Makanisa ya Kikristo ya Mungu

[100]

 

 

 

Maana ya Mkate na Divai [100]

 

(Toleo 2.1 19950408-19990214)

 

Jarida hili linahusuka na kuelezea Mfano wa sadaka ya mwili na damu na ashirio lake vinavyo husiana na asili masuala mazima ya imani yetu.

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Copyright © 1995, 1996, 1999 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

 

Masomo haya pia ynapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:
http://www.logon.org and http://www.ccg.org

 

 


Maana ya Mkate na Divai [100]

 


Umuhimu wa mkate na divai ni ya lazima katika kutimiliza adhimisho la Ushirika wa Meza ya Bwana. Sisi sito tungekuwa na uelewa mkubwa sana kuhusu maana ya mfano wake. Kuohsna miguu ni kitu cha lazima katika kukamilisha ushiriki wa Ushirika wa. Meza ya Bwana na kama ni kitu cha muhimu kwa kushiriki mkate na divai (tazama jarida la maana ya ishara ya Kuosha miguu, [099]. Mkate na divai vinatakiwa vishughulikiwe kwa pamoja na mambo kadhaa. Ni kwa umbali kiasi gani uelewa wa kina unahitajika kwa ajili ya kuhusisha mkate na divai kunaweza kuchukulikana katika maeneo mengi makuu katika Biblia. Mengi yake yanaashiria na mwili wa Kristo. Kwa mfano, tendo la kulisha makutano wengi kwa mikate na samaki. Muujiza huu unahusisha uelewa wa kujua ni nini maana ya mwili wa Kristo ulibidi uvunjwe vipande vipande. Mojawapo ya vifungu vinavyohitajika kuvitazama na kuvielewa ni cha Injili ya Yohana 6:17-22. Sura yote ya 6 inamambo yanayoshabihiana katika mayendo yote yanayohusiana ndani yake. Kuelewa sura ile kungeweza kutupa sisi maana yake ambayo kwayo tunaweza kuelewa juu ya mkate na divai.

 

Yohana 6:1-4 inasema: Baada ya hayo Yesu alikwenda zake ng’ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya Tibaria. 2 Na  mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa. 3 Naye Yesu akakwea mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. 4 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu.

 

Mtume Yohana anaturudisha kwenye sikukuu nzima ya Pasaka ya Wayahudi (Yoh. 2:13). Hapa, anasema, na Pasaka, sikukuu ya Wahahudi. Yohana anatia kibwagizo ndani kama njia ya kutolea maelekezo ya ki maandiko. Hakuwa na maana ya kwamba ilikuwa ni mlo wa Wayahudi. Ana maana ya kuwa Pasaka ni sikukuu ya Wayahudi, na hii ilikuwa ndio fafanuzi wa vifungu mbali mbali vya maandiko matakatifu.

 

Yohana 6:5 inasema: Basi Yesu alipoinua macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, akamwambia Filipo, Tununue wapi mikate ili hawa wapate kula?

 

Kristo alikuwa ameendeleza kufuatilia kwa sababu alikuwa anafanya mambo kwa ajili ya watu. Alikuwa anafanya miujiza. Iwapo kama tungeenda nje huko duniani leo, na kutoa kwa watu dawa za bure na kuponya watu, na tungewapa watu ushuhuda wa mambo ya kimiujiza, basi wangetufuata. Hii haina maana kuwa ni kuwa kuna watu wengi sana mfano ni kule India ambao wanafanya miujiza mikubwa na kuwafanya watu wawaandamie wao; kuwa wao ni watu wa Kristo au kuwa wana Mungu kwa namna yoyote ile. Utendaji wa miujiza hauna maana ya kuwepo kwa mahusiano ya moja kwa moja na Mungu au na Yesu Kristo. Kristo alifanya miujiza iwe kama ishara kwa wateule. Vile vile alimwuliza Filipo swali la kumjaribu.

 

Yohana 6:6-12 inasema: Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. 7 Filipo akamjibu, Mikate na dinari mia mbili haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu. 8 Wanafunzi wake mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia, 9 Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa? 10 Yeau akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale malikuwa na majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao. 11 Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. 12 Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee cho chote.

 

Kuna mfano wa kiroho katika kifungu hiki chote cha maandiko. Alisema sitaki kitu chochote kipotee, na anawalisha watu 5,000. Idadi hii yote ina maana Fulani. Hakuna kinachotakiwa kipotee, kwa sababu mkate, kama tutakavyoona huko mbele baadae, inaambatanishwa na vipande, kama sehemu ya mwili wa Yesu Kristo, na vimetolewa kwa Kristo na. Mungu. Kristo anawaambia wanafunzi wake hapa, hamtakiwi kumpoteza hata mmoja wapo wa watu hawa, na wala kimoja kati ya vipande hivi. Yale ndio maelekezo kuhusu huduma. Kila mmoja aliye na mtu fulani ambaye anaondoka na kuliaha kanisa, anatakiwa ajitahidi kwa uwezo wake wote ili mrudisha mtu huyo na kutafuta roho zilizopotea. Wanatakiwa wajihoji kuhusu kama kwa namana gani au sababu gani zilizo pelekea wawapoteze watu hao, au kuona kama wameshindwa kuleta ushuhuda mzuri kuhusu maisha yao katika Yesu Kristo jambo ambalo ni tatizo kubwa sana. Alisema kuwa hakuna kinachotakiwa kipotee.

 

Yohana 6:13 inasema: Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula.

 

Idadi ya makanda yaliyobakia yana maana yake. Makanda thenashara ya mkate yaliyosalia ina wakilisha utimilifu wa mataifa theneshara, wanamotokea wale 144,000. Hakuna kinachopotea kwenye hayo makanda. Kila kitu kinakwenda kwa mahali pa makabila, chini ya miyume thenashara.

 

Yohana 6:14 inasema: Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.

 

Hapa Kristo anatoa ushuhuda wa kinabii kwa kufanya mujiza.

 

Yohana 6:15 inasema: Kisha Yesu, hali akijua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.

 

Mara tu walipojua kuwa walikuwa na nabii, walikuwa na Masihi, ambaye ni nabii aliyetabiriwa kuwa angekuja siku za mwisho, walitaka hatimaye wamfanye ashikilie mfumo wa maongozi, ya utawala wa kidunia. Hatahivyo, hilo halikuwa ni lengo la sababu ya kuja kwake. Yeye atakuja kuchukua hatamu ya maongozi, lakini kwa muda ule ilikuwa bado muda haujatifika. Hivyo basi alipaswa aende peke yake, kwasababu wanafunzi wake wenyewe pia hawakuwa wamemuelewa.

 

Yohana 6:16-21 inasema: Hata ilipokuwa jioni wanafunzi wake wakatelemka baharini 17 wakapanda chomboni, wakaanza kuivuka bahari kwenda Kapernaumu. Nako kumekwisha kuwa giza, wala Yesu hajawafikia. 18 Na bahari ikaanza kuchafuka kwa kuvuma upepo mkuu. 19 Basi wakavuta makasia kadiri ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na kukikaribia chombo; wakaogopa. 20 Naye akawaambia, Ni mimi msiogope. 21 Basi wakataka kumpokea chomboni; na mara hiyo chombo kikafikilia nchi waliyokuwa wakiiendea.

 

Sehemu hii ya maandiko matakatifu ni ya muhimu sana. Hapa tuna aina ya mafundisho ya jinsi ya tafsiri za kiroho. Alikuja kwao kwa ajili ya mateso. Akawaambia wasiogope. Walimpokea mashuani. Ilikuwa ni hali ile ile kuwapata kanisa la Walaodikia wakati Ktisto akiwa mlangoni anabisha hodi. Alikuja kwao wakati wa dhiki, na kwa makusudi kabisa walimpokea mashuani, na maramoja kwa ghafla walijikuta mashua imeshafika upande na mahali walipokusudia kwenda. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba ule ulikuwa ni muujiza. Neno kuu hapa ni ghafla au mara moja. Lilikuwepo. Ktisto alikuja na kuingia ndani yake na kwa ghafula wakajikuta wakiwa pale walipokuwa wakienda. Kulikuwa na tatizo baharini. Lakini kwa ghafla matamoja, ikawa imeondoka yote, na kukawepo na kipindi kizuri cha faraja, na ghafla mara moja wakawa wamefika pahala wakipokuwa wana kusudia kwenda. Sasa ule ulikuwa ni muujiza ambao hauwezi kufananishwa na matukio mengine ya hadithi za kidunia zilizo wahi kuandikwa. Hii sio jambo lililo chukuliwa kuwa ni muujiza wa jumla. Hata hivyo, ni muujiza, na inauhusino na tendo la kumpokea Kristo moyoni mwako, ili ayachukue matatizo yote uliyo nayo. Sisi sote tumeitwa Kanisani tukiwa na hali mbaya sana ya kukata tamaa. Sote tumekubalika katika Ufalme wa Mungu. Wakati mwingi unapokuwa emeitwa, unakuwa katika awamu ngumu ya kujifikiria binafsi katika maisha yako. Kinachotokea ni kwamba, Mungu anakuleta kwenye toba kwa kupitia hayo hayo mateso. Kuanzia wakati ule mdiposa unaletwa kwenye Ufalme wa Mungu, na kumpokea Kristo katika maisha yako. Hii hutokea mara chache zaidi kuliko inavyotokea kwa kawaida, katika mazingira ya ziada visivyo kawaida sana. Kwa njia ya vitendo kabisa, Kristo anatembea juu ya maji ili akupate wewe, kwa kutipia magumu yawayo yote. Ndiposa wewe umepewa Roho Mtakatifu. Umepewa wokovu kama utapenda, na kwa mara moja, uko pahala ambapo umewekewa uende. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa, umepewa uwezo wa kuwa na sehemu katika Ufalme wa Mungu, mara moja pale unapompokea Kristo.

 

Yohana 6:22-24 inasema: Siku ya pili yake makutano waliosimama ng’ombo ya bahari waliona ya kuwa hakuna mashua nyingine huko ila moja, tena ya kuwa Yesu hakuingia katika mashua ile pamoja na wanafunzi wake, bali wanafunzi wake walikwenda peke yao. 23 (walakini zikaja mashua nyingine kutoka Tiberia mpaka karibu na mahali pale walipokula mikate, wakati Bwana aliposhukuru). 24 Basi mkutano, walipoona ya kuwa Yesu hayuko huko wala wanafunzi wake, waliingia mashuani wenyewe, wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu.

 

Aya hizi zinawahusu wateule, na tendo la Kristo la kuuvua mwili wake mbali naye, lakini wengi wanamwona Kristo pamoja na mwili. Kuna similizi katika Yohana 6, zinazoonyesha kuwa hazifungamani, lakini hazipo hivyo. Bali zimewekwa pamoja kwa madhumuni maalumu.

 

Yohana 6:25-26 inasema: Hata walipomwona ng’ambo ya bahari, walimwambia, Rabi wewe umekuja lini hapa? 26 Yesu akawajibu, akasema, amin, amin, nawaambia, ninyi mwanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.

 

Kristo anasema: Ninyi mwanifuata mimi kwa sababu ya Injili ya uponyaji/au utajirisho. Sasa mmeishashiba na kujaza matumboni mwenu. Ni kwakiasi gani mambo kama haya kuwa ndivyo yanavyotendeka katika Kanisa kwa siku za leo. Kama upo chini ya mshitaki, je, unamfuata Kristo ukiwa chini ya mshitaki au adui wako? Kwa hivyo basi kutakuwa na maana gani tunaposema juu ya mateso basi.

 

Yohana 6:27 inasema: Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.

 

Ukweli ni kwamba Kristo alitiwa muhuri na Mungu Baba. Mtu aweza kuuliza, je, kutiwa muhuri kuna maana gani? Biblia ya Kiingereza iitwayo Companion Bible inasema kuwa Wayahudi walijadili kuhusu muhuri wa Mungu. Kwa mfano Nini ni muhuri wa Mungu Mtakatifu Mbarikiwa?Rabi mmoja aitwae Bibai akasema Jibu ni Kweli, lakini Kweli ninini?Rabi mwingine aliyeitwa Boni akasema jibu ni Mungu aishiye na Mfalme wa Milele. Rabi mwingine aitwae Chanina akasema,…kweli ni muhuri wa Mungu. (yamo kwenye jarida liitwalo Lightfoot Babylonian Talmud, Sanhedr., Pitman and., v. 12, p.29). Ambayo inatuonyesha kuwa Fundisho la kinachoitwa Utatu Mtakatifu ni la makosa kabisa. Maandiko hayo yanatuonyesha kuwa Kristo alitiwa muhuri na Mungu Baba. Tendo la kutiwa muhuri lilieleweka na waalimu wa Sheria za Torati wa wakati ule walioitwa Marabi. Muhuri ulimaanisha kweli, na Roho Mtakatifu ni Roho wa kweli. Kristo alitiwa muhusi na Roho Mtakatifu, na kwa njia ya muhuri ule alitengwa mbali kwa wakfu. Kwa hiyo basi alishuhudiwa na Mungu Baba kuwa ni Masihi. Na sisi vile vile tumetiwa muhuhri kwa namna moja hiyo hiyo.

 

Yohana 6:28-33 inasema: Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzifanya kazi za Mungu? 29 Yesu akajibu, akawaambia,Hii ndiyo kazi ya Mungu, mwaminini yeye aliyetumwa na yeye. 30 Wakamwambia, Unafanya ishara gani basi ili tuione tukakuamini? Unatenda kazi gani? 31 Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. 32 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni. 33 Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.

 

Kwa muhtasari twaweza kusema kuwa: walikuwa wanatafuta ishara. Walisema. Unafanya ishara gani basi ili tuione.Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. Kristo alikuwa ameisha wapa chakula. Alikuwa amewalisha na mikate na samaki nao walijua hili. Walikuwa wanamwambia, Baba zetu walipewa mana, je, ndicho kitu unachofanya?  Walikuwa wanalichukulia lile tendo la Yesu kuwatendea miujiza, kama kuelekezea kwenye wazo la uwezekano wa yeye kuwalisha Israeli. Hivi ndivyo ile mikate mitano na wale samaki wawili walivyofanyiwa. Badala yake kisha walisema, je, sio kwambna unakwenda kututoa Misri, unakwenda kutukomboa. Kwa maana nyingine ni kusema: je, wewe ndiye Masihi? Hivyo ndivyo wanavyomwambia. Naye akajibu akawaambia: Amin, amin, nawaambieni, siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni,Bali anasema:Ule sio mkate ushukao toka mbinguni. Anasema kwa hakika kabisa kuwa: Musa aliwachukua ninyi mtoke kutoka Misri, nanyi mlipewa mana, lakini ule sio mkate unaoshuka toka mbinguni. Sipo hapa kwa ajili ya kuwakomboa ninyi kutoka mikono ya Warumi. Hili ndilo wazo yakinifu kwa hili swali lemye maana na la kijanja lililoulizwa na makutano: je, unataka kutukomboa sisi na mikono ya Warumi kama Musa alivyofanya kwa Misri?. Yeye kwa mkazo kabisa aliwajibu hapana!

 

Yohana 6:34-37 inasema: Basi wakamwambia, Bwana, siku zote utupe chakula hiki. 35 Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa; naye aniaminiye hataona kiu kamwe. 36 tLakini naliwaambia ya kwamba mmeniona wala hamwamini. 37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.

 

Hapa tunarudi tena kwa yale makanda kumi na miwili na kwa maelekezo yake. Kusanyeni yote, hakuna hata mmoja utakao potea, na wakatia yote na kuitia kwenye makanda na jumla yake ilikuwa makanda thenashara, kwa sababu walikuwa kwenye jumla ya makabila thenashara. Kilamtu-miongoni mwa Mataifa wasio Waisraeli watakuwa kwenye makabila kumi na mawili ya Israeli. Hakuna atakayepotea, na hii inathibitishwa na ile aya ya 37. Wote wametolewa kwa Kristo na Mungu Baba kwa kusema: Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa kamwe. Hakuna aliyetolewa kwa Kristo, atakaye tupiliwa mbali naye.

 

Yohana 6:38 inasema:Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.

 

Katika aya ya 27, tunaona Kristo akitiwa muhuri na Mungu Baba kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ni Roho wa Kweli. Kristo ametiwa mhuri na. Mungu. Mafundisho ya Utatu yanapingana na ufahamu huu mzima wa kuwa sehemu ya kuwa mwili wa Kristo. Yanapingana na ufahamu huu wa kuwa ni sehemu ya Kristo na kutiwa muhuri na Kristo katika mfumo na utaratibu wa Mungu. Kutoka katika hatua hii tunapata kujua kusudi la Mungu likishirikishwa kwa Kristo naye akikubaliana na kutii chini ya muhuri hii.

 

Yohana 6:39 inasema: Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho.

 

Haya ndiyo maana ya kuinua juu yale makanda, ambapo tumeona vipande vya mikate mitano na samaki wawili.

 

Yohana 6:40 inasema: Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana wa na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

 

Lakini katika Injili ya Yohana 17:3 inasema kuwa uzima wa milele haupo kwa kumwamini Yesu tu. Haijalishi wala kutosha tu kuita Bwana, Bwana, kwa kuwa si kila mtu amwitaye Bwana, Bwana ndiye atakayeuingia Ufalme wa Mungu, lakini ni kwa yule tu ayafanyaye mapenzi Baba. Kristo ameweka wazi kabisa katika (Mat. 7:21). Sio tu ni kule kumwamini Kristo, hii humtia mtu katika uzima wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli na, Yesu Kristo uliyemtuma. Huu ndio uzima wa milele, unahitaji umfahamu Mungu wa pekee na wa kweli, na unahitajika kumjua Kristo, ambaye alimtuma na kumtia muhuri (kwa mujibu wa Yohana 6:27). Unahitajika kuwajua hao ili uweze kuupata uzima wa milele. Ndivyo asemavyo Kisto ktika Yohana 6 kuwa wote, wamwonao Mwana na ku wamini, waweze kuwa na uzima wa milele na waeze kufufuliwa siku ya mwisho, wanakubalika kwa sifa ya kumwamini Mungu wa pekee wa kweli (Yoh. 17:3).

 

Yohana 6:41-44 inasema: Basi Wayahudi wakamnung’unikia, kwa sababu alisema, mimi ni chakula kilichoshuka kutoka mbinguni. 42 Wakasema, je! Huyu sio Yesu, mwana wa Yusufu, ambaye twamjua babaye na mamye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni? 43 Basi Yesu, akajibu, akawaambia, Msinung’unike ninyi kwa ninyi. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.

 

Huwezi kuwa tu ni mshiriki wa mkate na mwili wa Yesu Kristo hadi pale utakaletwa au kukuchaguliwa tangu asili kuwa katika mahali pale na Baba na kutolewa kwa Yesu Kristo. Ndiyo maana makutano makubwa yaliwafuata na kuja kwenye mashua walikokuwa. Waliacha shughuli na vyeo vyao kwa sababu sio kila mtu anaweza kuwa na Kristo. Hii ndiyo maana ya utenganisho wao. Dhana ya kuwa watu wanachaguliwa iliendelezwa na mtume Paulo kupitia Waraka wake kwa Warumi 8:29-32, anaposema kuwa tulijulikana tangu mwanzo.

 

Warumi 8:29-32 inasema: Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30 Na wale aliowachagua tangu asili, na hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza. 31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? 32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja nanye?

 

Mungu ameishaamua na kumfahamu yule atakayekuwemo katika ule Ufalme. Kwa hiyo Mungu anakualika, na anakutoa kwa Yesu Kristo. Kwa hiyo wewe umehesabiwa haki na kutukuzwa katika Kristo. Kila mtu huletwa kwa Kristo na Baba, na huwezi kuja kwa Kristo, wala huwezi kuufikia utimilifu wa uelewa pasipo Baba kukuita. Kwa hiyo ina maana kuwa ni Baba anayekuleta. Kuna watu wanaosikia na kupenda kusafiri na mashua ile ile. Kuna watu wanaosikia na wanaoitwa, lakini hawajachaguliwa. Wanausikia ujumbe, na wanauelewa na kuingia akilini maneno yake ndani yao, na wana sema nahitaji baadhi yake, nataka kuwa pale, lakini wamepewa mambo mengi ya shughuli za hapa duniani, ambao maisha yao huenda yatakuja kuokolewa katika siku za mwisho. Hii ni kwa sababu hawajastahili kuingia hukumuni sasa. Mwandamano huu wa matukio unaletwa na Yohana 6. Pale unaona miujiza ya kulishwa kwa watu 5,000, na muujiza wa utaratibu, na mashua. Kwa kipindi kile – usafirishaji – na uokozi, yote ni sehemu ya mafuatano ya matukio yaliyotolewa na Kristo – yataokoa, na kuwafufua katika siku za mwisho.

 

Yohana 6:45 inasema: Imeandikwa katika manabii; Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu.

 

Hapa ananukuu katika Isaya 54:13 na Yeremia 31:34.

 

Yohana 6:46 inasema: Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba.

 

Watu waliomuona Baba ni warohoni. Wanadamu si Mungu. Wanaitwa kuwa washiriki na Mungu kwa siku za mbeleni, nao watamuona Mungu hatimaye. Hakuna mtu aliyemuona Mungu (Yoh. 1:18). Hakuna aliyeweza kumuona Yeye, Mungu kamwe (1Tim. 6:16). Yeye pekeyake ndiye asiyekufa maishani.

 

Yohana 6:47 inasema: Amin, Amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele.

 

Kwa hiyo basi, kama unamwamini Kristo, basi utapata uzima wa milele na Mungu, na 1Timotheo 6:16 inasema kuwa ni Mungu tu ndio asiyeweza kupatwa na madhara ya kifo. Mungu ameshirikisha uzima wa milele na Kristo, kwa Jeshi la kimalaika, na kwetu.

 

Yohana 6:48-51 inasema: Mimi ndimi chakula cha uzima. 49 Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa. 50 Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife. 51 Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.

 

Kwa hiyo, Kristo anasema mwili wake ndio ule mkate, na tunapaswa kuula ule mwili wake ili tuweze kufanyika kuwa mwili wa Kristo. Mwili wake hufanyika kuwa mwili. Tunatakiwa kuula mwili wake kwa namna ya roho, ili tufanyike mwili wake. Ni mwandamano wa mambo.

 

Yohana 6:52 inasema: Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje kutupa sisi mwili wake ili tuule?

 

Unaweza kufikiriri kuhusu mawazo haya, kwa ajili ya sheria za vyakula. Wayahudi walifikiri hili katika mtazamo wa kimwili. Walipunguza kabisa umuhimu wa sheria kwa mtazamo wa kimwili.

 

Yohana 6:53-54 inasema: Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kunywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho

 

Tuna orodha ya mambo ya muhimu kwa ajili ya uzima wa milele. Wewe hatimaye unao ufahamu kuhusu Mungu wa pekee na wakweli, na mwana wake Yesu Kristo. La pili ni kwamba, unatakiwa umwamini Kristo ambaye amempa. Sasa una jambo la tatu kulijua na kulifanya, ambalo ni kushiriki ushirika wa sakramenti, kama ukipenda, kama Wakatiliki wanavyoita. Unatakiwa kushiriki wakati wa Pasaka, damu na mwili wa Yesu Kristo wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa hiyo tunaona kuwa kuna mambo matatu, ambayo ni ya muhimu kuyafanya kwa ajili ya kuupata uzima wa milele. Kama hushiriki Pasaka, na kuula mwili na damu ya Kristo wakati wa ,aandalizi ya mlo wa Pasaka au kwa jina jingine Chigigah, hutaweza kuurithi uzima wa milele. Hili ni jambo lililo la kweli na dhahiri kabisa:Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nimfufua siku ya mwisho. Kuna sifa muhimu tatu kwa ajili ya mtu aweze kufufuliwa katika siku ya mwisho.

 

Yohana 6:55-56 inasema: Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake

 

Kuna fafanuzi nzuri sana katika aya ya 53 katika Biblia ya Kiingereza iitwayo Companion Bible kuelezea kuhusu kula na kunywa. Waebrania walitumia kuelezea rejea za maarifa (katika lugha ya kimfano, kama somo), kama ilivyo kwenye kitabu cha Kutoka 24:11. Inawekwa kwa kuwa hai. Kwahiyo kula na kunywa ilikuwa ni inachukuliwa kama ni dhana itendayo kazi akilini, katika kupokea na kuyeyushwa ndani kwa ndani ukweli wa au kwa ajili ya neon la Mungu (tazama Kum. 8:3; Yer. 15:16; na Eze. 2:8). Hakukuwa na mkazo, madai yaliyokuwa ya kawaida katika siku za Bwana wetu. Kwa wao ni kama ilivyo kwetu, tendo la kula, linakuwa na maana pia ya kufurahia au kufaidi, hasa katika Mhubiri 5:19 na 6:2, kwa hiyo, raslimali haziwezi kuliwa, na Talmudi kwa kweli inaongelea kuhusu ulaji; kwa mfano, kufaidi au kuufurahia mwaka wa Masihi. Badala ya kukuta magumu yoyote katika lugha ya kifumbo, wanasema kuwa: siku za mfalme Hezekia zilikuwa nzuri sana, ni kana kwamba hakukuwa na haja ya Mashihi kuja tena katika Israeli, kwa sababu walikuwa wamemmalizia katika siku za mfalme Hezekia, (kwa mujibu wa kitabu kiitwacho: Lightfoot, kuanzia Vol. 12, pp. 296-297). Hata katika mahali pale ambapo neno kula lilitumika kuelezea kuwaangamiza maadui, ni hali ya kufaidia au kufurahia ushindi ndiyo inayojumlishwa.

 

Kidhana kabisa, maneno ya Bwana yangeweza kueleweka na wasikiaji, kwakuwa walifahamu semi za kisarufi lakini kwa ajili ya Ekaristi hawakujua chochote, na wasingeweza kuelewa. Kwa kufananisha na aya za 53 na 54, tunatakiwa kuweza kuona kuwa kumwanimi Kristo ilikuwa na maana sawa na ya kula na kunywa. Inakuwa sawa na mfano wa wazo kama ilivyokuwa inadaiwa kueleweka vema. Hatahivyo, ni mapema sana , kutokana na aya ya 52, Wayahudi walikuwa wanatazamia hili, na iliwapa wasiwasi. Ni ukweli ulio dhahiri kabisa hawakuelewa vizuri kile atbacho Kristo alichokuwa anakisema. Kulikuwa na maana ya juu kidogo mbali na vile walivyokuwa wanaelewa kuhusu kula kwa siku za Masihi kama walivyokuwa wakielewa. Kwa kusema kuwa alikuwa anafanya nini, Kristo kimsingi alikuwa aansema: Mimi ni Masihi kwa sababu ya kutumia dhana ya kula na kunywa. Ilikuwa sio aina ya kawaida iliyoeleweka au kuzoeleka ikitumika kuelezea jambo, la sivyo wangeweza kuelewa, lakini zaidi sana ilikuwa ni njia ya kizamani ya kuelezea jambo kimfano.

 

Yohana 6:57 inasema: Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.

 

Dhana hii inaondoa kabisa maana ya mafundisho ya Utatu na kufanya fundisho hili liwe halina mantiki kabisa. Kama vila Bbaba alivyomtuma Kristo, na Kristo akaishi kwa ajili ya Baba, na ndani ya Baba, na Baba akiwa ndani yake, na sisi, kwa kumchukua Kristo, kuishi ndani ya Kristo na ndani ya Baba. Basi tunafanyika kuwa familia hii. Waamini mafundisho ya Utatu wanaonekana kuliondoa jambo hilo, kumwondoa Kristo kama aliye sawa na kuondoa uhusiano na sisi. Kifungu hiki cha maandiko kinaonyesha kiwazi wazi sana kuwa tunafanyika kuwa sehemu na Baba na Kristo, na sisi sote tumefungamana kwa kutegemeana kila mmoja na mwenzake.

 

Yohana 6:58-60 inasema: Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele. 59 Mambo hayo aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha, huko Kapernaumu. 60 Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia walisema, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia?

 

Ni ukweli uliowazi, kuwa hata wanafunzi wake hawakuelewa usemi huu wa mkate ushukao kutoka mbinguni. Neno hili kama lilivyoandikwa katika Biblia ya Companion Bible, inaonyesha uelewa huu usemi huu ulikuwa ni wa kawaida na ulikuwa unaeleweka sana kila unaposomwa, si kweli kuwa inatokana na vifungu vya Biblia. Hata hivyo, ilikuwa ni mashauri au jinsi ya kuelewa ya Waandishi. Wangeweza kuelewa, yaani ni kuyaelewa Maandiko Matakatifu, na kwakusema kwake hivi Kristo ilikuwa ni aina ya usemaji ambao kwayo Maandiko Matakatifu yametimilika katika hali yake ya kufanyika kuwa mwanadamu. Lakini haikuwa imeeleweka kirahisi sana na watu.

 

Yohana 6:61-62 inasema: Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unikia neno hilo, akawaambia, je! Neno hili litakuwaje? 62 Itakuwaje basi, mmonapo Mwana wa Adamu, akipaa huko alikokuwako kwanza? 

 

Kwa maneno mengine ni sawa na kusema: Kwahiyo, kama hii inawachukiza ninyi, mtaenda kufanya nini nitakapoondoka, kama nikipaa kwenda kule nilikowako mwanzo, Kama nikirudi nyuma, Kama nikienda zangu, Kama hili linawatia hofu, mtafanya nini nitakapoondoka? Je, mtapataje kupona?

 

Yohana 6:63 inasema: Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliwaambia ni roho, tena ni uzima.

 

Aya hii ni wazo la Biblia kuwa ni unabii ulio hai. Neno la Mungu, likivuviwa na Roho Mtakatifu hufanya ajipunguze katika vifungu vya maandiko. Kuna njia tatu za kuliangalia neno lililovuviwa la Mungu. Kitabu cha Korani kinachukuliwa na Waislamu kuwa hakikuandikwa na mkono wa mwanadamu. Wanaamini kuwa imetoka kwa Mungu moja kwa moja kwa kuandikwa na malaika Gabrieli akipewa maelekezo na Mungu. Wakristo wa siku hizi wanasema kuwa Biblia ni mkusanyiko wa habari zilizoandikwa kwa mkono wa mwanadamu. Tunashikilia kuamini kuwa kifungu hiki cha maandiko matakatifu ni cha Uungu. Kwa hiyo, Biblia imeandikwa kwa maelekezo ya Mungu. Kwa kuongezea kwa hatua mbili, ya kwanza: ni kwamba hakuna uandishi wa kibinadamu na la pili ni kuwa: hiki ni kitabu cha kibinadamu, kwa mtazamo kuwa neno hili huwakilisha Roho wa. Mungu katika umbo la kimwili, lakini Mungu alitumia wajumbe kunena maneno kwa kuelekezwa kuandika. Hii ndio maana watu wanaweza kuisoma, na kuwa ni maneno tu kwao. Watu wengine walipokuwa kabla ya kuongoka, wamesema: Haya ni maneno matupu. Ninasoma haya lakini naona kuwa ni maneno tu. Inaishia kuwa ni maneno matupu hadi pale Mungu anapofungua akili zao na weak mbali Roho hii. Kwa kuwa Biblia hii ni Roho, sio kuwa ni maneno tu. Sasa hiki ndicho Kristo anachosema hapa. Maneno anayoyasema ni Roho, na hii ndiyo maana Maandiko Matakatifu hayawezi kutanguka. Wakati iliponenwa na manabii ina kuwa kweli. Hakuna mambo yanayopingana katika Biblia kwa sababu hii ni kweli. Kama ilivyonenwa.

 

Yohana 6:64 inasema: Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti.

 

Alimjua ni nani ambaye Mungu aliwachagua na kumpa yeye. Wakati alipopewa kwanza wale wanafunzi, alijua ni nani atakaye kabidhiwa kwake, nani angeweza kubakia, na nani ambaye asingeweza kubakia. Roho hushughulika na mambo haya yote na hupeleka taarifa kwa wateule. Watu huelewa kama ama wao ni sehemu ya mwili wa Kristo. Wanajua kama ama wanafanya dhambi. Watu wanajua ni lini waende na kujificha bustanini.

 

Yohana 6:65 inasema: Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipokuwa amejaliwa na Baba yangu.

 

Hii ndio maana Kristo alisema nao kwa mifano. Na hii ndiyo maana siri za Biblia zimefichwa kwa watu wengi, kwa sababu hawaruhusiwi kuja mbele za hukumu. Ni Mungu peke yake ndiye awatuoye watu kwa Kristo. Huwezi kuliitia jina la Yesu Kristo, hadi pale tu Mungu atakapokutoa Yesu Kristo. Pia kama hujui kuwa Yesu Kristo sio huyu Mungu wa kweli, hutaweza kuwa miongoni mwa watakaokuwemo katika ule ufufo wa kwanza. Uelewa huo ndio muhuri wa wateule, miongoni mwa mambo mengine.

 

Yohana 6:66 inasema: Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.

 

Hapa pana jambo muhimu. Kristo aliwapa mafundisho hayo, na halafu kile alichukuwa anakiongea kilikuwa ni kigumu, kwa hiyo walijikwaa kabisa. Sisi sote tumetolewa kwa kila mmoja wetu kwa mwingine kwa kusudi la kuhudumiana. Tunajua hilo kutokana na kitabu cha Wakorintho kuwa tumepewa karama za Roho Mtakatifu na sisi sote tumewekwa katika mwili wa Kristo, na sisi sote vipaji maalumu. Kila mmoja wetu anajua kuhusu ni kwa kiasi gani tuna nguvu au udhaifu wetu tulivyo. Kila mmoja wetu humtegemea mwingine. Kila mmoja wetu hufanya kitu. Kila mteule ana nguvu ambazo hazifanani kwa kadiri kila mmoja alivyo kirimiwa. Kila mmoja wetu ana vipaji zinazoendana katika ukamilifu na kufaidia wengine wote walio kwenye mwili – yeyote kati yetu. Baadhi yetu tuna idadi ya kadhaa ya vipaji tulivyo kirimiwa. Baadhi yetu tumepishana kwa mambo fulani, lakini kwa ujumla sisi tunashabihiana kikamilifu kabisa katika mashine moja, na Mungu ametuweka hapa kwa sababu maalumu.sisi ndi ule mwili. Ili kutufanya tuwemo katika huu mwili, Kristo ilimpasa Kristo avunjwe vipande vipande kama mkate, na kukusanywa katika makanda. Ili kutuwezesha sisi tuingizwe katika huu mwili, mwili mmoja ulipaswa uvunjwe vunjwe na kukusanywa kwenye makanda yaliyojaa tele. Kulikuwa na idadi ndogo tu, hivyo basi ilizidi kukua kupitia Roho.

 

Yohana 6:67 inasema: Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka kuondoka?

 

Kumbuka kuwa mapema kabisa katika Yohana 6 tunaona kuwa hawa thenashara wahakujua kwa wakati ule, kuwa walikuwa wanakwenda kuyakabidhi yale makanda thenashara. Haya makanda kumi na mawili yalichukuliwa wakapewa hawa wanafunzi kumi na wawili kama waamuzi. Walikuwa wanaenda kuwa wafalme kwa kupitia haya makanda thenashara ya mikate, na kisha mengine yakapoteza muelekeo. Walijazilia kwa pake nyuma yake. Na akasema: Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka kuondoka?

 

Yohana 6:68 inasema: Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.

 

Maneno kuhusu uzima wa milele ni ya Roho na kweli, na Biblia ndio uthibitisha wake. Kama watu hawaneni kufuatana na sheria ya ushuhuda, kutoka katika kitabu cha nabii Isaya 8:20, basi hakuna nuru ndani yao. Kwa hiyo unapaswa kwenda kule ambako kweli ina nenwa, na ambapo utafanyika kuwa ni mshiriki halisi wa mwili wa Kristo.

 

Yohana 6:69 inasema: Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu.

 

Hapa hakusema kuwa Niaamini kuwa wewe ni mmojawapo wa vichwa vitatu vya Mungu. Bali alisema kuwa naamini kuwa wewe ni Masihi, mwana wa Mungu aliye hai au neno la kweli.

 

Yohana 6:70 inasema: Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Tenashara, na mmoja wenu ni shetani?

 

Moja kati ya hizi kwa hakika ilitolewa kwake ili kwamba angeweza kumsaliti. Alitiwa kwenye nafasi na mwingine aliyechukua kikapu chake.

 

Yohana 6:71 inasema: Alimnena Yuda mwana wa Simoni Iskariote, maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Thenashara.

 

Fundisho lile la makanda na kuvunja mkate vipande vipande, ni sehemu ya mkate wa kawaida na ule wa jangwani uliojulikana kama mana. Sio sehemu ya mlolongo hadithi zenye kufungamana. Yohana 6 ina milolongo ya hadithi zilizowekwa pamoja kwa lengo la kutuwezesha sisi sote tufikie kwenye uelewa wa kuwa sisi ni washiriki katika mwili wa Yesu Kristo, na kwamba tumeokolewa kwa kupitia na muingilio wa Yesu Kristo na kipawa cha Roho Mtakatifu. Tumepewa pia kuelewa kwamba kuna miujiza pia inayohusiana, na kwamba Roho wa Bwana ni mwili. Hii inamaana kuwa Roho wa Bwana ni Roho wa kweli, aliyemtia muhuri Kristo nandiye aliyetutia sisi sote muhuri pia, na kutufanya tuwe washiriki katika mwili. Tunafanyika kuwa ni washiriki wa siri za Mungu, kama Kristo alivyokuwa ni sehemu ya Mungu. Tunaishi ndani ya Kristo, na Kristo na Mungu Baba huishi ndani ya kila mmoja wao. Sisi sote tuna mahusiano shirikishi yenye kutegemeana mmoja kwa mwingine. Ndiyo maana unapoamka asubuhi unaomba kwa Mungu kwa jina la Kristo na Kristo anaishi ndani yako. Utatu uliyeko hapa ni kwamba tu juu ya mmoja aliyeumba kila asubuhi, na kila dakika ya kila siku, unatembea pamoja na Kristo, akikuongoza, kwa mahusiano ya moja kwa moja na Mungu, chini ya mapenzi ya Mungu. Umetolewa kwa Kristo ili kufikia malengo hayo. Unayo kazi ya ziada ya kufanya, iliyoandaliwa siku nyingi sana zilizopita hata kabla hujazaliwa. Hata kabla hujaumbwa kwenye tumbo la mama yako, Bwana alikujua na aliziweka wakfu kazi zako. Nabii Yeremia aliambiwa hivyo (Yer. 1:5) Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Sisi tumewekwa pamoja ili kumfanyia kazi, na hatujui ni nini kitakuwa matokeo ya mwisho katika hatima yake. Tumewekwa katika maeneo mbalimbali. Mungu amekuweka mahali pale alipotaka wewe uwe. Yote yatakuwa kwa ajili ya uzuri na yote itakuwa kwa uwazi. wakati mwingine, inaonekena kuwa kwenye mabano wala kabla hakujapambazuka mahali tusipojua ni kitu gani kinatokea.

Kulikomboa Jeshi

Mafundisho ya kula na kunywa yalitumika pia kwenye matendo ya ibada za sanamu, kwa hiyo vilikuwa na mwingiliano wa kimahusiano. Tunaona katika Waraka kwa Wakorintho ukizungumzia kuhusu ibada za sanamu na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na jinsi ile tulivyo, katika kula na kunywa kwetu, kunywa katika Kristo na kushiriki katika Mungu katika mfumo wa kiroho kama washiriki katika Jeshi- washiriki wa Kristo, na washiriki wa madhabahu kama wana wa Mungu. Msafara wa kutoka utumwani na Pasaka vimeonyesha ukweli wa anguko la Jeshi, na uzibaji wa pengo wa elohim mwingine. 1Wakorintho 10:21-22 inasema kuwa huwezi kukinywea kikombe cha Bwana na kikombe cha Mashetani. Huwezi kushiriki meza ya Bwana na meza ya mashetani. Au je, twamtia Bwana wivu? Au je, sisi tunanguvu kuliko yeye? Unaona sasa, kumbe tunapokuwa tunashiriki kuula mwili na kuinywa damu ya Kristo, unakula na kukinywea kikombe cha Roho Mtakatifu na sheria ya Mungu. huwezi kuweka pamoja na kitu kingine chochote. Hutakiwi kuwa mshiriki wa sehemu yoyote ya mfumo wa kishetani. Ni ule Msafara wa Kutoka utumwani na Pasaka ndizo zinazokuweka wewe katika utaratibu wa Mungu na kukupa uzima wa milele. Kuna mkate mmoja tu, ambao nimwili wa Kristo, unaotufanya sisi sote tuwe mwili mmoja katika kushiriki huu mwili mmoja. Kuna kikombe kimoja tu, kikombe cha Bwana. Kwa hiyo tunaona kwamba tulikuwa na Msafara wa kwanza wa Kutoka utumwani Misri na kuanzisha taifa la Israeli ili kwamba tuweze kuanzisha mahala ambapo Mungu angepatumia katika kufunua mipango yake kwa kupitia manabii wake.

 

Yeremia 31:31-34 inasema: Angalia, siku zinakuja, asema BWANA; nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. 32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano languhilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA. 33 Nali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 34 Wala hawatafundishana kila mtu na jirani yake, na kila mtu na ndugu yake, wakisema, mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao, asema BWANA; maana nitawasamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.

 

Yeremia anatabiri juu ya agano. Utaratibu huu wote ulikuwa ni agano la dhabihu ya damu. Mfano wake uko katika Waebrania 8:3-6.

Waebrania 8:3-6 inasema: Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa vya dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa. 4 Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria; 5 watumikiao mfano wa kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana alisema, angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima. 6 Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.

 

Hii ndiyo maana makuhani walikuwa na idadi maalumu na kamilifu, na ndio maana walikuwa na migawanyo ishirini na nne ya makhani wakuu, na yule wa ishirini na tano alikuwa ndiye kuhani mkuu wao wote, kwa sababu kulikuwa na wazee ishirini na wa nne katika baraza la Elohimu, chini ya Yesu Kristo akiwa ni Kuhani Mkuu.  Mambo haya yote yalifanyika kama mfano kwa mfumo au utaratibu wa kimbinguni. Kwa hiyo, Kristo alijitoa nafsi yake kuwa sadaka, na hakuna kingine ambacho kingekuwa ni kizuri kiasi cha kutosheleza. Fundisho lenye kulinganisha mwili na wokovu, kama tulivyokwisha ona lipo kayika Yohana 6:58. Mkate ulioshuka kutoka mbinguni, si kama baba zenu walivyokula wakafa, bali yeyote aulaye mkate huu ataishi milele. Tunaona kuwa ile mana ilikuwa ni mfano, na mkate ulitoka mbinguni, na Kristo kiuwazi kabisa alisema kuwa uvunjaji na ulaji wa mikate ulikuwa ni mwili wake. Damu ilikuwa ni lazima iwe damu ya dhabihu, lakini vile vile kua idadi nyingi sana ya mifano katika fundisho la damu na matumizi ya divai. Fundisho kuhusiana na agano la Kristo linaweza kuwa moja tu, ni kama ilivyo kwa Roho haina haina mwili wala mfupa. Kristo alijitoa dhabihu mara moja tu na kwa wote. Huwezi kuwa na aina mbili ya dhabihu. Kama ni hivyo basi, Masihi asingali kufa zaidi ya vile alivyokufa mara moja. Alipaswa aje chini katika mwili, kisha afanyike kuwa Roho. Roho hana damu wala damu. Kwa hiyo, kusingekuweko na dhabihu nyingine zaidi ya ile iliyotolwa mara moja tu. Kulikuwa na dhabihu ya damu katika ulimwengu wa kiroho. Kwa hiyo, uasi katika Jeshi-uasi wote mzima-ulikuwa na ni wa lazima, mtu mmoja alijifanya mtu akafa. Kulilazimu kuwepo na dhabihu ya damu sawasawa na tendo la kulikomboa Jeshi. Tena hakuna roho ingaliyoweza kufanya jambo lile. Hakuna roho ingaliyoweza kufanya ukombozi kwa Jeshi kwa kupitia dhabihu. Ilibidi mmoja wao akubali kuchukua mwili wa kibinadamu ili afe, na shetani hakuwa tayari kufanya vile. Lakini Kristo alikuwa tayari, na hii ndiyo tofauti. Hii ni sawa na mlinganisho wa habari za Kaini na Abeli ambapo tunaona kuwa sadaka ya Abeli ilikubalika zaidi kuliko ya Kaini. Hakukuwa na hitajiko la dhabihu kwa ajili ya lile Jeshi la malaika walioanguka. Wajibu wetu wa uongozi ni mojawapo ya dhabihu za kujitoa dhabihu, yaani kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu wapendwa wengine. Ili kuweza kumkomboa mtu yeyote kwa Mungu, inatubidi kujiandaa kuyatoa maisha yetu, kama Kristo Bwana wetu alivyofanya.

Divai na Damu

Sasa divai inafanyika kuwa ni mfano wa damu. Tunajua hilo kwa sababu Kristo alituambia hivyo. Kila mwaka, ilikuwa kwa kupitia damu ya mafahali ya ng’ombe ndivyo Israeli walivyo takaswa, lakini kwa kupitia Kristo, ilifanyika mara moja tu na kwa wote. Aliwawezesha watu wote kuingia kwenye mahusiano na Mungu kwa kumpokea Roho Mtakatifu. Ili kuweza kufanya hilo, ni lazima tusamehewe au kuondolewa dhambi na kwa kupitia mfano wake na dhabihu ya Kristo. Katika Waebrania 1:3 inaonyesha Kristo akiukumbushia utukufu wa Mungu na kuchukua chapa za asili yake, akishikilia ulimwengu kwa neno la nguvu zake. Akiwa amefanya utakaso kwa ajili ya dhambi, alikaa chini aliketi chini katika mkono wa kuume wa Mwenye enzi na mtukufu. Kwahiyo Kristo anarudishia utukufu wa Mungu na anachukua chapa halisi ya asili yake, kama sisi tunapochukua chapa asili ya asili ya Mungu. Tunayo asili ya Mungu tuliyopewa. Sisi ni warithi wa mambo Kimbinguni tuliyowekewa. Neno lenye maana ni kuwa wateule wanatakiwa kuishi na kudhihirisha utukufu wa Mungu. Ni juu ya kufanya bidii tu ili kufikia pale. Kwa hiyo, Kristo alitenda kama mzabibu kwa namna ya mfano. Hii ndio maana ya kutolea mfano wa mkulima wa mizabibu katika Injili ya Yohana 15:1-6.

Yohana 15:1-6 inasema: Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha , ili lizidi kuzaa. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu, Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; nanyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.

 

Fundisho hili liko pale tunapokuwa pamoja, na kufanya kazi kulingana na mapenzi ya Mungu, sisi tuko na Kristo. Tumevalishwa na utnazaa matunda. Wakati tunapoacha kuyafanyia kazi mapenzi ya Mungu, basi tunasimama kuzaa matunda na tunakatiliwa mbali. Mifano ya hili anguko la kushindwa kuelewa ni lile la kwamba tunapaswa kuufanyia kazi wokovu wetu kwa hofu na kutetemeka kuna vitu vingi sana ambavyo Mungu anahitaji sisi tumfanyie, lakini la kushiriki kuula mwili wake na kuinywa damu Kristo, na kuzaa matunda kupitia Roho Mtakatifu kwa maana ya kugeuka, ni jambo lanye umuhimu na la kwanza. Maumbile ya kawaida ya divai kuwa inakuja kutoka kwenye tunda la mzabibu ni ishara sawa na ile ya Roho Mtakatifu. Kwa hiyo ni kwamba Roho Mtakatifu anafanyika kuwa ni mlango, au kama mzunguko, wakati anapokuja kwako, na unapomshiriki katika mwili na damu ya Kristo. Kisha wewe na divai huzaa matunda yenu wenyewe na huendelea kuzaa matunda mengi zaidi, ili kwamba iwe kama kitanzi kilichofungwa. Fundisho la mwili na damu ya Kristo limetuama kwa Ushirika wa Meza ya Bwana. Uelewa kuhusu maana ya mikate mitano na samaki wawili halieleweki kiurahisi sana. Kuna mambo mengi zaidi yanayotakiwa kuandikwa kuhusu vitu vyote viwili vya ulishaji. Wakati Kristo alipowaambia baada ya mafundisho yake ya mfano, alisema, je, sasa mnaelewa? Na wao hawakuelewa. Kuelewa nini? Hilo lilipaswa lifafanuliwe kwa kuhusianisha na maendeleo ya wateule. Sisi ni sehemu ya hatua hiyo. Tumewekwa pale na Mungu. Tumetolewa kwa Kristo. Tunaufanyia mfano ule kwa kupitia vielelezo vitatu vya ufahamu wetu kuhusu Mungu wa pekee wa kweli, na wa Mwanae wa pekee Yesu Kristo, kwa imani katika Kristo, na hatimaye kwa kushiriki kuula mwili na kuinywa damu ya Kristo. Haya ni mambo matatu muhimu kwa sisi ili tuuingie uzima wa milele. Hatuwezi kuuingia uzima wa milele kama tusipokuwa na Roho Mtakatifu, na kutembea na nguvu zake, na kuzishika sheria za Mungu ambazo Yohana anatueleza kuwa ni za muhimu katika kumpendeza Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, sisi, lazima tuziadhimishe Sabato na Pasaka ili tuweze kumpendeza Roho Mtakatifu na tuwemo katika ufufuo wa kwanza. Kwa kweli hili ni jambo la lazima! Kama hutaadhimisha Sabato na Pasaka, hutakuwa na sehemu katika ufufo wa kwanza. Huu ni mfano wa yote haya.

 

 

q