Makanisa Ya Kikristo Ya Mungu
[096]
Mkanganyiko Kuhusu
Sheria
Toleo La 3.0
19950318-19990614-20080128)
Jarida hili linatathmini tofauti iliyoko kati ya kanuni au sheria za kijamii na za utoaji wa dhabihu. Tofauti hii iweka sehemu ya msingi wa mambo yaliyotokee kwenye zama za uandishi wa kitabu cha Mwanzo. Jarida hili pia linafafanua kwa kina zaidi mambo kadhaa yanayohusiana na sheria za Mungu. Tofauti ya msingi iliyofanywa na Wanamatengenezo ileorodheshwa kama Msingi wa Imani tangia Waraka wa Pili wa Ukiri wa Imani wa Wahelvetiki kati ya Nyaraka Thelathini na tisa za Imani ya Kanisa la Uingereza za mwaka 1571 na nyingine za wana Matengenezo hadi kufikia za Wamethosti zilizojulikana kama Ukiri wa Imani ya Kidini ya mwaka 1784. Tangazo hili ni la muhimu kwa manufaa yao wenyewe.
Christian
Churches of God
E-mail: secretary@ccg.org
(Hati Miliki ©
1995, 1999,
2008 Wade Cox)
(Tr. 2014)
Masomo haya
yanaweza kunukuliwa na kuwapa watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu
bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la hati miliki ni
lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kwa
nakala yoyote atakayo pewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa
kukithi haja ya lugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.
Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org na http://www.ccg.org
Mkanganyiko Kuhusu
Sheria
Baadhi ya
mafundisho yaliyoko kwenye Ukristo wa leo ni kujaribu kudai kwamba Sheria au
Toari imepitwa na wakati na haihitajiki tena, jambo linalotokana na kutozielewa
vizuri nyaraka za Mtume Paulo zilizo kwenye Agano Jipya. Madai haya sio sahihi.
Mafundisho haya yameanzishwa kutokana na kutokuelewa kile kilichoondolewa na
kukomeshwa na dhabihu aliyoitoa Kristo na kugongolewa pale mtini au stauros,
kunakoelezwa kwenye Wakolosai 2:14. Kristo alifuta mashitaka (cheirographon) kwenye mashitaka yaliyokuwa yanatukabili
(au, yalikuwa
yanatukabili tukiwa tumeshitakiwa; soma fasiri ya Biblia ya Marshall’s Interlinear, RSV)
pamoja na madai yake. Iliondolewa mbali na kupigiliwa mtini au kwenye stauros.
Je,
ni yapi haya mashitak yanayoelezewa
hapa? Ni nini
kilichoondolewa kwa dhabihu hii ya Kristo?
Kwa
kweli haikuwa Torati ya Mungu iliyoondolewa. Tofauti iliyoelezwa na Mitume
inaonyesha kuwa Amri zilizowekwa na MUngu zilikuwa muhimu nab ado zinaendelea (soma
hapo chini). Cheirographon ni jalada au waraka uliotolewa kwa
ajili ya kufutiwa mashitaka. Linatokana na neno la Kiyunani dogmasin, ni mfumo wa utaratibu ambao unatokana
na Torati ya Musa (kutoka Waefeso 2:15). Uhusiano uliopo kati ya Mungu na Torati yake ni wa muhimu
sana.
Mungu ni |
|
|
Torati yake ni |
|
|
Mtakatifu |
(Ezr 9:15) |
|
Takatifu |
(Zaburi119:172) |
|
Mkamilifu |
(Mat. 5:48) |
|
Kamilifu |
(Zaburi 19:7) |
|
Mtakatifu |
(Law. 19:2) |
|
Takatifu |
(Warumi 7:12) |
|
Mwema |
(Zab. 34:8) |
|
Njema |
(Warumi 7:12) |
|
Mkweli |
(Kum. 32:4) |
|
Truth |
(Zaburi 119:142) |
|
Mungu habadiliki. Na
ndivyo ilivyo, kwamba Kristo ni yeye Yule, jana, leo na hata milele (Waebrania
13:8) kwakuwa ana ukamilifu wa asili ya kimbinguni (Wakolosai 1:19; 2:9). Torati
ni ya muhimu katika kuyaonyesha mapenzi ya Mungu, ikitangulia au kuonyesha
asili yake kamilifu, na iliyoandikwa kwenye mioyo ya wateule. Sheria za Mungu ni haki, ya
kweli na njema (Nehemia 9:13). Wateule wametahiriwa mioyo yao kwa kuwa
wanachukua hadhi ya umbinguni (2Petro 1:4), na kushindania ili kuwafanya wote
waufikilie utimilifu (pleroma) wa Mungu (Waefeso 3:19), kama alivyokuwa
Kristo. Watu wengine wote inawalazimu kuishika Torati ya Mungu. Wanahukumiwa
kwa kutobadilisha baadika kwao (KJV); au kwa maneno mengine, kwa kuwa
hawazishiki sheria (RSV, Zaburi 55:19). Heri walio kamili njia
zao, Waendao katika sheria ya Bwana. (Zaburi 119:1). Torati inatimilika ndani ndani yetu sisi
tunaoenenda sawasawa katika roho (Warumi 8:4). Sio wasikilizaji wa Sheria walio
watakatifu, bali ni wale wanaozitenda na kuzitii (Warumi 2:13).
Uashikaji
wa Amri za Mungu ni wa muhimu kwenye upendo na kumjua Mungu (1Yohana 2:3,4;
3:22; 5:3) na Kristo (Yohana 14:15,21), na kupokea maelekezo ya Roho Mtakatifu
(Yohana 14:21; 1Jn. 3:24; Matendo 5:32), na Baraka za Mungu (Ufunuo 22:14). Kitendo
cha kuvunja au kutozitilia maanani au mafundisho ya kuzipuuzia au kuzivunja Sheria
ilikatazwa na Kristo (Mathayo 5:19).
Mathayo 5:19 Basi mtu ye yote
atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo,
ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na
kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
Ukweli
wa mambo ni kwamba alichokuwa anakiongelea Paulo kwenye maandiko ni kwamba sio
tu aina mbili za sheria, bali pia kazi nyingine ya tatu iliyopotea kwa karne
kadhaa. Aliyaita matendo haya ergon nomou, iliyotafsiraiwa kama Matendo ya Sheria, ambayo kwa kweli yalikuwa ni kundi
lingine la maandiko lililopotea kwa kipindi cha takriban miaka elfu.
Yalionekana yalipochimbuliwa na yanajulikana kama Gombo za Bahari ya Chumvi au the Dead Sea Scrolls na imeelezwa kwa kina kwenye jarida la
Kazi za Maandiko ya Torati (Na. 104) [The Works of the
Law Text - or MMT (No. 104)].
Paulo
alifundisha kuwa kutahiriwa au kutotahiriwa kwao hakuna kinachoongezea chechote
ila la muhimu ni ushikaji wa Sheria za Mungu [ndiko muhimu] (1Wakorintho 7:19).
Ingekuwa vigumu sana ajichanganye mwenyewe tena kwa maandiko yake ya Wakolosai
au Wagalatia (mfano Wagalatia 3:10). Kwa hiyo anaongelea mambo mawili ya sheria.
Sheria
ile iliyokamilishwa na Kristo pale Kalvary, kwa hiyo alipaswa kuwa mojawapo ya
aina ya vitu ambavyo havibadiliki lakini vinatimilika. Tofauti ya kawaida ni
ile ya Sheria ya Maisha kwenye Jamii na Sheria za mambo ya Kidini. Sheria ya
madili ya Jamii zilizoongelewa kwenye Amri Kumi za Mungu. Sheria hizi za Taratibu za Kidini zinajulikana kama Torati ya Musa. Tofauti itaonekana kuwa
kama haitoshelezi. Andiko linaloelezea Matendo ya Sheria inaonesha kuwa jambo
moja kubwa la kukosa uelewa kunakoiathiri itikadi ya waantinomia walio kwenye Ukristo wa
leo. Tofauti imewekwa kwa wazi
zaidi kutokana na mlinganisho ufuatao.
|
|
Torati
ilikuwa |
Sheria za
Dhabihu au za Kidini zilikuwa |
1. Imetolewa na
Mungu kwa mkono wa Malaika pale Sinai (Kutoka 20: 1,22; Deut. 4:12;13; 5:22); |
1. Zilinenwa na YHVH;
zikaandikwa na Musa Musa (Kutoka 24:3,4,12); zilitolewa kama nyongeza ya zile
Amri Kumi (Kutoka 24:12); |
2. Ziliandikwa
na Yahova (Kutoka 31:18; 32:16); |
2. Ziliandikwa na Musa (Kutoka 24:4; Deut. 31:9); |
3. Kwenye mawe (Kutoka
24:12; 31:18); |
3. Kwenye kitabu
(Kutoka 24:4,7; Kumb. 31:24); |
4. Ilitolewa na Yahova na kupewa Musa (Kutoka 31:18) |
4. Ilitolewa na Musa kwa Walawi (Kum. 31:25,26); |
5. Iliwekwa na
Musa kwenye Sanduku la Agano (Kum.
10:5); |
5. Iliwekwa ndani ya sanduku la agano na Walawi (Kum 31:26) ambayo ilikuwa ni ushuhuda
kwa Israeli. |
Torati |
Sheria za
dhabihu au za Kidini |
6. Ilihubiriwa
pamoja na kanuni za kimaadili (Kut. 20:3-17); |
6. Inahusiana na
taratibu za mambo ya kiibada (kutoka kwenye matumizi yake yalivyoelekezwa
kwenye vitabu vya Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati); |
7. Inaidhihiridha
dhambi (Warumi 7:7); |
7. Inahusu
utoaji wa sadaka za dhambi zilizofanywa (soma Mambo ya Walawi); |
8. Inaonyesha
kuwa uvunjifu wa sheria ni dhambi (1Yohana 3:4) na mshahara wa dhambi ni mauti (Warumi 6:23). |
8. Hakuna dhambi
kuzivunja kwa kuwa zimetanguka (Waefeso 2:15); kwahiyo, pasipo sheria hakuna dhambi au uovu
utakaogundulika (Warumi 4:15). |
9. Tunapaswa kuzishika sheria zote (Yakobo 2:10); Tusiivunje hata yodi moja ya Torati (Mathayo 5:19) |
9. Mitume hawakuamuru hivyo (hawakufundisha au kuamuru; diesteilametha) kuzishika
sheria (Matendo 15:24); |
10. Kwakuwa tutahukumiwa kwa mujibu wa torati (Yakobo. 2:12); |
10. Hatupaswi
kuhukumiwa kwa kuzishika (Wakolosai 2:16); |
11. Mkristo
anayeishika torati hii amebarikiwa kwa matendo yake (Yakobo 1:25); |
11. Hatuhesabiwi
haki kwa sheria bali ni kwa imani (Wagalatia 5:1-6); |
12. Ni sheria kamilifu ya uhuru (Yakobo
1:25; sawa na Yakobo 2:12) kwa kuwa torati ni kamilifu (Zaburi 19:7); |
12. Uhuru
unatokana na imani na wala hatuhesabiwi haki kwa sheria (Wagalatia 5:1,3). |
13. Torati hii ilianzishwa kwa imani katika Kristo (Warumi 3:31); haikutanguka
(Mathayo 5:17); |
13. Kristo alikomesha
migawanyiko ya sheria (Waefeso 2:15); madeni (Wakolosai 2:14); na muundo wenyewe
(Wagalatia 3:19). |
14. Kristo alikuja kuitimiliza
sheria na kuzitukuza (Isaya 42:21); |
14. Kristo alifziutiliambali hati
zote za mashitaka yaliyokuwa dhidi yetu (Wakolosai
2:14). |
15. Tunajua kwamba torati ni ya kiroho (Warumi 7:14 sawa
na aya ya 7). |
15. Hizi sheria ni za mambo ya amri
za kimwili (Waebrania 7:16). Mungu aliwataabisha Israeli kwa kuwapa
sheria ambazo wasingeweze kuishi kwazo kwa kuzihalifu kwao na kuzivunja
(Ezek. 20:25). Sheria hizi
hazikufanya jambo lolote kamilifu. |
|
|
Muundo wa kimwili wa sheria
ya utoaji dhabihu na alama au ishara zinazoonekana vilipaswa virudiwe kila
mwaka hadi pale Kristo alipolipa mara moja tu na kwa wote kwa ajili ya dhambi
zetu.
Sheria ya utoaji wa
dhabihu zilipaswa kuondolewa kabisa ili ituwezeshe kuuimariha uhuiano wetu na
Mungu kwa kiwango kikamilifu cha kimo cha kiroho. Ni kwa kupitia Krito tu na karama
za Roho Mtakatifu jambo hili linaweza kufanyika, kama sisi wenyewe tulivyo kuwa
ni sadaka iliyo hai za mfumo huu, tukiyatoa maisha yetu ili kutumikiana.
Maandiko ya Musa
yanaelezea Amri Kuu mbili ambazo kwazo zinajumiuha mambo haya mawili. Torati yote
na Manabii (sawa na majarida ya Amri Kuu
ya Kwanza (Na. 252) na Amri Kuu ya Pili
(Na. 257) [The First Great Commandment (No. 252) and The Second
Great Commandment (No. 257)].
Kwa hiyo, kunamkanganyo
wa heria na mkanganyo huu unazihusu wazi sheria za mambo ya kijamii. Sheria za
Mungu za kijamii zinamfanya mtu wa kiroho awe mkamilifu kama zilivyoanzihwa,
kuheshimika na kutukuzwa na Kristo kwa njia ya imani na kutoa uhuru.
Ziliandikwa kwa chanda
cha mkono wa Mungu na zinaitwa Sheria za Ufalme
(Kutoka 31:18; Yakobo 2:8). Tunahukumiwa kwa sheria hizi, ambazo Kristo amezitukuza
kwa kadiri zote. Kwa hiyo kufanya kinyume chake ni awasawa na kuzini. Sheria yote ni kuu na wala hakuna iliyo ndogo
kwenye umuhimu wa kumfanya mtu awe mtakatifu. Manabii wamezitafiri sana sheria
hii ya mambo ya kjamii kama zilivyoainishwa kwenye Amri Kuu Mbili ambazo zinazifafanua.
Kwa hiyo, zile zinazoitwa ama kujulikana kama ‘sheria za mambo ya kidini’
ambazo kwa kweli zimegawanyika tena kwenye kundi la ‘sheria za dhabihu’ na
fafanuzi za kiheria zinazotafsiri ‘sheria za kimaadili’. Kushindwa kuuelewa
mkanganyo huu ni makoa makubwa ya Ukristo wa leo, yakirithi imani ya
kiantinomia na Wanostiki. Ukristo huu mamboleo umefanya makosa ya kujaribu
kuziondoa Sheria za Mungu kutokana na kukosea kuyaelewa maana ya nyataka za
Mtume Paulo, na maana ya neno Ergon Nomou au Matendo
ya Sheria. Kwa kufanya hitimiho hili na kuyakumbatia mafundisho yote ya
Vitabu vya Musa au Torati kwa kile kinachoitwa sheria ya mambo ya kidini ndipo
walizifananiha na taratibu za ibada za kipagani na ndipo walipojikuta wanaanzisha
imani zi dini ya kuabudu Juan a Imani-siri. Ndipo Sabato ikabadilishwa na kuwa
siku ya Jumapili na maadhimiho ya ikukuu ya Easter yakawekwa mahala pa
maadhimisho ya Pasaka..
Kuzihika Amri za Mungu
na Ushuhuda wa Yesu Kristo ni muhimu ili kuurithi ule mti wa uzima, kama
tunavyoona kwenye Ufunuo 14:12 na 22:14. Sheria ya amri ilimeandikwa kwenye
kanuni (Waefeo 2:15; Wakolosai 2:14) ilikuwa ni kivuli cha mambo mema
yanayokuja (Waebrania 10:1), na iliondolewa kutokana na udhaifu wake na kutokuwa na tija kwake (Waebrania 7:18; 10:3). Ilitolewa kwa
ajili ya maovu, yakianzihwa na malaika mikononi mwa mwombezi (Wagalatia 3:19). Kwa
hiyo tunautarajia utaratibu wa kuondolewa dhambi kwa kupitia sheria ya dhabihu
ambayo uiikuwa wa muhimu kutokana na kuendelea kwetu kwa kuhindwa kwendana na
mfumo na makusudi ya Sheria. Kwa sababu hii, kumtahiri muumini mkubwa aliyebatizwa
ilikuwa ni ishara ya kimwili wa utambulisho wa utaifa wa taifa ambalo lenyewe
tu lilikuwa ni la kiroho, na ambalo lilikuwa na fungamano la kimwili la
kitaifa. Kwa hiyo haukuwa na faida yoyote zaidi tu ya mambo ya kiroho ya kila
mtu binafi yake (sawa na jarida la Utakao na
Tohara (Na. 251) [Purification and Circumcision (No. 251)].
Cha kuhangaza kingine
ni kwamba, Torati ilitolewa huko Sinai. Sheria nyingine za Mungu za kijamii
hazikutolewa Sinai. Ilikuwepo tangu uumbaji, tangu mwanzo wa kuwepo kwa Mungu.
Dhali ilikuwepo hata kabla hata ya kutolewa Torati na kukabidhiwa Musa (Warumi
5:13), kwa hiyo, madhara ya kuzivunya Torati yalikuwa yamekwisha julikana tayari
tangu Adamu, kwa hiyo dhambi haihesabiwi mahali passipo sheria. Wakati dhambi
zilipozidi chini ya Sheria huko Sinai, ndipo neema iliongezeka (Warumi
5:15-21). Dhambi ni matendo yaliyo kinyume na asili na mapenzi ya Mungu (Zaburi
51:4).
Shetani alimtenda
dhambi Mungu kwa kumdanganya Hawa atende kinyume na mapenzi ya Mungu na kwa
hiyo aliwaibia wote wawili taji zao, yaani ya Adamu na ya Hawa na kuuharibu
uhusiano wao mwema na Mungu. Shetani alivunya Amri ya Kwanza, ya Tano, ya Sita, ya
Nane, ya Tisa, nay a Kumi (Mwanzo 3:1-4;
Isaya 14:13-14; Ezekieli 28:2-10). Shetani mara nyingi anafanya viwakilishi vya
kimapepo, wanaojifanya kuwa vitu vya kuabudiwa na kulitia unajisi au kulikufuru
jina la Mungu, na hivyo kuzivunja Amri za Pili na ya Tatu za Mungu.
Nyakati
za Kristo, ilieleweka kuwa Shetani na mapepo waliacha makazi yao ya kwanza, na
kuja kushiriki matendo ya uzinifu na binti za wanadamu na huko kulikuwa ni
kuivunja Amri ya Saba (Mwanzo 6:4; 1Wakorintho 11:10; Yuda 6; tzama na kuisoma
hasa tafsiri ya Biblia ya New
English Bible kwa maelekezo zaidi ya
hili andiko la Yuda 6; pia soma DSS, Genesis
Apocryphon and 1Enoch). Kwa
kipitia imani za dini za uwongo, Shetani na mapepo wameishambulia Amri ya Nne.
Kwa hiyo, Torati inafanya mahusiano ya kweli kati ya viumbe wasio na mwili
pamoja na wale wenye mwili. Kwa hiyo hawa ni wa kiroho wakati kwamba wanadamu
ni wa kimwili. Waliouzwa kwenye utumwa wa dhambi (Warumi 7:7,14), wakiwa ni
mapepo waliofukuzwa watoke mbele ya machoni pa Mungu. Mwongofu anaifurahia
Sheria ya Mungu kutoka moyoni (Zaburi 119:1 ff.; Warumi 7:22). Wao sio
hawadaiwi au sio watumwa wa mwili, bali wako Rohoni kama Wana wa Mungu (Warumi
8:9-17).
Mwanadamu
aliasi kwa kuzivunja Amri za Kwanza, Pili, Nane na Kumi kwenye Bustani ya Edeni
(Mwanzo 3:17) (pia soma jarida la Fundisho la Dhambi ya Asili
Sehemu ya 1 Bustani ya Edeni (Na. 246) na Fundisho la Dhambi ya Asili Sehemuj ya 2,
Kizazi cha Adamu (Na. 248) [The Doctrine of Original Sin Part 1 The Garden of
Eden (No. 246) and Doctrine of Original Sin Part
2 The Generations of Adam (No. 248)].
Kaini
alitenda dhambi na kuvunja Amri ya Sita na Kumi kwa kumuua ndugu yake Abeli (Mwanzo
4:7-8). Kaini na Abeli wanamwakilisha Kristo na Shetani kwa Watakatifu. Sadaka
ya mifugo ya Abeli ilikubalika zaidi na Mungu, ikiashiria dhabihu ya hiyari
aliyojitoa kwayo Krito zaidi ya maongeo yaliyotolewa na Kaini yaliyotokana na
mazao ya Ardhini. Maana ya sadaka hizi ni ya kiroho (soma jarida la Imani ya Uvijiteriani Kwenye
Biblia (Na. 183) [Vegetarianism and the Bible (No. 183)].
Wanefili
walitenda dhambi ya kuua watu na kufanya machafuko na machukizo kabla ya
Gharika Kuu na Mungu akawahukumu na kuwaangamiza (Mwanzo 6:4-5, 11-13).
Henoko
aliingia rahani mwa Bwana kwa kuwa alikuwa mwenye haki, na huyu anaiwakiliha
imani ya Sabato (Mwanzo 5:22-24) (pia soma jarida la Mashahidi (Na. 135) [The Witnesses
(No. 135)] kwa kujifunza zaidi kuhusu Henoko). Uumbaji
umeendelea kuwa ihara ya Sabato na maadhimisho ya Siku Takatifu zilizoamriwa (Mwanzo
1:1-2:3). Kutokana na majira ya mavuno ndipo mwonekano wa Mpango wa Mungu
unavyoonekana tangu uumbaji.
Hamu
au Kanaani aliivunja Amri ya Tano kwa kumvunjia heshima Nuhu (Mwanzo 9:20-27). Kitabu
cha ufafanuzi cha Wasoncino kinaonyesha kwamba kuna mgawanyiko wa kimaoni kati
ya wenye mamlaka kuhusu kama huyu Hamu au Kanaani alikuwa na makosa ama la au
kama uovu alioufanya ulihusiana na uhamisho au ni kitendo cha upotovu (Soncino:
Rashi, Sforno).
Farao
alitenda dhambi kwa kumchukua Sara afanyenaye uzinifu na kuivunja Amri ya Saba
ingawa hakuwa anajua kama alikuwa anakosea kutokana na udanganyifu wa Ibrahimu,
ambaye pia alitenda dhambi kwa kushuhudia uwongo, na ndipo aliivunja Amri ya
Tisa. Pia aliivunja Amri ya Saba kwa kuwa alimpeleka mke wake akawe mtumwa
ngono, ili akazini naye mfalme (Mwanzo 12:15-20). Uzao wake uliteseka kwa
utumwa huko Misri kwa kipindi cha miaka mia nne (Mwanzo 15:13). Kwa hiyo, kuna
kanuni mbili zinazoonekana kuwepo hapa. Ya
kwanza ni kwamba, hali ya kutozijua Amri za Mungu hakuwezi kuwa sababu ya kutoa
udhuru. Ya pili ni kwamba wateule wanawajibika kutokana na kusamambisha mataifa
wajikwae au kutenda dhambi, kwa kushindwa kwetu kuwaonya ili wayaache maovu yao
(Ezekieli 33:1-6).
Abimeleki
pia alijikuta akivunja Sheria za Mungu kutokana na uwongo alioufanya Abrahamu.
Mara hii Mungu aliingiliakati (kuwaokoa Israeli), kwa kuwa Abimeleki hakuwahi
kumuingilia Sara. Hata hivyo, alionywa kwamba angekufa kwa kuwa alikuwa
anamchukua mke wa mtu mwingine (Mwanzo 20:3-4).
Wote
wawili, yaani Farao na Abimeleki walikuwa wanajua sana kwamba walikuwa
wamezivunja Sheria za Mungu Aliye Juu Sana. Kwa hiyo kitendo cha kuwapa Torati
Israeli pale Sinai kilikuwa ni cha kutilia
mkazo Torati hii (au maadili) ya Mungu, na kutoa maelekezo ya ziada ya
kiutawala katika Israeli, na kuyaelekeza kumuashiria Kristo.
Ibrahim
alisaidiwa na Mungu kwenye vita dhidi ya mataifa yaliyomfuatia ili kuishambulia
miji ya uwandani kwa kuwa walikuwa wamezivunja Amri za Sita na Nane, ingwaje
watendo yalijumuisha miji mingi miji hiyo ya Sodoma na Gomora kwenye maangamizo
makubwa (Mwanzo 14:11-24). Kwa hiyo kwa Mungu hakuna upendeleo wala haangalii sura
ya mtu (Kumbukumbu la Torati 1:17; 16:19; 2Samweli 14:14; 2Nyakati 19:7; Mithali
24:23; 28:21; Warumi 2:11; Waefeso 6:9; Wakolosai 3:25; Yakobo 2:1); (sawa na
jarida la Kupendela Watu (Na. 221) [Respect of Persons (No. 221)].
Ayubu
angetenda dhambi pia kwa kuivunja Amri ya Tatu kama angemlaani Mungu ili afe (Yakobo
1:22; 2:9-10). Yakobo anajulikana kuwa aliishika Torati kabla ya kutolewa kwake
pale Sinai. Kwa hiyo, maana ya dhambi (Ayubu 2:10) pia iliitangulia Sinai.
Esau alishindwa
kumheshimu baba yake kwa kumuuzia Yakobo haki yake ya uzaliwa wa kwanza, ambaye
aliichukua na kuchukua mahala pake pia (Mwanzo 25:31-34), na hivyo aliivunja
Amri ya Tano. Na kwa kuwa amri hii ya Tano ndiyo yenye ahadi, kupoteza kwa haki
ya uzaliwa wa kwanza kulitokea kama adhabu au hukumu yake. Kwa hiyo, Mungu
aliingilia kati ili kuilinda kanuni hii hata kama Yakobo alikuwa ameivunja Amri
ya Kumina kama angeivunja pia Amri ya Tisa.
Musa
alifanyika kuwa ni elohim kwa Farao (Kutoka 4:16; 7:1) kwa kuwa nchi ya Misri
ilikuwa imezivunja Amri za Mungu.
Wale
waliotenda dhambi kwa kuvunja maamrisho ya Torati ni wale waliokuwa hawako
kwenye mwili wa washika Torati. Dhambi ilikuwepo hata kabla ya kutolewa kwa
Torati pale Sinai, na kwamba pasipo Torati dhambi inakuwa imekufa (Warumi 7:8).
Paulo anadokeza kusema kwamba kutojua kunatoa uhuru kwenye maneno yasemayo
kwaba yeye alikuwa huru mbali na Torati lakini amri ilikuja ili dhambi ziweze
kufunuliwa, na akafa (Warumi 7:9). Ni wazi kabisa, kanuni zote za ushikaji wa
sheria za Torati zilikuwepo wakati anaandika andiko hili. Kwa kweli hakuna
kilichotanguliwa katika kipindi hiki. Agano Jipya lilikuwa halijachukua bado
mahala pa Agano la Kale kipindi ambacho Agano hili Jipya lilipokuwa linaandikwa.
Waebrania 8:13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la
kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu
na kutoweka.
Lilikuwa
limekwisha isha nguvu zake tayari au
litatokomea hivi punde. Njia ya
kupaendela Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa
haijakuwepo kabisa.
Waebrania 9:8 Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba
njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza
ilipokuwa ingali ikisimama;
Njia
iliweza tu kuwepo kwa kuangamizwa Helaku mwaka 70 BK, na kutawanyika kwa watu
wa Yuda. Na hii ndiyo maana kamilifu ya Ishara
ya Yona nay a unabii wa ‘juma la sabini la miaka’ lililoandikwa kwenye Danieli
9:25 (soja jarida la Ishara ya Yona na Hoistoria
ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of
the Temple (No. 13)], ambalo
lilihusiana na ukomo wa Agano la Kale na kuanza kwa Agano Jipya. Kwa hiyo,
Agano Jipya lilihusika na sheria ya utoaji dhabihu, ambayo iliweza kukomeshwa
sambamba na tukio kuhusuriwa kwa Hekalu. Agano Jipya lilihusika na ukomeshaji
wa sheria za kutoaji dhabihu za wanyama, na sio kuondolewa au kukomeshwa kwa
Torati yote.
Uhusiano
uliokuwepo ni kwamba Amri Kumi zilikuwa ni sehemu pekee ya muundo mzima wa
Torati ya Mungu, chini ya kichwa cha habari kisemacho sheria au kanuni ya kimaadili ambayo ilikuwepo kabla ya zama za Sinai,
sio sahihi.
Amri
Kumi za Mungu ni mhimili wa Torati kwenye Amri Kuu Mbili za Kwanza na ambazo
zinatokana kwenye Sheria zao zote za Manabii.
Sheria
za vyakula ilikuwepo mapema kabla ya Gharika Kuu. Utofauti uliokuwepo kati ya
wanyama safi na najisi ulifahamika na Nuhu na alielekezwa na Mungu ili
awaingize kwa utaratibu wake elekevu kwenye Safina (Mwanzo 7:2-3). Kwa hiyo, utoaji
wa sheria ya vyakula ulifanywa kutoka kipindi cha uumbaji. Tofauti hii ilikuwepo
na ilionekana tangu kipindi cha Adamu hadi cha Abeli (tazama hapo juu). Madai
ya kwamba sheria hii ya vyakula ilikuwa kwa Wayahudi eke yao yanaonyesha
ukosefu mkubwa wa uelewa juu ya misingi ya kanuni za kitabibu na au za kiafya
na za kimazingira zinazohusiana na mambo ya vyakula na uhusiano wake na uumbaji
au afya za viumbe(sawa na ukisoma jarida la Sheria ya Vyakula (Na. 15) [The
Food Laws (No. 15)).
Sambamba
na hiyo, fundisho la kwamba sheria ya utoaji zaka imefungamanishwa kwenye
sheria za utoaji dhabihu zilizotolewa pale Sinai pia ni ya uwongo. Ibrahimu alitoa
zaka yake kwa Melkizedeki wa Salemu kipindi cha takriban miaka mia nne kabla ya
kutolewa kwa Torati mlimani Sinai (Mwanzo 14:18-20) (sawa na majarida ya Utani wa Zaka (Na161) [Tithing (No. 161)].
Kwa
hiyo kuna mchakato endelevu kuhusu Torati, unaoendela zaidi ya kikomo cha
maandiko haya ya Musa maarufu kama Torati na yanafunika mambo ya muhimu ya maisha
ya kila siku ya Waisraeli nay a dunia. Masihi ataanzisha ufalme wake katika
siku za mwisho, na kwahiyo ataanzisha na kusisitiza tena maadhimisho ya Sabato,
Miandamo ya Mwezi Mpya (Isaya 66:20) na Sikukuu zake alizoziamru (Zekaria
14:16-19; pia tazama Ezekieli 45:1 hadi mwisho, na sura ya 46:1 hadi mwisho). Kwa
hiyo, maandiko ya Mambo ya Walawi 23 yana umuhimu unaoendelea na mataifa
yhatalazimishwa kuishika na kuiheshimu Torati.
Kristo
ni yeye yule; jana, leo na hata milele (Waebrania 13:8), kwa hiyo
hatazipindisha wala kuzibadili Siku Takatifu ambazo atawaambia watu
kuziadhimisha. Ni sawa tu na mataifa wanatakiwa kuziadhimisha Sabato na nchi
itapewa mapumziko kwa ajili ya kushindwa kuzitunza sheria hizi kimatendo.
Kitakachotokea kati ya ushikaji wa Torati na mapatilizo yake yhatgakwenda
kuonekana pia.
Kwa
hiyo kuna mkanganyiko wa wazi kati ya Torati yha Mungu na sheria ile iliyotanguliwa
na Kristo. Hii ilikuwa ni sheria ya utaji dhabihu iliyokuwa kwenye maagizo ya
kidini tu. Sheria za utoaji dhabihu hazikuzihusisha Sabato zile zilizoelekezwa
kwenye Torati. Bali zilielekeza kile kilichokuwa kinafanyika siku za Sabato
kipindi cha kabla ya kuangushwa kwa Hekalu zikiwa kama taswira wa Masihi
anayekuja na mwanzo wa mfumo mpya, ambayo ilikuwa inanenwa tu hapo kabla. Kwa
hiyo, Sabato hazijatanguliwa bado kwa kifo cha Masihi. Sabato zimefanyika kuwa
za muhimu sana kwa kuanzishwa kwa Kanisa, ambalo kwazo zinafasiriwa na kupewa
umuhimu. Itikadi ya kuabudu siku ya Jumapili ilichukuliwa kutoka kwenye imani
za kipagani na dini za kuabudu Jua na wala hazina uhusiano wowote na Ukristo (sawa
na jarida la Chimbuko la Krismas na Easter (Na. 235) [The Origins of Christmas and
Easter (No. 235)].
Kuelewa
mkanganyo uliopo kwenye Torati na kati ya Maandiko ya Musa na sheria za utoaji
wa dhabihu ni ya siku nyingi sana na yanamaana. Wanamatengenezo waliweka wazi
mambo yanayokanganya. Orodha ya matangazo mengi ya ikiri wa imani na tafiti
hizi na yenye nguvu yanaonekana kwenye kanisa la Waadventista wa Sabato kwenye
Kitabu kinachoitwa Maswali Kuhusu Fundisho (Review
and Herald Publishing, 1957, pp. 131ff.). Yana mambo yafuatayo:
Mkutano wa pili
cha Ukiri wa imani wa Helvetic (1566), wa kanisa liinaloitwa Reformed Church of Zurich, na mojawapo ya
alama zenye nguvu za kila Bara (Philip Schaff, The
Creeds of Christendom, Vol. 1, pp. 391, 394, 395), kwenye sura ya 12, “Au
Sheria ya Mungu,” baada ya kuchanganya zile za “kawaida” na zile za “kiibada,
kuhusu sheria za kimaadili, “Tunaamini katika mapenzi yote ya Mungu, na
maelekezo yoyote yanayowezekana, kwa kila eneo la maisha haya, yametolewa kikamilifu
kutoka kwenye sheria hii” (sio ile tunayoweza kuhesabiwa haki kwayo, bali ni
ile tunayoweza kumrudia Kristo kwa imani). Aina na kiwango kinacotakiwa
kukamilisha sheria ya mambo ya ibada vimekomeshwa. “Kivuli kilikoma wakati
mwili ulipokuja,” lakini sheria za kimaadili kijamii hazipaswi kuachwa au
kuondolewa, na mafundisho yote
yanayopinga sheria yanapaswa kulaaniwa (soma
kitabu cha Schaff, Vol. 3, pp. 854-856 (msisitizo umeongezwa)).
Makala Thelathini
na tisa za Dini ya Kanisa la Uingereza (1571). Kifungu
cha VII kinasema kwamba “sheria alizopewa Musa na Mungu” zilikuwa zinahusu
“mambo ya ibada ya madhabahu” hazina kifungo, “hakuna muumini Mkristo awayeyote
aliye huru asiyetakiwa kuzitii amri za Mungu, ambazo zinaitwa za maadili ya
jamii.” (Schaff, vol. 3, pp. 491, 492) [spelingi za zamani zimetumika].
Toleo Jipya la
Kiamerika lenye Vifungu Thelathini na tisa la Kanisa la Kiaskofu la
Kiprotestanti (1801) linajulikana kwa kuendeleza kuamini
hivyo. (Soma kitabu cha Schaff, vol. 3, p. 816.)
Makala ya
Kiyahudi ya Kidinin (1615), inaaminika ilitungwa na Askofu Mkuu Ussher,
baada ya kusema kwamba sheria ya mambo ya ibada imekoma, anasema: “Hakuna mtu
aliyewekwa huru kutoka ushikaji wa Amri ambazo zinaitwa za Kimaadili ya jamii.”
(Soma kitabu cha Schaff, vol. 3, pp. 526,541.)
Azimio
la Ukiri wa Imani la Westminster (1647), baada ya kuonyesha tofauti kati ya sheria za
kiibada na za mahusiano ya kijamii na utanguaji wa maandiko ya zamani nay a
milele kwenye sura ya 19 inatangaza kwamba “sheria ya mahusiano ya jamii
inawahusu watu wete,” na sio kwa kuhesabiwa haki, bali ni kanuni ya maisha, ili
kuutambua uweza utendao kazi wa Kristo. Sheria hii inaendelea kuwa “kanuni
kamilifu ya haki”. Na inaongeza “Wala hakuna mahali kwenye Maandiko ambapo
Kristo amezitangua, bali mara zote amekazia sana sheria hii.” (Soma kitabu cha
Schaff, vol. 3, pp. 640-644.)
Azimio la Savoy la
Makusanyiko wa Makanisa (1658). Hakuna
mabadiliko kama ilivyo kwenye sura ya 19, “Ya Sheria za Mungu,” kutokana na
Azimio la Ukiri la Westminster. (Soma kitabu cha Schaff, vol. 3, p. 718).
Tamko la Ukiri la
Wabaptist 1688 (Philadelfia),
linatuama kwenye lile la London, 1677, ambalo halina mabadiliko na lile la
Westminster kwenye sura ya 19, “La Sheria ya Mungu.” Linashughulika na
mkanganyiko kati ya sheria za kijamii na za kiibada, na kusisitiza kwamba
hakuna Mkristo aliye huru kutoka kwenye sheria hizi za kijamii. (Soma kitabu
cha Schaff, vol. 3, p. 738.)
Makala ya Kidini ya
Wameethodist (1784). Hizi makala ishirini na tano ziliandikwa na John
Wesley kwa Wamethodist wa Marekani, ni za muhimu sana (sawa) na zile Malaka
nyingine Thelathini na tisa za Kanisa la England, na zinatangaza: “Ingawa
Sheria zilitolewa na Mungu na kumpa Musa, kama kanuni zenye mguso za kiibada na
utakaso, hazimlazimishi Mkristo wala kwa mambo ya kijamii yaliyomo ambayo
yanaumuhimu wowote kwenye mafungamano, tena, hata kama hakuna Mkristo kwa
vyovyote vile aliyehuru kutokana na kuzitii Amri hizi zinazoitwa za mahusiano
kwenye jamii.” (Soma jarida la Schaff, vol. 3, pp. 807,808.)
Kwa
kujua maneno haya, Waadventista Wasabato wanaamini kuwa:
Imani hii imehusihwa
na Waadventista Wasababo kwa kuzingatia uhusiano
wao na Vitabu vya Musa au Torati, na tofauti yake kati ya sheria ya kijamii na
maadili na ile ya mambo ya ibada, zinaendelea kuwepo kwa uongozaji wa ukiri wa
imani, makala za ukiri wa imani, na katekisimu ya historia ya Uprotestanti.
Sababu iliyofanya Torati kuwa ilitanguka na kuishia kwenye kifo cha Kristo
inahusiana kwa kiasi kikubwa. Kwa hakika haikufundishwa na mababa waanzilishi
wa Uprotestanti kwa kuwa huo ni mgongano mkubwa na kamilifu wa imani yao (SDA Questions On Doctrine, pp.
131-134).
Ukweli
ambao mtu anaweza kuukubaliana na hawa mababa waanzilishi wa Uprotestani unaweza
kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa sana, kwa kuwa walikuwa wamekosea kabisa kwa
kuwa waliacha kurejea nyuma hadi kipindi cha Augustine wa Hippo kwenye harakati
zao za Matengenezo. Kwa hiyo wanamatengenezo walishindwa kuyarejesha mafundisho
asilia ya Kanisa.
Kosa
la kuanzisha imani sahihi ya kuabudu kwa kufuata Kalenda ya Mungu (sawa na
jarida la Kalenda ya Mungu (Na. 156) [God’s
Calendar (No. 156))], na kisha walishindwa kuanzisha
uhusiano sahihi na Sheria za Mungu na mkanganyiko wa Sheria.
Jambo
moja na kosa walilolifanya lilikuwa ni kushindwa kwao kuyaonysha makosa yaliko
kwenye imani ya Utatu, ambayo ilianzishwa kuanzia kwenye Miitaguso ya Constantinople
(381 BK) na Chalcedon (451 BK). Kwa hiyo matengenezo yalishindwa na kwa hiyo
walizuiwa kuanzisha maadhimisho ya Siku Takatifu kwa mpango wa kimbinguni na
uingiliwaji kati.
Siku
hizi Takatifu na Sabato ziliondolewa kwa makusudi. Hii ni ahadi ambayo Mungu
mwenyewe aliitoa kwa kupitia manabii. Mungu alinena kupitia nabii Amosi na
kuwafananisha Israeli katika Siku za Mwisho na kikapu cha matunda ya majira ya
hari (Amosi 8:1 nk).
Hukumu
kwa ajili ya kushindwa kumtii Mungu ni kwamba hizi Sabato na Sikukuu kugeuka
kuwa maombolezo. Hii inafuatia njaa ya kukosa kulisikia neno la Yahova (Amosi
8:11-14). Kwa ajili ya kutojua ukweli kuhusu asili ya Mungu wa Pekee na wa
Kweli (Yohana 17:3; 1Yohana 5:20), watu wanaadhibiwa (Hosea 8:5-9). Hata
mashetani yanajua kwamba Mungu ni mmoja kwa kutetemeka (Yakobo 2:19). Mambo
makuu kwenye Torati ya Mungu waliandikiwa Israeli kwakuwa waliyachukulia kama
mageni kupitia uvunjifu wao wa Amri ya Kwanza ya Mungu na ueneaji au mlipuko wa
dhambi kwenye ibada (Hosea 8:11-12; soma biblia ya the Interlinear Bible na pia jarida la Torati na Amri ya Kwanza (Na. 253) [Law
and the First Commandment (No. 253)].
Sheria
au umuhimu kati ya maadhimisho ya Sikukuu na utoaji dhabihu iliyoandikwa kwenye
Kumbukumbu la Torati 12:8-14 iliondolewa pamoja na sheria ya utoaji dhabihu siku
za Sabato za juma. Mtu hawezi kuiunganisha Kalenda Takatifu na Sikukuu na sheria
ya utoaji dhabihu pasipo kuyatendea kazi mawazo mengine yote kwa mambo mengine
yote ya Sheria. Muundo wote wa serikali ya Mungu umeondoa taratibu za utoaji
dhabihu, pamoja na maadhimisho ya Siku Takatifu. Pasaka yenyewe ilianzishwa
kabla ya kutolewa kwa Torati mlimani Sinai. Mchakato mzima wa kuwaingiza wateule kwenye imani ya Kikristo
umekuwa amehalifu na utaratibu wa Siku Takatifu tangia hapo hadi kwenye Ufufuo
wa Pili wa Wafu. Haziwezi kutanguka hadi kufikia Siku Iliyokuu ya Mwisho au
Siku ya Mkutano wa Makini. Kila Sikukuu inawakilisha mchakato unaoendelea wa
Mpango wa Mungu ambao bado unafunuliwa. Zinamaanisha kuwa mchakato wa mavuno
bado unaendelea na unafunuliwa (sawasawa na jarida la Sikukuu za Mungu Kama Zinavyohusiana
na Uumbaji (Na. 227) [God’s Feasts as they relate to the Creation (No. 227)].
Torati
ilkuwa ni kivuli cha mambo yajayo (Waebrania 10:1). Kivuli kinaonyesha jambo
lililo la kweli’ hakiwezi kuondolewa au kutenganishwa nacho. Kivuli hiki
kilifungamanishwa kikamilifu na dhabihu (Waebrania 10:1-10), na sio kwenye hizi
Sikukuu. Makanisa ya Kikatoliki na hata ya Kiprotestanti badi yanajua kwamba
Sikukuu za zamani zinatakiwa ziadhimishwe bado hata sasa. Wameichanganya Pasaka
na sikukuu ya kipagani ya Easter na kuanza kuhesabu siku za kuelekea kwenye
Pentekoste kimakosa tangia siku ya Easter, hata hivyo, hawaupingi umuhimu wake.
Kwaajili ya makosa yao ya kiuelewa katika fundisho la Ufalme wa Mungu na kupiga
kwao kuhusu kuwepo kwa kipindi cha utawala wa Millennia na Ufufuo wa Pili wa
wafu, ndipo wanashindwa kuelewa mana ya Sikukuu hizi nyingine.
Mlo
unaoliwa siku ya 14 Nisan, ambao hatimaye ulikujakuwa ni Ushirika wa Meza ya
Bwana, uliunganishwa kwenye maadhimisho ya Pasaka na ililiwa nje ya miji, kama
iliyoagizwa kwenye Kumbukumbu la Torati 16:6-7 (sawa na majarida ya Pasaka (Na. 98); Malumbano ya
Wakotadesiman (Na. 277); Mwezi Mwandamo na Mwaka Mpya (Na. 2131) [The Passover (No. 98); The QuartodecimanDisputes (No. 277); The Moon and the New Year (No. 213)]. Kwa hiyo, kipindi chote cha saa ishirini na nne
cha siku ya 14 Nisan na jioni ya siku ya 15 Nisan, kinafanya jumla ya masaa 36,
yaliyotumiwa kwa watu kuwa nje ya miji yao katika Israeli kwa Sikukuu moja tu.
Mlo wa Meza ya Bwana ulifanyika na kuadhimishwa Kristo. Unaitangulia Pasaka,
ukiadhimishwa usiku wa siku ya 14 Nisan. Dhabihu ya Pasaka ambayo ndiye alikuwa
Kristo mwenyewe, ilifanyika au kutolewa siku ya 14 Nisan, na mlo wa Pasaka
uliliwa siku ya 15. Jioni zote mbili zinapaswa kuadhimishwa, na ifanywe hivyo
nje ya matuo na miji yetu. Kwa hiyo, adhimisho la Meza ya Bwana linatakiwa
lifanyike mara moja tu kwa mwaka na likifungamanishwa na maadhimisho ya Pasaka
na Mikate Isiyo na Chachu.
Biblia
inatufundisha kwamba makwazo au unajisi kwenye Sikukuu yanasababishwa na wale
walio kwenye Ushirika lakini wanaojitoa wenyewe kwa minajiri ya kufuata faida
zinazotokana na makosa ya Balaam, kuangamia kwenye uasi wa Kora (Yuda 11-12). Kwa
maneno mengine, wanafundisha kwa minajiri ya mashahara au watumishi wa mshahara
na hawaoni shida kuzitia unajisi au kuzigeuza Sikukuu na kuielewa Torati na
Ushuhuda. Hakuna nuru ndani yao (Isaya
8:20, KJV) au hakuna mapambazuko (RSV) kwao. Wamekufa mara mbili na wameng’olewa.
Watu hawa hawana au hawaenendi kwa Roho na wanasababisha matengano katika Siku
za Mwisho (Yuda 19). Uasi wa Kora ni mchakato unaoendelea dhidi ya neno la
Mungu (sawa na jarida la Wanikolai (Na.v202) [The
Nicolaitans (No. 202)].
Kristo
anaweza kuwalinda wateule wasianguke na kuwawakilisha mbele za Mungu Mwokozi (Yuda
24-25; pia soma Marshall’s
Interlinear, RSV). Hata hivyo, mgawanyiko kwenye Mwli wa Kristo umeruhusiwa
uweze kuwadhihirisha wanaoishika kweli na waliokubalika na Mungu (1Wakorintho
11:19). Malumbano yasemayo kwamba aya ya Wagalatia 3:10 imeliondolea neno Sikukuu
yanaonyesha kutoijua asili ya kipindi cha nyuma ya Sabato. Marejesho ya Sikukuu
kwa adhabu ya kukosa chakula ni ya lazima na nyongeza ya mwanzoni mwa kipindi
cha Milenia (Zekaria 14:16-19). Kristo habadili nia yake kwa kuwa anapenda
ziadhimishwe.
Makanisa
ya Mungu, linajumuisha Kanisa la Kristo na lile la Mitume (Mathayo 26:17-20; Luka
2:41,42; 22:15; Yohana 2:13,23; 5:1; 7:10; 10:22; Matendo 18:21(KJV); 19:21;
20:6,16; 24:11,17), yame zishika Sikukuu hizi kwa kipindi cha zaidi ya miaka
elfu mbili ukiliondoa Kanisa moja kutoka karne ya kumi na tisa. masalio ya
Makanisa ya Mungu Yayayozishika Sabato huko Ulaya na ambayo yameshindwa
kuzishika Amri za Mungu au yaliyoangukia kwenye ukengeufu ndiyo hatimaye
yalipoteza ushikaji wa Sikukuu hizi (soma majarida ya Kazi ya Amri ya Nne Kwenye
Historia ya Makanisa ya Mungu Yanayozishika Sabato (Na. 170, Torati ya Mungu
(Na. L1) [The Role of the Fourth Commandment
in the Historical Sabbath-keeping Churches of God (No.
170), The Law Of God (No. L1)] na Mlolongo wa majarida yanayohusu Torati (Namba zote 252-263)).
Ni sawa kama Kristo na
Mitume wake wengine wote na Wazee
Waangalizi, Paulo pia alizishika Sikukuu hizi, kama tunavyoona kwenye
Matendo ya Mitume. Kwa hiyo, kwa kweli hakudiriki kuzipotosha wala luzikomesha.
Hekalu lilichaguliwa kuwa ni dhabihu (2Nyakati 7:12), baada ya Maskani
ziliyokuweko huko Hebron na Shilo. Hata hivyo, maadhimisho ya Sikukuu
hayakufungamanishwa na huduma za Hekaluni. Bwana aliuchagua mji wa Sayuni kuwa
ni mahala pa kuweka miguu yake (Zaburi 132:13-14), lakini uchaguzi ule
uliahirishwa kwa Kanisa kutangatanga jangwani hadi kurudi kwa Masihi. Kitendo hiki
kilipimwa kwa kulinganishwa na kipindi cha miaka arobaini waliyokuwa chini ya
nguzo ya moto na mawingi jangwani (sawa na jarida la Hesabu ya
Nyakati za Zama (Na. 272) [Outline Timetable of the Age (No. 272)]. Ile ilikuwa ni ishara mahsusi ambayo Kristo aliweza
kuionyesha kiini cha ibada kupitia wateule.
Chini ya Kanisa la
Mitume, Kanisa lilishika Sikukuu kwa maeneo mbalimbali, ingawaje Mtume Paulo
alitaka arudi mjini Yerusalemu kwenda kuadhimisha Sikukuu kama ilivyoonyeshwa
kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume 18:21; 19:21 (soma tafsiri za KJV; The Interlinear Bible). Matendo
20:6 inaonyesha kwamba Paulo alizishika siku za Mikate Isiyo na Chachu akiwa
Filipi akiwa amekawia kawia. Hatimaye alipenda awepo Yerusalemu siku ya
Pentekoste (Matendo 20:16). Imani zote mbili, yaani Wayahudi na Wakristo
walizishika Sikukuu kwenye nchi za utawanyiko walikokwenda. Sikukuu
zilitangulia zama za Hekalu na ziliendelea hata baada ya kubomoshwa kwake. Ni dhabihu
za wanyama tu ndizo zilitakiwa kutolewa Hekaluni. Hata hivyo, dhabihu
zilionekana zikitolewa hahali penginepopote vipindi vyote viwili, yaani wakati
Hekalu likiwepo na hata baada ya kubomolewa kwake kipindi chaa utumwa wa Babeli.
Hekalu huko Elephantine liliaminika kufanya shughuli zake za utoaji dhabihu
hadi kipindi cha ujenzi mpya wa Hekalu siku za utawala wa Dario II. Hatimaye
Hekalu la Elephantine lilibomolrwa kwa kushambuliwa (soma kitabu cha Pritchard, The Ancient Near East, vol. I,
pp. 278-282). Maandiko ya Kiaramu kwenye tafsiri ya Pritchard, ya Ginsberg, inaonyesha
rekodi za maelekezo ya maadhimisho ya Pasaka kwenye dola iliyotajwa na nabii
Ezra (soma jarida la Ishara ya Yona, Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13)
[The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)].
Michango kwa ajili ya
majenzi mapya ya Hekalu imetajwa, sambamba na mazingira ya uharibifu wa Hekalu
huko Elephantine katika mwaka wa 14 wa Dario II. Maliwali wa yuda
pia alikuwa na sera ya kuwadhibiti makuhani huko Elephantine. Andiko linaonyesha
kwamba dhabihu hazikukoma kamwe kipindi cha kuangamizwa kwake Yerusalemu, na
Hekalu lilijengwa upya huko Yerusalemu wakati wa ujengaji mpya wa Hekalu huko.
Dhabihu zilikoma kwa Agano Jipya na kwa maangamivu ya mwisho ya Hekalu huko
Yerusalemu, lakini Sikukuu ziliendelea huko walikotawanyikia. Kanisa limeshika
Sikukuu huku likiwa linapitia kipindi cha mateso kwa kipindci cha miaka elfu
mbili.
Hekalu linguine
lilijengwa pia huko Misri mahali panapoitwa Leontopolis, kwenye Nome ya
Heliopolis, na Kuhani Mkuu Onias IV. Hekalu hili lilitabiriwa na Mungu kupitia
nabii Isaya (Isaya 19:19). Lilifungwa kwa amri ya Vespasian mwaka 71 BK, baada
ya kubomolewa kwa Hekalu la Yerusalemu, ingawaje liliendelea kutoalewa dhabihu
tangu kujengwa kwake mwaka 160 KK.
Wateule watahukumiwa
kwa kumjua kwao Mungu wa Pekee na wa Kweli. Kutokana na kumjua Mungu, ujuzi wa
kuzijua Sheria unaendelea na unaingia akilini na mioyoni mwa kila mtu. Jambo
hapa sio Sabato, au Sikukuu, au Torati, bali ni kuhusu ukweli kwamba Mungu Baba
ni Mungu Mmoja na wa Pekee na wa Kweli (Yohana 17:3; 1Yohana 5:20), na kamba ni
yeye peke yake ndiye asiyepatwa na madhara wala kufa (1Timotheo 6:16). Kama hatutaishikilia
imani hii basi tutaondolewa kati ya wateule na tunaweza pia kupewa nguvu za
upotevu ili tuuamini uwongo (2Wathesalonike 2:11). Marshall’s Interlinear inaitafsiri ayah ii kama mkakati wa
makosa unaokusudia kuwafanya
wauamini uwongo. Hawawezi kujisaidia wenyewe tena. Ni kwamba
wameondolewa kutoka kwa wateule na uelewa wao umeondolewa pia. Hawawezi kuelewa
ijapo kuwa walipenda kuyajua makosa.
Uelewa wote wa wateule
umetegemea na uhusiano wao na Mungu wa Pekee na wa Kweli na kumjua kwao Mwana
wake Yesu Kristo (Yohana 17:3; 1Yohana 5:20). Uvunjaji wa Amri ya Kwanza ndio
unaowafanya wafikiri kuwa Sikukuu zimeondolewa. Hawawezi kuzishika hata kama
wale walio kwenye makosa wanapenda kuzishika. Mungu ataingilia kati kukatiza juhudi
zo. Kwa wale wanaozishika Sheria au Torati, Sikukuu ni mkumbushiaji wa muhimu
wa Mpango wa Mungu. Zaidi ya yote, marejesho ya lazima ya kipindi cha utawala
wake yanaonyesha kwamba Sikukuu ni za lazima na kwa kweli ni Baraka kwa wafuasi.
Kitendi cha kuziondoa
Amri hizi Kumi kutoka kwenye mambo muhimu ya Torati na mkanganyiko wao wa sheria za kimmandiko, kunatokana kiwango
chao kikubwa cha kutojua mafundisho ya Kristo nay a Mitumem jambo ambalo hata
wanamatengenezo wa Kiprotestant waliangukia kwenye makosa. Ni matokeo ya udhaifu
wa kiroho, makosa kushindwa kwa Kanisa la Siku za Mwisho. Udhaifu huu
imeonekana kwenye ahadi za Makanisa yaliyo kwenye Ufunuo sura za 2 na 3, ambapo
Kanisa la Wasardi liliambiwa limekufa na Kanisa la Walaodikia liliambiwa
litatapikiwa mbali. Hakuna hata mtu mmoja kwenye Makanisa haya atakayeuingia
Ufalme wa Mungu. Bali ni wachache kati yao ndio watakuwepo kwenye Ufufuo wa
Kwanza wa Wafu.
Uzao wa mwanamke,
ambao ni Kanisa, ni wale wote wanaizishika Amri za Mungu na Ushuhuda au Imani
ya Yesu Kristo (Ufunuo 12:17; 14:12). Soma jarida la Upendo na
Kanuni za Sheria (Na. 200) [Love and the Structure of the Law (No.200)].
q