Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[086]

 

 

 

 

Imani na Matendo

(Toleo La 2.0 19950701-20000327)

Jarida hili linaonyesha uhusiano uliopo kati ya Imani na Matendo. Linaonyesha umuhimu wa kuzitubia kazi zisizo na maana na mfu. Mwonekano wa imani unaonekana kuwa ulizingatiwa sana na mitume, kuwa ni kwakupitia matendo ndopi imani inaonekana.

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

Email: secretary@ccg.org

 

 

(Hatimiliki © 1995, 2000 Wade Cox)

(tr. 2013)

 

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki.

 

 

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:
http://www.logon.org au http://www.ccg.org

 

 

Imani na Matendo


Ni kanuni ya Ukristo kuamini kwamba mwenye haki ataishi kwa imani (Habakuki 2:4; Warumi 1:17; Waebrania 10:38). Dhana au mawazo yanayozoelekeka vichwani mwa watu siku hizi ni kwamba imani ni muhimu na imeyazidi matendo na kwamba sheria za Mungu au torati imekoma umuhimu wake. Na zaidi sana imedhaniwa kwamba kitendo cha kuzishika sheria za Mungu ni sehemu ya matendo na kwamba matendo hayana umuhimu katika wokovu wa mwanadamu. Mawazo haya yanatokana na kukosa uelewa uliopo kati ya wokovu na neema na umuhimu wa sheria. Uhusiano huu umefafanuliwa sana kwenye jarida la Uhusiano Uliopo Kati ya Wokovu Unaopatikana kwa Neema na Torati (Na. 82) [The Relationship Between Salvation by Grace and the Law (No. 82)].

Jarida hili liafafanua uhusiano uliopo kati ya Imani na Matwndo.

Ni ukweli usiopingika kwamba Kristo aliashiria kwamba sheria au torati imefanywa kwa sehemu na kwamba mambo yaliyo mazito zaidi yahusuyo torati ni Haki na Rehema na Imani. Kristo alisema kwamba mambo haya yanapaswa yafanyike pasipo kuyaacha na mengine (Mathayo 23:23).

Kwa hiyo suala ni kwamba kulikuwa na mambo mazito zaidi. Yalikuwepo pia mambo maodgomadogo yaliyohusiana na torati na ambayo yalitakiwa yafanyike pia. Kristo hakusema kwamba haya yamemekoma na hayana umuhimu tena. Bali alisema kwamba: hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Kwa hiyo, yanatakiwa yafanywe yote, lakini mambo mazito zaidi yalichukua umuhimu na yakachukua mahala pa kipaumbele cha mengine yaliyoonekana kuwa ni madogo kwa mujibu wa sheria au torati. Kitendo cha kutoa zaka ya mnaanaa au jira kutoka kwenye bustani yako, hakukupi haki yaw ewe kupuuzia kwenda kuwatendea mambo mema majira zako. Ni jambo lililo kweli kwamba watu wengi hudhani kwamba hawana hatia na ni watakatifu kwakuwa wanayafanya mambo fulani madogomadogo katika kumtumikia Mungu. Lakini wanabakia wakiwa wanapuuzia kuzifanya kazi nyingine za Mungu na zilizo muhimu na kubwa wasizifanye, au wakizikimbia na kuziepa. Kristo anasema kwamba watu hawa, Waandishi na Mafarisayo hawa walijua kikamilifu kile ambacho torati ilikuwa imeletwa kwacho na umuhimu ambao kwawo torati ilitolewa kwetu, wanapokuwa wanatilia mkazo kuhusu mambo hayo ambayo yalikuwa nje ya yale yaliyokuwa mambo muhimu ambayo walitakiwa washughulike nayo. Hutakiwi kuyaacha tu pasipo kuyatenda, mambo muhimu yahusuyo sheria au torati.

Kristo alituita ili tufanye kazi. Hakutuita ili tukae chini tu na kuomba vyumbani mwetu. Hutaweza kuuingia Ufalme wa Mungu kwa ajili ya kitendo chako cha kuomba dua tu chumbani mwako, wakati ukiwa na uwezo wa kufanya mambo mengine. Kuna watu wengi sana ambao hawaezi kutoka nje ya vyumba vyao na wanaomba kwa juhudi na huku wakizifanya kazi za Bwana Mungu, kwa kuwa maombi ya mwenye haki yananguvu kuu sana. Kuna mlolongo wa mambo mengi sana ambayo watu walitakiwa kuyafanya ambayo wamepewa kwa kulinganishwa na uwezo wao na nia na umahiri wa kuyafanya. Watu wengi wanaona ni vigumu kufanya hili na lile wakidhania kuwa kunasheria au taratibu ambazo kwazo zinawafanya waishi.

Kutokana na maelekezo ya Kristo yaliyo kweny Mathayo 23:23 yanaweza kuonekana kuwa imani ni msingi wa torati zaidi kuliko uwekezaji wake.. kwa hiyo, Haki na rehema na imani ni mambo makuu matatu yanayoitimiliza sheria au torati ambayo Kristo alisema kuwa vinatakiwa vishikwe. Kwa kweli imani ni nyenzo muhimu ambayo kwayo torati iliweza kutumika kwenye mazingira ya kiuadui na hatarishi. Pasaka iliadhimishwa kwa imani, na sio mbadala wa imani. Wazo fikirika ni kwamba, kabla torati haijatolewa kwa nabii Musa, Pasaka hii iliadhimishwa na Musa kwa njia ya imani. Kwa hiyo, imani iliitangulia torati na ni sehemu ya torati (Waebrania 11:28).

Hii ni muhimu kwakuwa Waprotestant na wale wanaojiita Wakristo mamboleo wanakuja na wazo kwamba torati ilikomeshwa na haina umuhimu tena na muhimu sasa imani na kuwa ndivyo linavyofundisha Agano Jipya na kwamba liliondolea mbali umuhimu wa matendo. Zaidi ya yote wanaamini kwamba imani katika Yesu Kristo ndicho kitu pekee kinachohitajika na kwa njia ya imani katika Yesu Kristo wataokolewa. Hili lina sehemu tu ya ukweli.

Andiko muhimu ambalo ambalo maranyingi wanalitoa kujifariji hivyo ni Waebrania 6:1 kwa ajili ya wito wake wa kuwataka watu wazitubie kazi zao mfu. Andiko hili linasomeka hivi kwa mwonekano wake.

Waebrania 6:1-12 Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, 2 na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele. 3 Na hayo tutafanya Mungu akitujalia. 4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

Andiko hili linawahusu wale walio sehemu ya wateule, waliompokea Roho Mtakatifu na kisha wakaanguka dhambini mbali na kweli ya Mungu. Haiwezekani kuwarejesha tena kwenye ukweli. Wanakwenda kwenye ufufuo wa pili.

7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu;

Ikiwa kama wewe umehesabiwa (umeandaliwa) na kupewa Roho Mtakatifu, basi hiyo ni Baraka toka kwa Mungu.

8 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa. 9 Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika habari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokovu.
10 Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia. 11 Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho; 12 ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.

Hili ni jambo lililo wazi sana. Hupaswi tena kuendelea kujifunza mafundisho ya awali. Mafundisho ya awali ya Kristo ni toba ya kuzitubia kazi na matendo mafu na yasiyo na maana, imani kwa Mungu na maelekezo juu ya umuhimu wa torati, ufufuko wa wafu na hukumu ya milele. Haya ni sawa na maziwa. Bali sisi tunaenda mbele na mbali zaidi kuyaangalia mambo makuu. Hii haina maana kuwa kazi au matendo vimekufa na kwamba vinapaswa kuondolewa mbali kabisa kutoka kwenye umuhimu wake.

Dhana iliyoko hapa ni kututaka kuyatubia matendo maovu na yasiyo na maana. Hata hivyo, andiko hili linawapeleka Wakristo hadi kwenye kiwango cha juu cha pande mbili za mafundisho ya awali. Kwa hiyo kiwango cha ukuaji ni zaidi ya uelewa au hisia za kawaida za kuzitubia kazi na matendo yasiyofaa. Kumbuka kuwa kinachosemwa hapa ni kuzitubia kazi zisizofaa na sio kuyatubia matendo (sawa na Wagalatia 5:19-22). Ni opotovu mkubwa wa kifasiri kuamini kwamba kazi zote zimekufa na hazifai. Hiyo sio sahihi kabisa.

Hili ni kosa kufikiri hivyo kuhusu jambo hili. Unapokuwa unampokea tu Roho Mtakatifu na ukaweka bega lake kwenye gurudumu na ukahesabiwa kwenye jeshi la Mungu, basi huruhusiwi kuendelea tena kuishi dhambini. Hili sio tu suala la kusema kwamba "Nitaubeba msalaba wangu tena; na nitautua chini na kumzika baba yangu, au nitamjaribu punda wangu; au nitafanya kitu fulani kingine na kisha nitaubeba unapowezekana kufanya hivyo”. Hivyo sivyo imani hii inavyotakiwa kuwa. Unapojiorodhesha kwa shughuli za kulima shamba hadi kufikia kuchwa kwa jua na ukaitwa kwa wakati ule ule. Mfano wa wakulima walioajiriwa shambani unatuonyesha kwamba wote walilipwa mshahara wa namna moja, ni swa kama ulivyo wokovu wetu. Bali wote walifanya kazi na kulima hadi kuchwa kwa jua, hadi mwisho wa siku. Ni jambo sawa na Yule anayeitwa amechelewa, bali wote walifanya kazi pamoja tangu wakati walioitwa shambani. Ikiwa utaliacha shamba hutaweza kulipwa ujira wako.

Matokeo ya mwisho ya jambo hili yamo kwenye 1Wakorintho 5:5 – utolewe kwa adui na mshitaki wako ili kwamba maisha yako yaokolewe siku ya mwisho. Hii ndiyo hukumu. Unakwenda kwenye ufufuo wa pili. Mtu anahitaji kufanya toba kutokana na msimamo wa kushikilia kuwa na Kristo na imani pekee iliyo kama dhana fikirika tu. Tuna kazi ya kufanya na sote tunawajibika tuihitimisha kazi hii kwa kiwango tunachoweza kukifikia. Baadhi yetu tumekirimiwa uwezo zaidi waliopewa wengine. Baadhi yetu tuna uwezo na vipaji vya aina mbalimbali. Baadhi yetu tuko mahiri na uwezo mkubwa katika maombi na kufunga saumu. Wengine wamekirimiwa vipawa vya aina nyingine mbalimbali. Lakini sisi sote tumeitwa kufanya kazi tukiwa kama washiriki wa mwili mmoja na kichwa chetu ni Yesu Kristo. Ni muhimu kukumbuka kwamba kichwa cha kanisa ni Yesu Kristo na kufikiri vingine mbali ya hivi ni uwongo.

Sura iliyowaorodhesha mashujaa wa imani katika Waebrania 11 ni ya muhimu sana katika kuonyesha jinsi imani ilivyokuwa inashikwa na jinsi watu walivyoiendeleza imani. Hili sio wazo tu lililo kwenye Agano Jipya peke yake. Agano Jipya liko wazi kabisa katika kuitilia mkazo imani kutoka kwenye ulimwengu halisia.

Webrania 11:1-39 inasema: Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. 2 Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. 3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. 4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena. 5 Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. 6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. 7 Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

Nuhu alionywa juu ya mwisho wa zama aliyokuwa anaiishi na alianza kujenga safina. Ilimchukua kipindi cha zaidi ya miaka mia na aliambulia kejeli na dhihaka kutoka kwa watu wote waliokuwepo katika kipindi kile. Tumepewa kitabu cha Ufunuo baada ya kuondoka kwake Yesu Kristo kikikusudia kutupa maonyo ya siku za mwisho. Mwishoni mwa zama hizi tunazoishi kuna ishara za uhakika na kwa imani tunatarajia kurudi kwa Masihi na pia kufikia kikomo cha zama hizi. Na ndivyo ilivyokuwa kwa manabii walioishi zama za kabla ya kutolewa kwa Ufunuo, walitoa maonyo kuhusu kuja kwa Masihi nay a mwisho wa dunia. Nasisi pia tumo kwenye mzingiro huo huo wa wenye kutukejeli na kutudhihaki kwa ajili ya kuamini hivi. Watu wengi zaidi na zaidi wanaojiita kuwa ni Wakristo wanasema kwamba Bwana amechelewa kurudi. Na wengine wengi sana wataachana na imani na mafundisho ya kurudi kwa Masihi na kuongeza tena na tena siku na tarehe. Kitu cha hatari zaidi kinajitokeza hapa, na kile wanachoweza kukifanya kuwafanya watu waachane na matumaini ya kurudi kwa Masihi. Kinachopiganiwa zaidi hapa ni kile kinacholingana na juhudi za kuwasahaulisha watu kuhusu kurudi tumaini hili. Ni hadi pale tu watakapo kabiliwa na uharibifu au maafa makubwa yatokanayo na uharibifu na maangamizo, na ndipo watakapojirudi na kuanza kuomba kurudi kwa Masihi. Ni watu wachache sana wanaomba ombi la Ufalme wako uje kwa sasa.

8 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. 9 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. 11 Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.

Mungu alimpa Sara ahadi. Ingawaje alikuwa kwenye kipindi cha umri ulio zaidi na ule wa mtu kuzaa mwana, bali yeye alizaa. Aliweza kumtimizia ahadi hii.

12 Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.

Ndipo uzao wa Ibrahimu ulikuwa mwingi kama nyota za mbinguni. Walizidi kuenea hadi kufikilia Yuda.

13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. 14 Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. 15 Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. 16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.

Utafutaji huu kwa kweli ni wa uzungukaji wa dunia, katika kumngija Mungu aushushe Yerusalemu mpya hapa chini na kuipatanisha sayari yetu hii na watakatifu wake kutoka mbinguni. Mafundisho na matumaini haya kwa sasa vimo kwenye mashambilizi makubwa na jamii za ulimwengu huu—yaani ukweli wa kwamba Wakristo wajione kuwa ni wapitaji na watumwa hapa ulimwenguni.

17 Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; 18 naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa,

Mungu alitoa tamko hili, na kwamba Ibrahimu aliamriwa kabisa na wajumbe wa Mungu (Malaika wa Mungu) kuahirisha mchkato ule.

19 akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.

Kwa hiyo Ibrahimu alikuwa na imani kubwa kiasi kwamba hata kama Mungu angemwambia amuue mwana wake, alijua kwamba alikuwa na uwezo wa kumfufua tena na kuwaita wazao wa dunia hii kupitia kwa Isaka. Alikuwa na ujasiri usio na shaka na imani kamilifu kwamba hata kama Mungu angemuamuru amtoe mwana wake ili afe, ni kwamba angeweza kumfufu tena mwana wake. Hili ni tendo la hatari sana katika kuitendea kazi imani. Watu wengine hawana hata imani ya ile ndogo ya kuihatarisha kazi yao, kwa juhudi ya kumtafuta au kumuishia Mungu wa kweli, achilia mbali kuwaambia wawatoe watoto wao.

20 Kwa imani Isaka akawabariki Yakobo na Esau, hata katika habari ya mambo yatakayokuwa baadaye. 21 Kwa imani Yakobo, alipokuwa katika kufa, akambariki kila mmoja wa wana wa Yusufu, akaabudu akiegemea kichwa cha fimbo yake.

Na hii ndiyo maana aliwabarikia Efrraimu na Manase. Baraka hizi walipewa watu wetu kwa njia ya imani, wakujua kwamba zitatimilika na zilitimilika. Baraka walizopewa wana wa Yusufu zilitimilika miaka takriban elfu tatu (au zaidi) baada ya kifo cha mababa yao. Hii inamaanisha kwamba ni zaid ya miaka elfu tatu tangia kifo cha Yakobo, kabla Baraka kamili hawajaziona wakipewa hawa Efraimu na Manase. Hata sasa hazijaonekana kikamilifu, kwa kuwa Masihi hajawapa Baraka kamili ambazo ni za amani na za haki ya mzaliwa wa kwanza.

22 Kwa imani Yusufu, alipokuwa amekaribia mwisho wake, alitaja habari za kutoka kwao wana wa Israeli, akaagiza kwa habari ya mifupa yake.

Yusufu aliomba wamchukue na kumrejesha hadi nchini Israeli ili wakamzike huko. Alijua kwamba watu wake walikuwa utumwani kama watumwa tu huko Misri kama taifa, na tena alimpa maelekezo mwanawe kwamba watarejea tena nchini Israeli na watamzika yeye huko kipindi watakachotoka huko maarufu kama cha Kutoka. Haya yote yanatokana na uelewa wa unabii na kuielewa imani. Haya ni matendo na kazi ya Roho Mtakatifu ambaye ndiye aliyekuwa anatenda kazi miongoni mwa watu hawa, akiwaambia yale yaliyokuwa yanakuja kutokea na kutimilika katika siku zilizokuwa mbele yao. Mambo haya yote yako mbali sana kutimilika. Sura hii inayoelezea imani ina maana nay a muhumu sana.

23 Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme. 24 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; 25 akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo; 26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.

Huyu ni nabii Musa ambaye anapitia mashutumu makubwa kwa ajili ya Masihi. Utawezaje kumtenganisha Musa na matendo yake kumhusu Masihi, wakati Agano Jipya linaeleza kwa wazi sana kwamba mateso na mashutumu aliyoyapitia Musa huko Misri yalikuwa ni kwa ajili ya Masihi. Alifanya yote haya kwa niaba ya Yesu Kristo. Nili ni fundisho la muhimu na lenye nguvu sana.

27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana. 28 Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao. 29 Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa. 30 Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba. 31 Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani. 32 Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; 33 ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, 34 walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. 35 Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora; 36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; 37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; 38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi. 39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; 40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.

Mambo mawili na ya muhimu kwenye andiko hili ni:

1. Imani ilikuwa ni kitu cha muhimu sana katika kuzitii sheria na kanuni za Mungu; na

2. Licha ya kuwa walikuwa na imani kuu hivi, bali hawakuweza kuzifikilia na kuzipata ahadi. Hivyo ni kwamba imani peke yake haimpi hakikisho mtu la wokovu.

Hicho ndicho kigezo kikubwa cha matendo. Kuna mlolongo wenye masharti wa matendo unaohitajika kuwanao wateule wote. Imeni ni kitu kimoja tu kuhitajika kwanza ili kuupata wokovu. Vitu vingine ni toba na ubatizo kwa kupitia ndani ya mwili na damu ya Yesu Kristo na kuanza kuzitunza amri za Mungu na kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono na kuendelea kiimani katika roho. Masharti haya yote yanaendana pamoja na ni ya muhimu. Imani yenyewe isipokuwa na matendo imekufa. Wewe sio Mkristo kabisa kama utathani kwamba kwa imani peke yake unaweza kuurithi Ufalme wa Mungu. Hutaweza kuurithi kwa namna hiyo peke yake.

Yakobo anasema kwamba Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. (Yakobo 5:15) Sababu ya kuandikwa kwa andiko hili kunahusiana na injili inayofundisha masuala ya kiafya na ustawi na mafundisho yahusuyo magonjwa yatokanayo na maisha ya dhambi ambayo pia yanahusiana na upotoshaji. Uponyaji wa mtu binafsi yake kwa njia ya imani unajiri kwa mambo yote mawili, yaani kimwili na kiroho na hivi ndivyo inavyotenda kazi. Hatuna shaka kabisa kuamini kwamba magonjwa ni matokeo ya maadhi ya dhambi, lakini sio magonjwa yote yanasababishwa moja kwa moja na dhambi alizozitenda mtu.

Huu ni ukweli uliodhahiri. Dunia hii sasa imekuwa ni mahala pasipo na utulivu kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu sita sasa ya utunzaji mbaya. Sio kweli kwamba unapokuwa unaumwa basi umetenda dhambi. Na wala sio ishara ya kutokuwa na imani tunapomshuhudia mtu akifa kwa ugonywa wa saratani.

Imani ni kitu muhimu sana kwa ajili ya uponyaji, bali dhambi ni lile tendo la kuzivunja au kuasi amri za Mungu (1Yohana 3:4). Kwa hiyo, imani inauhusino wa moja kwa moja na sheria kwa ustawi wa kila mwanadamu (hususan ustawi wa kiroho). Kuna dhambi nyingine zinazompelekea mtu kupatwa na hukumu ya kimwili. Kama ukichagua kuwa mlevi basi unakabiliwa na adhabu ya kimwili kuibeba. Adhabu yenyewe ni ukweli kwamba hutaweza kula vizuri na mfumo wako wa kimwili utadhoofika.

Uasi wa aina yoyote ni dhambi (1Yohana 5:17). Haki na utakatifu ni mambo yaliyo sawa na vinatokana na neno moja tu la Kiebrania (Zedek au Zadok). Kwa hiyo, maneno yote haya; yaani haki na utauwa na imani yote yanahusiana kwenye torati yakisomeka kama mwenye haki au mtauwa ataishi kwa imani (Habakuki 2:4 iliyonukuliwa kwenye Warumi 1:17; Waebrania 10:38). Kwa hiyo imani ni ya muhimu ambayo kwayo wateule watatembea katika utii au kumpendeza Mungu kwa kuzishika amri za Mungu. Hii ndiyo muhimu ambayo kwayo mtu anatakiwa aendelee kuwa na imani, akiwa imara na kujisimamia, na asiyumbe na kutoka nje ya tumaini la injili (Wakolosai 1:23).

Mtume Yakobo analipanua suala la imani kwenye Yakobo sura ya 2. Chanzo cha tatizo kinakutikana kusababishwa na hali ya kuwapendelea watu. Kitendo hiki cha kuwapendelea watu fulani kimekuwa ni tatizo kubwa sana kwenye Makanisa ya Mungu kwa kipindi cha karne kadhaa sasa. Mungu hana upendeleo (2Samweli 14:14) na ilikuwa hivyohivyo kwa Kristo hakumpendelea mtu yeyote (Mathayo 22:16; Marko 12:14). Yakobo aliliona tetizo hili na kuliandika kwenye waraka wake wa Yakobo 2:1 (kwa sehemu akaandia kwa kutumia neno prosoopolempsiais linalomaanisha kuwaonyesha upendeleo au kuwaonea haya watu tazama kwenye kamusi ya Marshall’s Interlinear) (sawa na ilivyoandikwa kwenye jarida la  Kuwapendelea Watu (Na221) [Respect of Persons (No. 221)].

Yakobo 2:1-26 Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu.

Kwa hiyo imani ina namna nyingi mbalimbali (ni ya namna mbalimbali) au namna ambayo kwayo wewe unaweza kuishikilia imani.

2 Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; 3 nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, 4 je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? 5 Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? 6 Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! Matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu? 7 Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa? 8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema. 9 Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji. 10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. 11 Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. 12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru. 13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.

Kwa maneno mengine tunaweza kusema kwamba, kwa kadiri unavyohukumu wengine ndivyo na wewe utakavyohukumiwa. Ukihukumu bila huruma na kama unakuwa mkali kwa wengine na kama ukiwa ni mtu mwenye hasira ya karibukaribu na ikiwa unawachukulia hatua kuwahukumu wengine kirahisirahisi, ndivyo vivyohivyo watu wale watakavyokushughulikia wewe. Ndivyo hivyohivyo wale watu watakavyokukasirikia na kuchukizwa na kukuchukulia hatua wewe na kukutendea wewe kwa mintaarafu ileile uliyowatendea wengine. Mungu anautumia utaratibu huu ili kukurudi wewe na kukurejesha kwake, anapokuwa anakushughulikia wewe.

Watu wanaosimama kwenye kazi ya Mungu, au wanaojaribu kuyageuza mambo yaliyokusudiwa ya matendo ambayo Mungu ameyafundisha, yafanyike hivyo. Anauwezo wa kuwaondoa watu na anauwezo pia wa kuwaua. Kuna sababu za muhimu sana. Ni jambo la kutisha kuangukia kwenye mikono ya Mungu aliyehai. Mambo yanayofanywa kwa Baraka au pasipo na Baraka zake Mungu. Kama yanafanywa na Baraka zake Mungu na kama unaifanya kazi ya Mungu, basi usijaribu kamwe kuiharibu kazi ya Mungu, kwa kuwa unapigana na Mungu na atakushughulikia.

Uhusiano kati ya imani na maingiliano yake na sheria vinaonekana kwenye maandiko haya (Yakobo 2:1-13). Cha umuhimu zaidi anachoonyesha hapa ni ubaya mkubwa uliopo kwenye tabia hii ya kuwapendelea watu, kuwa inaonekana pia kwamba ni ukiukaji wa haki na hivyo inakuwa ni dhambi au uovu. Hakutakiwi kuwepo na tabia hii ya kuwapendelea watu kwenye Kanisa la Mungu.

Mtume Yakobo anakwenda mbali zaidi kwa kufananisha uhusiana uliopo kati imani na matendo ambavyo anavielezea kwenye maandishi haya.

14 Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa? 15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, 16 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? 17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. 18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu. 19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. 20 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? 21 Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? 22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale. 23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. 24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake. 25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine? 26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

Yakobo sura ya 2 inaungana mkono na Waebrania sura ya 11. Imani na matendo vinakwenda pamoja. Tendo hilohilo ndilo linatakiwa kufanyika hata leo..moja ni lile la imani na jingine ni la matendo. Matendo yenyewe yanatuama kwenye imani.

Kwa hiyo imani iliendana na matendo hata kabla ya Musa na Ibrahimu na Ibrahimu alihesabiwa haki kwa matendo yake. Imani ilionekana kwa matendo yake na imani inakamilika kwa matendo. Imani pasipo matendo imekufa. Imuhimu wa sheria ni kwamba amri kuu nay a kwanza inashikwa kwa njia ya imani na kwa kupitia matendo haitenganishwi. Kuilinda kwa bidii amri ya kwanza miongoni mwa nne za kwanza, utaona kwamba amri kuu ya kwanza inahusu kumpenda Mungu ndivyo inavyosisitiza.

Jambo la nne la muhimu kulijua katika kumuabudu Mungu ni utunzaji wa Sabato na hili ni jambo la muhimu sana. Hili ni jaribio linaloweka ufafanuzi wenye kutambuliwa kuwa unamuabudu Mungu mmoja na wa kweli. Amri ya kuishika Sabato ni amri ya jaribio miongoni mwa amri kuu na ya kwanza. Tunapaswa tukumbuke hivyo sisi sote. Na hii ndiyo sababu watu wengi wanaipinga sana; na kwa nini waamini Utatu wanajikuta kuwa ni vigumu sana kuishika amri hii.

Wakati kwamba amri hii kuu na ya kwanza inaweza kushikwa kwa imani miongoni mwa hizi tatu za kwanza, matendo ni ya muhimu katika kuishika amri hii ya nne. Zaidi sana kwamba amri kuu ya pili inayosisitiza kumpenda jirani yako, inaonekana kwa njia ya matendo tu na ndiyo maana imani bila matendo imekufa.

Neno lililorudiwarudiwa la Usifanye ni la kinyume au makatazo kwenye amri hizi kumi, bali kuna mambo yanayoruhusiwa au kuagizwa yatendwe pia. Amri ya tano na ya kumi ni amri zenye ahadi na zina mambo mazuri ndani yake. Amri ya kwanza pia ni amri yenye ahadi ndani yake. Amri ya kumi inayosema Usitamani inahusika na nia ya moyoau mawazo ya mtu. Unapaswa kuwa na mawazo chanya ili uweze kuishika amri hii ya kumi, jambo litakalokusaidia hatimaye uweze kuishika sheria nyingine ya kumpenda jirani yako. Mungu hana upendeleo (Matendo 10:34; Warumi 2:11) na wala hampendelei mtu anapotoa hukumu zake (Mithali 24:23) kwa liwa sio vizuri kufanya hivyo (Mithali 28:21) na kwa hiyo imani bila matendo kutamzuia mtu yeyote kuuingia ufalme wa mbinguni. Kitu muhimu ili kuuingia Ufalme wa Mungu uitii kwa njia ya imani katika Yesu Kristo, na sio kwa imani katika Yesu Kristo tu pasipo kujali suala la utii.

Ikiwa una imani katika Yesu Kristo, basi ziti amri zake sasa. Ikiwa unataka kuwa na Roho Mtakatifu, basi zitii amri za Mungu sasa. Utii wa wateule unaonekana kwa kuzitii amri za Mungu. Hebu mtii Mungu na kuzishika amri zake (Mhubiri 12:13). Hata amri iliyondogo sana haipaswi upuuziwe ama ivunjwe (Mathayo 5:19). Ikiwa tunataka kuingia uzimani, basi tunatakiwa kuzishika amri zake (Mathayo 19:17). Mathayo 19:16-22 inaonyesha umuhimu na nia ya amri za Mungu.

Mathayo 19:16-22 16 Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? 17 Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. 18 Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, 19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 20 Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena? 21 Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. 22 Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Nia yake ni kwamba tunapaswa kujitoa sadaka kwa kusaidiana na kwa matendo. Tukisema kwamba tunampenda Mungu na huku tukiwa hatutendi jambo lolote, ndipo tutakuwa hatuishiki imani na hatutaweza kabisa kuuingia Ufalme wa Mungu. Inatunapasa kujitoa mhanga kwa ajili ya Ufalme wa Mungu na kumfuata Kristo. Kumbuka kuwa maneno matupu na yasiyo na matendo hayana maana.

Waraka kwa Waefeso unakazia kwenye fundisho lake kuu kuwa ni utii kwa Mungu na kuvumilia mateso hapa duniani, na kile ambacho ulimwengu huu wa sasa unakita kuwa utawala usiozingatia haki.

Waefeso  6:1-20 inasema: 1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. 2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia. 4 Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. 5 Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo; 6 wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; 7 kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu; 8 mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru. 9 Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo. 10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,

Idadi hii ya silaha inamaana sana. Zinahusu maandalizi ya kuzibeba zilaha za Bwana zinazotokana na kweli. Ngao ya silaha hizi zote ni kweli. Haitakiwi kuwe na uganganifu kwenye kile unachokifanya; wala kusiwe na hila na kusiweko na kujidanganya mwenyewe.

15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

Kazi kubwa uliyotupiwa ni kutokubaliana na mashambulizi yahusuyo imani yako; imani ambayo kwayo sisi tumefanyika kuwa ni sehemu ya mwili wa Yesu Kristo; ambayo kwayo tunaifanya kazi ya Mungu, ambayo tunaongoizwa na Roho Mtakatifu na ambayo kwayo sisi tunaunena ukweli na jinsi unavyotakikana kuwa. Haya yote yanaanzisha mabishano. Njia pekee ambayo adui wetu anaipata kwako ni kutoka kwa watu walio karibu nawe ambao kwao anaweza kuwatumia kukushutumu wewe. Atafanya hivyo kwa kupitia kwa watu wanaojidhania kuwa wao ni watakatifu.

17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;

Kofia ngumu ya kichwani ya wokovu hulinda kichwa chako. Neema iokoayo ya Jesu Kristo inalinda mawazo yako pia. Umepewa fursa ya toba, ambayo kupitia kwa kuielewa dhimbi kunatupelekea hukumu. Kisha kwa ajili ya kujisikia kuhukumiwa moyoni ndipo tunafikilia kutubu kwenye neema iokoayo ya Yesu Kristo. Ukamilifu wa dhabihu ya Kristo ndiyo ngao ya wokovu.

Silaha tunayoizungumzia ni neno la Mungu. Huu ndiyo upanga ukatao kuwili tulionao mikononi mwetu. Na hii ndiyo maana tunaweza kuwashughulikia watu hawa ambao wanaiyumia vibaya. Ni silaha zetu na sio zao, kwa kuwa yale wanayoyasema hayawezi kustahimili, wakati yanapojaribiwa.

18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; 19 pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili; 20 ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena.

Maombi haya yanapaswa yaombwe na kila mmoja anayeliitia jina la Yesu Kristo, na kunenwa katikati ya wateule wanaozihubiri siri za Injili.

Wazo linaloshinikiziwa hapa ni kwamba malaika walioasi ndiyo msingi au sababu ya vita tunayoendelea kupigana nayo. Mamlaka na nguvu hizi zimeanzisha mfumo usio wa haki. Imani ndiyo moja ya kitu muhimu katika silaha za Mungu. Silaha kuu ni upanga war oho ambao ndio neno la Mungu. Kwa hiyo, Biblia na hasa Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale yalikuwa ndiyo silaha kuu ya wateule. Umuhimu wa kukesha ni kitu muhimu sana. Adui anatafuta fursa ya kuwapotosha wateule kwa mafundisho ya uwongo yanayolenga kufutilia mbali umuhimu wa kuzishika sheria na amri za Mungu na kuwadanganya wateule kama ikiwezekana. Ili kufanikisha hilo wanajaribu kuzibadili amri za Mungu na mahala pake kufidia amri za wanadamu (Mathayo 15:9; Marko 7:7). Tunamjua Mungu kwa kuzishika amri zake (1Yohana 2:3). Kama mtu yeyote atasema kuwa anamjua Mungu na huku akisema kuwa sio muhimu kuzishika amri zake basi yeye ni mwongo na kweli haimo ndani yake (1Yohana 2:4). Na yeye hayumo kabisa miongoni mwa wateule.

1Yohana 2:1-6 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, 2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. 3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. 5 Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake. 6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.


Tunatembea kwenye mapito aliyoyapitia Kristo na tunazishika amri za Mungu na kwa hiyo tunaonyesha upendo wetu kwa Mungu katika Kristo. Kwa kutembea kwenye mapito aliyoyapitia Kristo ndipo upendo wetu kwa Mungu unakamilika.

Tusidanganyike na mabishano yanayotafuta kuzipunguza amri kwa Usemitism. Waalimu kama hawa wa uwongo wanafundisha mafundisho ya mapepo na mashetani. Na hakuna nuru kwao (Isaya 8:20).

q