Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[089]
Mafundisho ya Kizushi Kwenye Kanisa la Mitume
(Toleo La Edition
2.0 19950128-20000311)
Jarida hili linashughulikia
sababu za kijipenyeza kwa mafundisho ya uzushi kwenye makanisa ya Wakolosai na
Wagalatia. Kwa kweli hii ni sehemu ya
mlolongo wa majarida ya mafundisho ya Sheria ya Neema na inashugulika na nafasi
ya Sheria au Torati kwa mujibu wa Mtume Paulo. Andiko linaendelea mbele kwa
kuendeleza nafasi yake kwenye Makanisa yaliyosimamiwa na Mtume Yohana.
Mafundisho ya Wanostiki yamechambuliwa pia. Nafasi ya kanisa la karne ya kwanza
kuhusu Masihi ya Ujio wake mara mbili pia imechambuliwa kutokana na ushahidi wa
Gombo zililogunduliwa kwenye Bahari ya Chumvi. Nafasi ya Paulo inaonekana kuwa
imekosewa kiuandishi na waorthodoxi wa siku hizi. Jarida hili linashughulika na
jarida linalofuatia la Tofauti Iliyo Kwenye Torati (Na. 96) na Mandiko
ya Matendo ya Sheria-au MMT (Na. 104).
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati
Miliki © 1995, 2000 Wade
Cox)
(tr.
2015)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Mafundisho
ya Kizushi Kwenye Kanisa la Mitume
Kumbuka: jarida hili yapasa lisomwe sambamba na kanda
ya tepu.
Utangulizi
Vitabu vya
Wakolosai na Wagalatia vinachukuliwa kuwa na idadi kadhaa ya mambo ya
kimafundisho yasiyo sahihi kuhusu Agano Jipya. Miongoni mwa mambo mengine, ushindaniau
mabishano ya sheria unaondolewa mbali ukituama kwenye kuubiri ni makosa.
Mabishano makubwa kuhusu kosmolojia sahihi ya Agano Jipya yanahitaji kuendelezwa.
Mafundisho ya Uzushi kwenye Kanisa la Mitume yangeweza kuunda sura ya kazi ile.
Historia ya Mambo Yaliyopita
Kanisa la Mitume
lilikabiliwa na mlolongo wa matatizo wakati wa uchanga wake. Makanisa mengi
miongoni mwa yale tuliyonayo kwenye rekodi ya Biblia yalianzishwa na au chini
ya Mtume Paulo kwa kuwepo kwake. Matendo mengine kama vile wale watu wa
Korintho walijiunga na matendo ya kawaida ya kimwili, ambayo yalikuwa yamepotoshwa
au kudunishwa na hali ya halisi ya kiroho ya Kanisa. Matatizo mengine yalikuwa
yamejikita sana na yaoonekana kuwa hayajamalizika kabisa na kueleweka. Hii
inaonekana kuwa ilitokea kwa sababu ya kosmolojia iliokuwa imekubalika na Makanisa
ya Agano Jipya hayakueleweka vyema na teolojia ya kipindi cha kabla ya mtaguso
wa Nikea. Waraka kwa Wakolosai ni wa muhimu sana kwa ajili ya kuielewa kosmolojia
ya Kanisa la Agano Jipya.
Andiko linguine
la muhimu, lakini kwa upana mdogo, ni lile la Wagalatia. waraka kwa Waebrania
ni andiko muhimu na la maana sana kuhusu uhusiano mtambuka uliopo kati ya Agano
la Kale na Jipya na kosmolojia yake. Kwa kuyajua makosa ambayo kwayo makanisa
haya yaliangukia tunaweza kuelewa vyema juu ya kosmolojia yake asilia. Wakati
maandiko yanapotathiminiwa tunaweza kuona kiusahihi sana kuhusu jinsi makosa
haya yalivyo, na kwa zaidi sana, tunaweza kujua jinsi yalivyotokea.
Wakolosai
Asili ya
Andiko
Makosa na uzushi
wa kimafundisho wa Wakolosai yalikuwepo--yaliandelea na kutoonekana kwa kipindi kirefu
kwa msingi wa kukubalika kwa uelewa kuwa Wakolosai waliyachukua na kuyaendeleza
au kuyakumbatia kutoka kwenye imani na mafundisho ya Wanostiki, ambayo hayakuweza
kubuniwa au kutungwa vizuri na kikamilifu kutokana na maandiko.
Makosa haya
yalidhaniwa kuwa yalihusika pia kuwa ni sehemu ya uhafidhina. Hii ilitokana na
kutoelewa au kuelewa vibaya maneno yaliyotumiwa na Mtume Paulo kwenye maandiko
au uandishi wake. Muono na mtazano wa Paulo kwenye andiko lenye dhana na lengo
hilo ni la kificho na inahitaji kutathiminiwa na kuandikwa upya.
Wakolosai 2:8-10,16
inaeleza kuhusu dhana au nadharia ifuatayo:
· mapokeo (B"DV(@F4<) [paragosin]
(2:8);
· ukamilifu (B8ZDT:") [plerõma] (1:9; 2:9,10);
· filosofia (N48@F@N4") [philosophia] (2:8);
· kula na kunywa ($DfF,4, B`F,4) [brõsei,
posei] (2:16);
· falme na mamlaka (•DP"4, ¦.@LG4"4) [archai,
ezousiai] (2:15); na
· mambo mengine
ya duniani (FJ@4P,Ä" J@Ù 6`F:@L) [stoicheia tou kosmau]
(2:8,20).
Maneno haya
yanakutikana yakitumika pia kwenye imani ya Wanostiki
wa Kiyahudi na kwa Wahelekini wa
mrengo wa Kisynkretism. Kwa mujibu wa
Bacchiocchi (kitabu chake cha From
Sabbath to Sunday: A Historical Investigation into the Rise of Sunday
Observance in Early Christianity, Appendix, pp. 343f. [Kutoka kwenye Sabato hadi Jumapili: Udadisi na Utafiti wa Kihistoria
Kuhusu Kuinuka au Kuanza kwa Maadhimisho ya Jumapili kwa Wakristo wa Zamani])
anasema kuwa maneno haya ni
Yalitumika sawasawa na
wafafanuzi katika kuelezea au kufafanua utohoaji wa maneno haya kytoka kwenye
imani ya Kinostiki ya Wakolosai.
Bacchiocchi
anaweka rejea maandiko ya Jacques Dupont, E. Percy, Lightfoot na Lyonnet na
kuwafanya kuwa ni wanazuoni wa mfano waliouelezea uzushi kuwa ni mtindo wa Unostiki wa Kiyahudi. Kwa namna nyingine,
Günther Bornkamm kwenye kitabu chake cha “The Heresy of Colossians” in Conflict
at Colossae, [yaani “Mafundisho ya Kizushi ya Wakolosai” Yanavyopingana Kinyume na Wakolosai], p.
126 anasema kimtazamo wa ndani sana:
Bilashaka inaonekana
kuwezekana kwangu hata hivyo, kwa upande mwingine. Mafundisho ya Wakolosai
kuhusu vitu vinavyohusiana na imani za kizamani za kale na nadharia ya
Kiteolojia ya Aeon-wa mashariki, ambayo yalikuwa yameenea sehemu zote na
kuaminika kiutendaji na imani ya Waeleniki wa mrengo wa kisynkretism; sawa na
alivyoandika na kuamini Ernst Lohmeyer, kwenye kitabu chake cha Der Brief an die Kolosser, 1930, pp. 3
f.; M. Dibelius, An die Kolosser,
Epheser, An Philemon, 1953, excursus on 2:8, and 2:23. (Bacchiocchi, fn. to
p. 343.)
Bacchiocchi
anaendelea mbele kwenye pango kitita kwa kusema kuwa
Wengine
wanatafsiri mafundisho haya ya kizushi ya Wakolosai kuwa kama usynkretism ya
Kiheleniki na nasaba za Kiyahudi; soma kitabu cha Edward Lohse, cha A Commentary on the Epistles to the
Colossian and to Philemon, yaani Ufafanuzi
wa Waraka kwa Wakolosai na Filemoni 1971, pp. 115-116; Norbert Hugedé, Commentaire de l'Épître aux Colossiens,
pp. 9, 143; W. Rordorf, Sunday, p.
136: 'Sisi kwa kweli tunashughulika na uwezekano wa mkondo wote mzima wa kisynkretistiki
ambayo kwayo matirio za Wakristo wa Kiyahudi yamekuwa na mwingiliano kwa ndani
zaidi na mafundisho ya walio wa jamii ya Kiheleniki na uthibitisho wa kimashariki';
sawa kama na asemavyo Handley C.G. Moule, kwenye kitabu chake cha Colossian Studies, 1898, aliyeelezea
mafundisho ya kizushi kuwa ni kama ni 'mchanganyo wa mafundisho ya Kiyahudi na
Unostiki, kwa rejea pana wa neno la baadae.'
Uelewa
unaweza kuchambuliwa kutoka kwenye waraka na kosmolojia ya rejea za Agano Jipya
hususan kwenye Ufunuo na kwa kusababishwa au kufanywa upya tena kwenye
mlinganisho uliofanywa uliofanywa hapa kwenye sura ya 2, 3 na 4 [Alioufunua Mungu]. Mara tu kosmolojia ya
biblia inapoeleweka, sababu ya asili ya tatizo huko Kolosai ilisahihishwa kwa namna
iliyoonyeshwa kwamba Kanisa la huko Kolosai lilikuwa linakosea au linapotoka na
kwamba upotoshwaji wao yalitokana na kutoelewa vizuri kwa sehemu ya kanisa kwa
mtazamo mpana ambalo halikuwa ni kwa ajili yao wenyewe kuchukua jukumu la
kukanusha au kuyapinga. Kwa hiyo tunakabiliwa na upotoshaji na makosa ya utenda
kazi wake zaidi ya kuwa tu ni muigo mzima wa pamoja. Kutajwa kwa teolojia ya Aeon kulikofanywa na Bornkamm ni ishara
au alama au nembo kubwa na muhimu kwenye mshangao. Teolojia inayojulikana kama ya aeon inadaiwa pia kuwa ni ya Kiebrania.
Bacchiocchi anayachukulia
mafundisho ya kizushi ya Wakolosai kuwa yalianzishwa uzushi wa kiteolojia na kiutendaji. Anachukulia na kuona kwamba
Kiteolojia,
‘wanafilosofia’ wa Kikolosai (2:8) walikuwa wanashindana na Kristo kwa madai ya
kibinadamu. Chanzo chake cha mamlaka, kwa mujibu wa Mtume Paulo ilikuwa ni mapokeo
yaliyotengenezwa au kuratibiwa na - B"DV*@F4H [paradosis]
(2:8) na lengo lake lilikuwa ni kushirikisha hekima ya kweli - F@N4" [sophia] (2:3,23), 'ujuzi- (<äF4H [gnosis]
(2:2,3; 3:10) na- Fb<,F4H [sunesis]
(1:9; 2:2). Ili kuupata ujuzi kama huu Wakristo waliaswa kuheshiku kwa kiasi
kikubwa kanuni za kikosmikia (2:10,15) na kwenye mambo ya kilimwengu- J FJ@4P,Ã J@Ø P`F:@L [ta
stoieea tou kosmou] (2:8,18,20).
Ni huhimu
kutenganisha kabisa makosa ya kiteolojia nay ale ambayo Mtume Paulo aliyokuwa
akiyasema kuliambia kanisa la Kolosai. Elohim, kama ilivyoonyeshwa na dhima ya
kibiblia, ni Watakatifu wengi ambao kwamba Mwanakondoo ni Kuhani Mkuu, lakini
yeye ni mmoja wao aliwa kama mwenzao au mshirika mwenzao wa dhati. Ufunuo 5 inaonyesha
kuwa kuna majukumu yaliyotolewa kwenye Baraza la Elohim. Ufunuo 5:8 inasema
wazi kwamba kila mmoja wao kati ya wazee ishirini na nne amepewa vinubi na vitasa
vya dhahabu vilivyojaa manukato ambayo ni maombi ya watakatifu. Ni wazi sana
kwamba wazee hawa wana jukumu la kuwaweka sawa wateule. Ni wazi na dhahiri sana
kwamba katika Kolosai urukaji wa msingi ulifanyika wakati kwamba kulikuwa na Elohim
ambaye alikuwa amefanyiwa maombi moja kwa moja. Matendo ya zama kale ya
kuwaomba wafu na mashetani yalishamiri kwa itikadi au imani zote mbili za Kishamanism
na Kibabeloni. Muonekano au kujitokeza wa kimizimu iliyokutikana kwenye imani
na hekalu la kimythilia huko Merkabah inaonekana kufanya msukumo wake kwenye maeneo
ya Palestina kwenye karne hii ya kwanza. Jarida la Imani ya Ulaji wa Mbogamboga Tupu Kwenye Biblia (Na. 183) linaonyesha kuendelea kwa imani ya Kinostiki
yenye mchanganyiko wa upaaji kwenye imani ya Kikristo. Ingeonekana kuwa matulizo ya imani ya kuwaomba malaika na anayepaa kwa
kiasi fulani iliingia kwenye kanisa la Kolosai, huenda msingi wake ulituama
kwenye sababu zilizotuama kwenye Ufunuo 5:8. Kitendo cha kuabudu sanamu
kiligeuzwa na kubadilishwa na matulizo ya watakatifu na hatimaye ilijipenyeza
kwenye imani za Ukristo Mkongwe. Hata hivyo, taratibu za utakaso za kiupaaji
ilionekana kuwa na mafanikio yenye kikomo kikubwa zaidi. Mapokeo yal;oyotajwa
na Mtume Paulo yanaonekana kutuama kwenye roho msingi za mwanzoni na
zimeingiliana kwa undani na filosofia. Hiki ni kifungu kigumu sana kueleweka kinachojumuisha
mikondo mitatu tofauti ya kinadharia – iliyojulikana kuwa ni mvuto au msukumo
wa upande mmoja au mwingine zaidi wa wanafilosofia; yaliyotuama kwenye mapokeao
ya wanadamu ambayo kwayo, mambo au desturi za Kiyahudi zimepata mashiko; na
mwisho kabisa, utendaji au ushabihiano wa imani za kuomba roho za wafu. Bila
shaka kabisa kwamba inahusiana na uheri wa viumbe duni kwa kuwa Mtume Paulo
anaendelea kwenye Wakolosai 2:9-10 kumwelezea Kristo kuwa:
Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Na
ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.
Inapasa ijulikane
kuwa neno utimilifu au ukamilifu wa kimungu
limetoholewa kutoka kwenye neno 2, `J0J@H [theotetos].
Kama ilivyoonekana kutoka kwa Thayer (ukurasa wa 288) uungu unatofautiana na umbinguni
kama kitu kinachotofautiana na ubora au mwonekano. Kwa hiyo, mungu au uungu
unaotajwa hapa uliokuwa ndani ya mwili wa Kristo, ni roho wa Mungu. Ilikuwa ni kitu
hiki muhimu inayotoka kwa Mungu ambayo inamwezesha Kristo kuwa mmoja na Mungu.
Wakati Elohimu mwingine alipochukua roho hii, jambo ambalo Mtume Paulo
anachoonekana kufanya ni kwamba Kristo ana mamlaka na ukamilifu wa ubora au
kiwango cha kiuungu na kwamba aliwakilisha tabia za Baba. Hii inafanya
kuonekana kwa vitu vingine visivyofanana kwenye uthibiti wa wateule. Kristo ni
kiongozi au kichwa cha tawala na mamlaka zote (Wakolosai 2:10). Mungu ndiye
mlengwa kwenye maombi. Kristo na wazee viongozi wanatenda kazi kwa uwakilishi tu.
Kwa hiyo, suala lilikuwa ni yule anayetamalaki na kwenye mamlaka. Bacchiocchi
(loc. cit.) anasema kuwa uhusiano uliopo wa ulimwengu (Wakolosai 2:8,18,20) kwamba:
Nyingi ya ufafanuzi wa fasili ya maandiko, zimetoholewa kwenve tafsiri ya stoicheia (hususan kwenye msingi wa kifungu kinachowiana kwenye Wagalatia 4:3,9; sawa na 3:19); vinavyowaonyesha wao kuwa ni malaika wapatanishi wa sheria (Matendo 7:53; Wagalatia 3:19; Waebrania 2:2) na miungu ubashiri wa kinyota wa kipagani ambao waliaminiwa na kuchukuliwa kuwa ni wadhibiti na kuhusika na hatima ya wanadamu. Ili kupata ulinzi kutokana na nguvu hizi za kikosmiki na falme, “wanafalsafa” wa Kikolosai walikuwa wanawasihi na kuwataka Wakristo kufanya mkakati potofu wa kuwafundisha watu mafundisho ya kizushi ya kuwapa heshima malaika na kuziamini nguvu na uweza wao (2:15,18,19,23) na kuzifuata taratibu za kidini na matendo ya kiascentiki (2:11,14,16.17,21,22). Kwa mchakato ule mtu alihakikishiwa kuingia kwa kwenda na kushiriki kwenye “utimilifu wa kimungu- (B8ZDT:")" [plerõma]" (2:9,10, cf. 1,19). Makosa au upotofu wa kiteolojia, ndipo kimsingi yalitokana na kuwaingiza malaika duni waombezi kwenye mbadala wa Kichwa Mwenyewe (2:9,10,18,19) (pp. 344-345).
Bacchiocchi anaendelea
mbele kwa kusema hivi:
Matokeo yaliyo dhahiri ya nadharia hizi za kiteolojia yalikuwa ni msisitizo wa uascetiki wenyewe na itikadi kali ya mapokeo ya kidini. Hii inajumuisha na “kujivua mwili wa kibinadamu” (2:11) (inamaanisha wazi kabisa kuwa ni kutoka kwenye dunia); kuutendea mwili kitendo cha kujinyima (2:23); kukataza ama kutoonja au kutogusa vitu fulani fulani vya vyakula au vinjwaji (2:16,21), na kuadhimisha kiumakini siku takatifu na nyakati za sikukuu, miandamo ya mwezi na Sabato (2:16). Waktisto wanadhaniwa na kuaminika kuwa walifundishwa waamini kwamba kwa kujitoa kwao kutenda hivyo, hawakuwa wanajitoa imani yao kwa Kristo, bali zaidi tu ni kwamba walikuwa wanajongezea ulinzi na walikuwa wanajihakikishia kupata njia ya kuupata ukamilifu kamili (p. 345).
Dhana hii iliendelea
ikahusisha kuonekana kuwa na dhamira ya kuvikana vitu vilivyofuatia na
kupelekea kwa mtu anayemiliki kupitia kwa Kristo. Maombi yote yanapaswa
yaelekezwe kwa Mungu Baba, kwa jina la Kristo. Ingawa kuna nguvu
zinazomshawishi mwanadamu kuna Mwombezi au Mpatanishi mmoja tu kati ya Mungu na
mwanadamu. Wala kunana mahala popote kwenye Biblia panapoonesha kuwa aliwahi
kulengwa au kuombwa mtu mwingine yeyote ila Mungu peke yake ambaye ni Baba yetu
pia. Kitendo cha kuwa tulizo
la wazee kingeweza kuendeleza dhana ni ya kikosmolojia. Hata hivyo, kilichowazi
ni kwamba baadhi ya mapokeo ya Mafarisayo walioshika sheria au torati
yalijipenyeza kwenye Kanisa kwenye mchakato huu. Dhana ya kuamini roho za
mwanzoni za ulimwenguni ilikanganya kwa kiasi kikubwa sana suala la hili (sawa
na linavyosema jarida la Mandiko Kuhusu Matendo ya Sheria - au MMT (Na. 104)).
Tatizo la Sabao
Andiko la Isaya
1:14 kwa kawaida linatumika ili kuhalalisha ushikaji au kuadhimisha sikukuu za
Wakaldayo za Easter na sikukuu ya Krismasi inayoadhimishwa mwezi wa Desemba
katikati ya majira ya baridi, ambazo zimekatazwa na kupingana na sheria na
mafundisho ya Biblia. Kwa kweli, kwenye tafsiri ya Mfalme Yakobo ambayo maarufu
kama King James Version kwenye Matendo 12:4, andiko hili limepotoshwa kitafsiri
kwa makusudi kabisa kwa kuandika Easter
badala ya Pasaka. Kudhania au kufundisha kuwa Kristo aliliruhusu Kanisa
kuzibadilisha sikukuu zilizopangiliwa kwa mujibu wa mpango wa wokovu kwa kuzigeuza
kimbadala na sikukuu za kipagani wakati sikukuu hizi takatifu ziliwekwa na
kuanzishwa kwa maelekezo kutoka kwa Mungu kunaonyesha kutokuwa jambo la kawaida
na lisiloaminika wala kuingia akilini. Tertullian aliangukia kwenye kosa kama
hili wakati alipompinga Marcion kuhusu Sabato. Haieleweki vizuri ni kwa kiasi
gani Masihi alishiriki akiwa kama Elohimu au Malaika wa Yahova wa Agano la Kale,
Tertullian alionysha kuwepo kwa watu waliotenganishwa na walidhaniwa wote kuwa
ni Yahova wa Agano la Kale na Kristo kwenye Agano Jipya walioichukia Sabato. Tertullian
alilimtumia andiko hili la Isaya kuwa ni kama la juu sana kwenye Agano la Kale
na akahoji kuhusu Kristo kwa kusema kuwa:
Hata kama kiumbe
huyu hatakuwa ni Yule Kristo wa Wayahudi, bado yeye [yaani Kristo wa Agano
Jipya] alionekana kuchukizwa na siku hii takatifu sana kwa Wayahudi, alikuwa
anadaiwa au kuonekana sana kuwa anamfuata Muumbaji, kwa kuwa ni kama Kristo
[Masihi], kwenye mkakati huu wa kuichukia Sabato; kwa kuwa yeye alitambulishwa
kwa mdomo wa nabii Isaya kwa kusema: 'Miandamo yenu ya Mwezi na Sikukuu zenu
roho yangu inazichukia' (kitabu cha Bacchiocchi cha From Sabbath To Sunday: A Historical Investigation into the Rise of
Sunday Observance in Early Christianity [Kutoka Sabato Hadi Jumapili; Utafiti
wa Kihistoria ya Kuanza kwa Maadhimisho ya Jumapili Kwenye Ukristo wa Zamani],
The Pontifical Gregorian University Press, Rome, 1977 akinukuu Kinyune cha Marcion 1,1, ANF, Vol.
III, p. 271; (lakini mrejea wake ni kwenye mwanzo au chimbuko la uandishi wake
peke yake)).
Maoni ya Bacchiocchi
yalikuwa kwamba upingaji wa Tertullian kwenye Vitabu vyake vya I, II, III &
V ulionyesha kinyume cha utofauti na kile alichofundisha Marcion, kwamba aina
ya utunzaji wa Sabato uliofundishwa na Mungu wa Agano Jipya na ambaye ni Kristo
ulionekana. Mafundisho yote mawili yalikuwa yanashabihiana. Yote mawili
yalitokana na Mungu huyohuyo mmoja ambaye alikuwa ni Mungu wa migawanyiko yote
miwili. Kwa kupinga kwake kuhusu ushabihiano wake, hata hivyo, alipotosha kwa kuona
kuwa Sabato ni kama taasisi ambayo mara zote Mungu alikuwa ameipuuzia au
kuidharau. (Bacchiocchi, ibid., p. 187, fn. 61)
Torati
Ni kwenye Kitabu
cha V Sura ya IV ndiko Tertullian anajadili na kuibua wazo la kiumbe au mtu ambaye Warumi walimlinganisha na kiini cha mafunzo. Tertullian alimlinganisha
mtu huyu na hata chimbuko la sheria
au ya torati iliyodhaniwa kabisa kulingana au kufanana na kwamba torati ni
sheria iliyotolewa ili kuwaelimisha wateule kiimani. Anataja au kufanya rejea
kwenye dhana ya kwamba inayodhaniwa kutokana na Wagalatia, lakini hapa Paulo
anaonekana kutaja au kuelezea kuwa ni mafundisho ya kizushi, huenda ni undani, unaohusiana
na utulizaji wa nguvu au mamlaka za kiroho zinazoonekana kuwa ziliingia kwenye
Kanisa la Galatia na kufanikiwa kuingia kwenye sikukuu za kibiblia na kisha
kufanyika kuwa namna ya uhalali kwa kuambatana na sheria zaidi kuliko neema (Wagalatia
5:4). Tatizo hapa ni jinsi ya kuwakabili au kuwaendea Wakolosai. Tatizo la
Wagalatia yanaonekana kufanana na imani ya Kinostiki ambalo limeanzisha mafundisho
ya kizushi ya Wakolosai. Mafundisho ya kizushi yaliyokuwa huko Kolosai, kama
tulivyojionea, yalihusu “mambo” na “mapokeo” na yanaonekana kuwa ni ya kuzipamba
imani potofu ya kuamini nguvu au mamlaka za malaika au mapepo ambazo kupendeka
kwake kulihusiana na maadhimisho au kutazama “nyakati au kanuni zake- *Î(:"J"" [dogmata].
Kama tulivyoona,
imani hii potofu inaweza kuwa ilihusiana na kuanzishwa kwa imani au mwonekano wa
kisiri-fumbo ya Hekaloth kwenye imani au dini ya Kiyahudi kwenye karne ya
kwanza (soma kitabu cha Kaplan, cha Meditation
and Kabbalah [Tafakari ya Kabbala], Samuel Weiser, Maine, 1989 ili kupata
dondoo zaidi na za kina za imani au dini hii). Dhana ya kwamba utakaso unaweza kupatikana
kwa kuadhimisha au kuangalia nyakati (na, kwa hiyo, ni kuwatumikia malaika) ilikuwa
ni dhana ya kwamba “iligongomelezewa msalabani” na sio ile ya torati. Mabishano
haya yaliendelea kuenea kwenye ukweli kwamba ndani ya Kristo, utimilifu wote wa Mungu uko katika mwili
(2:9), na kwamba kwa hiyo aina zote za mamlaka yanayodumu yanamsaidia yeye ambaye ni kchwa cha tawala zote na mamlaka (2:10),
na ni kwa kupitia kwa Kristo peke yake (ambaye hana hali kamilifu ya uungu bali
pia kwa ukamilifu ukombozi na msamaha wa dhambi) (soma 1:14; 2:10-15;
3:1-5) ambayo kwayo, muumini anafikia ukamilifu
wa maisha (2:10). Paulo, kinyume na utaratibu huu wa kawaida, hafanyi
ionekane kuwa sheria ionekane hivyo, bali ni kwa njia ya ubatizo kama Bacchiocchi
anavyokubaliana na Harold Weiss aanayepinga. Torati kama inavyoitwa (<`:@H [nomos])
iko nje ya isemavyo Wakolosai 2 kwenye mjadala wenye utata na hii ilihusiana na
madai ya kwamba:
Mfundisho ya kizushi ya
Wakolosai kwa kweli hayakutokana na itikadi kali ya kihafidhina ya Kiyahudi
bali zaidi tu ni kwenye aina (syncretistic) isiyo ya kawaida ya kanuni za kiasetiki
na kikalti (*Î(:"J" [dogmata]) unaodharau
utimilifu wote wa ukombozi wa Kristo. (Bacchiocchi, ibid., p.347)
Hoja za Paulo kwa
Wagalatia na Wakolosai yalieleweka vibaya na mara nyingi yalieleweka vibaya, hususan
na wapinga Sheria au Nomia lakini hasahasa na wa Athanasians. Tertullian alikuwa
ni wa kwanza kati ya waamini Utatu wa mwanzoni ambao waliuchukulia upungufu huu
wa kiteolojia. Waamini Utatu hawakuyajua au kuyaelewa maana ya mabishano
yaliyopamba moto kwenye kanisa la Wakolosai kwa kuwa hawakuielwa kosmolojia ya
kwanza ya Ukristo. Mafundisho ya kizushi ya Wakolosai (nay ale ya Wavalentiniani)
yalikuwa yanawezekana tu kwa kuwa Kanisa la Kwanza lilikumbatia mafundisho ya
kikosmolojia (Ufunuo 4 et seq.) ambayo yalimwendeleza Elohimu kwa kumfanya kuwa
ni mshirika wa tatu ambaye Wavalentiniani walimuita Aeons wakimlinganisha na
mugu Aeon aliyekuwa anachongwa kwa kumuweka kichwa cha simbe. Jambo hili
lilifanyika kila mahali pengine popote.
Wagalatia
Tertullian anadai
kwamba kutokana na nukuu za Wagalatia na nyinginezozote penginepo zilikosea kwa
kiasi kikubwa kwamba Mungu alizidharau Sabato na sikukuu nyingine ziolizoamriwa
kwenye maandiko kwa kupinga kama ifuatavyo:
'Mnashika siku, na
miezi, na nyakati, na miaka.' [Wagalatia 4:10] -
Sabato, bado naamini, na ‘maandalizi yake' [tafsiri ya ANF inasema 'Coenas puras': huenda ni kama ilivyo kwenye B"D"F6,L"4 inayosema paraskeuai au maandalizi] ya kwenye Yohana
xix. 31'; soma kifungu chinachoitaja 'Pasaka' kwa unyumbulisho wa jambo hili] na
kifungu cha sikukuu, na ‘siku nyingine takatifu' [pia kwenye Yohana 19:31?]. kwa
kuachana hata na hizi, sio hata chini ya mazingira ya tohara, iliyoamriwa kwa
amri za Muumba, zilizonenwa na nabii Isaya, ‘mwezi mpya na sabato, kuita
makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada. Sikukuu zenu za mwezi mpya
na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia;’ [Isaya 1:13,14]; pia
nabii Amosi, ‘Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na
makutano yenu ya dini.’[Amosi 5:21]; pia na nabii Hosea, ' Tena nitaikomesha
furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato
zake, na makusanyiko yake yote yaliyoamriwa.' [Hosea 2:11]. Maelekezo ambayo
aliyaweka mwenyewe unauliza kuwa kama aliyatengua? Ndiyo, zaidi ya kudhania tu
vinginevyo. Sawa, na kama kuna mengine yanayopingana nayo, basi aliyasaidia kwa
lengo la Muumba, kwa kuondoa hata kile ambacho alishawahi kukikemea. Bali hapa
sio mahala pa kulijadili suala la kwamba ni kwa nini Muumba alizibatilisha
sheria au torati yake mwenyewe. Inatosha tu kwa sisi kuthibitisha kuwa
alikusudia kufanya mabatilisho kama hayo, ambayo kwamba yaweze kuimarika zaidi
na kuonekana kuwa mtume hakuamua kufanya kitu chochote cha kuonekana kuwa
alipingana na Muumba (Tertullian Against
Marcion, Bk. V, Ch. IV, ANF, Vol.
III, p. 436).
Tertullian anaonyesha
kuwa Marcion anaweza kuonekana kwanza kuwa kama mzushi kwa kuitenganisha injili
mbali na torati (soma kitabu cha Against
Marcion, ibid., Ch. XXI, p.286). inavutia sana na kuweka maswali mengi, kujiuliza
kwamba ni chimbuko hili la mafundisho ya kizushi ya wafuasi wa Marcion kuona
kuwa ndiyo yanayoaminika na kujulikana ulimwenguniulimwenguni kote leo kwenye
mafundisho yaliyookubaliwa na Wakristo ya kuondoa umuhimu wa maagizo ya torati kwa
namna mbili zote, yaani kwa kufanya ibada siku hiyo na kuadhimisha sikukuu zake
zilizoamriwa, na hasahasa kwa habari ya Sabato. Dhana yenyewe ni ya kifilosofia
zaidi na haina mashiko kabisa na haina maana inayoonekana kuwa yalistahili yaenee
kila mahali. Zaidi sana, vikwazo viliinuka kutoka kwa amtu aliyejulikana kama Lord
Russell kwenye kile kilichojulikana kama sheria za kimungu au za mbinguni (zilizoitwa
na kulikana hivyo, na kwamba hazikuwa zimetolewa kwa kuagizwa peke yake tu,
bali ni budi kungekuwa na msingi mkubwa mwingine wa sauti) ambayo ilionekana
kupingana na sababu au kiini cha sababu za kuamini na kuona mashiko ya msimamo
wa Tertullian. Inadhihirika wazi sana kwa kusoma vitabu vyake kwamba haendani
na mambo yenyewe ya kweli yaliyo nyuma ya maneno yaliyo kwenye vitabu vya
manabii Isaya, Amosi na Hosea ambavyo sikukuu zimeetajwa na kuamriwa ziadhimishwe
na makundi yote mawili, yaani ya Israeli na Yuda na wakilaumiwa kuwa wamezitia
unajisi na kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya kukosa kwao kutenda haki na utakatifu
(Amosi 5:24) kwamba lilikuwa ndilo tatizo lao ni kama ilivyo dhahiri na hata ni
haraka kuyasoma maandiko hayo. Kristo ni vivyo hivyo alibatilisha umuhimu wa kuidhimisha
Sabato na Mafarisayo wanafiki.
Torati yapasa
iendelee kutokana na misingi iliyo kwenye uasilia wa Mungu kuliko kufuata mambo
yaliyo kwenye maneno na nadharia za kibinadamu peke yake kama anavyoeleza na
kuonyesha Russell. Kwa bahati mbaya sana, uhusiano wa kimadaraja ya vyeo uliona
kuwa ni humimu msimamo wa Russell na kukubaliana mtazamo wa Kinostiki na kuona
kuwa ni sahihi sana hakika. Hata hivyo, Russell hakutafiti kikamilifu sana
kosmolojia ya kweli zaidi ya kuonyesha (Kwa
Nini Mimi Sio Mkristo) na kwamba suala la sheria za Mungu kwenye imani ya
Utatu kwao ni upuuzi na hazina umuhimu kabisa. Suala la Sabato mara nyingi limeondolewa
kutoka kwenye sheria ili kuzifanya amri zibakie tisa na sio kumi na zionekane kuwa
sio amri muhimu, bali ni mapendekezo tu – kwa kuwa sheria au amri zenyewe
zimekwisha koma umuhimu wake na zimeondolewa mbali. Hoja hhii inaonyesha kuwa
Waprotestantii kutoshikamana au kukubaliana na asili au umuhimu wa amri hizi.
Kitendo cha Waprotestanti cha kuikubali ibada ya siku ya Jumapili, ambayo kwa
yenyewe tu chimbuko lake linatokana na mabaraza ya kihalmashauri ya kanisa la
Waathanasiani, jammbo ambalo kimsingi ni upuuzi na haina mashiko. Kama kanisa
lilipewa mamlaka ya kuibadili au kuitengua sheria yoyote ile, basi lingekuwa
pia na mamlizwa kwenye torati na ndipo kanisa na imani ya Kiprotestanti ni
waasi wasio na mamlaka. Hata hivyo, kile walichokiita Matengenezo yalishindwa
kabisa na kuangukia kwenye hali iliyoonekana kuwa Matengenezo haya yalikuwa ni
ya kurudi nyuma zaidi kwa kushikilia mafundisho ya kiteolojia ya Augustine na
teolojia yake na teolojia hiyo sio sahihi kabisa kibiblia. Maandiko ya
Augustine yametuama kwenye filosofia na haiungwi mkono kabisa na Biblia.
Paulo anachukuliwa
kimakosa kuwa anaunga mokono matendo ya hawa wapinga sheria, wanaodai kuwa
sheria zimeondolewa mbali umuhimu wake, kwa kutuama kwenye nadharia tu za upotofu
wa tafsiri za nyaraka zake. Matatizo mengi ya Wagalatia yanatokana na kutoja
vizuri maana aliyoikusudia Mtume Puulo. Alishambuliwa kwa kulaumiwa na pande zote
mbili, yaani wahafdhina kwa upande mmoja na Wapinga torati kwa upande mwingine.
Tatizo la Wagalatia halitokani tu na Wayahudi wahafidhina. Mapokeo ya kikaltiki
yameelekezwa, kama tutakavyojionea, kwa nguvu za malaika waasi au mapepo wanaochukuliwa
kuwa si theoi kwa sababu ya jinsi
walivyo na asilia yao.
Kwa kweli Mtume Paulo
alianzawaraka wake baada ya kusalimia na kujitambulisha (Wagalayia 1:1-5), na kwa kuutetea utume wake
(Wagalatia 1:6 hadi 2:21). Hatimaye akaendelea kuitetea injili yake (Wagalatia
3:1 hadi 4:31). Dokezo la kimaadili la injili ndipo pia linaonekana kwenye
Wagalatia 5:1 hadi 6:10 na hitimisho linafanywa kwenye Wagalatia 6:11-18.
Tatizo
lililokuwepo kwenye Kanisa la Galatia laweza kuonekana kuhaika au kunyumbulika vizuri
kati ya nafasi hizi mbili zote. Hoja ya kwamba sheria zimekoma kutokana na kuzisoma
nyaraka za Wagalatia na Wakolosai inatokana na mkakati wa kabisa wa Wapinga-sheria
maarufu kama Waantinomia na hoja zao zinazoonekana kukataliwa na kupingwa sana
na Mtume Paulo (na hata Yakobo na Yohana pia), kama ilivyo kwenye itikadi kali
ya kihafidhina ya Mafarisayo wa Kiyahudi pia ilivyopingwa na kutokubalika (soma
majarida ya Uhusiano kati ya Kuokolewa kwa Neema na Sheria (Na. 82); Imani na Matendo (Na. 86) na Maandiko ya Matendo ya Sheria au MMT (Na. 104)). Kukosekana
kwa shukurani na uungaji mkono wa injili nyinginezo kumepingwa au kukanushwa na
kamusi ya the Interpreter’s Dictionary of
the Bible (Vol. 2, art. ‘Galatians’, pp. 338-343) kama kuashiria mshituko
wa habari za upotoshaji na ushurutishaji
wa kupigania irudishwe tena.
Hakuna mashaka
kwamba Kanisa liliigeukia injili nyingine, ambayo haikuwa injili kabisa.
Mtume Paulo alifika
Yerusalemu na kuwaona Petro na Yakobo (kwa maneno yake mwenyewe). Baada ya
miaka Kumi na nne mingine alitembelea Yerusalemu tena ili kuweka msingi (pamoja
na kina Yokobo, Petro na Yohana), injili yenye teolojia ya kisasa (kwa mujibu
wa Interp. Dict., p. 341) hakumaanisha
kuwa ni kama kuwa na uhuru mbali na sheria.
Kutokana na
utembeleaji wa Paulo ilikuwa wazi kwamba ilimpasa kuhudumu kwa Wamataifa na kwa
Wayahudi. Petro alikuwa ni mtume kwa Wayahudi kama inavyoonyesha Wagalatia.
watu waliokuwa wahafidhina wasilobadilika kwenye Kanisa, kina Petro, Yakobo na
wengineo, wanaonekana kuacha kushirikiana na Wamataifa Kanisani kama
inavyoonyesha Wagalatia 2:11-14. Petro (Kefa) ametajwa hapa.
Wagalatia 2:11-14
Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu
alistahili hukumu. 12 Kwa maana kabla hawajaja watu
kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa;
lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.
13 Na hao Wayahudi wengine wakajigeuza pamoja naye,
hata na Barnaba pia akachukuliwa na unafiki wao. 14 Walakini,
nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia
Kefa mbele ya wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala
si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi?
Hii inaonyesha uelewa
wa Kanisa. Kufunguliwa kwa Kanisa kulikuwa ni kutoka kwenye mapokeo ya
Mafarisayo na itikadi zao. Petro aliachana na mapokeo. Sehemu au upande wa Yerusalemu
ulikuwa unaendelea kuyashika mapokeo. Kuwa huko Yerusalemu ilikuwa rahisi sana
kuendelea kuyashika mapokeo kuliko kupingana nayo. Wamataifa kwa upande
mwingine iliwalazimu kujipanga vilivyo ili kuyashika mapokeo, ambayo yalikuwa
hayapo miongoni mwa sheria au torati iliyoagizwa. Zaidi sana, kuendeleza
desturi kulizuia pia kwa sehemu kama vile utaratibu wa kutoa sadaka au dhabihu,
ambao uliondolewa na kukomeshwa na Kristo.
Hoja ya kwamba sheria
au torati imeondolewa mbali na kukomeshwa iliyotokana na dhama ya kwamba
ilitimilizwa na Kristo inatokana na hali ya kutoelewa maana ya neno kutimilika.
Kutimilika maana yake (kwenye Kamusi ya Oxford
Universal Dictionary) ni
1. kupitiliza. Kujaza
hadi juu, kuwezesha kujaa ...
2. Kukithi haja au
hamu - 1601.
3. Kuhitimisha; kueneza
au kutoa kilichopungua humo. Pia kutoa au kugawia sehemu ya (kitu); kufidia
kwenye ...
4. Kuchukua au kupeleka (unabii,
ahadi, nk.); kutosheleza (hamu, shauku, maombi). Neno la asili la Kiebrania. M.E.
5. Kutenda, kuondoa,
fanya, tii au fuata M.E.; kujibu (kusudi au lengo), kwendana na (mazingira au
masharti).
6. Kufikia mwisho,
kumaliza M.E.
Kwa hiyo
inaweza kuonekana kuwa kuondolea mbali hakumaanishi
na wala hakuwezi kumaanisha neno lililo kwenye tofauti nyingine yoyote ya maana
ya Kiingereza. Zaidi tu, ni kwamba neno hili ni la Kiebrania. Kwa hiyo, maneno
ya Kristo kwenye injili yhanapasa
yaeleweke kwenye tafsiri ya neno. Mathayo 5:17 kuna maneno aliyonena Kristo
akisema:
Mathayo
5:17-20 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au
manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa
maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala
nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. 19 Basi
mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha
watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu
atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. 20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki
ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Kristo hakuja kutangua torati wala manabii. Alisema hivyo. Alikuja
kuzitimiliza (plerõsai). Amri za Mtume
Paulo kwa Wagalatia yapasa ziwe zinamaanisha kwenye mtazamo huu. Iwapo kama
hazijikanganyi zenyewe au kumkanganya Kristo, ni wazi kwamba Paulo kwa maana hii
atakuwa anamkanganya Kristo na hivyo Wagalatia wangekuwa hawahamasiki. Paulo
hawezi kushinda mdahalo dhidi ya Kristo. Zaidi sana, Biblia haiwezi
kujikanganya yenyewe kimafundisho.
Amri hizi kwa hiyo sio tu kuwa zinatakiwa kushikwa tu bali hazitakiwi
zichukuliwe kiwepesi. Maana ya kutimiliza yanaweza kuonekana pia kutoka kwenye
maana mbalimbali iliyotafsiriwa kwenye maandiko ya Agano la Kale. Neno la
kwanza ni mala (SHD 4390) kutia au
kujaza hadi juu, kutimiliza uthibitisho, kutakatifuza au kuwa mwishoni dhana ya
kuzungushiwa ukuta na pia kukusanyika pamoja au kuwa wote kikamilifu. Maana ya
kinadharia haimaanishi kutenga mbali bali zaidi tu ni kufikia kiomo na kuwa
kwenye uimara na kitu fulani na hivyo, ni sheria. Vifungu vya maandiko zilikuwa
ni neno lililotumika kwenye Mwanzo 29:27, Kutoka 23:26, 1Wafalme 2:27, 2Nyakati
36:21 na Zaburi 20:4,5.
Neno la pili ni kalah (SHD 3615) kukomesha
kwenye maana ya mpito. Kukoma,
kumaliza, au kuangamia na kusafirisha, kuhitimiisha,
kuandaa au kumeza, kwa hiyo inaweza kuwa kumeza au kuangamiza. Neno hili
limetumika kwenye Kutoka 5:13 kwa maana ya kuhitimisha kila siku majukumu au
kazi. Huu haimaanishi kuharibu au kukomesha. Haiwezi kuwa na maana ya ukomo, wa
sheria na amri za Kristo mwenyewe. Neno la tatu linapatikana kwenye 1Nyakati
22:13: Kusudia kutimiliza amri na sheria.
Neno lililotumika hapa ni ’asah (SHD
6213) kufanya au kutenda kwa maana pana zaidi. Kwa hiyo, neno hili
linamaanisha kwendana na amri na
sheria kwenye maana hii.
Neno lililotumika kutafsiri kile alichesema Kristo kwenye Mathayo 5:17 ni
aina ya neno plerõ ambalo maana yake
ni kufanya ujazo, ujazo moja kwa moja (kama wavu), kusawazisha (kutukuza) au kutia
moyo kwa kung’arisha,, kushawishi, kutosheleza au kufanya kazi na kuwajibika
ofisini. Kwa hiyo Kristo alieleweka wazi sana kuongeza kwenye torati mkakati wa
kuifanya isitanguke wala kusiondolewe hata nukta moja ya maagizo ya torati kwa
sababu zozote. Kudai kuwa Kristo alikuwa anafanya hivyo ni kupotosha uelewa kwa
maneno yaliyotumika kwenye lugha zote, yaani: Kiyunani. Kiebrania na Kiaramu ambazo
Kristo aliziongea, au kwenye Kiingereza ambacho hatimaye neno hilo lilitafsiriwa
kwayo. Alitimiliza sheria au torati kwa kutuma au kumleta Roho Mtakatifu. Hiyo
ndiyo maana halisi nay a kweli ya hoja za Paulo na za mitume wengine wote na
manabii.
Jambo muhimu kwa Wagalatia ni andiko la Wagalatia 3:1-5.
Wagalatia 3:1-5
Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu
Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? 2 Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho
kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? 3
Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka
kukamilishwa sasa katika mwili? 4 Mmepatikana na
mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli. 5 Basi,
yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia
kunakotokana na imani?
Msimamo ni kwamba
Roh ameletwa si kwa kuja kuzitenda sheria bali ni kwa imani. Dhana kuhusu uzima
wa milele ni kwamba ndiyo iliyoondolewa kutoka kwenye msimamo anaoushikilia
kila mmoja kwa kujikita kwenye mapenzi ya Mungu kwa kuyatendea kazi na kwa
imani. Dhana hiyo ndipo imeendea kutoka kwa Ibrahimu ambaye ni baba wa imani.
Wagalatia 3:6-9
Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki. 7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana
wa Ibrahimu. 8 Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu
zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu
habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. 9 Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu
aliyekuwa mwenye imani.
Mtazamo huo umendelea
hadi wale wanaozitegemea kazi au matendo yao yatimilizwe kuliko dhabihu ya Yesu
Kristo.
Wagalatia 3:10-14
Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana;
maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa
katika kitabu cha torati, ayafanye. 11 Ni dhahiri ya
kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu
Mwenye haki ataishi kwa imani. 12 Na torati haikuja
kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo. 13 Kristo
alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu;
maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; 14
ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo,
tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
Kwa hiyo, upokeaji wa ahadi ni kwa kupitia imani.
Sharti au stahili ya kupokea ahadi ni kwa njia ya utii. Ahadi ya kumpokea Roho Mtakatifu ilitabiriwa
kutimilika kwa watiifu wote wanaozitii sheria na kuzishika amri za Mungu (Mathayo
19:17); soma pia majarida ya Roho Mtakatifu (Na. 117) na Uzima wa Milele (Na. 133).
Wayahudi walikuwa
wanajaribu kuupata wokovu kwa matendo yao ya sheria na walikuwa wanapotosha
kusudi la torati na kuihoji asili ya Mungu. Upotoshaji huu ulianza kujipenyeza
kwa wateule.
Wagalatia 3:15-18
Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la
mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala
kuliongeza neno. 16 Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu
na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni
mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo. 17 Nisemalo ni
hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne
na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi. 18 Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi;
lakini Mungu alimkirimia Ibrahimu kwa njia ya ahadi.
Inaweza kuonekana
kwamba ahadi hii iliwekwa kwa Kristo na kwamba hakuna mtu anayeweza kuja kwa
Mungu na kuokolewa isipokuwa ni kwa kupitia kwa Kristo. Wayahudi waliamini
kwamba wanaweza ukwepaji wa umuhimu wa imani kwa kushikilia matendo peke yake.
Lengo hapo ni kwamba kulikuwa na aina ya utakaso ulioingia kwenye Kanisa la
Wagalatia, ambao ulikuwa unakutikana pia kwa Wanostiki na wa namna moja, lakini
sio wa aina moja, kama ule uliokutikana kwa Wakolosai.
Paulo anaelezea
maana na malengo ya torati.
Wagalatia 3:19-20 Torati
ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao aliyepewa ile
ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe. 20 Basi aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni
mmoja.
Torati ilikuwepo hadi
alipokuja Kristo kwa kuwa watu hawakuweza kuishi sawasawa na mapenzi ya Mungu
ambaye kwake torati ilitoka na kuamriwa. Kristo hakufanya hivyo na kwa wale
ambao walipewa Roho Mtakatifu kwa njia ya imani. Kwa hiyo sasa, Roho alikuwa
ametolewa kwa manabii peke yao na waliirithi ahadi, lakini wengi walioitegemea
matendo hawakeweza kutokea hadi Kristo na wateule wake. Maadui wa Mungu
walibakia kwenye nafasi ya Roho Mtakatifu kwa malaika kwa njia ya mwombezi na
mtetezi, anayetuwezesha sisi kuwa wamoja na Mungu kama Kristo alivyo mmoja na
Mungu.
Torati haipingani
na ahadi bali zaidi tu inaiweka wazi zaidi kwa umuhimu wake kwenye imani katika
Kristo.
Wagalatia 3:21-22 Basi
je! Torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha! Kwa kuwa, kama ingalitolewa
sheria iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sheria. 22 Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi,
makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.
Torati ilitenda
kazi kama kuhitimisha hadi Kristo alipokuja kwa kuwa hatukuweza kuishi sawasawa
na mapenzi na asili ya Mungu hadi tulipopewa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu
hakutolewa kwa kuombwa Kristo. Ni manabii tu na wale waliochaguliwa na Mungu
kuuelewa mpango wa Mungu wa wokovu ndio walishirikishwa neema hii ya kumpokea
Roho, kwa hiyo ni kwamba tangu wakati wa Kristo ilikuwa wazi kwa kundi kubwa la
watu.
Wagalatia 3:23-29
Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria,
tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa. 24 Hivyo
torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. 25 Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya
kiongozi. 26 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa
Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 27 Maana
ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28 Hapana
Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke.
Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. 29 Na
kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na
ahadi.
Katazo la Mungu
alilolifanya kwa kanuni na taratibu zake lilikuwa ndilo kivuli ekee cha
uhusiano wa kweli ambao wateule walikuwanao wakiwa pamoja na Mungu kupitia kwa
Kristo. Tunaishiriki asili ya Mungu na kufanya kwa hiyari yetu wenyewe kwa
mambo hayo, ambayo mwanzoni sana tulipasa kufanya kwa msukumo wa nje. Amri za
Mungu zinaendelea sasa kwa wateule kwa kupitia Roho Mtakatifu. Wateule sasa ni
uzao wa Ibrahimu ni kama Kristo alivyo kuwa ni uzao wa Ibrahimu na wakiwa ni
warithi wa ahadi. Kwa njia hiyo tutakua hadi kwenye kimo cha Mwana wa Mungu kwa
uweza kwa kupitia Roho Mtakatifu kwa kufufuliwa kwetu kutoka kwa wafu kama
alivyofanya Kristo (Warumi 1:4).
Paulo anaendelea
kwenye Wagalatia 4 kushughulikia dhana nyingine kwa pale anapoeleza roho muhimu
ya kiroho. Kutoka juu, mstari huu haupo mtupu pasipo na umuhimu au maana.
Wagalatia 4:1-7
Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na
mtumwa, angawa ni bwana wa yote; 2 bali yu chini ya
mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba. 3 Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa
tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia. 4 Hata
ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na
mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, 5 kusudi
awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa
wana. 6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma
Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. 7 Kama
ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa
Mungu.
Wateule walitumikishwa na roho zitendazo nguvu za kidunia hadi alipokuja
Kristo. Hivyo, hawa mapepo walitajwa kama roho zisumbuazo. Hivyo, dhana hii
ilihusisha mawazo ya kipagani yaliyoendelea ambayo yalikuwa ni ya kawaida kwa
wote wawili, yaani Wayunani na Warumi. Ni kama ilivyo sasa kuwa tunakabiliwa na
aina fulani ya uenezwaji wa usynkretism ya Kihelleniki ambayo sio imani halisi
ya Kiyahudi, bali angalau, inaweza tu kuwa ni mwanzo na utangulizi au
mwanzilishi wa imani ya kimafumbo.
Anatajwa kwa wazi sana kabisa kwa Malaika walioasi kwenye Wagalatia 4:8ff. Dhana
iko wazi wakati Paulo anaposema kuwa hapo mwanzoni sana tulipokuwa hatumjui
Mungu tulikuwa kifungoni kwa wale ambao kwa asili walikuwa sio Theoi tukiyatenda mapenzi yao. Kifungu
hiki kinaendelea kusema kuwa:
Wagalatia 4:8 Lakini
wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si
miungu.
Kifungu
kinaendelea kuchambuliwa kwenye Kamusi ya Marshall’s Interlinear kifungu kikubwa kwamba:
Lakini wakati ule, kwa kuwa
hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu.
Ni wazi kwamba
kuwatumikia Malaika walioasi kunahusishwa na kwamba anawataja wao kama maroho
yenye nguvu. Ni wazi sana kwamba Galatia iliwa inajaribu kufariji au kutuliza, kwa kuyashika mapokeo, maroho yatesayo, wakikosa
kujua kwamba walikuwa pamoja na Malaika hawa waasi au mapepo. Walikuwa
wanashirikiana nao Kanisani shughulii za utakaso ambazo zilikuwa ni ugonjwa
ulionea kwenye imani ya Upythagoreani na ambazo zilikuwa zimejipenyeza huko
Italia na kwa Warumi siku nyingi sana huko nyuma. Kwa hiyo, waongofu Wamataifa hawakuwa
wakiendana na kanuni zilizopaswa kuzifuata kwenye uhalisia wa seria au torati
na hawakujua mahali pake kwenye mambo ya imani. Tunaona jambo hilo kutoka
kwenye aya za 9-11.
Wagalatia 4:9-11 Bali
sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea
tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka
kuyatumikia tena? 10 Mnashika siku, na miezi, na
nyakati, na miaka. 11 Nawachelea, isiwe labda
nimejitaabisha bure kwa ajili yenu.
Uadhimishaji huu
uliotajwa hapa unaweza kuonekana wazi kuwa umehamasisha kwa kiasi kikubwa
makanisa kongwe ya kale kwa kipindi cha takriban miaka elfu mbili. Andiko hili
haliiondoi Sabato na maadhimisho yake wala sikukuu zake.
Andiko la mtumwa na mtu huru linataja matumizi ya
sheria au torati huko Yerusalemu.
Wagalatia 4:12-31 Ndugu zangu, nawasihi, iweni kama mimi, maana mimi ni kama ninyi. Hamkunidhulumu kwa lo lote. 13 Lakini mwajua ya kuwa naliwahubiri Injili mara ya kwanza kwa sababu ya udhaifu wa mwili; 14 na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu. 15 Ku wapi, basi, kule kujiita heri? Maana nawashuhudu kwamba, kama ingaliwezekana, mngaling'oa macho yenu, mkanipa mimi. 16 Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo kweli? 17 Hao wana shauku nanyi, lakini si kwa njia nzuri, bali wanataka kuwafungia nje, ili kwamba ninyi mwaonee wao shauku. 18 Navyo ni vizuri kuonewa shauku katika neno jema sikuzote, wala si wakati nikiwapo mimi pamoja nanyi tu. 19 Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu; 20 laiti ningekuwapo pamoja nanyi sasa, na kuigeuza sauti yangu! Maana naona shaka kwa ajili yenu. 21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22 Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. 27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29 Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. 31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.
Hatuzishiki sheria kwa kuwa tu watumwa wa sheria inazoendana sawa na
mapenzi ya mwili, ambayo ni ulimwengu wa mapepo na wa mungu wa dunia hii.
Tunamtumikia Mungu na ni sehemu ya Yerusalemu Mpya. Usemi wa Paulo aliowaambia
wa kuwa kama alivyo yeye, unaonyesha kuwa haongelei tu ushikaji wa sikukuu kwa
kuwa alizishika sikukuu na Sabato (kama tunavyojua kutoka kwenye Matendo na
nyaraka zake) kama walivyofanya mitume wote. Na kama atakuwa anasema kuwa
sikukuu hizi zimetanguliwa mbali, ndipo anamfanya Kristo kuwa ni muongo aliyenena
na manabii na kusema kwamba Sabato na Miandamo ya Mwezi Mpya na sikukuu (Isaya
66:23) zinaendelea kuadhimishwa (Zekaria 14:16-19). Kama wateule watazipuuzia
kwa kuacha kuadhimisha Siku hizi Takatifu na Sabato, basi itakuwa ni ugeugeu kwa
kuwa Mungu atayahukumu mataifa kwa kutozishika siku hizi wakati wa utawala wa
millennia. Mungu hana upendeleo na kwa hiyo anahitaji usawa wa viwango vya
wanadamu.
Wateule wana kazi kubwa sana ya kuzitenda, kuendenda kwa imani. Kama mtu
yeyote atasema kuwa sheria au torati imetanguliwa mbali, basi yeye ni mjinga tu,
asiyeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo hayawezi kutanguka, na asiyeijua asili
ya Mungu. Zaidi sana hasa, watakuwa ni wajinga wa kutojua mambo ya kweli nay a
muhimu mbali na vile walivyokuwa wenyeji wa Galatia na Kolosai. Kiwango cha
makosa au upotoshaji kwenye makanisa hayo walianza kudai wenyewe kuwa ni
Wanostiki kwenye hatua ya mwanzoni kabisa. Michakato ya kimawazo inabakia pia
kwenye Teoljia ya Uhuru na, hususan kwenye imani ya Kibudha. Mawazo hayo
yangali yanaendelea bado kwenye Teolojia Mchakato. Wanostiki waliachana na
uwepo huo huo wa Mungu (jarida la Maandiko ya Matendo ya Sheria - au MMT (Na. 104) linafafanua vya kutosha jambo hili).
Mafundisho ya Kizushi Kwenye
Kanisa la Yohana
Kila moja ya nyaraka tatu za Yohana ziliandikwa ili kushughulikia matatizo
au chngamoto ya mafundisho na mamlaka ya injili kama ilivyokuwa imefundishwa
kwao na Yohana.
Uzushi mkubwa sana kuliko yaonekana kuwa ulihusika na fundisho la Uungu na
ulikuwa ni jaribio la kumuinua juu Kristo ili aonekane kuwa ni huyu Mungu
Mmoja, wa Pekee wa Kweli. Mtume Yohana anaonyesha uhusiano huu kwenye andiko la
Yohana 17:3 na tena alipokuwa anashughulikia mafundisho ya kizushi kwenye 1Yohana
(hususan kwenye 1Yohana 5:20).
Upotoshaji ulikuwa wazi sana kutoka kwenye madai yake haya kuwa ni wateule (1Yohana
1:6) ndio waliohusika kujidai kuwa wao hawana dhambi (1Yohana 1:8). Suala
lilikuwa ni uwezo wa kumjua Mungu, ambaye ni Ujuzi. Unostiki ulijumuisha nadharia
au fundisho la kuwa sheria za Mungu au torati imetanguka au fundisho la kwamba
amri za Mungu hazihitajiki kushikwa tena (1Yohana 2:4). Wajibu au fursa ya Roho
Mtakatifu kuwa ndani ya wateule na kisha katika Mungu (1Yohana 2:6) alitegemea
upendo wa wote wawili, yaani Mungu na ndugu wapendwa. Wateule hawapaswi kuwachukia
ndugu zao (1Yohana 4:20).
Madai haya yanashabihiana kwa dhahiri. Maana kusudiwa ni kwamba upinzani
ulioko ni:
… kumekuwa
kukifanyika madai kwenye ujuzi kamili maalumu na upendo wa Mungu na kwa
ushirika maalumu na mkubwa wa karibu na yeye ambao umewafanya wawe juu ya
uwezekano wa kawaida wa kutenganisha kati ya wema na ubaya na kwa hiyo kuwa juu
zaidi madai ya maadili na imani ya Kikristo. Ni huenda, zaidi sana, kwamba
ujumbe muhimu wa waraka ni; “Mungu ni nuru na hakuna giza lolote ndani yake,” unaelekezwa
dhidi ya teolojia inayoshikilia kudai kwamba Mungu alijidhihirisha mwenye kwa
namna zote mbili, yaani nuru na giza (kwa mujibu wa Kamusi ya The Interpreter’s Dictionary of the Bible,
Vol. 2, p. 947)
Aina au mtindo wa teolojia ya Kiyunani inashabihiana kwa karibu sana
kuangukia kwenye mrengo huu ulikuwa ni aina ya itikadi za Kiplatoni au
Upithagoreani. Hoja ya kwamba Mungu ni mambo yote na, hivyo, kiukweli kabisa haiwezi
kuwa leo. Kimsingi, inaonekana kuwa ni kama Uanimism ulio kwenye dini ya
Kibabeloni. Waalimu walikuwa pia wanakataa kuwa Yesu alikuwa ndiye Masihi (1Yohana
2:22). Kamusi ya The Interpreter’s
Dictionary inaungana kwa kusema hivi:
Hatuwezi kuhitimisha
hili kuwa hawa walikuwa ni Wayahudi au Wazayuni waliokuwa wanapinga Umasihi
wake, lakini zaidi ni kwamba tu walikuwa Wakristo waliokuwa wanapinga fundisho
la Inkaneshi au kwamba alikuwepo akiwa timamu hata kipindi cha kabla ya
kuzaliwa kwake tumboni mwa mama yake. Kwa hiyo upotofu wao unaonekana kwa
waziwazi kabisa na kudhihirika zaidi baadae kwenye waraka kama ukano kwamba
“Yesu Kristo ametokana na mwili” (4:2) (ibid.).
Onyo juu ya
kuzijaribu roho ili kuziona kama zina uhusiano na Mungu au sivyo, linafanya
ionekane dhahiri tunashughulika na kukabiliwa na mwingiliano na maroho
yasumbuayo na unenaji unaopingana na kuhesabiwa haki na Mungu kwa njia ya Roho
Mtakatifu. Neno geni la chrism au unction ambalo limetumika mara mbili kwenye
maandiko (kwenye 1Yohana 2:20,27) kuelezea karama za Roho ambazo kwazo kila
Mkristo anashiriki limetumika kwenye kifungu hiki cha maandiko kwa sababu ya
wafundisha uzushi hawa kwanza alilitumia
ili kuelezea kile wanachokiamini kuwa ni kuwa ni utoaji au kujitoa kwa
mshikamano wao wenyewe wa kiroho (Kamusi ya Interp. Dict., ibid.). hivyo, upako (Chrisma) wa Roho Mtakatifu ni kinyume na kutiwa upako wa maroho
mengine haya yanayozidi kuendelea. Fundisho hili hapa limepewa jina ya kuwa ni
la Mpingakristo, ambalo ni la yeye anayempinga Baba na Mwana pia. Ilionekana
kuwa kilichokuwa kikipingwa ni kule kumfanya Kristo kuwa ni sehemu ya Baba kama
kitu kimoja kama hakuwa amekufa kiujumla. Fundisho la kwamba Kristo ni Mungu
kama moja ya mfumo unaomhusidha Roho kwa sasa limeenea na kushinda sana kwenye
mawazo na imani za Ukristo wa dini kongwe. Hata hivyo, hoja zake yapasa
zichukuliwe kwamba na utaratibu uliowekwa, na kwa utaratibu ulionenwa hapa, na
wafundisha uzushi wa wakati wa Yohana.
Fundisho kuhusu
Mungu kwenye maandiko ya Yohana liko wazi na laonyesha wazi kuwa ni la mrengo
wa Kiyunitari na Kristo anaonekana wazi kuwa ni mwana wa Mungu wa Pekee wa
Kweli (Yohana 17:3) aliyekufa kwa ajili ya wateule. Wamodalisti na ambao baadae
walikuja kuwa Waaamini Utatu au Watrinitari wakijua hivyo sana, walikuwa na
ugumu mkubwa sana kwenye maandiko haya ya Yohana (sawa
na ilivyo kwenye majarida ya Mawazo Yaliyopo Kwenye Kati (Na. 74) na Imani ya Kibinitariani na Utrinitari (Na.
76)).
Kwenye 1JYohana anaelezea
kifupi na kwa wazi sana kuhusu makosa au upotoshaji na hila zilizopelekea kufanya
hivyo. Andiko linaonesha kusudi lake.
Wateule
wamebatizwa kwenye mwili wa Kristo na sio kwenye kanisa lolote au kuwa mali
dini yoyote. Maneno hayo yananenwa na karibu kila mteule wakati anapobatizwa.
Kwa hiyo wateule ni wale waliofungamanishwa kwenye mwili wa Yesu Kristo
wakimuabudu Mungu wa Pekee wa Kweli kama inavyosema Yohana 17:3. Kwa hiyo,
wakati wateule wanapokusanyika kwenye maeneo ya makanisa, walikuwa wakikusanyika
kwa msingi wa mshikamano wao kwenye kweli na kumuabudu Mungu wa Pekee wa Kweli
na kumtumikia Mwana wake Yesu Kristo. Wakati kanisa lilipokabiliwa na fundisho
lililojaribu kumfanya Kristo kuwa ni zaidi ya kuwa mwana wa Mungu na kumfanya
kuwa ni sawa na Mungu na kumtenganisha na ubinadamu wake mbali na hali yake ya
kimbinguni ndipo wateule walilazimika kujipanga au kujikusanya upya na
kujitenga kutoka kwa hao walioanzisha mafundisho ya uwongo, ambayo yalipewa
jina la wazi kabisa kuwa ni mafundisho ya Mpingakristo.
Msingi wa imani
ni kweli na hakuna giza kwa wale wanaotembea kwene kweli.
1Yohana 1:1-10 Lile lililokuwako tangu mwanzo,
tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu
ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; 2 (na
uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule
uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 3 hilo
tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate
kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake
Yesu Kristo. 4 Na haya twayaandika,
ili furaha yetu itimizwe. 5 Na hii ndiyo
habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala
giza lo lote hamna ndani yake. 6 Tukisema ya
kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala
hatuifanyi iliyo kweli; 7 bali tukienenda
nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake
Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. 8 Tukisema
kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. 9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni
mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu
wote. 10 Tukisema kwamba
hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.
Kwa hiyo, ni
lazima kwa wapendwa kutembea pamoja kwenye kweli.
1Yohana 2:1-6 Watoto
wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda
dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, 2 naye
ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa
dhambi za ulimwengu wote. 3 Na katika hili twajua ya
kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 4 Yeye
asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani
yake. 5 Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo
upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani
yake. 6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake,
imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.
Kristo ni mtetezi kwa Baba. Wakili ananena kwa niaba ya mwingine. Wakili
hawezi kuwa na kusema yeye mwenyewe tu.
1Yohana 2:7-11 Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri
ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile
mlilolisikia. 8 Tena nawaandikia amri
mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile
nuru ya kweli imekwisha kung'aa. 9 Yeye asemaye
kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. 10 Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika
nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.
Upendo ni alama
ya mteule. Mahali ambapo kundi linapenda ushirika wao, au viongozi wao, zaidi
kuliko kupendana wao wenyewe kwa wenyewe na wanapofikia hata hali ya kutoijali
kweli, kisha ndipo kundi hilo lina ishara ya kuwa imani potofu au kalti na wala
halipo sehemu ya mwili wa Kristo. Mtume Yohana anaandika kuhusu neno la Mungu
kukaa kwa wingi kwa wateule na kufanya hivyo, watamshinda muovu.
1Yohana 2:12-17 Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa
sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. 13 Nawaandikia
ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia
ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto,
kwa sababu mmemjua Baba. 14 Nimewaandikia
ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia
ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi
mmemshinda yule mwovu. 15 Msiipende dunia,
wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo
ndani yake. 16 Maana kila kilichomo
duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima,
havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na
dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu
hata milele.
Agizo la
kupendana wateule ni la Baba kabisa. Upendo wa wateule na umuhimu wa kupendana
kila mmoja na mwezake unawezekana tu kwa kuwa na Roho Mtakatifu ndani ya kila
mteule kutoka kwa Kristo na kuendelea. Kristo alijitoa mwenyewe kwa ulimwengu kwa njia ya pendo la Baba. Yohana 3:16
inasema kuwa Baba alimtoa Mwana.
Yohana 3:16 Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Hatuwezi kutoka
kitu kisicho cha kwetu. Hakuna usawa kwenye karama za Mwana na Baba.
Zaidi sana, Kristo
alitumwa na Baba kwa mapenzi na maelekezo kamili.
Yohana 4:34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake
aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.
Kwahiyo, kazi ni
ya Baba na yapasa kufanywa na Roho Mtakatikatifu kwa ndani na ya mwanadamu na
kwa kupitia kwa huyo mtu, kwanza kabisa ikiwa ni kwa Kristo na pili ni kwa
mteule. Ni kwa jinsi gani basi mteule hapo zamani au hata sasa anaweza kubaki kwenye
shirika linalofundisha kinyume na maagizo ya torati na ushuhuda na ikawa bado
ni kazi ya Baba?
Mafundisho ya
Mpingakristo hayahitimiki kwa kila mtu mmoja mmoja ni mafundisho, yanayotafuta
kushusha hadhi au kudharau ukuu wa Mungu wa Pekee wa Kweli na ukamilifu au
ukomo wa kifo na dhabihu ya Mwanae wa Pekee, Yesu Kristo. Kitendo cha kutoka
kati ya wana wa dunia hii cha wateule ni cha kibiblia na kimafundisho na sio
cha msingi wa ushirikiano tu peke yake.
1Yohana 2:18-29 Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile
mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi
wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. 19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu.
Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili
wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. 20 Nanyi
mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote. 21 Sikuwaandikia
ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba
hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli. 22 Ni
nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga
Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. 23 Kila
amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia. 24 Ninyi
basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo
mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya
Mwana, na ndani ya Baba. 25 Na hii ndiyo
ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele. 26 Nimewaandikia
haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. 27 Nanyi,
mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu
kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote,
tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake. 28 Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake,
ili kusudi, atakapofunuliwa, mwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika
kuja kwake. 29 Kama mkijua ya kuwa
yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.
Hapa wazo la
kutoka kati yao tulilonalo sisi limeendelea kufundishwa na Yohana. Hoja iliyoendelezwa
Kanisani lililotajwa na Yohana lilionekana wazi sana hapa kuwa ni zaidi ya
Uungu na uhusiano wa Baba na Mwana. Hoja ilikuwa ni linawasuta waamini Utatu.
Ilijaribu kutenganisha ubinadamu wa Kristo kutoka kwenye hali yake ya
kimbinguni. Kimsingi, ilijaribu kudai kuwa Kristo alikuwa na chembechembe ya
ubinadamu iliyobakia imetenganishwa na ubinadamu wake na hakufa. Zaidi sana,
ilibakia sehemu ya kitu tunachokijua leo kuwa Mungu. Kimsingi, yalijaribu
kumfanya Kristo kuwa na sehemu yake na kuwa sawa na Mungu. Haya ni mafundisho
ya Mpingakristo. Ilikuwa hivyo dhahiri na kuhusiana na imani ya Utrinitari
ambavyo andiko la 1Yohana 4:1-2 lilibadilishwa ili kugeuza au kupotosha ukweli.
Wazo la kuwa sehemu
ya mteule kwa mwenendo wa utakatifu. Kiini cha andiko la Yohana ni kwamba: atendaye haki yu na haki – naye
atendaye dhambi ni wa ibilisi (diabolos).
Kwa hiyo, haiwezekani kuunganishwa au kushirikiana na wale wasiohubiri ukweli.
Amri za Mungu ni za muhimu. Dhambi maana yake ni uvunjifu wa amri za Mungu au
hapa ni kitendo cha kuvunja sheria au kutojali kuhusu sheria. Amri ya kwanza inahusiana na kitendo cha
kumuabudu na kumpenda Mungu. Sababu yake ni rahisi. Ni kwamba, tunawezaje
kumwabudu Mungu wa Pekee wa Kweli na huku tukiwa ni sehemu ya mfumo unaojaribu
kumpinga Kristo kwa kujaribu kumlinganisha kuwa yu sawa na Mungu wa Pekee wa
Kweli na kutenda dhambi hiyohiyo aliyoitenda Shetani? Kwa hiyo, inatupasa sisi
kujitakasa kama Kristo alivyo mtakatifu.
1Yohana 3:1-10 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa
Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu
haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapenzi,
sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya
kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. 3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye
hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. 4 Kila
atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. 5 Nanyi
mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani
yake. 6 Kila akaaye ndani
yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. 7 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye;
atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; 8 atendaye
dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi
hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. 9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi
dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa
sababu amezaliwa kutokana na Mungu. 10 Katika hili
watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda
haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
Kama hatutendi
vyema ndipo tunakuwa si wa Mungu. Hatuwezi kuwa tunawapenda watu wetu, iwapo
kama hatutawahubiria neno la Mungu kwa kweli isiyoghoshiwa.
1Yohana 3:11-24
Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi
kwa sisi; 12 si kama Kaini
alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa
sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki. 13 Ndugu
zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia [mkolezo wa rangi ni msisitizo]. 14 Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka
mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa
katika mauti. 15 Kila amchukiaye
ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele
ukikaa ndani yake. 16 Katika hili
tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa
na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. 17 Lakini
mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia
huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? 18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa
ulimi, bali kwa tendo na kweli [imekolezwa rangi ili kusisitiza]. 19 Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa
kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake, 20 ikiwa
mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua
yote. 21 Wapenzi, mioyo yetu
isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; 22 na
lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda
yapendezayo machoni pake. 23 Na hii ndiyo
amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi
kwa sisi, kama alivyotupa amri. 24 Naye
azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili
tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.
Kwa hiyo Mungu
yuko tofauti na halinganishwi wala hafanani na Mwana na tunasika amri zake
tukitembea katika kweli. Wateule wanatakiwa kuzijaribu roho ili kuziona kama
zinatoka kwa Mungu.
1Yohana 4:1-3 Wapenzi,
msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa
sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. 2 Katika
hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika
mwili yatokana na Mungu. 3 Na kila roho
isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo
mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Andiko na kifungu
hiki kuhusu mafundisho ya Mpingakristo limebadilishwa na kupotoshwa kwa
makusudi kwenye maandiko ya zamani. Maandiko yenewe sahihi na halisi yanaweza
kuonekana kutoka kwenye maandiko ya vitabu vya Irenaeus (soma kitabu cha Ante-Nicene Fathers, Vol 1, fn. p. 443).
Andiko hili linasomeka hivi:
Katika hili
mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika
mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na
hii ndiyo roho ya mpinga Kristo
Socrates wanahistoria
anasema (VII, 32, p. 381) kwamba kifungu hiki kimepotoshwa na wale waliokusudia
kuutenhanisha uwanadamu wa Yesu Kristo
kutoka kwenye hali yake ya kimbinguni. Kwa hiyo, hoja ya kwamba sehemu ya
Kristo ilibakia kuwa ni ya kimbinguni akiwa sehemu ni Mungu tofauti na
ubinadamu wake na kufa kwake msalabani akikataa kabisa ufufuko na ni fundisho
la Mpingakristo. Kwa hiyo, imani ya Utrinitariani inaangukia kabisa kwenye mafundisho
ya Mpingakristo.
1Yohana 4:4-6 Ninyi,
watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye
ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. 5 Hao
ni wa dunia; kwa hiyo wanena ya dunia na dunia huwasikia 6 Sisi
twatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu
hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu.
Hivyo roho wa
kweli alikuwa anahitajika na bado anahitajina kutengana na roho wa upotevu.
Jaribio hili ni kwa wateule kuonyesha yule aliye mteule na Yule aliyeitwa
lakini hajachaguliwa bado.
1Yohana 4:7-21 Wapenzi,
na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na
Mungu, naye anamjua Mungu. 8 Yeye
asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. 9 Katika
hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee
ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye. 10 Hili
ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi,
akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. 11 Wapenzi
ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. 12 Hakuna
mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu,
na pendo lake limekamilika ndani yetu. 13 Katika
hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa
ametushirikisha Roho wake. 14 Na sisi
tumeona na kushuhudia ya kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu. 15 Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa
Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu. 16 Nasi
tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo,
naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. 17 Katika hili pendo limekamilishwa kwetu,
ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo
tulivyo na sisi ulimwenguni humu. 18 Katika pendo
hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina
adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo. 19 Sisi
twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. 20 Mtu
akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana
asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba
yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
Wale walio na
upendo mkamilifu hawahofii mtu yeyote, hebu na tuwaache na kujiepusha wale
walio kwenye upotoe na kuikosa kweli. Umuhimu wa kuushinda ulimwengu umetajwa
wazi kwenye 1Yohana 5:1-5.
1Yohana 5:1-5 1 Kila mtu aaminiye
kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa,
ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. 2 Katika
hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika
amri zake. 3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu,
kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. 4 Kwa
maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko
kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. 5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani,
isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?. [msisitizo
umeongezwa].
Tukimpenda Mungu
basi na tushike amri zake. Kwa hilo tunajua kuwa tunawapenda watoto wa Mungu.
Kuzaliwa na Mungu yatupasa kuushinda ulimwengu. Ili kuushinda ulimwengu
yatupasa tuamini kwamba Masihi ni Mwana wa Mungu. Kwa hiyo, uhusiano wake uko
wazi. Kitendo cha kugeuz ili kuyapotosha maandiko au vifungu vya biblia au
kutafsiri kwa uwongo na upotoshaji kinyume na maana yake halisi na iliyo wazi
ya maneno yanayoonekana hapo chini (hususan kwenye 1Yohana 5:7 inapolinganishwa
na maandko ya uwongo yalivyo kwenye tafsiri ya Mfalme Yakobo ya KJV).
1Yohana 5:6-12 Huyu
ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika
maji na katika damu. 7 Naye Roho ndiye
ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. 8 Kwa
maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na
watatu hawa ni umoja. 9 Kisha wako watatu
washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa
habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi;
kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. 10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani
yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo
ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. 11 Na
huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo
katika Mwanawe. 12 Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima;
asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
Kumbuka kuwa
Mungu alitupa sisi uzima wa milele na uzima huu upo kwa Mwana wake. Kwa hiyo,
Mwana anao uzima wa milele kutoka kwa Baba, ambao pia tumepewa sisi kwa namna
hiyohiyo.
1Yohana 5:13-21 Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. 14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. 16 Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo. 17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti. 18 Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi. 19 Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu. 20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele. 21 Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.
Maandiko yaliyo
kwenye 1Yohana yamefanya udanganyifu na upotoshaji kwa kipindi cha karne kadhaa
sasa. Mkakati wa mwanzoni kabisa wa kughushi ulikuwa ni ugeuzaji au upotoshaji
wa maandiko yanayoelezea vizuri kuhusu mafundisho ya Mpingakristo. 1Yohana 5:7
(tafsiri za Receptus na KJV) ilighushiwa kwa kugeuzwa mapema kwenye kipindi
kilichojulikana kama cha Matengenezo. Ujanja na ulaghai wa pili zaidi wa
utendaji ni kufanya ulaghai wa maana asili iliyokusudiwa kwenye maandiko, kama
vile ugeuzi wa maana asilia iliyokusudiwa na maana ya wazi ya maneno
yanayodaiwa kwao. Ulaghai kama huu yanapelekea aina ya hoja au mabishano
yaendelee kwenye kitabu cha fasihi cha G.L. Haydock commentary to the
Douay-Rheims Bible (1850 reprint of the 1819 version), kuhusu andiko hili la Yohana
17:3, yanayofanya rejea kwenye 1Yohana.
Aya ya 3. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Kwa maneno haya Waariani wanajifanya kwamba huyu Baba ndiye Mungu wa kweli. S. Aug. na wa-kukwepa wengine wanajibu kwamba maana na urekebishaji ni sehemu isemayo, ili wakujue wewe, na pia Yesu Kristo Mwanao, uliyemtuma kuwa ni Mungu wa Pekee wa Kweli. Tunaweza pia kuendelea kuwaona na kuungana na kina S. Chrys. Na wengineo ili kwamba Baba hapa anaitwa Mungu wa pekee wa kweli, pasipo kuwajuuisha Mwana na Roho Mtakatifu, ambaye ni yeye huyu Mungu wa pekee wa kweli na Baba, bali ni kutenganisha tu na miungu yaa uwongo ya Wamataifa. Hebu na Wasosiniani wajue na kukumbuke kuwa (1Yohana aya ya 20), Mwana wa Mungu, Kristo Yesu ndiye anayeitwa kwa haraka haraka Mungu wa Pekee wa Kweli, hata kwene mandiko ya Kiyunani, ambayo kwayo wanayategemea sana kujenge hoja zao.
Kumbuka pia
matumizi ya nembo ya zisiyo sahihi na potofu za kukejeli au kudhalilisha, kama
vile Waariani wanaotafuta kupotosha au kukataa uhalali wa imani ya
kiyunitariani ya Biblia. Hakuna uwezekano kwamba huyu Mungu wa Pekee wa kweli
kwenye Yohana 17:3 au 1Yohana 5:20 anayetajwa sio Yesu Kristo kabisa, kwa
kusaidiwa au pasipo kusaidiwa na maandiko. Ukweli wa kwamba chapisho au tafsiri
ya the Douay-Rheims ni tafsiri ya Vulgate ya Kilatini na, hivyo maandiko haya
yametoholewa kutoka kwenye Kilatini hayakutajwa. Neno lililo kwenye maandiko
asili hayataji Kristo bali yanamtaja tu Mungu wa Pekee wa Kweli ambaye Mwanae
ni Kristo. Maana yake yanajulikana na yanaeleweka.
1Yohana 5:20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele
Yeye aliye wa
kweli ni Mungu wa Pekee wa Kweli. Tunamjua yeye na tu ndani yake, yeye aliye wa
kweli na mwanae Yesu Kristo. Tunamuabudu yeye aliye wa kweli, na sio mwana
wake, Yesu Kristo.
Makosa na
upotoshaji uliolikumba Kanisa la Mitume yaliendelea kutokana na mashambulizi
yaliyokuwepo ya kuishambulia sheria au torati kwa ujumbe mzuri na wa heri wa
Malaika, ambao kwa jinsi ulivyokuwa tu ulikuwa ni rahisi sana kuuhubiri na kuufundisha
na kukomesha, hali hii ya kumuinua Kristo kwa kumlinganisha sawa na Mungu. Kila
upotoshaji ulikusudiwa kulitenganisha Kanisa na mamlaka na amri za Mungu. Mara
tu Uungu unapochanganwa na kweli kusahauliwa, wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo
wanapewa na kulimbikiziwa nguvu za upotevu ili wauamini uwongo (2Wathesalonike
2:11). Andiko hili linatoka kwene Isaya 66:1-4 ambapo Mungu anachagua upotevu
au vitisho au shuruti za dini za uwongo, kutokana na neno ta’a’uwl (SHD 8586) maana yake ni kuchanganya au mchanganyo
(kuwa ni kitu kilichopangiliwa) ambacho ni shuruti, na usahihi wake ni vitisho,
ambavyo ni ubabe au upotevu. Hivyo, Paulo alikuwa ananukuu
Mandiko Matakatifu yote mawili hapa na pia kwenye Warumi 1. Hivyo, vitisho vya
dini za uwongo vinahusisha mateso na mikakati ya kikatili ya kuikomesha kweli.
Na hii ndiyo sababu imani ya Kiyunitari imekuwa ikipitia vipindi vya mateso
makali tkwa kipindi cha karne nyingi. Mara tu Uungu unapochanganywa na
kuanzishwa kwa Utrinitari, ndipo upotofu unaanza na sheria au torati kushindwa.
Mashambulizi juu
ya Uungu yameenda mbali zaidi ya hatua za majaribio rahisi kama ilivyojitokeza
kwenye jaribio la kudai kuwa na usawa wa kicheo na wa umilele. Mbali na
kuvifanya au kujitengenezea na kuviabudu vitu vilivyokufa au visivyo na uhai na
kuviabudu, kwa mfano imani ya kumuomba Mariamu na kuwaabudu waliowapachika
majina ya watakatifu na masalia ya miili au mifupa ya wafu malumbano yamekuwa
yakiendelea na kupamba moto jambo linalokinza na kuishia kwenye uwepo huu huu
wa Mungu akiwa kama ni nguvu inayoendelea. Hoja zenyewe zinatuama kwenye
misingi ya imani za Uanimism wa Kibabeloni pamoja na machipukizi yake ya
kimasgakiri ya mbali na ya karibu. Hoja hizi na malumbano haya vilikuwa ni vitu
vya kawaida kwenye Unostiki na sasa yanaonekana au kujitokeza kwene Teolojia
Endelevu, ambayo ni mrithi wa siku hizi wa nadharia ya Kinostiki.
Unostiki na Kutokuwepo Uwepo wa
Mungu
Mungu anatajwa
kuwa ni kama kiumbe. Kiumbe inatafsiriwa
kwenye lugha ya Kiingereza kuwa ni uwepo, iwe rasimali au isiyo raslimali (Kamusi
ya Universal Oxford Dictionary). Mapatilizo
ya hatari sana ya mafundisho ya Ukristo wa baadae, ni kwamba Kristo ni Mungu
kwa maana ya kwamba Mungu Baba ndiye Mungu, kimsingi umekuwa ni Uditheism. Utenganishaji
wa mara kwa mara wa Roho Mtakatifu kama kitu chenye hisia na akili kilicho tofauti
na mbali na Mungu Baba na Yesu Kristo kuendeleza Utritheism. Vitu vilivyowazi
kwenye kuinuka umuhimu asilia wa Umoonotheism ulipelekea kwenye jaribio la
kwenye karne ya tatu ili kuweza kuwa na utambulisho wa vitu hivi vitatu kwenye
muundo mmoja. Mwendelezo huu na wa zaidi unatuama na kushikamana na imani ya mrengo
wa waabudu miungu mingi. Kwa mfano, madai ya kwamba Mungu (au ktu na mtu
mwingine yeyote anayedhaniwa kuishi kwa namna hiyo) wa ngozi ya mtu asiyeishi
kwenye Teolojia ya Ukombozi kama inavyokutikana kwenye imani za Kibudha, Uhindu
au dini ningine za ki-wahamiaji wa kuhamahama.
Kwenye itikadi ya
imani ya Mungu Mmmoja au Umonotheism, nadharia kama hiyo kimsingi ni ya kipuuzi
(kama ilivyo upuuzi, na kwa kweli ni kufuru) kwa Mkristo au mwamini Mungu Mmoja
kuamini kwamba Mungu haishi. Kutoka juu, Mungu anatajwa kuwa ni kama kiumbe na kiumbe anatafsiriwa kuwa ni kama kiumbe
anayeishi, ama kimwili au visivyo kimwili. Kwa hiyo, jaribio la kukitenganisha
kitu au kiumbe, muundo wa kuabudu miungu mingi ulienea mbali hadi tangu kabla
ya kuwepo kwake. Kutokana na imani ya wa Parmenidean ya Umonism, ya kwamba
jinsi inavyoweza kufanya uwepo wake. Imani ya Baadae ya Umonism inadai kuwa
hali ya kutanganisha kla mmoja peke yake ni imani ya kufikirika tu au ni dhana
isiyo tekelezeka.
Tumeona kwamba
msimamo wa kibiblia una Mungu mmoja tu mkuu na mwenyezi, Eloa, na Kristo na
wana wa Mungu ni viumbe wadogo na wasaidizi. Kwenye Dola ya Kipagani ya Warumi,
sheria au amri kama ilivyotolewa kwa Wayahudi ilipingwa vikali sana na wenye
fikra wote waliofuatia baadae. Ukataaji au upuuziaji wa sheria kwa msingi
endelevu na wanateolojia wanaopinga maazimio ya mtaguso wa Nikea ulipelekea
kuwepo kwa msimamo wa kihafidhina wa wapinga Usemitiki wa vitabu na maandishi
ya Athanasius na wanateolojia wa zama kale za kabla ya mtaguso wa Nikea. Sababu
yake inadai kama ifua avyo.
Torati au sheria iliyotolewa
na Mungu Baba haiipo imara kiasi cha mwanadamu kushindwa kuibadilisha kwa kusingizia
hadhi yake ya kimamlaka ya kuwa msaidizi. Kwa hiyo, ndipo Kristo alipoinuliwa
na kanisa kwa kiasi cha kumlinganisha na Mungu, kwa kanisa kudai kuwa limepewa mamlaka
ya kuigeuza au kuyarekebisha maandiko ya Agano Jipya. Lakini mchakato huu ulikuwa ukifanyika taratibu sana
na bila papara.
Catherine Mowry
LaCugna na Karen Armstrong wote wawili walionyesha kwamba kwa sehemu kubwa
kanisa lilikuwa msaidizi hadi kufikia karne ya nne na kwamba mafundisho ya
umilele na usawa wa hawa wote wawili yalikuwa ni madai yao ya baadae. Lengo hapa
ni kutilia maanani mafundisho asilia ya mwanzoni. Mchakato wa kuyaingiza mawazo
haya ulianza kwa kushambulia uwepo wa Mungu kama ni mtu mmoja na kumuinua zaidi
ya uwepo wake. Fundisho la kwamba Mungu hakunenwa kuwa yupo, likawa zaidi ya
hali yake ilivyo, lililetwa na kupendekezwa kwanza na Basilides mwanazuoni na
msomi wa Kinostik aliyekuwa anafundisha huko Alexandria wakati wa utawala wa
Mfalme Hadrian. Itikadi na mafundisho yake yalishika kasi kwenye mwaka 125 BK
lakini hakumudu kuupata umaarufu mkubwa (soma kitabu cha Schaff, History of The Christian Church, (Historia
ya Kanisa la Kikristo), Vol. II, pp. 467-468). Uthibitisho wa kimapokeo kuhusu
uwepo wa Mungu kama vile hoja za kiontolojia na kiontolojia hauwezi kuonyeshwa
hapa kuwa ni michoro au alama muhimu. Hoja za kwamba Mungu yuko zaidi ya uwepo
wake au hafungiki mahali pamoja kama kuwa hawezi kuwa kwenye umoja au peke yake
ambaye anaitendea kazi ya stara au Ghiliba
unafafanuliwa vya kutoksha kwenye Kitabu cha 2 kinachoshughulikia teolojia iliyopelekea
kwenye mtguso wa Nikea na ule wa Constantinople na kuingizwa kwa imani ya Utatu
au Utrinitari.
Kimsingi, madai
kama haya ni ya ki Mmonistiki na, kwa inavyoonekana hapo juu ni kwamba hayana
msingi wowote wa kibiblia. Hata
hivyo, mafundisha ya namna hii yalielezewa tu baada ya miaka 400. Hatua za
muhimu ni za muhimu kwa uelewa wowte wa mchakato ule na utaelezewa kwa msingi
endelevu kwenye Kitabu cha 2. Kinachojiri kueleweka ni kwamba Ukristo wa siku
hizi hauna uhusuano wowote na wala haufanani kwa lolote na Ukristo wa karne ya
kwanza uliokuwa umejumuisha Wayahudi na Wakristo waliokuwa wa mrengo wa kuamini
Mungu mmoja au Umonotheism hasahasa kwa jinsi ulivyoelezwa kwenye maandiko ya
Agano Jipya. Shambulio lililofuatia kwenye teolojia ya Kiyahudi kuhusu ujio wa
Masihi na mamlaka ya Maandiko Matakatifu lilianza kwa kukataa marejesho ya
kipindi cha Milenia yanayofuatia ujio wake wa mara ya pili. Hoja yenyewe
ilikuwa ya kawaida na ilijulikana sana katika karne ya ishirini kwa wanazuoni
wasomi wa Kiathanasian.
Masihi Mwenye Ujio wa Aina Mbili
Kurudi au ujio wa
Masihi utakuwa ni kwa ajili ya kuja kuansiaha Utawala au Ufalme wa Mungu wa
millennia, ambao utaongozwa kwa mujibu wa maandiko ya Torati na sheria za Mungu
kwenye utaratibu wa utawala wa kawaida wa kimwili. Ili kufanikisha mkakati huu
wa kiutawala, ni muhimu kuwa Masihi ashike hatamu za utawala wa dunia kwa nguvu
katika siku za mwisho. Vitabu vya kinabii vya Isaya, Ezekieli, Danieli, Zekaria
na Ufunuo zimeeleza kwa wazi sana kuhusu kipindi hiki cha kuanza na kuendelaa
kwa Ufalme huu. Hususan kitabu cha Ufunuo kimeelezea wazi kuwa kipindi hiki
kitadumu kwa miaka elfu moja (Ufunuo 20:1-4). Wanazuoni wa siku hizi wanajaribu
kupinga ukweli na uhalisia wa unabii kwa kudai kwamba maandiko haya yaliandikwa
na Kanisa la karne ya kwanza lililokuwa linatuama kwenye msingi wa mafundisho
ya kinadharia bahatishi tu (mfano wake waweza kuuona kwenye kitabu cha Bob
Barnes (ANU) The Bulletin, 24-31
January 1995, art. ‘Apocalypse Sometime’, pp. 42-43). Kitabu cha the DSS kinaonyesha kwamba imani ya Kiyahudi ilitarajia
Masihi wa ujio wa aina mbili (soma kitabu cha G. Vermes, cha The Dead Sea Scrolls in English [Nakala ya
Kiingereza ya Gombo la Bahari ya Chumvi], hasahasa mahali pasemapo Messianic Anthology [Antholojia ya Masihi]
na tafsiri ya sehemu ya kumi na tatu kutoka sehemu unayosema pango XI). Mstari
wa uzao wa Masihi ulikuwa ni wa Nathani na Lawi (soma Zekaria 12:10; sawa na
kwenye Luka 3). Antholojia ya Masihi inatilia
maanani na iko makini sana na ahadi za Lawi zilizo kwenye Kumbukumbu la Torati 33:8-11
na 5:28-29. Maandiko yanamuonyesha nabii anayetajwa kwenye Kumbukumbu la Torati
18:18-19 na inamtaja au kumuonyesha Masihi kama inavyofanya Hesabu 24:15-17. Masihi
Haruni na Masihi wa Israeli walikuwa ni mtu mmoja huyohuyo kwa Kanuni au Sheria
za Kidameski (VII) na nyaraka nyingine zisizochapishwa wala kufundishwa za
pangoni IV (Vermes, p. 49). Tafsiri ya Korani inamtaja Melkizedeki kuwa kama Elohim na El. Hii inatokana na dhana ya hukumu ya mwisho iliyotabiriwa
kufanywa na Masihi Kuhani na ukuhani wake. Isaya 52:7 inatumia jina elohim ikimaanisha
ujio wa Masihi akirudi huko Sayuni (soma Waebrania 12:22-23). Ilijulikana kuwa
alikuwa anafahamika na malaika mkuu Mikaeli na alikuwa ni kiongozi au mkuu wa Wana wa Walioko Mbinguni au Mungu Mwenye Haki.
Kwa hiyo, dini za
mrengo wa Kiyahudi zilifundisha,kuwa Masihi ni kama Mikaeli (aliye kwenye Danieli
12:1). Nadharia na fikra hizi zilikuwa ni makosa. Jina Melkizedeki lilikuwa na
maana ya kuwa Mungu Wangu Ndiye Haki au
Mfalme Wangu ni wa Haki (Haki na
Utakatifu vinafanana maana zake) (kwa kujibu wa kitabu cha Vermes, cha Dead Sea Scrolls in English [Toleo la
Kiingereza la Gombo la Bahari ya Chumvi], p. 253). Ilidhania pia kwamba
Melkizedeki lilikuwa ni jina la kiongozi wa Jeshi au Nuru, ambao tuliyemuona, ni
kazi ya Masihi (Vermes, p. 260).
Nadharia hizi za
kifikra zimetokana na kuharibiwa kwa Agano
la Amram. Ambacho kilibakia kwenye sheria na msisitizo wa Melkizedki-Masihi
huko Essene. Kama Melkizedeki angelipokuwa Masihi ndipo kungekuwa na tatizo
kubwa kuwezekana aje kuzaliwa hapa duniani na kujitoa dhabihu.
Fikra za Wakristo
kudhani kwamba Melkizedeki ni Masihi zinatokana na kutoelewa maandiko yaliyo
kwenye Waebrania 7:3. Maneno yasemayo hana
baba, wala mama na wala hana mwana au zao (apator nk.) yanataja umuhimu wa kuandikwa rekodi yake kwenye mstari
wa ukoo wa Haruni (Nehemia 7:64) kwa ukuhani wa Walawi.
Neno mwanzo wa siku na mwisho wa maisha lina
maanisha umuhimu wa kuanza kazi akiwa na umri wa miaka thelathini (Hesabu
4:47). Kuhani Mkuu alirithi huduma yake tangu siku ya kufa kwa mtangulizi wake.
Melkizedeki hakuwa na sharti kama hilo. Kitabu cha Waebrania kinaandika kuwa
alikuwa mtu au mwanadamu (Waebrania 7:4). Aliumbwa kama Mwana wa Mungu (Waebrania 7:3) lakini hakuwa Mwana wa Mungu ambaye alikuwa Kuhani Mwingine (Waebrania 7:11). Hivyo basi, wateule wote wanaweza
kushiriki kwenye huduma hii ya kikuhani, wakifanyika kuwa kama Mwana wa Mungu,
pasi kujali uhusiano wao wa kinasaba wa uzao wala umri wao, wakiendelea milele.
Ni kama Melkizedeki alivyokuwa nasi pia twaweza kuhudumu (soma jarida la Melkizedeki (Na. 128)). Waessene walipotosha andiko linalomwelezea Masihi ni kama wanavyofanya
wahafidhina wa nyakati hizi. Inaonekana kuwa kitabu cha Waebrania kuwa
kiliandikwa hivyo na kusahihisha kosa hili lakini chenewe kikiwa kimekosewa
pia. Mwandishi Midrash anasema kuwa alikuwa Shemu (Rashi) akiwa mfalme (melek) wa mahali pa haki (tsedek) (kwa mujibu wa Abraham ibn Ezra
& Nachmanides). Mahala hapa palikuwa ni pale ambapo Hekalu linapaswa kujengwa
kwa ajili ya Uwepo wa Mungu au wa Kimbinguni, ambapo hii Midrash inapasa kuwa
huko Yerusalemu kwa ujumla, kutokana na andiko linalosema haki itakuwa ndani yake (Isaya 1:21) (kwa mujibu wa ibn Ezra &
Nachmanides, soma pia Soncino, fn. Hadi
Mwanzo 14:18).
Lakini lililo
muhimu sana ni wazo kuhusu Baraza la
Elohim lilikuwa kamili na halikanushiki au kupingika kama ni maana
iliyoeleweka vizuri kwenye maandiko ya Agano la Kale yanayomhusisha elohim. Mfumo au muundo wa usaidizi wa elohim unaeleweka kwa upande mmoja ila
haueleweki kwenye uhusiano wake na Mikaeli na Melkizedeki. Ufunuo 4 na 5 inaonyesha
kuwa kundi hili lilikuwa na idadi ya washiriki thelathini wakiwemo makerubi
wanne. Kwa hiyo vipande thelathini vya fedha vilihitajika ili kumsaliti Kristo (Mathayo
27:3,9; sawa na Zekaria 11:12-13) kama ilivyokuwa chukizo dhidi ya Uungu wote
au Baraza la ndani. Wazzee walipangiwa kusimamia maombi ya watakatifu (Ufunuo
5:8) na Kristo ndiye Kuhani wao Mkuu. Alikuwa ni mshirika mwezao aliyeonekana
kustahili kufungua kitabu au gombo la mpango wa Mungu aliwaondolea dhambi
wanadamu na kuwafana kuwa ufalme na makuhani wa Mungu wetu, yaani Mungu wa
Baraza la Kristo (Ufunuo 5:9-10). Msamaha wa dhambi wa wanadamu ni sehemu ya marejesho
au matengenezo yatakayotokea au kufanyika wakati wa kurudi kwake Masihi akiwa
kama Mfalme wa Israeli, kwenye ujio wake wa kwanza anajulikana kama Masihi wa
Haruni. Ujio huu wa kwanza wa Kimasihi ulikuwa ni upatanisho kwa ajili ya
dhambi na kuanzisha ukuhani wa Melkzedeki.
Marejesho ya
nyakati za mwisho yalijulikana kuwa ni mwendelezo wa elohim kama ulivyoonyeshwa kwenye Zekaria 12:8. Kwenye marejesho ya
siku za mwisho wakati atakapokuja Masihi huko Sayuni, kama ilivyoeleweka kwenye
Waebrania 12:22-23, mchakato wa matukio ya ujio wake yatahusisha mkakati wa
kuulinda mji wa Yerusalemu na kuwaimarisha wakazi wake watakaokuwemo kwenye mji
huo kwa utawala wa millennia. Lakini kumbuka kuwa Zekaria anaenda mbali sana
kwa kusema:
Na yeye aliye dhaifu
miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama
Mungu (elohim), kama Malaika wa YHVH
mbele yao. (msisitizo umewekwa).
Maana yake hapa yalikuwa kwamba Zekaria alipewa kujua kwamba Malaika wa YHVH
alikuwa ni elohim na kwamba watu wa nyumbani wa Daudi (ambao walikuwa wamekwishakufa
muda mrefu uliopita) walitakiwa kujumuika na wale ambao kwa wenyewe t uni elohim
kama sehemu ya watu wa nyumba ya Daudi.
Zekaria aliandika mwishoni mwa kipindi cha Agano la Kale akiwa ni moja ya
vitabu vya mwishoni kuandikwa (inadhaniwa kuwa ni takriban mwaka. 410-403 KK, Nyongeza
77 ya tafsiri ya Companion Bible inasema).
Kuelewa mfululizo wa matukio ambayo hayajabadilishwa kwa kudumu kwa kipindi cha
kuyaweka pamoja maandiko.
Hitimisho
Utokana na tafsiri ya DSS tunajua uelewa ulikuwa wa haraka wakati wa Kristo.
Mafundisho mapotovu nay a kizushi ya Wakolosai yalijumuisha mhimili wa Baraza
la Elohim. Huko Galatia walianza kuamini ushikaji wa mapokeo kwenye utimilifu
au mkakati wa maroho machafu yatesayo na yadanganyayo watu wakikosa kujua kuwa
walikuwa ni mapepo.
Nyaraka
zilizoandikwa kwa makanisa yote mawili ya Kolosai na Galatia zinatumika ili
kumfanya Kristo kuwa ni mwombezi pekee na kamili na anayetosheleza kati ya wateule
na Mungu. Nyaraka hizi hazikuandika ili kuitangua torati. Kamwe Mtume Paulo
hawezi na kumkanganya Kristo. Vivyohivyo Yohana alikanusha na kupinga toleo
lililoenea zaidi kwa uzushi wa namna hiyohiyo bali, kipindi hiki, mtu
anayetafuta kumuinua Kristo na huku akipinga kufa au kifo chake au dhabihu yake
kamilifu aliyoitoa. Kujua kuhusu Uungu kukaanza kubadilishwa kwenye karne ya
pili. Ushahidi wa kupotosha kosmolojia unaelezwa kwenye maandiko mengi. Hoja
kuhusu makosa haya kuhusu Kristo kuwa Mungu alikutatanazo Mtume Yohana na ilisababisha
kuanza kwa hila makanisani.
Nyongeza
Matumizi ya
Neno Uzushi Kwenye Kanisa la Mitume
Neno uzushi linatumika kwene maandiko au
nyaraka za mitume na limetafsiriwa kwa namna mbalimbali ili kuweka maana
mbalimbali tofauti. Kwa mfano ni:
Matendo 5:17 inahusisha
na vikundi vikubwa vya kidini au sehemu ya Masadukayo waliokuwa wanatumia airesis.
Matendo 15:5 inatumia
neno aireseõs kutaja kundi la Mafarisayo.
Kwa hiyo kazi kuu mbili za kiutendaji wa Wayahudi walioyataja mafundisho haya
kuwa n uzushi. Kwa hiyo, hakuna uhusiano wa kikashifa.
Matendo 24:5 inatumia
neno uzushi kwenye muundo wa kigrama aireseõs inapoelezea vikundi vya dini za
Wanazarayo. Hivyo, kanisa la kwanza lilitajwa kuwa ni kama la wazushi.
Matendo 24:14 inatumia
neno uzushi kwa muundo wa kigrama airesin inayomaanisha kuwa ni njia. Kanisa lilikuwa ni njia wanayoiita kikundi cha kidini (uzushi).
Matendo 26:5 inamnukuu
Paulo kama kusema kwamba kwa mujibu wa sekti yenyewe kabisa ya dini ya Kiyahudi,
aliishi kama Farisayo. Neno lililotumika ni airesin
au uzushi. Tena hakuna kusudi la kufanya
kashifa ya wazi.
Matendo 28:22 inataja
kuwa aireseõs au uzushi ambayo imetafsiriwa kama kikundi cha kidini au sekti kwakuwa ni wazi sana kwamba
kanisa linachukuliwa na mtazamo wa kiutofauti wa mawazo haukuwekwa sawa kwa
namna sawa kama zilivyokuja kufanyiwa na Kanisa la baadae la Kiathanasian.
2Petro 2:1 inaiita mafundisho
ya kizushi (aireseis) ya uharibifu ambayo yanatafsiriwa kuwa ni mawazo au nadharia
yenye kuharibu na kuangamiz (RSV). Tafsiri ya KJV imetafsiri andiko hili kama
ni mafundisho ya kizushi tu.
Wagalatia 5:20 inayaita
migawaniko na aireseis imetafsiri sekti au sehemu
ya maroho (RSV). Andiko hili hapa haliitaji tofauti yoyote ya kimtazamo au
mawazo kuhusu mafundisho. Andiko hili linajiri matawi ya sheria au torati
ambayo yalipasa yawe wazi kwa wale wenye Roho Mtakatifu. Kwa hiyo Paulo
anatumia neno hili ili kufunika makosa ambavyo inatumika kwa kuwaelimisha
wateule kama tunavyoona kwenye 1Wakorintho.
1Wakorintho 11:19
inaonyesha kuwa mafundisho haya ya kizushi (aireseis)
yametafsiriwa sekti (RSV) kwenye makanisa
yanaruhusiwa na ni ya muhimu. Tofauti kati ya mawazo makanisani inawafanya
wateule kuichunguza na kuinisha au kuipima kweli na pia kuwaonyesha wale wateule
wenye Roho Mtakatifu na kuipambanua kweli. Kwa hiyo, kitendo cha kuzima kwa
shuruti mawazo stahiki (mahali yanapokuwa hayavunji sheria) ni kinyume kabisa na
mafundisho yaliyo kwenye 1Wakorintho.
q