kuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anaye samehe mengi. Bila shaka imekujieni
kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru na Kitabu kinacho bainisha.
Korani imesema
waziwazi kabisa kuwa ni kitabu cha ufafanuzi na kuithibitisha Torati na
Ushuhuda ambao ulikuwa ni Maandiko Matakatifu, na inahubiri yale isiyowahi
kuyatenda kwenye bodi ya maandiko. Kwa hiyo karibu watafsiri wengi wa siku hizi
wa Uislam kwa wanazuoni wa Hadithi hawako sahihi, na wao wenyewe wanajikuta
wako nje ya uwanja wa imani, kwa sababu hawayashiki, au kunena sawasawa na
ilivyo, Torati na Ushuhuda (Isaya 8:20).
[5.48] Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu [Koran] hichi kinacho sadikisha
yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu
[Maandiko Matakatifu\] na kuyalinda.
Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate
matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea
sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni
nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa
mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja
kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.
q