Makanisa Ya Kikristo ya Mungu

[101]

 

 

 

Usiku Wa Kuangaliwa Sana

(Jarida 1.0 19990306-19990306)

 

Imeandikwa: Nawe utaikumbuka siku hii na kuiweka katika kumbukumbu zako; nawe utamfanyia Bwana sikukuu katika vizazi vyenu vyote; nawe utafanya sikukuu kwa amri ya milele.

 

 

 

 

 

Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA

 

E-mail: secretary@ccg.org

 

(Copyright ă  1999 Wade Cox)

(Tr. 2005)

 

Masomo haya yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwagawia watu bure ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kutufa maneno. Jina la mchapishaji na anuami yake pamoja na hati miliki ni lazima iwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpewaji kutoa au kuchangia kwa ajili ya nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zaweza kuwekwa toka kokote ikiwa zitafaa kukithi haja ya maelezo na kilugha lakini bila kukiuka maadili ya sheria ya hati miliki.

 

Masomo haya pia yanapatikana Ulimwenguni kote katika tovuti yetu ya:

 

http://www.logon.org and http://www.ccg.org


Usiku Wa Kuangaliwa Sana [101]

 


Usiku wa Kuangaliwa Sana ni tukio la muhimu sana katika kalenda ya kibiblia.

 

Lakini imesahauliwa sana kabisa na watu walioko katika Ukristo wa mfumo wa kimadhebu na kupuuzwa kwenye Makanisa ya Mungu katika karne ya ishirini. Dini ya Kiyahudi pia imefanya makosa na kuanzisha mfumo wa kalenda potofu ili kuharibu lengo na ukweli wa kuadhimishwa kwake sawa sawa na Sheria za Mungu kwa siku iliyo sahihi. Ni masalia ya Wasamaria tu na makanisa madogo machache ya Mungu huiadhimisha kulingana na mujibu wa kalenda ya ya Kipindi cha Pili cha Hekalu na iliadhimishwa wakati wa Kristo na kanisa la kwanza.

 

Umeitwa pia kuwa Ni Usiku wa Makesho na jina hili lina kusudi fulani maalumu.

 

Mlolongo wote mzima wa matukio ya Pasaka umeelezewa katika jarida liitwalo Pasaka [098]. Kipindi cha kimapokeo kinachoelezewa cha kama Pasaka katika Kanisa la kwanza la Kikristo ni kipindi kinachofunika kuanzia usiku wa Ushirika wa Meza ya Bwana wakati ambapo Kristo alikuwa amechukuliwa nyara baada ya mlo alioshiriki pamoja na wanafunzi wake katika usiku ule wa siku ya maandalizi kabla hajatiwa kwenye nyara na kujaribiwa kwenye baraza la Kiyahudi la Sanhedrini na mbele ya Pilato na hatimaye kusulibiwa. Alisulibiwa na kuuawa alasiri ya Siku ya Kumi na nne ya mwezi wa Nisani, sawa sawa na mujibu wa uchinjaji wa Pasaka. Alikufa mnamo majira ya saa 9 ya mchana yaani alasiri muda ambao wana kondoo walikuwa wana uawa kwa ajili ya mlo wa Pasaka jioni ile iliyoanzia katika Usiku wa Kuukumbuka Sana katika Siku ya Kumi na Tano ya Mwezi wa Kwanza. Mwana zuoni Yosefus alinukuu kuwa kulikuwa na maelfu mengi ya kondoo ambao waliuawa au kuchinjwa alasiri hii ya Siku ya Kumi na Nne kuanzia saa 9 alasiri na kuendelea. Pasaka kwa siku za kanisa la kwanza lilikuwa ni namna ya neno lililokuwa linachukua kipindi chote cha kuanzia siku ya 14 ya mwezi wa Nisani hadi kufikia siku ya Jumapili ya Mganda wa Kutikiswa bila kujalisha idadi ya siku zilikuwa ni ngapi. Siku zilizobakia zilichukuliwa kama za Mikate Isiyotiwa Chachu.

 

Jinsi ambavyo Pasaka ilivyokuwa inasherehekewa katika siku za kipindi cha Hekalu imeandikwa na Yosefus. Wana kondoo wa Pasaka walichinjwa kuanzia saa tisa hadi saa kumi na moja [kwa mujibu wa jarida liitwalo Yosefus, Vita ya Wayahudi (War of the Jews), Bk. VI, Ch. IX, Whinston, Kregel, 1981, p.588]. Katika nyakati za kumbu kumbu za Cretius Josephus iliaminika kuwa walikuwa wanachinjwa kondoo takriban laki mbili na elfu hamsini na watano na mia tano huko Yerusalemu kwa kipindi cha Pasaka moja tu peke yake na kwa mlingano wa si chini ya watu kumi kushiriki mwana kondoo mmoja (ibid.)

 

Sote tnajua kwa usahihi sana kwamba Wasamaria na Masadukayo wote wawili walipinga aina yoyote ya mapokeo ya kimaneno au ya kigeni na wote walizitunza sheria zilizoandikwa. Yusefus anatuambia kwamba John Hyrcanus alitangua sheria za Mafarisayo na kuanzisha madhehebu ya Masadukayo na kusimamia na ingawaje ilihusika kwa mapana sana hadi kufikia kwenye mtazamo wa ukoo bora, sheria zao zilianzishwa. Mafarisayo walipata umaarufu kwa watu wengi kwakuwa walikuwa wanajali sana kutoa hukumu zao kingwana na kwa kiasi. [Tazama jarida la Masalia ya mambo ya kale ya Wayahudi, yaani Antiquities of the Jews, Bk. XIII, Ch. X (Whiston, ibid., p. 28]. Yosefus mwenyewe alikuwa ni Farisayo na aliandika mambo mengi yenye kuwapa kipaumbele sana wao kuliko hata vile alivyoweza, lakini pia anandika tamaduni za kimapokeo alizozisoma katika Agano Jipya. Uhairisho haukuwepo kwa wakati huu kwa kadiri ya kama tunavyoona kutoka katika Mishnah. Mapokeo yalianzishwa kwa kiwango cha madaraja na Mafarisayo tokea baada ya utumwa wa Babeli, ambao walikataa kushirikiana na aina nyingine yoyote ya madhehebu. Mashutumu ya Mafarisayo yaliendelea chini ya usimamizi wa John Hyrcanus mtoto wa Alexander Jannaeus lakini baada ya kifo chake mke wake Alexandra aliwasaidia Mfarisayo kwa muda wa miaka minane. Waliweza kumtawala kwa njia hila kubwa na tena wakajaribu kuanzisha desturi zao za kimapokeo. Wakati wa kifo chake Aristobulus na kaka yake mkubwa Hyrcanus, ambaye Alexandra alifanya awe kuhani mkuu, alipigana vita ya kuwania urithi wa kiti. Hyrcanus akaondolewa madarakani kisha na yeye akakabidhiwa mamlaka ya Mafarisayo (ibid. p.289). Hyrcanus alisaidiwa na Antipater Muidume na hatimaye Pompey akalazimika kuingilia mashindano haya. Akiwa amechukizwa na kiburi au majivuno yake, Pompey alimshambulia Aristobulus na kuingia Yerusalemu na Hekalu hata kiasi cha kwenda mbali hadi kuingia Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu la Mungu. Ilikuwa ni kwa wakati ule ulitumiwa kwa ajili ya kukusanya na kuhifadhi hazina pia aliyoacha kwa wakati ule. Alimhifadhi Hyrcanus na wafuasi wake waliokuwa wameshiriki na aliowachinja idadi kubwa ya makuhani wa mtaa au kitongoji.

 

Kwa njinsi hii, Mafarisayo wakapewa nguvu lakini walikuwa na majivuno na kiburi. Walishiriki katika matendo ya hila, udanganyifu na kukosa kuaminika na pia walihusika na utoaji wa unabii wa uongo chini ya Herode. Alikuwa na kanuni yao ya wanaume waliouawa mbali na Bagoas toashi, Carus Msodoma au mwenye kupenda matendo ya Wasodoma, na mkatami na kanuni ambayo ni ya watu wa jamaa ya Herode wenyewe ambao walipatikana na unabii wa uongo kwa ajili ya kusimamishwa kwa sheria. Wale waliouawa wanaonekana kuwa ni wa jamaa wa mke mdogo wa Farao, na mama yake na dada yake, na Doris mama wa Antipater (kwa mujibu wa jarida la A ya J, ibid, p. 358). Kwa hiyo, chini ya Waherode, Mafarisayo alikuwa na kikomo cha mamlaka ingawaje walihesabu kiasi cha takriban wanachama elfu sita kwenye dhehebu lao.

 

Hekalu liliendeshwa kwa kufuata mujibu wa kalenda ya zama za kale ambayo iliadhimishwa au kuaminiwa na Masadukayo na kama ilivyokuwa ikiadhimishwa na Wasamaria. Baada ya kipindi cha utawanyiko madhehebu ya kirabi ambao walichukua pahala pa Mafarisayo walijaribu kuanzisha uahisisho na kwa hiyo hatimaye Wasamaria wanadhaniwa kuwa walikuwa na mtazamo mpya kwa ajili ya uwashaji wa minara kwa miandamo wa mwezi mipya. Wakati wa kipindi cha Hekalu minara ilikuwa ikiwashwa kama miandamo ya mwezi ilivyokuwa inajulikana kwa mjumuisho ambao haukuwa ni mfumo wa maadhimisho. Hakuna ushahidi yakinifu kuonyesha kuwa Wasamaria waliwahi kubadilisha utaratibu wao wa jinsi ya kuhesabu Miandamo ya Mwezi katika historia kwa wakati wa ama wakati wenyewe au baada ya kipindi cha Hekalu la Pili. Wao bado wanaendelea kuadhimisha mfumo ule ule hadi leo [tazama jarida la Kalenda ya Mungu [156] (toleo la pili).

 

Uwekaji wa Sheria

Sheria za namna hiyo hiyo kwa ajili ya Pasaka zinapatikana kwenye kitabu cha Kutoka 12

 

Kutoka 12:1-51 inasema: BWANA akanena na Musa, na Haruni katika nchi ya Misri akawaambia, 2 Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. 3 Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkmwammbie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana koondoo kwa watu wa nyumba moja; 4 na ikwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na atwae mwana kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yulr mwana kondoo. 5 Mwana kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi. 6 Nanyi mtamweka katika siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. 7 Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla. 8 Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chacu; tena pamoja na mboga zenye uchungu. 9 Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani. 10 Wala msisaze kitu kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto. 11 Tena.mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya BWANA. 12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA. 13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoingia nchi ya Misri. 14 Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyot, kwa amri ya milele. 15 Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli. 16 Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa na kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu. 17 Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele. 18 Mwezi wa kwanza, siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata siku ya mwezi ishiri na moja jioni. 19 Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi. 20 Msile kitu chochote kilichochachwa; mtakula mikate isiyochachwa katika makao yenu yote. 21 Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo, mkamchinje pasaka. 22 Nanyi twaeni tawi la hisopo, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini, na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. 23 Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. 24 Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele. 25 Itakuwa, hapo mtakapoifikilia hiyo nchi, BWANA atakayowapa, kama alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu. 26 Kisha itakuwa hapo watoto wenu watakapowauliza, N’nini maana yake utumishi huu kwenu? 27 ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia. 28 Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama BWANA alivyo waamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya. 29 Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawapiga wazaliwa wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama. 30 Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu. 31 Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, mkamtumikie BWANA kama mlivyosema. 32 Twaeni kondoo zenu na ng’ombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu, mkanibariki mimi pia. 33 Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote. 34 Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabagani. 35 Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi. 36 BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara. 37 Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto. 38 Na kundi kubwa la watu waliochangamana nao wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng’ombe, wanyama wengi sana. 39 Nao wakaoka mikate isiyochachwa ya ule unga waliochukua walipotoka Misri, maana, haukutiwa chachu, kwa sababu walitolewa watoke Misri, wasiweze kukawia, nao walikuwa hawajajifanyia tayari chakula. 40 Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana, muda waliokaa ndani ya Misri, ulikuwa ni miaka mia nne na thelathini. 41 Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya BWANA yalitoka nchi ya Misri. 42 Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za BWANA, kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa BWANA, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao. 43 BWANA akawaambia Musa na Haruni, Amri ya pasaka ni hii; mtu mgeni asimle; 44 lakini mtumishi wa mtu awaye yote aliyenunuliwa kwa fedha, ukiisha kumtahiri, ndipo hapo atamla pasaka. 45 Akaaye kwenu hali ya ugeni, na mtumishi aliyeajiriwa, wasimle pasaka. 46 Na aliye ndani ya nyumba moja; asiichukue nje ya nyumba nyama yake ye yote; wala msivunje mfupa wake uwao wote. 47 Na wafanye jambo hili mkutano wa Israeli wote. 48 Na mgeni atakapoketi pamoja nawe, na kupenda kumfanyia BWANA pasaka, waume wake wote na watahiriwe, ndipo hapo akaribie na kufanya pasaka; naye atakuwa mfano mmoja na mtu aliyezaliwa katika nchi; lakini mtu ye yote asiyetahiriwa asimle. 49 Sheria ni hiyo moja kwa mtu aliyezaliwa kwenu, na kwa mgeni akaaye kati yenu ugenini. 50 Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli wote; kama BWANA alivyomwagiza Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya. 51 Ilikuwa siku ile moja, BWANA akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao.

 

Kifungu hiki cha Maandiko Matakatifu kinaanzisha pia mwandamano au mlolongo wa muda kamili. Kuanzia ile aya ya 18 tunaona kuwa kipindi cha siku saba za Mikate isiyotiwa Chachu zinahesabiwa kuanzia siku ya kumi na nne ya Mwezi wa Kwanza, siku saba hadi kufikia Siku ya Ishirini na Moja ya mwezi. Siku hii ya saba ya sikukuu, Siku ya Ishirini na Moja ya Mwezi wa kwanza, yenyewe ni Siku Takatifu. Kwa hiyo jioni ya Siku ya Kumi na nne ni mwanzo wa Siku Takatifu ya Kwanza ya Mikate isiyotiwa Chachu ambayo tunaambiwa kuwa ni siku ya Kumi na tano ya mwezi wa Kwanza. Kwa hiyo, sisi tunaongelea mwisho wa siku ya Kumi na Nne ya mwezi wa Kwanza ambao ni mwezi wa Abibu au Nisani. Aya ya 16 inaonyesha kwamba kuna Kutaniko takatifu katika Siku ya Kwanza ya Mikate isiyotiwa Chachu ambayo tunaiona katika kitabu cha Mambo ya Walawi 23:6 ni Siku ya Kumi na tano ya Mwezi wa Kwanza. Hakuwezi kuwa na mchanganyo kama kwenye mwanzo wa Mikate isiyotiwa Chachu au kama wakati wa kumuua mwana kondoo wa Pasaka kwa mujibu wa maandiko.

 

Tunaiona namna nyingine ya siku katika kitabu cha Matendo ya Mitume 27.

 

Matendo ya Mitume 27:27-36 inasema: Hata usiku wa kumi na nne ulipofika, tulipokuwa tukichukuliwa huko na huko katika bahari ya Adria, katika usiku wa manane baharia wakadhani ya kuwa wanaikaribia nchi kavu. 28 Wakatupa bildi wakapata pima ishirini, wakaendelea kidogo wakatupa bildi tena, wakapata pima kumi na tano. 29 Wakachelea tusije tukapwelewa mahali penye miamba, wakatupa nanga nne za tezi, wakaomba kuche. 30 Na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha merikebu, wakiishusha mashua baharini kana kwamba wanataka kutupa nanga za omo, 31 Paulo akawaambia akida na askari, Hawa wasipokaa ndani ya merikebu hamtaweza kuokoka. 32 Basi askari wakazikata kamba za mashua, wakaiacha ianguke. 33 Na kulipokuwa kukipambazuka Paulo akawasihi wote wale chakula, akisema, Leo ni siku ya kumi na nne kungoja na kufunga, hamkula kitu cho chote. 34 Basi nawasihi mle chakula, maana itakuwa kwa wokovu wenu; kwa maana hapana hata unywele wa kichwa cha mmoja wenu utakaopotea. 35 Alipokwisha kusema hayo akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula. 36 Ndipo wakachangamka wote, wakala chakula wenyewe.

 

Sasa tendo hili halikutokea mwezi wa Kwanza lakimi ni baada ya mfungo wa saumu ya mwezi wa Saba siku ya Upatanisho. Hata hivyo, tunaweza kuogundua hapa ni kuwa siku inayoitwa kuwa ni siku ya kumi na Nne ilikuwa kwa dhahiri sana imeamuriwa kutokana na utaratibu wa kihesabu ya siku wa jioni hadi jioni nyingine. Usiku wa siku ya kumi na nne iliyotanguliwa na siku ya kumi na nne. Hii inathibitisha kuwa ukweli kuwa siku ilionekana kuwa inaanzia jioni hadi jioni nyingine na sio asubuhi hadi asubuhi; au usiku wa manane hadi usiku mwingine wa manane; au kwa aina nyingine ya mfumo wowote. Zaidi ya yote, wazo la wokovu wa Malaika wa Bwana, ambaye Mtume Paulo alimtegemea na kumtumikia, pia anaonekana kwenye maandiko ya Matendo 27:23.

 

Mtazamo wa kuuona mwezi wa Tishri kama ni Mwaka Mpya kama ilivyo Rosh Hashanah unatokana na matendo ya kizamani ya kipagani yaliyokuwa yanafanyika siku za zamani kabla ya kujengwa kwa Hekalu ambayo yalijipenyeza na kuingia kwenye dini ya Kiyahudi katika zama za kane ya tatu kwa mujibu wa hesabu ya miaka iliyopo. Rabi Kohn, Rabi Mkuu wa Budapest, anaandika kutoka mwaka 1894, anaelezea humo ukweli huu wa muhimu wa kazi ya Watunza Sabato wa Transylvania akielezea kuwa iliingia katika karne ya tatu na siku za “kabla ya Biblia” (kwa mujibu wa kitabu cha Talmud Rosh haShnah 8a at n. 18 hadi sura ya 7) (Toleo la W. Cox, lililotafsiriwa na T. McElwain na B. Rook, na Kuchapishwa na CCG, USA, 1998, kifungu cha v, 58, 106, nk. Mlolongo na nn) tunaona kuwa kibiblia Mwaka Mpya uko ndani ya Abibu ambao ni mwezi wa Kwanza.

 

Kwa mijibu wa Mishnah (takriban 200BK) inasema kwamba kuna aina nne ya miaka mipya na siku ya Kwanza ya mwezi wa Nisani ni mwaka mpya kwa wafalme na sherehe. Kwa hiyo tunaona kwamba kuhesabu kwa mujibu wa Ezra na Nehemia ilikuwa ni kwa kufuata mujibu wa siku ya 1 ya mwezi wa Nisani na sio kabisa kwa siku ya 1 ya mwezi wa Tishri (tazama jarida la Kusoma kwa Sheria na Ezra na Nehemia [250]. Mwezi wa Tishri ulitumika kwa siku zile kwa kuhesabia miaka, Miaka ya Sabato na kwa ajili ya Yubile [Rosh Hashanah 1.1 E (3)]. Tunaona kwamba wazo la Tishri, ambalo lilitokea kutoka kwa Wababeli, lilinukuliwa kwa mara ya kwanza katika Mishnah kama ni kwa kutiwa mbele na R. Eliezar na R. Simeoni (ibid. 1.1 D). Ulikuwa hauadhimishwi kama ni Mwaka Mpya kwa zama za kipindi cha Hekalu. Pia Mishnah inajaribu kuweka uwezekano wa kuatenganisha mwanzo wa utoaji wa zaka za mifugo katika siku ya 1 ya mwezi wa Eluli (ibid. 1.1 C). nyumba ya Shammai iliadhimisha mwaka mpya kwa miti ilikuwa ni siku ya 1 ya mwezi wa Shebati ambapo nyumba ya Hilleli iliiadhimisha siku ya kumi Nne ya mwezi ule. Kuadhimisha Mwaka mpya kwa wakati wa Mwezi Mkamilifu ni tendo la kipagani lililo dhahiri kabisa ambalo pia lilianzishwa kutokana na mfumowa Kibabeli na bila shaka lilihusiana na upandaji wa mimea ya maadhimisho ya jedwali za miezi. Maamuzi haya yote ni ya siku za kabla ya Hekalu cha marabi wa Kiyahudi. Tunaona hapa kwamba ni kwenye karne ya Tatu tunaona kwamba mwezi wa Tishri unatukuzwa na marabi. Hii pamoja ma mfumo wake wa ahirisho, sasa unatazamwa kama unawayawaya sana kwa utofauti kati ya dini ya Kiyahudi na neno la Mungu.

 

Usiku Ulio wa Kuuangalia

Neno Usiku wa Kuuangalia au wa Kukesha unatokana na andiko lililoko kwenye kitabu cha Kutoka 12:42.

 

Kutoka 12:42 inasema: Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za BWANA, kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa BWANA, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao.

 

Neno lililotafsiriwa hapa kama adhimishwa ni Shimmurim hivyo basi maana ya usiku wa kuuangalia na neno hilo limeonekana malaki hapa peke yake. Wazo la kuangalia linatokana na tendo la kupita juu kwa Makaila wa mauti na kutazamia ukombozi wa watu wetu. Neno hili kwa mujibu wa kamusi ya SHD 8107, shimmur lina maana ya adhimisho lililochukuliwa kwenye chimbuko la 8104 shamar ambalo maana yake ni kuzungushia (kama kwa miiba au michongoma) ili kuzuia au kulinda, au kuhudhuria.

 

Inafika mbali kiasi cha kuwa sawa na kutilia maanani au kuwa makini binasfi yako na kuwa mwangalifu.

 

Utendaji wake sio ni kukaa sana tu na kulinda bali kulindwa kama wigo unavyozungushiwa kwa michongoma au miiba. Pia inamaana ya kutazama tukio linaloulizwa.

 

Hiyo ndiyo maana ya Pasaka ambayo kwayo tunalindwa kwa damu ya mwana kondoo kutokana na harira kali ya Mungu inayo onyehwa katika mfano huu. Hivyo basi, kuadhimishwa kwetu kunatokana na utunzaji na ufafanuzi wa mifano ya maandiko haya. Sio jambo la lazima kwamba tuutumie usiku wetu wote kufanya maadhimisho kama tulivyolinwa na malaika wa kifo kwenye Pasaka. Vitu vyote viwili, yaani Ushirika wa Meza ya Bwana ufanyikao siku ya kumi na Nne na mlo wa siku ya kumi na Tano ya mwezi wa Kwanza (yaani Abibu au Nisani) kwa pamoja hutulinda sisi. Nia kwa vyo vyote vile ni kwamba usiku huu uendelezwe kwa kusoma na kwa uangalifu. Ingekuwa ni kutofanya kiusahihi kwa mfano kwenda kulala mapema katika usiku huu.

 

Andiko lililoko katika kamusi ya SHD 8107 linautenga usiku huu mbali kama ni usiku wa maadhimisho maalumu kama ilivyochukuliwa katika 8104. Bidii ya kukesha usiku mzima inatakiwa na kutiliwa maanani lakni sio ya lazima sana. Kwa hakika, Israeli walipaswa kukesha waliwa macho wakisubiri mtitiriko wa amri zilizokuwa zinatolewa. Baadi yao bila shaka waliweza kulala kwa kadiri walivyoweza.

 

Neno shimmur linatokana na maana ya kamusi ya 8104 na maana yake ni adhimisho zaidi kuliko maana ya kusimamia ulinzi kama tungalivyoweza kuchukua kwenye 8104 nano shamar.

 

Badiliko lililoko katika 8107 shomer (tazama kamusi ya SHD 7763) pia linachua maana nyingine kutoka kwenye neno shabar kwenye 7763 linalomaanisha ya kutafiti ili kupata maana yake, kungojea kwa matazamio.

 

Kama Yuda angekesha na kumngojea Masihi basi wasingeweza kwenda uhamishoni kwenye nchi ya utumwa. Kwa hiyo, usiku ule ulikuwa unamaana ya maadhimisho kutegemea ujio wake na kuonyesha kuelekea kwenye Kusulibiwa na kuzuia kukitanguliwa na kipindi cha kufikia siku ya kutoa sadaka ya Mganda wa kutikiswa.

 

Badala ya kukaa macho kwa kukesha tu, jambo ambalo kwa hakika linaruhusiwa, ni vema zaidi kuutumia usiku huo kwa kujifunza maana ya adhimisho ilihusishwa ujio wa Masihi kwa watoto. Hii ni maana ya kweli na halisi ya uadhimishaji tunaotakiwa kuwa nao.

 

Jinsi mlo huu inavyoliwa ni ishara ya kuonyesha kuharakisha ukombozi wetu tunao utazamia kututoa kwenye mifumo iliyoko ya kidunia.

 

Kutoka 12:11 inasema: Tena.mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya BWANA.

 

Linganisha utaratibu wa ulaji wa mlo na jinsi Kristo na Wanafunzi walivyokula mlo wa jioni ya maandalizi ya Chagigah.

 

Yohana 13:25 inasema: 25Basi yeye, hali amemwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?

 

Marko 14:50-52 inasema: 50Ndipo wakamwacha, wakakimbia wote. 51 Na kijana mmoja akamfuata, amejitanda mwili wake nguo ya kitani; wakamkamata; 52 naye akaiacha ile nguo ya kitani, akakimbia yu uchi.

 

Kiuwazi kabisa kutokana ina nukuu utandaji kazi wa Meza ya Bwana na kukamatwa kwake kuwa haikuwa jioni ya siku ya Pasaka. Inayofuata inaonyesha kuwa ilikuwa ni jioni ya siku ya maandalizi ya siku ya Kumi na Nne ya mwezi wa Kwanza ili kufanya tayari kwa Pasaka ambaye angeweza kuchinjwa marira ya alasiri ya siku inayofuata kuanzia usiku hadi kufikia saa kumi na moja au kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 11 jioni. Aliwekwa kaburini jioni mwanzoni mwa siku ya kumi na Nne ya mwezi na siku ya kwanza ya Mkate Usiotiwa Chachu wakati ambapo mwana kondoo wa Pasaka alikuwa ameandaliwa tayari kwa kuokwa na kuliwa kwa usiku ule.

 

Kumbu kumbu la Torati 16:2 inaruhusu mlo w Pasaka kuwa ama wa kutoka katika mifugo au katika wanyama na kwamba wanaweza kutokana miongoni mwa nyama ya wanyama wengine walio safi mbali na mwana kondoo. Inatakiwa iwe imeokwa na kuliwa mahali palipochaguliwa kwa kusudi hilo.

 

Kumbu kumbu la Torati 16:5-7 inatuamuru kuula mlo wa Pasaka nje ya malango yetu. Kwa hiyo tunatakiwa kurejea kwenye mahema yetu asubuhi yake. Hii ni siku ya Kumi na tano ya mwezi wa Kwanza, ambayo ni Siku Takatifu ya Kwanza ya Mikate Isiyotiwa Chachu ambayo twaweza hemani mwetu kwa maana ya majumbani mwetu mwa kawaida tunamoishi. Kifungu hiki cha maandiko sio lazima kitafsiriwe kama kuwa nje ya upenu wowote ule. Kwa mfano, tendo la kukaa nje kwa usiku mzima nje ya milango ya nyumba kwa mtu mwenye umri wa miaka themanini ni jambo la hatari sana. Ina maana kuwa Pasaka inatakiwa iadhimishwe nje ya malango ya nyumba, mahali ambapo ni pa kupangishwa kwa muda kama tunavyoweza kuona isemavyo baadhi ya vifungu vya maandiko.

 

Wasamaria waliadhimisha na hata sasa bado wakali wakiiadhimisha Pasaka ya Bwana siku ya Kumi na Nne ya mwezi wa Kwanza (unaoitwa Nisani) ukitegemea kutoka muingilano, na kuchinja mwana kondoo alasiri ya takriban saa 9 alasiri.

 

Kisha wanamuandaa na kumla siku ya Kumi na Tano ya mwezi wa Kwanza (uitwao wa Nisani au Abibu) baada ya machweo ya jua. Maandalizi na ulaji vinafanyika huku wakiwa wamejifunga mishipi na fimbo au bakora mikononi mwao.

 

Wanafanya haya yote nje ya malago ya nyumba zao na kwenye Mlima Gerizi. Ni sikukuu ya wahujaji na walipaswa nje ya mji wa Nablus mlimani.

 

Wanafanya hivi kwenye Mlima wa Gerizi kwa sababu ya Kumbu kumbu la Torati 27:4-7 kwenye vifungu vya vya tafsiri yao ya Kiebrania. Aya ya 4 na Biblia ya maandiko ya Masoretic inautaja Mlima Ebali (maana yake mafungu) kama mlima wa uumbaji wa sheria. Huu ulikuwa pia ni Mlima wa Laana. Mlima wa Gerizi ulikuwa ni Mlima wa Baraka na mlima wa kufanyia ibada za Wasamaria na hivyo, ulirudisha mfano wake wa kidini katika sura ile. Nukuu za kwamba MT ziligeuza maana yake kutoka gerizi na kuwa Ebali.

 

Kwa ujumla ilibishaniwa kuwa Ebali ni mageuzo ya kwewnye Maandiko ya Masoretic na ilikuwa isomwe Gerizi. Aya za kenye kumbu kumbu la Torati 27:11-26 zinaonyesha kuwa Gerizi ulikuwa ni kwa ajili ya baraka na Ebali ulikuwa ni kwa ajili ya laana. Kiundani ni kwamba, sadaka za amani hazikufanyika mlimani kwa laana na madhabahu ilitakiwa isimamishwe kwenye mlima huu.

 

Wasamaria waliziadhimisha Sabato na sikukuu kwa mujibu wa Torati na Sheria za Musa, wakati ambapo yuda walizifuata sheria 613. Wale wanaoitwa Wakristo kutoka kwenye madhehebu makubwa wanaofuata na kuadhimisha mfumo wa Easter ya Kipagani na mabadiliko madogo yaliyofuatia ya hesabu za kalenda.

 

Wanazuoni wengi pia wanakubali kuwa matendo ya kidini ya Wasamaria ni sawa na ya Wayahudi kwa Kipindi cha Pili cha zama za Hekalu. Wasamaria bado wanafuata matendo ya Kipindi cha Pili cha Hekalu kwa mahali patakatifu.

 

Walikuwa na Maskani au Hama ya Kukutania pale. Iliharibiwa na Mmakabayo John Hyrcanus I. Aliowatiisha Waidumea kwa haraka hiyo hiyo na kuwalazimisha kuingia kwenye uongofu wa dini ya Kiyahudi. Hakuhitaji kushughulika na Wasamaria zaidi ya kuiangamiza Maskani yao au Hema yao ya kukutania kwa kuwa mfumo wao wa kalenda ulikuwa ni sawa na ule wa Wamasadukayo ambao kwao Hekalu lilikuwa linaendeshwa kwa kuutegemea utaratibu huu. Mafarisayo walikuwa bado hawajapata utamaduni wao wa kimapokeo kiasi cha kufikia kujaribu kupanga jins ya kuahirisha na kurudi kwenye Sabato zilizokuwa za kawaida kwa kipindi chote kizima cha Hekalu kama inavyoelezea Mishnah (tazama jarida la Kalenda ya Mungu [156].

 

Wasamaria pia walikataa kufuata au kuadhimisha sikukuu za Hanuka na Purimu.

 

Walihesabu Miandamo ya Mwezi Mpya miezi minane mapema kabla ya kuhesabu kwenye muunganiko. Baada ya maangamizo ya Hekalu la Pili Wayahudi walionekana kama walidharau au “kupoteza” fursa ya uwezo wao wa kuhesabu Miandamo ya Mwezi ili kupelekea kwenye uahirisho. Marabi walikataa kukubaliana na namna ya hesabu za Wasamaria na wakatengeneza kalenda yao wenyewe ambayo waliichanganya hesabu zake na uahirisho na maadhimisho ya mwezi mpevu.

 

Kristo alishutumiwa kwa kudhaniwa kuwa ni Msamaria halisi kabisa kwa sababu hakukubaliana na mapokeo ya Mafarisayo (Yoh. 8:48).

 

Usiku wa Kuukumbuka Sana ni usiku wa kuwafundisha watoto kusudi na maana ya jioni ile na mambo wanayotakiwa kufanya katika usiku ule.

Kutoka 12:25-38 inasema: Itakuwa, hapo mtakapoifikilia hiyo nchi, BWANA atakayowapa, kama alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu. 26 Kisha itakuwa hapo watoto wenu watakapowauliza, N’nini maana yake utumishi huu kwenu? 27 ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia. 28 Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama BWANA alivyo waamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.

 

Kutazamia kwa ukombozi kwenye usiku wa Pasaka uliadhimishwa kama ukumbusho wa milele (Kut. 12:14). Katika usiku ule tunasubiria ukombozi wetu. Katika jioni hii Kristo alizikwa na kulazwa kaburini kwa muda wa siku tatu yaani siku za usiku tatu na za mchana tatu kwenye moyo wa nchi kuanzia siku ya Jumatano jioni hadi siku ya Jumamosi jioni wakati alipofufuliwa na Mungu Mmoja wapekee na Wakweli na siku ya Jumapili asubuhi akapaa kwenda Mbinguni akiwa kama ni sadaka ya Mganda wa Kutikiswa saa 3 asubuhi ambayo ni mwanzo wa hesabu za siku kuelekea kwenye Pentekoste na mavuno ya Kanisa katika Roho Mtakatifu.

 

Kwa tendo kama hili Mungu alimchukua mzaliwa wa kwanza wa kuumbwa kwa ulimwengu na Wokovu ulienea kwa Mataifa wapagani.

 

Inaendelea: 29 Hata ikawa, usiku wa manane BWANA akawapiga wazaliwa wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama. 30 Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu. 31 Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu, ninyi na wana wa Israeli; enendeni, mkamtumikie BWANA kama mlivyosema. 32 Twaeni kondoo zenu na ng’ombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu, mkanibariki mimi pia. 33 Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote. 34 Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabagani. 35 Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi. 36 BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara. 37 Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto. 38 Na kundi kubwa la watu waliochangamana nao wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng’ombe, wanyama wengi sana.

 

Makutano hawa mchanganiko walifanyika kuwa ni sehemu ya Israeli.

 

Kwa hiyo Wokovu ulipaswa uendelee kuenea kupitia Masihi hadi kwa Mataifa wapagani pia. Ushirika wa Meza ya Bwana ni sehemu ya utaratibu wa maadhimisho ya sikukuu hii. Ushiriki wa Meza ya Bwana ni usiku wa kwanza wa siku ya Kumi na Nne ya mwezi wa Kwanza na hatimaye usiku unaofuatia wa Kumi na Tano katika mlo wa Pasaka ambao unaashiria muunganiko wa ulimwengu chini ya Masihi katika Israeli.

 

Ni ya kukumbukwa miongoni mwa watu wetu ni amri ya milele.

 

Kutoka 13:14-16 inasema: Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza keshoni, akisema, Ni nini hivi? Utamwaambia, BWANA alitutoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake; 15 basi ilikuwa hapo Farao alipojifanya kuwa mgumu ili asitupe ruhusa kuondoka, BWANA akawapiga wazaliwa wa kwanza wote waliokuwa katika nchi ya Misri, wa binadamu na wa mnyama; kwa ajili ya hayo namtolea BWANA wote wafunguao tumbo, wakiwa waume; lakini wazaliwa wa kwanza wote wa wana wangu nawakomboa. 16 Jambo hilo litakuwa ni ishara mkononi mwako, na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa BWANA alitutoa Misri kwa uwezo wa mkono wake.

 

Pia inaelekea kwenye Mfafara wa pili wa kutoka ambao utatokea kwa mkono wenye nguvu wa Mungu.

 

Isaya 66:18-24 inasema: Nami nayajua matendo yao na mawazo yao; wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu. 19 Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu; katika mataifa. 20 Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi. 21 Na baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani na Walawi, asema BWANA. 22 Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazifanya, zitakavyokuwa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. 23 Na itakuwa mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA. 24 Nao watatoka nje na kuitazama miziga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika; nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.

 

Kwa hiyo usiku huu sio tu ni kwa siku zilizipita. Pia itakuwepo katika siku zijazo, na Maandiko matakatifu hayawezi kutanguka.

 

Yeremia 6:16-19 inasema: BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo. 17 Nami naliweka walinzi juu yenu, wakisema, Isikilizeni sauti ya tarumbeta, lakini walisema, Hatutaki kusikiliza. 18 Kwa sababu hiyo sikilizeni, enyi mataifa, mkajue, Ee kusanyiko, ni jambo gani litokealo kati yao. 19 Sikia, Ee nchi; tazama, nitaleta mabaya juu ya watu hawa, naam, matunda ya mawazo yao, kwa sababu hawakuyasikiliza maneno yangu; tena kwa habari ya sheria yangu, wameikataa.

 

Tunatakiwa kuanzisha tena njia za zamani na kurudi kwenye sheria na kuachana na kalenda ya wapagani na ngano za fumbo za Wababeli zilizoanzishwa chini ya mapokeo ya Marabi chini ya usimamizi wa Hilleli II mnamo mwaka 358 BK.

 

Mhubiri 3:15 inasema: Yale yaliyoko yamekuwako; na yale yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.

 

Tunatakiwa kurudishwa tena kweli ya neno la Mungu mara moja kadiri inavyotolewa.

 

Warumi 15:4 inasema: 4Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.

 

Yeye ajaribuye kushindana na Maandiko matakatifu ili kuyabadilisha sheria na kubadili majira na nyakati hana sehemu katika ufalme wa Mungu. Na kama vile ilivyo kwa maadhimisho ya Sabato kuwa yanaendelea na kusimama kama yalivyo, ndivyo ilivyo kwa hii Miandamo ya Mwezi Mpya na Sikukuu zote za Mungu. Siku ya Upatanisho haiwezi kuahirishwa tena zaidi kama ilivyo kwa Sabato na Miandamo ya Mwezi Mpya au Pasaka. Italiwa kwenye nyumba moja yaani mahali pamoja (Kut. 12:46).

 

Kutoka 12:42 inasema: Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za BWANA, kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa BWANA, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao.

 

Kesheni basi kwa kuwa hamjui ni saa ipi ya kuja kwake bwana arusi (Mat. 25:13).

 

Marko 13:30-37 inasema: Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie. 31 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. 32 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walioko mbinguni, wala Mwana, ila Baba. 33 Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. 34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. 35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; 36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. 37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.

 

Neno Kizazi hapa lililosemwa na Kristo katika injili ya Marko 13:30 lina maana ya kizazi cha mwisho. Katika kizazi kimoja, au miaka arobaini, vita vyote vya mwisho vitapita. Wakati wa miaka ile arobaini Upimaji wa Hekalu na kazi zote za siku za mwisho zitatimilizwa (tazama jarida la Upimwaji wa Hekalu [137]. Masihi atarudi na Sheria zitarejezwa. Kesheni basi kwa kuwa hajui wakati wa kurudi kwa bwana wenu.

 

Wimbo Ulio Bora 5:2 inasema: Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.

 

(Tazama jarida la Wimbo Ulio Bora [145].

 

Katika mwaka 2027/28 tutaona yubile na marejesho.

 

Na kwa hiyo tunakazi ya kuwajibika kwa Mungu aliye hai.

 

Matendo ya Mitume 20:28-35 inasema: Jilindeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damuyake mwenyewe. 29 Najua mimi ya kwamba baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, walihurumie kundi; 30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao. 31 Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kuwaonya kila mtu kwa machozi. 32 Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa. 33 Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu. 34 Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. 35 Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.

 

Kwa hiyo na tuhakikshe kuwa jambo hili linajulikana na watu wote.

 

 

 

 

 

 

 

 

q